name
stringclasses
429 values
text
stringlengths
0
767k
null
Justin Welby: Ifahamu kashfa iliyomuondoa askofu mkuu wa Anglikana Justin Welby amejiuzulu wadhifa wake kama Askofu Mkuu wa Canterbury baada ya kukabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka ajiuzulu kutokana na kushindwa kumripoti mnyanyasaji wa watoto John Smyth. Yafuatayo ni matukio yaliyopelekea Bw Welby kujiuzulu baada ...
null
WARIDI WA BBC: 'Sijamsamehe baba wa kambo kwa kunidhulumu kingono" - Author, Anne Ngugi - Nafasi, BBC Swahili Victoria Itenyo ni mama na mwanaharakati wa haki za watoto na pia anatoa ushauri nasaha juu ya masuala yanayohusu watoto na vijana nchini Kenya. Hatua hii ya kushughulikia afya ya akili kwa watoto na vijana ili...
null
Tanzania: Wanne waliombaka na kumlawiti binti mmoja wahukumiwa maisha jela Na Ronald Sonyo akiwa Dodoma & Yusuf Jumah akiwa Nairobi Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imewahukumu kifungo cha maisha jela watuhumiwa wanne kwa kesi ya ubakaji na ulawiti kwa kundi dhidi ya binti wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam Nje ya Maha...
null
Changamoto za wafanyakazi katika shamba la maua Kenya - Author, Ismail Einashe - Nafasi, BBC Usiku usio na mwezi katika mji wa Naivasha, kando ya ziwa nchini Kenya, Anne ameketi ndani ya nyumba yenye vyumba viwili, akiwa amechoka baada ya kazi ngumu ya kuchuma na kupanga maua ya waridi. Anne (si jina lake halisi), ni m...
null
Bilionea mwendazake Mohamed Al Fayed anatuhumiwa kwa ubakaji na wafanyakazi wake wa zamani - Author, Cassie Cornish-Trestrail, Keaton Stone, Erica Gornall & Sarah Bell - Nafasi, BBC Onyo: Makala hii ina maelezo ambayo baadhi ya watu yanaweza kuwahuzunisha. Wanawake watano wanasema walibakwa na mmiliki wa zamani wa duka...
null
Mbegu za kiume zamsaliti mwanaume aliyemuua mtalaka wake baada ya miaka 45 Polisi wamemkamata na kumfungulia mashitaka mwanaume mmoja ambaye amekuwa akitoroka kwa miaka 45 baada ya kumuua mke wake wa zamani huko Scotland. Christopher Harrison anatokea Aberdeen kaskazini-mashariki mwa Scotland. Alimuua mke wake mwaka 19...
null
Malawi: Kundi la WhatsApp lilivyowaokoa wanawake waliosafirishwa kwenda Oman - Author, Florence Phiri & Tamasin Ford - Nafasi, BBC Africa Eye BBC Africa Eye imechunguza jinsi kikundi cha WhatsApp kilivyosaidia kuokoa zaidi ya wanawake 50 wa Malawi waliosafirishwa hadi Oman kufanya kazi katika mazingira kama ya watumwa....
null
Kupigwa na kutishiwa: Jinsi wanawake wa Uzbek wanavyolazimishwa kufanya kazi ya ngono nchini India Kupigwa na kutishiwa: Jinsi wanawake wa Uzbek wanavyolazimishwa kufanya kazi ya ngono nchini India Wanawake wawili wa Uzbek waliolazimishwa kufanya kazi za ngono nchini India walifichua unyanyasaji, vitisho na ukatili amb...
null
Waridi wa BBC: Jinsi umasikini unavyozima ndoto za wasichana wa Tanzania - Author, Martha Saranga - Nafasi, Mwandishi Safari yangu kama msichana wa kitanzania ninafahamu umasikini unavyozima ndoto za wasichana.'' ‘Kati ya wanafunzi 200 waliohitimu na mimi kidato cha nne, ni 9 tu ndiyo tulifaulu kuendelea na masomo ya k...
null
'Mimi ni mbakaji', mume akiri katika kesi ya ubakaji Ufaransa Tahadhari: Taarifa hii ina maelezo ya kusikitisha kuanzia mwanzo. Dominique Pelicot, mwanamume mwenye umri wa miaka 71 anayekabiliwa na mashtakiwa kwa kumtilia mke wake dawa za kulevya ili alale na kuwalipa makumi ya wanaume kumdhulumu kwa zaidi ya miaka 10,...
null
'Mambo ya kutisha yalitokea'-Ndani ya kanisa la TB Joshua lenye simulizi za kuogofya - Author, Na Charlie Northcott na Helen Spooner - Nafasi, BBC News, Africa Eye TB Joshua, kiongozi wa Nigeria mwenye mvuto wa moja ya makanisa makubwa zaidi ya kiinjili duniani, alitenda uhalifu wa kingono kwa siri kwa kiwango kikubwa,...
null
Fahamu kwanini madaktari wa kike wa Pakistan wanahofia usalama wao - Author, Farhat Javed - Nafasi, BBC Urdu - Akiripoti kutoka Pakistan Wanawake wanaofanya kazi katika hospitali nchini Pakistan wanasema mara kwa mara wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na matusi kutoka kwa wenzao wa kiume, wagonjwa na familia zao....
