text
stringlengths
1k
17.3k
label
int64
0
5
WATAHINIWA 1,358,217 wamesajiliwa kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) 2018, unaofanyika leo na kesho katika shule za msingi 17,336 Tanzania Bara.Kati ya watahiniwa hao wanaotarajiwa kufanya upimaji huo, wavulani ni 682,193 sawa na asilimia 50.23 na wasichana ni 676,024 sawa na asilimia 49.77. Aidha watahiniwa wenye mahitaji maalum wapo 3,336 kati yao 715 ni wenye uoni hafifu, 120 ni wasioona, 725 ni wenye ulemavu wa kusikia na 1,776 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.Ofisa Habari na Mahusiano wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), John Nchimbi alisema jana kuwa maandalizi yote kwa ajili ya upimaji huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani itakayotumika katika upimaji huo. Nchimbi alisema nyaraka zote muhimu zimeshafikishwa katika Manispaa na halmashauri zote za Tanzania Bara kwa ajili ya upimaji huo.Alisema mwaka 2007 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 1,195,970 hivyo kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 162,247 sawa na asilimia 13.57 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na mwaka 2017.Alisema, upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa hupima uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yale yote waliyojifunza kwa kipindi cha miaka minne na pia huwezesha kujua kiwango cha wanafunzi wanaomudu stadi za juu za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.“Matokeo ya upimaji wa daarasa la nne hubainisha maeneo muhimu yanayohitaji kufanyiwa maboresho katika vitendo vya ujifunzaji wa wanafunzi shuleni,” alisema.Nchimbi alitoa wito kwa Kamati za Mitihani za Mikoa, Halmashauri na Manispaa kuhakikisha kuwa taratibu zote za upimaji wa Kitaifa zinazingatiwa ipasavyo na kuhakikisha mazingira ya vituo vya upimaji yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.Pia alitoa wito kwa wasimamizi wote kufanya kazi zao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu na kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani baraza litachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa upimaji wa kitaifa.“Baraza linaamini kwamba kwa upande wa wanafunzi, walimu wao wamewaanda vizuri katika kipindi chote cha miaka minne ya elimu ya msingi, hivyo ni matarajio ya NECTA kuwa wanafunzi watafanya upimaji huo kwa kuzingatia kanuni za upimaji,” alisema.Aliwataka watahiniwa wote kutambua kwamba, kukiuka kanuni za upimaji au kufanya uanganyifu kutafanya wafutiwe matokeo yao yote. “Wamiliki wote wa shule mtambue kwamba shule zenu ni vituo maalum vya mitihani, hivyo hamtakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa upimaji,” alisema. Nchimbi alisema, baraza hilo halitasita kukifutia kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa upimaji wa Taifa.
3
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema itaangalia uwezekano wa kubadilisha sheria ya Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) iweze kumnufaisha msanii hata kama atakuwa ametangulia mbele za haki.Akizungumza kwenye kumbukizi ya wasanii iliyoandaliwa na Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania (Kamusata), Dar es Salaam jana, Waziri Dk. Harrison Mwakyembe alisema wasanii waliotangulia mbele za haki miaka 50 iliyopita hawanufaiki kutokana na sheria hiyo kusema kuwa baada ya miaka hiyo nyimbo zinakuwa urithi wa dunia.“Ndugu zetu waliingia mikataba lakini haiwanufaishi hasa wale waliotangulia mbele za haki, wameacha familia na watoto lakini changamoto iliyopo ni sheria ya Cosota inayosema nyimbo ikifikisha miaka 50 ni urithi wa dunia, familia hazinufaiki inabidi suala hili liangaliwe,” alisema.Pia, alisema serikali iko mbioni kujenga majengo ya sanaa na michezo, ambapo baadhi ya kuta zake zitabandikwa picha za wasanii maarufu waliofariki. Aliiagiza Basata kuhakikisha wasanii zaidi ya 300 waliotajwa katika kumbukizi hiyo zipatikane picha zao au michoro ya sura zao ili katika tukio la mwakani Kamusata itumie kutengeneza kalenda maalum kwa ajili ya kuziuza.Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mjumbe wa Kamusata, Hashim Kambi, alisema tukio hilo ni la kwanza kufanyika likiwa na sura ya kitaifa ili jamii itambue wasanii waliotangulia mbele za haki ni tunu kwa taifa. Tukio hilo lilienda sambamba na uzinduzi wa kamati hiyo chini ya udhamini wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Basata.“Malengo ya kumbukizi hii ni kuwakumbuka, kuwaenzi, na kuwaombea dua na maombi wasanii wa fani zote waliotangulia mbele ya haki, kuhamasisha na kutangaza shughuli za sanaa ili msanii aweze kunufaika wakati wa uhai wake katika nyanja za kiafya, kifedha na kiuchumi, “ alisema.Baadhi ya wasanii waliotangulia mbele ya haki na kukumbukwa ni Maalim Gurumo, Shakila Said, Steven Kanumba, Mbaraka Mwinshehe, Marijani Rajabu, Morris Nyunyusa, Salum Abdallah, Nasma Hamis, Siti binti Saad, Omar Kopa, na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Onesmo Kayanda, alisema amefarijika kuona wazee wanaandaa tukio kama hilo la kuwakumbuka wasanii waliofariki dunia ambalo limeunganisha makundi mbalimbali na ndugu wa marehemu.Alisema kadiri siku zinavyosogea matukio ya sanaa yamekuwa yakiongezeka na kuwahimiza wasanii watengeneze jukwaa maalum kwa ajili ya kuburudisha watu licha ya kwamba ni kazi. Mwakilishi wa Bodi ya filamu Tanzania, Simon Pete, aliwahimiza wasanii kufanya kazi kwa nidhamu na kwamba hata hao wanaokumbukwa ni kwasababu walifanya kazi nzuri.
4
VIJANA waendeshaji bodaboda wa Kata za Berege na Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani hapa, wamepatiwa mafunzo ya kulinda wanafunzi hasa wale wanaotembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni wasipate mimba katika umri mdogo.Mafunzo hayo yanatolewa kwa vikundi vya malezi kwa wanaume wanaotoka katika kata hizo yanayotolewa na Shirika lisilokuwa na kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF).Mmoja wa vijana hao, Frank Mdoga (27) ambaye ni Mwenyekiti wa waendesha bodaboda kata ya Kibakwe, alisema sasa wamekuwa wakipinga na kukemea mimba za utotoni baada ya kupata elimu kutoka CDF na sasa wamekuwa walinzi wa wasichana ili waweze kusoma na kufikia malengo yao.Hata hivyo, alisema jamii ina mtazamo mbaya juu ya waendesha bodaboda kuwa wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi hasa wale wanaotembea umbali mrefu kufika shuleni.Alisema mimba za utotoni zinasababishwa na malezi duni na ugumu wa maisha, hali inayochangia wanatunzi wengi kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo.Alisema bodaboda wamekuwa rahisi kuwapata wanafunzi hao kwa kuwa huwasaidia kuwabeba wanapokwenda au kurudi shuleni.Alisema asilimia kubwa ya wanafunzi wanatoka vijiji vya mbali kama Iyenge, Kingiti, Lukole, Chamtumile wanakuja kusoma Kibakwe na asilimia kubwa ya hao wanafunzi wamepanga mitaani.Alisema mazingira wanayoishi ni rahisi kushawishika na vijana wa mitaani, lakini jamii inaona vijana wa bodaboda ndio wanaowanyemelea wanafunzi hao, jambo ambalo sio lazima liwe la kweli.“Unapobeba abiria lazima kutakuwa na maongezi baadaye mnaanza kujenga mahusiano, lakini sasa mambo ni tofauti, tumekuwa tukitumia vizuri muda tunaokuwa vijiweni kuelimishana juu ya kuwalinda watoto wa kike na hili kwa kiasi kikubwa limefanikiwa,” alisema.Alisema baada ya kupatiwa elimu ya malezi kutoka CDF Sasa wamebeba kaulimbiu inayohoji, “Wewe ni mlinzi wa mwenzako”? Alisema sasa pindi bodaboda anapobeba abiria anaanza kutoa elimu, jambo ambalo limesaidia. Pia alisema mafunzo yanayotolewa na CDF yanawafunza jinsi ya kuishi na familia. “Elimu ya familia imenisaidia sana,” alisema.
3
VIJANA wa Zanzibar wanatakiwa kutambua kwamba Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 ndiyo yaliyomkomboa mwananchi na sio uhuru wa Desemba 10 mwaka 1963 kama ambavyo wameanza kujitokeza baadhi ya watu wakidai. Hayo yanasemwa na Waziri wa Vijana, Utamaduni na Sanaa, Ali Karume wakati akihutubia kongamano la Vijana katika kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil mjini Unguja. Jumapili iliyopita, Wazanzibari waliadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi, sherehe ambazo zilihudhuriwa pia na Rais John Magufuli. Waziri Karume anasema uhuru wa Desemba 10 mwaka 1963 haukuwa uhuru wa kweli kwa wananchi wazalendo wa Zanzibar kwa sababu ulikuwa bado unamtambua Sultani wa Oman kama mtawala.Anafafanua kwamba uhuru huo haukutolewa kwa lengo la dhati la kuwafanya wazalendo kuwa huru katika nchi yao kwa kumiliki mambo muhimu ya msingi ikiwemo ardhi bali kuendelea kuwa watwana katika nchi yao. Anakanusha kauli za baadhi ya watu ikiwemo wanasiasa wanaojaribu kuupa heshima uhuru wa Desemba 10 wa mwaka 1963 wakidai eti uliwalenga wananchi wa Zanzibar kuwa huru katika nchi yao. ‘’Mapinduzi ya 1964 ndiyo yaliyomkomboa mwananchi wa Zanzibar kuwa huru katika nchi yake... Uhuru wa Desemba ulikuwepo lakini uliwalenga watu wachache na makundi ya makabila fulani,” anasema. Anawataka Vijana kuyaunga mkono Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 kwa sababu miongoni mwa kundi ambalo limefaidika sanana na hatua hiyo ni vijana ambao wengi hawakuwpo wakati wa mainduzi hayo.Anataoa mfano kwamba mara baada ya Mapinduzi, Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Karume alitangaza elimu kutolewa na serkikali bure kwa wananchi Septemba 23 mwaka 1964 na hivyo kutoa fursa kwa kundi kubwa la vijana kusoma katika shule mbali mbali zilizotaifishwa na serikali. Aidha anasema wananchi walikuwa hawamiliki ardhi kwa ajili ya kujenga makazi wala kilimo, lakini mara baada ya mapinduzi ardhi ilitaifishwa na kuwa milki ya wananchi Baraka Shamte, kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye baba yake mzazi Mohamed Shamte ndiye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Desemba 10 anasema bila kumung’unya maneno kwamba serikali iliyoongozwa na baba yake ilikuwa kiini macho cha kutaka kuidanganya dunia kwamba Zanzibar ni huru. Shamte anasema nchi haiwezi kuwa huru na wananchi wake kama utawala wa kigeni utaendelea kushika hatamu za uongozi na kuwakandamiza wazalendo. Anasema hicho ndicho kilifanyika kwa uhuru wa Disembar 10 mwaka 1963 uliodaiwa kutolewa kwa wananchi huku ukweli ukiwa kwamba Sultani alikuwa anaendelea kushika hatamu za uongozi wa dola. Anasema siasa za Zanzibar katika harakati za kisiasa zilikuwa zenye mwelekeo wa chuki na kuwagawa wananchi wake. ‘’Mimi baba yangu alikuwa Hizbu na kiongozi wa ngazi za juu akiwa Waziri Mkuu... Mimi nilitofautiana naye na nilikuwa (ASP) wa hali ya juu... Sikutaka kutawaliwa na kusikiliza kasumba za wapinzani.’’Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ussi Yahya ambaye alipata kufanya kazi katika Serikali ya Sultani kabla ya Mapinduzi anasema madhila na ukandamizaji wa wananchi kutoka kwa Sultani ndiyo yaliyowasukuma Wazanzibari kufanya Mapinduzi. Anasema wapo watu wanajaribu kupotosha ukweli na kusema utawala wa Sultani haukuwa na madhara yoyote kwa wananchi wa Zanzibar jambo analosema ni mtazamo wa ajabu sana. Anasema utawala huo unawezaje kuwa sahihi wakati umiliki wote wa ardhi kwa shughuli za kilimo na makazi ulikuwa ulikuwa chini ya Sultani pamoja na familia yake au ndugu wa karibu. Kwa mfano, anasema Unguja na Pemba yalikuwepo jumla ya mashamba 745 ambayo yote yalimilikiwa na familiaa au ndugu wa Sultani. Anasema ilipofika tarehe Novemba 11, hayati Karume alianza kazi ya ugawaji wa ardhi katika mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na familia ya Kisultani kwenda kwa wananchi wazalendo.‘’Karume aligawa eka tatu tatu kwa wananchi wazalendo ili kuzitumia kwa shughuli za Kilimo,’’ anasema. Ussi anasema kabla ya Mapinduzi alikuwa tarishi na alikuja kuajiriwa na kuanza masomo nje ya nchi mara baada ya Mapinduzi mwaka 1964. Anasema kupitia serikali huru ya wazalendo, alikwenda China kusoma kuhusu namna ya kuendesha shughuli za kifedha na Benki.‘’Nilipelekwa China kwa ajili ya masomo ya miaka miwili kuja kuanzisha Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ).’’ Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi, Khadija Jabir anasema wanawake kabla ya Mapinduzi walikuwa hawana sauti huku wakinyimwa haki ya kupiga kura katika chaguzi mbali mbali zilizopita. Anasema Mapinduzi ndiyo yaliyofungua milango na kuwafanya wanawake kutambuliwa hadi kushika nafasi mbalimbali za uongozi. ‘’Mapinduzi ndiyo yaliyokuja kumpandisha hadhi mwanamke na kumtambua mwanamke na kumpa nafasi za uongozi,’’ anasema. Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa anasema utawala wa Kisultani uliwanyima wananchi haki zote za msingi ikiwemo umiliki wa ardhi, elimu na masuala mengine ya kijamii. Anasema kwa mfano katika kisiwa cha Pemba Ardhi yote yenye rutba ilikuwa ikimilikiwa na familia ya Sultani pamoja na mashamba ya mikarafuu.
3
Na MAREGESI PAUL-DODOMA SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ameziagiza kamati mbili za Bunge, ziwahoji wabunge wawili wa upinzani, Saed Kubenea (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), baada ya kutuhumiwa kwamba wametoa kauli zisizofaa juu ya Bunge na Spika. Akizungumza bungeni jana, Spika Ndugai aliiagiza Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, imhoji Kubenea ambaye ni Mbunge wa Ubungo, baada ya kukaririwa akiwa katika kanisa moja akizungumzia tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema). Pia, Spika aliiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imhoji mbunge huyo kutokana na kauli yake aliyoisema kanisani humo kwamba Spika Ndugai ni mwongo kwa kuwa alitaja idadi chache ya risasi zilizotumika kumshambulia Lissu wiki iliyopita. Kuhusu Zitto, Spika Ndugai aliiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imhoji mbunge huyo baada ya kukaririwa katika mitandao ya kijamii, akilalamikia uamuzi wa Spika wa kutoruhusu taarifa za kamati za kuchunguza madini ya tanzanite na almasi, zijadiliwe bungeni. “Kuna mjadala umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu juu ya ni chombo kipi kati ya Bunge, Serikali na Mahakama, kina nguvu kuliko chombo kingine. “Kuna watu wanasema Bunge ndilo lenye nguvu kwa sababu ndilo linalotunga sheria, wengine wanasema Serikali ndiyo ina nguvu kwa sababu inatekeleza sheria zilizotungwa na Bunge na wanaosema mahakama ndiyo ina nguvu wanasema hivyo kwa sababu ndicho chombo kinachotafasiri sheria. “Kwa hiyo, nawaomba wabunge tuwe makini tunapolizungumzia Bunge kwa sababu wakati mwingine tunamweka Spika katika ‘bad light’, jambo ambalo si jema kabisa. “Pamoja na hayo, mbunge mwenzetu Kubenea amekuwa mara kadhaa akitoa kauli zinazolifedhehesha Bunge na kuna maneno ameyasema madhabahuni hivi karibuni kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. “Katika maelezo yake, inaonekana mheshimiwa Kubenea analijua vizuri tukio hilo, hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge imwite ili imhoji ili aweze kusaidia upatikanaji wa taarifa muhimu. “Pia, mheshimiwa Kubenea amesema mimi nililidanganya Bunge kwa sababu nilitaja idadi ndogo ya risasi zilizotumika kumshambulia mheshimiwa Lissu wakati akijua mimi nilitoa taarifa ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma. “Sasa basi, kwa kuwa amesema mimi nililidanganya Bunge, aitwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili aeleze nililidanganyaje Bunge. “Naagiza popote alipo mheshimiwa Kubenea, ahojiwe na Kamati ya Adadi (Adadi Rajabu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama) kesho na afike kwa utaratibu wowote ule,” alisema Spika Ndugai. Akizungumzia suala la Zitto na kamati za kuchunguza biashara ya tanzanite na almasi, Spika alisema kauli za mbunge huyo ni za upotoshaji kwa kuwa kamati hizo ziliundwa na Spika na hivyo hakukuwa na haja ya kuziwasilisha bungeni kwa ajili ya mjadala. “Zitto amezungumzia suala la taarifa za kamati kutowasilishwa bungeni wakati kamati hizo niliziunda mimi na si Bunge. “Siku zote, kamati au tume huundwa kutokana na mapendekezo ya wabunge baada kuwa nimewahoji na nyie mkakubali. “Inapotokea hivyo, taarifa itakayoandaliwa na kamati au tume husika, basi italetwa bungeni kwa ajili ya mjadala kwa sababu Bunge ndilo lililokubali kuundwa kwa kamati husika. “Sasa, naomba niwaulize ni lini wabunge mliulizwa hapa juu ya kuundwa kwa kamati za tanzaniate na almasi mkakubali ziundwe? “Ninavyojua mimi, ni mimi Spika ndiye niliyeona busara, nikaziunda mimi na nikasema zitakuwa kamati za ushauri kwa Serikali na nikasema watakapokuwa kazini, watafuata mambo haya na watakapokamilisha kazi zao, wataniletea ripoti zao. “Kwa hiyo, huyu Zitto naye lazima ahojiwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa sababu ameonekana kunituhumu mimi wakati kamati hazikuundwa na Bunge,” alisema Spika Ndugai. Pamoja na hayo, Spika alionekana kumshutumu Zitto kwa kutofika bungeni bila taarifa tangu Bunge lilipoanza Septemba 5, mwaka huu. Baada ya uamuzi huo wa Spika Ndugai, Zitto aliandika katika akaunti yake ya Twitter  ambapo alisema kuwa anamuheshimu lakini kiongozi huyo amekuwa haoni heshima ya Bunge ikiporomoka. “Anajua ninavyomheshimu (Ndugai). Kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushuhudia mbunge anapigwa risasi mkutano wa Bunge ukiendelea,” alisema Zitto.
3
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema chama hicho, kitaheshimu maamuzi ya wananchi, kitazingatia siasa safi na hakutakuwa na siasa chafu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Aliyasema hayo akiwa mkoani Kagera katika Salamu zake za Mwaka Mpya wa 2020 alipokutana na wenyeviti wa mitaa, waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana 2019.Alisema wenyeviti hao ni watu muhimu, ambao wanaweza kusimamia siasa safi kuanzia ngazi ya nchini hadi juu. Alisema siasa safi ndo kitu pekee, ambacho kinaweza kumfanya mwananchi kupiga kura kwa hiyari yake. Alisema takwimu zinaendelea kuonyesha kuwa tangu mwaka 2010, hamasa ya upigaji kura inaendelea kushuka, kutokana na siasa chafu, zilizotawala maeneo makubwa.“Napenda kusema kuwa hii ni mara ya kwanza kuzungumza tangu tumeuaga mwaka 2019. Salamu hizi zinaendana na kuimarisha Chama tunapoelekea uchaguzi mkuu. Hamasa ya kupiga kura inashuka kutokana na watu kupiga kura kabla hata uchaguzi. CCM inawahakikishia wananchi kuwa hakuna siasa chafu zitakazotawala katika uchaguzi mkuu,” alisema.Pia alisema chama hicho kitahakikisha kinazingatia haki za wanawake, kwa kuhakikisha wanapata viti vingi zaidi; na kuongoza bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Alifafanua kuwa mara nyingi inapofika uchaguzi, wanawake ndio wanachimbwa zaidi na kushutumiwa kwa mambo mengi, bila kujali huko nyuma wamepambana na mambo mangapi, ambayo yamesaidia kujenga nchi.Alisema sababu kubwa inayosababisha wanawake kutojitokeza ni baadhi ya wanasiasa, kusambaza sumu mbaya na kusababisha watu kujigawa makundi, hivyo kutoa nafasi kubwa ya kunyanyapaa wanawake na kuwadhalilisha.“CCM inapingana na udhalilishaji ambao mara nyingi unajitokeza katika uchaguzi mkuu. Wanawake kabla ya kugombea wanaitwa majembe, lakini wakichukua fomu za kugombea wanaanza kuchimbwa sana. Wanawekewa kashfa nyingi mpaka wanaogopa. Mwaka huu hatutakubali, maana tunataka wanawake wapate kura nyingi zaidi na viti vinavyotawaliwa na wanawake viongezeke, hii ni kwa sababu wanawake wana upendo mwingi zaidi kuliko mtu yeyote yule,” alisema.Akitoa ufafanuzi kuhusu mchakato wa kura za maoni, ambazo zitafanyika ndani ya chama kabla ya uchaguzi mkuu, alisema ni marufuku kwa wagombea uongozi ndani ya Chama, kufanya sherehe kabla ya kuteuliwa.Katibu Mkuu alisisitiza kuwa mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM ni mrefu na unasimamiwa kwa misingi mikubwa. Pia, alikemea baadhi ya watu walioanza kununua wapiga kura ndani ya CCM, kabla ya mchakato wa uteuzi haujaanza.Alisema muda wa kupitishapitisha bado haujafika. Vile vile, alikemea makundi yenye lengo la kugawa chama na kufanya siasa chafu. Alisema ni marufuku kufanya siasa za aina hiyo. Dk Bashiru alifanya ziara katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera katika kipindi hiki cha mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Alitembelea wilaya za Bukoba, Missenyi, Muleba na Biharamulo.
3
['Muogeleaji wa Italia Filippo Magnini amemuokoa Anrea Benedetto ambaye alikuwa akizama kwenye maji siku ya Jumapili.', 'Bingwa wa zamani wa michuano ya kuogelea alijitosa majini baada ya marafiki wa mwanaume huyo kuanza kupiga kelele katika ufukwe wa Cala Sinzias.', 'Magnini aliunyanyua uso wa Benedetto juu ya maji mpaka wahudumu waokoaji walipowasili.', "''Nilianya nilichotakiwa kufanya,'' mwanamichezo huyo mstaafu alisema.", 'Ni siku mbili pekee kabla, bwana Benedetto, 45, alikua amefunga ndoa na mpenzi wake wa jinsia moja.', 'Tukio hilo la Jumapili lilishuhudiwa na rafiki wa wapenzi hao na mwandishi wa habari wa eneo la uajemi, Soroush Paksad.', 'Wapenzi hao walikuwa wakielea wakiwa juu ya boya, kabla ya Benedetto kuangukia kwenye maji, yaliyokuwa yabaridi kuliko ilivyotarajiwa, hivyo hakuweza kusogeza miguu yake kutokana na hali ya kiafya. ', 'Kelele za marafiki zake kuomba msaada zilisikiwa na wafanyakazi waokoaji, ambao waliharakisha kwenda kumuokoa.', 'Lakini muogeleaji Magnini alikuwa karibu wakati huo hivyo aliharakisha na kumfikia Benedetto.', "'' Alikuwa akisumbuka sana: alikuwa akiogopa, pia alikunywa maji, ''Magnini alieleza.", ' Idadi ya vifo ajali ya boti DRC yafikia 45', "''Nilipomfikia hakuweza hata kuzungumza, na haikuwa rahisi kumnyanyua, hivyo tulimlaza kwenye boya la kitanda walilokuwa nalo waogaji wengine.", "''Nilipopata fahamu jambo la kwanza kulifikiria lilikuwa mume wangu,''alieleza.", "''Saa chache baada ya ajali nilikuwa hospitalini ndipo nilipogundua kuwa Filippo Magnini ndiye aliyemuokoa lakini sikupata muda wa kumshukuru kwa kuwa sikuwa na mawasiliano.Nina matumaini nitaweza kumshukuru mimi binafsi.''", 'Magnini alikuwa ufukweni na mpenziwe Giorgia Palmas, mwanamitindo na mtangazaji wa televisheni.', 'Magnini aliwahi kushinda medali ya shaba mwaka 2004 aliposhiriki michuano ya kuogelea kwa mitindo huru, michuano ya Olimpiki mjini Athens.', 'Pia alikuwa mshindi wa dunia mita 100 mitindo huru mwaka 2005, na kulitetea taji lake mwaka 2007.', 'Utajuaje kuwa mtu anataka kuzama']
4
KOCHA wa Simba SC Patrick Aussems amezipata mbinu za wapinzani wake AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kuwamaliza mapema katika mchezo dhidi yao utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii.Wekundu hao baada ya kupata pointi tatu katika mchezo wa kwanza dhidi ya JS Saoura ya Algeria, hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, wanatarajia kucheza mchezo dhidi ya timu hiyo ya DR Kongo Jumamosi.Simba ilishinda 3-0 Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.“Kocha amekuwa akitizama mikanda mbalimbali ya video ya michezo ya AS Vita, amekuwa akiwafuatilia hata katika mchezo dhidi ya Al Ahly aliwatizama kujua mbinu zao, na kujipanga vizuri kwa mchezo ujao,”amesema Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori.Magori amesema wakati Aussems anajipanga kimbinu, viongozi wanajiandaa kimkakati kwa kuhakikisha wanakuwa vizuri ndani na nje ya uwanja katika mchezo huo wa ugenini.“Tunajipanga kwenda Kinshansa tukijua wazi aina ya timu tunayokwenda kukutana nayo ni ngumu, ilifika fainali Kombe la Shirikisho Afrika, kwa hiyo mechi yetu haitakuwa rahisi ni lazima kujipanga kimkakati ndani na nje ya uwanja,” alisema.Wekundu hao wa Msimbazi wanatarajiwa kuwafuata AS Vita Alhamisi ya wiki hii tayari kwa mchezo huo.Katika Kundi D, Simba ndiye kinara kwa pointi tatu na mabao matatu iliyopata dhidi ya JS Saoura katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.Anayefuatia ni Al Ahly iliyopata ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya AS Vita wa mabao 2-0. Ikifuatiwa na AS Vita na Saoura, ambazo hazina pointi baada ya kupoteza michezo yao iliyopita.Mchezo ujao huenda ukawa mgumu hasa kwa Simba, kwani inakwenda kukutana na Vita ambayo haina pointi na itahitaji matokeo mazuri nyumbani kwake kujiweka katika nafasi nzuri.
