name
stringclasses
429 values
text
stringlengths
0
767k
Bakari Kiango na Juma Issihaka, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Uamuzi wa
Bakari Kiango na Juma Issihaka, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuondoa Alphayo Kidata kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), umetajwa na wadau kuwa, unalenga kumweka karibu zaidi na Rais kwa ajili ya kumshauri namna ya kuyaenenda masuala ya kikodi. Ing...
Uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuondoa Alphayo Kidata kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuondoa Alphayo Kidata kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), umetajwa na wadau kuwa, unalenga kumweka karibu zaidi na Rais kwa ajili ya kumshauri namna ya kuyaenenda masuala ya kikodi. Ingawa wengine wanayatazama mabadiliko hayo kwa sura hiyo, baadhi ya wadau wameona kilichofany...
Muda wa zabuni iliyotangazwa ya kumsaka mkandarasi atakayekifanyia matengenezo makubwa kivuko cha MV
Muda wa zabuni iliyotangazwa ya kumsaka mkandarasi atakayekifanyia matengenezo makubwa kivuko cha MV Kigamboni umefika mwisho, huku kampuni mbili za Tanzania zikiomba kazi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa ya zabuni hiyo yenye namba X8/2023/2024/W/53 mkandarasi aliyehitajika ni yule atakayekuwa na uwezo wa kufanya ukarabati...
Lilikuwa suala la muda tu, kwa Mchungaji Peter Msigwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndivyo
Lilikuwa suala la muda tu, kwa Mchungaji Peter Msigwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndivyo unavyoweza kueleza baada ya kada huyo wa zamani wa Chadema kutimkia katika chama hicho tawala. Kwa mujibu wa wanazuoni na wanasiasa, uamuzi wa Msigwa kuihama Chadema na kujiunga na CCM ulitarajiwa, kutokana na mienendo y...
Ukimya katika taarifa za mwenendo wa tuhuma za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda u
Ukimya katika taarifa za mwenendo wa tuhuma za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda umewashtua wadau wa sheria, wakitaka upelelezi uharakishwe ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani. Msisitizo wa wataalamu hao wa taaluma ya sheria, unatokana na kile walichofafanua, ni mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka ya ku...
Utoaji wa miradi mbadala ya kujikimu kiuchumi kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi
Utoaji wa miradi mbadala ya kujikimu kiuchumi kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi ni moja ya hatua iliyopendekezwa kukomesha uharibifu wa hifadhi nchini. Hatua hiyo pia, imetajwa kusaidia kupunguza au kukomesha kabisa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa dhidi ya wananchi wanaoishi...
Wakati Serikali za Tanzania na Kenya zikipitia vipindi vigumu vya mgomo wa wafanyabiashara na maanda
Wakati Serikali za Tanzania na Kenya zikipitia vipindi vigumu vya mgomo wa wafanyabiashara na maandamano ya wananchi, wadau wamependekeza hatua zilizopaswa kuchukuliwa kukabili haraka matukio hayo. Sambamba na hatua hizo, wanazuoni hao wa biashara na uchumi, wameeleza kilichofanywa katika mataifa hayo kinaonyesha nguvu...
Malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu utitiri wa kodi, tozo na ushuru wa bidhaa hayakuanza jana, ni k
Malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu utitiri wa kodi, tozo na ushuru wa bidhaa hayakuanza jana, ni kilio cha miongo kadhaa katika awamu mbalimbali za Serikali. Aghalabu malalamiko hayo yanaishia kusikika kupitia wawakilishi wao na ulifika wakati hadi baadhi ya biashara zilishindwa kustahimili hali hiyo zikajifia. Leo h...
Upinzani umeendelea kuishukia kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk M
Upinzani umeendelea kuishukia kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Mohamed Dimwa, aliyetaka Rais Hussein Mwinyi aongezewe muda wa kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi saba. Msingi wa kauli hiyo ya Dimwa ni kile alichoeleza, sekretarieti ya kamati maalum ya chama hicho imetathmini na...
Licha ya kusambaa kwa taarifa ya mgomo wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo utakaoanza leo, ku
Licha ya kusambaa kwa taarifa ya mgomo wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo utakaoanza leo, kumekuwa na mgongano wa kauli miongoni mwa wafanyabiashara hao. Mgongano huo unatokana na kauli za viongozi wa wafanyabiashara hao, wanaodai kutohusika na uandaaji wa mgomo huo, huku baadhi ya wafanyabiashara wakisema hawa...
Licha ya sekta ya kilimo kuwa msingi wa ajira za Watanzania lukuki, wakulima wengi nchini wanakosa m
Licha ya sekta ya kilimo kuwa msingi wa ajira za Watanzania lukuki, wakulima wengi nchini wanakosa maarifa sahihi ya namna ya kuienenda shughuli hiyo. Kukosekana kwa maarifa hayo miongoni mwa wakulima wengi nchini, kunasababisha kilimo kifanyike kwa mazoea na hatimaye kukosa tija katika uzalishaji. Asilimia 75 ya Watan...
Hatma ya maumivu au unafuu wa maisha kwa wananchi, itaamuliwa na wabunge wiki hii wanapokwenda kupit
Hatma ya maumivu au unafuu wa maisha kwa wananchi, itaamuliwa na wabunge wiki hii wanapokwenda kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25. Sambamba na hilo, wiki hii ndiyo itakayoamua hatma ya tuhuma za kudharau mamlaka ya Spika na Bunge zinazomkabili Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina. Wiki mbili zilizo...
Siku tatu baada ya kupatikana mwili wa mtoto, Asimwe Novath (2) mwenye ualbino, hatimaye Jeshi la Po
Siku tatu baada ya kupatikana mwili wa mtoto, Asimwe Novath (2) mwenye ualbino, hatimaye Jeshi la Polisi limewakamata watu tisa wanaodaiwa kuhusika na mauaji yake, akiwemo Paroko Msaidizi na Baba mzazi wa mtoto huyo. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, tisa hao wamekamatwa wakiwa na viungo mbalimbali vinavyodaiwa kuwa...
