name
stringclasses
429 values
text
stringlengths
0
767k
Kama umewahi kushangazwa na matokeo mazuri ya mwanafunzi katika mtihani wa kuvuka ngazi moja kwenda
Kama umewahi kushangazwa na matokeo mazuri ya mwanafunzi katika mtihani wa kuvuka ngazi moja kwenda nyingine ya elimu, ilhali hakuwa na historia ya umahiri darasani Mwananchi inakufichulia siri iliyojificha nyuma ya muujiza huo. Si bahati kama wengi wanavyodhani, yapo mambo mengine yanayochagiza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kipimo cha umahiri kama gazeti hili linavyobainisha baada ya kufanya uchunguzi wa kina. Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini uwepo wa mtandao wa siri wa udanganyifu katika mitihani ya taifa, unaohusisha walimu, maofisa mitihani, watumishi wengine na hata wazazi. Kulingana na uchunguzi huo, imebainika walimu wana mchango mkubwa katika hatua mbalimbali za mchakato wa mitihani, kuanzia usajili, upangaji wa mitihani hadi uangalizi, usimamizi na usahihishaji. Hata hivyo, changamoto za kiuchumi zinazowakabili walimu kutokana na maslahi kiduchu ya utumishi wa taaluma yao, ni miongoni mwa mambo yaliyobainika kuwaingiza wanataaluma hiyo katika vitendo vya udanganyifu. Mambo mengine yaliyobainika kuwa chanzo cha udanganyifu wa mitihani ni usimamizi na utawala wa shule, shinikizo la matakwa ya matokeo bora kutoka kwa wazazi na hata tamaa ya kudumisha au kukuza sifa ya shule. Inavyofanyika Mwananchi ilibaini uwepo wa ushirikiano kati ya wazazi na shule katika kuchanga fedha za kuwapa wasimamizi wa mitihani ili watoe mwanya wa udanganyifu na kupatikana matokeo mazuri. "Wengi wetu tumekata tamaa na kazi. Mazingira ya kazi hayana motisha hata kidogo ukizingatia shule zetu zinahitaji ufaulu bora. Hapa ndipo tunaposhawishika," anaeleza mmoja wa walimu mwenye uzoefu wa miaka mingi katika usimamizi wa mitihani. Mwalimu huyo aliyezungumza kwa sharti ya kutotajwa jina, anasema posho kiduchu ya kusimamia mitihani na mazingira magumu ya ualimu yanashawishi kukengeuka. Kwa mujibu wa mwalimu huyo, ushawishi wa fedha ambazo aghalabu hutolewa kwa ajili ya kuruhusu udanganyifu katika mitihani, huwa zaidi ya kima cha ujira wa kazi ya ualimu kwa mwezi. "Baadhi yetu tunafanya kazi katika mazingira magumu sana. Kwa hivyo, unapata fursa ya kusimamia mtihani wa taifa, ambapo unalipwa Sh55,000 kwa siku, Sh165,000 tu kwa siku tatu. Hapa ndipo tatizo linapoanzia," anasimulia. Kinacholipwa Mwalimu huyo anafafanua kwa baadhi ya shule msimamizi hulipwa kati ya Sh500,000 hadi Sh1 milioni kwa ajili ya kuruhusu udanganyifu ufanyike. “Ukikuta kikundi kilichojipanga vizuri kinakupa bahasha ya Sh500,000 au Sh1 milioni, utafanyaje? wanachotaka ulale au usiwe mkali. Kunakuwa na mtu bafuni wakati mtihani unaendelea," anasema. Anaeleza kwa takriban dakika nne hadi tano wanafunzi walioandaliwa huenda kuchukua matokeo kwa zamu na kugawa kwa wengine wote. Anataja tamaa ya kutaka shule ipate sifa ya kufaulisha inachangia vitendo hivyo kufanyika katika shule binafsi na hata za umma. “Baadhi ya viongozi wa shule za umma wanahusika kwa sababu zipo shule ambazo hazitaki kushusha hadhi zao, huku ubadhirifu huo ukipangwa zaidi na baadhi ya halmashauri za manispaa zilipo shule hizo,” anasema. Wengine waliohojiwa wamebainisha hali hiyo inachagizwa na ukosefu wa umahiri kitaaluma, tabia mbaya, wasiwasi, hofu, ufundishaji usiofaa, mpangilio duni wa viti na msongamano wa watahiniwa katika kumbi za mitihani. Teknolojia na mazoezi Hata hivyo, uchunguzi huo umebaini maendeleo ya teknolojia ni silaha nyingine inayotumika katika ubadhirifu huo, wengi huunda makundi ya mtandao wa WhatsApp kufnikisha shughuli hizo. Makundi hayo hurahisisha kusambaza maswali na kuyatafutia majibu kabla ya siku ya mtihani kwa ajili ya kuyagawa wakati utakapofika. Akizungumzia hilo, Mwalimu mkuu msaidizi katika moja ya shule zilizofanya vizuri jijini Dar es Salaam (jina linahifadhiwa), anasema uwepo wa simu janja umeongezeka na kuleta njia mpya za udanganyifu katika mitihani. “Sasa hivi vikundi vinaundwa mapema kabla ya muda uliopangwa wa mitihani, ujumbe mfupi wa simu unatumwa, na wakati mwingine baadhi ya maswali yanapokelewa kabla hata mtihani haujasambazwa kwa shule binafsi, imekuwa rahisi na salama zaidi kwa wadanganyifu,” anasema. Hata hivyo, anaeleza siri ya ufaulu mzuri kwa miaka mingi shuleni kwake ni kuundwa kwa kamati kati ya wazazi na uongozi wa shule kupanga njama za upatikanaji wa matokeo bora. "Tuliwaambia wazazi wachangie Sh30,000 kila mmoja wazazi na walezi wote 200 ambao watoto wao walikuwa watahiniwa waliitikia vema. Zilipatikana takriban Sh10 milioni na zilitumika kuwarubuni wasimamizi wakuu wa mitihani katika kituo chetu," anafichua. Mwalimu huyo alionyesha moja ya kundi la WhatsApp waliloanzisha baada ya kuhakikishiwa kupata maswali ya mitihani ya masomo matatu siku moja kabla ya mtihani. “Cha kushangaza ni kwamba asilimia 90 ya maswali tuliyotumwa yalikuwepo ndipo tukamlipa aliyetupa maswali hayo,” anafichua na kuongeza kuwa kila mkuu wa shule au mmiliki alitoa Sh200,000, huku kundi hilo likiwa na wanafunzi 30. Hata hivyo, alibainisha, “Necta imekuwa na nia ya dhati kwa miaka ya hivi karibuni, lakini juhudi zaidi zinatakiwa kufanyika kwa sababu wanaovujisha maswali wanapata fedha nyingi... Kwa mitihani mitatu tu, tulimpa jumla ya Sh6 milioni.” Juhudi za Serikali Rais Samia Suluhu Hassan alieleza kutoridhishwa kwake na hali ya uvujishaji wa mitihani, katika maadhimisho ya miaka 50 ya Necta Desemba 2023. Aliitaka Wizara ya Elimu na Necta, kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wizi na udanganyifu katika mitihani. Rais Samia alisisitiza umuhimu wa upimaji wa haki katika kujenga nguvu kazi yenye tija, huku akitaka hatua kali zichukuliwe ili kuondoa mianya inayoruhusu kujitokeza kwa wahitimu wasio na tija. Licha ya juhudi zinazoendelea za kupunguza ubadhirifu huo, dosari zinaonekana kuendelea. Necta imetekeleza hatua za kukabiliana na udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa shule zilizotajwa kuwa ni vituo vya udanganyifu. Mwaka 2022, shule 24 zilifungiwa na matokeo ya watahiniwa 2,194 yalifutwa kwa sababu ya majaribio yaliyothibitishwa ya udanganyifu. Mwaka 2023, watahiniwa 31 walifutiwa matokeo na kusababisha vituo viwili vya mitihani kufungiwa. Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda alikiri kuwepo kwa changamoto za uvujaji wa mitihani siku za nyuma lakini amedai kuna mafanikio katika kudhibiti hilo. “Kilichokuwa kinafanyika ni udanganyifu wa kitaasisi, ambapo shule moja inashirikiana na baadhi ya viongozi, mtihani unafunguliwa mkoa mwingine, inapigwa picha, kisha inafungwa tena na picha inapelekwa mkoa mwingine,” alifafanua. Waziri huyo alibainisha baada ya jitihada mbalimbali za udhibiti zinazofanywa na kamati za mitihani za mikoa na wilaya, rushwa imedhibitiwa na majaribio hayo yamepungua ulinganisha na zamani. Hata hivyo mmoja wa wajumbe wa kamati ya mitihani kutoka mkoa wa Shinyanga alibainisha pamoja na jitihada hizo hila zimeendelea kudumu huku akisisitiza kuwepo kwa umakini. Alisisitiza haja ya ushirikishwaji wa idara za usalama wa taifa na ujasusi kufuatilia na kuzuia vitendo viovu kabla. "Uchunguzi wa kina kabla ya mitihani ya taifa uwe unafanyika. Walengwa wawe mameneja na kamati zinazohusika na kupanga udanganyifu, unapaswa kufanywa kila wakati mwisho wa mitihani." Kuboresha mazingira ya kazi ya walimu, kuimarisha mafunzo na umahiri wao na kutekeleza hatua kali dhidi ya rushwa ni njia zinazopendekezwa kufanyika kutatua changamoto zilizopo. "Kuwekeza katika teknolojia ili kuhakikisha mchakato wa mitihani na kuhusisha vyombo vya usalama vya taifa katika ufuatiliaji makini ni muhimu ili kuzuia udanganyifu," alisema mtaalamu wa elimu, Dk Amos Majula. Alipendekeza mamlaka za Serikali, wadau wa elimu na jamii kwa ujumla zishirikiane ili kupata suluhu madhubuti itakayokomesha changamoto za kiuchumi, mifumo ya teknolojia na utovu wa nidhamu kwa walimu. "Ni wakati wa kulinda uadilifu wa mfumo wa elimu wa Tanzania na kupata mustakabali ambao mafanikio ya kitaaluma yaakisi ujuzi na uwezo wa vijana," alisema Dk Majula.
Serikali imeagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kunusuru kupanda kwa b
Serikali imeagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kunusuru kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo nchini. Hatua hiyo ya Serikali imechagizwa na ongezeko la bei na uhaba wa bidhaa hiyo katika Mikoa mbalimbali. Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la ghafla la bei ya sukari. Mathalan katika Mkoa wa Manyara kilo moja inauzwa Sh4,000 kutoka Sh3,000 ya awali. Hali ni mbaya zaidi katika Mkoa wa Arusha, ambapo bei ya kilo moja ya sukari imeongezeka kutoka Sh3,000 hadi 4,500 na Sh5,000 kulingana na wakazi wa eneo hilo. Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro, kilo moja ya bidhaa hiyo kwa sasa inauzwa kwa Sh3,800 kutoka Sh3,000 ya awali. Hata hivyo, wazalishaji wa sukari wamesema kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo viwandani, kumesababishwa na mvua za El-Nino. Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari (SBT), Profesa Kenneth Bengesi alisema kilichotokea si uhaba ni dharura ya kupungua kwa uzalishaji viwandani. Uzalishaji huo, alisema umeathiriwa na mvua za El-nino zilizosababisha viwanda vingi kusimama kuzalisha. “Mvua ina athari kubwa kwenye uzalishaji wa sukari kwa sababu mashamba ya miwa mengi yapo mabondeni, ikinyesha mvua kubwa miwa inanyonya na inapunguza sukari. “Lakini uvunaji unakuwa mgumu huwezi kuingiza trekta kwa sababu yatakwama na miundombinu ya kuifikia miwa ni changamoto nyingine iwapo mvua zinanyesha ina haribika zaidi,” alisema. Kwa kuzingatia kwamba mvua zinaweza kuendelea, Profesa Bengesi alisema Serikali imeshaagiza tani 50,000 za sukari nje ya nchi kwa ajili ya tahadhari. Lingine lililofanyika, alisema ni kuhakikisha viwanda vyote vinarudi kuzalisha na tayari hilo limeanza kutekelezwa, hivyo siku chache baadaye kinachotokea sasa kitakwisha. Hatua nyingine kwa mujibu wa Profesa Bengesi, ni kuwaonya wafanyabiashara wanaotumia mwanya wa kupungua kwa uzalishaji, kupandisha bei, ilhali viwandani bei haijaongezeka. “Waache tabia hiyo wanawaumiza wananchi, Serikali haitakaa kimya kuona wananchi wake wanaendelea kuuziwa sukari kwa gharama kubwa ilhali bei za viwandani haijaongezeka,” alisema. Kuhusu changamoto ya uzalishaji, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mkulazi Holding ltd, Selestine Some alitaja mvua za El-nino kuwa sababu ya kupunguza uzalishaji wa sukari viwandani. “Oktoba hadi Desemba ndiyo vipindi vya uzalishaji mkubwa wa sukari. Katika vipindi hivyo mvua zinaendelea kunyesha, zinaponyesha inabidi msubiri ikate ndiyo muendelee. “Kwa mfano sisi (Mkulazi) tulikuwa tunafanya matengenezo na tukapanga leo (jana) tuanze uzalishaji, usiku imenyesha mvua kubwa tumeshindwa kuzalisha,” alisema. Kulingana na Some, hakuna sababu nyingine ya kuadimika na kupanda kwa bei ya sukari, zaidi ya kupungua kwa uzalishaji kulikosababishwa na mvua zisizotabirika. Hata hivyo, alieleza uhaba uliopo si mkubwa na unaweza kumalizwa kwa viwanda vya ndani pekee. “Deficit (uhaba) sio kubwa ni vile tu viwanda vimepunguza uzalishaji sababu ya mvua, lakini tukizalisha kawaida ni jambo linalokwisha mara moja,” alisema. Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli alisema hivi karibuni Serikali inatarajia kutoa taarifa za kina kuhusu changamoto hiyo inayoendelea. "Tumesikia kuhusu jambo hilo na tunalifanyia kazi, hivi karibuni tutatoa taarifa ya kina kupitia Bodi ya Sukari (SBT)," alisema. Alipoulizwa kuhusu sababu za hali hiyo, alisema hayo yote yatabainishwa kupitia taarifa hiyo.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema athari za vita na Ugonjwa wa Uviko-19, ndizo zilizochagiza mdororo
Rais Samia Suluhu Hassan amesema athari za vita na Ugonjwa wa Uviko-19, ndizo zilizochagiza mdororo wa kiuchumi duniani kwenye sekta ya uzalishaji na hatimaye kuathiri upatikanaji wa Dola za Marekani. Rais Samia ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Desemba 31, 2023 alipotoa salamu za mwaka mpya 2024 kwa Watanzania. Amesema majanga hayo yameongeza gharama na mfumuko wa bei kwa bidhaa za msingi kama chakula na mafuta ya vyombo vya usafiri na mitambo. “Hali hii kwa ujumla imevuruga mnyororo wa ugavi wa kimataifa. Riba kwenye masoko ya fedha imepanda na upatikanaji wa Dola za Marekani pia umeathiriwa,” amesema. Katika kukabiliana na hali hiyo, Rais Samia amesema Tanzania ilinza kutekeleza sera madhubuti za fedha ili kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa bei. Sera hizo pia, amesema zimechochea ukuaji na kuimarisha udhibiti katika sekta hiyo ya fedha. “Tumeendelea kudhibiti mfumuko wa bei, ambao katika kipindi cha Januari hadi Novemba, 2023 ulipungua hadi wastani wa asilimia 3.9 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 4.3 kipindi kama hicho mwaka jana,” amesema. Pato la taifa mwaka 2023 amesema lilikadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.7 mwaka 2022. Katika mwaka 2022/23, Serikali ilipokea Sh1.3 trilioni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo, sawa na asilimia 100 ya kiasi kilichopangwa kukopwa. “Deni la Taifa limeendelea kuwa himilivu. Uwiano wake kwa pato la Taifa, kwa thamani ya sasa, ni asilimia 35.6 ukilinganisha na ukomo wa asilimia 50,” amesema. Kwa upande wa ukusanyaji wa kodi, kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2023, amesema makusanyo yalifikia Sh22.6 trilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia nane ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2022. “Jinsi uchumi wetu unavyokua, tutaendelea kuongeza makusanyo kupitia mifumo madhubuti ya ukusanyaji na kuhakikisha kodi inakusanywa kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria,” amesema.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatakubali kuzibwa au kuongozwa na itikadi za kisiasa k
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatakubali kuzibwa au kuongozwa na itikadi za kisiasa katika kazi ya Mungu. Mbowe alitoa kauli hiyo mkoani Kilimanjaro jana, alipoongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa kanisa la Bethel, Usharika wa Nshara wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambalo yeye ni muumini pia. Katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa, Serikali na wafanyabiashara, zimepatikana zaidi ya Sh817 milioni. Mwanasiasa huyo alisema ni lazima kuungana kupitia kazi ya Mungu, kwani mambo mengi yatawezekana kufanyika. Alisema katika harambee hiyo aliwafikia wengi takriban watu 250 wakiwemo wale ambao wana itikadi tofauti za kisiasa na kwamba hakuna aliyegoma kuchangia. “Hatukubali kuzibwa kwa sababu za kisiasa na hatukubali kuongozwa na itikadi za kisiasa katika kazi ya Mungu, kwa hiyo ni lazima tusaidiane kwa pamoja,” alisema. Miongoni mwa viongozi aliowafikia, alisema ni Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko, Mawaziri kadhaa na wabunge bila kujali mipaka ya vyama. "Wengine wameshanitumia michango yao na wengine wameniahidi kunitumia michango yao wengine wanaendelea kunitumia michango yao,” alisema. Askofu Shoo Akiongoza ibada hiyo, Askofu Fredrick Shoo aliwataka watanzania kuendelea kumwamini Rais Samia kwa kuwa amekuwa akiwaunganisha wananchi bila kujali itikadi zao za dini na siasa. Alitumia jukwaa hilo, kuwataka wale ambao bado hawajamuelewa mkuu huyo wa nchi wamuelewe vizuri bila kujali vyama walivyopo. "Umeendelea kuugusa moyo wangu na tumezidi kuuona moyo wake kwa kuwapenda wananchi wake wote bila ubaguzi, lakini na hili nimelisema mwanzoni, wale ambao hamjamuelewa Rais Samia Suluhu Hassan vizuri bila kujali upo chama gani mueleweni yule mama vizuri," alisema. Alikwenda mbali zaidi na kueleza, uwepo wa kiongozi huyo umetokana na matakwa ya Mungu: " Mungu amemleta huyu mama kwa makusudi yake, moyo wa huyu mama ni wa tofauti sana, huyu ni mcha Mungu na ndio maana aliposhirikiswa sio hapa tu na mahali pengine pote tumeona akitoa anapoamini ni kazi ya Mungu.” “Ametoa kwa moyo wa upendo si kwa wakristo, waislam ,mama ametoa ni kwasababu yeye ni mcha Mungu na anataka kutuambia 'massage' ni ile ile kwenye jambo lile lile tusibaguane kivyama tusibaguane kiitikadi ,Mungu hana uitikadi," alisema Askofu Shoo. Profesa Mkenda Alipopata nafasi ya kuzungumza, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alieleza namna Mbowe alivyompigia simu na kumwalika, huku akimhoji iwapo tofauti ya itikadi zao za kisiasa zinakwamisha hilo. Katika maelezo yake, Profesa Mkenda alisema kunahitajika mshikamano katika masuala ya kijamii bila kujadi itikadi za kisiasa. "Wakati mbowe ananipigia aliniambia tuna tofauti zetu za kiitikadi na kisiasa zitakuwa sababu za wewe kutokuja, baba askofu, mambo mengi ya kijamii na yote ya kijamii kwa uongozi wenu tunataka mshikamano bila kujali itikadi zetu za kisiasa," alisema. Mwingine aliyezungumza katika harambee hiyo ni Mbunge wa Hai, Saasisha Mafue aliyempongeza Rais Samia kwa kuchangia Sh150 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo. "Kwanza tunamshukuru sana Mungu kwa kutupa kibali cha kuweza kushiriki kwenye umaliziaji wa jengo hili la kanisa letu la hapa KKKT Nshara ambalo ni Bethel. “Lakini kubwa tunamshukuru Rais Samia kwa kutuunga mkono kwa kutuchangia Sh150 milioni, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ametupatia Sh10 milion, Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko naye Sh10 milioni," alisema. Alijumuisha pongezi hizo kwa viongozi wengine akiwemo Profesa Mkenda, wabunge Halima Mdee na Esta Bulaya ambao pia walikuwepo kanisani hapo.
Saa 22 ziligeuka shubiri kwa wakazi wa Mtaa wa Mwanamtoti Darajani, Mbagala jijini Dar es Salaam, ku
Saa 22 ziligeuka shubiri kwa wakazi wa Mtaa wa Mwanamtoti Darajani, Mbagala jijini Dar es Salaam, kutokana na eneo hilo kubainika kitu kilichodaiwa kuwa bomu. Hali hiyo ilizua hofu kwa wakazi hao, kutokana na kile walichoeleza imechukua muda mrefu kwa Jeshi la Polisi kuliondoa bomu hilo, licha ya kuarifiwa mapema. Kulingana na wakazi hao, bomu hilo lilionekana saa 11 jioni na saa 12 walikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Maturubai Mbagala, lakini jeshi hilo liliishia kuzungusha utepe katika nyumba lilipokuwepo na kuahidi kuliondoa kesho yake. Hofu zaidi ilitokana na kile walichoeleza, hata ilipofika kesho (jana) bomu hilo halikuondolewa hadi saa 9 alasiri, hivyo imechukua saa 22 kuondolewa. Ule usemi wa uking’atwa na nyoka hata jani litakustua, umeakisi maisha ya wakazi hao, kwani bomu hilo linashuhudiwa ikiwa ni miaka 14 imepita, tangu eneo hilo lilipokumbwa na milipuko ya mabomu iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 20, kujeruhi zaidi ya 200 na kuwaacha wengine bila makazi. Hadi Mwananchi Digital inaondoka katika eneo la tukio, yalipita masaa 17 bila hatua za kuteguliwa bomu hilo kuchukuliwa na alipotafutwa Kamanda wa Polisi Temeke, John Malulu alisema wameshawasiliana na mamlaka husika kulitekeleza hilo. “Tumewasiliana na mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi, lakini wananchi wana haki ya kulalamika. Wametoa taarifa tangu jana jioni (Desemba 30) hadi sasa (Desemba 31, saa 7 mchana) bomu halijateguliwa,” alisema. Hata hivyo, baadaye Mwananchi iliarifiwa kuwa bomu hilo liliondolewa saa 9 alasiri na watu waliovalia mavazi ya kawaida. Eneo la tukio kabla ya bomu kuondolewa Mwananchi Digital jana ilifika katika eneo la tukio na kushuhudia watoto wakicheza karibu na utepe wa polisi, huku wananchi wakiingia mara kwa mara kuonyeshana bomu hilo bila tahadhari yoyote. Si hivyo tu, mahali lilipo bomu hilo ni sentimita chache kutoka ilipo nyumba ya vyumba viwili yenye wakazi wawili, lakini ni mita chache (takriban tano) kutoka katika makazi mengine ya watu. Mwandishi wa habari hii alishuhudia takriban nyumba 15 zenye wakazi muda wote, zilizozunguka eneo hilo. Badala ya kukaa mbali na eneo hilo, Mwananchi Digital ilishuhudia wakazi wengi wakisalia katika makazi yao, kwa kile walichoeleza kubaki kwao nyumbani ni kuchukua tahadhari. “Tumebaki nyumbani tunajua watoto wetu hawasikii ni watundu mno. Utamwambia usiende pale kuna hatari, mwenzio ndiyo anaenda akajue hatari gani. Ule utepe uliowekwa na polisi haumzuii mtu kuingia,” alisema Fatma Twaha mkazi wa eneo hilo. Kazi zimekwama Hamis Seif ni mkazi wa nyumba hiyo lilipokutwa bomu hilo, alisema ameshindwa kwenda kazini kwa kuwa nyumba yake imezungushiwa utepe. Seif alisema alirudi nyumbani usiku na kukuta utepe nyumbani kwake, baadaye majirani walimpa taarifa kuhusu bomu na kwamba haruhusiwi kuingia ndani kwake hadi litakapoteguliwa. “Wameahidi leo wangekuja kulitegua lakini hadi sasa bado nimelala hapa nje nasubiri liteguliwe niingie ndani mambo mengine yaendelee. “Wananikwamisha nashindwa kwenda kwenye mihangaiko yangu,” amesema Seif. Mkazi mwingine wa eneo hilo, amesema matarajio yake ni kuona mamlaka zikichukua hatua ili kuepuka kujirudia kwa yale yaliyotokea mwaka 2019. Serikali ya Mtaa Mjumbe wa Mtaa huo, Rehema Omary alieleza kushangazwa na polisi kuchelea kulitoa bomu hilo licha ya kuarifiwa mapema. “Lingekuwa kwenye maeneo yenye watu wenye hadhi fulani wangeshalitoa, lakini wanajua lipo kwenye nyumba ya wakazi wa hali duni ndiyo maana hawachukulii umuhimu,” alisema mjumbe huyo. Alisema hali hiyo inawaacha kwenye hofu hasa, ukizingatia eneo hilo lina kumbukumbu ya kulipukiwa na mabomu. Polisi Akizungumza na Mwananchi kabla ya bomu hilo kuteguliwa, Malulu alikiri jeshi hilo kupokea taarifa tangu jana na kwamba wananchi wana haki ya kulalamikia juu ya hatua kuchelewa kuchukuliwa. Lakini, alisema tayari jeshi hilo limeshawasiliana na mamlaka zinazohusika na uteguzi wa mabomu kwa ajili ya hatua zaidi. Hili ndilo bomu lenyewe Kulingana na tovuti ya American Grenades and Ordance, bomu hilo linatambulika kwa jina la MK 2 Grenade ambalo aghalabu huwa na uzito wa gramu 52 na ukubwa wa milimita 9.5. Bomu hilo, huwa na pini maalum ya usalama inayozuia kulipuka na inapotolewa huchukua kati ya sekunde mbili hadi sita kulipuka. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, bomu hilo lina uwezo wa kuuwa umbali wa mita 10 kutoka lilipo iwapo litalipuka. Kadhalika lina uwezo wa kujeruhi kuanzia umbali wa mita 20 hadi 200. Bomu hilo, lililotengenezwa miaka ya 1950, asili yake ni Marekani na ni miongoni mwa silaha zilizotumika katika vita mbalimbali ikiwemo Vita vya Pili vya Dunia, Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini China, Vita vya Korea na Vietnam.
Kukithiri kwa matukio ya vifo vya watu wa familia moja kutokana na ajali, kunatajwa kusababisha maba
Kukithiri kwa matukio ya vifo vya watu wa familia moja kutokana na ajali, kunatajwa kusababisha mabadiliko ya mtindo wa kusafiri kwa wanafamilia katika siku za hivi karibuni. Mabadiliko hayo, yanahusisha kuwagawa ndugu katika usafiri tofauti badala ya ilivyozoeleka kwamba kwa safari moja familia hutumia usafiri wa pamoja. Ingawa mtindo huo unaonekana mpya kwa siku za hivi karibuni, wakongwe wamesema ulitumika zaidi zamani na kwamba ilikuwa uchuro familia kusafiri kwa usafiri wa pamoja. Kurejewa kwa mtindo huo wa kale wa kusafiri kwa familia kumetokana na mfululizo wa matukio ya ajali yaliyoondoa uhai wa ndugu kadhaa wa familia moja katika maeneo mbalimbali nchini. Juzi, Diwani wa Kabuku, Nurudin Semnangwa alipoteza mke, mtoto na dada wa kazi baada ya ajali ya gari aina ya Alphard walilokuwa wakisafiria, kugongana na lori mkoani Tanga. Agosti 3, mwaka huu, ndugu wanne wa familia moja walipoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Prado, walilokuwa wakisafiria lilipogongana uso kwa uso na Scania. Wanne hao ni Siah Msuya (53), Diana Sukulu Mageta (47), Dk Norah Msuya (45) na Neech Msuya, waliokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Same, mkoani Kilimanjaro. Si hao tu, Aprili 24, mwaka huu, ajali ya gari ilikatisha uhai wa ndugu watatu wa familia moja, baada ya usafiri walioutumia kusombwa katika barabara ya Arusha-Moshi wilayani Arumeru mkoani Arusha. Waliofariki katika ajali hiyo ni Angela Metili (26), Martha Metili (40) na Lisa Metili (8) mwanafunzi wa shule ya Msingi Ilboru Arusha. Kama hiyo haitoshi, ndugu wanne wa familia moja walifikwa na umauti mkoani Mtwara Julai 2, mwaka huu, baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongwa kwa nyumba na gari aina ya Fuso. Waliofariki katika ajali hiyo ni Omega Danford, Mosses Danford, Norah Mpili na Danford Milanzi. Kubwa zaidi ni tukio la Februari 14, mwaka huu lililopoteza maisha ya watu 12 wa familia moja baada ya gari walilokuwa wakisafirishia msiba wa baba yao kupata ajali. Waliofariki katika ajali hiyo ni Augustina Mrema, Nestory Mrema, Lizybetha Lamasey, Elizabeth Mrema, Godwin Mrema, Kenedy Mrema, Avelina Mrema, Emiliana Mrema, Rozina Lamosai, Suzana Mrema, Julietha Mrema na Ethan Peter. Wengine watatu wa familia moja walifikwa na umauti baada ya gari walilokuwa wamepanda (Toyota Hilux) kugongwa na gari lingine, wilayani Namtumbo katika Mkoa wa Ruvuma. Wanne wengine wa familia moja walipoteza maisha Dumila mkoani Morogoro, kwa ajali iliyohusisha gari walilokuwa wamepanda aina ya Toyota Spacio lililogongana na Lori. Wabadili mbinu Juzi Disemba 28, 2023 Mwananchi ilishuhudia familia ya Jonson Kasevela, Mkazi wa Dar es Salaam ikiwagawa wanafamilia wake katika mabasi manne tofauti ili kuepuka wasisafiri kwenye basi moja kutoka Iringa. Mmoja wa watoto wa familia hiyo, Ayubu Kasevela alisema baba yake aliwataarifu mapema kwamba hawatasafiri pamoja kutokana na visa vya baadhi ya wanafamilia kuteketea pamoja ajalini. “Tumesafiri watu nane, baba na mama wameondoka na gari ya nyumbani, sisi wametugawa kwenye mabasi manne tofauti, mawili amepanda mmoja mmoja na mengine wawili wawili. Hii ni nzuri hata mimi nitaiga,” alisema Ayubu. Alisema vifo vya jirani zao zao, waliopoteza maisha mwaka 2020 Mkoani Tanga wakati wanaenda kwenye mahafari ya mtoto wao viliwafanya waache mtindo wa kusafiri pamoja. “Walikuwa jirani zetu, waliteketea wote kwa pamoja na kumuacha binti yao Anna Zambi ambaye hakuwa nao. Kama wangetengana haya yote yasingetokea,” alisema Ayubu. Ksevela alisema kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akisafirisha familia yake kwenye magari tofauti ili hata inapotokea ajali, wasidhulike wote. “Hata zamani wazee wetu walfanya hivi, kinachotuponza ni ukisasa kwa sababu familia wanamiliki gari basi wote wanajazana humo na kuondoka. Hakuna sababu, wengine wasafiri kwa mabasi tu,” alisema na kuongeza; “Nilikuja likizo na familia yangu na tunaondoka kurudi Dar, nimewagawa wote lakini yote kwa yote Mungu ndiye anatulinda.” Mtazamo wa wahenga Zamani ilikuwa uchuro kwa kundi la familia moja kusafiri kwa chombo kimoja cha usafiri, ilitafsiriwa kama uchuro, kama anavyofafanua Chifu wa Wachaga, Mangi Marealle. Sababu ya hatua hiyo si uchuro kama ilivyokuwa inatamkwa, bali alisema ni tahadhari iwapo itatokea hatari yoyote ndugu wote wasiathirike. “Tulikuwa tunafanya vile kuchukua tahadhari. Ili ikitokea ajali familia moja isiathirike zaidi. Ilikuwa si rahisi watu watatu au wanne wa familia moja kupata ajali pamoja,” alisema. Ingawa ni utaratibu wa kale, Marealle alishauri udumishwe kwani uliokoa na utaokoa familia nyingi dhidi ya athari za majanga ya pamoja. Hata hivyo, alieleza hilo halikufanyika kwa usafiri pekee, hata njia ya kupita iwapo familia inakwenda safari moja. Walijigawa ili likitokea lolote wasiathirike wote. Dereva wa magari makubwa, Abdulkadir Hussein alisema binafsi haoni hatari kusafiri na familia ikiwa dereva atakuwa makini. “Mambo ya muhimu ni kuhakikisha kuwa gari ni nzima, ukaguzi ufanyike kabla ya safari, dereva awe anajua mazingira ya hiyo barabara lakini kikubwa mwendo uwe wa wastani na sheria za barabarani dereva azingatie,” alisema na kuongeza; “Dereva asifanye mambo ya kipuuzi kama ulevi, mwendo kasi, kelele za mziki kwenye gari, kusimama hovyo barabarani na usingizi. Usingizi umeua watu wengi kwa ajali.” Mhadhiri wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Mabula Mkuba alieleza kisaikolojia binadamu ameumbwa kutafuta mbinu ya kuendana na jambo iwapo imekosekana namna ya kulidhibiti. Kuhusu ajali hasa za familia moja, Dk Mkuba alisema inaonekana zimeshindwa kudhibitiwa, hivyo mabadiliko ya mtindo wa usafiri kwa wanafamilia ni mbinu ya kuendana na tatizo. “Ni kwamba ajali zipo, tatizo lipo na watu bado mnataka kusafiri. Kwa hiyo imetafutwa mbinu ya kuendana na hali iliyopo kwa kupunguza kiwango cha athari,” alisema. Alieleza hilo ni jambo la kawaida kwa kila binadamu kwa sababu amepewa ufahamu huo.
Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Wanawake Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Em
Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Wanawake Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Emmanuel Silanga kuhusu eneo la uchimbaji madini mkoani Simiyu, umefika mwisho. Hatua ya kufika mwisho kwa mgogoro huo, imetokana na Serikali ya mkoa wa Simiyu kuingilia kati na kuamua uendeshaji wa leseni hiyo ufanywe kwa ubia kati ya Silanga na Tawoma. Awali ilidaiwa mzizi wa mgogoro huo ni mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji kwenye mgodi wa Dutwa Namba 10 ambao, Silanga ndiye mwenye leseni halali. Hata hivyo, imeelezwa Tawoma walikuwa wakiendesha shughuli zao kwenye mgodi huo huku wakidai sehemu ya mrabaha licha ya kutokuwa na umiliki. Akizungumza baada ya kutatua mgogoro huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda alisema kuanzia sasa shughuli zote za uendeshaji wa leseni ya mgodi huo zitafanywa kwa ubia. “Kuanzia Jumatatu tumekubaliana shughuli zote za usimamizi zitafanywa na kina mama hawa, ninachowaomba kama kukiwa na jambo lingine lolote fikeni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa,” alisema. Alieleza dhamira ya uamuzi huo ni kuhakikisha maslahi ya pande zote yanapatikana, kwa kuwa wote wanalipa kodi na ushuru serikalini. “Mkianza tena mambo ya sintofahamu mrudi tena ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wala msiite vyombo vya habari, ili tumalize mgogoro, nilitumwa na chama changu (CCM) nimalize tatizo hili na nashukuru nimemaliza,” alisema. Kwa upande wake, Silanga alisema haukuwa mgogoro mkubwa japo ulichagizwa na masuala ya kisiasa na kwamba, amekuwa tayari kufanya shughuli kwenye mgodi huo kwa kushirikiana na Tawoma. Hata hivyo, ameagiza kuwa ni lazima uwepo ushirikishwaji wa wanawake wadau wa madini wa mkoa wa Simiyu na isiwe kwa maslahi ya kikundi cha wachache kama ilivyo sasa. “Hawa kina mama wasitumiwe na wanasiasa wanaoweza kuharibu taswira ya Simiyu, mimi ninamiliki leseni halali hapa na nimewaalika tushirikiane kufanya kazi. Nahitaji ushiriki wa wanawake wengi zaidi ndani ya mkoa wetu, isiwe kikundi cha watu wachache tu. Nawapenda sana kinamama zangu kwa sababu mimi ni baba natakiwa niwatunze nao watutunze,” amesema Silanga. Mwenyekiti wa Tawoma, Nimeri Chacha alisema wamepitia magumu mengi lakini Mkuu wa Mkoa na viongozi wa CCM wamepambana kuwafikisha katika hatua hiyo. “Wametupigania hatimaye leo tumekuja kupata haki yetu, tunashukuru sana CCM Mkoa huu wa Simiyu,” alisema.
Kama kwako Krismas ilikwenda sawa ni jambo la kumshukuru Mungu, maana wapo iliyowaacha na huzuni, ik
Kama kwako Krismas ilikwenda sawa ni jambo la kumshukuru Mungu, maana wapo iliyowaacha na huzuni, ikiwemo familia ya Isaya Ndindindi, iliyopoteza vijana wawili katika fukwe za Bahari ya Hindi. Vijana hao, Elisha Isaya (18) na Richard Robert (14) walipoteza maisha walipojaribu kuvuka katika moja ya mikondo ya bahari hiyo ili wakaogelee karibu na fukwe ya South ‘South Beach’ eneo la Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulingana na ndugu wa marehemu, kabla ya uamuzi wa vijana hao kwenda katika fukwe walionywa kuhusu kwenda baharini, kwa kuwa ni maeneo hatari kwa usalama wao. Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema lilishatoa tahadhari kuhusu wanaokwenda kuogelea katika siku za sikukuu, bahati mbaya watu hawazingatii. Kadhalika, Jeshi hilo limesema mbali na wawili hao waliopoteza maisha, halijapokea taarifa nyingine yoyote mbaya iliyotokea katika sikukuu hiyo ya krismas. Akisimulia tukio hilo jana, dada wa marehemu, Pili Isaya alisema ndugu zake hao waliianza safari kutoka nyumbani kwenda katika fukwe hizo, muda mchache baada ya kupata chakula cha mchana. “Hawakuwa nyumbani. Walikuwa eneo la jirani, chakula kilipokuwa tayari waliitwa kwa ajili ya kuja kula. Baada ya kula walipigiana simu na wenzao wakaenda kuogelea baharini,” alisema Pili. Dada huyo alieleza tangu walipoonekana wakati huo, hawakuwaona tena hadi baadaye saa 11 jioni, vijana waliokuwa nao baharini waliporudi nyumbani kutoa taarifa ya kuzama kwa wenzao. Kilichotokea kinaakisi msemo wa ‘sikio la kufa halisikii dawa’ kwa kile kilichoelezwa na Pili kuwa, kabla ya safari ya vijana hao mama yao aliwazuia kwenda baharini kuogelea, ili kuepuka madhira yoyote. “Baada ya kula mama aliwaambia wasiende baharini kwa wanaweza kupatwa na tatizo lolote. Lakini walipigiana simu na wenzao wakaamua kwenda bila taarifa,” alisema. Mshuhuda Aboubakar Ismail ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema safari yao kwenda baharini, ilitokana na simu aliyopokea kutoka kwa rafiki yake Elisha (kwa sasa ni marehemu). “Elisha alinipigia simu akasema twende baharini tumpeleke mgeni (Richard ambaye pia ni marehemu) kuona mazingira na tukaogelee naye, tukaenda tukiwa wanne,” alisema. Alisema kabla ya kufika katika eneo lenye watu wengi wanaoogelea inakupasa kuvuka mkondo na walipofika eneo hilo, Elisha aliwaambia anajua kuogelea hivyo ataanza kumvusha mgeni kisha atawarudia wengine. Harakati za kumvusha mgeni zilianza, alisema baada ya kufika katika kina kirefu Richard alikunywa maji na ndipo alipomkumbatia Elisha. Baada ya purukushani za kukumbatiana, Ismail alisema wawili hao walishuhudiwa wakihangaika yaani wanazama na kuibuka ndani ya kina hicho kirefu cha maji. Kulingana na Ismail, hali hiyo ilimlazimu kujitosha ndani ya maji kujaribu kuwaokoa, lakini alishindwa kwa kuwa hawezi kuogelea. Mwenzake naye alijitosha kwenda kuwaokoa, lakini alisema naye hakufanikiwa kwani alipofika walipo, Richard alimshikilia nguo kiasi cha kushinda kutoka. “Richard alimshika nguo mwenzangu ikabidi aivue ili ajiokoe, akafanikiwa kutoka na tulipoona tunashindwa tukaenda kutoa taarifa kwa wavuvi walikuwa jirani wakati wanaendelea kuwatafuta, sisi tulirudi nyumbani kutoa taarifa,” alisema. Licha ya juhudi zote, Ismail alisema walipofika eneo hilo na familia hawakufanikiwa kuona chochote, isipokuwa taarifa zilitolewa kwa Jeshi la Polisi na masaa matano baadaye mwili wa Richard ulionekana kando ya fukwe hiyo. Baada ya mwili wa Richard, Ismail alisema mwili wa Elisha ulionekana saa 11 alfajiri ya kuamkia jana. Polisi Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo alisema tahadhari ilitolewa kabla ya sikukuu kuhusu watu wanaokwenda kujifunza kuogelea. “Haiwezekani hujui kuogelea eti siku ya sikukuu ndiyo uende kuingia kwenye maji kuogelea. Tulitoa tahadhari mapema kuepuka madhira kama haya,” alisema. Alipoulizwa kuhusu matukio mengine katika sikukuu hiyo, Murilo alisema zaidi ya wawili hao waliopoteza maisha hakupokea taarifa nyingine yoyote. “Mkoa wa Dar es Salaam upo shwari sijapokea taarifa nyingine yoyote kuhusu Krismas kikubwa watu wazingatie tahadhari tunazotoa wakati huu wa sikukuu,” alisema.
Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Emmanuel Si
Hatimaye mgogoro kati ya Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Simiyu (Tawoma) dhidi ya Emmanuel Silanga kuhusu eneo la uchimbaji madini mkoani Simiyu, umefika Mwisho. Hatua ya kufika Mwisho kwa mgogoro huo, imetokana na Serikali mkoani humo kuingilia kati na kuamua umiliki wa mgodi huo uwe kwa ubia kati ya Tawoma na Silanga. Akizungumza baada ya kutatua mgogoro huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda alisema kuanzia sasa shughuli zote za uendeshaji wa leseni ya mgodi huo zitafanywa kwa ubia. “Kuanzia Jumatatu tumekubaliana shughuli zote za usimamizi zitafanywa na kina mama hawa, ninachowaomba kama kukiwa na jambo lingine lolote fikeni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa,” alisema. Alieleza dhamira ya uamuzi huo ni kuhakikisha maslahi ya pande zote yanapatikana, kwa kuwa wote wanalipa kodi na ushuru serikalini. “Mkianza tena mambo ya sintofahamu mrudi tena ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wala msiite vyombo vya habari, ili tumalize mgogoro, nilitumwa na chama changu (CCM) nimalize tatizo hili na nashukuru nimemaliza,” alisema. Mmiliki mwenza wa mgodi huo, Silanga alisema haukuwa mgogoro mkubwa, isipokuwa ulichagizwa na hatua ya usikilizwaji kufanyika kwa upande mmoja. Hata hivyo, aliwataka Tawoma kuacha kuwasikiliza baadhi ya wanasiasa ili kuepuka kuichafua taswira ya Mkoa wa Simiyu. “Hawa kina mama wasitumiwe na wanasiasa wanaoweza kuharibu taswira ya Simiyu, kina mama mimi nawapenda sana kwa sababu mimi ni baba natakiwa niwatunze nao watutunze. “Haukuwa mgogoro, ilikuwa ni lugha gongana lakini dhamira yetu ni kuwaendeleza kina mama na hilo tunaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa hiyo mimi nitakuwa napata ripoti kutoka kwa wakina mama,” alisema. Mwenyekiti wa Tawoma, Nimeri Chacha alisema wamepitia magumu mengi lakini Mkuu wa Mkoa na viongozi wa CCM wamepambana kuwafikisha katika hatua hiyo. “Wametupigania hatimaye leo tumekuja kupata haki yetu, tunashukuru sana CCM Mkoa huu wa Simiyu,” alisema.
Joto la Uchaguzi Mkuu katika taifa la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, linaendelea kupanda, huku Watan
Joto la Uchaguzi Mkuu katika taifa la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, linaendelea kupanda, huku Watanzania wakisisitiza umuhimu wa amani ili kulinda uhusiano wa kibiashara na kindugu baina ya wananchi wa mataifa hayo. Kupanda kwa joto hilo la uchaguzi wa Desemba 20, mwaka huu kunatokana na ukweli kwamba, zimesalia siku chache kabla ya wananchi wa DR Congo kupiga kura ya kumchagua Rais, Wabunge wa kitaifa, majimbo na madiwani. Wanazuoni wa uchumi na baadhi ya Wakongo waliopo nchini Tanzania, wanautazama uchaguzi huo kuwa ndiyo utakaoamua ama kuimarisha au kuzorotesha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo jirani na wananchi wake wanaohusiana kwa miongo kadhaa. Uhusiano kibiashara Uchaguzi huo, unafanyika katika kipindi ambacho mauzo ya Tanzania nchini DR Congo yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 18 katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Ongezeko hilo ni kutoka Dola za Marekani milioni 7.53 mwaka 1997 hadi kufikia Dola za Marekani milioni 280.54 mwaka 2022, kwa mujibu wa takwimu za kanzidata ya Shirika la Umoja wa Mataifa la COMTRADE. Sambamba na hilo, takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), zinabainisha taifa la DR Congo limewekeza miradi 19 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 463.34 nchini Tanzania. Ingawa mataifa hayo yanapakana, pia raia wake wanaunganishwa na lugha ya Kiswahili. Zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania ni wazungumzaji wa Kiswahili. Upande wa DR Congo inakadiriwa asilimia 40 ni wazungumzaji wa lugha hiyo hasa waliopo katika Mikoa ya Mashariki mwa nchi hiyo. Uhusiano wa mataifa hayo umekwenda mbali zaidi Septemba mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilipotangaza kuondoa viza kwa raia wote wanaotoka Congo DR. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa nchini Tanzania ya mwaka 2020, Congo DR, ndiyo nchi jirani inayoongoza, ikiwa ni zaidi ya asilimia 30 ya mizigo yote. Mtazamo kiuchumi Uchaguzi huo unapaswa kuendeleza amani baina ya mataifa hayo kwa kuwa Congo DR ni turufu ya uchumi kwa Tanzania kama anavyofafanua Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu Mzumbe nchini Tanzania, Profesa Aurelia Kamuzora. Mchumi huyo anasema Congo DR ni miongoni mwa nchi zisizo karibu na bahari, hivyo itaendelea kutumia zilizopo Tanzania iwapo amani na uhusiano baina ya nchi hizo itaendelea kuwepo. "DRC ni moja ya nchi zisizo karibu na bahari (landlocked countries), wataendelea kutumia bandari zetu endapo tutaendelea kuwa na mahusiano mazuri na amani kama ilivyo kwa sasa," anasema. Siri ya msisitizo wake wa amani katika uchaguzi huo ni kile alichokifafanua kuwa, amani ya Tanzania itaimarika zaidi iwapo majirani zake watakuwa na amani pia. "Utulivu uliopo kwa sasa katika nchi za maziwa makuu unaongeza amani yetu. Endapo kutatokea vurugu huko kwa sababu ya uchaguzi, haitaathirika mifumo ya ugavi ya DRC tu, hata Tanzania pia," anaeleza na kuongeza: "Pia ikumbukwe nchi hufanya biashara zaidi na nchi zilizo jirani kuliko nchi zilizo mbali. Hivyo ujirani wenye amani utakuza uchumi Tanzania," anasema. Endapo kuna cha kuwafundisha DRC kuhusu uchaguzi wenye amani nchini mwao, anasema Tanzania inapaswa kuwa mstari wa mbele kufanya hivyo kwa kuwa ni jirani yake. "Raia wa DRC wajitahidi kudumisha amani kwenye uchaguzi wakijifunza kutoka kwetu. Wajue baada ya uchaguzi kuna maisha na wafahamu pia kuwa viongozi wazuri hutokana na raia wenyewe. Wajione sehemu ya uongozi wao, wasitegemee kuwa na kiongozi bora kama wenyewe hawamsaidii kiongozi huyo. Wakubali kuwa kiongozi anatokana na wao, hivyo atakayechaguliwa wamkubali ili wabaki na amani," anasema. Anasema amani ya DRC, ndiyo msingi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi katika nchi za Africa Mashariki na duniani. Uhusiano uendelezwe Lakini, Mchambuzi wa Masuala ya Uchumi na Siasa, Gabriel Mwang'onda anasema uchaguzi huo unapaswa kuleta kiongozi atakayeendekeza uhusiano baina ya nchi hizo. "Hatujui bado nani akashinda lakini yeyote atakayeshinda uhusiano wetu ni mkubwa kiuchumi anapaswa kuendeleza," anasema. Anaeleza uchaguzi huo ndiyo utakaoamua ama kuongeza idadi ya mizigo ya DRC inayohudumiwa katika Bandari ya Tanzania au kupunguza kwake. Hata hivyo, anasema matarajio yake makubwa ni kupatikana kiongozi atakayesimamia umaliziaji wa bandari ya Kalemie ambayo upande wa Tanzania tayari imeshakamilika. Wakongo waliopo Tanzania Majesté Kimpir ni Mongo anayeishi nchini Tanzania kwa shughuli za biashara, anasema hatamani kuona uchaguzi huo unazorotesha uhusiano kati ya nchi hizo kibiashara na mambo mengine. Anasema uhuru alionao wa kufanya kazi na biashara nchini Tanzania, umetokana na Uhusiano mzuri uliopo baina ya mataifa hayo, akisisitiza ni muhimu ikatafutwa mbinu ya kuendeleza sio kukatisha. Kwa hali ilivyo, anasema kuna wasiwasi juu ya amani kuelekea uchaguzi huo kwa kuwa wananchi wanalalamika kukosekana kwa viongozi wenye uzalendo kama ilivyo Tanzania. "Kule kwetu (DRC) viongozi wanapendekezwa na Ufaransa, hawana uzalendo na hata nchi yetu haina demokrasia kama ilivyo Tanzania, kwa maslahi ya uchumi na uhusiano wa kibiashara, uchaguzi unapaswa uwe na mfano wa huu wa Tanzania," anasema. Uchaguzi huo pia, umemuibua Dekanto Bass raia wa Kongo anayefanya shughuli za muziki nchini Tanzania, anayesema amani ndiyo msingi wa kila kitu. "Tukivuruga amani au akipatikana kiongozi atakayevuruga amani na majirani zetu, sisi hatutapata nafasi ya kuendelea kufanya kazi huku nje kama hivi. Viongozi wahakikishe kunakuwa na amani katika uchaguzi," anasema. Undani kuhusu uchaguzi DRC Huu unakuwa miongoni mwa chaguzi zinazoandaliwa kwa amani baada ya misukisuko ya kisiasa na mapinduzi ya Serikali katika taifa la DRC. Katika uchaguzi huo, Felix Tshisekedi anawania muhula wa pili wa miaka mitano ya urais, baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya uongozi wake, aliyohudumu tangu mwaka 2019, alipoachiwa kijiti na Joseph Kabila. Taifa hilo tajiri la madini duniani, linaingia katika uchaguzi likiwa na jumla ya wagombea 22, baada ya wanne kujiengua na kumuunga mkono mgombea wa upinzani, Moïse Katumbi. Mbali na Katumbi, wapinzani wakuu wa Tshisekedi katika uchaguzi huo ni Martin Fayulu na Dk Denis Mukwege. Marie-Josée Ifoku Mputa na Joëlle Bile ndiyo wagombea wa kike pekee waliojitokeza kuwania kinyang'anyiro hicho. Hata hivyo, uchaguzi huo unafanyika wakati DRC ikiwa miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani duniani. Inakadiriwa watu milioni 6.9 wamelazimika kuyahama makazi yao tangu mwaka 2022 kutokana na machafuko yanayoendelea. Umoja wa Mataifa, unakadiria asilimia 28 ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao Kivu Kaskazini huku asilimia 39 wakihama Ituri. Hatua hiyo imetokana na kukithiri kwa ghasia hasa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri nchini humo. Si hivyo tu, makundi ya waasi yakiwemo M23, Allied Democratic Forces (ADF) na Codeco yanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya raia na wanajeshi.
Matumaini ya utekelezwaji wa mabadiliko ya kikokotoo kwa watumishi wastaafu wa Jeshi la Polisi, yapo
Matumaini ya utekelezwaji wa mabadiliko ya kikokotoo kwa watumishi wastaafu wa Jeshi la Polisi, yapo mikononi mwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni aliyesema kinachofanywa naye sasa ni utekelezaji. Hata hivyo, Masauni hakuweka wazi juu ya hatua hizo za utekelezaji zilizofikiwa, kwa kile alichokisisitiza, kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo, kinachofanyika ni utekelezaji tu. Hicho kinachoitwa maelekezo ya Rais Samia, kimsingi ilikuwa ahadi aliyoitoa miezi mitatu iliyopita baada ya kupokea malalamiko kuhusu kikokotoo. Katika ahadi yake hiyo, Rais Samia alisema: “Tuko tunakifanyia kazi kuona jinsi ambayo tutaweza kwenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo.” Alisema kwa kuwa kimepigiwa kelele sana, si tu na Jeshi la Polisi, bali na watumishi wengine, wataangalia kwa kuwa siku zote Serikali ni sikivu. Hata hivyo, sababu ya ahadi ya Rais Samia siku hiyo ni kikundi cha burudani kilichowasilisha ujumbe wa kikokotoo kwa mkuu huyo wa nchi kwa njia ya sanaa ya kibati, katika kikao kazi cha maofisa waandamizi wa jeshi hilo, iliyofanyika Oysterbay Dar es Salaam. “Mama kikokotoo kiangalie hakika kitatuua. Maana wastaafu wengi huko nje wanalia. Hakika uamuzi wako ni wa busara, tunangoja huruma yako utusaidie,” alisema mmoja wa wanakikundi hao. Msingi wa malalamiko ya watumishi hao wanaotarajia kustaafu jeshi hilo ni kuwepo kwa utofauti kati yao na Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Majeshi hayo, hayamo katika utaratibu wa kikokotoo, hivyo mtumishi akistaafu anapewa kiinua mgongo chake chote, huku wa jeshi la polisi anapewa asilimia 33.3 kwa mkupuo na kilichobaki anapewa kidogo kidogo kila mwezi. Kwa hiyo, hoja ya askari hao wa jeshi la polisi ni utaratibu kama wa JWTZ na JKT ufanyike kwao pia. Baadhi ya askari waliozungumza na gazeti hili, waliliitaka Bunge litafakari upya sheria zinazogusa maslahi ya wafanyakazi huku wenye taaluma ya sheria wakisema sheria hizo zina viashiria vya ubaguzi kwa watumishi kwa kuwaweka katika matabaka katika suala la mafao. Ibara ya 13(2) ya Katiba ya 1977 inasomeka “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, askari Polisi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mara, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Ruvuma, walisema wanatamani kumsikia Rais Samia akisema kitu juu ya kikokotoo kabla ya mwaka mpya 2024. “Tuko askari nafikiri zaidi ya 1,000 ila sina hakika na idadi, ambao tutastaafu 2024. Sasa wanasema ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji. Tumeona wenzetu waliostaafu walicholipwa. Hakilingani na uzalendo wetu,” alidai askari ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini. Askari huyo mwenye cheo cha Stesheni Sajini anayefanya kazi Moshi mkoani Kilimanjaro, alisema haikuwa sawa kuweka ubaguzi kwa majeshi katika kikokotoo kati ya Polisi, Magereza, JWTZ na JKT. “Wenzetu wakistaafu wanalipwa fedha yao yote, sisi tunalipwa asilimia 33 ya michango halafu unaambiwa hizo nyingine wanakutunzia then (halafu) wanakupa pensheni ya kila mwezi ambayo kwa kweli ni ndogo,” alidai askari huyo. Suala hilo lilitajwa hata katika Ripoti ya Tume ya Haki Jinai aliyoiunda chini ya Jaji mkuu mstaafu Othuman Chande ilieleza eneo ambalo limelalamikiwa sana na Polisi na Magereza ni kikokotoo hususan kwa askari wa vyeo vya chini. Ripoti hiyi ilieleza msingi wa malalamiko hayo ni utaratibu mpya wa kukokotoa mafao ya mkupuo, umeathiri kwa kiasi kikubwa kiwango cha malipo hayo kutokana na malipo yao kuhusisha posho nyingi na umri wa kustaafu kuwa mdogo. Kauli ya Masauni Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema ni vigumu kueleza lolote sasa, kwa kuwa wizara imeshapokea maelekezo. “Rais ameshatoa maelekezo mimi ni nani niseme chochote zaidi ya kutekeleza. Mnachotakiwa kufanya ni kusubiri utekelezaji,” alisema. Aliongeza atakuwa na la kuzungumza, utakapofika wakati wa kufanya hivyo, lakini si sasa. “Nitasema lolote utakapofika wakati wa kusema lakini sasa hivi kwa sababu Rais ameshatoa maelekezo Naomba subiri, nisiseme chochote,” alisema. Alipoulizwa iwapo lini utekelezaji unatarajiwa kuanza, Masauni alisema: “Nitaeleza wakati utakapofika.”
Hatimaye Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na
Hatimaye Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022. Wito huo uliotolewa jana na Mahakama ya Wilaya ya Babati, umekuja baada ya Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka kumfungulia mwanasiasa huyo kesi ya jinai Novemba 11, mwaka huu. Hata hivyo, wito huo unaamsha upya sakata hilo linalodaiwa kusababisha Gekul aondolewe katika wadhifa wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Novemba 25, mwaka huu. Kulingana na barua ya wito huo (Mwananchi tunayo), iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa. Katika wito huo, mlalamikaji ni Hashim Ally dhidi ya Pauline Gekul. Gekul anapokea wito huo, kipindi ambacho jamhuri nayo imewasilisha jadala la kesi hiyo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi. Mzizi wa yote hayo ni tuhuma zilizoibuliwa na kijana Hashim Ally, zilizosambaa mitandaoni akiomba msaada kwa watetezi wa haki za binadamu ilia pate haki yake baada ya kufanyiwa ukatili na mbunge huyo. Katika kipande hicho cha video, Ally alieleza ukatili aliofanyiwa unatokana na kile kilichodaiwa kuwa ameshiriki kuweka dawa katika eneo la kazi na sumu kwenye chakula. Kijana huyo alieleza baada ya kukana hayo, mbunge huyo alimtaka avue nguo na kuingizwa chupa kwenye tundu la makalio. Mbali na hilo, kijana huyo alieleza pia alitishiwa bastola na kupelekwa polisi.
Katika kukabiliana na migogoro ya kikodi iliyopo baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na walipa
Katika kukabiliana na migogoro ya kikodi iliyopo baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na walipakodi, Serikali imeanzisha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania (TOST). Katika taasisi hiyo, mlalamikaji hatalazimika kuwa na uwakilishi wa mwanasheria ili awasilishe malalamiko, badala yake anaruhusiwa kupeleka mwenyewe. Hata hivyo, taasisi hiyo imeanzishwa kipindi ambacho, kumekuwa na malalamiko katika utekelezwaji wa sheria za kikodi. Mei mwaka huu, wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo walianzisha mgomo kuishinikiza Serikali itatue changamoto zao, yakiwemo masuala ya tozo na kodi. Mgomo huo, umesababisha kuundwa kwa kamati ya kufuatilia changamoto zote za wafanyabiashara iliyozunguka nchi nzima kufanikisha kazi hiyo. Miongoni mwa malalamiko ya kikodi ya wafanyabiashara ni TRA kutumia nguvu, kufunga biashara na wakati mwingine kukadiria kodi isiyolingana na thamani ya biashara iliyofanyika. Hatua ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ilitangazwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa TOST, Robert Manyama mbele ya wahariri na waandishi wa habari. Alisema madhumuni ya kuanzishwa kwake ni kushughulikia malalamiko yatokanayo na usimamizi wa sheria za kodi kwa kuzingatia uhuru katika utendaji, ufanisi, uwazi, uhalisia na haki. Dhumuni lingine, alisema ni kuainisha maeneo yenye matatizo katika usimamizi wa sheria za kodi ambayo ni vyanzo vya malalamiko na kutoa mapendekezo ya marekebisho. "Madhumuni mengine ni kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani na kuongeza imani kwa wananchi na ulipaji wa kodi wa hiari," alisema. Manyama alisema mtu yeyote anayeona kutoridhishwa na utendaji wa mamlaka inayosimamia utekelezaji wa sheria ya kodi anaweza kuwasilisha malalamiko yake. Kulingana na Mkurugenzi huyo, malalamiko hayo yanaweza kuhusu TRA, Kamishna wa TRA au hata Mtendaji yeyote wa mamlaka hiyo. Kuhusu namna yanavyoshughulikiwa, Manyama alisema baada ya lalamiko kuwasilishwa kwa mujibu wa sheria linapaswa kusuluhishwa ndani ya siku 30. "Malalamiko yanapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 90 tangu yalipotokea na kama usuluhishi wake utahitaji marekebisho tutayapendekeza na kuwasilisha kwa Waziri wa Fedha," alisema. Wafanyabiashara Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe alisema tatizo kubwa la sasa ni utaratibu uliopo. Kabla ya kuanzishwa kwa TOST, alisema TRA ikimkadiria mfanyabiashara kodi hana pa kwenda kulalamika hata ikiwa kinyume na uhalisia. "Rufaa inakatwa kwa Kamishna wa TRA, yaani huyo hiyo aliyekukadiria ndiye unayekwenda kukata rufaa kwake. "Na ili usikilizwe unapaswa ufanye malipo ya awali theluthi moja ya fedha ulizokadiriwa, ambazo wakati mwingine uhalisia wa kodi unayodaiwa haifiki hata kiwango hicho," alisema. Alisema uwepo wa TOST unawapa wafanyabiashara jukwaa la kwenda kulalamika, ingawa bado walipakodi wana wasiwasi. Wasiwasi walionao, alisema ni taasisi hiyo kuwa chini ya Wizara ya Fedha, ambayo pia ndiyo mlezi wa TRA. "Sasa wakienda kuwa watoto wa Baba mmoja yaani Waziri anayeisimamia TRA na TOST ni mmoja, huenda wakawa washirika, ndiyo wasiwasi wa walipakodi lakini tutaona kwenye utendaji wao," alisema. Hata hivyo, alisema Desemba 15, mwaka huu amealikwa kushiriki uzinduzi wa taasisi hiyo, jukwaa wanalotarajia kulitumia kuuliza maswali na kupata taarifa zaidi kuhusu TOST. Mtazamo wa kiuchumi Kwa muktadha wa kiuchumi, hatua hiyo inatajwa kupunguza gharama ya kupeleka kesi mahakamani kama inavyofafanuliwa na Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, Profesa Aurelia Kamuzora. Alieleza kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni utekelezaji wa nadharaia ya uchumi ya ubadilishanaji fedha, inayoeleza gharama nyingi za mahakama zinatokana na kutofanya usuluhishi kabla ya kosa. “Iwapo kutakuwa na taasisi hii maana yake hakutakuwa na haja ya kupeleka kesi mahakamani, kulipa gharama za mawakili na mambo mengine, haya yote yatakuwa yanafanyika kwa usuluhishi. “Kwa mfano mtu hajalipa kodi, TRA akafika mlangoni akafunga biashara yake. Kwa kufanya hivyo, TRA itapoteza kodi zaidi wakati duka limefingwa, lakini kukiwa na taasisi ya usuluhishi wawili hawa watazungumza kupata suluhu,” alisema.
Licha ya Serikali ya Tanzania kuweka wazi juu ya sababu ya kutoonekana hadharani kwa Makamu wake wa
Licha ya Serikali ya Tanzania kuweka wazi juu ya sababu ya kutoonekana hadharani kwa Makamu wake wa Rais, Dk Philip Mpango bado ukimya wa kiongozi huyo umeendelea kuibua mashaka kwa baadhi ya Watanzania. Hoja kuhusu ukimya wa Dk Mpango, imeibuliwa na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii, wakihoji yu wapi Makamu huyo wa rais. Hoja hiyo inapata mashiko zaidi kutokana na ukweli kwamba, zimepita zaidi ya siku 30 bila kiongozi huyo wa ngazi ya juu ya Serikali kuonekana hadharani. Ingawa Desemba 5, mwaka huu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kiongozi huyo yupo nje ya nchi kikazi bila kuweka wazi ni kazi ipi, bado kauli hiyo inaonekana kutoafikiwa na Watanzania. Kwa mara ya mwisho, Dk Mpango alionekana hadharani Oktoba 31, mwaka huu aliposhiriki mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan. Tangu siku hiyo, mwanasiasa huyo hakuonekana katika shughuli yoyote ya kiserikali, wala picha zilizotumwa akisafiri kwenda popote katika ziara ya kikazi kama ulivyo utaratibu wa siku zote. Kinachoibua wasiwasi zaidi, ni kumbukumbu ya tukio kama hilo dhidi ya Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli ambaye naye hakuonekana hadharani kwa siku kadhaa na Serikali ilidai yupo salama, lakini baadaye Machi 17, 2021 alitangazwa ameaga dunia. Maoni mitandaoni Kupitia mtandao wa Jamii Forum, Mtanzania Robbin amechapisha ujumbe akisema: “Tuliuliza yu wapi Rais wetu (Hayati Magufuli), tukajibiwa, hajambo, anachapa KAZI!!! “Hazikupita siku chache, tunaambiwa, hatunaye. . Tungejua Yu, mgonjwa ,tungemwombea, baada ya siku kadhaa, tukapokea msiba, tukazika. “Hata miaka mitatu, haijeisha, Mh Mpango (Makamu wa Rais) naye haonekani!! Msitutoneshe bado tuna maumivu,” aliandika na kuongeza… “Tuambiwe ikiwa mgonjwa tuambiwe tumuombee. Mungu ibariki nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania,” aliandika. Mwanasiasa wa chama cha upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu naye amechapisha katika ukurasa wake wa X, akisema, “Je, Serikali hii haikujifunza lolote kutokana na usiri wa kifo cha Magufuli miaka miwili iliyopita?” “Kifo au magonjwa ya viongozi wa Serikali hayapaswi kufichwa. Usiri huzaa uvumi mchafu. Sema ukweli! Tuambie Makamu wa Rais Phillip Mpango yuko wapi sasa,” ameandika. Si mara ya kwanza kwa Dk Mpango Mwaka 2021, akiwa Waziri wa Fedha, Dk Mpango aliwahi kupotea machoni mwa Watanzania kwa takriban wiki tatu na taarifa zilisambaa mitandaoni kuwa anaugua. Baadaye, mwanasiasa huyo aliibukia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kuzungumza na waandishi wa habari, akiwaeleza alikuwa akiugua ugonjwa wa Uviko-19 kwa takriban siku 30. Mtazamo wa wasomi Akizungumzia hilo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mohammed Bakary amesema unapokuwa kiongozi mkubwa faragha yako inapungua. “Kiongozi yeyote mkubwa privacy (faragha) yake inakuwa limited tofauti na raia wa kawaida,” amesema. Iwapo kuna taarifa zozote, amesema inapaswa kuelezwa hadharani badala ya kusubiri watu walalamike katika mitandao ya kijamii. “Si vizuri kukawa na usiri katika taarifa za kiongozi wa juu, Serikali inapaswa kutoa taarifa ya kina ieleze ukweli watu wasipotoshe,” amesema. Ametolea mfano Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliwahi kuweka wazi kuhusu taarifa za ugonjwa wake na kwamba amekwenda kutibiwa nchini Marekani. Kwa sababu kuna historia ya Watanzania kuwahi kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu viongozi wao, kinachoendelea amesema kinaathiri imani ya wananchi kwa Serikali yao. “Athari zake Serikali haitaaminika kwa sababu kama ilivyotokea wakati wa Magufuli, Serikali ilisema yuko salama, kumbe alikuwa anaumwa na akafariki, tena aliyesema alikuwa Waziri Mkuu na sasa yeye tena ndiyo amesema, inafanya wananchi wasiiamini Serikali yao,” amesema. Mtazamo huo unatofautiana na maoni ya Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe aliyesema kwa kuwa Serikali imeshaeleza ni vigumu kufikiri tofauti. Anasema madai kuhusu kuumwa kwa kiongozi huyo, hayawezi kuthibitishwa kwa kuwa tayari Serikali imeeleza wapi alipo kiongozi huyo. "Serikali imesema yupo nje kikazi haya madai ya kwamba anaumwa ni vigumu kuyathibitisha hadi uwe na ushahidi," anasema. Anaeleza ukimya wake ungekuwa tatizo iwapo kungeliibuliwa malalamiko ya kukwama kwa utendaji kazi wa ofisi yake. "Lakini kama mambo yanaenda maana yake hakuna tatizo kungekuwa na tatizo malalamiko yangeibuliwa," anasema. Hata hivyo, anasema kikatiba Makamu wa Rais ni msaidizi wa karibu wa Rais na kwa kuwa hakuna kinachoonekana kukwama sababu ya kutoonekana kwake, hakuna tatizo. "Hatujasikia malalamiko ya kisheria kuhusu alipo na labda kungekuwa na malalamiko kwamba hatimizi wajibu wake ingekuwa hoja," anasema. ‘Yupo salama’ Hata hivyo, mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa Serikali ya Tanzania (jina lake limehifadhiwa), amesisitiza kuwa kiongozi huyo yupo salama. “Yupo nje kwa safari binafsi ya likizo. Haumwi. Anarudi karibuni,” amesisitiza Ofisa hiyo bila kuweka wazi ni nchi gani aliyopo. Amesema kinachoendelea kuelezwa katika mitandao ya kijamii ni uzushi na si vinginevyo.
Ni usiku wa vilio na hasara kwa wafanyabiashara, ndiyo maneno mafupi unayoweza kutumia kuelezea uhal
Ni usiku wa vilio na hasara kwa wafanyabiashara, ndiyo maneno mafupi unayoweza kutumia kuelezea uhalisia wa matukio matatu ya ajali ya moto yaliyotokea katika maeneo tofauti katika Jiji la Dar es Salaam. Matukio hayo yamehusisha kuungua moto kwa maduka ya bidhaa mbalimbali eneo la Mwenge, kuungua kwa maduka ya samani za ndani Mbezi Beach, Tangibovu na kuungua kwa bweni la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, yote hayo yametokea jijini Dar es Salaam. Kulingana na mashuhuda wa matukio yote, ni watu pekee ndiyo waliofanikiwa kutoka salama, lakini si bidhaa, vitu wala fedha zilizokuwepo ndani ya maduka hayo zilizookolewa. Matukio haya yanatokea miezi miwili tangu Jiji hilo lishuhudie tukio kubwa la ajali kama hiyo katika Soko la Kariakoo, lililohusisha kuungua moto kwa vibanda vidogo vya biashara 500 na maduka, karibu na kituo cha mafuta cha Big Bon. Hata hivyo, bado kamati ya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo inaendelea kukuna vichwa, ingawa taarifa za awali zinatajwa kuwa ni hujuma baina ya wafanyabiashara, kama alivyoeleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila. Timu ya waandishi wa habari wa Mwananchi jana, ilitembelea maeneo yote ya ajali hizo na inakusimulia uhalisia wa iliyoyashuhudia. Mwenge Tukio hili limetokea karibu na kilipo Kituo Kidogo cha Polisi Mwenge, likihusisha nyumba iliyokuwa na jumla ya fremu 32 na maduka 30 yaliyoungua moto saa 6 usiku. Vipande vya noti za Sh10,000 vilishuhudiwa katika eneo la tukio hilo, baadhi vikipeperuka baada ya kuungua. Lakini ilikuwa vigumu kutambua baadhi ya bidhaa kwa kuwa zote ziligeuka jivu. “Moto huo ulianza saa sita usiku katika fremu moja na baadaye uliendelea kusambaa katika maeneo mengine. Tulifanya jitihada za kuuzima huku tukiwasiliana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji,” alisema Ramadhan Issa, mmoja wa mashuhuda. Alieleza moto huo ulisambaa kwa kasi kabla ya askari wa jeshi la zimamoto kufika eneo la tukio. Lucy Mona ni mmoja wa wafanyabiashara walioathirika na tukio hilo, alisema juzi alipanga kuchukua fedha zote dukani kwake na kuzipeleka benki, hajui nini kilikwaza asilitekeleze hilo. “Naona ni Mungu mwenyewe ndiyo amepanga ziungue maana hapa katikati kulikuwa na mauzo makubwa hela niliacha ndani zimeungua zote,” alieleza huku akilengwa na machozi bila kutaja kiasi cha fedha hizo. Kinachomtia shaka zaidi ni kile alichoeleza, hakuwa na bima na yeye ndiye tegemezi la familia yake, hivyo kuungua kwa duka hilo la viatu kumekatisha matumaini yake ya kuihudumia familia. Majanga kama hayo yamemkuta Lilian Mrindoko aliyekuwa na fremu ya biashara ya nguo, anayesema thamani ya bidhaa zilizoungua ni zaidi ya Sh10 milioni. Maumivu zaidi ni kwa Lucy Mwalongo aliyepata hasara ya Sh30 milioni uliokuwa mtaji wa bidhaa zilizokuwa kwenye duka ambalo limeungua. “Serikali iangalie namna gani itatusaidia tuendelee na biashara zetu. Ifanye uchunguzi tumjue aliyefanya hivi,” alisema. Katikati ya huduni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aliibua kauli ya faraja kwa wafanyabiashara hao, alipoutaka uongozi wa Wilaya ya Kinondoni yalipotokea majanga hayo, itafute namna ya kuwakopesha waathirika wote. “Uongozi wa Kinondoni ni muhimu kukaa na wafanyabiashara wote 32, ili kuangalia njia ya haraka na kama kuna fedha za kuwakopesha wapewe ili walipe kwa riba kidogo,” alisema. Hata hivyo, alisema tukio hilo linathibitisha changamoto ya wafanyabiashara kutotumia benki kuhifadhi fedha zao, kwani wengi zimeungua zikiwa dukani. Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Saad Mtambule aliunda kamati inayohusisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wataalamu wa Ardhi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuchunguza chanzo cha moto huo. Tangibovu Katika tukio la tangibovu, Mwananchi imeshuhudia takriban maduka sita ya samani za ndani yameungua moto, bila kifaa chochote kuokolewa. Mmoja wa wamiliki wa duka hilo, Kurwa Maembe alisema thamani ya bidhaa zake zilizoungua ni Sh55 milioni, nje ya vifaa vya kazi ambavyo pia vimeteketea. “Nilichukua mkopo, biashara zetu tunaendesha kwa mikopo, sikuwa na bima, sijui hata nafanyaje,” alisema. Alieleza taarifa za tukio hilo, alizipata saa nne usiku muda ambao moto huo ulianza kuwaka na kwamba hakuna alichofanikiwa kukiokoa. “Tulipigia simu zimamoto wamefika hapa na gari moja baadaye wakasema wameishiwa maji, basi moto uliendelea kuteketeza bidhaa,” alisema. Alisema ingawa chanzo kamili hakijafahamika, lakini kulikuwepo na hitilafu ya umeme tangu mapema juzi, kwamba ulikuwa unawake na kukatika. Bweni la Chuo cha Ardhi Katika tukio hili, Mwananchi ilishuhudia majivu yaliyotokana na kile ilichoambiwa ni vifaa mbalimbali vya wanafunzi 14 waliokuwa wanaishi katika mabweni hayo. Kulingana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mlalakuwa, lilipo bweni hilo, Suleiman Masare kati ya wanafunzi waliokuwa wanaishi hapo, wanawake walikuwa 10 na wanaume ni wanne. Alieleza tayari wanafunzi hao walishatafutiwa utaratibu wa hifadhi ya muda na wote wamepata, hivyo taratibu nyingine zinaendelea. Ingawa haijathibitishwa, katika tukio hili pia Tanesco imetajwa kwa kile alichoeleza Masare kuwa, inadaiwa kulikuwa na changamoto ya umeme. Tanesco yafafanua Akitoa ufafanuzi wa madai ya hitilafu ya umeme, Kaimu Meneja wa Tanessco Kanda ya Kinondoni Kaskazini, Mhandisi Tumaini Nyari alisema kunapotokea hitilafu yoyote masuala hayo yanahitaji uchunguzi. Alisema kila moto huwa unakisababishi ikiwemo kuacha vifaa vya umeme bila kuzima ikiwemo chaji ya simu. "Kila kitu lazima kiwe na kisababishi, maeneo yote hayo tunaendelea kuyafanyia uchunguzi ukikamilika tutawapa taarifa," alisema Mkahandisi Nyari. Hata hivyo, Nyari alitoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na kujenga utamaduni wa kuzima swichi kipindi ambacho hawapo, ili kuepuka madhara.
Serikali imeshauriwa kuwa na sera itakayowashawishi mawakili wake kuendelea kufanya kazi nayo, badal
Serikali imeshauriwa kuwa na sera itakayowashawishi mawakili wake kuendelea kufanya kazi nayo, badala ya kutafuta fursa katika kampuni binafsi. Imeelezwa hatua hiyo itawezesha mawakili nguli kuendelea kufanya kazi na Serikali na hivyo, kuwezesha kushinda kesi za madai hasa za kimataifa ambazo Tanzania haina historia nzuri. Ushauri huo umekuja kipindi ambacho, kumekuwepo na idadi kubwa ya kesi za madai ambazo aghalabu Serikali inashindwa. Suala hilo, liliwahi kuzungumziwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi mwaka jana Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi aliyesema sababu za kushindwa kesi hizo ni kukosa ushirikiano wa dhati kwa baadhi ya maofisa wa Serikali hasa wakati wa kutoa ushahidi mahakamani. Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwanzilishi wa kampuni binafsi ya uwakili ya IMMMA Advocates, Protase Ishengoma alipozungumza na waandishi wa habari. "Serikali imekuwa ikisomesha mawakili wengi na ukifika muda fulani mtu anaona anaweza kupata ajira nje ya Serikali, kwahiyo wanawaandaa watu kisha wanawapoteza," alisema. Ili kukabiliana na hilo, alisema Serikali inapaswa kuwa na sera ya kuhakikisha wanasheria wake hawashawishiki kusaka fursa kwingine ili ibaki nao. Hatua nyingine ili kutatua hilo, Ishengoma alisema ni vema Serikali inapoona kuna udhaifu ikusanye jopo la wanasheria binafsi kwa ajili ya kushirikiana nao. "Asitumwe mtu ilimradi aende tu ni muhimu kuongeza ushirikiano na watu wenye weledi. Hata mimi inaniuma kushindwa kesi kwa sababu nchi yetu ni ya walipakodi na tunaposhindwa kodi hizo ndizo tunazolipia hizo fidia," alisema. Alieleza hilo linapaswa kufanywa kwa ada ndogo tofauti na inayotumika kulipa mawakili wa Kimataifa, ilhali wapo wenye uzalendo na uwezo wa kusimamia kesi hizo kutoka nchini. Katika hatua nyingine, Ishengoma alitangaza uamuzi wa kustaafu kufanya kazi ya uwakili ndani na nje ya kampuni hiyo, akisema anawaachia wengine waendeleze alipoishia. Aliitaja historia ya kampuni hiyo ni tangu mwaka 1997 ilipoanzishwa na mawakili wanne lakini sasa ina washirika zaidi ya 20. Mwanzishi mwenza wa kampuni hiyo, Sadock Magai alisema pamoja na kusherehekea utumishi wa Ishengoma, pia wanasherehekea miaka 26 ya IMMMA Advocates. "Tumefanya kazi nyingi ambazo hadi sasa tunajivunia ikiwemo kuishauri Serikali kuhusu mabadiliko ya sera na sheria mbalimbali ikiwemo ya madini," alisema. Kingine wanachojivunia, alisema ni hatua ya kuwa wakufunzi wa awali baada ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, walioifanya bure kwa miaka mitatu.