4
Yanga imefuzu hatua ya makundi ya Kombe la CAF, baada ya kuwatoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1.Akizungumza na gazeti hili, Mayanja alisema Yanga hawapaswi kufurahia kutinga hatua hiyo kwa sababu bado wana kazi kubwa ya kufanya na ni vyema wangekitumia kipindi hiki kurekebisha upungufu waliokuwa nao ili waweze kuwa imara zaidi.“Nawapongeza kwa juhudi ambazo wamezionesha, lakini ninachofahamu bado wana kazi kubwa, naifahamu vizuri michuano hii imekuwa na visa vingi na uonevu, lakini kwa timu zinazocheza nyumbani. Dawa yake pekee ni kujenga timu imara ambayo itaweza kukabiliana na kila hali,” alisema Mayanja.Mayanja alimtaka kocha wa Yanga, Hans Pluijm, kuwaongezea mbinu za kimchezo wachezaji wake ili kubadilika wanapokutana na ugumu katika baadhi ya michezo yao watakayokutana nayo.Alisema ameiona Yanga ikicheza vizuri kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly, na kuwataka kuboresha baadhi ya vitu ikiwemo uelewano wa safu ya kiungo na ushambuliaji ili waweze kulinda mpira na kuzitumia vizuri nafasi wanazozipata.Mayanja alisema endapo Yanga watazingatia hayo wanaweza kufika mbali kwa sababu wana kikosi kizuri chenye wachezaji wenye uwezo wa kupambana bila kuogopa ukubwa wa timu wanayokutana nayo.
4
  NA JIMMY CHIKA YALIKUWA ni matukio makubwa ya kimuziki mwaka 1984, ukiacha kadhia mbaya kwa Watanzania ile ya kumpoteza aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine. Tunazidi kumuombea, apate mapumziko mema peponi, Amina. Tunairejea mada ambayo Kijaruba leo kimeikuta katikati ya akiba zake zinazoletwa kwenu kupitia ukurasa huu kila siku ya Jumamosi. Kwa taarifa tu, ni kwamba ndani ya Kijaruba kuna hazina kubwa isiyokauka, iliyohifadhi mambo mengi yaliyokuwa yakitokea enzi hizo, ambazo pengine ni muhimu kwa wahenga kuzikumbuka na wale ambao miaka hiyo walikuwa bado hawajakanyaga ardhi hii ya Jalali, basi wapate faida ya kujua mambo hayo. Leo tunayakumbuka matukio mawili ya kimuziki yaliyojiri mwaka 1984 na kuitikisa familia ya tasnia hiyo kiasi cha kuibakisha historia hiyo katika vichwa vya watu mbalimbali. Kwanza ulishuhudiwa mpasuko wa bendi kubwa mbili, Mlimani Park na Vijana Jazz ambao wanamuziki wake tegemeo walichukuliwa na bendi moja ambayo kabla ya tukio hilo halikuwemo kwenye orodha ya bendi zenye tabia ya kupora wanamuziki wa bendi nyingine. Tumeikumbuka Bima Lee ambayo kabla ya mwaka huo ilikuwa na staili za muziki wake ukiwapa nafasi kubwa waimbaji mahiri Roy Bashekanako, Jumbe Batamwanya, Belesa Kakere na Kassim Bosanga. Walifanikiwa kuwateka mashabiki wake vilivyo hasa zile tungo za awali zilizoandaliwa muda mfupi baada ya kuanzishwa bendi hiyo mwaka 1970. Ilikuwa kazi nzuri ya mpuliza saxafoni, Comson Mkomwa kuachia vibao kama Rafiki karibu ya nyumbani na vingine vingi ambavyo leo siyo mada yake kuvichambua sana. Tukio kubwa ni pale ilipodhihirika kwamba wanamuziki mashuhuri Tanzania, Joseph Mulenga, Abdalah Gama na Suleyman Mwanyiro ni kweli wamekimbia katika bendi waliyoanzisha mwaka 1978 Orchestra Mlimani Park na kwenda Bima Lee. Haikuwaingia akilini mashabiki wa muziki kwani umaarufu wa wanamuziki hao kwenda Bima ilionekana kama vile wanakwenda kushusha hadhi yao hasa ikizingatiwa enzi hizo umaarufu wao ulikuwa unamithilika na hawa vijana wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya. Lakini ilikuwa hivyo kwani haikuchukua muda wakali hao wa magitaa walipokea vichwa vingine vya waimbaji waliong’olewa Vijana Jazz, Othman Momba na Jerrys Nashon na kisha viongozi wa Bima wakarudia tena pale Mlimani Park na kumng’oa Shaaban Dede na kuimarisha kikosi chao. Kwa nini matukio hayo yanafananishwa na leo? Katika Ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam, leo kutakuwa na mpambano wa wanamuziki, ambapo bendi kongwe ya Msondo Ngoma iliyoasisiwa tangu mwaka 1964 itavaana na magwiji wa muziki wa dansi. Kabla ya tukio hilo Watanzania walizoea kusikia bendi za Msondo na Sikinde zikiumana, lakini safari hii watayarishaji wamaunda timu ya Taifa ya Muziki wa dansi na kisha kuipambanisha na Msondo. Kama ulitamani kuona ilivyowahi kutokea siku hizo, basi unaweza kupata nafasi hiyo adimu ambayo itaweza kukuonyesha ilivyokuwa au itakupa ufahamu wa jinsi ulivyokuwa ushindani wa muziki wa dansi. Unadhani ni bei mbaya basi? Tsh. 10,000 inatosha au 20,000 kwa VIP. Unakosaje kwa mfano? Uje na washikaji zako.
1
Na CLARA MATIMO – MWANZA WASICHANA 300 wanaoishi Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, ambao walikatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali, wanatarajia kupatiwa mafunzo yatakayowawezesha kufikia malengo yao. Mafunzo hayo yatatolewa na Shirika lisilo la Serikali la Mikono Yetu linalojishughulisha kuwawezesha wanawake na wasichana kumiliki rasilimali zalishi  ili waweze kujikwamua kiuchumi, ikiwemo ardhi na mifugo kupitia mradi wa Msichana ni Tai kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Novo Foundation la nchini Marekani. Akizungumza jijini hapa  hivi karibuni  katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo  kwa viongozi wa Kata ya Buswelu iliyopo wilayani humo,  Meneja Programu wa Shirika la Mikono Yetu, Sophia Nshushi, alisema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wasichana ambao hawakuhitimu masomo yao kutimiza ndoto zao kwa kuwapatia mafunzo yatakayowawezesha kujikwamua kiuchumi. “Mikono Yetu tunaamini hata wasichana walio nje ya shule wana ndoto ambazo walishindwa kuzitimiza wakati wanasoma, wapo ambao walipata ujauzito na wengine maradhi mbalimbali, hivyo wakashindwa kuendelea na masomo, kupitia mradi wa Msichana ni Tai  watainuka tena na kuendelea na harakati za kutimiza ndoto zao.  “Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius  Nyerere aliamini katika nguvu ya mwanamke akasema  “mwanamke ni tai sio kuku, anaweza kutumia mbawa zake akaruka na akafikia malengo yake”, ndiyo maana Mikono Yetu tukaona tulete mradi huu ili tuwape nafasi wasichana walioshindwa kutimiza ndoto zao,” alisema Sophia. Ofisa mradi huo, Halima Juma, alisema wanufaika ni wasichana kuanzia miaka tisa hadi 17,  watafundishwa mbinu mbalimbali za ujasiriamali, afya ya uzazi, haki na wajibu wa msichana pamoja na jinsi ya kujiamini ili waweze kufikia ndoto zao, hivyo kuepuka kuwa tegemezi pamoja na vitendo vya ukatili. “Mradi huu ni wa miaka mitatu, tutaanza kuutekeleza Agosti mwaka huu hadi mwaka 2023  katika Kata ya Buswelu iliyopo Wilaya ya Ilemela,  tutawafikia wasichana 300 pamoja na wazazi ama walezi wao 300, hivyo  tutakuwa na jumla ya wanufaika 600, tumeamua kushirikiana na wazazi ama walezi ili tupate matokeo chanya,” alisema Halima. Ofisa Mtendaji wa Kata ya Buswelu, Nhikilo Joseph, aliwataka wazazi na walezi wa wasichana ambao watanufaika na mradi huo kushirikiana na Shirika la Mikono Yetu bega kwa bega  katika kuutekeleza mradi huo kwa sababu  unafufua matumaini kwa wasichana.
3
KIPA Klaus Kindoki ameipeleka Yanga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Alliance kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) uliochezwa jana.Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza, timu hizo zilicheza dakika 90 na kutoka sare ya bao 1-1. Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la uongozi dakika ya 38 lililofungwa na Heritier Makambo kwa shuti kali baada ya kupata pasi ya Pius Buswita kisha Alliance ikasawazisha dakika ya 62 kupitia kwa Joseph James kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Godlove Mdumule. Kindoki aliibuka shujaa baada ya kupangua mikwaju miwili ya penalti kati ya mitano iliyopigwa na Alliance.Waliokosa penalti kwa upande wa Alliance ni Martin Kigi mpira uligonga mwamba huku mipira ya Dickson Ambundo na Siraji Juma ikipanguliwa na kipa huyo. Wengine waliopata kwa upande wa wenyeji hao ni Joseph James, Geofrey Luseke na Sameer Vicent. Kwa upande wa Yanga beki Kelvin Yondani na Mrisho Ngassa walikosa penalti hizo huku Thaban Kamusoko, Haruna Moshi ‘Boban’, Paul Godfrey na Deus Kaseke wakipata. Kwa ushindi huo Yanga inaungana na Azam FC, KMC na Lipuli kutinga hatua hiyo ya nusu fainali.Katika mchezo wa nusu fainali Yanga itakuwa tena ugenini dhidi ya Lipuli mwezi ujao. Yanga: Kindoki, Paul Godfrey, Gustapha Simon, Said Juma, Yondani, Feisali Salum/Kamusoko dk.78, Ngassa, Papy Tshishimbi, Makambo, Buswita/Kaseke dk.78 na Amis Tambwe/Boban dk.61. Alliance: John Mwanda, Godlove Mdumule, Siraji Juma, Wema Sadoki, Geofrey Luseke, Joseph James, Michael Chinedu/Sameer Vicent dk. d8, Paul Maona/ Hussein Javu dk.56, Bigirimana Blaise/Martin Kigi dk.90, Mapinduzi Balama na Dikson Ambundo.
4
Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemwachia huru Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Theophillo Bwekea, baada ya Jamhuri kuonyesha haina nia ya kuendelea na kesi hiyo. Bwekea alikuwa akituhumiwa kupokea rushwa ya Sh milioni 161.7 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira. Wakili wa Serikali, Odossa Olombe, alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respiciou Mwijage kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Hivyo aliomba kuondoa kesi hiyo chini ya kifungu cha sheria namba 98(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) aya ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hakimu Mwijage aliyakubali maombi ya upande wa Jamhuri na kuamuru mshtakiwa kuachiwa huru chini ya kifungu cha sheria namba 98(a) cha CPA. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka Januari 20, 2015. Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai, awali akisoma mashtaka alidai kuwa mshtakiwa anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh 161,700,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira, ambazo ni sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow. Kabla ya kufanya kazi REA, Theophillo alikuwa Wizara ya Nishati na Madini, kitengo cha kusimamia umeme, ambako anadaiwa alishiriki kutunga sera ya kampuni binafsi kuuza umeme Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na ilipoanza kutumika, Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ilikuwa ya kwanza kupata zabuni. Wakili Swai, alidai Februari 12, 2014 katika Benki ya Mkombozi, mshtakiwa akiwa Mhandisi Mkuu wa REA, kwa rushwa alijipatia Sh milioni 161.7 kupitia akaunti namba 00410102643901 fedha ambazo ni sehemu ya zilizokuwapo katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Alidai fedha hizo aliingiziwa katika akaunti yake na Rugemalira ambaye ni mshauri binafsi wa kimataifa, Mkurugenzi wa VIP Engineering na alikuwa Mkurugenzi wa IPTL. Fedha hizo zinadaiwa alipewa zawadi kwa kuwa alikuwa mmoja wa wajumbe walioandaa sera zilizoruhusu sekta binafsi kuuza umeme Tanesco. Mshtakiwa huyo alikuwa nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Serikali ama kutoka taasisi inayotambulika waliotakiwa kuwa na barua za utambulisho na kila mmoja kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 25.
3
Na Ashura Kazinja -Morogoro MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata ole Sanare ameagiza Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Charles Komba asimamishwe kazi mara moja kutokana na utoro kazini na kutohudhuria kikao cha Baraza la Madiwani kilichotakiwa kufanyika Mei 26, mwaka huu. Sanare alitoa agizo hilo mwanzoni mwa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kilicholenga kujadili taarifa na majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, jana. Akiendesha kikao hicho, Sanare alitaka kujiridhisha iwapo wakuu wa idara wote na vitengo wameshiriki kama ilivyokuwa imeelekezwa siku chache kabla ya kikao hicho, ndipo alibaini kutokuwepo ofisa huyo. Alisema kibali alichokuwa ameomba kusafiri tangu siku ya kikao hicho, kilikuwa hakijapitishwa na mkurugenzi wa halmashauri, huku akiwa hayupo kazini. Alipoulizwa mkuu wake wa Idara ya Uhasibu kuhusu kutokuwepo kwake kazini, alikiri mtumishi huyo aliomba ruhusa, hakuruhusiwa na alitaarifiwa asiondoke. Sanare alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Rehema Bwasi kumsimamisha kazi mara moja, huku akimtaka pia kusimamisha mshahara wake hadi pale suala lake litakapopatiwa ufumbuzi. “Yaani nikitoka sasa hivi hapa uwe umemwandikia barua ya kumsimamisha kazi huko huko alipo kwa utoro wake, usimlipe mpaka jambo lake litakapopatiwa utatuzi,” alisema Sanare.
3
Katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi jana, mkulima huyo alisema ni wakati wa Watanzania kubadilika na kufanya biashara ya asali kimataifa kutokana na wanunuzi kutoka nje ya nchi kuongezeka.Alisema amekuwa akiwapata wateja wa asali kupitia kwenye mitandao ya intaneti. “Huwa natafuta wateja kwenye mtandao ambapo wanunuzi wa asali wakijitokeza nakubaliana nao ninatuma ‘sample’ (sampuli) na hawa waliporidhika wakanilipa kwa dola, ambapo bei ya tani moja ni Sh milioni 10 baadaye wawakilishi wao wakafuata mzigo,” alisema.Alisema asali aliyovuna mwaka huu aliuza tani mbili Uingereza na tani nyingine mbili aliuza Uarabuni. Alisema asali nyingine amekuwa akiuza rejareja na amekuwa na wateja wengi jambo ambalo limekuwa likimhamasisha aendelee kufuga na kutoa elimu ya wafugaji kwa watu wengine.Mkulima huyo alisema ni vizuri hata wasomi wakabadilika kifikra na kujiajiri na si kusubiri kuajiriwa kwani mikoa mingi imekuwa na fursa nyingi.“Wengi wanasoma ili kufaulu na elimu iwasaidie katika kupata ajira, na hawafikirii kusoma ili elimu hiyo iwasaidie katika kujiajiri, kuna fursa kubwa zaidi katika kujiajiri unaweza kujiajiri na kupata fedha nyingi zaidi ambazo ni sawa na kiinua mgongo cha mfanyakazi aliyefanya kazi miaka mingi,” alisema.Alisema ufugaji nyuki ni mzuri kwani hauna palizi kama ilivyo kwenye kilimo, hauhitaji dawa ya kumwagilia ni kutundika mizinga na kusubiri kwenda kuvuna asali.Rubi alisema alianza kufuga mwaka 2007 kwa kutumia vyungu kutokana na kukosa uwezo wa kununua mizinga ya kufugia nyuki.Alisema alianza kwa mtaji wa Sh 75,000 ambapo alinunua vyungu 50 vyenye ujazo wa debe moja na nusu kila moja na baada ya kuvuna asali alipata fedha ambazo zilimuwezesha kununua mizinga 70 ya kienyeji ambapo kila mzinga alinunua kwa Sh 5,000.“Katika mavuno ya mwaka 2008 hadi 2009 baada ya kuvuna kwenye mizinga 70 nilipata zaidi ya Sh milioni 7.5,” alisema.alifanya juhudi za kuongeza mizinga mingine na kutafuta eneo kwa ajili ya kuendesha ufugaji ambapo mpaka sasa ana mizinga 1000 ambapo kati ya hiyo 700 ni ya kisasa na 300 ni ya kienyeji. Mkulima huyo ana elimu ya kidato cha nne aliyoipata shule ya Wavulama ya Tabora.
5
NAIBU Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya amewataka wakazi wa mkoa wa Singida kukuza zaidi kilimo cha alizeti ili kuweza kuinua uzalishaji wa mafuta yake, kuboresha maisha ya watu wake na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.Alitoa mwito huo katika kijiji cha Mtinko, Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati wa ziara yake kuhamasisha uzalishaji mafuta ya kula ambapo alitembelea Kongano la Alizeti katika tarafa hiyo kujionea jitahida za Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na wadau wake katika kuhamasisha uanzishwaji viwanda mkoani humu.Alisema kuwa wakati Tanzania imelenga kufikia uchumi wa kati utakaotegemea zaidi viwanda ifikapo 2025, lengo hilo haliwezi kufikiwa iwapo juhudi za maksudi hazitafanyika kuanzisha na kudumisha viwanda vyetu, hasa katika sekta ya kilimo ambapo maisha ya wananchi wengi yanayetegemea.Hata hivyo, alisema kuwa viwanda hivyo vitaweza kudumu tu iwapo wakulima nao wataboresha kilimo chao na kuzalisha kwa wingi zao la alizeti ili kulisha viwanda vilivyopo na hivyo kuleta fursa ya ajira kwa wananchi, hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.Alisema kuwa serikali kwa makusudi imeongeza kodi kwa mafuta yanayotoka nje ili mafuta ya ndani yaweze kupata soko, hivyo ni juu ya Wananchi kutumia vyema fursa hiyo na zaidi ya yote kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazozalishwa humu nchini.Naibu Waziri huyo alisema kuwa kwa hivi sasa kuna upungufu wa tani 600,000 za mafuta ya kula nchini, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa wakulima kujizatiti na hakikisha pengo la upungufu huo linazibwa haraka iwezekanavyo kwa kuongeza tija katika kilimo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji alisema ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda, Shirika lake limekuwa likianzisha na kuendeleza Viwanda vidogo na vya kati, kuhudumia uendelezwaji teknolojia, kutoa Mafunzo ya biashara, huduma za masoko na fedha.Kwa mujibu wa Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida, Shoma Kibende kuna jumla ya viwanda 1,305 mkoani Singida, kati yake kikubwa ni kimoja, vya kati Saba, vidogo 276 na vidogo sana ni 1,021.
3
SERIKALI imeelezea mafanikio makubwa iliyopata katika sekta ya afya hasa kuimarisha usimamizi katika upatikanaji wa huduma za kibingwa za afya huduma.Aidha, katika hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana, Ummy Mwalimu serikali imesema kumekuwa na maendeleo chanya katika huduma za kinga.Waziri Mwalimu amesema kutokana na kuimarishwa kwa huduma za kibingwa za kibobezi zinazotolewa katika hospitali ya Taifa na hospitali maalumu idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje wamezidi kupungua.Amesema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019 hospitali za rufaa za kanda na Taifa ziliwasilisha wizarani idadi ya wagonjwa 62 waliokuwa na mahitaji ya kupatiwa matibabu nje ya nchi, ikilinganishwa na wagonjwa 114 katika kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018.Aliyataja magonjwa yaliyoongoza ni pamoja na saratani wagonjwa wa moyo, mifupa, mishipa ya fahamu, mishipa ya damu, figo na magonjwa mengine.Aidha alisema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019 wizara kupitia hospitali za kitaifa, kanda na hospitali maalumu imehudumia jumla ya wagonjwa milioni 1.4 huku wagonjwa wa nje wakiwa milioni 1.1 na wa kulazwa wakiwa 247,979. Katika hospitali zote, hospitali ya Muhimbili iliona wagonjwa 419,931 badala ya wagonjwa 300,000 waliokadiriwa awali.Aidha, kuna wagonjwa milioni 3.3 waliohudumiwa na hospitali za rufaa za mikoa kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019.Ongezeko la wagonjwa katika ngazi zote limetokana na kuboreshwa kwa miundombinu na kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali hasa za upasuaji ukiwemo mkubwa na wa dharura, upandikizaji wa figo na upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto.Katika hospitali za rufaa kuna upasuaji aina 13 unaofanyika. Pia taasisi kama ya MOI imefanikiwa kuanza kwa mara ya kwanza upasuaji wa vivimbe vya damu kwenye ubongo, baada ya kununua kifaa cha kisasa cha kufanyia upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo.Akizungumzia mafanikio katika ugonjwa wa saratani, Waziri Ummy aliwataka wabunge kuwahimiza wananchi kupima saratani angalau mara moja kwa mwaka na kwamba saratani ikiwahiwa inatibika.Waziri Ummy pia alisema hali ya upatikanaji wa dawa za wagonjwa wa akili imeimarishwa na kufikia asilimia 100 katika hospitali ya Mirembe na Isanga.Aidha hospitali ya Mirembe imeendelea kutoa huduma za kibingwa za saikolojia, mishipa ya fahamu na ubongo.Amesema taifa likiwa na vituo vya kutolea huduma za afya 8,119 kutoka vituo 7,678 vilivyokuwapo mwaka 2018, serikali imekuwa ikiimarisha upatikanaji wa dawa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi
3
Mwandishi wetu-Dodoma WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amepiga marufuku operesheni za polisi kukamata wananchi, bodaboda bila kutoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya. Simbachawene alisema hayo jana wakati akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na baadaye kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya. Alisema ukamataji usio na mpangilio hauna tija na unaweza kuvunja amani badala ya kujenga amani. “Wananchi wanawalalamikia askari wetu sana kukamata bodaboda bila sababu, sio bodaboda tu hata kukamata kamata hovyo watu, ukamataji mwingine unakua kama kukomoana, hauna tija, hauleti amani, badala yake unasababisha amani itoweke.  “Yaani msako fulani unatungwa hauna kichwa wala miguu, hauna maelekezo yoyote ya Mkuu wa Jeshi la Polisi au chombo, ni watu tu wanajitungia wanaondoka na pikipiki yao wamepakiana wanaenda kufanya operesheni ambayo haina utaratibu,” alisema Simbachawene. Alisema vyombo vya ulinzi na usalama ni vya wananchi, na operesheni yoyote haipaswi kufanyika bila mkuu wa wilaya kupewa taarifa ambapo ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo. Pia Simbachawene aliupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuifanya wilaya hiyo kuendelea kuwa na amani na utulivu na wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi hao. “Endeleeni kuwa karibu na wananchi, kwa kusikiliza kero zao na pia kuzitatua, epukeni malalamiko ya hapa na pale yasiyokuwa ya lazima,” alisema Simbachawene. Simbachawene aliewaomba viongozi wa wilaya hiyo kujipanga vizuri katika maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. “Mwaka huu ni wa uchaguzi, wananchi kupitia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na taasisi zote za utawala, mnapaswa kuwa na ushirikiano mkubwa ili kujenga msingi wa uchaguzi utakaokuwa wa amani na utulivu,” alisema Simbachawene. Alisema mwaka wa uchaguzi haupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao unapaswa kuwa na utulivu kwasababu ni jambo zuri la kidemokrasia linafanyika. “Rai yangu kwa wananchi, tunapaswa kujenga utulivu kuanzia sasa kuelekea uchaguzi mkuu, hatupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao amani na utulivu wa nchi unajengwa kuanzia sasa, mshikamano wa vyombo vyetu ndio msingi wa kujenga uchaguzi utakao kuwa wa huru na haki ambao utafanya mwaka huu,” alisema Simbachawene.   Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jabir Shekimweri, alimshukuru waziri huyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yake. Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa (OCD), Maulidi Manu, alisema ujio wa waziri huyo umewasaidia zaidi kwa kujipanga zaidi, na kufuata maagizo yote aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi wilayani humo.
3
DIWANI wa Kata ya Kilimani Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Neema Mwaluko (CCM) amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya kata kwa kipindi cha miaka minne.Amesema ameweza kushughulikia tatizo la ardhi katika eneo la Chinyoyo, lililodumu kwa miaka 20. Kata ya Kilimani ambayo ni miongoni mwa kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ina mitaa minne na jumla ya wakazi 6,831. “Nimeshughulikia tatizo la ardhi kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, nimefanikiwa kutatua kero kubwa ya upimaji wa mtaa wa Chinyoyo iliyodumu takribani miaka 20, sasa mtaa umeshapimwa kwa njia ya maboresho kila mtu atabaki pale alipojenga tupo katika hatua ya mwisho ya maboresho kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa Jiji,” alisema. Pia, alisema katika uwezeshaji wananchi kiuchumi, amehamasisha na kutoa elimu ya namna bora ya kukuza biashara na kuziboresha, uundaji wa vikundi na jinsi ya upatikanaji wa mikopo inayotolewa na halmashauri. Alisema katika kipindi cha miaka minne, vikundi 43 viliundwa na kukaguliwa na kupatiwa usajili. Alisema vikundi 18 vilipatiwa mikopo ya halmashauri ya Sh 65,129,500. Alisema wamefanikiwa kutenga eneo la kujenga soko mtaa wa Chinyoyo, lenye ukubwa wa mita za mraba 5,518.Kwamba soko hilo litafanya mzunguko wa fedha kuwa mkubwa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali. Alisema kata hiyo ni miongoni mwa kata zinazopokea huduma ya kunusuru kaya maskini chini ya TASAF. Kuna jumla ya walengwa 113 na fedha walizopatiwa mpaka sasa ni Sh ilioni 89.4. Alisema mtaa wa Chinyoyo una walengwa 80, mtaa wa Nyerere walengwa 11, Imagi walengwa 11 na Kilimani walengwa 11.“Kupitia mradi wa Tasaf tumefanikiwa kuwapatia walengwa elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya uundaji wa vikundi vya uzalishaji mali ambapo hadi sasa vimekwishaundwa vikundi vine na vimesajiliwa.
