name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | DAR ES SALAAM – MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani wafanyabiashara watatu wanaodaiwa ni wamiliki wa jengo lililoporoka Kariakoo, wakikabiliwa na mashitaka 31 ya kuua bila kukusudia. Washitakiwa hao ni mkazi wa Mbezi Beach na mfanyabiashara, Leondela Mdete (49), mkazi wa Kariakoo Mwarabu Zenabu Isla... |
null | NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumoikolojia Vijijini (EBARR) umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake kwa upande wa Zanzibar. Amesema hayo leo Novemba 7 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge... |
null | MAREKANI : MWANAMUZIKI wa nyimbo za Rap nchini Marekani, Sean Diddy Combs amenyimwa dhamana kwa mara ya tatu kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu akiwa gerezani. Hapo awali timu ya majaji wawili walikataa nguli huyo wa muziki kuachiliwa kwa dhamana kwa sababu ya kuwepo kwa wasiwasi wa kuwachezea mashahidi, wakiona... |
null | NAIROBI: Kampuni ya utoaji huduma ya mtandao ya Kenya, Mawingu imeitwaa kampuni ya IPS Habari yenye makao makuu jijini Arusha kwa dola za Kimarekani milioni 15 (takribani Shilingi bilioni 39). Kampuni ya ISP Habari, yenye uzoefu wa miaka 25, ina mtandao ulioenea katika mikoa saba na kuzifikia kaya na biashara maeneo vi... |
null | MATOKEO ya Utafi ti wa Taifa wa Lishe uliofanyika Novemba 2018 yanaonesha uwepo wa udumavu kwa watoto walio chini ya miaka 5 kwa asilimia 42.3. Yanaonesha pia, kuna utapiamlo mkali kwa asilimia 3.2 na wa kadri asilimia 4.7. Watoto wanaozaliwa na uzito pungufu ni asilimia 5.6 na wajawazito wenye lishe duni ni asilimia 6... |
null | WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametambulisha na kuwakabidhi wakandarasi wazawa kutoka Kampuni ya Salum Motors na Jonta Investment kwa wananchi watakaoanza ujenzi wa madaraja makubwa manne ya Ubagwe, Kasenga, Ng’hwande na Mwabomba yaliyoathiriwa na mvua za El Nino katika Halmashauri ya Ushetu yatakayogharimu Sh bi... |
null | SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na madhehebu ya dini katika kuwaletea wananchi maendeleo. Akizungumza leo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wakati wa kukabidhi fedha Sh milioni 100 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Tandahimba, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara K... |
null | UUNDAJI wa Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ni hatua muhimu na ya kimkakati kukabi li changamoto za kifedha nchini na kuchochea mabadiliko chanya ya kiuchumi. Tume hiyo inajumuisha wata alamu wenye uzoefu kutoka sekta mbalimbali za kiutawala, taaluma, fedha, sheria na hata sekt... |
null | Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mjadala wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwenyemaadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya hiyo leo Novemba 29, 2024. ARUSHA – Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mjadala wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwenye maadhimisho ya miaka... |
null | SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuongeza kampuni nyingine ya mabasi yaendayo haraka ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam. Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 29, na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki mkoani Singida, Francis Mtinga wakati akizungumza bungeni jijini... |
null | RAIS Dk Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani. Mjadala huo ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususa... |
null | WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la ofisi za Jimbo Katoliki la Bunda ambapo jumla ya Sh milioni 272.6 imekusanywa. Harambee hiyo imefanyika Novemba 10, 2024 wilayani Bunda mkoani Mara ambapo pamoja na mambo ... |
null | MMFUMO wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki (NeST) umeshinda tuzo ya “Mfumo Bora Zaidi wa Ununuzi wa Umma Barani Afrika” katika tuzo za African Association for Public Administration and Management (AAPAM), zilizokuwa zikishindaniwa chini ya uangalizi wa Umoja wa Afrika (AU), jijini Kampala, Uganda. Akizungumza... |