Taarifa za hadi jana za madhara ya maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang, zinaonyesha wanawake ndiy
Taarifa za hadi jana za madhara ya maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang, zinaonyesha wanawake ndiyo walioathirika zaidi ukilinganisha na wanaume. Katika tukio hilo lililoanza kutokea juzi, waliopoteza maisha ni 63 kati yao wanawake ni 40 sawa na asilimia 67 na wanaume 23 sawa na asilimia 33. Kwa upande wa majeruhi ni 116, kati yao wanawake ni 60 na wanaume ni 56. Tofauti ya asilimia saba. Hata hivyo, Serikali imetangaza kugharimia mazishi ya waliopoteza maisha, huduma kwa majeruhi na waliopoteza makazi. Taarifa kuhusu idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza na wananchi wa Hanang katika hafla ya kuaga miili ya waliofariki. Akitoa mchanganuo wa waliopoteza maisha, Majaliwa alisema kati ya 63 watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea ni 40 na wenye umri chini ya hapo ni 23. Kwa upande wa majeruhi, alisema wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ni 60 na walio chini ya umri huo ni 66. “Hili ni jambo la dharura maafa ni jambo linalotokea ambalo mtu huwezi kujiandaa, tatizo hili tunalifananisha na lile lililotokea Ndanda, Mtwara ambapo kulitokea maporomoko lakini hayakuwa makubwa kama haya,” alisema. Alisema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kupata taarifa kuhusu tukio hilo, alimpigia simu akiwa Rufiji mkoani Pwani kikazi akimtaka aende kushughulikia. Kwa mujibu wa Majaliwa, Serikali inawajibika kusimamia kwa mamna yoyote ili wafiwa na wahanga wote wahudumiwe vema. Kutokana na hayo, Majaliwa alisema Rais Samia alielekeza huduma za miili yote itafanywa na Serikali kwa kupewa majeneza na usafiri, huku maziko zikiachiwa familia kwa taratibu za kimila na kidini. Kuhusu waliojeruhiwa, alisema Rais Samia ameelekeza watibiwe bure hadi watakaporejea katika hali nzuri, huku waliopoteza nyumba wakitakiwa kwenda kukaa katika kambi tatu zilizoandaliwa na huko watapatiwa huduma zote na Serikali. “Kwenye eneo hili la huduma za waliokosa maeneo ya kuishi tunatambua uwepo wa ndugu na jamaa waliokuwa tayari kuwapokea wahanga, tunashukuru kwa ukarimu huo, tutafanya sensa kujua idadi yao,” alisema Hata hivyo, alieleza kwa maelekezo ya Rais Samia tathmini ya madhara itafanyika na kwamba taasisi na wizara zote zinazoguswa na madhira hayo zipo katika eneo hilo kwa hatua. Zaidi ya hayo, alisema maporomoko hayo yanafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa miamba na taarifa za kina zitatolewa baadaye.
Simanzi zaidi imeikumba familia ya Magreth Daraja, aliyepoteza ndugu watano baada ya kufunikwa na to
Simanzi zaidi imeikumba familia ya Magreth Daraja, aliyepoteza ndugu watano baada ya kufunikwa na tope hilo katika maeneo mbalimbali. Kulingana na Magreth ndugu aliowapoteza ni mjukuu wake, dada yake, kaka zake wawili waliofunikwa na tope wakiwa ndani ya nyumba, huku mama yake akisombwa hadi mtoni na kufariki. “Hapa naelekea Singida kwa ajili ya taratibu za mazishi, ndugu zangu watano wamefariki, mama alisombwa na tope hadi kwenye mto na akapoteza maisha lakini ndugu zangu wengine wamefukiwa wakiwa ndani,” alisema. Magreth hakupoteza ndugu pekee, kutokana na madhira yako amesema nyumba yao imebomoka, mifugo imepoteza maisha na trekta limesombwa na tope. Mwingine aliyekumbwa na simanzi hiyo ni Deusi Rashidi mkazi wa wilaya ya Simajiro aliyesema tayari ameshafika eneo la tukio kwa taratibu za mazishi ya ndugu zake watano ambao miili yao imepatikana. Petro Mjenji naye amekutwa na majonzi baada ya tope hilo kuondoa uhai wa wajukuu zake wanne na mama yao katika Kijiji cha Gendabi. "Nimepoteza wajukuu wanne na mama yao, kijana wangu yeye alisombwa na maji amejeruhiwa kwa sasa yuko anapatiwa matibabu. Ni masikitiko sana," alisema. Samia asitisha ziara yake Tukio hilo, limemlazimu Rais Samia Suluhu Hassan kusitisha ziara yake katika Falme za Kiarabu alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28). Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus jana, inaeleza mkuu huyo wa nchi amesikitishwa na anatoa pole kwa wafiwa wote. “Rais Samia ameamua kufupisha safari yake na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa ukaribu janga hilo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. Kupitia taarifa hiyo, Rais Samia aliamtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhakikisha Serikali inagharamia mazishi ya wote waliopoteza maisha na janga hilo. “Majeruhi wote waliopo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama ya Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji,” imeeleza taarifa hiyo. Aliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha upatikanaji wa makazi ya muda kwa wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji. “Tathimini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo kwa eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida,” imesema taarifa hiyo. Idadi ya kaya zilizoathirika kulingana na taarifa hiyo, ni 1,150, watu 5,600 na mashamba 750 yameharibika. Umeme, barabara zaathirika Kutokana na maporomoko ya matope hayo, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Manyara, Jahulula Maendeleo alisema jumla ya nguzo za laini ndogo 60 zimesombwa na maji na nguzo kubwa tano zimeanguka. Kuanguka kwa nguzo hizo, kulingana na meneja huyo kunaathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa eneo hilo lenye wateja 13,326. “Kwa kadri hali inavyozidi kuimarisha tunasimika nguzo ili wananchi waendelee kupata huduma, kwa sasa (jana mchana) tunaendelea kufanya maboresho na kutembelea maeneo mbalimbali kujua kiwango cha athari,” alisema. Mbali na kuanguka kwa nguzo hizo, alisema kwa ajili ya usalama wa wananchi, shirika hilo lililazimika kuziondoa transfoma 76 juzi. Alisema tayari transfoma 63 zimesharudishwa kwenye mfumo, ingawa idadi ya wateja imepungua kutokana na nyumba zao kusombwa na maji. “Pamoja na kurudisha transfoma hizo, lakini kwa kiasi kikubwa nyumba tulizokuwa tukizihudumia hazikuwepo kwa sababu zimesombwa na mafuriko,” alisema. Alieleza kinachofanywa sasa ni kupata katika maeneo mbalimbali kujua kiwango cha madhara na kuona namna ya kufanya maboresho ya huduma hasa katika maeneo ya katikati. Kuhusu miundombinu, Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) mkoani Manyara, Salim Bwayi alisema madhara yamejitokeza katika barabara mbili. Moja ya barabara hizo, alisema ni Mugitu Ngendabi yenye urefu wa kilomita 10.9 ambayo kuna eneo limekatika na kusababisha ugumu wa kupitika. “Kuna sehemu imekatika vibaya na kupitika kwa shida kwa sasa tupo katika eneo hilo kufanya jitihada za kuhakikisha panafunguka ili wahanga wafikiwe,” alisema. Barabara nyingine, alisema ni Indasaki Dawari yenye urefu wa kilomita 33.5 iliyokatika sehemu nne na kuacha makorongo ambayo yasiyopitika kwa usafiri wa aina yoyote. Alisema kukatika kwa barabara hiyo kunafanya wananchi wa maeneo yaliyoathirika wasiwe na mbadala wa usafiri zaidi ya miguu. Kutokana na kukatika kwa barabara hizo, alisema wakazi wa vijiji vya Gendabi na Kateshi ndiyo wanaoathirika zaidi na ndiyo walioathiriwa na mafuriko hayo kwa kuwa wapo nyuma ya mlima. “Baada ya jitihada kubwa za jana, barabara imefunguka kwa kiasi fulani na kwa sasa matope yanazolewa barabarani na tunaangalia namna ya kufanya angalau makongoro yaondolewe kwa hatua za dharura,” alisema. Hata hivyo, alisema baadhi ya maeneo barabara hiyo yana mawe makubwa yasiyobebeka kwa mkono, hivyo kesho yanatarajiwa kuondolewa kwa vifaa maalum. Hata hivyo, alisema kutokana na sehemu nne zilizokatika ili kupata suluhu ya kudumu, kunahitajika madaraha makubwa. Wataalamu wawasili Tukio hilo lilisababisha timu ya wataalamu wa miamba kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya uchunguzi wa kilichotokea. Taarifa kuhusu wataalamu hao, ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama alipofika katika eneo hilo Alisema wataalamu hao wa miamba wameshafika wilayani Hanang' ili kubaini chanzo cha tope zito lililotokea mlima Hanang' na kusababisha vifo na majeruhi. "Serikali imeshaleta wataalamu wa miamba na watatoa taarifa ya nini kilichotokea na nini kidanyike katika mlima wa Hanang,” alisema. Kwa upande wa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alisema tayari Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), tayari imefungua barabara ya Singida-Arusha ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani. Historia ya majanga nchini, nini kifanyike Kwa mujibu wa Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Majanga wa mwaka 2022/27, katika kipindi cha miongo miwili iliyopita yaani mwaka 1997/2017, kuna majanga matano ya asili yaliyosababisha maafa nchini. Majanga hayo ni mafuriko asilimia 40, magonjwa ya mlipuko asilimia 34, tetemeko la ardhi asilimia tisa, ukame asilimia 6 na mvua zinazoambatana na upepo mkali asilimia 6. Lakini, mkakati huo unabainisha magonjwa ya mlipuko ndiyo yaliyosababisha idadi kubwa zaidi ya vifo ambavyo ni asilimia 92 ya jumla ya vifo vya maafa. Hata hivyo, mkakati huo unaitaja Tanzania kuwa nchi ya 51 kati ya 180 katika orodha ya hali ya hatari ya kuathirika na majanga ya asili duniani. Akizungumzia suala hilo, James Mbatia ambaye ni mtaalamu wa majanga alisema kilichotokea Hanang ni hatua ya pili ya janga linaloweza kutokea kwa sababu ya shughuli mbalimbali za binadamu zinazochangia kuharibu mazingira. Alisema kama nchi inafahamu uwepo wa milima kama Hanang, Kilimanjaro na mingineyo inayoweza kusababisha athari mbalimbali ikiwa itakumbwa na mitikisiko, mvua kubwa, mitetemo au Volcano. “Bila kujua lini lakini ni lazima kuwapo kwa utayari wa kupambana na janga hilo, tutengeneze miundombinu rafiki kwa ajili ya usalama wa watu. kwa mfano mlima Hanang, tuangalie stendi imetengenezwa wapi katika mkondo wa maji? shughuli za kibinadamu zinafanyika wapi katika mkondo wa maji,” alihoji. Alisema janga kama hilo linapotokea lina matokeo yake hivyo ni lazima kuhakikisha miundombinu inayowekwa maeneo kama hayo inakuwa na uwezo wa kumsaidia mtu baadaye. Alisema umefika wakati sasa wa kuendelea kutoa tahadhari kwa watu wengine wakati suala hilo likishughulikiwa watu wakumbushwe pia kuhusu Elnino hasa katika mikoa ambayo uwezekano wa mvua hizo kutokea. “Watu wafundishwe kwa uharaka na ulazima ili wajue namna ya kupambana na mjanga hayo na namna wanavyoweza kujikinga. Wakati akiyasema hayo, taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza kuwa mvua ya El Niño mwaka 2015/16 iliathiri moja kwa moja watu 84,643, kuharibu nyumba 1,006 na hekta 11,167.4 za mazao ya chakula. Pia mvua hiyo iliharibu shule, vituo vya afya, barabara, madaraja, miundombinu mingine ya umma na binafsi katika mikoa ya Mwanza (Ilemela), Mtwara (Mtwara Mikindani na Vijijini), Pwani (Rufiji) na Iringa (Manispaa ya Iringa). Katika upande wa maporomoko ya ardhi kwa mujibu wa mkakati huo, hutokea wakati nguvu ya mvuto inayofanya kazi kuimarisha miamba katika mteremko inashindwa na nguvu nyingine na kukatika. Maporomoko ya ardhi yaliyowahu kutokea ni pamoja na yale ya mwaka 2009 huko Same yalisababisha vifo vya watu 24 na kuua ng’ombe 60, kuharibu kilomita 15 za barabara na mabwawa 15 ya umwagiliaji kutokana na athari ya tope. Matukio ya maporomoko ya ardhi pia yalitokea katika Wilaya ya Makete mwaka 2010 ambayo yalifunga barabara ya kwenda Njombe kwa siku kadhaa. Pia Manispaa ya Arusha, Aprili 2019 ilishuhudia suala hili ambapo watu 3 walifariki dunia na 2 kujeruhiwa. Wilaya ya Mbogwe mnamo Oktoba mwaka 2019 watu 2 walifariki. Tukio lingine la maporomoko ya ardhi lilitokea Wilayani Ludewa mkoani Njombe, Machi 2020 ambapo watu 2 walifariki dunia, watu 5 kujeruhiwa na nyumba 13 kuharibiwa. Matukio mengine ya maafa ya kijiografia yalihusisha mlipuko wa mara kwa mara wa Volkano katika vilima vya Oldonyo Lengai mnamo mwaka 1880, 1917, 1921, 1940, 1966, 1967, 2007 na 2008 ambapo watu, mifugo na mazingira yaliathiriwa. Mtazamo wa kijiolojia Mtaalamu wa Jiolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Emmanuel Kazimoto alisema hilo si tukio la kwanza, liliwahi kutokea katika mlima Meru. Hata hivyo, alieleza eneo hilo lipo ndani ya Bonde la ufa la Afrika Mashariki linaloambatana na milipuko ya volcano na michakato mbalimbali ya kijiolojia. “Milipuko ya Volcano ndio inayotengeneza milima ya Volcano kama ilivyo Manyara na maeneo mengine ya bonde la ufa,” alisema. Alisema kutokea kwa milipuko hiyo hutengeneza milima ambayo baadaye huzalisha majanga kama yaliyotokea katika Mlima Hanang. Katika tukio la Mlima Meru, Dk Kazimoto alisema: ”yalitokea maporomoko makubwa yaliyotambulika duniani ambapo tani bilioni 55 za mawe zilioporomoka.” Alisema ni vema wakazi wa maeneo ya Manyara na Arusha wakatambua uhalisia wa mazingira waliyopo ili kujikinga dhidi ya madhara hayo. Alishauri elimu itolewe kwa wananchi hao ili wachukue tahadhari zaidi. “Mfano kufuatilia taarifa za kijiolojia sio tu milima kubomoka kuna milipuko pia inayoweza kutokea, kwahiyo ni muhimu kufuatilia hiyo milima na hatari inayoweza kutokea,” alisema.
Madhara ya maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, yamesababisha kusombwa kwa n
Madhara ya maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, yamesababisha kusombwa kwa nguzo 60 za laini ndogo ya umeme, huku nguzo za laini kubwa tano zikianguka. Kusombwa na kuanguka kwa nguzo hizo, kumesababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya Wilaya hiyo yenye jumla ya wateja 13,326. Lakini, kutokana na madhara hayo, barabara mbili za Mugitu Ngendabi na Indasaki Dawari zimekatika na hivyo kushindwa kupitika kwa usafiri wowote zaidi ya mguu. Akizungumzia madhara katika huduma za nishati leo Jumatatu Desemba 4, 2023 Meneja wa Tanesco mkoani Manyara, Jahulula Maendeleo amesema kinachofanywa sasa ni kuangalia maeneo ambayo usalama umeimarika na kusimika nguzo hizo ili wananchi waendelee kupata huduma. “Tunasimika nguzo hizi kubwa pale tu tunapoona eneo lipo shwari, kazi hii inaendelea leo hii hadi itakapokamilika,” amesema. Mbali na kuanguka kwa nguzo hizo, amesema kwa ajili ya usalama wa wananchi, shirika hilo lililazimika kuziondoa transfoma 76 jana. Amesema tayari 63 zimesharudishwa kwenye mfumo, ingawa idadi ya wateja imepungua kutokana na nyumba zao kusombwa na maji. “Pamoja na kurudisha transfoma hizo, lakini kwa kiasi kikubwa nyumba tulizokuwa tukizihudumia hazikuwepo kwa sababu zimesombwa na mafuriko,” amesema. Ameeleza kinachofanywa sasa ni kupata katika maeneo mbalimbali kujua kiwango cha madhara na kuona namna ya kufanya maboresho ya huduma hasa katika maeneo ya katikati. Kuhusu miundombinu, Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) mkoani Manyara, Salim Bwayi amesema madhara yamejitokeza katika barabara mbili. Moja ya barabara hizo, amesema ni Mugitu Ngendabi yenye urefu wa kilomita 10.9 ambayo kuna eneo limekatika na kusababisha ugumu wa kupitika. “Kuna sehemu imekatika vibaya na kupitika kwa shida kwa sasa tupo katika eneo hilo kufanya jitihada za kuhakikisha panafunguka ili wahanga wafikiwe,” amesema. Barabara nyingine, amesema ni Indasaki Dawari yenye urefu wa kilomita 33.5 iliyokatika sehemu nne na kuacha makorongo ambayo yasiyopitika kwa usafiri wa aina yoyote. Amesema kukatika kwa barabara hiyo kunafanya wananchi wa maeneo yaliyoathirika wasiwe na mbadala wa usafiri zaidi ya miguu. Kutokana na kukatika kwa barabara hizo, amesema wakazi wa vijiji vya Gendabi na Kateshi ndiyo wanaoathirika zaidi na ndiyo walioathiriwa na mafuriko hayo kwa kuwa wapo nyuma ya mlima. “Baada ya jitihada kubwa za jana, barabara imefunguka kwa kiasi fulani na kwa sasa matope yanazolewa barabarani na tunaangalia namna ya kufanya angalau makongoro yaondolewe kwa hatua za dharura,” amesema. Hata hivyo, amesema baadhi ya maeneo barabara hiyo yana mawe makubwa yasiyobebeka kwa mkono, hivyo kesho yanatarajiwa kuondolewa kwa vifaa maalum. Hata hivyo, amesema kutokana na sehemu nne zilizokatika ili kupata suluhu ya kudumu, kunahitajika madaraha makubwa.
Tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa inayoishia mwaka 2025, inaonyesha wastani wa pato la mtanza
Tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa inayoishia mwaka 2025, inaonyesha wastani wa pato la mtanzania mmoja umeongezeka kutoka Sh322,597 mwaka 2000 hadi Sh2.88 milioni Desemba 2022. Ongezeko hilo, linatajwa kuwa sehemu ya mafanikio ya utekelezaji wa dira hiyo ya kwanza, inayotarajiwa kukoma miaka miwili ijayo na hivyo kufungua pazia la mchakato wa maandalizi ya dira mpya itakayoishia mwaka 2050. Dira ya taifa hutekelezwa kwa kipindi cha miaka 25 na iliyopo sasa ilianza mwaka 2000, wakati Tanzania ikiwa mikononi mwa Hayati Benjamin Mkapa. Ongezeko la pato hilo la Mtanzania lilidokezwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo aliposoma sehemu ya tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa ya mwaka 2025, mbele ya waandishi wa habari. Alisema mwaka 2000 wastani wa pato la mtanzania mmoja ulikuwa ni Sh322,597 lakini sasa umeongezeka na kufikia Sh2.88 milioni. “Sasa hapa kuna watu watasema mbona mimi sina hiyo Sh2.88 milioni, hesabu zinapatikana kwa kujumlisha mapato ya watu wote nchi nzima kisha yanagawanywa kwa idadi ya watu. Kwa hiyo huu ni wastani, wapo wenye zaidi ya kiasi hicho na wengine wana chini ya kiasi hicho,” alisema. Kwa mujibu wa Profesa Mkumbo, tathmini hiyo inaonyesha mafanikio katika kujitosheleza kwa chakula ambapo Tanzania imefikia asilimia 124 na lengo ni kufikia asilimia 140 mwaka 2025. Mafanikio mengine kulingana na tathmini hiyo, ni kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami na zege na kupungua kwa vifo vya wajawazito. Hata hivyo, alieleza mafanikio na changamoto za utekelezaji wa dira hiyo yatasomwa siku ya uzinduzi wa tathmini ya dira hiyo itakayofanyika Desemba 9, mwaka huu mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan. Waziri huyo alisema miaka 22 iliyopita Tanzania ilianza kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo ya kwanza na kwa miaka 25 na kwa kuwa inaelekea mwisho Rais Samia ameelekeza kuanza kwa mchakato wa kuandaa dira mpya. “Desemba 9, mwaka huu Rais Samia atafungua mkutano wa kwanza wa kitaifa wa dira ya maendeleo ya taifa, utakaofanyika jijini Dar es Salaam,” alisema. Katika uzinduzi huo, alisema mkuu huyo wa nchi ndipo atakapopokea taarifa ya kitafiti ya tathmini ya utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025. “Taarifa hiyo imeainisha kwa kina mafanikio na changamoto zilizojotokeza katika utekelezaji wa dira hiyo,” alisema. Katika mikutano huo, alisema Rais Samia atazindua timu na kamati ya usimamizi wa maandalizi ya dira hiyo ikihusisha wataalamu kutoka kada mbalimbali. Kwa mujibu wa Profesa Mkumbo, mikutano huo utahudhuriwa na wadau 971, wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, wanasiasa, taasisi za dini, sekta binafsi, makundi ya kijamii, wavuvi, jumuiya za kimataifa na wengine. Alisema siku hiyo pia, Rais Samia atatoa ujumbe maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania bara. Akizungumzia hali ya uchumi kuendana na uhalisia wa kipato cha Watanzania, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Laurence Mafuru alisema kutokana na hilo, Serikali kwa sasa imejikita katika uchumi jumuishi. Alisema ili kuwa na uchumi jumuishi Serikali inawekeza rasilimali katika sekta inayogusa Watanzania wengi kama ya kilimo. "Serikali imeamua kufanya juhudi za makusudi kuhakikisha kunakuwa na ukuaji jumuishi wa uchumi, ndiyo maana bajeti kwenye sekta kama kilimo imeongezeka," alisema. Alisisitiza uchumi jumuishi utafikiwa iwapo uwekezaji utafanywa zaidi kwenye sekta ambazo zinagusa wananchi wengi kama kilimo.
Kama ni umri wa binadamu sasa amefikia utu uzima, hivi ndivyo unavyoweza kuielezea miaka 36 ya Chama
Kama ni umri wa binadamu sasa amefikia utu uzima, hivi ndivyo unavyoweza kuielezea miaka 36 ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa). Tamwa iliyozaliwa miaka 36 iliyopita, kwa mujibu wa waasisi wake, chimbuko la kuanzishwa kwake ni juhudi za kusaka nguvu ya sauti ya wanawake katika vyumba vya habari. Historia ya taasisi hiyo, inasimuliwa na waasisi wake, huku baadhi ya wanahabari wakitoa mwelekeo wa safari ya chama hicho katika miaka 36 ijayo. Hayo yaliibuliwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa kwanza wa Tamwa, Fatma Alloo alipozungumza akiwa mwanajopo lililozungunzia tathmini ya miaka 36 ya chama hicho. Akisimulia chimbuko la Tamwa, Fatma alisema ni kipindi ambacho yeye alikuwa mwanahabari katika Gazeti la Dailynews na alikuwa na uhusiano mzuri na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Wakati huo, alisema hakukuwa na kituo chochote cha televisheni, bali ilikuwepo redio RTD na magazeti mbalimbali. Katika kipindi hicho, alieleza UDSM ilikuwa ikifanya tafiti mbalimbali na inashindwa kuzifikisha kwa wananchi. "Mimi niliwachallenge (niliwapa changamoto) kwamba sasa tafiti zenu zina tija gani kama hamzifikishi kwa wananchi, ndipo walipofanya utafiti kuhusu mimba kwa wanafunzi na kuamua kutupatia," alisema. Baada ya kupewa utafiti huo, Fatma alisema alishirikiana na Eda Sanga aliyekuwa RTD kutengeneza vipindi mbalimbali vya redio na vilirushwa hewani. "Tulianza kutengeneza vipindi vya redio na hivyo vilifanywa na Eda Sanga na Rose Haji, watu walipenda sana na sisi tulipata moyo," alisema. Baada ya utafiti huo, alisema ulifanyika mwingine wa namna wanawake wanavyopigwa na wenza wao. Alieleza katika mkakati wa kutengeneza vipindi vya redio kuhusu utafiti huo na kwa sababu wafanya maamuzi katika vyumba vya habari walikuwa ni wanaume, walikataa vipindi hivyo kurushwa. Kwa mujibu wa Fatma, hilo ndilo lililoianzisha Tamwa ambapo wanawake walitaka kuwa na sauti katika vyumba vya habari. Hata hivyo, alisema kitu kilichoifanya Tamwa iendelee kuishi kama ilivyo ni kuheshimu Katiba ya chama hicho. Alieleza kila mwaka ndani ya chama hicho, uongozi unabadilika. "Wakati ule Mwalimu Nyerere alitupa moyo sana. Vijana wa sasa mjitathmini kwamba nini kinawapa mwamko wa kufanya jambo gani la kuandika historia," alisema. Alieleza lazima Afrika iandike historia yake yenyewe kama haiandikwi na waafrika nani mwingine atakayeandika. Akisisitiza hilo, Mkurugenzi wa TBC, Dk Ayoub Rioba alieleza dunia ya sasa imebadilika na imekuwa ukombozi kwamba kwa sasa mwanamke anaweza kurekodi kitu katika mtandao na akasema anachotaka. "Kina mama Alloo walifanya kazi kubwa ya kubomoa ukuta wa watu waliokuwa wanaona kwamba bila wao hakuna lolote linaloweza kufanyika," alisema. Historia ya safari ya miaka 36 iliyopita iliibua mjadala wa tathmini ya Tamwa katika miaka 36 ijayo. Akichangia mjadala huo, Mwanahabari kutoka Zanzibar, Rahma Suleiman alisema kuna haja kwa Tamwa kuongeza uchechemuzi kwa jamii kuhusu haki za wanawake na watoto. "Tukianza kuwajengea uwezo watoto watakuwa na uwezo wa kujiamini, kujitambua na kusimamia haki zao," alisema. Alieleza kwa wanaume wanaolinda haki za wanawake na watoto wanapaswa kuwekwa karibu ili waendelee kuwashawishi wengine kutekeleza hilo. Kuhusu udhalilishaji mitandaoni, alisema kwa sasa ni mkubwa hasa kwa makundi ya wanawake na watoto. Mwanahabari mwingine aliyechagia mjadala huo ni Joseph Sabinus wa Gazeti la Dailynews aliyesema anatarajia kuiona Tamwa itakayokuwa na ushirikishwani mkubwa wa wanaume kwa kuwa imeshaanza. "Tamwa wameanza kushirikisha wanaume hiyo ni alama kubwa ninaiona inawapeleka Tamwa mbali," alisema. Alieleza kwa kufanya hivyo, wamewafanya wanaume wawe kama silaha ya vita na sio kuwatazama kama maadui. Kuhusu utafiti Kulingana na utafiti uliofanywa na Tamwa Julai hadi Septemba mwaka huu, imebainika asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na unyanyasaji wa kingono katika vyombo vya habari. Hayo ni kulingana na utafiti wa hali ya usalama wa wanahabari wanawake katika vyumba vya habari uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika vyombo vya habari 22. Akisoma muhtasari wa utafiti huo, Mkurugenzi wa Tamwa, Dk Rose Reuben isema kati ya wanahabari hao waliokumbwa na unyanyasaji wa kijinsia, asilimia 27 wamekumbana nao kutoka kwa vyanzo vyao vya habari. Alieleza asilimia 59, wamekumbana na kadhia hizo kutoka katika vyumba vyao vya habari na hasa watendaji wakubwa wakiwa ni wahariri, mameneja na wamiliki wa vyombo hivyo. "Unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono unaathiri ubora na uaminifu wa waandishi wa habari iwapo changamoto hizo zitakaa kwa muda mrefu," alisema Dk Rose. Hata hivyo, alusema utafiti huo umefaywa kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu katika Mikoa kadhaa nchini. Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew aliahidi kufanyia kazi changamoto zote za kisheria na kisera zinazoihusu taaluma ya habari. "Serikali inaendelea kufanyia maboresho sera na sheria zilizopitwa na wakati na kwamba maoni na ushauri katika sheria zinazoenda kutungwa utafanyiwa kazi," alisema. Alisema tasnia ya habari imekuwa na changamoto lukuki na Serikali imeendelea kuzishughulikia kupitia mabadiliko mbalimbali yakiwemo ya kisheria. Akizungumzia usawa wa kijinsia katika vyumba vya habari, alisema tafiti zinaonyesha asilimia 34 ya waandishi wa habari wanaume wana uhakika wa kupewa mikataba ya kazi na mabosi huku asilimia 66 ya wanahabari wanawake wakikosa uhakika wa hilo. Alieleza ili kuhakikisha masuala ya usawa wa jinsia yanaingizwa katika taaluma Wizara hiyo, imeona haja ya kuwepo na Ofisa maalum anayeshughulikia ujumuishaji wa jinsia katika taaluma ya habari. Kutokana na utafiti wa Tamwa, Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Keneth Simbaya alisema kinachofanywa na umoja huo ni kukusanya kanzidata ya matukio na kuvifuata vyombo vya habari kimoja kimoja. Alisema umoja huo umekuwa ukipokea taarifa nyingi za unyanyasaji katika vyumba vya habari na jukumu inalotarajia kufanya ni kuelimisha vyumba vya habari. "Kwa sasa tunaunda kanzidata ili tutoe ripoti na kuona namna ya kuvifikia vyumba vya habari kwa kuwa yapo mambo yanayohitaji kuelimishana tu," alisema. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwepo muongozo wa kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vyombo vya habari, lakini kwa sehemu kubwa hayakuanzishwa. Alieleza wakati hilo likitarajiwa kufanyika ni vema elimu ianze kutolewa ili wanahabari wasione aibu kuyatumia madawati hayo. "Watu wasione wanapokwenda kuripoti watajidhalilisha au pengine wamewahi kuona walipripoti na hakuna hatua iliyochukuliwa," alisema. Akichangia mjadala kuhusu hali ya rushwa katika vyumba vya habari, Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dorothea Mrema aliwasisitiza wanaokumbwa na madhira watoe taarifa kwa taasisi hiyo. Alisema mapambano dhidi ya aina hiyo ya rushwa na nyingine ni jukumu la wananchi wote, hivyo kila mmoja na kila taasisi inapaswa kuonyesha juhudi za mapambano hayo. "Kila taasisi inapaswa kushiriki mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa mkakati wa mapambano dhidi ya rushwa wa kitaifa unataka kila taasisi ipambane na rushwa, huu ni wajibu na jukumu la kila mmoja," alisema. Hata hivyo, alisema Takukuru imekuwa ikipokea taarifa kuhusu matukio hayo na aghalabu huwachukulia hatua kwa kuwapeleka mahakamani baada ya kuthibitika.
Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na uny
Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na unyanyasaji wa kingono katika vyombo vya habari. Hayo ni kulingana na utafiti wa hali ya usalama wa wanahabari wanawake katika vyumba vya habari uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika vyombo vya habari 22. Akisoma muhtasari wa utafiti huo, Mkurugenzi wa Tamwa, Dk Rose Reuben amesema kati ya wanahabari hao waliokumbwa na unyanyasaji wa kijinsia, asilimia 27 wamekumbana nao kutoka kwa vyanzo vyao vya habari. Ameeleza asilimia 59, wamekumbana na kadhia hizo kutoka katika vyumba vyao vya habari na hasa watendaji wakubwa wakiwa ni wahariri, mameneja na wamiliki wa vyombo hivyo. "Unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono unaathiri ubora na uaminifu wa waandishi wa habari iwapo changamoto hizo zitakaa kwa muda mrefu," amesema Dk Rose. Hata hivyo, amesema utafiti huo umefaywa kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu katika Mikoa kadhaa nchini. Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew ameahidi kufanyia kazi changamoto zote za kisheria na kisera zinazoihusu taaluma ya habari. "Serikali inaendelea kufanyia maboresho sera na sheria zilizopitwa na wakati na kwamba maoni na ushauri katika sheria zinazoenda kutungwa utafanyiwa kazi," alisema. Alisema tasnia ya habari imekuwa na changamoto lukuki na Serikali imeendelea kuzishughulikia kupitia mabadiliko mbalimbali yakiwemo ya kisheria. Akizungumzia usawa wa kijinsia katika vyumba vya habari, alisema tafiti zinaonyesha asilimia 34 ya waandishi wa habari wanaume wana uhakika wa kupewa mikataba ya kazi na mabosi huku asilimia 66 ya wanahabari wanawake wakikosa uhakika wa hilo. Alieleza ili kuhakikisha masuala ya usawa wa jinsia yanaingizwa katika taaluma Wizara hiyo, imeona haja ya kuwepo na Ofisa maalum anayeshughulikia ujumuishaji wa jinsia katika taaluma ya habari. Kutokana na utafiti wa Tamwa, Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya alisema kinachofanywa na umoja huo ni kukusanya kanzidata ya matukio na kuvifuata vyombo vya habari kimoja kimoja. Alisema umoja huo umekuwa ukipokea taarifa nyingi za unyanyasaji katika vyumba vya habari na jukumu inalotarajia kufanya ni kuelimisha vyumba vya habari. "Kwa sasa tunaunda kanzidata ili tutoe ripoti na kuona namna ya kuvifikia vyumba vya habari kwa kuwa yapo mambo yanayohitaji kuelimishana tu," alisema. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwepo muongozo wa kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vyombo vya habari, lakini kwa sehemu kubwa hayakuanzishwa. Alieleza wakati hilo likitarajiwa kufanyika ni vema elimu ianze kutolewa ili wanahabari wasione aibu kuyatumia madawati hayo. "Watu wasione wanapokwenda kuripoti watajidhalilisha au pengine wamewahi kuona walipripoti na hakuna hatua iliyochukuliwa," alisema. Akichangia mjadala kuhusu hali ya rushwa katika vyumba vya habari, Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dorothea Mrema aliwasisitiza wanaokumbwa na madhira watoe taarifa kwa taasisi hiyo. Alisema mapambano dhidi ya aina hiyo ya rushwa na nyingine ni jukumu la wananchi wote, hivyo kila mmoja na kila taasisi inapaswa kuonyesha juhudi za mapambano hayo. "Kila taasisi inapaswa kushiriki mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa mkakati wa mapambano dhidi ya rushwa wa kitaifa unataka kila taasisi ipambane na rushwa, huu ni wajibu na jukumu la kila mmoja," alisema. Hata hivyo, alisema Takukuru imekuwa ikipokea taarifa kuhusu matukio hayo na aghalabu huwachukulia hatua kwa kuwapeleka mahakamani baada ya kuthibitika.
Wingi wa watu, fursa na huduma ni miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wengi nchini Tanzania, ku
Wingi wa watu, fursa na huduma ni miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wengi nchini Tanzania, kufungasha virago kutoka vijijini na kwenda kuanza maisha katika maeneo ya Miji. Kulingana na mtazamo wa vijana wengi wa Tanzania, ni rahisi kufanikiwa unapokuwa mjini kwa kuwa kuna kazi nyingi za kufanya, tofauti na kijijini. Licha ya mtazamo huo, wapo waliojikuta wanatamani kurudi kijijini kwa kile wanachokieleza kuwa, maisha ya mjini ni msoto mkali (magumu) kuliko walivyotarajia. Utafiti Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi (Repoa) mwaka 2021, unasema kiwango cha watu wanaohama kutoka vijijini kwenda mijini nchini Tanzania kimefikia wastani wa asilimia 15. Kulingana na utafiti huo wenye kichwa cha habari 'Mageuzi ya Miji nchini Tanzania' inakadiriwa kufikia mwaka 2030 idadi ya watu katika Miji nchini humo, itaongezeka na kufikia 35.5 milioni. Ongezeko limekadiriwa zaidi kufikia mwaka 2050, ambapo Miji ya Tanzania itakuwa na jumla ya watu 76.5 milioni. Utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), unakadiria kwamba, watu katika Jiji la Dar es Salaam wataongezeka na kufikia 10 milioni, wakati Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 imebainisha uwepo wa watu 7.4 milioni katika jiji hilo. Haukuishia hapo, utafiti huo uliofanywa katika Mikoa ya Njombe, Arusha na Dar es Salaam, unabainisha asilimia 38 ya wakazi wa Mikoa hiyo wamehama katika maeneo walikozaliwa. Kati ya hao waliohama, asilimia 58 wamehamia katika Jiji la Dar es Salaam, huku kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15-35 likiwa kubwa zaidi ya wenye umri wa miaka 35-55 na hakuna mwenye umri zaidi ya hapo. Ugumu wa maisha Ugumu wa maisha ya kijijini ndiyo unaochagiza vijana wengi kuhamia mjini, wakidhani kuna maisha rahisi, kama inavyoelezwa na Luca Isaya mzaliwa wa Kijiji cha Ruvu Mferejini katika Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania. Luca alikihama Kijiji hicho tangu mwaka 2012 na sasa sehemu kubwa ya maisha yake ni katika Jiji la Dar es Salaam, eneo ambalo ndilo msingi wa kipato chake kwa shughuli za ulinzi. Kwa mujibu wa kijana huyo wa kimaasai, kilichomshinda kijijini ni ugumu wa maisha na uchache wa fursa za kazi, hivyo hakuona namna nyingine tofauti na kwenda Dar es Salaam. "Kijijini kazi zinakosekana kwa mfano zingekuwa zinapatikana hata mimi mwenyewe nisingekuja huku (mjini). Ningekuwa na mtaji wa kulima ningebaki huko huko (kijijini," anaeleza na kuongeza: "Kazi ninayofanya (Dar es Salaam) ni ulinzi na kijijini nilikuwa mfugaji nina mifugo kidogo sio nyingi, nimeacha zinahudumiwa na wadogo zangu," anasema Luca. Uamuzi wake wa kutafuta fedha mjini, anasema umekuwa shubiri kwa nyakati fulani, kwani familia yake inaamini ana kipato kikubwa tofauti na anachokituma. Hata hivyo, anasema aliyokutana nayo mjini ni tofauti na alivyotarajia, kila kitu kinahitaji fedha ikiwemo malazi, chakula na hata maji ya kunywa na huduma nyingine, ambazo kijijini zingepatikana bure. "Ugumu wa mjini ni hela tu hazipatikani mara kwa mara. Unataka uwe na hela za kula, za kulipia sehemu za kulala na za kutuma nyumbani ndiyo zinakuwa changamoto. "Kijijini tukihamisha ng'ombe porini tunakwenda kuchunga, kwa hiyo haulipii chochote," anasema. Wingi wa fursa Mbali na Luca, Glory Mrema mzaliwa wa Mkoa wa Manyara Kaskazini mwa Tanzania amejikuta amezamia katika Jiji la Dar es Salaam tangu mwaka 2014 alipoingia kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu. Anasema tangu alipohitimu elimu hiyo mwaka 2016, hakuona sababu ya kurejea kijijini kwa kuwa kuna shughuli anazofanya zinazomuingizia kipato, ambazo asingezifanya iwapo angelikuwa kijijini. Kulingana na Glory, alipokuwa chuoni alianza biashara ya kuuza nguo mtandaoni, shughuli ambayo imemfanya asitamani tena kurudi kijijini, licha ya kwamba amekosa ajira ya taaluma aliyosomea. "Nilisoma Uhifadhi wa Nyaraka (Records) sijapata ajira lakini nimejiajiri katika biashara ya nguo mtandaoni. Sioni haja ya kurudi kijijini kwa sababu huku ninaingiza chochote. "Kama si shughuli hii muda huu ningekuwa kijijini nafanya shughuli za kilimo ambacho si cha uhakika," anasema. Kinachombakiza Glory katika Jiji la Dar es Salaam, ni kile anachokiita uwepo wa mzunguko wa fedha ambao kwa kijijini ni vigumu kuwepo. Anaeleza hata biashara yake ya kuuza nguo mtandaoni, isingefanikiwa iwapo angelikuwa kijijini kwa kuwa inahitaji uwepo wa mtandao 'internet' ambayo kijijini kwao haipo. Lakini shughuli za kilimo ni sababu nyingine anayoitaja Glory iliyomfanya ayaache makazi yake ya asili na kubaki Dar es Salaam, akisisitiza kilimo kinachosha. Anasema safari yake kutoka kijijini hadi mjini imekuwa na mafanikio kwa kuwa uwepo wa wateja wengi katika Jiji la Dar es Salaam, unamwezesha kufanya biashara na kujikimu kimaisha. "Mimi sijutii kuja mjini kwanza nilikuja kusoma, ajira sijapata nimejiajiri nafanya biashara zangu hii ni nzuri kwangu, nalisha familia," anasema. 'Mjini kuna msoto mkali' Alex John aliyetokea Mkoa wa Mbeya uliopo Kusini Magharibi mwa Tanzania na sasa anaishi Dar es Salaam, anasema si rahisi kuishi mjini kama wengi wanavyodhani, akifafanua kuna msoto mkali. Anasema aliuhama Mkoa huo kwenda Dar es Salaam mwaka 2016 baada ya Baba na Mama yake kufariki, akidhani mjini isingempa tabu kuishi vema, mtazamo ambao wanao hata marafiki zake aliowaacha kijijini. "Unakuta hata marafiki tuliowaacha kule huwa wananipigia simu kwamba ile... Nirushie buku (Sh1,000). Yaani wale kule wanajua ukishafika mazingira ya Dar es Salaam yaani mshikaji katoboa (kafanikiwa). "Hawajui kama huku kwenyewe msoto mkali, huku msoto mkali," anasisitiza. Magumu aliyokutana nayo katika Jiji hilo, anasema yamemfanya atamani kurudi nyumbani kwao (Mbeya), lakini kwanza anatafuta fedha zitakazomwezesha kufanikisha hilo. "Nilikuwa nafiriki nikifika Dar es Salaam maisha yanaweza kidogo yakawa afadhali, lakini nilipofika hapa (mjini Dar es Salaam) tofauti na kile nilichokitarajia, maisha yamenichapa," anasema Alex. Sitamani kurudi kijijini Mambo ni tofauti kwa Said Sued aliyetokea Mkoa wa Kagera uliopo Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania, anayesema hatamani kurudi kijijini kwa kuwa atakwenda kuanza upya. "Siwezi kutamani kurudi kijijini kwa sababu nikisema narudi kijijini naenda kuanza upya. Anayetamani kuja mjini aje Kwa sababu huku biashara yoyote unafanya na kuna mkusanyiko wa watu," anasema. Said anasema safari yake kutoka kijijini kwenda mjini mwaka 2011, ilitokana na wito wa mmoja wa watu aliyekuwa anafahamiana naye, aliyemtaka aende mjini kwa ajili ya shughuli mbalimbali. "Akanambia njoo Dar es Salaam tumekutafutia kazi, kwa hiyo nikafika. Nikipouliza nafanya kazi gani akanambia kwani huzioni? Nikaambiwa usiku tumekula umeona vyombo vichafu na mama atakupa nguo chafu ndiyo kazi zenyewe hizo. "Niliamua nitulie siwezi kusema nikimbie nirudi Bukoba, moja kwa moja nikawa nimejua kazi nilizoitiwa ni za ndani," anasema. Anasema ameifanya kazi hiyo kwa miaka miwili na baadaye aliuhama kutafuta shughuli nyingine na ndipo alipojikuta katika Soko la Shekilango alifanya biashara ya mbogamboga. Hatari vijana kukimbilia mjini Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Faraja Kristomus anasema vijana wanahitajika vijijini ili waendeleze uchumi wa maeneo hayo. "Tusipokuwa makini, vijana wengi wakihamia mjini, nguvu kazi ya vijijini itapotea, tutabaki na kundi kubwa la wazee. Shughuli za uchumi zitadorora kama kilimo, ufugaji na nyingine," anasema. Wanafuata faida Anasema vijana wengi hufanya uamuzi wa kwenda mijini kutokana na kukosa faida ya kile wanachokizalisha vijijini. "Wanadhani mijini ni rahisi kutengeneza fedha na faida. Bahati mbaya wanapofika mijini wanakutana na mazingira tofauti na kile walichoaminishwa walipokuwa kijijini," anasema. Anasema kinachowafanya wengi waamini mjini kuna fedha ni namna wenzao waliokwenda huko wanavyoonekana wamependeza na kunawiri. Mambo ya kuzingatia Kabla ya kuamua kwenda mjini, Dk Faraja anasema inakuhitaji ujue nini utakwenda kufanya. "Wale vijana wenye karama ya biashara, ujuzi mbalimbali mjini ni rahisi kupata kazi kwa sababu mtaji mkubwa wa mjini ni wingi wa watu na biashara inayokuwa na watu wengi huingiza faida," anasema. Wito kwa Serikali Anasisitiza ili kuvutia vijana wengi vijijini ni vema Serikali za nchi za Afrika, ziongeze tija kwenye shughuli wanazozifanya katika maeneo hayo, mathalan kilimo. Anasema ni vema vijana wa kijijini wakafundishwa mbinu mbalimbali za matumizi ya fedha, teknolojia na kuwepo miundombinu itakayowafanya wabaki vijijini. "Uwepo wa barabara, umeme, maji, Mawasiliano vitu kama hivyo vinaweza kuwafanya vijana wakashawishika kubaki vijijini kwa sababu wengi wanapoteza ndoto zao kwa kuja Mijini," anasema. Anasema anayetamani kwenda mjini ni vema akawa na ujuzi wa kumuingizia kipato na ajue atakwenda kufanya nini, vinginevyo atakutana na makundi ya watu wasio salama akaharibu ndoto zake.
Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na uj
Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na ujuzi na maarifa muhimu ili kujenga ustawi wa karne ya 21. Kwa kutambua hitaji hilo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua mpango wa kuanzisha klabu za kidigitali, unaolenga kukuza ujuzi wa kidijitali na ubunifu kwa vijana nchini. Kuhusu Klabu za Kidigitali Klabu za Dijitali ni mtandao wa vilabu vilivyoanzishwa katika shule mbalimbali nchini. Vilabu hivi hutumika kama jukwaa la wanafunzi kufuatilia vipengele mbalimbali vya teknolojia, kutoka kwa usimbaji 'coding' na upangaji programu hadi muundo wa wavuti na uuzaji wa dijiti. Kupitia shughuli za mikono, warsha na mashindano, washiriki wa klabu za Dijitali hupata ujuzi muhimu unaoboresha uwezo wao wa kuajiriwa na kuwaandaa kwa mahitaji ya uchumi wa kidijitali. Majukwaa haya pia yanawapa motisha wanafunzi kupenda ujuzi wa kidijitali kupitia kujifunza masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu (STEM). Kupitia vilabu hivyo, wanafunzi pia wanaonyeshwa fursa mbalimbali na wanakutanishwa na washikadau katika sekta hiyo. Kuimarisha ujifunzaji wa masuala ya digitali na ubunifu, klabu hizi zitaongeza ujuzi wa kiufundi, kadhalika kutakuza ubunifu na utatuzi wa changamoto. Kukuza usomaji wa digitali na ubunifu mpango wa klabu za digitali unajikita zaidi katika kutoa ujuzi wa kiufundi, pia inalenga kukuza ubunifu, utatuzi wa matatizo na kazi ya pamoja miongoni mwa washiriki. Kwa kuwahimiza wanafunzi kutumia maarifa yao mapya kutatatua changamoto za ulimwengu na hivyo klabu za kidigitali zitakuza utamaduni wa ubunifu, uvumbuzi na ujasiriamali miongoni mwa vijana. Zaidi ya hayo, klabu hizi zinahamasisha, wanafunzi, wasomi na watafiti kupenda masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Kuimarisha Fursa za Kielimu Klabu za Kidigitali sio tu zitaboresha maisha ya washiriki wake, bali pia zitaimarisha mazingira ya elimu nchini. Kwa kuwapa wanafunzi fursa ya kupata teknolojia na rasilimali za kidijitali, klabu hizo zitahakikisha vijana nchini wanapata fursa ya kushiriki katika ulimwengu wa kidijitali. Wajibu wa TCRA TCRA, ndiyo itakayoendesga mpango wa klabu hizo na itahusika kutoa msaada wa miundombinu muhimu ili kuhakikisha programu inafanikiwa. Katika kufanikisha hilo, TCRA imeshirikiana na wadau mbalimbali, zikiwemo shule, vyuo vikuu na washirika wa sekta hiyo, ili kuunda mfumo mpana wa ikolojia unaokuza maendeleo ya ujuzi wa kidijitali miongoni mwa vijana wa Tanzania. Mpango huu ni mustakabali mwema kwa vijana nchini utakaowawezesha kuwa na ujuzi na maarifa yanayohitajika ili kufanikiwa katika zama za kidigitali. Kwa kukuza elimu ya kidijitali, uvumbuzi na ujasiriamali, Vilabu vya Dijitali vinaweka msingi wa mustakabali mwema kwa vijana nchini. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, aliahidi Serikali kuunga mkono mpango huo. Alisisitiza dhamira ya Serikali kuunda mfumo wa sera utakaokuza uvumbuzi wa kidijitali kote nchini. Abdulla pia alitoa wito wa kuchukua hatua na kuzitaka shule, vyuo, vyuo vikuu na wadau wote wanaohusika na sekta ya elimu kushiriki kikamilifu katika kuanzisha Vilabu vya Digital ndani ya taasisi zao. Alipongeza juhudi za TCRA katika kuendeleza uanzishwaji wa vilabu hivyo na kuhimiza kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa na kuleta matokeo makubwa. Ushiriki wa Wizara na wito wake, unasisitiza umuhimu wa mpango wa Klabu za Dijitali katika kuwawezesha vijana wa Tanzania kwa ujuzi unaohitajika ili kustawisha karne ya 21. Kwa dhamira ya Serikali, kujitolea kwa TCRA na ushiriki wa taasisi za elimu, mpango wa klabu za digitali uko tayari kubadilisha hali ya kidijitali ya Tanzania na kutengeneza mustakabali mzuri wa vijana nchini.
Wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ikitabiri kuendelea kwa mvua nchini, wataalamu mbalimbali wames
Wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ikitabiri kuendelea kwa mvua nchini, wataalamu mbalimbali wameshauri mbinu za kuepuka madhara yatakayotokana na hali hiyo, ikiwemo kuwataka wananchi wapunguze safari zisizo za lazima. Wamekwenda mbali zaidi wakipendekeza mbinu kama ilivyofanyika wakati wa Uviko-19 zitumike, ikiwemo kufanyia kazi nyumbani, kuepuka msongamano barabarani, kuepuka kuvuka mifereji na mito kwa miguu ili kulinda usalama wa mali na maisha. Kauli hizo zinakuja kipindi ambacho, TMA imetangaza uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kuanzia Novemba 15 hadi 18 mwaka huu, inayotarajiwa kusababisha madhara mbalimbali, yakiwemo mafuriko, vifo, athari za usafiri na baadhi ya barabara kushindwa kupitika. Kulingana na mamlaka hiyo, mvua hizo zitaambatana na upepo unaotarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 40 kwa saa katika Mikoa ya Tanga, Morogoro, Pwani, Visiwa vya Mafia, Lindi, Pemba na Unguja. Akizungumza na gazeti hili jana, Mtaalamu wa Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Dk Leah Omar alisema ni muhimu wazazi wakafuatilia taarifa za TMA ili kuchukua tahadhari dhidi ya athari za mvua hizo kwa watoto. Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, ongezeko la mvua linaweza kusababisha maafa, akipendekeza kama kuna safari isiyo ya lazima ni vema kuiepuka. "Wananchi wanapaswa kununua mahitaji yatakayokaa muda mrefu kwa wale wenye uwezo ili kuepuka safari za mara kwa mara kwenye sokoni katika nyakati kama hizi,” alisema. Mabadiliko ya utendaji kazi, ni jambo lingine alilopendekeza akisisitiza kama aina ya kazi husika inaruhusu kufanyika nyumbani ni vema kufanya hivyo ili kuchukua tahadhari. Mbali na Dk Leah, mtaalamu wa tabia za watu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Profesa Deodatus Kakoko alisisitiza umuhimu wa kuepuka kukaa karibu na kingo za mito na maziwa, akisema ni maeneo hatari kuporomoka nyakati za mvua. Lakini, alisema iwapo utaona kivuko au daraja limejaa maji ni vema kuepuka kuvuka ama kwa mguu au kwa usafiri, kwa kuwa kuna uwezekano wa kusombwa na mvua. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mshikamano, Baraka Mwijande alitaka wazazi wawaepushe watoto kucheza katika maeneo ya mifereji na wahakikishe wanakunywa maji yaliyochemshwa au yaliyokingwa kwa dawa. “Katika kipindi hiki cha mvua, usalama ni jambo la muhimu kwa kuwa wezi wanatumia kelele za mvua kama fursa ya kuvunja milango na madirisha kuiba. Tukakikishe tunawasha taa kwenye nyumba zetu wakati wa mvua,” alisema. Mtaalamu wa mazingira wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Pius Yanda alisema: “Tunaishi kwenye jamii ambayo watu wengine hawana fikra mbadala na utamaduni wa kijamaa umekwisha. Kila familia inajali watoto wake tu,” alisema. Alisema katika kipindi ambacho Serikali imetoa taarifa kuhusu mvua, “Jambo la muhimu ni kutafuta mbinu za kuepusha madhara zaidi kwa sababu hata ukiwaambia wahame, watakwenda wapi na hata ukiwapa ardhi, hiyo ndiyo suluhu?” alihoji. Serikali Kutokana na utabiri huo, Serikali ilitoa tahadhari kwa wananchi ikiwataka kuchukua hatua mbalimbali ili kupunguza madhara ya kiafya yatakayosababishwa na mvua hizo. Miongoni mwa tahadhari hizo, iliwataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto hawachezi kwenye mvua au maji, watu wote waepuke kucheza kwenye kingo za mito na wasivuke kwenye vivuko vilivyofunikwa na maji. Tahadhari nyingine, kwa mujibu wa Serikali ni kuepuka kuegesha vyombo vya usafiri chini ya miti, madereva waongeze umakini na mwendo barabarani na wananchi wasijikinge na mvua kwa kusimama chini ya mti. Nyingine ni kutoshika wala kukanyaga waya wa umeme uliokatika, wanaoishi mabondeni au kando ya fukwe wahame na kuchemsha maji ya kunywa au kuyatibu kwa dawa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Matumaini ya wadau wa siasa juu ya kukoma kwa utaratibu wa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia ucha
Matumaini ya wadau wa siasa juu ya kukoma kwa utaratibu wa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia uchaguzi yanaendelea kuyeyuka, baada ya Serikali kuwasilisha bungeni muswada unaopigia msumari uhalali wa jambo hilo. Kwa mujibu wa wadau hao, wakurugenzi kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Rais kuwa na mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kunafanya uchaguzi usiaminike. Hata hivyo, Serikali imejibu hoja hizo za wadau ikisema kabla ya muswada huo kufikishwa na kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni, ilitoa nafasi ya kusikiliza maoni ya makundi mbalimbali ya wananchi. Mbali na majibu hayo, lakini wadau hao wanasema kitendo cha Ibara ya 74(1) (a) na (b) kumpa Rais mamlaka ya kuteua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa NEC, kunaifanya tume hiyo ipoteze sifa za kuwa huru. Hii ni kwa sababu, kwa utamaduni wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho ndicho chama tawala, Rais huvaa pia kofia ya mwenyekiti wa CCM taifa, hivyo kuteua wajumbe wa NEC watakaosimamia uchaguzi kunaleta ukakasi. Hofu nyingine ni kauli ya Rais wa awamu ya tano, John Magufuli 2017 anayodaiwa kusema haiwezekani ateue mkurugenzi, amlipe mshahara na bado amtangaze mpinzani kuwa ameshinda, hivyo kutaka wasimamizi wasiwe wateule wa Rais. Juni 13, 2023, mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, ilitoa hukumu ya kuwapiga marufuku wakurugenzi maarufu kama Ma-DED kusimamia uchaguzi na kuipa Serikali ya Tanzania miezi 12 kupeleka ripoti ya utekelezaji wa amri hiyo. Lakini Mei 2019, jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu lilibatilisha kifungu 7(1) cha sheria ya uchaguzi kilichokuwa kinaipa NEC mamlaka ya kuwafanya Ma-DED kusimamia uchaguzi, uamuzi uliotenguliwa na mahakama ya Rufani Oktoba 2019. Miswada na Ma-DED, mwenyekiti NEC Ibara ya 74(14) ya Katiba ya Tanzania inasema itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga iliyotajwa katika Ibara ya 5 ya Katiba. Lakini kifungu cha 6(1) cha muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2023 uliowasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita, kimezidi kufifisha matumaini ya wao kutosimami uchaguzi. Kifungu hicho kinasema kila mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, mji na wilaya atakuwa msimamizi wa uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika jimbo au kata na msimamizi huyo anaweza anaweza kusimamia jimbo zaidi ya moja. Lakini kifungu kidogo cha (2) cha sheria kinasema NEC inaweza kuteua kwa kuzingatia nafasi aliyonayo, mtu katika ofisi au kwa jina kutoka miongoni mwa watumishi wa umma mwenye sifa za mkurugenzi, kuwa msimamizi wa uchaguzi. Kifungu kidogo cha (5) kinasema msimamizi wa uchaguzi, kwa kuzingatia maelekezo ya mkurugenzi wa uchaguzi, anaweza kuteua watendaji kwa idadi inayohitajika, kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika jimbo au kata. Ukiacha sheria hiyo, lakini Muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa mwaka 2023 haujatoa suluhusho la muda mrefu la wadau wa uchaguzi, wanaotaka Rais na mwenyekiti wa CCM, asiteue mwenyekiti na makamu wa NEC. Kifungu cha 5(1) kinasema NEC itakuwa na mwenyekiti, makamu na wajumbe wengine watano watakaoteuliwa na Rais lakini hapo hapo sheria inasema NEC itakuwa ni chombo huru, kinachojitegemea na maamuzi yake hayataingiliwa. Sheria hiyo inasema wajumbe hao watano, watateuliwa baada ya majina yao kupatikana baada ya usaili utakaofanywa na kamati itakayofanya uchunguzi na kumshauri Rais, lakini muundo wa kamati hiyo nao unadaiwa kuwa na ukakasi. Hii ni kwa sababu wajumbe wa kamati hiyo karibu wote ni wateule wa Rais hivyo wadau wa demokrasia wanadai kifungu hicho ni kama changa la maji kwa kuwa wateuliwa hao kwa hisia tu, wanaweza kupokea maelekezo kutoka kwa Rais. Wajumbe hao ni Jaji wa Mahakama ya Rufani atakayekuwa mwenyekiti, Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Kamishina wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Bara na yule wa Zanzibar. Katika muundo huo, wamo pia wajumbe wawili wenye uzoefu wa masuala ya uchaguzi kutoka Tanzania Bara na mwingine kutoka Zanzibar na Rais atateua mjumbe mmoja kadri atakavyoona inafaa lakini kwa kuzingatia Jinsia. Walichokisema viongozi wa vyama Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje ya Chadema, John Mrema alisema bado usimamizi wa uchaguzi na uandikishaji wapiga kura limeachwa kwa Ma-DED. “Suala la Sheria ya Tume haina jambo jipya zaidi ya kuyaacha mamlaka ya Rais kuteua na kuondoa. Kuunda kamati ya Usaili ya watu wanne ni cosmetics (vipodozi) kwa sababu wote ni watu wa Serikali. Hakuna jipya,”alisema Mrema. Mrema alisema Muswada umeondoa suala la Wagombea kupita bila kupingwa isipokuwa Mgombea atapigiwa kura ya ndio au hapana na atahesabiwa kuchaguliwa ikiwa amepata kura nyingi haikusema apate zaidi ya asilimia 50. “Hakuna mabadiliko makubwa katika muswada unaopendekezwa. Sheria ya Tume haina kitu kipya isipokuwa Rais atashauriana na Kamati ya Usaili wakati wa kuteua au kumuondoa Mjumbe wa Tume. Kamati ya Usaili ina Wajumbe wanne pekee” Ni kejeli Mtaalamu wa Sheria, Dk Regemeleza Nshallah alikifananisha kilichofanywa katika miswada ya sheria hizo na kejeli na mzaha dhidi ya watu waliokuwa wanadai mabadiliko hayo. Kejeli na mzaha huo, unatokana na kile alichokifafanua, kilichobadilika katika miswada hiyo ni lugha kutoka Kiingereza kuwa Kiswahili, lakini si muktadha uliotarajiwa. “Kilichofanyika ni sawa na kujaza upepo kwenye tairi lenye pancha, mwisho wa siku hizi ni hadaa, kejeli na mzaha dhidi ya waliokuwa wanadai mabadiliko,” alisema. Dk Nshalla ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa, aliijenga hoja yake kwa ufafanuzi kuwa, licha ya ripoti ya kikosi kazi na vikao vya mapendekezo ya mabadiliko, hakuna kilichotiliwa maanani katika miswada hiyo. Kutokana na ufafanuzi huo, alisema kuna ishara kwamba hakuna nia njema ya kuwa na sheria za kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchaguzi huru na wa haki. “Kuna watu wapo kazini kuhakikisha mfumo wa uchaguzi unabaki kuwa kama ulivyo na kuhakikisha Rais na Wabunge wanapatikana si kwa kuchaguliwa na wananchi bali kwa kuteuliwa na tume,” alisema. Matobo mengi Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Mohamed Bakary alisema muswada huo una matobo mengi na haujatatua matatizo ya msingi. Aliyataja baadhi ya matobo hayo ni hatua ya wakurugenzi kuendelea kusimamia uchaguzi, akifafanua kwa mfumo wa utawala wa Tanzania jambo hilo si sawa. Aliufafanua mfumo huo wa utawala, akisema uteuzi wowote nchini unafanywa kwa kuangalia uelekeo wa kisiasa na kwamba wakurugenzi hao ni wanachama wa CCM, watatendaje haki kwa vyama vya upinzani. “Pamoja na uwezo wao wa kutawala lakini mfumo wa utawala wa Tanzania anayeteuliwa kushika wadhifa huo anatakiwa kuwa na imani ya chama cha CCM kwa maana nyingine ni wanachama wa CCM,” alisema. Hata hivyo, alieleza pamoja na miswada hiyo kupunguza baadhi ya matatizo, lakini matatizo ya msingi yatatatuliwa hadi hapo itakapopatikana Katiba Mpya. Majibu ya Serikali Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo alisema Serikali ilitoa nafasi ya kusikiliza maoni ya umma ‘public hearing’ kabla ya muswada huo kufikishwa na kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni. Alieleza hiyo ndiyo iliyokuwa nafasi ya wananchi wa makundi mbalimbali kushauri kuhusu kilichomo. “Tulitoa nafasi ya Public Hearing ile ndiyo ilikuwa fursa ya wananchi kutoa mapendekezo, kabla muswada haujafikishwa na kusomwa bungeni,” alisema.
Safari ya kuisaka suluhu ya mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, imeonekana kuwa m
Safari ya kuisaka suluhu ya mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, imeonekana kuwa mfupa mgumu uliowashinda viongozi wengi, baada ya ahadi na hatua zilizowahi kutangazwa nao kukosa matokeo chanya. Historia ya janga la mafuriko katika eneo hilo ina miongo kadhaa, huku vifo na familia kuachwa bila makazi zikiwa baadhi ya athari. Kukithiri kwa mafuriko katika eneo hilo, ndiko kulikoisababisha Serikali ya awamu ya nne, mwaka 2010 kuamua kuwahamishia Mabwepande wakazi wa eneo hilo, ingawa wengine waligomea uamuzi huo. Mgomo wa baadhi ya wananchi hao, uliisababisha Serikali kusaka mbinu za kudhibiti mafuriko katika eneo hilo na ndipo mwaka 2011, Rais wa wakati huo Jakaya Kikwete alipokuja na mpango wa kusafisha mto msimbazi. Uamuzi wake huo, ulitokana na kile alichoeleza, kwa kuwa wananchi wamegoma kuhama angalau mto usafishwe kuruhusu maji yapite bila usumbufu. Mpango huo nao haukufua dafu, mafuriko yaliendelea kushuhudiwa katika eneo hilo, huku kila kiongozi akizungumza lake bila kupata utatuzi wa tatizo. Baadaye mwaka 2018, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango aliutaarifu umma juu ya kupatikana suluhu ya kudumu, akisema Benki ya Dunia imekubali kufadhili maboresho ya bonde la mto msimbazi, utakaohusisha ujenzi wa daraja la Jangwani. Kama hiyo haitoshi, mwaka mmoja baadaye, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitangaza kujengwa kwa daraja hilo ingawa hakufafanua kwa kina kuhusu utekelezwaji wake. Ahadi hiyo ilipoteza nuru Desemba mwaka 2020, pale Mfuko wa Barabara ulipotangaza utayari wa kupitisha Sh4 bilioni kwa ajili ya kugharimia ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 300 katika eneo la Jangwani. Kabla ya mpango huo kutekelezwa, Novemba mwaka 2022, Serikali iliibuka tena na kuweka wazi juu ya ujenzi wa daraja la Jangwani na mikataba ya mradi huo kati yake na benki ya dunia ilisainiwa. Juzi katika eneo hilo, kumeshuhudiwa mafuriko yaliyosababisha kukwama kwa shughuli za usafiri na usafirishaji kwa watumiaji wa barabara ya Morogoro kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Suluhu ya kudumu Akizungumza na Mwananchi jana, Mratibu wa mradi wa Bonde la Mto Msimbazi, Nyariri Nanai alisema kutekelezwa kwa mradi wa bonde la mto msimbazi ndiko kutakapoleta suluhu ya kudumu ya changamoto hiyo. Alisema mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Tanroads. Katika mradi huo, Nanai alisema Tamisemi itahusika na ujenzi wa maeneo salama ya kuishi na Hifadhi ya Jiji ‘City Park’ huku Tanroads ikihusika na ujenzi wa daraja kutoka Magomeni Mapipa hadi Fire. Nanai alifafanua tayari fedha za kutekeleza mradi huo kiasi cha Dola za Marekani 260 milioni (zaidi ya Sh 651.3 bilioni) kutoka Benki ya Dunia, Serikali ya Uholanzi na Hispania, zimeshapatikana na michakato wa utekelezaji wa mradi husika imeanza. Alichanganua fedha hizo, akisema Benki ya Dunia imetoa Dola za Marekani 200 milioni (zaidi ya Sh501 bilioni) ambazo ni mkopo, Serikali ya Hispania Dola za Marekani 30 milioni (zaidi ya Sh75.15 bilioni) za mkopo na Uholanzi imetoa Dola za Marekani 30 milioni ambazo ni ruzuku. “Kwa sasa (Tamisemi) tupo katika hatua ya fidia na tunatarajia kuanza kuitoa jumatano (Novemba 15, mwaka huu) baada ya hapo tutatangaza zabuni kumpata mkandarasi,” alisema. Alifafanua kazi zitakazotekelezwa na Tamisemi mbali na ujenzi wa City Park, ni kuongeza kina cha mto kwa kuondoa mchanga na udongo na kwamba utahifadhiwa kwa ajili ya shughuli nyingine. Alieleza Desemba mwaka huu hatua ya manunuzi itaanza na hadi Aprili mwakani, tayari mkandarasi atakuwa amepatikana kwa ajili ya kazi hizo. Kuhusu ujenzi wa daraja, Nanai alisema tayari Tanroads wameshatangaza tenda na kupata mkandarasi na kwamba Januari mwakani ataanza ujenzi huo. “Hakuna suluhu nyingine zaidi ya mradi huu, hizi shughuli zinazofanywa sasa ni kupanua mto ili kurahisisha maji yapite, kwa sababu changamoto kubwa ya jangwani ni mto kujaa mchanga,” alisema. Kuhusu hatua za muda mfupi, alisema ndizo shughuli zinazofanywa na Serikali katika eneo la Jangwani angalau kupunguza kiwango cha athari. Kulingana na Nanai, kazi hiyo inafanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), ikihusisha kupunguza mchanga katika mto msimbazi ili kuruhusu maji yapite kwa urahisi wakati wa mvua. “Kazi inayofanywa sasa ni hatua za muda mfupi kupunguza kiwango cha athari nyakati za mvua, inafanywa na Tanroads, wakati kuna suluhu ya kudumu inaendelea,” alisema. Kauli ya Waziri Muda mchache baada ya Nyariri maelezo hayo, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alipotembelea eneo hilo jana, alieleza kusudio la Serikali kufumua ramani ya ujenzi wa daraja hilo. Uamuzi huo, unatokana na kile alichofafanua, ramani iliyopo isingeweza kuleta suluhu ya changamoto hiyo na kwamba itachorwa mpya kwa ajili ya kufanikisha hilo. Hata hivyo, alieleza uamuzi huo umetokana na ushauri wa Rais Samia Suluhu Hassan, ili kupata suluhu ya kudumu na kuondoa tatizo hilo linalojirudia mara kwa mara. "Novemba 16, tutafanya kikao na mkandarasi anayetakiwa kujenga mradi huu kupitia upya ramani ya ujenzi ili tuje na nyingine tunatamani ianzie Magomeni hadi Fire ili kuondoa kabisa changamoto hii ya muda mrefu badala ya kujenga kidogo," alisema. Lakini, alisema mazungumzo hayo hayataathiri ujenzi uliotarajiwa kuanza Februari mwakani, isipokuwa kinachofanywa ni kuboresha ili athari zisijirudie. "Pamoja na Serikali kuendelea kujenga miundombinu ya barabara na madaraja kukabiliana na athari za mvua zinazonyesha kutokana na mabadiliko ya tabianchi na Wananchi tunavyoishi tunapaswa kuwa sehemu ya suluhu kuacha kutupa takataka ovyo, chupa na mifuko ya plastiki," alisema. Kuhusu suluhu ya muda mfupi, alimtaka Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, John Mkumbo kuendelea kuondoa uchafu na mchanga katika mto huo ili maji yapite kwa urahisi. "Najua umeripoti na hujamaliza hata mwezi, sasa kipimo chako cha kwanza ili niweze kujiridhisha kwamba unatosha ni hapa kwenye kuzibua tope kutoka katika daraja hili na wakandarasi wasiwe wavivu kwenye kutafuta suluhu," alisema. Katika hatua nyingine, Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa aliwataka watendaji wa Mikoa mbalimbali kuangalia athari za mvua katika maeneo yao. "Wakati wa ukaguzi ni huu kwa sababu mvua zikinyesha ndizo zinazotuonyesha matobo yalipo. Tokeni maofisini mkaone changamoto zilizopo na mjipange kuona ni namna gani tutaweza kujenga barabara ambazo hazitaathiriwa na mvua," alisema. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aliahidi kusimamia hatua ya kuondoa mchanga na taka katika mto huo ili kuruhusu maji yapite. “Na tutatoa elimu ya usafi wa mazingira ukiangalia daraja hili na siku mbili zilizopita kulikuwa na chupa na uchafu mwingi uliojaa ukionesha kunashughuli nyingi za binadamu zinafanyika,” alisema. Kwingineko Arusha nako hali si shwari, baada ya mvua hizo kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi sita huku ikiwaacha wengine bila makazi. Akithibitisha vifo hivyo, Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, ACP Salvas Makweli aliwataka waliofariki ni Living Shirima, Ally Abdi, Wilson Lesikar, Zamzam Masudi na Innocent Shirima. "Hadi sasa waliopatikana ni hao na bado maaskari wetu wako kazini kuona kama kuna wengine lakini hawa pia tupate taarifa zao vizuri hivyo tunawaasa wananchi watoe taarifa wanapoona madhara mengine," alisema. Kamanda wa zimamoto na uokoaji wa mkoa huo, Osward Manjejele alisema mbali na miili hiyo pia watu sita wameokolewa na wako hai. "Mbali na hao tumeokoa watu sita usiku saa saba katika maeneo mbali mbali lakini niwaombe wana Arusha wachukue tahadhari wenyewe kwa maisha yao hasa wanaoishi mabondeni," alisema. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela alisema kamati ya maafa na ulinzi na usalama inafanya tathimini kujua madhara zaidi ya mvua hizo na taarifa rasmi itatolewa. "Kikubwa madhara bado ni makubwa na hatukutegema niombe wakazi wa Arusha wachukue tahadhari juu ya mvua zinazoendelea kunyesha lakini pia watoe taarifa juu ya mambo yote yanayotokea katika maeneo yao maofisa wetu wanaweza kuwahi na kupunguza athari,” alisema. Mwenyekiti wa mtaa wa msasani, kata ya Muriet, Rashid Jumaa alisema walikabidhiwa moramu yenye mawe lakini mchina aliyekuwa anatengeneza barabara chini ya idara ya Maji Arusha walikuwa wanauza na kuleta vumbi kumwaga. "Hapa moramu iliyokuwepo kwa kununuliwa Sh60,000 hadi Sh80,000 kwa gari wao waliuza kwa gari moja Sh30,000 hadi Sh40,000 na kwenda kutuletea mavumbi yasiyo na uzito na wala hawakushindilia hivyo mvua ilivyoanza ya mwezi Octoba ikasomba" alisema. Alipotakiwa kujibu hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi mkoa wa Arusha (AUWSA), John Ndetico aliahidi kushughulikia. "Hili swala sijui imekuwaje mkuu lakini kutokana na madhara yaliyotokea tunaomba radhi na tunaanza kazi leo ya kurekebisha barabara hizi,” alisema. Kutokana na hilo, Mongella alitoa siku tatu kwa AUWSA kufanya kazi ya kuhakikisha barabara zote zinatengenezwa upya. "Siku tatu nawapa hizi barabara zirudi kwenye hali yake na mimi nitakuwa napita asubuhi kabla ya kwenda kazini na jioni kabla ya kwenda nyumbani hakika tutaonana wabaya,” alisema. Wasomi washauri Kukithiri kwa matukio ya mafuriko, kunaonyesha haja ya kupitiwa upya kwa mipango miji, kama anavyofafanua Mkurugenzi wa Taasisi ya Tathmini ya Rasilimali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda. Alieleza shughuli hiyo ihusishe usanifu wa miundombinu inayotarajiwa na kuhakikisha ushirikishwaji wa wataalam wa hali ya hewa katika kupanga na kutoa makadirio sahihi ya mabadiliko ya tabianchi katika siku zijazo. "Hii ni muhimu kwa sababu mabadiliko ya hali ya hewa yapo hapa. Athari ni zinashuhudiwa na zitakua kwa kiasi kikubwa baada ya muda," alisema. Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wafanyabiashara wamedai mvua hiyo imekwamisha baadhi ya shughuli zao kwa kiasi kikubwa na hivyo kuongeza wasiwasi wa kiusalama. “Sisi wakazi wa mabondeni tunalala kwa wasiwasi tukihofia maji yasiingie majumbani mwetu, tunakaa usiku kucha tukijaza mchanga ili kuzuia mafuriko,” alisema Khadija Ali mkaazi wa Kawe Marani. Omary Pambe ni mwendesha pikipiki ‘bodaboda’ alitaja hali hiyo kuwakosesha abiria kwa sababu wateja wao wengi ni wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ikiwamo Mwenge. “Abiria ninaowapakia huwa wanafanya biashara Mwenge, mvua ikinyesha wanasema hakuna biashara, wanabaki nyumbani, abiria tunaowapata wanasema hatuna miamvuli na hawataki kupanda bodaboda tena,” alieleza Pambe.