3
Mkopo huo unalenga kuwezesha waendesha bodaboda wa Dar es Salaam kukua, kuinuka kimtaji na kumiliki bodaboda zao kwa kuwa wengi si za kwao bali wameajiriwa.Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa alisema hayo baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya kudhamini NSSF kutoa mikopo kwa Dabosa itoe mikopo kwa wanachama wake.“Fedha hizo za kudhamini mikopo hii zitawekwa kwenye akaunti ya mfuko huo,” alisema na kuongeza kuwa watatoa mkopo kwa riba ya asilimia 9.32 na Dabosa itatoza kwa wanachama wake kwa asilimia 12.3.Alifafanua zaidi, Issa alisema mpango huo ni wa kitaifa wenye lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi, hivyo watashirikiana na mfuko huo kuwapatia mafunzo ya utawala bora, kuweka akiba na ujasiriamali. “Mafunzo yameshaanza kutolewa Dar es Salaam na yataendelea kufanyika pia katika mikoa mingine nchini,” alisisitiza.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema mikopo hiyo ni njia ya kuwezesha vijana kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili.“Mfuko umejiweka tayari kutoa mikopo hii, lakini jambo la msingi ni kwa vijana waweze kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu katika biashara zao ili waweze kurejesha mikopo,” alisema Dk Dau.Mkurugenzi huyo mkuu aliwaelezea waendesha bodaboda kuwa mfuko unatoa huduma za jamii zikiwemo za mafao ya ajali na mafao ya afya, hivyo wanaweza kujiunga na kunufaika nayo wakati wanaendelea na shughuli zao.Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji, Omari Issa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), alisema programu ya kuwezesha bodaboda ni moja ya mambo yaliyomo katika BRN.“Baraza limeondokana na mfumo wa zamani wa kutoa mikopo kwa wananchi moja kwa moja na sasa inadhamini taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wananchi,” alisema.Alisema wanafanya hivyo na Benki ya Posta, TIB, NSSF na watashirikiana na taasisi nyingine ili kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mwenyekiti wa Dabosa, Said Kagomba alisema chama chao ni cha vijana wa jiji la Dar es Salaam kina wanachama 439. Kinondoni wako wanachama 135, Ilala ni 163 na Temeke ni 141.“Lengo ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya maisha yetu” na mpaka sasa wamekusanya kiasi cha Sh milioni 24.7,”alisema Kagomba.
5
HATUA ya Marekani kufungia kampuni ya Huawei kushirikiana na kampuni zake imeshutumiwa kwamba itaathiri mabilioni ya wateja. Aidha, kampuni hiyo inaendelea na mchakato wa kufungua mashitaka dhidi ya serikali ya Marekani kutokana na hatua ya kuizuia.Akizungumza na waandishi wa habari, mwanasheria wa kampuni hiyo ya Huawei, Song Liuping alisema zuio hilo la biashara pia litaleta madhara kwa kampuni za Marekani na wakati huohuo kuathiri ajira. Hivi karibuni Marekani ili- iweka Huawei kwenye orodha ya kampuni ambazo kampuni za Marekani haziwezi kufanya nazo biashara isipokuwa ziwe na leseni.Huawei ambayo ni kampuni ya China ni kinara wa dunia wa utengenezaji wa vifaa vya mawasiliano. Kwa mujibu wa Marekani, zuio hilo limezinga- tia usalama wa taifa. Kampuni hiyo imekuwa ikikanusha madai ya kutumia bidhaa zake kuhatarisha usalama, huku ikisisitiza kuwa haiko chini ya serikali ya China.Song alisema uamuzi huu unatishia na kuathiri wateja katika nchi zaidi ya 170 wakiwamo zaidi ya wateja bilioni tatu wanaotumia bidhaa na huduma za Huawei duniani. “Kwa kuzuia kampuni za Marekani kufanya biashara na Huawei, moja kwa moja serikali itaathiri zaidi ya kampuni 1,200 za Marekani. Hii itaathiri pia maelfu ya ajira za Wamarekani,” alisema.Kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Marekani kuiorodhesha Huawei katika kampuni ambazo ni marufuku kwa kampuni zake kushirikiana nayo isipokuwa kwa kibali, kampuni ya Google ilipiga marufuku Huawei kutumia baadhi ya huduma kutoka mfumo wa uimarishaji kazi ya simu, Android.Kutokana na marufuku hiyo, aina mpya za simu za Huawei hazitaweza kutumia baadhi ya programu kutoka Google apps. Huawei ambayo ni kampuni ya pili kubwa duniani, imesema itaendelea kutoa mfumo wa kuimarisha matumizi ya simu zake na huduma za baada ya mauzo ya bidhaa zote za simu ambazo zimeshauzwa na zinazosubiri kuuzwa duniani. Mvutano huu umetajwa kuwa utakuwa na athari kwa wateja wa bidhaa za Huawei hususani Afrika.
2
Janeth Mushi, Arusha Katika kukabiliana na kupambana na maambukizi ya virusi vya corona nchini, Kanisa la Anglikana Tanzania, limejipanga kupunguza msongamano wa waumini kwa kuongeza idadi ya ibada zake. Hayo yamesemwa leo Alhamisi Machi 19, jijini Arusha na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania, Dk. Maimbo Mndolwa ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha maaskofu wake 28 kutoka Dayosisi zote zilizopo Tanzania Bara na Visiwani. “Moja ya tahadhari tunazochukua ni pamoja na kupunguza idadi ya watu katika ibada kwa kuongeza ibada kama vile; mahali penye ibada moja sasa kutakuwa na ibada mbili,” amesema. Kikao hicho mbali na ajenda hiyo kimejadili kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo nchini tangu mwaka 1970 yanayotarajiwa kufanyika makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo mkoani Dodoma Septemba mwaka huu. “Kutokana na hali hiyo, tumeelekeza kila Dayosisi itenge siku maalumu ya maombi kuanzia leo Machi 19 na Ibada ya Ijumaa Kuu, itakuwa siku ya ibada ya pamoja ya Kanisa Anglikana Tanzania kuombea Taifa letu dhidi ya virusi hivyo vya corona,” amesema.
0
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba Leo watakuwa na kibarua kigumu ugenini cha kusaka pointi tatu muhimu wakati watakapowakabili wababe wao, Kagera Sugar katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini hapa. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote kutokana na viwango bora vya timu hizo baada ya kila moja kushinda michezo yao yote iliyopita na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 20. Kagera hadi sasa ndio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zake zote tatu ilizocheza ugenini hadi sasa ilipozifunga Biashara United, Alliance FC, na Mbao FC wakati Simba nayo ikishinda mechi zake mbili Mbele ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar na kuwafanya kuwa na pointi sita.Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema jana kuwa katika kipindi cha wiki mbili alikuwa akikinoa kikosi chake ili kuhakikisha kinaondoka na pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na kurejesha heshima mbele ya wapenzi wa soka.Alisema pamoja na kuwakosa wachezaji wake, Michael Gadiel Mbaga pamoja na kiungo wa juu, Clatous Chama katika kikosi cha wachezaji 22, wanatarajia matokeo chanya katika mchezo huo.Nyota 22 waliotarajia kuondoka jana asubuhi kwenda Bukoba ni pamoja na Aishi Manula, Beno Kakolanya, Pascal Wawa, Tarone Santos, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Mzamiru Yassin, Francis Kahata, Sharaf Shiboub na Hassan Dilunga.Wengine ni Meddie Kagere, Kennedy Juma, Yusuph Mlipili, Haruna Shamte, Rashid Juma, Said Ndemla, Jonas Mkude, Miraj Athuman, Deo Kanda, Ibrahim Ajib, Wilker Da Silva na Erasto Nyoni.Kwa upande wake, kocha wa Kagera, Macky Mexime alisema maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba yamepewa kipaumbele kama michezo mingine ya ligi hiyo waliyokwishacheza, huku Serikali ya mkoa wa Kagera ikiwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kuishanglia timu yao ikicheza dhidi ya Simba.Mexime alisema pamoja na Simba kupania kupata ushindi timu yake haiwezi kukubali kirahisi kupoteza mchezo huo wa kwanza nyumbani, baada ya kuanza kwa ushindi ugenini kwa kushinda mechi zote tatu.
4
WATU watano, wakiwamo wazazi wawili wa maharusi na bibi harusi mtarajiwa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Igokero wilayani Misungwi, Mwanza (jina kapuni) aliyekuwa anaolewa, wamekamatwa wakati wakisherehekea harusi ya kimila ya kuoza watoto wao.Tukio hilo lilitokea jana saa tisa mchana katika Kitongoji cha Nera pale watuhumiwa hao walipotiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Misungwi, ambapo sherehe ilikuwa ikiendelea nyumbani kwa mzee Mathayo Lugheto ambaye kijana wake, Masalu Mathayo alikuwa akimuoa mwanafunzi huyo. Kutokana na tukio hilo, taharuki kubwa ilitokea, ambapo sherehe iligeuka kuwa chungu hasa baada ya wazazi hao wa familia za pande mbili kutiwa mbaroni pamoja na ng’ombe watano wa mahari.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Igokero, Lucas Bukundi alisema kuwa alipata taarifa za kuozwa kwa mwanafunzi huyo kutoka kwa raia mwema. Alisema baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na uongozi wa shule hiyo ili kuthibitisha kuwa binti aliyekuwa anaolewa ni mwanafunzi, ambapo alithibitishiwa na mkuu wa shule hiyo, Amisa Mwalikumba kuwa ni kweli.Alisema mwanafunzi huyo alikuwa amesajiliwa shuleni hapo Januari 15, mwaka jana kwa Na. 2099 akiwa amesoma shuleni hapo hadi mwezi Februari mwishoni na baada ya hapo mahudhurio yake yalianza kuwa ya kusuasua. Alisema baada ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Swedi kuwasili ofisini kwake aliongozana naye akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama hadi kwenye eneo la tukio katika mtaa wa Nira na kufanikiwa kuwakamata watu watano.Alisema miongoni mwao alikuwepo mzazi wa mwanafunzi Jackson Songoma na mzazi wa kijana aliyekuwa anaoa Lugeto na wengine watatu ambao majina yao hayajafahamika. “Bwana na bibi harusi walikimbia, inaonekana wakati tunaelekea kwenye eneo la tukio waliona msafara wetu wa magari na hivyo wao walifanikiwa kukimbia na kuelekea kusikojulikana, ila tumewakamata wazazi wa pande zote mbili na mahari ya ng’ombe watano zilizokuwa zimetolewa kwa mzazi wa binti, “ alisema Bukundi.Akizungumza na gazeti hili, Mkuu wa Shule ya Sekondari Igokero, Mwalukumba alikiri kuwa mwanafunzi aliyekuwa akiozwa alisajiliwa shuleni kwake. Alisema baadhi ya wazazi wilayani Misungwi wamekuwa wakiwafanya wanafunzi wa kike kama vitega uchumi vya kujipatia mali badala ya kuwaendeleza kitaaluma ili waweze kutimiza ndoto zao za maisha za kuajiriwa na kulitumikia taifa. Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Swedi ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema baadhi ya wazazi na walimu wilayani Misungwi wanafanya udanganyifu kwa kuomba uhamisho wa wanafunzi kutoka wilayani humo kwenda mikoa jirani na baadaye huwaozesha.
3
“TUKIELEKEA mwisho wa mradi tumejitahidi kuacha alama kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Njombe kwa kuwapa mafunzo ya kibiashara, kuwaunganisha na taasisi za kifedha na masoko, na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uzalishaji,” anasema Meneja wa T-LED wa mikoa ya Iringa na Njombe, Stella Mdahila.T-LED ni mradi wa miaka mitano (Aprili 2005 –Machi 2020) wa kuwasaidia na kuwaendeleza wajasiriamali Tanzania katika kukuza kilimo biashara ambao mbali na kutekelezwa mkoani Njombe, unatekelezwa pia katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Shinyanga na Mtwara na Lindi.Mdahila anasema mradi huo unaotekelezwa na shirika la Voruntary Service Overseas (VSO) kwa ufadhili wa serikali ya Canada unashirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO), Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) ili kufikia malengo yake.“Katika kukuza kilimo biashara mradi unawasaidia wajasiriamali wadogo na wakati kuongeza thamani katika biashara zao kama vile alizeti, mahindi, asali, kuku, maziwa, karanga, viungo na mvinyo kama vile ulanzi na mvinyo,” anasema.Anasema mradi huo pia unawasaidia wajasiriamali katika mchakato wa kuwaunganisha na taasisi za usajili na ubora wa bidhaa kama vile Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Alama za Mistari za Utambulisho wa Bidhaa-Msimbomilia (BARCODE).Katika kipindi hicho cha miaka mitano, Mdahila anasema zaidi ya wajasiriamali 700 wa mikoa ya Njombe na Iringa, asilimia 60 kati yake wakiwa wanawake wamefikiwa na mradi na kupata mafunzo na ushauri wa biashara, na baadhi yao wamepewa ruzuku kwa ajili ya kununua mashine za kisasa za kuzalisha bidhaa zao na wameunganishwa na kunufaika na taasisi za kifedha.“Kwa upande wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini ukiwemo mkoa wa Njombe; mradi umejikita zaidi kuangalia wajasiriamali wanaoongeza thamani mazao ya chakula kwa sababu ni ukanda wa kilimo, hivyo kuna fursa nyingi wanazozipata kupitia kilimo biashara,” anasema.Frank Msigwa, mkulima anayejishughulisha na kilimo hai cha parachichi, nanasi, mbegu za maboga, chia, mbogamboga pamoja na ufugaji wa nyuki katika Kijiji cha Mgala na Madeke wilayani Njombe ni mmoja kati ya wajasirimali hao walionufaika na mradi huo wa T-LED. Kwa kupitia mradi wa T-LED, Msigwa amepata mafunzo ya kilimo biashara lakini pia alipewa (ruzuku) asilimia 60 ya zaidi ya Sh Milioni 30 iliyomuwesha kununua mashine ya kisasa ya kusindika juisi pamoja na vifaa vya kukaushia matunda.“Kwa msaada wa T LED sasa tunazalisha juisi za matunda mbalimbali na tuna soko kubwa mkoani Njombe. Tunapenda kuzalisha zaidi ili kufikia masoko mengi zaidi lakini changamoto ya vifungashio na gari maalumu la kupooza bidhaa hiyo wakati ikisafirishwa, zinatukwamisha,” anasema.Akizungumzia kilimo biashara, Msigwa anasema anatarajia kupata tani 12 hadi 15 za asali mwaka 2019/2020 kutoka katika mizinga yake 650, parachichi tani 20, mbegu za chia na maboga tani tano na kwamba bidhaa zote hizo zina soko la uhakika ndani na nje ya nchi. Akizungumzia soko la nje, Msigwa anasema bidhaa hizo za kilimo hai anauza nchini Denmark katika soko alilopata kupitia taasisi ya Tanzania Organic Agriculture Movement (Toam) ambayo yeye ni mwanachama baada ya kupata cheti cha kimataifa cha ubora wa bidhaa.“Nimelipa zaidi ya Sh Milioni 12 kupata cheti hicho kinachoniwezesha kuuza nje na baada ya kupata cheti, Toam ikanitafutia mteja, akatembelea mashamba yangu mara tatu pamoja na wakaguzi walionipa ushauri zaidi wa namna ya kuongeza na kuboresha kilimo hai,” anasema.Huku akiiomba serikali iwasaidie watanzania wawekeza katika kilimo hai kwa kuwa bidhaa zake zina soko kubwa, la uhakiika na lenye tija nje ya nchi, Msigwa anasikitika; “Kwanini kiwango change cha uzalishaji bado ni kidogo.”Anasema msimu huu wa 2019/2020 alitakiwa kuuza kwa mteja huyo tani 22 za asali, tani 1,000 za parachichi, tani 220 za mbegu za maboga na tani 23 za chia, lakini ameshindwa kwa sababu ya uzalishaji wake mdogo na hivyo atauza tani nne za asali, tani tano za mbegu za maboga na chia na tani 20 za parachichi.Kutokana na mahitaji ya bidhaa za kilimo hai kuwa kubwa, anasema anatakiwa kuongeza ukubwa wa mashamba yake na kutoa mafunzo kwa wakulima wengi wa kilimo hai ili wazalishe kwa kuzingatia viwango vya soko la nje.Ruiza Pola, mfugaji wa kuku mjini Njombe ameumaliza mwaka 2019 akifurahia mafunzo na ruzuku toka mradi wa T-LED iliyomuwezesha kununua mashine ya kutotolea vifaranga na mabanda ya kuku ya kisasa 10.Kwa kupitia mashine hiyo, Pola ameongeza kipato chake kutokana na malipo anayopata kutoka kwa watu mbalimbali wanaotaka kutotolesha vifaranga huku yeye mwenye akiongeza idadi ya kuku anaofuga na idadi ya mayai anayozalisha kwa siku.“Kwa wanaokuja na mayai yao, natotolesha kwa Sh 10,000 kwa trei moja, lakini pia nauza vifaranga ninavyototolesha pamoja na mayai kutoka katika kuku wangu zaidi ya 1,200,” anasema.Anasema nusu ya zaidi ya Sh Milioni 20 zilizotumika kununua mashine na mabanda hayo ya kisasa zimekwisharudi ndani ya kipindi hicho kifupi na kwamba juhudi zake sasa anazielekeza katika kupata mashine ya kutengenezea chakula cha kuku ili kupunguza gharama ya kununua.Lucy Yono Kitavile ni mjasiriamali mwingine wa mjini Njombe aliyenufaika na mradi wa T-LED kupitia shughuli yake kuu ya kusindika unga wa sembe wenye virutubisho ukiwa na nembo ya Mama Seki.Kitavile anasema ana uwezo wa kusindika hadi tani 7.5 za unga huo katika kiwanda chake hicho kilichounganishwa na taasisi za kifedha na kupata mkopo wa mashine mpya zenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 158 zikiwa na uwezo wa kupepeta, kuloweka, kukoboa na kusaga na kushona kiloba cha unga.“Tuliunganishwa Benki ya Wakulima na kupata mkopo wa kununua mashine hizo; mkopo ambao malipo yake yatachangiwa na Shirika la kimataifa la Acra lenye lengo la kuondoa umasikini katika makundi yaliyotengwa kwa kutumia njia mbalimbali za uvumbuzi na ufumbuzi wa pamoja,” anasema.Pamoja na kupewa mafunzo ya kilimo biashara, utunzaji wa fedha na kuunganishwa na taasisi za kifedha, anasema alibahatika kuwa kati ya wajasirimali wachache waliopewa ruzuku na T-LED ili kununua teknolojia itakayoboresha uzalishaji wake.“Ili niweze kuzalisha malighafi ya kiwanda yaani mahindi badala ya kuendelea kununua kwa asilimia 100, TLED waliniwezesha asilimia 60 ya Sh Milioni 53.4 ambayo ni kama Sh Milioni 32 kununua treka nitakalotumia kulima mashamba yangu mwenyewe yenye ukubwa wa eka 300,” anasema.Anasema unga anaozalisha kiwandani kwake anauuza katika mikoa ya Njombe, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na Lindi na ana mpango wa kupanua zaidi soko lake baada ya kufunga mashine hizo mpya zitakazomuwezesha kuzalisha zaidi ya tani 15 kwa siku.Kitavile anamshukuru Rais John Magufuli kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji yanayowawezesha wajasirimali wadogo na wakati kuingia katika soko la ushindani na wajasirimali wakubwa. Naye Theodory Mlowe ni mjasirimali mwingine wa mjini Njombe anayejishughulisha na utengenezaji wa mvinyo aliyenufaika na mradi wa T-LED.“Nilipata ujuzi wa uzalishaji wa ‘wine’ (mvinyo) za zabibu na majani mwaka 2016 kwa kupitia mafunzo niliyopewa na SIDO, lakini baadae nikabahatika kwenda nchini Ujerumani kujifunza zaidi na niliporudi nikafikiria kuanzisha kiwanda,” anasema.Anasema alianzisha kiwanda kidogo nyumbani kwake na baada ya kuanza kutengeneza wine hizo ikiwemo ya ndizi, avocado, lozera na apple ndipo alipokutana na wataalumu kutoka mradi wa T-LED na kumshirikisha katika mafunzo yao.“Mbali na Mafunzo T-LED wameniwezesha kununua mashine ya kisasa ya kuchujia wine ili kuongezea ubora wa kinywaji hicho chenye faida mbalimbali mwilini,” anasema na kuongeza kwamba, kiwanda chake chenye thamani ya Sh milioni 25 kina uwezo wa kutengeneza lita 1,000 za wine kwa siku.Wakati akiendelea na taratibu za kupata lebo ya TBS ili bidhaa yake hiyo iiingie katika ushindani wa soko kubwa la ndani na nje ya nchi, anasema soko lake la uhakika lipo katika mikoa ya Njombe, Iringa, Songea na Mbeya. Mlowe aliyekiri kupwaya kwenye mtaji wa vifaa vidogo vya uzalishaji kama chupa ambazo hupatikanaji wake una changamoto kubwa, anaiomba serikali ianzishe utaratibu wa kutoa msamaha wa kodi kwa wajasirimali wadogo kwa kuwapa kipindi fulani kitakachowezesha biashara zao kusimama.Violet Hongo mjasirimali mwingine wa mjini Njombe aliyekuwa akijishughulisha na utengenezaji wa biskuti na keki, anajivunia mafanikio aliyopata baada ya kuwezeshwa na mradi wa T-LED.“Kabla ya kukutana na T-LED nilikuwa natengeneza vitafunio vidogovividogo, lakini kwa msaada wa mradi huo nikawezeshwa kununua mashine saba za kutengeneza mikate na sasa nina kiwanda kikubwa kinachotegemewa mjini Njombe kwa uzalishaji wa mikate,” anasema.Mshauri wa Biashara wa Mkoa wa Njombe, Lusungu Mbede anasema: “Tangu awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwepo ongezeko la viwanda kutoka 561 mwaka 2015 hadi viwanda 766 mwaka 2019. Anaongeza kuwa, kati ya viwanda hivyo 766; viwanda sita ni vikubwa, vya kati 62, vidogo 157 na vidogo zaidi 541.“Kwa jumla, viwanda vingi vinategemea malighafi za kilimo na mazao ya misitu na vinapofanya kazi vinagusa wakulima wadogo kwa sababu vinaongeza bei kwa mazao ya mkulima na kukuza vipato vyao,” anasema.Akitoa mfano wa kilimo cha parachichi jinsi kinavyowainua wakulima wa mkoa huo anasema inalimwa katika wilaya zote za Mkoa wa Njombe ambazo ni Ludewa, Makete, Wanging’ombe, Makambako, Njombe na na hivyo kuwa mkombozi wa wakulima wa kawaida.Kushamiri kwa kilimo hicho, anasema kumelivuta Shirika la Olvado Tanzania lililoamua kujenga kiwanda cha kusindika pararachi kilichopo katika hatua za mwisho kukamilika katika kijiji cha Italalumba, wilayani Wanging’ombe.Amewataka wananchi wa mkoa kuongeza uzalishaji wa zao hilo, asali na mengineyo ambayo soko lake ni la uhakika ndani na nje ya nchi ili wainue vipato vyao na kuboresha uchumi wao na wa Taifa. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka anaupongeza mradi wa T-LED kwa jinsi ulivyowasaidia kuwatambua wajasirimali wa mkoa huo, kuwapa elimu na kukuza mitaji yao.Ole Sendeka anasema: “Tunaamini waliopata ujuzi na maarifa yao, watayapeleka kwa wenzao ili nao waongeze tija katika shughuli zao.”Anasema sheria, sera ya uendelezaji biashara ndogo na za kati na miongozo mingine inahitaji kushirikisha wadau na jamii kwa jumla katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia urasimishaji wa biashara ili kuleta maendeleo ya jamii husika.Anasema ni muhimu kutambua kuwa, kufanya biashara katika mfumo rasmi unaotambulika kisheria ni jambo muhimu kwa kuwa kunakuza uchumi wa wafanyabiashara husika na kuchangia maendeleo ya mji, wilaya na mkoa na pia, kuchangia kukuza pato la taifa.