null
Mji wa Colombia uliosifika kwa kuwa kitovu cha 'utalii wa ngono' Na Jose Carlos Cueto Mwandishi wa BBC Mundo,Colombia Ninachokuambia kilitokea kabla ya janga, kabla ya utalii wa ngono kukua sana huko Medellín. Rafiki yangu aliniwezesha kuwasiliana na baadhi ya Wamarekani. Mmoja wao, 'Herbie', alikuwa na umri wa miaka 3...
null
'Siwezi kulala': Mauaji ya mwanariadha yanaashiria nini kuhusu usalama wa wanawake nchini Kenya Mauaji ya mwanariadha Rebecca Cheptegei na mpenzi wake wa zamani yamezidisha wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya mauaji ya wanawake nchini Kenya. Raia huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 33 alifariki siku chache baada ya...
null
Jane Birkin: Maisha ya msanii na gwiji huyu wa mitindo katika picha Mwimbaji na mwigizaji Jane Birkin aliyefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 76, alikuwa na asili ya Uingereza na alifanya shughuli zake zaidi nchini Ufaransa. Aljulikana kwa uhusiano wake wa kikazi na wa kibinafsi na mwanamuziki Serge Gainsbourg na ...
null
Wanawake wa Afghanistan wanaopinga utawala wa Taliban kupitia muziki Wanawake wa Afghanistan wanaopinga utawala wa Taliban kupitia muziki Waimbaji wa Afghanistan nje ya nchi hiyo wamekuwa wakitumia muziki kuonyesha uungaji mkono wao kwa watu wanaoishi chini ya Taliban. Video nyingi, ambazo kwa kawaida huchezwa na wanaw...
null
Jinsi nyota wa muziki walivyochangia kuboresha viwango vya soka Tanzania Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania inalenga kupita hatua ya makundi ya dimba la Afcon kwa mara ya kwanza katika historia yake. Huku timu hiyo ikijiandaa kufungua kampeni yake ya Afcon mwaka huu na pambano dhidi ya Morocco hiyo kesho, mwan...
null
Walalamika kuhusu gharama za juu za pombe Zanzibar Alfred Lasteck BBC Swahili Si watalii, si wenyeji lakini hata waandaji wa Tamasha la 21 Sauti za Busara wameeleza kuwa pombe kuwa gharama ya juu ilipunguza shangwe za tamasha hilo. “Tamasha lilikuwa zuri lakini mwaka huu bei imepanda, kuna wasanii tuliwatarajia. Leo na...
null
Mwanamuziki anayepiga ala ya muziki kutumia vidole vya miguu yake Ukitazama bango la matangazo la BBC mwaka huu utaona baadhi ya watu mashuhuri kiongozi wa muziki Sir Simon Rattle na mwimbaji nyota Sheku Kanneh Mason. Lakini angalia kwa karibu zaidi na utamuona mcheza ala ya muziki anayetumia vidole vyake vya miguu. Fe...
null
Trump atafanya nini siku ya kwanza Ikulu? - Author, Laura Blasey & Jessica Murphy - Nafasi, BBC News World Donald Trump na Chama chake cha Republican wana udhibiti wa Bunge la Marekani. Timu yake ya kampeni imesema kutarajiwe msururu wa maagizo kutoka kwa rais wa Marekani katika wiki ya kwanza. Wataalamu wa sera na wan...
null
'Nilimuuzia nyumba mtu aliyekuwa akisakwa na FBI' Mwanamume mmoja ambaye alimuuzia nyumba yake mtu ambaye alibainika kuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa sana na FBI amesema kuwa hilo lilikuwa eneo linalofaa "ikiwa ungetaka kujificha. Daniel Andreas San Diego alilipa pauni 425,000 kwa ajili ya nyumba hiyo karibu na ...
null
Kwa nini ndege zisizo na rubani zinapaa karibu na vituo vya kijeshi vya Marekani, nchini Uingereza? Eneo la anga karibu na vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko Norfolk na Suffolk limekuwa likichunguzwa kufuatia matukio kadhaa ya hivi karibuni ya uvamizi wa ndege zisizo na rubani. Wanaohusika na ndege hizo bado hawa...
null
'Machafuko yanatawala' - jela maarufu inayomshikilia Sean 'Diddy' Combs - Author, Kayla Epstein - Nafasi, BBC News, New York Kwa kawaida, Jaji wa Wilaya ya Marekani Gary J Brown angeagiza mtu huyo kushikiliwa katika jela ya serikali ya eneo hilo ili kutumikia kifungo chake kwa ulaghai wa kodi. Lakini jambo moja lilimzu...
null
Utawala na Sheria Uchaguzi wa Marekani 2024: Kipi kitatokea kwa Trump na kesi zake mahakamani? 7 Novemba 2024 Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, kwanini watafuta hifadhi wa Afrika wana wasiwasi? 30 Oktoba 2024 Kesi ya Diddy inaanza lini? Na unayofaa kujua kuhusu matatizo yake ya kisheria 11 Oktoba 2024 Kwanini mageuzi ya k...
null
Sanaa Maana zilizofichika katika mchoro wa utupu wa karne ya 16 25 Novemba 2024 'Alijiona kama Mfalme': Tafrija zilizosababisha anguko la Diddy 18 Oktoba 2024 Picha za maeneo 5 ya kuvutia zaidi yaliyotelekezwa duniani 24 Agosti 2024 Waridi wa BBC: 'Mruhusu mtoto asomee anachokitaka' 21 Agosti 2024 Wakenya wamkumbuka St...