Mjue Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wa kipekee ba
Mjue Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wa kipekee barani Afrika, anayewakilisha mafanikio na mwendelezo wa siasa za kidemokrasia Tanzania. Akichukua nafasi ya uongozi wakati mgumu baada ya kifo cha ghafla cha Rais John Pombe Magufuli mwaka 2021, Samia aliweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika madaraka hayo makubwa. Hata hivyo, safari yake kuelekea urais haikuwa ya ghafla wala ya bahati; ni matokeo ya miaka mingi ya kujituma, kujenga sifa kama kiongozi mwenye maono na ushawishi katika siasa za Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki. Katika maelezo haya, tutachambua safari ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu kuzaliwa kwake hadi alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania. Kuzaliwa na Maisha ya Awali Samia Suluhu Hassan alizaliwa mnamo tarehe 27 Januari, 1960, kisiwani Zanzibar. Akiwa ni mtoto wa familia ya kawaida ya Waislamu, maisha ya Samia yalitawaliwa na misingi ya nidhamu na heshima, pamoja na utayari wa kujifunza. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa umma aliyefanya kazi ya kawaida, wakati mama yake alijishughulisha zaidi na shughuli za nyumbani. Hali hii ya maisha ilimjenga Samia kuwa mtu anayeelewa changamoto za maisha ya mwananchi wa kawaida, jambo ambalo liliendelea kumshawishi katika siasa zake baadaye. Akiwa mdogo, Samia alionesha bidii katika masomo na aliazimia kupata elimu bora, licha ya vikwazo vya kiuchumi ambavyo vilikumba familia yake. Alianza masomo yake ya awali huko Zanzibar kabla ya kuhamia Tanzania Bara kwa masomo ya juu. Elimu na Mafunzo Elimu ya Samia ni sehemu muhimu ya safari yake ya uongozi. Baada ya kumaliza masomo ya msingi na sekondari, aliendelea na elimu ya juu katika Chuo cha Utawala wa Umma, Mzumbe (zamani kikiwa kinaitwa Institute of Development Management). Huko, alisomea masuala ya utawala na usimamizi, taaluma iliyomwandaa kwa kazi mbalimbali katika utawala wa umma. Alihitimu na kuanza kufanya kazi serikalini, ambapo alitoa mchango mkubwa katika sekta ya mipango na maendeleo. Lakini Samia hakusita kujiongezea maarifa; alisomea shahada ya uzamili ya Maendeleo ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza. Mafunzo haya yalimpa uelewa wa kimataifa na uwezo wa kushughulikia changamoto za kiuchumi, siyo tu kwa Zanzibar, bali kwa Tanzania nzima. "Nilikua nikiwa mdogo nikiwa na ndoto nyingi, lakini maisha ya familia hayakuwa rahisi. Baba yangu alikuwa mtumishi wa serikali, na sikuzote alinisisitiza kuhusu umuhimu wa elimu. Niliamini kuwa njia pekee ya kubadilisha hali yangu ni kupitia elimu, na nilijitahidi sana kusoma." Rais Samia, akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za wanawake wa Afrika mwaka 2019. Katika maneno haya, Rais Samia aliweka wazi kuwa licha ya changamoto za kifamilia, alielewa thamani ya elimu na umuhimu wake katika maisha ya mwanadamu. Alihitimu elimu ya sekondari na kujiandaa kwa hatua zaidi za kitaaluma. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Samia alijiunga na Chuo cha Utawala wa Umma, Mzumbe, ambapo alisomea Utawala na Usimamizi wa Maendeleo. Kiwango hiki cha elimu kilimjengea uwezo wa kutatua changamoto za utawala na maendeleo ya jamii. Mafunzo haya yalimpa uelewa wa namna serikali inavyoweza kusimamia miradi ya maendeleo na kusimamia rasilimali kwa ufanisi. Mchango wake katika kazi za utumishi wa umma ulionekana kupitia mafanikio aliyopata katika miradi aliyosimamia. Akiwa Mzumbe, Samia alijifunza umuhimu wa uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, jambo ambalo limekuwa msingi muhimu katika uongozi wake baadaye. Kwa kutambua umuhimu wa kuongeza elimu yake zaidi, Samia alijiunga na Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza, ambako alisomea Shahada ya Uzamili katika Maendeleo ya Uchumi. Mafunzo haya ya juu yalitoa msingi wa kitaaluma ulioimarisha zaidi uwezo wake wa kiutawala. Katika hotuba yake huko Manchester, aliwahi kusema: "Niliposoma Manchester, niligundua kuwa maendeleo ya kweli ya kiuchumi hayaji tu kwa kuweka sera, bali kwa kuwekeza katika rasilimali watu. Watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kuchangia uchumi wa taifa lao. Hapa ndipo nilipojifunza umuhimu wa kuwawezesha wananchi kiuchumi na kijamii." Rais Samia, akizungumza kwenye Chuo Kikuu cha Manchester mwaka 2015. Maneno haya yanaonyesha jinsi mafunzo aliyopata Uingereza yalivyompa mtazamo wa kipekee kuhusu jinsi maendeleo ya kiuchumi yanavyopaswa kusukumwa na uwekezaji kwa watu. Elimu yake ilimpa mbinu za kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuleta mabadiliko ya kijamii. Mbali na masomo ya darasani, Rais Samia alipitia mafunzo mbalimbali ya uongozi, yakiwemo mafunzo ya siasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mafunzo haya yalimuandaa vyema kwa majukumu ya kisiasa na kiutawala, hasa wakati alipokuwa Waziri na Makamu wa Rais. Elimu ya uongozi aliyoipata ilimuwezesha kufahamu namna ya kuongoza kwa busara na kushirikisha pande zote katika kufanya maamuzi muhimu kwa maendeleo ya nchi. Samia amewahi kueleza kuwa elimu aliyopata haikua tu ya darasani, bali pia kutokana na maisha halisi. Katika mojawapo ya hotuba zake muhimu, alisema: "Elimu ni mchakato unaoendelea, kila hatua ya maisha ni somo jipya. Kwa wanawake wenzangu, ninawaambia kuwa elimu inatufungua macho kuona fursa nyingi mbele yetu. Haijalishi umeanza wapi, lakini ni wapi unaelekea. Kwa hiyo, tuchape kazi na tusome zaidi ili tuweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu." Rais Samia, akizungumza katika hafla ya kitaifa ya elimu mwaka 2020. Katika maneno haya, Samia anaonyesha jinsi anavyotambua elimu kama silaha muhimu kwa maendeleo, hasa kwa wanawake ambao mara nyingi hukabiliwa na changamoto zaidi katika kufikia mafanikio. Pia alisisitiza kwamba elimu haimaliziki kwenye vyeti vya darasani, bali inaendelea kwa kila hatua ya maisha. Elimu ya Rais Samia imekuwa na matokeo makubwa katika mtindo wake wa uongozi. Uelewa wake wa masuala ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa umetokana kwa kiasi kikubwa na elimu yake ya kitaaluma pamoja na mafunzo ya uongozi. Katika nafasi zake kama Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Naibu Waziri wa Ardhi, na Makamu wa Rais, aliweza kutumia maarifa aliyopata katika chuo kikuu na mafunzo mengine kutekeleza sera zenye mwelekeo wa kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Akiwa Rais wa Tanzania, Samia ameendelea kusisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya taifa. Katika mojawapo ya hotuba zake za mwanzo baada ya kuwa Rais, alisema: "Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali, lakini ili kuufikia utajiri huo, tunahitaji kuwapa watu wetu elimu bora. Elimu ndiyo njia pekee ya kuwakomboa wananchi wetu kutoka kwenye dimbwi la umaskini. Serikali yangu itaendelea kuweka msisitizo mkubwa kwenye elimu ya ubora wa juu ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa sawa." Rais Samia, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa elimu mwaka 2021. Rais Samia ameweka wazi kuwa moja ya vipaumbele vya serikali yake ni kuimarisha elimu nchini Tanzania, ili iwe na mchango mkubwa zaidi katika kukuza uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya watu. Kuingia Kwenye Siasa Samia aliingia kwenye siasa rasmi miaka ya 2000, wakati ambapo Zanzibar ilikuwa inapitia mabadiliko ya kisiasa baada ya utawala wa muda mrefu wa chama cha ASP. Samia alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho ndicho chama tawala Tanzania. Akiwa mwanachama mwenye uwezo wa kipekee wa kuwasiliana na wananchi, haraka alijijengea heshima na ushawishi ndani ya chama. Mnamo mwaka 2000, alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Wete katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambapo alifanya kazi kubwa ya kuwasemea wananchi na kutetea haki zao. Umahiri wake katika kuwasilisha hoja zenye mantiki na kushirikiana na wenzake ulimfanya kuwa kiongozi anayeheshimika na mwenye mvuto. Katika kipindi hicho, aliweza kujifunza jinsi siasa za Zanzibar zilivyokuwa na changamoto zake za kipekee, hasa kwa sababu ya siasa za kikanda na mvutano baina ya chama tawala CCM na upinzani, hususan CUF. Samia alitumia muda wake mwingi kujifunza na kujenga mtandao wa watu waliomsaidia baadaye alipokuwa katika nafasi ya juu ya uongozi. Kuwa Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Samia alipata nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mwaka 2005, wakati wa utawala wa Rais Amani Abeid Karume. Hii ilikuwa nafasi muhimu katika maisha yake ya kisiasa, kwani aliweza kujifunza kwa undani masuala ya usimamizi wa maendeleo, sera za kiuchumi, na ustawi wa wananchi. Akiwa Waziri, alifanya juhudi kubwa za kuboresha maisha ya watu wa Zanzibar, hasa katika eneo la uwezeshaji wanawake na vijana. Alianzisha na kuongoza miradi kadhaa ya kiuchumi, ambayo ililenga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na kutoa mikopo midogo kwa wanawake na vijana. Kazi yake ilianza kumpa umaarufu sio tu Zanzibar, bali pia Tanzania Bara. Kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Makunduchi na Nafasi za Kitaifa Mwaka 2010, Samia alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Makunduchi, Tanzania Bara, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hii ilikuwa hatua kubwa kutoka siasa za Zanzibar kwenda kwenye siasa za kitaifa. Katika nafasi hii, aliweza kushiriki kikamilifu katika kutunga sheria na kujadili masuala muhimu ya maendeleo kwa Taifa zima. Wakati akiwa mbunge, Samia pia alipewa jukumu la kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Katika nafasi hii, alifanikiwa kuboresha mfumo wa umiliki wa ardhi na kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo ilikuwa tatizo kubwa katika maeneo mengi ya Tanzania. Aliendelea kupanda ngazi kisiasa kwa umahiri wake katika kutatua matatizo kwa njia za busara na ufanisi. Hakuwahi kuonesha haraka, bali aliweka msisitizo katika kutafuta suluhu za kudumu kwa matatizo yaliyokuwa yakiikumba jamii. Kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Mwaka 2015, Samia Suluhu Hassan aliteuliwa na Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi wa urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hatua hii ilishangaza wengi kwani Samia hakuwa ameonekana kama mwanasiasa mwenye nia ya kuwania nafasi za juu zaidi. Hata hivyo, uteuzi huo ulionesha wazi kwamba ndani ya CCM, umahiri wa Samia ulitambulika na kuheshimika. Katika uchaguzi huo wa kihistoria, CCM chini ya uongozi wa Magufuli na Samia walishinda kwa kishindo. Hivyo, Samia alikua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa taifa hilo. Kazi ya Makamu wa Rais na Changamoto za Uongozi Kama Makamu wa Rais, Samia alishughulikia masuala mengi ya kitaifa, huku akisaidiana na Rais Magufuli kusukuma mbele ajenda ya maendeleo, hasa katika ujenzi wa miundombinu na vita dhidi ya ufisadi. Alisimamia kwa karibu miradi ya maendeleo ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere, na utekelezaji wa mpango wa elimu bure. Samia pia alihusika moja kwa moja katika kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kusimamia mipango ya kimataifa kuhusu mazingira, jambo ambalo liliongeza umaarufu wake ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, nafasi yake kama Makamu wa Rais haikuwa na changamoto chache. Wakati mwingine alijikuta akikabiliana na masuala magumu ya kisiasa, hasa wakati wa mivutano ya kisiasa kati ya chama tawala na upinzani. Licha ya hayo, aliweza kushirikiana vizuri na Rais Magufuli na kuhakikisha ajenda ya maendeleo inaendelea kusonga mbele. Kifo cha Rais Magufuli na Kuapishwa kwa Samia Machi 17, 2021, Rais John Magufuli alifariki dunia ghafla, tukio ambalo lilitikisa nchi nzima. Katika hali ya kushtua na huzuni kubwa, Tanzania ilikumbwa na ombwe la uongozi. Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Makamu wa Rais ndiye anayechukua nafasi ya Rais endapo Rais aliyeko madarakani atafariki dunia au kushindwa kutekeleza majukumu yake. Mnamo Machi 19, 2021, Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kuchukua madaraka hayo makubwa, hatua ambayo ilisherehekewa kama ushindi wa demokrasia na usawa wa kijinsia Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Wakati wananchi wakilalamikia kuongezeka kwa makato ya kodi ya majengo kuanzia Julai 1 mwaka huu, Sh
Wakati wananchi wakilalamikia kuongezeka kwa makato ya kodi ya majengo kuanzia Julai 1 mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema ongezeko hilo ni malipo ya deni walilopaswa kukatwa Julai mwaka jana. Kwa mujibu wa shirika hilo, kodi ya jengo kwa nyumba za kawaida imesalia kuwa Sh1,500 kwa mwezi na ghorofa ni Sh7,500 tangu mabadiliko ya Julai mwaka jana. Ufafanuzi wa Tanesco unakuja wakati ambao, wananchi kupitia mitandao ya kijamii wanalalamikia kuongezeka kwa Sh500 katika makato ya kodi hiyo inayolipwa kupitia luku. Msingi wa malalamiko ya wengi ni kile anachodhani kuwa, Serikali imeongeza kodi ya majengo kutoka Sh1,500 hadi Sh2,000 kwa nyumba za kawaida. Katika mitandao ya kila aliyekatwa Sh2,000 alituma nakala ya muamala wake, akilalamikia Serikali kuongeza kodi kimya kimya. Baada ya hali hiyo, Tanesco jana kupitia kurugenzi yake ya mawasiliano na mahusiano kwa umma, ilifafanua hilo, ikisema hakuna kodi ya jengo iliyoongezeka. Badala yake, makato yanayoshuhudiwa kwa baadhi ya wateja, ni malipo ya deni la Sh500 walilopaswa kukatwa Julai mwaka jana, wakati utekelezaji wa ongezeko la kodi hiyo unaanza. “Tunapenda kuufahamisha umma kwamba hakuna ongezeko lolote lililofanyika kwenye viwango vya kodi ya majengo nchini isipokua ni madeni ya nyuma yaliyotakiwa kulipwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024,” ilieleza taarifa hiyo. Kwa mujibu wa Tanesco, baada ya mabadiliko ya kodi hiyo yaliyotangazwa Julai 26, mwaka jana kutoka Sh1,000 hadi Sh1,500 kwa nyumba za kawaida na Sh5000 hadi Sh7500 kwa nyumba za ghorofa. “Hii ilimaanisha kwa mteja aliyenunua umeme kati ya Julai 1 hadi 25 mwaka jana (kabla ya mabadiliko ya viwango vya kodi kuanza) alilipa kiwango cha zamani, yaani Sh1000 na hivyo kuwa na baki ya deni la Sh500 ambayo alitakiwa kulipa,” ilieleza taarifa hiyo. Ilieleza kwa kuwa madeni ya fedha hizo hayakulipwa kwa baadhi ya wateja, kinachotokea sasa ambao ni mwaka mpya wa fedha 2024/25 ni kwa mteja kukatwa kiwango ambacho hakikulipwa kwa mwaka wa fedha. “Makato ya madeni hayo yatafanyika kwa mara moja tu na yanatakiwa kulipwa kwa pamoja wakati mteja akifanya manunuzi ya umeme kwa mara ya kwanza kuanzia Julai 2024,” ilieleza. Hata hivyo, baada ya Julai, Tanesco ilisema mteja ataendelea kulipia viwango vya kawaida kulingana na aina ya nyumba anayoishi. Matumizi ya Shilingi badala ya Dola Katika hatua nyingine, baadhi ya taasisi na wakala za Serikali zimeanza kutekeleza agizo la Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba aliyetaka malipo yote yanayofanyika nchini yafanywe kwa shilingi badala ya dola. “Kuanzia Julai 1, 2024 naelekeza wadau wote wa ndani, taasisi za umma, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa na watu wote waliopo nchini Tanzania wenye tabia ya kuweka bei kwenye huduma au kuuza bidhaa kwa fedha za kigeni kuacha mara moja na kuhakikisha bei za bidhaa na huduma hizo zinatangazwa na kulipwa kwa Shilingi ya Tanzania,” alisema Dk Nchemba wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali. Kutokana na maelekezo hayo, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), zimetoa tangazo kwa wadau wote wa utalii kuhakikisha zinafanya na kupokea malipo kwa shilingi. Wadau wahofu Akizungumzia hilo, Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli za Kitalii Tanzania (HAT), Kennedy Mollel alikiri hatua hiyo ina tija katika kuongeza thamani ya shilingi, lakini katika sekta ya utalii inapaswa kuangaliwa vinginevyo. Hiyo inatokana na kile alichoeleza, kulikuwa na kiasi maalumu cha dola kilichokuwa kinatozwa kwa kampuni za kitalii na ziliwekwa kwa mujibu wa sheria. Mabadiliko yaliyofanyika, alisema yanamaanisha mamlaka zitaendelea kuhesabu kinachotozwa kwa dola, lakini kampuni ya kitalii itapaswa kulipa kiasi hicho kwa shilingi. “Hii maana yake, mteja akinilipa kwa dola kutoka nje, mimi nitatakiwa kulipa tozo kwa shilingi, ikitokea thamani ya dola imepanda nitalazimika kulipa zaidi, ikitokea imeshuka Serikali itapata hasara. “Ilipokuwa inatozwa kwa dola kama ni dola 60 maana yake utalipa kiasi hicho tu hakibadiliki, lakini ukitakiwa kuilipa hiyo kwa shilingi, leo itapungua kesho itapanda kutokana na thamani ya dola ya siku husika, kwa sekta binafsi tutaumia,” alisema. kwa mujibu wa Mollel, mpango huo ni mzuri lakini kwenye baadhi ya sekta kama ya utalii inahitaji kuangaliwa kwa umakini, kujua nani ataumia na nani atanufaika. Ili kuwepo ufanisi katika mpango huo, alipendekeza Wizara ya Maliasili na Utalii iweke kiwango elekezi cha tozo kwa shilingi ili kusiwe na mabadiliko. “Tukisema iwe Sh150,000 maana yake kila kampuni itapaswa kulipa kiwango hicho, yaani tusitoze kwa mtindo wa dola, lakini malipo yafanywe kwa shilingi, tozo zitambulike kwa shilingi na zitozwe kwa shilingi,” alisema. Njia nyingine aliyopendekeza ni kudhibitiwa kwa malipo ya dola taslimu, badala yake tozo hizo ziendelee kutozwa kwa fedha hiyo lakini lazima zilipwe kielektroniki. “Tukifanya hivi maana yake tutaendelea kudhibiti matumizi ya dola kwa njia ya taslimu, italipwa kwa mtandao na hakuna atakayetoa kuitumia. “Katika sekta ya utalii serikali inaweza kufikiria kuamua tozo zilipwe kwa dola lakini kielktroniki tu isiwe fedha taslimu. Hapo tutadhibiti matumizi ya dola na bado thamani ya shilingi itakuwa,” alieleza. Mhadhiri wa Utawala wa Biashara wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk David Amani alilitazama suala hilo kwa pande mbili, akigusia tija katika kuongeza dola nchini na kuimarisha thamani ya shilingi. Kwa upande wa pili, alieleza linaweza kusababisha changamoto ya michakato mingi kwa baadhi ya biashara kama utalii. Kuhusu tija, alisema matumizi ya shilingi yatafanya mtu yeyote anayekuja na fedha ya kigeni apewe fedha ya Tanzania, hivyo kutakuwa na kiwango kikubwa cha fedha ya kigeni nchini. Hatua hiyo, alieleza yataongeza thamani ya shilingi na kusisimua uchumi wa nchi. “Hatua hii itaondoa changamoto ya uhaba wa dola, tutakuwa na hifadhi kubwa ya dola na thamani ya shilingi itakuwa kubwa na hatimaye uchumi utaimarika,” alisema. Kwa upande mwingine, aliiona changamoto hasa kwenye biashara kama za utalii, akidhani pengine itamwongezea mtalii michakato ya kubadilisha fedha ndiyo aingie. “Jambo hili linaweza kuwa usumbufu kwa mtalii, kama hatutaboresha mifumo yetu ya kubadilisha fedha na ikawa rahisi na ya haraka,” alisema. Alisisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo wa ubadilishaji wa fedha wenye ufanisi ili mteja kutoka nje asione usumbufu wa kupata huduma. Kwa upande wa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Timoth Lyanga alisema hatua hiyo kwanza inaongeza heshima ya fedha ya Tanzania, kadhalika inakuza thamani yake. Iwapo fedha ya Tanzania itakuwa na thamani, alieleza itakuwa na nguvu katika manunuzi na hivyo uchumi wa nchi unaimarika. Madhara ya kuendelea kutumia dola nchini, alisema ni kuinyong’onyesha shilingi na hatimaye inakosa thamani na hadhi ilhali ipo kwenye nchi yake. “Unapotumia hela yako ya ndani unaiheshimu ili itumike kwa ajili ya kubadilishana bidhaa na huduma na unawafanya watu wengi wapate huduma kwa sababu upatikanaji wa shilingi ni rahisi kuliko dola,” alisema. Mvinyo Baada ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/25, wamiliki wa viwanda vya mvinyo walisema ongezeko la ushuru kwenye ethani utadhorotesha kilimo cha zabibu nchini. Ongezeko la kodi hiyo lilipendekezwa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba aliposoma bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 akisema kila lita ya ethane itatozwa ushuru wa Sh7,000 kwa zile zenye kilevi cha asilimia 80 au zaidi inayotoka nje ya nchi. Pia, alipendekeza kutozwa kwa ushuru wa Sh5,000 kwa kila lita ya Un-denatured Ethyl Alcohol yenye kilevi cha asilimia 80 au zaidi inayozalishwa ndani ya nchi. Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kusindika Mvinyo cha Alko Vintages, Archard Kato alisema kupanda kwa ushuru huo ni kuongeza changamoto kwa wasindikaji. Mbali na hiyo, alitaja changamoto nyingine ni ni kupanda kwa bei ya dola ambako kumeongeza gharama za uzalishaji wa mvinyo. “Sasa niwaambieni hakuna kampuni inayoathirika na suala la upandaji wa dola kama sisi bei tunayouzia wine ni wakati ule dola ikiwa ni Sh2,100 lepo hii dola ni 2,700 ama na zaidi bado bei ile ile. Na tunapoongezewa kodi kwenye spiriti (ethane), tena ni changamoto nyinge,” alisema. Kato alisema unapopandisha ushuru katika ethani, ni kurudisha nyuma kilimo cha zabibu kwa sababu uwezo wa kuuza utakuwa mdogo na hawatakuwa na uwezo wa kushindana na mvinyo kutoka nje. “Hatutaweza kuchukua zabibu nyingi kutoka kwa wakulima. Hili jambo inawezekana watu wasilione. Kama mkakati wa Serikali ni kuendeleza zabibu basi sera zetu zisipingane na nia tuliokuwa nayo,” alisema Kato. Akijibu hilo, Waziri wa Mipango na Uwezeshaji, Profesa Kitila Mkumbo alisema hatua ya Serikali kupitisha kodi katika ethani ililenga wanaozalisha vinywaji vikali nchini ambao watu wanapofanya manunuzi hurudishiwa kodi hiyo. “Sasa hii tumepokea ndio maana Serikali iko kila siku na Bunge linakaa mara kwa mara kwa hiyo tunaipokea, tutaichakata na huko mbele tutarekebisha vizuri tu,” alisema Profesa Kitila.
Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Yusuph Manji amezikwa jana Florida nchini Marekani, akiacha histori
Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Yusuph Manji amezikwa jana Florida nchini Marekani, akiacha historia ya kuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa waliowahi kutokea nchini. Heshima na jina lake, lisingekuwa kitu kipya katika masikio ya Watanzania wengi nyakati hizo, hiyo ilitokana na utajiri wake, kadhalika kujihusisha kwake na uwekezaji katika mpira wa maguu. Manji aliyefariki dunia juzi nchini Marekani, alikuwa mmoja kati ya wafanyabiashara wenye uwekezaji wa takriban Dola 700 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.8 trilioni) katika kampuni yake ya Quality Group Limite (QGL). Katika nyakati zake, Klabu ya Soka ya Young Africans ilistawi, ikifurahia msururu wa ushindi katika Ligi Kuu, ingawa dhamira yake ya kujenga uwanja wa klabu hiyo halikuwahi kutimia. Ni katika nyakati hizo, Manji aligeukia siasa na kuwa Diwani wa Mbagala, lakini upepo wake ulianza kubadilika mara tu ilipoingia madarakani Serikali ya awamu ya tano. Awamu hiyo iliyoongozwa na Hayati John Magufuli, ilianza kwa kuonyesha msimamo wa kupinga ufisadi na uzembe, huku akiahidi kusafisha Serikali na kurejesha uwajibikaji. Utawala wa Magufuli ulianzisha uchunguzi mkali katika sekta mbalimbali, ukiwa na lengo la kuondoa ufisadi na usimamizi mbaya. Hatimaye uchunguzi huo ulimfikia Yusuf Manji na kampuni yake ya QGL. Madai yaliibuka kuhusu ukwepaji wa kodi na mbinu zisizo sahihi za biashara ikiwa ni pamoja na tenda ya kusambaza sare za jeshi. Serikali kupitia maagizo ya Magufuli, ilianzisha uchunguzi wa shughuli za kifedha za biashara nchini, ikijumuisha himaya ya Manji. Ni katika kipindi hicho, ndipo utajiri wake ulianza kuingia katika mashaka, baada ya uchunguzi kubaini makosa ya kibiashara, ukwepaji wa kodi na hata kusababisha mfanyabiashara huyo kuingizwa hatiani. Mwaka 2017, katika moja ya kesi hizo kubwa, kampuni yake ya Farm Equipment ilifungiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akidai zaidi ya Sh12 bilioni, ambazo hazikuwa zimelipwa. Baadaye aliingia katika siasa na kuchaguliwa kuwa Diwani wa Mbagala Kuu, hili nalo likawa tatizo. Kutokana na changamoto za kisheria, akiwa rumande alipoteza nafasi yake kama Diwani, baada ya kushindwa kuhudhuria vikao sita vya baraza mfululizo. Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo alisema Manji amevunja kifungu cha 8, kifungu cha 25(5) (a) (b) cha sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kanuni za manispaa. Hata hivyo, uamuzi huo ulifanyika wakati Manji akiwa rumande kwa miezi kadhaa akisubiri kusikilizwa kwa mashtaka ya kiuchumi na usalama wa taifa yaliyokuwa yakimkabili enzi za utawala wa Hayati Magufuli. Licha ya kuachiliwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuondoa mashtaka hayo, bado hali ilikuwa mbaya kwa Manji baada ya Magufuli kumfutia umiliki wa shamba lake la ekari 714 Kigamboni, Dar es Salaam. Vyombo vya habari, ambavyo hapo awali vilijaa habari za umahiri wa biashara na misaada yake kwa kijamii, vikageuka kumwandika kuhusu ripoti za uchunguzi na changamoto zinazomkabili. Hali ilizidi kuwa mbaya kutoka pande zote. Taasisi za udhibiti zilimtaka kuzingatia sheria, wanahisa walihitaji hakikisho la uimara wake, na umma ulifuatilia kwa karibu habari hizo. Mfanyabiashara ambaye aliwahi kuwa na nguvu alijikuta akijikunyata kwenye vita ya kisheria na kukabiliana na changamoto nyingi ili kuokoa sifa na maslahi yake ya biashara. Manji na timu yake ya kisheria walijitahidi kujitetea, wakipinga madai hayo na kusisitiza dhamira yao ya kufanya kazi ndani ya mipaka ya sheria. Hata hivyo, hali ya kisiasa haikuwa na huruma, na msimamo wa Serikali kuhusu uwajibikaji haukuacha nafasi ya maafikiano. Kila siku iliyopita, himaya ya QGL iliyokuwa haiwezi kuguswa ilianza kusambaratika. Vita ya kisheria iligusa rasilimali, shughuli za biashara zilipungua kutokana na uchunguzi uliokithiri na mtazamo wa umma ulitetereka. Historia ya Yusuf Manji kama mwekezaji mkubwa wa biashara ilibadilika na kuwa mfanyabiashara anayepitia nyakati ngumu, akipambana kulinda urithi wake. Baadaye ulifika wakati kama maji unaweza kusema yameshamwagika. Alikabiliwa na changamoto za kisheria zinazoongezeka, msukosuko wa kifedha, na mabadiliko ya kisiasa, aliamua kujiondoa kwenye biashara zake. Himaya ya QGL, ambayo hapo awali ilikuwa nguzo ya mandhari ya biashara ya Tanzania, ilipitia mabadiliko na kugawanywa wakati mwanzilishi wake alipokabiliana na athari za mabadiliko ya kisiasa yaliyobadilisha bahati zake. Baada ya kipindi akiwa nje ya nchi, Manji alirejea Tanzania, akikaa chini kwa utulivu na kuonekana hadharani mara ya mwisho kwenye mechi ya Young Africans katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Vilio vya watu kutoweka na kutekwa vimeendelea kushika kasi nchini, huku wadau wakiinyooshea kidole
Vilio vya watu kutoweka na kutekwa vimeendelea kushika kasi nchini, huku wadau wakiinyooshea kidole Serikali kwa madai kuwa kuna viashiria vya kuhusika kwake. Kwa mujibu wa wadau hao wa kada mbalimbali, kinachoashiria ushiriki wa Serikali ni madai kuwa, watekaji wengi wanapokwenda kumchukua mtu hujitambulisha kuwa ni askari. Ukimya wa mamlaka zinazohusika na hatua dhidi ya watekaji ni jambo lingine lililotajwa na wadau hao, kusababisha mashaka zaidi kwa Serikali na taasisi zake kuhusika na matukio hayo. Mashaka na hoja hizo zinakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kutoweka kwa watu kutokana na kutekwa yaliyofululiza katika siku za hivi karibuni. Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa ni kielelezo cha matukio hayo, aliyetoweka Juni 23 jijini Dar es Salaam na Juni 27, mwaka huu alipatikana katika Hifadhi ya Wanyamapori Katavi akiwa amejeruhiwa. Kwa mujibu wa maelezo yake, alitekwa na watu wasiojulikana, walimlaza katika karakana ya Polisi Oysterbay na kumpeleka katika Mikoa ya Arusha kisha Katavi. Kijana huyo kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam. Tukio la Sativa lilifuatana na lililomtokea Kombo Mbwana aliyetoweka tangu Juni 29, mwaka huu na hadi sasa hajaonekana. Kombo alitoweka baada ya kufuatwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake na kumchukua kwa nguvu kwa mujibu wa mama yake, Hellena Joseph. Desemba 7, 2023, mfanyabiashara Mussa Mziba naye alitekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajapatikana. Mwingine ni Deo Mgassa aliyetekwa Oktoba 14, mwaka jana na kwa mujibu wa ndugu zake, alifuatwa nyumbani na askari wawili kisha wakaondoka naye na hadi sasa hajapatikana. Kuhusu Mgassa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amewahi kusema hawahusiki isipokuwa nao wanamtafuta kwani ni mtuhumiwa wa wizi wa kutumia silaha. Hiyo ni mifano michache kati ya mingi ya watu waliotekwa, wengine wakipatikana hai, wengine hadi sasa haijulikani walipo na wengine imeishia kupatikana miili yao. Serikali inadaiwa kuhusika Akizungumza na Mwananchi jana, Mwenyekiti wa Shura ya Maimamu, Sheikh Issa Ponda aliyahusisha matukio ya utekaji na mamlaka za Serikali hasa vyombo vya dola. Sababu za mtazamo wake huo ni kile alichoeleza, kuna viashiria lukuki kwamba matukio hayo, ama yanafanywa na vyombo vya dola au vinahusika nayo kwa namna yoyote. Katika ufafanuzi wa hoja yake hiyo, Sheikh Ponda alisema mara nyingi watekwaji au familia zao, wanapopatikana hueleza walioonekana kutenda matukio hayo, walijitambulisha kuwa ni maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama. Hisia zake hizo haziishii kwenye kujitambulisha kwao pekee, alieleza hata wanapofika aghalabu huwa na silaha, magari hasa aina ya Land Cruiser, vitu ambavyo si rahisi kumilikiwa na mtu binafsi. Kama hiyo haitoshi kwa mujibu wa Sheikh Ponda, watekaji kama inavyosimuliwa na familia zilizowahi kushuhudia ndugu zao wakitekwa, hutekeleza uharamia huo bila wasiwasi. “Nini kinawafanya wajiamini, kwanini wasiogope kukamatwa ni kwa sababu wanajua wao wenyewe ndiyo wakamataji kwa hiyo wanachokifanya hatatokea wa kuwakamata mwingine,” alisema. Kutokana na viashiria hivyo, Sheikh Ponda alisema Serikali inapaswa ieleze inapata faida gani kwa kutenda vitendo hivyo vinavyoweka rehani amani ya wananchi wake. Hata hivyo, kwa mwenendo uliopo, alisema hakuna dalili inayoonyesha kwamba vitendo hivyo vitakoma, kwa sababu Serikali haijaonyesha utashi wa kujichunguza. “Serikali kwa namna moja ama nyingine inahusika kwenye hali ngumu inayowakuta wananchi, itueleze inapata faida gani kwa kuwateka watu. “Kama watu hawa ni watuhumiwa mamlaka zipo zitumike kuwapeleka mahakamani ili hatua zichukuliwe dhidi yao, sio kuwateka,” alisema. Katika maelezo yake, alisema shura ya maimamu imeandika kitabu kinachohusisha familia 200 za watu waliotekwa na wakati wa uzinduzi baadhi zilikuwepo na Serikali ilikuwepo, lakini hakuna chochote kilichofanyika kudhibiti. Inatia mashaka Kinachompa wasiwasi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga ni uwezo na nguvu ya Serikali kuwajua wanaohusika na kuwakamata, lakini kwanini inaonekana kushindwa kwa watekaji. "Hata kama aliyetekwa hana simu janja, lakini Serikali ina mifumo yake ya kuangalia hali ya usalama hadi ngazi ya chini hasa vijijini tena katika mtaa akiingia mtu au mgeni anajulikana,” alisema. Kwa mkono mrefu ilionao Serikali, Henga alisema ni rahisi kufuatilia mwenendo wa usalama na kuwajua kadhalika kuwamata wanaohusika na vitendo hivyo. "Nadhani haijashindikana kuwakamata kwa haraka wanaodaiwa kuhusika na vitendo hivi, kinachotakiwa Serikali kuweka kipaumbele zaidi kwamba mtu anapopotea kuwepo na uharaka wa kumtafuta," alisema Henga. Hata hivyo, alisisitiza umuhimu wa Serikali kudhibiti vitendo hivyo kwa kufuatilia haraka ili aliyetekwa asipate madhara ya kujeruhiwa. Alieleza matukio kama hayo muda mwingine yanakuwa ya kihalifu au kuhusishwa na masuala ya uchaguzi. Lema kukutana na familia za waliotekwa Wakati wengine wakiwa na mitazamo hiyo, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbles Lema ametangaza kukutana na familia za waliotekwa nyumbani kwake mkoani Arusha. Katika mkutano huo, alisema atazungumza na kupata mlo wa pamoja na waathirika hao, kisha atakodisha magari kwa ajili ya kuwapeleka Ikulu ya Dodoma. Sababu ya kufanya hivyo, alisema: “Serikali inajua wahuni wanaofanya matukio haya.” Alieleza tayari ameanza kuratibu namna ya kuwapata ndugu wa watu hao kupitia ofisi za Chadema kila Wilaya na mkoa. “Serikali inapaswa kukomesha vitendo hivi, watambue tu kuwa wanaotekwa sio kuku ni binadamu,” alisema. Sambamba na uamuzi wake huo, Lema alimtaka Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati matukio hayo, kinyume cha kufanya hivyo kuna hatari ya kusababisha machafuko siku zijazo. Kwa mujibu wa Lema, matukio ya wananchi kutekwa hayaleti taswira nzuri kwa Serikali inayoongozwa na CCM. “Tunaitaka Serikali ichukue hatua hraka na za madhubuti, ili kuepusha machafuko yatayosababishwa na hali hii,” alisema. Akizungumza na Mwananchi Bagonza alieleza kushangazwa na hatua ya Serikali kushindwa kuwakabili watekaji, akirejea tukio la kutekwa kwa Edgar Mwakabela maarufu Sativa. Alisema kwa maelezo ya Sativa mwenyewe, watekaji hao walipita naye kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Arusha kisha Katavi imeshindikanaje walioteka kujulikana licha ya vizuizi vyote vilivyopo barabarani. “Yaani mtu achukuliwe Dar es Salaam, apelekwe Arusha hadi Katavi na vizuizi vilivyopo barabarani waliombeba wasijulikane,” alisema. Katika maelezo yake, alionyesha wasiwasi kwamba imewezekanaje kupatikana haraka kwa waliohusika na mauaji ya mtoto Asimwe Novath mwenye ualbino na ishindikane kwa watekaji. “Juzi mkoani Kagera aliuawa mtoto mwenye ualbino, Rais akatoa tamko kesho yake ndani ya saa 24 wahusika walipatikana, ebu fikiria? Sasa mengine yanatokea viongozi wanakaa kimya hadi mtu anachukua wiki kuonekana baada ya kutekwa hapo tueleweni nini,” alihoji Askofu Bagonza. Akizungumzia hilo, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa alisema umefika wakati Rais Samia Suluhu Hassan aone umuhimu wa kuunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa matukio hayo. Umuhimu wa uamuzi huo, alisema ni kujirudia mara kwa mara kwa aina hiyo ya matukio ambayo kimsingi yanavunja misingi ya haki ya kuishi. Hata hivyo, alieleza iwapo Rais Samia hatatekeleza hilo, atarajie kuona matukio ya namna hiyo yakiendelea kwa kuwa wahusika hawatakuwa na hofu ya kuteka. Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime simu yake iliita bila majibu. Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, alipopigiwa aliomba kutafutwa baadaye na hata alipotafutwa tena simu yake haikupokelewa. Ili kupata majibu ya Serikali kuhusu matukio hayo, Mwananchi iliwasiliana kwa simu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba aliomba litafutwe Jeshi la Polisi kwa taarifa zaidi. Kuhusu Sativa Kwa mujibu wa mratibu wa matibabu wa Sativa, Martin Masese alisema hali ya mgonjwa inaendelea vema katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam anakopatiwa matibabu. Wakati huohuo, THRDC imeungana na wadau mbalimbali kugharamia matibabu ya Sativa ili kuhakikisha anarudi katika hatua yake ya kawaida na kuendelea na majukumu ya kujiingiza kipato. “Tumekuwa tukifuatilia jambo hili tangu hatua ya kwanza, najua kuna wadau mbalimbali wanaendelea kuchanga na sisi tutagharamia matibabu yake. Zile fedha zinazochangwa zitamsaidia pindi atarudi katika hali ya kawaida maana sasa hivi amelala tu kitandani,” alisema Ole Ngurumwa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema atakuwa tay
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema atakuwa tayari kushiriki mdahalo wowote nchini unaolenga kujadili kwa hoja kuhusu utendaji wa Serikali na mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kauli kama hiyo imewahi kutolewa na mtangulizi wa Makalla katika nafasi hiyo, Paul Makonda ambaye Machi 31, mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Makalla ametoa kauli hiyo alipokuwa anajenga hoja juu ya wenye wasiwasi na uwezo wake katika kutekeleza majukumu ya uenezi wa CCM baada ya yeye na wenzake watatu kuteuliwa kuziba nafasi nne za wajumbe wa Sekretarieti ya CCM zilizokuwa wazi. Wenziwe watatu walioteuliwa pamoja naye ni John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Ally Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho. Hata hivyo, kauli hiyo ya Makalla imejibiwa na Mkurugenzi wa Habari, Uhusiano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema akimtaka asiishie kujinadi kuhusu mdahalo, bali auitishe ili wakutaje kujenga hoja. Makalla alieleza hayo jijini Dar es Salaam jana, alipohutubia katika hafla ya mapokezi yake na wajumbe wenzake watatu wa sekretarieti ya CCM walioteuliwa jana na NEC. Nipo tayari kwa mdahalo "Nataka niwaeleze nayaelewa majukumu ya nafasi yangu ya mwenezi, maana ninasoma mitandaoni baadhi wananikumbusha majukumu ya mwenezi. Nayaelewa yapo katika Katiba ya CCM. "Nipo tayari kwa mdahalo wa aina yoyote wa kujibu hoja na katika hilo upele umepata mkunaji" alisema. Chadema wamjibu Wakati Makalla akionyesha utayari huo, mwenezi wa Chadema, John Mrema alimtaka mwanasiasa huyo aandae hicho anachokita mdahalo kisha amwite wajenge hoja. Alisema kabla hajafikiria kuomba mdahalo na mtu, anapaswa kujua historia yake, akisema yupo tayari hata kesho (leo), iwapo Makalla atauitisha. “Anataka mdahalo kuhusu nini, anapaswa ajue historia ya mtu anayeomba kufanya naye mdahalo, nipo tayari hata kesho aitishe twende tukashindane kwa hoja,” alisema Mrema. Ilichosema CUF Kwa upande wa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa chama cha CUF, Mohamed Ngulangwa alieleza kiu yake ya mdahalo huo, akitaka unapaswa kuanza na wenezi wa vyama. Lakini, alisema jambo hilo litawezekana iwapo kutakuwa na ulinzi kwa wanamdahalo ili yasijirudie yaliyomkuta Jaji mstaafu, Joseph Warioba. “Warioba aliwahi kupigwa kofi katika mdahalo na mtu kwenye mdahalo na huyo aliyempiga hadi leo CCM inamuona anafaa kuwa kiongozi, kwa hiyo mjadala uhusishe ulinzi pia,” alisema. ACT Wazalendo Katibu wa Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT- Wazalendo, Salim Bimani alisema chama chake kimejipambanua katika siasa za midahalo. Alieleza wakati wowote kipo tayari kufanya aina hiyo ya siasa kwa kuwa ndiyo msingi wake na ndizo zinazojenga demokrasia ya kweli na ushindani wa hoja. Alisema kama maneno ya CCM ni uhalisia, alisema Makalla anapaswa kuandaa huo mdahalo kwamba yupo tayari kusimama naye. “Nipo tayari kushiriki katika mdahalo wowote, asiishie kusema aandae nitasimama kupambana naye kwa hoja,” alisema Bimani. Katika hotuba yake hiyo wakati wa mapokezi Makalla alisema atayatekeleza majukumu yake kuwa kuanza ulipo msingi wa chama hicho, kwa maana kuanzia ngazi ya mashina ili kuwaelimisha wananchi juu ya kuichagua CCM katika chaguzi zijazo. Hata hivyo, alisisitiza kuendeleza pale alipoishia mtangulizi wake, Makonda huku akifafanua anautekeleza wajibu huo ipasavyo. "Mimi Amos Makalla nimerudi nyumbani mna mashaka juu ya hilo, mna mashaka na historia yangu? Nimerudi nyumbani mara nyingi nimekuwa nikiwaeleza, nimetokana na CCM," alisema. Alisema uteuzi wa wajumbe hao uliofanywa na NEC umekamilisha kile alichokiita timu, huku akisisitiza wote wanajuana kutoka na historia zao ndani ya CCM. Kadhalika, Mwenezi huyo mpya alitaka kufanywa kwa siasa za kistaarabu kwa kuwa ndiyo mwenendo wa Rais Samia. Hapi Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wazazi wa CCM, Ally Hapi alianza kwa kufananisha mabadiliko ya sekretarieti yaliyofanyika na mabadiliko yanayofanywa dakika za mwisho katika mchezo wa mpira wa miguu "Sisi wachezaji tunaoingia dakika za majeruhi huwa ni 'Super Sub' Rais Samia ni kama vile kocha, anapopanga safu ya kwanza inaweka msingi, anapohitaji kiungo mtoa mipira amemuingiza Dk Emmanuel Nchimbi, kuna wale wakumaliza mchezo ndiyo sisi tulioingia dakika za mwisho," alisema. Hata hivyo, alisema chama hicho hakitakuwa na huruma ya kumwachia yeyote ushindi katika chaguzi zote, badala yake kitasimama kuhakikisha kinatafuta na kupata kura za kushinda maeneo yote. Katika hotuba yake hiyo, hakuacha kutupa kijembe kwa vyama vya upinzani, akisema vimekosa shukurani pamoja na kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara na kupewa ruzuku. "Wale jamaa wa upande wa pili ambao kazi yao ni kulialia, Rais amewatengenezea mazingira mazuri wanafanya mikutano na wamepata ruzuku shukurani hawana, niwaambie katika uchaguzi huu CCM haitakuwa na huruma," alisema. Akijibu hoja hiyo, Mrema alisema kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya wateule wa NEC ya CCM awamu hii wanaishia kuzungumza yasiyoeleweka akitaja wanapayuka. Alisisitiza chama chake cha upinzani hakitarajii huruma ya yeyote katika uchaguzi na ushindi wowote utatokana na juhudi zake, kama kinavyoendelea kufanya. “Kama wanataka kuona kivumbi wasibiri Aprili 20, mwaka huu ratiba tulishaitangaza tulipotoa azimio la Mtwara, kwa hiyo wakae tayari kusubiri maandamano mwezi huu. Tulisema tunasimama kupisha wenzetu wa mfungo wa Ramadhan na Kwaresma,” alisema. Kuhusu nafasi yake, alisema ndiyo mlezi wa makundi yote hivyo atafanya kazi hiyo kuhakikisha anawaandaa vijana na wanawake. Aliijenga hoja hiyo kwa kusisitiza kuwa, hana ugeni katika uongozi ndani ya chama hicho kwa kuwa amewahi kutumika nafasi mbalimbali katika Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (UVCCM). "Lakini mimi sio mgeni, nilikuwa vijana nikaazimwa na Serikali na sasa nimerudi, Waswahili wanasema kisu kimerudi katika ala lake," amesema. Ameeleza utayari wake wa kukitumikia chama hicho na Serikali hauna mashaka hata kidogo. Jambo lingine, amesema anakwenda kufanya kazi usiku na mchana na kushirikiana na watendaji wote ili kuifanya jumuiya ya wazazi isadifu ukubwa wake. Mongella Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella amesema kwa kuwa Rais Samia ameonyesha uvumilivu katika siasa, ni muhimu nao wakafuata mwendo huo. Lakini, amesema iwapo atatokea na atakayefanya siasa kinyume na mwendo huo, CCM kuna wataalamu wa kutosha wa mambo hayo. Hata hivyo, ameeleza asitarajiwe kuonekana zaidi kwenye majukwaa kwa kuwa nafasi yake ni kusimamia utendaji ndani ya chama hicho. "Kama mtu ana akili timamu baada ya kumsikia Jokate, Hapi, Gavu na Makalla maana yake muziki umeanza. Kama kuna mtu alikuwa hamuelewi Rais Samia hii safu ni ujumbe tosha," amesema. Amewakabidhi vijana wa chama hicho, kuhakikisha viongozi wa Serikali wanalindwa. "Mimi nakumbuka enzi zetu vijana tulipiga marufuku watu kutishwa, vijana ndiyo walinzi wa Chama," amesema. Jokate Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Jokate Mwegelo amesema uteuzi huo umempa fursa ya kuweka historia ndani ya UVCCM kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya utendaji mkuu wa jumuiya hiyo. Ameeleza alikuwa katika viwanja hivyo hivi karibuni chini ya UWT na kwamba anaweka historia nyingine ya kuwa mtendaji pekee aliyetumikia jumuiya mbili za chama hicho. Jokate amesema vijana wako timamu na wanajua nafasi yao kama walinzi wa viongozi wote na wasaka kura wa CCM. "Tunatuma salamu kwa wanaowatazama vijana wa CCM wanaosubiri wakosee, vijana wa CCM hatutakosea na hatutafanya makosa, tutashambulia kila kona kuzisaka kura za chama," amesema. Ameeleza vijana hawatakuwa nyuma katika kushiriki kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya uchaguzi kuanzia wa Serikali za Mitaa.
Kwa kumbukumbu zangu mjadala kuhusu vazi la taifa umekuwepo tangu enzi za Serikali ya awamu ya nne,
Kwa kumbukumbu zangu mjadala kuhusu vazi la taifa umekuwepo tangu enzi za Serikali ya awamu ya nne, ni kumbukumbu zangu, sijui ilikuwaje kabla ya wakati huo. Wakati huo wizara iliyokuwa na dhamana hiyo iliitwa, Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na waziri wake alikuwa Emmanuel Nchimbi, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mipango ilipangwa, mikakati ikawekwa na kauli na matamko yalitolewa, kadhalika ahadi pia, lakini kilichotarajiwa hakikuonekana. Enzi za Nchimbi zilipita, aliyemfuata naye hakuwa na mwenendo tofauti juu ya vazi la taifa, ni kama ilivyokuwa kwa Nchimbi tu. Ahadi kama kawaida, lakini hakuna aliyewahi kuona hata kipande cha vazi hilo. Mambo yaliendelea hivyo kwa kila aliyefuata na ulifika wakati, mawaziri walioiongoza wizara hiyo, sijui walijisahau au ilikuwaje, lakini neno vazi la taifa lilipotea midomoni mwao. Halikusikika kwa kipindi fulani. Rasmi vazi hilo limerudi kutamkwa wakati wizara hiyo ikiwa chini ya Innocent Bashungwa na Dk Harrison Mwakyembe alilitajataja lakini sio kiviile. Wakati wa Bashungwa, Serikali ilifanikiwa kurudisha matumaini ya wananchi kuhusu kupatikana kwa vazi hilo, lakini bahati mbaya mambo yalikuwa kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake. Hadi anaondolewa katika wizara hiyo, bado mwafaka kuhusu vazi hilo haukuwa umepatikana. Vikao vilifanyika na matamko yalisikika pia, lakini matokeo pengine tusubiri kiama. Kitabu cha Bashungwa kilifungwa hivyo, aliyemfuatia ni Dk Damas Ndumbaro naye anachechemea kwenye mienendo ya watangulizi wake kuhusu vazi hilo, lakini naona kama yale yale hivi. Nimeona nirejee historia kidogo ndiyo nijenge msingi wa hoja yangu kuhusu hiki kitendawili hiki kisichoteguka kwa takriban muongo mmoja na ushee. Tuache utani, hivi kweli vichwa vyote vilivyopita kuiongoza wizara hiyo vimeshindwa kupata vazi? Serious vazi? Kwa mtazamo wangu kuna zaidi ya kinachopatikana katika mchakato wa kulitafuta vazi hilo. Napata ujasiri wa kueleza hili, kwa sababu sioni nini kinaweza kukwamisha kupata nguo itakayotumika kuitambulisha Tanzania, labda kama si muhimu. Kama inawezekana kujenga vituo vya michezo kila Mkoa, tunaweza kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa na mengine mengi kwenye sanaa, utamaduni na michezo, vazi haliwezi kutushinda bwana. Ninazo taarifa juu ya vikao kadhaa ambavyo watendaji wa wizara husika wameshakaa na wanamitindo kuhusu kujadili vazi hilo, bado imekuwa vigumu kulipata. Tuachane na wanamitindo labda wanafanya mambo yawe magumu, kwa kuwa vazi la taifa ni suala la utamaduni, mila na desturi zetu, tutafute machifu, niamini mimi hawatashindwa. Michakato na ahadi zisizotimia zinajenga picha kuwa, nyuma ya kulisaka vazi hili kuna mtu anatupiga. Pengine yupo aliyekaa pembeni kazi yake kurefusha mchakato ili aendelee kuvuna. Sioni sababu ya michakato kuwa mirefu kama tunajua kinachotakiwa ni vazi la taifa, hivi tungepewa kazi ya kubuni la dunia ingechukua karne ngapi. Hata hivyo, Serikali inapaswa kuratibu na sio kuingilia utalaamu katika kubuni vazi hilo, tunapoteza fedha nyingi kwenye jambo lililopaswa kufanywa kwa wiki mbili. Ina maana miaka zaidi ya 10 tuliyotumia, tumeshindwa hata kwenda nchini Rwanda, Uganda na mataifa mengine ya Afrika Mashariki ambayo tayari yamefanikiwa kuwa na vazi hilo. Hatma ya upatikanaji wa vazi hilo ipo mikononi mwa Dk Ndumbaro kwa sasa na iwapo atalitekeleza hilo pengine itakuwa alama kubwa katika uongozi wake. Nachelea kuamini juu ya kupatikana kwa vazi hilo, kama bado utaratibu wa kupatikana kwake utaendelea kuwa ule ule ulioifanya Serikali ishindwe kwa miaka zaidi ya 10. Tuache kutumia kivuli cha vazi la taifa kutengeneza posho za vikao na kuvuna maburungutu ambayo kimsingi yangesaidia utekelezaji wa vipaumbele vingine vya Serikali. Lakini, wakati tunatafuta vazi hilo la taifa, turudi kwa wananchi kuwaeleza nini maana yake, manufaa na hata umuhimu wake kwao na kwa taifa kwa ujumla. Naeleza hili kwa sababu, wapo baadhi ya wananchi wameshaanza kuhoji kuna haja gani ya kuhangaika na kulisaka vazi la taifa, ilhali kuna mambo mengine yanayohusu huduma bado hayajakamilika.
Hatua ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kufanya mabadiliko katika sekretarieti ya CCM,
Hatua ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kufanya mabadiliko katika sekretarieti ya CCM, imehusishwa na maandalizi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani. Mambo mengine yanayotajwa kuchagiza mabadiliko hayo kwa mujibu wa wanazuoni mbalimbali ni kukisafisha chama hicho, huku wengine wakisema yasitarajiwe mambo mapya katika safu hiyo mpya iliyopangwa. Wasomi hao wamesisitiza hatua hiyo pia inalenga kuhakikisha sekretarieti inakuwa na safu inayoendana na kuwa na muunganiko utakaochagiza ufanisi katika utendaji wa chama hicho. Mitazamo hiyo ya wasomi inakuja muda mchache baada ya NEC ya CCM iliyoketi jana kuwateuwa makada wanne kuziba nafasi nne za wajumbe wa sekretarieti zilizokuwa wazi tangu Machi 31, mwaka huu. Walioteuliwa ni Amos Makalla kushika nafasi ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akimrithi Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Mwingine ni John Mongella ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akirithi mikoba ya Anamringi Macha aliyepelekwa Shinyanga kuwa Mkuu wa Mkoa huo. Kadhalika, Jokate Mwegelo amepokea kijiti cha nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) kutoka kwa Fakii Lulandala aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Safu hiyo inakamilishwa na Ally Hapi aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, akimrithi Gilbert Kalima aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro. Hata hivyo, mabadiliko hayo yaliyofanyika yanaacha wazi nafasi ya Katibu Mkuu wa UWT iliyokuwa ikishikiliwa na Jokate tangu mwaka jana hadi jana alipobadilishiwa majukumu. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachambuzi wa masuala ya siasa walitaja maandalizi ya uchaguzi na mbinu za kukisafisha chama hicho kuwa ndizo sababu za mabadiliko hayo. Kusafisha chama Kwa mtazamo wa mchambuzi wa masuala ya siasa Nassor Seif, uamuzi wa mabadiliko ya viongozi hao, umelenga kukiacha chama hicho katika usafi uliotukuka. Alieleza baadhi ya waliokuwepo kabla ya mabadiliko hayo, walihusishwa na tuhuma mbalimbali na wengi waliwalalamikia, pengine ndiyo sababu CCM imeamua kuwabadili. “Ndani ya CCM kuna mikakati, viongozi waliokuwepo katika nafasi hizo baadhi yao walilalamikiwa na wananchi, vyama vya upinzani, kwa chama makini hakiwezi kuwaacha watu wa namna hiyo, ni vema kiwaondoe ili kujisafisha,” alisema Seif. Hata hivyo, alieleza hakutakuwa na athari hasi juu ya uamuzi huo, akisisitiza walioteuliwa ni wazoefu na wanakijua chama hicho vema. “Ukiachana na uzoefu utendaji wa CCM umekuwa wa kubebana kama mtu anapwaya atapewa usaidizi na kuonekana kuwa bora kumbe kuna watu nyuma yake wanaoratibu utendaji wake, kwa hiyo sioni kama kutakuwa na athari hasi,” alisema. Shabaha ya uchaguzi Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Aviti Mushi alisema msingi wa mabadiliko hayo ni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani. “Kwa namna yoyote kilichofanyika ni kujiandaa na uchaguzi huu wa mwaka huu na ule wa mwakani, ndiyo maana wameamua kufanya mabadiliko,” alisema. Ingawa mwanazuoni huyo alieleza kushangazwa na hatua ya mabadiliko katika nafasi ya mwenezi wa chama hicho, akisema aliyekuwepo (Makonda), alifaa zaidi. “Kwa mtazamo wangu wangu ile nafasi (Makonda) aliiweza sana japokuwa kuna wakati alikuwa anazungumza vitu vinavyowapa wasiwasi, lakini aliwajengea imani sana wananchi, sasa kina Makala sijui kama wanayaweza mambo hayo,” alisema. Alieleza mabadiliko hayo ni kama yanakwenda kuipoozesha CCM, kutoka kwenye siasa za amsha amsha zilizokuwa zikifanywa na mwenezi aliyepita. “Japokuwa nguvu ya upinzani ni kama imefubaa lakini huwezi jua pengine karibu na uchaguzi wakawa na amsha amsha zile za maneno makali huenda chama kikajikuta kinapata shida,” alisema. Tusitarajie jambo jipya Hata hivyo, mabadiliko yaliyofanyika yalitarajiwa na wengi na walioteuliwa ni wale wale ambao wameonekana serikalini, kama inavyoelezwa na mwanazuoni mwingine kutoka Udsm, Dk George Kahangwa. “Ni watu walewale wanabadilishwa, inatupa picha hatupati jambo jipya isipokuwa kubadilisha nafasi na inatupa picha Rais ndiye mwenyekiti wa chama, anatoa watu ndani ya serikali na kuwapeleka kwenye chama na anatoa kwenye chama na kuwpeleka serikalini.” Dk Kahangwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa) alisema: “Yote yanayofanyika ni maandalizi ya uchaguzi wa seriali za mitaa na uchaguzi mkuu.” Mhadhiri huyo ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa alisema uteuzi huo ni vigumu kuutenganisha na Katibu Mkuu wa chama Dk Emmanuel Nchimbi: “Kwa sababu hadi Rais au Mwenyekiti anateua kuna watu wanaomwandalia, sasa upande wa chama katibu mkuu ana nafasi kubwa kwenye hili, kuwa huyu anafaa hapa na huyu hapa.” Alisema Dk Nchimbi amewahi kufanya kazi kwa karibu ndani ya chama na Makalla na Mongella hivyo kuna uwezekano mkubwa safu hiyo ni maandalizi ya chaguzi hijazo. Wasifu wa wachaguliwa: Makala Makalla alizaliwa Septemba 16, mwaka 1971 na kupata elimu ya Sekondari katika shule ya Galanos mkoani Tanga. Mwanasiasa huyo ni msomi wa shahada y uzamili katika biashara, aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro. Katika safari yake ya kuisaka elimu ya juu, Makalla pia amewahi kusoma katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Wasifu wake wa uongozi unaanzia ngazi ya UVCCM, kwani aliwahi kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo na baadaye alishika nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM. Nje ya CCM mwanasiasa huyo aliwahi kuwa Mbunge wa Mvomero mwaka 2010 na mwaka 2013 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na baadaye Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Kadhalika, Makalla amewahi kutumikia Mikoa mbalimbali kwa nafasi ya Mkuu wa Mkoa, ukiwemo Kilimanjaro, Mbeya na Katavi katika Serikali ya awamu ya tano. Chini ya uongozi wa Rais Samia, Makalla amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza alikohudumu hadi Machi 31, mwaka huu. Mongella Jina la John Mongella si geni sana katika masikio ya Watanzania, lakini pengine asiwe na umaarufu katika nafasi za uongozi ndani ya CCM. Kujulikana kwake kumetokana na nyadhifa mbalimbali alizowahi kuhudumu serikalini, ikiwemo Mkuu wa Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini. Utumishi wake katika nafasi za uteuzi, ulianza mwaka 2010 alipoteuliwa na Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Alihudumu kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2012 alipohamishiwa Wilaya ya Arusha ambako nako hakuhudumu muda mrefu hadi pale alipopandishwa kuwa Mkuu wa Mkoa. Novemba mwaka 2014, Rais wa wakati huo, Kikwete alimteuwa Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, akipanda kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Baadaye Machi mwaka 2016, Rais wa awamu ya tano, John Magufuli alimteuwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, nafasi aliyohudumu hadi Mei mwaka 2021. Kisha mwanasiasa huyo aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, wadhifa ambao alibadilishiwa siku ya kuapishwa kwake. Katika uapisho wa nafasi hiyo, Rais Samia alitangaza kumhamisha Mongella kutoka Mkoa wa Simiyu kwenda mkoani Arusha kwa kile alichoeleza, kiongozi huyo ameshakuwa na uzoefu wa kuongoza majiji. Alihudumu katika wadhifa huo hadi Machi 31, mwaka huu Rais Samia alipomteuwa Makonda kurithi nafasi hiyo, huku taarifa ikieleza Mongella atapangiwa kazi nyingine. Hapi Kwa upande wa Hapi ni msomi mwenye shahada ya kwanza ya sheria na shahada ya uzamili ya masuala ya biashara na utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Aprili 16, mwaka 2016 hayati John Magufuli alimteua kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, akichukua nafasi ya Paul Makonda ambaye kwa wakati huo alipandishwa na kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Julai 28 mwaka 2018, aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa, kisha Mei 15, mwaka 2021 Rais Samia alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, lakini hakudumu kwa muda mrefu akahamishiwa mkoa wa Mara. Julai 28, mwaka 2022 Rais Samia alitengua uteuzi wake na tangu wakati huo alionekana katika mitandao ya kijamii akijihusisha na shughuli za kilimo mkoani Iringa. Jokate Jokate alizaliwa Machi 20, mwaka 1987 na akasoma elimu ya Sekondari katika shule ya Mtakatifu Anthony Mbagala wilayani Temeke kisha kujiunga sekondari ya Loyola wilayani Ubungo kwa masomo ya kidato cha tano na sita. Mwaka 2007 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu shahada ya kwanza ya sanaa katika sayansi ya siasa. Baadaye mwaka 2018 hayati Magufuli alimteua kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe. Julai 2021 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke, mwaka jana ahamishiwa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Safari yake ya Utumishi ndani ya serikali ilifikia hapo na Oktoba mwaka 2023 NEC ya CCM ilimteuwa nkuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT). Hata hivyo, kuteuliwa kwake ndani ya UVCCM si mara ya kwanza, kwani aliwahi kuwa Katibu Hamasa na Chipukizi wa jumuiya hiyo. Aidha katika kikao hicho cha NEC ya CCM taifa, Serikali zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar zimepongezwa kwa kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020/25.
Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kufikia Desemba mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ahakikishe
Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kufikia Desemba mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ahakikishe mifumo yote ndani ya Serikali inasomana. Hii si mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa nchi kutoa maelekezo hayo, aliwahi kufanya hivyo Juni 9, mwaka jana katika Baraza la Biashara Dar es Salaam, akitaka kuharakishwa kwa maboresho yatakayofanya mifumo ya taasisi za umma isomane. Agizo kama hilo alilitoa tena Agosti 11, mwaka jana kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kuhakikisha mifumo yote ya Tehama inayotumika ndani ya Serikali inasomana. “Nilishasema mara mbili hii mara ya tatu natarajia kuona utekelezaji,” alisema Rais Samia. Rais Samia ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Aprili 3, 2024 alipohutubia hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC). “Mifumo yote ya Tehama isomane, sio yule anakwenda kushoto kulia, mashariki, magharibi hakuna kusomana hakuna mawasiliano ndani ya Serikali,” amesema. Katika maelekezo yake hayo, ametaka hilo likamilike kufikia Desemba mwaka huu na aliwataka Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali kuhakikisha wanasimamia utekelezwaji wake. “Kuna taasisi muhimu zipo maeneo mbalimbali IGA ipo Utumishi na tume hii ipo Wizara ya Habari, niombe basi kuwe na mratibu ambaye yupo katikati,” amesema. Mbali na agizo hilo, Rais Samia ameitaka PDPC kuhakikisha inazisajili taasisi zote za umma na binafsi zinazoshughulika na uchakataji na usafirishaji wa taarifa binafsi kabla ya Desemba mwaka huu. “Pia hakikisheni zinazingatia matakwa ya kisheria katika shughuli hizo na tume itoe elimu kwa taasisi hizo,” amesema. Amewataka maofisa wa tume hiyo kuifanya kazi hiyo ya usajili wa taasisi za umma na binafsi kwa ubora na kuhakikisha wananchi wanaridhika na utunzaji wa taarifa zao. Hata hivyo, mkuu huyo wa nchi amesema kuna umuhimu wa faragha katika taarifa binafsi, ndiyo maana Serikali imeamua kutunga sheria na kuwa na tume hiyo. “Ingekuwa taarifa zetu zote ziko wazi na watu wanazijua tusingetazamana usoni, au hii dunia ingekuwa kitu kingine, lakini kwa sababu kila binadamu anahitaji faragha na staha ndiyo maana tumekuja na sheria hii ili kutunza utu wa mwanadamu,” amesema. Ameeleza baadhi ya taarifa zinaweza kuhujumu jamii na wakati mwingine kusababisha unyanyapaa. “Unaweza kutoa taarifa ya mtu na ikaleta vurugu kwenye jamii, vita na pengine kuuwa mtu, kwa hiyo kuna kila haja ya kuwa na sheria hii,” amesema. Kwa upande mwingine, amesema taarifa binafsi ni biashara kubwa kwa kampuni za kimtandao hivyo hapana budi kuzilinda. Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema wakati dunia inajenga uchumi wa kidigitali uliozifanya taarifa kuwa bidhaa muhimu, kuzingatia faragha, heshima na utu wa watu ni jambo la msingi. Ameeleza umuhimu wa tume hiyo ni hata katika kulinda maslahi ya wawekezaji ndani na nje ya nchi, wawekeze kwa tija. “Tume inatarajiwa kuimarisha misingi ya demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria, mazingira haya yatavutia uwekezaji wa ndani na nje kwani wawekezaji watakuwa na uhakika na uwekezaji wao,” amesema.
Taasisi za umma na binafsi zinazohusika na shughuli ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi z
Taasisi za umma na binafsi zinazohusika na shughuli ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi za watu, zimetakiwa kuhakikisha zifanyanya kazi hiyo zikiwa na vibali stahiki. Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Aprili 3, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Emmanuel Mtulya alipozungumza katika hafla ya uzinduzi wa tume hiyo. Amesema kwa sababu tayari tume inayohusika na usimamizi wa taarifa hizo imeanzishwa hapana budi kwa taasisi zinazofanya kazi ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi kuomba vibali vya kufanya kazi hiyo. “Nazisihi taasisi za umma na binafsi zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi kuomba vibali vya kufanya shughuli hizo,” amesema. Mwenyekiti wa bodi ya tume hiyo, Balozi Adadi Rajabu ameahidi kuhakikisha ulinzi wa taarifa binafsi za watu na kusimamia utendaji kazi kwa weledi. “Chombo hiki kimeshaanza kazi na tuemanza na mikakati maalum ya kukijenga na kutoa elimu kwa wananchi. Chombo hiki ni kigeni sisi tumechelewa sana kukianzisha. Bodi tunakuhakikishia mheshimiwa Rais kuwa chombo hiki kinafanya kazi zake kwa weledi,” ameeleza. Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alitoa hakikisho la usalama katika Jiji hilo, huku akidokeza watakaothubutu kuharibu amani watakiona. “Tumetoka kwenye pasaka, kuna gazeti liliandika mauaji yarindima, nikuhakikishie mheshimiwa Rais, hakuna mauaji yaliyorindima Dar na kama yatakuja kurimba basi watakaosababisha yatawakuta makubwa,” alisema. Hata hivyo, alisema katika nyakati zinazokaribia uchaguzi aghalabu wawekezaji huogopa kuweka mitaji kwa hofu ya vurugu zinazoweza kujitokeza. “Mwaka huu tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sisi viongozi tunathibitisha kwamba uchaguzi utakuwa imara, amani na utulivu itakuwa ndiyo kipaumbele chetu,” alisema.
Huenda mrithi wa Paul Makonda katika nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na
Huenda mrithi wa Paul Makonda katika nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, asitofautiane sana na mwanasiasa huyo, kwa maana ya mtindo wa uongozi. Mtindo wa Makonda katika miezi michache ya uongozi wake ndani ya CCM, zimeshuhudiwa amsha amsha zilizokiwe hai chama hicho nap engine kuvutia makundi ya wananchi wengi, hilo linathibitisha na umati uliokuwa ukijitokeza katika mikutano yake ya hadhara. Mwenezi mpya atakayechaguliwa na NEC kesho (Aprili 3, 2024) pia huenda asikaribiane na Makonda kwa kila kitu katika uongozi lakini wakafanana kwa vitu vichache. Kwa sababu hadi Makonda anakabidhiwa uenezi kwa lugha nyepesi chama hicho tawala hakikuwa na mtu anayeweza kuamsha amsha. Mfano kabla ya Makonda alikuwapo Sophia Mjema ambaye hakuwa mtu wa amsha amsha, sambamba na Shaka Hamdu Shaka, lakini mtu pekee aliyejitahidi kwa kiwango fulani kuleta hamasa au amsha amsha ndani ya CCM ni Hamphrey Polepole. Lakini Oktoba 22 mwaka 2024 Makonda alipopewa kijiti hicho, kutoka kwa mtangulizi wake Mjema ‘vibe’ hamasa ikawa kubwa kama ambavyo watoto wa mjini hupenda kutumia msemo ili kueleweka kwa urahisi. Hata hivyo, safari ya Makonda kwenye nafasi hiyo imekuwa ya muda mfupi, tofauti na watangulizi wake, kwa kuwa amedumu kwa miezi mitano hadi Machi 31, 2024 Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya mabadiliko kwa kumtoa kwenye nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Ndani ya miezi mitano ya Makonda kuhudumu kwake katika nafasi ya uenezi, mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni amekuwa ni kiongozi asiyeogopa mtu katika utekelezaji wa majukumu yake. Alipenda kujishusha na kujiweka karibu na wananchi hasa wenye hali ya chini kwa lengo la kujua matatizo na kuyapatia ufumbuzi kupitia ziara zake alizozifanya kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka jana hadi mapema mwaka huu. Makonda alikuwa tayari kuwavaa watendaji wa juu wa Serikali au chama kwa lengo la kuwataka ufumbuzi wa kero zinazowakabili wananchi kulingana na nyadhifa zao ndani ya CCM na serikalini. Ilikuwa kawaida kuingia kwenye mikutano yake ya hadhara kwa mitindo mbalimbali, ikiwemo kupanda farasi, guta, pikipiki, baiskeli, lori la mchanga na hata trekta, jambo ambalo lilizua gumzo na kuibua shauku ya wengi wakitamani kujua ataibuka na mtindo upi. Alikuwa na staili ya kuwabana watendaji wa chama chake na Serikali, alikuwa haoni aibu kumuambia ukweli kiongozi kuhusu utekelezaji wa majukumu katika idara au eneo husika alilopewa dhamana. Makonda ni kiongozi ambaye muda ambao haumtegemei anatoa kauli au maagizo yanayowaacha watu na mshangao au kuzua mjadala na kutafakarisha jamiii. Mfano Novemba Mosi, 2023 akiwa jijini Dodoma, Makonda alimpa miezi sita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushughulikia changamoto ya ardhi inayojitokeza mara kwa mara. Ingawa agizo lake hilo liliibua mjadala, wengi wakihoji inawezekanaje mwenezi amuagize Waziri Mkuu, lakini kwake ilikuwa kawaida na baadaye alishuhudiwa akiwa na kiongozi huyo kwa mazungumzo, huku wakifurahia. Kama hiyo haitoshi Makonda aliwataka viongozi wakuu wa Chadema, Freeman Mbowe (mwenyekiti) na Tundu Lissu (makamu mwenyekiti wa chama hicho, bara) kuketi mdahalo badala ya kuhamasisha Watanzania kuandamana. Lakini hivi karibuni katika mapokezi ya ndege ya Boeing B737-9 Max kutoka Makonda alitoa kauli akisema kuna kasumba inayoendelea ya kutaka kumtofautisha Rais Samia na mtangulizi wake, hayati John Magufuli. Katika mapokezi hayo, Makonda alinukuliwa akisema “Huwezi kuwatenganisha hawa watu na viongozi wengi wanafiki wanaotafuta kujipendekeza kwa Rais Samia kila wakipata jukwaa wanataka kumfanya Samia kama si sehemu ya Dk Magufuli. Kama msemaji wa chama kila anachokifanya Rais Samia, ndicho alikifanya Magufuli. Wenezi wengi waliopita Polepole aliteuliwa kuwa mwenezi wa CCM enzi za utawala wa Magufuli mwaka 2016, akimrithi Nape Nnauye, lakini wadhifa wake huo ulikoma muda mchache baada ya uenyekiti wa Samia. Kuondoka kwake, wengi wamekuhusisha na kile kinachoelezwa kuwa, Samia alipoingia madarakani alilazimika kuunda timu mpya itakayomsaidia kuyakabili makundi dhidi ya utawala wake. Ndipo Aprili 30, 2021 akamteua Shaka kuwa Mwenezi amsaidie kumjenga zaidi kichama kutokana na hulka yake ya kufanya harakati za kukutana na makundi mbalimbali. Baada ya muda si mrefu naona maono na matamanio ya Mwenyekiti (Rais Samia) kwa Shaka yalikuwa hayatimii ikiwemo ajenda ya kuwaunganisha wanachama na kufafanua ajenda vizuri. Hilo likatoa nafasi kwa makundi mengi kujitokeza na kujinasibisha kama wasemaji wa chama baada ya yeye kuonekana zaidi kama msemaji wa Rais na siyo wa Chama. Inaelezwa katika kipindi cha Shaka, ndipo makundi yaliyojinasibu kwa majina mbalimbali yalijitokeza zaidi, ikiwemo ‘Chawa wa Mama’. Huenda alilifanya kwa nia njema, lakini haikufaa kwa wakati wake. Baadaye Rais Samia akaona amweke kando Shaka na kuamua kuandamana na Mjema kama msemaji wa CCM. Safari hii aliona amteuwe mwanamke kwenye nafasi hiyo ili amsaidie kutimiza maono yake ya kukifanya Chama na yeye mwenyewe wakubalike zaidi kwa wananchi. Inadaiwa Mjema alionekana kupwaya zaidi kwa kuwa kimya zaidi katika kukisemea Chama. Hakuwa na ujasiri wa kukisemea chama na kukisafisha ilipotokea kinashutumiwa au kushambuliwa na wapinzani. Katika kipindi chake, ndio uliokuwa wakati mgumu zaidi katika utawala wa Rais Samia na chama chake, kwani ilikuwa katikati ya mjadala kuhusu uwekezaji wa bandari. Mjadala huo ulioshikiliwa kidedea na wanaharakati na vyama vya upinzani ndiyo uliodhihirisha mapungufu ya idara ya uenezi ya CCM juu ya kujibu hoja. Serikali iliamua kuingilia kati kwa kuunda timu ya kuzunguka nchi nzima kujibu hoja na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uwekezaji huo, uliokuwa unapingwa na wanaharakati na wanasiasa wa upinzani. Katika nyakati hizi ambazo siasa zinatarajiwa kupamba moto kutokana na Uchaguzi wa serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji kukaribia, unaweza ukasema mwenezi machachari na anayeijua siasa ya watu wa tabaka la chini ndiye stahiki ya CCM.
Katika siku za hivi karibuni, hautalazimika tena kutembea na nauli mkononi kwa ajili ya kupanda dala
Katika siku za hivi karibuni, hautalazimika tena kutembea na nauli mkononi kwa ajili ya kupanda daladala, baada ya mpango wa Serikali kutumia tiketi mtandao katika usafiri huo. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zinatarajia kuanzisha mfumo wa matumizi ya tiketi mtandao, utakaomfanya abiria kulipa nauli ya daladala kwa kadi. Utekelezwaji wa hilo kwa mujibu wa Latra, utafikiwa baada ya kusimikwa mfumo utakaoingiliana na ule wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), ili kumruhusu abiria kufanya malipo ya nauli ya usafiri huo kwa kadi. Akizungumza na gazeti hili kuhusu hilo, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri Ardhini wa Latra, Johansen Kahatano alisema hatua za mwanzo za ujenzi wa mifumo itakayounganishwa na BRT zimeshaanza. "Tukikamilisha ujenzi wa mifumo, mifumo ya daladala na BRT itaoana ili kuruhusu abiria kutumia kadi katika aina zote za usafiri yaani wa BRT na daladala,” alisema. Kulingana na Kahatano, hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi, kuboresha mifumo ya uendeshaji, kunusuru abiria kutozwa nauli isiyostahili, kukomesha wapiga debe, kuhamasisha malipo ya mtandao na kuiwezesha Serikali kukusanya mapato. Baada ya kuanza kwa mfumo huo, Kahatano alisema wamiliki wa daladala watapokea fedha kulingana na safari zilizofanyika, tofauti na sasa ambapo dereva anawekewa kiwango cha fedha anachopaswa kuwasilisha kwa mmiliki. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kwa sasa wamiliki wa daladala wanahamasishwa kuunda makundi au kuanzisha kampuni ili kurahisisha malipo ya nauli kwa abiria. “Mfano daladala kutoka Tabata kupitia Chang’ombe kwenda Kivukoni, tunahitaji angalau mabasi 25 yawe katika makundi ili kutoa huduma,” alisema. Hata hivyo, taarifa kuhusu kuanzishwa kwa mfumo huo si jambo jipya kwani limeshawekwa hadi katika sheria ya mamlaka hiyo, kama inavyoelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (Darcoboa), Shifaya Lema. Alisema Latra imekuwa na matarajio ya kuanzisha mfumo huo kwa muda mrefu kwa maslahi ya kuwanufaisha wafanyabiashara ya usafiri wa daladala. Hata Darcoboa alisema imekuwa ikitamani kuanza kwa mfumo huo ili wanufaike na biashara ya daladala, kwa kuwa utaratibu wa sasa dereva anaamua lini awasilishe na lini asiwasilishe fedha kwa mmiliki. “Iwapo mfumo wa tiketi mtandao utaanza, utatufaidisha wamiliki, madereva, makondakta na Serikali itapata mapato yake. Jambo muhimu zaidi ni kwa Latra kuingia mikataba na kampuni sahihi zitakazokuwa na uaminifu katika ukusanyaji nauli,” alisema. Lema alisisitiza kwa kuitaka Latra kuanza kwa kuwajengea uelewa wamiliki wa daladala kabla ya utekelezwaji ili wasione kama jambo jipya. "Hata zamani, baadhi ya wamiliki wa daladala hasa yale mabasi ya Eicher, walianzisha mfumo huo lakini kwa bahati mbaya hawakufanikiwa na hatujui kwanini. Tumeona baadhi ya mabasi ya mikoani bado yanaendelea kutoa tiketi za kawaida kwa abiria,” alisema. Mmoja wa abiria, Juma James alisema tiketi mtandao zimeonekana kushindwa kutumika ipasavyo katika mabasi ya mikoani, hivyo si sawa kuanzishwa katika daladala. "Latra inapaswa kuanza na kuimarisha tiketi mtandao katika mbasi yanayosafiri umbali mrefu na BRT kwa sasa, maana hayatumii kadi na mabasi mengi ya mikoani yanatoa tiketi za kawaida,” alisema. Alisisitiza si abiria wote wanaelewa kuhusu tiketi mtandao na namna zinavyofanya kazi. "Ni muhimu kwa mamlaka kujenga uelewa kabla ya kufikiria kuanzisha mfumo huo. Namna ya uendeshaji, namna utakavyofanya kazi na jinsi wanafunzi watakavyoweza kuutumia bila kubughudhiwa na makondakta,” alisema.
Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaketi leo, katika kikao chake cha kikatiba amba
Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaketi leo, katika kikao chake cha kikatiba ambacho aghalabu hufanyika mara mbili kila mwaka na inapolazimika hufanyika zaidi. Kinaweza kuwa miongoni mwa vikao vilivyobeba shauku kubwa ya wana-CCM na wadau wa siasa, kutokana na mazingira yaliyopo wakati wa kufanyika kwake. NEC hiyo ya CCM inakutana katika kipindi ambacho sekretarieti ya chama hicho ina nafasi nne nyeti zilizowazi, baada ya waliokuwa wanaziongoza kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali serikalini. Nafasi hizo ni Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo iliyokuwa chini ya Paul Makonda, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara iliyoongozwa na Anamringi Macha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi aliyokuwa nayo, Gilbert Kalima na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) aliyokuwa nayo, Fakii Lulandala. Katika taarifa ya uteuzi ya Machi 31, mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteuwa Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro na Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, huku Macha alishateuliwa tangu Machi 12 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kinachosababisha shauku ya makada wa chama hicho na wadau wa siasa ni juu ya kina nani watakaorithi nafasi hizo, zilizopitia mabadiliko kadhaa tangu uenyekiti wa Samia. Ingawa wapo waodhaniwa kuwa karibu na uteuzi kwenye nyadhifa hizo, kikao cha NEC ndicho kitakachoamua ni nani atapewa nafasi ipi na hilo ndilo hasa linalosubiriwa na wengi. Miongoni mwa wanaotabiriwa kuhusishwa kuzikwaa nyadhifa hizo ni Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Mwanza Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthon Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Jokate Mwegello na John Mongella aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ni muhimu zijazwe? Nyadhifa hizo nne zilizowazi ni sehemu ya wajumbe 12 wanaounda Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Kwa msingi huo, chama hicho kwa sasa kimesalia na wajumbe nane wa sekretarieti hiyo. Umuhimu wa kujazwa kwa nafasi za wajumbe hao wa sekretarieti unatokana na ukubwa wa majukumu yao kama yanavyofafanuliwa katika Ibara ya 106(1), (a hadi e) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017. Ibara hiyo inaweka wazi wajumbe hao ndiyo wasimamizi wa shughuli zote za utendaji za chama hicho kitaifa, ndiyo waandaaji wa shughuli za vikao kitaifa na ndiyo wanaowateuwa Makatibu Wasaidizi Wakuu na Wakuu wa Vitengo vya Makao Mkuu ya chama hicho. “Kuwateuwa Manaibu wa Katibu Mkuu wa kila jumuiya ya CCM na kuwateuwa Makatibu wa CCM Mikoa, Makatibu wa CCM wa Wilaya na watumishi wengine wa CCM,” inaeleza ibara hiyo majukumu mengine ya sekretarieti. Mbali na majukumu yao kikatiba, mwanazuoni wa uchumi wa siasa, Profesa Joseph Mbwiliza alisema umuhimu wa kujazwa kwa nafasi hizo unatokana na matakwa ya Katiba ya chama hicho. Si matakwa ya katiba pekee, alisema lazima zijazwe tena kwa haraka kwa sababu wajumbe hao ndiyo wanaoendesha chama hicho na wakipungua kuna hatari ya mzigo kuwahelemea wengine. “Kwa sababu chama hicho kina watu wengi, lazima nafasi zitajazwa na zitajazwa kwa haraka kwa sababu ya unyeti wake. Isingekuwa wajumbe wa sekretarieti Mwenyekiti angeamua kuziacha wazi na kisitokee chochote,” alisema Profesa Mbwiliza. Zitarajiwe sura mpya? Ingawa nafasi hizo zinatajwa kurithiwa na wanasiasa wabobezi kutoka ndani ya chama hicho, akiwemo Jokate Mwegelo, Martine Shigella, Amos Makalla, Anthon Mtaka na John Mongella, huenda watakaotauliwa wakaushangaza umma. Katika teuzi za hivi karibuni za wajumbe wa sekretarieti ya chama hicho taifa, wameibuliwa watu ambao aghalabu hawakuwa vichwani mwa wengi, huku waliotajwa wakikosa nafasi hizo. Hii si mara ya kwanza mtu kama Martine Shigalla kuhusishwa na uteuzi ndani ya chama hicho, lakini awamu zote hakuwahi kuteuliwa, badala yake walioteuliwa ni wale ambao hawakuwa hata midomoni mwa wengi. Uteuzi pekee uliotarajiwa na wengi ulikuwa wa Katibu Mkuu wa sasa wa chama hicho, Emmanuel Nchimbi na Makonda kama mwenezi, lakini waliobaki haikuwezekana kutabirika. Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho cha leo, aliiambia Mwananchi kuhusu kujazwa kwa nafasi hizo, huku akisisitiza hawatakuwa miongoni mwa mwajina tajwa. “Kwa wanaotajwa labda mmoja (hakumtaja jina), lakini wengine hapana ni sura mpya lakini inajulikana,” alieleza kwa ufupi akitaka mwandishi achunguze kubaini ni nani. Lakini mjumbe mwingine wa kikao hicho, alieleza kusikia majina yanayotajwa kama ambavyo watanzania wanasikia na hadi sasa hafahamu ni nani atakuwa miongoni mwa wateule hao. “Pengine ni wewe hatuwezi kujua. Ukweli sina jina lolote name nasikia tu watu wanatajwa, lakini Mwenyekiti wetu ni mtu wa ‘surprise’ utashangaa anateuliwa mtu tofauti na aliyetajwa,” alisema mjumbe huyo huku akiomba hifadhi ya jina lake.
Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema iwapo kitendo cha kushambuliwa k
Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema iwapo kitendo cha kushambuliwa kwake kwa risasi kimesababishwa na hatua yake ya kuwatetea wafugaji, akisisitiza ataendelea kufanya hivyo. Hata hivyo, mwanasiasa huyo aliweka wazi kuwa tukio la kushambuliwa kwake halihusiani na utetezi wake wa ardhi kwa wananchi wa jimboni mwake, kwa kuwa hivi karibuni alikuwa na mazungumzo na viongozi wa Serikali. Kauli ya Ole Sendeka inakuja siku chache baada ya kushambuliwa kwa risasi Kiteto mkoani Manyara jioni ya Machi 29, mwaka huu alipokuwa safarini akirejea Simanjiro. Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi kupitia Msemaji wake, David Misime ilielekeza kikosi mkoani humo kwa ajili ya uchunguzi dhidi ya waliohusika na hadi sasa bado hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa. “Polisi wanafuatilia tukio hilo kwa ukaribu baada ya kupokea taarifa, timu ya uchunguzi wa kitaalamu inayohusisha matumizi ya risasi kutoka polisi makao makuu imetumwa kushirikiana na timu ya Mkoa wa Manyara kuchunguza kwa kina tukio hilo ili kubaini waliohusika kina nani au kusudio lao nini,” alisema Misime. Taarifa ya awali ya jeshi la polisi iliweka wazi kuwa, katika shambulio hilo, risasi nne zilipigwa na kuishia kwenye gari la mbunge huyo. Awali, akisimulia tukio hilo, Ole Sendeka alisema alibaini kufuatiliwa na gari akiwa safarini na baadaye dereva wake aliipisha, hapo ndipo walipoanza kushambuliwa kwa risasi. Baada ya tukio hilo, leo Aprili 1, 2024 Ole Sendeka alizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Orkesumet na kusisitiza kuendelea kuwatetea. Katika kauli yake hiyo, alisema hausishi tukio hilo na hatua yake ya kutetea ardhi ya wananchi jimboni kwake, kwani wiki iliyopita alikuwa katika mazungumzo na viongozi wa Serikali kuhusu suala hilo. "Mimi na viongozi wakubwa tulijadili suala hilo na wakihakikisha kuwa hatutakubali kubadilisha ardhi yenu ya ufugaji iwe hifadhi ya wanyama" alisema Ole Sendeka. Hata hivyo, alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haihusiki na kushambuliwa kwake kwa risasi. Hata hivyo, alisema alishambuliwa akiwa na gari lake lililopigwa risasi 18 kwa kutumia silaha mbili tofauti za bunduki za kijeshi baina ya SMG au AK47. "Mimi nilipiga juu risasi mbili katika kujihami ila tukio hili lilichukuwa kama dakika mbili ila ilikuwa vita kubwa mno," alisema Ole Sendeka. Baada ya tukio hilo, alisema alipigiwa simu ya kupewa pole na viongozi wakubwa wakiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyeki wa CCM Abdulrahaman Kinana. "Nilipigiwa simu ya kupewa pole na hadi Ikulu na marafiki wengine mbalimbali ambao hata siwajui," alisema Ole Sendeka. Alisema nchi 15 duniani zilimpigia simu kumpa pole kutokana na kushambuliwa kwake na kunusurika kuuawa na watu wasiojulikana. "Nimepata pole kutoka mashirika mbalimbali ya haki za binadamu duniani na nchi mbalimbali za Afrika wakinipa pole kwa kupigwa risasi na kunusurika kuuawa," alisema Ole Sendeka. Alisema hawezi kumtaja mtu yeyote anayehusika na tulio hilo kwani hana uhakika na aliyemshambulia kwa risasi. "Namuachia Mungu kwani atamuumbua na kumuweka hadharani aliyetaka kuchukua maisha yangu kwa kunipiga risasi," alisema Ole Sendeka. Mbunge wa Afrika mashariki, James Ole Millya aliyekuwa kwenye mkutano huo alisema tukio hilo ni la kinyama na linapaswa kulaaniwa. Ole Millya alisema Tanzania ni nchi ya amani ila matukio ya viongozi kutaka kuuawa kwa risasi yanawapa hofu wananchi. "Kama tukio hili limetokea kwa sababu Ole Sendeka anatetea ardhi ya wafugaji tutamuunga mkono kwani anajali maslahi ya watu wengi," alisema Ole Millya. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Baraka Kanunga alisema wana Simanjiro wapo nyuma ya mbunge wao hivyo asiogope kuwatetea. "Huwezi kutaka kuchukua maisha ya kiongozi wa watu kwa sababu ya maslahi yako binafsi hili ni tukio baya mno katika maisha ya kisiasa," alisema Kanunga. Diwani wa kata ya Langai, Jackson Sipitieck alisema serikali ina mkono mrefu hivyo ichukue hatua kwa kuwatia mbaroni wahusika wote. "Hao wahuni waliosababisha tukio hilo wanapaswa kutiwa mbaroni kupitia mkono mrefu wa serikali," alisema. Diwani wa kata ya Ruvu Remit, Yohana Maitei alisema tukio hilo ni la kinyama na lenye ukatili mkubwa hivyo wahusika wachukuliwe hatua. Kwa upande wake, kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu alisema hadi hivi sasa hawajamkamata mtu yeyote anayehusika na tukio hilo. "Bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na tunatarajia kuwakamata wale wote waliohusika kufanya uhalifu huo," alisema Mwakatundu.
Bunge la bajeti linaanza leo huku Watanzania wakitaka wabunge kujielekeza katika mambo yanayojikita
Bunge la bajeti linaanza leo huku Watanzania wakitaka wabunge kujielekeza katika mambo yanayojikita kwenye kupunguza umasikini wa watu ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi. Machi 11, 2024 akiwasilisha ukomo wa bajeti na mapendekezo ya mpango wa Taifa wa maendeleo wa mwaka 2024/25 Waziri wa FedhaDk Mwigulu Nchemba alisema katika mwaka 2024/25 bajeti ya Serikali inatarajiwa kuwa Sh49.33 trilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ya bajeti ya mwaka 2023/24 ambayo ilikuwa ni Sh44.38 trilioni. Baadhi ya maeneo mbali na miradi ya maendeleo, inayoelekezwa ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Maeneo mengine ni maamdalizi yamichuano ya kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) na ugharamikiaji wa dira mpya ya maendeleo ya 2050. Leo wabunge wataanza kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatiwa na wizara nyingine na kukamilisha na bajeti ya serikali. Jana wananchi mbalimbali waliozungumza na Mwananchi waliwataka wabunge kujikita katika mambo ya yanayoigusa jamii huku wakitaka pia bajeti ijikite kwenye kuimarisha udhibiti wa mianya ya ubadhilifu. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Dk Lutengano Mwinuka alisema ni kawaida bajeti kuongezeka kila mwaka lakini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mara nyingi haifikii asilimia 100 kutokana na upatukanaji wa fedha. "Mjadala mkubwa wa wabunge utajielekeza katika huduma za kijamji kama nishati, elimu, afya, maji na nyingine ambazo japokuwa kuna maboresho makubwa yamefanyika lakini bado kuna mahitaji ya huduma hizo wananchi wangependa yafikiwe," alisema. Alisema hiyo itafanya mjadala kujielekeza zaidi kwenye maeneo hayo ya namna gani Serikali itashirikiana na Sekta Binafsi (PPP) katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo itakayoboresha huduma za jamii inatekelezwa. Mkazi wa Nkuhungu Belinda Mollel alisema kuwa ni matarajio yao Serikali itajielekeza katika kuhakikisha kuwa huduma za kijamii kama maji na miundombinu ya barabara inaboreshwa ili kufanikisha maendeleo ya jamii kwa haraka. "Ukitazama bado maji na umeme sio wa uhakika nchini, hii inarudisha maendeleo ya watu nyuma sana. Kwenye kilimo bado uzalishaji ni mdogo mkulima anatumia nguvu kubwa katika kulima lakini anachoambulia ni kidogo anabakia kulalamika tu, hii ni tabu sana. Tunawaomba wabunge waondoe tofauti zao za kiitikadi waaangalie maslahi ya walio wengi ambao wengi hawana itikadi za siasa," alisema Belinda ambaye anajishughulisha na mama ntilie. Naye Mwanasheria Nyabiri alisema ni kawaida kila wakati bajeti ya Taifa kupanda lakini utekelezaji wake umekuwa haufiki asilimia 100 hasa katika miradi ya maendeleo kutokana na upatikanaji wa fedha za kugharamia miradi hiyo. "Maboresho makubwa yamefanyika kwenye maeneo mbalimbali lakini uboreshaji unatakiwa kujielekeza zaidi katika huduma za kijamii kwa kuangalia ni namna gani tunaweza kupata fedha kwakushirikiana na huduma za jamii katika utekelezaji wa huduma za jamii," alisema. Alisema Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inaonyesha bado kuna udhaifu katika matumizi ya fedha, jambo ambalo sijui kwanini baadhi ya viongozi wanaonyesha ubinafsi na kutowajali wananchi. Alishauri bajeti hiyo kugusa maeneo yatakayosaidia kuondoa umasikini kwa watanzania ambao ni pamoja na wakulima, wafugaji na wavuvi ambao hivi sasa katika baadhi ya maeneo wanakabiliwa na upungufu wa samaki. Juzi juzi niliona stori katika gazeti lenu mkisema kuwa samaki wamepungua Mtera na.nasikia hali ndio hivyo hivyo kwa Kigoma ambapo nasikia wanataka kufunga uvuvi. Bajeti iguse maeneo yatakayoondoa umasikini kama vile kilimo, uvuvi na.ufugaji," alisema. Mwenyekiti wa Wakulima wa Zabibu mkoa wa Dodoma David Mwaka alipongeza hatua ya Serikali kuongeza bajeti ya kilimo kwa zaidi ya mara moja na kupendekeza iendelee kuongezwa zaidi ili kuwezesha sekta ya kilimo kuchangia asilimia 10 ya pato la Taifa kama lengo la Malengo endelevu ya maendeleo yanavyotaka kuwa Tanzania iwe imefikikia mwaka 2030. "Bajeti hii inaumuhimu mkubwa katika kuhakikisha kilimo kinakuwa kwa haraka haraka. Kinachotakiwa Maoni ya wasomi Kwa mtazamo wa mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Mohamed Bakary, sehemu kubwa ya bajeti itaelekezwa kwenye utekelezwaji wa miradi mikubwa. Na kwa sababu hiyo, alisema bunge la bajeti pamoja na mambo mengine halitaweza kuepuka kujadili kuhusu mambo hayo, kwa kuwa tayari yapo ndani ya utekelezaji. Katika mambo mengine nje ya miradi hiyo, Profesa Bakary alipendekeza mijadala ijikite katika kuinua sekta zinazozalisha ajira nyingi kwa watanzania. “Hii ni kwa sababu ajira ndilo tatizo kubwa nchini, kila mtu analalamika ajira kwa hiyo, wabunge wajikite katika kujadili uwezeshaji wa sekta zitakazozalisha ajira kwa wananchi,” alisema. Katika hoja yake hiyo, mwanazuoni huyo alieleza sekta ya viwanda imeonekana kuwa na mchango mdogo wa ajira kwa wananchi, hivyo ni vema kutafutwa sekta mbadala. Alipendekeza kuwekwa mpango madhubuti katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuwa zina uwezo wa kuleta matokeo ya haraka katika uzalishaji wa ajira. “Kama ikiwekwa mikakati makini kwenye sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi hakika kutakuwa na tija tarajiwa. Bunge la bajeti lijikite katika kuchagiza uwekezaji kwenye sekta hizi muhimu,” alisema.
Nani kurithi mikoba ya Paul Makonda na Anamringi Macha? swali hili ndilo linalofanya macho na masiki
Nani kurithi mikoba ya Paul Makonda na Anamringi Macha? swali hili ndilo linalofanya macho na masikio ya Wana-CCM na Watanzania kuelekezwa katika vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) vinavyotarajiwa kuanza kesho. Vikao hivyo vya kamati kuu na Halmashauri kuu, kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha ndani ya chama hicho, vitaanza kesho (Aprili 3, mwaka huu) jijini Dar es Salaam na tayari baadhi ya wajumbe wamekwishaanza kuwasili. Vikao hivyo vinakutana kukiwa na nafasi nne wazi za wajumbe wa sekretarieti baada ya waliokuwa wakiongoza kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali serikalini. Nafasi hizo ni Naibu Katibu Mkuu-Bara, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho. Fakii Lulandala alikuwa Katibu Mkuu UVCCM ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Gilbert Kalima aliyekuwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi akiteuliwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Kwa upande wa nafasi ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo aliyokuwa nayo Paul Makonda, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, huku Anamringi Macha aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa CCM (Bara) yeye akiteuliwa Machi 12 mwaka huu kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga. Tayari alikwisha kuapishwa. Ingawa ndani ya chama hicho kuna nafasi nne zinazohitaji kujazwa, lakini mijadala ya wana CCM na Watanzania imejikita zaidi katika nafasi hizo mbili hasa kutokana na umuhimu wake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025. Nafasi aliyoiacha Makonda aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, inaonekana kuwa moto huku baadhi ya makada wa chama hicho wakitajwa zaidi kuweza kuziba nafasi hiyo ambayo ni muhimu kuelekea katika chaguzi hizo mbili. Katika kuonyesha bado CCM haijapata mtu wa kumudu nafasi hiyo, Tangu Rais Samia ashike wadhifa wa mwenyekiti wa Taifa wa CCM miaka mitatu nyuma, nafasi hiyo imeshashikiliwa na makada wa nne na aliyehudumu muda mfupi zaidi ni Makonda, akihudumu miezi 5 sawa na siku 160. Wengine ambao wameshika wadhifa huo ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia ni pamoja na Humphrey Polepole ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Cuba na Sophia Mjema ambaye sasa ni mshauri wa Rais masuala ya wanawake na makundi maalum. Pia, katika orodha hiyo yumo Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka. Wanaotajwa kuwa huenda wakapata nafasi ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makala na aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa na baadaye Mara, Ally Hapi wakati wa utawala wa Rais John Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021. Katika orodha hiyo, anatajwa pia aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ambaye katika mitandao ya kijamii wanamuona kama mmoja wa makada wa CCM mwenye uwezo wa kujenga hoja na mikakati. Wengine wanaotajwa kuwa na uwezekano wa kuvaa viatu vya uenezi ni; Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM, Jokate Mwengelo na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenani Kihongosi, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM. Mwenezi anayetakiwa ni huyu… Kwa unyeti wa nafasi ya uenezi na kwa kuwa ndiyo inayobeba taswira ya chama, atakayemrithi Makonda anapaswa kuwa mtu mwenye uelewa wa kina juu ya siasa za watu wa tabaka la chini, kulingana na mtazamo wa Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Sabatho Nyamsenda. Dk Nyamsenda alisema tabaka hilo ndilo lenye idadi kubwa ya watu na kwa namna lilivyo ni kama limeachwa bila mtetezi, hivyo anayehitajika ni yule atakayelimudu kundi hilo. Mwanazuoni huyo aliweka wazi kuwa Mwenyekiti aliyepita wa chama hicho, John Magufuli alifanikiwa kujenga ushawishi mkubwa kwa kundi hilo na ndipo umaarufu wake ulipotokea. Lakini kwa sasa, alisema ndani ya chama hicho kuna mnyukano wa makundi mawili, lile linalosimamia misingi ya Magufuli na lingine la mtandao. Kundi la mtandao, alisema ndilo lile lenye wana-CCM wa muda mrefu likihusisha wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji kutoka ndani nan je ya nchi, lakini wanahusishwa na vitendo vya ufisadi na kukandamiza wanyonge. Kwa upande wa kundi linaloshinikiza kuendelezwa kwa misingi ya Magufuli, alisema ndilo lile linalotaka kusimamiwa kwa maslahi ya watu wa tabaka la chini. “Atahitajika mtu anayefahamu sio kwa kuigiza, afahamu kwamba watu wa tabaka la chini wanahitaji nini ili kukisukuma chama chake kiende mbele na awe na nguvu ya kukishinikiza chama chake kifuate hilo la kuangalia maslahi ya watu wa tabaka la chini,” alisema Dk Nyamsenda. Mpatanishi Kwa mtazamo wa mwanazuoni huyo, CCM inahitaji mwenezi mwenye uwezo wa kuleta upatanishi wa makundi hayo mawili yanayokinzana ndani ya chama hicho. “Tumeona makundi hayo yameonekana wazi wazi hivi karibuni na kusababisha Katibu Mkuu wa chama hicho (Daniel Chongolo) aondolewe kwa kashfa ambayo huwezi kuelewa kwa chama kilichoshika dola kama kinashida ya kumuondoa Katibu Mkuu kimuondoe kwa kumdhalilisha namna ile,” alisema. Kinyume na kupatikana kwa mtu mwenye uwezo huo, alieleza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 huenda chama hicho kikaingia kwenye mpasuko mkubwa. Mtafiti na uwezo wa kujibu hoja Sifa nyingine, alisema anahitajika mtu mwenye uwezo wa kufanya tafiti, kujibu hoja na mwenye haiba inayoweza kuwajibu wapinzani bila kutegemea vyombo vya dola. “Bahati mbaya hiyo haina mtu aliyekuwa nayo alikuwa ni Humphrey Polepole, unaweza usimpende kwa jambo Fulani lakini ni mtu ambaye uwezo wake wa kufanya tafiti ni mkuwa mno,” alisema. Kuhusu wanaotajwa Kuhusu wanaotajwa kurithi nafasi hiyo, Dk Nyamsenda alimtolea mfano Amos Makalla akisema kwa wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshapitwa na wakati, badala yake apatikane mtu mwenye mvuto kwa vijana kwa kuwa ndilo kundi kubwa. “Kwa hiyo mtu kama Makalla kushika nafasi kama hiyo haitasaidia. Kwa mbali mtu kama Jokate kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kutafiti lakini naye simuoni akiwa na uwezo wa kufanya siasa za amsha amsha kujibizana na wapinzani,” alisema. Kwa upande wa Kihongosi alieleza si mzuri kwenye nafasi hiyo kwa kuwa amejikita zaidi kwenye propaganda lakini si mtafiti mzuri katika kujenga hoja. Alieleza kuingizwa kwa watu wa namna hiyo, utashinikiza wakatumie nguvu za dola kufanikisha kazi katika nyadhifa hiyo. Akizungumza kuhusu hilo, Mchambuzi wa masuala ya Siasa, Ezekiel Kamwaga alisema CCM inahitaji mtu mwenye nguvu ya kuunganisha wanachama. Kigezo kingine ni mtu mwenye uwezo wakukisaidia chama hicho kushinda chaguzi zijazo, bila kujali mazingira ya siasa za sasa. “Watachagua mtu anayeaminiwa na Rais kwa sababu huu si wakati wa kupata mtu ambaye maneno na matendo yake yanapishana na Mwenyekiti wa Chama, mfano mwenezi aliyepita ukimtazama maneno anayozungumza ni tofauti na Mwenyekiti wake lugha zao zilikuwa zinapishana,” alisema Kamwaga. Mtazamo wa makada Makada wa CCM wanaona nafasi hiyo inahitaji mtu anayeweza kukabiliana na hoja za viongozi machachari wa upinzani kama mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu wake, Tundu Lissu na wabunge wa zamani, John Heche na Godbless Lema. “Kwa siasa za sasa baada ya kifo cha Magufuli (John) na kuelekea chaguzi zilizo mbele yetu nakuambia tunahitaji Katibu mwenezi aina Makonda na Sabaya ambao wana uwezo wa kujenga hoja. Ndio hivyo Makonda kateuliwa RC,” alidokeza kada mmoja. “Usisahahu mwenyekiti wetu ni mtu wa Surprise (kufanya uamuzi usiyotarajiwa). Nani alijua kama atamteua Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na sasa RC Arusha?. Alifanya hivyo kwa Jokate Mwegelo kuwa katibu mkuu wa UWT,” alieleza kada huyo. “CCM kwa sasa tunaangalia nani atatuvusha kwenye hiki kitimtim cha uchaguzi. Uchaguzi unaokuja ni mgumu sana sio lelemama hasa kauli za Rais kutaka uchaguzi huru na wa haki. Chama kinahitaji safu yenye watu wa kujenga hoja na wenye msimamo. Hata Mtaka (Anthony-RC Njombe) anaweza” Mmoja wa wabunge wa mikoa ya Kanda ya Ziwa aliliambia gazeti hili mwingine anayetajwa kuwa anaweza mikiki mikiki ya kisiasa kwa sasa Kheri James aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa ambaye sasa ni mkuu wa wilaya ya Iringa. Ukiacha nafasi hiyo, lakini wapo wanaotajwa kumrithi Macha ambao ni pamoja na RC Mtaka, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela ambaye ameachwa katika uteuzi wa juzi kwa kile kilichoelezwa atapangiwa kazi nyingine, mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigella.
“Nikiwa na umri wa miaka 19, baba yangu alinilazimisha niolewe, sikuwa namjua mwanaume, hakutaka kum
“Nikiwa na umri wa miaka 19, baba yangu alinilazimisha niolewe, sikuwa namjua mwanaume, hakutaka kumtambulisha na hata nimuone,” Ni maneno ya binti Ruwaida Ally (21), akisimulia namna alivyowekwa katikati ya mtego wa ndoa, ambayo hakuwa na mpango nayo. Ruwaida alijikuta katika mtego huo baada ya kuhitimu kidato cha nne mwaka 2020, katika shule ya Sekondari Mtoni Kigomeni, Unguja visiwani Zanzibar. Ingawa kuolewa ni tamanio la baadhi ya wanawake wengi, kwa Ruwaida ilikuwa kinyume chake, hakutamani kuingia katika ndoa kwa kile alichoeleza, alitamani kujiendeleza kielimu kwanza. Lakini, matamanio yake hayo ya kujiendeleza kielimu yaliingia kikwazo, pale Baba yake mzazi alipomtaka aolewe na mwanaume asiyemfahamu. Simulizi ya maisha ya Ruwaida kitinda mimba wa Ally Maulid inaanzia mwaka 2003, alipozaliwa Unguja visiwani Zanzibar na siku saba baadaye alimpoteza mama yake mzazi. Kuanzia hapo, maisha yake yalikuwa chini ya usimamizi wa Bibi yake mdogo, yaani mdogo wa Bibi aliyemzaa mama yake. Aliishi chini ya malezi ya walezi wake hao hadi alipohitimu elimu ya Sekondari, kisha alitakiwa kwenda kwa baba yake mzazi anayeishi Kigamboni jijini Dar es Salaam. Hatihati ya kuolewa Kwa Baba yake, alipata kibarua cha kuuza duka la vipodozi na hapo ndipo wanaume kadhaa kwa nyakati tofauti walipoingia tamaa ya kumuoa. Kwa mujibu wa Ruwaida, wanaume hao kwa nyakati tofauti walionana na baba yake kumweleza kuhusu madhumuni yao na hatimaye mzazi wake huyo alikubali kumuozesha. “Alifuatwa na mwanaume wa kwanza akakataa, wa pili alimfuata akaniambia akifuatwa na mwingine ataniozesha, kweli akaja mwanaume wa tatu, Baba akataka kuniozesha,” anasema. Kipindi anatakiwa kuolewa, alikuwa na miaka 19, ingawa ulikuwa umri stahiki kisheria kuingia kwenye ndoa, lakini hakuwa radhi kwa kile alichoeleza, alikuwa na malengo ya kujiendeleza kielimu zaidi. Hata hivyo, Ruwaida anasema hakuwa na matumaini ya asilimia 100 ya kujiendeleza kielimu kwa kuwa kipato chake kisingetosheleza kujilipia ada ya masomo ya upishi ambayo ndiyo iliyokuwa ndoto yake. Hali aliyokuwa nayo wakati wa shinikizo hilo la kuolewa, anasema ni vigumu kuelezeka kutokana na ukweli kwamba, hakuwa na nguvu ya kugomea uamuzi wa baba yake na isingekuwa rahisi kusikilizwa. Mbaya zaidi, anasema matokeo yake ya mtihani wa kidato cha nne hayakutosheleza kumwezesha kuendelea na ngazi nyingine ya elimu, hivyo hakuwa na utetezi wa kukwepa ndoa hiyo. Anasema katika kipindi hicho alitamani kumpata mtu mzima atakayesimama kumtetea dhidi ya uamuzi wa baba yake. “Kilichokuwa kinanishangaza, baba hakutaka nimjue huyo muoaji, aliniambia nitaolewa na mwanaume na sikuwa namjua na hakutoa nafasi hata nimuone, ulikuwa mtihani mkubwa kwangu,” anasema Ruwaida. Alinusurikaje? Katikati ya kukosekana kwa matumaini ya kujiendeleza na elimu ya upishi, huku akigubikwa na hofu ya kuingia kwenye ndoa, Ruwaida anasema ilitokea faraja isiyotarajiwa. Faraja hiyo ni kile alichokifafanua, kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2022, wakati anazindua Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), wilayani Bukoba katika Mkoa wa Kagera, alipotangaza kufadhili masomo ya wanafunzi 20 kati yao 10 kutoka Zanzibar. Baada ya tangazo hilo, anasema shangazi yake aliona na kumuuliza iwapo yupo tayari kwenda kusoma katika chuo hicho kwa ufadhili wa Rais Samia, alipokubali maombi yalifanyika na hatimaye akawa miongoni mwa waliochaguliwa kutoka Zanzibar. “Hapo nilimsimulia shangazi kuhusu masuala ya kuolewa, alimwambia baba kwamba haiwezekani kwa sababu nakwenda kusoma. Shangazi alinifanyia mchakato mwisho wa siku nikapata nafasi ya ufadhili ndiyo nasoma kwa sasa,” anasema. Anasema ufadhili huo ndiyo uliomwepusha na mtego wa ndoa, akisisitiza kama si kufadhiliwa huko pengine wakati huu angeshangua mwanandoa mkongwe. “Ningeshaolewa saa hizi maana sikuwa na namna, sikuwa na nia ya kuolewa lakini mazingira ndiyo yalikuwa hivyo,” anasema. Tofauti na fani ya ndoto yake ya upishi, katika chuo hicho Ruwaida anasema anasoma ufundi wa umeme, fani ambayo amejikuta anavutiwa nayo baada ya kuona miundombinu ya chou hicho. Kwa mujibu wa Ruwaida, kwa sasa yupo ngazi ya pili ya fani hiyo na baada ya kuhitimu mwakani, anatarajia kuanzisha kampuni ya ufundi wa umeme. “Nikimaliza ninalenga kujiajiri, lakini sitakataa ajira kama itakuja. Kwa sababu mimi ni mtaalamu kwa sasa na naipenda kazi hii nitakuwa tayari kuifanya katika mazingira yoyote,” anasema. Katika simulizi yake hiyo, Ruwaida anamshukuru Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, kwa kufikiria kufadhili wanafunzi hao, akisisitiza ni muhimu aongeze kuwafadhili wengine. “Nyumbani kuna vijana wengi wana changamoto na wengine wamepoteza matumaini, unapokuja ufadhili kama huu unawarudisha kwenye mstari,” anasema Ruwaid ambaye ni mtoto wa sita kuzaliwa. Mwalimu wake Mwalimu wa Ruwaida katika chuo hicho, Yohana Mwanchali anasema mwanafunzi huyo ni mmoja kati ya watu waliozoea mazingira haraka ukilinganisha na wengine waliotokea visiwani Zanzibar. Hatua ya Ruwaida kuyazoea mazingira, ilitokana na kile kilichoelezwa na mwalimu huyo, ni mchangamfu na mtu wa kujichanganya na wenzake. “Hata kitaaluma kati ya wanafunzi 20 waliofadhiliwa na Rais Samia katika chuo hiki, Ruwaida anafanya vizuri zaidi na anaonekana ana uchungu na kile anachokitarajia,” anasema Mwanchali. Kuhusu chuo hicho Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Athuman Mussa anasema ujenzi wake umefadhiliwa na Jamhuri ya Watu wa China, tangu mwaka 2022 na kilikamilika mwaka Oktoba mwaka huo. Anasema rasmi chuo hicho kilianza mafunzo mwaka 2023 na kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 400 wa kozi ndefu, huku uwezo wa chuo ukiwa ni kupokea wanafunzi 420. “Kati ya wanafunzi 320 wanaweza kukaa bweni na wengine 100 wanaweza kusoma kwa kutwa na kurudi nyumbani,” anasema. Kwa mujibu wa Mussa, wakati chuo hicho kinakabidhiwa kwa Rais Samia Oktoba mwaka 2022 alitangaza kuwafadhili wanafunzi 20 ambapo 10 kutoka Bara na 10 kutoka Zanzibar. Kigezo cha ufadhili huo, anasema ni watoto wanaotoka katika mazingira magumu, wakiwemo yatima na wale wenye wazazi wasiokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu.
Kama umewahi kula msoto kitaa kwa miaka kadhaa baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu, bila shaka u
Kama umewahi kula msoto kitaa kwa miaka kadhaa baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu, bila shaka utaelewa ni magumu gani ameyapitia kijana John Alexander (29). Alexander ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa uunganishaji umeme wa majumbani katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida, ni kielelezo sahihi cha vijana waliokaribia kuzisaliti ndoto zao. Licha ya kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita mwaka 2016, katika Shule ya Sekondari Tunduru, ugumu wa maisha ya wazazi wake ulimweka kando na safari ya kuisaka elimu kwa takriban miaka nane. Akizungumza na Mwananchi, Alexander anasema mwaka 2016 alihitimu kidato cha sita na kafaulu kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu akichaguliwa katika Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa. Ingawa hatua hiyo iliifurahisha nafsi yake, kwa kadri siku zilivyokwenda iliishia kuwa maumivu ndani ya moyo wake, akiifananisha na kidonda kilichowekwa chumvi. Maumivu hayo, yalitokana na kile alichoeleza moyo ulitamani aendelee na masomo ya elimu ya juu, lakini hali ya uchumi wa wazazi wake ilimvuta shati ikimtaka asalie mtaani. "Wazazi wangu hawakuwa na fedha za kunisomesha kwa sababu hali yao kiuchumi ni mbaya. Wote wanajishughulisha na kilimo na wanachokipata kisingetosheleza kumsomesha yeye na wadogo zake," anasimulia. Kulingana na Alexander, wakati anahitaji kuendelea na elimu ya juu, wadogo zake pia walikuwa katika ngazi za chini za elimu ikiwemo Shule ya Msingi na Sekondari, hivyo kipato kilichokuwepo kilitosheleza kuwasomesha hao pekee. "Hali ilikuwa mbaya, fedha ndogo iliyokuwepo ilitosha kuwasomesha wadogo zangu ambao kwa ngazi yao ya elimu kiasi kilichokuwepo kilitosha," anasema. Mazingira hayo, anaeleza yalimlazimu kuanza kuzisaka fedha walau apate ada kwa ajili ya kuendelea na elimu ya juu. Juhudi hizo kwa mujibu wa Alexander, alizielekeza katika shughuli za kilimo cha vibarua na kuchunga mifugo alizozifanya kwa miaka nane. Hata hivyo, anaeleza kilichopatikana wakati huo kiliishia kutosheleza mahitaji ya familia yake, ikiwemo kula na huduma nyingine muhimu na hivyo alijikuta muda wote aliotumikia katika vibarua, haukufaa kuzitimiza ndoto zake. VETA ilivyohuisha ndoto yake Kutoka miaka nane ya kukata tamaa juu ya elimu, matumaini ya kijana huyo yaliibuka upya mwaka 2023 alipopata fursa ya kuchaguliwa kujiunga na Chuo cha VETA wilayani Ikungi mkoani Singida. Hata hivyo, kuchaguliwa kwake anasema kumetokea baada ya maombi katika awamu mbili za miaka miwili tofauti bila mafanikio. "Nilianza kuomba VETA tangu mwaka 2021, Chag'ombe, Dar es Salaam lakini ushindani ulikuwa mkubwa nikikosa nafasi, nilijaribu mara ya pili nilikosa tena na mara ya tatu ndiyo nimefanikiwa," anasema. Hatua hiyo inamfanya Alexander kueleza kile alichokiita VETA ndiyo mwanzo wa safari ya uhuishaji wa ndoto yake ya kuwa mwanataaluma atakayejiajiri au kuajiriwa. Anayafungamanisha maelezo yake hayo na hatua ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu, ilivyoweka mkazo wa ujenzi wa vyuo hivyo katika kila Wilaya. Kilichofanya awe sehemu ya wanafunzi katika chuo hicho licha ya hali duni ya uchumi wa familia yake, Alexander anasema ni kiasi kidogo cha ada anachopaswa kulipa kupata taaluma hiyo VETA. "VETA gharama hadi najiunga hazijafika hata Sh200,000 tofauti na Chuo Kikuu. Kiasi hicho mimi na wazazi wangu tulijichanga tukapata na sasa nasoma hapa. Naishukuru sana Serikali na Rais Samia kwa kufikiria kujenga vyuo hivi," anasema. Mkuu wa Chuo Akizungumzia chuo hicho anachosoma Alexander Mkuu wa Mafunzo, Mathias Pastory anasema ujenzi wake ulianza mwaka 2020 na kukamilika mwaka jana kwa Sh2.6 bilioni. Pamoja na Alexander, anasema Chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 45 na uwezo wake halisi ni kudahili wanafunzi 150. Pastory anaeleza hicho ni chuo cha pili cha VETA kuwepo katika Mkoa huo, cha kwanza kipo Singida Mjini, ambapo ni mbali na vijiji vingi walipo wanafunzi. Kuhusu Alexander, anasema ni miongoni mwa wanafunzi waaoonyesha uelewa mkubwa katika masomo, kadhalika ana shauku kubwa na masomo. "Anaonyesha juhudi na ni miongoni mwa wanafunzi wanaofanya vizuri sana, historia yake inasisimua, bahati nzuri hakujiingiza katika makundi mabaya," anasema. Wanafunzi wenzake Anneth Mkama ni mwanafunzi wa chuo hicho aliyetokea Mkoa wa Morogoro, anaungana na Alexander kueleza umuhimu wa vyuo hivyo katika kutimiza ndoto za vijana. "Mimi nikipata taarifa ya Chuo kufunguliwa katika matangazo mbalimbali. Niliomba nikafanikiwa na kwa sasa nasoma ushonaji nguo fani ya ndiyo yangu," anasema. Anaeleza asingekuwa na tumaini lingine zaidi ya VETA kwa kuwa matokeo yake katika mtihani wa kidato cha nne, yasingemwezesha kuendelea na ngazi nyingine ya elimu. "Namshukuru Rais Samia kwa mpango wake wa kujenga vyuo vya VETA katika kila Wilaya, hii itatimiza ndoto za vijana wengi," anaeleza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa am
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ametoa miezi saba kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), kuhakikisha inapatikana kampuni binafsi itakayotoa huduma ya usafiri. Iwapo hilo halitatekelezwa hadi Oktoba mwaka huu, Mchengerwa amewataka Wakurugenzi Dart na Udart kuwasilisha kwake barua za kujiuzulu. Kauli hiyo ya Mchengerwa inatokana na kile alichobainisha, kuna changamoto katika utoaji huduma za mabasi hayo, hivyo ni muhimu kuishirikisha sekta binafsi. Hata hivyo, alipotafutwa kuzungumzia agizo hilo, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu wa Dart, Dk Philemon Mzee alisema kinachofanyika ni utekelezaji. "Serikali ikisema ni agizo hilo kinachofuata ni utekelezaji na hivyo tutatekeleza, lakini mengine Mkurugenzi Mkuu (Athuman Kihamia), ndiye aliye katika nafasi nzuri ya kuzungumzia," alisema DK Mzee. Danadana mwekezaji mpya Mchengerwa si kiongozi wa kwanza kueleza kuhusu kupatikana kwa mwekezaji mpya, suala hilo limekuwa mithiri ya danadana. Awali, kampuni iliyopewa fursa ya kutoa huduma katika mradi huo ni Simon Group, iliyokuwa na takriban mabasi 100. Utoaji huduma wa Kampuni hiyo, ulitajwa kuwa wa majaribio wakati mtoa huduma rasmi anaendela kutafutwa, ili angalau anunue mabasi 150. Mchakato wa kumsaka mtoa huduma huyo zilianza mwaka 2018 na Serikali ilitangaza kupatikana kwake, lakini haijulikani aliishia wapi. Baadaye Serikali ilitangaza kumsaka mtoa huduma mpya atakayekuwa na uwezo wa kununua mabasi 170, yaliyotarajiwa kutosheleza huduma wakati huo. Hiyo ilikuwa mwaka 2019 na ahadi ziliendelea hadi mwaka 2022 bila hata mtoa huduma huyo kupatikana. Mwaka 2022 nao ulikuja na ahadi mpya, pale Serikali ilipotangaza kupatikana kwa mwekezaji mpya ambaye ni kampuni ya Emirates National Group. Kampuni hiyo kutoka Falme za Kiarabu ilitajwa kununua mabasi 750, yatakayosafirisha abiria kati ya 600,000 hadi 700,000 kwa siku. Changamoto Katika kipindi hicho chote mradi wa mabasi yaendayo haraka, umekuwa ukilalamikiwa kwa huduma mbovu na zinazokinzana na matarajio ya mradi. Miongoni mwa malalamiko hayo ni mrundikano wa abiria vituoni bila kupata huduma kwa muda muafaka, baadhi ya mabasi kupitia vituoni bila abiria na hayapakii. Lakini, mzizi wa changamoto hizo ni uchache wa mabasi yasiyoiendana na mahitaji ya usafiri huo. Kauli ya Mchengerwa Mchengerwa alitoa maelekezo hayo wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Fungu namba 56 na Fungu namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bungeni jijini Dodoma. "Wala hakuna mjadala ikifika Oktoba wakishinda kuhakikisha kwamba watu wa Dar es Salaam wanahudumiwa vizuri walete barua za kujiuzulu. "Kwa sababu hatuwezi kwenda kama kawaida watu wanataka huduma huduma hazitolewi, watu wanatoa huduma wanavyotaka wao, mtu anaweza akaamua tu kusimamisha basi," alisema. Iwapo itashirikishwa sekta binafsi, alisema haitawezekana huduma zikadorora. "Wakati mwingine unaona basi inakatiza haiwachukui hata wananchi kwa sababu tu alitengewa kwamba muda fulani awe sehemu fulani wanashindwa hata kujiongeza," alisema Mchengerwa. Hata hivyo, Mchengerwa alieleza matumaini yake juu ya uongozi mpya wa Mkurugenzi wa Dart, Athuman Kihamia na Mkurugenzi wa Udart, Waziri Kindamba. Darcoboa Akizungumza na Mwananchi kuhusu kauli hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki Daladaka Dar es Salaam (Darcoboa), Shifwaya Lema alisema chama hicho ninayo nia ya kufanya uwekezaji huo. Lakini alisema hilo linahitaji majadiliano ya kina baina ya wanachama ili wajiunge kushirikiana kutoa huduma. "Nia ipo lakini tatizo ni kuaminika, hizi kampuni za kitajiri zinapewa kwa sababu zinaaminika. Tanzania watu hawana elimu kuhusu ushirikiano wakisikia wanachama wanataka kushirikiana wanatafsiri kuwa ni ushirika ule ambao mara zote unafeli," alisema. Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart), Waziri Kindamba alisema ni mapema kusema chochote kwa kuwa bado anajifunza mengi kuhusu Ofisi hiyo. "Hapa mezani kwangu kumejaa nyaraka nasoma ili nielewe kuhusu Ofisi hii kwa hiyo naomba mnipe muda kisha tutapata nafasi ya kuzungumza," alisema Kindamba.
Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa
Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya nishati. Rais Samia aliianza safari ya urais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, Hayati John Magufuli, aliyefariki Machi 17, mwaka huo. Safari yake ya utendaji katika wadhifa wa urais, ilianza na mashaka kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakidhani uendelezaji wa miradi hasa ya nishati iliyoachwa na mtangulizi wake, kisingekuwa kipaumbele chake. Wengi walibaki na dhana kuwa, kifo cha mtangulizi wake ndiyo mwisho wa mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), linalotarajiwa kuzalisha jumla ya megawati 2,115. Fikra za wengi zilijikita kwenye mabadiliko ya mbinu za kukabili changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika, wakidhani Rais Samia angekuja na mikakati tofauti. Mashaka yalizidi kuongezeka wakidhani kuwa, hadi mikakati mipya itakapofanikiwa, tayari wananchi watakuwa wameshaumizwa na changamoto ya upatikanaji wa nishati hiyo kwa muda mrefu. Aprili 22, mwaka 2021 ndiyo siku ambayo Watanzania walifumbuliwa macho juu ya msimamo wa Rais Samia kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya umeme. Rais Samia alifanya hivyo alipolihutubia Bunge jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, aliahidi kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake, kadhalika kubuni mipya ili kuwahudumia wananchi. Katika hotuba yake hiyo, Rais Samia aliweka wazi kuwa, kukatika kwa umeme ni miongoni mwa malalamiko mengi aliyokuwa akipokea wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020, alipokuwa akimnadi Hayati Magufuli. "Miradi yote ya umeme inayoendelea kutekelezwa katika ni lazima ikamilike katika kipindi changu chote cha uongozi," alisema Rais Samia alipolihudumia Bunge jijini Dodoma. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa shughuli za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, nalo lilijiweka sawa kuianza safari hiyo na hadi sasa linahesabu mafanikio. Mwanzo wa safari Baada ya kujenga msingi wa msimamo wake, mkuu huyo wa nchi alifungua ukurasa wa utendaji katika sekta ya nishati hasa baada ya Bunge kupitisha bajeti ya matumizi ya Wizara ya Nishati ambayo karibu robotatu ya fedha zimeekekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya kufua, kusafirisha na kusambaza umeme nchini. Miongoni mwa miradi hiyo, upo mradi wa JNHPP unaotazamwa kama muarobaini wa changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini. Rais Samia alipokea kijiti cha urais, kipindi ambacho mradi wa JNHPP ulitekelezwa kwa takriban asilimia 36 na kwamba hadi inafika miaka mitatu ya uongozi wake mradi huo umefikia asilimia 97. Hadi inafikia hatua hiyo, kulikuwepo na juhudi lukuki zilizofanywa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia. Miongoni mwa juhudi hizo ni kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa mradi ambazo kwa ujumla wake unatekelezwa kwa Sh6.6 trilioni. Matumaini ya awali yalianza Desemba 22 mwaka 2022, kipindi ambacho Rais Samia aliongoza ujazaji maji katika bwawa hilo. Mafanikio Lakini Februari 25, mwaka huu ndiyo uliokuwa wakati muhimu zaidi kwani mtambo mmoja kati ya tisa katika Bwawa hilo, uliwashwa na kuanza kuingiza umeme katika gridi ya taifa Mtambo huo, ulizalisha na kuingiza megawati 235 za nishati hiyo kwenye gridi ya taifa na hivyo kupunguza adha ya mgawo wa umeme, iliyokuwa unawasumbua Watanzania kwa wakati huo. Wakati mtambo huo unawashwa na kuingizwa umeme huo katika gridi ya taifa, Tanzania ilikuwa katikati ya changamoto ya upatikanaji wa umeme iliyosababishwa na uzalishaji duni katika vyanzo mbalimbali hasa vya maji. Kutokana na hali hiyo, hatua ya kuwashwa kwa mtambo huo, ilifufua matumaini ya upatikanaji wa umeme nchini, kadhalika matunda ya JNHPP yalianza kuwagusa wananchi. “Kufikia mwezi wa tatu Mungu akipenda tutaingiza jumla ya megawati 470 (kutoka katika mitambo miwili), tutakuwa na megawati za ziada zaidi ya 70. Baada ya mwezi wa tatu hatutazungumza upungufu wa umeme tena,” alisema Dk Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati alipokuwa kwenye mradi huo Februari mwaka huu. Faida nyingine za mradi Iwapo Bwawa hilo litakamilika mafuriko katika bonde la mto Rufiji yatabaki kuwa historia. Kwa kawaida kabla ya ujenzi wa bwawa hili, maji kutoka Mikoa 11 wakati wa masika yalikusanyika kwa wingi katika Mto Rufiji na kusababisha mafuriko kwa wananchi. Adha hiyo sasa itakwisha. Maji yatatoka kwa kiwango cha wastani wa lita milioni 2 kwa sekunde na kiwango hiki kitaendelea kutoka iwe wakati wa kiangazi au masika. Hii inatoa fursa kwa watu wanaoishi kwenye Bonde la Mto Rufiji kujipanga na maeneo yaliyokuwa yanafurika maji, sasa kupitia kilimo cha umwagiliaji wanaweza kulima mwaka mzima. Ukiacha sasa uhakika uliojitokeza kwa mazingira kutomomonyolewa na mafuriko, Wahandisi Watanzania walioshiriki katika ujenzi wa mradi huu wamepata ujuzi mkubwa ambao nchi itaendelea kuutumia kwa kujenga miradi mingine ya mabwawa kama walivyofanya Misri kwa kujenga Aswan High Dam na Aswan Low Dam katika Mto Nile, yanayowapatia umeme kwa wastani wa megawati 2,370, kwa maana ya Aswan High Dam megawati 2,100 na Low Dam Megawati 270. Kauli za wateja Kuingizwa kwa megawati 235 za umeme katika gridi ya taifa, kumeleta ahueni ya upatikanaji wa umeme kwa wateja kama inavyoelezwa na Mwanahamisi Hassan mkazi wa mabibo Dar es Salaam. Anasema kabla ya kuwashwa mtambo huo, umeme katika eneo analoishi ulipatikana asubuhi hadi jioni na usiku ulikatika, lakini kwa sasa hakuna tena changamoto hiyo. Kulingana na Mwanahamisi, baada ya kusikia kuhusu kuwashwa kwa mtambo huo, kumekuwa na uhakika a upatikanaji wa nishati hiyo. “Sikuwa naamini kama ungefika wakati mgawo ungeisha namna hii. Ilikuwa shida sana lakini kwa sasa mambo yamekwisha. Kwa kweli hii miaka mitatu ya Rais Samia na Tanesco kwa ujumla kazi imeendelea,” anasema Mwanahamisi. Mbali na Mwanahamisi, Mwananchi mwingine anayeeleza kuguswa na upatikanaji wa umeme ni Donald Mayunga Mkazi wa Dar es Salaam, anasema kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa umeme umeimarika. “Hali ilikuwa mbaya sana, lakini naona kabisa tunaondoka kwenye changamoto. Kwanza sikuamini kama mama (Rais Samia) angemalizia ujenzi wa Bwawa hilo kwa sababu kila mtu ana utashi wake. “Lakini hadi leo hii tunapata umeme, huyu Rais Samia amefanya kazi kubwa sana,” anasema Mayunga. Miradi mingine iliyokamilika Katika kipindi hicho, TANESCO imekamilisha mradi wa upanuzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa Gesi asilia cha Kinyerezi I kinachozalisha megawati 185, kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 188. Mradi mwingine ni wa kuzalisha umeme wa Megawati 80 wa Rusumo unaotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi tatu ambazo ni Tanzania, Rwanda na Burundi. Kwa upande wa Tanzania gharama za mradi huo ni Dola za Marekani milioni 113. Kadhalika, ndani ya miaka mitatu, Shirika hilo limetekekeza ujenzi wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400, urefu wa kilomita 414 kutoka Kenya hadi Tanzania wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 258.82. Kama hiyo haitoshi, shirika hilo limekamilisha njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa 220kV, yenye urefu wa kilomita 144 kutoka Geita hadi Nyakanazi yenye thamani ya Euro milioni 45. Si hiyo tu, mradi mwingine uliotekelezwa katika kipindi hicho ni njia ya kusafirisha umeme msongo wa 220kV, yenye urefu wa kilomita 94 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 35. Mradi mwingine ni kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 66 kutoka Nyakanazi hadi Ngara, kituo cha Nyakanazi hadi Kakonko na ufungaji wa Regulating Transfoma 20MVA Kasulu yenye thamani ya Sh4.72 bilioni. Miradi inayoendelea Katika kipindi hicho cha miaka mitatu ya Rais Samia, baadhi ya miradi inaendelea kutekelezwa ukiwemo wa umeme wa Jua megawati 150. Kwa awamu ya kwanza, megawati 50 zitazalishwa katika eneo la Nginga -kishapu Mkoa wa Shinyanga wenye thamani ya Euro milioni 43. Mradi mwingine unaendelea ni wa Grid Imara wenye lengo la kuboresha miundombinu mbalimbali ya umeme nchini (mikataba 26) ili kuleta utulivu wa Gridi ya Taifa. Utiaji saini wa mradi huo ulifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan. Kadhalika, ipo miradi ya Ukarabati na Uboreshaji wa Gridi ya Taifa (TTGRUP) yenye thamani ya shilingi bilioni 175.9. Mradi wa kupitisha umeme chini ya ardhi Ili kukabili changamoto ya kupotea kwa umeme, Tanesco katika kipindi hicho cha miaka mitatu ndipo ilipoanza utaratibu wa kupitisha nishati hiyo chini ya ardhi. Mradi wa Kurasini unaopitisha nyaya chini ya ardhi zenye urefu wa zaidi ya kilomita sita ni miongoni mwayo. Akizungumza kuhusu hilo, Msemaji wa Tanesco, Kenneth Boymanda anasema kwa sasa mkandarasi anaendelea na kazi kufanikisha mradi huo. Ingawa haujakamilika, anasema shughuli zinaenda vema na kama zilivyotarajiwa. "Mradi tulionao kwa sasa ni wa Kurasini na mkandarasi yupo kazini anaendelea kutandika nyaya chini ya ardhi, kuhakikisha kazi hiyo itakamilika," anasema Boymanda. Hali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme Kufikia Juni 30, mwaka 2023 jumla ya mitambo ya kuzalisha umeme ilikuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1,911.37. Uzalishaji huo ni ongezeko la asilimia 9.61 lililochangiwa na kuwashwa kwa upanuzi wa Kinyerezi I wenye uwezo wa kuzalisha megawati 185. Katika mwaka 2022/23, mahitaji ya juu ya umeme yaliyopatikana yalikuwa ni megawati 1,470.5 ikilinganishwa na mahitaji ya megawati 1,401.07 mwaka uliopita. Katika kipindi kinachoangaziwa, Shirika lilirekodi upatikanaji wa asilimia 88 wa mitambo ya uzalishaji umeme. Hadi kufikia Februari mwaka 2024 tayari mtambo mmoja kati ya tisa ya mradi wa JNHPP uliingia kwenye gridi ya taifa na kuanza kuchangia megawati 235. Kuhusu usafirishaji, mifumo ya vituo vidogo 64 vilivyounganishwa na njia za upokezaji 68 ni vituo vya msingi vya usambazaji. Mtandao wa njia za kusambaza umeme unajumuisha kilomita 1085 za 400kV, kilomita 3347 za kV 220, kilomita 1835.19 za kV 132 na kilomita 580 za 66kV. Shirika pia, hudumisha na kusimamia miundombinu ya mawasiliano ya umeme na mtandao wa fiber optic kwa usaidizi wa uendeshaji wa gridi kwa shughuli za ndani za ICT na usaidizi wa wateja kutoka nje (Mkongo wa Kitaifa wa TEHAMA) TANESCO na matumizi ya nishati safi Mei 29, mwaka jana, Tanesco ilisaini mkataba wa Sh274.7 bilioni kwa ajili ya mradi wa umeme wa nishati ya jua Megawati 150 wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga. Kulingana na Meneja wa Miradi, Usafirishaji na Usambazaji kutoka Tanesco, Frank Mashalo mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 50 za umeme. Anasema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja na mkandarasi kutoka China, Sinohydro Corporation. “Mradi huu unalenga kuongeza uhakika wa usambazaji nishati nchini na ni sehemu ya dhamira ya Tanesco kuhakikisha kunakuwa na mchanganyiko wa nishati kutoka vyanzo mbalimbali,” alisema Mashalo. Mashalo alisema mradi huo pia utachangia sehemu ya juhudi za kuhamia katika nishati safi. Mradi huo ni mmoja kati ya miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua katika nchi za Afrika Mashariki. Miaka mitatu na huduma za kidigitali Ndani ya uongozi wa Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu, ndipo huduma za kidigitali ziliboreshwa zaidi huku programu mbalimbali zikizinduliwa. Miongoni mwa programu hizo, ipo Nikonekt kwa ajili ya kuunganisha huduma ya umeme kwa wananchi. Huduma hiyo ya kidigitali inampunguzia mteja kazi ya kwenda zilipo Ofisi za Tanesco kuomba huduma ya kuunganishiwa umeme, badala yake atatumia simu janja kuwasiliana na watoa huduma kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo. Mbali na huduma hiyo ya kidigitali kuwaondolea wananchi ulazima wa kusafiri hadi zilipo Ofisi za Tanesco kuomba huduma, pia imesaidia kupunguza muda wa mteja kuunganishiwa umeme. Kutoka kusubiri kwa takriban mwezi mmoja Hadi kupata huduma ya kuunganishiwa umeme, Nikonekt imefanya huduma hiyo ipatikane ndani ya siku tatu hadi nne. Lakini, matumizi ya huduma hiyo yanaondoa urasimu na kukomesha vishoka na vitendo vya rushwa, kwani huduma zinatolewa kupitia njia ya mtandao bila kulazimisha watu kuonana faragha. Kwa sasa hautalazimika tena kumtafuta Ofisa wa Tanesco, kumuomba akusaidie kuharakisha uunganishwaji wa umeme, badala yake itatumia simu yako janja kuomba huduma na utapatiwa ndani ya muda muafaka. Hayo yote yamefanyika katika kipindi cha uongozi wa miaka mitatu ya Rais Samia. TANESCO na usawa wa kijinsia Katika kuendeleza jitihada za kumuinua mwanamke Tanesco kwa mwaka 2022/2023 limechukua hatua kadhaa katika kuweka usawa wa kijinsia na kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika nyanja mbalimbali za ajira ndani ya Shirika. Kutokana na Tathmini ya Pengo la Jinsia iliyofanyika Septemba 2020, kumefanyika maendeleo katika ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi kutoka asilimia 7.9 hadi asilimia 20 mpaka sasa. Sambamba na hayo, tangu Novemba 2023, TANESCO imefanya utekelezaji wa ufadhili wa masomo kwa wanawake 20 wafanyakazi katika fani ya uhandisi, ambapo wamepata nafasi ya kusomea Shahada ya Uzamili 18 na Shahada ya Kwanza 2. Hii imefanyika kwa ushirikiano na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Pia kuanzishwa kwa programu maalumu ya Mafunzo ya Ufundi kwa Wahitimu wa Kike wa Uhandisi 40 inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa ushirikiano na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB). Programu za kuongeza uwezo na kuhamasisha kuhusu Ushirikishwaji wa Jinsia kwa Viongozi na wawakilishi kutoka idara za kampuni, mikoa, na kanda zitafanyika hivi karibuni kwa ushirikiano na ESAMI na TGNP. Uzinduzi wa Mpango wa Kazi wa Miaka 4 wa Jinsia uliofanyika tarehe 30 Machi 2023 ukiwa na maeneo matano ya kuingilia kati kwa mkakati. Shirika limejipanga kuhakikisha mwanamke anapata nafasi ili kuunga mkono jitihada za Mhe Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika sekta ya Nishati.
Ilianza siku, wiki, mwezi, mwaka na hatimaye miaka mitatu ndani ya wadhifa wa urais, ndivyo unavyowe
Ilianza siku, wiki, mwezi, mwaka na hatimaye miaka mitatu ndani ya wadhifa wa urais, ndivyo unavyoweza kuichambua safari ya Rais Samia Suluhu Hassan kama mkuu wa nchi. Rais Samia aliapishwa kuwa Rais, Machi 19, mwaka 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, John Magufuli, aliyefariki Machi 17, mwaka huo. Matakwa ya Ibara ya 37(5) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ndiyo yaliyohalalisha mabadiliko hayo ya uongozi, hivyo aliyekuwa Makamu wa Hayati Magufuli, Samia Suluhu Hassan aliapishwa kupokea kijiti cha urais. "Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano..." Inaeleza Ibara hiyo ya 37(5). Kama utafananisha muda aliokaa Rais Samia madarakani na umri wa binadamu, basi ni sawa na mtoto aliyeanza kukimbia. Kifo cha Hayati Magufuli, kilitazamwa na wengi kama ndiyo ukomo wa kila alichokiasisi wakati wa utawala wake. Katika kipindi cha miaka sita ya vipindi viwili vya urais wa Hayati Magufuli, alijikita zaidi katika utekelezaji wa miradi hasa ya miundombinu. Ndani ya uongozi wake, ndipo utekelezaji wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) ulianza, Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), Daraja la Tanzanite, Daraja la JP Magufuli Kigongo-Busisi, Daraja la Mfugale na Makutano ya Barabara Ubungo, nikitaja kwa uchache. Alifariki ikiwa tayari ameshakamilisha miradi ya daraja la Mfugale na alishazindua makutano ya barabara Ubungo aliyoyapa jina la Kijazi Interchange. Sababu za kuelekeza nguvu za utendaji wake katika utekelezaji wa miradi hiyo ni kile alichowahi kukisema enzi za uhai wake kuwa, anahofia iwapo kuna kiongozi atakayefuata atakayekuwa na uwezo wa kuifanya kazi hiyo. "Ninawaambia ukweli tusipozitatua (changamoto) katika awamu hii, sina uhakika kama atakayekuja atakuwa na uwezo wa kuzitatua. Kwa sababu katika kutatua changamoto unakutana na magumu mengi, ambayo huwezi kuyataja yote," aliwahi kusema Hayati Magufuli Januari 29, 2019. Katika miaka sita ya utawala wake, Hayati Magufuli aliishi katika dhana kuwa, hakuna mwingine atakayekuwa na uwezo wa kutekeleza kile anachokifanya iwapo hatakuwepo duniani. "Je, nikiondoka leo Stieglers Gorge itajengwa? Nikiondoka leo Standard Gauge itajengwa? Je, nikiondoka leo ndege zitaendelea kununuliwa? Hapo ndipo napata nguvu za kusema acha niendelee kufanya kazi kwa ajili ya Watanzania walionichagua," amewahi kusema Hayati Magufuli. Kauli hizo ndizo zilizozusha hofu kwa Watanzania wengi kuwa, kifo chake ndiyo mwisho wa utekelezwaji wa kile alichokianzisha, lakini katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia umeshuhudiwa uhalisia tofauti. Baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan aliweka wazi msimamo wake juu ya yote yaliyoachwa na mtangulizi wake. Katika hotuba yake ya kwanza bungeni jijini Dodoma Aprili 22, 2021 Rais Samia alionyesha msimamo wa kuendeleza yale yaliyoanzishwa na mtangulizi wake. "Mimi na Hayati Magufuli ni kitu kimoja, kwa maana hiyo mambo mengi ambayo Serikali ninayoiongoza imepanga kuyatekeleza ni yale ambayo yalielezwa na Hayati Magufuli wakati akilizindua Bunge hili," alisema Rais Samia. Hilo linathibitika na kinachoshuhudiwa sasa, ambapo miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake anaendelea kuitekeleza ndani ya uongozi wake. Miongoni mwa miradi hiyo ni JNHPP. Magufuli alifariki dunia katika kipindi ambacho utekelezaji wa mradi huo ulikuwa katika asilimia 33. Katika kipindi hicho, hakukuwa na aliyeamini kama kutakuwa na mwendelezo wa utekelezaji na ndipo matumaini ya kupatikana kwa nishati ya umeme wa uhakika yaliyeyuka vichwani mwa Watanzania. Lakini, Rais Samia ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake, mradi huo umeshuhudiwa aliendelea kutekelezwa na hadi sasa umefikia asilimia 97. Hadi hivi tunavyoadhimisha miaka mitatu ya Rais Samia, tayari Watanzania wameanza kunufaika na mradi huo, baada ya mmoja kati ya mitambo tisa kuwashwa na kuanza kuingiza umeme katiia gridi ya taifa. Pamoja na mtambo huo unaoingiza megawati 235 katika gridi ya taifa, mtambo mwingine namba nane unatarajiwa kuwashwa hivi karibuni, nao utaingiza megawati 235 za umee katika gridi hiyo. Ukiachana na mradi wa JNHPP, ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia daraja la JP Magufuli, Kigongo Busisi linaendelea kutekelezwa. Wakati Magufuli anafariki, utekelezaji wa daraja hilo ulikuwa ni asilimia 16, lakini ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia, daraja hilo limefikia asilimia 85 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu. Mradi mwingine ni Reli ya SGR, iliyoachwa na Hayati Magufuli ikiwa katika awamu ya kwanza wa Dar es Salaam-Morogoro, kipande ambacho katika uongozi wa Rais Samia kimekamilika na sasa vipande vingine vinaendelea kutekelezwa. Nini maana yake? Akizungunzia hatua hiyo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe anasema uendelezaji wa miradi hiyo ni janbo jema kwq kuwa ina maslahi ya wananchi. Mara nyingi, anasema Afrika huangushwa na kukosekana mfumo wa uendelezaji wa maono mazuri pale inapotokea mwenye maono ameomaliza muda wake au kufariki dunia. Lakini, kwa Rais Samia, Dk Kabobe anasema amefanya vema kwa kuwa pamoja na miradi aliyoibuni yeye binafsi, anaendeleza pia iliyoachwa na mtangulizi wake. "Angalia mradi wa JNHPP, Daraja la Kigongo-Busisi, miundombinu mbalimbali. Anastahili pongezi maana Afrika tumekuwa na tatizo kubwa pindi kiongozi anapomaliza muda wake anayefuata huja na mambo yake kabisa," anasema. Anatolea mfano wa miradi iliyowahi kuachwa katika awamu zilizopita, ukiwemo wa gesi Mtwara iliyotarajiwa kuzalisha umeme kiasi cha kuuza nje ya nchi, enzi za utawala wa Jakaya Kikwete. "Jiulize ule mradi mkubwa wa gesi ya Mtwara uko wapi leo? Tuliambiwa utazalisha umeme hadi tuuze kwa nchi jirani ila leo utakubaliana na mimi kuwa ndoto hizo ziko ICU kama bado hazijafa," anasema. Anasema kumekuwa na viongozi wenye maono makubwa na ya kuleta maendeleo kwa watu, lakini kunakosekana mwendelezo, hasa pale kiongozi husika anapotoka madarakani. "Rais Samia ana maono makubwa kwa nchi yetu ila swali linakuja, akiondoka madarakani aliyoanzisha na anayoyafanya yataendelezwa?" anahoji Dk Kabobe. Anasema kwa nchi za Afrika, utashi binafsi wa kiongozi unapewa nafasi kubwa na mifumo ya utawala hasa Katiba. Anaeleza kuna haja ya kutengeneza mifumo thabiti yenye mizizi imara ya kikatiba. "Kama leo ningeonana na Rais Samia, pamoja na mambo mengine ningemuomba atujengee mifumo imara ya utawala na mifumo hiyo ijengwe na Katiba ili tuwe na usimamizi imara na mwendelezo wa yale mema yanayoanzishwa na viongozi wetu," anasema. Pasi na kuwa na mifumo imara, Dk Kabobe anasema Tanzania haitafika mbali kwa sababu kila anayekuja atakuja na yake na kuondoka nayo, haitakuwa rahisi kumpata kama Rais Samia anayeendeleza ya mtangulizi wake.
Wakati leo ukitimia mwaka wa tatu tangu alipofariki Rais wa awamu ya tano, John Magufuli, familia ya
Wakati leo ukitimia mwaka wa tatu tangu alipofariki Rais wa awamu ya tano, John Magufuli, familia yake imeweka wazi namna kifo cha kiongozi huyo kilivyoonyesha sura halisi za binadamu. Kulingana na wanafamilia ya Hayati Magufuli, enzi za uhai wa kiongozi huyo, familia hiyo ilidhani ina marafiki na watu wengi wanaoipenda, lakini kifo chake kimeibua uhalisia tofauti na walivyodhani. Magufuli alifariki dunia Machi 17, mwaka 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya mfumo wa umeme wa moyo yaliyomsumbua kwa miaka kadhaa. Hadi anafariki dunia, mkuu huyo wa nchi alishahudumu katika vipindi viwili vya urais, yaani miaka mitano ya awamu ya kwanza na mwaka mmoja wa awamu ya pili. Baada ya kifo chake kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, Makamu wake, Samia Suluhu Hassan aliapishwa kupokea kijiti cha wadhifa huo, tukio lililofanyika Machi 19, mwaka huu. Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo, mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli alisema kifo cha baba yake kimeionyesha familia sura halisi za binadamu. Kauli yake hiyo, inatokana na kile alichofafanua, enzi za uhai wa baba yake familia ilidhani ina marafiki na watu wengi wanaoipenda, lakini alipofariki ndipo ilipouona uhalisia. "Kuondoka kwa baba (Hayati Magufuli) kumetufundisha kuelewa ni watu wa aina gani. Kuna mahala tulidhani tuna watu wengi, marafiki na kupendwa sana lakini kutokuwepo kwa baba kumetufanya kuwafahamu binadamu kwa sura zao halisi," alisema Jesca. Kwa mujibu wa Jesca, hali hiyo ndiyo inayowakumbusha mafunzo aliyokuwa akiwapatia Hayati Magufuli enzi za uhai wake ya kuishi kwa kumtegemea Mungu, badala ya binadamu. "Na ndipo tunapokumbuka mafundisho yake ya kumtegemea Mungu na sio binadamu," alisema Jesca ambaye ni mziwanda wa Hayati Magufuli. Hata hivyo, Jesca alisema kutokuwepo kwa Baba yake ni jambo lisilozoeleka kwa familia, kwani hana mbadala katika familia, akiwa baba, mume na babu na kiongozi mwa nchi yake. "Tunaendelea kumuenzi na kumkumbuka kwa namna alivyotupenda na kutuwekea msingi mzuri unaotufanya tuweshe kuishi bila manung’uniko kwa sababu alituandaa kwamba hakuna mtu wa kutusadia bila kufanya kazi," alisema. Kulingana na mwana huyo, Hayati Magufuli aliamini katika kufanya kazi, akiwahakikishia hakuna mtu wa kuwasaidia pasipo kufanya kazi katika maisha. Lakini, alisema kiongozi huyo alijua kutenganisha kazi na familia hasa pale walipomwomba fedha, pamoja na nyadhifa zake lakini aliomba muda wa kuitafuta. "Hata tulipomuomba pesa tukiamini yeye ni Rais au pindi alipokuwa Waziri aliomba muda atafute na kutuasa kuwa cheo chake hakihusiani na majukumu yake kama baba wa familia, alitufundisha kujitegemea na kutambua kufanya kazi ndio msingi katika maisha," alisema Jesca. Sifa nyingine ya Hayati Magufuli inayokumbukwa na Jesca ni mwenye upendo kwa familia yake. "Hata tulipomkosea, tulimuomba msamaha na kutusamehe na baada kusamehe hakuwa mtu wa kuweka kinyongo bali alikuwa akitoa nafasi nyingine ya kujirekebisha," alisema. Pamoja na wingi wa majukumu yake, Jesca alisema Hayati Magufuli alikuwa na muda wa kufuatilia maendeleo ya kila mtoto katika familia na kuwakumbusha kufanya kazi na kujituma. Kwa upande wa uongozi, Jesca alisema anatambua Baba yake alikuwa tayari hata kupoteza uhai wake ili kuhakikisha anailinda nchi yake na Watanzania wote. "Hata alipopitia katika nyakati ngumu za uogozi alikuwa mtu wa kumtangiliza Mungu mbele, hata alipopitia nyakati za kusemwa na kudhalilishwa tulikuwa tukikutana naye kwenye corridor za ikulu na kutuomba tuzidi kusali sana na kumuombea na kuamini palipo Mungu yote yatapita," alisema. Alisema baba yake alilitanguliza taifa lake mbele na kulipenda kwa moyo wake wote kuliko hata familia na uhai wake. Katika kipindi cha miaka sita ya uongozi wake kama Rais, Hayati Magufuli ameacha alama kadhaa ikiwemo miradi ya miundombinu. Miongoni mwa miradi hiyo ni Daraja la Mfugale, Barabara za Mzunguko Kijazi, Bwawa la Umeme la Julius Nyerere ambalo alifariki likiwa limetelekezwa kwa asilimia 33. Hata hivyo, baada ya kifo chake, aliyetokea kijiti cha wadhifa wa urais, Samia Suluhu Hassan ameendeleza miradi yote iliyoachwa naye.
Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020/25, imeielekeza Serikali kufanikisha upati
Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020/25, imeielekeza Serikali kufanikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 95 kwa maeneo ya mijini, lakini asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini. Hata hivyo, hotuba ya makadirio ya fedha, mapato na matumizi ya Wizara ya Maji katika mwaka wa fedha 2023/24, imeweka wazi kuwa hali ya upatikanaji wa huduma hiyo mijini ni asilimia 88. Kadhalika katika maeneo ya vijijini, hali ya upatikanaji wa maji ni asilimia 77, ikiongezeka kutoka asilimia 74 ya mwaka 2021. Licha ya hatua hiyo, bado kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo katika baadhi ya maeneo nchini, ndiyo sababu Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kulikabili hilo. Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto hiyo, ikielezwa wananchi hununua ndoo moja ya lita 20 ya maji kwa Sh300 na baadhi hulazimika kutumia ya visima. Kwa ujumla, hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya hiyo yenye wakazi 303,000 kulingana sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, ni asilimia 76. Matumaini ya kukoma kwa changamoto ya huduma hiyo katika Wilaya ya Same yamebaki kwenye mradi wa maji unaotekelezwa na Serikali wa Same-Mwanga-Korogwe. Mradi huo ni miongoni mwa mingi inayotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ukitarajiwa kuzinufaisha Wilaya za Same, Mwanga mkoani Kilimanjaro, kadhalika na Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Namna utakavyomaliza tatizo la maji Msimamizi Msaidizi wa mradi huo, Emmanuel Magembe anasema kufikia Juni mwaka huu changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Wilaya hizo inatarajiwa kuisha. Kuisha kwake kutatokana na kile alichofafanua kuwa, mwezi huo mradi wa Same-Mwanga-Korogwe unatarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma. Anaeleza utekelezaji wa mradi huo, umegawanywa katika awamu mbili ambazo nazo zimegawanywa kwa vipande vipande. Kwa mujibu wa Magembe, utekelezaji wa awamu ya kwanza unahusisha vipande vinne ambavyo ndani yake kuna kazi za kusafisha maji na kuyatibu. Katika vipande hivyo kulingana na Magembe, kumefanyika ujenzi wa chanzo, kituo cha kupoza umeme, laini ya umeme kilomita 10 na laini ya kusafirisha maji. Kadhalika kazi hiyo, Magembe anasema inahusisha ujenzi wa tenki la Kisagara, shughuli zote zikifadhiliwa na Serikali na hadi sasa hatua ya utekelezaji ni asilimia 85. "Sasa vipande hivi ndivyo vinavyotarajiwa kukamilika Juni mwaka huu na huduma ya maji itaanza kupatikana kwa wakazi wa maeneo husika," anasema. Hata hivyo, matumaini mengine ya kukamilika haraka Kwa mradi huo, anasema ni msukumo uliopo serikalini, ambapo karibu kila wiki viongozi kutoka Wizara ya Maji hutembelea kwenda kuona hatua za utekelezwaji. Vipande vingine, anasema vinahusiana kupeleka maji katika Vijiji tisa vya Bwawa la Nyumba ya Mungu na tayari utaratibu wake unaandaliwa. "Kipande cha tatu ni kupeleka maji katika Mji wa Mwanga na mkamdarasi kwa sasa analaza mabomba na kufikia Juni tayari watu wa Mwanga wataanza kupata huduma," anasema. Anasema kipande cha nne ni kwa ajili ya kupeleka maji katika Wilaya ya Same na kazi hiyo inaendelea na itakamilika Juni mwaka huu. Mradi huo unaogharimiwa kwa Sh6.26 bilioni na Dola za Marekani 166.1 milioni (zaidi ya Sh421.52 bilioni) zinazogharimiwa na Serikali na Kuwait, unatarajiwa kuhudumia jumla ya vijiji 38 vya wilaya hizo. Magembe anasema takriban wananchi 456,931 katika Wilaya hizo wananufaika na mradi huo. Wanufaika Hassan Mkubwa ni mkazi wa Kata ya Same Mjini, anasema kwa sasa wanategemea visima kupata huduma hiyo na matumaini yao yamebaki katika mradi wa Same-Mwanga-Korogwe. "Maji safi na salama tunayasikia kwa wenzetu, sisi tunatumia ya visima ambayo si salama, lakini tunamshukuru, Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuruhusu mradi huu uendelee," anasema. Gurisha Lishingo ni dereva bodaboda katika Wilaya ya Same, anasema matarajio ya kukamilika kwa mradi huo ni kwa wananchi wa maeneo hayo. "Suala la maji Same ni janga la muda mrefu sana hata sasa hivi hali unayoiona sio kwamba hakuna shida hapana, ni kwa sababu tu ya mvua ndogondogo zilizonyesha ndiyo zimesaidia kidogo. "Lakini kiuhalisia suala la maji Same ni mtihani, ikifika Juni hadi Agosti huwa na mtihani sana. Tunatarajia makubwa kutoka kwenye mradi huu ambao Rais Samia ameukwamua baada ya kukwama kwa miaka kadhaa," anasema. Mamalishe katika Wilaya hiyo, Hadija Nassor anasema changamoto ya maji inasababisha gharama za uendeshaji wa biashara yake, lakini angalau yupo kwenye matumaini makubwa. Anaeleza kwa sasa ananunua dumu moja la liga 20 la maji kwa Sh300 hadi Sh500 na hivyo kuongeza gharama za uzalishaji. "Hatua tu ya Rais Samia kuleta wakandarasi wawili huku na kule Korogwe mkoani Tanga ni jambo kubwa maana angebaki mkandarasi mmoja hiyo huyo anafanya huku na kule kidogo ingekuwa shida. Tunamshukuru (Rais Samia)," anasema. Historia ya mradi Haikuwa safari nyepesi hadi kufikia hatua za mwisho za utekelezaji wa mradi huo, ulipitia milima na mabonde lukuki. Kulingana na Magembe, mradi huo rasmi ulianza mwaka 2014 na ulitarajiwa kukamilika mwaka 2021. Anasema kuliibuka mgogoro wa kimkataba uliolazimu mkataba wa mkandarasi wa awali, Kharafi & Sons na Badr, usitishwe mwaka 2020. "Baada ya kusitishwa mikataba ya Wakandarasi wa awali Wakandarasi wapya Helpdesk, Central na Advent waliajiriwa na Kharafi & Sons, hivyo ujenzi wa mradi ulianza upya rasmi mwaka 2022," anasema.
Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa
Ilianza kama ndoto, baadaye ukawa uhalisia, ndivyo unavyoweza kuitafsiri miaka mitatu ya utendaji wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya nishati. Rais Samia aliianza safari ya urais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, Hayati John Magufuli, aliyefariki Machi 17, mwaka huo. Safari yake ya utendaji katika wadhifa wa urais, ilianza na mashaka kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakidhani uendelezaji wa miradi hasa ya nishati iliyoachwa na mtangulizi wake, kisingekuwa kipaumbele chake. Wengi walibaki na dhana kuwa, kifo cha mtangulizi wake ndiyo mwisho wa mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), linalotarajiwa kuzalisha jumla ya megawati 2,115. Fikra za wengi zilijikita kwenye mabadiliko ya mbinu za kukabili changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika, wakidhani Rais Samia angekuja na mikakati tofauti. Mashaka yalizidi kuongezeka wakidhani kuwa, hadi mikakati mipya itakapofanikiwa, tayari wananchi watakuwa wameshaumizwa na changamoto ya upatikanaji wa nishati hiyo kwa muda mrefu. Aprili 22, mwaka 2021 ndiyo siku ambayo Watanzania walifumbuliwa macho juu ya msimamo wa Rais Samia kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya umeme. Rais Samia alifanya hivyo alipolihutubia Bunge jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, aliahidi kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake, kadhalika kubuni mipya ili kuwahudumia wananchi. Katika hotuba yake hiyo, Rais Samia aliweka wazi kuwa, kukatika kwa umeme ni miongoni mwa malalamiko mengi aliyokuwa akipokea wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020, alipokuwa akimnadi Hayati Magufuli. "Miradi yote ya umeme inayoendelea kutekelezwa katika ni lazima ikamilike katika kipindi changu chote cha uongozi," alisema Rais Samia alipolihudumia Bunge jijini Dodoma. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa shughuli za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, nalo lilijiweka sawa kuianza safari hiyo na hadi sasa linahesabu mafanikio. Mwanzo wa safari Baada ya kujenga msingi wa msimamo wake, mkuu huyo wa nchi alifungua ukurasa wa utendaji katika sekta ya nishati hasa baada ya Bunge kupitisha bajeti ya matumizi ya Wizara ya Nishati ambayo karibu robotatu ya fedha zimeekekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya kufua, kusafirisha na kusambaza umeme nchini. Miongoni mwa miradi hiyo, upo mradi wa JNHPP unaotazamwa kama muarobaini wa changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini. Rais Samia alipokea kijiti cha urais, kipindi ambacho mradi wa JNHPP ulitekelezwa kwa takriban asilimia 36 na kwamba hadi inafika miaka mitatu ya uongozi wake mradi huo umefikia asilimia 97. Hadi inafikia hatua hiyo, kulikuwepo na juhudi lukuki zilizofanywa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia. Miongoni mwa juhudi hizo ni kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa mradi ambazo kwa ujumla wake unatekelezwa kwa Sh6.6 trilioni. Matumaini ya awali yalianza Desemba 22 mwaka 2022, kipindi ambacho Rais Samia aliongoza ujazaji maji katika bwawa hilo. Mafanikio Lakini Februari 25, mwaka huu ndiyo uliokuwa wakati muhimu zaidi kwani mtambo mmoja kati ya tisa katika Bwawa hilo, uliwashwa na kuanza kuingiza umeme katika gridi ya taifa Mtambo huo, ulizalisha na kuingiza megawati 235 za nishati hiyo kwenye gridi ya taifa na hivyo kupunguza adha ya mgawo wa umeme, iliyokuwa unawasumbua Watanzania kwa wakati huo. Wakati mtambo huo unawashwa na kuingizwa umeme huo katika gridi ya taifa, Tanzania ilikuwa katikati ya changamoto ya upatikanaji wa umeme iliyosababishwa na uzalishaji duni katika vyanzo mbalimbali hasa vya maji. Kutokana na hali hiyo, hatua ya kuwashwa kwa mtambo huo, ilifufua matumaini ya upatikanaji wa umeme nchini, kadhalika matunda ya JNHPP yalianza kuwagusa wananchi. “Kufikia mwezi wa tatu Mungu akipenda tutaingiza jumla ya megawati 470 (kutoka katika mitambo miwili), tutakuwa na megawati za ziada zaidi ya 70. Baada ya mwezi wa tatu hatutazungumza upungufu wa umeme tena,” alisema Dk Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati alipokuwa kwenye mradi huo Februari mwaka huu. Faida nyingine za mradi Iwapo Bwawa hilo litakamilika Magufuli katika bonde la mto Rufiji yatabaki kuwa historia. Kwa kawaida kabla ya ujenzi wa bwawa hili, maji kutoka Mikoa 11 wakati wa masika yalikusanyika kwa wingi katika Mto Rufiji na kusababisha mafuriko kwa wananchi. Adha hiyo sasa itakwisha. Maji yatatoka kwa kiwango cha wastani wa lita milioni 2 kwa sekunde na kiwango hiki kitaendelea kutoka iwe wakati wa kiangazi au masika. Hii inatoa fursa kwa watu wanaoishi kwenye Bonde la Mto Rufiji kujipanga na maeneo yaliyokuwa yanafurika maji, sasa kupitia kilimo cha umwagiliaji wanaweza kulima mwaka mzima. “Umeme utakaozalishwa ni megawati 2,115. Kwa sasa tunatumia wastani wa megawati 1,500. Hivyo hata kikitokea kiangazi maji yakapungua kwa nusu, bado tutakuwa na megawati zaidi ya 1,000, hivyo hata ukitokea ukame Tanzania baada ya mradi huu haiwezi tena kurudi kwenye unyonge wa umeme,” anasema Dk Biteko. Ukiacha udhibiti wa mafuriko na kuongezeka kwa umeme kwenye gridi ya taifa, ongezeko hili la umeme linaongeza mapato ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Serikali kwa ujumla. Kuingia kwa megawati 2,115 ina maana mapato ya mauzo ya umeme ya TANESCO yanaongezeka mara mbili, hivyo kuongeza mapato ya shirika na Serikali. Mradi huu pia utawezesha kilimo cha umwagiliaji kwa wastani wa hekta 450,000. Ukiacha sasa uhakika uliojitokeza kwa mazingira kutomomonyolewa na mafuriko, Wahandisi Watanzania walioshiriki katika ujenzi wa mradi huu wamepata ujuzi mkubwa ambao nchi itaendelea kuutumia kwa kujenga miradi mingine ya mabwawa kama walivyofanya Misri kwa kujenga Aswan High Dam na Aswan Low Dam katika Mto Nile, yanayowapatia umeme kwa wastani wa megawati 2,370, kwa maana ya Aswan High Dam megawati 2,100 na Low Dam Megawati 270. Kupitia Bwawa hili la Nyerere wanyama watapata maji ya kutosha, kutakuwapo uvuvi endelevu na utalii kama inavyofanyika kwa nchi nyingine zenye mabwawa ya kimkakati kama haya. Kuna dhana ya masuala la maendeleo ya jamii, ambapo umeme wa kutosha utasaidia maendeleo ya viwanda. Maeneo mengine ya Bwawa hilo Mradi huu umejengwa katika maeneo manane hadi uanze kuzalisha umeme kama ifuatavyo:- 1. Kazi za kuchepusha mto (Diversion works), 2. Tuta Kuu (Main Dam), 3. Njia za maji ya kuendesha mitambo (Power Waterways), 4. Jengo na mitambo (Powerhouse), 5. Kituo cha kusafirisha umeme (Switchyard), 6. Matuta madogo (Saddle Dams), 7. Makazi ya kudumu (Operation Village) na 8. Barabara na daraja la kudumu (Permanent Roads & Bridge). Bwawa hili lina mahandaki matatu yenye urefu wa mita 12 kwa 17 na njia tatu za kupitisha maji, ambayo mbele yanagawanyika na kuwa na mitambo tisa ya kuzalisha umeme. Kila mtambo utazalisha megawati 235, ambapo mitambo 9 kwa ujumla itazalisha megawati 2,115. Kwa upande wa tuta la Bwawa la Nyerere kwenye kitako chini ukuta una upana wa mita 100 na ukuta huo unakwenda unapungua hadi juu ambako una upana wa mita 10. Ukuta wa tuta una urefu wa mita 190 kutoka usawa wa bahari. Juu ya ukuta huu wa bwawa hili itakuwapo barabara inayopitisha magari. Mito inayojaza maji kwenye bwawa Mito kutoka mikoa 11 inajaza maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere. Mito mikubwa mitatu inayojaza maji kwenye Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere inaanzia katika mikoa 10. Mito hiyo ambayo ni Ruaha, Kilombero na Luwengu, inakusanya vijito kutoka mikoa ya Tabora, Singida, Dodoma, Iringa, Mbeya, Morogoro, Pwani, Ruvuma, Dar es Salaam na Njombe. Mito kutoka mikoa hii yote inamwaga maji katika Bonde la Mto Ruvu. Wataalamu wanasema kutokana na sababu hii, Bwawa la Mwalimu Nyerere halitakaukiwa maji kwa urahisi kama ilivyo kwa Bwawa la Mtera ambalo kwa mwaka 2022 pamoja na ukame, uzalishaji wa umeme ulipungua kwa megawati 5 tu, ikilinganishwa na Kihansi iliyopoteza megawati 153. Hii ni kwa sababu bwawa hili litakuwa linakusanya maji, halitiririshi kama mto. Bwawa hili linalokadiriwa kudumu kwa miaka 100 na zaidi, limeleta faida kubwa nchini. Saruji yote inayojenga Bwawa la Nyerere ambayo ni tani 850,000, nondo tani 70,000 na udongo maalumu tani 250,000, ajira 12,298 vyote hivi vimekuwa vya manufaa kwa Tanzania. Ujazo wa bwawa Bwawa hili lenye urefu wa kilomita 100 kutoka ncha moja kwenda nyingine na ukubwa sawa na nusu ya Mkoa wa Dar es Salaam, litajaza maji wastani wa lita za ujazo bilioni 33.2. Bwawa la Mwalimu Nyerere utafiti unaonyesha kuwa bwawa hilo halina uwezekano wa kujaa tope kama walivyokuwa wakidai wanaharakati wa mazingira, kwa Afisa Mwandamizi kusema: “Utafiti umeonyesha kuwa ndani ya miaka 100 ijayo bwawa linaweza kuwa na tope wastani wa asilimia 0.92. Hiki ni kiwango kidogo sana.” Baada ya kusaini mkataba makandarasi walianza kazi ya kutengeneza miundombinu wezeshi, ikiwemo barabara, maji, umeme na reli kwa ajili ya kubebea mizigo ya kwenda eneo la mradi. Mwaka wa kwanza walifanya kazi ya kuchepusha maji ambapo mtaro (tunnel) ulijengwa na kuuhamisha njia mto wote kuruhusu ujenzi wa tuta kwenye kitanda cha mto. Kwa sasa ujenzi wa mradi unaelekea ukingoni kwa kuanza uzalishaji, tayari umekamilisha ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme kutoka kwenye mradi kwenda Chalinze mkoani Pwani na ambapo baada ya kufika Chalinze njia moja inakwenda Dar es Salaam na nyingine Dodoma ili kuwezesha umeme huo kusambazwa nchi nzima. Umeme wa maji ndio umeme rahisi kuliko umeme wowote hapa duniani. Gharama ya kuzalisha uniti moja ya umeme wa maji ni Sh36 na baada ya muda mrefu gharama hizi hushuka, ilhali kwa sasa kupitia vyanzo mbalimbali Tanzania inazalisha uniti moja kwa wastani wa senti 10.7 za dola sawa na Sh249 kwa uniti. Misri inazalisha umeme kwa senti 4.6 za dola sawa na Sh107, Afrika Kusini senti za dola 7.4 sawa na Sh172, Ethiopia wanatumia maji senti za dola 2.4 sawa Sh56 na India senti za dola 6.8 sawa na Sh158 Kauli za wateja Kuingizwa kwa megawati 235 za umeme katika gridi ya taifa, kumeleta ahueni ya upatikanaji wa umeme kwa wateja kama inavyoelezwa na Mwanahamisi Hassan mkazi wa mabibo Dar es Salaam. Anasema kabla ya kuwashwa mtambo huo, umeme katika eneo analoishi ulipatikana asubuhi hadi jioni na usiku ulikatika, lakini kwa sasa hakuna tena changamoto hiyo. Kulingana na Mwanahamisi, baada ya kusikia kuhusu kuwashwa kwa mtambo huo, kumekuwa na uhakika a upatikanaji wa nishati hiyo. “Sikuwa naamini kama ungefika wakati mgawo ungeisha namna hii. Ilikuwa shida sana lakini kwa sasa mambo yamekwisha. Kwa kweli hii miaka mitatu ya Rais Samia na Tanesco kwa ujumla kazi imeendelea,” anasema Mwanahamisi. Mbali na Mwanahamisi, Mwananchi mwingine anayeeleza kuguswa na upatikanaji wa umeme ni Donald Mayunga Mkazi wa Dar es Salaam, anasema kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa umeme umeimarika. “Hali ilikuwa mbaya sana, lakini naona kabisa tunaondoka kwenye changamoto. Kwanza sikuamini kama mama (Rais Samia) angemalizia ujenzi wa Bwawa hilo kwa sababu kila mtu ana utashi wake. “Lakini hadi leo hii tunapata umeme, huyu Rais Samia amefanya kazi kubwa sana,” anasema Mayunga. Mradi wa kupitisha umeme chini ya ardhi Ili kukabili changamoto ya kupotea kwa umeme, Tanesco katika kipindi hicho cha miaka mitatu ndipo ilipoanza utaratibu wa kupitisha nishati hiyo chini ya ardhi. Mradi wa Kurasini unaopitisha nyaya chini ya ardhi zenye urefu wa zaidi ya kilomita sita ni miongoni mwayo. Akizungumza kuhusu hilo, Msemaji wa Tanesco, Kenneth Boymanda anasema kwa sasa mkandarasi anaendelea na kazi kufanikisha mradi huo. Ingawa haujakamilika, anasema shughuli zinaenda vema na kama zilivyotarajiwa. "Mradi tulionao kwa sasa ni wa Kurasini na mkandarasi yupo kazini anaendelea kutandika nyaya chini ya ardhi, kuhakikisha kazi hiyo itakamilika," anasema Boymanda. TANESCO na matumizi ya nishati safi Mei 29, mwaka jana, Tanesco ilisaini mkataba wa Sh274.7 bilioni kwa ajili ya mradi wa umeme wa nishati ya jua Megawati 150 wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga. Kulingana na Meneja wa Miradi, Usafirishaji na Usambazaji kutoka Tanesco, Frank Mashalo mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 50 za umeme. Anasema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja na mkandarasi kutoka China, Sinohydro Corporation. “Mradi huu unalenga kuongeza uhakika wa usambazaji nishati nchini na ni sehemu ya dhamira ya Tanesco kuhakikisha kunakuwa na mchanganyiko wa nishati kutoka vyanzo mbalimbali,” alisema Mashalo. Mashalo alisema mradi huo pia utachangia sehemu ya juhudi za kuhamia katika nishati safi. Mradi huo ni mmoja kati ya miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua katika nchi za Afrika Mashariki. Miaka mitatu na huduma za kidigitali Ndani ya uongozi wa Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu, ndipo huduma za kidigitali ziliboreshwa zaidi huku programu mbalimbali zikizinduliwa. Miongoni mwa programu hizo, ipo Nikonekt kwa ajili ya kuunganisha huduma ya umeme kwa wananchi. Huduma hiyo ya kidigitali inampunguzia mteja kazi ya kwenda zilipo Ofisi za Tanesco kuomba huduma ya kuunganishiwa umeme, badala yake atatumia simu janja kuwasiliana na watoa huduma kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo. Mbali na huduma hiyo ya kidigitali kuwaondolea wananchi ulazima wa kusafiri hadi zilipo Ofisi za Tanesco kuomba huduma, pia imesaidia kupunguza muda wa mteja kuunganishiwa umeme. Kutoka kusubiri kwa takriban mwezi mmoja Hadi kupata huduma ya kuunganishiwa umeme, Nikonekt imefanya huduma hiyo ipatikane ndani ya siku tatu hadi nne. Lakini, matumizi ya huduma hiyo yanaondoa urasimu na kukomesha vishoka na vitendo vya rushwa, kwani huduma zinatolewa kupitia njia ya mtandao bila kulazimisha watu kuonana faragha. Kwa sasa hautalazimika tena kumtafuta Ofisa wa Tanesco, kumuomba akusaidie kuharakisha uunganishwaji wa umeme, badala yake itatumia simu yako janja kuomba huduma na utapatiwa ndani ya muda muafaka. Hayo yote yamefanyika katika kipindi cha uongozi wa miaka mitatu ya Rais Samia.
Udhibiti wa mianya ya wizi wa makusanyo na kutegua kitendawili cha mkwamo wa vipuli vya mabasi katik
Udhibiti wa mianya ya wizi wa makusanyo na kutegua kitendawili cha mkwamo wa vipuli vya mabasi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni sehemu ya mzigo unaomkabili Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart), Waziri Kindamba. Mengine yanayosubiri utendaji wake ni kuboresha huduma za usafiri wa mabasi hayo, ambazo kwa sasa zimegubikwa na malalamiko kutoka kwa wananchi. Waziri Kindamba anakabiliwa na majukumu hayo, baada ya juzi Rais Samia Suluhu Hassan kumteuwa kuwa Mkurugenzi wa Udart, akichukua nafasi ya Gilliard Ngewe ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kindamba anakuwa Mkurugenzi wa nne ndani ya Dart tangu ilipoanzishwa. Aliyeanza ni Charles Newe, alifuatiwa na John Nguya kisha Ngewe na sasa ni Kindamba. Hata hivyo, utendaji katika nafasi hiyo Udart unatajwa kukwamishwa na changamoto zilizopo, ikiwemo wizi uliokithiri wa makusanyo unaosababisha kukosekana fedha za kuboresha huduma kama ambavyo Mwananchi limearifiwa. Kulingana na chanzo cha taarifa hiyo, kikwazo kingine cha utendaji katika kampuni hiyo ni mkwamo wa mzigo wa vipuli vya mabasi hayo TRA. Changamoto zilizopo Chanzo hicho cha kuaminika ndani ya Udart, kinaeleza ubovu wa mabasi na kupotea kwa mapato kulikokithiri ndilo jinamizi linaloikabili kampuni hiyo. Kulingana na chanzo hicho, katika kampuni hiyo yenye mabasi takriban 200, karibu nusu yake (mabasi 80) hayatembei, yameegeshwa kwa sababu ya ubovu. Hali hiyo, chanzo kinaeleza inasababisha kudorora kwa huduma, kwa kuwa idadi ya mabasi hailingani na mahitaji halisi akisisitiza, "hapo ndipo malalamiko ya abiria yanapoanzia." Mkwamo wa vipuri TRA Lakini yote hayo, mzizi wake anasema ni kukwama kwa kontena za vipuli vya mabasi hayo, jambo linalokwaza ufanyikaji wa matengenezo kwa yale yaliyoharibika. "Unaangalia utapata wapi fedha ya kununua vipuli wakati vilivyopo vimezuiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)," anasema. Chanzo hicho kinaweka wazi vipuli vilivyozuiwa TRA, ni vya mabasi 140 na kwamba iwapo vingeachiwa na kuanza kutumika, angalau mabasi 50 yangefanyiwa matengenezo. Kilipoulizwa chanzo hicho kueleza sababu za mkwamo wa vipuli hivyo TRA, kilidokeza kwa ufupi kuwa, "ni misunderstanding (hali ya kutoelewana." Hata hivyo, chanzo hicho hakijaweka wazi ni nani aliye katika hali ya kutoelewana na TRA kiasi cha kusababisha mkwamo wa vipuri hivyo. Kauli ya Tamisemi Alipotafutwa kuzungumzia mkwamo wa vipuli hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa alikiri uwepo wa jambo hilo. Pamoja na kukiri, Mchengerwa alisema mazungumzo yanaendelea kati ya TRA na wizara hiyo kukwamua mkwamo huo. "Tunaendelea na mazungumzo kuona namna ya kuliweka hilo vizuri," alijibu kwa ufupi akidokeza you kikaoni. Mapato kuvuja Katika mazingira hayo, chanzo hicho kinabainisha bado kuna upotevu uliokithiri wa mapato, unaosababishwa na wizi katika mfumo wa ukusanyaji nauli. "Mfumo wa ukusanyaji mapato ni manual wale wahudumu wanaamua wanachokitaka, anaweza kumpa abiria tiketi ya mwanafunzi ya Sh200, ilhali ni mtu mzima aliyelipa Sh650, kwa hiyo iliyobaki mkusanyaji anaweka mfukoni," anasema. Kutokana na mfumo uliopo, chanzo hicho kinaeleza ni vigumu kumkamata yeyote na haiwezekani kusimamia wasiibe. Chanzo hicho kinaeleza suluhu pekee ya uvujaji unaoendelea ni kubadili mfumo kutoka wa sasa na kutumia kadi ili kusiwe na utaratibu wa kupokea fedha mkononi. Kinachoshangaza chanzo hicho, kinasema uamuzi wa kutumia mfumo huo umekuwa kizungumkuti. Kinaweka wazi kuwa, kulikuwepo makubaliano kati ya Udart na Dart juu ya Desemba mwaka jana, utaratibu wa matumizi ya kadi uanze, lakini kilichofanyika ni kusaini mkataba na mkandarasi wa kuifanya kazi hiyo pekee. "Desemba kilichofanyika ni Dart kusaini mkataba na mkandarasi wa mfumo huo na hadi sasa haujaanza," anasema. Ilichokisema Dart kuhusu mfumo Alipotafutwa kuzungumzia hatua za mabadiliko ya mfumo, Mtendaji Mkuu wa Dart, Athuman Kihamia alisema tayari kadi 200,000 zimeshanunuliwa tangu Februari mwaka huu, kwa ajili ya mfumo huo. Sambamba na kadi hizo, Kihamia alisema kazi iliyobaki ni utengenezaji wa mageti janja, kazi ambayo inafanywa na mkandarasi kutoka Italia. "Matarajio yetu ni mwezi huu Machi au mwanzoni mwa Aprili kazi hiyo itakamilika na mfumo wa kadi utaanza kutumika," alisema. Chanzo hicho kilipoulizwa kuhusu nini anapaswa kufanya Mkurugenzi mpya wa Dart, kinasema ni kuhakikisha anafanikisha kufufua mabasi mabovu yaingie barabarani kufanya kazi. Lingine litakalorekodiwa kama mafanikio kwa Mkurugenzi mpya, chanzo hicho kinaeleza ni kuhakikisha abiria wanasafiri kama ilivyotarajiwa. Jambo lingine, kinasema ni kudhibiti mfumo wa ukusanyaji mapato.
Licha ya kupatikana kwa uongozi mpya wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) na Wakala wake (Da
Licha ya kupatikana kwa uongozi mpya wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) na Wakala wake (Dart), wadau wameonyesha mashaka, wakieleza uwezekano wa utenguzi wa mabosi hao kuendelea kutokana na uhalisia wa huduma. Kwa mujibu wa wadau wa usafirishaji, kuendelea kwa utenguzi na uteuzi mpya wa mabosi wa Dart na Udart, kutatokana na mzigo mkubwa ambao taasisi hizo zimejitwisha. Kauli hizo za wadau wa usafirishaji zinakuja siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya Mkurugenzi Mkuu wa Udart ikiwa ni miezi sita yangu alizofanya mabadiliko kama hayo. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus mabadiliko hayo yanahusisha uteuzi wa Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi wa Udart akichukua nafasi ya Gilliard Ngewe atakayepagiwa kazi nyingine. Hata hivyo, miezi mitatu iliyopita Januari 15, mwaka huu Rais Samia alifanya mabadiliko ya uongozi Dart akimteuwa Dk Athuman Kihamia kuwa Mtendaji Mkuu, akimrithi Dk Edwin Mhede. Teuzi na tenguzi katika taasisi hizo, zinatokana na wingi wa malalamiko yanayohusu huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka, Dar es Salaam. Kulingana na wadau sio kwamba waliowahi kuteuliwa hawana uwezo, bali wamezitwiaha taasisi hizo mzigo ulio nje ya uwezo wake. Mabadiliko mabosi Dart, Udart Oktoba 24, mwaka jana, Gilliard Ngewe alitambulishwa kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), akichukua nafasi ya John Nguya aliyekuwa Mkurugenzi wa pili tangu kampuni hiyo ilipoanzishwa mwaka 2016. Wa kwanza alikuwa Charles Newe. Kwa ujumla Ngewe amehudumu nafasi ya ukurugenzi wa Udart kwa miezi sita hadi jana, Rais Samia alipomteuwa Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo. Kindamba anaukwaa wadhifa huo, akitokea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nafasi aliyohudumu kwa mwaka mmoja, tangu Februari 26, mwaka jana. Kwa upande wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart), aliyeanza kuwa Mkurugenzi ni Ronald Rwakatare tangu mwaka 2016, miaka mitano baadaye Mei 15, 2021 nafasi yake ilirithiwa na Dk Edwin Mhede. Dk Mhede alihudumu katika wadhifa huo hadi Januari 15, mwaka huu pale mamlaka ya uteuzi ilipokabidhi mikoba ya bosi wa Dart kwa Dk Athuman Kihamia. Kwa maneno mengine kampuni na wakala huo kwa sasa zipo chini ya viongozi wapya, walioteuliwa wakipishana miezi mitatu. Dk Kihamia aliteuliwa Januari 15, mwaka huu kuwa Mkurugenzi mpya wa Dart na Kindamba aliteuliwa jana kuwa mkuu wa Udart. Mabosi hao ni kina nani? Wawili hao si mara ya kwanza kutokeza katika nafasi za uteuzi, wote wamewahi kushika nafasi mbalimbali katika awamu tofauti za uongozi. Kindamba kwa mara ya kwanza alichomoza katika nafasi za uteuzi, Septemba 23, mwaka 2016 Rais wa wakati huo, John Magufuli alipomteuwa kukaimu wadhifa wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL). Baadaye Julai 6, 2017 aliteuliwa kushika wadhifa huo, badala ya kukaimu na alihudumu kwa miaka takriban saba hadi Machi 14, mwaka 2022 alipompisha Peter Ulanga. Baada ya TTCL, Kindamba akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe na baadaye kuhamisha Tanga. Dk Kihamia naye hakuanzia Dart. Kabla ya hapo alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha tangu Mei 30, 2021. Si wadhifa huo tu, Dk Kihamia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, lakini kubwa zaidi aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuanzia Julai 10, 2018. Wadhifa wake ndani ya NEC ulikoma baada ya kuhudumu kwa siku 457 hadi Oktoba 1, 2019 aliporithiwa na Dk Charles Mahela. Malalamiko ya huduma Mzizi wa kuanzishwa kwa Dart na Udart ni kusimamia na kutoa huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam. Lakini shabaha kuu ya huduma hiyo ni kupunguza msongamano wa daladala katika Jiji hilo, kadhalika kurahisisha usafirishaji wa abiria. Tangu kuanzishwa kwake, huduma za usafiri huo zimegubikwa na malalamiko kutoka kwa abiria na uhaba wa mabasi ndilo lililokuwa lalamiko kubwa zaidi. Msingi wa malalamiko yao, ilikuwa ni kusongamana kwa abiria muda mrefu vituoni bila kupata huduma, kadhalika baadhi ya mabasi yalionekana wakishusha abiria na kuondoka bila kupakia wengine. Oktoba 10, mwaka 2018 aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo aliweka wazi juu ya utendaji usioridhisha ndani ya Dart. "Jambo hili katika ofisi yangu halitutii amani kabisa. Kutokana na hilo, Rais Magufuli ameridhia kutenguliwa kwa Mtendaji Mkuu wa Dart, Ronald Rwakatare na nafasi yake itachukuliwa na Leonard Kapongo," alisema Jafo. Hata hivyo, dakika 10 baadaye Jafo alitangaza mabadiliko katika uamuzi huo, akisema Rwakatare ataendelea na wadhifa wake lakini ajitathmini. Hata, Mohammed Mchengerwa naye katika uongozi wake ndani ya Tamisemi, ameonyesha kusikia malalamiko dhidi ya mradi huo. Katika maelekezo yake Oktoba 25, mwaka jana, alisema: "Sitaki nisikie kuna mabasi yametelekezwa, yarekebishwe mabasi yote yaingie kutoa huduma. “Ndoto za Rais watanzania wawe na furaha, watumiaji mwendo kasi wawe na furaha wasibugudhiwe. “Msimamie mtoa huduma UDART kelele zimekua nyingi hatutaki watu wababaishaji, hawafuati ratiba na kusababisha mrundikano vituoni Mwendokasi iwe chini ya nusu saa," alisema. Uongozi mpya utakuwa suluhu? Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (Darcoboa), Shifwaya Lema alisema licha ya mabadiliko ya viongozi hao, kuna uwezekano utenguzi ukaendelea kushuhudiwa. Alieleza hilo litatokea iwapo wateule wapya katika taasisi hizo, hawatajifunza kutoka kwenye makosa ya watangulizi wao. Kwa mtazamo wa Lema, kinachosababisha mdororo wa huduma katika usafiri huo ni mzigo mkubwa ambao Dart na Udart zimejitwisha. Mzigo huo unatokana na kile alichoeleza, taasisi hizo zimekiuka utaratibu kwa kuanzisha huduma katika maeneo mengine, ilhali yake zinayopaswa kuyahudumia hazijakidhi haja. "Shida wanakiuka utaratibu, walipaswa kutoa huduma Kimara, Morocco, Gerezani, Kivukoni lakini wameanza kwenda Mbezi hatimaye Kibaha ilhali bado kwenye maeneo hayo hawajakidhi," alisema. Kufanya hivyo, alisema ni sawa na kujitwisha mzigo usioweza kuubeba na kwamba hapo ndipo shida inapoanzia. Alieleza huduma za mabasi hayo kutokana na uhalisia wa miundombinu na uwezo wa Taasisi hizo, zilipaswa kuishia kwenye maeneo waliyopaswa kabla ya kuamua kwenda kwingineko. "Naamini tutaendelea kuona wakitenguliwa kama hawatajifunza kutoka kwa wale waliotangulia. Mabasi yenyewe mengi yameharibika unapoongeza eneo la kuhudumia hutaweza," alisisitiza. Hata hivyo, alieleza hakukuwa na haja ya kuongeza maeneo hayo ilhali kuna Daladala za kutosha kuendelea kusogeza abiria hadi vilipo vituo vya Mwendokasi. Mtazamo kama huo, alikuwa nao Mwenyekiti wa Madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMADA), Majura Kafumu aliyesema mabadilimo ya uongozi hayatakuwa chochote kama wateuliwa hawatabadili maono. Hadi unafikiwa uamuzi wa kutenguliwa, alisema maana yake Mkuu wa nchi hakuridhishwa na utendaji. Lakini, alieleza Dart na Udart zimeshindwa kukidhi huduma za usafirishaji katika ngazi zote. "Wamefeli kwanza wakati wanajenga awamu ya kwanza, wanatengeneza boksi ambalo gari ya mbele ikiharibika za nyuma zinashindwa kupita. Angalau hilo wamerekebisha. "Katika uteuzi huu tuwaombee wawe na maono mbadala yatakayosaidia usafiri wa mwendokasi ufanye kazi katika ufanisi," alisema. Alisema kwa sasa mradi huo unahodhi barabara za mjini na Daladala zimeminywa kuingia huko. "Unahodhi vipi maeneo ilhali haukidhi huduma, hawa wanashida sana," alisema. Ili kupata suluhu, alisema kampuni hizo zinapaswa kushirikisha wadau kwenye maamuzi yoyote, badala ya kufanya kazi kama watawala. "Lazima wawashirikishe walaji. Lakini kama tunataka kupata suluhu ya msongamano wa magari ni kupanua barabara, tuache mfumo wa njia mbili zianzie nne," alisema.
Kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kimefuta matumaini ya wananchi katika kiji
Kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kimefuta matumaini ya wananchi katika kijiji cha Binga wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani kupata Shule ya Sekondari na Hospitali. Kufutika kwa matumaini hayo, kunatokana na kile walichoeleza, Hayati Mwinyi enzi za uhai wake aliwaahidi kuwajengea shule hiyo ili kuwaepusha wanafunzi kutembea umbali mrefu kupata huduma ya elimu. Kwa sasa, wanafunzi wa Sekondari waliopo katika Kijiji hicho wanalazimika kusafiri kwa masaa mawili hadi katika kijiji cha Dondo ilipo shule ya sekondari. Kwa upande wa huduma za afya, wamesema wanalazimika kwenda katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga takriban masaa matatu ili kupata huduma zikiwemo za kujifungua. Hofu ya kufutika kwa matumaini yao, inatokana na kile walichoeleza, hawaoni kama watoto wa Hayati Mwinyi watatimiza ahadi za baba yao, kwani hata hawaonekani wakitembelea Kijiji hicho. Wakizungumza na Mwananchi jana kwa nyakati tofauti, walisema matumaini yao yalibebwa na ukweli wa ahadi za Hayati Mwinyi. Maulid Omary ni mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, alisema wanachosubiri ni kuona iwapo watoto wa kiongozi huyo watatekeleza ahadi za baba yao au laa. "Alijenga madrasa kwa ajili ya watoto kusoma, msikiti, kisima kirefu cha maji na nyumba ya kukaa Sheikh. Tulikuwa na matumaini makubwa kuhusu shule na Hospitali," alisema. Mzee Hamza Bazoka alisema huduma hizo ndiyo changamoto kubwa kwa wakazi wa eneo hilo na Hayati Mwinyi aliliona hilo. "Mimi nimepoteza tumaini kwa kuwa ameshafariki. Sioni kama wanawe watakuja kuendeleza maana hata kuja hatuwaoni wakija," alisema. Ndugu yake Mariam Abdallah ni mkwe wa Hayati Mwinyi, alisema nyumbani kwake ndiko alikokuwa akifikia kiongozi huyo kila alipokwenda katika Kijiji hicho. "Alikuwa anafikia nyumbani kwa sababu pale ni kwa mwanawe yaani Baba yake mume wangu na Baba yake Hayati Mwinyi walizaliwa na baba na mama mmoja. Alifikia pale kila alipokuwa," alisema. Aliwaaga Kabla ya kifo chake, Mariam alisema Hayati Mwinyi alifika kijijini hapo miezi minne iliyopita na aliwaaga kwa kuwaambia anakwenda kupata matibabu nje ya nchi. "Alitwambia kwaherini nakwenda kupata matibabu nje ya nchi, Mungu akipenda nitarudi," alisema Mariam. Mbali na kuwaaga kwa kauli hiyo, mkwewe huyo alisema Hayati Mwinyi alimuasa mwanawe Maulid Magandi kwamba ahakikishe anasimamia mali na wafanyakazi wote. "Alimwambia mimi naondoka naomba uwasimamie hawa wanangu (wafanyakazi), hakikisha wanaendelea na kazi na wanakuwa na amani. Alimwambia aangalie na mashamba pia," alisema. Wosia Kwa mujibu wa Mariam, siku walipoagwa na Hayati Mwinyi aliwaambia wahakikishe wanaishi kwa amani na kumpenda kila mmoja. "Alitwambia yeye hakugombana na watu nasi tusigombane na yeyote tuishi kwa amani na watu," alieleza. Mfanyakazi wake Mmoja wa wafanyakazi wake ilipo nyumba yake, Gerard Boaz alisema kila alipofika kijijini hapo, hakuacha kutembelea maeneo matatu. Maeneo hayo ni yalipo makaburi ya Bibi na babu yake, shambani kwake na yalipokuwa makazi ya Baba yake. Kati ya mashamba aliyokuwa anatembea, Boaz alisema zipo ekari takriban 30 za korosho zilizopo eneo la Vikalakala pembezoni mwa Kijiji hicho. "Kila akija alitembelea maeneo hayo akawa anatuuliza maendeleo ya mashamba yake mawili," alisema. Atamkumbuka kwa haya Boaz aliyeanza kazi kwa Hayati Mwinyi Julai mwaka 2022, alisema hatasahau pale alipokuwa akipewa fedha nje ya mshahara kila Hayati Mwinyi alipofika nyumbani hapo. "Alikuwa akinipa fedha ananiambia nikanunulie sabuni, hiyo ni nje ya mshahara wangu. Alikuwa mkarimu sana," alisema Boaz. Jambo lingine analolikumbuka ni mazungumzo yake ya mara kwa mara na Hayati Mwinyi kila alipofika kijijini hapo. "Alikuwa ananiuliza kuhusu maendeleo ya shamba na alikuwa ananishauri niwe na panda mbogamboga ili niuze kupata hela za ziada kwa ajili ya matumizi yangu. "Alikuwa ananiambia mshahara anaonilipa haunitoshi na hata anaolipwa yeye haumtoshi inabidi tutafute vyanzo zaidi. Kwa hiyo akawa ananishauri nipande mbogamboga ili nipate hela nje ya mshahara anaonilipa," alisema Boaz. Ilivyokuwa safari hadi kijijini kwao Ni safari ya takriban saa 1:50 kwa usafiri wa umma kutoka Mbagala Rangitatu, Dar es Salaam hadi Kijiji cha Binga, Tarafa ya Kisiju mkoani Pwani, kunachotajwa kuwa ndiyo asili ya Hayati Mwinyi. Gazeti la Mwananchi liliifunga safari hiyo kwa daladala na Mwandishi wa habari hii anasimulia ilivyokuwa. Saa 6:48 nafika Kituo cha magari ya Mkuranga kuanza safari ya kuelekea Kisiju. Bahati njema nikipata basi la moja kwa moja kutoka kituoni hapo hadi Kisiju. Nikiwa na dhana kuwa Kisiju ndilo eneo ninalopaswa kushuka, njiani baada ya udadisi kwa abiria wenzangu nilielekezwa nyumbani kwa Hayati Mwinyi ni kabla ya mwisho wa gari. Niliambiwa nyumbani kwao ni Katika Kijiji cha Binga, kilichopo dakika 30 kabla ya kufika Kisiju zinakoishia gari. Safari hiyo ya usafiri wa umma ilinakshiwa na burudani ya muziki, tungo mbalimbali za msanii 20 Percent ambaye pia asili yake ni Pwani. Kulikuwepo na stori za hapa na pale kutoka kwa baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye usafiri huo, kuhusu Rais huyo mstaafu. "Sasa hivi washauri wakuu wa Serikali wamepungua amebaki Kikwete (Jakaya, Rais wa awamu ya nne)," alisikika abiria mmoja. Wengine walisikika wakizungumzia umri wake wa miaka 98 aliofariki akiwa nao, wakidai amebahatika kuishi muda mrefu. Barabara ya lami imeishia katika eneo la daraja la Mbezi ambalo mwendo wake hadi Binga ni takriban dakika 45. Saa 8:38 nilifika kijijini hapo nakuonyeshwa nyumbani kwao, lakini nilianzia kijiweni kupiga Stori na wazee niliowakuta. Kila mmoja alieleza lake kuhusu anavyomfahamu Hayati Mwinyi, lakini wengine walinong'ona kwamba safari zake kwenda kijijini hapo alizifanya zaidi baada ya kustaafu uongozi. Kwa bahati mbaya nilikosa Mzee aliyewahi kucheza naye utotoni, lakini mmoja alidai Hayati Mwinyi aliondoka kijijini hapo akiwa kijana mdogo kwa ajili ya kwenda kusoma madrasa Zanzibar na huko ndiko alikopata elimu ya sekula. Nilisindikizwa na mmoja wa wazee hao Hadi nyumbani kwa Mwinyi na hakukuwa na watu wengi zaidi ya mfanyakazi, Boaz. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale na mfanyakazi huyo, niliomba anitembeze huku na kule hadi yalipo makaburi ya wazazi wa Hayati Mwinyi. Niseme ukweli tu, hii ndiyo iliyokuwa safari ngumu maana ni mwendo wa vichaka kwa vichaka hadi makaburini. Usingeamini kama eneo hilo ndiko yaliko makaburi ya Bibi na babu wa Rais Mstaafu, yamezingirwa na vichaka na mapori, kiasi cha kushindwa kugundua kaka eneo hilo lina makaburi. Kwa mujibu wa mfanyakazi niliyeanbatana naye, mwisho wa makaburi hayo kusafishwa ni miezi minne iliyopita, Hayati Mwinyi alipokwenda kijijini hapo.
Bohari ya Dawa (Msd), imesema kuna haja ya kuwa na akiba ya mifuko ya kuhifadhia damu itakayodumu kw
Bohari ya Dawa (Msd), imesema kuna haja ya kuwa na akiba ya mifuko ya kuhifadhia damu itakayodumu kwa kipindi cha kuanzia miezi mitano hadi tisa, ili kuepuka kuadimika kwake. Kauli hiyo ya MSD inakuja katika kipindi ambacho, akiba ya mifuko hiyo kwa sasa ni miezi mitatu, jambo linalopaswa kuongezeka kutokana na ongezeko la mahitaji ya damu linalosababishwa na ajali. Katika kufanikisha hilo, MSD imesema kuna haja ya kutafutwa mbinu thabiti itakayowezesha kuwa na akiba kubwa ya mifuko na hivyo kuwa na uhakika wa upatikanaji wa damu salama kwa wananchi. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai alipohutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalamu wa Maabara. Alisema damu ni suala linaloamua maisha ya watu na mahitaji yake ni muhimu hasa kwa wajawazito, hivyo kuna haja ya kuhakikisha inapatikana kwa uhakika. Katika kufanikisha hilo, alisema kuna haja ya kuwa na akiba ya mifuko ya kuhifadhia damu itakayodumu kwa miezi mitano hadi tisa, badala ya mitatu ya sasa. “Serikali imejitahidi katika kuhakikisha kunakuwa na mifuko ya kuhifadhia damu. Kwa sasa akiba inaweza kudumu kwa miezi mitatu, lakini kunahitajika collective approach (mbinu za pamoja) kukabiliana na hilo,” alisema. Alieleza kwa kutumia mbinu hizo za pamoja taifa litakuwa na uwezo wa akiba ya mifuko kwa zaidi ya miezi mitano na kuwezesha uhakika wa upatikanaji wa damu kwa wananchi. “Kuna eneo bado tunaweza tukafanya vizuri zaidi ili taifa liwe na mifuko isiyopungua miezi mitano hadi tisa,” alisema. Alisema akiba ya mifuko iliyopo sasa ni miezi mitatu na kwamba kuna haja ya kutafuta mbinu za kuongeza akiba hiyo. Wakati Tukai anakuja na hoja hiyo, Aprili mwaka jana, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliwakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya kuzalisha mifuko hiyo. Hatua yake hiyo ilitokana na kile alichoeleza, itapunguza gharama za uagizaji wa mifuko hiyo nje ya nchi. Akizungumzia hilo, Ofisa Uhamasishaji Damu salama wa Mpango wa Taifa wa Damua Salama, Kizito Tamba alisema kwa sasa kuna akiba kubwa ya mifuko hiyo, tangu Serikali ilipobadili utaratibu wa uagizaji. Alieleza zamani jukumu la uagizaji wa mifuko hiyo lilikuwa chini ya Vituo vya Afya, lakini sasa ni Serikali yenyewe ndiyo inayoagiza na vituo vya afya vinaeleza uhitaji wao na kupelekewa. “Kwa sasa hiyo changamoto hakuna tena, ilikuwepo wakati utaratibu wa uagizaji wa mifuko hiyo ulipokuwa chini ya vituo vya afya vyenyewe,” alisema. Katika hatua nyingine, Tukai alisema kikao hicho kinalenbga tathmini ya utendaji katika maabara ili kuhakikisha kunakuwa na ubora wa huduma. “Tunachotaka ni kuwa na uratibu wa pamoja na uwazi nje ya kufanya hivyo kuna watu hawataelewa kama bidhaa fulani ipo eneo fulani,” alisema. Lakini hatua hiyo, alisema itawezesha kupunguza kuisha muda wa baadhi ya vifaa kabla ya kutumika, ilhali kuna taasisi zinavihitaji. “Tunataka kupunguza ile hali ya vitendanishi kuisha muda wake kabla ya kutumika ilhali kuna maeneo vilikuwa vinahitajika ila tu hawakuwa wanajua,” alisema.
Miaka mitatu si safari nyepesi, aghalabu inahusisha milima na mabonde, katika hiyo kuna hesabu za ma
Miaka mitatu si safari nyepesi, aghalabu inahusisha milima na mabonde, katika hiyo kuna hesabu za mafanikio na maanguko lukuki, ndivyo ilivyo hata katika utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya muda huo. Rais Samia aliapishwa kuwa Rais, Machi 19, mwaka 2021 siku mbili baada ya kutangaza kifo cha aliyekuwa na wadhifa huo, John Magufuli. Hatua ya Rais Samia kuapishwa kushika wadhifa huo, ilitokana na matakwa ya kikatiba yanayoelekeza, iwapo Rais aliyepo madarakani atafariki, Makamu wake ataapishwa kushika nafasi hiyo. Tangu mkuu huyo wa nchi aapishwe, amedumu madarakani kwa miaka mitatu, huku uongozi wake akihusishwa na mafanikio na maanguko katika siasa, demokrasia na utawala bora. Mkuu huyo wa nchi ameingia madarakani akijipambanua kuiongoza Serikali yake kwa falsafa ya 4R, kama msingi wa kile alichokiita ustawi wa demokrasia na maelewano miongoni mwa vyama vya siasa. Kwa maneno ya Kiswahili, falsafa hiyo inamaanisha maridhiano, ustahamilivu, mageuzi na kujenga upya “Tutajitahidi kuijenga Tanzania yenye haki, demokrasia na usawa na mafanikio na ndiyo maana katika kipindi hiki tulikuja na ‘idea’ ya 4R. Vyama vya siasa tunazungumza, tunaelewana,” alisema Rais Samia mwaka 2021 alipoitambulisha falsafa hiyo kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, wanazuoni mbalimbali, wanasema ni vigumu kutenganisha mafanikio na changamoto za utendaji wa Rais Samia ndani ya miaka mitatu, kwa kuyatenganisha na falsafa hiyo. Alichofanikiwa kwenye 4R Kulingana na wanazuoni hao, mafanikio ya 4R yanatafsiriwa kwa mabadiliko ya mfumo wa uongozi tangu alipoingia madarakani, kutoka ule wa mtangulizi wake, John Magufuli. Mbobezi wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Revocatus Kabobe anasema Rais Samia ameingia madarakani katika kipindi ambacho nchi haikuwa na mshikamano wa kitaifa. “Ni kipindi ambacho siasa za upinzani zilionekana kama uadui na kuondoa dhana nzima ya lengo kuu la kurejesha siasa za vyama vingi mwaka 1992,” anasema. Katikati ya mazingira hayo, Dk Kabobe anasema ndipo mkuu huyo wa nchi alipoitambulisha 4R na kuazimia kuwepo maridhiano kati ya CCM na vyama vya upinzani. “Tumeona nia yake ya dhati kwenye hili kupitia mabaraza ya vyama vya siasa na kikubwa zaidi mazungumzo ya takribani mwaka mmoja kati ya CHADEMA na CCM,” anasema. Ingawa mazungumzo hayo hayakufikia tamati, mwanazuoni huyo, anasema kilichoyakwamisha ni hali ya kutoaminiana iliyokuwepo kati ya pande zote zilizokuwa zinazungumza. “Unapofanya siasa za maridhiano lazima itafika wakati upande mmoja ukubali kupoteza hiki au kile kwa maslahi ya taifa na watu wake. “Tumesikia mara kadhaa viongozi ya Chadema wakitoa hadharani kauli za kuonesha kushindana na CCM kwenye maridhiano,” anasema. Pamoja na mkwamo huo, anasema bado matunda ya maridhiano yameendelea kuonekana, yakiwemo kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara na hata kupatikana kwa ruzuku za vyama zilizokuwa hazijatolewa. Ni vigumu kuzitofautisha sana siasa katika uongozi wa Rais Samia na zile zilizokuwepo wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete katika ustahimilivu, kama inavyofafanuliwa na Dk Kabobe. "Huyu mama (Rais Samia) amekuwa mstahimilivu sana yeye binafsi na hata waandamizi wake. "Najaribu kuwaza maandamao yanayoendelea ya Chadema ingekuwa kipindi cha awamu iliyotangulia (ya Magufuli) ingekuwaje," anasema Dk Kabobe. Anasema hata vyombo vya dola katika maandamano hayo vinaishia kutekeleza wajibu wake wa kisheria, akisisitiza hicho ndicho kinachopaswa kuendelea katika siasa za vyama vingi. "Wengine wanaweza kusema sio ustahimilivu wa rais na Serikali yake kwenye kuruhusu maandamano bali ni sheria. Sipingani nao ila wajaribu pia kuwaza awamu iliyopita sheria kuhusu maandamano ya vyama ilikuwa hii hii ila hayakufanyika. Kwanini? "Kwenye siasa hasa za kiafrika, rais ana nafasi kubwa sana kuamua aina gani ya siasa zifanyike ukizingatia hata Katiba nyingi za kiafrika zinatoa mamlaka makubwa kwa kiongozi mkuu wa nchi," anasema. Mageuzi, kujenga upya bado Kinachowakilisha R ya tatu ndani ya falsafa hiyo ni mageuzi, kwa mujibu wa Dk Kabobe, nia njema imeonekana lakini bado kuna mapungufu. "Kwa maoni yangu, mageuzi yamekuwa mfupa mgumu kidogo, si kwa upande wa Rais na Serikali yake tu bali hata kwa vyama vya upinzani," anasema. Msingi wa mageuzi, anasema ni katiba mpya itakayobeba misingi mipya ya siasa za vyama vingi. Aliijenga hoja hiyo akirejea mwaka 1992 Tanzania ilipoingia katika mfumo wa siasa za vyama vingi lakini Katiba inayoendelea kutumika ni ile iliyoandaliwa katika mfumo wa siasa za chama kimoja. "Natambua juhudi za Rais na Serikali yake katika kufanya mabadiliko ya sheria mbalimbali hasa za uchaguzi na mfumo wa uendesha siasa zetu. "Mchango wa mabadiliko haya kwa mfumo wetu wa siasa na uchaguzi ni mdogo tu, ni sawa na mgonjwa kumpa dawa ya maumivu ya kichwa kumbe tatizo ni malaria," anasema Dk Kabobe. Anasema mabadiliko hayo yanakosa uungwaji mkono wa baadhi ya wadau muhimu hasa vyama vya siasa, asasi za kidini na za kiraia. "Tiba sahihi ya mageuzi ni kuwa na katiba mpya itakayoweka misingi ya haki na demokrasia za vyama vingi. Tume mbalimbali zimeonesha kuwa namna bora zaidi ya kufanya mageuzi ya mfumo wetu wa uchaguzi na uendeshaji wetu wa siasa ni katiba mpya. "Rejea tume ya Nyalali 1992, Warioba 2014 na hata kikosi kazi cha Mukandara," anasema. Kujenga upya nako, Dk Kabobe anasema bado hakufanyikiwa kwa kuwa ni jambo linalohusisha mchakato. "Ni mchakato endelevu wenye changamoto nyingi, ni hatua ya mwisho ila hufanyika kwenye hatua zote tatu zilizotangulia," anasema. Hata hivyo, Dk Kabobe anasema bado kuna changamoto ya kutofautiana na wadau muhimu wa siasa hasa vyama vya siasa na baadhi ya asasi za kiraia na dini. Wakati Serikali inaamini kujenga upya kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali kama zilizopelekwa bungeni, anasema wadau wengine wanaamini katiba mpya kwanza ndio msingi wa mabadiliko. "Nafasi bado tunayo hatujachelewa, ni vema sasa tukae kama taifa tukubaliane njia bora ya kufanikisha 4R za Rais Samia tukiongozwa na tafiti zilizopo mathalan Tume ya Nyalali, Jaji Warioba na kikosi kazi cha Profesa Mukandara," anasema. Mafanikio mengine Julai mwaka jana, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliviandikia vyama vya siasa ikivitaka vitoe mapendekezo ya mabadiliko ya sheria nne, ikiwemo ya uchaguzi, vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. Hatua hiyo ya nia ya mabadiliko ya sheria hizo, inaakisi utashi wa kisiasa wa Rais aliyepo madarakani na hivyo jambo hilo ni moja ya mafanikio ya Rais Samia katika miaka mitatu ya utendaji wake, kama inavyofafanuliwa na mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Conrad Masabo. “Angalau ameruhusu sheria fulani zipitiwe, mambo ambayo watangulizi wake walishindwa kuyafanya, kwa hiyo utashi ni sehemu ya mafanikio katika uongozi wa Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu,” anasema. Hoja nyingine inayoweka msisitizo wa utashi wa kisiasa katika utawala wa Rais Samia ni ruhusa ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, aliyoitoa mwaka jana. Pamoja na ruhusa hiyo, aliomba na kupata baraka za Kamati Kuu ya chama chake cha CCM, kwa ajili ya mabadiliko hayo, hatua ambayo watangulizi wake hawakuifikia. Hata hivyo, Masabo anasema mambo mengi yanayoonekana kama mafanikio katika uongozi wa miaka mitatu ya Rais Samia, yanabebwa na magumu yaliyotokea katika awamu iliyopita. “Tunapotaka kufananisha matendo yake, tusimfananishe na awamu ya tano, tufananishe na awamu ya nne. Kwa sababu awamu ya tano iliharibu mambo mengi,” anasema Masabo. Uhuru wa maandamano Januari 23, mwaka huu Jeshi la Polisi lilitoa kibali cha kuruhusu maandamano ya amani yaliyotangazwa na chama cha upinzani cha Chadema. Hiyo ni mara ya kwanza tangu uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, chama cha upinzani kipate ruhusa ya maandamano, katika miaka mitatu ya Rais Samia hilo limefanyika, hili nalo ni moja ya mafanikio. Kwa mtazamo wa kisomi, Masabo anaitafsiri hatua hiyo kama turufu na mafanikio katika utendaji wa Rais Samia katika miaka yake mitatu. “Walau umefika wakati Polisi wanaweza kutoa kibali, maandamano yanafanyika, hayo ni mafanikio katika uongozi wa Rais Samia, ametusaidia kuona pande zote. Kumbe tukiwa na utawala bora na kuheshimu sheria kuna uwezekano nchi yetu ikawa inayofuata taratibu nzuri,” anasema Masabo. Mtaalamu mwingine wa Sayansi ya Siasa kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST), Profesa Ambrose Kessy anaitafsiri miaka mitatu ya kiongozi huyo kuwa yenye mafanikio zaidi kuliko changamoto. Tafsiri yake inajengwa na msingi wa hoja kwamba, ndani ya miaka mitatu, Rais Samia amerudisha uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa maoni na hata wa kukusanyika. Mwanazuoni huyo ambaye pia ni Mkuu wa LST, Mipango, Fedha na Utawala, anasema hatua ya Rais Samia kuongoza kwa falsafa ya R4 ni moja ya mafanikio hayo, akifafanua imewezesha majadiliano katika siasa na hata uchumi. Miaka mitatu hiyo, anasema inatafsiriwa kuwa ya mafanikio kwa sababu mkuu huyo wa nchi ameonyesha uharaka wa kuchukua hatua dhidi ya mtendaji yeyote aliyelalamikiwa na wananchi. “Ni mtu anayesikia kwa haraka na kutenda na kuna watu amewachukulia hatua baada ya kusikia vilio vya wananchi. Haoni haya kama anaona mtu haufanyi vizuri,” anasema. Profesa Kessy anasema kiongozi huyo alijinasibu kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake na kweli hilo linashuhudiwa, huo ni utawala bora. Ni kiongozi aliyeonyesha ubunifu, anasema wakati wa mkopo wa fedha kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF), alizitumia kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, badala ya kununua dawa kama ilivyofanywa na wengi. Katika utendaji wake ndani ya muda huo, mwanazuoni huyo anasema amekuwa mzuri katika kuifungua Tanzania kwa mataifa mengine duniani. “Ameifungua Serikali na jumuiya ya kimataifa imeijua Tanzania maana ni vigumu Rais kufanya kazi katika mazingira ambayo hushirikiani na wengine,” anasema. Mapungufu Pamoja na mafanikio hayo katika utendaji wa miaka mitatu ya Rais Samia, Masabo anagusia uwepo wa changamoto katika safari hiyo pia hasa kwenye eneo la demokrasia. Lakini mwanazuoni huyo anasema changamoto nyingi za demokrasia, zimeshuhudiwa wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya tano chini ya John Magufuli, huku Rais Samia akiwa msaidizi wake. Katika awamu hiyo, Masabo anaeleza Samia alikuwa Makamu wa Rais, hivyo inakuwa vigumu kumtenganisha na changamoto za kidemokrasia zilizokuwa zinaendelea. Lakini yote yaliyotokea katika awamu hiyo, yalisababishwa na kile kilichoelezwa na Masabo kuwa, kukosekana misingi thabiti ya utawala wa sheria. Jambo hilo, anasema linasababisha mabadiliko yoyote ya mifumo ya utendaji ndani wa Serikali yategemee utashi wa kiongozi aliyepo madarakani na si ulazima wa kisheria. “Demokrasia haijajikita katika misingi thabiti ya utawala wa sheria ndiyo maana mabadiliko yake yanategemea kiongozi na sio sheria,” anaeleza. Jambo hilo ni moja ya changamoto zinazoikabili demokrasia nchini na katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia bado hajafanikiwa kulitatua. Kinachojenga hoja ya kutotatuliwa kwake ni kile kilichoelezwa na Masabo kuwa, katika kipindi chote cha mkuu huyo wa nchi madarakani, hakukamilisha mabadiliko yoyote ya kisheria yanayosimamia utawala wa sheria. “Katika utawala wa Rais Samia, hakuna sheria mpya iliyobadilishwa kwa ajili ya kusimamia na kuhakikisha kunakuwa na utawala wa sheria kwenye hili hajafanikiwa,” anasema. Uimara wa bunge Kulingana na Masabo, mfumo wa utawala na sheria za Tanzania haujamtenganisha Rais wa nchi na muhimili wa bunge, hivyo Rais Samia ni sehemu ya muhimili huo. Lakini, mwanazuoni huyo anasema utendaji wa bunge umejikita katika utendaji unaoegemea kwenye maslahi ya chama tawala badala ya wananchi. Kwa maneno mengine, Masabo anasisitiza pamoja na miaka mitatu ya utawala wake madarakani, Rais Samia hajafanikiwa kuimarisha utendaji wa bunge. “Changamoto kubwa ni kwamba Bunge linafanya kazi kwa maslahi ya chama na sio wananchi,” anasema. Kwa sababu ya mazingira hayo, Masabo anasema hata utashi wa kisiasa anaouonyesha mkuu huyo wa nchi, inafika wakati unashindwa kupata usimamizi wa maamuzi kwa kuwa bunge haliko imara. Kwa upande wa Profesa Kessy, bado zipo changamoto za kiuwajibikaji katika utawala wa Rais Samia hasa zinasababishwa na wasaidizi wake. Anasema bado kumekuwepo na malalamiko dhidi ya utendaji wa viongozi mbalimbali na wakati mwingine analazimika kutatua mwenyewe baadhi ya changamoto ilhali kuna kiongozi wa kisekta. “Ni mahali panapohitaji ufuatiliaji wa karibu, ingawa sio yeye lakini wasaidizi wake wanapaswa kuelewa falsafa ya kazi iendelee, hili bado hajafanikiwa linahitaji hatua zaidi,” anasema. Lingine alilolihesabu kama changamoto ni kuendelea kwa malalamiko ya wananchi juu ya kukosa baadhi ya huduma muhimu, kadhalika vitendo vya rushwa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuja na Azimio la Mtwara, ikiwa ni hatua ba
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuja na Azimio la Mtwara, ikiwa ni hatua baada ya kumalizika kwa maandamano yaliyofanyika katika Majiji manne nchini. Kulingana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, msingi wa azimio hilo ni kutoa jawabu la nini kitafuata chenye sura ya mapambano baada ya kumalizika kwa maandamano katika majiji hayo. Kauli hiyo ya Mbowe inakuja baada ya kuhitimishwa kwa maandamano katika Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha yaliyohusisha matembezi ya jumla ya Kilomita 169. Chama hicho kiliamua kuingia barabarani kuandamana baada ya kikao cha Kamati Kuu yake kuazimia kufanywa kwa maandamano hayo katika maeneo hayo. Licha ya kutamatika kwa maandamano katika majiji hayo, Mbowe alisisitiza maandamano ndiyo utakaokuwa utaratibu mpya wa chama hicho kuwasilisha hoja zake dhidi ya Serikali. Mbowe alitoa kauli hiyo jijini Arusha jana, alipohutubia wananchi baada ya kuhitimisha matembezi ya maandamano yaliyoanzia maeneo mbalimbali mkoani humo. Baada ya kuhitimisha maandamano katika Mkoa huo, mwanasiasa huyo alisema kesho (leo) wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi wa juu wa chama hicho wanatarajia kwenda Mtwara. Safari hiyo, alisema itafuatiwa na vikao vitakavyoanza wiki ijayo na kufanyika kwa wiki nzima ndani ya Mkoa huo na kwamba huko ndiko litakapotengenezwa Azimio la Mtwara. “Tunapomaliza mkutano wetu wa leo (jana), kesho (leo) tunaondoka wote tunakutana Mtwara, wiki ijayo tutakutana Mtwara kwa wiki nzima. Kamati Kuu ya chama chetu na watendaji wakuu wa chama chetu, tunakwenda kutengeneza Azimio la Mtwara,” alisema. Azimio hilo, alisema litatoa jawabu la nini kitafuata chenye sura ya mapambano baada ya kumaliza mikutano na maandamano katika Majiji manne nchini. “Tukimaliza Mtwara tutalitangazia taifa hatua zinazofuata,” alieleza Mbowe. Hata hivyo, alisema kilichochagiza chama hicho kuingia barabarani kuandamana ni kile walichokiona kwamba CCM haijaonyesha nia ya mabadiliko ya sheria zozote. Alieleza hadi sasa wametembea jumla ya kilomita 169 katika maandamano yaliyofanyika Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha. Ndiyo utaratibu wetu Alieleza kuanzia sasa maandamano ndiyo utakaokuwa utamaduni wa maisha ya chama hicho hadi pale kitakapoona yanapatikana mabadiliko ya kweli nchini. “Tunapoandamana kwa kilomita 20 ni kielelezo tosha cha ujenzi wa hisia. Huko nyuma CCM walisema Watanzania hawapendi kuandamana ni uongo,” alisema. Kwa mujibu wa Mbowe, maandamano yanalenga kupeleka ujumbe kwa watawala kwamba kinachozungumzwa na viongozi wa vyama vya upinzania ni kwa niaba ya watanzania wengi. Alisema maandamano hayo yanalenga kuwafanya watawala watambue Chadema kinawakilisha wananchi wengi wenye maumivu na wasio na furaha katika nchi yao. “Tunaandamana ili kuonyesha kwamba tuko tayari kuumia ili kurekebisha,” alisema. Katika hilo, alisema kuna haja ya kuunganisha Watanzania wote wa ndani ya chama hicho na hata wasio wanachama ili kuipata kesho bora ya Tanzania. “Tutaendelea kuandamana kwa sababu wenzetu waliopo ndani ya Serikali hawaujui uchungu wa maisha ya Watanzania,” alisema. Alisema vikao vingi vimefanyika vya maridhiano kati ya Chadema na CCM na Serikali kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya, lakini havijaleta mafanikio. “Wenzetu hawa hawapo tayari kutusikiliza, maandamano yataendelea wenzetu hawa watatuelewa,” alisema. Hata hivyo, Mbowe alieleza kushangazwa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye mara kadhaa anaonekana akiambatana na Rais Samia katika safari mbalimbali, jambo linaloongeza gharama za utendaji serikali. “Nimesema tumemaliza raundi hii ya maandamano, najua na sitaki kusema kabla hatujazungumza, lakini nimesema utamaduni huo tutauendeleza maeneo mbalimbali ili tufike mahali tuone Serikali inachukua hatua,” alisema. Aliwataka Watanzania kuchoka kulalamika na badala yake waanze siasa za vitendo na ili kufanikisha hilo, lazima kujenga miundombinu ya vyama vya siasa vyenye nguvu vitakavyoweza kuwa na msukumo wa hilo. Onyo kwa Polisi Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Tundu Lissu alitumia hotuba yake kulionya Jeshi la Polisi kuacha kuwapangia waandamanaji watumie barabara moja ya magari, akisema hilo linaweza kusababisha maafa. “Dunia nzima ukiitisha maandamano, mtakubaliana njia na mapolisi kazi ya kwanza wanayofanya ni kusafisha njia ni kuondoa magari barabarani ili wandamanaji wapiti. “Watu huwa hawaandamani kwa sababu wamefurahi bali wanaandamana kwa sababu wamechoka,” alieleza. Alieleza haiwezekani kuchanganya waandamanaji na magari kwani wakitokea watu wenye hasira watasababisha maafa. Alipendekeza taratibu za polisi katika maandamano ziwe kuondoa magari barabarani ili watu waandamane bila kuharibu cha mtu. “Kwenye nchi nyingine, polisi wanatoa ushauri kwa wafanyabiashara kwamba waandamanaji watapita hapa wanaweza wakafanya fujo,” alieleza. Katika maelezo yake hayo, alihusianisha kuwepo kwa Katiba mbaya na ugumu wa maisha, akisema biashara zinapandishwa bei kuholela kwa sababu ya changamoto za kisheria. “Bei zikipandishwa kuna wanaoneemeka na kuna wanaoangamia. Sio kila mtu anaumia na bei zinapopanda,” alisema. Alipopata fursa ya kuhutubia wananchi, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema alidokeza vikwazo vilivyowekwa hadi kufanikishwa kwa maandamano hayo. Miongoni mwa vikwazo hivyo, alisema ni bodaboda kulipwa ili wasishiriki maandamano, lakini walishiriki kwa kuwa wana mapenzi na Chadema. Kingine, alisema ni ratiba ya kuaga miili ya 25 waliopoteza maisha kwa ajali ya magari matatu mkoani Arusha, akisema ilipangwa kudhoofisha maandamano ya chama hicho. “Walikuwa na nia ya kuzuia watu wasije kwenye maandamano, wameshindwa,” alisema. Maandamano yalivyokuwa Kama ilivyokuwa katika maandamano ya awali, Viongozi wakuu wa kitaifa wa chama hicho waligawanyika katika makundi matatu, Makamu mwenyekiti bara, Tundu Lissu aliongoza kundi lake, Mwenyekiti Freeman Mbowe alikuwa na lake na Godbles Lema alikuwa na la kwake. Katika msafara ulioongozwa na Lissu walikuwepo pia wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, John Heche, Peter Msigwa na Spika wa Bunge la Wananchi la chama hicho, Suzan Lyimo. Msafara huo ulishereheshwa na wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Blad Key ‘Vinapanda Bei’ uliokuwa ukisikika ukipigwa, huku waandamanaji wakiendelea na safari. Kama ilivyokuwa katika Mikoa yote ambayo maandamano yameshafanyika (Dar es Salaam na Mbeya), Polisi katika Mkoa wa Arusha walionekana mbele na nyuma ya waandamanaji kulinda usalama. Bendera za Chadema na mabango yenye jumbe mbalimbali yalikuwa sehemu ya maandamano hayo. Miongoni mwa jumbe hizo ni “Serikali ipunguze gharama za maisha”, lingine lilisomeka, “Samia ruhusu huduma za kijamii Ngorongoro kama kuhama ni hiari.” Msafara ulioongozwa na Mbowe, wenyewe ulisindikizwa na burudani ya matarumbeta yaliyokuwa yakipiga nyimbo mbalimbali ikiwemo ‘Tutatoana roho’ ulioimbwa na Ottu Jaz Band. Kwa umati uliojitokeza ni kama watu hawakwenda makazini, ilhali maandamano hayo yamefanyika katika siku za kazi. Mvua kubwa iliyonyesha haikuwa kikwazo cha maandamano hayo, kwani waandamanaji waliendelea na matembezi.
Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo (UKEF), imewatangazia fursa wafanyabiashara na waw
Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo (UKEF), imewatangazia fursa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania ya kuwadhamini katika taasisi za kifedha za kimataifa pale watakapohitaji mikopo. Udhamini huo ni kwa wafanyabiashara wanaotarajia kukopa katika taasisi za fedha, lakini wamekosa dhamana zinazowawezesha kukopesheka. Hayo yalielezwa jana kupitia mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu fursa ya kupata udhamini wa taasisi hiyo kwa sekta binafsi na umma ya Tanzania, ulioratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Naibu Mkuu wa taasisi hiyo, Emma Thomas alisema katika miradi na biashara za usafi nchini, taasisi inaweza kutoa udhamini hadi wa pauni 2 bilioni (zaidi ya Sh6.4 trilioni). “Asilimia isiyopungua 20 ya thamani tunayoisaidia lazima itumike kwenye bidhaa za Uingereza. Bidhaa za Uingereza ni gharama za kununua bidhaa, huduma, mali zisizojulikana kutoka kwa wauzaji wa Uingereza na wakandarasi wa Uingereza," alisema. Kwa mujibu wa Emma, taasisi hiyo inatoa miaka 15 ya muda wa malipo kwa miradi mingi na miaka 22 kwa miradi ya Nishati ya Hewa Safi, ikiwemo maji, reli na umeme. Katika mwaka wa 2022-2023, alisema shirika hilo la mikopo limetoa pauni bilioni 6.5 kwa mkataba wa mauzo nje ulimwenguni, likisaidia moja kwa moja makampuni 532. Mkuu wa nchi wa UKEF kwa Afrika Mashariki, Isaac Kahara alisema mojawapo ya mambo muhimu yanayopewa uzito ni miradi maalum inayochangia bidhaa za Uingereza. "UKEF inaweza kutathmini miradi mbalimbali ya ukubwa tofauti katika sekta zote - sekta zote zinaweza kupata ufadhili isipokuwa sekta ya nishati ya mafuta, tunachunguza kujua kama kuna hatari za kijamii na haki za binadamu na athari za miradi kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa. “Piua tunaangalia pamoja na Mipango ya Ikweta na Viwango vya Utendaji vya Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) - haya yanapaswa kuzingatiwa katika hatua za awali za maendeleo ya miradi," alisema. Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki alisema Tanzania na Uingereza zina uwezekano mkubwa zaidi wa kujenga ushirikiano utakaoleta manufaa kwa nchi zote kwa miaka mingi ijayo. "Ninaamini kwa dhati kuwa biashara na uwekezaji kati ya Uingereza na Tanzania zitaongezeka kwa kiasi kikubwa ikiwa wafanyabiashara wa sekta binafsi na umma wataelewa fursa zilizopo chini ya UKEF na kuzitumia," alisema. Kwa upande wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alisema dhamana hiyo ni fursa muhimu kwa taasisi za Tanzania. Hata hivyo, alieleza taasisi hiyo itawezesha kukamilishwa kwa fedha iliyopungua katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano wa Tanzania. “Jambo muhimu ni kwamba Tanzania tuna uhusiano wa muda mrefu katika maeneo mbalimbali na Uingereza na nchi hiyo inabaki kuwa moja ya wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi,” alisema. Kwa mujibu wa Profesa Mkumbo, Uingereza ni taifa la pili kwa uwekezaji nchini na lina miradi 1,000 yenye thamani ya takriban Paundi bilioni nne (zaidi ya Sh12.9 trilioni).
Kama kuna changamoto kubwa na pengine wenye mamlaka ya kuchukua hatua hawana taarifa nayo, basi ni h
Kama kuna changamoto kubwa na pengine wenye mamlaka ya kuchukua hatua hawana taarifa nayo, basi ni hii ya huduma katika Vituo vya Afya na Zahanati nyakati za usiku. Naeleza hili kwa sababu nimeshuhudia, wala sikuhadithiwa. Katika baadhi ya zahanati na vituo vya afya, huduma zinatolewa mchana pekee, nyakati za usiku hasa kuanzia saa 4 na kuendelea zinapatikana kwa shida. Napozungumzia vituo vya afya na zahanati, sina maana vyote vilivyopo Tanzania, lakini vingi nyakati za usiku vinatoa huduma kwa kusuasua. Kitakachoamua kupata huduma bora na kwa haraka nyakati hizo ni ukaribu wako na muuguzi au fedha ulizonazo, kinyume na hivyo utasugua sana benchi. Nimewahi kwenda katika moja ya vituo vya afya katika Wilaya ya Kinondoni, kuanzia muda niliofika (saa 4:23) hadi nahudumiwa yalishapita masaa mawili. Picha lilikuwa hivi, mapokezi sikukuta mtu, nikamrudia mlinzi kumtaka akaniitie wahudumu. Ilichukua kama nusu saa hivi hadi mlinzi anarudisha majibu kwamba hakuwaona, labda watakuwa wamelala. Nilikwenda kwenye vyumba vilivyoandikwa daktari sikukuta mtu na hakukuwa na dalili ya uwepo wa mhudumu, maana hata taa zilizimwa. Nilitumia dakika kadhaa kugonga kila eneo ambalo ukienda mchana unapata huduma, juhudi hazikufua dafu. Mwisho wa picha nilirudi kwa mlinzi kumuomba anielekeze eneo wanakolala, nilielekezwa napo niligonga vya kutosha ndiyo baadaye mlango ulifunguliwa kwa kasi ya ajabu. Sijui ni hasira? Alikuja mwanadada baada ya kumuuliza, kwa sauti ya usingizi mzito alinijibu anakuja, niende mapokezi. Sikumbuki nilitumia dakika ngapi kumsubiri mapokezi, lakini nikifananisha na ratiba zangu za kazi za nyumbani, muda niliomsubiri ungetosha kuivisha ugali na mayai kwa jiko la gesi. Alifika akiwa mchovu, kama unavyojua mtu aliyetoka usingizini. Kila aliponiuliza jambo niliitika mara mbili mbili maana sikusikia kwa urahisi kutokana na sauti ya chini aliyokuwa anaongea. Hadi naandikishwa, hakika nilishakuwa mwenyeji wa eneo lile, maana karibu kila kona nilishakwenda kujaribu kuwasaka wahudumu. Pamoja na yote hayo, bado sikuonewa huruma ilinibidi nisubiri tena kwa dakika zaidi ya 15, daktari kwa ajili ya huduma zaidi, naye alininyoosha. Maana alitumia muda haswa. Alivyokuja sasa, hakuhangaika hata kuuliza naumwa nini, wakati najishauwa kuataka kueleza alinikatisha na kunipa karatasi aliyodai ya rufaa niende katika hospitali ya rufaa kwa huduma zaidi. Haya yote yanatokea si kwamba nilikuwa naumwa mahututi, nilikuwa naumwa kweli kiasi cha kushindwa kuvumilia kulala hadi asubuhi, sasa sijui rufaa bila kusikilizwa ilitokana na nini. Nimeanza na ushuhuda huo, angalau kuonyesha hali ilivyo katika zahanati na vituo vya afya vinapotakiwa kutoa huduma hasa nyakati za usiku. Pamoja na hayo niliyoyashuhudia mwenyewe, wapo watu lukuki waliowahi kulalamikia hilo. Wengine wanadai ili uhudumiwe usiku unapaswa kutanguliza chochote kwa mhudumu, hapo utaiona kila rangi ya huduma bora kwa mwananchi. Kwa ninavyofahamu, wauguzi na watoa huduma wote katika maeneo haya hufanya kazi kwa zamu, anayepangiwa mchana si yule atakayekuwepo usiku. Kwa sababu ya ratiba hiyo kila mmoja ana nafasi ya kupumzika. Nafikiria tu, jambo lililonikuta linamkuta mjamzito aliyefika kituoni hapo kwa huduma za uzazi, si atajifungulia kwenye benchi? Wizara ya afya na watendaji wote wanaohusika, badala ya kufanya kaguzi mbalimbali za ubora wa huduma nyakati za mchana, angalau mbadili mtindo. Lakini, hata ukaguzi msifanye kwa kutoa taarifa wajipange kuwapokea, muwe mnastukiza, itasaidia kubaini madudu mengi ambayo wananchi wanakabiliana nayo kwa wahudumu ambao mchana wanakuwa wema. Tabia hii inachagiza kuendelea kwa vitendo vya rushwa na inajenga mtazamo huo kwa wananchi. Kabla hajaenda kupata huduma anajipanga kuwa na fedha ya ziada atakayomlipa mhudumu anayelipwa na Serikali kuhudumia wananchi. Lakini wakati mwingine, tusiwalaumu sana pengine ni wachache kiasi cha kushindwa kupanga zamu za mapumziko, hivyo wanajikuta wanahelemewa na wagonjwa. Kama hali iko hivyo, mamlaka zinapaswa kutafuta namna ya kupata suluhu kabla matatizo hakujatokea madhara. Wakati mwingine hali kama hiyo inasababishwa na kukosekana kwa molari ya kazi, nashauri kuwepo na namna itakayowashawishi watoa huduma za afya kuwa na ari ya kuwahudumia wananchi. Pamoja na hilo lililonitokea, nimesikia matukio kadhaa, yakiwemo ya wajawazito kufariki kutokana na kucheleweshewa huduma katika kituo cha afya, nyakati za usiku. Sitaki kueleza zaidi kuhusu lugha zinazotumika kujibu wagonjwa nyakati hizo kwa kuwa leo nimejikita katika huduma kwa ujumla wake, lakini suala la lugha ya mazungumzo na mgonjwa ni tatizo lingine. Kama Serikali inashindwa kwenda yenyewe kufanya uchunguzi wa kubaini madudu yaliyopo itume mamluki wanaoaminika, lakini uhalisia ni kwamba kuna mazingira tata ya huduma katika zahanati na vituo vya afya nykati za usiku.
Safari ya miezi saba bila ya huduma ya nishati ya uhakika nchini imebakiza siku 18 kukoma rasmi, hii
Safari ya miezi saba bila ya huduma ya nishati ya uhakika nchini imebakiza siku 18 kukoma rasmi, hii ni baada ya matarajio ya kuingizwa kwa megawati 470 za umeme katika gridi ya taifa. Megawati hizo zitatokana na umeme utakaozalishwa na mitambo miwili kati ya tisa ya mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) unaotekelezwa na Serikali kwa Sh6.558 trilioni. Kulingana na Serikali, kiwango hicho cha umeme kitakachozalishwa na kuingizwa kwenye gridi ya taifa katikati ya Machi mwaka huu, kitaifanya Tanzania iwe na ziada ya megawati 70 za nishati hiyo. Hata hivyo, tayari mtambo mmoja unaozalisha na kuingiza megawati 235 za umeme kwenye gridi ya taifa, umewashwa jana na unaendelea kufanya kazi. Licha ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kuwa kidonda kilichoisibu Tanzania tangu kitambo, changamoto zaidi zilianza Septemba mwaka jana, pale Serikali ilipotangaza mgawo wa nishati hiyo. Taarifa ya matumaini ya kukoma kwa mgawo huo ilitolewa wilayani Rufiji mkoani Pwani jana Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko alipofanya ziara ya kutembelea mradi wa JNHPP unaotarajiwa kuzalisha jumla ya megawati 2,115 utakapokamilika Bado siku 18 Baada ya kuwashwa kwa mtambo namba tisa, Dk Biteko alisema mtambo namba nane unatarajiwa kuwashwa Machi mwaka huu na kwa pamoja itazalisha jumla ya megawati 470. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, uzalishaji huo utaifanya Tanzania kuwa na ziada ya megawati 70 za umeme. Mahitaji ya umeme kwa sasa ni megawati 400. "Katika mitambo hii miwili, namba tisa na nane tutakuwa na megawati 470, ukichukua upungufu tulionao wa megawati 200 mpaka 400 maana yake ni kwamba tutakuwa na ziada ya megawati 70," alisema Dk Biteko. Hata hivyo, alieleza siku hiyo ya Machi, uzinduzi utafanyika kwa ajili ya mitambo miwili (tisa na nane) na Rais Samia Suluhu Hassan ndiye atakayekuwepo, huku Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi akitarajiwa pia. Katika hatua nyingine, Dk Biteko alisema Desemba mwaka huu mitambo yote tisa inatarajiwa kukamilika. Hata hivyo, alieleza baada ya mawasiliano na mhandisi ndipo itakapojulikana kwamba tarehe ngapi hasa mitambo inayofuata ukiwemo namba saba na kuendelea itakamilika. “Tutaeleza utaingia lini baada ya kuwa tumewasiliana na mkandarasi, tusingependa kutoa ahadi kesho ikaonekana sio. Lakini utafuata baada ya Machi,” alisema Dk Biteko. Mshikemshike saiti Haikuwa rahisi kwa mkandarasi, kukamilisha kazi hiyo kabla ya Juni, mwaka huu muda ambao ndiyo aliopangiwa kukamilisha mradi huo. Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi kutoka kampuni zinazotekeleza mradi huo (Arab Contractors na Elsewedy Electric) Mohamed Zaky, msukumo na msisitizo wa Dk Biteko tangu alipokuwa Waziri wa Nishati, uliwalazimu kufanya kazi usiku na mchana na ndiyo sababu wamemaliza kabla ya muda uliopaswa. “Tulipaswa kukamilisha Juni, lakini mradi huu umekamili hivi sasa kutokana na msukumo tuliokuwa tukiupata kwa Dk Biteko, simu zilikuwa ni nyingi mara kwa mara wakitusisitiza kuumaliza mapema na tumefanikiwa," alisema. Kilichochagiza msukumo huo, ni kile kilichoelezwa na Dk Biteko kuwa, alilenga kuwafanya Watanzania wapate umeme ambayo ndiyo nia ya Rais Samia. Awali, akizungumza katika ziara hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba alisema mtambo wa kwanza uliowashwa utasaidia kupunguza makali ya mgawo wa umeme kwa zaidi ya asilimia 85. "Huko majumbani, kuna maeneo hakuna mgao tena, mwezi ujao tutaingiza umeme wa mtambo namba nane, kisha namba saba utafuata ambao nao upo kwenye hatua nzuri,” alisema. Pamoja na kuanza kazi kwa mtambo huo namba tisa, Mramba aliyekuwa sehemu ya viongozi katika ziara hiyo, alisema ujenzi wa mtambo namba nane, umefikia asilimia 99.9. “Kwa hiyo na wenyewe uko mbioni kukamilika,” alisema Katibu Mkuu huyo. Vijana kupewa vyeti Fursa waliyoipata Watanzania 10,000 ya kushiriki katika ujenzi wa mradi huo, inaambatana na kupewa vyeti maalum kutoka Taasisi ya Ufundi Stadi (VETA). Kulingana na Mramba, vyeti hivyo vitakuwa utambulisho wao na watavitumia kupata fursa za utekelezaji wa miradi mingine ya kimkakati itakayoendelea kutekelezwa nchini. "Tulifanya kazi na Veta, wakawatathmini na kuwapa vyeti maalumu vya utambuzi vijana hawa wazawa ambao mbali na hapa tutaendelea kuwatumia kwenye miradi mingine," alisema. Kuhusu maji katika bwawa la JNHPP linalohitaji jumla ya mita za ujazo bilioni 32.7, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema ni mita za ujazo bilioni nne ndizo zilizosalia. Alisema kwa sasa bwawa la Nyerere limejaa kufikia mita za ujazo bilioni 28. Ahadi kuhusu umeme Ahadi za kukoma kwa mgawo wa umeme hazikuanza leo wala jana, zilikuwepo tangu enzi za Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. Oktoba mwaka 2012, akizindua mradi wa ujenzi wa mitambo ya kusafishia na kusafirisha gesi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema mgawo wa umeme utakoma mwaka 2015. Kilichobeba matumaini ya Kikwete juu ya kukoma kwa mgawo huo ni kukamilika kwa mradi huo, uliotarajiwa kuzalisha megawati 3,600, lakini utabiri huo ulibaki kuwa hewa. Kauli inayofanana na ya Kikwete ilitolewa tena Novemba mwaka 2022 na aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati wakati huo, Stephen Byabato, akitabiri matatizo ya kukatika kwa umeme yangekoma Desemba ya mwaka huo. Alichokitaja kukomesha matatizo hayo ni kukamilika kwa mradi wa Kinyerezi 1 Extension utakaozalisha megawati 185 za umeme. Mradi ulikamilika na tabu ilibaki pale pale. Septemba mwaka 2023 mgawo wa nishati hiyo uliendelea, huku sababu ikitajwa ni upungufu wa uwezo wa uzalishaji umeme kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kikiwemo cha maji. Sababu ile ile iliyowahi kutolewa katika migawo yote iliyowahi kutokea. Kutokana na mazingira hayo, Rais Samia alipomuapisha Mkurugenzi mpya wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Gissimo Nyamo-Hanga alimpa miezi sita kumaliza mgawo wa nishati hiyo. Miezi sita aliyopewa Nyamo-Hanga kumaliza mgawo huo, inakwisha Machi 25, mwaka huu na hatua iliyofikiwa inaonyesha tumaini la utekelezaji wa maagizo hayo ya Rais Samia.