3
Dirisha la usajili lilifunguliwa rasmi Juni 15, mwaka huu na sasa linaelekea mwisho lakini hadi jana, hakuna timu hata moja ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosajili kupitia mtandao wa usajili wa wachezaji.Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jonas Kiwia alisema jana timu tatu za madaraja ya chini ndio zimekamilisha mchakato huo. Kiwia alisema iwapo Yanga, Simba na timu nyingine za Ligi Kuu na daraja la kwanza zitashindwa kukamilisha mchakato ndani ya siku zilizopangwa, zitashushwa daraja kwani hazitaruhusiwa kushiriki ligi husika.“Hakuna timu hata moja za Ligi Kuu iliyosajili kupitia mtandao, tunazihimiza kuanza usajili mapema kuepuka usumbufu baadaye wa kushushwa daraja,” alisema. Alisema imejengeka tabia kwa timu za Tanzania kila msimu kuchelewa kumaliza usajili mapema na kusubiri dakika za mwisho ambapo kuna athari kubwa.Alitaja athari mojawapo ni kukwama kwa mtandao kwani kila timu inakimbizana na muda wa kufungwa kwa dirisha hilo. Kiwia amesema ni muhimu timu zote za ligi hizo kuanza mchakato huo mapema kukwepa adhabu ya kushushwa daraja.Timu nyingi bado zinakimbizana kusajili wachezaji wakisubiri baadhi ya wachezaji ziliowasajili kumaliza mikataba walikotoka. Wachezaji wengi mikataba yao na timu za zamani inatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi huu, mwezi ujao na Oktoba.Mbali ya Yanga na Simba, nyingine ni Mtibwa Sugar, Azam, Majimaji Songea, Lipuli, Mbao FC, Kagera Sugar na Mwadui, Ruvu Shooting, Mji Njombe, Ndanda, Singida United, Stand United, Mbeya City,
4
['Manchester United wameongeza dau la £30m juu ya thamani ya kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la £180m kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la £89m in 2016.(Star)', 'Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail)', "Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves - iwapo watamkosa beki a leicester na Uingereza Harry Maguire, 26. (L'Equipe, via Express)", 'Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban £90m ili kuweza kuwa na fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph)', 'Arsenal itataka kulipwa dau la £8.8m ili kumuuza nahodha wake na beki wa Ufaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na alikataa kuondoka na wenzake kuelekea Marekani kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)', 'Arsenal imeimarisha hamu yake ya kumsaini beki wa Benfica na Ureno Ruben Dias, 22, kufautia maamuzi ya hivi karibuni yaKoscielny . (Mail)', 'West Ham infanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt over a deal to sign 25-year-old French striker Sebastian Haller for around £40m. (Sky Sports)', 'Mshambulaji wa Manchester United na Jamhuri ya Ireland Mipo Odubeko, 16, ambaye aliifungia magoli 35 shule yake ya mafunzo ya soka msimu uliopita amekataa kuongeza kandarasi mpya.. (Mail)', 'Juventus imekubali dau la £63m kumnunua beki wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 19. (De Telegraaf - in Dutch)', 'West Ham wametaka kulipwa kitita cha £10m ili kumsajiuli kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang, 27, licha ya klabu za Itali kama vile Bologna na Sassuolo kuonyesha hamu ya kumnunua mchezaji huyo. (Sun)', 'Tottenham inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leeds na Uingereza Kalvin Phillips, ambaye klabu hiyo ya York Shire inasema ana thamani ya £30m. (Mirror)', 'Manchester United bado ina hamu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Sean Longstaff kutoka Newcastle licha ya klabu hiyo kutokubaliana juu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)', 'Lakini bei ya Newcastle ya £50m inaweza kuilazimu United kumaliza hamu yao.. (ESPN)', 'Barcelona inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid kwa dau la £107m . (Mirror)', 'Duru kutoka Barcelona zimekana ripoti kwamba tayari klabu hiyo imetoa dau hilo (Sport)', 'Mshambuliaji Gareth Bale, 29, alishiriki mazoezi na wenzake wa Real Madrid nchini Canada huku akiendelea kujilazimisha katika mipango ya mkufunzi Zinedine Zidane. (Mail)', 'Newcastle inajiandaa kumteua mkufunzi wa Sheffield Wednesday Steve Bruce kuwa kocha wake na wanatumai ataweza kujiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu ujao ziarani China. (Telegraph)', 'Newcastle inajadiliana kuhusu fidia ya takriban £5m na klabu ya Sheffield Wednesday ili kumsajili Bruce. (Times)', 'Manchester United na Manchester City zimepigwa jeki katika harakati za kumsajili Bruno Fernandes huku klabu yake ya Sporting Lisbon ikikaribia kumsajili mchezaji atakayechukua mahala pake.. (Mirror)', 'Manchester United imeanza majadiliano na Roma kuhusu kumuuza mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku. (Goal.com)', 'Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Inter Milan Piero Ausilio amesafiri kuelekea mjini London ili kukutana Manchester United ili kuona iwapo dau watakaloliwakilisha kumsajili Lukaku litafanikiwa kumnunua (Guardian)', 'Ajenti wa beki wa Tottenham Toby Alderweireld amefanya mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 mwenye thamani ya £22.5m. (Calciomercato)', 'Mchezaji wa Real Madrid na Jamhuri ya Dominican Mariano Diaz, 25, hana hamu ya kujiunga na Arsenal msimu huu. (AS, via Mirror)', "Paris St-Germain wanatarajiwa kuimarisha hamu yao ya kutaka kumsajili mchezaji wa Everton Idrissa Gueye kwa dau la £27m kwa kiungo huyo wa Senegalr. (L'Equipe, via Sun)", "Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Real Madrid's Dani Ceballos kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amekuwa akifanya mazungumzo na klabu ya Tottenham. (Sky Sports)", 'Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuzuia jaribio la Steven Gerrard kumrudisha winga Ryan Kent katika klabu ya Rangers msimu huu. Mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 22 alihudumu msimu uliopita kwa mkopo na klabu hiyo ya Uskochi.. (Express)', 'Ajenti wa winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn, 21, ameiambia klabu ya Bayern Munich kwamba mteja wao anayekumbwa na uvumi wa kuhamia klabu ya Manchester United yuko tayari kuhamia Ujerumani. (Express)', 'Manchester United wamefutilia mbali hamu yao inayoripotiwa ya kumsaini mchezaji wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25, ambaye amehusishwa na Arsenal. (Manchester Evening News)', 'Mshambuliaji wa Bournemouth na Uingereza Callum Wilson, 27 - anayelengwa na West Ham - anatarajia kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na The Cherries. (Talksport)', 'Bournemouth inajiandaa kumruhusu mchezaji mwenye umri wa miaka 25 winga wa Uskochi Ryan Fraser, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal, kuondoka kwa dau la bila malipo mwisho wa msimu ujao badala ya kumuuza msimu huu. (Express)', 'Mchezaji wa zamani wa Uingereza Peter Crouch, 38, hajaamua iwapo atastaafu baada ya kandarasi yake na Burnley kuisha msimu huu . (Talksport)', 'Wachezaji wanaolengwa na Newcastle Joelinton, mchezaji wa Hoffenheim ,22 raia wa Brazil pia ananyatiwa na Wolves. (Newcastle Chronicle)', 'Winga wa Crystal Palace 26 Wilfried Zaha, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal hakushirikishwa katika picha za jezi mpya ya ugenini ya klabu hiyo. (Express)']
4
TANZANIA imepaa kwa nafasi mbili kwenye ubora wa viwango vya Fifa vilivyotolewa jana na sasa inashika nafasi ya 135. Kwa mujibu wa viwango hivyo, Ubelgiji bado inashika namba moja ikifuatiwa na mabingwa wa dunia Ufaransa, Brazil ikishika nafasi ya tatu, England ya nne na Ureno ni nia tano. Kupanda kwa nafasi mbili za Stars kunatokana na kufanya vizuri katika michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia Qatar 2022 ambapo imefuzu hatua ya makundi. Uganda bado inaongoza kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikishika nafasi ya 80, ikifuatiwa na Kenya kwenye namba 107 na Sudan inayotarajiwa kucheza na Taifa Stars kesho kutwa iko nafasi ya 128. Rwanda ni ya 130, Burundi 144, Ethiopia ya 151, Sudan Kusini ya 173,Djibouti ya 186, Somalia 199 na Eritrea ya 207. Senegal ndio kinara wa Afrika ikishika nafasi ya 20 ikifuatiwa na Nigeria nafasi ya 34 huku Mabingwa wa Afrika Algeria ni wa 38, Morocco 39 na Misri ni wa 49. Kwenye 10 bora zimeendelea kuwa nchi zilezile zikibadilishana tu namba, ambapo Uruguay ni ya sita, Hispania inashika nafasi ya saba, Croatia ni ya nane, Colombia ya tisa na Argentina inashika nafasi ya 10.
4
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania imeunga mkono kauli ya Rais John Magufuli ya kuwataka wafanyabiashara ndogo maarufu machinga wasifukuzwe maeneo ya kati kati ya miji kama hawajaandaliwa maeneo rafiki na mwafaka kwao.Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mchungaji Silver Kiondo, alipozungumza na gazeti hili jana.Alisema Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wanapaswa kujua kwamba siyo kama Dk Magufuli anataka wamachinga wafanye biashara kwenye maeneo hatarishi kama vile barabarani au karibu na vituo vya mafuta, bali watafutiwe maeneo rafiki ambayo watapata wateja kwa urahisi.Mchungaji Kiondo alisema kuwa Serikali ina maeneo mengi kati kati ya miji ambayo yanaweza kubadilishwa matumizi yake na kuwajengea machinga ili kwa njia hiyo waweze kuwarasimisha na kulipa kodi serikalini.Alisema kuwaondoa machinga kati kati ya miji siyo rahisi kwa kuwa maeneo hayo ndiyo yenye wateja wengi, lakini viongozi hao wa Serikali wanaweza kuondoa changamoto hiyo ya wamachinga kwa kubadilisha matumizi ya baadhi ya maeneo ya Serikali yaliyo katikati ya miji kwa ajili ya wamachinga.“Baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wamekaa kimya na kuwaacha machinga kufanya biashara maeneo hatarishi, wanadhani Rais Magufuli anataka hivyo, hapana, anachotaka Rais ni kwamba wamechinga watafutiwe maeneo rafiki kati kati ya miji badala ya kuwafukuza kabla ya kutafutiwa maeneo hayo, kuwaacha kufanya biashara barabarani au karibu na vituo vya mafuta ni hatari,” amesema Mchungaji Kiondo.Ametaja baadhi ya maeneo ya Serikali jijini Dar es Salaam ambayo yanaweza kujengwa majengo maalumu kwa ajili ya wamachinga kuwa ni Kariakoo DDC na iliyokuwa Bilicanas huko Posta.Mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Razack Lokina, alisema kuwa kama watu wa mipango miji wataweza kutenga maeneo hayo rafiki, watasaidia wafanyabiashara wadogo na wakubwa kufanya biashara zao bila migongano.Profesa Lokina alisema kwa kuwa tabia ya wamachinga ni kufanya biashara mahali ambapo kuna msongamano wa watu, hivyo kuwaondoa na kuwapeleka mbali na maeneo ya kati kati ya miji ni jambo gumu.Mhadhari mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, alisema kuwa maeneo rafiki kwa wamachinga ni yale yanayoweza kufikika kwa urahisi, yenye mzunguko mzuri wa fedha na yasiwe mbali ili wateja waweze kufika kwa wepesi.Kwa mujibu wa Dk Bana, Wakurugenzi wa halmashauri za miji, madiwani pamoja na wataalamu wa mipango miji, wanaweza kuwasaidia wakuu wa mikoa katika kufikia suluhisho la kuwafanya wamachinga kufanya biashara zao bila bugdha.Ikumbukwe kwamba, mara kadhaa Rais John Magufuli amewataka wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa Serikali kutowafukuza wamachinga maeneo ya kati kati ya miji kama hawajawatafutia maeneo mengine rafiki ambayo wataweza kufanya biashara zao kwa mafanikio.
3
MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC), Habel Chidawali ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwaunga wanahabari katika mfumo huo ili wapate bima za matibabu.Aidha amesema pamoja na wao kuwa tayari kusaidia kuhamasisha jamii kujiunga na bima hiyo ipo haja ya mfuko huo kuona namna ya kuwaingiza wanahabari katika mfumo wa matiba kwani wanaamini vigezo wanavyo.Akizungumza katika semina ya wanahabari wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na NHIF juzi, Chodawali alisema wamekuwa wakijitahidi kujiunga na Mfuko huo, lakini mara zote jitihada zao ziligonga mwamba. Alisema waandishi wengi wanafanya kazi kwenye vyombo binafsi na wengi wao ni wale wa kujitegemea.Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga pamoja na kusema kwamba atafuatilia suala hilo. Konga alisema nia ya serikali ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanakuwa katika hifadhi ya matibabu.Kutokana na nia hiyo utaratibu wa kutoa huduma kwa kutumia vifurushi vya matibabu unaandaliwa ili kuwezesha wanaojiunga na Mfuko huo kutumia vifurushi wanavyotaka. “Kwenye bima kuna namna ya kudesign vifurushi na sasa tunakwenda kuwa na huduma ya vifurushi na Kila mtu atakuwa na hiari ya kujiunga na kifurushi anachoona kinamfaa,” alisema.Alisema lengo kuu la mfuko ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya bila kikwazo. Konga alisema wananchi wengi bado hawajapata uelewa wa dhana nzima ya bima ya afya.Pia alisema wataendelea kuimarisha mahusiano na watoa huduma. Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha wanahabari kuzifahamu shughuli za mfuko. Alisema kama wanahabari watakuwa na uelewa mpana juu ya mfuko huo wataweza kuusemea.“Tunataka kuwa na namna bora ya kuwafikia wananchi wengi zaidi, wengi hawajapata uelewa, tunataka wapate elimu waelewe na wajiunge na mfuko,” alisema. Alisema wakati mfuko huo ukianzishwa ulilenga zaidi wafanyakazi, lakini sasa kila kundi lina haki ya kujiunga.Alisema hilo limefungua mlango mpana kwa wananchi kujiunga bila kujali ni mkulima, mjasiriamali au mtoto.Alisema watoto chini ya miaka 18 watalipia sh 50,400 kwa mwaka. Kwa upande wake, Meneja wa NHIF Mkoa wa Dodoma, Fidelis Shauritanga alisema asilimia 33 ya Watanzania wamejiunga na NHIF na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Alisema elimu zaidi inahitajika ili watu wengi zaidi wajiunge na mfuko huo.
3
MOSCOW, Urusi RAIS wa Urusi, Vladimir Putin jana aliadhimisha siku ya kutimiza miaka  66  ya kuzaliwa kwake ambapo aliitumia kupumzika karibu na ndugu wa familia, marafiki na wasaidizi wake. Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Ikulu ya  hapa,  Dmitry Peskov   wakati wa mahojiano na Shirika la Habari la nchi hii, TASS tofauti na walivyo viongozi wengine ambao huwa wanafanya sherehea kubwa kiongozi huyo huwa anaitumia siku hiyo kwa kupumzika huku akipokea ujumbe mbalimbali wa kumtakia kila la kheri. Alisema kuwa kama jana kiongozi huyo alipokea salamu mbalimbali kutoka kwa viongozi wan je na miongoni mwa waliompigia simu ni Rais wa  Belarusi,  Alexander Lukashenko, Rais wa Azerbaijani,  Ilham Aliyev  na wa  Armenia, Armen Sarkissian. Alisema kwamba pia Waziri Mkuu,  Dmitry Medvedev  alimpigia simu Rais  Putin  akimtakia afya njema na mafanikio makubwa kwa kazi anayoifanya kwa ajili ya maslahi ya wananchi wan chi hii. Mwaka jana Rais  Putin aliitumia siku hiyo akiwa nje ya mji huu ambapo aliamua kukutana na maofisa wa  Baraza la Usalama mkutano ambao ulifanyika mjini  Sochi. Mwaka  2016, pia Rais Putin aliitumia siku kama hiyo bila kufanya shughuli yoyote ikiwa ni baada ya mwaka mmoja kwenda kushuhudia mechi ya mpira wa magongo na huku mwaka 2014 akiisherehekea akiwa ziarani nchini Siberian.
2
MARSEILLE, UFARANSA BEKI wa pembeni wa klabu ya Olympique Marseille, Patrice Evra, juzi alioneshwa kadi nyekundu kabla ya kuanza kwa mchezo wa Kombe la Ligi ya Europa dhidi ya Vitoria Guamares. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United na klabu ya Juventus, alioneshwa kadi hiyo baada ya kumpiga teke shabiki wake wakati wakipasha misuli kuelekea mchezo huo. Baadhi ya mashabiki wa Olympique Marseille walionekana kuwazonga wachezaji wao mara kwa mara na kuwazomea jambo ambalo mchezaji huyo alionekana kuchukizwa na kuamua kuwafuata ili kuzungumza nao, lakini maelewano bado hayakuwa mazuri, hivyo aliamua kumrukia shabiki huyo na kumpiga shingoni. Tukio hilo lilimfanya Evra aonyeshwe kadi nyekundu moja kwa moja na kuukosa mchezo huo japokuwa bado ulikuwa haujaanza. Hata hivyo, katika mchezo huo, Evra hakuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wangeanza kwenye kikosi cha kwanza, lakini alikuwa kwenye kikosi cha akiba. Katika mchezo huo, Olympique Marseille walikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Vitoria Guamares. Kutokana na kitendo alichokifanya Evra, Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA), kimeweka wazi kuwa kinatarajia kuchunguza zaidi tukio hilo na kutoa adhabu kubwa zaidi ya hiyo ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa. Kocha wa klabu hiyo ya Marseille, Rudi Garcia, ameonekana akimtetea Evra kwa kusema kwamba, mashabiki walimwandama sana na ndio maana aliamua kuchukua hatua hiyo kwa hasira. “Nadhani mashabiki walikuwa wakali sana hata sijui kwanini, kitendo hicho kilimfanya Evra achukie na kufikia hatua ya kumpiga shabiki wake, hakukusudia kwenda kumpiga lakini kutokana na maneno yao hicho kitu kikatokea,” alisema Garcia. Tukio ambalo amelifanya Evra kumpiga shabiki linafananishwa na nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa, Eric Cantona mwaka 1995. Kitendo hicho kilimfanya afungiwe kujihusisha na soka kwa miezi 9. Hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Evra kukumbana na kifungo cha muda mrefu na Chama cha Soka barani Ulaya endapo kitafanya uchunguzi na kuthibitisha kuwa mchezaji huyo alifanya kosa.
4
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema wizara inapitia upya sheria ya utoaji wa leseni ndogo za biashara ya madini na wachimbaji, ambayo kwa sasa utekelezaji wake unazingatia kila kipindi cha kuanza kwa mwaka wa fedha wa serikali.Alisema hayo hivi karibuni mjini Mahenge wilayani Ulanga, mkoa wa Morogoro baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara wa madini wa wilaya hiyo wakati wa uzinduzi wa soko la madini la Mahenge. Alisema sheria za leseni za uchimbaji madini zinaanza kutolewa kila Julai mosi na kumalizika Juni 30, mwisho mwa mwaka wa fedha wa serikali.Alisema jambo hilo limelalamikiwa na waombaji wa leseni ndogo za biashara ya madini na wachimbaji wakiwemo wa migodi ya Mahenge. “Wizara tumeliona na tunaifanyia marekebisho sheria ili leseni iweze kukatwa wakati wowote bila kuangalia ni mwezi gani,” alisema. Mabadiliko ya sheria hiyo inakusudia kumwezesha mchimbaji wa madini na mfanyabiashara kukata leseni mwezi wowote bila kufuata kalenda ya mwaka wa fedha wa serikali.“Mfano mtu akikata leseni Agosti mosi, mwaka huu atahesabiwa kipindi chake cha mwaka mmoja hadi Julai 30, 2020 na hapo atalazimika kulipia tena leseni yake kwa mwaka mwingine,” alisema. Kwa upande wa masoko ya madini, Naibu Waziri alisema kuwa serikali haitarajii kuona kunajitokeza ukiritimba na vikwazo kwa wauzaji na wanunuzi katika masoko yanayofunguliwa mikoa mbalimbali nchini.“Tumeibiwa sana kupitia mikataba mibovu, sasa mimi na waziri wangu pamoja na wizara tumesema tutahakikisha tunalala mbele na watoroshaji mpaka kieleweke,” alisema Nyongo na kuongeza: “Tunataka fedha kutoka sekta ya madini, hatumchekei mtu na wala hatubabaishani na mtu, ndiyo maana tumeweka masoko haya ili wachimbaji wanufaike na serikali ipate kodi yake “.Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini Wilaya ya Ulanga, Protas Lunkombe alisema sheria ya sasa inamtaka mchimbaji kukata leseni kila mwanzo wa mwaka wa fedha wa serikali. Badala yake sheria hiyo ifanyiwe marekebisho ili kuwezesha leseni ziwe zinakatwa mwezi wowote ili kuwawezesha wenye mitaji wanaohitaji kuingia katika uchimbaji wa madini wasisite kutokana kwa kubanwa na sheria.Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema licha ya wilaya ya Ulanga kuwa na utajiri mkubwa wa madini, lakini wachimbaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikuwemo ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya sekta nzima ya madini . Malenya pia alisema leseni nyingi za wamiliki wadogo hazifanyi kazi, hivyo kuzuia uhalali kwa wenye uhitaji kupata leseni za kuendelea na uchimbaji wa madini.
3
Na WAANDISHI WETU- DAR ES SALAAM KIPA tegemeo wa timu ya Medeama ya Ghana, Daniel Agyei, ametua nchini kumalizana na vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ili aweze kusajiliwa dirisha dogo na kuimarisha kikosi hicho katika mzunguko wa pili. Kipa huyo aliyewasili jijini Dar es Salaam jana akitokea nchini Ghana, ataungana na makipa wengine wa Simba, Vincent Angban na Peter Manyika Jr, ikiwa atasaini mkataba wake na kumalizana na Wekundu hao wa Msimbazi. Agyei ambaye alikuwa kipa namba moja wa kikosi cha Medeama ya Ghana, anatarajia kumalizana na uongozi wa Simba muda wowote ili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Simba imejipanga kuanza duru ya pili ya ligi kuu ikiwa na safu imara ya ulinzi, kwani kabla ya kumleta kipa huyo tayari walikuwa wamemalizana na beki wao wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa kumuongezea mkataba wa miaka miwili. Wakati Simba wakiimarisha safu ya ulinzi, mahasimu wao Yanga wameimarisha eneo la kiungo baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo mkabaji wa zamani wa klabu ya Zesco United ya Zambia, Justine Zulu. Zulu aliyetua nchini juzi kimya kimya, amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili katika klabu ya Zesco United. Usajili wa Zulu ni wa kwanza kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu katika dirisha dogo na umefanyika siku chache baada ya kutambulishwa kwa kocha mpya, Mzambia George Lwandamina, aliyerithi mikoba ya Mholanzi Hans van der Pluijm. Pluijm aliyeipa Yanga ubingwa wa ligi kuu kwa mara mbili mfululizo, amepewa majukumu ya kuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo. Yanga imefikia uamuzi wa kumsajili Zulu, baada ya juhudi za kumnasa kiungo mwingine wa Zesco United, Meshack Chaila, kugonga mwamba. Wakati huo huo, mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga, amesema hana haraka ya kuongeza mkataba na klabu yake hiyo hadi muda mwafaka utakapofika. “Kwa sasa siwezi kuzungumzia suala la mkataba kwa sababu sina haraka, hivyo taarifa zilizoenea kuwa nimesaini mkataba mwingine, hazina ukweli wowote,” alisema Tambwe.
4
Simba ilibuka na ushindi huo ukiwa ni mchezo wa kiporo cha muda mrefu, hivyo kuongeza pengo la pointi tatu dhidi ya wapinzani wao, Yanga. Katika mchezo huo, Njombe Mji ilionekana kuanza vizuri kwa kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba, hali iliyowapa wakati mgumu mabeki wa Simba kuhakikisha wanawazuia Ditram Nchimbi na Mustapha Bakari, ambao walionekana moto ndani ya dakika 10 za kipindi cha kwanza. Utulivu wa mabeki wa Simba ulikuwa na faida kwa upande wao baada ya kuwadhibiti vyema wachezaji hao.Mbinu ya kutumia mipira mirefu iliwapa faida baada ya dakika ya 17 mshambuliaji John Bocco kuipatia timu yake bao la kuongoza kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango David Kisu, baada ya kupokea mpira uliopigwa na beki Yusuph Mlipili. Vijana wa Alli Bushiri waliendelea kucheza mpira wa pasi fupifupi huku wakifanya mashambulizi mfululizo, ambapo mpaka dakika ya 25 Njombe ilikuwa na kona tatu wakati mbili kwa wapinzani wao.Pamoja na usumbufu wa washambuliaji wa Njombe lakini umakini ulikuwa mdogo, ambapo hata hivyo hawakuweza kuona lango la wapinzani wao na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyumba kwa mbao 1-0. Kipindi cha pli kilianza kwa Simba kutawala mchezo na kufanya mabadiliko ya kumtoa Okwi na kuingia Mavugo, kabla ya dakika ya 60 kutoka James Kotei ambaye aliumia na kuingia Salim Mbonde ambaye alirejea kwa mara ya kwanza.Baada ya mabadiliko hayo dakika nne baadaye mshambuliaji John Bocco alikwamisha tena bao la pili akipokea krosi safi ya Shomary Kapombe na kufanya mchezo huo kumalizika mabao 2-0. Nahodha wa Kikosi cha Simba, John Bocco alizungumza baada ya mchezo alisema anawashukuru mashabiki na uongozi wa timu hiyo kwa kuwapa sapoti ya kila hatua na sasa wanajipanga kushinda kila mchezo ili kutimiza ndoto yao ya kuchukua ubingwa.
4
KIUNGO wa KMC FC, Ally Msengi amesema amefurahi kusajiliwa na klabu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini na kudai changamoto mpya zitamsaidia kumjenga. Msengi amesajiliwa na Stellenbosch ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini humo kwa mkataba wa miaka mitatu. “Ninafurahia kwenda kuanza changamoto mpya nje ya Tanzania na ninaamini zitanijenga badala ya kuendelea kubweteka hapa nyumbani,” alisema Msengi. Msengi ambaye alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya U17 kilichofuzu kucheza fainali za Gabon 2017 amefanya vizuri akiwa na klabu ya KMC aliyoichezea kwa msimu mmoja na nusu pia amekuwa katika kikosi cha timu ya Taifa U20 Pia ameushukuru uongozi wa KMC kwa ushirikiano mkubwa tangu alipotua hapo na kumruhusu kuondoka kucheza soka nje ya Tanzania. Msengi amepelekwa Afrika Kusini na kampuni ya Siyavuma Sports Group, inayosimamiwa na Michael Mwebe ambaye amesema ni muendelezo wao wa kuwapatia fursa ya kucheza soka la nje ya nchi wachezaji Watanzania na walianza na Abdi Banda, Himid Mao, Eliud Ambokile, Yahya Zaydi na sasa Msengi.
4
Christina Gauluhanga, Dar es salaam Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir ameagiza madrasa zote nchini kufungwa kuanzia leo Jumatano Machi 18, ili kupunguza ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa corona. Akizungumza na Mtanzania leo Jumatano Machi 18, jijini Dar es Salaam Sheikh Zubeir amesema agizo hilo linapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo na kwamba taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Amesema kuhusu Swala ya Ijumaa na ile ya Jamaa zitaruhusiwa kwa sasa na huenda itabadilishwa kulingana na mazingira ya ugonjwa huo. “Kuanzia sasa swala za Jamaa zinapaswa kuswaliwa kwa kuachiana nafasi na kuzingatia usafi ili kupunguza maambukizi,” amesema Sheikh Zubeir. Amesema kwa maeneo ambayo yanawashukiwa wa ugonjwa huo na yamewekwa karantini hairuhusiwi kuendelea na swala hizo kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kuwa ni dhambi kumuambukiza ugonjwa mwenzio kwa makusudi,” amesema. Amesema muislamu yeyote atakayepata na maradhi haya ni haramu kwake kuhudhuria swala za Ijumaa na Jamaa kama ambavyo ni haramu kwake kuchanganyika na wengine kwani kufanya hivyo ni kuisambaza na kueneza ugonjwa huo kwa wenzake.