null | DAR ES SALAAM; SIMBA inaleta heshima. Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), baada ya Simba leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Bao hilo pekee lilifungwa na kiungo Jea... |
null | HEKAHEKA za usajili kuelekea msimu ujao kwa timu za Simba, Yanga na Azam zimezidi kushika kasi kila upande ukipambana kupata wachezaji ambao wanaamini watawapa mafanikio msimu ujao wa 2023/24. Ikumbukwe timu hizo msimu ujao zitapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Simba na Yanga zitashiriki Lig... |
null | WIZARA ya Nishati imetoa rai kwa mashirika na wadau mbalimbali nchini wakiwemo Puma Energy Tanzania kushirikiana kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo mkakati wa taifa wa nishati safi ya kupikia unaolenga asilimia 80 ya wananchi kutumia gesi ifikapo mwaka 2034 . Akizungumza katika hafla ya ut... |
null | SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema Mradi wa Utafiti wa Mafuta ghafi na gesi kwenye Bonde la Eyasi Wembere lililopo katika mikoa ya Simiyu, Singida na Arusha utekelezaji wake umefikia asilimia 40. Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za serikali zaidi ya Sh bilioni 40 ulianza mwaka 2015 ambapo shughul... |
null | PAMOJA na kutokuwa na malengo yoyote ya kisiasa wala ya kibiashara, Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya inawataka waumini wake kuwa raia wema na watiifu kwa serikali iliyopo madarakani. Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Khawaja Muzaffar Ahmad, amewahimiza waumini wa dini hiyo kudumisha amani, kuwapenda watu wo... |
null | Mrembo aliyetwaa taji la Miss Rwanda wa mwaka 2022 Divine Muheto akamatwa kwa kuendeshea gari akiwa amelewa Polisi nchini Rwanda wamemkamata Miss Davine wa taji la taifa la urembo kwa kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi” na kuharibu miundombinu. Divine Muheto, 21 pia anatuhumiwa kwa kuendesha gari bila le... |
null | MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema uamuzi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania kutoa mitungi 1,000 ya gesi katika mkoa huo kuwapatia mama lishe na baba lishe unakwenda kuchochea kasi ya kuzuia matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa. Akizungumza leo Oktoba 11, katika viwanja vya Biafra Kinondoni, D... |
null | KATAVI: NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Deus Sangu ameupongeza Mkoa wa Katavi kwa usimamizi bora wa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi inayowanufaisha walengwa wa mfuko huo. Deus Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela mkoani Rukwa am... |
null | DAR ES SALAAM – Baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa wamejumuika na familia kupokea mwili wa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Marehemu Dk Faustine Ndugulile baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na kisha kuupeleka katika Hospitali ya Lu... |
null | DAR ES ES SALAAM: Kampuni ya mawasiliano, Vodacom Tanzania Plc imeungana kwa kushirikiana na Sanlam Investments East Africa Limited, leo wamezindua M-Wekeza, huduma ya kibunifu ya uwekezaji iliyoundwa ili kuleta fursa rahisi za uwekezaji kwa watumiaji wa M-Pesa kupitia njia ya kidijitali ya simu zao za mkononi. M-Wekez... |
null | MSEMAJI Wa Taasisi ya Dini ya Kiislam ya Twarika Kitengo Cha Idara Ya Habari, Shekhe Harun Hussein amewaomba wananchi wote nchini kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kuwasihi wananchi ikiwemo viongozi wa dini kuhamasisha wananchi kujiandikisha. Shekhe Harun ametoa rai hiyo Arusha wakati a... |
null | DAR ES SALAAM – YANGA leo itakuwa ugenini kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Lindi. Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa michezo miwili mfululizo ambapo ilifungwa na Tabora United 3-1 na kufungwa na Al Hilal kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa bao... |
null | HAIKUWA jambo la ajabu kuwa safarini zaidi ya wiki kwa usafiri wa treni kutokana na changamoto za hapa na pale. Treni ndio ulikuwa usafiri wa wengi kati ya Dar es Salaam na Kigoma na Mwanza pamoja na mikoa mingine ambayo Reli ya Kati ilipita. Kwa wanafunzi waliokuwa wakitoka mikoa hiyo, watakumbuka walivyopewa mabehewa... |
