name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
Baada ya kukamilisha ripoti ya mapendekezo ya mageuzi ya mifumo na taasisi za haki jinai, tume iliyo | Baada ya kukamilisha ripoti ya mapendekezo ya mageuzi ya mifumo na taasisi za haki jinai, tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuifanya kazi hiyo, imebadilishiwa jukumu na sasa inasimamia utekelezwaji wake.
Tume hiyo iliyokuwa na wajumbe tisa iliundwa Januari 31, mwaka huu ikipewa jukumu la kupendekeza mageuzi y... |
Hofu dhidi ya Serikali na kunyemelea uteuzi ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa kuwa sababu ya kufifia | Hofu dhidi ya Serikali na kunyemelea uteuzi ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa kuwa sababu ya kufifia kwa mijadala ya wasomi nchini.
Kulingana na mwanazuoni Profesa Issa Shivji, Tanzania imepitia kipindi cha wingu zito la mijadala ya wasomi, jambo alilolitaja kama kikwazo cha maendeleo ya nchi.
Kauli ya mwanazuoni huyo ... |
Mbinu zinazotumiwa na Serikali jijini Dar es Salaam kukomesha biashara ya ukahaba, zimekosolewa na w | Mbinu zinazotumiwa na Serikali jijini Dar es Salaam kukomesha biashara ya ukahaba, zimekosolewa na wadau, wakiitaka ianze kwa kuangalia mzizi wa tatizo, badala ya kuwakabili wahusika wa vitendo hivyo.
Kulingana na wadau hao wa haki za binadamu na wataalamu wa sheria, ni muhimu kuzikabili sababu zilizowafanya wajihusish... |
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imesema imekamilisha maandalizi ya vitabu vya kiada katika madarasa | Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imesema imekamilisha maandalizi ya vitabu vya kiada katika madarasa yote yanayotarajiwa kuanza kutekeleza sera na mitalaa mipya ya elimu mwaka 2024.
Madarasa yanayotarajiwa kuanza kutekeleza sera hiyo kwa shule za msingi ni darasa la awali, la kwanza hadi la tatu, huku upande wa Sekonda... |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteuwa Aziza Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Jamhuri ya Muung | Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteuwa Aziza Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapunduzi (CCM).
Aziza anateuliwa kushika wadhifa huo, ulioachwa wazi na Bahati Ndingo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.
Bahati alijiuzulu nafasi ya ubunge wa v... |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteuwa Aziza Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Jamhuri ya Muung | Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteuwa Aziza Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapunduzi (CCM).
Aziza anateuliwa kushika wadhifa huo, ulioachwa wazi na Bahati Ndingo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.
Bahati alijiuzulu nafasi ya ubunge wa v... |
Licha ya mapendekezo mbalimbali yanayoelekeza uchunguzi dhidi ya utaratibu wa kukiri makosa kwa hiar | Licha ya mapendekezo mbalimbali yanayoelekeza uchunguzi dhidi ya utaratibu wa kukiri makosa kwa hiari (Plea Bargaining), wahanga wa utaratibu huo wameonyesha wasiwasi wa suala hilo kutekelezwa.
Wasiwasi wao unatokana na kile walichoeleza, kumekosekana utashi wa kisiasa wa kuchukua hatua za kiuchunguzi dhidi ya utaratib... |
Imechukua zaidi ya karne tangu mabaki ya miili ya Watanzania yahifadhiwe katika makumbusho mbalimbal | Imechukua zaidi ya karne tangu mabaki ya miili ya Watanzania yahifadhiwe katika makumbusho mbalimbali nchini Ujerumani na sasa uamuzi wa kuyarejesha umefikia hatua nzuri.
Baadhi ya mabaki hayo ni yake ya miili ya machifu na viongozi mbalimbali waliokuwa vinara katika vita vya Tanganyika dhidi ya Ujerumani (Maji Maji),... |
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, anatarajiwa kufanya ziara ya ki | Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini kuanzia kesho hadi Novemba 1, 2023.
Hayo yameelezwa leo, Oktoba 29, 2023 kupitia taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kulingana na taari... |
Ili kuongeza upatikanaji wa taarifa za Serikali kwa wananchi, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Mati | Ili kuongeza upatikanaji wa taarifa za Serikali kwa wananchi, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema ofisi yake inatarajia kwenda katika Mikoa mbalimbali nchini kuwapa nafasi Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa halmashauri waeleze kilichofanywa na Serikali katika maeneo yao.
Amesema utaratibu huo unatarajiwa ku... |
Tanzania imetupa karata yake kugombea nafasi ya Urais wa Bunge la Dunia (IPU) katika uchaguzi unaota | Tanzania imetupa karata yake kugombea nafasi ya Urais wa Bunge la Dunia (IPU) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, huku Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akiteuliwa kuipeperusha bendera ya nchi kuwani nafasi hiyo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki kinyang’anyiro hicho, kadhalika iwapo itash... |
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inatarajia kuongeza siku za usafiri bila viza kwa wananch | Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inatarajia kuongeza siku za usafiri bila viza kwa wananchi wa Zambia wanaoingia nchini kutoka siku 90 za sasa hadi 190.
Utekelezaji wa hilo, utatoa uhuru wa usafiri kwa W azambia kuingia nchini na kukaa kwa siku 190 bila kulazimika kununua viza.
Rais Samia ametangaza mpango hu... |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Jokate Mwegelo amewataka wabunge wa viti maa | Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Jokate Mwegelo amewataka wabunge wa viti maalum wasiishie kujipendekeza kwa wajumbe pekee, badala yake wawe wanafanya vikao vya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kwani ndiyo msingi wa nafasi walizopewa.
Kauli ya Jokate, inatokana na kile alichodokeza, kumek... |
Wakati wananchi wakitaka kuwekwa wazi kwa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bandari ya Dar es Sala | Wakati wananchi wakitaka kuwekwa wazi kwa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bandari ya Dar es Salaam, Serikali imesema ni vigumu kutekeleza hilo, kwa kuwa ni kinyume na matakwa ya kisheria.