3
Na MWANDISHI WETU FISTULA si neno geni kwa wengi wetu, ingawa inawezekana tusijue maana halisi ya neno hili. Fistula ni tundu linalounganisha njia mbili za mwili zilizo wazi. Kuna fistula za aina nyingi, lakini inayozungumziwa hapa ni fistula ya uzazi (obstetric fistula), ambayo ni tundu lisilo kawaida ambalo halikutakiwa kuwapo kati ya kibofu cha mkojo na njia ya uke (Vesico-Viginal Fistula – VVF) au kati ya njia ya haja kubwa na uke (Recto-Vaginal Fistula – RVF). Wanawake wengi hupata VVF, wachache RVF na wachache zaidi hupata zote kwa pamoja. Inaelezwa kuwa, fistula mara nyingi hutokana na uzazi pingamizi (obstructed labour) wa muda mrefu, ambao haukuhudumiwa kwa wakati mwafaka. Hali hii inapotokea kunakuwa na msuguano kati ya mfupa katika nyonga na kichwa cha mtoto unaopelekea jeraha katika njia ya haja kubwa au ndogo, ambalo baadaye hugeuka kuwa tundu. Uzazi au uchungu pingamizi ni uzazi usioendelea aidha kwa sababu mtoto ni mkubwa kuliko njia ya uzazi, nyonga za mama kuwa na tatizo(aidha mama hakuwa na ukuaji mzuri kutokana na utapiamlo utotoni au ajali iliyoathiri nyonga) ama ulalo mbaya wa mtoto tumboni. Upasuaji kwa ajili ya uzazi au matibabu mengine katika viungo vilivyopo maeneo ya nyonga huweza kusababisha fistula. Hii hutokea pale daktari ama kwa bahati mbaya ama uzembe anatoboa kuta za njia ya haja kubwa au ndogo ya mgonjwa na kusababisha fistula. Benki ya NMB ni sehemu ya wadau muhimu katika mapambano ya ugonjwa wa fistula ambapo hivi karibuni, wafanyakazi wake waliwatembelea wagonjwa wa fistula wanaoendelea kupata matibabu katika Hospitali ya CCBRT, jijini Dar es Salaam. Ugeni huo kutoka NMB kwa CCBRT, hasa Kitengo cha Fistulam ulikuwa wenye Baraka, kwani NMB ilikabidhi msaada wa Sh milioni 13 ili kusaidia mahitaji mbalimbali yanayotakiwa katika kuuguza kundi hili la akina mama amboa ni wahanga wa fistula. Hafla hiyo imehudhuriwa na maofisa wa NMB kutoka Morogoro, Bagamoyo, Kibiti na Dar es Salaam. Hospitali ya CCBRT ina kauli mbiu inayosema “Fistula Inatibika”, hii ni kutokana na ukweli kwamba, jamii imekuwa na mtazamo hasi juu ya mwanafamilia anapokutwa na dalili au kupata tatizo la fistula. Familia nyingi zimekuwa zikichukulia tatizo hili kama laana au kuhisisha na mambo ya kishirikina na wengine kudhani kwamba ni ugonjwa ambao unasababishwa na mwanamke kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume zaidi ya mmoja. Wengine wamekwenda mbali zaidi kufikiri kwamba, fistula ni mmoja ya magonjwa hatari ya zinaa na hauna tofauti na HIV. Akizungumza na ugeni huo, Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji wa Huduma CCBRT, Brendaali Msangi, anasema Fistula inatibika kwa kipindi kifupi pindi mgonjwa anapopatiwa matibabu stahiki. “Fistula inatibika, tena kwa muda mfupi sana, inachukua wiki tatu hadi mwezi mmoja kutoka siku ya operesheni kwa mhanga wa fistula kupona na kuendelea na matibabu ili kupona kabisa. “Tunapokea wagonjwa wengi sana kupitia mabalozi wetu ambao tunao katika jamii. Hii ni kutokana na watu wengi wamekuwa hawajui kama tatizo linatibika au wengine wamekuwa wakiona aibu kujitokeza ili watibiwe. “Nina furaha kubwa sana leo tumeongeza idadi ya mabalozi wengine ambao ni NMB.  NMB ina matawi zaidi ya 213 nchi nzima, maofisa wa NMB watakuwa mabalozi  wazuri juu ya elimu waliyoipata hapa leo. Naomba nishukuru uongozi wa NMB kwa kuona umuhimu wa kusaidia kundi hili la akina mama, tunashukuru sana msaada huu utasaidia katika kukidhi mahitaji ya wagonjwa wa Fistula hapa CCBRT,” anasema Msangi. Naye Meneja wa Kanda ya Mashariki wa NMB, Aikansia Muro, anasema benki yao imejikita zaidi katika kusaidia jamii, hasa katika sekta ya elimu na afya. “NMB imejikita zaidi katika kusaidia jamii inayoizunguka kwa kutoa msaada kwenye  sekta ya elimu, afya pamoja na majanga mbalimbali. Hivyo leo tumekuja CCBRT kutoa msaada wa shilingi milioni 13 ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kutatua changamoto za afya ambazo zinawakumba kina mama wengi, hasa wakati wa uzazi,” anasema Muro. Kutokana na hali hiyo, anasema wanawajali wateja wao na wangependa kuona kina mama na watoto wanapata afya nzuri, kwa kuwa wanatambua watoto ndio Taifa la leo na kesho, ila wasipokuwa na usimamizi wa mama mwenye afya bora ni hakika hawatafikia malengo yao. Kwa hali hii, imefika wakati sasa kwa jamii iondokane na dhana hiyo potofu, lakini pia wanajamii wote tunatakiwa kuwa mabalozi wazuri wa afya ya mama na mtoto kwa kuhakikisha usalama wao wakati wote.
0
MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema uzalishaji katika kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama cha TanChoice kitakachokuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 1,000 na mbuzi na kondoo 4,500 kwa siku, unaanza rasmi mwanzoni mwa mwaka ujao.Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alisema kiwanda hicho ambacho kimejengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 23 na ambacho kitatoa ajira za moja kwa moja kwa watu zaidi ya 500, kilipata leseni ya ujenzi na uendelezaji katika maeneo maalumu ya uwekezaji kutoka EPZA mwaka jana.Alisema kiwanda hiki ambacho kitakuwa na migawanyo mitano ya machinjio inakifanya kuwa kiwanda kikubwa cha nyama Afrika Mashariki na cha pili kwa ukubwa baada ya kile cha Ethiopia ambacho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 3,000 na mbuzi pamoja na kondoo 6,000 na kuzalisha tani 300 za nyama kwa siku moja.“Pamoja na kuwa na asilimia 11 ya mifugo yote barani Afrika, mchango wa sekta ya mifugo kwa pato la taifa bado umekuwa mdogo ambao ni asilimia 7.4, wakati sekta hiyo inakuwa kwa wastani wa asilimia 2.6 kwa mwaka,” alisema na kuongeza: “Kiwanda hiki cha kuchinja na kuchakata nyama kitapunguza kwa kiasi utoroshaji wa mifugo kwenda nchi jirani ambao wamekuwa wakitumia fursa hii kuongeza uzalishaji kwenye viwanda vyao na mauzo nje ya nchi”.Takwimu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaonesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe zaidi ya milioni 13.5, kondoo milioni 5.5, mbuzi milioni 3.6, nguruwe 400,000 na kuku milioni 23.2.Uwekezaji huu mkubwa wa kiwanda cha kuchinja na kuchakata nyama unategemewa kuingizia nchi fedha nyingi za kigeni kwa kuuza nyama nchi za Ulaya na Uarabuni. Sehemu ambapo mradi huu unatekelezwa ni karibu na inapopita treni ya umeme ya SGR, hivyo kukifaidisha kiwanda na wepesi wa kufikisha mizigo bandarini na pia kuleta ng’ombe kutoka sehemu mbalimbali nchini.Kiwanda cha TanChoice kitaweza kutengeneza biashara kubwa kwa vijana inayohusisha unenepeshaji wa mifugo ambayo itahitajika kama malighafi kwenye kiwanda cha nyama.“Mwekezaji huyu hawezi kufanya kila kitu, hivyo wawekezaji wa ndani wanaweza kuchangamkia fursa hii ya kunenepesha mifugo ambayo itahitajika katika kiwanda hiki,” alisema.Mabaki yatakayotokana na kuchinja na uchakataji wa nyama yatauzwa ndani ya nchi na sehemu nyingine zitauzwa China ambako soko lake ni kubwa. Pia mabaki kama damu ya mifugo itakayochinjwa inatumika katika kutengeneza chakula cha kuku hivyo kuongeza fursa kwa wazalishaji wengine wa vyakula vya mifugo. Kwato na pembe za ng’ombe hutumika kutengeneza vifungo vya nguo na mabegi.
3
AZIZA MASOUD Na AGATHA CHARLES – DAR ES SALAAM WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema ingawa baadhi ya watu wanazungumza kwa kumbeza Rais Robert Mugabe baada ya kujiuzulu, mchango alioutoa kwa Zimbabwe ni mkubwa. Akizungumza na MTANZANIA jana, Jaji Warioba alisema  yaliyotokea Zimbabwe ni mabadiliko, lakini yamekuwa faraja kwakuwa yamefanyika kwa amani na kuiacha nchi ikiwa na utulivu. “Hatua ya kujiuzulu kwa Mugabe imetokana na matatizo yaliyopo kwenye chama chake (ZANU-PF) kwa muda mrefu sasa, hata kabla ya Uhuru. Mara ya kwanza walikuwa na chama kimoja, lakini vurugu zilifanya wapate vyama viwili vya ZANU na ZAP, nadhani kwa sasa la muhimu ni nchi hiyo ipo salama,” alisema Jaji Warioba. Aliongeza kuwa pamoja na kiongozi huyo kujiuzulu, mchango wake aliutoa kwa nchi hiyo ni mkubwa na hata kipindi alipokuwa akipigania uhuru aliwahi kukaa jela miaka 10. “Amejiuzulu watu wanaongelea kwa hisia tofauti, lakini mimi naona mchango wake alioutoa kwa taifa la Zimbabwe ni mkubwa, kilichotokea kwake kinachangiwa na tatizo  la viongozi kukaa madarakani kwa muda mrefu, hatua aliyochukua ni nzuri kwakuwa katoka kistaraabu bila kupoteza utu wake,” alisema Jaji Warioba. Alisema Mugabe na Mnangagwa walishiriki kikamilifu kutatua matatizo mbalimbali yaliyopo ndani ya nchi hiyo.   WASOMI NAO WASEMA YAO Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, alisema anaamini Zimbabwe itaendelea na mapambano ya kiuchumi hata kama Mugabe hayupo madarakani. “Kwa sasa Zimbabwe inatakiwa kuendelea kujipanga na mapambano dhidi ya uchumi, Mugabe yeye alifanya kazi ya kuikomboa nchi hiyo kisiasa, akafanya makosa katika nyanja za uchumi, basi watakaoiongoza kwa sasa ni jukumu lao kutekeleza suala hilo,” alisema. Alisema uchumi wa nchi hiyo kwa sasa umeharibika kutokana na kuwapo kwa vikwazo vingi ambavyo viliwekwa na Mugabe.
3
  Na EVANS MAGEGE MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema,  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hakuwa mjinga kufa masikini. Butiku alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akichangia maada kwenye kongamano la Kibweta cha Mwalimu Nyerere kilichoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere   Kigamboni. Maada kuu ya kongamano hilo   ilisema, “Mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Jamii”. Akichangia, Butiku alisema Nyerere alikuwa muumini wa usawa hivyo alijituma kuweka misingi ya maendeleo kwa utaifa wa Watanzania wote. Alisema  kama Baba wa Taifa angekuwa na moyo wa ubinafsi na mroho wa mali, angeanza kwa kujilimbikizia mali kabla ya maendeleo ya nchi na asingekufa masikini. Alisema Nyerere aliona mbali katika kuleta maendeleo yenye usawa kwa wananchi kwa kuanzisha viwanda. Butiku alisema kwa sasa yapo malengo ya kuanzisha  viwanda kama alivyofanya Baba wa Taifa. Alisema wakati malengo hayo yakiwapo, Watanzania wanatakiwa kujua kwamba viwanda siyo maendeleo bali ni matokeo ya watu   walioendelea. “Mwalimu alikuwa ni mtu anaona huko, anaona watu wake, anaona watu anaowaongoza, ametokea miongoni mwao, anajua mahitaji yao,  kwa hiyo alikua anajua afanye nini   watu wote wapate. “Viwanda vyetu vipo? Na kama havipo kwa nini? Tukubali makosa, kung’ang’ania kitu ambacho hakijafika halafu kikakushinda… Kwa hiyo ukipewa usisahau kuwa si vyako kwa hiyo usiibe,” alisema Butiku. Alisema Hayati Baba wa Taifa alipokuwa anaiweka nchi iwe ya Watanzania wote alikuwa na maana ya wananchi wote kushiriki kwa usawa katika kujenga maendeleo yenye umoja na usawa. Alisema bila amani   viwanda  haviwezi kuwapo badala yake ni kushindania  na kugombania vyeo. “Nawauliza mnaendelea kushughulika na viwanda au mnaendelea kushughulika na vyeo vyenu? Mnaendelea kushughulika na viwanda, elimu na afya au mnaendelea kushughulika na kula?. “Haya ni maswali magumu. Nyerere huyu tunayemzungumza leo alikufa masikini, kwani alikuwa mpumbavu?  Alikuwa mjinga au alikuwa hana elimu?  Jibu utapata, aliwapendeni ninyi,” alisema Butiku. Kwa muktadha huo, alisema Nyerere aligombania amani na utulivu ili   wananchi wote wapate chao. “Kuwa na nchi mnajenga Chuo Kikuu Dodoma halafu mnapeleka watoto wajinga 7000,  Je hayo ni maendeleo?” aliuliza. Alisema kama nchi haijaendelea kutakuwa na msululu wa viwanda vya watu wageni na Watanzania watakuwa makuwadi. Alisema viwanda ambavyo Hayati Baba wa Taifa alivijenga vilikuwa ni viwanda vidogo  ambavyo vinaendana na kilimo. “Kwa sasa  tumetilia mkazo sana viwanda vinavyotumia fedha nyingi kuviendesha, hayo mabilioni ya kuviendesha mnayo? “Lakini nimeona sera ya serikali… tuipongeze kwa sababu imeanza kutufufulia viwanda katika sekta ya kilimo,” alisema. Alisema viwanda vya kilimo vitawapa Watanzania fedha za mifukoni lakini viwanda vya mafuta na gesi ndivyo vitampa fedha Rais Magufuli. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Mark Mwandosya, alisema Watanzania wanatakiwa kujiuliza kwamba unapozungumzia ujenzi wa viwanda, vinajengwa kwa nini, sehemu gani vinajengwa na kwa faida ya nani? Mwanasiasa mwingine mkongwe, Ibrahim Kaduma ambaye alifungua kongamano hilo, alisema unafiki umelifikisha taifa mahali pabaya. Alisema Hayati Baba wa Taifa alijenga misingi ya taifa lakini viongozi waliofuata wamesuasua kuujenga ukuta. Alisema wakati Hayati Baba wa Taifa na wenzake wanatafuta uhuru wa nchi hii, hawakuthamini fedha kuupata kwa sababu fikra yao ilikuwa ni ukombozi  wa nchi.
3
NA ADAM MKWEPU UONGOZI wa Yanga umetamba kuendelea kutumbua majipu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha wanashinda michezo yake mbalimbali ya ligi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,  Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa  wamejiandaa kupata ushindi dhidi ya Stand United katika mchezo wao utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya ‘figisufigisu’ wanazoendelea kufanyiwa na  wapinzani wao. “Tutaendelea kutumbua majipu, licha ya wapinzani wetu kutufanyia figisufigisu, lakini tunawaambia watasubiri sana mwaka huu na hawataweza,” alisema. Alitoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kwenda kwa wingi kuishangilia uwanjani katika mchezo wao na Stand. Akizungumza juu ya usajili wao, Muro alisema wamesajili wachezaji wawili, akiwamo aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City na baadaye Mwadui ya Shinyanga, Paul Nonga na Mniger, Issoufou Boubacar. Yanga kwa sasa ipo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 27 mbele ya klabu ya Azam, walio na pointi 26.
4
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
5
MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali saba kwa kila nchi kutoka Tanzania na China, yamesaini mkataba wa ushirikiano katika nyanja tofauti kwa lengo la kuondoa umasikini.Aidha, imeelezwa kuanza safari za ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (TTCL) kuelekea Guangzhou China moja kwa moja, kutahamasisha uhusiano wa watu wa nchi hizo mbili.Hatua hiyo imefikiwa jana wakati wa uzinduzi wa mpango wa ujenzi wa jumuiya ya njia ya hariri, mpango huo wa China unakuwa wa kwanza kuzinduliwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini na kusaidia katika usalama na amani, ardhi, afya ya wanawake na watoto katika kuondoa umasikini.Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na Naibu Spika wa China, Ji Bingxuan, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, Balozi wa Tanzania China, Mbelwa Kairuki na wawakilishi wa asasi zilizosaini mkataba za China na Tanzania. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alisema katika mkutano wa pili wa kimataifa wa ushirikiano wa njia moja ukanda mmoja, uliofanyika Aprili mwaka huu, mtandao wa taasisi zisizo za kiserikali China ulizindua mpango huo.Alisema lengo lake ni kutoa misaada kwa asasi za kiraia kutoka nchi za ukanda mmoja na njia moja kwa kufanya semina, kutembeleana na miradi ya kuboresha maisha, jambo lililopata mrejesho chanya. Ndugai alisema ushirikiano huo ni wa pekee, kwa kuwa imezoewa ule wa kiserikali, bunge au nyinginezo, lakini kwa taasisi zisizo za kiserikali ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Watanzania.Alisema baada ya Rais wa China, Xi Jinping kusaidia fedha nyingi nchi za Afrika ili kuleta maendeleo hiyo ni fursa ya taasisi katika kuleta maendeleo ya wananchi. Mwenyekiti wa Taasisi ya Kukuza Uhusiano kati ya China na Tanzania (TCFPA), Dk Salim Ahmed Salim katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu wa Taasisi hiyo, Joseph Kahama alisema taasisi hizo zimeungana katika kuondoa umasikini, kwa kuhakikisha wanafuata sheria zinazosimamia asasi hizo. Pia, kuheshimu mipaka ya nchi, bila kuingilia masuala ya ndani ya nchi husika na usawa na manufaa kwa wote.“Naomba kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa uongozi wake imara ikiwemo kuwezesha ndege ya Air Tanzania kwenda moja kwa moja Guangzhou China Februari mwakani hatua itakayoongeza uhusiano wa watu wa nchi hizi,”alisema.Alisema taasisi hiyo ya kuhamasisha mahusiano, itahakikisha fedha zitakazotolewa zinafikia walengwa, kutoa ripoti serikalini huku wakihakikisha zinafanya kazi kwa matakwa ya kisheria.“Hakuna hofu katika utekelezaji wa makubaliano hayo yanayohamasisha muingiliano wa watu wa nchi hizi mbili, kwani uzinduzi wake umeshuhudiwa na spika wa bunge China ambaye ni kiongozi mkubwa,” alisema.
3
TANZANIA jana ilifuzu hatua ya makundi ya mbio za kusaka nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia 2022 Qatar baada ya kuichapa Burundi kwa penalti 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijin Dar es Salaam. Hatua hiyo ya kupigia mikwaju mitano kwa mi tano ya penalti ilikuja baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 za kawaida zikiwa sare ya 1-1 na baadae kuendelea na sare hiyo hata baada ya kuongezwa dakika 30 na hivyo kufanya mchezo huo kuchezwa kwa dakika 120. Mashujaa wa Taifa Stars walikuwa Juma Kaseja (Tanzania One) baada ya kuokoa penalti ya kwanza ya Burundi, Erasto Nyoni, Himid Mao na Gadiel Michael waliofunga penalti zao na kuiwezesha Taifa Stars kupiga hatua moja mbele kusaka tiketi ya Kombe la Dunia.Burundi wenyewe walikosa penalti zao tatu, ambazo zilipigwa na Ngado Omary, Berahino Saido na Bigirmana Gael. Katika dakika 90 za kawaida, Taifa Stars ilipata bao la kuongoza kupitia kwa nahoha wake, Mbwana Samatta katika dakika ya 29 akiusukuma kwa tumbo mpira wa kona uliochongwa na Mohamed Hussein kutokea upande wa kulia.Kaseja akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo alisema kikubwa watanzania wanatakiwa kuwa na mshikamabo mkubwa ili kuendelea kufanya vizuri na kutokuwepo kwake katika timu ya taifa kwa mrefu sio kama alishuka viwango, ila ni mpango wa makocha waliokuwepo.Taifa Stars sasa inasubiri kupangwa katika makundi na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) ili kujua wataangukia katika kundi gani na wapinzani gani katika mbio hizo za kusaka tiketi ya kwenda Qatar 2022.Tanzania sasa itaungana na timu zingine 14 zilizofuzu baada ya kupata ushindi wa jumla kutoka katika mechi mbili walizocheza na kuungana na zingine 26 ambazo ziko katika nafasi ya juu na hazikucheza raundi hiyo ya awali ili kutimiza timu 40, zitakazopangwa katika makundi 10, katika hatua ya pili ya kufuzu. Dakika ya 40 Burundi walilisakama lango la Stars baada ya mshamnbuliaji wao kupokea pasi baada ya Kelvin Yondan kukosea kuokoa kutokana na walinzi wa Stars kujichanganya.Dakika 45, Burundi walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Abdul Fiston kwa mkwaju hafifu baada ya walinzi wa Taifa Stars kujichanganya baada ya kushindwa kuondosha hatari.Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika, timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana bao 1-1. Dakika ya 57 Samatta nusura afunge licha ya kuwa katika nafasi nzuri, alipiga shuti kubwa juu ya lango la Burundi.Dakika ya 75 Idd Seleman Nado nusura afunge baada ya Gadiel Michael kufanya kazi kubwa ya kuwatoka wachezaji kadhaa wa Burundi na kutoa pasi kwa Nado, aliyepiga mpira nje.Kikosi cha Taifa Stars: Juma Kaseja, Hamis Ramadhani, Mohamed HusseinGadiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Gerald Mkude, Idd Seleman, Aboubakar Salum/ Shaban Idd, Mbwana Samatta/Himid Mao na Hassan Dilunga/Farida Mussa.
4
BENKI ya NBC imesema itaendelea kushirikiana kikamilifu na Serikali ya Awamu ya Tano katika azma ya kukuza uchumi wa wananchi na maendeleo kwa ujumla.Akizungumza wakati wa kongamano la wadau juu ya upatikaji wa fedha na usimamizi wa hatari zinazoweza kujitokeza katika miamala ya kifedha lililoandaliwa kwa wadau jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko wa NBC, Peter Nalitolela alisema NBC imejizatiti kuhakikisha nchi inafaidika na kiasi cha pesa inachotumia katika miradi mikubwa ya maendeleo inayofanyika.Kongamano hilo lililohudhuriwa na wadau kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Shirika la Umeme (Tanesco), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Wizara ya Fedha na Mipango.Alisema lengo lake kuu ni kuangalia vyanzo mbalimbali vya fedha vinavyopatikana katika miradi mbalimbali mikubwa inayofanywa na serikali pamoja na kuangalia usimamizi wa hatari katika miamala ya kifedha inayoweza kutokea katika miradi hiyo.“Kama mjuavyo miradi mbalimbali mikubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kama vile mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi wa umeme wa Mto Rufiji wa Stiegler’s Gorge, ujenzi wa barabara na madaraja.“Baadhi ya miradi hufanywa kwa mikopo kutoka pande tofauti, hivyo tulitaka kuonesha uwezo wetu kama NBC katika kusaidia upatikanaji wa fedha na pia linapokuja suala la uzimamizi wa hatari za kifedha katika miamala hiyo.“Kilicho kikubwa ni kwa NBC kuangalia uwezo wetu kwa njia tofauti tofauti ikiwemo katika kukopesha, lakini pia kuona serikali haipati hasara kutokana na masuala ya riba, fedha za kigeni na kushuka kwa thamani ya shilingi.“Hivyo NBC tumejiandaa kushirikiana na serikali kikamilifu katika kutimiza azma yake, kwa uwezo wetu tunaweza kushirikiana zaidi na zaidi,” aliongeza Nalitolela.Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo alisema kama inavyofahamika kuwa NBC inamilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania, Benki ya Absa ya Afrika Kusini na Benki ya Dunia, hiyo huiweka NBC katika nafasi nzuri ya kusaidia juhudi za serikali.Katika kongamano hilo pia NBC Ilileta wataalam kutoka benki mama ya Absa ili kuweza kuonesha uzoefu wao walioupata kupitia miamala waliyofanya na serikali za nchi mbalimbali barani Afrika.