Michakato ya kuelekea uchaguzi imehusishwa kama moja ya sababu za mauwaji ya watu wenye ualbino, huk
Michakato ya kuelekea uchaguzi imehusishwa kama moja ya sababu za mauwaji ya watu wenye ualbino, huku wadau wakitaja kasoro zilizopo katika kuyakabili matukio hayo. Miongoni mwa kasoro zilizobainishwa na wadau hao ni uwepo wa mianya ya uholela katika shughuli za uganga wa jadi na kukosekana mrejesho wa hatua zinazochuk...
Haki na uwazi katika uchaguzi, maadili, afya ya akili na amani ni miongoni mwa hoja zilizopewa uzito
Haki na uwazi katika uchaguzi, maadili, afya ya akili na amani ni miongoni mwa hoja zilizopewa uzito katika hotuba za viongozi mbalimbali wa dini la Kiiislamu katika Ibada ya Eid Al-Adha na Baraza la sikukuu hiyo. Nasaha za viongozi hao kuhusu uwazi na haki katika uchaguzi zinatokana na ukweli kwamba, imesalia miezi mi...
Usiri wa jamii unapofanyika ukatili kwa watoto ni moja kati ya sababu nyingi zilizotajwa na watoto w
Usiri wa jamii unapofanyika ukatili kwa watoto ni moja kati ya sababu nyingi zilizotajwa na watoto wenyewe, zinazochagiza kuendelea kwa vitendo hivyo dhidi yao. Kwa mujibu wa watoto hao, pamoja na kundi hilo kuwa katika hatari ya kukatiliwa, aghalabu jamii imekuwa ikiwaficha wanaotenda vitendo hivyo, jambo linalowafany...
Kuna nini Ikulu, ndilo swali linaloonekana kuwasumbua Watanzania wengi kwa sasa, baada ya Rais Samia
Kuna nini Ikulu, ndilo swali linaloonekana kuwasumbua Watanzania wengi kwa sasa, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko mengi ya wasaidizi wake katika kipindi kifupi hasa cha Mei na Juni. Katika kipindi cha miezi hiyo, mkuu huyo wa nchi amefanya mabadiliko ya wasaidizi wake 10, yaani wanane kwa Juni pekee...
Hatua ya Serikali kupendekeza msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mafuta ya kupikia
Hatua ya Serikali kupendekeza msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mafuta ya kupikia yanayozalishwa nchini, imetajwa kuongeza hamasa ya uwekezaji kwenye mafuta, kilimo cha mazao ya mafuta, kadhalika itapunguza bei ya bidhaa hiyo. Wasindikaji wa ndani wa mafuta wamekwenda mbali zaidi na kueleza kwa uhalis...
Baada ya kilio cha muda mrefu kuhusu kikokotoo hatimaye, Serikali imeongeza fao la mkupuo watakaloli
Baada ya kilio cha muda mrefu kuhusu kikokotoo hatimaye, Serikali imeongeza fao la mkupuo watakalolipwa wastaafu kutoka asilimia 33 iliyopo sasa hadi asilimia 40. Ongezeko la fao hilo la mkupuo linajibu vilio vya wastaafu, ambao awali walilalamikia asilimia 33 waliokuwa wanalipwa, isingewasaidia kuzikabili gharama za m...
Licha ya usafiri wa bodaboda kuwa fursa kubwa ya ajira nchini, kwa upande mwingine ni chanzo cha aja
Licha ya usafiri wa bodaboda kuwa fursa kubwa ya ajira nchini, kwa upande mwingine ni chanzo cha ajali kilichopoteza uhai wa vijana wengi, kadhalika kuwaacha baadhi yao na ulemavu wa kudumu. Siifungamanishi hoja yangu hii na mjadala wowote kuhusu hadhi ya ajira ya bodaboda, kwa kuwa si muktadha wa ninachokiandika, bali...
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza kwa safari za mwanzo za treni ya mwendokasi kutoka
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza kwa safari za mwanzo za treni ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kuanzia Juni 14, mwaka huu. Kuanza kwa safari hizo kunafanyika karibu wiki mbili kabla ya siku ambayo Rais Samia Suluhu Hassan atazindua rasmi safari ya treni hiyo, Juni 25, mwaka huu. Hata h...
Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu kusimama imara katika mchakato
Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu kusimama imara katika mchakato wa mageuzi wa mashirika ya umma na kupuuza kelele atakazokutana nazo kwenye mageuzi hayo. Rais Samia amesema anafahamu mchakato huo ni lazima uhusishe kelele kwa kuwa kuna watu watakaoumizwa na mageuzi hayo lakini ni laz...
Kama umewahi kuwasikia waswahili wakisema kisicho riziki hakiliki, basi methali hiyo imeakisi uhalis
Kama umewahi kuwasikia waswahili wakisema kisicho riziki hakiliki, basi methali hiyo imeakisi uhalisia katika familia ya Kwangaya yenye makazi yake Rufiji mkoani Pwani. Familia hiyo iliyokuwa katika matarajio ya mipango ya harusi, ghafla mpango huo umegeuka huzuni, baada ya aliyetarajiwa kuolewa kupoteza maisha. Bi har...
Safari ya mwanafunzi Khadija Makalani kuhitimu elimu ya msingi huenda ikaishia njiani, baada ya kuko
Safari ya mwanafunzi Khadija Makalani kuhitimu elimu ya msingi huenda ikaishia njiani, baada ya kukosa Sh10,000 ya kununua sare za shule. Mwanafunzi huyo wa darasa la sita katika shule ya Msingi Myumbu wilayani Kilwa katika Mkoa wa Lindi, amejikuta katika hali hiyo baada ya sare za shule alizokuwa nazo kusombwa na maji...