null | DAR ES SALAAM – WADAU wa soka nchini wameisifu Tanzania kupanda kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Kwenye viwango vya ubora vya Novemba vilivyotolewa juzi, Tanzania imepaa mpaka nafasi ya 106 kutoka nafasi ya 112 iliyokuwepo mwezi uliopita. Ushindi wa Taifa Stars wa bao 1-... |
null | DAR ES SALAAM – Mamlaka ya Mapato tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa jumla kwenye uandaaji wa hesabu za kifedha zinazozingatia viwango vya kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) na Sekta za Kibiashara (IFRS). Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) Novemba 29. Vilevile... |
null | SERIKALI imesema itaendelea kuchukua hatua kuboresha utoaji elimu katika maeneo ya jumla na ya amali ili kuwezesha wadhibiti ubora wa shule na kubuni mbinu mbalimbali zitakazowezesha wanafunzi kuwa na ujuzi ikiwemo fursa za kujiajiri pasipo subiri kuajiriwa. Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 1, 2024 na Mkurugenzi wa I... |
null | RAIS wa Kenya, William Ruto amemteua Profesa, Kithure Kindiki kuwa naibu rais akichukuwa nafasi ya Rigathi Gachagua, ambaye aliondolewa madarakani na maseneta jana. Prof. Kindiki ambaye anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini ya bunge kabla ya kushika nafasi ya rasmi nafasi hiyo.... |
null | ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, Profesa Owdenburg Mdegela, amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James, kufuatilia kwa makini shughuli zinazofanywa na makanisa yanayomilikiwa na watu binafsi, ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika mji wa Iringa. Akizungum... |
null | ZANZIBAR: Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said amewataka wanaume kwenye maeneo mbalimbali kuwapa ushirikiano wanawake haswa wenye maono makubwa ya kiuchumi na kijamii. Zena ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo katika kilele cha tuzo za Malkia wa nguvu zinazotolewa na Clouds Media Gro... |
null | WANANCHI wa Mkoa Kigoma wanatarajia kupokea mitungi 19,530 ya gesi safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia. Mhandisi Mwandamizi wa Wakala wa nishati Vijijini (REA), Deusdedit Malulu amesema hayo akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye alipofi... |
null | MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango amesema marehemu Dk Faustine Ndugulile alikua kiongozi mwenye nidhamu, rafiki wa kila mtu na kiongozi aliyeweza kutetea vema maslahi ya Taifa. Makamu wa Rais amesema hayo leo Novemba 30 alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (... |
null | DESEMBA 20, mwaka uliopita, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambayo ni moja ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ilifanya uchaguzi mkuu ambao pamoja na viongozi wengine, ulikuwa kumchagua rais. Awali, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) ilitangaza watia nia 26 waliokidhi vigezo vya kugombea k... |
null | BORUSSIA Dortmund leo inaikaribisha Bayern Munich kwenye uwanja wa nyumbani wa Signal Iduna katika ‘dabi’ ya Ujerumani ukiwa mchezo wa Ligi Kuu ya Bundesliga. Bayern inaongoza Bundesliga ikiwa na pointi 29 baada ya michezo 11 wakati Dortmund ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 19. Mechi nyingine za Bundesliga pamoja na ... |
null | KATIKA mojawapo ya falsafa zake za R nne za Rais Samia Suluhu Hassan, zipo mbili zinazozungumzia kuhusu mariadhiano na mageuzi. Falsafa nyingine mbili zinahusu ustahimilivu na kujenga upya. Katika hotuba yake kwa taifa kwa ajili ya kuukaribisha mwaka huu wa 2024, Rais Samia aligusia kuhusu kasi ya utekelezaji wa falsaf... |
null | BARAZA la Mtihani Tanzania NECTA limepanda miti ,zaidi ya 2000 katika shule tano za msingi katika Jiji la Tanga ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupanda miti 100,000 kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu kote nchini . Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Said Mohamed leo katika shul... |
null | KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imepongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga Sh bilioni 8 kuanza kutelekeza mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) katika eneo lililopo pembezoni mwa uwanja wa mpira wa Afcon uliopo kata ya Olmort Jiji la Arusha . Pongezi hizo zimet... |
null | DAR ES SALAAM; TAASISI ya Al Ameen Foundation yenye makao makuu Kijitonyama, Dar es Salaam imetoa msaada wa vitimwendo 50 kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Msaada huo ulikabidhiwa hivi karibuni kwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Bin Ally, tukio lililofanyika makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanza... |
null | KIGOMA: WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuleta mapinduzi sekta ya umwagiliaji hivyo miradi yote aliyoahidi itatekelezwa Bashe alisema hayo akizungumza na wadau wa umwagiliaji katika uzinduzi wa mradi wa umwagiliaji katika bonde la Luiche wilayani Kigoma. “ Utekelezaji wa mir... |
null | SERIKALI ina jukumu kubwa la kuweka mikakati ya kuendelea kurasimisha biashara nchini na kuhamasisha utumiaji wa mashine za kielektroniki katika utoaji wa risiti ikiwa ni pamoja na kutumia risiti hizo kujipatia zawadi kupitia Tuzo ya Uzalendo inayotarajiwa kufunguliwa rasmi hivi punde. Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, ... |
null | UONGOZI wa Shirika la Ndege la Kenya (KQ) umethibitisha kifo cha abiria kilichotokea katika ndege ya shirika hilo namba KQ003 iliyokuwa inatoka katika Mji wa New York nchini Marekani kuelekea katika Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi wiki iliyopita. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo hivi karibuni ilisema mmoja wa abiria wa n... |
null | WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya Mwanga Hakika (MHB) kwa kuendelea kutanua mtandao wake ambao hadi sasa umeigusa sekta ya miundombuinu na wajasiriamali wadogo wadogo. Dk Mwigulu aliyasema hayo jijini Arusha Jumapili wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo kuongeza kuwa kuendelea kuong... |
null | KAHAMA, Shinyanga: NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewaelekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wanaongeza nguzo 40 ambazo ni sawa na kilometa mbili ili wananchi wa vijiji vya Manzwagi na Kidunyashi wapate nishati ya umeme kabla ya Julai 27, 2024. Kapinga amesema hayo alipokuwa anahitimisha ziara y... |
null | TIMU ya wanawake ya Vijana Queens iliyokuwa inashiriki Ligi ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam imefutiwa matokeo ya mchezo wake wa nusu fainali namba 504 ilipocheza dhidi ya JKT Stars. Taarifa ya Kamati ya Ufundi na Mashindano ya Chama cha Kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD), iliyotolewa na Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindan... |
null | WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Dk Ashatu Kijaji ameliomba Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) liwezeshe jamii kiuchumi kukabili uharibifu wa mazingira. Ametoa ombi hilo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Sera na Utetezi wa WWF Dk Lin Lin katik... |
null | MIAMBA ya soka nchini, Simba inashuja dimbani ugenini kuikabili Mashujaa katika mchezo pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo. Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. SOMA: Simba presha inapanda, inashuka Kwa mara ya mwisho timu hizo kukutana katika mchezo wa Ligi Kuu Machi 15, 2024, Simba ili... |
null | TIMU za Geita Gold na TMA STARS zinazoshiriki ligi ya Championship ndizo pekee hazijaguswa nyavu zao kwenye Ligi hiyo katika michezo sita zilizocheza mpaka sasa. Geita ambayo ni kinara wa ligi ikiwa na pointi 14 katika michezo sita, imeshinda minne na sare mbili, wakiwa hawajapoteza mchezo huku TMA ikishinda mitatu na ... |
null | KWA mujibu wa tetesi za usajili klabu ya Barcelona imeripotiwa kufuatilia “hali ngumu” ya mlengwa wake wa muda mrefu wa uhamisho Rafael Leao inayomkabili msimu huu katika timu ya AC Milan. Leao amekuwa muhimu katika klabu ya Milan tangu alipojiunga mwaka 2019 lakini ghafla amejikuta si muhimu katika wiki za hivi karibu... |