Hoja ya uwazi wa mikataba hiyo iliambatana na pongezi za kuzingatiwa kwa maoni ya wananchi katika utengenezaji wa mikataba hiyo ... |
Kama umestaajabu uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM, kumteuwa Paul Makonda kuwa Katibu wake wa Itikadi | Kama umestaajabu uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM, kumteuwa Paul Makonda kuwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, makada wa chama hicho na wanazuoni mbalimbali wanaeleza sababu za kwanini amekuwa yeye na si mwingine.
Uamuzi wa uteuzi wa Makonda katika nafasi hiyo, kwa mujibu wa wanazuoni hao, umetokana na malengo ya cham... |
Uteuzi wa Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM ndio habari ya mjini, kwani mijadala ni | Uteuzi wa Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM ndio habari ya mjini, kwani mijadala ni mizito lakini wadau wa siasa wanataja sifa tano zilizombeba huku uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 ukitajwa.
Wadau hao wanaona kwa aina ya siasa za ushindani mkali wa Tanzania kwa sasa na baada ya ... |
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa DP World, Sultan Ahmed Bin Suleim amesema matarajio ya kampuni | Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa DP World, Sultan Ahmed Bin Suleim amesema matarajio ya kampuni hiyo ni kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa na ushindani wa kidunia.
Suleim ameyasema hayo leo, Oktoba 22, 2023 alipohutubia wakati wa hafla ya kusainiwa kwa mikataba ya utekelezaji kati ya Serikali ya Tanzania na DP ... |
Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda ndiye aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri | Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda ndiye aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi akimrithi Sophia Mjema.
Makonda anaukwaa wadhifa huo akimrithi Sophia ambaye Rais Samia Suluhu Hassan amemteuwa kuwa mshauri wake wa masuala ya wanawake na makundi maalum.
Ule msemo wa dun... |
Rais Samia Suluhu Hassan amemteuwa Sophia Mjema kuwa Mshauri wake kwenye masuala ya Wanawake na Maku | Rais Samia Suluhu Hassan amemteuwa Sophia Mjema kuwa Mshauri wake kwenye masuala ya Wanawake na Makundi Maalum.
Sophia anaukwaa wadhifa huo, akitoka kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi alioutumikia kwa miezi tisa.
Uteuzi wa Mjema umetangazwa leo, Oktoba 22, 2023 kupitia taarifa kwa vyombo vya... |
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa siku 14 kwa Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Fedha, kuchunguz | Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa siku 14 kwa Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Fedha, kuchunguza na kutoa suluhu ya gharama kubwa za usafirishaji mizigo kupitia ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Malalamiko ya gharama hizo, yaliibuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi aliye... |
Serikali imethibitisha kuilipa kampuni ya Winshear Gold Sh75 bilioni kama stahiki yake, baada ya maz | Serikali imethibitisha kuilipa kampuni ya Winshear Gold Sh75 bilioni kama stahiki yake, baada ya mazungumzo nje ya mahakama.
Taarifa za malipo hayo yaliyofanywa na Serikali ya Tanzania kwa Winshear zilitolewa juzi na kampuni hiyo, ikifafanua ni sehemu ya fidia baada ya kumaliza migogoro baina ya pande hizo mbili.
Mzizi... |
Singida ni miongoni mwa Mikoa yenye umri mkubwa nchini ikiwa ya mwanzo kuanzishwa baada ya muungano | Singida ni miongoni mwa Mikoa yenye umri mkubwa nchini ikiwa ya mwanzo kuanzishwa baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ulianzishwa Oktoba 15, 1963 mwaka mmoja baada ya kupatikana kwa jina la Tanzania lililotokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ukongwe wake umebebwa na historia maridhawa ambayo kimsing... |
Serikali imethibitisha kuilipa kampuni ya Winshear Gold Sh75 bilioni kama stahiki yake, baada ya maz | Serikali imethibitisha kuilipa kampuni ya Winshear Gold Sh75 bilioni kama stahiki yake, baada ya mazungumzo nje ya mahakama.
Taarifa za malipo hayo yaliyofanywa na Serikali ya Tanzania kwa Winshear zilitolewa juzi na kampuni hiyo, ikifafanua ni sehemu ya fidia baada ya kumaliza migogoro baina ya pande hizo mbili.
Mzi... |
Rais Samia Suluhu Hassan ametaka upendo, mshikamano na umoja kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa | Rais Samia Suluhu Hassan ametaka upendo, mshikamano na umoja kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, akisema hatua hiyo itatoa taswira ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Katika kauli yake hiyo, Rais Samia amewasihi wanachama wa CCM kuepuka kukibomoa chama hicho na kuunda makundi kwa sababu ya kukosa nafasi watakaz... |
Huenda suala la kupanda kwa bei ya mbegu za mahindi nchini likafika mwisho, baada ya Serikali kuweka | Huenda suala la kupanda kwa bei ya mbegu za mahindi nchini likafika mwisho, baada ya Serikali kuweka mkakati wa kutangaza bei elekezi ya bidhaa hiyo kwa wakulima.
Uamuzi wa kutangazwa kwa bei hizo, kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe unatarajiwa kufanywa Oktoba 20, mwaka huu.
Haja ya kutangazwa kwa bei hizo, ... |
Hatma ya uwanachama wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ndani ya chama chake cha ADC upo katik | Hatma ya uwanachama wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ndani ya chama chake cha ADC upo katika mashaka, kutokana na viongozi wake kudai kanuni za chama hicho zimemuondoa.
Kulingana na viongozi hao wa ADC, kanuni za chama hicho zinabainisha uhalali wa mwanachama utatokana na ushiriki wake kwenye shughuli za chama... |
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Bara, Innocent Siriwa amesema miongoni mwa mambo yanayokwamisha m | Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Bara, Innocent Siriwa amesema miongoni mwa mambo yanayokwamisha maendeleo ya kisiasa ya vyama vya upinzani nchini ni ubinafsi wa vyenyewe kwa vyenyewe
Kauli yake hiyo inatokana na kile alichoeleza, kuna hali ya kuzibiana nafasi ya kufikia maendeleo kama yaliyofikiwa na vyama vingine... |
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametaka kutambuliwa kwa maeneo hatarishi yenye viashiria vya kuath | Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametaka kutambuliwa kwa maeneo hatarishi yenye viashiria vya kuathirika na maafa yatakayotokana na mvua za Eli-Nino na uandaliwe mpango wa kuyakabili.