Licha ya kukoma kwa mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini, bado athari zake zinaendelea kuacha vi
Licha ya kukoma kwa mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini, bado athari zake zinaendelea kuacha vilio na maumivu kwa wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na majanga hayo katika siku za karibuni. Mafuriko hayo yaliyotokana na mvua zilizoanza kunyesha tangu Oktoba mwaka jana, yameathiri maeneo mengi nchini na Kijiji cha Myu...
Nafuu ya kodi, ushuru na tozo katika huduma za mawasiliano, kupungua kwa gharama ya data na kuimaris
Nafuu ya kodi, ushuru na tozo katika huduma za mawasiliano, kupungua kwa gharama ya data na kuimarishwa kwa elimu ya Tehama na Akili Bandia ni miongoni mwa matarajio ya wadau kuhusu sekta ya mawasiliano kuelekea Bajeti Kuu ya Serikali. Matarajio ya wadau hao, wakiwemo wanazuoni yanakuja wakati Juni 13, mwaka huu Serika...
Ni kipindi cha wakazi wa Kigamboni kufunga mkanda, kauli hiyo inaakisi uhalisia wa uvumilivu wa zaid
Ni kipindi cha wakazi wa Kigamboni kufunga mkanda, kauli hiyo inaakisi uhalisia wa uvumilivu wa zaidi ya mwaka wanaopaswa kuwa nao watumiaji wa vivuko katika eneo la Kigamboni-Magogoni. Wanachopaswa kuvumilia hasa ni huduma hafifu katika eneo hilo kwa kipindi cha karibu mwaka, zitakazosababishwa na uchache wa vivuko, b...
Licha ya Wizara ya Ardhi kupiga marufuku uuzaji wa ardhi kupitia kampuni za madalali zenye mabango k
Licha ya Wizara ya Ardhi kupiga marufuku uuzaji wa ardhi kupitia kampuni za madalali zenye mabango katika maeneo mbalimbali nchini, wadau wamesema hatua hiyo haitakuwa muarobaini wa utapeli na migogoro katika sekta ya ardhi. Marufuku ya uuzaji wa ardhi kupitia kampuni hizo za udalali, ilitolewa juzi na Waziri wa Ardhi,...
Baada ya kivuko cha MV Kigamboni kupitiliza muda wa matengenezo makubwa kwa zaidi ya mwaka sasa, hat
Baada ya kivuko cha MV Kigamboni kupitiliza muda wa matengenezo makubwa kwa zaidi ya mwaka sasa, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imetangaza kukipeleka katika matengenezo hayo. Uamuzi huo wa Temesa unakuja ikiwa imepita wiki moja, tangu gazeti la Mwananchi lichapishe mfululizo wa ripoti maalum kuhu...
Wizi kwa njia ya mifumo unaendelea kuota mizizi serikalini na sasa umegeukia kwa askari wa usalama b
Wizi kwa njia ya mifumo unaendelea kuota mizizi serikalini na sasa umegeukia kwa askari wa usalama barabarani, huku wanazuoni wakieleza namna unavyofanyika na kupendekeza mbinu za kuudhibiti. Katika Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, zaidi ya askari 10 kutoka mikoa ya Iringa, Pwani na Kilimanjaro wanadaiwa ...
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema tayari ameukutanisha Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa)
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema tayari ameukutanisha Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) na Kampuni ya Azam Marine Ltd, kujadili namna bora ya kushirikiana ili kuboresha utoaji huduma ya usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni - Kigamboni. Kauli hiyo ya Bashungwa inakuja ikiwa ni siku ya pili gazeti la Mw...
Takriaban wanafunzi 240 wanawake katika Shule ya Sekondari Namanga, wameepukana na safari ya kutoka
Takriaban wanafunzi 240 wanawake katika Shule ya Sekondari Namanga, wameepukana na safari ya kutoka nyumbani kwenda shule, badala yake wataanza kuishi bweni. Hatua hiyo ni baada ya shule hiyo kukabidhiwa jengo la bweni litakalolaza wanafunzi 240, kutoka kwa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Huduma za Kisheria (LSF). A...
Magonjwa kama homa ya mapafu na mengine yanayohusiana na baridi, yanatarajiwa kuwakabili wananchi ka
Magonjwa kama homa ya mapafu na mengine yanayohusiana na baridi, yanatarajiwa kuwakabili wananchi katika kipindi cha kuanzia Juni hadi Agosti mwaka huu. Uwezekano wa kutokea kwa magonjwa hayo, unatokana na matarajio ya kuanza kwa msimu wa kipupwe (JJA), utakaosababisha hali ya baridi ya wastani na joto kiasi. Kwa mujib...
Mashaka ya kukamilika kwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) yanaendelea kupata mashiko, baada ya kuendel
Mashaka ya kukamilika kwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) yanaendelea kupata mashiko, baada ya kuendelea kushuhudiwa ahadi zisizotimia katika za kukamilishwa utekelezwaji wa vipande mbalimbali. Sambamba na ahadi zisizotimia, kumeshuhudiwa makundi ya wafanyakazi katika kambi mbalimbali wakiondolewa kambini na mkandarasi k...
Mifumo ya uendeshaji iliyojikita katika utoaji huduma badala ya kufanya biashara, ni moja ya mambo y
Mifumo ya uendeshaji iliyojikita katika utoaji huduma badala ya kufanya biashara, ni moja ya mambo yanayotajwa kuuweka rehani uhai wa Wakala wa Huduma na Umeme Tanzania (Temesa), Mwananchi imebaini. Mifumo hiyo kwa mujibu wa uchunguzi wa takriban miezi mitatu uliofanywa na gazeti hili, inaisababisha Temesa kufanya kaz...
Licha ya dhamira ya Serikali ya kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya vivuko Kiga
Licha ya dhamira ya Serikali ya kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya vivuko Kigamboni na Magogoni, huenda mpango huo ukabaki kuwa ndoto isiyotimia. Kutotimia kwake, kunatokana na uhalisia wa mazingira yaliyowekwa na Serikali ya utoaji huduma katika eneo hilo, ambayo si rafiki kwa sekta binafsi. Ni...