null
Mgonjwa wa saratani Uganda: Jinsi kitanda kilivyookoa maisha yangu - Author, By Anne Okumu - Nafasi, BBC Wakati familia ya Dorcas Cherop mwenye umri wa miaka 14 ilipoambiwa anahitaji kufanyiwa matibabu ya mwaka mzima ya saratani ya kibofu cha mkojo nchini Uganda, mustakabali wake ulionekana kuwa mbaya. Changamoto haiku...
null
Tazama: Baiskeli ya kipekee iliyotengenezwa kutokana na mmea wa mwanzi Kutana na Noordin Kasoma ambaye ameanzisha karakana ya kutengeneza fremu za baiskeli kutoka kwa mmea wa mwanzi. Kupitia kampuni yake kwa jina ''Boogali'' Kijana huyu mjasiriamali pia anawaajiri vijana wenzake. Mwandishi wetu Shuayib Ibrahim amemtemb...
null
Jinsi makomando wa Israeli walivyowaokoa mateka 102 waliofichwa Uganda kwa dakika 58 Serikali ya Israel imeapa kulipa kisasi kwa shambulio la kushtukiza la kundi la wanamgambo wa Hamas ambalo ni baya zaidi katika historia ya miongo ya hivi karibuni. Tayari mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza ambao upo chini ya utawala...
null
Makali ya shoka la gharama ya maisha yanavyoziponda nchi za Afrika Mashariki Na Peter Mwangangi BBC Swahili, Nairobi Raia wa mataifa tofauti ya Afrika Mashariki wamekuwa wakishuhudia ongezeko la gharama ya maisha baada ya bei za huduma na bidhaa kadhaa kupanda. Baadhi ya bidhaa ambazo zimeathirika ni chakula, mafuta ya...
null
Sheria ya Uganda dhidi ya LGBTQ inachochea unyanyasaji - mashirika ya kutetea haki Ripoti mpya imerekodi zaidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu 300 dhidi ya jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ) unaofanywa na watendaji wa serikali na wasio wa serikali kufuatia kupitishwa kwa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja...
null
Sokwe 'wanajitibu' kwa dawa za mitishamba-Utafiti wagundua - Author, Victoria Gill - Nafasi, Mwandishi wa sayansi, BBC News - Twitter, Sokwe mwitu hula mimea ambayo ina uwezo wa kutuliza maumivu na kuzuia bakteria kujiponya, kulingana na wanasayansi. Walielezea "kazi yao ya upelelezi" katika misitu ya Uganda - kuangali...
null
Mwanajeshi mtoto aliyekuwa katika kundi la LRA aliyeanza maisha mapya katika sanaa Furaha anayoipata aliyekuwa mpiganaji mchanga Peter Oloya katika Sanaa hii ya uchongaji wa sanamu, iliibuliwa alipokuwa akimtafutia bibi yake udongo wa aina ya CLAY huko kaskazini mwa Uganda, eneo ambalo limejipatia sifa mbaya ya mashamb...
null
Vita vya Ukraine 'kutakuwa na maeneo mapya zaidi ndani ya Urusi'- Medvedev Naibu mkuu wa Baraza la usalama la Urusi Dmitry Medvedev alisema kwamba idadi ya kile kinachoitwa "maeneo mapya" ya Urusi itaongezeka katika siku zijazo. Moja kwa moja Majeruhi wa Ligi Kuu - 'Wachezaji hawawezi tena kukabiliana na mzigo huu ulio...
null
‘Ulemavu wetu ndiyo nguvu yetu’: Kijiji ambacho watu wote wana upofu - Author, Na Agnes Penda & Gem Oreilly - Nafasi, BBC News Moses Mugabe ni mwanamme wa umri wa miaka 53 anayeishi mashariki mwa Uganda. Hajui ni kitu gani kilimfanya apoteze uwezo wa kuona ila anakumbuka mara ya mwisho kuona jua likichomoza, kumbukumbu...
null
Mamia ya wanajihadi wawaua wanajeshi nchini Niger Mamia ya wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wakiendesha pikipiki wameshambulia mji wa kusini-magharibi mwa Niger na kuua wanajeshi 12, wizara ya ulinzi imesema. Moja kwa moja Mbwa alaumiwa kwa kumnyima Mkenya ushindi katika marathon Seneta mmoja nchini Kenya amekosoa mash...
null
Afcon: Morocco itakuwa mwenyeji 2025 na Kenya-Uganda-Tanzania 2027 Shirikisho la Soka barani Afrika Jumatano lilizipa Kenya, Uganda na Tanzania haki ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2027. Rais wa CAF Patrice Motsepe alitangaza Zabuni ya Pamoja ya Afrika Mashariki kama mshindi wa haki za kuandaa bonanza la kwanza l...
null
Kwa nini mzozo wa mafuta kati ya Kenya na Uganda unasababisha wasiwasi katika kanda hii Na Basilioh Rukanga BBC News, Nairobi Mzozo mkali kuhusu usambazaji wa mafuta umezuka kati ya Kenya na jirani yake Uganda isiyo na bandari, huku kiongozi wa Uganda Yoweri Museveni akisema nchi yake "inadanganywa" na "vimelea" na waf...