Kauli hiyo ya Dk Biteko inakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Agosti 24, mwaka huu itangaze uwezek... |
Ili kurahisisha upatikanaji wa bima za magari, kampuni ya Bima ya Jubilee imetangaza kuanza kutoa hu | Ili kurahisisha upatikanaji wa bima za magari, kampuni ya Bima ya Jubilee imetangaza kuanza kutoa huduma katika vituo vya mafuta jijini Dar es Salaam.
Imesema hatua hiyo itawaondolea wananchi usumbufu wa kufuata huduma hiyo katika matawi ya kampuni hiyo, badala yake watazipata pale watakapokwenda kuweka mafuta.
Hayo ya... |
Kama ulidhani kushamiri kwa teknolojia ya akili bandia (AI) kutazika kibarua chako, bado unayo nafas | Kama ulidhani kushamiri kwa teknolojia ya akili bandia (AI) kutazika kibarua chako, bado unayo nafasi ya kutumikia nafasi yako katikati ya ulimwengu huo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia iwapo utazingatia.
Mwananchi limezungumza na wataalamu mbalimbali wa teknolojia hiyo, wanaokupa mbinu za kulinda kibarua chako dh... |
Nguvu za wananchi wa Kijiji cha Hoyoyo wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani kujitolea katika ujenzi wa za | Nguvu za wananchi wa Kijiji cha Hoyoyo wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani kujitolea katika ujenzi wa zahanati na Kituo cha afya, hazikuwafaa kupata huduma za afya kijijini hapo.
Hiyo ni kutokana na kukwama kwa hatua ya kuwekwa miundombinu ya huduma hizo na uzinduzi wa majengo hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Mwandishi wa ... |
Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa kukiimarisha kitengo cha diplomasia ya u | Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa kukiimarisha kitengo cha diplomasia ya uchumi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Nafahamu diplomasia ya uchumi ni miongoni mwa misamiati migumu kwa baadhi ya Watanzania, ingawa imekuwa ikisikika kutoka kwa viongozi mbalimbali.
... |
Licha ya unywaji pombe hufanywa kama sehemu ya starehe, kwa upande mwingine kuna machungu ndani ya k | Licha ya unywaji pombe hufanywa kama sehemu ya starehe, kwa upande mwingine kuna machungu ndani ya kiburudisho hicho kikihusishwa moja kwa moja na athari katika afya ya akili.
Kulingana na wataalamu wa afya ya akili, pamoja na athari za afya ya mwili zitakazomkabili mtumiaji wa mvinyo kwa muda mrefu, mtu huyo yupo hata... |
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limesema hakuna kiongozi wa Serikali aliyewahi kutumia ndege za sh | Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limesema hakuna kiongozi wa Serikali aliyewahi kutumia ndege za shirika hilo kwenda ama ndani au nje ya nchi bila kulipia.
Limesema safari zote za viongozi zinazoshuhudiwa wakitumia ndege za shirika hilo, huwa wanazikodi na kulipia gharama kama ilivyo kwa wateja wengine.
Hayo yanaibuka... |
Changamoto katika utaratibu wa urasimishaji ardhi, zimetajwa kuwa chachu ya kukithiri kwa migogoro y | Changamoto katika utaratibu wa urasimishaji ardhi, zimetajwa kuwa chachu ya kukithiri kwa migogoro ya ardhi katika Jiji la Dar es Salaam, huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akitoa siku saba za kutafutwa jawabu.
Malalamiko juu ya changamoto za urasimishaji, yameibuliwa na viongozi mbalimbal... |
Uteuzi wa Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetajwa kuibua damu c | Uteuzi wa Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetajwa kuibua damu changa ndani ya jumuiya hiyo.
Hilo linatokana na ukweli kwamba, Jokate ndiye anayeonekana kuwa Katibu Mkuu kijana zaidi kuteuliwa katika wadhifa huo alioukwaa akiwa na umri wa miaka 36.
Kauli kuhusu ingizo hilo la vijan... |
Mwenza wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere amesema mtazamo kuwa kundi fulani limepitwa na wakati ni mion | Mwenza wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere amesema mtazamo kuwa kundi fulani limepitwa na wakati ni miongoni mwa mambo yaliyolirudisha nyuma taifa.
Maria ameihusianisha hoja yake hiyo na mtindo wa maisha wa zamani, akisema wazee na vijana walikutana kujadili mambo mbalimbali ya nchi.
Maria aliyasema hayo jijini Dar es Sa... |
Benki ya Dunia inachunguza tuhuma za mauaji, ubakaji na kufukuzwa kwa nguvu kwa wananchi wanaoishi k | Benki ya Dunia inachunguza tuhuma za mauaji, ubakaji na kufukuzwa kwa nguvu kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya karibu na hifadhi zilizofadhiliwa na mradi wa utalii wa REGROW wa benki hiyo.
Mzizi wa uchunguzi huo, ni tuhuma zilizoibuliwa dhidi ya benki hiyo, ikidaiwa kuwezesha matukio hayo katika Hifadhi ya Ruaha, ... |
Mageuzi ya utendaji katika balozi, intelejensia ya masoko na mageuzi ya mfumo wa uchumi ni miongoni | Mageuzi ya utendaji katika balozi, intelejensia ya masoko na mageuzi ya mfumo wa uchumi ni miongoni mwa matarajio ya Tanzania, baada ya kuimarishwa kwa kitengo cha diplomasia ya uchumi cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Matarajio hayo, yanatokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kukiima... |
Wakazi wa Kijiji cha Mwabasabi, wilayani Buchosa Mkoa wa Mwanza, wameeleza namna Mpango wa Kusaidia | Wakazi wa Kijiji cha Mwabasabi, wilayani Buchosa Mkoa wa Mwanza, wameeleza namna Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (TASAF) ulivyogeuza maisha yao kutoka hali duni hadi nzuri.