Kama umewahi kuhisi maumivu ya kutwishwa mzigo wenye uzito zaidi ya nguvu zako halisi, basi hali hiy
Kama umewahi kuhisi maumivu ya kutwishwa mzigo wenye uzito zaidi ya nguvu zako halisi, basi hali hiyo inaukabili Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), katika jukumu la uendeshaji wa vivuko nchini. Temesa inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake ya mwaka 2005, inayotaka pamoja na majukumu mengine ...
Usalama wa zaidi ya watu 60,000 wanaotumia huduma ya vivuko kuvuka Kigamboni na Magogoni kila siku u
Usalama wa zaidi ya watu 60,000 wanaotumia huduma ya vivuko kuvuka Kigamboni na Magogoni kila siku upo katika mashaka. Mashaka ya usalama wa watu hao, yanatokana na ubovu wa vivuko hivyo, unaosababishwa na kutofanyiwa matengenezo makubwa kwa mujibu wa sheria, ratiba na matakwa ya kitaalamu. Hali hiyo inazua hofu ya k...
Jumuiya ya wafanyabiashara katika Jiji la Shaoyang nchini China, imesema inalenga kushirikiana na wa
Jumuiya ya wafanyabiashara katika Jiji la Shaoyang nchini China, imesema inalenga kushirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania ili kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo. Kadhalika, imedokeza mpango wa kuanzisha ghala la bidhaa zake nje ya nchi, litakalotumika kupokea bidhaa za mitambo na umeme kutoka China kuja Tanz...
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart), umesema Julai mwaka huu, utaanza matumizi ya
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart), umesema Julai mwaka huu, utaanza matumizi ya mageti ya mfumo wa kadijanja kwa ajili ya abiria watakaopanda usafiri huo. Kwa mujibu wa Dart, hatua hiyo ni baada ya kukamilika kwa kazi ya kufungwa kwa mfumo wa mageti hayo katika vituo mbalimbali vya mabasi yaendayo h...
Serikali imesema ipo katika hatua ya kuainisha mahitaji, sifa na aina ya teknolojia zinazohitajika k
Serikali imesema ipo katika hatua ya kuainisha mahitaji, sifa na aina ya teknolojia zinazohitajika katika sekta mbalimbali na kuweka muda maalum kwa ajili ya kupatikana. Hatua hiyo kwa mujibu wa Serikali, inalenga kuhakikisha sayansi na teknolojia inapewa kipaumbele katika maendeleo ya rasilimali watu na ubunifu. Katik...
Helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi imeanguka baada ya kupata shida katika kutu
Helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi imeanguka baada ya kupata shida katika kutua. Kwa mujibu wa televisheni ya Taifa ya Iran, helikopta hiyo imeanguka leo, Mei 19, 2024 karibu na Mji wa Jolfa, uliopo mpakani na taifa la Azerbaijan. Hata hivyo, taarifa hiyo haijaweka wazi chanzo cha moja kwa moja ch...
Tuhuma za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma, zim
Tuhuma za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma, zimekiweka katika mashaka kibarua cha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Hamsini na wenzake. Mashaka hayo, yanatokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda aliyemwagiza Katibu Tawala wa mkoa huo, Missaile Mussa aw...
Hali imeendelea kuwa ngumu katika ufaulu wa mtihani wa leseni ya Baraza la Famasia Tanzania kada ya
Hali imeendelea kuwa ngumu katika ufaulu wa mtihani wa leseni ya Baraza la Famasia Tanzania kada ya watoa dawa na fundi dawa wasaidizi, baada ya robo tatu ya wanafunzi kufeli. Katika mtihani huo uliohusisha watahiniwa 200, wanafunzi 184 wameshindwa kufaulu katika awamu ya kwanza, hivyo baadhi yao wametakiwa kurudia mti...
Umewahi kupangiwa mtindo wa maisha kwa masharti ya mkataba wa nyumba ya kupanga unayoishi au uliyowa
Umewahi kupangiwa mtindo wa maisha kwa masharti ya mkataba wa nyumba ya kupanga unayoishi au uliyowahi kuishi? Swali hili linaakisi uhalisia wa karaha, vituko na maajabu ya masharti yaliyopo kwenye mikataba ya nyumba za kupanga yanayowakumba Watanzania wengi. Masharti hayo kwa mujibu wa baadhi ya wapangaji, yanalazimu ...
Baada ya kupotea kwa siku nne mfululizo, hatimaye huduma ya intaneti imerejea, huku ikiacha maumivu
Baada ya kupotea kwa siku nne mfululizo, hatimaye huduma ya intaneti imerejea, huku ikiacha maumivu kwa watumiaji, wakiwemo madereva wa taksi mtandao, vyombo vya habari, benki na mawakala. Kwa siku nne hizo, intaneti ambayo ndiyo msingi wa baadhi ya huduma muhimu za mtandaoni, ilikosekana nchi nzima na kusababisha mkwa...
Hatma ya nani na nani watakaoteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwania nafasi z
Hatma ya nani na nani watakaoteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwania nafasi za uenyekiti wa kanda, inatarajiwa kujulikana katika siku tatu zijazo kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu. Pamoja na kujulikana kwa wateule hao, ndani ya siku hizo tatu ndipo msimamo wa chama hicho kuhusu kauli ya Makamu Mweny...
Mwezi mmoja baada ya Serikali kubaini jokofu la nyumbani likitumiwa kuhifadhia damu mkoani Shinyanga
Mwezi mmoja baada ya Serikali kubaini jokofu la nyumbani likitumiwa kuhifadhia damu mkoani Shinyanga, jambo kama hilo limetokea katika Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe katika Mkoa wa Tanga. Kutokana na vitendo hivyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dug...
Huenda bei ya gesi ya kupikia ikapungua kutoka ile inayouzwa sasa, baada ya Serikali kuanza utekelez
Huenda bei ya gesi ya kupikia ikapungua kutoka ile inayouzwa sasa, baada ya Serikali kuanza utekelezaji wa mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia. Dalili ya kupungua bei ya nishati hiyo, imetokana na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Wizara ya Nishati ishirikiane na sekta binafsi kuona namna ya kuifa...