null
Upi msimamo wa nchi za Afrika Mashariki kuhusu vita vya Israel-Hamas? - Author, Michael Bishku - Nafasi, The conversation Majibu ya baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kuhusu mzozo unaoendelea huko Gaza yamekuwa madogo ukilinganisha na majibu ya nchi kama Afrika Kusini. Bunge la Afrika Kusini limepitisha azimio la kutak...
null
Waafrika nchini Lebanon: 'Kila mtu chuoni ana wasiwasi' Farai, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 27 kutoka Zimbabwe, amekuwa akiweka vitabu vyake vya masomo ya chuo kikuu kwenye dawati lake nyumbani mjini Beirut. Lakini wiki hii, kwenye dawati lake ameweka hati za kusafiria, na pesa taslimu. "Nimejipanga mwenyewe ikiwa n...
null
Maandalizi, Fursa na Changamoto ya AFCON Afrika Mashariki - Author, Rashid Abdallah - Nafasi, BBC Swahili - Twitter, Baada ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika - AFCON yatakayo fanyika Ivory Coast mwaka 2024, yatafuata yatakayo shindaniwa Morocco mwaka 2025 na kisha Kenya, Uganda na Tanzania itakuwa zamu yao kuw...
null
Balozi wa Ufaransa nchini Niger awasili Paris Balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itté amerejea Paris, kulingana na wizara ya Ulaya na mambo ya nje ya Ufaransa. Moja kwa moja Habari za hivi punde, Balozi wa Ufaransa nchini Niger awasili Paris Balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itté amewasili Paris, kulingana n...
null
William Ruto na Bola Tinubu: Wakosolewa kwa kusafiri sana - Author, Basillioh Rukanga - Nafasi, BBC Rais William Ruto wa Kenya na Rais Bola Tinubu wa Nigeria, wanakabiliwa na ukosoaji kwa safari zao za mara kwa mara nje ya nchi. Wawili hao wamekuwa wakikosolewa kutokana na gharama zinazohusiana na safari nyingi za ndeg...
null
Tanzania yaua ndege wavamizi milioni tano aina ya kwelea Ndege aina ya Kwelea kwelea mara nyingi huharibu nafaka kama mchele na ngano. Moja kwa moja Viktor Sokolov: Urusi yatoa video 'kuonesha kwamba kamanda wa meli za Bahari Nyeusi bado yuko hai' Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetoa video inayomuonyesha kamanda wa Meli ya...
null
“Nilidhani nitaolewa na tajiri, lakini nikagundua sio rahisi hivyo” “Nilidhani nitaolewa na tajiri, lakini nikagundua sio rahisi hivyo” Kutana na Zarinah Hassan maarufu kama Zari the Boss Lady, mfanyabiashara na mmoja kati ya wanawake wenye ushawishi katika mitandao ya kijamii ambaye ana asili ya Uganda akijibu maswali...
null
Siku ya Kiswahili: Lugha ya wakati wa amani na vita - Author, Rashid Abdallah - Nafasi, BBC Swahili - Twitter, Bila shaka si kosa la lugha, ikiwa lugha fulani itatumika na majambazi, waasi au watu wowote waovu. Lugha ni chombo tu cha mawasiliano, waweza itumia kumbembeleza mke wako asikukimbie, na kinyume chake waweza ...
null
Ni kwanini mitandao gushi ya propaganda ya Uganda iliiba sura yake? Uchunguzi wa BBC umebaini mtandao wa akaunti bandia za mitandao ya kijamii nchini Uganda. Chini ya utambulisho bandia , walieneza propagandaza kuunga mkono serikali na kutoa vitisho vinavyowalenga wakosoaji . Lakini watu walio nyuma yake ni akina nani?...
null
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah auawa - Jeshi la Israel Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah ameuawa. Katika taarifa iliyoshirikishwa kwenye akaunti ya mtandao wa X ya IDF, inasema: "Hassan Nasrallah hataweza tena kutishia ulimwengu." Kauli hiyo inafuatia mfululizo wa m...
null
Walionusurika waelezea shambulio la Israel huko Beirut ambalo liliua watu 18 - Author, Orla Guerin - Nafasi, BBC Mohammed Sukayneh alipitia kwenye vifusi, akiwa ameshika mifuko michache ya plastiki – imebeba vitu alivyovipata kutoka katika nyumba yake ya miaka 45. Ilishambuliwa yeye akiwemo na familia yake jana usiku k...
null
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah ni nani? Nasrallah hajaonekana hadharani kwa miaka kadhaa sasa kutokana na hofu ya kuuawa na Israel. Na siku ya Jumamosi, wanajeshi wa Israel walisema walimuua Nasrallah katika shambulio la Beirut. Pia, Hezbollah imethibitisha kifo cha kiongozi Hassan Nasrallah baada ya Israel kus...
null
Shambulio la droni dhidi ya Israel lafichua udhaifu wa Iron Dome - Author, Jonah Fisher - Nafasi, BBC News - Akiripoti kutoka Northern Israel Zinatembea polepole, ndogo na za bei nafuu katika kutengeneza, ndege zisizo na rubani zimekuwa zikiiumiza kichwa Israel katika vita hivi vya mwaka mzima. Shambulio la Hezbollah k...
null
Uvamizi wa ardhi ya Lebanon: Ni matukio gani yanayoweza kutokea? Siku ya Jumatano, mkuu wa majeshi ya Israeli aliwataka wanajeshi wake kujiandaa kwa "uwezekano wa kuingia " nchini Lebanon, wakati jeshi la Israeli lilitangaza kwamba limeita vikosi viwili vya akiba kwa ajili ya "operesheni za kazi" kaskazini. Waziri wa u...