Takriban watu 25, wamepoteza maisha na wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mann
Takriban watu 25, wamepoteza maisha na wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne, likiwemo lori moja na mengine madogo matatu. Idadi hiyo ya waliofariki imeongezeka kutoka vifo 15 vilivyoripotiwa juzi kutokana na ajali hiyo, iliyotokea katika eneo la Kibaoni, barabara kuu ya Arusha-Namanga mkoani Arusha. Tukio hilo linajumuisha jumla ya ajali nne zilizopoteza uhai wa watu wengi kwa mara moja nchini, katika kipindi cha miezi minne iliyopita, Mwananchi linachambua. Ajali nyingine Novemba 26, mwaka jana watu 15 walipoteza maisha kwa ajali ya basi la kampuni ya Baraka Classic, lililopinduka baada ya kufeli breki likiwa kwenye mwendokasi. Katika ajali hiyo iliyotokea Mputa wilayani Mtama katika Mkoa wa Lindi, mbali na waliofariki dunia, wengine 26 walijeruhiwa. Siku tatu baadaye, watu 13 waliiaga dunia kwa ajali nyingine ya basi la abiria lenye namba za usajili T178 DVB la kampuni ya Ally’s Star, lililogongana na kichwa cha treni. Ajali hiyo ilitokea katika makutano ya reli na barabara wilayani Manyoni katika Mkoa wa Singida, huku kati ya waliofariki wanawake walikuwa sita na wanaume saba na 25 walijeruhiwa. Ajali nyingine iliyotwaa roho za watu wengi, ni ile ya Desemba 25, mwaka jana, iliyohusisha basi dogo la abiria lililogongana uso kwa uso na lori katika Kijiji cha Kilemba mkoani Kigoma. Watu nane walifariki dunia kutokana na ajali hiyo, huku wengine sita wakijeruhiwa. Kuhusu ajali ya Arusha Katika ajali hiyo ya Arusha iliyotokea Jumamosi Februari 24, mwaka huu, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji, alisema kati ya waliofariki wanaume ni 14 na wanawake 11, akiwamo mtoto mdogo wa kike. Kulingana na Haji, kati ya watupoteza uhai, watu saba ni raia wa kigeni (mtaifa na majina yao bado hayajajulikana). Ajali ilihusisha lori lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi nchini Kenya. Magari mengine yaliyopata ajali katika tukio hilo ni T 623 CQF aina ya Nissan Caravan, T 879 DBY aina ya Mercedes Benz Saloon na T 673 DEW aina ya Toyota Coaster mali ya shule ya mchepuo wa Kingereza ya New Vision. Chanzo Ingawa uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha ajali bado unaendelea, Haki alisema taarifa za awali zinaonyesha kilichosababisha tukio hilo ni kufeli kwa mfumo wa breki wa lori, ndicho kilicholifanya liyagonge magari mengine. Hata hivyo, alieleza msako wa dereva wa lori hilo unaendelea, kwani kwa sasa inadaiwa alitoroka baada ya ajali. Katika taarifa ya juzi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, kati ya watu 15 waliofariki, watatu ndiyo waliokuwa raia wa kigeni.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi amemshitaki Wakili wa Kujitegemea, Peter Madel
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Eliezer Feleshi amemshitaki Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kitaaluma. Msingi wa tuhuma dhidi ya Madeleka kulingana na maelezo yake, ni hatua yake ya kumwakilisha mteja wake, Hashim Ally katika kesi iliyowahi kufunguliwa naye dhidi ya Mbunge wa Babati, Pauline Gekul. Barua ya wito wa wakili huyo mbele ya kamati hiyo ya maadili ya mawakili, ilisambaa katika mitandao ya kijamii, ikieleza AG amewasilisha malalamiko dhidi ya Madeleka kuhusu kukiuka kwa maadili ya kitaalum. Hata hivyo, Madeleka si wakili wa kwanza kukumbana na hilo, iliwahi kumtokea Boniface Mwabukusi Oktoba mwaka jana, aliyeitwa mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu zilizoibuliwa na AG, Dk Feleshi. Mwaka 2018, Fatma Karume naye alikumbana na kadhia hiyo, aliposhitakiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa wakati huo, Profesa Adelardus Kilangi. Lakini kesi yake ilikwenda mbali zaidi hadi kusimamishwa kutoa huduma za uwakili. Hao ni mawakili wachache kati ya wengi waliowahi kupitia msalaba huo. Hata hiyo, alipotafutwa kuzungumzia kesi hiyo, Dk Eliezer Feleshi alisema ni mapema mno kuizungumzia, huku akishauri wanahabari wasubiri siku iliyotajwa ili wakasikilize au kupewa taarifa. “Huu ndiyo kwanza wito, unaandikaje habari kutokana na wito. Mnapaswa msubiri siku iliyopangwa kwa ajili ya kesi kusikilizwa kama kuna nafasi ya ninyi kuingia mtaingia kusikiliza au kama sivyo mtapewa taarifa na mamlaka sahihi,” alieleza kwa ufupi. Alichokisema Madeleka Akizungumza na Mwananchi kuhusu hilo jana, Wakili Madeleka alikiri kupokea wito huo, akifafanua si barua pekee bali ilihusisha na nyaraka nyingine za kesi aliyofunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Maudhui ya kesi hiyo, alisema anashitakiwa katika Kamati ya Maadili ya Mawakili, kwanini alimwakilisha mteja wake Hashim Ally katika kesi dhidi ya Mbunge wa Babati, Pauline Gekul. Baada ya kupokea barua na nyaraka za kesi hiyo, Madeleka alieleza anafanya mchakato wa kusambaza nakala kwa mawakili watakaosimama kumtetea. “Kwa sasa nafanya mchakato wa kutoa nakala ili nisambaze nyaraka hizi kwa mawakili watakaosimama kunitetea, lakini hata kwa Watanzania na wapenda haki,” alisema Madeleka. Kwa mtazamo wa kisheria kulingana na wakili huyo, kilichofanyika dhidi yake ni kinyume na taratibu, kwani AG hana mamlaka ya kumshitaki katika kamati hiyo. Mamlaka ya AG yanakosekana kutokana na kile alichoeleza, kiongozi huyo ni sehemu ya kamati ya maadili ya mawakili na hivyo haiwezekani akawa mlalamikaji kwenye kesi inayohukumiwa naye. “Kanuni za haki za asili zinasema mtu hawezi kuwa hakimu kwenye kesi yake mwenyewe. Kwa vyovyote atajipendelea,” alisema Madeleka. Hoja nyingine inayovunja utaratibu kwa mujibu wa Madeleka ni kesi ya Gekul bado ipo mahakamani kwa maana ya rufaa na inatarajiwa kusikilizwa Machi 18, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Manyara. Kwa madhumuni ya kulinda uhuru wa mahakama, alisema haipaswi jambo ambalo lipo mahakamani, lifunguliwe kesi na mahakama nyingine, hiyo ni kuingilia. “Jambo lenyewe lipo mahakamani kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara mjini Babati. Jambo likiwa mahakamani halipawswi kujadiliwa na mahakama nyingine,” alisema. Kilichomo kwenye barua Barua ya wito wa Madeleka mbele ya kamati hiyo ya mawakili, imebeba ujumbe unaosema ‘tuhuma za kuvunja miiko ya kitaaluma kutoka kwa AG. Katika maudhui ya ndani ya barua hiyo iliyotiwa saini na Katibu wa kamati, Faraji Ngukah inasema kamati hiyo imepokea malalamiko dhidi ya Madeleka kutoka kwa AG. “Unatakiwa kisheria ujibu tuhuma zilizoibuliwa katika hati ya kiapo, nakala yake imeambatanishwa. Majibu yako yanapaswa kufika ndani ya siku 21, kutoka siku uliyopokea,” imeeleza barua hiyo. Kulingana na barua hiyo, iwapo hatozingatia ndani ya muda uliopangwa, kamati hiyo itaendelea bila kutoa taarifa nyingine zaidi.
Serikali imetangaza mikakati ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa sukari, ikiwa ni hatua za kudu
Serikali imetangaza mikakati ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa sukari, ikiwa ni hatua za kudumu za kumaliza tatizo hilo ambalo aghalabu hujitokeza kila mwaka. Ingawa si mara ya kwanza Serikali kuibuka na mikakati ya kumaliza tatizo hilo, lakini hii iliyotangazwa kwa mtazamo wangu naona uhai ndani yake. Mikakati hii inayotangazwa inakuja katika kipindi ambacho bei ya bidhaa hiyo kwa wauzaji wa rejareja imefikia Sh4,000 hadi Sh5,000 kwa kilo. Ongezeko la bei hiyo ni karibu mara mbili ya bei iliyokuwepo awali ambayo ni Sh2,500 hadi Sh2,700 kwa kilo. Kwa maneno mengine unaweza ukasema chai hainyweki. Hali imekuwa mbaya zaidi hata pale Serikali kupitia Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), ilipotangaza bei elekezi ya bidhaa hiyo, ikitaka kilo moja iuzwe kuanzisha Sh2,800 na isizidi Sh3,200, bado watu waliuza zaidi ya hapo. Katika nyakati hizo, kila kilichokuwa kinazungumzwa na mamlaka kilionekana ahadi isiyo na matumaini na sababu zilizotolewa zilitafsiriwa kama visingizio na wapo walioziita kauli za kisiasa. Kupotea kwa matumaini ya wananchi kumetokana na rejea ya kauli lukuki zilizowahi kutolewa na viongozi mbalimbali juu ya kutamatika kwa uhaba wa sukari, lakini hazikuzaa matunda. Angalau hii mikakati iliyotangazwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe inaonekana kuwa na dalili za kukomesha tatizo hilo, iwapo itatekelezwa kama ilivyoelezwa. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kubadili utaratibu wa uagizaji wa sukari nje ya nchi, kutoka kutoa vibali kwa wazalishaji waagize, hadi kuipa Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA), iingie mikataba na kampuni mbalimbali kwa ajili ya kuagiza bidhaa hiyo. Hatua hii inapunguza mtazamo uliokuwepo kwamba, idadi ndogo ya waagizaji wa bidhaa hiyo bado inawapa nguvu ya kupanga michezo mbalimbali ambayo matokeo yake ni kuendelea kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo. Jukumu hilo kupewa NFRA ni kama tumepeleka kazi kwa anayestahili kuifanya kwa sababu sukari si bidhaa tu, bali inabeba usalama wa watu na usalama wa chakula kwa ujumla. Sitaki kuingia ndani zaidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi ya wazalishaji wa sukari, lakini yapo mambo yanayoonyesha dalili ya uhalisia kwamba kulikuwa na michezo iliyochagiza uhaba kuendelea. Kilichokuwa kinafanyika ni kutafuta sababu, ikitokea itatumika kufaidisha watu fulani wakati wananchi wanaendelea kuumia. Mkakati mwingine ambao napata jeuri ya kuuita kabambe ni mabadiliko ya sheria yatakayohusisha kuwaondoa wazalishaji kuwa na wajibu wa kupewa vibali vya kuagiza bidhaa hiyo unapotokea uhaba. Badala yake, suala la kuagiza sukari litabaki kuwa na ushindani, yaani kampuni za ndani na nje ya nchi zitashindanishwa na itakayoshinda ndiyo itakayopewa jukumu hilo. Maana yake, yule bora na mwenye uwezo ndiye atakayeingiza sukari. Lakini kwenye hili Serikali iweke mpango wa kudhibiti janjajanja za watu kuja na kampuni zao mifukoni. Kuwepo na mazingira ya uwazi katika utangazaji zabuni hizo ili anayepata awe amestahili kupata na hata akitokea aliyekosa ionekane dhahiri kwamba amestahili kukosa kutokana na vigezo. Kuunga kwangu mkono hatua hii, hakulengi kufurahia kuwapokonya tonge mdomoni wazalishaji, bali natamani kuona hizi lawama na changamoto katika bidhaa ya sukari zinakoma. Naamini kama muingizaji sukari atapatikana kwa ushindani, hata wazalishaji wanayo nafasi ya kushinda kama wanakidhi vigezo na kama hawakidhi maana yake walikuwa wanatuingizia mzigo, ilhali hawakuwa na uwezo huo. Katika hili, wazalishaji wasimtafute mchawi, ni suala la kujipanga na kampuni yako, ikitangazwa zabuni omba shindana na kama una vigezo utashinda hatimaye utaagiza sukari. Nakumbuka kabla ya mikakati hii, kauli zilizokuwa zinatolewa kukabiliana na uhaba wa sukari ni kuongeza uzalishaji wa miwa ili kuhakikisha viwanda vilivyopo vinapata malighafi ya kutosha. Miwa ilizalishwa na inaendelea kuzalishwa na hatimaye mingine inaozea shambani na bado sukari ilibaki kuwa changamoto. Wapo waliodhani ni muhimu kuvibana viwanda vya ndani viongeze uzalishaji, nalo halikufua dafu kwani wakati mwingine kiwango cha kiwanda kuzalisha kiliamriwa na mazingira yaliyopo. Kwa mfano katika nyakati hizi ambazo Tanzania na mataifa mengine mbalimbali yanakabiliwa na mvua za El-Nino, viwanda vyote vilipunguza maradufu uzalishaji na vingine vilisitisha kabisa. Kwa hiyo, upungufu wa sukari utakabiliwa kwa kuhakikisha kunakuwa na mifumo mizuri ya kuagiza kutoka nje, tija inaongezwa katika kilimo cha miwa na viwanda vinaongezeka kwa ajili ya kuzalisha sukari. Mambo hayo yote matatu ndiyo yatakayoleta matokeo katika uhakika wa upatikanaji wa sukari, tukitegemea kwenye moja kati ya hayo tutakwama na imewahi kutokea miaka kadhaa iliyopita. Hiki kilichofanyika cha Serikali kutoka hadharani na kufafanua kuhusu mambo yaliyokuwa yakilalamikiwa na wananchi ni miongoni mwa mambo muhimu yanayopaswa kuendelezwa.
Hatma ya kukoma kwa mgawo wa umeme nchini ipo ndani ya muda mchache, baada ya matarajio ya kuingizwa
Hatma ya kukoma kwa mgawo wa umeme nchini ipo ndani ya muda mchache, baada ya matarajio ya kuingizwa kwa megawati 235 katika gridi ya taifa. Matumaini ya kukoma kwa mgawo huo, yanatokana na kile kilichoelezwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba kwamba muda wowote kuanzia sasa, mtambo kutoka Bwawa la Jilius Nyerere (JNHPP) utawashwa. Hatua ya kuwashwa kwa mtambo huo inafuatia majaribio kadhaa uliyowahi kufanyiwa na kwamba utakapowashwa, utapunguza kwa zaidi ya asilimia 80 ya changamoto ya mgawo wa umeme. Mgawo wa umeme ulianza Septemba mwaka jana, ukitokana na upungufu wa uwezo wa uzalishaji wa nishati hiyo kutoka kwenye vyanzo mbalimbali yakiwemo maji. Tangu kuanza kwa mgawo huo, kumekuwa na ahadi lukuki za viongozi juu ya kukoma kwake, ikiwemo iliyowahi kutolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga. Kapinga aliahidi mgawo huo unatarajiwa kukoma Februari 17, mwaka huu na baadaye aliibuka na kueleza utakoma Machi, mwaka huu. Wingi wa ahadi hizo ndiyo uliopoteza matumaini ya wananchi juu ya kukoma kwa mgawo huo, wakihofu pengine ahadi wanazopewa zitabaki kuwa hewa. Matumaini ya kutamatika kwa mgawo huo yametolewa jijini Dar es Salaam jana na Mramba alipozungumza katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu na Wahariri wa Vyombo vya Habari, uliofanyika Ikulu. Mramba alisema matarajio ya kukamilizika kwa mgawo ni bwawa la JNHPP ambalo kwa sasa kuna mitambo miwili iliyopo katika hatua za mwisho za kukamilika kwake. Kati ya mitambo hiyo, alisema wa kwanza umeshafanyiwa majaribio na kilichobaki ni kuingiza umeme wake kwenye gridi ya taifa. “Ninaposema muda wowote namaanisha muda wowote kwa sababu wataalamu wanaendelea na kazi kuhakikisha wanaingiza megawati 235 za umeme huo kwenye gridi ya taifa,” alisema. Kwa kuwa mahitaji ya nishati hiyo kwa sasa ni takriban megawati 300 hadi 400, kiwango hicho cha umeme kitakachoingizwa kitapunguza angalau asilimia 80 ya matatizo ya umeme yaliyopo. “Kwa kuwasha tu ule mtambo, zaidi ya asilimia 80 ya matatizo yatakuwa yamekwisha. Taratibu za mtambo huu ziko mwishoni kabisa, unaweza ukajikuta umeamka asubuhi kesho ukashangaa mgawo haupo au keshokutwa, lakini niseme tu tupo katika hatua za mwisho,” alisema. Kuhusu mtambo wa pili, alisema umeshafanyiwa majaribio ya awali na kinachotarajiwa kufanyika ni majaribio ya awamu ya pili wiki hii kisha itafuata awamu nyingine. “Kwa kawaida majaribio ya namna hii yanachukua wiki mbili kwa hiyo tumekadiria kufikia katikati mwa Machi mtambo wa pili na wenyewe utakuwa umekamilika,” alisema. Alisisitiza kilichoelezwa na Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ni sahihi kwamba mitambo hiyo itakayoingiza jumla ya megawati 470 ipo katika hatua za mwisho. “Watu wana hofu na hawaamini, lakini niwaondolee hofu, JNHPP sasa hivi lina maji mengi na mwaka huu umekuwa wa maajabu kwa sababu katika wiki tatu zilizopita kiasi cha maji yanayoingia kwenye mabwawa yamevunja rekodi,” alisema. Hata hivyo, mtendaji mkuu huyo wa wizara hiyo alisema matatizo ya umeme nchini yapo katika eneo la uzalishaji na usambazaji na si usafirishaji. Kinachotokea kwenye uzalishaji, alisema ni kukosekana uwezo wa kuzalisha umeme unaoendana na mahitaji ya nchi na jambo hilo ndilo linalosababisha mgawo. “Mahitaji ni makubwa , lakini kiwango kinachozalishwa ni kidogo huo ndiyo mgawo unavyotokea,” alisema. Kwa upande wa usambazaji, alisema matatizo hutokea pale ambapo umeme unazalisha wa kutosha, lakini miundombinu inakuwa na tatizo na hivyo kusababisha wananchi wasiupate. “Unakuta umeme unaozalishwa unatosha lakini transfoma ina hitolafu au nguzo imeanguka, haya ndiyo matatizo kwenye usambazaji, lakini haya hayasababishi mgawo ni kukatika kwa kawaida,” alisema Mramba. Hata hivyo, alisisitiza kukatika huko kwa sababu ya hitilafu ya miundombinu ni jambo linalotarajiwa kuwepo hata baada ya kukoma kwa mgawo wa umeme. “Kwa hali ya mifumo ya usambazaji ilivyo, hatutarajii kwa kweli hizo changamoto za kukatika kwa umeme hapa na pale zitakuwa zimeisha kabisa,” alisema. Aliijenga hoja hiyo akitolea mfano wa matukio ya wizi wa mafuta ya transfoma katika Wilaya za Temeke, Mbagala na Kigamboni. “Transfoma inavyoungua inakuwa imeunganishwa na wateja takriban 100 kwa hiyo inapoungua wateja hawa watakuwa gizani hadi transfoma mpya itakapoenda kuwekwa,” alisema. Alieleza changamoto nyingine zitakazosababisha kukatika kwa huduma hiyo ni mvua inayosababisha nguzo kuloa maji na kusababisha shoti. “Wakati wa mvua kwa sababu ya kuwepo kwa maji mengi na kwa sababu yanaweza kusababisha shoti, hizo ndizo changamoto zinazoweza kuwepo,” alisema. Alieleza kukatika kwa kawaida kila mtu anaelewa na litakapotatuliwa suala la mgawo hayo mengine yatakomeshwa taratibu.
Jukumu la uingizaji sukari kutoka nje ya nchi, halitakuwa tena mikononi mwa wazalishaji, baada ya Se
Jukumu la uingizaji sukari kutoka nje ya nchi, halitakuwa tena mikononi mwa wazalishaji, baada ya Serikali kutumia Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) kuingia mikataba na kampuni mbalimbali zitakazotekeleza wajibu huo. Hatua hiyo itafuatiwa na mabadiliko ya sheria Juni mwaka huu, itakayowaondoa wazalishaji kuwa na haki hiyo, badala yake atakayepata fursa ya uagizaji sukari nje ya nchi, atatokana na kushindanishwa na kampuni mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Mambo hayo ni miongoni mwa mikakati ya kudumu iliyotajwa na Serikali kukabiliana na uhaba wa sukari nchini, uliosababisha kuongezeka maradufu kwa bei ya bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali nchini. Ingawa kinachotajwa kuchagiza hali hiyo ni kupungua kwa uzalishaji kulikosababishwa na mvua za El-Nino, wazalishaji nao ni sehemu ya kundi lililotuhumiwa kuhusika katika changamoto inayoendelea kama ilivyofafanuliwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe. Bei ya sukari tangu kuanza kwa Januari mwaka huu imekuwa ikiongezeka na kufikia Sh4,000 hadi Sh5,000 katika baadhi ya maeneo kutoka Sh3,000 kwa kilo, iliyokuwepo awali. Hayo yametokea wakati Bodi ya Sukari (SBT), ilishatangaza bei elekezi ya bidhaa hiyo kuanzia Sh2,800 na isizidi Sh3,200 lakini bado sukari inauzwa bei zaidi ya hiyo. Hata hivyo, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete alimtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuwa imara katika kipindi hiki cha changamoto ya sukari, maji na umeme, kwa kuwa ni mambo ya kawaida katika uongozi. “Tunamshukuru Rais Samia kwa uongozi wake tunaona mambo yanakwenda vizuri, changamoto ni sehemu ya maisha, kungekuwa hakuna changamoto isingekuwepo haja ya kuwa na viongozi. Changamoto hazitaisha hata kwa mataifa makubwa kama Marekani iliyopata uhuru mwaka 1774 hadi leo hawajamaliza changamoto,” alisema Kikwete katika hafla ya kusaini mikataba sita ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Mikoa ya Lindi, Kagera, Dar es Salaam na visiwani Zanzibar. Bashe alitaja mikakati hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu na Wahariri wa vyombo vya habari, uliofanyika Ikulu. Mikakati ya kudumu Moja ya mikakati hiyo ni kuitumia NFRA katika uagizaji wa sukari nje ya nchi, badala ya kuliacha jukumu hilo kwa wazalishaji kwa mujibu wa sheria. Alifafanua NFRA imepewa mamlaka ya kuingia mikataba na kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuagiza bidhaa hiyo. “Tumeitumia NFRA, hii sukari inayopakuliwa sasa hivi imeletwa na kampuni iliyoingia makubaliano na wakala huo sio viwanda kwa sababu hili ni suala la usalama wa nchi na chakula,” alisema. Msingi wa uamuzi wa kutoa jukumu hilo kwa NFRA ni kile alichokiita mchezo mchafu unaofanywa na wazalishaji kwa kuacha kuagiza sukari kulingana na matakwa ya vibali walivyopewa. Alieleza wazalishaji hao licha ya kukabiliwa na mvua za El-Nino, walipewa vibali vya kuagiza tani 10,000 za sukari kila mmoja, lakini hadi sasa ni watatu pekee ndiyo wameshaingiza na hakuna aliyeingiza zaidi ya asilimia 20 ya mzigo aliopaswa kuuingiza. “Viwanda vyote vilipewa fursa ya kuagiza tani 10,000 na aliyeagiza ni Kilombero tani zisizozidi 2,000 Kagera Sugar naye ameingiza tani zisizozidi 2,000 TPC bado na Bagamoyo Sugar bado Mtibwa Sugar ndiyo wameingiza na bado haijashuka,” alisema Bashe. Katika ufafanuzi wake juu ya uamuzi huo, Bashe alieleza: “Kama Serikali isingechukua hatua ya NFRA kuingilia uagizaji wa sukari, nchi ingekuwa katika hali mbaya zaidi,” alisema. Mabadiliko ya sheria Mkakati mwingine ni mabadiliko ya sheria aliyosema yanatarajiwa kufanyika Juni mwaka huu (mwisho wa mwaka huu wa fedha), ili kuondoa kabisa ruhusa ya vibali vya uagizaji sukari kwa wazalishaji. Badala yake alisema sheria hiyo inatarajiwa kutoa fursa ya uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi kwa ushindani na atakayepata ni yule atakayeshindania na kushinda dhidi ya kampuni mbalimbali. “Watashindana na kampuni kutoka nje, lakini hatuwezi kuwalinda watu kwa miaka 30. Kuanzia baada ya mabadiliko ya sheria ukitokea upungufu wa sukari, hautaagizwa na wao (wazalishaji),” alisema. Michezo michafu Katika maelezo yake, Bashe alisema mchezo mchafu mwingine unaochezwa na wazalishaji ni kutoeleweka kwa mitandao yao ya usambazaji sukari nchini. Si kutoeleweka tu, alieleza hata Serikali inapotaka kuiingilia inakumbana na changamoto kubwa na kwamba sasa hivi yupo tayari kukabiliana na hilo. “Unakuta Kagera Sugar anatoa sukari inaenda Mwanza alafu inarudisha Bukoba, alafu yule mtu wa Mwanza ndiye msambazaji katika maeneo ya karibu asilimia 33 ya nchi,” alisema. Waziri huyo alisema haikubaliki wazalishaji wa sukari pamoja na kupewa misamaha mbalimbali ya kodi, bado wanashiriki kuhujumu wakati wa mvua za El-Nino. “Incentive za kodi wanazopewa sekta ya sukari hakuna sekta inapewa hizo kwenye nchi hii, wanapewa ardhi bure kwa ajili ya kulima wengine, wamepewa ulinzi kwa zaidi ya miaka 20 kwenye nchi hii. “Alafu imetokea El-Nino wanaamua kufanya walichokifanya, najua ni maumivu kwa watanzania kwa muda mfupi lakini hii ndiyo itakayokuwa tiba ya sekta ya sukari kwa muda mrefu,” alisema. 84 wakamatwa Hata hivyo, alisema kuongezeka kwa bei ya sukari kumetokana na kile alichokiita uhuni unaofanywa na wafanyabiashara wa rejareja, wanaoamua kupandisha bei kinyume na matakwa ya Serikali. Kutokana na hilo, alisema tayari wafanyabiashara 84 wameshakamatwa na wanatarajia kufikishwa mahakamani. “Tumeshawakamata wafanyabiashara 84 na tunawachukua kuwapeleka mahakamani. Nini kinatokea sukari inaingia anauzia kwa Sh2,500 hadi Sh2,800 akiinunua yeye anaenda kuuza Sh4,000 hadi Sh4,500. “Wafanyabiashara wana machaguo mawili tu, waache kuuza sukari Serikali itatafuta namna nyingine. Wenye viwanda nao waamue wafuate utaratibu wa Serikali, hawawezi waache hii kazi,” alisema. Alisisitiza kuanzia sasa kila mfanyabiashara atakayepewa sukari inayoingizwa kutoka nje jina lake litapelekwa kwa Mkuu wa Mkoa husika naye atatakiwa kuwasilisha majina ya aliowauzia na bei aliyowapangia. Tani 300,000 kuagizwa Badala ya tani 100,000 zilizotangazwa awali, Bashe alisema Serikali imepanga kuagiza jumla ya tani 300,000 za sukari nje ya nchi mwaka huu. “Hili tatizo la bei sasa hivi linabadilika tunaamini kufikia Machi 15, mwaka huu tutakuwa tumeshaingiza nchini tani 60,000 na tunatarajia kufikia mfungo wa Ramadhan hali itakuwa vema,” alisema. Hadi sasa, alisema sukari iliyoagizwa nje ya nchi iliyofika na kuanza kusambazwa ni tani 31,000 na kwamba kuna meli yenye tani 25,000 inaendelea kushusha mzigo bandarini. Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa SBT, Profesa Kenneth Bengesi alisema mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida ni tani 552,000, huku ile ya viwanda ni tani 255,000. Lakini, alisema uwezo wa uzalishaji uliopo ni tani 445,000 kwa sukari ya matumizi ya kawaida, huku hakuna kabisa uwezo wa kuzalisha sukari ya matumizi ya viwandani. Kwa mujibu wa Profesa Bengesi, upungufu uliopo ni tani 200,000 kwa sukari ya matumizi ya kawaida, huku tani 225,000 kwa sukari ya viwandani. Hata hivyo, alisema hadi Februari 21, mwaka huu sukari iliyokuwepo nchini ni tani 8,116. Tani 3,445 zilikuwa mikononi mwa wazalishaji na tani 4,771 zilikuwa mikononi mwa wafanyabiashara, huku kiasi kilichoingia kutoka nje ya nchi ni tani 4,449.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametaka ukarabati wa miundombinu ya umeme kuf
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametaka ukarabati wa miundombinu ya umeme kufanyika kwa wakati ili kuwaepusha wananchi na adha ya kukosa nishati hiyo kwa muda mrefu. Maelekezo hayo ya Dk Biteko, yametokana na malalamiko yaliyoibuliwa na Mbunge wa Wanging’ombe, Dk Festo Dugange aliyelalamikia kuungua kwa transfoma 50 hadi 60 kila mwaka, huku matengenezo yakichelewa kufanyika. Kuharibika kwa transfoma hizo, kulingana na Dk Dugange kunasababishwa na kupigwa na radi ambazo mara nyingi hutokea katika Wilaya ya Wanging’ombe. Kutokana na hali hiyo, Dk Biteko aliyekuwa ziarani katika Mkoa wa Njombe alikoshiriki kuwasha umeme katika Kijiji cha Ikwavila na Shule ya Sekondari ya Wasichana Njombe, amesisitiza matengenezo kufanyika kwa haraka. Akizungumza katika ziara yake hiyo leo, Jumatano Februari 21, 2024 kiongozi huyo amesema hakuna sababu ya matengenezo au mabadiliko ya vifaa kuchelewa kwa kuwa vinazalishwa nchini. Dk Biteko ambaye pia ameshiriki kukagua mindombinu ya uzalishaji umeme na nguzo za umeme katika kiwanda cha TANWAT, amesisitiza kinachochelewesha kazi hizo ni uzembe. "Hili suala la transfoma inaungua halafu inachukua hadi mwezi mmoja kubadiliswa, uzembe huu haukubaliki. Idara ya Manunuzi Tanesco tumeibadilisha kutokana na sababu hizi. “Vifaa hivi vinazalishwa kwenye viwanda vya ndani, tunataka watendaji hawa waone shida wanazopata wananchi na kuzitatua, kweli kuna changamoto ya umeme lakini kuna baadhi ya matatizo Tanesco wanaweza kuyamaliza," amesema. Hata hivyo, ameweka wazi kuwa Serikali isingependa kuona changamoto ya umeme inaendelea, ndiyo maana inatekeleza kwa kasi mradi wa Umeme wa Julius Nyerere (JHNPP). Amesema kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 99 na mtambo mmoja umekamilika utakaoingiza megawati 235 kwenye gridi mwezi huu. “Mtambo mwingine unatarajiwa kuingiza megawati nyingine 235 mwezi Machi mwaka huu,” amesema. Katika ziara hiyo, mbunge wa Wanging'ombe aliomba laini ya umeme inayojitegemea, kwa kuwa ya sasa inatumiwa na Lupembe na TANWAT hivyo kupunguza kasi ya umeme. Akijibu ombi hilo, Dk Biteko ameiagiza Tanesco kujenga kituo cha kupoza umeme wilayani humo ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma hiyo. Kuhusu usambazaji wa umeme, Dk Biteko amesema vijiji vyote 108 vya Wilaya hiyo vina umeme, huku asilimia 56 ya vitongoji tayari vimeshasambaziwa nishati hiyo. “Kazi inaendelea Sh9 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme katika Wilaya hii,” amesema. Katika hatua nyingine, Dk Biteko amewataka wananchi watumie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi sahihi, huku akiwaagiza viongozi wa Serikali kujikita katika kutatua kero za wananchi. Lingine aliloagiza ni kuhakikisha watoto wote wenye umri unaostahili kuanza shule wakaripoti kwa kuwa huduma hiyo inatolewa bila ada. Mbunge Dugange, ametumia ziara hiyo ameshukuru hatua ya Wilaya hiyo kupata umeme karibu vijiji vyote. Awali, akizungumza katika ziara hiyo, mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini ( REA), Godfrey Chibulunje amesema Sh70.44 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini huku Wangingombe ikipata Sh9.35 bilioni.
Shaka ya usalama imewagubika wakazi wa maeneo ya jirani na jengo la Motel Agip jijini Dar es Salaam,
Shaka ya usalama imewagubika wakazi wa maeneo ya jirani na jengo la Motel Agip jijini Dar es Salaam, wakihofu kuangukiwa na jengo hilo kutokana na kuchoka kwake. Jengo hilo, kwa mujibu wa taarifa ilizonazo Mwananchi limejengwa tangu miaka ya 1940 na mwaka 1998 liliacha kutumika wala kufanyiwa matengenezo hadi sasa. Kinachozusha hofu zaidi ni hali ya uchakavu wake pasi na matengenezo. Kwa namna lilivyo na miti ilivyootea ndani yake na kutokeza nje, ni kama limetelekezwa. Kama ni mwenyeji wa Dar es Salaam tangu miaka ya kabla ya 1998, Motel Ajip ilikuwa miongoni mwa vijiwe maarufu vya starehe Dar es Salaam, ikitajwa kuwa hoteli iliyoyakutanisha makundi ya watalii lukuki hasa kutoka Italia. Hata hivyo, kumekuwa na taarifa tata juu ya mmiliki halali wa jengo hilo ambalo licha ya kuwa na hali hatarishi, mamlaka zimeonekana kusuasua kuchukua hatua kuokoa maisha ya watu kabla hakujatokea madhara. Kinachoshangaza ni uwepo wake katika eneo muhimu kwa biashara, lakini halina mpangaji wa makazi wala biashara, huku Mwananchi likiarifiwa, imekuwa hivyo tangu mwaka 1998, huduma za hoteli zilipositishwa. Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lilipo jengo hilo, umedai kuanza ufuatiliaji baada ya malalamiko hayo, ingawa nao umesema hauna taarifa za kina kulihusu. "Wewe ndiyo unayenipa taarifa. Nitawatuma watu wa mazingira ili waende wakaangalie usalama wa jengo. Tutafuatilia," alijibu Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alipoulizwa iwapo Serikali ina mpango wowote kuhusu jengo hilo. Siku nne baada ya kauli hiyo ya Mpogolo, gazeti hili lilimtafuta Ofisa mazingira wa halmashauri ya jiji hilo kujua iwapo ameanza ufuatiliaji na alisema hahusiki na jukumu hilo. "Mimi sihusiki na mambo hayo, wasiliana na Mhandisi wa Jiji ndiye mwenye mamlaka namajego yote," anasema Ofisa Mazingira huyo wa Ilala. Mmiliki huyu hapa… Ingawa majibu ya Serikali yanaonyesha sintofahamu ya mmiliki halali, uchunguzi wa gazeti hili umebaini jengo hilo linamilikiwa na kampuni ya Wellworth Group of Companies yenye ofisi zake katika jengo la Raha Tower, Mtaa wa Maktaba jijini Dar es Salaam. Kulingana na chanzo cha kuaminika ambacho Mwananchi imezungumza nacho, kampuni hiyo chini ya Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wake, Gulam Ismail, ililinunua jengo hilo, tangu mwaka 2011. Ununuzi wa jengo hilo, ulihusisha na jengo la Hotel Embassy iliyopo takriban mita 200 kutoka ilipo Ajip, kinaeleza chanzo hicho. "Wakati Gulam (CEO wa Wellworth Group) ananunua hoteli hizo(Ajip na Embassy) ilipita miaka 13 tangu ilipofungwa Machi mwaka 1998 na kusababisha wafanyakazi 150 wapoteze ajira," kinaeleza chanzo hicho kilichohudumu ndani ya jengo hilo kwa miaka kadhaa. Uchunguzi zaidi umebaini kabla ya Wellworth Group, jengo hilo lilikuwa chini ya mwekezaji, Karmali Juma na wanawe. Karmali na wanawe walinunua asilimia 40 ya hisa ambazo Serikali ilikuwa inazimiliki katika jengo hilo kwa Dola za Marekani 538,640 miaka ya 1990. Tangu hapo Serikali haikuwa sehemu ya mmiliki wa jengo hilo tena, badala yake Karmali na wanawe ndiyo lililokuwa chini yao. Kauli ya mmiliki Ilipotafutwa kampuni ya Wellworth Group kueleza kuhusu jengo hilo, Ofisa wa Sheria na Utawala wa kampuni hiyo, Saimon Nguka alikiri kulimiliki jengo hilo. Hata hivyo, alieleza pamoja na kulimiliki, inashindikana kufanya lolote kwa kuwa, jengo hilo lina kesi mahakamani kwa muda mrefu sasa. “Ni vigumu kulizungumzia zaidi, kitu pekee nachoweza kujibu ni kwamba jengo lina kesi mahakamani. Sina cha kuzungumza zaidi,” alijibu Nguka katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo. Yapo mengi kama Ajip Ofisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji hilo, Emmanuel Kiwia anasema si hilo tu, katika Wilaya ya Ilala kuna majengo mengi yaliyoachwa kama magofu bila kuendelezwa. Kwa sababu kuna majengo, anasema inakuwa vigumu kuchukua hatua, ingekuwa ardhi iliyoachwa bila kuendelezwa hatua zingechukuliwa ikiwemo kuitaifisha. Hata hivyo, aneleza kila aliyeacha jengo lake bila kuliendeleza ana sababu, ikiwemo kuwa na kesi mahakamani na wengine mikopo benki. "Majengo mengi hayajaendelezwa mjini na mengi ukifuatilia kila mmoja ana sababu zake, wapo wenye kesi mahakamani," anasema. Hata hivyo, anakiri hakufuatilia kujua mengi kuhusu jengo hilo, ingawa mengi huwa na sababu za kutoendelezwa. Alipoulizwa kuhusu umiliki, anasema hana taarifa zaidi na anapendekeza atafutwe Msajili wa Hazina kwa kuwa kuna wakati jengo hilo lilikuwa chini ya umiliki wa Serikali. Alipotafutwa kuhusu hilo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu anasema jengo hilo linamilikiwa na mwekezaji binafsi na si sehemu ya mali za Serikali. Hata hivyo, Mchechu naye anaweka wazi hajamjua mwekezaji huyo binafsi ni nani, isipokuwa taarifa alizonazo ni kwamba lipo chini ya umiliki wa mtu binafsi. "Si jengo la Serikali. Kwa ninavyojua jengo hilo linamilikiwa na sekta binafsi tena ni kampuni zinashirikiana," anasema Mchechu. Hudumu kwa miaka 100 Kwa kawaida jengo kama jengo linapofanyiwa matengenezo mara kwa mara hudumu kwa miaka 100, kama inavyofafanuliwa na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Edwin Nnunduma. Kulingana na viwango vya ujenzi nchini, Mnunduma anasema jengo la namna hiyo hudumu miaka 100 bila kuanguka baada ya kujengwa, kama litafanyiwa matengenezo. "Kitaalamu ukarabati unapaswa kufanywa kulingana na eneo jengo lilipo na mazingira yake. Kila baada ya miaka 10 kitaalamu unapaswa ufanye matengenezo madogo, kinyume na kufanya hivyo halitafika miaka 100," anasema.
Siku ya kazi haikuwa kikwazo kwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Mkoa
Siku ya kazi haikuwa kikwazo kwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Mkoa wa Mbeya, kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho mkoani humo. Maandamano hayo yamefanyika jana (Jumanne), siku ambayo kimsingi ni katikati ya wiki na isingetarajiwa umati huo kujitokeza kwa kuwa yamefanyika katika siku ya kazi. Hata hivyo, maandamano hayo ni mwendelezo wa hatua ambayo chama hicho iliianza Januari 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kilipoandamana hadi katika ofisi za Umoja wa Mataifa kupeleka malalamiko yao. Malalamiko hayo ni Serikali kuchukua hatua dhidi ya ugumu wa maisha kwa wananchi, Serikali isikilize maoni ya wananchi, kadhalika iridhie kuanza mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Licha ya umati uliojitokeza kushiriki maandamano hayo yaliyohusisha safari ya kilomita 30.4 kwa ujumla kutokea maeneo mbalimbali, baadaye mvua kubwa iliyonyesha ilikatisha utamu wa hotuba za viongozi zilizopangwa kutolewa katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa kutamatisha shughuli hiyo. Katika mkutano huo ulioanza saa 10:05 jioni ni viongozi wanne pekee ndiyo walipata nafasi ya kuhutubia taifa, huku viongozi wa kitaifa, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti bara, Tundu Lissu wakikosa nafasi hiyo kutokana na mvua kubwa. Ilivyokuwa Katika maandamano hayo, viongozi wa kitaifa wa chama hicho waligawanyika katika maeneo matatu. Mbowe alianzia Mbalizi, Lissu akitokea Uyole, huku Mnyika akianzia Isanga na makutano ya wote yalikuwa katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe. Safari ya Mbowe kutokea Uyole hadi katika makutano yaliyopangwa, ilikuwa na umbali wa takriban kilomita 18, Lissu kilomita nane na Mnyika ni Kilomita 4.5 zote zikijumuisha safari ya kilomita 30.4 ya maandamano katika Mkoa huo. Katika maeneo yote wananchi walionekana kuitikia kwa wingi, huku Jeshi la Polisi likionyesha ushirikiano kama ilivyokuwa katika maandamano ya Dar es Salaam. Katika hali isiyotabirika, msafara wa Lissu ulikutana na msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko. Kukutana kwa misafara hiyo kulizua mzozo kati ya waandamanaji na Jeshi la Polisi likiongozwa na Kamanda wake, Benjamin Kuzaga. Baada ya mzozo huo uliodumu kwa takribani dakika nne, Jeshi la Polisi lilitumia busara na kupisha kwa kutumia njia ya mchepuko na kuondosha msafara wa Dk Biteko. Hotuba Kwa upande wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, aliyejitambulisha kuwa Kiongozi wa Taasisi ya Sauti ya Watanzania, Dk Willibrod Slaa alitumia dakika tano za hotuba yake kujenga hoja mbili. Moja ya hoja zake hizo ni kuweka sawa tafsiri ya taasisi hiyo ya Sauti ya Watanzania, akisema si chama cha siasa kama inavyopotoshwa na wengi, bali ni watu waliojiunga kushinikiza mabadiliko katika taifa. “Tunapambana na Serikali dhidi ya gharama za maisha, tunapambana na Serikali kupata Katiba Mpya ili tufanye uchaguzi vizuri,” alisema. Hoja ya pili ya mwanasiasa huyo aliyewahi kutangaza kukacha siasa za ndani ya vyama, ilikuwa ni kile alichokisema Rais Samia Suluhu Hassan hapaswi kuwaeleza wananchi kwamba muda uliobaki hautoshi kufanya mabadiliko ya Katiba. Hoja yake hiyo, aliijenga kwa msingi kwamba, Katiba iliyopo ilitengenezwa na watu wasiozidi 20 na kwa siku chache hivyo inawezekana kuifanyia mabadiliko kwa muda mchache. Alilisisitiza hilo kwa kueleza Rais Samia ni mwajiriwa wa Watanzania na hivyo wananchi ndiyo wanaopaswa kumwandikia mkataba wa ajira na si yeye mwenyewe kufanya hivyo. “Tunaungana na Chadema kwa nguvu zote na tutaungana na Aasasi na wale wote wanaopigania, kupunguza gharama za maisha na wale wote wanaopambana tupate Katiba Mpya,” alisema Slaa. Hotuba ya Dk Slaa ilifuatiwa na Wakili Boniface Mwabukusi, aliyetumia takriban dakika saba, akidokeza kuendelea kwa kesi dhidi ya mkataba wa uendelezaji na uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kati ya Serikali na DP World. Katika kauli yake hiyo, Mwabukusi alisema pamoja na uamuzi wa awali wa mahakama ya mkoa wa Mbeya kuhusu shauri la mkataba huo, wanatarajia kwenda katika mahakama ya rufaa kuendelea na kesi hiyo. “Kuna watu wanasema suala la bandari limekwisha tunawaambia hivi, tulishasema na tunarudia tena. Bandari ni urithi wetu haitauzwa kamwe wala hautakwenda kwenye mikono ya mgeni,” alisema. Alisema Serikali ya CCM inakabidhi mali za asili kwa mikataba ya kizembe kupitia mtu anayejiita muadilifu kutoka Mbeya ndiye anayekaa kuongoza Bunge anajiita Spika. “Mungu anapoumba eneo lolote anakupa ardhi, mbingu yako na mipaka yako ambayo haiwezi kugawanyika au kuwekwa kwenye mikono ya wageni,” alisema. Alieleza Serikali ya Tanzania inakabidhi rasilimali za asili kwa mikataba isiyofaa kupitia mtu anayejiita mwadilifu kutoka Mbeya anayekaa katika bunge kuliongoza kwa jina la Spika. “Kwa hili tuna wajibu wa kuomba radhi kwa watanzania wote kwa aibu tulioisababisha, sisi wazee wetu kina Mwangoka hawakuwahi kuwa wa ovyo wa kulifanyia hivi watanzania,” alisema. Hoja nyingine iliyoibuliwa na Mwanasheria huyo ni kile alichodai anaiambia Serikali kwamba Tanzania ni nchi inayoundwa na makabila yenye mila, itikadi, mfumo wa maisha na maeneo yao ya asili. “Wamasai kwao ni Ngorongoro, kwa hiyo wana Mbeya popote mlipo mjue adui wa kwanza wa Tanzania ni Spika wa Bunge, Tulia Ackson Mwansasu,” alisema. Alieleza kazi inayopaswa kufanywa na wananchi ni kuhakikisha kiongozi huyo wa muhimili huo wa Serikali harejei tena bungeni katika uchaguzi mkuu ujao. Kuhusu sababu za kuiunga mkono Chadema, “Mungu huwa anainua chama anainua watu, anainua taasisi kusimama kwa ajili yake, hakuna mahali utamuona Mungu akitembea, tuiunga mkono Chadema.” Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alitumia takriban dakika tano za hotuba yake, akidokeza kile alichokiita figisu za kuzuia mkutano huo, akimtaja Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa kama mmoja wa waliohusika na hilo. “Namuonya DC Benno Malisa, amewaita Bajaj wote leo kule Mkapa ili wasiwepo hapa, sasa Malisa kwa bahati mbaya sana Malisa anapenda bata, anapenda kuzurura kwenye maeneo yetu. “Tutampiga marufuku asitembee usiku kama ataendelea kutuingilia kwenye masuala yetu ya siasa Mbeya Mjini,” alisema mwanasiasa huyo. Alitumia jukwaa hilo pia kueleza Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko aliyetaka kuwagonga na gari walipokuwa kwenye maandamano, akisema alipaswa kuambatana nao ili awaeleze wananchi wa Mbeya lini watapata umeme. “Sisi hatuna tatizo naye, alitakiwa aje hapa, tumkaribishe kama Naibu Waziri Mkuu, ili kupitia umma huu wa Mbeya awaambie Watanzania ni lini watapata umeme wa uhakika na sio kuja kutugonga na gari wakati tupo kwenye maandamano,” alisema. Aliahidi kuendelea kushusha maandamano hayo katika ngazi za chini kuanzia Kata hadi Mitaa.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na maboresho yaliyofanywa katika bandari y
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na maboresho yaliyofanywa katika bandari ya Dar es Salaam, kuna haja ya kuongezwa gati namba 13 hadi 15 ili kuongeza ufanisi wa bandari hiyo. Katika kufanikisha kazi hiyo, Profesa Mbarawa amezikaribisha kampuni za uwekezaji kutoka Misri kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye ujenzi wa magati hayo. Kauli ya Profesa Mbarawa inatokana na kile alichoeleza, licha ya maboresho yaliyofanywa na Serikali katika bandari hiyo, bado kuna msongamano wa meli, akidokeza kwa sasa zipo takriban 18 zinasubiri kuhudumiwa. Hata hivyo, Oktoba 22, mwaka huu Serikali ilisaini mkataba na Kampuni ya Dubai Port World (DP World) wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4 hadi 7 wa bandari ya Dar es Salaam. Kulingana na mkataba huo, Gati namba 0 hadi 3 katika bandari hiyo yatatumiwa kwa pamoja kati ya DP World na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa ajili ya shughuli nyingine za kibiashara na Serikali. Hatua hiyo, ilifanyika ikilenga kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa kuwa, kuongeza ufanisi wa utendaji katika Bandari ya Dar es Salaam. Profesa Mbarawa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika kikao cha Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania na Wizara ya Uchukuzi ya Misri kilichohusu ushirikiano wa uwekezaji katika sekta ya uchukuzi. Alisema kuna haja ya kuongeza magati katika bandari hiyo, ili kupunguza msongamano wa meli zinazohudumiwa. Alieleza magati hayo anatarajia yajengwe kwa ushirikiano na wawekezaji kutoka katika taifa la Misri. "Pamoja na maboresho ya bandari yaliyofanywa na Serikali bado hivi sasa kuna takriban meli 18 zinasubiri kuhudumiwa. "Yote yatafanyika lakini hayatafaa kama hatutajenga magati mapya na kufanikisha hilo, tunahitaji kushirikiana na wenzetu wa Misri," alisema. Katika hotuba yake hiyo, Profesa Mbarawa alisema licha ya maboresho yaliyofanywa na Serikali katika bandari hiyo, bado kuna changamoto ya msongamano wa meli bandarini. Kuhusu ushirikiano kati ya Misri na Tanzania, alisema utawezesha watu wa Tanzania na Misri kubalilishana ujuzi na hatimaye kukuza uchumi. Akihitimisha kikao hicho, Profesa Mbarawa alimuomba Waziri wa Uchukuzi wa Misri kuridhia kuwapokea watanzania kadhaa watakaokwenda kujifunza uendeshaji wa Mradi wa Reli ya Kisiasa (SGR). Ombi lake hilo, limetokana na kile alichoeleza, Misri ina uzoefu mkubwa wa uendeshaji wa SGR, hivyo ni vema wakati Tanzania Julai mwaka huu ikitarajia kuanza mradi huo, wawepo wataalamu waliopata ujuzi huo. Ombi lingine aliloliwasilisha kwa Waziri huyo ni ushirikiano kati ya Chuo cha Baharia cha Tanzania na Taasisi ya Mafunzo ya Ubaharia ya Misri. Hata hivyo, alutaka kikao hicho kifungue milango ya ushirikiano kati ya mataifa hayo katika sekta ya uchukuzi. Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa alizikaribisha kampuni za Misri kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), maboresho ya bandari za Tanzania na Reli katika Majiji ikiwemo Dar es Salaam na Dodoma. Katika hotuba yake kwenye kikao hicho, Waziri wa Uchukuzi nchini Misri, Luteni Jenerali Kamel Alwazeer alieleza kuridhishwa na fursa za uwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini na kwamba wapo tayari kuwekeza. Kitakachofanyika, alisema ni kuwasilisha maswali kadhaa kuhusu sekta hiyo kwa Wizara ya Uchukuzi Tanzania ili kupata ufafanuzi kabla ya kuanza uwekezaji. "Tutawasilisha maswali yetu kupitia Ubalozi wetu wa hapa (Tanzania) kwenda Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania ili tupate ufafanuzi kwa ajili ya kuanza uwekezaji," alisema Alwazeer. Hata hivyo, alisema kama hatua ya mwendelezo wa kikao hicho, amemkaribisha Profesa Mbarawa kwenda Misri Kwa mazungumzo kama hayo. "Sisi tupo tayari kuwekeza na kubadilishana uzoefu tulionao kwa watendaji wa Tanzania ili kuongeza ushirikiano wetu na kuhakikisha Tanzania inanifaika," alisema.
Kama ulidhani kupaa kwa bei ya bidhaa kumeishia kwenye sukari pekee mambo ni tofauti, hali hiyo imeb
Kama ulidhani kupaa kwa bei ya bidhaa kumeishia kwenye sukari pekee mambo ni tofauti, hali hiyo imebainika hata katika bidhaa nyingine za nafaka, vikiwemo viazi, vitunguu na pilipili hoho. Kuongezeka kwa bei ya bidhaa hizo, kunazusha hofu kwa waumini wa dini ya kiislamu ambao Machi 10 au 11, mwaka huu wanatarajia kuanza ibada ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan. Bidhaa hizo za nafaka na sukari, ndizo hasa zinazotumika zaidi katika maandalizi ya futari kwa waumini wa dini hizo na hatua ya kuongezeka bei kunaibua tafsiri kuwa Ramadhan hii huenda ikawa miongoni mwa zile ngumu. Hali ilivyo mtaani Kwa upande wa sukari, kwa mujibu wa wakazi wa baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, kilo moja inauzwa kati ya Sh4,500 hadi Sh5,000 huku Arusha hali ikiwa mbaya zaidi, kilo moja ya bidhaa hiyo inapatikana kwa Sh5,000 hadi Sh6,000. Bei hizo za sukari zinaendelea kipindi ambacho zimepita takriban wiki mbili tangu, Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), itangaze bei elekezi ya bidhaa hiyo ambayo ni kuanzia Sh2,800 na isizidi Sh3,200. Uamuzi wa kutangaza bei hiyo elekezi, ulitanguliwa na kutolewa vibali vya uagizaji wa tani 50,000 za sukari nje ya nchi na tayari imeshaanza kuingia na kusambazwa, lakini hali imebaki kuwa tete. Matumaini pekee kuhusu kushuka kwa bei ya sukari yamebaki kwa viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo, ambavyo baadhi vimeanza uzalishaji bila kueleza kiwango sahihi. Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Kilombero Sugar inayozalisha Bwana Sukari, Derick Stanley alieleza kiwanda hicho kinaendelea na uzalishaji kwa sasa, isipokuwa si kwa kiwango ambacho kilikuwa kinazalisha awali. Stanley aliweka wazi kuwa, uwezo halisi wa kiwanda hicho ni kuzalisha kati ya tani 600 hadi 700 kwa siku, lakini kwa sasa kinazalisha pungufu zaidi. “Kwa sasa tunazalisha kidogo mno kutokana na hali ya mvua za El-Nino. Kimsingi tunasuasua lakini hatujasitisha uzalishaji,” alisema Derick. Kwa upande wa kiwanda cha Bagamoyo Sugar chenye uwezo wa kuzalisha tani 160 kwa siku, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Bakhresa Group inayomiliki kiwanda hicho, Hussein Sufian alisema wameanza kuzalisha ingawa kwa kiwango kidogo. “Tunaendelea na uzalishaji lakini kwa kiwango kidogo sana, hatuwezi kusema ni kiasi gani kwa sababu kinatofautiana siku hadi siku kutokana na hali inavyokuwa,” alisema. Kulingana na Sufiani, kinachoamua uzalishaji zaidi ni kutengemaa kwa hali akimaanisha mvua zitakapokata. Mbogamboga, nafaka Gunia moja la vitunguu lililokuwa linauzwa kwa Sh250,000 hadi Sh300,000 kwa sasa linapatikana kwa Sh500,000 hadi Sh550,000 katika soko la Mabibo, Dar es Salaam kama anavyoeleza Mwenyekiti wa Madalali wa Vitunguu na Viazi katika soko hilo, Maulid Ally. Hali si mbaya sana kwa upande wa viazi mbatata, alisema gunia linapatikana kwa Sh70,000, imeongezeka Sh10,000 kutoka bei ya awali ambayo ni Sh60,000. “Ndoo moja ya viazi hivyo (mbatata) inauzwa kati ya Sh15,000 hadi Sh20,000, zamani iliuzwa Sh13,000,” alisema Ally. Bei ya pilipili hoho ni balaa tupu, kiroba kilichokuwa kinauzwa Sh80,000 kwa sasa kinauzwa kati ya Sh250,000 hadi Sh280,000, kulingana na Mudy Ngoma anayeuza bidhaa hiyo, katika soko la Mabibo. Ahueni ipo kwenye karoti na nyanya ambazo zenyewe zimeshuka, kwa mujibu wa Ngoma. Kiroba kidogo cha karoti kinauzwa Sh45,000 hadi Sh50,000 ilhali awali kiliuzwa Sh100,000, huku tenga la nyanya linauzwa Sh50,000 kutoka Sh60,000. Kwa mujibu wa Ngoma, kupanda bei kwa baadhi ya bidhaa hizo kumetokana na kuadimika kwake sokoni, hivyo wafanyabiashara wanauza bei wanayotaka. Futari usiseme Katika soko la Buguruni, Katibu wa wafanyabishara, Juma Kizuki alisema kumekuwa na bei zisizoridhisha kwa bidhaa za mizizi tangu ilipoanza Februari mwaka huu. “Kwa mihogo tumepokea gari nane wakati kwa kawaida huwa tunapokea gari 24 hadi 25 na roba moja linauzwa Sh150,000 kutoka Sh70,000 ya awali,” alisema. Kwa upande wa viazi vitamu, alisema roba linauzwa Sh150,000 hadi Sh160,000 badala ya Sh54,000 iliyokuwa inauzwa awali. Nafaka afadhali Wakati mbogamboga zikishuhudiwa kupanda, hali ni shwari kwa bidhaa za nafaka. Mwenyekiti wa soko la Tandale, Juma Dikwe alisema gunia la mahindi limeshuka bei kutoka Sh90,000 miezi mitatu iliyopita hadi Sh60,000 huku kilo ikiuzwa Sh600 kutoka Sh900. “Maharage yameshuka kutoka Sh350,000 kwa gunia moja hadi Sh250,000 huku kilo ikitoka kuuzwa Sh3500 hadi Sh2500,” alisema. Kwa upande wa mchele, alisema gunia lililokuwa linauzwa kwa Sh400,000 sasa linauzwa kwa Sh300,000 kwa ule wa daraja la kwanza huku kilo iliyokuwa ikiuzwa Sh4000 sasa ni Sh3000. "Mchele wa daraja la chini kabisa kwa sasa gunia ni Sh200,000 na kilo ikiwa Sh2000," alisema mwenyekiti huyo. Kushuka kwa bei ya bidhaa hizo za nafaka, mwenyekiti huyo alisema kunatokana na wingi wa upatikanaji wake uliosababishwa na mavuno makubwa kutoka kwa wakulima. Alieleza kwa sasa sokoni hapo, wanapokea magari kati ya 100 hadi 200 kwa siku kutoka Mikoa mbalimbali yanayoleta nafaka tofauti na awali ambapo magari 50 tu ndiyo yaliyokuwa yanafika. Alieleza kuna matarajio ya bei ya mahindi kushuka zaidi kwa kuwa wiki hii nafaka hiyo mpya kutoka Tanga inatarajia kuingia.
Mambo matatu yamebainika kuwa chanzo cha bei ya sukari kuendelea kupaa, licha ya Serikali kuagiza ta
Mambo matatu yamebainika kuwa chanzo cha bei ya sukari kuendelea kupaa, licha ya Serikali kuagiza tani 50,000 nje ya nchi na kupanga bei elekezi ya bidhaa hiyo. Mambo hayo ni changamoto katika utaratibu wa usambazaji, mahitaji makubwa yanayozidi sukari iliyoagizwa na janja janja za wauzaji wa rejareja. Sababu hizo zinabainika katika kipindi ambacho, bei ya bidhaa hiyo madukani ni kati ya Sh5,000 hadi Sh6,000 kwa kilo, kinyume na bei elekezi ya Serikali inayoanzia Sh2,700 na isiyozidi Sh3,200 kwa kilo. Hatua ya Serikali kupanga bei ya bidhaa hiyo inatokana na kile kilichoelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli kuwa, sukari iliyoagizwa imesamehewa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Kulingana na kampuni zilizopewa vibali vya usambazaji wa sukari iliyoingia kutoka nje ya nchi, kila moja imepokea mzigo wa kontena tatu zinazojumuisha kati ya tani 70 hadi 80 na wote zimeshausambaza. Mahitaji makubwa Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Vraj Distributors iliyopewa kibali cha kusambaza sukari Dar es Salaam, Treecash Shah alisema mzigo alioupokea ni kontena tatu zinazojumuisha tani 79.5 na tayari wote umeshasambazwa kwa wateja. Kutokana na ukubwa wa mahitaji, alisema kati ya wateja waliomfuata kila mmoja alitaka zaidi ya mifuko 200, lakini ameshindwa kuwasambazia kwakiwango hicho. “Ilibidi nisambaze mifuko 100 hadi 200 kwa mteja mmoja ili angalau wengi wapate. Maana kwa sukari niliyoletewa ingeisha kwa mteja mmoja tu,” alisema msambazaji huyo. Aliongeza badala ya Februari 9, yeye alipokea mzigo wa sukari, Februari 10, mwaka huu na alitumia siku moja kuusambaza. “Mimi nilikuwa nauza Sh2,800 kwa kilo moja ili angalau kila mtu hadi wale masikini wapate chai,” alisema msambazaji huyo wa Dar es Salaam. Murichi Shomari ni mfanyabishara wa sukari soko kuu la Mtwara alisema bidhaa hiyo imefika lakini imekwisha kutokana na ukubwa wa mahitaji. Alieleza kupokea mifuko 530 ya sukari na kwamba yote imekwisha, huku wateja wakiendelea kuhitaji bidhaa hiyo. Said Mtandi mkazi wa Mtwara Mjini alisema sukari iliyoletwa ni ndogo isiyolingana na mahitaji. “Yaani tumejikuta wengi kwenye eneo moja na sukari haijatutosha hii inaonyesha bado mahitaji makubwa ya sukari ikilingalisha na sukari iliyoletwa,” alisema. ‘Inasambazwa wapi’ Kwa baadhi ya wafanyabiashara wa rejareja kumjua msambazaji na mahali inaposambazwa kimekuwa kitendawili kwao, kama anavyohoji mmiliki wa duka la rejareja aliyejitambulisha kwa jina la Ngewa. Alihoji nani anayesambaza na anasambazia wapi, kwa sababu madukani haipo na wafanyabiashara wanaihitaji. Hata hivyo, aliibua hoja nyingine ya kuendelea kwa uhaba kwa kile alichoeleza, sukari iliyoagizwa (tani 50,000) ni ndogo kulingana na mahitaji ya sasa. “Tani 50,000 ni sawa na mifuko 1,000 ya kilo 50 ya sukari. Hizo tani 50,000 hazitoshi hata Wilaya ya Temeke ya Mkoa wa Dar es Salaam pekee,” alisema. Alisema dukani kwake pekee anahitaji karibu mifuko 30 ya kilo 50 ya sukari na ana uhakika itakwisha haraka itakapofika. “Mimi mwenyewe sina sukari natamani mzigo unifikie. Tunasikia habari ya wasambazaji lakini hatuwaoni wala hatujui wako wapi, sukari haifiki madukani,” alisema mfanyabiashara huyo. Licha ya hoja ya mahali inaposambazwa sukari hiyo kutoka kwa mfanyabiashara huo wa rejareja, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya DMG Trading and Distribution Ltd, Masangula Ryakitimbo alisema kampuni hiyo imepokea kontena tatu zenye jumla ya tani 80. DMG iliyopewa kibali cha kusambaza sukari katika Mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Pwani, mwakilishi wake alieleza mzigo wote uliopokelewa nao umeshasambazwa kwa wateja katika Wilaya za Ubungo, Kigamboni, Ilala na Temeke mkoani Dar es Salaam. Kulingana na Ryakitimbo, kila kontena lilikuwa na sukari ya wastani wa tani 26.5 na kontena la kwanza lilipofika ilisambazwa kwa wateja siku hiyo hiyo. “Kontena la pili lilifika Ijumaa (Februari 9) na lingine Jumapili (Februari 11, mwaka huu) na kila moja lilipofika tulihakikisha ndani ya saa 8 linasambazwa,” alisema. Kwa sukari waliyoipokea alieleza kilo moja waliuza kwa Sh2,800 kwa kila mteja na mzigo ulikuwa ukisambazwa kwa kumfuata mteja dukani kwake na wenye uhitaji wa haraka walifika katika kampuni hiyo kufuata. Alifafanua kontena la kwanza lilihudumia wastani wa wateja 18, la pili wateja takriban 50 zikiwemo shule za msingi za bweni na la tatu lilihudumia wateja 25. Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo kutoka kwa wateja, lakini Serikali imeahidi kuendelea kuleta mzigo zaidi. “Tayari kulishakuwa na uhaba na bei ilishapanda, tusitarajie mzigo ukiingia leo eti bei itashuka leo leo, bado itachukua siku kadhaa ndiyo bei iwe sawa. Hili tunaliona huko madukani sukari inahitajika sana,” alisema. DMG inayosambaza sukari katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, alisema bidhaa hiyo wameisambaza kwa wateja wao wa siku zote kwa kuwa walianza shughuli hizo tangu muda mrefu. Wiki moja tatizo kuisha Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Gerard Mweli aliahidi changamoto iliyopo itamalizika ndani ya wiki moja baada ya usambazaji kuongezeka kwa kadri sukari iliyoagizwa itakavyoingia nchini. Aliwatoa hofu hata waumini wa dini ya kiislamu wanaotarajia kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, akisema wataanza ibada hiyo ikiwa tayari sukari imeshuka bei. Wauzaji rejareja lawamani Pamoja na hilo, Mweli alieleza uwepo wa changamoto kwa wauzaji wa rejareja akidokeza inawezekanaje wauze bei kubwa ilhali Serikali imesamehe kodi ili kushusha bei ya bidhaa hiyo. “Kuna shida kwenye mauzo ya rejareja, Serikali imeshatekeleza wajibu wake wa kwanza wa kuhakikisha sukari inaanza kuingia kwa sasa tupo kwenye wajibu wa pili wa kuhakikisha inashuka bei, kwa kuwa iliyoingia imesamehewa kodi,” alisema. Hata hivyo, mtendaji mkuu huyo wa wizara hiyo alifafanua kinachofanya biashara ya sukari isifuate misingi ya soko ni udhibiti wa uagizaji uliofanywa na Serikali. “Kuna watu wanalalamika eti kwanini Serikali iingilie bei ya sukari, kwanini tusiingilie wakati tumewekeza fedha yetu kwa kusamehe kodi? Kama wakitaka tusiingilie maana yake turuhusu kila mtu aagize sukari. “Tukifanya hivyo, matokeo yake viwanda vya ndani vitakufa. Tumewapa wachache vibali vya kuagiza ili kudhibiti kila mtu asiagize. Wenzetu watuelewe wasione hii ni Serikali ya kiimla inasimamia bei, tunasimamia kwa sababu tumewekeza fedha yetu kwa kusamehe kodi,” alisema Mweli.
Safari ya mwisho wa maisha ya duniani ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa itakamilikia kijijini k
Safari ya mwisho wa maisha ya duniani ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa itakamilikia kijijini kwao Ngarash, Monduli mkoani Arusha. Katika kijiji hicho, ndiko mwanasiasa huyo aliyewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali serikalini atazikwa Februari 17, mwaka huu. Lowassa aliaga dunia Februari 10, mwaka huu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Pamoja na taarifa ya maziko yake, watu wake wa karibu waliozungumza na Mwananchi wamefichua uhalisia wake nje ya mtazamo wa umma ambao aghalabu umemshuhudia kupitia majukwaa ya kisiasa. Miongoni mwa watu wake wa karibu ni Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba aliyemtaja kuwa mwanasiasa aliyesimamia anachokiamini, huku wengine wakieleza namna mbalimbali walivyoshirikiana naye. Taarifa ya maziko yake, ilitolewa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam jana na Msemaji wake binafsi, Aboubakar Liongo. Alisema ratiba rasmi ya mazishi itaanza Februari 13, 2024 itakayohusisha taratibu zote za kiserikali. "Taarifa zaidi kuhusu mazishi itatolewa baadaye lakini kwa sasa, maziko yatafanyika Ngarash Monduli mkoani Arusha siku ya Jumamosi saa 8 mchana," alisema Liongo. Usiyoyajua kuhusu Lowassa Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi ni miongoni mwa marafiki wa karibu wa Lowassa, alimtaja kuwa mmoja wa walimu wake katika utendaji serikalini. Alieleza alipoteuliwa kwa mara ya kwanza, hakuwa na ujuzi wa uongozi wa kisiasa ndani ya Serikali, hivyo Lowassa ndiye aliyesimama kama mwalimu wake kumshauri. Wakati huo Lowassa alikuwa Waziri Mkuu na kwa mujibu wa Karamagi, ndiye aliyekuwa mshauri wake hadi alipopata uzoefu. "Katika utendaji wangu wa kazi, alikuwa anajipa ushauri wa hapa na pale kama kuniongoza na kwa kujua kwamba mimi ni mara ya kwanza kuteuliwa serikalini," alisema. Mtu wa kutimiza ahadi Nje ya siasa, alieleza Lowassa ni mtu mwema ambaye aghalabu anachoahidi ndicho anachokifanya. Wema wake, alisema unathibitishwa na kauli za watu mbalimbali ambao hata hawamfahamu wanasifua na kueleza mazuri waliyowahi kufanyiwa naye. "Anaonekana hakuwa mtu anayependa watu waonewe au wateseke, kila mahali alipogundua kwamba kuna uonevu umetokea aliibuka. "Alionekana kuwa mtu anayependa haki itokee, hakutaka watu waonewe," alisema. Alieleza katika maisha yake amejifunza kuwa rafiki wa kweli kutoka kwa Lowassa, jambo ambalo mara nyingi amekuwa akilionesha. Warioba Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba alimtafsiri Lowassa kuwa mtu wa rika la tatu la makundi ya uongozi tangu Serikali ya awamu ya kwanza hadi sasa. Alisema kundi la kwanza liliwahusisha kina Rashid Mfaume Kawawa, la pili yeye na tatu ni kina Lowassa. Hata hivyo, alieleza pamoja na milima na mabonde aliyopitia kiongozi huyo, walikuwa pamoja wakati wote kwa mazungumzo na kujadiliana mambo mbalimbali. "Nilikuwa najua msimamo wake, pamoja na matatizo aliyopitia lakini hakuwahi kukata tamaa," alisema. Alisema mwanasiasa huyo aliamini katika elimu na ajira hasa kwa vijana. "Wakati wa uongozi wake hasa Waziri Mkuu alikua anachukua maamuzi hata magumu na zaidi kazi nyingi alizofanya alikuwa mfuatiliaji mzuri wa utekelezaji," alisema. Alieleza hilo kwa kurejea uamuzi wa Lowassa kujenga shule za Sekondari za Kata, kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Shinyanga. Alisema mara chache wamekuwa wakikutana kwa ajili ya kubadilishana mawazo. "Mara ya mwisho kukutana ilikuwa Muhimbili nilipokwenda kumuona lakini hali yake haikuwa nzuri," alisema Alisema Lowassa alikuwa kiongozi aliyesimamia msimamo wake na hakutetereka. Kapinga Kwa upande wa Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alisema atamkumbuka kwa mambo matatu ambayo kimsingi ni alama na funzo la uongozi kwa vijana. Aliyataja mambo hayo ni uzalendo, kuthamini watu kwa sababu ya utu wao na si madaraka waliyonayo, kadhalika kuweka ajenda ya maendekeo ya nchi mbele. Nyakati zake ngumu Rafiki yake mwingine, Gooluck Ole-Medeye alisema miongoni mwa nyakati ngumu alizowahi kuzipitia Lowassa ni pale alipoamua kuondoka CCM na kuhamia Chadema. Kwa mujibu wa Ole-Medeye, ugumu huo ulitokana na mapenzi aliyokuwa nayo mwanasiasa huyo kwa CCM. Lowassa aliihama CCM Julai 28, 2015 baada ya jina lake kukatwa na chama hicho katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo na John Magufuli ndiye aliyepitishwa kuwa mgombea wa chama hicho. Alisema Watanzania ndiyo waliochagiza afanye maamuzi hayo. Alisema wakati jina lake linakatwa Watanzania walionyesha kiu ya kumtaka awe kiongozi wao, ndiyo maana alitafuta jukwaa lingine litakalofanikisha haja ya wananchi. "Unakumbuka wakati ule alifanyiwa kitendo kibaya na Katiba ya chama ilikiukwa na ninaamini hivyo hadi leo, ndiyo maana akaamua kutafuta jukwaa lingine la kuhakikisha anatimiza haja ya kuwatumikia watanzania kama walivyohitaji," alisema Ole-Medeye aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Serikali ya awamu ya tatu. Akikazia hoja hiyo, Karamagi alisema mwaka 2015 ndiyo wakati uliokuwa na hekaheka zaidi katika siasa kwa Lowassa kuliko kipindi kingine chochote. Hekaheka hizo, alisema zilitokana na uamuzi wa mwanasiasa huyo kuondoka CCM na kuhamia Chadema. Hata hivyo, Karamagi alisema ili usifikie wakati kama huo tena ni muhimu CCM inapofanya uteuzi wa wagombea wake wake isimuonee mtu. "Tujaribu kufuata taratibu zetu zote za Chama wakati wa uteuzi, tukioneana tutapata upinzani ndani ya chama," alisema Karamagi ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera. Ilivyokuwa msibani Mbali na hao waliozungumza, viongozi wengine mbalimbali wamehudhuria nyumbani kwa Lowassa kutoa salamu za rambirambi, akiwemo mwenza wa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi. Wengine ni Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, Mkuu wa Majeshi, Jacob Mkunda, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi na mawaziri wa wizara mbalimbali. Msiba huo kwa siku ya kwanza umehudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki walipokuwa wanaingia na kutoka. Saa 10:25 Makamu wa Rais Dk Philip Mpango na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana waliwasili nyumbani hapo.
Kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi na mapenzi, mabadiliko ya utendaji wa Jeshi la Polisi na kudumishwa
Kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi na mapenzi, mabadiliko ya utendaji wa Jeshi la Polisi na kudumishwa kwa utawala wa sheria ni miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa na viongozi wa dini kama suluhu ya matukio ya kutoweka kwa watu. Mengine yaliyoonekana kuleta jawabu la matukio hayo, kwa mujibu wa viongozi hao wa dini ni kudumishwa kwa maadili, watu kurudi katika imani za dini na wenye mamlaka kutenda haki. Mapendekezo ya viongozi hao wa dini, wanaharakati na wanazuoni, yanaibuka kipindi ambacho kumekuwa na matukio mengi ya kutoweka au kutekwa kwa watu katika maeneo mbalimbali nchini, jambo linalotajwa pia kuzua taharuki. Vuguvugu la kukithiri kwa matukio hayo, liliibuliwa la gazeti hili hivi karibuni liliporipoti kuhusu uwepo wa wananchi wengi wanaolalamikia kutoweka kwa ndugu zao kwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mfunzo wa CCM, Paul Makonda katika ziara yake inayoendelea katika Mikoa 20. Ukiachana na waliolalamika kwa Makonda, msururu wa waliotoweka au kutekwa ni mrefu. Ndani yake yumo aliyekuwa mfanyabiashara na fundi simu eneo la Kariakoo Dar es Salaam, Innocent Elias Liveti (34) maarufu Macheni aliyefikisha siku 66 bila kujulikana alipo. Kwa mujibu wa mashuhuda na picha za video zilizochukuliwa na kamera za usalama, Desemba Mosi, 2023 saa 1:30 asubuhi Liveti alikuwa amekaa mbele ya duka lake lililopo Mtaa wa Narung'ombe, walitokea watu wawili waliovalia kofia na kuingia naye ndani ya gari na kuondoka naye. Mwingine anayeingia kwenye msururu huo ni mfanyabiashara Mussa Mziba (37), ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Mziba Empire Investment Ltd, yenye ofisi zake Mikocheni, Dar es Salaam anayedaiwa kutoweka baada ya kutekwa pia. Mziba alitekwa na watu wawili waliofika ofisini kwake saa 2 usiku Desemba 7 wakijitambulisha kuwa ni maofisa Polisi. Hadi sasa ni siku 58, Mziba hajulikani alipo. Matukio hayo yalitanguliwa na kutoweka kwa Charles Wetinyi, aliyedaiwa kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa polisi eneo la Mugumu wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Oktoba 23, 2023. Amefikisha siku 106 hajulikani aliko. Pia, Wilson Damas alitoweka tangu kampeni za uchaguzi mwaka 2020 sasa ni zaidi ya miaka mitatu hajulikani aliko pamoja na Richard Kayanda, wote wakazi wa Nyandoto Tarime, Mkoa wa Mara. Wengine waliopotea kwa pamoja Desemba 26, 2021 ni waliokuwa mafundi simu na wafanyabiashara katika soko la Kariakoo, kadhalika wapo wengine baba na mwanawe waliopotea mkoani Mwanza. Kauli ya Waziri Wingi wa matukio hayo uliibua mjadala bungeni jijini Dodoma juzi, wabunge walipomtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni atolee ufafanuzi juu ya kinachoendelea. Katika kulitekeleza hilo, Msauni aligusia vyanzo vya matukio hayo ni wivu wa mapenzi, ushirikina, kugombania ardhi, urithi, kujiteka, visasi na utapeli. Akichangia katika taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwa mwaka 2023, Masauni alisema hoja ya wananchi kutekwa inaweza kutoa taswira kama labda kuna tatizo kubwa sana na kuzua taharuki kubwa katika jamii. Alisema kwa takwimu alizonazo kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2023, asilimia 72.5 ya watu waliopotea walishapatikana. “Sio kwamba watu wanapotea hakuna kilichofanyika Polisi hawawapati wahalifu wahanga sio sahihi, kuna kazi kubwa imefanyika na matunda yake ni hayo niliyozungumza.” “Vyanzo vilivyobainika ni wivu wa mapenzi, ushirikina, kugombania ardhi, mpaka kujiteka ipo, visasi, utapeli, asilimia kubwa ya vyanzo ni mambo haya,” alisema. Dosari utawala wa sheria Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Charles Kitima alitafsiri wingi wa malalamiko ya watu kupotea ni kama ishara ya kushuka kwa utawala wa sheria nchini. Aliijenga hoja yake hiyo kwa kurejea ibara ya 14 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, inayompa mtu haki ya uhai, kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake. “Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria,” inaeleza ibara hiyo iliyonukuliwa na Kitima. Kadhalika, alidokeza juu ya mikataba mbalimbali ya kulinda uhai wa watu na haki ya kuishi ambayo Tanzania imeisaini na kuiridhia na kwamba utekaji na kutoweka kwa watu ni dalili mbaya. Katika kusisitiza kuporomoka kwa utawala wa sheria, kiongozi huyo wa kiroho alirejea matukio ya kutoweka kwa Ben Saanane na kupigwa risasi kwa Tundu Lissu (Makamu Mwneyekiti wa Chadema Bara), lakini Serikali haikuonekana kuchukua hatua zozote hadi sasa. Ben Saanane alitoweka Novemba mwaka 2016 katika mazingira ya kutatanisha, huku Lissu akipigwa risasi Septemba 2017. Kwa mujibu wa Kitima, Tanzania inapaswa ijitafakari juu ya namna ya kulinda na kuthamini uhai wa Watanzania. “Tunapaswa kutafakari juu ya namna gani ya kulinda haki ya uhai. Serikali ifanye kazi yake na vyombo vya usalama vitumie sheria katika kuwawajibisha wale wote wanaoonekana wamevunjwa sheria,” alisema. Mamlaka zihurumie wa chini Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Nuhu Mruma alisema kinachopaswa kufanywa ni mwenye mamlaka awe na huruma kwa mtu wa chini na yule wa chini awe na heshima kwa mamlaka. Sambamba na hilo, alitaka kila mwenye mamlaka ahakikishe anatenda haki kwa kuwa ndiyo inayosimama kutengeneza mtengamano wa amani na utulivu wa moyo. “Lakini kila mwenye eneo la kufanyia kazi atende haki kwa kuwa ndiyo inayosimama kutengeneza mtengamano wa mustakabali wa amani na utulivu wa moyo,” alisema Sheikh Mruma. Pamoja na hilo, alieleza kulaani matukio hayo huku akiwataka watu warudi kuwa na imani za dini, ndizo zitakazowaondoa kuwa na mitazamo na fikra za kujichukulia sheria mkononi. “Hata kama katendewa isivyo na mwenzake, si jambo jema kuchukua sheria mkononi na kuamua kumuangamiza mwenzake ama kwa kumteka au kumficha,” alisema. Alisema kama mtu anaonekana mbaya sheria na taratibu zifuatwe katika kumuelimisha na kumuadabisha. Migogoro itatuliwe Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Mchungaji John Kamoyo aliungana na Masauni akisema migogoro inachangia watu kujichukulia sheria mkononi. “Inategemea na mtu anauchukuliaje mgogoro, wapo wanaouchukulia kawaida lakini wapo wanaoumizwa nao kiasi cha kufanya maamuzi hatarishi,” alisema. Lakini kwa ujumla wake, alieleza matukio hayo na kauli hiyo inaonyesha ishara ya umuhimu wa kuwa na viongozi watakaokuwa na uwezo wa kutatua migogoro isifikie hatua mbaya. “Nchi ina migogoro mingi ya ardhi ambayo haijatatuliwa na nafikiri wananchi wanapoingia kwenye uchaguzi ni vema kuchagua watu watakaosaidia kutatua migogoro,” alisema. Alieleza kwa sasa familia nyingi zinaishi kwa uhasama kwa kuwa hazina maelewano na mzizi wa hayo ni migogoro. “Mengi yanayotokea ni athari za migogoro,” alisema Mchungaji huyo. Polisi ibadilike Mwanaharakati wa haki za binadamu, Fulgence Massawe alisema kilichoelezwa na Masauni huenda kisiwatosheleze watu, iwapo jeshi la polisi halitabadili utendaji kazi wake. Eneo la utendaji wa polisi aliloeleza lina haja ya mabadiliko ni ukamataji, akisema wengi wanakama bila kufuata sheria kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. “Unakuta Polisi anakamata kimya kimya hatoi taarifa popote hata kwa ndugu wa aliyekamatwa. Inakuwa rahisi kwa mhalifu kujipitisha katika mwanya huo naye akamteka mtu na watu wakadhani ni polisi wapo kazini,” alisema. Massawe ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchechemuzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), alieleza mara nyingi wanaotekwa wanakosa usaidizi kwa kuwa wananchi wanadhani polisi wapo kazini. Alisema watu hawanyooshei kidole jeshi la polisi kwa sababu halifanyi uchunguzi, bali utaratibu wake wa kukamata unaruhusu uvunjifu wa sheria. Kadhalika mtaalamu huyo wa sheria alieleza wingi wa malalamiko dhidi ya matukio hayo, unatokana na hofu za yaliyofanyika katika utawala wa awamu iliyopita. Vyombo haviaminiki Kwa mtazamo wa kisiasa, Mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe alisema kilichoelezwa na Masauni hakitoshi kumridhisha mtu juu ya matukio ya kutoweka kwa watu yanayoendelea kulalamikiwa. Dk Kabobe anatamani Serikali ingepiga hatua moja zaidi kujua kwanini baada ya watu kuzurumiana mashamba kama inavyoelezwa na Masauni waamue kutekana, badala ya kushitakiana kwenye vyombo vya sheria. “Hii inaonyesha wazi kuwa kuna tatizo kwenye mifumo yetu ya uongozi au haki. Inawezekana watu wamekosa imani na vyombo vya sheria hadi wanaamua kutekana,” alisema. Uthibitisho wa watu kupoteza imani dhidi ya vyombo hivyo, unatokana na kile alichoeleza Dk Kabobe, katika ziara ya Makonda wananchi mbalimbali pia wanalalamikia kukosa haki licha ya kuvifuata vyombo hivyo. “Haiwezekani watu wamsubiri Makonda ilhali katika eneo hilo kuna mamlaka mbalimbali zenye wajibu wa kushughulika na kesi hizo,” alieleza mwanazuoni huyo.
Takriban Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni), zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ma
Takriban Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni), zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya Reli ya Tanzania-Zambia, yenye umri wa karibu miongo mitano sasa. Taarifa kuhusu gharama za maboresho ya reli hiyo, imetolewa na taifa la China, kupitia balozi anayeliwakilisha taifa hilo nchini Zambia, Du Xiaohui Februari 8, mwaka huu. Reli hiyo inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Mashariki na Mji wa Kapiri Mposhi nchini Zambia ni miongoni mwa miradi mikubwa ambayo taifa la China iliwahi kufadhili ujenzi wake uliokamilika mwaka 1975. Tangu kukamilika kwa ujenzi wake, miaka 49 iliyopita reli hiyo baadaye ilihitaji matengenezo makubwa ambayo kimsingi ndiyo yatakayofufua ushindani wake. Katikati ya wiki hii, Xiaohui aliwasilisha pendekezo la mradi wa matengenezo ya reli hiyo kwa Waziri wa Usafirishaji wa Zambia, Frank Tayali. “Gharama za uwekezaji zitakuja miaka ijayo,” alinukuliwa balozi huyo alipokuwa akizungumza katika matangazo mubashara yaliyorushwa na vyombo vya habari nchini Zambia. Hata hivyo, hatua ya matengenezo hayo inakuja miezi kadhaa baada ya Serikali ya Tanzania na Zambia zisaini mkataba wa kukabidhi uendeshaji wa reli hiyo kwa kampuni inayomilikiwa na taifa la China. Katika kuthibitisha taarifa ya pendekezo lililowasilishwa na China, Mwananchi ilimtafuta Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara Februari 9, mwaka huu ambaye hata hivyo hakuwa tayari kulitolea maoni suala hilo. Uamuzi wa kutozungumzia suala hilo, unatokana na kile alichoiambia Mwananchi, ni vema kuandaa mahojiano kwa ajili ya ufafanuzi zaidi wa hilo. “Tupange mahojiano kwa ajili ya kulielezea suala hili kwa uzito wake,” alisema Profesa Kahyarara. Mbali na kauli hiyo ya Kahyarara, Mwananchi ilithibitishiwa juu ya kuwasilishwa kwa pendekezo hilo, ingawa bado halijakabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania na Tazara. Uthibitisho huo ulitolewa na Mkuu wa Uhusiano kwa Umma wa Tazara, Conrad Simuchile aliyesema anafahamu kuhusu China kuwasilishwa pendekezo, ingawa bado halijafikishwa Tazara. “Limekabidhiwa wizarani nchini Zambia, lilipaswa kuwasilishwa kwa Tanzania ambaye ni mshirika pia. Tutakuwa na nafasi nzuri ya kuzungumzia hilo baada ya nyaraka hiyo kuwasilishwa kwetu,” alisema. Desemba 12, mwaka jana, kabla ya China kuwasilisha pendekezo la maboresho ya mradi huo, Tazara ilitangaza kuunda kikosi kazi kutoka kampuni ya uhandisi ya China (CCECC), kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa reli hiyo. Simuchile alipoulizwa kuhusu kikosi kazi hicho, alijibu tayari kimeshakamilisha kazi yake na taarifa zake ndizo zilizotumika kuandaa pendekezo hilo, linaloitarajiwa kuwasilishwa Tazara pia. Pamoja na jukumu la ukaguzi huo, taarifa ya Tazara ya mwaka jana, ilisema kikosi kazi hicho kilikuwa na jukumu la majadiliano kuhusu masuala muhimu ikiwemo mifumo ya uendeshaji na usimamizi wa mamlaka, mapendekezo ya mpango wa fedha unaosimamiwa na Benki ya Maendeleo ya China (CDB), kodi za ndani, sera na mambo mengine. Kulingana na taarifa hiyo, kikosi kazi hicho, kilikuwa kikiongozwa na Shirika la Reli ya Ethiopia-Djibout, Peng Danyang, linaloendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Ethiopia na Djibout na CCECC. "Majadiliano haya yanalenga kuboresha pendekezo la kuifufua Tazara na kuliandaa shirika lizingatiwe na watu wote,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo. “Mapendekezo hayo yatachunguzwa na Kamati ya Pamoja ya Ufundi ya Tanzania na Zambia, ikifuatiwa na tathmini ya Kamati ya Uongozi ya Tanzania na Zambia na hatimaye, pendekezo lililoboreshwa litawasilishwa kwenye kikosi kazi cha Tatu, ambacho kinachojumuisha Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania na Zambia, kadhalika Mabalozi wa China nchini Tanzania na Zambia,” inaeleza taarifa hiyo. China ilijenga na kufadhili ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,860 (maili 1,156) katika miaka ya 1970, lakini tangu ilipoharibika imekuwa ikifanya kazi taratibu. Reli hiyo iwapo itaboreshwa inatarajia kuleta ushindani na reli nyingine ambayo Marekani inaunga mkono ujenzi wake, itakayounganisha Zambia kwenye bandari ya Lobito hadi Pwani ya Atlantiki ya Angola. Zote zikiwa ni sehemu ya juhudi za kupanua njia za usafirishaji nje ya nchi kwa migodi ya shaba na kobalti kutoka Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). China, Tanzania na Zambia zitaifufua reli hiyo kwa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, kulingana na mwakilishi wa Beijing mjini Lusaka. Tangazo hilo lilikuja siku moja kabla ya Marekani kuwa mwenyeji wa kongamano la uwekezaji katika ukanda wa Lobito nchini Zambia, huku mshauri wa Rais Joe Biden wa masuala ya nishati na uwekezaji, Amos Hochstein na Rais Hakainde Hichilema wakiwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu.
Kutokana na wizi wa transfoma 85 uliofanyika katika kipindi cha Januari mwaka huu, Shirika la Umeme
Kutokana na wizi wa transfoma 85 uliofanyika katika kipindi cha Januari mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema thamani ya hasara iliyopatikana kutokana na wizi huo ni takriban Sh500 milioni. Taarifa kuhusu wizi wa transfoma hizo, iliwekwa wazi bungeni jijini Dodoma juzi na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu umeme. Hata hivyo, wapo wanaohusisha wizi wa vifaa hivyo na watumishi wa shirika hilo, wakihoji inawezekanaje mtu asiyefahamu masuala ya umeme aibe tranfsoma. “Wanaozifungua transifoma ni wenye kampuni zinazojihusisha na ujenzi wa laini za umeme au watu binafsi wanaojihusisha na vitu vya umeme ambao wakishazichukua wanakwenda kuziuza kwa hao wasambazaji. “Na ili uifungue, kwanza huwezi kuwa mtu mmoja na lazima wawasiliane na watu waliozijenga, kama ni Kibaha wanatafuta mwenyeji anayehusika na eneo hilo ambao ni Tanesco au Rea na huyo mwenyewe ndio anawaelekeza nendeni kafungue eneo fulani,” alisema mmoja wa wafanyakazi katika kampuni ya usambazaji umeme vijijini aliyeomba hifadhi ya jina lake. Akifafanua kuhusu wizi huo jana, Msemaji wa Tanesco, Kenneth Boymanda alisema kinachoibiwa si transfoma yote kama wengi wanavyodhani, bali ni vifaa ndani ya mtambo huo. Vifaa vinavyoibwa, alisema ni kopa inayopatikana ndani ya transfoma na wakati mwingine mafuta. “Wezi hawaibi transfoma yote hapana. Ndani ya transfoma kuna kopa hiyo ndiyo inayoibwa, au mafuta lakini wezi wa mafuta wamepungua kwa sasa ni kopa,” alisema. Alieleza kopa hiyo inakwenda kuuzwa na hata hivyo haina gharama kubwa kama inavyodhaniwa, ni kiasi kidogo cha fedha kati ya Sh15,000 hadi Sh20,000. Hata hivyo, alisema tayari timu ya usalama wa miundombinu ya shirika hilo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama inaendelea na upelelezi kubaini waliohusika. Alisema uchunguzi unaendelea kufanyika kubaini wezi ni kina nani na wanauzia wapi hicho wanachokiiba, ili mtandao wote udhibitiwe. Alipoulizwa kuhusu hasara, alisema inawakumba wananchi na Tanesco kwa ujumla. Kwa upande wa wananchi, alisema transfoma moja inahudumia kati ya wananchi 50 hadi 200, hivyo ikiharibiwa wote hao watakosa huduma. Kwa upande wa Tanesco, alieleza hasara inakuja pale zinapohitajika fedha kwa ajili ya ununuzi wa transfoma nyingine ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi. Kwa transfoma hizo zilizoibiwa, alieleza hasara yake ni takriban Sh500 milioni. Hata hivyo, alisema wizi wa vifaa hivyo hutekelezwa na watu wenye ujuzi kiasi wa umeme, kwa kuwa ili uibe kifaa hicho inabidi ukitoe kwenye nishati hiyo. “Kuwa na ujuzi wa umeme haimaanishi eti uwe mtumishi wa Tanesco. Siku hizi kuna vyuo vingi vya umeme, lakini kuna wale vibarua leo anachimba shimo kesho akipata ujuzi kama si mwaminifu anaweza kuja kuiba,” alisema. Kwa upande wa mfanyakazi huyo wa kampuni ya usambazaji wa umeme, aliongeza: “wakishafungua wanakwenda kuwauzia kampuni zinayojenga sehemu nyingine, wanachokwepa ni kununua transifoma mpya. Alisema kiwandani transifoma zinaanzia Sh15 milioni hadi Sh30, “sasa anaona kwa nini atoe Sh20 milioni au Sh30 milioni wakati anaweza kupata kwa Sh5 milioni au Sh10 milioni.” “Kwa hiyo katika hili la wizi wahusika ni wenyeji kwa sababu wanapokwenda wanakwenda kama kuzifanyia matengenezo, wanaifungua na kuondoka nayo na hata wananchi wakiona wanadhani wanatengeneza kumbe ndio wanaziiba,” alisema. Kilimanjaro Katika hatua nyingine, mkoani Kilimanjaro wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kujipatia zaidi ya Sh8 milioni kwa kuwaunganishia watu 21 umeme kinyemela. Kulingana na Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, Simon Maigwa, wananchi hao wanaoishi Kibosho wilayani Moshi, kila inadaiwa kila mmoja alitozwa Sh400,000 kuunganishiwa huduma hiyo. Hata hivyo, alisema tayari watu hao wamekamatwa na miongoni mwao, yupo kinara anayedaiwa kuwa kiongozi wa vishoka mkoani humo. "Tumeshamkamata kiongozi wao mkubwa wa hicho kikosi, amekuwa akishirikiana na mtandao mkubwa uliopo ndani ya watumishi wa Tanesco, wote hawa tumewakamata na tuko kwenye hatua nzuri," alisema Maigwa. Akizungumzia hilo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori alisema watu hao wamekuwa wakiihujumu Serikali kwa manufaa yao wenyewe na kuikosesha Serikali mapato yake. Alisema hadi sasa watu 21 maeneo ya Kibosho , wilayani humo wamefungiwa umeme kinyume na taratibu na kila mwananchi amelipishwa Sh400,000 na fedha hizo haziingi serikalini. Alipotafutwa Meneja wa Tanesco mkoani hapa, Grace Ntungi kuhusiana na kukamatwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo , alisema hawezi kuzungumia suala ambalo lipo kwenye upelelezi na kwamba viachiwe vyombo hivyo viendelee na kazi yake. "Hizi taarifa zipo chini ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi, taratibu za uchunguzi zitakapokamilika tutatoa pia taarifa, ili tusije vuruga taratibu za Jeshi letu la polisi." alisema Meneja huyo.
Kutokana na msongamano wa malori yanayosubiri kushusha Kopa katika bandari kavu, Bandari ya Dar es S
Kutokana na msongamano wa malori yanayosubiri kushusha Kopa katika bandari kavu, Bandari ya Dar es Salaam imepanga kuitumia bandari kavu ya Kwala kuwa kituo cha kushushia mizigo yote ya madini hayo. Kitakachofanyika kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho ni malori yote kupeleka mzigo huo Kwala, kuondoa msongamano uliopo katika bandari kavu mbalimbali ikiwemo ya Ubungo. Uamuzi huo unafikiwa kukabili kukithiri kwa msongamano wa malori katika bandari kavu mbalimbali, ikiwemo ya Ubungo, ambayo kwa sasa madereva wanalazimika kusubiri kwa takriban siku 10 kabla ya kushusha mzigo, kama anavyoelezwa na Ismail Issa. Issa ambaye ni dereva anayesubiri kushusha mzigo wa Kopa katika msongamano wa malori Ubungo, amefika eneo hilo tangu Januari 22, mwaka huu hadi jana hakuwa amefanikiwa, akisubiri waliotangulie washushe kwanza. "Hapa tunasubiriana, wenzio wakishusha wewe unasubiri kuna wakati kunajaa na ikitokea hivyo inabidi subiri mzigo upungue. Hapo ndiyo huwa tunasubiri muda mrefu zaidi," alisema Issa. Manemba Osward ameonyesha kukosa tumaini la kuondoka katika eneo hilo kwa kile alichoeleza, ndiyo kwanza amefika juzi. "Wenzangu waliomaliza wiki hapa bado wapo hawajui wataondoka lini. Mimi ndo nimefika jana (juzi), sioni kama nitaondoka nipo nipo sana," alieleza. Kinachomuumiza Lucas Lucas dereva mwingine aliyekwama katika msongamano huo ni kile anachoeleza, kusalia eneo hilo ni hasara kwake. Hasara hiyo inatokana na ufafanuzi wake kuwa, bosi wake amegoma kumlipa posho tangu siku nne zilizopita, akimdai anamwambia hayupo nje ya Mkoa au nchi. "Amesema hawezi kunipa posho kwa sababu nipo Dar es Salaam na nyumbani ni hapa hapa ningekuwa nje ya Mkoa angenilipa. "Sio kwamba hataki Mzee wa watu (bosi wake) ameishiwa anapata hasara sana. Nipo hapa wiki ya pili leo, kila siku analipa ada ya kuchelewesha kontena, amenilipa posho na sasa amechoka," alisema. Lucas hana cha kufanya zaidi ya kuendelea na kazi kwa kile anachoeleza, "ukiacha kazi wenzio wanasubiri kwa hamu, madereva ni wengi sana Kaka wanasubiri gari." Lakini, wamiliki wa malori nao, wanaufananisha msongamano huo na mlango wa hasara kweye biashara, hasa wakitaja tozo la Dola 60 kwa siku ya kuchelewesha kurudisha kasha. Mbali na hasara kwa wamiliki wa malori, Mussa Hassan dereva mwingine aliyekwama katika eneo hilo, alisema kuna hofu ya wizi wa Kopa. "Ukiibiwa mzigo tajiri hatakuelewa, hapa kuna walinzi lakini hawatoshelezi kudhibiti uhalifu, Pwani huko tunasikia kuna wenzetu wameibiwa. Mtu anaogopa hata kutoka kwenda kula," alisema. Kutokana na hali hiyo, Mrisho aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kwamba bandari hiyo imepanga kuwa na kituo kimoja cha kushusha mzigo wa Kopa. Kituo hicho, alisema ni bandari kavu ya Kwala iliyopo Kibaha mkoani Pwani. Alisema tayari mazungumzo kati ya Bandari ya Dar es Salaam na wadau wa usafirishaji yanaendelea kufanyika kufanikisha hilo. Kulingana na Mrisho, Kopa ndiyo mzigo mkubwa unaosafirishwa kutoka bandari ya Dar es Salaam, ndiyo maana uamuzi wa kuwa na eneo moja la kuhifadhi umefanyika. “Mzigo mkubwa unaoingia katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirishwa ni Kopa na kwa sababu hiyo tumeona kuwepo eneo moja la kuhifadhia mizigo hiyo,” alisema bila kuweka wazi kiwango cha mzigo huo. Hata hivyo, alieleza kumekuwa na malalamiko ya kukwama kwa malori ya kopa Misugusugu mkoani Pwani, ndiyo maana uamuzi wa kupelekwa katika bandari kavu hiyo unapangwa kufanyika. “Mizigo hiyo ya Kopa itafikishwa katika bandari ya Kwala kisha itasafirishwa kwa njia ya reli kutoka Kwala hadi bandari ya Dar es Salaam, tayari kusafirishwa kwenda nje,” alieleza. Wasafirishaji Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Wadogo wa Malori Tanzania (Tamstoa), Chuki Shaaban alisema hatua hiyo itaponya donda ndugu lililokuwa likisumbua wakati wote. Kwa sasa, alieleza malori yanakaa hadi siku 20 kusubiri kushusha mzigo wa kopa kutokana na uhaba wa maeneo ya kuhifadhi mzigo huo, jambo ambalo ni hasara kwa wasafirishaji. Iwapo lori litakaa kwenye foleni kwa siku moja, alisema msafirishaji atagharimika malipo ya posho ya dereva na dola 60 kwa siku ada ya kuchelewesha kasha. “Lakini msongamano huu umekuwa ukisababisha hadi mizigo kuibiwa. Wiki mbili zilizopita malori matatu yameibiwa mzigo wa kopa,” alisema. Alueleza uamuzi wa kupeleka mzigo huo katika bandari kavu ya Kwala utapunguza msongamano na changamoto nyingine zinazowakabili wasafirishaji. Ufanisi wa bandari Sambamba na uamuzi huo, Mrisho alieleza kuanzia Februari 1 hadi jana, zaidi ya meli 10 zimehudumiwa. Kwa Januari pekee, alisema meli 86 zimehudumiwa, licha ya changamoto ya mvua za Eli-Nino zilizokuwa zinaendelea kunyesha. Alieleza bandari hiyo kwa sasa inahudumia tani milioni 2.5 kwa mwezi, kutoka tani milioni 1.6 kwa muda huo. Kwa upande wa makasha, alieleza zaidi ya 90,000 yanahudumiwa kwa mwezi, ukilinganisha na makasha 50,000 yaliyokuwa yanahudumiwa awali. Kwa mujibu wa Mrisho, matarajio ni kuongeza ufanisi wa huduma zaidi.
Bandari ya Dar es Salaam imepanga kupitisha mizigo yote ya Kopa katika bandari kavu ya Kwala mkoani
Bandari ya Dar es Salaam imepanga kupitisha mizigo yote ya Kopa katika bandari kavu ya Kwala mkoani Pwani kabla ya kufikishwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirishwa. Hatua hiyo, inalenga kupunguza msongamano wa malori katika bandari kavu inayotumika sasa iliyopo Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam. Kwa sasa mizigo mingi ya Kopa kabla ya kusafirishwa katika bandari ya Dar es Salaam, inapitishwa katika bandari kavu iliyopo Ubungo Maziwa na kusababisha msongamano wa malori. Msongamano huo unatokana na bandari hiyo kuwa na uwezo mdogo na hivyo kusababisha malori kusubiriana wakati wa kushusha. Desemba 29, mwaka jana, malori ya mizigo ya Kopa kutokea nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, yaling’olewa namba za usajili na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), baada ya kuegesha kwenye eneo lisilostahili yakisubiri msongamano wa kushusha mizigo katika bandari hiyo. Katika kutatua changamoto hiyo jana, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema tayari mazungumzo kati yao na wadau wa usafirishaji yanaendelea kufanyika kufanikisha hilo. Kulingana na Mrisho, Kopa ndiyo mzigo mkubwa unaosafirishwa kutoka bandari ya Dar es Salaam, ndiyo maana uamuzi wa kuwa na eneo moja la kuhifadhi umefanyika. “Mzigo mkubwa unaoingia katika bandari ya Dar es Salaam ni Kopa na kwa sababu hiyo tumeona kuwepo eneo moja la kuhifadhia mizigo hiyo,” amesema. Hata hivyo, ameeleza kumekuwa na malalamiko ya kukwama kwa malori ya kopa Misugusugu mkoani Pwani, ndiyo maana uamuzi wa kupelekwa katika bandari kavu hiyo unapangwa kufanyika. “Mizigo hiyo ya Kopa nitafikishwa katika bandari ya Kwala kisha itasafirishwa kwa njia ya reli kutoka Kwala hadi bandari ya Dar es Salaam, tayari kusafirishwa kwenda nje,” ameeleza. Wasafirishaji Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Wadogo wa Malori Tanzania (Tamstoa), Chuki Shaaban amesema hatua hiyo itaponya donda ndugu lililokuwa likisumbua wakati wote. Kwa sasa, ameeleza malori yanakaa hadi siku 20 kusubiri kushusha mzigo wa kopa kutokana na uhaba wa maeneo ya kuhifadhi mzigo huo, jambo ambalo ni hasara kwa wasafirishaji. Iwapo lori litakaa kwenye foleni kwa siku moja, amesema msafirishaji atagharimika malipo ya posho ya dereva na dola 60 kwa siku ada ya kuchelewesha kasha. “Lakini msongamano huu umekuwa ukisababisha hadi mizigo kuibiwa. Wiki mbili zilizopita malori matatu yameibiwa mzigo wa kopa,” amesema. Ameeleza uamuzi wa kupeleka mzigo huo katika bandari kavu ya Kwala utapunguza msongamano na changamoto nyingine zinazowakabili wasafirishaji.
Licha ya ugonjwa wa macho mekundu 'Red Eyes' ulioibuka nchini Tanzania kuwa tishio kwa wakazi wa nch
Licha ya ugonjwa wa macho mekundu 'Red Eyes' ulioibuka nchini Tanzania kuwa tishio kwa wakazi wa nchi hiyo, wapo wanaofaidika kutokana na kuwepo kwake. Ugonjwa huo ulioripuka tangu wiki tatu zilizopita, kwa mujibu wa mamlaka za Tanzania takriban Mikoa 17 ya taifa hilo la Afrika Mashariki inataabika nao. Wizara ya Afya ya Tanzania, wiki iliyopita ilitoa taarifa kueleza idadi hiyo ya Mikoa iliyoathiriwa, huku wagonjwa wengine wakitajwa kuambukizwa visiwani Zanzibar upande wa pili wa nchi hiyo. Kwa sababu ugonjwa huo kwa baadhi ya wagonjwa wanaumizwa na mwanga wa jua na simu, kumekuwa na mahitaji makubwa ya miwani za kupunguza mwanga inayotumiwa na wagonjwa. Hapo ndipo ule msemo wa 'kufa kufaana' unapoakisi uhalisia, mauzo ya bidhaa hiyo yameongezeka maradufu na hata bei imepanda, ukilinganisha na awali. Hassan Mpecha anayefanya biashara ya miwani, Kariakoo, Dar es Salaam Mashariki mwa Tanzania, anasema kwa sasa anauza takriban miwani 20 hadi 30 kwa siku. Mauzo hayo hayalingani na yale aliyokuwa akiuza awali, ambayo ni kati ya miwani tano hadi 10 kwa siku. Kutokana na mauzo ya sasa, kijana huyo anayeuza miwani hiyo kwa kutembeza mtaani, anasema kwa siku ana uhakika wa kuiingiza angalau Sh80,000 hadi Sh100,000. "Zamani tulikuwa tunauza miwani kwa wale wanaovaa kama urembo, haikuwa lazima aliyependa ndiye aliyenunua. Lakini sasa hivi wengi waaokuja kununua tayari wanaumwa Red Eyes," anasema. Mtanzanía mwingine anayefanya biashara hiyo, Dacoz Mobi anasema hata bei ya miwani imebadilika kwa sasa. Ile iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh2,000, kwa sasa inauzwa Sh5,000 hadi Sh7,000 kutegemea na maelewano na mteja. Pamoja na ugonjwa huo kuwa tishio kwa wananchi wengine, Dacoz anaeleza kwa upande mwingine umeibua fursa kwa vijana hasa wanaouza miwani. Kwanini miwani Wagonjwa wengi wa Red Eyes huumizwa na mwanga wa jua na simu, hivyo wanashauriwa kutumia miwani ya kupunguza mwanga ili kuepuka maumivu, kama inavyoelezwa na daktari bingwa wa Macho wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Neema Moshi. Hata hivyo, si kila miwani inastahili kutumiwa na mgonjwa, bali ile inayosaidia kupunguza mwanga ndiyo sahihi. Hoja kama hiyo ya kitaalamu inaungwa mkono na Daktari mwingine bingwa wa macho wa Hospitali ya Mloganzila, Anna Sanyiwa. Kulingana na Dk Anna, sio wagonjwa wote wanapata maumivu kutokana na mwanga, hiyo huwakuta baadhi. Lakini kama mgonjwa anasumbuliwa na hali hiyo, miwani ya kupunguza mwanga ndiyo kitu kinachoweza kumpa afua ya haraka. "Sio miwani ilimradi miwani, anapaswa kutumia miwani ya kupunguza mwanga, ili asipigwe moja kwa moja na mwanga machoni," anasema Dk Anna. Wateja wa miwani Ingawa bidhaa hiyo imekuwa hitaji muhimu kwa sasa, lakini baadhi ya wananchi wanahofu juu ya usalama wake. Dennis Malya anasema kila anayekwenda kununua lazima ajaribu kwanza, jambo linalohatarisha kuongeza maambukizi. "Tunashauriwa mgonjwa akigusa kitu kama hajasafisha mikono yake wewe usuguse. Lakini kwenye miwani wagonjwa wanajaribu kisha sisi wengine tunaenda kujaribu bila kuisafisha miwani. Hii ni hatari maambukizi yanaweza kuongezeka," anasema. Kuhusu hilo, Dacoz anasema kwa biashara ya miwani ni vigumu kutembea na maji na sabuni kuosha kila baada ya mteja kujaribu. Isipokuwa anasema baadhi yao hutembea na vitakasa mikono 'Hand Sanitizer' na kupulizia kwenye miwani kila baada ya mteja kujaribu. "Unapita mteja anajaribu miwani karibu yote, utaosha ngapi. Itakupasa ubebe ndoo ya maji, baadhi tunatumia vitakasa mikono lakini ni wachache," anasema Dacoz. Undani kuhusu Red Eyes Kwa mujibu wa Dk Neema, mgonjwa anayepona ugonjwa huo hana uwezekano wa kuambukizwa tena. Uwezekano wa mgonjwa huyo kupata maambukizi hayo, anasema utatokana na mabadiliko ya kirusi na wingi jipya la Red Eyes. "Ujue huu ugonjwa sio mpya, umekuwepo muda mrefu isipokuwa kila awali unakuja kwa kasi tofauti. Mgonjwa aliyeugua haambukizwi tena labda wimbi jipya," anasema. Lakini, unapougua ugonjwa huo, anasema makadirio ya kusalia nao mwilini ni kati ya siku tatu hadi wiki. Kupona haraka au kuchelewa, kunatokana na kinga ya mtu. Kwa upande wa Dk Anna, kuna uwezekano ugonjwa huo ukasababisha upofu, iwapo mgonjwa atatumia dawa zisizostahiki. Anasema kati ya dawa za magonjwa ya macho zipo zinazopunguza kinga ya jicho na iwapo hiyo ndiyo itakayotumika inaweza kusababisha athari zaidi kwa mgonjwa. "Kwa sababu kinga ya jicho ikipungua maana yake uniruhusu virusi washambulie zaidi kioo cha nje ya jicho na wakikishambulia zaidi hatimaye unapoteza uoni kabisa," anasema. Katika mazingira hayo, anasema ni muhimu kujiepusha na matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari wa macho. Hata wale wanaotumia dawa wanazoziita za asili ikiwemo chumvi, maji ya bahari, mkojo wa binadamu, Dk Anna anasema si sahihi kutumia. Hata hivyo, Wizara ya Afya ya Tanzania ilishatoa vipeperushi kadhaa kuelimisha jamii juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo. Matumizi ya dawa zinazoitwa za asili, ni moja ya vitu vilivyoharamishwa katika vipeperushi hivyo. Kwa upande wa walioambukizwa, Wizara hiyo imewataka kuhakikisha wanasalia majumbani ili kuepuka kuwasambazia wengine.
Kutoka kuwa na nchi wanachama 15 wa sasa, huenda Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Magharibi (Ecow
Kutoka kuwa na nchi wanachama 15 wa sasa, huenda Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) ukabaki na wanachama 12 pekee. Hatua hiyo itafikiwa iwapo juhudi za mazungumzo hazitafua dafu kuhakikisha jumuiya hiyo inasalia na idadi ya siku zote ya wanachama wake. Hofu ya Ecowas kupoteza wanachama wake watatu, inatokana na notisi iliyowasilishwa na mataifa ya Mali, Burkina Faso na Niger ya kujivua uanachama. Msingi wa uamuzi wa nchi hizo za Afrika Magharibi ni kile zilichokieleza katika taarifa yao ya pamoja ya wiki iliyopita kuwa, ECOWAS imekiuka itikadi yake na hivyo kuwa tishio kwa wanachama wake. Hicho kinachoitwa Ecowas kukiuka itikadi yake kinahusiana na hatua za hivi karibuni za Ecowas kuziwekea vikwazo nchi hizo baada ya kufanya mapinduzi ya kijeshi. Mali ilitekeleza mapinduzi hayo mwaka 2020 na 2021, Burkina Faso mwaka 2022 na Niger mwaka 2023. Katika hali ya kujibu kilichotokea, Mwenyekiti wa ECOWAS ambaye pia ni Rais wa Nigeria, Bola Tinubu alionyesha upinzani dhidi ya mapinduzi hayo, katika moja ya vikao vya viongozi wa jumuiya hiyo, kilichofanyika Julai mwaka jana. "Ecowas inakataa mapinduzi na ukiukwaji wa utaratibu wa kikatiba," alisema Tinubu baada ya kikao cha viongozi wa juu wa jumuiya hiyo kufuatia mapinduzi ya mataifa hayo ikiwemo Niger. Hakuishia hapo, alilitaka jeshi la Niger litoe mamlaka ndani ya wiki moja, kumwachilia mara moja na kumrejesha madarakani rais Mohamed Bazoum. Sambamba na hatua hiyo, kiongozi huyo wa Ecowas alisisitiza iwapo hilo halitatekelezwa umoja huo, utachukua hatua zote zinazohitajika kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger, pamoja na matumizi ya nguvu. Kadhalika, viongozi hao wa Ecowas walikubaliana kuweka vikwazo vya kifedha na usafiri kwa viongozi wa kijeshi wa Niger walioshiriki katika mapinduzi hayo. Vikwazo hivyo viliambatana na kupiga marufuku usafiri wa ndege za kibiashara za nchi za Ecowas kwenye eneo la nchi hiyo. Hatua zaidi zilihusisha kufungia mali za Niger katika benki kuu na za kibiashara za nchi za ECOWAS. Mbali na Niger, mataifa mengine wanachama wa umoja huo, Burkina Faso na Mali zilifanya mapinduzi ya kijeshi na kuishutumu Ecowas kwa hatua yake ya kupinga mapinduzi hayo. Mkataba wa Ecowas kuhusu vikwazo Ingawa mataifa hayo yanatafsiri hatua hiyo ya Ecowas dfhidi yao kama uonevu, kwa upande mwingine uamuzi wa jumuiya hiyo kuweka vikwazo kwa mataifa hayo, unahalalishwa na Ibara ya 77 ya Mkataba wa Ecowas. Hata hivyo, ibara hiyo haijaweka wazi kuhusu tukio la mapinduzi ya kijeshi kuwa moja ya sababu zinazochagiza mwanachama wake kuwekewa vikwazo. Kulingana na ibara hiyo, Ecowas itamwekea vikwazo mwanachama wake, pale ambapo atashindwa kutekeleza wajibu wake kwa jumuiya. Vikwazo vingine vinavyotajwa kwa mujibu wa vipengele vya ibara hiyo ni kusitishwa kwa mikopo mipya ya jumuiya au usaidizi na kusimamishwa kwa malipo ya miradi au usaidizi wa Ecowas kwa program zinazoendelea katika nchi husika. Kikwazo kingine ni kutengwa katika kuwasilisha wagombeaji wa nyadhifa za kisheria na kitaaluma ndani ya jumuiya hiyo, kusimamishwa kwa haki za kupiga kura; na kusimamishwa kushiriki katika shughuli za jumuiya. Hata hivyo, pamoja na hoja hizo za mataifa hayo matatu, swali linaloulizwa zaidi ni iwapo uamuzi wa Mali, Burkina Faso na Niger utapunguza au kuiongezea chochote Ecowas? Hakuna athari kubwa Kuondoka kwao hakutakuwa na tishio kubwa la kiuchumi kwa ECOWAS kwa kuwa zinaondoka zikiwa zimeziacha nchi nyingine zenye uchumi mkubwa zaidi, kama inavyoelezwa na Mtaalamu wa uchumi na diplomasia kutoka Tanzania, Balozi Ali Karume. “Hakutakuwa na matokeo hasi kwa kiwango kikubwa iwapo Mali, Burkina Faso na Niger zitajiondoa ndani ya ya ECOWAS kwa sababu zitaondoka huku zikiacha wanachama wengine wenye uchumi mkubwa zaidi yao, kama Nigeria na Ghana,” amesema. Zitayumba kiuchumi Badala uamuzi wa nchi hizo tatu kujitoa utazisababishia kuyumba kiuchumi, kulingana na Balozi Karume. Kuyumba kwa huko, kutatokana na kile alichoeleza kuwa, hazitakuwa tena sehemu ya wanufaika wa fursa za Ecowas ikiwemo masoko, uhuru wa biashara na viza kwa wakazi wake katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Fursa nyingine zitakazozikosa, Karume amesema ni misamaha ya ushuru na kodi za kibiashara katika mataifa wanachama. Baada ya kujiondoa, Balozi huyo aliyewahi kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Ubelgiji, Ujerumani na Italia, amesema nchi hizo zitalazimika kufanya biashara na mataifa hayo bila fursa zozote zinazotokana na kuwa wanachama wenza wao. Ukurasa mpya wa ushirikiano Kwa upande mwingine, amesema kujiondoa kwa nchi hizo katika ECOWAS kutazifungulia milango ya kutafuta washirika wengine wasio wanachama wa jumuiya hiyo. “Nchi hizo zikishajiondoa zinaweza kuamua kushirikiana na jumuiya nyingine nje na ECOWAS au na nchi yoyote duniani kwa sababu hazitkuwa zinabanwa na miiko ya ECOWAS,” ameeleza Balozi Karume ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume. Ni uamuzi sahihi kujiondoa Kwa mtazamo wake, mwanadiplomasia huyo ameeleza uamuzi wa kujiondoa kwao ni hatua muhimu na ilipaswa kuchukuliwa nao kutokana na kile ambacho jumuiya hiyo imekifanya. Licha ya mapinduzi na utawala wa kijeshi unaoendelea katika mataifa hayo, Balozi Karume amesema bado zina uhuru binafsi na ECOWAS haikupaswa kutishia kuvamia. “ECOWAS ni jumuiya ya kiuchumi, haikupaswa kuingilia masuala ya kisiasa ya nchi wanachama wake. Mbaya zaidi ni pale ilipotishia kuvamia Niger baada ya mapinduzi, haukua uamuzi sahihi. Ni sawa kwa nchi hizo kujiondoa,” amesema. Amesisitiza kwa kuwa nchi hizo zina haki ya kiutawala, hazikupaswa kuingiliwa kwenye mambo yao, badala yake ECOWAS ingeishia kujikita katika masuala ya kiuchumi kama msingi wa kuanzishwa kwake. “Lakini hatua ya kuweka vikwazo ni jambo lingine baya zaidi, kama ningepewa nafasi ya kuzishauri nchi hizo tatu, ningeziambia zijiondoe,” amesema Balozi Karume. ‘ECOWAS ijitafakari’ Mtaalamu Mwandamizi wa uchumi, Profesa Anna Tibaijuka amesema hilo ni pigo kwa ECOWAS kwa kuwa uamuzi wa nchi hizo utaitikisha jumuiya hiyo yenye nchi wanachama 15 kutoka Afrika Magharibi. Kwa upande mwingine amesema ni jambo linaloonyesha umuhimu wa jumuiya hiyo kujitafakari, kuona kwanini wanachama wake hao watatu wanataka kuondoka. “Hilo ni jambo la kusikitisha na kujitathmini kwa ECOWAS, sio kawaida mtu ataamua kujitenga na atakapojiondoa utaathirika kwa sababu utaukosa mchango wake na unavunja umoja,” amesema. Hata hivyo, mkataba wa jumuiya hiyo unaweka wazi kuwa, itachukua muda wa mwaka mmoja kwa nchi mwanachama kukamilisha michakato ya kujiondoa ndani ya Ecowas.
Jeshi la Uhamiaji limesema hatua yake ya kumkamaka mwanaharakati, Mdude Nyangali katika mpaka wa Nam
Jeshi la Uhamiaji limesema hatua yake ya kumkamaka mwanaharakati, Mdude Nyangali katika mpaka wa Namanga akielekea nchini Kenya, imetokana na maelekezo kutoka Jeshi la Polisi. Taarifa za kukamatwa kwa mwanaharakati huyo, zilisambaa kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), zikichapishwa na Wakili Peter Madeleka. Katika ukurasa wake wa X, Madeleka aliandika, “Mwanaharakati Mdude amekamatwa na Uhamiaji katika mpaka wa Namanga alipokuwa anaelekea Kenya kwa madai eti ana kesi ya uhaini kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Namanga. Kwa kuwa Mdude sio mkimbizi natoa wito aachiwe haraka.” Alipotafutwa na Mwananchi kufafanua taarifa hiyo, Madeleka alisema taarifa ya kukamatwa kwa mwanaharakati huyo ameipokea kutoka kwake mwenyewe katika Mpaka wa Namanga akielekea nchini Kenya. Alieleza sababu aliyoelezwa kuwa chanzo cha kukamatwa kwake ni kesi ya uhaini anayodaiwa kuwa nayo, ingawa kwa mujibu wa Madeleka haijulikana ya lini. “Wamemwambia ana kesi ya uhaini, mimi na wewe hatujui hiyo kesi ya lini na juzi Mdude alikuwa Dar es Salaam kwenye maandamano ya Chadema kwanini hakukamatwa hapo,” alihoji Madelaka. Hoja nyingine iliyoibuliwa na Madeleka ni utaratibu wa kisheria kuhusu kesi ya uhaini, akisema kwa kawaida kesi hizo huwa hazina dhamana imekuwaje Mdude alikuwa nje. Mbali na hoja kuhusu kesi inayodaiwa kusababisha kukamatwa kwake, Madeleka alisema kwa kuwa mwanaharakati huyo ni binadamu ana haki ya kutembea popote ikiwemo nje ya nchi. Alieleza haki hiyo inabainishwa katika Ibara ya 17 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, hivyo alikuwa na haki ya kwenda anakokwenda. Ibara hiyo 17(1) inaeleza: “Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.” Uhamiaji Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Jeshi la Uhamiaji, Paul Mselle alikiri jeshi hilo kumkamata mwanaharakati huyo. Uamuzi wa kukamatwa kwake, alisema umetokana na maelekezo kutoka katika Jeshi la Polisi Tanzania na kwamba ndilo linalomshikilia kwa sasa. “Kama unavyofahamu sisi ni walinzi wa mipaka, sisi tulimkamata baada ya kuelekezwa na jeshi la polisi na nadhani jeshi hilo ndilo linalofahamu sababu ya jambo hilo. Kwa sasa amezuiliza na jeshi la polisi,” alisema. Alisisitiza uhamiaji haina tatizo lolote na mwanaharakati huyo, badala yake uamuzi wa kumkamata umetokana na maelekezo hayo na ukizingatia wana jukumu hilo kisheria. “Sisi uhamiaji hatuna shida naye kabisa, hata sasa hivi jeshi la polisi likimuachia na tutamruhusu aendelee na safari yake bila shida,” alisema. Licha ya kutafutwa kwa simu yake ya mkono, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Maseja na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime wote simu zao ziliita bila majibu.
Baada ya ahadi kadhaa za utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Mbamba Bay, hatimaye mradi huo upo mbion
Baada ya ahadi kadhaa za utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Mbamba Bay, hatimaye mradi huo upo mbioni kuanza kutekelezwa. Awali Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliahidi kuanza utekelezaji huo Januari mwaka jana, baadaye Machi ilielezwa Sh70 bilioni zimeshatolewa na Serikali kuianza kazi hiyo. Hatimaye sasa, TPA imethibitisha kuanza utekelezaji wa mradi huo kwa gharama ya Sh80.85 bilioni kwa muda wa miaka miwili. Kwa mujibu wa taarifa ya juzi ya TPA, utekelezwaji wa mradi huo unatokana na utafiti na upembuzi yakinifu uliofanyika na kuonyesha bandari hiyo na nyingine mbili ndizo zenye sifa na vigezo vya kiuchumi na kibiashara kufanyiwa uwekezaji wa kimkakati. Mbali na Mbamba Bay bandari nyingine mbili zilizobainika kuwa na sifa hizo ni Manda na Kiwira na kwamba uwekezaji wake utasaidia kuongeza uwezo wa kutoa huduma na mapato kwa TPA. Mradi huo wa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, unatarajiwa kutekelezwa na kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Co Ltd ya nchini China. Kulingana na taarifa huo, tayari TPA imeshakabidhiana mradi huo utakaotekelezwa kwa miaka miwili na mshauri mwelekezi ambayo ni Kampuni ya Anova Consulting Company Ltd. Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa, Manga Gassaya alisema kwa sasa mradi huo utaanza kutekelezwa. Gassaya aliyezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa alisema mradi huo utakapokamilika utakuwa makamo makuu mapya ya bandari za Ziwa Nyasa. “Bandari hii itakuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na nchi za Malawi na Zambia ambazo ni soko muhimu kwa mazao ya chakula na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mwambao wa Ziwa Nyasa,” alisema. Aliongeza: “Ujenzi huu unatajwa kuwa na faida nyingi zikiwemo kuwa chanzo cha ajira kwa wananchi wa maeneo ya jirani na Mkoa wa Ruvuma.” Faida nyingine, alisema ni kuongeza kiwango cha shehena na abiria, kuchagiza maendeleo ya shughuli za kiuchumi kama kilimo, ujasiriamali na viwanda vya ngazi zote. Taarifa hiyo inaeleza mradi huo utaongeza ufanisi wa Bandari za mwambao wa Bahari ya Hindi, baada ya kuunganishwa na Mbamba Bay, kupitia ushoroba wa Mtwara.
Rais Samia Suluhu Hassan ameweka dhamira ya kuvutia uwekezaji wa Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi y
Rais Samia Suluhu Hassan ameweka dhamira ya kuvutia uwekezaji wa Dola za Marekani 1 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni) kutoka nchini Indonesia, huku akitaja sababu tano za kwanini Tanzania ni eneo sahihi la kuwekeza. Jukumu la kufanikisha upatikanaji wa uwekezaji huo, amelitoa kwa taasisi za Serikali, alipozungumza na jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Indonesia kwenye jukwaa la uwekezaji na biashara lililofanyika mjini Jakarta nchini Indonesia. Jukwaa hilo ni sehemu ya ziara ya siku tatu ya Rais Samia nchini Indonesia, aliyoanza Januari 24, mwaka huu na inatarajiwa kuhitimishwa leo. Sababu tano Katika jukwaa hilo, Mkuu huyo wa nchi alisisitiza uwepo wa utulivu wa kisiasa, mazingira bora ya kijiografia na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini kama sababu za kuwavutia wawekezaji hao. “Sekta binafsi ya nchini Tanzania inalindwa na sheria...na tuna mkataba wa kutangaza na kulinda uwekezaji na nchi nyingi na kwa Indonesia tunaendelea kujadiliana nao," alisema. Sababu nyingine iliyotolewa na Rais Samia ni uwepo wa utashi wa kisiasa na urahisi wa kufanya biashara baada ya Serikali kumtambua nafasi ya sekta binafsi kama msingi wa ukuaji uchumi. “Sababu ya tano ni kuwepo na utawala thabiti wa uchumi na fedha nchini Tanzania,” alisema Akizungumza katika jukwaa hilo, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri alisema tayari kituo hicho kimeweka.lengo la kufikia uwekezaji huo mwaka 2028. “Ni wajibu mzuri sana, lakini tunaelewa iwapo wawekezaji watakuja, Watanzania watapata kazi na ajira, tutapata walipakodi wapya, tutakusanya mapato na kuzalisha bidhaa nzuri kwa ajili ya kuuza nje. "Kabla Rais hajatuekekeza sisi kama TIC tulishabaini kuwa Jakarta ni fursa nzuri ya wawekezaji. Timu ya wataalamu ilitembelea Miji mitatu ya Indonesia Desemba mwaka jana na ilikutana na wawekezaji kama mkakati wa awali wa kuwavutia," alisema. Awali, katika mazungumzo yake na waandishi wa habari Januari 21, mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba alisema Indonesia imewekeza miradi mitano nchini Tanzania. Alieleza jumla ya gharama za uwekezaji huo ni Sh6.5 bilioni katika sekta za Kilimo, uzalishaji viwandani na ujenzi. Katika mazungumzo yake kwenye jukwaa hilo, Makamba alisema Indonesia itabaki kuwa mshirika muhimh wa Tanzania, wakati nchi hizo zikisherehekea miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia. “Hii ni ziara ya tatu ya Rais ya kwanza ilikuwa mwaka 1971 na ya pili ilikuwa mwaka 1987," alisema Makamba. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alisema taifa hilo la Asia ni miongoni mwa yale yanavyokuwa kwa kasi kiuchumi. “Ni miongoni mwa nchi 19 duniani zenye pato la zaidi ya Dola za Marekani 1 trilioni," alisema. Mikataba iliyosainiwa Katika ziara hiyo jana pia, mikataba ya ushirikiano minne imesainiwa ikiwemo wa ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu, madini na kilimo. Mkataba mwingine, ni wa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Mambo ya nje ya Indonesia katika kujengeana uwezo kwenhe diplomasia. Mingine ni kati ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) na PT, Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Taasisi ya Teknolojia ya TeknologiBandung, kadhalika chemba ya biashara ya Tanzania (TCCA), Chemba ya biashara Zanzibar (ZNCC) na chemba ya biashara ya Indonesia (KADIN). Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Samia nchini Indonesia tangu aingie madarakani, lakini ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu ulipoanza mwaka 2024. Katika mkutano na waandishi wa habari, Rais wa Indonesia, Joko Widodo alisisitiza juhudi za nchi hizo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na afya. Katika maelezo yake hayo, alisema taasisi za tiba nchini Indonesia zingetamani kukidhi haja ya mahitaji ya huduma za matibabu za Tanzania. Kadhalika, Mkuu huyo wa nchi, alieleza matarajio yake kwa Tanzania kushiriki na kusaidia katika Jukwaa la Indonesia-Afrika II lenye lengo la kuongeza ushirikiano hasa katika sekta za uchumi.
Safari ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai haki kwa njia ya maandamano ndiyo imeanz
Safari ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai haki kwa njia ya maandamano ndiyo imeanza, huku Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akisisitiza kuendelea kufanya hivyo katika Mikoa mbalimbali hadi Serikali itakapowaelewa. Msingi wa maandamano ya chama hicho ni kuishinikiza Serikali itekeleze mambo manne ambayo ni kuondoa muswada ya sheria za uchaguzi bungeni, kufanya maboresho ya Katiba, izingatie maoni ya wananchi na kupunguza gharama za maisha. Kulingana na Chadema, licha ya kupelekwa muswada ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi, bado kuna kasoro zile zile zilizokuwa zikilalamikiwa ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuendelea kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Katika kusisitiza utekelezwaji wa hayo, chama hicho jana kilifanya maandamano kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kuelekea zilipo Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yake. Akizungumza baada ya mazungumzo na UN jana, Mbowe alisema pamoja na hatua hiyo iliyofikiwa, chama hicho kitaendelea kufanya maandamano hadi pale Serikali itakapokielewa. “Tutaendelea kuandamana katika taratibu na Mikoa mbalimbali hadi wenzetu watuelewe tunamaanisha nini, kila dirisha linalofaa kugongwa litagongwa. “Ili sauti na kilio cha Watanzania kuhusu mabadiliko chanya wenye nchi yetu kikasikike kwa wale wenye kiburi na jeuri ya kuwa watawala,” alisema. Nini wamezungumza Kuhusu kilichojiri katika mazungumzo ya viongozi wa Chadema na UN, Mbowe alisema wamewasilisha barua yenye ujumbe wa malalamiko ya kero dhidi ya Serikali kwa Mratibu Mkazi wa jumuiya hiyo nchini, ili ayatume kwa Katibu Mkuu wa UN Marekani, Antonio Guterres. “Barua yetu imepokelewa kwa niaba na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, barua hiyo ikishapokelewa rasmi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tutaisambaza kwa vyombo vyote vya habari,” alisema. Kwa sasa, alieleza chama hicho kinaendelea kufuatilia na kuwasiliana na jumuiya hiyo, kitakapothibitisha kupokelewa kwa barua hiyo, kitaisambaza kwa wanahabari. Kilichomo kwenye barua Kuhusu kilichomo ndani ya barua hiyo, alisema imebeba ujumbe wa mambo yale yale ambayo aghalabu chama hicho kimekuwa kikiyalalamikia dhidi ya Serikali. “Mabango yetu yameandika, vipeperushi vyetu vimesema, kauli za viongozi mimi na wenzangu tumesema, mambo ya msingi tunayoyalalamika ni pamoja na Serikali ya CCM kutotaka kusikia maoni na mawazo ya wananchi,” alisema. Mengine yaliyohusishwa kwenye barua hiyo iliyowasilishwa UN, alisema ni haja ya maboresho ya mifumo ya uchaguzi, kupanda kwa gharama za maisha na kupatikana kwa Katiba mpya. Akizungumzia maandamano hayo kwa ujumla, Mbowe alisema yamefanyika bila yeyote kuumizwa, akisisitiza hiyo ndiyo tabia ya chama hicho iwapo Jeshi la Polisi litaelewa hoja zao. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Tundu Lissu alijikita katika haja ya kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya. Kwa mujibu wa Lissu, mahitaji ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi hayakutokana na Chadema, bali tangu miaka 30 iliyopita wakati wa tume ya Jaji Francis Nyalali. “Tume ya Nyalalai ndiyo iliyosema kwamba Tanzania inahitaji Katiba Mpya na mfumo mpya wa uchaguzi utakaokidhi matakwa ya vyama vingi. “Baada ya miaka 33 bado CCM inatuambia kwamba wao hawadhani nchi hii inahitaji Katiba Mpya au mfumo mpya wa uchaguzi,” alisema. Kwa kuwa hilo wameliomba kwa takriban miaka 30, alieleza kwa sasa wameanza kulidai kupitia maandamano barabarani na kilichofanyika ni mwanzo. Polisi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema jukumu kubwa la jeshi hilo ni suala la amani, utulivu, kuzuia vitendo vya kihalifu, kuhakikisha usalama na kusimamia sheria za nchi kuhakikisha hazivunjwi. “Sisi jukumu letu ilikuwa ni kufuatilia kwa karibu kuona kwamba haki moja inapoliliwa na kundi fulani haivunji haki ya kundi lingine ambalo nalo lipo kisheria,” alisema. Akilifafanua hilo, Muliro alisema kilichokuwa kinafanywa na jeshi hilo ni kuhakikisha maandamano hayo hayawi kikwazo cha shughuli nyingine za wananchi. “Kwa hiyo usijifanye wewe upo kwenye maandamano basi watu wengine wawe na tatizo, hicho ndicho tulichokuwa tunagombana kwenye hatua za awali. “Watu wanafikiri haki ya maandamano ni kusimamisha kila kitu, mtu mwingine hastahili kufanya kitu kingine ni wewe tu, sisi hapo ndipo tulipokuwa tunapaangalia kwa ukaribu,” alisema. Hata hivyo, kamabnda huyo aliyataka makundi yote kutawanyika kwa amani na kwamba yeyote atakayefanya jambo lenye tafsiri ya kuvunja sheria hatua zitachukuliwa dhidi yake. “Bado nasubiri kufanya tathmini ya jumla taarifa zaidi nitaitoa baadaye,” alisema. Ilivyokuwa Waandamanaji walifika katika ofisi za UN zilizopo katika barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam saa 9:30 alasiri. Baada ya kuwasili katika ofisi hizo, viongozi wanne wa chama hicho ndiyo walioruhusiwa kuingia ndani ya ofisi hizo, kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe huo. Walioingia ni Mbowe, Lissu, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bwacha), Sharifa Suleiman. Walitumia dakika 25 katika mazungumzo hayo, baadaye saa 9:55 alasiri viongozi hao walitoka katika ofisi hizo na kuzungumza na vyombo vya habari, kabla ya kuruhusu wananchi watawanyike. Baada ya mazungumzo na waandishi wa habari, Mbowe aliwataka waandamanaji kutawanyika, huku Wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kukutana katika Makao Makuu ya chama hicho Oysterbay, Dar es Salaam. Pamoja na hilo, Mbowe alisisitiza kuendelea kwa maandamano ya amani katika Mikoa mbalimbali, huku akiahidi kurudia tena katika Jiji la Dar es Salaam iwapo kinacholalamikiwa hakitafanyiwa kazi. Kadhalika, mwenyekiti huyo alieleza msimamo wa chama hicho kukubali mazungumzo na Serikali, lakini yatafanyika huku maandamano yakiendelea.
Bandari ya Tanga inatarajiwa kuwa na uwezo wa kupokea tani milioni 3 za mizigo kwa mwaka, hatua itak
Bandari ya Tanga inatarajiwa kuwa na uwezo wa kupokea tani milioni 3 za mizigo kwa mwaka, hatua itakayofikiwa kutokana na maboresho ya miundombinu mbalimbali katika bandari hiyo. Kutokana na miundombinu iliyopo sasa, bandari hiyo ina uwezo wa kupokea tani 750,000 kwa mwaka. Akizungumza mkoani Tanga, Meneja wa bandari hiyo, Masoud Mrisha alisema ongezeko la mizigo hiyo litatokana na bandari hiyo kuongezewa ufanisi na miundombinu itakayowezesha meli kubwa kuegesha. Alieleza maboresho hayo pia yanalenga kuiongezea bandari hiyo ufanisi katika kupakua na kupakia mizigo na hatimaye kuifanya kuwa lango kuu la biashara kitaifa na kimataifa. “Iwapo miradi inayotekelezwa itakamilika, tutatatua changamoto zilizopo na kuongeza ubora kwa ajili ya maendeleo ya bandari yetu,” alisema. Kuhusu mradi huo, alifafanua ulianza kutekelezwa Agosti mwaka 2023 na kampuni ya China Harbor Engineering Company (CHEC) kwa awamu mbili. Katika awamu ya kwanza, alisema mradi huo unagharimu Sh172.3 bilioni zikihusisha upanuzi wa bandari na kuongeza kina katika eneo la kuingilia kutoka mita tatu hadi 13. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika awamu hiyo, alisema ni ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uendeshaji wa bandari hiyo. Awamu ya pili ya mradi huo, Mrisha alisema itagharimu Sh256.8 bilioni itakayohusisha uwekezaji katika kina cha maji kutoka mita tatu hadi 13 na uboreshaji wa magati namba moja na mbili yenye jumla ya urefu wa mita 450. “Pia awamu ya pili itahusisha ufungwaji wa mifumo ya Tehama, bomba la maji na mifumo ya kuzimia moto ambayo ni nyenzo muhimu katika uboreshaji wa shughuli za bandari,” alisema. Aliwataka wateja kutoka mataifa mbalimbali kuhakikisha wanatumia bandari hiyo ya jirani ipasavyo, badala ya kwenda kwenye nyingine zilizopo mbali zaidi. Aliwahakikishia kutolewa kwa huduma bora kwa saa 24, usalama wa mizigo, unafuu wa gharama na kwamba bandari hiyo haina msongamano katika kupakia na kupakua mizigo. “Bandari imetayarisha vituo 50 vya kushughulikia makontena yanayohitaji uhifadhi wa baridi kwa bidhaa zinazoharibika. Kwa hivyo wakulima au wauzaji wa parachichi sasa wanaweza kutumia Bandari ya Tanga kupeleka mazao hayo kwa wateja nje ya nchi,” alisema. Hata hivyo, alitumia jukwaa hilo kuishukuru Serikali kwa kutenga Sh429.1 bilioni kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa bandari hiyo. “Ahadi ya Rais inaonyesha ari ya Serikali katika kuimarisha miundombinu ya biashara, kuwezesha na kukuza uchumi. Aidha, hatua za awali zinaendelea za ujenzi wa kontena mpya na gati za abiria,” alisema. Alieleza iwapo mradi huo utakamilika utatatua changamoto ya gharama za kushughulikia mizigo kwa wateja. Hata hivyo, alieleza kwa miaka mingi bandari hiyo ilikuwa na changamoto ya mabomba ya maji yenye kina kifupi yaliyosababisha huduma za meli zifanywe kwa mkono umbali wa kilomita 1.7 kutoka kwenye gati. “Shughuli hizo ni upakuaji wa mizigo kutoka kwenye meli hadi kwenye majahazi ambayo yalivutwa na boti kwa kamba hadi kwenye sehemu ambayo shehena inashushwa,” alisema. Akitoa historia ya bandari hiyo, Mrisha alisema ilijengwa mwaka 1888 na mwaka 1891 ilianza kufanya kazi wakati huo ikijulikana kama Marine Jetty. Mwaka 1914, alisema gati la kwanza lilijengwa huku la pili likijengwa mwaka 1954 na vyumba viwili vilivyofanya jumla ya urefu wa mita 450. “Kihistoria bandari hii ilikuwa ya kilimo, ikilenga kufanya usafirishaji nje ya nchi hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Bidhaa kuu zinazouzwa nje ni pamoja na mkonge, mbao, kahawa, chai nyeusi, alizeti na makadamia. Hata hivyo, alisema kufuatia mradi huo wa kisasa, bandari hiyo sasa inasafirisha madini aina ya shaba, huku ikiagiza malighafi, pet-coke, mabomba ya maji, malori, ammonium nitrate, klinka na sehemu za mashine.
Miongoni mwa malalamiko makubwa ya wananchi katika Mikoa mbalimbali nchini kwa sasa ni kuongezeka kw
Miongoni mwa malalamiko makubwa ya wananchi katika Mikoa mbalimbali nchini kwa sasa ni kuongezeka kwa bei ya sukari kutoka Sh2,500 na Sh3,000 hadi Sh5,000. Ongezeko hilo la bei hiyo limetokana na uhaba wa bidhaa hiyo madukani, unaosababishwa na kupungua kwa uzalishaji wa sukari viwandani. Kupungua huko kwa uzalishaji ni matokeo ya mvua zisizotabirika na El-Nino zinazoendelea kunyesha, ambazo kimsingi zinafanya viwanda visimame kuzalisha. Hayo ni sehemu ya majibu ya Serikali kuhusu ongezeko la bei ya sukari na kupungua kwa bidhaa hiyo madukani, ingawa yapo mambo yanayofikirisha kuhusu hali hiyo. Binafsi naamini kuhusu kupungua kwa uzalishaji wa sukari viwandani kulikosababishwa na mvua zinazofululiza katika kipindi hiki na hata baadhi ya wazalishaji wamelithibitisha hilo. Lakini, napata wasiwasi kuamini kama hiyo ndiyo sababu mahsusi ya kupanda kwa bei ya sukari, au kupungua kwa bidhaa hiyo sokoni. Msingi wa wasiwasi wangu ni ukweli kwamba, hii si mara ya kwanza Tanzania inakuwa na uhaba wa sukari hasa katika kipindi kama hiki. Lakini hii si mara ya kwanza, bei ya bidhaa hiyo inaongezeka katika kipindi kama hiki na aghalabu sababu zinazotajwa ni wafanyabiashara wasio waaminifu wanaficha sukari ili wapandishe bei na mambo mengine. Kila jambo kama hilo linapotokea Serikali inakuja na mkakati wa kuwasaka wafanyabiashara inayodai wameficha sukari ili kusababisha upungufu na baadaye inawakamata na taarifa zinaishia hapo. Nakumbuka Oktoba 17, mwaka 2022, Serikali ilitangaza kuwa mbioni kuondokana na changamoto ya upungufu wa sukari ya nyumbani na ya viwandani utakapofika mwaka 2023, lakini hii ni 2024 na hali ndiyo kama unavyoiona. Matumaini hayo yaliyotolewa na Serikali yalitokana na kile ilichokieleza kuwa, katika kipindi hicho ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi II utakamilika na kuanza kufanya kazi pamoja na upanuzi wa viwanda vingine vya sukari utakamilika. Kipindi Serikali inaeleza hivyo, ujenzi wa kiwanda cha Sukari Mkulazi II ulifikia asilimia 63 na ilielezwa kitakapokamilika kitazalisha sukari ya viwandani na kufidia zile tani 165,000 zinazoagizwa nje ya nchi. Haikuishia hapo, Waziri wa Viwanda na Biashara wa wakati huo, Dk Ashatu Kijaji alisema kiwanda hicho na vingine kama Kagera, Mtibwa, Kilombero, TPC na Manyara vinavyoendelea na upanuzi kwa lengo la kuzalisha sukari inayotosheleza mahitaji ya ndani, mwaka 2025, vitaweza kuuza nje. Baada ya yote hayo, makadirio ya uzalishaji wa sukari ulikuwa ni tani 655,000 kwa mwaka na hivyo kuziba pengo la sukari kwa mwaka ambalo ni tani 42,000 lilioanza kupungua baada ya Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kuanza uzalishaji wa tani 17,000 kwa mwaka. Mikakati hiyo ilikwenda kama ilivyoelezwa lakini hadi sasa changamoto ya uhaba wa sukari imeibuka tena. Kinachoniacha hoi ni ahadi za kumalizika kwa changamoto hiyo zilizowahi kutolewa mara kadhaa na Serikali, karibu kila mwaka lakini hadi sasa baadhi ya sababu zimebaki kuwa zile zile. Miongoni mwa sababu zinazojirudia ni ile ya baadhi ya wafanyabiashara kuficha sukari ili kusababisha uhaba na hatimaye kuongeza bei ya bidhaa hiyo. Ina maana Serikali imeshindwa kudhibiti wafanyabiashara hawa? Tumesikia mara kadhaa wakikamatwa huwa hatma yao ni nini? Hatua baada ya kukamatwa ni mara chache tumewahi kusikia, huwa wanafanywaje? Wananchi wanashindwa kuelewa wanapoambiwa kuhusu changamoto hiyo, hasa ukizingatia wanajua sukari inazalishwa kutokana na muwa na kuna mashamba lukuki ya zao hilo. Si hivyo tu, wapo wakulima wa miwa wanaolalamika mazao yao kuozea shambani kwa sababu wanakosa soko na kuna wakati viwanda vinalalamikia kukosa malighafi. Yote hayo ni mambo yanayochanganya kuhusu changamoto zinazojitokeza za uhaba wa sukari na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo. Kupanda kwa bei ya sukari kumesababisha baadhi ya wananchi waone bidhaa hiyo kuwa anasa na hivyo wapo walioamua kuacha kupata mlo wa asubuhi unaohusisha chai. Lakini, maumivu yanabaki kwa wale wanaotumia sukari kama moja ya viungo muhimu ili kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuuza. Mathalan, waoka keki, mikate, maandazi na vitafunwa vingine, bila shaka gharama za uzalishaji wa bidhaa zao zimeongezeka. Kuna baadhi ya maeneo, kitumbua kilichokuwa kinauzwa kwa Sh100 kimepanda bei hadi Sh200 anayeumia hapa ni mteja ambaye ni mwananchi.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na m
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na mabadiliko ya taasisi za familia. Hali hiyo, alisema inaibua haja ya kila anayepaswa kulinda taasisi hiyo kujitathmini juu ya wajibu wake Rais Samia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipohutubia katika hafla ya kusimikwa kwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa. Katika hotuba yake hiyo, alisisitiza umuhimu wa kudumisha taasisi ya familia nchini, jambo alilolitaja kuwa na changamoto lukuki. "Ndugu zangu taasisi ya familia hapa nchini na ulimwenguni inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali," alisema. Aliijenga hoja yake hiyo kwa kurejea katika ripoti ya utafiti wa ufuatiliaji wa kaya ya mwaka 2022 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Ripoti hiyo inaeleza zaidi ya nusu ya Watanzania walio katika umri wa kuoa au kuolewa hawajaingia kwenye ndoa. Kulingana na Rais Samia, takwimu hizo zinaonyesha kwa wakazi wa mijini ni wastani wa asilimia 64.5. "Wote ni mabachela wanazunguka tu huko na ndiyo maana tunazungumzia ubakaji hauishi, kuna mibachela inazunguka huko," alisema. Kwa upande wa vijijini, alisema takwimu hizo zinaonyesha wastani wa asilimia 55.5. Aidha, alisema hata wanaofanikiwa kuingia katika ndoa kuna changamoto mbalimbali zinazosababisha migogoro ya ndoa. Mathalan mwaka 2022/23, kulikuwa na mashauri ya migogoro ya ndoa 39,571 na katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023/24 mashauri hayo yapo 28,773. "Jambo hili inabidi tulitafakari kwa kina kama wanajamii, kwani asilimia kubwa ya migogoro hii inahusisha ndoa za vijana au ndoa changa. "Tunatoa fedha nyingi, masherehe makubwa, michango mingi, baada ya mwaka, miaka miwili watoto kila mtu kwake," alisema. Kutokana na hilo, alisema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha taasisi ya familia inapaswa umuhimu wake. Kwa upande mwingine, alisema familia zinakabiliwa na changamoto ya ukatili. Alisema takwimu za jeshi la Polisi mwaka 2022, kulikuwa na matukio 30,566 yakilinganishwa na matukio 29,373 yaliyoripotiwa mwaka 2021. "Hapa kuna kazi kubwa, baina ya Serikali, viongozi wa dini na jamii. Hapa ndipo panapotakiwa ile kazi ya uokovu wa roho," alisema. Alieleza yote yanayotokea ni kwa sababu roho za watu zimeharibika, kila mmoja anamuwinda mwenziwe. "Tukiangalia taasisi za dini zinavyokuwa, dini zote na matokeo haya yanavyokuwa. Haviendani kwa hiyo lazima tujitafakari kama wanajamii wajibu wetu kila mmoja," alisema. Kadhalika, alisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi wahame, hasa kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na mvua a El-Nino. Ilivyokuwa kanisani Shughuli hiyo ilipambwa na burudani za muziki wa Injili kutoka kwaya mbalimbali, ikiwemo ile ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), eneo ambalo Askofu Malasusa alikuwa anahudumu kabla ya kuukwaa wadhifa huu mpya. Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali haikuwa kikwazo cha shughuli hiyo kuendelea, kila muumini alitafuta eneo aliloona lingefaa kujikinga nayo. Mkuu wa Kanisa hilo anayemaliza muda wake, Askofu Frederick Shoo ndiye aliyepewa nafasi ya kumsimika kiongozi mpya, kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya KKKT. Saa 5:30 asubuhi, ndiyo muda ambao Askofu Shoo alimuuliza Askofu Malasusa swali la ithibati ya uapisho wa kusimikwa kwenye nafasi hiyo. Baada ya kiapo hicho kwa Askofu Malasusa, Maaskofu wa Kanisa la KKKT na wajumbe wa halmashauri kuu wa kanisa hilo, nao waliulizwa na kuthibitisha kutoa ushirikiano kwa mkuu huyo mpya wa kanisa. Tukio hilo, lilifuatiwa na maaskofu kwenda kumpa mkono mkuu mpya wa kanisa na baadaye Rais Samia naye alipewa nafasi hiyo. Dakika mbili baadaye, Askofu Shoo alitekeleza jukumu la kumpeleka mbele mwenza wa mkuu wa kanisa, Erica Malasusa kwa ajili ya kukabidhiwa kwa Mungu kupokea nafasi hiyo. Hilo lilifuatiwa na kumkaribisha mkuu wa kanisa kwa ajili ya kupeana mikono na mwenza wake na wawili hao walikabidhiwa maua kama ishara ya upendo. Kwa pamoja wawili hao, walipelekwa mbele ya meza ya Rais Samia kwa ajili ya kutambulishwa kama viongozi wa kanisa hilo. Utambulisho huo pia ulifanywa na Askofu Shoo. Maombi ya Matoleo ndiyo shughuli iliyofuata baada ya utambulisho huo. Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Rais Samia ndiyo viongozi wa mihimili mitatu waliokuwepo katika hafla hiyo. Wageni wengine walioshiriki ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusiluka, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye. Kadhalika, walikuwepo Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Philemon Luhanjo, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Daniel Chongolo, Mama Janeth Magufuli na Mama Anna Mkapa. Katibu Mkuu wa CCM Balozi Emmanuel Nchimbi, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba nao walikuwepo. Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini walikuwa sehemu ya waalikwa katika shughuli hiyo na walishiriki. Baada ya utambulisho huo, salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania zilitolewa.