Hivi unajua barabara inapowekwa kiraka, kinapaswa kidumu kwa saa 72 tu, kisha kiondolewe na ufanyik
Hivi unajua barabara inapowekwa kiraka, kinapaswa kidumu kwa saa 72 tu, kisha kiondolewe na ufanyike ukarabati? Si hivyo tu, hata barabara inapokatwa kwa ajili ya kuwekwa kiraka, utekelezwaji wake unapaswa kufanyika kwa muda usiozidi saa 48. Kwa mujibu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), uwekaji wa kiraka ni ...
Safari ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chama cha ACT Wazalendo imefikia leo, huku viongozi wake wak
Safari ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chama cha ACT Wazalendo imefikia leo, huku viongozi wake wakitabiri taswira ya chama hicho katika miaka 10 ijayo. Kwa mtazamo wa viongozi hao, katika miaka 10 ijayo, chama hicho ndicho kitakachoshika hatamu ya uongozi serikalini, kielelezo cha ushirikishwaji wa vijana katika sia...
Baada ya mfululizo wa mvua za El-Nino kwa takriban miezi saba, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa ku
Baada ya mfululizo wa mvua za El-Nino kwa takriban miezi saba, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa kukumbwa na Kimbunga Hidaya kwa siku tano mfululizo. Iwapo hilo litatokea, hii itakuwa mara ya tatu kwa Tanzania kukumbwa na kimbunga tangu nchi ikiwa chini ya mkoloni, kama ilivyoelezwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya...
Vyama vya Wafanyakazi, vimesema matumaini yao kuhusu utekelezaji wa mabadiliko ya kanuni ya kikokoto
Vyama vya Wafanyakazi, vimesema matumaini yao kuhusu utekelezaji wa mabadiliko ya kanuni ya kikokotoo na nyongeza ya mishahara yamebaki kwa Serikali. Kauli hiyo ya wafanyakazi inakuja siku moja, baada ya Serikali kuweka wazi kuwa, tayari imesikia maoni yao kuhusu madai ya mabadiliko ya kanuni ya kikokotoo, kadhalika ny...
Matumaini ya wafanyakazi juu ya kutangaziwa nyongeza ya mishahara na mabadiliko ya kanuni ya kikokot
Matumaini ya wafanyakazi juu ya kutangaziwa nyongeza ya mishahara na mabadiliko ya kanuni ya kikokotoo cha mafao ya wastaafu katika sherehe za Mei Mosi yametoweka, baada ya Serikali kuonyesha mchakato wa utekelezwaji wa hayo unaendelea. Nyongeza ya mishahara na mabadiliko ya kanuni ya kikokotoo ni miongoni mwa taarifa ...
Katikati ya sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Ta
Katikati ya sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limetaja mambo tisa yanayowasibu wafanyakazi nchini na kupendekeza utatuzi wake. Miongoni mwa mambo hayo ni kupandishwa kwa mishahara, usuluhishi wa migogoro, ajira za mikataba, likizo ya uzazi kwa wanawak...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameonyesha hofu ya kuzungumza mambo mengi mbele ya Makamu wa Ra
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameonyesha hofu ya kuzungumza mambo mengi mbele ya Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kwa kile alichoeleza, akifanya hivyo atayakoroga. Hofu yake hiyo inatokana na kile alichoeleza, yupo katika furaha na katika nyakati kama hizo akizungumza zaidi atayakoroga. Kauli yake hiyo inakuja w...
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka uwazi na usimamizi madhubuti wa fedha katika utekelezwaji wa mi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka uwazi na usimamizi madhubuti wa fedha katika utekelezwaji wa miradi ya umwagiliaji nchini. Majaliwa ametoa maelekezo hayo kwa watendaji watakaohusika na usimamizi wa miradi hiyo, akisisitiza kufanya hivyo kutachagiza kukamilika haraka kwa kazi hizo. Kauli ya Mtendaji Mkuu huyo wa Se...
Ili kuimarisha utaalamu na mbinu za kisheria katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao, Serikali inas
Ili kuimarisha utaalamu na mbinu za kisheria katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao, Serikali inashirikiana na Urusi kubadilishana uzoefu na elimu juu ya masuala hayo. Katika kufanikisha hilo, wataalamu kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi wamewasili nchini na kutoa mafunzo kwa wanafunzi na wanataaluma ya...
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na maendeleo shindani duniani,
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na maendeleo shindani duniani, ni muhimu taasisi za fedha za kimataifa zizingatie utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu. Msisitizo wa mkuu huyo wa nchi katika hoja yake hiyo ni kuzitaka taasisi za fedha za kimataifa kurahisisha masharti ya mikopo yake...
Utunzaji wa uoto wa asili kwenye maeneo yenye miinuko mikubwa ni moja ya mbinu zilizotajwa na wataal
Utunzaji wa uoto wa asili kwenye maeneo yenye miinuko mikubwa ni moja ya mbinu zilizotajwa na wataalamu za kupunguza hatari ya kutokea kwa maporomoko ya tope, baada ya mvua nyingi. Kwa mujibu wa wanazuoni hao waliobobea katika taaluma ya jiolojia na miamba, ingawa matukio hayo si rahisi kuyadhibiti, angalau kuepuka kuj...
Licha ya uwepo wa daraja la Zingiziwa katika Mtaa wa Zingiziwa wilayani Ilala, Dar es Salaam safari
Licha ya uwepo wa daraja la Zingiziwa katika Mtaa wa Zingiziwa wilayani Ilala, Dar es Salaam safari ya kutoka mtaa huo kwenda mwingine imekuwa kikwazo. Hiyo inatokana na mvua zinazoendelea kunyesha eneo hilo na mengine nchini, zilizosababisha daraja hilo kujaa maji na sasa yanapita juu. Kwa mujibu wa watumiaji wa daraj...