5
Na SAMWEL MWANGA-MASWA HALMASHAURI ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imetoa siku 90 kwa watu wote waliojimilikisha mali zake bila kufuata utaratibu kuzirejesha mara moja vinginevyo watashtaki kwa makosa ya wizi. Wito huo umetolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dk. Fredrick Sagamiko wakati akizungumza na MTANZANIA wakati akielezea utekelezaji wa zoezi la urejeshaji mali za wananchi wa wilaya hiyo zilizochukuliwa na baadhi ya watu bila kufuata taratibu. Alisema Serikali inaendelea kusimamia urejeshaji wa mali za umma zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango wa kupambana na uhalifu wa mali za serikali ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na kutaifishia mali hizo pindi ushahidi unapopatikana. “Huu ni mpango wa kurejesha mali za serikali haukuanza leo ni tangu mwaka 2012 upo sisi kama halmashauri tunachokifanya na kuuendeleza tu ni lazima tupambane na uhalifu tutakachokifanya ni kuwashitaki na kisha tutataifisha mali zao hizo walizopewa wakishindwa kuzirejesha kama tulivyoagiza,”alisema. Alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya serikali wilayani humo kuunda timu ya kufuatilia mali za halmashauri na kubaini mali nyingi zikiwemo vituo vya mafuta,viwanja na nyumba zikiwa zinamilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara, wanasiasa na watumishi wa Umma bila kufuata utaratibu na tayari wahusika wameshajulishwa kwa barua. Dk Sagamiko aliongeza kwamba mhusika ambaye atakaidi agizo hilo atashitakiwa na mali aliyoipata kinyemela  kutaifishwa kulingana na kosa lake pia suala hili litamgusa kila mtu wakiwemo watumishi wa umma. Aidha alisema kurejeshwa kwa mali hizo kutawasaidia wananchi wa wilaya hiyo katika shughuli za kujiletea maendeleo na siyo kama ilivyo sasa kuwa baadhi ya watu wachache wananufaika na raslimali za umma.  “Ni kweli nimepokea barua toka halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikinitaka ndani ya siku 90 niwe nimerejesha kiwanja cha halmashauri ambacho ninafanya biashara ya kuuza mafuta pale nimeweka kituo cha kuuzia mafuta kwa kile kinachodaiwa kuwa nilikipata kwa njia zisizo halali,” alisema.
3
Faraja Masinde -Zanzibar RIPOTI ya pamoja iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Benki Kuu (BOT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Idara ya Uhamiaji na Tume ya Utalii ya Zanzibar (ZCT ), ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa kiwango cha mapato yanayotokana na sekta ya utalii kimeongezeka kwa asilimia 7.13 ikilinganishwa na mwaka 2017. Mapato hayo yametajwa kufikia kiasi cha Dola za Marekani bilioni 2.43 mwaka 2018 kutoka Dola bilioni 2.19 mwaka 2017, huku watalii waliotembelea Tanzania wakiongezeka kufikia milioni 1.49 ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo walikuwa ni milioni 1.33. Ripoti ya wageni wa kimataifa wanaotoka na kuingia ya mwaka 2017 iliyotolewa na (NBS), watalii waliotembelea nchini mwaka 2016 walikuwa ni milioni 1.2 ambapo idadi hiyo imegawanywa katika ukanda huku watalii kutoka Ulaya wakiwa wengi zaidi wakifuatiwa na Bara la Asia na Pacific kisha Amerika, Afika na Mashariki ya Kati. Kama hiyo haitoshi, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, siku chache zilizopita alifafanua kuwa Kampuni ya China National Travel Service Group Corporation (CTS), iko mbioni kuwekeza nchini katika sekta ya utalii, uwekezaji ambao utahusisha ujenzi wa hoteli Tanzania Bara na visiwani Zanzibar. Sekta ya utalii nchini inatajwa kuchangia asilimia12 ya ajira za moja kwa moja ambazo ni zaidi ya milioni moja, huku Watanzania wakiwa ni 467,000 sawa na asilimia 4.3 ya ajira zote. Pamoja na yote haya, ni wazi kuwa unapotaja sekta ya utalii nchini huwezi kuviacha visiwa vya Zanzibar ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kuchochea utalii. Kwa nyakati tofauti, visiwa hivyo vimekuwa kivutio kwa wageni wengi na hata kusaidia kamisheni ya utalii visiwani humo kuvuka malengo waliyojiwekea kama alivyonukuliwa kamishna wa utalii visiwani humo, Khamis Mbeto, mapema mwaka huu. “Kamisheni hiyo kwa sasa tayari imevuka malengo iliyoelekeza kuwa ifikapo mwaka 2020 Zanzibar itakuwa na watalii 500,000 ambapo kwa sasa tayari idadi ya watalii inakaribia kufikia 600,000 kabla ya mwaka 2020,” anasema Mbeto. Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa idadi kubwa ya watalii waliotembelea visiwa hivyo vyenye marashi ya karafuu, wamekuwa wakihitaji kupatiwa taarifa za kutosha kutoka kwa wenyeji wao watakao waongoza. Lakini changamoto imekuwa ni kwamba siyo kila mtu anaweweza kutoa taarifa sahihi kwa wageni na kuwashibisha maarifa ya kutosha juu ya visiwa hivi ikiwamo kama yanavyokuwa matarajio yao wakati wa kupanga safari hizo, kwani siyo kila mtu anaweza kujua historia ya visiwa hivyo vyema, achilia mbali changamoto ya lugha ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya wageni wanaofika visiwani humo hutumia lugha tofauti mbali na Kiswahili. Hii inasababisha baadhi ya wanaoongoza wageni kushindwa kuwapa taarifa sahihi zenye kuwawezesha kukata kiu yao ya kuufahamu vyema Mji wa Zanzibar. Hata vijana wa visiwa hivyo waliokuwa wakitamani kwenda darasani na kupata maarifa kwa ajili ya kuwasaidia kuongoza wageni kikamilifu ikiwamo kujiajiri waliishia kutamani kutokana na kushindwa kujimudu kifedha. Changamoto hiyo na nyinginezo ndizo zilizoisukuma Taasisi ya kimataifa ya Tui CareFoundation kuanzisha chuo cha Kawa Training Centre, kilichopo Mji Mkongwe kwa lengo maalumu la kusaidia maeneo muhimu ikiwamo kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaotaka kuongoza wageni. Tangu kuwapo kwa chuo hicho ni wazi kuwa imekuwa na mwamko katika kuchochea utalii visiwani humo, kwani vijana wengi wa kike na wa kiume waliohitimu chuoni hapo wamekuwa ni msaada mkubwa katika kuwaongoza wageni na kuchangia pato la taifa kwa ujumla. Mkurugenzi wa chuo hicho, kilichopo Mji Mkongwe, Suzanne Degeling, anafafanua kuwa uwapo wa chuo hicho umekuwa na msaada mkubwa katika kufanikisha shughuli za utalii visiwani humo. “Kwa kweli hili ni jambo la kujivunia kuona kwamba vijana wengi ambao awali walikuwa na ndoto ya kuwa waongoza watalii wametimiza ndoto zao na kuwa sehemu ya uchumi wa Zanzibar. “Baada ya kufika hapa miaka kadhaa iliyopita nikitokea nyumbani Uholanzi, nilibaini kuwa vijana wengi wanapenda kazi ya kuongoza wageni lakini hawana maarifa ya kutosha, nikalazimika kuanzisha chuo hiki kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali kwa nia moja tu ya kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao,” anasema Suzzane. Anasema licha ya kwamba mwanzo huwa mgumu, alipata nguvu baada ya kuungwa mkono na Shirika la Tui Care Foundation, lenye makao makuu yake nchini Ujerumani ambalo limejikita kuhamasisha utalii sehemu mbalimbali ulimwenguni. “Hivyo, walikuwa na ndoto za kutaka kuongoza watalii lakini walikuwa hawajui ni kwa namna gani wanaweza kuifanya kazi yao kwa ustadi mkubwa, hapo ndipo nikafikia hatua ya kuanzisha chuo hiki ili kuwasaidia vijana jambo ambalo limekuwa na mchango mkubwa kwao na jamii kwa ujumla,” anasema Suzzane. Anafafanua kuwa pamoja na kwamba awali ilikuwa ni ngumu kwa vijana wa Zanzibar kutumia fursa hiyo ya uwapo wa chuo hiko, lakini kwa sasa anafurahi kuona wengi wamekuwa na mwamko na kwa kiwango kikubwa wameweza kufanikiwa kupitia chuo hicho. “Awali wengi walikuwa wakiogopa kujiunga na chuo kwa sababu hawakuwa na fedha, nikatoa fursa kwa wenye nia ya dhati kuja kusoma kwa mkopo kwa kuwa lengo langu lilikuwa ni kuwaona wao wakifanikiwa kufikia malengo yao, fedha sikuzipa kipaumbele. “Leo nafurahia kuona kwamba maendeleo yameendelea kuwa mazuri, vijana wengi wameajiriwa na kujiajiri kupitia chuo hiki japo mwamko wa wasichana umekuwa ni hafifu ukilinganisha na wavulana ambao wamekuwa wengi zaidi. “Tunajitahidi kuona kuwa tunaondoa hii dhana ya kuamini kuwa kazi ya kuongoza watalii inapaswa kufanywa na wanaume pekee, tunaendelea kuwajengea vijana mtazamo wa kimataifa zaidi,” anasema Suzzane. Anasema anaamini kuwa kuandaa waongoza watalii waliobora kupitia chuo hicho ndiyo mwendelezo mzuri wa kuendelea kuwa na idadi kubwa ya wageni kwani wanapokuja na kupewa taarifa sahihi basi ni wazi kuwa wataenda kuwa mabalozi wazuri kwa wengine na hivyo kufanya ongezeko la pato la uchumi wa Zanzibar. “Tunawasaidia vijana kuwa sehemu ya uchumi wa nchi yao kwa kuchangia pato la taifa, ambapo kupitia ada wanazolipa kama waongozaji wageni zinaingia serikalini na hivyo kusaidia katika shughuli nyingine za maendeleo, hatimaye kuinua uchumi kwa ujumla. “Lakini mwisho wa yote nashukuru ushirikiano mkubwa ambao nimeendelea kuupata kutoka serikalini, ambao nao kwa kauli thabiti wanaunga mkono jitihada za Kawa,” anasema Suzzane. Mkurugenzi Mtendaji wa Masuala ya Nje na Maendeleo wa TUI Care Foundation, Alexander Panczuk, anafafanua kuwa wamekuwa bega kwa bega na chuo hicho cha Kawa ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa fedha na vifaa vya kufundishia ili kuwasaidia vijana kuhitimu na kuwa sehemu ya uchumi wa Zanzibar. “Tumekuwa na jukumu la kuimarisha maeneo mbalimbali ya utalii duniani, ndiyo maana hatukusita kuonyesha ushirikiano wetu kwenye chuo hiki ili kuimarisha utalii wa Zanzibar na uchumi wa visiwa hivi kwa ujumla kupitia pato linalotolewa na wahitimu wa chuo hiki pale watakapoanza kuongoza wageni, “Tutaendelea kuboresha mazingira mazuri zaidi ya utalii kwa sababu kwa kufanya hivyo tunakuwa tumeisaidia nchi husika katika kuongeza mapato yake na hivyo kunyanyua uchumi wake,” anasema Panczuk. Miongoni mwa wanafunzi walionufaika na uwapo wa chuo hicho ni Ally Mussa Jappe(24), ambaye anasema kuwa ni miongoni mwa vijana walionufaika na uwapo wa chuo hicho ambacho mbali na kupata mafunzo chuoni hapo, pia amekuwa mwalimu wa chuo hicho pamoja na muongoza watalii mahiri, jambo ambalo limebadilisha maisha yake kwa kiwango kikubwa. “Baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari, nilisikia juu ya kuwapo kwa chuo hiki cha Kawa Training Centre, nikasema ni sehemu ambayo naweza kupata uzoefu ikiwamo kuimarisha Kiingereza change. Nilijiunga hapa kwa nia ya kufahamu lugha na urithi wetu ambao tunao hapa Zanzibar. “Nafurahi kuona nimeweza kuwa sehemu ya vijana waonachangia pato la taifa kupitia sekta hii ya utalii, lakini mbali na kuingiza fedha pia imenisaidia kunijengea mtazamo wa kimataifa ninaoupata kutoka kwa wageni mbalimbali ninaowaongoza,” anasema Jappe. Anaongeza kuwa mbali na kufanikiwa kupata elimu na kuwa mwalimu chuoni hapo, anakiri kwamba Kawa wamekuwa na muunganiko wa kimataifa unaowasaidia vijana wengi kutimiza ndoto zao huku akigusia mtazamo wa wazazi. “Kumekuwa na changamoto mbalimbali zikiwamo kuwa na waongoza watalii wasiofuzu vyema mafunzo ya kuongoza watalii, lakini pia mtazamo hasi kutoka kwa wazazi wanaoamini kuwa kusomea masuala ya utalii ni uhuni. “Niwahimize wazazi kuwapa msukumo zaidi watoto wao kwani elimu ndiyo msingi na urithi pekee wanaoweza kuwaachia, tofauti na mali na fedha, thamani ya elimu ni kubwa zaidi,” anasema Jappe.
3
Na Kulwa Mzee-DAR ES SALAAM MWANAHABARI nguli Jenerali Ulimwengu, leo anatarajia  kuwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba kuungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  katika kesi ya katiba iliyofunguliwa hivi karibuni. Ulimwengu anaomba kuunganishwa katika kesi ya katiba namba 1 ya 2017 kama mdai dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. “Maombi ya kumuunganisha yameandaliwa na kesho(leo) yatakuwa mahakamani kuomba naye awe mdai. Anaomba kujiunga kwa kuwa mambo anayopigania Mbowe naye ana maslahi nayo kwa sababu ni mambo muhimu ya katiba,” alisema mmoja wa jopo la Mawakili kutoka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya Chadema, Peter Kibatala.   Katika kesi hiyo ya katiba, Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke   kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na kukamata. Mbowe pia anaomba mahakama itengue vifungu vya 5 &7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki ya katiba. Mbowe alifungua kesi hiyo akidai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekiuka sheria na taratibu katika kushughulikia watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini. Kesi hiyo ya katiba inasikilizwa na majaji watatu, Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday. Baada ya kufungua kesi hiyo Mbowe pia aliomba mahakama itoe amri asikamatwe mpaka maombi yake ya zuio yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi. Mahakama ilitoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi  kutomkamata Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani yatakaposikilizwa. Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki lakini upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata uliwasilisha pingamizi, ukiomba mahakama iyatupilie mbali kwa sababu  hana msingi katika sheria. Upande wa mdai ulijibu hoja za kupinga maombi yao na Mahakama ilisikiliza hoja za pande zote mbili na kupanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Machi 2, mwaka huu.
3
Na JANETH MUSHI UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi na kusababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 12.4, inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Otterlo Business Limited (OBC), Isaya Mollel, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa upelelezi uko katika hatua za mwisho. Jana mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Ahmed Khatibu na Hellen Osujaki (Takukuru) huku Mollel akiwakilishwa na mawakili Daudi Haraka, Goodluck Peter, Valentine Nyalu na Elvaison Maro. Wakili Khatibu alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa na kuwa Jamhuri wako katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wake na kuomba mahakama hiyo kuiahirisha na kuipangia tarehe nyingine. Upande wa utetezi wakiongozwa na wakili Maro, walikubaliana na hoja hiyo na kuieleza mahakama kuwa wanahifadhi hoja zao hadi hapo upande wa Jamhuri watakapokuwa wamekamilisha upelelezi ndipo wataziwasilisha. Hakimu Mwankuga alikubaliana na pande zote mbili na kuahirisha shauri hilo hadi Desemba 4 litakapotajwa tena. Awali Novemba 7, mwaka huu, kesi hiyo iliahirishwa kwa madai kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Martha Mahumbuga, anayepaswa kuisikiliza hakuwepo mahakamani. Aidha Oktoba 25, mwaka huu kesi hiyo iliahirishwa na kwamba madai mwafaka baina ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) na mawakili wa Mollel haujafikiwa. Oktoba 15 mwaka huu, shauri hilo lilipotajwa mahakamani hapo, wakili wake alidai Mollel amemwandikia barua DPP kuomba kukiri mashtaka 10 yaliyokuwa yanamkabili awali, yakiwemo ya utakatishaji fedha haramu, kukwepa kodi na kusababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 2.8 katika kesi ya awali. Katika kesi hiyo, moja ya mashtaka yanayomkabili Mollel ni kusababisha hasara ambapo ilidaiwa kati ya Januari 2010 na Aprili 2018 akiwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam na Arusha, aliwasilisha nyaraka za uongo, kushindwa kulipa kodi mbalimbali za Serikali, aliisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 12.4.
3
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime- Rorya, limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi akiwemo aliyewahi kudaiwa kunyang’anywa bunduki aina ya SMG na mwanamke mkazi wa Buriba katika Kata ya Sirari wilayani Tarime.Kamanda wa Polisi wa Tarime-Rorya, Henry Mwaibambe alisema jana katika tukio hilo, zimepatikana bunduki 2; moja AK 47 na goboro, na risasi 5 zikiwa ndani ya magazine.Alisema majambazi hao walikufa Novemba 7, mwaka huu saa nne usiku baada ya majibizano ya risasi walipovamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa samaki, David Ogutu maarufu Baba Ouma Kijiji cha Obwere Shirati wilayani Rorya kupora fedha.“Kundi la majambazi hao likiwa limejihami kwa silaha za moto, lilivamia nyumbani kwa mfanyabaishara huyu wa samaki kwa nia ya kufanya uhalifu wa kupora fedha; walifyatua risasi hewani kuwatishia wananchi wasijitokeze kutoa msaada lakini mfanyabiashara huyo alipiga simu kwa askari polisi Kituo cha Shirati waliofika,” alisema Mwaibambe.Aliongeza kuwa, “majambazi hao walipowaona polisi, waliwarushia risasi na kuanza majibizano ya risasi hatimaye polisi kufanikiwa kuwajeruhi majambazi hao watatu… wananchi na polisi walifuatia nyayo na damu iliyoonekana katika eneo la tukio.”Kutokana na mwito wa polisi wa kutaka taarifa zitolewe mapema kuhusu watu watakaoonekana wamejeruhiwa, siku iliyofuata (Novemba 8, mwaka huu), wananchi Mjini Tarime walimwona mtu aliyejitambulisha kwa jina la Kesanta Chacha akiwa na majeraha amejifunika jaketi akipanda gari dogo la abiria kutaka kwenda Sirari.Kamanda Mwaibambe alisema walimtilia shaka na kutoa taarifa kwa polisi kabla gari hilo halijaondoka na kumkamata mkazi huyo wa Kebeyo aliyewahi kupatikana na bunduki AK 47, lakini akaachiwa na mahakama akiwa na umri wa takriban miaka 16.
3
THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM KIKOSI cha Simba, kinatarajia kuendelea na mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, ukiwa ni kiashiria cha ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mbali ya mchezo huo utakaochezwa Agosti 17, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mazoezi hayo pia ni maandalizi ya kipute cha marudiano cha Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji. Katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye Uwanja wa Estadio da HCB, jijini Beira, Simba iliwabana UD Songo na kutoka nao suluhu. Akizungumza na MTANZANIA jana, kocha wa viungo wa timu ya Simba, Aden Zrane, alisema waliwapa wachezaji wao mapumziko ya siku moja kwa sababu ya Sikukuu na leo wataendelea na mazoezi. “Tulivyorejea, tulifanya mazoezi katika viwanja vya Gymkhana, lakini leo (jana), tuliwapa mapumziko wachezaji na baada ya hapo, tutaendelea na mazoezi kujiandaa na michezo inayotukabili mbele yetu,” alisema. Alisema wanahitaji kuwaweka fiti zaidi wachezaji wao, kutokana na kukabiliwa na mechi ngumu na zenye ushindani. Simba ndio mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii, waliyoitwaa msimu uliopita kwa kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Simba imepania kuendeleza ubabe wake msimu huu katika kila michuano watakayoshiriki, kuanzia Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na mingineyo.
4
Mwandishi Wetu -Dar es salaam KAULI ya Jeshi la Polisi kwamba Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula alipewa sumu, imeacha maswali mengi na mjadala mkubwa miongoni mwa jamii. Februari 28, mwaka huu, Mangula alidondoka ghafla katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichokuwa kikijadili masuala mbalimbali, ikiwamo adhabu kwa wanachama watatu waliokuwa na tuhuma za ukiukwaji wa maadili ndani ya chama hicho. Katika kikao hicho, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alivuliwa uanachama kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na kanuni ya maadili na uongozi. Tuhuma hizo pia zilikuwa zikiwakabili makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ambaye atakuwa chini ya uangalizi kwa miezi 18 na Yusuf Makamba aliyesamehewa makosa yake. Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, wamebaini ndani ya mwili wa Mangula kulipatikana sumu. “Machi 2 tulipokea taarifa kutoka uongozi wa CCM kuhusu kuwekewa sumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mangula. Katika taarifa hiyo tulielezwa kwamba Mangula alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kulazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU). “Uchunguzi kuhusu tuhuma ya sumu hiyo ilivyoingia mwilini upelelezi bado unaendelea. Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kupanga, kuratibu au kusimamia utekelezaji wa uhalifu huo. “Haitajalisha awe ni mwanafamilia, awe ni mtu kutoka ndani ya CCM au vyama vingine vya siasa, mwananchi wa kawaida, awe ndani au nje ya nchi, awe serikalini au taasisi yoyote hatua kali zitachukuliwa,” alisema Mambosasa. Aliwataka wananchi wajiepushe na vitendo hivyo kwani si tu vya kinyama, bali pia vinalenga kukiuka sheria za nchi. MASWALI KUMI TATA Kutokana na uzito wa tukio hilo bado limezua sintofahamu katika jamii, huku kukiibuka maswali ambayo hadi sasa bado yamekosa majibu na kusubiri taarifa ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi. Baadhi ya maswali hayo ambayo jamii inahitaji kujua majibu yake ni kwamba Mangula alikuwa wapi baada ya kutoka nyumbani kwake. Je, aliamkia wapi? Kifungua kimya gani alipata? Usafiri gani alitumia kwa siku hiyo kabla ya kuanguka? Je, alisalimiana na nani? Je, ofisini aliingia saa ngapi na alikutana na nani? Je ni nani alimuhudumia kupata kifungua kinywa ? Je wakati wa kikao alikula na kunywa? Je, alihudumiwaje? Na mfumo wa huduma ulikuwaje? Pamoja na hayo bado Watanzania wanasubiri na kutaka kujua maendeleo ya afya yake. JPM ALIVYOMJULIA HALI Februari 29, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea na kumjulia hali Mangula ambaye alikuwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Ikulu, Gerson Msingwa, Mangula aliugua ghafla na kisha kukimbizwa hospitali kwa matibabu. Kwa mujibu wa video za Ikulu, Magufuli alionekana akimwombea Mangula kupona kwa haraka. “Utapona na Mungu atakusimamia utarejea katika majukumu yako, nilikuona jana (Februari 28) umeanguka,  ilitushtua,” alisema Rais Magufuli huku Mangula akisema “sijui niliangukaje.” Hata hivyo Rais Magufuli, alisema kuwa hawezi kujua kwani wanamkabidhi Mungu ambaye atamsimamia siku zote kwa sababu wanadamu wanalindwa na Mungu ambaye huwapenda sana. Rais Magufuli alimwomba Mangula kufanya ibada hospitalini hapo na alifanya hivyo. VIONGOZI NA SUMU Novemba 12, 2019 Rais Magufuli alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya tatu, alinyweshwa sumu kutokana na utendaji wake wa kazi. Alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa kilichoelezea maisha yake. “Tulipofanya kazi vizuri kwenye kujenga barabara, mzee Mkapa alifurahi sana, akatamka kwamba mimi ni askari wake wa mwavuli namba moja, ameligusia hili kwenye ukurasa wa 107 wa kitabu chake.
0
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imesema uhalifu kwa ujumla umepungua kwa asilimia 1.4 kutoka matukio 34,998 mwaka 2017 hadi matukio 34,518 mwaka huu sawa na upungufu wa matukio 480.Aidha, matukio makubwa yaliyoripotiwa katika jeshi hilo mwaka huu ni 3,231 ukilinganisha na matukio ya mwaka jana, ambayo ni 4,086 sawa na upungufu wa matukio 855 ikiwa ni sawa na asilimia 21. Pia jeshi hilo limekusanya zaidi ya Sh bilioni 29.3 za faini ya makosa 762,710 ya usalama barabarani kwa mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mkoa wa Kipolisi unaoongoza kwa matukio ya uhalifu kwa mwaka huu ni Kinondoni yenye matukio 15,502, ikifuatiwa na Ilala matukio 10,040 na Temeke yenye matukio 8,969. Mambosasa alisema kuwa matukio ya jinai yaliyoripotiwa kwenye kanda hiyo ni kwamba matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yamepungua kutoka 31 mwaka jana hadi sita mwaka huu sawa na asilimia 81, matukio ya unyang’anyi kwa kutumia nguvu pia yamepungua kutoka 140 hadi 57 sawa na asilimia 59.3.‘’Matukio ya uvunjaji kwa mwaka 2017 yalikuwa 1,150 lakini yamepungua hadi kufikia 885 sawa na asilimia 23, wizi wa magari umepungua kutoka 69 hadi 42 sawa na asilimia 39.1, wizi wa pikipiki umepungua kutoka 538 hadi 455 sawa na asilimia 15.4 na wizi wa mifugo umeongezeka kwa matukio mawili kwa maana mwaka 2017 yalikuwa 46 na mwaka huu 48,’’ alisema Kamanda Mambosasa. Pia alisema matukio ya mauaji yamepungua kutoka 77 mwaka jana hadi 66 mwaka huu na kwamba inajumuisha upatikanaji wa miili ya watu waliokutwa wamekufa katika ufukwe wa Coco, hivyo upungufu huo ni sawa na asilimia 21.Alisisitiza ubakaji umepungua kutoka matukio 324 mwaka jana hadi kufikia matukio 252 mwaka huu sawa na asilimia 22.2, ulawiti umepungua kutoka matukio 107 hadi 85 ambayo ni sawa na asilimia 20 huku matukio ya wizi wa watoto yakipungua kutoka matukio sita hadi matano. Pamoja na hayo, matukio ya kutupa watoto yamepungua kutoka 10 hadi sita ikiwa ni sawa na asilimia 40 na matukio ya kudhuru binadamu hayakuwepo kabisa ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na matukio matatu. ‘’Kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka huu majambazi sugu nane walikamatwa kutokana na makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, nguvu uvunjaji na wizi wa magari,’’ alisema.Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani, Kamanda Mambosasa alisema kutokana na kupungua kwa makosa hayo, kumesaidia kupungua kwa ajali ukilinganisha na mwaka jana. Kuhusu mwaka mpya Mambosasa alisema wamejipanga kuhakikisha wakazi wa mkoa huo wanasherehekea sikukuu za Mwaka Mpya kwa amani na usalama kuanzia wakati wa ibada hadi kurudi majumbani mwao. ‘’Ni marufuku kuchoma matairi kwani hatutawavumilia vitendo hivi vikiendelea hivyo mnapaswa kujiepusha kwa sababu tutawakamata.Ni marufuku kufunga barabara kwa moto wala kutumia milipuko yoyote kwani hairuhusiwi,’’ alisema Mambosasa. Alifafanua kuwa zipo baadhi ya hoteli za nyota tano, ambazo zimeruhusiwa kupiga fataki kwa sababu kuna wageni wenye utamaduni huo na kuonya kutopiga fataki zenye vishindo vya mabomu. Alisema fataki zinazopaswa kupigwa na wamiliki wa hoteli hizo ni zile nyepesi zisizoleta mshituko kwa wananchi, ambazo zitapigwa kwa dakika tano na kwamba tayari wameagiza wakaguzi kuhakikisha wanafuatilia suala hilo ili kutokiuka masharti waliyopewa.