Akizungumza kijijini hapo, Ernest Ezary alisema kabla ya TASAF alikuwa na maisha magumu kiasi cha kushindwa kulipa kodi ya nyumba aliyokuwa akiish... |
Hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya ghafla na mara kwa mara ya viongozi, imetajw | Hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya ghafla na mara kwa mara ya viongozi, imetajwa kuakisi mvurugano ndani ya Serikali yake, huku ikiwajaza hofu ya kudumu kwenye mamlaka watendaji wake.
Kulingana na viongozi waandamizi wa Utumishi na wanazuoni, mvurugano huo unasababishwa na kasoro katika mamlaka ya ... |
Umewahi kujiuliza kwanini baadhi ya bunifu na tafiti nchini zinaishia kabatini?
Kama haukuwahi kuji | Umewahi kujiuliza kwanini baadhi ya bunifu na tafiti nchini zinaishia kabatini?
Kama haukuwahi kujiuliza bila shaka umewahi kusikia kilio cha wabunifu kuhusu kukosekana utashi wa kuendelezwa kwa bunifu zao.
Kumbe, swala si bunifu na tafiti kuwekwa kabatini, kilichomo ndani yake ndicho kinachoamua matokeo yake kama an... |
Makali ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mc | Makali ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa yameanza na watumishi saba wa Halmashauri ya Liwale mkoani Lindi, baada ya kuagiza wachukuliwe hatua za kinidhamu.
Agizo la hatua dhidi ya watumishi hao, lilitolewa jana kupitia barua ya Mchengerwa iliyosainiwa ... |
Kitendawili cha mpango wa afya kwa wote nchini, kinatarajiwa kupata majibu Oktoba mwaka huu, katika | Kitendawili cha mpango wa afya kwa wote nchini, kinatarajiwa kupata majibu Oktoba mwaka huu, katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya kongamano la Afya Tanzania (THS) litakalowakutanisha wadau wa sekta ya afya kutoka ndani na nje ya nchi.
Kongamano hilo, litakalowakutanisha wadau 1,000 wa sekta hiyo, linatarajiwa kuf... |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa siku chache baada ya kuteuliwa kushika w | Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa siku chache baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, ameelekeza watendaji wake kutumia siku 100 kutatua migogoro yote ya ardhi nchini.
Siku 100 ni sawa na miezi mitatu na siku 10 za uongozi wake ndani ya Wizara hiyo inayotajwa kuwa mfupa mgumu kwa mawaziri weng... |
Rais Samia Suluhu Hassan amesema migogoro ya wakulima na wafugaji na athari za wanyama waharibifu wi | Rais Samia Suluhu Hassan amesema migogoro ya wakulima na wafugaji na athari za wanyama waharibifu wilayani Nachingwea ni miongoni mwa mambo yatakayoshughulikiwa na Serikali Kuu.
Kauli hiyo ya Rais Samia imekuja baada ya hatua mbalimbali za Wilaya na Mkoa wa Lindi kushindwa kufua dafu juu ya changamoto hizo.
Kero ya wan... |
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi wilayani Liwale katika Mkoa wa Mtwara, kuacha tabia ya kuw | Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi wilayani Liwale katika Mkoa wa Mtwara, kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wa kike badala ya kuwapeleka shuleni.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Septemba 17, 2023 alipohutubia katika mikutano wa hadhara wilayani Liwale mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika Mikoa y... |
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imetangaza zabuni tatu za ujenzi wa bandari mbalimbali nchini ikiw | Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imetangaza zabuni tatu za ujenzi wa bandari mbalimbali nchini ikiwemo ya Kisiwa Mgao mkoani Mtwara, ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa maboresho ya bandari hizo.
Zabuni nyingine zilizotangazwa ni ile inayohusisha uundaji na ujenzi wa bandari ya Mbegani wilayani Bagamoyo, kadhalika banda... |
Katika kila wanafunzi 10 wa sekondari waliofanya mtihani wa hesabu kwa kipindi cha miaka mitano ni w | Katika kila wanafunzi 10 wa sekondari waliofanya mtihani wa hesabu kwa kipindi cha miaka mitano ni wawili pekee ndiyo waliofaulu.
Hii ni sawa na kusema ni asilimia 20 pekee ya wanafunzi wa sekondari wanaofanya mtihani wa hesabu wanafaulu, huku asilimia 80 wakifeli.
Kulingana na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA), mr... |
Katikati ya hoja kuwa bandari zote nchini imeuziwa kampuni ya DP World, Mamlaka ya Bandari Tanzania | Katikati ya hoja kuwa bandari zote nchini imeuziwa kampuni ya DP World, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imetangaza zabuni za ujenzi wa bandari zake mbalimbali ikiwemo ya Mbegani Bagamoyo.
Hatua hiyo ya TPA kutangaza zabuni hizo, inathibitisha ukweli wa kile ilichokuwa inakisisitiza tangu awali kwamba, mkataba wa ushi... |
Bado safari ya miaka 30 ya demokrasia nchini, haijafua dafu katika kuleta chachu ya ushiriki wa wana | Bado safari ya miaka 30 ya demokrasia nchini, haijafua dafu katika kuleta chachu ya ushiriki wa wanawake kwenye ushindani wa kisiasa majimboni.
Hilo linathibitishwa na kile kilichoelezwa na wadau wa demokrasia nchini, tangu kuanza kwa mfumo wa siasa za vyama vingi ni asilimia 9.4 pekee ya wanawake ndiyo walioshinda ub... |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), kuwapa zabu | Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), kuwapa zabuni wahandisi wazawa katika miradi ya ujenzi wa barabara ili kuongeza ufanisi wao.