Rais Samia Suluhu Hassan amesema tathmini zinaonyesha Tanzania ipo mbioni kufikia uchumi wa kati nga
Rais Samia Suluhu Hassan amesema tathmini zinaonyesha Tanzania ipo mbioni kufikia uchumi wa kati ngazi ya juu, kutokana na mwenendo mzuri wa ukuaji uchumi. Mkuu huyo wa nchi amedokeza hilo, katika kipindi ambacho Tanzania imetambuliwa na Benki ya Dunia (WB), kuwa na uchumi wa kati ngazi ya chini. Kwa tafsiri za kiuch...
Ni wimbi la majanga lililopoka uhai wa binadamu, kuathiri makazi yao na hata kukwaza shughuli za kiu
Ni wimbi la majanga lililopoka uhai wa binadamu, kuathiri makazi yao na hata kukwaza shughuli za kiuchumi, ndiyo lugha nyepesi unayoweza kuitumia kuakisi kiwango cha athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. Mvua hizo za El-Nino zilizoanza kunyesha Oktoba mwaka jana, hadi sasa zimefululiza ...
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema 2023 ni mwaka ambao uzingatiwaji wa haki za bi
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema 2023 ni mwaka ambao uzingatiwaji wa haki za binadamu ulidorora ukilinganisha na mwaka 2022. Msingi wa tathmini hiyo ya LHRC, ni utafiti wa haki za binadamu wa mwaka 2023 ilioufanya katika mikoa 20 ya Tanzania bara na mikoa yote ya Zanzibar. Hali hiyo kwa mujibu wa r...
Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana imemuhoji kwa takribani saa tatu Mkuu wa Mkoa wa
Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana imemuhoji kwa takribani saa tatu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda. Makonda ambaye Aprili 16, mwaka huu, alitumiwa barua ya wito ikimtaka kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, mwaka huu, lakini jana Aprili 22, 2024 ndio .amefika mbele ya kamati hiyo kwa mahojiano....
Ili kudhibiti upotevu wa mali na mapato yake, Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeanzisha mifu
Ili kudhibiti upotevu wa mali na mapato yake, Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeanzisha mifumo ya kidigitali kwa ajili ya kuratibu shughuli zake. Kabla ya matumizi ya mifumo hiyo, Baraza hilo lilikabiliwa na changamoto lukuki katika urasimishaji wa rasilimali zake na wakati mwingine kushindwa kudhibiti ubadhili...
Safari ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imefikisha miongo sita, umri ambao unatajwa kuwa mrefu
Safari ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imefikisha miongo sita, umri ambao unatajwa kuwa mrefu zaidi kati ya miungano yote iliyowahi kutokea katika bara la Afrika. Mataifa hayo yaliungana Aprili 26, 1964 chini ya waasisi wake, Mwalimu Julius Nyerere kwa Tanganyika na Abeid Amani Karume kwa upande wa Zanzibar. Unaw...
Ni mkakati wa wagombea au ni mapenzi ya wanachama? Ndilo swali unaloweza kuuliza kutokana na kinacho
Ni mkakati wa wagombea au ni mapenzi ya wanachama? Ndilo swali unaloweza kuuliza kutokana na kinachoendelea katika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Katika mchakato huo, imeonekana harufu ya ushindani mkali kuelekea uchaguzi huo wa Mei, mwaka huu baada ya sehemu kubw...
Katika kutekeleza mpango wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, wauguzi kutoka Mikoa 10 nchini, wan
Katika kutekeleza mpango wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, wauguzi kutoka Mikoa 10 nchini, wanatarajiwa kupatiwa majiko ya gesi. Hatua hiyo inakuja katika kipindi ambacho Serikali imeweka mpango wa kuhama kutoka matumizi ya nishati chafu kwenda safi kwa ajili ya kupikia. Tangu kuanza kwa mpango huo, wananchi wa m...
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesema msingi wa kuimarisha muungano katika miaka 60 ijayo ni k
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesema msingi wa kuimarisha muungano katika miaka 60 ijayo ni kuhakikisha sera na mipango inayowekwa kwa pande zote mbili inajali maslahi ya wananchi, badala ya madaraka. Katika kauli yake hiyo, amesema msisitizo wa mijadala kuhusu muungano isijikite kwenye siasa, bali kwa sasa ni v...
Uimara katika usimamizi wa sekta fulani na kuwa na mchango katika taifa lake ni miongoni mwa sababu
Uimara katika usimamizi wa sekta fulani na kuwa na mchango katika taifa lake ni miongoni mwa sababu zilizotajwa na wasomi kuwa chachu ya Rais Samia Suluhu Hassan kutunukiwa shahada ya nne ya heshima ya udaktari. Kwa mujibu wa wasomi hao, mara nyingi shahada hizo hutolewa kwa mtu aliyeonyesha mchango mkubwa katika taifa...
Shughuli ya kuendesha bodaboda kwa mkataba imeingiwa na majanga, baada ya malalamiko ya madereva dhi
Shughuli ya kuendesha bodaboda kwa mkataba imeingiwa na majanga, baada ya malalamiko ya madereva dhidi ya wamiliki wakidai kupewa mikataba ya kinyonyaji. Hatua hiyo kwa mujibu wa madereva hao, inasababisha wengi waishie kunyang’anywa bodaboda wanapokaribia kumaliza mikataba hiyo na hivyo, wanabaki kuwa watumwa wa wamil...
Mtindo wa wapigakura kuwachukulia fomu wagombea ndilo jambo linaloonekana kuchagiza uchaguzi wa wana
Mtindo wa wapigakura kuwachukulia fomu wagombea ndilo jambo linaloonekana kuchagiza uchaguzi wa wanaowania nafasi mbalimbali katika Kanda nne za Chadema. Katika mchakato wa kuelekea uchaguzi huo, imeshuhudiwa wafuasi mbalimbali wakiwalipia ada za fomu na kuwachukulia wagombea mbalimbali wanaowaunga mkono. Hilo lilishuh...