null
Netanyahu aionya Lebanon na ‘uharibifu kama wa Gaza' - Author, David Gritten - Nafasi, BBC Waziri Mkuu wa Israel ametoa wito wa moja kwa moja kuwataka watu wa Lebanon kuindoa Hezbollah na kuepuka "uharibifu na mateso kama huko Gaza." Ombi la Benjamin Netanyahu la siku ya Jumanne lilikuja wakati Israel ikipanua uvamizi ...
null
Hezbollah inamchaguaje kiongozi wake mpya baada ya kuuawa kwa Nasrallah? Na Ithar Shalaby BBC BBC Arabic Kwa miaka 32 iliyopita, Hezbollah haijamjua kiongozi na katibu mkuu isipokuwa Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa Ijumaa iliyopita katika mashambulizi ya Israel yaliyolenga makao makuu ya chama hicho kusini mwa mji mku...
null
Kwa nini mashambulizi ya Israel dhidi ya Hezbollah yafanyika sasa "Vita vya maangamizi unayoweza kuyaelezea." Hivi ndivyo Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati alivyoelezea mashambulizi ya Israel dhidi ya nchi yake siku ya Jumatatu ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 550, wakiwemo watoto 50, na kuwajeruhi wengine...
null
Mwaka mmoja wa mauaji umeipeleka Mashariki ya Kati kwenye ukingo wa vita vikubwa zaidi - Author, Jeremy Bowen - Nafasi, BBC Vita vinatengeneza upya siasa za Mashariki ya Kati. Mashambulizi ya Hamas yaliuwa watu 1,200, wengi wao wakiwa raia wa Israel. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alimpigia simu Rais Joe Bi...
null
Uvamizi wa Lebanon: Je! Jeshi la Lebanon liko wapi wakati Israel inavamia? - Author, Carine Torbey - Nafasi, BBC News - Akiripoti kutoka Beirut Mgogoro wa sasa kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah unatokana na mambo mawili makubwa, ambayo yamedumu kwa zaidi ya miongo minne. Israel inasema inataka kuisamba...
null
Je, uwepo wa Marekani katika Mashariki ya Kati umeongezeka kiasi gani tangu Oktoba 7? Kama sehemu ya lengo lake la "kudumisha utulivu wa kikanda na kuzuia kuenea zaidi kwa mgogoro," Marekani imekuwa ikituma wanajeshi wake Mashariki ya Kati tangu mgogoro ulipozuka mnamo Oktoba 7, 2023. Mwaka mmoja uliopita, Hamas ilizin...
null
Lebanon: 'Waajiri wangu walinifungia nyumbani na kuondoka Israel ilivyoanza kudondosha mabomu' - Author, Manal Khalil & Ethar Shalaby - Nafasi, BBC News Arabic Wakati shambulio la anga la Israeli lilipopiga nyumba ya mwajiri wake kusini mwa Lebanon, Andaku (si jina lake halisi) alijikuta peke yake, akiwa amejifungia nd...
null
Ushindi wa Trump una maana gani kwa Iran? Katika mojawapo ya nafasi chache za maafisa wakuu wa Iran, msemaji wa serikali alipuuza athari za matokeo ya uchaguzi wa Marekani kwa Iran. Fatemeh Mohajerani alieleza kwamba haijalishi nani atakuwa rais wa Marekani. Mpango wetu tayari umefanikiwa. Bi Mohajerani alisema kwamba ...
null
Vita vya Ukraine: Ni nchi gani zinazoipa Urusi silaha? - Author, Jeremy Howell - Nafasi, BBC World Service Urusi inatuma mamilioni ya makombora kwa mwaka kwenye vita vyake nchini Ukraine, pia hufanya mashambulizi ya anga – na inasemekana silaha hizo hutolewa na washirika wa kigeni. Wakati mataifa ya Magharibi yakijarib...
null
Kilichomo katika tathmini ya Marekani iliyovuja na kufichua mipango ya Israel kuishambulia Iran Frank Gardner Mwandishi wa Habari za Usalama Wachunguzi wa Marekani wanajaribu kufahamu jinsi nyaraka mbili za kijasusi zenye usiri mkubwa sana zilivyovujishwa mtandaoni. Nyaraka hizo, ambazo zilionekana kwenye programu ya k...
null
"Je, Iran Imebadilisha mstari wake mwekundu Mashariki ya Kati?" Leo, katika mapitio ya magazeti yetu, tunapitia makala kutoka Jerusalem Post ambayo inazungumzia mabadiliko ya mistari myekundu ya Iran katika Mashariki ya Kati, na kuibua suala la mzozo juu ya ukanda wa Zangezur na uhusiano kati ya Iran, Armenia, Azerbaij...
null
Daniel Khalifa, mwanajeshi wa Uingereza aliyekuwa na ndoto ya umaarufu na kuwa jasusi wa Iran Ilikuwa majira ya saa moja unusu asubuhi mnamo tarehe 6 Septemba mwaka jana wakati Sky Walkins alipokuwa akiendesha gari kwenye barabara mbili kusini mwa Wansworth Square ya London. Hakuamini kile alichokuwa akikiona. Mtu mmoj...