Hatua hiyo, Majaliwa amesema itaimarisha uwezo wa wahandisi wa Tanzania kusimamia miradi na kadri watakavyoimarika, Wakala wa Barabara Ta... |
Ili kuiepushia Serikali hasara ya kulipa fidia kwa makosa mbalimbali ya kisheria, Waziri wa Katiba n | Ili kuiepushia Serikali hasara ya kulipa fidia kwa makosa mbalimbali ya kisheria, Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana ameitaka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutoa elimu kwa taasisi za umma na halmashauri nchini.
Elimu hiyo, amesema inapaswa kulenga taratibu zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuvunja mikataba ... |
Rais Samia Suluhu Hassan ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu | Rais Samia Suluhu Hassan ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCA).
Hatua hiyo inamfanya Rais Samia kuwa mkuu wa nchi wa pili ndani ya bodi hiyo inayojumuisha wajumbe watano, akiwemo Rais wa Senegal, Macky Shall.
Mbali na marais hao, wajumbe wengine kati... |
Katika kipindi cha mwaka 1994 hadi 2019, zaidi ya Sh9 bilioni zimetumika kulipa madeni ya bima kwa w | Katika kipindi cha mwaka 1994 hadi 2019, zaidi ya Sh9 bilioni zimetumika kulipa madeni ya bima kwa wanachama mbalimbali wa NiC Insurance.
Malipo hayo ni yale ya wanachama walioshindwa kulipwa kwa wakati, kutokana na changamoto zilizokuwa zikilikabili shirika hilo.
Kulingana na Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Elirehema... |
Unajua tangu ruhusa ya mikutano ya hadhara, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefanya zi | Unajua tangu ruhusa ya mikutano ya hadhara, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefanya ziara nyingi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ukilinganisha na kanda nyingine?
Katika kipindi cha miezi nane tangu ruhusa ya mikutano hiyo, iliyokuwa katika kibano kwa miaka saba, Chadema imezuru mara tatu katika kanda hiyo, ... |
Vigogo kumiliki ardhi na watumishi wa ardhi kuwa na maslahi katika upimaji ni miongoni mwa mambo mag | Vigogo kumiliki ardhi na watumishi wa ardhi kuwa na maslahi katika upimaji ni miongoni mwa mambo magumu yatakayomkabili Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.
Kulingana na wabunge, ugumu wa wizara hiyo unakuja pale ambapo maeneo nyeti nchini yanamilikiwa na wale waliowaita vigogo, hivyo inahitaji ... |
Upinzani dhidi ya elimu ya miaka mitatu ya Katiba kwa wananchi kabla ya mchakato wa mabadiliko yake | Upinzani dhidi ya elimu ya miaka mitatu ya Katiba kwa wananchi kabla ya mchakato wa mabadiliko yake unaendelea kushika kasi, baada ya wadau kuitaja hatua hiyo kama mbinu ya kuchelewesha.
Kauli hiyo ya wadau inakoleza moto kwenye hoja za mawaziri wakuu wastaafu, akiwemo Joseph Warioba, Cleopa Msuya na Frederick Sumaye, ... |
“Nilipofika nje, nilishangaa kuwaona niliowaacha ndani tayari wako nje,” ni maneno ya Kurwa Magwa, m | “Nilipofika nje, nilishangaa kuwaona niliowaacha ndani tayari wako nje,” ni maneno ya Kurwa Magwa, mhariri wa gazeti la Mwanaspoti akielezea saa tatu za mshikemshike wa tukio la ajali ya moto, lililotokea katika Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
Magwa ni miongoni mwa wafanyakazi kadhaa walioshuhudia tu... |
Mpango wa Serikali kutumia miaka mitatu kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, umeendelea kupata upinza | Mpango wa Serikali kutumia miaka mitatu kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, umeendelea kupata upinzani kutoka kwa Mawaziri Wakuu watatu wastaafu, baadhi wakihoji uelimishaji huo ni wa nini.
Wakati wengine wakihoji hivyo, wapo wanaoshauri elimu inayotolewa isiathiri kuendelea kwa mchakato wa mabadiliko, wakisisitiza yot... |
Hatua ya mamlaka ya uteuzi kutengua nafasi ya mteule muda mchache baada ya kumteuwa au kumbadilishia | Hatua ya mamlaka ya uteuzi kutengua nafasi ya mteule muda mchache baada ya kumteuwa au kumbadilishia wadhifa, imetajwa na wanazuoni, kuashiria changamoto katika mifumo ya uteuzi.
Msingi wa hoja ya wanazuoni hao ni kilichofanyika Agosti 30, mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alipomteuwa Profesa Kennedy Gaston kuwa Kati... |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza uamuzi wake wa kuweka mkakati wa kuelekeza n | Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza uamuzi wake wa kuweka mkakati wa kuelekeza nguvu zake vijijini kwa kuwa ndilo eneo lenye changamoto lukuki.
Uamuzi huo wa Chadema unaenda sambamba na kile ilichokieleza, itaimarisha uongozi wa mabaraza yake yote kuanzia ngazi ya vitongoji.
Hayo yameelezwa leo, Sep... |
Hatma ya nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Vijijini, Hanafi Msabaha na Mkurugenzi wa halmashauri hi | Hatma ya nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Vijijini, Hanafi Msabaha na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Tatu Issike imeamuliwa na wanachama 250 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kurudisha kadi za uanachama wa chama hicho.
Uamuzi wa wanachama hao 250 kurudisha kadi za CCM, ulilenga kuishinikiza Serikali ikamilishe u... |
Ni kama wamewekwa kitanzini, ndivyo unavyoweza kuelezea kilichowakuta Wakuu wa Mikoa na Makatibu Taw | Ni kama wamewekwa kitanzini, ndivyo unavyoweza kuelezea kilichowakuta Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi, waliposhindwa kumuuliza lolote Rais Samia Suluhu Hassan.
Hoja ya kuwa kitanzini inatokana na hatua ya Rais Samia kuwapa uhuru wa dakika tatu za kumuuliza chochote ... |
Huenda ikawa ngumu kushinda uchaguzi wa urais katika mazingira tata nchini, hili litatokea iwapo Ser | Huenda ikawa ngumu kushinda uchaguzi wa urais katika mazingira tata nchini, hili litatokea iwapo Serikali itatekeleza azimio la wadau wa siasa lililotaka uhuru wa kisheria wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais mahakamani.