null | NAIBU Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema vijiji vyote 76 vya Jimbo la Newala Vijijini Mkoa wa Mtwara vimefikiwa na huduma ya umeme kwa umbali wa kilometa 1. Kapinga amesema hayo leo Oktoba 29, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala Vijijini aliyetaka kufahamu lini Serikali ita... |
null | DODOMA: WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewata wataalamu kufanya utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji jijini Dodoma ili kuruhusu uchimbaji wa visima virefu kwa haraka katika mkoa huo kutatua tatizo la upungufu wa maji linalotokana na ongezeko la watu katika jiji hilo. Aweso amesema hayo Oktoba 31,2024 akiwa katika ziara... |
null | Seattle Locksmith is a directory of highly experienced professionals who have a reliable trustworthy reputation in all the USA. A commercial locksmith is somebody who offers locksmith services to businesses and industries. We are proud to be one of the only locksmiths in the area who can fix mortise locks. However any ... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa usalama wa chakula katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na kuzisihi nchi hizo kuwekeza kwenye uchumi wa buluu. Rais Samia amependekeza hayo katika Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika Kinshasa Mji Mkuu wa Jamhuri ya Kid... |
null | Cortexi is a supplement that is reportedly effective in managing ear inflammation. This product not only boosts brain activities but also reduces oxidative stress and enhances metabolic health, thanks to its natural composition. By utilizing nature’s gifts, Cortexi promises to deliver optimal results through its carefu... |
null | At 2.4 miles, as you approach the pond, a sign post points to Mud lake one way and Route 58 in the opposite direction. The more difficult route goes down to follow the creek bed while the more moderate trail goes up and avoids the rough rocks. Scala Build Tool (sbt) is a build tool for Scala, Java, and more. After all,... |
null | ISRAEL: WAZIRI Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amemfuta kazi waziri wake wa ulinzi, Yoav Gallant, na kusema amekosa imani naye. Kwa mujibu taarifa iliyotolewa ofisini kwake, Netanyahu amesema hapo awali Gallant alikuwa muaminifu katika utendaji kazi hasa katika mipango ya kivita lakini sasa uaminifu huo haupo tena. ... |
null | MOJA ya malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 – 2025 ni kuimarisha sekta mbalimbali za kiuchumi ili kuliwezesha taifa kupata fedha za kuwaletea wananchi maendeleo. Moja ya sekta hizo ni utalii, ambayo CCM katika ilani yake hiyo ya uchaguzi imeeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ... |
null | WANANCHI wa Zambia, Alhamisi ya Agosti 12 walifanya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge. Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo imemtangaza Hakainde Hichilema kuwa mshindi katika uchaguzi wa Rais, akimuangusha Rais wa sasa, Edgar Lungu. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zambia, Esau Chulu alitangaza matokeo rasmi ... |
null | MAPEMA wiki hii Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepitisha kanuni ya kutumia wachezaji 12 wa kigeni katika mchezo mmoja kwa timu za Ligi Kuu. Ikumbukwe kuanzia msimu uliopita idadi ya wachezaji wa kigeni ilikuwa ni 12 na wanaoruhusiwa kucheza katika mchezo mmoja ni wanane. Kanuni hiyo ni kama inakwenda ku... |
null | DAR ES SALAAM katika viunga vya Chamazi inashuhudia Ligi ya Mabingwa Afrika wa Ukanda wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa wanawake ikitimua vumbi katika Uwanja wa Azam Complex. Ligi hiyo ambayo inadhaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan inashirikisha timu nane zilizopangwa katika makundi maw... |
null | Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kibiti mkoani Pwani kimepata viongozi wapya baada ya kufanyika uchaguzi wa ndani wa chama hicho hapo mwishoni mwa wiki huku Juma Kassim Ndaruke ameibuka mshindi. Kada huyo ameshinda kinyang’anyiro hicho baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu, Abdujabiri Malombwa ambaye alikuwa akitetea... |
null | WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amewaasa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuongeza ubunifu na kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazojitokeza wakati huu ikiwemo ya kuwekeza katika biashara ya kuvuna hewa ukaa. Balozi Dk Chana alitoa agizo hilo Jumatatu Dodoma wakati akifungua mkutano wa kwan... |
null | Mbunge Hamis Kigwangala ameomba mwongozo bungeni akitaka wabunge wakatwe kiasi cha Sh 50,000 kutoka kwenye posho zao za leo kwa lengo la kumchangia kijana Majaliwa Jackson. Akijibu hilo, Spika Dk Tulia Ackson ametoa utaratibu wa namna ya kumchangia kijana huyo aliyefanya kitendo cha kishujaa kilichosababisha abiria 24 ... |
null | MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Dustan Kyobya leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Meneja Huduma za Habari za Lugha za Kigeni, Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Christopher Majaliwa, kuhusu fursa za kimaendeleo zilizopo katika Wilaya na Mkoa wa Mtwara. Viongozi hao pia walijadili mikakati ambayo itawezesha kutan... |
null | Kanda Tanzania Wizara yaridhishwa uzalishaji mbegu za mazao Missenyi byNa Diana Deus, MissenyiOctober 20, 2022 |
null | WAKATI dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesisitiza kuwa teknolojia kuwa ni nyezo muhimu katika kuchochea usawa wa kijinsia itakayowaweza wanawake kukuza biashara zao. Akitoa salamu zake za maadhimisho ya siku hiyo, Mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula amesema taasisi anayoi... |
null | DODOMA: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usambazaji umeme kwenye vijiji, vitongoji na usimamizi wa miradi ya nishati jadidifu ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya Wizara ya Nishati. Ametoa po... |
null | MWANDISHI wa habari mwandamizi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Zaituni Mkwama, ameshinda tuzo ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) akiwa mwandishi bora wa taarifa za mamlaka hiyo. Tuzo hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Jaji Mshibe Ali Bakari. Akizungumza katika ug... |
null | ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Doha,Qatar ambapo anatarajia kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa kutimiza miaka Thelathini ya Familia Duniani utakaofanyika 29 Oktoba 2024 nchini humo. Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa... |
null | MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Viti Vitatu Bara, Shamira Mshangama ametembelea kituo cha kulea wazee na wasiojiweza akiwa katika ziara fupi ya kichama Bukoba, mkoani Kagera. Katika kituo hicho chenye wazee 19 wakiwemo 15 wanaume na 4 wanawake, Shamira alipata muda wa kuzun... |
null | VIJANA wahandisi 123 waliosajiliwa na Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) wamepewa mafunzo ya ujasiliamari na ubunifu wa kibiashara ili waweze kujiajiri wenyewe kwa kufungua makampuni yao binafsi ya ujenzi na shughuli nyingine mbalimbali kulingana na kozi walizosoma badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini. Seris Foundat... |
null | SERIKALI imesema Wizara ya Maliasili na Utalii imekubaliana kushirikiana na Urusi kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii. Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amezungumza hayo katika kikao na ujumbe kutoka Urusi ulioongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Kiuchumi nchini Urusi, Maxim Gennadyevich Reshetnikov, ... |
null | LIGI Kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka 2022/23 inatarajiwa kuanza Septemba 2 mwaka huu. Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 inatarajiwa kumalizika Juni mwakani. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na bodi ya ligi ya Shirikisho la Soka Zanzibar, (ZFF) jana, siku hiyo kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Black Sailor na Malindi. Mec... |
null | CHECHE za Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka zimemuunguza Mrajis Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Tabora, Absolom Chaliga baada ya kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. Barua iliyoandikwa na Dk Benson Ndiyege ambaye ni Mrajis wa Vyama vya Ush... |
null | WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa jana ameliaga kundi lingine la wakazi wa Ngorongoro 115 linaloelekea eneo la Msomera lililoko Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambako serikali imeweka miundombinu ya kuwawezesha kuishi katika hali ya utulivu. Kundi hilo la wakazi 115 lenye kaya 25, linakuwa ni la awamu ya tano ambapo awamu zi... |
null | MATAIFA makubwa ya Ulaya “yamepunguza” msaada wa kijeshi kwa Ukraine tangu Aprili mwaka huu, ikilinganishwa na ule unaotoka Marekani, mtandao wa POLITICO, umeripoti. Nchi sita kubwa zaidi barani Ulaya, Uingereza, Ujerumani, Poland, Ufaransa, Italia na Uhispania, hazikutoa “ahadi mpya za kijeshi kwa Ukraine” mwezi Julai... |
null | KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameagiza watumishi waliohusika na upotevu wa Sh bilioni 1.6 katika mradi wa ujenzi wa bwawa la umwagiliaji Kijiji cha Inara Wilaya ya Tabora, watafutwe ili kueleza wapi walikopeleka fedha hizo. Pia, ametoa maeleke... |
null | Infographics Kanda Maisha ya Vijijini Tanzania Mtaka awapa angalizo ambao hawajahesabiwa byOscar JobAugust 25, 2022 Infographics Kanda Maisha ya Vijijini Tanzania Tanga sensa ni shwari byAmina Omari, TangaAugust 25, 2022 Infographics Kishikwambi kilichoporwa kwa karani wa sensa Katavi chapatikana byNa Swaum Katambo, Ka... |
null | PANZI mwenye rangi sawa na bendera ya Tanzania, anayepatikana katika hifadhi ya mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi, Wilaya ya Kisarawe, Pwani amejengewa mnara katika mzunguko uliopo eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, ili kutoa uelewa kwa Watanzania wamjue. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Elia... |
null | UBALOZI wa Tanzania nchini China umesema filamu ya ‘Tanzania: The Royal Tour’ imeoneshwa katika mtandao maarufu wa Haokan nchini China. Kupitia ukurasa mtandao wa kijamii wa twitter, ubalozi huo umeeleza kuwa zaidi ya watu milioni moja walikuwa wameitazama kupitia Haokan ndani ya siku tatu. Pia Ubalozi Mdogo wa Tanzani... |
null | MBUNGE wa Kilosa, mkoani Morogoro, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka wananchi kutunza misitu. Profesa Kabudi alisema hayo jumatano katika Kata ya Rudewa, wilayani humo mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2022, Sahili Geraruma. Mwenge ulifika katika kata hiyo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mra... |
null | SERIKALI ya Tanzania, imepokea Euro milioni sita, sawa na Sh bilioni 13.2 kutoka Shirika la Ujerumani la GIZ, kwa ajili ya mradi wa kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyamapori hasa kwenye maeneo ya pembezoni mwa hifadhi. Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa ziara ya kikazi katika Chuo cha Mafunzo ya Ma... |
null | BODI ya Mkonge Tanzania (TSB) imesema iko tayari kushirikiana na Falme ya Babina Noko Ba Mampuru iliyopo katika Jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini kuendeleza mkonge. Ushirikiano huo utahusu mambo mbalimbali ikiwamo kutoa wataalamu wake na kubadilishana uzoefu. Kaimu Mkurugenzi wa TSB, Saddy Kambona alisema hayo jana... |
null | SHIRIKA la kimataifa la wanyamapori limesema Kenya imekuwa na ongezeko la asilimia 11 ya idadi ya faru kutoka 1,441 mwaka 2019, hadi 1,605 mwaka jana na hakuna waliopotea kwa ujangili. Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Ustawi wa Wanyama Afrika Mashariki (IFAW, James Isiche amesema miaka nane iliyopita kulikuwa na vit... |
null | MADIWANI wa Halmashauri wa Mji wa Geita wameiomba ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuweka wazi mapato na matumizi ya timu ya Geita Gold ili kujibu fununu za baadhi ya wachezaji kutolipwa mishahara. Hoja hiyo imeibuliwa na diwani wa viti maalumu, Farida Mfuruki katika kikao cha baraza la madiwani na kuhoji mwenen... |
null | KAMATI ya kudumu ya Miundombinu ya Bunge imefanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupata maelezo ya usimamizi wa mnada wa msafa utakaoiwezesha Serikali kupata Dola za Kimarekani milioni 187.4. Aidha wajumbe wa kamati hiyo wameelezwa namna vitalu vya masafa vitakavyowezesha utoaji wa hudu... |