3
Serengeti Boys ilitwaa ubingwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuifunga Somalia mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Bujumbura, Burundi.Timu hiyo iliyopangwa kundi B ilianza mashindano kwa kutoka sare ya 1-1 na Uganda, wakawachapa Sudan 6-0 kisha wakawafunga Kenya 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali.Akizungumza wakati wa mapokezi ya timu hiyo ilipotua nchini alfajiri ya jana, Mwakyembe alisema kuwa kitendo kilichofanywa na vijana hao ni cha kishujaa na ndio maana Watanzania wengi wamejitokeza kuwapokea.Amesema kwa muda mrefu nchi imekuwa na hamu ya kuona ikipata ushindi kimataifa hivyo vijana hao wanastahili kupewa sifa kwa kitendo walichokifanya.Amesema ubingwa huo umetoa taswira ya wazi kwa jinsi uwekezaji wa maana umefanyika katika kuinua soka la vijana na ana imani kubwa kuwa mambo mazuri yatazidi kujitokeza siku zijazo.Ameagiza kuwa licha ya kutwaa ubingwa huo, lakini vijana hao wasiache tu bali wanatakiwa waongezewe mazoezi ya kiufundi pamoja na kupewa mechi nyingi za kimataifa ambapo zitasaidia kuwajenga zaidi ya hapa.“Vijana wetu wamefanya kitendo cha kishujaa ndio maana mpaka sasa watu tumejitokeza kuwapokea, hii inaonesha jinsi tulivyowekeza kwa Serengeti, mwaka jana tumeona kule Gabon wakifanya vizuri tunaamini tutazidi kufanya vizuri kwenye mashindano yajayo.“Tumejipanga vizuri tunawaandaa kwa ajili ya mashindano ya mwakani, sisi timu yetu ilikuwa ndio na vijana wadogo kuliko wenzetu, vijana wetu wameshinda kwa weledi na sio nguvu hivyo tunatakiwa kuwapa mechi za kimataifa ili waweze kufanya vizuri zaidi,” amesema Mwakyembe.
4
MCHEZAJI mkongwe wa TP Mazembe, Tresor Mputu amesema timu yao itakuwa ya kwanza kuifunga Simba nyumbani kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Simba ina sifa ya kutopoteza mechi za nyumbani kwenye michuano hiyo tangu hatua ya awali. Mazembe iliwasili nchini juzi kwa ajili ya kuikabili Simba kwenye mechi ya robo fainali ya michuano hiyo inayotarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mputu aliyasema hayo baada ya kuwasili nchini ambapo alisema anajua kuwa Simba ni timu inayocheza mchezo wa nguvu na inayofanya vizuri kwenye uwanja wake hivyo wamejiandaa kupambana na kuwashangaza.“Tunajua Simba wanafanya vizuri nyumbani tumekuja kucheza nao, tutafanya nguvu tushinde na kuwa timu ya kwanza kuwafunga nyumbani kwao,” alisema. Aliongeza kuwa, “tumekuja kucheza kabumbu, mechi itakuwa nzuri sana, tunajua Simba ni timu ya nguvu sana na sisi tutafanya nguvu tushinde mechi.” Wekundu wa Msimbazi waliokuwa Morogoro kwa ajili ya mechi ya ligi iliyokuwa ichezwe juzi dhidi ya JKT Tanzania ilitarajiwa kuwasili jana Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo.Hata hivyo, Simba haikucheza mchezo huo wa ligi na kuahirishwa baada ya kunyesha mvua kubwa. Awali, Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori alisema atahakikisha timu hiyo inaweka historia nyingine kwa kufanya vizuri hatua hiyo ya mtoano kushinda nyumbani na kujipanga zaidi kwa ugenini. Alisema malengo yao ni kufika fainali na kwamba watajipanga kutimiza kile walichokusudia. Mara ya mwisho wekundu hao kufika fainali za michuano ya kimataifa ilikuwa mwaka 1993 na tangu hapo hakuna timu yoyote ya Tanzania iliyofikia mafanikio hayo.
4
TAKRIBAN mwaka mmoja tangu alipoteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), nyota ya Kamishna wa Polisi, Diwani Athuman Msuya, imezidi kung’aa. Septemba 6, mwaka jana, Rais Magufuli alimteua Kamishna Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, lakini jana akamteua na kumuapisha kuongoza taasisi nyingine nyeti nchini, Idara ya Usalama wa Taifa. Kuanzia jana, Kamishna Athuman anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, akichukua nafasi ya Dk Modestus Kapilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Kamishna Athuman aliteuliwa na kuapishwa jana kushika wadhifa huo nyeti nchini. Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Kamishna Athuman kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.Ikumbukwe kabla ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takururu, Kamishna Athuman alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera (RAS), wadhifa ambao aliteuliwa kuanzia Novemba 18, 2016 na kudumu nao hadi Septemba 6, mwaka jana. Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Kamishna Athuman alikuwa ameondolewa katika wadhifa wake wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), hatua ambayo ilionekana kama vile ndio ametupwa benchi moja kwa moja. Mbali ya kushika wadhifa wa DCI, Kamishna Athumani pia amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
3
Elizabeth Joachim Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani  Jafo, amewataka viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abuubakar Zubeiry, kuombea baadhi ya mambo machafu machafu yanayoendelea nchini. Jafo ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 20, akimwakilisha Rais Magufuli katika Baraza Kuu la Maulidi ambalo kitaifa limefanyika Korogwe, mkoani Tanga. “Mambo hayo machafu machafu yanayoendelea kufanyika nchini na kusababisha mmonyoko wa maadili hayana budi kuombewa,” amesema Jafo. Aidha, jafo pia amewataka viongozi hao kuendelea kumuombea Rais John Magufuli, ili aendelee kuleta maendeleo ya nchi hasa katika suala la elimu , miundombinu, viwanda na katika sekta ya afya. “Maendeleo yaliyopo katika nchi yetu si watu wote wanapenda, kuna wengine wanapenda yaharibike lakini kupitia dua zenu mambo yataenda sawa. “Mwaka 2015 kuelekea 2016 kulitokea tatizo la ukame ambalo lilisababisha mifugo mingi kufa lakini ndani ya miaka mitatu ya serikali ya Rais Magufuli tatizo hilo limekwisha hii ni moja ya maendeleo,” amesema Jafo.
0
LONDON, UINGEREZA MAHAKAMA ya Juu nchini Uingereza imesema Waziri Mkuu Theresa May lazima apate idhini ya Bunge kabla ya kuanzisha mchakato wa nchi hiyo kujiondoa Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit. “Leo (jana) kwa wingi wa majaji wanane dhidi ya watatu, mahakama inahukumu kuwa Serikali haiwezi kuanzisha kipengele cha 50 kama inavyotaka bila sheria ya Bunge inayoiruhusu kufanya hivyo,” alisema Jaji David Neuberger wakati akisoma hukumu hiyo. Katika hukumu hiyo, mahakama ilisema muswada kama huo ambao unatarajiwa kupelekwa bungeni ama baadae wiki hii au wiki ijayo, unaweza kuwa mkataba mfupi sana. Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo, waziri anayehusika na Brexit, David Davis, alisema Serikali itawasilisha sheria ya waziwazi ndani ya siku chache kutaka idhini ya Bunge kuanzisha mchakato huo. “Tutawasilisha ndani ya siku chache zijazo muswada wa sheria kuipa Serikali mamlaka ya kisheria ya kuanzisha kipengele cha 50 na kuanza mchakato rasmi wa kujiondoa,” alisema Davis na kuongeza kuwa huu ndiyo utakuwa muswada wa wazi zaidi iwezekanavyo kutekeleza uamuzi wa watu na kuheshimu hukumu ya Mahakama ya Juu. mwanaharakati Gine Miller ndiye aliyefungua shauri hilo mahakamani, akitaka Bunge liwe na usemi katika kuanzisha mchakato wa Brexit. Wakati wa kura za maoni kuhusu kujiondoa Umoja wa Ulaya, wabunge wengi walipiga kura kutaka Uingereza ibakie katika chombo hicho. Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani cha Labour, kilisema hakitazuia Brexit ingawa kitajaribu kuifanyia marekebisho sheria hiyo. Taarifa za vyombo vya habari zimesema wabunge 80 wa Labour kati ya 650 katika Bunge la Uingereza watapuuza msimamo wa Kiongozi wa chama chao, Jeremy Corbyn, na kupiga kura kupinga kuanzisha mchakato huo. Aidha chama kidogo cha Liberal Democratic kimesema kitapinga mchakato mzima wa Brexit isipokuwa iitishwe kura ya pili ya maoni kuhusu makubaliano ya mwisho. Wakati huo huo, Waziri Kiongozi wa Scotland, Nicolas Sturgeon ameibua uwezekano wa kura nyingine ya kutaka uhuru wa Scotland baada ya mahakama hiyo kuamua kwamba Bunge la Scotland halihitaji kushauriwa kuhusu kuanzisha mchakato wa Brexit.
2
WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wametakiwa kutojiingiza katika migongano ya kisiasa, bali watekeleze wajibu wao kama wataalamu wa serikali katika halmashauri hiyo. Wito huo ulitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Anna Chambala alipokuwa akitoa salamu za chama katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika kumbi wa FDC wilayani humo. Alisema halmashauri ndiyo mtekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na wataalamu wa halmashauri ndio wamepewa dhamana ya kuhakikisha miradi ya wananchi iliyoainishwa inatekelezwa kwa vitendo kinyume na hapo chama hakitawafumbia macho.Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo kujiingiza katika mihemko ya kisiasa, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wao. Alibainisha wazi kuwa CCM haiingilii utendaji wa halmashauri lakini inapoona mtumishi wa umma anashadadia migongano ya kisiasa ambayo inaweza kuathiri utendaji wa halmashauri lazima wasimame na kukemea hali hiyo. ‘CCM haitamvumilia mtumishi yeyote wa halmashauri anayejiingiza katika malumbano au migongano ya kisiasa badala ya kufanya kazi yake ya kitaalamu iliyomleta, siasa waachie wanasiasa wenyewe’, alisema.Alionya kuwa chama tawala hakitasita kuchukua hatua kwa mtumishi yeyote wa umma anakayejiingiza katika vurugu au migongano ya kisiasa badala ya kutekeleza majukumu yake ya kitaalamu. Alifafanua kuwa migongano ya kisiasa inaathiri shughuli za maendeleo ya wananchi, na mtaalamu yeyote akijiingiza huko hawezi kutekeleza wajibu wake ipasavyo. Aidha, aliwataka viongozi wote katika halmashauri hiyo kuanzia DC, Mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji, Wataalamu na Watendaji wote kuwa kitu kimoja ili kuharakisha maendeleo ya wananchi. Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo aliyemaliza muda wake Upendo Mgombozi na Mrithi wake Juma Rajabu Mdullah waliunga mkono kauli ya Mwenyekiti huyo na kuwataka wataalamu hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wabadilike ili kwenda na kauli mbiu ya hapa kazi tu na si vinginevyo.
3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema, hafurahii kuendelea kuongoza wanawake walioumizwa mioyo kwa kuahidiwa kuolewa na kuachwa.Amesema, ataangalia namna ya kukomesha tabia ya wanaume waliooa kuwa na mahusiano nje ya ndoa zao na kuwadanganya wanawake kuwa watawaoa.Ametoa mwito kwa wanaume wanaopenda kuahidi ndoa watoe mawazo yao kuhusu jambo hilo na kwamba, huenda baadhi yao wanahitaji maombi tu.“Inawezekana ukaona ni jambo la kawaida kwa sababu hujawahi kuumizwa katika mahusiano lakini walioumizwa wanajua mateso waliyokuwanayo na ndio maana hata akija kazini ana hasira tu kumbe kuna mtu ameshamuumiza, inapunguza hata performance ya utendaji wake wa kazi”amesema Makonda ofisini kwake.Amesema, ipo haja ya kuwaita akina dada walioahidiwa kuolewa na wakaachwa ili wasaidiwe na hatimaye Dar es Salaam iwe yenye amani na utulivu kwa kuwa usalama wa taasisi ya ndoa ni usalama wa jamii na taifa kwa ujumla.“Lakini yapo mawazo ya kwamba yawezekana tuanzishe database (kanzi data) ya kuingiza taarifa za ndoa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo itamwezesha binti akiahidiwa kuolewa ana uwezo wa kuingia kwenye hiyo data base akaangalia jina…”Amesema itaanzishwa kanzi data yenye taarifa sahihi za ndoa za kiislamu na kikristu na kwamba, vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) vitasaidia kufanikisha hilo.“kama ni mwanaume anaitwa Paul Makonda ataingia ataangalia, kama ni ahadi ya ndoa atapata taarifa huyu ameoa, na kama ameoa atajua cha kufanya, lengo ni kuwaepusha akina dada wasiendelee kuumia na matapeli wanaoahidi kuwaoa na mwisho wa siku wanatumia mali zao, na kuwatumia, na kuwa-abandon (kuwaacha) bila kuendeleza kutumia ndoto walizokuwanazo”amesema.Amesema, anatumaini kutakuwa na mjadala mpana kwa kuwashirikisha wananchi na kwamba, Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali utatumika kupata mawazo na uzoefu wa nchi nyingine kuhusu jambo hilo.
3
OFISA Wanyamapori wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, Shaban Matwili amenusurika kifo wakati akijaribu kumuua nyati aliyevamia makazi ya watu katika Mtaa wa Kakese, Manispaa ya Mpanda na kujeruhi watu wawili.Amebainisha mjini Mpanda kuwa kilichomuokoa asiuawe na nyati huyo ambaye alikuwa tayari amempiga risasi ya moto na kumjeruhi, ni kwamba alilala chali.“Majukumu yangu ya kikazi ni kusimamia rasilimali za wanyamapori katika Halmashauri ya Nsimbo na maeneo mengine ambayo yamehifadhiwa katika Wilaya ya Mpanda, pia yale ambayo hayajahifadhiwa,”amesema.Akisimulia mkasa huo, alisema ulitokea hivi karibuni ambako nyati alivamia Mtaa wa Kakese jioni na kuzua taharuki kubwa baada ya kuanza kuwakimbiza watu mtaani hapo.“Nyati huyu alivamia na kuzua taharuki kubwa katika Mtaa wa Kakese, Manispaa ya Mpanda alikuwa akikimbiza watu ambapo alijeruhi watu wawili, baada ya kupokea taarifa kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa nilifika eneo la tukio saa 10:00 jioni …. Nyati huyo alikuwa amejificha kichakani hivyo kulikuwa hakuna haja ya kumswaga, nilipiga risasi na akaanguka chini nilijongea ili kujiridhisha kama nimemuua, ghafla aliamka na kuchachamaa,”amebainisha.Aliongeza kuwa alipoona mnyama huyo anakimbilia upande wake, alimfyatulia risasi shingoni, lakini aliendelea kumsogelea kwa kasi alikokuwa amesimama ambapo aliamua kulala chali.“Nilifanya maamuzi ya haraka ili kunusuru maisha yangu, nililala chali, nyati huyo alifika na kuanza kunishambulia kwa pembe zake, alinipiga pembe chini ya kwapa na kunitoboa, bila shaka alidhani ameniua kwani aliondoka na kuniacha hapo,”alisema.Aliongeza kuwa kwa ujasiri aliinuka na kumuua nyati huyo baada ya kupiga risasi za moto.“Nilikimbizwa na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi mjini Mpanda na kuruhusiwa kurejea nyumbani...wakati huo huo niliacha ugawaji nyama ya nyati hiyo kwa wananchi ukiendelea chini ya usimamizi wa viongozi wa mtaa huo,”alieleza.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wakazi wa Manispaa ya Mpanda wamekiri kujawa hofu ya usalama wa maisha yao kutokana na wanyamapori wakiwemo viboko na nyati kuvamia makazi yao mchana na kuzua taharuki kubwa miongoni mwao.
3
IS-HAKA OMAR-ZANZIBAR NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema chama hicho kimejizatiti kutatua kero za wananchi   na kusimamia demokrasia kwa kukemea vitendo viovu vinavyohatarisha amani na utulivu wa nchi. Kauli hiyo aliitoa katika ziara yake ya kukagua uhai na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja. Alisema vipaumbele   ni kutekeleza kwa kasi ahadi zilizotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi wakati wa  Uchaguzi Mkuu uliopita. Alisema CCM kinaendelea kuaminiwa, kupendwa na kuthaminiwa na mamilioni ya Watanzania kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa sera zake  kwa kutatua changamoto za  jamii kwa wakati mwafaka.   Dk. Mabodi alisema katika kusimamia dhana ya demokrasia, CCM haitasita kukemea vitendo viovu vinavyoonyesha  kuvunja sheria za nchi, hasa vinavyotekelezwa na baadhi ya vyama vya upinzani. “Tumekubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi  tushindane kwa sera na siyo kushindana kwa vituko na vurugu. “Ni muhimu kila mwanasiasa kujitathimini juu ya mwenendo wake kwa jamii anayoiongoza,” alisema Dk. Mabodi. Alisema zama hizi CCM mpya imekuwa ni kimbilio la wananchi wanaoamini katika siasa za maendeleo ambao wametelekezwa na vyama vyao na kupokewa  vizuri ndani ya chama hicho ili wanufaike na demokrasia iliyotukuka. Aliwataka viongozi na watendaji wa CCM kutowawekea vikwazo wananchi wanaotaka  kujiunga na chama na badala yake wapewe fursa hiyo bila masharti magumu   na kuwasomea miongozo na itikadi za taasisi.
3
NA BADI MCHOMOLO WANAMICHEZO wengi wanakuwa matajiri sio kwa sababu ya mishahara wanayolipwa kwa wiki au mwezi kwenye timu zao, kuna kiasi kikubwa cha fedha ambacho wanakipata zaidi ya mishahara kutokana na mikataba ya matangazo. Mbali na kufanya matangazo, wanamichezo wengi wanatumia kiasi chao kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye biashara mbalimbali ili kuja kunufaika mara baada ya kutangaza kustaafu mchezo husika. Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya wanamichezo matajiri duniani, mchezaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Juventus ya nchini Italia akitokea Real Madrid wakati huu wa majira ya joto, anaongoza kwa kuchukua kiasi kikubwa kuliko wanasoka wote nchini Italia. Anachukua kiasi cha pauni milioni 19.4 kwa mwaka, huku kabla ya mchezaji huyo alikuwa anaongoza Gonzalo Higuain anayechukua kiasi cha pauni milioni 8.6 kwa mwaka baada ya kuondoka Juventus na kujiunga na AC Milan. Hata hiyo Ronaldo anachukua kiasi cha pauni 538,000 kwa wiki, ambazo ni zaidi ya bilioni 1 na milioni 500 kwa wiki kabla ya kufanyiwa makato mbalimbali ya kodi. Kwa sasa tajiri huyo ameingia kwenye kesi ya kashfa ya ubakaji, ambapo tukio hilo alilifanya mwaka 2009, katika hoteli jijini Las Vegas. Inadaiwa kwamba mchezaji huyo alilazimisha kufanya mapenzi na mrembo Kathryn Mayorga, kitendo hicho cha ulazimishaji kinajulikana kama ubakaji. Hata hivyo Ronaldo mwenyewe amekanusha kashfa hiyo, huku polisi jijini Las Vegas wakiweka wazi kuwa, wapo kwenye uchunguzi wa tukio hilo ambalo lilitokea miaka tisa iliopita. Katika wachezaji wa soka, Ronaldo anatajwa kuongoza kwa kuwa na mikataba mingi ya matangazo na makampuni ya biashara kama vile Nike, Herbalife, JBS, Samsung, Exness, PanzerGlass, Egyptian Steel, American Tourister, EA Sports na Toyota. Hizo ni baadhi za kampuni ambazo hadi sasa bado ana mkataba nazo na zinamfanya aonekane kuwa miongoni mwa wachezaji matajiri kutokana na kiasi cha fedha anazochukua kwa kila kampuni hadi sasa. Mwaka 2010 mchezaji huyo alisaini mkataba wa maisha na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike, huku mkataba huo ukitajwa kuwa na thamani ya dola bilioni 1. Lakini baada ya wiki iliopita kuenea kwa taarifa za kashfa ya ubakaji kwa mchezaji huyo, Nike imeonesha dalili za kutaka kuvunja mkataba na mchezaji huyo. Nike wamedai kuwa, kwa sasa wanasubiri uchunguzi unaofanywa na polisi juu ya tuhuma hizo ili na wao waweze kuchukua hatua, wamesema hawawezi kusapoti vitendo hivyo vya unyanyasaji wa kijinsia kama tuhuma hizo zitakuwa za kweli. Nike imekuwa ikipambana kumtengenezea viatu mchezaji huyo ambapo hadi sasa tangu mwaka 2003 ametengenezewa zaidi ya viatu 70 vyenye muonekano tofauti uwanjani. Mbali na Nike kuoneshwa kuguswa na kitendo hicho, kampuni ya EA Sports, imejitokeza na kusema wanafuatilia tuhuma ambazo zinamkumba mchezaji huyo na kama zitakuwa na ukweli basi na wao watatoa tamko lao. Hizo ni baadhi ya kampuni ambazo anazitangazia mchezaji huo na kumuongezea kipato chake, lakini kama kutakuwa na ukweli wa tuhuma hizo basi kuna uwezekano mkubwa wa kampuni zingine kujitokeza na kutoa matamko mazito. Endapo itafikia hatua hiyo, basi Ronaldo atapoteza kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinamfanya awe juu katika pato la mwaka. Klabu ya Juventus kwa kutetea maslahi yao wameonesha wazi kumtetea mchezaji huyo huku wakidai kuwa ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu hivyo hawezi kufanya jambo kama hilo. Makampuni ya matangazo siku zote yamekuwa yakijitoa kwa mastaa ambao wanafanya kitu kinachopingwa na jamii. Bingwa wa zamani wa mchezo wa tenisi kwa upande wa wanawake nchini Urusi, Maria Sharapova, aliwahi kuingia kwenye msukosuko wa baadhi ya kampuni kujitoa kwenye udhamini baada ya kugundulika kuwa alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni. Tukio hilo lilitokea mwaka 2016, hivyo Nike ambao walikuwa miongoni mwa kampuni ambazo zilikuwa zinamdhamini mchezaji huyo ilitangaza kuvunja mkataba wake wa udhamini na mchezaji huyo.
4
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao  Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40)  na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele  ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa  kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020  maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam  kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
5
LONDON, UINGEREZA KUNDI la madaktari na wataalamu wa saikolojia wapatao 120 wametoa wito wa dharura, kutaka mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange, apewe huduma nzuri za afya. Katika waraka waliouchapisha katika jarida maarifa la kitabibu la The Lancet, wataalamu hao wamesema Assange ambaye hivi sasa yuko jela, amepitia mateso ya kisaikolojia na mahitaji yake kiafya kupuuzwa. Waliema katika waraka huo kuwa Assange anateseka kutokana na athari za kuzuiliwa kwa muda mrefu katika ubalozi wa Equador mjini London, na baadaye kufungwa katika jela lenye ulinzi mkali la Belmarsh jijini humo. Kwa mujibu wa wataalamu hao, upo uwezekano wa Assange mwenye umri wa miaka 48 kufia gerezani. Julian Assange anayetafutwa na Marekani, amekuwa katika gereza la Belmarsh mashariki mwa London tangu Aprili mwaka 2019. Madaktari hao pamoja na Shirika la Kutetea Haki za Waandishi wa Habari Ulimwenguni (RSF) wanasema mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange anayeshikiliwa nchini Uingereza anateswa kisaikolojia. Madaktari hao zaidi ya 100 pamoja na Shirika la Kutetea Haki za Waandishi wa Habari Ulimwenguni, RSF, wanasema Assange anayeshikiliwa nchini Uingereza anateswa kisaikolojia kwa kwa kutopewa huduma bora ya kiafya. Hayo yamo kwenye barua iliyoandikwa na madaktari na shirika hilo wiki moja kabla ya mahakama ya Uingrereza kuanza kusikiliza kesi ya Assange, ambayo huenda ikaamuwa apelekwe Marekani. Madakatari hao  pamoja na shirika la waandishi wasiokuwa na mipaka ( Reporters Sans Frontieres) wamelaani mateso ya kisaikolojia anayofanyiwa kiongozi huyo wa mtandao wa WikiLeaks ambaye yuko hatarini kupelekwa Marekani ili kujibu mashtaka ya ujasusi. Kwenye barua ya pamoja iliyotangazwa kwenye gazeti la kitabibu la Uingereza, The Lancet, kundi hilo la madakatari 117 kutoka nchi 18 wameituhumu serikali ya Uingereza kukanyaga haki za kimsingi za Julian Assange za kupata matibabu. Tuhuma hizo zimekuja wiki moja kabla  ya mahakama ya Uingereza kusikiliza kesi ya kupelekwa marekani kwa raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 48, na ambaye ameshikiliwa kwenye gereza ya ulinzi mkali ya Belmarsh, Kusini mwa Jiji la London. “Ikiwa Assange atafariki ndani ya gereza la Uingereza” kama alivyotahadharisha mjumbe wa umoja wa mataifa kuhusu mateso, Nils Melner mwezi Novemba uliopita, ni wazi kwamba “aliteswa hadi kufa,” welezea madaktari hao. Toka mwaka wa 2015 ambao Assange alifanyiwa uchunguzi na daktari kwenye ubalozi wa Equador alikokimbilia kwa miaka mitatu kabla, mapendekezo ya madaktari wake ya kupewa huduma bora ya kiafya “yaliendelea kupuuzwa”. Madktari hao pamoja na shirika la “Reporters Sans FrontieresL wametuhumu kile wanachoelezea kuwa ni “kufanyiwa siasa kwa maadili za kimsingi za kigangas”. Madaktari hao wametoa mwito wa kuachiwa kwa Julian Assange ili apewe huduma bora za kiafya. Likipinga hatua ya kupelekwa Marekani kwa Julian Assange, kwa kile inachoelezea kwamba Assange ”alitoa taarifa kwa faida ya umma”, shirika la wandishi habari wasiokuwa na mipaka lilikusanya saini 20.000 juzi Jumatatu. Mwanzoni mwa Novemba, mjumbe maalumu wa wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso, aliliambia shirika la AFP kwamba wasiwasi wake ni kutokana na taarifa za kuaminika kwamba hali ya kiafya ya Assange siyo nzuri. Assange ambaye alikamatwa na polisi wa Uingereza kwenye ubalozi wa Equadorwa akitafutwa na Marekani kwa makosa ya kuvujisha maelfu ya nyaraka za siri kuhusu jeshi la Marekani na mabalozi wake. Akikutwa na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 175 jela kwa makosa ya ujasusi.