Uhuru huo wa kisheria ni moja kati ya maazimio 10 yaliyotolewa na wadau wa siasa katika mkutano w... |
Ni mjadala wa kupeana makavu, ndivyo unavyoweza kuuelezea mkutano wa wadau wa siasa kuhusu hali ya D | Ni mjadala wa kupeana makavu, ndivyo unavyoweza kuuelezea mkutano wa wadau wa siasa kuhusu hali ya Demokrasia nchini, uliohusisha minyukano ya hoja miongoni mwa viongozi wa kisiasa.
Katika mkutano huo, uliohusisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa juu wa vyama vya siasa nchini, ilikuwa ni majibizano ya hoja.
Baad... |
Ni matumaini, ndivyo unavyoweza kuielezea kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), A | Ni matumaini, ndivyo unavyoweza kuielezea kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akieleza Tanzania itakwenda kwenye uchaguzi wa 2024 na 2025 ikiwa na muafaka wa tume huru na haki.
Kauli ya Kinana, inasadifu matarajio ya wanasiasa wengi ambao aghalabu wamekuwa wakidai tume huru ya u... |
Kama ni umri wa binadamu, unaweza kusema amebakiza miaka mitano kustaafu, huu ndiyo uhalisia wa miak | Kama ni umri wa binadamu, unaweza kusema amebakiza miaka mitano kustaafu, huu ndiyo uhalisia wa miaka liliyonayo Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), lililoanzishwa Juni 19, 1963.
Kanisa hilo ambalo mwaka huu, linatimiza umri wa miaka 60 tangu lilipoanzishwa, msingi wa kuanzishwa kwake ni muungano wa makani... |
Sakata la uwekezaji bandari linaweza kuwa moja ya mitihani migumu kuwahi kumkabili Rais Samia Suluhu | Sakata la uwekezaji bandari linaweza kuwa moja ya mitihani migumu kuwahi kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan tangu aapishwe kushika wadhifa huo.
Kulingana na wataalamu wa masuala ya siasa na utawala, sakata hilo limefikia hatua ya hata kuamua imani ya wananchi juu ya Serikali yao, iwapo haitazichanga vema karata zake.
H... |
Hatimaye rasimu ya maboresho ya mitalaa na sera ya elimu imezinduliwa na kuzua mjadala kutoka kwa wa | Hatimaye rasimu ya maboresho ya mitalaa na sera ya elimu imezinduliwa na kuzua mjadala kutoka kwa wadau wa sekta hiyo, baadhi wakipongeza wengine wakilalamikia kurejewa kwa mambo nayoyapinga.
Miongoni mwa mambo hayo ni lugha ya Kiingereza kutumika kufundishia kuanzia ngazi ya sekondari hadi elimu ya juu, wakitaka kitum... |
Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu, kimeendelea kuwa kitendawili kisicho | Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu, kimeendelea kuwa kitendawili kisichoteguka, licha ya mijadala ya muda mrefu ya kulishinikiza hilo.
Huu ni mwaka wa 55 sasa tangu mijadala kuhusu Kiswahili kitumike kufundishia ngazi zote za elimu ianze, lakini bado haijawahi kuzaa matunda.
Matumaini ya w... |
Safari ya mabadiliko ya sekta ya elimu imepitia milima na mabonde, huku kila awamu ikikumbana na upi | Safari ya mabadiliko ya sekta ya elimu imepitia milima na mabonde, huku kila awamu ikikumbana na upinzani wake.
Mabadiliko ya sekta hiyo, yalianza baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, yakilenga kuvua minyororo ya wakoloni walioitoa elimu kwa maslahi yao.
Historia ya mabadiliko ya elimu nchini, ilitokana na malengo ... |
Serikali imesema itawawezesha wafugaji wadogo kupata pembejeo zinazohitajika ili kuboresha mnyororo | Serikali imesema itawawezesha wafugaji wadogo kupata pembejeo zinazohitajika ili kuboresha mnyororo wa thamani wa shughuli hiyo.
Hatua hiyo inatarajiwa kufanyika kupitia mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) unaotekelezwa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo nchini.
Kutokana na hatua hiyo, uzalishaji wa kuku unatara... |
Licha ya Dar es Salaam kuonekana Jiji pendwa na watu, hivi unajua kuwa Pwani ndiyo Mkoa kimbilio la | Licha ya Dar es Salaam kuonekana Jiji pendwa na watu, hivi unajua kuwa Pwani ndiyo Mkoa kimbilio la wengi nchini?
Kwa taarifa yako, katika mwaka 2022 jumla ya watu 667,676 walikimbilia Pwani, huku 142,910 wakifungasha virago kulihama Jiji la Dar es Salaam.
Kulingana na taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, ... |
Viongozi wa dini nchini wamezuiwa kufanya siasa kupitia majukwaa ya vyama vya siasa, huku wanasiasa | Viongozi wa dini nchini wamezuiwa kufanya siasa kupitia majukwaa ya vyama vya siasa, huku wanasiasa nao wakizuiwa kutumia mimbari za dini kufanya siasa.
Zuio hilo, linatokana na kile kilichoelezwa na wadau mbalimbali wa siasa na viongozi wa dini kuwa, hayo yote mbali na kuchochea vurugu, pia ni kinyume na utaratibu wa... |
Harakati za kupigania ruhusa ya vazi la Hijabu kuvaliwa shuleni na wanafunzi wa dini ya Kiislamu ni | Harakati za kupigania ruhusa ya vazi la Hijabu kuvaliwa shuleni na wanafunzi wa dini ya Kiislamu ni miongoni mwa kumbukumbu zilizoachwa na Sheikh Ally Abasaleh katika kipindi cha uhai wake.