Unapotaja orodha ya vyama vya siasa vyenye umri mdogo nchini, ACT Wazalendo ni miongoni mwavyo, inga
Unapotaja orodha ya vyama vya siasa vyenye umri mdogo nchini, ACT Wazalendo ni miongoni mwavyo, ingawa muda kiliyoishi unahusisha mambo mengi yanayokipa taswira isiyolingana na uchanga wake. Licha ya umri wake mdogo, ACT Wazalendo ni moja kati ya vyama vitatu vikubwa nchini na hilo linathibitishwa na wingi wa wafuasi w...
Kama utaifananisha safari ya miaka 60 kwa maisha ya binadamu, basi atakuwa amekaribia umri wa kustaa
Kama utaifananisha safari ya miaka 60 kwa maisha ya binadamu, basi atakuwa amekaribia umri wa kustaafu utumishi wa umma, ndivyo unavyoweza kusema kuakisi uhalisia wa umri wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano wa mataifa hayo yaliyounda jina Tanzania, ulifanyika Aprili 26, mwaka 1964 chini ya waasisi wake, Mwa...
Hivi unajua kuwa uwepo wa vivuko viwili vidogo vya kampuni ya Azam Marine ‘Sea Tax 1 na 2’ vinavyovu
Hivi unajua kuwa uwepo wa vivuko viwili vidogo vya kampuni ya Azam Marine ‘Sea Tax 1 na 2’ vinavyovusha abiria Kigamboni, vinaugharimu Wakala wa Huduma za Umeme na Ufundi Tanzania (Temesa) Sh5 milioni kwa siku? Kwa malipo hayo, Temesa inagharimika kulipa Sh1.8 bilioni kwa mwaka na ndicho kiasi ilichoilipa Azam Marine k...
Uhuru wa biashara, kuishi popote na muingiliano wa watu ni baadhi ya mambo yanayotajwa na wadau kuwa
Uhuru wa biashara, kuishi popote na muingiliano wa watu ni baadhi ya mambo yanayotajwa na wadau kuwa faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Faida hizo zinatajwa zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Tanzania kuadhimisha miaka 60 ya Muungano, ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa Tanganyika na A...
Wakati baadhi ya taasisi za Serikali zikilia uhaba wa bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya k
Wakati baadhi ya taasisi za Serikali zikilia uhaba wa bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kipaumbele, imebainika Sh4.05 bilioni zipo mifukoni mwa baadhi ya mashirika kwa miaka saba bila kutumika. Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, fedha hizo zipo katik...
Kikiendelea kufanya siasa zake kisasa na kutanua wigo wa kusajili wanachama na wafuasi kwenye maeneo
Kikiendelea kufanya siasa zake kisasa na kutanua wigo wa kusajili wanachama na wafuasi kwenye maeneo mbalimbali nchini, Chama cha ACT Wazalendo kitavamia mkoa wa Kilimanjaro ambao kwa muda mrefu umekuwa ukiaminika kuwa ngome ya Chadema, kufanya uzinduzi wa kishindo kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Chama hic...
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imebaini mambo manne
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imebaini mambo manne, ikiwa ni changamoto katika ufanisi wa utendaji ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco). Kulingana na hoja za Kichere katika ripoti hiyo, kati ya mambo hayo yapo yanayoliacha shirika hilo katika madeni, mgogoro na ...
Chama cha Wananchi (CUF) kimebaki kuwa miongoni mwa taasisi zilizopata hati yenye shaka kwa mujibu w
Chama cha Wananchi (CUF) kimebaki kuwa miongoni mwa taasisi zilizopata hati yenye shaka kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kuangukia kwenye orodha hiyo, baada ya ukaguzi wa CAG mwaka jana kukipa chama hicho hati yenye shaka. Ukiachana na CUF...
Hivi unajua kuwa asilimia 71 ya Wazanzibari wanaishi kwenye maeneo wasiyoyamiliki? Jambo hilo linata
Hivi unajua kuwa asilimia 71 ya Wazanzibari wanaishi kwenye maeneo wasiyoyamiliki? Jambo hilo linatajwa kukwaza upatikanaji wa fursa zikiwemo za mikopo kwa wananchi hao. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Finscope Zanzibar ya mwaka 2023, inayoeleza sababu za hali hiyo ni uwepo wa majengo mengi ya kale ambayo mara nyingi n...
Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda juu ya uwepo wa watu wakiwemo mawaziri wanaotuma watu
Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda juu ya uwepo wa watu wakiwemo mawaziri wanaotuma watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan imezua mjadala, huku ikigawa mtazamo wa Watanzania katika makundi manne. Katika makundi hayo, wapo wanaoitazama kauli hiyo kama taarifa nyeti na haipaswi kupuuzwa na vyombo vya ulinzi n...
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema miongoni mwa nyak
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema miongoni mwa nyakati ambazo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunashamiri fitina ni pale Uchaguzi Mkuu unapokaribia huku Rais aliyepo madarakani akipaswa kuendelea na muhula wa pili. Kauli ya Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli ...
Serikali imetangaza rasmi mabadiliko ya jina la Tume ya Taifa la Uchaguzi (NEC) kuwa Tume Huru ya Ta
Serikali imetangaza rasmi mabadiliko ya jina la Tume ya Taifa la Uchaguzi (NEC) kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Mabadiliko hayo yanakuja siku chache baada ya uliokuwa muswada wa sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi, kuwa sheria rasmi kutokana na kupitia michakato yote halali. Muswada wa sheria hiyo na nyingine tatu...
Msisitizo kuhusu Watanzania kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni moja ya ujumbe uli
Msisitizo kuhusu Watanzania kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni moja ya ujumbe ulioguswa katika sehemu kubwa ya hotuba za viongozi wa dini ya kiislamu wakati wa ibada ya swala ya Idd El Fitri iliyofanyika maeneo mbalimbali nchini. Pamoja na ushiriki wa waumini wa dini hiyo katika uchaguzi huo unaotara...