null
Timu zinahitaji nini ili kufuzu Afcon 2025? Kufikia wakati huu wiki ijayo tutajua timu 24 zitakazoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2025, huku duru mbili za mwisho za mchujo zikiwa zimepangwa kuchezwa. Ghana ndio jina kubwa lililo katika hatari ya kukosa kushiriki michuano hiyo nchini Morocco, huku Black Stars wakih...
null
'Tuliambiwa alikufa kutokana na njaa' - Author, Bushra Mohamed - Nafasi, BBC News Ni katika eneo la Yaqshid iliyoko Mogadishu, mpakani Somalia,ambalo familia ya Fathi Hussein mwenye umri wa miaka 26 imejawa na simanzi. Familia hiyo inasimulia siku za mwisho za Fathi kwa majonzi. “Tulijulishwa na manusura kuwa Fathi ali...
null
'Mnibake mimi na sio binti zangu' - vita vya kutisha vya Sudan - Author, Barbara Plett Usher - Nafasi, BBC Africa correspondent, Omdurman Sudan iko katika hali mbaya. Baada ya miezi 17 ya vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoiangamiza nchi hiyo, jeshi limefanya mashambulizi makubwa katika mji mkuu Khartoum,...
null
Mvutano wa Dangote na mafia wa mafuta Nigeria: Nani atashinda? - Author, Will Ross - Nafasi, BBC Africa Uzalishaji wa petroli katika kiwanda cha mafuta cha mfanyabiashara tajiri, Aliko Dangote chenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 20, huenda ikawa ni habari njema kwa Nigeria. Kwa muda mrefu tangu mafuta yalipogu...
null
'Tunaishi kwa uoga' - utekaji wawatia hofu wakimbizi na waomba hifadhi Kenya - Author, Wycliffe Muia - Nafasi, BBC News, Nairobi Kenya kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa kimbilio salama kwa wakimbizi, lakini taswira hiyo imeanza kubadilika pole pole na kuwa mahali pa kulipiza kisasi watu wanaotafuta ulinzi dhidi ...
null
Kesi ya kumuondoa Gachagua inasikilizwa Seneti - Author, Basillioh Rukanga - Nafasi, BBC News, Nairobi Bunge la Seneti nchini Kenya limeanza hatua ya mwisho ya kumuondoa mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua. Wiki iliyopita wabunge walipiga kura katika Bunge la Kitaifa kuidhinisha kuondolewa kwake madarakani, na hivyo ...
null
Kuanzia mpiganiaji wa uhuru hadi kuwa rais wa kwanza mwanamke Namibia - Author, Wedaeli Chibelushi & Frauke Jensen - Nafasi, BBC News London & Windhoek Netumbo Nandi-Ndaitwah kwa jina maarufu NNN, ameandikisha historia baada ya kuchaguliwa kama rais wa kwanza mwanamke nchini Namibia. Akiwa na umri wa miaka 72 alishinda...
null
'Maiti zimetapakaa kila mahali' - wanakijiji wanaomboleza vifo vya watoto waliodondoshewa makombora - Author, Azeezat Olaoluwa - Nafasi, BBC News, Tudunbiri Maalim wa madrassa ,Masud Abdulrasheed, anatafuta faraja ili kukabiliana na kifo cha binti yake mwenye umri wa miaka saba ,Habeebah, aliyeuawa kufuatia mashambuliz...
null
Jinsi washirika walivyogeuka maadui katika taifa la Afrika lenye utajiri wa Almasi - Author, Damian Zane in London & Innocent Selatlhwa in Gabarone - Nafasi, For BBC News Sauti ya upole ya Ian Khama haifichi tena ghadhabu aliyonayo. Katika mahojiano kadhaa tangu 2019, rais wa zamani wa Botswana hakusita kuelezea kutori...
null
Ajuza wa Kiafrika mwenye miwani mikubwa na mtindo wa mavazi wa kipekee Bibi mmoja katika maeneo ya vijijini nchini Zambia amekuwa mwanamitindo na mwenye hisia za mtandao, baada ya kukubali kucheza na mavazi yake kwa kuyavaa kwa njia tofauti tofauti na kubadilishana mavazi na mjukuu wake ambaye ni mwanamitindo. Margret ...
null
Sababu za kutaka kumuondoa madarakani naibu rais wa Kenya - Author, Abdalla Seif Dzungu - Nafasi, BBC Swahili - Twitter, - Akiripoti kutoka Nairobi Kenya Wandani wa Rais wa Kenya William Ruto waliwasilisha hoja bungeni siku ya Jumanne ya kumshtaki Naibu Rais Rigathi Gachagua wakimtuhumu kwa kuchochea chuki za kikabila ...
null
Biashara, misaada, usalama: Ushindi wa Trump una maana gani kwa Afrika? Wedaeli Chibelushi BBC News Huku ikidhihirika kuwa Donald Trump ameshinda uchaguzi wa urais Marekani kwa mara ya pili, viongozi kutoka kote barani Afrika walianza kutuma pongezi zao kwenye Twitter. "Zimbabwe iko tayari kufanya kazi nanyi", aliandik...
null
Alizaliwa Ufaransa lakini anatafuta fursa barani Afrika Menka Gomis alizaliwa Ufaransa lakini ameamua mustakabali wake utakuwa nchini Senegal, ambako wazazi wake walizaliwa. Jamaa huyu mwenye umri wa miaka 39 ni sehemu ya idadi inayoongezeka ya Waafrika wa Ufaransa wanaoondoka Ufaransa, wakilaumu kuongezeka kwa ubaguzi...