Kabla ya miaka ya 1990 vazi hilo halikuruhusiwa kuvaliwa na wanafunzi shuleni, kadhalika lilizuiwa hata katika ofisi mbalimbali z... |
Ukichukua fomu ya kugombea nafasi ya kisiasa na kwa makusudi ukaacha kuirejesha ili kutoa nafasi kwa | Ukichukua fomu ya kugombea nafasi ya kisiasa na kwa makusudi ukaacha kuirejesha ili kutoa nafasi kwa mgombea mwenzako kupita bila kupingwa, upo hatarini kuzuiwa kugombea kwa miaka 20.
Si aliyeacha nafasi pekee, hata kama kwa makusudi umeamua kutorudisha fomu utakumbana na msukosuko wa uchunguzi mkali wa Tume ya Taifa y... |
Hatua ya Chadema kukaidi barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi iliyotaka kisitis | Hatua ya Chadema kukaidi barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi iliyotaka kisitishe mkutano wake uliojadili uwekezaji bandari, imekiweka katika mitego miwili, ama kiadhibiwe au kielimishwe.
Mkutano huo ulifanyika jana, katika Uwanja wa Bulyaga Wilayani Temeke, ukilenga kuzungumzia mkataba wa ushirik... |
Ingawa ndoto ya Tanzania kuuza umeme nje ya nchi hutafsiriwa kama kauli ya kisiasa, upo uwezekano wa | Ingawa ndoto ya Tanzania kuuza umeme nje ya nchi hutafsiriwa kama kauli ya kisiasa, upo uwezekano wa kutimia iwapo mambo kadhaa yatazingatiwa kuelekea utekelezwaji wake.
Kiu ya biashara hiyo ya nishati nchini kwenda nchi za jirani, ilianza tangu mwaka 2013, Tanzania ikiwa mikononi mwa uongozi wa Dk Jakaya Kikwete.
Ju... |
Umefikia umri wa kuoa? umewahi kwenda kwa wazazi wa mwenza wako kuanza taratibu za kufanikisha hilo? | Umefikia umri wa kuoa? umewahi kwenda kwa wazazi wa mwenza wako kuanza taratibu za kufanikisha hilo? Walikueleza nini? Kipi kilikufurahisha na kipi kilikukera au kukukatisha tamaa?
Maswali haya yanaakisi uhalisia wa wanayoyapitia vijana wengi wanapoanza mchakato wa kufunga ndoa, hali inayotajwa kuchagiza uwepo wa ndoa ... |
Uwekezaji katika sekta ya elimu, ufadhili wa taasisi za fedha, kujenga uwezo wa ndani na ushirikishw | Uwekezaji katika sekta ya elimu, ufadhili wa taasisi za fedha, kujenga uwezo wa ndani na ushirikishwaji wa sekta binafsi ni miongoni mwa mapendekezo ya Tanzania katika kuwezesha nchi za Afrika kuwa na rasilimali watu yenye tija.
Mapendekezo hayo yanakuja wakati ambao, nchi za Afrika zinatajwa kuwa na hali ngumu ya kufi... |
Hatua ya Chadema kukaidi barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi iliyotaka kisitis | Hatua ya Chadema kukaidi barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi iliyotaka kisitishe mkutano wake uliojadili uwekezaji bandari, imekiweka katika mitego miwili, ama kiadhibiwe au kielimishwe.
Mkutano huo ulifanyika jana, katika Uwanja wa Bulyaga Wilayani Temeke, ukilenga kuzungumzia mkataba wa ushirik... |
Kumekuwepo na sintofahamu kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya tume na kamati mbalimbali zinazoundwa | Kumekuwepo na sintofahamu kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya tume na kamati mbalimbali zinazoundwa na viongozi wakuu wa Serikali. Tume na kamati hizo huundwa ili kuchunguza masuala mbalimbali, lakini baada ya kukabidhi taarifa zao kwa viongozi, suala la utekelezaji wa mapendekezo hubaki kuwa kitendawili hivyo kusabab... |
Tume ya kuboresha utendaji wa taasisi za haki jinai, imesema katika utendaji wake, imebaini baadhi y | Tume ya kuboresha utendaji wa taasisi za haki jinai, imesema katika utendaji wake, imebaini baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliotekeleza kinyume na sheria utaratibu wa kuwaweka watu mahabusu kwa saa 48.
Kauli ya tume hiyo, inakuja baada ya kukamilisha kazi yake ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu maboresh... |
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema upinzani unaoendelea dhidi ya mkat | Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema upinzani unaoendelea dhidi ya mkataba wa uwekezaji na uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai, ni ishara ya kuwepo kwa tija katika uwekezaji huo.
Hoja yake hiyo inatokana na kile alichokifafanua kuwa, si kawaida ya adui kuunga mk... |
Kauli ya kashfa dhidi ya wananchi ni jambo linalotarajiwa kumuingiza hatiani Juma Homera ambaye ni M | Kauli ya kashfa dhidi ya wananchi ni jambo linalotarajiwa kumuingiza hatiani Juma Homera ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Hilo linatokana na kusudio la Wakili Philip Mwakilima la kumshitaki Homera kutokana na kile alichoeleza kuwa, amewakashifu wateja wake watatu kwa kuwaita wezi.
Ingawa katika barua yake kwa Homera, w... |
Hatimaye matumaini ya kurejea kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kulitheri (KKKT) Dayosisi ya Ku | Hatimaye matumaini ya kurejea kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kulitheri (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki mkoani Mtwara yanaonekana, baada ya kupatikana kwa uongozi mpya wa nyumba hiyo ya ibada ya waumini wa dini ya kikristo.
Kupatikana kwa uongozi mpya, kumetokana na uchaguzi uliofanyika Julai 18, mwaka huu u... |
Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti | Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Jecha amefariki dunia leo, Julai 18, 2023 katika Hospitali ya Lugalo alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kumbukumbu ya wengi kwa Jecha ni tukio alilolifanya Oktoba 29, mw... |
Benki ya Uwekezaji barani Ulaya (EIB), inatarajia kutoa Sh1.8 trilioni nchini ili kuongeza uwekezaji | Benki ya Uwekezaji barani Ulaya (EIB), inatarajia kutoa Sh1.8 trilioni nchini ili kuongeza uwekezaji wake katika sekta ya umma na kukopesha benki za biashara, taasisi ndogo za fedha na wajasiriamali.