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema haonei aibu urafiki wake binaf
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema haonei aibu urafiki wake binafsi na sehemu kubwa ya viongozi wa vyama vya upinzani. Msingi wa kauli yake hiyo ni kile alichofafanua kuwa, huwezi kujivunia utanzania kama huna mapenzi na Watanzania wenzako, hivyo itikadi za vyama haziwezi kukwaza ura...
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa wito kwa taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha kujenga utara
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa wito kwa taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha kujenga utaratibu wa kurudisha fadhila kwa jamii, akisema kufanya hivyo ni ibada yenye tija kwa taasisi husika. Dk Tulia ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, alipozungumza baada ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Viongozi wa Seri...
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) utakaofanyika kesho hadi Januari 19, mwaka huu. Katika mkutano huo, utakaofanyika nchini Uswisi, Dk Mpango atashiriki akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, aliyebaki nchini kwa majukumu mengine. Taarifa ...
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameeleza alivyoruka kiunzi cha shinikizo la kusitisha vibali vya kua
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameeleza alivyoruka kiunzi cha shinikizo la kusitisha vibali vya kuagiza mchele kutoka Tanzania, huku akitaja sababu nne zilizochagiza asipige marufuku hiyo. Hatua ya Museveni kutakiwa kupiga marufuku uingizaji wa mchele wa Tanzania katika nchi yake, lilitokana na kile alichoarifiwa kuwa...
Licha ya bei ya sukari kufikia Sh5,000 kwa kilo katika baadhi ya maeneo nchini, Serikali imesema mwe
Licha ya bei ya sukari kufikia Sh5,000 kwa kilo katika baadhi ya maeneo nchini, Serikali imesema mwezi mmoja baadaye bidhaa hiyo inatarajiwa kurejea katika bei ya kawaida. Kurejea kwa bei hiyo kwa mujibu wa Serikali, kutatokana na hatua iliyochukuliwa na kutoa vibali kwa wazalishaji kuagiza tani 50,000 za sukari, lakin...
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ametaka kufutwa kwa miswada
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ametaka kufutwa kwa miswada ya sheria za uchaguzi inayotolewa maoni sasa, badala yake upelekwe muswada wa marekebisho ya Katiba. Miswada aliyopendekeza ifutwe ni ule wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na muswada wa sheria ya Tume ya...
Hivi unakumbuka zamani isingewezekana kijana amekalia kiti kwenye chombo cha usafiri wakati mtu mzim
Hivi unakumbuka zamani isingewezekana kijana amekalia kiti kwenye chombo cha usafiri wakati mtu mzima amesimama? Lakini wakati wa kula pia, ilikuwa haramu kwa mtoto kuanza kunawa kabla ya mkubwa na aghalabu wakubwa ndiyo waliokuwa wa kwanza kunawa hata baada ya kula. Ule utaratibu wa kumsalimu mkubwa kwa kubonyea kama ...
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa Bandari ya
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo, pale itakapokamilisha taratibu za kumpata mzabuni. Huu ni miongoni mwa mipango iliyopangwa muda mrefu na Serikali, lakini haukuwahi kuwa katika vitendo, badala yake kila awamu ilikuja na hoja zake. Dhamira ya ...
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inatarajia kutumia takriban Sh2.1 trilioni kwa ajili
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inatarajia kutumia takriban Sh2.1 trilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kukabiliana na ongezeko la mizigo bandarini. Fedha hizo ni kwa ajili ya upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam kwa kujenga gati nne, kadhalika ujenzi wa gati mbili katika mradi wa Ba...
Kama ulidhani mfanyakazi wa nyumbani ‘house girl’ ni kiumbe anayestahili majukumu makubwa bila haki,
Kama ulidhani mfanyakazi wa nyumbani ‘house girl’ ni kiumbe anayestahili majukumu makubwa bila haki, sheria inamlinda. Hii inatokana na uhalisia kwamba, waajiri wengi wa wafanyakazi wa nyumbani, huwatumikisha kazi bila kufuata utaratibu na aghalabu ni kazi inayodharaulika. Kwa taarifa yako, haki aliyonayo mtumishi wa u...
Imepita miongo mitatu bila mafanikio ya kutamatika kwa mgogoro wa ardhi kati ya Bakari Ismaili (75)
Imepita miongo mitatu bila mafanikio ya kutamatika kwa mgogoro wa ardhi kati ya Bakari Ismaili (75) dhidi ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Babati. Mzizi wa mgogoro huo ni madai ya Ismaili kwamba alinyang’anywa eneo hilo la ekari tatu analodai lilikuwa la kwake mwaka 1994 na likakabidhiwa kwa kanisa. Hata hivyo, kanis...
Huenda tabu ya usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam imebakiza muda mchache, baada ya Serika
Huenda tabu ya usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam imebakiza muda mchache, baada ya Serikali kufungua milango ya ushirikiano na sekta binafsi katika uwekezaji wa ujenzi wa miundombinu ya reli na utoaji huduma za usafiri huo. Kabla ya kufunguliwa milango hiyo, mwekezaji katika miundombinu hiyo na huduma ilibak...
Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesisitiza
Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesisitiza kuzingatiwa kwa maoni ya wadau kuhusu miswada ya sheria za uchaguzi, akisema jambo hilo lisifanyike kisaniisanii. Katika kulitekeleza hilo, amewaonya wabunge na Serikali wasicheze na maoni ya wananchi, huku wakiwataka ku...
Hatua ya bandari ya Dar es Salaam kuwa chaguo la wawekezaji, imetajwa kuchagizwa na maboresho ya miu
Hatua ya bandari ya Dar es Salaam kuwa chaguo la wawekezaji, imetajwa kuchagizwa na maboresho ya miundombinu yaliyofanyika na ujuzi wa wafanyakazi. Vingine vinavyowavutia wasafirishaji kutumia Bandari hiyo kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ni uwepo wake katika jiografia sahihi na usalama wa ...