null
Fahamu magonjwa yanayoweza kusambazwa na wanyama wafugwao nyumbani na vidokezo 5 vya kuyaepuka Ni jambo lisilopingika kuwa wanyama tunaowapenda kuwafuga nyumbani wamekuwa sehemu muhimu ya familia nyingi na wanapata nafasi zaidi na zaidi (na kupendwa) kutoka kwa wanaowafuga (binadamu). Kuishi na wanyama mfano mbwa, paka...
null
Wanyama wanaoota kama binadamu Wakati fulani ilifikiriwa kuwa uwezo wa kuota ulikuwa tabia ya kipekee ya mwanadamu. Lakini aina kadhaa za spishi za zinaweza kufanya hivyo pia. Buibui wachanga wanaoruka huning'inia kwenye uzi usiku kucha, kwenye sanduku, kwenye maabara. Kila mara, miguu yao inapinda na utando wao hutiki...
null
Mambo saba ambayo sayansi imefichua kuhusu viumbe wa ajabu Kwa miaka mingi, BBC Future imeangazia simulizi mbalimbali kuhusu jinsi maisha kutoka ulimwengu mwingine yanavyoweza kuwa, na nini athari ya kugundua viumbe vya ajabu vinaweza kuwa vipi. Tunapoanza wiki ya makala maalum kuhusu viumbe wa ajabu - yote haya kuadhi...
null
Biolojia Fahamu ugonjwa wa preeclampsia ambao umewashangaza wanasayansi 27 Novemba 2024 Je, viumbe wa ajabu wanaweza kumrejeshea binadamu uhai kwa kutumia kifaa hiki? 8 Novemba 2024 Sokwe 'wanajitibu' kwa dawa za mitishamba-Utafiti wagundua 21 Juni 2024 Kwa nini bahari za dunia zinabadilika rangi? 26 Mei 2024 Wanasayan...
null
Kwa nini miili ya wanadamu haijafunikwa kabisa na nywele kama wanyama wengine Ikiwa wageni wangekuja Duniani na kuwaweka wanadamu katika mstari sawa na nyani wengine wote, mojawapo ya tofauti za kwanza ambazo wangeona, pamoja na umbo letu la kusimama wima na njia ya kipekee ya kuwasiliana, ingekuwa miili yetu inayoonek...
null
Ikiwa nyoka ataingia nyumbani kwako, fanya hivi Na Murugesh Madkannu, BBC Tamil Nilipokuwa mtoto, kulikuwa na miti na vichaka vingi kuzunguka nyumba yetu. Jioni moja kulitokea tukio. Umeme ulikatika wakati tunakula. Baada ya kumaliza chakula kilichobaki tukiwa gizani, nilienda kwenye bomba lililokuwa karibu na ukuta wa...
null
Kakakuona: Mnyama anayewindwa zaidi duniani Kakakuona anashika nafasi ya kwanza katika orodha ya mamalia wanaosafirishwa kwa magendo duniani. Umoja wa Mataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ulibaini kuwa kati ya mwaka 2000-2019, karibu kakakuona laki 9 walisafirishwa. Kwa upande mwingine, mnamo 2019, mamlaka ya Malaysia ilik...
null
Kwanini wanyama wa jamii ya mbwa hugagaa kwenye kinyesi? - Author, Richard Gray - Nafasi, BBC Mbwa wana mvuto wa ajabu wa kupenda kuzunguka katika vitu vyenye harufu mbaya. Na ndicho alichokishuhudia mtafiti Simon Gadbois kila alipomchukua mbwa wake, Collie Zyla katika safari zake za utafiti. Wakati akiwafuatilia wanya...
null
Mamilioni ya punda huuawa kila mwaka kutengeneza dawa Na Victoria Gill na Kate Stephens BBC, BBC News Siku hiyo ilianza kama siku yoyote ya kawaida. Asubuhi, aliondoka nyumbani kwake viungani mwa jiji la Nairobi na kwenda shambani kuchukua mifugo yake. "Sikuwaona," anakumbuka. "Nilitafuta siku nzima, usiku kucha na sik...
null
Kimeta ni nini na ni ugonjwa wa kutisha kiasi gani? Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti Jumatatu kuwa nchi tano za Afrika Mashariki na Kusini zinakabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa bakteria wa kimeta (anthrax). Zaidi ya visa 1,100 vya maambukizi, visa 37 vilivyothibitishwa na vifo 20 vimerekodiwa katika miezi ya h...
null
Sokwe asiyetaka kutenganishwa na mtoto wake aliyekufa miezi 3 iliyopita - Author, Darius Brooks - Nafasi, BBC Hii ni mara ya pili kwa sokwe Natalia kupoteza mtoto. Alijifungua mwanzoni mwa Februari mwaka jana na kila kitu kilionekana kuwa sawa katika mbuga ya wanyama ya Bioparc, katika jiji la Valencia, Uhispania. ''La...
null
Kwa nini tunapenda wanyama wenye sura mbaya? - Author, Isabelle Gerretsen - Nafasi, BBC Kila mwezi Juni huko Petaluma, California, Marekani majaji hutupia jicho safu ya mbwa ili kuamua mshindi wa shindano la Mbwa Mbaya Zaidi Duniani. Shindano hili huvutia mioyo ya wapenzi wa wanyama ulimwenguni. Swali, kwa nini tunavut...