null | MADIWANI wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelalamikia kushindwa kufanyika shughuli za maendeleo katika robo mbili za mwaka kutokana na mfumo wa kuhamisha fedha kushindwa kufunguka. Madiwani hao ambao ni diwani kutoka kata ya Kisuke Joseph Bundala na diwani kutoka kata kinamapuka Samweli Shari... |
null | WIZARA ya Fedha na Mipango imezindua Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma awamu ya sita itakayoimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato na matumizi ya serikali, na itaendelea kuadhibu watendaji wenye nia mbovu za kucheza na mifumo hiyo. Progrogramu hiyo pia itaangalia kwa undani ushirikishaji wanawake katika... |
null | WIZARA ya Fedha na Mipango itakuwa na Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa wiki moja kwa lengo la kutoa elimu ya kifedha kwa Watanzania nchini. Akizungumza jijini Dodoma juzi Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Charles Mwamwaja alisema maadhimisho hayo yatatumik... |
null | WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi imesema inajipanga kubadilisha sheria ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika huduma ya usafi ri wa reli kwa kununua mabehewa na kuyaendesha. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameyase... |
null | Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekutana jijini Dodoma. Kikao hicho kimeongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk. Ashatu Kijaji ambapo Mwenyekiti Mwenza alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ... |
null | TIMU ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 inashuka dimbani leo dhidi ya Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) Kanda ya CECAFA. Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa KMC uliopo, Mwenge, Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam. SOMA: Ngorong... |
null | MICHEZO ya Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea leo baada ya kusimama kupisha mechi za kimataifa ambapo viwanja vitatu vitawaka moto. Coastal Union iliyohamia Arusha itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Coastal ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 7 wa... |
null | MWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kufuzu klabu bingwa Ligi ya Kikapu Afrika (BAL) timu ya JKT imepoteza mchezo wa pili dhidi ya GNBC ya Madagascar kwa pointi 89-72. Mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya Filbert Bayi vilivyopo eneo la Mkuza, Kibaha mkoani Pwani, ulikuwa wenye ushindani mkali baina ya timu zo... |
null | KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen baada ya miaka mitatu jana alimjumuisha kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan). Kakolanya mechi ya mwisho ilikuwa 2019, Stars ilipocheza dhidi ya... |
null | KLABU ya Yanga jana ilitarajia kumtambulisha rasmi beki wake mpya, Yannick Litombo baada ya mchezaji huyo kukamilisha taratibu zote za kujiunga na miamba hiyo ya soka Tanzania Bara. Yanga ipo nchini Morocco katika jiji Marrakesh ambako imeweka kambi ikijifua kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na m... |
null | Mahusiano Michezo na Burudani Muziki Sanaa Utamaduni Ndoa ya Wolper Novemba byNa Martin MazugwaAugust 19, 2022 |
null | WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewashukuru wanamichezo na wasanii kwa mchango walioonesha katika kampeni za kuhamasisha jamii umuhimu wa kushiriki sensa Agosti 23, mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya Sensa, Majaliwa alisema wote wamefanya kazi kubwa na kuwaomba kuendelea kuhamasisha... |
null | MFANYABIASHARA na mbunifu wa mavazi, Rich Mitindo ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii wa filamu, Jaqueline Wolper ameweka wazi kuwa anatarajia kufunga pingu za maisha na nyota huyo Novemba 19, mwaka huu. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rich alisema kuwa amefikia maamuzi hayo ya kufunga ndoa na Wolper baada ya k... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.