Licha ya miezi sita iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
Licha ya miezi sita iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumaliza mgao wa umeme nchini kukaribia ukingoni, bado kuna mashaka ya mgawo huo kumalizika. Septemba 26, mwaka jana, wakati akimuapisha bosi mpya wa Tanesco, Rais Samia alilitaka shirika hilo kuhakikisha linamaliza mgawo huo kwa miezi sita. Tangu agizo hilo lilipotolewa miezi sita itamalizika Machi 26, mwaka huu. Msingi wa hofu ya kuendelea kwa mgawo huo, ni kukosekana kwa maji ya kutosha katika vyanzo vya uzalishaji umeme, licha ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha. Kulingana na Tanesco, kinachokwaza uhakika wa upatikanaji wa umeme nchini ni kukosekana kwa maji katika vyanzo (mabwawa), hali inayosababishwa na matumizi mabaya ya rasilimali maji katika vyanzo hivyo. Shirika hilo, limezitaja shughuli kama kilimo holela cha umwagiliaji na ufugaji ndizo hasa zinazosababisha ukosefu wa maji katika vyanzo hivyo. Hata hivyo, wamiliki wa viwanda wameeleza changamoto ya upatikanaji wa umeme inasababisha kuongezeka kwa gharama za uzalishaji viwandani na hivyo kuwatia hasara. Akizungumzia na Mwananchi kuhusu hali ya upatikanaji wa nishati hiyo nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga alisema licha ya mvua zinazoshuhudiwa, bado kuna upungufu mkubwa wa kina cha maji katika vyanzo vinavyotumika kuzalisha umeme nchini. Si kwamba upungufu huo unasababishwa na kiwango kidogo cha mvua, alisema kinachosababisha ni utumiaji mbaya wa rasilimali maji hasa katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji kwenye vyanzo vikuu. “Kama una nafasi uje uone bwawa la Mtera kwanza halina maji pamoja na mvua zinazonyesha. Lakini kabla hujauliza kwanini Mtera halijai maji, jiulize kwanini Mto Ruaha unaoleta maji Mtera ambao zamani ulikuwa unafurika wakati wa mvua kwa sasa hauna maji,” alisema. Nyamo-Hanga alisema vyanzo hivyo vyote mzizi wake ni Ihefu na Mbarari mkoani Mbeya, ambako shughuli za kilimo cha umwagiliaji zimeshamiri, kuzidi kiwango cha maji yaliyopo na hivyo kusababisha athari kwa matumizi mengine ya rasilimali hiyo. Alieleza kuna uchepushaji holela wa rasilimali maji, hivyo mvua inanyesha badala ya kujaza mabwawa, maji yanaanza kujikusanya kujaza mashamba ya mpunga ndipo yaende kwenye vyanzo vya umeme. Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alidokeza utolewaji holela wa vibali vya shughuli za kilimo bila kuzingatia mahitaji ya matumizi mengine ya maji. “Mtu amepewa kibali cha kulima na masharti aliyopewa ni kutumia lita 10 za maji, lakini wengi wanavunja utaratibu wanatumia zaidi ya hizo na hakuna wa kumfuatilia wala kumkataza,” alisema. Mbali na shughuli hizo holela za kilimo, Namo-Hanga alitaja ufugaji katika maeneo hayo, unaathiri pia vyanzo vya maji na hivyo mabwawa kuendelea kukosa rasilimali hiyo. “Ukiitazama haraka haraka unaweza kuhisi ni shida ya Tanesco na pengine ukailaumu Tanesco, lakini tatizo ni uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira. “Tunapaswa kufahamu na kuungana pamoja tuelezane kwamba suala la matumizi mabaya ya rasilimali maji na yaliyozidia kipimo ni tatizo, pia tuhakikishe hatushiriki kuharibu mazingira,” alisema. Alipoulizwa kuhusu hali ya matengenezo ya mitambo, mkurugenzi huyo alisema hiyo ni shughuli endelevu kwa kuwa, inafanywa kila tatizo linapotokea. “Gari yako inapoharibika ukatengeneza huwezi kusema haitaharibika tena, unaweza ukatembea kilomita moja ikaharibika na kuhitaji matengenezo. Kwa hiyo matengenezo ni shughuli endelevu hatuwezi kusema itaisha lini,” alisema. Alisisitiza hata kama hayakupangwa wakati mwingine linatokea jambo linalohitaji kufanya matengenezo. Wenye viwanda Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Sufiani alisema changamoto hiyo inapunguza uzalishaji. Ingawa bado CTI haijafanya stadi ya hasara, alisema kwa ujumla kinachoshuhudiwa kinasababisha upungufu wa uzalishaji ambao aghalabu huwa na matokeo hasi mengi. "Shida kubwa hapa ni uzalishaji kupungua, kama ulikuwa unazakisha kiasi fulani utapunguza, hii kwa kiwanda ni hasara kubwa," alisema. Hata hivyo, alisema Hali hiyo inakuwa mbaya zaidi kwa baadhi ya viwanda hasa vile ambavyo kwa mahitaji yake ya umeme haiwezi kutumia jenereta. "Hawawezi kuzalisha kwa sababu kunakosekana uhakika wa upatikanaji wa nishati kwa hiyo ni hasara kwao. Hasara inakuwa kubwa zaidi pale ambapo wafanyakazi bado wataendelea kuhitaji mishahara," alisema. Kwenye eneo hilo la uzalishaji, Sufiani alisema viwanda kinashindwa kutimiza mahitaji ya wateja, jambo linalosababisha umpoteze mteja husika. Lakini, alieleza changamoto ya umeme iliyopo inawasababishia kuongeza gharama za uzalishaji kwani, wakati mwingine wanahitaji kutumia jenereta. "Jenereta linatumia mafuta ni gharama kubwa zaidi ya umeme kwa hiyo, ukiongeza gharama za uzalishaji maana yake hasara itakuwa kwako mzalishaji vinginevyo uongeze bei ya bidhaa," alisema. Hali hiyo, imebadili mtindo wa maisha ya Neema Nichorous Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam, anayesema kwa sasa analazimika kupiga pasi nguo anazitarajia kuvaa wiki nzima kwa kuwa hana uhakika wa uwepo wa umeme siku zote. "Umeme unaweza kukatika saa 12 asubuhi ukarudi jioni, hata kama unataka kupiga pasi ni changamoto yaani ni tatizo kubwa," alisema Neema.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na m
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kukuwa kwa taasisi za dini nchini, lakini hakuendani na mabadiliko ya taasisi za familia. Hali hiyo, alisema inaibua haja ya kila anayepaswa kulinda taasisi hiyo kujitathmini juu ya wajibu wake Rais Samia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipohutubia katika hafla ya kusimikwa kwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa. Katika hotuba yake hiyo, alisisitiza umuhimu wa kudumisha taasisi ya familia nchini, jambo alilolitaja kuwa na changamoto lukuki. "Ndugu zangu taasisi ya familia hapa nchini na ulimwenguni inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali," alisema. Aliijenga hoja yake hiyo kwa kurejea katika ripoti ya utafiti wa ufuatiliaji wa kaya ya mwaka 2022 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Ripoti hiyo inaeleza zaidi ya nusu ya Watanzania walio katika umri wa kuoa au kuolewa hawajaingia kwenye ndoa. Kulingana na Rais Samia, takwimu hizo zinaonyesha kwa wakazi wa mijini ni wastani wa asilimia 64.5. "Wote ni mabachela wanazunguka tu huko na ndiyo maana tunazungumzia ubakaji hauishi, kuna mibachela inazunguka huko," alisema. Kwa upande wa vijijini, alisema takwimu hizo zinaonyesha wastani wa asilimia 55.5. Aidha, alisema hata wanaofanikiwa kuingia katika ndoa kuna changamoto mbalimbali zinazosababisha migogoro ya ndoa. Mathalan mwaka 2022/23, kulikuwa na mashauri ya migogoro ya ndoa 39,571 na katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023/24 mashauri hayo yapo 28,773. "Jambo hili inabidi tulitafakari kwa kina kama wanajamii, kwani asilimia kubwa ya migogoro hii inahusisha ndoa za vijana au ndoa changa. "Tunatoa fedha nyingi, masherehe makubwa, michango mingi, baada ya mwaka, miaka miwili watoto kila mtu kwake," alisema. Kutokana na hilo, alisema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha taasisi ya familia inapaswa umuhimu wake. Kwa upande mwingine, alisema familia zinakabiliwa na changamoto ya ukatili. Alisema takwimu za jeshi la Polisi mwaka 2022, kulikuwa na matukio 30,566 yakilinganishwa na matukio 29,373 yaliyoripotiwa mwaka 2021. "Hapa kuna kazi kubwa, baina ya Serikali, viongozi wa dini na jamii. Hapa ndipo panapotakiwa ile kazi ya uokovu wa roho," alisema. Alieleza yote yanayotokea ni kwa sababu roho za watu zimeharibika, kila mmoja anamuwinda mwenziwe. "Tukiangalia taasisi za dini zinavyokuwa, dini zote na matokeo haya yanavyokuwa. Haviendani kwa hiyo lazima tujitafakari kama wanajamii wajibu wetu kila mmoja," alisema. Kadhalika, alisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi wahame, hasa kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na mvua a El-Nino. Ilivyokuwa kanisani Shughuli hiyo ilipambwa na burudani za muziki wa Injili kutoka kwaya mbalimbali, ikiwemo ile ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), eneo ambalo Askofu Malasusa alikuwa anahudumu kabla ya kuukwaa wadhifa huu mpya. Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali haikuwa kikwazo cha shughuli hiyo kuendelea, kila muumini alitafuta eneo aliloona lingefaa kujikinga nayo. Mkuu wa Kanisa hilo anayemaliza muda wake, Askofu Frederick Shoo ndiye aliyepewa nafasi ya kumsimika kiongozi mpya, kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya KKKT. Saa 5:30 asubuhi, ndiyo muda ambao Askofu Shoo alimuuliza Askofu Malasusa swali la ithibati ya uapisho wa kusimikwa kwenye nafasi hiyo. Baada ya kiapo hicho kwa Askofu Malasusa, Maaskofu wa Kanisa la KKKT na wajumbe wa halmashauri kuu wa kanisa hilo, nao waliulizwa na kuthibitisha kutoa ushirikiano kwa mkuu huyo mpya wa kanisa. Tukio hilo, lilifuatiwa na maaskofu kwenda kumpa mkono mkuu mpya wa kanisa na baadaye Rais Samia naye alipewa nafasi hiyo. Dakika mbili baadaye, Askofu Shoo alitekeleza jukumu la kumpeleka mbele mwenza wa mkuu wa kanisa, Erica Malasusa kwa ajili ya kukabidhiwa kwa Mungu kupokea nafasi hiyo. Hilo lilifuatiwa na kumkaribisha mkuu wa kanisa kwa ajili ya kupeana mikono na mwenza wake na wawili hao walikabidhiwa maua kama ishara ya upendo. Kwa pamoja wawili hao, walipelekwa mbele ya meza ya Rais Samia kwa ajili ya kutambulishwa kama viongozi wa kanisa hilo. Utambulisho huo pia ulifanywa na Askofu Shoo. Maombi ya Matoleo ndiyo shughuli iliyofuata baada ya utambulisho huo. Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Rais Samia ndiyo viongozi wa mihimili mitatu waliokuwepo katika hafla hiyo. Wageni wengine walioshiriki ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusiluka, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye. Kadhalika, walikuwepo Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Philemon Luhanjo, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Daniel Chongolo, Mama Janeth Magufuli na Mama Anna Mkapa. Katibu Mkuu wa CCM Balozi Emmanuel Nchimbi, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba nao walikuwepo. Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini walikuwa sehemu ya waalikwa katika shughuli hiyo na walishiriki. Baada ya utambulisho huo, salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania zilitolewa.
Mambo bado magumu kwa chama cha siasa tarajiwa cha IPP kuhusu kupata usajili wa muda, kikieleza kuum
Mambo bado magumu kwa chama cha siasa tarajiwa cha IPP kuhusu kupata usajili wa muda, kikieleza kuumiza na ucheleweshwaji wa usajili wake unaofanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, huku ofisi hiyo ikitaja kutokidhi masharti ndiyo sababu ya yote. Malalamiko ya chama hicho tarajiwa juu ya kucheleweshewa usajili yanatokana na kile kilichoeleza, imepita miezi minane tangu kiombe usajili, lakini hadi sasa hakijafanikwa. Hii si mara ya kwanza kwa chama hicho kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya ofisi hiyo, kikiilalamikia kuchelewesha usajili wake, licha ya kukamilisha matakwa yote. Kiliwahi kufanya hivyo, Juni mwaka jana kikihoji kwanini baada ya kukamilisha taratibu zote za maombi ya usajili wa muda, ofisi hiyo ya msajili haitekelezi wajibu wake. Kilisema kuchelewa kulitekeleza hilo, kinavunja Sheria ya Vyama Vya Siasa kipengele namba 4(a) kinachomtaka Msajili baada ya kupokea maombi kutangaza katika magazeti mawili yanayosambazwa nchi nzima ili kukaribisha pingamizi. Hata hivyo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alijibu suala si kuhesabu muda uliopita tangu chama hicho kilipowasilisha maombi, kinapaswa kihesabu ni muda gani kilitimiza masharti ya kupata usajili. Malalamiko ya chama hicho, yalitolewa jana kupitia taarifa kwa umma ya waanzilishi wa chama hicho, Andrew Bomani na Gregory Urima. Katika taarifa hiyo, waanzilishi hao walieleza kuona kile walichokiita giza juu ya mwenendo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Giza hilo linatokana na hoja kuwa, imepita miezi minane tangu wawasilishe nyaraka katika ofisi hiyo kwa ajili ya kuomba usajili wa muda wa chama hicho, bila mafanikio. “Ofisi hiyo imekuwa ikituzungusha katika hali ambayo inatutia simanzi kubwa kuhusiana na haki za msingi nchini. Kwa kweli tumewavumulia sana na kufikia sehemu ya kuona GIZA totoro kuhusu usajili wa IPP,” walieleza kupitia taarifa hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa nao, matendo hayo wanayofanyika yamewalazimu kutangaza maandamano watakayoyafanya Februari 1, mwaka huu. “Tunakusudia kufanya jambo la aina yake siku hiyo. Tunawaomba Watanzania wazalendo watuunge mkono kwa hili. Dunia ifahamu kwamba Tanzania kuna ukiukwaji wa wazi wazi wa haki za binadamu,” walisema. Walikihusisha wanachofanyiwa na rejea ya maombi mengine ya Watanzania kusajili vyama vya siasa tangu mwaka 2016, wakisema wote hawakufanikiwa. “Fikirieni hiyo balaa! Walifikia hatua ya mwezi Desemba kumwandikia Rais Samia. Na izingatiwe hakuna chama cha siasa kilichosajiliwa tangu 2014. Ni jambo la kustaajabisha kwamba wasomi wetu mbalimbali hawajashtuka kabisa na hali yetu mbaya,” waliandika katika taarifa hiyo. Kulingana na taarifa yao hiyo, siku hiyo itakuwa maadhimisho ya siku ya sheria duniani, hivyo wataitumia kuonyesha changamoto za katika utekelezwaji wa sheria nchini. “Siku ya Sheria ina umuhimu wake lakini upande wa pili usimamizi wa sheria nchini ni aibu tupu. Haiwezekani watu wakutane tu na kupongezana. Tunaambiwa haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa,” waliandika katika taarifa hiyo. Msajili ajibu Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza aliwataka waombaji hao wasihesabu muda uliopita tangu wameomba, badala yake wahesabu ni muda gani wametimiza masharti ya kupata usajili. “Wasihesabu muda uliopita tangu wameomba usajili, wanapaswa kuhesabu kwa muda gani wametimiza masharti ya kusajiliwa. Kwa sababu hatuwezi kutoa usajili kwa muombaji asiyekidhi matakwa ya kisheria,” alisema. Hata hivyo, alieleza msingi wa malalamiko ya vyama vilivyoomba usajili ni kutaka mambo yaende bila kuzingatia taratibu na sheria, jambo alilosema haliwezekani. Kwa mujibu wa Nyahoza, ili chama kipate usajili kinapaswa kuwasilisha nyaraka takriban tano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ikiwemo Katiba, Kanuni, nembo la chama, sera, malipo na uthibitisho wa uraia. Kilichotokea kwa vyama hivyo, alisema viliwasilisha nyaraka zikiwa na makosa, hivyo ofisi hiyo ilivitaka vifanye marekebisho kisha viwasilishe tena. Baada ya kuwasilisha tena, alieleza kuna milolongo kadhaa inayopaswa kufanyika ili kuthibitisha usahihi wa nyaraka zilizowasilishwa, jambo alilosema ni vigumu kutekelezwa kwa siku moja. “Hizo nyaraka zilizowasilishwa tunatakiwa kuzipitia na kuthibitisha kama ziko sahihi na zimewasilishwa vema, huo ni mchakato sio kwamba leo unaleta na leo lazima tutapitia. Wengi wanataka mambo yafanyike kinyume na utaratibu,” alisema. Alisisitiza ofisi hiyo mara zote imekuwa ikiviambia vyama hivyo kuwa, usipokamilisha masharti lazima usubiri, ili ukamilishe ndipo usajiliwe.
Serikali imeanza kuwapika mawakili wake kwa kuwajengea uwezo wa kuzikabili kesi zitakazojitokeza baa
Serikali imeanza kuwapika mawakili wake kwa kuwajengea uwezo wa kuzikabili kesi zitakazojitokeza baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo kwa mawakili hao yanatokana na kile kilichoelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi kuwa, kuna matarajio ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi, hivyo kinachofanyika ni kuwaandaa mapema. Hata hivyo, Serikali imekamilisha hatua ya kupokea maoni ya wadau kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali za uchaguzi, ambazo miswada yake iliwasilishwa bungeni tangu Novemba 10, mwaka jana. Dk Feleshi alitoa kauli hiyo mkoani Pwani jana, katika hotuba yake ya kufungua mafunzo ya siku tano yanayowahusisha watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutoka Mikoa 16 nchini. “Tulichokifanya ni kuangalia kwa pamoja kwamba, sasa hivi huenda kukawa na mabadiliko ya sheria zetu (za uchaguzi) huwezi kuacha mawakili wako wasubiri kinachotokea kwa sababu itakuwa too late (tumechelewa sana),” alisema alipotafutwa na Mwananchi kufafanua zaidi kuhusu mafunzo hayo. Alifafanua kazi ya ofisi yake ni kuhakikisha kunakuwa na utawala wa sheria, hivyo kuwaandaa mapema mawakili hao ni jambo muhimu. "Baadaye nchi itafanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani ni Uchaguzi Mkuu, hivyo kuna umuhimu wa ninyi kujiimarisha ili kama itatokea kesi zinazohusu maswala ya uchaguzi mzisimamie kwa weledi na kuhakikisha zinaisha kwa wakati bila kuleta hasara," alisema. Katika mafunzo hayo, Dk Feleshi aliwataka mawakili hao kujifunza maarifa mapya na stadi za kazi bila kukoma, kufanya utafiti bila kukoma, kujilinda na uovu na kuwa waaminifu muda wote. Kwa kuwa teknolojia zinabadilika, alisema ni wajibu wa mawakili hao kuongeza maarifa mapya yatakayoboresha utendaji wa kazi zao na kuwa waangalifu katika maneno na mawasiliano wanayofanya. "Tunajifungia na kukumbushana wajibu ili hata hapo tutakapolazimika kuchukua hatua kwa wanaokwenda kinyume kusiwe na lawama hili lipo hata kwenye vitabu vitakatifu waliposema mkulima alishauri mti umwagiliwe mbolea na usipozaa mwakani utakatwa,” alisema. Akizungumza katika mafunzi hayo, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhende alisema mafunzo hayo yataboresha ufanisi wa watendaji hao na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali. Alisema kwa kipindi cha miaka mitatu ofisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa Menejimenti yake. Wananchi Mwananchi ilifanya mazungumzo na wananchi mbalimbali mkoani Pwani kuhusu mafunzo hayo, walisisitiza umuhimu wa mawakili kuwa karibu wakati Serikali inasaini mikataba mbalimbali ili kuepuka uvunjwaji wa sheria. "Nashauri wanasheria wetu wawe wanazingatia kwa makini kuhusu mikataba inayohusu Serikali na mashirika na hata kwa baadhi ya wawekezaji ili kabla ya kusaini waangalie vipengele vya sheria ili kutojiingiza kwenye hasara na kama mikataba hiyo ni migumu basi ni bora kuachana nayo," alisema Asia Omary mkazi wa Pwani.. Mwananchi mwingine, Said Mselem aliwataka mawakili hao kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya sheria za uchaguzi kwa baadhi ya wananchi hususa wenye nia ya kugombea uongozi ili waepuke makosa yanayoweza kuvuruga amani na hata wao kujikuta mikononi mwa sheria. “Kuna baadhi ya wanachama wamekuwa wakijiingiza kwenye mkumbo wa kushabikia mambo ya siasa na kuvunja sheria hususan unapokaribia uchaguzi na kusabaisha mlundikano wa kesi kwenye mahakama. “Ni vema wakapewa elimu ili wasijiingize kwenye hatari hiyo kwa kuwa inachangia kuvuruga amani ya nchi jambo ambalo si jema,” alisema.
Wafanyabiashara wadogo sita walioathiriwa na maporomoko ya tope wilayani Hanang mkoani Manyara, wame
Wafanyabiashara wadogo sita walioathiriwa na maporomoko ya tope wilayani Hanang mkoani Manyara, wamesamehewa deni la Sh22 milioni walilotakiwa kurejesha kwa kipindi cha miezi mitatu. Fedha hizo walikuwa wanadaiwa na Taasisi ya kifedha ya VisionFund Tanzania na Metro Life Assurance, walizozikopa kwa shughuli za biashara, kabla ya kukumbwa na athari za maporomoko ya tope hilo. Maporomoko ya tope kutoka mlima Hanang, yalitokea usiku wa kuamkia Desemba 3 mwaka 2023 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 80, huku wengine zaidi ya 100 wakiachwa bila makazi. Hata hivyo, hivi karibuni Benki ya NMB iliwalipa wafanyabiashara 18 Sh270 milioni ikiwa ni fidia ya bima za mikopo yao baada ya kukumbwa na janga hilo. Hayo yameelezwa mkoani Manyara leo Jumatano, Januari 17, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja baada ya wafanyabiashara hao kukabidhiwa hundi ya msamaha. Amesema kilichofanywa na taasisi hizo ni ishara kwamba athari za maporomoko hayo ziliwagusa wengi. "Jumla ya wafanyabiashara 11 wamapata athari katika biashara zao ambao sita wamewafutiwa mikopo kabisa hawatalipa na watano wamesahemewa marejesho miezi mitatu wataaanza kulipa marejesho rasmii mwezi Aprili mwaka huu," amesema. Amezitaka taasisi nyingine kujitokeza kuonyesha uhalisia wao nyakati za majanga na kwamba kufanjya hivyo itawezesha kujua kama zinawasaidia wateja wake wakati wa majanga. Mkurugenzi wa VisionFund, Chilala Hakoom amesema lengo la taasisi hiyo ni kusaidia jamii na kuboresha maisha ya mtoto kwa kuwezesha familia kupitia huduma za kifedha. Amesema taasisi hiyo inatambua ugumu wa kifedha unaotokana na waathirika hivyo imechukua hatua muhimu kufuta mkopo kwa wadeni walioathirika kupitia huduma ya Bancassurance. Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Metro Life Assurance, Amani Boma amesema ushiriki wao katika jambo hilo unatokana na uhalisia wa majukumu yao, ukizingatia ni shirika la bima. "Ni wajibu wetu kuungana na kushirikiana Serikali katika masuala ya majanga na bima kushiriki kwa wakati na Watanzania mnapaswa kuwa na bima ziwasaidiea wakati wa matatizo," amesema. Mmoja wa wafanyabiashara hao mkoani humo, Fura Massawe amesema wengi wao walipoteza mali baada ya kusombwa na tope hilo. Mwishoooo Kuminyia maziwa ya mama kwenye jicho, kuliosha kwa maji na chumvi au kwa chai ya rangi, si miongoni mwa tiba za maambukizi ya ugonjwa wa macho mekundu kama wengi wanavyodhani, wataalamu wanafafanua. Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo nchini, zimeshuhudiwa imani mbalimbali zikitumika kusaka suluhu ya maambukizi ya Red Eyes, hapo ndipo wengine hutumia dawa hizo wanazoziita za asili. Kwa taarifa yako, bado hakuna tiba ya moja kwa moja ya maambukizi hayo na unapoambukizwa yatadumu kwa wiki ama mbili au sita kabla ya kupotea, kama inavyofafanuliwa na wataalamu wa ugonjwa huo. Katika mahojiano yake na Mwananchi, Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho, Wizara ya Afya, Dk Bernadetha Shilio anasema zipo hatua zinazochukuliwa na wananchi ambazo ni hatari kwa afya ya macho yao. Miongoni mwa hatua hizo, anasema ni kuminyia ziwa la mama kwenye jicho lililoambukizwa ugonjwa huo, kuliosha kwa maji yenye chumvi au kwa chai ya rangi. “Hairuhusiwi kutumia maji ya chumvi, chai ya rangi wengine wanatumia kunawa uso au macho na mama anayenyonyesha huwa anaweka maziwa ya mama, vyote hivyo haviruhusiwi na vinaweza kuleta madhara kwenye macho,” anasema. Unapopatwa na maambukizi hayo kwa mujibu wa Dk Bernadetha, unapaswa kuendelea na utaratibu wa siku zote wa kujisafisha, kama kuoga na kuosha uso kawaida. “Mtu akipata shida anaoga kama kawaida, anatumia taulo lake kujifuta uso kama kawaida lakini asichangie na mtu yeyote taulo hiyo. “Kama kuna tongotongo au machozi yanayotoka machoni, unashauriwa kujifuta kwa tishu tena pembeni ya jicho na sio katikati,” anasema. Kufuta katikati au kutumia nguo ngumu, anasema kunaweza kusababisha uvimbe zaidi au macho kuuma, kisha unapaswa kutupa hicho unachotumia kujifutia na unawe mikono. Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, haishauriwi kutumia kitambaa kwa kuwa utakihifadhi na baadaye kukitumia tena, jambo linalosababisha kujiongezea ugonjwa. Hata hivyo, anasema matumizi ya kitambaa yanaweza kusababisha maambukizi ya bakteria jichoni au jeraha la kemikali na hivyo kupoteza uwezo wa kuona kabisa. Kulingana na mtaalamu huyo, inashauriwa mgonjwa wa ugonjwa huo asikimbilie hospitali haraka, labda pale anapokabiliwa kiasi cha kushindwa kuvumilia. Msingi wa ushauri huo ni kile kilichoelezwa na Dk Bernadetha kuwa, kuna hatari ya kusambaza zaidi ugonjwa huo kwa kuwa hospitali unakutana na watu wengi. “Mtu akipata hiyo shida, atulie, augulie mwenyewe, azingatie kunawa mikono kwa vitakasa mikono au sabuni na inapotokea unapiga chafya funika pua pamoja na mkono ili usisambaze. “Kwa sababu kuna uhusiano mikubwa kati ya ugonjwa wa macho na pua na mdomo kwa kuwa ugonjwa unaweza kuenea kwa njia mbalimbali,” anasema. Hakuna tiba Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Rugajjo anasema bado hakuna tiba maalum ya maambukizi hayo, badala yake dalili zake zinakadiriwa kuisha kwa muda wa wiki mbili hadi sita kwa baadhi ya watu. “Wagonjwa wanashauriwa kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya kupimwa na kupatiwa dawa ya kupunguza madhara kulingana na ishara zinazoonwa na daktari,” anasema. Profesa Rugajjo anasema kuna namna lukuki zitakazokuwezesha kuzuia ugonjwa huo, ikiwemo kuepuka kugusa macho yako na iwapo utafanya hivyo unapaswa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni. Anasema vile vinavyogusa macho yako unapaswa ama kuvitupa au kuvisafisha kwa maji ya moto na sabuni, lakini haupaswi kuchangia vipodozi, taulo za karatasi, nguo na dawa za macho. “Funika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya, pia tumia taulo tofauti na leso kwa kila mwanafamilia,” anasema. Mtu anaambukizwa ugonjwa huo, kwa kugusa machozi au tongotongo kutoka kwenye macho yenye ugonjwa huo. Anasema kugusana mikono na mtu mwenye maambukizi hayo ni sababu nyingine ya kuambukizwa ugonjwa huo na kwamba dalili zake huanza kujitokeza kuanzia siku tano hadi 14 baada ya kupata vimelea. Hata hivyo, anasema wanafunzi wanaougua wanashauriwa kukaa nyumbani hadi dalili zinapoisha kwa kuwa ni ngumu kuzuia maambukizi yasisambae kwenye mazingira ya shule. “Watu wazima wanaweza kwenda kazini ila wanapaswa kuzingatia kanuni za kuzuia maambukizi kwa kufuata kanuni, lakini watumishi wa afya wazingatie kuepuka kupeleka maambukizi hayo nyumbani,” anasema. Profesa Rugajjo anasema unapoona jicho linakuwa jekundu, linawasha na kuchomachoma, macho yanavimba, yanaogopa mwanga, yanatoa matongotongo meupe na ya njano ujue una dalili za ugonjwa huo. “Uwezo wa kuona unakuwa kama kuna ukungu na unasikia maumivu ya macho hizi zote ni daalili za Red Eyes,” anasema. Kwa ujumla wake, anasema ugonjwa huo unasababishwa na kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho ‘Viral Keratoconjunctivitis’ na husambaa kwa kasi kubwa. Kwa asilimia 80 mlipuko huo, anasema unasababishwa na kirusi cha ‘Adenovirus’. Angalizo Iwapo umebainika kuwa na ugonjwa huo, anasema ni vema kuepuka kutumia dawa zisizo rasmi na ambazo hazikuandikwa na daktari kwa wakati huo. “Usitumie dawa za macho anazotumia mgonjwa mwingine au alizoandikiwa yeye awali alipokuwa na tatizo la jicho ili kuepuka madhara kwa kuwa dawa za macho ni tofauti kwa matumizi,” anasema.
Safari ya kuifikisha Tanzania katika matumaini ya uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme si hadi
Safari ya kuifikisha Tanzania katika matumaini ya uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme si hadithi tena, bali ni jambo lenye uhalisia. Kinachoubeba uhalisia huo ni kile kinachoshuhudiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati hasa Mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Ulianza kama hadithi, ukakumbwa na upinzani mkali, lakini umuhimu na tija inayotarajiwa baada ya kukamilika kwake, ndiyo iliyofanya Serikali iendelee kuutekelezwa. Hatimaye mradi huo ulioanza kutekelezwa Disemba 12, mwaka 2018 hadi Desemba 31, mwaka 2023, ujenzi wake ulifikia asilimia 95.83 na kwamba kazi zinafanyika usiku na mchana. Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati upo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na utakapokamilika, unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme. Mahitaji ya sasa ya umeme nchini Tanzania ni megawati 1,363.9 hivyo ziada itakayozalishwa na bwawa hilo, kulingana na Serikali inatarajiwa kuuzwa nje ya nchi. Siri ya utekelezwaji wake kufanyika usiku na mchana ni kile kinachoelezwa na Wizara ya Nishati kuwa, dhamira iliyopo ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa. JHPP kwa ujumla wake, unatekelezwa kwa gharama ya Sh6.558 trilioni, fedha zote zinatoka kwa Watanzania. Tuta Kuu (Main Dam) Kiwango kilichofikiwa cha utekelezaji ambacho ni asilimia 95.83 kinahusisha maendeleo ya kazi mbalimbali zinazojumuisha mradi wote kwa ujumla. Miongoni mwa kazi hizo ni ujenzi wa Tuta Kuu la kuhifadhi maji ya Bwawa la Julius Nyerere (MAIN DAM) ambao kwa sasa umefikia asilimia 99.26. Katika ujenzi wa tuta hilo, kazi zinazoendelea kufanyika ni zile za umaliziaji zinazohusisha ujenzi wa nyumba za kufungua na kushusha mageti. Kwa sasa, maji yanapita kwenye mageti ya kuzuia maji ya tuta kuu (Spillway Gates) kwa ajili ya kuruhusu maji hayo kutumika na wanyama, mimea na viumbe hai waliopo upande wa chini wa bwawa hilo. Mahandaki ya kupitisha maji (Power Water Ways) Ujenzi wa tuta kuu unaenda sambamba na ujenzi wa mahandaki matatu ya kupitishia maji (Power Water Ways), ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.71. Mahandaki hayo matatu yamejengwa kwa zege na yana kipenyo cha mita 12 kila moja. Katika mahandaki hayo ndipo ambapo maji kutoka katika bwawa yatakapopita kwenda kwenye mitambo tisa ya kufua umeme (turbines). Lakini, ujenzi wa mahandaki hayo unaenda sambamba na matenki matatu (Surge Tanks), yenye kipenyo cha mita 22 kila moja. Hapa ndipo ambapo handaki linalopitisha maji hupumua wakati wa ufuaji umeme. Jengo la mitambo (Power House) Katika jengo la mitambo ndiko inakotarajiwa kusimikwa mitambo tisa yenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 2,115 na kila mmoja utakuwa na uwezo wa kufua megawati 235. Shughuli zinazoendelea katika eneo hilo ni usimikaji wa mitambo katika mashine za kufua umeme namba 6, 5 na 4 ambapo mashine namba 9 imeshakamilika ikifuatiwa na mashine namba 8 na saba zilizopo katika hatua za mwisho za usimikaji. Kazi nyingine zinazoendelea ni ufungaji wa mifumo ya kuzuia moto pamoja na uunganishwaji wa nyaya kwa ajili ya kudhibiti madhara yatokanayo na umeme. Katika eneo hili zimeshasimikwa mashine umba (Transfoma) zote 27, zitakazohusika na upokeaji wa umeme kutoka kwenye jenereta na kuukuza, kisha kuupeleka kwenye kituo cha kupokea na kusafirisha umeme. Ujenzi katika eneo hilo kwa sehemu kubwa unatumia vyuma (Embedded parts), zege na nondo (steel reinforcements). Kazi ya uumbaji wa mashine za kufua umeme namba 6 na 5 zinaendelea. Lakini, kazi za ujenzi kwa pamoja na usimikaji wa mitambo katika eneo hili zimefikia asilimia 88.44. Kituo cha kupokea na kusafirisha umeme wa kilovoti 400 (Switch yard) Kituo hiki ndicho kinachotarajiwa kupokea na kusafirisha umeme wa kilovoti 400 kutoka ulipo mradi huo hadi katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Chalinze na kuingia kwenye gridi ya Taifa. Kituo hiki ndicho kinapokea umeme kutoka kwenye mashine umba (transforma 27) zilizopo kwenye jengo la mitambo. Switch Yard ina urefu wa mita 500 ambazo ni sawa na nusu kilomita au unaweza kuufananisha na urefu wa viwanja vitano vya mpira wa miguu. Ujenzi katika eneo hili upo katika hatua za mwishoni, kwa sasa tayari umekamilika kwa asilimia 99.93. Kingo za kuzuia maji (Saddle dam) Bwawa la Julius Nyerere, lina kingo nne za kuzuia maji (Saddle Dams), zenye jumla ya urefu wa kilometa 17.4 na kazi yake ni kuzuia maji yasitoroke kwenye maeneo ya bwawa yenye mabonde hivyo kuyahifadhi kwa ajili ya uzalishaji wa umeme. Ujenzi katika eneo hili umefikia asilimia 99.78 na kazi zinazoendelea ni zile za umaliziaji ikiwemo uchimbaji wa mitaro na utengenezaji wa barabara za kufikia maeneo hayo. Nyumba za kudumu (Permanent houses) Kwa kuwa mradi huo utakapokamilika utahitaji wafanyakazi kwa ajili ya kusimamia na kuendesha shughuli mbalimbali katika eneo hilo, utekelezaji wake unahusisha na ujenzi wa nyumba za makazi ya wafanyakazi hao. Ujenzi wa nyumba hizo za kudumu kwa ajili ya wafanyakazi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 98.55. Kwa sehemu kubwa ujenzi wa nyumba hizo umekamilika kwa kuwekwa samani na kutengeneza miundombinu ya kuzunguka mazingira ya nyumba. Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa barabara, ujenzi wa maeneo ya michezo na kazi za kumalizia (Finishing works). Kituo cha kupokea na kusambaza umeme cha Chalinze (Chalinze substation) Mbali na shughuli hizo nyingine zinazoendelea kutekelezwa, upo ujenzi wa kituo kikubwa cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Chalinze. Kituo hicho, kinatarajiwa kupokea umeme wenye ukubwa wa kilovoti 400 kutoka katika mradi wa JHPP na kisha kuupoza hadi kilovoti 220 na 132. Baada ya kuupooza, kazi itakayofanywa na kituo hicho ni kuupeleka umeme huo katika Gridi ya Taifa, tayari kwa ajili ya kuusambaza kwenda Kinyerezi mkoani Dar es Salaam, Segera mkoani Tanga na Zuzu mkoani Dodoma. Katika eneo hilo, kazi zinazoendelea kufanyika ni usimikaji wa mitambo na majaribio ya ufanisi wa mitambo hiyo. Hata hivyo, utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho kwa ujumla umefikia asilimia 88.28. Aidha, ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme umbali wa kilometa 160 kutoka kwenye mradi wa JHPP umekamilika na tayari shughuli za ukataji wa laini zinazotoka Morogoro kuingia kituo cha Chalinze zimeshafanyika. Hadi kufikia sasa umeme wa gridi ya taifa kutoka kituo hicho umeshafika katika kituo cha kupokea umeme kilichopo mradi wa Julius Nyerere (Switch Yard). Hata hivyo, hatua zilizofikiwa za utekelezaji wa mradi huo ni matokeo ya juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mkuu huyo wa nchi amefanya jitihada za kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakamilika kwa kuendelea kutoa fedha zitakazowezesha hilo kutekelezwa. Hadi sasa tayari Serikali imeshamlipa mkandarasi takribani Sh5.7 trilioni ikiwa ni asilimia 88 ya malipo yote ya kimkataba. Serikali kwa kushirikiana na wadau wote, tunaahidi kusimamia utekelezaji wa mradi huu kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na tutaendelea kuifanya kazi hii usiku na mchana bila kuchoka,” imeeleza Wizara ya Nishati. Faida Mbali na kufikisha matumaini ya upatikanaji wa umeme wa uhakika baada ya mradi huo kutekelezwa, zipo faida nyingine lukuki zilizoanza kupatikana. Miongoni mwazo ni ajira kwa vijana zaidi ya 7,000 wa Tanzania wanaotekeleza shughuli mbalimbali za ujenzi katika mradi huo. Idadi hiyo ya Watanzania walioajiriwa katika mradi huo ni sawa na asilimia 89 ya wafanyakazi wote 8,635 waliopo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Hata hivyo, kukamilika kwa mradi huo mbali na kuongeza upatikanaji wa umeme nchini, ujenzi wa bwawa hilo utaondoa mafuriko hasa katika maeneo ya karibu. Maeneo yanayotarajiwa kunufaika kwa kutokana na ujenzi wa bwawa hilo ni Ikwiriri, Mtanza na Mloka katika Mikoa ya Pwani na Morogoro ambayo yote kwa sasa yanasumbuliwa na mafuriko yanayotokana na maji ya mto Rufiji. Mbali na kuondoa mafuriko hayo, kukamilika kwa mradi huo pia kutawezesha kilimo cha umwagiliaji katika ukubwa wa heka 200,000 kutokana na kuwepo kwa chanzo cha uhakika cha maji. Kutoka katika bwawa hilo. Lakini, katika bwawa hilo, shughuli mbalimbali zitafanyika zikiwemo za uvuvi, ambazo pia zinatajwa kuwa turufu nyingine ya uchumi kwa wakazi wa maeneo ya karibu. Kupungua kwa bei ya umeme ni faida nyingine inayotarajiwa kutokana na mradi huo, kwa kuwa utakaozalishwa utazidi mahitaji ya nchi na hivyo kusababisha bei kupungua. Mradi huo pia, unatarajiwa kuwa chachu ya kuvutia wawekezaji, watakaoshawikisha kutokana na kuwepo kwa nishati ya umeme wa uhakika. Hata hivyo, ujenzi wa mradi huo utahusisha miradi mingine ya kijamii katika Vijiji vya karibu, jambo linalotarajiwa kuchangamsha uchumi wa vijiji husika na kuboresha maisha ya wananchi wa vijiji hivyo. Kauli ya Rais Samia Hata hivyo, mwaka huu kinu cha kwanza kati ya tisa vilivyopo katika bwawa hilo kitawashwa na kuruhusu uzalishaji wa nishati hiyo kuanza. Kauli hiyo iliyokewa na Rais Samia Suluhu Hassan alipohutubia hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora (PMAYA) Desemba 17, mwaka jana. Katika hotuba yake hiyo, alisema baada ya kuwashwa kwa kinu hicho cha kwanza, cha pili kinatarajiwa kuwashwa, Aprili mwaka huu. Hata hivyo, kuwashwa kwa vinu hivyo pia kutapunguza malalamiko ya kukatika kwa umeme, kwani vitaongeza sehemu ya uzalishaji wa nishati hiyo. “Pamoja na jitihada nyingine za gesi, sola na mambo mengine, lakini umeme wa maji tunatarajia nadhani katikati ya mwakani (mwaka huu) malalamiko mengi yatakuwa yamepungua,” alisema. Hata hivyo, mradi huo unatarajiwa kukamilika Februari 2024, badala ya Juni kama ilivyotangazwa awali. Katika ziara zake kwenye eneo la utekelezaji wa mradi huo Desemba 28, 2023, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko alisema kuna matumaini makubwa ya kukamilika kwa mradi huo. “Kwa mikakati tunayoiona na wakandarasi wetu, usimamizi mzuri uliopo tutakamilisha shughuli hii kwa kipindi tulichopewa na Rais Samia Suluhu Hassan, ili kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme. “Mipango ya awali bwawa lilikuwa lianze kuzalisha umeme ifikapo Juni, 2024, lakini wakandarasi wameharakisha mchakato kutoka mwezi wa sita hadi Februari na tunaweza kukamilisha majaribio ya mitambo hii,” alisema. Kulingana na Dk Biteko, hadi siku hiyo bwawa hilo lilishajaa maji mita 166.65 kutoka usawa wa bahari wakati kiwango kinachohitajika ni mita 163. Hata hivyo, alisema wingi huo wa maji umeharakisha hatua ya kuzalisha umeme tofauti na mipango ya awali ya kuanza shughuli hiyo Juni mwaka 2024. “Niwahakikishie Watanzania mradi huu lazima uwe jawabu la matatizo ya umeme tuliyonayo. Tanzania inakuwa kwa kasi maendeleo ya watu yanakuwa kwa kasi pia,” alisema Dk Biteko. Kwa mujibu wa Dk Biteko, baada ya kukamilika kwa mradi huo Serikali itajikita katika kuviendeleza vyanzo vingine vya umeme, vikiwemo jua na upepo. Historia Chimbuko la mradi huo ni utafiti wa uzalishaji umeme kutoka mto Rufiji, uliofanywa miaka ya 1970. Utafiti huo uliofanywa na Shirika la Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) kwa kushirikiana na kampuni ya kigeni ya M/s Norplan/Hafslund, ulionyesha kuwa mradi wa Stiegler’s Gorge (kwa sasa JHPP) una uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme mwingi wa maji (hydro-power) zaidi ya unaohitajika Tanzania. Matokeo ya utafiti huo pia yalionyesha kuwa mpalio wa Stiegler’s Gorge una uwezo wa kuhimili mitambo mitatu mikubwa ya kuzalisha umeme. Mtambo wa kwanza ukizalisha megawati 400 ambao ungefungwa upande wa Kaskazini mwa Bwawa, mtambo wa pili ungekuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 800, ambao ungefungwa upande wa chini ya bwawa, na mtambo wa tatu wenye uwezo wa kuzalisha megawati 900 ambao ungefungwa upande wa kusini mwa bwawa. Kwa ufupi, jumla ya megawati 2,100 zingezalishwa kutoka Stiegler’s Gorge, kiasi ambacho ni karibu mbili ya kinachohitajiwa Utafiti huo ulifanywa chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya kwanza nchini, Mwalimu Julius Nyerere na miaka 40 baadaye ndipo utekelezwaji wa mradi huo ulipotiwa saini rasmi, wakati mkuu wa nchi akiwa, Hayati John Magufuli.
Ukiingia ‘Gesti’ huwa unaandika jina lako halisi? Swali hili linaakisi tabia ya wateja wengi wa nyum
Ukiingia ‘Gesti’ huwa unaandika jina lako halisi? Swali hili linaakisi tabia ya wateja wengi wa nyumba za kulala wageni, ambao aghalabu hutumia majina bandia kuandika katika vitabu vya wageni. Achana na hoteli ambazo kwa kawaida huwa na utaratibu unaolazimu kuchukua taarifa za mteja kabla ya kuingia, wakati mwingine hadi kitambulisho kinahitajika, hapa nazungumzia ‘Gesti’ na ‘Loji’ yaani nyumba za kulala wageni. Taarifa zilizokusanywa na Mwananchi Digital kutoka kwa wamiliki, wahudumu na wateja wa nyumba hizo, kuna uwezekano kwamba wateja wengi huandika majina ambayo si halisi na wengine hawandiki kabisa, jambo linaloikosesha Serikali mapato. Kulingana na wateja hao, shughuli inayompeleka gesti ndiyo itakayoamua aandike jina lake halisi, la uongo au asiandike kabisa. Wahudumu nao wanasema wamekatazwa na mabosi zao kuhoji taarifa za mteja, wanachopaswa kufanya ni kumpa daftari na kumwacha aandike, ili asiamue vinginevyo. Hata hivyo, kuna ukimya wa kisheria kuhusu mteja wa nyumba hizo anayedanganya jina, isipokuwa inamlazimu muhudumu kuhakikisha anamwandikisha mteja huyo, bila kujali alichoandika ni halisia au kadanganya. “Kila mhudumu wa hoteli anapaswa kuweka kitabu cha wageni katika hoteli yake kitakachotumika kuandika majina na anwani ya kila mgeni anayepanga katika hoteli hiyo na taarifa nyingine zitakazohitajika,” inaeleza Ibara ya 18 ya Sheria ya Hoteli sura ya 105. ‘Kuandika inategema umefuata nini’ Uamuzi wa kuandika jina au kutoandika, unategemea na gesti uliyoingia na ulichokwenda kufanya katika nyumba hiyo, kama inavyoelezwa na Benson Mlacha, mmoja wa wateja wa nyumba hizo jijini Dar es Salaam. “Kwani wao wanataka hela au wanataka kukubana, mara nyingi wao wanaangalia hela tu hawana muda wa kukulazimisha uandike jina,” anasema. Mtazamo huo unashabihiana na ule wa Nickson Bidodi anayesema shughuli iliyompeleka kwenye nyumba hiyo ndiyo itakayoamua aandike jina halisi au la uongo. “Kama nimekwenda kwa maovu, mfano nipo na mwanamke asiye mke wangu huwa naandika jina la uongo. Lakini kama nipo mikoni kikazi huwa naandika jina halisia ili lolote likitokea nipatikane,” anasema. Anaeleza hakuwahi kuhojiwa chochote na mhudumu wa gesti na zaidi anapofika huwa anapewa daftari kwa ajili ya kuandika jina na hakuna anayemsimamia kulifanya hilo. Katika daftari hilo, anasema anachoandika ni jina lake na baadhi ya taarifa kama siku unayoingia, utakayotoka, unapokwenda na namba yako ya simu. Hata hivyo, umeonekana ugumu wa kubaini uhalisia wa jina la mteja kwa kuwa anapofika katika nyumba hiyo, hakuna anayemjua. Kulingana na mmoja wa wamiliki wa nyumba hizo, Ahmidiwe Mmari, haitakuwa kazi rahisi kutambua hilo kwa kuwa “Kama anaandika jina la uongo au ukweli hutajua kwa sababu anakuja mgeni humjui anapotokea. Kujua jina lake inabidi muwe mnafahamiana kabla,” anasema. Mteja mwingine wa nyumba hizo (jina lake limehifadhiwa), anasema kila anapofika huwa anaandika jina lake halisi, akihofu kutotambulika iwapo atapatwa na madhira yoyote ikiwemo kuuawa. Mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni mkoani Mtwara, anasema kwanza bosi wake amewakataza wahudumu kumchunguza mteja. “Haturuhusiwi hata kumuuliza kuhusu kile anachokiandika, yeye akiandika taarifa zake basi anapewa huduma nyingine anazostahili, haturuhusiwi kuchunguza sio jukumu letu,” anasema. Alipoulizwa iwapo yupo mwenye jukumu hilo ndani ya nyumbani hiyo, anasema hakuna isipokuwa kinachoandikwa na mteja ndiyo hicho hicho kinachohifadhiwa. Mhudumu mwingine katika moja ya nyumba hizo jijini Dar es Salaam, Mariam Malima anasema wateja wenyewe ndiyo wanaokataa kuandika, akifafanua wengi hawataki ijulikane kama waliingia gesti. “Unkuta ni mume wa mtu amekuja gesti na mwanamke mwingine, hawezi kutaka aandikwe jina. Analipia anakwambia jina hapana we utaandika unavyojua. Kwa kuwa bosi anataka hela unampokea,” anasema. Hotelini hutoboi Mchezo huo si rahisi kuucheza katika hoteli zenye hadhi ya nyota tano, kama inavyosimuliwa na Maselina Rweyemamu, mhudumu katika moja ya hoteli hizo jijini Dar es Salaam. Anasema taarifa za mteja ni moja ya vitu vinavyozingatiwa katika hoteli hizo na kwamba ni bora kumkosa mteja kuliko kuruhusu aingie bila kuacha vielelezo vyake. Kulingana na Maselina, kwa wateja wanaotoka nje ya nchi hutakiwa kutoa pasi ya kusafiria, ambayo kimsingi huwa na majina yake kamili, kisha anajisajili. Kwa wale wa nchini, anaeleza pamoja na taarifa nyingine muhimu lazima waache kitambulisho ama cha uraia, kupiga kura au leseni ya udereva na kisha anaandikishwa ndiyo apatiwe huduma. “Hilo linafanyika hata kwa mgeni wa mteja, kwa mfano mteja kaingia na vielelezo vyote kakamilisha, baadaye amekuja mgeni wake, hataruhusiwa kuingia hadi kwanza ithibitike ni mgeni wa nani, pia atatakiwa kuacha kitambulisho chake mapokezi hadi atakapotoka ndiyo atapewa,” anasema. Hayo yote, anasema yanafanyika kudhibiti uhalifu na matukio mengine mabaya katika hoteli. Mtazamo wa kisheria Ingawa huduma za nyumba za kulala wageni husimamiwa na sheria ndogondogo zinazotungwa na halmashauri ilipo nyumba husika, Wakili Jebra Kambole anasema ipo Sheria ya Hotel sura ya 105 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2006, inayotoa mwongozo wa huduma hizo. Ibara ya 18 ya sheria hiyo, inawalazimu wahudumu wa hoteli kuhakikisha wanaweka rejista itakayotumika kuandika majina ya wateja watakaolala katika nyumba hiyo na maelezo mengine yatakayohitajika. Kulingana na kifungu hicho, kutakuwa na kitabu kitakachowekwa katika hoteli husika kwa ajili ya kuandikia majina hayo kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Vileo. Kifungu hicho cha 15 (2) cha Sheria ya Vileo ya mwaka 1968, inasema mmiliki wa leseni ya hoteli anapaswa kuweka kitabu cha wageni katika nyumba hiyo na kumlazimu kila mteja kuandika jina na anwani yake mara tu anapoingia. Kumbe mapato yanapotea! Kitendo cha kutoandika jina kwa namna nyingine ni hasara kwa Serikali kwani kinapoteza mapato yaliyopaswa kuingia katika halmashauri ilipo nyumba ya kulala wageni. Kifungu cha 26 (2) cha sheria hiyo ya hoteli, kinamtaka mmiliki kulipa asilimia 20 ya jumla ya mapato yanayotokana na malipo ya wateja wanaolala kwenye nyumba husika kwa kila mwezi. Ushuru huo kwa mujibu wa sheria hiyo, unapaswa kulipwa kuanzia tarehe 1 hadi 7 ya kila mwezi. Kitabu cha wageni katika nyumba hiyo ndicho kitakachotumika kujua idadi ya wateja waliolala na kiwango cha ushuru kitakachopaswa kutozwa. Hii ni kwa wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni ambazo hawajasajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Kinyume na kutekeleza hilo, sheria hiyo inaweka wazi kuwa asilimia 25 itatozwa kwa nyumba husika iwapo itabainika imechelewa kulipa ushuru zaidi ya siku saba, kwa mujibu wa ibara ya 32(a). Lakini ukidanganya mapato na kutokuwa na kitabu cha kumbukumbu itakulazimu ulipe faini ya Sh500,000, huku atkayebainika kutolipa ushuru tangu hoteli ilipoanzishwa atatozwa faini ya Sh2 milioni.
Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumteuwa Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu wake Mkuu, wanasiasa wa
Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumteuwa Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu wake Mkuu, wanasiasa wa chama hicho wamesifu uteuzi wake, huku wapinzani wakimtahadharisha na siasa za mabavu. Dk Nchimbi ameteuliwa leo Januari 15, 2024 na Kamati Kuu ya CCM na baadaye kuridhiwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho, iliyoketi visiwani Zanzibar na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan. Kuteuliwa kwa Dk Nchimbi kunakuja wiki sita tangu CCM ilipokosa Katibu Mkuu, baada ya aliyekuwa na wadhifa huo, Daniel Chongolo kujiuzulu kwa madai ya kuchafuliwa mitandaoni. Uteuzi huo uliwaibua wadau mbalimbali waliozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Januari 15, 2024, akiwemo Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Sophia Simba aliyeeleza kufurahishwa na hilo. Sophia amesema Dk Nchimbi ni mtu sahihi kwenye wadhifa huo kwa kuwa hana unafiki na ni muwazi. Amesema CCM ilihitaji mtu kama Dk Nchimbi kwenye nafasi hiyo huku akisisitiza kwamba anastahili kwa uzoefu na uwezo wake. “Mashaallah…sasa CCM tumepata Katibu Mkuu, anafaa kwa kuwa hana unafiki wala makundi na ni muwazi. Chama kilihitaji mtu kama yeye, sio hao wanaopitapita,” amesema. Ikumbukwe Sophia ni mmoja wa wanasiasa waliowahi kukumbwa na adhabu pamoja na Dk Nchimbi baada ya kutuhumiwa kwa hujuma ndani ya CCM katika uchaguzi wa mwaka 2015. Kutokana na tuhuma hizo ambazo hatua zilichukuliwa mwaka 2017, Sophia alifukuzwa uanachama, huku Dk Nchimbi akipewa onyo kali na kutoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne. Mbali na Sophia mwingine aliyezungumzia uteuzi huo ni Balozi Christopher Liundi aliyesema Dk Nchimbi ni miongoni mwa wanasiasa wenye mizizi ndani ya chama hicho kwa kuwa walianza kukitumikia kitambo. “Nakumbuka baba yake (Mzee John Nchimbi) alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, wakati huo mimi nikiwa mkuu wa mkoa huo, kwa hiyo Nchimbi alianza mbali sana na CCM,” amesema. Kwa uzoefu wa Dk Nchimbi, Balozi Liundi aliyewahi kuiwakilisha Tanzania nchini Ethiopia, amesema utamwezesha kukiongoza chama hicho katika dira inayostahili na kupata manufaa makubwa kwa wanachama na Taifa kwa ujumla. Ameongeza fani yake (Dk Nchimbi) katika diplomasia itampa nafasi ya pekee kutumia mbinu mbalimbali za kidiplomasia kutatua matatizo mbalimbali sio tu ya wanachama bali kitaifa. “Nina matumaini makubwa wala sina mashaka lakini la msingi ni tumsaidie, pale ambapo utahitajika ushauri ashauriwe ili apate mafanikio mazuri kwenye kazi yake kubwa na manufaa makubwa kwa chama hicho na taifa kwa ujumla,” amesema Balozi Liundi aliyewahi pia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Wapinzani wamtahadharisha Alipoulizwa kuhusu uteuzi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amemkaribisha Dk Nchimbi kwenye mapambano ya kisiasa, huku akimtahadharisha na siasa za mabavu. “Anapaswa kutambua kuwa amerithi nafasi katika chama ambacho kinaogopa mijadala ya wazi na maandamano, kwa hiyo ataamua awe hivyo au abadilike,” amesema. Hata hivyo, Mrema amemtaka mtendaji mkuu huyo mpya wa CCM, ajiandae kukabiliana na ushindani wa hoja na sio kutumia nguvu ya dola. “Akiamua kutumia nguvu ya dola na mabavu hatadumu kwa muda mrefu kwenye nafasi yake, kwa sababu duniani kote siasa za mabavu hazijawahi kushinda,” amesema Mrema. Wakati huohuo, katika ukurasa wake wa Instagram, aliyekuwa na wadhifa huo, Chongolo amempongeza Dk Nchimbi kwa kuaminiwa na kupewa nafasi hiyo, akisema hana mashaka naye. “Hongera saaana Balozi Dk Emmanuel Nchimbi kwa kuaminiwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan na kupendekeza jina lako na NEC kuridhia wewe kupeperusha bendera ya CCM kwa dhamana ya Mtendaji Mkuu, Katibu Mkuu. “Imani ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwako ni kubwa sana nasi wana CCM hatuna mashaka nawe. Hongera saaana na kila lakheri!” ameandika.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimempitisha Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichuk
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimempitisha Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, mwaka jana. Kujiuzulu kwa Chongolo, kulitokana na kile alichoandika katika barua yake Novemba 27 mwaka jana kuwa, amelazimika kuwajibika kutokana na kudhalilishwa katika mitandao ya kijamii. Hata hivyo, uteuzi wa Dk Nchimbi katika nafasi hiyo ulitabiriwa na wadau mbalimbali wa siasa akihusishwa yeye, Martin Shigella, William Lukuvi na Amos Makalla, wote ni makada wa kitambo ndani ya chama hicho. Makada na wanadiplomasia wenzake, wanasema ni mtu sahihi kwenye nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake wa uongozi wa CCM, lakini si mnafiki na hana makundi. Historia ya Dk Nchimbi ndani ya CCM unaweza kuifananisha na umri wa mtu mzima. Ameanza kuwa kiongozi katika chama hicho mwaka 1998 alipochaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Hakuishia hapo, baadaye alichaguliwa na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kuwa Mwenyekiti wao na hivyo aliiongoza jumuiya hiyo pia. Mwaka 2005, mwanasiasa huyo alijitosha katika kinyang’anyiro cha kuwania ubunge wa Songea Mjini, alikopata ushindi wa asilimia 67.6 dhidi ya mpinzani wake mkuu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edson Mbogoro. Ubunge wake, ulifungua milango mingine ya nyadhifa ndani ya Serikali, Januari mwaka 2006, Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete alimteuwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. Alidumu kwenye wadhifa huo kwa miezi tisa na Oktoba mwaka huo alihamishiwa Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana akiwa na nafasi ile ile hadi Februari mwaka 2008. Mwanasiasa huyo alihamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwa Naibu waziri, alikohudumu hadi mwaka 2010. Kipyenga cha uchaguzi kilipopigwa mwaka 2010, aliwania tena ubunge katika eneo lile lile na alishinda na kuanzia hapo nyadhifa zake ndani ya Serikali ziliongezeka. Rais Kikwete alimteuwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo hadi Mei mwaka 2012, alipohamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani kabla ya kuamua kujiuzulu Desemba mwaka 2013. Msingi wa kujiuzulu kwake ni shinikizo, baada ya ripoti ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, iliyoongozwa na Mbunge wa Kahama, James Lembeli juu ya “Oparesheni Tokomeza”. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Dk Nchimbi alikuwa miongoni mwa makada wa CCM waliotangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya chama hicho. Hata hivyo John Magufuli ndiye aliyepitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho. Baada ya Uchaguzi huo, mwaka 2016, Dk Nchimbi aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil kisha mwaka 2022 aliteuliwa kuiwakilisha Tanzania nchini Misri alikohudumu hadi mwaka 2023 na kurudi nchini. Misukosuko ndani ya CCM Machi mwaka 2017, akiwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil Dk Nchimbi aliwahi kukumbwa na msukosuko ndani ya chama chake, akipewa onyo kali na adhabu ya kutogombea nafasi yoyote kwa kipindi cha miaka minne. Adhabu hiyo ilitokana na kile kilichoelezwa na CCM kuwa, ni usaliti katika uchaguzi wa mwaka 2015. Hata hivyo makada wengine wa chama hicho walifutwa uanachama akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT), Sophia Simba. Katika uchaguzi huo, Dk Nchimbi alijitokeza hadharani kupinga uamuzi wa CCM kumpendekeza Magufuli kuwa mgombea wake wa urais. Wasifu zaidi Kada huyo alizaliwa Desemba 24, mwaka 1971 mkoani Mbeya na alianza masomo katika Shule ya Msingi Oysterbay, Dar es Salaam mwaka 1980 hadi 1986. Mwaka 1987 hadi 1989 alisoma elimu ya Sekondari katika shule ya Uru na baadaye kuhamia Shule ya Sekondari Sangu alikomalizia kidato cha nne mwaka 1990. Kidato cha tano na sita alisoma katika Shule ya Sekondari ya Forest Hill mkoani Morogoro mwaka 1991 hadi 1993. Alijiunga katika Chuo cha IDM Mzumbe na kuhitimu Stashahada ya Juu ya Utawala 1997. Baadaye alisoma shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara katika chuo hicho, mwaka 2001 hadi 2003 akibobea kwenye maeneo ya benki na fedha na mwaka 2011 alihitimu shahada ya uzamivu (PhD) katika chuo hicho. Dk Nchimbi ni mume na baba wa watoto watatu. Anafaa si mnafiki Akizungumzia uteuzi huo, kada wa chama hicho, Sophia Simba alisema Dk Nchimbi ni mtu sahihi kwenye wadhifa huo kwa kuwa hana unafiki na ni muwazi. Alieleza CCM ilihitaji mtu kama Dk Nchimbi kwenye nafasi hiyo, akisisitiza amestahili kwa uzoefu na uwezo wake. “Mashaallah… Sasa CCM tumepata Katibu Mkuu, anafaa kwa kuwa hana unafiki wala makundi na ni muwazi. Chama kilihitaji mtu kama yeye sio hao wanaopitapita,” alisema Sophia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa UWT Taifa. Ana mizizi ndani ya CCM Mwanadiplomasia mbobezi, Balozi Christopher Liundi alisema Dk Nchimbi ni miongoni mwa wanasiasa wenye mizizi ndani ya chama hicho kwa kuwa walianza kukitumikia kitambo. “Nakumbuka baba yake (Mzee John Nchimbi) alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, wakati huo mimi nikiwa Mkuu wa Mkoa huo, kwa hiyo Nchimbi alianza mbali sana na CCM,” alisema. Kwa uzoefu wa Dk Nchimbi, Balozi Liundi aliyewahi kuiwakilisha Tanzania nchini Ethiopia, alisema utamwezesha kukiongoza chama hicho katika dira inayostahili na kupata manufaa makubwa kwa wanachama na taifa kwa ujumla. Lakini, alisema fani yake ya diplomasia itampa nafasi ya pekee kutumia mbinu mbalimbali za kidiplomasia kutatua matatizo mbalimbali sio tu ya wanachama bali kitaifa. “Nina matumaini makubwa wala sina mashaka lakini la msingi ni tumsaidie, pale ambapo kutahitajika ushauri ashauriwe ili apate mafanikio mazuri kwenye kazi yake kubwa na manufaa makubwa kwa chama hicho na taifa kwa ujumla,” alisema Balozi Liundi aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.
Nchi zilizoendelea zinatarajiwa kukumbwa na athari ya asilimia 60 katika ajira zake, kutokana na kui
Nchi zilizoendelea zinatarajiwa kukumbwa na athari ya asilimia 60 katika ajira zake, kutokana na kuingia kwa teknolojia ya akili bandia (AI). Hayo yameelezwa leo Jumatatu, Januari 15, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Kristalina Georgieva alipozungumza katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF). “Mataifa yaliyoendelea kiuchumi na yeenye masoko makubwa, yatakabiliwa na athari katika ajira zake kwa asilimia 60,” amesema akinukuu ripoti ya IMF iliyochapishwa jumapili. Amesema kwa nchi zenye uchumi wa chini ajira zitakazoathiriwa na teknolojia hiyo ni asilimia 26 pekee na kwamba athari katika ulimwengu mzima itakuwa ni asilimia 40. Ripoti ya IMF inaeleza karibu nusu ya ajira zitakumbwa na athari hasi, huku nyingine zikizaa matokeo chanya yanayotokana na ongezeko la ufanisi na uzalishaji kupitia tekmolojia ya AI. "Kazi zenu ama zinaweza kupotea au AI inaweza kuziboresha zikawa na tija zaidi na kipato kitaongezeka,” amesema mkurugenzi huyo. Kulingana na IMF, mwanzoni teknolojia hiyo itaathiri masoko yanayoibukia na nchi zinazoendelea kiuchumi, kadhalika zitachelewa kufaidika kutokana na kutokuwa na teknolojia hizo. "Hii inaweza kuzidisha mgawanyiko wa kidijitali na tofauti ya mapato ya nchi mbalimbali," ripoti hiyo inaeleza. Hata hivyo, Georgieva amesema ni muhimu mataifa yakawa na sera zinazosaidia kuendana na teknolojia hizo ili kukabiliana na athari tarajiwa. “Lazima tujikite katika kuzisaidia nchi za kipato cha chini hasa zisonge mbele kwa kasi ili kupata fursa zitakazotokana na akili bandia. "Akili bandia ndiyo, inatisha kidogo. Lakini pia ni fursa kubwa kwa kila mtu," amesema.
Huenda leo swali kuhusu mrithi wa Daniel Chongolo katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduz
Huenda leo swali kuhusu mrithi wa Daniel Chongolo katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) likapata majibu, hii inatokana na kufanyika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho. Kikao hicho kinachofanyika visiwani Zanzibar leo Jumatatu, Januari 15, 2024 kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, ndicho chenye mamlaka ya kupendekeza jina la mtu wa kushika wadhifa huo. Hiki ni kikao cha ngazi ya juu cha kwanza ambacho CCM inakifanya bila kuwa na Katibu Mkuu, baada ya wiki sita zilizopita Chongolo kuandika barua ya kujiuzulu na Rais Samia kuridhia uamuzi huo, Novemba 29, mwaka jana. Kilichosababisha Chongolo ajiuzulu wadhifa huo ni kile alichokibainisha katika barua yake ya kujiuzulu ya Novemba 27, mwaka jana kuwa, amelazimika kuwajibika baada na kudhalilishwa katika mitandao ya kijamii. Baada ya ridhaa hiyo ya Rais Samia, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Anamringi Macha ndiye aliyekaimishwa kushika nafasi hiyo. Lakini, makada wa chama hicho, wanasema pamoja na kwamba uamuzi wa kupendekeza jina la atakayeshika wadhifa huo kuwa chini ya mamlaka ya sekretarieti, lakini ni muhimu kupatikana kwa kiongozi huyo. Mjumbe mstaafu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Angel Akilimali amesema lazima chama kiwe na mtendaji mkuu, kwa kuwa kwa sasa hakinaye. Hata hivyo, amesema ajenda zilizowekwa ndizo zinazoamua mwelekeo wa kikao hicho, hivyo ni vigumu kujua kama atapatikana leo au laa kwa kuwa hajaziona ajenda hizo. “Ni kweli hatuna Katibu Mkuu ni muhimu tuwe naye kwa sababu lazima chama kiwe na mtendaji mkuu, kwa sababu sekretarieti inaongozwa na Katibu Mkuu hivyo ni muhimu apatikane,” amesema. Lakini amesema uamuzi wa kupatikana kwake, utafanywa na kikao hicho na kupitishwa na halmashauri kuu ya chama. Mwananchi Digital imedokezwa na chanzo cha kuaminika kuwa, pendekezo la jina la Katibu Mkuu mpya ni moja ya mambo yatakayofanywa na kikao hicho. “Hiyo ipo,” kimeeleza chanzo hicho kilipoulizwa iwapo kuteuliwa kwa Katibu Mkuu mpya ni moja ya mambo yatakayofanyika katika kikao hicho. Hata hivyo, chanzo hicho hakikutaja jina lililopendekezwa, kwa kile kilichoeleza bado halijawekwa wazi mbele ya wajumbe. Hata hivyo, wapo wanaotajwa kuwa katika uwekezakano wa kupewa nafasi hiyo, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla, Mwanadiplomasia Emmanuel Nchimbi na Mshauri wa Rais, Siasa na Uhusiano wa Jamii, Abdallah Bulembo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella.
Ili kuongeza tija ya ushirikiano baina ya Tanzania na Angola, mataifa hayo yamekutana kujadili masua
Ili kuongeza tija ya ushirikiano baina ya Tanzania na Angola, mataifa hayo yamekutana kujadili masuala ya kisiasa, diplomasia, ulinzi na usalama. Mkutano huo wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPU), umeanza kufanyika leo, Januari 14 hadi 16, mwaka 2024, ukihusisha ngazi ya maofisa waandamizi wa Serikali na Mawaziri. Hii ni mara ya pili kwa mataifa hayo kukutana kwa mkutano huo, awali yalikutana Oktoba, 1988 jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, mkutano huo unafanyika kipindi ambacho nchi hizo zimesaini Hati mbili za Makubaliano (MoUs) za kuhuisha au kufufua Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola mwezi Februari 2023 Addis Ababa. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, leo Januari 14, 2024, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa amesema kinachojadiliwa ni ushirikiano katika sheria, kilimo, uchumi wa buluu, biashara na uwekezaji. Maeneo mengine yatakayojadiliwa kwa mujibu wa Balozi Mussa ni miundombinu, ujenzi, uchukuzi, nishati, madini, tehama na huduma za kijamii yaani afya, elimu, sayansi na teknolojia ya Habari na mawasiliano. Amesema maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Angola, yanatarajiwa kuibuliwa kutokana na mkutano huo. “Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo uchumi hususan biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, miundombinu na fedha,” amesema. Mipango na mikakati, amesema itatolewa kupitia mkutano huo, inayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote. Katika hotuba yake, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola, Balozi Carlos Dias amesema mikutano ya JPC inatoa fursa za kujadili masuala ya kisekta katika maeneo mahususi ya kipaumbele kwa maslahi ya pande zote. “Mikutano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano itaendelea kujadili masuala ya kisekta katika maeneo mahususi ya ushirikiano katika nyanja za diplomasia, usalama, ulinzi na uboreshaji wa huduma za kijamii,” amesema. Mkutano huu umejumuisha Mabalozi, Watendaji Wakuu na Maofisa mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania na Angola.
Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na uny
Imebainika kuwa asilimia 77 ya wanahabari wanawake 137 waliohojiwa wameeleza kuwahi kukumbana na unyanyasaji wa kingono katika vyombo vya habari. Hayo ni kulingana na utafiti wa hali ya usalama wa wanahabari wanawake katika vyumba vya habari uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) katika vyombo vya habari 22. Akisoma muhtasari wa utafiti huo, Mkurugenzi wa Tamwa, Dk Rose Reuben amesema kati ya wanahabari hao waliokumbwa na unyanyasaji wa kijinsia, asilimia 27 wamekumbana nao kutoka kwa vyanzo vyao vya habari. Ameeleza asilimia 59, wamekumbana na kadhia hizo kutoka katika vyumba vyao vya habari na hasa watendaji wakubwa wakiwa ni wahariri, mameneja na wamiliki wa vyombo hivyo. "Unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono unaathiri ubora na uaminifu wa waandishi wa habari iwapo changamoto hizo zitakaa kwa muda mrefu," amesema Dk Rose. Hata hivyo, amesema utafiti huo umefaywa kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu katika Mikoa kadhaa nchini. Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew ameahidi kufanyia kazi changamoto zote za kisheria na kisera zinazoihusu taaluma ya habari. "Serikali inaendelea kufanyia maboresho sera na sheria zilizopitwa na wakati na kwamba maoni na ushauri katika sheria zinazoenda kutungwa utafanyiwa kazi," alisema. Alisema tasnia ya habari imekuwa na changamoto lukuki na Serikali imeendelea kuzishughulikia kupitia mabadiliko mbalimbali yakiwemo ya kisheria. Akizungumzia usawa wa kijinsia katika vyumba vya habari, alisema tafiti zinaonyesha asilimia 34 ya waandishi wa habari wanaume wana uhakika wa kupewa mikataba ya kazi na mabosi huku asilimia 66 ya wanahabari wanawake wakikosa uhakika wa hilo. Alieleza ili kuhakikisha masuala ya usawa wa jinsia yanaingizwa katika taaluma Wizara hiyo, imeona haja ya kuwepo na Ofisa maalum anayeshughulikia ujumuishaji wa jinsia katika taaluma ya habari. Kutokana na utafiti wa Tamwa, Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya alisema kinachofanywa na umoja huo ni kukusanya kanzidata ya matukio na kuvifuata vyombo vya habari kimoja kimoja. Alisema umoja huo umekuwa ukipokea taarifa nyingi za unyanyasaji katika vyumba vya habari na jukumu inalotarajia kufanya ni kuelimisha vyumba vya habari. "Kwa sasa tunaunda kanzidata ili tutoe ripoti na kuona namna ya kuvifikia vyumba vya habari kwa kuwa yapo mambo yanayohitaji kuelimishana tu," alisema. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwepo muongozo wa kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vyombo vya habari, lakini kwa sehemu kubwa hayakuanzishwa. Alieleza wakati hilo likitarajiwa kufanyika ni vema elimu ianze kutolewa ili wanahabari wasione aibu kuyatumia madawati hayo. "Watu wasione wanapokwenda kuripoti watajidhalilisha au pengine wamewahi kuona walipripoti na hakuna hatua iliyochukuliwa," alisema. Akichangia mjadala kuhusu hali ya rushwa katika vyumba vya habari, Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dorothea Mrema aliwasisitiza wanaokumbwa na madhira watoe taarifa kwa taasisi hiyo. Alisema mapambano dhidi ya aina hiyo ya rushwa na nyingine ni jukumu la wananchi wote, hivyo kila mmoja na kila taasisi inapaswa kuonyesha juhudi za mapambano hayo. "Kila taasisi inapaswa kushiriki mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa mkakati wa mapambano dhidi ya rushwa wa kitaifa unataka kila taasisi ipambane na rushwa, huu ni wajibu na jukumu la kila mmoja," alisema. Hata hivyo, alisema Takukuru imekuwa ikipokea taarifa kuhusu matukio hayo na aghalabu huwachukulia hatua kwa kuwapeleka mahakamani baada ya kuthibitika.
Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na uj
Katika kipindi cha maendeleo ya kasi ya digitali, ni muhimu vijana wa Tanzania wawezeshwe kuwa na ujuzi na maarifa muhimu ili kujenga ustawi wa karne ya 21. Kwa kutambua hitaji hilo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua mpango wa kuanzisha klabu za kidigitali, unaolenga kukuza ujuzi wa kidijitali na ubunifu kwa vijana nchini. Kuhusu Klabu za Kidigitali Klabu za Dijitali ni mtandao wa vilabu vilivyoanzishwa katika shule mbalimbali nchini. Vilabu hivi hutumika kama jukwaa la wanafunzi kufuatilia vipengele mbalimbali vya teknolojia, kutoka kwa usimbaji 'coding' na upangaji programu hadi muundo wa wavuti na uuzaji wa dijiti. Kupitia shughuli za mikono, warsha na mashindano, washiriki wa klabu za Dijitali hupata ujuzi muhimu unaoboresha uwezo wao wa kuajiriwa na kuwaandaa kwa mahitaji ya uchumi wa kidijitali. Majukwaa haya pia yanawapa motisha wanafunzi kupenda ujuzi wa kidijitali kupitia kujifunza masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu (STEM). Kupitia vilabu hivyo, wanafunzi pia wanaonyeshwa fursa mbalimbali na wanakutanishwa na washikadau katika sekta hiyo. Kuimarisha ujifunzaji wa masuala ya digitali na ubunifu, klabu hizi zitaongeza ujuzi wa kiufundi, kadhalika kutakuza ubunifu na utatuzi wa changamoto. Kukuza usomaji wa digitali na ubunifu mpango wa klabu za digitali unajikita zaidi katika kutoa ujuzi wa kiufundi, pia inalenga kukuza ubunifu, utatuzi wa matatizo na kazi ya pamoja miongoni mwa washiriki. Kwa kuwahimiza wanafunzi kutumia maarifa yao mapya kutatatua changamoto za ulimwengu na hivyo klabu za kidigitali zitakuza utamaduni wa ubunifu, uvumbuzi na ujasiriamali miongoni mwa vijana. Zaidi ya hayo, klabu hizi zinahamasisha, wanafunzi, wasomi na watafiti kupenda masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Kuimarisha Fursa za Kielimu Klabu za Kidigitali sio tu zitaboresha maisha ya washiriki wake, bali pia zitaimarisha mazingira ya elimu nchini. Kwa kuwapa wanafunzi fursa ya kupata teknolojia na rasilimali za kidijitali, klabu hizo zitahakikisha vijana nchini wanapata fursa ya kushiriki katika ulimwengu wa kidijitali. Wajibu wa TCRA TCRA, ndiyo itakayoendesga mpango wa klabu hizo na itahusika kutoa msaada wa miundombinu muhimu ili kuhakikisha programu inafanikiwa. Katika kufanikisha hilo, TCRA imeshirikiana na wadau mbalimbali, zikiwemo shule, vyuo vikuu na washirika wa sekta hiyo, ili kuunda mfumo mpana wa ikolojia unaokuza maendeleo ya ujuzi wa kidijitali miongoni mwa vijana wa Tanzania. Mpango huu ni mustakabali mwema kwa vijana nchini utakaowawezesha kuwa na ujuzi na maarifa yanayohitajika ili kufanikiwa katika zama za kidigitali. Kwa kukuza elimu ya kidijitali, uvumbuzi na ujasiriamali, Vilabu vya Dijitali vinaweka msingi wa mustakabali mwema kwa vijana nchini. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, aliahidi Serikali kuunga mkono mpango huo. Alisisitiza dhamira ya Serikali kuunda mfumo wa sera utakaokuza uvumbuzi wa kidijitali kote nchini. Abdulla pia alitoa wito wa kuchukua hatua na kuzitaka shule, vyuo, vyuo vikuu na wadau wote wanaohusika na sekta ya elimu kushiriki kikamilifu katika kuanzisha Vilabu vya Digital ndani ya taasisi zao. Alipongeza juhudi za TCRA katika kuendeleza uanzishwaji wa vilabu hivyo na kuhimiza kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa na kuleta matokeo makubwa. Ushiriki wa Wizara na wito wake, unasisitiza umuhimu wa mpango wa Klabu za Dijitali katika kuwawezesha vijana wa Tanzania kwa ujuzi unaohitajika ili kustawisha karne ya 21. Kwa dhamira ya Serikali, kujitolea kwa TCRA na ushiriki wa taasisi za elimu, mpango wa klabu za digitali uko tayari kubadilisha hali ya kidijitali ya Tanzania na kutengeneza mustakabali mzuri wa vijana nchini.
Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Romania, Klaus Iohannis atakayewasili nchini kesho kwa
Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Romania, Klaus Iohannis atakayewasili nchini kesho kwa ziara ya kitaifa ya siku nne. Ziara ya mkuu huyo wa taifa hilo la Ulaya, inatazamwa kama tumaini jipya la kufufuka kwa biashara kati ya Tanzania na Romania iliyoshuhudiwa ikidorora kwa miaka ya hivi karibuni. Hilo linathibitishwa na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyobainisha kushuka kwa mauzo ya Tanzania katika taifa hilo kwa karibu mara mbili katika miaka ya 2021 na 2022. Kulingana na taarifa hiyo, mwaka 2021 Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani 7.9 milioni (zaidi ya Sh 19.7 bilioni) ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo iliuza Dola za Marekani 4.06 milioni (zaidi ya Sh10.14 bilioni). Manunuzi ya Romania kwa bidhaa za Tanzania yalipungua pia, ikinunua bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani 11.6 milioni (zaidi ya Sh28.97 bilioni) huku mwaka 2022 ikinunua zenye thamani ya Dola za Marekani 2.4 milioni (zaidi ya Sh5.9 bilioni). Taarifa iliyotolewa leo, Novemba 15, 2023 na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inabainisha ziara ya mkuu wa taifa hilo ni mwitikio wa mwaliko aliopewa na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ziara ya Iohannis ni ukurasa mpya wa kuimarika kwa ushirikiano wa nchi hizo ulioanza mwaka 1964 katika sekta za afya na elimu. Taarifa hiyo inasema maeneo mapya ya ushirikiano yanatarajiwa kupatikana katika ziara hiyo, ambayo ni uwekezaji, elimu, utalii, afya na utamaduni. “Kwa sasa uhusiano wa Tanzania na Romania unahusisha uwekezaji na biashara ya minofu ya samaki aina ya sangara, chai, tumbaku na parachichi. “Lakini, Tanzania inanunua bidhaa za mshine za umeme, vifaa vya matrekta, magari na vifaa vya matibabu kutoa Romania,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. Si biashara pekee, hata uwekezaji na sekta ya utalii inatarajiwa kuimarika kutokana na ziara hiyo, kwani kwa sasa Romania imewekeza nchini katika miradi ya usafirishaji, viwanda na utalii yenye thamani ya Dola za Marekani 6.04 milioni na kuzalisha ajira 89. Kwa upande wa visiwani Zanizibar miradi mitatu yenye thamani ya Dola za Marekani 7.5 milioni kwa mwaka huu na kuzalisha ajira 64. “Ziara hiyo ni fursa muhimu kwa Tanzania kuvuna soko la utalii kutoka taifa hilo, ambalo kwa sasa watalii kutoka Romania wameongezeka kutoka 6,418 mwaka 2018 hadi 12,148 mwaka 2022,” ilieleza. Ziara itakavyokuwa Mkuu huyo wa taifa hilo la Ulaya, anatarajiwa kuwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNICC) na atapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba. Novemba 17, mwaka huu kiongozi huyo atapokelewa rasmi Ikulu ya Dar es Salaam na atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Samia yatakayofuatiwa na mazungumzo rasmi kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Romania. Baada ya shughuli hiyo, wawili hao watashuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano kati ya Tanzania na Romania katika sekta za kilimo, mifugo, misitu, chakula na uokoaji wakati wa dharura. Kulingana na taarifa hiyo, wawili hao watadokeza sehemu ya mazungumzo yao ya faragha mbele ya waandishi wa habari. Siku inayofuata, Iohannis atasafiri kwenda visiwani Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa visiwani humo, Dk Hussein Ali Mwinyi na akiwa huko atatembelea kivutio cha utalii cha Mji Mkongwe.