null
Kwa nini wanyama wengine hufadhaika wakati wa kupatwa kwa jua? Wanadamu hustaajabishwa na kupatwa kwa jua, lakini wanyama wengine huhisije mchana unapogeuka kuwa usiku kwa muda mfupi? Katika matukio maalum sana, wakati hali inapokuwa sawa tu, mwezi huzuia jua na anga linakuwa jeusi. Ingawa kupatwa kwa jua kwa jumla hud...
null
Wanyama 9 wanaoweza kuishi bila chakula wala maji kwa muda mrefu Chakula ndio chanzo kikuu cha nishati kwa mwili wetu kufanya kazi vizuri. Chakula pia huongeza usagaji chakula huku kikiipa nguvu mifupa, misuli na mishipa ya fahamu. Ikiwa hatutakula, tunaweza kuwa na hasira na upungufu wa maji mwilini. Wanadamu hawawezi...
null
Wanyama watatu wenye uwezo wa kugundua magonjwa kwa wanadamu - Author, Jacqueline Boyd - Nafasi, BBC Linapokuja suala la kutambua ugonjwa kwa usahihi, unaweza kufikiri mara zote unahitaji mashine za gharama kubwa na vifaa vinavyoweza kuangalia kwa undani kile kinachotokea katika mwili. Ingawa vyombo hivi vinafanya kazi...
null
Wanasayansi wanajifunza kuzungumza lugha ya nyangumi - Author, Katherine Latham - Nafasi, BBC Ilikuwa mwaka 2021, nje ya pwani ya kusini-mashariki mwa Alaska, ambapo timu ya wanasayansi sita ilicheza rekodi ya sauti ya salamu kupitia spika iliyo chini ya maji. Walipigwa na butwaa walipogundua nyangumi mmoja waliyemwita...
null
Ucheshi sio kwa binadamu tu,wanyama pia hufanyiana utani Unapofikiria juu ya kile kinachotofautisha spishi zetu na wanyama wengine, basi ucheshi inaongoza kwenye orodha. Tunapenda kucheka - sana, kiasi kwamba furaha inayotokana na vichekesho inaonekana usoni mwetu. Watoto walio na umri wa miezi mitatu pia hucheka, kati...
null
Nyoka aliyezaa watoto 14 bila kupewa mimba na mwenza Nyoka ambaye amekuwa akidhaniwa kuwa dume kwa miaka mingi amezaa watoto 14 bila ya kujamiiana. Ronaldo, mwenye umri wa miaka 13, anaishi katika Chuo cha City of Portsmouth. Pete Quinlan, mtaalamu wa wanyama katika chuo hicho, alidhani ni nyoka wa kiume hadi Ronaldo a...
null
Chatu alivyommeza mwanamke mwenye umri wa miaka 36 Mwanamke mmoja amepatikana amekufa ndani ya chatu nchini Indonesia. Kwa kawaida nyoka hawa huwameza binadamu mara chache, lakini hiki ni kisa cha pili ambacho kimefahamika cha chatu kummeza binadamu katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja. Mwanamke huyo mwenye umri wa ...
null
Jinsi ya kuwashinda duma kukimbia Duma ni maarufu kwa kuwa mnyama wa nchi kavu mwenye kasi zaidi - lakini utafiti unapendekeza kuna mengi kwa jinsi wanavyokimbia zaidi tu ya kasi. Fikiria wewe ni swara, unayekimbia katika eneo la savana huko Afrika kujaribu kumtoroka duma - mnyama wa nchi kavu mwenye kasi zaidi duniani...
null
Vladimir Demikhov: Mwanasayansi wa Soviet aliyeushangaza ulimwengu kwa majaribio ya mbwa wenye vichwa viwili Mwaka 1959, mwanasayansi wa Soviet, Vladimir Demikhov, alimwalika mpiga picha wa Jarida la LIFE, Howard Zochurek kumpiga picha yeye na msaidizi wake, Dk Vladimir Goriainov, wakifanya upasuaji wa mwisho, wa kuund...
null
Nini cha kufanya kwanza unapoumwa na nyoka, ili kuokoa maisha? Karibu 300% ya nyoka wote duniani wana sumu, na 50% ya visa vya nyoka wanaowauma binadamu huwa hawaachi sumu ndani ya mwili wakati wa wanapomuuma binadamu. Kwa hivyo ni karibu visa 15 kati ya 100 ya nyoka ambapo muathiriwa huhitaji matibabu. Nini cha kufany...
null
Utafiti: Kwanini tausi dume hutoa sauti ya uwongo ya kushiriki tendo la ngono? Wanasayansi wanasema tausi dume hutoa sauti kama anafanya ngono ili kumvutia tausi jike aliye mbali. Watafiti kutoka Canada wanasema kuchezesha mkia wake pia ni sehemu ya kutoa mvuto wa kingo. Tausi hutoa sauti za aina nyingi. Wana sauti tof...
null
Mwamba mkubwa ulioua Dinosaria haukuwa peke yake - Author, Georgina Rannard - Nafasi, BBC Mwamba mkubwa (asteroid) ambao uligonga dunia na kuwaangamiza Dinosaria ama Dinosa miaka milioni 66 iliyopita, haukuwa peke yake, wanasayansi wamethibitisha. Mwamba wa pili, uilianguka baharini karibu na pwani ya Afrika Magharibi ...