Fedha hiyo inayotarajia kuitoa ni tofauti na Sh454 bilioni ilizotoa kugharimia uwekezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo in... |
Ziara ya Rais wa Hungary nchini, Katalin Novak inatarajiwa kuwa ukurasa mpya wa kuimarika kwa ushiri | Ziara ya Rais wa Hungary nchini, Katalin Novak inatarajiwa kuwa ukurasa mpya wa kuimarika kwa ushirikiano wa mataifa hayo katika maeneo ya biashara na utalii, ambayo kwa sasa yamedorora.
Rais Katalin amewasili nchini Tanzani juzi kwa ziara ya kiserikali anayotarajia kuihitimisha Julai 20, mwaka huu ikiwa ni sehemu ya m... |
Tume ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoiunda kwa ajili ya kutathmini utendaji wa taasisi za haki jina | Tume ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoiunda kwa ajili ya kutathmini utendaji wa taasisi za haki jinai imekabidhi ripoti yake iliyohusisha mapendekezo ya wadau mbalimbali juu ya mwenendo wa mfumo wa haki jinai.
Kwa sehemu kubwa kilichopendekezwa ndicho kile ambacho mara nyingi tumekuwa tukikisikia kutoka kwa wadau mbali... |
Kuimarika kwa ushirikiano katika sekta ya elimu na kuibuka kwa maeneo mapya ya uhusiano ikiwemo uwek | Kuimarika kwa ushirikiano katika sekta ya elimu na kuibuka kwa maeneo mapya ya uhusiano ikiwemo uwekezaji na biashara ni miongoni mwa matarajio ya wadau kutokana na ziara ya Rais wa Hungury, Katalin Novák.
Rais Katalin aliwasili nchini jana usiku na anatarajia kufanya ziara ya kiserikali hadi Julai 20, mwaka huu ikihus... |
Rais Samia Suluhu Hassan ametetea ile hatua yake ya kutengua mara kwa mara viongozi mbalimbali wa Se | Rais Samia Suluhu Hassan ametetea ile hatua yake ya kutengua mara kwa mara viongozi mbalimbali wa Serikali, akisema uamuzi huo unafanywa na mamlaka za uteuzi kwa lengo la kulinyoosha taifa.
Katika hoja yake hiyo, Mkuu huyo wa nchi amewataka ndugu na jamaa wa viongozi wanaotenguliwa, waache kulalamikia uamuzi wa mamlaka... |
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeazimia mambo 16 ikiwemo kuongeza suala | Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeazimia mambo 16 ikiwemo kuongeza suala la Bandari kuwa sehemu ya operesheni yake.
Kutokana na maazimio hayo, operesheni ya chama hicho ya '+255 Katiba Mpya' kwa sasa itajulikana kama '+255 Katiba Mpya, Okoa Bandari Zetu.'
Oparesheni +255 Katiba Mpya ilizindu... |
Hatua ya Serikali kuanza mchakato wa mabadiliko ya sheria ikiwemo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imei | Hatua ya Serikali kuanza mchakato wa mabadiliko ya sheria ikiwemo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imeibua maswali kutoka kwa wadau, wakihoji kipi kilipaswa kutangulia kati ya tume na Katiba Mpya.
Wamekwenda mbali zaidi, wakifananisha kuanza na mchakato wa sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ni sawa na kutangu... |
Huenda kusuasua kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulichagizwa na mambo matano ikiwemo janja | Huenda kusuasua kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulichagizwa na mambo matano ikiwemo janjajanja katika matumizi ya kadi za wanachama wa mfuko huo.
Kulingana na NHIF, kadi 1,346 zimekamatwa zikitumika na wasio wanachama wala wanufaika wa mfuko huo, ikielezwa kuwa wameazimwa na wanachama.
Hayo yamebainika kupit... |
Swali wanalojiuliza Watanzania kutoka maeneo mbalimbali kwa sasa ni kwanini Bandari ya Dar es Salaam | Swali wanalojiuliza Watanzania kutoka maeneo mbalimbali kwa sasa ni kwanini Bandari ya Dar es Salaam si tegemezi la kikanda pamoja na kuzungungwa na fursa lukuki.
Kimkakati, bandari ya Dar es Salaam ipo katika nafasi nzuri la kuhudumia nchi nyingi kwa gharama nafuu na hatimaye kuipa faida kubwa kulinganisha na washind... |
Dhana ya uendelezaji na uendeshaji wa Bandari na ushiriki wa sekta binafsi ni mfumo wa kisasa unaotu | Dhana ya uendelezaji na uendeshaji wa Bandari na ushiriki wa sekta binafsi ni mfumo wa kisasa unaotumika katika bandari nyingi Duniani.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa nyakati tofauti imechukua hatua za kushirikisha sekta binafsi katika shughuli z... |
Kauli mbalimbali zinazotolewa na Balozi Ali Karume kukituhumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba hakun | Kauli mbalimbali zinazotolewa na Balozi Ali Karume kukituhumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba hakuna demokrasia imezidi kuibua sintofahamu kuhusu mustakabali wake.
Balozi Karume ambaye ni mwanachama wa chama hicho kwenye tawi la Mwera, katika kipindi cha miezi kadhaa sasa amekuwa akitoa shutuma dhidi ya chama hicho ik... |
Hatma ya kuadhibiwa au kusamehewa kwa Balozi Ali Karume itajulikana baada ya vikao vitatu vya Chama | Hatma ya kuadhibiwa au kusamehewa kwa Balozi Ali Karume itajulikana baada ya vikao vitatu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vilivyoanza jana visiwani Zanzibar na kingine kinachofanyika leo, jijini Dodoma.
Katika vikao hivyo hasa vya Zanzibar, kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM visiwani humo, Dk Mohammed Said Mohammed,... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.