2
VIONGOZI walioteuliwa juzi na Rais John Magufuli wataapishwa leo saa nane Ikulu, Dar es Salaam.Aidha, Kampuni ya Bharti Airtel International itatoa Dola za Marekani milioni moja sawa na Sh bilioni 2.270 ili kuunga mkono juhudi za serikali katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.Hayo yapo katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kwa vyombo vya habari jana.Kwa upande wa viongozi watakaoapishwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa anayechukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ambaye uteuzi wake ulitenguliwa lakini akateuliwa tena kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.Kiongozi mwingine atakayeapishwa ni Dk Edwin Mhede aliyeteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.Kuhusu Kampuni ya Bharti Airtel International kuchangia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, taarifa hiyo ya Ikulu ilisema Rais Magufuli atashuhudia kampuni hiyo leo ikitoa mchango wa Dola za Marekani milioni moja sawa na Sh bilioni 2 na milioni 270.Mchango huo ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo, na Sh bilioni 3 ambazo zinatokana na malipo ya Sh bilioni 1 kila mwezi kwa serikali ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni hiyo kuhusu umiliki wa hisa za Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
3
RWANDA, mwenyeji wa kihistoria wa mkutano ujao wa marais na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM), imetangaza kufanya maandalizi ya kihistoria ya mkutano huo, lengo likiwa ni kuipa heshima nchi na majirani katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).Tayari Serikali ya Rwanda imetenga Faranga bilioni 20.1 kwa ajili ya mkutano huo wa 26 wa Madola, utakaofanyika mapema mwakani jijini hapa.Rwanda ambayo kiuhalisia haikuwahi kutawaliwa na Uingereza, ambayo ni sifa mojawapo ya kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola, iliomba kujiunga na kukubaliwa uanachama. Pia imepata bahati kuandaa mkutano huo, likiwa taifa la kwanza kuandaa mkutano huo, licha ya kutotawaliwa na Mwingereza.Akizungumza hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Richard Sezibera alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba mpaka sasa, ingawa mkutano utafanyika mwaka kesho, tayari vyumba hadi 8,000 vimeshatengwa kwa ajili ya washiriki.“Sehemu ya kulala hadi wageni 10,000 zipo, kwa sasa tayari tuna vyumba 8,000. Wote watakaofika watakuwa na uhakika wa usalama, mahali bora pa kula na kulala, utalii wa ndani lakini pia utalii wa kiwango cha juu katika nchi jirani ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.“Tumejipanga kwelikweli ili tuweke historia katika ukanda huu, kwani manufaa yake hayatabaki kwa Rwanda pekee, bali kote katika EAC,” alisema Sezibera aliyewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa EAC.Alisema katika maandalizi, sehemu kubwa ya fedha, kiasi cha Faranga bilioni 10.87 zitatumika kuimarisha miundombinu, ikiwemo upanuzi wa sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Kigali na viwanja vingine vya ndege.Barabara katika Jiji la Kigali zimetengewa Faranga bilioni 3. Jonathan Nzayikorera, mmoja wa maofisa waandamizi katika Wizara ya Fedha na Mipango ya Uchumi, alisema nchi itanufaika sana na mkutano huo.“Kuna faida nyingi za kiuchumi za kuandaa mkutano huu, ndiyo maana tumeeleza katika maandalizi ya uhakika,” alisema.Akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha maandalizi ya mkutano wa Rwanda, Mkurugenzi wa Masuala ya Amani na Utawala Bora katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, Katalaina Sapolu alisema wamefurahishwa na mwelekeo wa Rwanda katika kuandaa mkutano huo muhimu duniani.Mkutano wa marais na wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Madola hufanyika kila baada ya miaka miwili. Samoa itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 27 utakaofanyika mwaka 2022.
5
NAIROBI, KENYA MAELFU ya wagonjwa katika hospitali za umma wanahangaika bila matibabu baada ya mgomo wa nchi nzima wa madaktari na wahudumu wengine wa afya, huku karibu wagonjwa 100 wakiripotiwa kutoroka Hospitali Kuu ya Wagonjwa wa Akili ya Mathari jijini Nairobi. Katika mgomo huu ulioanza wiki hii, madaktari wanaishinikiza Serikali kutekeleza makubaliano ya mwaka 2015 yaliyofikiwa na Muungano wa Wahudumu wa Afya ukiwa na lengo la kuboresha mazingira ya kazi. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, polisi walisema wamefanikiwa kuwarejesha baadhi ya wagonjwa wa akili hospitalini, ambao inaaminika walitoroka wakitumia fursa ya kutokuwapo kwa madaktari waliogoma. Wagonjwa wengine katika hospitali za umma nchini hapa, wamelazimika kurudi nyumbani au kutafuta matibabu katika zahanati binafsi ambazo gharama zake ni kubwa. Mwaka 2013, sekta ya afya nchini Kenya ilipeleka baadhi ya huduma zake chini ya mamlaka za kaunti, hatua iliyosababisha hospitali za umma kuwa chini ya usimamizi wa magavana. Hata hivyo, Wizara ya Afya bado inasimamia hospitali kuu za kitaifa, ikiwamo ya Kenyatta iliyoko Nairobi na Moi iliyoko Magharibi mwa Kenya. Tangu sekta ya afya kuwekwa chini ya usimamizi wa kaunti, huduma za afya zimeonekana kudorora, huku wauguzi na madaktari wakifanya migomo ya kila mara kulalamikia mazingira duni ya kazi.
2
Hatahivyo, ushindi huo umeendelea kuibakiza Yanga katika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam baada ya kujikusanyia pointi 28. Washindi hao katika mechi hiyo walishuka dimbani huku wakicheza bila ya wachezaji wake karibu saba ambao ni majeruhi, lakini walicheza kandanda safina la kuvutia.Aidha, mchezaji wa Azam FC Abubakari Salum ‘Sure Boy’ alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumsukuma kwa makusudi, Hassan Kessy mbele ya mwamuzi wa kati Israel Nkongo.Azam ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya tatu baada ya kuanza kwa mchezo huo huku bao hilo likifungwa na Shaban Chilunda, na Obrey Chirwa kwa upande wa YANGA akisawazisha bao hilo dakika ya 30 na la ushindi likifungwa na Gadiel Michael.Ushindi huo umeendelea kuibakiza Yanga katika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikifikisha jumla ya pointi 28, nyuma ya Azam yenye pointi 30 na Simba 32. Azam FC ilianza mpira kwa kasi na kufanikiwa kupata bao hilo la uongozi baada ya Chilunda kutengenezewa pasi na Bruce Kangawa.Baada ya Azam kuongoza bao hilo walianza kupunguza kasi na kuwapa nafasi wapinzani wao kusawazisha kupitia kwa Chirwa aliyepata pasi ya Ibrahim Ajibu ambapo alimzunguka kipa Razaki Abalora na kufunga.Azam baada ya kusawazishiwa walirudi tena kwenye kasi na kufanya mashambulizi mengi lakini hayakuzaa matunda, na kutoa nafasi zaidi kwa Yanga kujiamini ambapo Gadiel alipiga shuti kali nje ya 18 na kuifungia Yanga bao la pili. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Azam ilikuwa ikiongoza kwa mashambulizi lakini Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.Kipindi cha pili Azam iliendeleza kasi ya mashabulizi bila mafanikio kwani tayari Yanga iliweka ukuta uliowafanya Azam kupata wakati mgumu kufunga magoli. Kocha wa Azam alijaribu kufanya mabadiliko kadhaa lakini hayakuzaa matunda.Dakika 36 alimtoa Bernard Arthur na kumuingiza Salmin Hoza, pia, kipindi cha pili dakika 55 na 65 alimtoa Stephen Kingue na Shaban Chilunda na kuingia Mbaraka Yusufu na Paul Peter. Kwa upande wa Yanga dakika ya 66 iliwatoa Emmanuel Martin na kuingia Geofrey Mwashiuya.Dakika 68 alimtoa Ibrahim Ajibu na kuingia Juma Mahadhi.hadi mwisho wa mchezo Yanga 2- 1 Azam. Kikosi cha Azam FC kilikuwa na wachezaji; Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Agrey Morris, Yakubu Mohamed, Stephan Kingue, Salum Abubakari, Joseph Mahundi, Bernard Arthur, Shaban Chilunda na Enock Atta.Kikosi cha Yanga. Youthe Rostand, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Hassan Kessy, Raphael Daud, Andrew Vicent, Said Juma, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.Mechi nyingine zilizochezwa ni Mwadui dhidi ya Njombe waliopata sare ya mabao 2-2 na Mbeya City dhidi ya Mtibwa sare ya bila kufungana 0-0. Na Kagera Sugar na Lipuli pia zikitoka sare ya 0-0.
4
UAMUZI wa Tanzania kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, umelikuna shirika la kimataifa linalopigania usafi ri wa mazingira, Greenpeace Africa na kuzitaka nchi za Uganda, Burundi na Sudan Kusini nazo kufuata nyayo.Kwa uamuzi huo, Tanzania imekuwa nchi ya tatu katika Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuzuia mifuko ya plastiki. Tayari Kenya na Rwanda zilishafanya hivyo. Ukomo wa matumizi ya plastiki kwa Tanzania ulifikia tamati Mei 31 mwaka huu.Kenya walizuia mwaka 2017 na ikafuatia Rwanda. Meneja wa kampeni za mazingira wa Greenpeace Africa, Renee Olende amesema Tanzania inapaswa kuungwa mkono na nchi nyingine ndani ya Jumuiya huku akisisitiza kuwa, ikiwezekana, Bunge la Afrika Mashariki (EALA) litunge sheria ya kudhibiti mifuko ya plastiki ndani ya nchi wanachama.Magufuli kicheko Baada ya kuanza kutekelezwa kwa agizo la Serikali, Rais John Magufuli amewapongeza Watanzania kwa kuitikia mwito wa Serikali wa kuacha kutumia mifuko ya plastiki huku akiwataka wafanyabiashara kutotumia mwanya huo kuuza vifungashio na mifuko mbadala kwa bei kubwa.Pia, ameziagiza mamlaka zinazohusika, kuhamasisha utengenezaji wa mifuko na vifungashio mbadala hapahapa nchini ili kuongeza ajira katika viwanda vya kutengenezea bidhaa hizo badala ya kuacha wafanyabiashara wakigeuza nchi kuwa mahali pa kuingiza bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.Aliyasema hayo Juni 3, mwaka huu alipozungumza na wafanyabiashara wa soko la samaki la Feri Dar es Salaam baada ya kufanya ziara ya kushtukiza sokoni hapo na kujionea wafanyabiashara na wanunuzi wa samaki wakitumia mifuko mbadala.Mwitikio Marufuku au zuio hilo limepokewa kwa mikono miwili na wanamazingira ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipigia kelele matumizi ya mifuko ingawa kwa wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kwao umekuwa mtihani, wana hofu kupoteza ajira na viwanda kufungwa.Kenya ilivyofanikiwa Pamoja na malalamiko hayo, nchini Kenya hasa jiji la Nairobi ikiwa ni takribani miaka miwili sasa marufuku hiyo imefanikiwa, mifuko ya plastiki haipo, vifungashio rafiki kwa mazingira ndivyo vilivyochukua nafasi ya mifuko ya plastiki.Mafanikio ya marufuku ya Kenya yanatajwa kuchangiwa na sheria kali iliyowekwa, mtu akikutwa anauza, kuzalisha au kutumia mifuko ya plastiki adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka minne jela au faini inayotajwa kufikia hadi Sh milioni 80 za Tanzania.Kwa Tanzania, faini ya watakaokutwa na mifuko ni Sh milioni 20. Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), John Chikomo amesema tatizo la mifuko ya plastiki si la Tanzania pekee, bali ni duniani kote na kusisitiza kuwa, kila nchi imekuwa ikilalamikia mifuko ya plastiki, ina madhara kwenye ardhi, kwa wanyama na viumbe wa baharini.
3
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao  Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40)  na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele  ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa  kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020  maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam  kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
5
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imekiri kuwepo kwa changamoto nyingi baada ya serikali kuanzisha mfumo wa elimu bila malipo kwa shule za msingi.Akijibu swali la mbunge wa Handeni, Omar Kigoda (CCM), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwita Waitara amesema serikali imejipanga kutatua changamoto hizo.Amesema moja ya njia za kutatua changamoto hizo itahamisha walimu zaidi ya 11,000 wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi.Waitara amesema kwa sasa wamepata kibali cha kuajiri walimu kwa awamu na pia waalimu 6,000 wanatarajia kuajiriwa hivi karibuni ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu.Akizungumzia kuhusu umaliziaji wa maboma ya vyumba vya madarasa 15 katika Halmashauri wa Mji wa Handeni yaliyoanza kwa nguvu za wananchi, Waitara alisema maboma sita yapo katika hatua ya lenta.Amesema hadi Januari mwaka huu, halmashauri hiyo imeshapokea jumla ya Sh milioni 46.6 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma yaliyoanza kwa nguvu za wananchi ili yaanze kutumika.Waitara amesema serikali kwa kushirikiana na wadau kupitia Programu ya Lipa kwa Matokeo (EP4R) na Programu ya kuimarisha Ubora wa Elimu Tanzania itaendelea kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kwaajili ya ukamilishaji wa maboma.Amesema halmashauri ya zinahimizwa kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma yaliyopo kabla ya kuanzisha miradi mipya.Katika swali lake Kigoda alitaka kujua ni lini Halmashauri ya Handeni na zinginezo zitakamilisha majengo ya madarasa yaliyotokana na nguvu za wananchi.
3
LONDON, England TIMU ya Manchester United jana iliifunga Swansea mabao 4-0, katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu England, uliochezwa Uwanja wa Liberty, Wales. Mabao ya Eric Bailly, Romelu Lukaku, Paul Pogba na Anthony Martial yaliipatia Manchester United ushindi wa pili katika kampeni yao ya kunyakua ubingwa msimu huu, baada ya kushinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya West Ham. Nyota hao wanaifanya United kuanza msimu wakiwa na mabao mengi zaidi katika michezo ya kwanza ya Ligi Kuu  tangu msimu wa 1907/08. Mabao nane kwenye michezo miwili yanaifanya United kuongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi sita. United ilifunga bao dakika ya 45, baada ya Jordan Ayew wa Swansea kufanya makosa yaliyoigharimu safu ya ulinzi, ambapo Eric Bailly aliandika bao la kuongoza. Bao la pili la United lilifungwa na Lukaku dakika ya 80, kabla ya Paul Pogba kufunga la tatu dakika ya 82 na kuhitimishwa na Anthony Martial dakika ya 84. Akizungumza baada ya ushindi huo, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, alisema: “Tunajiamini, kwa kuwa tunafahamiana kila mmoja, ni msimu wa pili, unatakiwa kubadili kikosi ukiwa kocha kwa mara ya kwanza. “Ndiyo, kwenye mwaka wa kwanza tulishinda taji, lakini sasa tunajiamini na rahisi kwetu kufanikiwa.” Kabla ya ushindi huo, United hawakuwa na rekodi nzuri dhidi ya Swansea katika michezo ya hivi karibuni. Mchezo wa mwisho katika Uwanja wa Old Trafford Aprili mwaka huu, kikosi hicho cha Paul Clement kilipata ponti ya muhimu kubaki Ligi Kuu England. Sare hiyo ilikuwa ya 10 katika Uwanja wa Old Trafford msimu uliopita, ilikuwa moja ya mechi ambazo Mourinho  alichemka kwa msimu wake wa kwanza.
4
Mwanachama na shabiki wa klabu ya Yanga, Bilionea Rostam Aziz leo ametokea hadharani na kusema kwamba haungi mkono klabu yake kumilikiwa na mtu mmoja. Rostam ameyasema hayo leo mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Rostam amesema hakubaliani na suala la mtu mmoja kumiliki klabu hiyo au kufadhili, badala yake anaunga mkono udhamini. Rostam hivi karibuni aliichangia Yanga Shilingi 300 milioni alisema iwapo timu itakuwa ikimilikiwa na mtu au kutegemea ufadhili, itapoteza maana na hadhi ya klabu hiyo. “Kwa mtazamo wangu, Yanga haitakiwi kumilikiwa na mtu binafsi wala kutegemea ufadhili kwa sababu ni klabu yenye wanachama na mashabiki wengi. “Yanga inatakiwa kumilikiwa na wanachama wake wote. Kunapokuwa na ufadhili au umiliki wa mtu binafsi unawanyima au kuwabinya wale walio wengi hivyo naamini Yanga inatakiwa ibakie kwa wanachama.” “Ufadhili nao ni kama umiliki kwa sababu ufadhili ni mlango wa nyuma wa umiliki. Kwa sababu inawezekana kuna watu wanataka kuingia kwenye klabu, lakini wakahofia uwepo wako. Kwa hiyo huwezi kusema unapinga umiliki halafu wakati huohuo unasapoti ufadhili,” amesema Rostam.
4
Mwijage alibainisha mpango huo bungeni wakati akifanya majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Alisema katika utoaji huo wa elimu ya biashara, maofisa hao watashirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo (Sido).“Maofisa biashara wa wilaya kazi yenu isiwe kukusanya leseni tu , muwafundishe wananchi namna ya kufanya biashara na hiyo mtashirikiana na Sido…unawakatisha leseni kwani uliwapa elimu ya biashara?” Alisema.Alisema serikali imejipanga kuanzishwa viwanda vingi vidogo na vya kati na kufafanua “nitavijenga viwanda kila mahali vidogo na vya kati na nyinyi wabunge msiogope, mbona Lema (Godbless, Mbunge wa Arusha) kwa ushauri wangu ameweka oda ya toothpicks (vijiti vya meno), tomato sauce…”.Alitamba kuwa tangu amekuwa Waziri wa Viwanda, anafanya kazi sana na kwenye wizara hiyo kuna mabadiliko makubwa, ambapo sasa hali si kama zamani ya kufanya kazi kwa mazoea.Akizungumzia hatua ya Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara ya kuuza saruji Sh 13,500 kwa mikoa ya Kusini, lakini Dar es Salaam na mingine ikiuzwa Sh 12,500, alisema anafanya hivyo kushambulia soko la Dar es Salaam.“Nadhani Dangote anazuia saruji ya Simba na Twiga kwa Dar es Salaam, anashambulia soko la Dar es Salaam, nitamuita nizungumze naye,” alisema. Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema serikali itaondoa tozo zote zisizo na tija na orodha ya tozo hizo, zitaletwa bungeni ili kuungwa mkono na wabunge.
5
IDADI ya tembo na wanyamapori waliokuwa wakiwindwa na majangili imeendelea kuongezeka kutokana na juhudi za Wizara ya Maliasili na Utalii kudhibiti na kufanikiwa kutokomeza vitendo vya ujangili nchini.Pia sensa iliyofanywa katika mfumo wa ikolojia wa Selous na Mikumi mwaka 2018 inaonesha kuwa idadi ya tembo haipungui na vile vile sensa hiyo haikubaini mizoga mipya ya tembo waliouawa na majangili katika mfumo huo wa ikolojia.Akitoa hotuba yake wakati wa kuwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla alisema serikali imepiga hatua na kupata mafanikio makubwa katika kutokomeza ujangili.Alisema sensa iliyofanywa ya mfumo wa ikolojia wa Selous na Mikumi mwaka 2018 yanaonesha idadi ya tembo haipungui na idadi ya wanyamapori wengine waliokuwa wakiwindwa imeongezeka hali inayosababisha wanyamapori kuanza kuonekana katika maeneo ambayo awali haikuwa rahisi kuwaona.Waziri Kigwangalla alitoa mfano kuwa hivi karibuni tembo wameonekana eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma mara mbili na kuongeza kuwa mafanikio hayo makubwa ya kudhibiti ujangili pia umewezesha mapapa wakubwa wa ujangili kukamatwa, kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo vya miaka mingi akiwemo mhalifu sugu Yang Lan maarufu kama Malkia wa Ndovu.Alisema pia juhudi hizo za kupambana na ujangili zimewezesha kutambua mbinu mbalimbali na mitandao haramu ambayo imekuwa ikifanikisha vitendo hivyo na kuongeza kuwa hivi karibuni walinaswa baadhi ya watumishi wa umma na hakimu mmoja kwa tuhuma za kushiriki kwenye mtandao wa kusaidia na kulinga majangili. Kwa mujibu wa waziri huyo, wizara inaendelea kuwasaka watu wote wanaofadhili, kuwezesha na kulinda ujangili hadi kutokomeza kabisa uhalifu huo wa kuhujumu rasilimali za Taifa.Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba katika mwaka wa fedha 2019/2020 idhinishiwe na Bunge Sh 120,202, 638, 734 kwa matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kati ya fedha hizo Sh 71,312, 649,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 48,889,988,734 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
3
SERIKALI imeombwa kuhakikisha kila kiwanda kinachozalisha mafuta ya alizeti kinakaguliwa na kupewa alama ya ubora ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo na kuleta usawa kuhimili ushindani.Rai hiyo ilitolewa mjini hapa na baadhi ya wazalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka viwanda vya kati na vikubwa waliodai wao walikaguliwa na mamlaka husika kabla ya kupatiwa alama ya ubora wa bidhaa wanayozalisha na waliingia gharama kubwa kukamilisha hilo na wanalipia kila mwaka alama ya ubora. Walidai waliingia gharama kubwa kupata alama ya ubora, wenye viwanda vidogo hawana alama hiyo kwa kuwa hawajawahi kukaguliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wala Shirika la Viwango (TBS) hali ambayo haileti usawa wa ushindani kibiashara.“Kuna ushindani usio sawa kutokana na kuwepo kwa mafuta yasiyokaguliwa wala kuthibitishwa ubora wake na TFDA au TBS. Hii inaathiri viwanda vikubwa ambavyo hutumia mamilioni ya fedha katika kujiendesha,” alisema Meneja wa Masoko wa Mount Meru Millers mjini Singida, Nelson Mwakabuta.Mzalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka kiwanda cha Kati cha Singida Fresh, maarufu kama “ Kilimo Kwanza”, Jamal Shaban aliisihi serikali kusimamia kikamilifu suala la kila kiwanda kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa bidhaa zake ili walaji waweze kupata mafuta yasiyochakachuliwa. Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Dk Engelbert Bilashoboka alisema jukumu la kusimamia ubora wa mafuta ya alizeti yanazozalishwa na viwanda vidogo lipo kwa Halmashauri za wilaya, miji au manispaa.Katibu Mtendaji wa Chemba ya Wakulima, Wafanyabiashara na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoa wa Singida, Culvert Nkurlu alisisitiza umuhimu wa kuvilinda viwanda vidogo na kuwatia moyo wamiliki wake viwanda hivyo vidogo viweze kukua akikariri usemi kuwa “mbuyu nao ulianza kama mchicha.” Kutokana na alizeti kuwa moja ya zao kuu la biashara Singida, mkoa sasa una viwanda 140 vya alizeti, kimoja kikubwa, vya kati na vidogo vinavyotumia mbegu za zao hilo ili kuzalisha mafuta ya kula.
3
Mwandishi Wetu -Maswa JESHI la Polisi wilayani Maswa mkoani Simiyu, limelalamikiwa kuwafumbia macho watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi na kuharibu kesi zinazotolewa taarifa katika vituo vya polisi. Malalamiko hayo yametolewa juzi kwa waandishi wa habari na baadhi ya wananchi waliokuwa nje ya viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Maswa waliokuwa wakifuatilia kesi za wanafunzi kupatiwa ujauzito. Akitoa malalamiko hayo, mkazi wa Kijiji cha Mpindo, Shigela Golani, alisema licha ya Serikali kupambana na watu wanaowapatia ujauzito wanafunzi wa shule, lakini jitihada zimekuwa zikivunjwa nguvu na askari wa kituo cha polisi cha wilaya hiyo. “Serikali Wilaya ya Maswa imekuwa ikipambana na watu wanaowapatia mimba wanafunzi, cha kushangaza Kituo cha Polisi Wilaya ya Maswa ukipeleka kesi ya mimba, wamekuwa kikwazo kwa kuharibu ushahidi, hata zikienda mahakamani zinakosa nguvu,” alisema. Alisema kutokana na mazingira hayo, inawakatisha tamaa wananchi, hasa wazazi na walezi wa watoto wanaopatiwa ujauzito na kuondoa imani kwa jeshi hilo. “Ni vizuri mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa afuatilie malalamiko haya na kukisafisha kituo hiki, maana wananchi tunakosa imani na askari wanaoshughulikia kesi za mimba za wanafunzi, wamegeuza mtaji na waathirika kutopatiwa haki,” alisema. Alisema vitendo hivyo vinaashiria kuwapo vitendo vya rushwa na kuiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuingilia kati kesi hizo ili haki ipatikane kwa walalamikaji na washtakiwa wakapata adhabu stahiki. Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Maswa (OC-CID), Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Mily Mathias, alisema kesi zote za mimba za wanafunzi zinashughulikiwa na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ambayo anayoiongoza, na kusisitiza kuwa wamekuwa wakizipeleka mahakamani. “Kesi zote za mimba zinashughulikiwa na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai na si mkuu wa kituo, niwahakikishie mimi ndiye mkuu wa idara ya upelelezi, tunajitahidi kuzipeleka mahakamani kwa haraka zaidi, iwapo yupo askari anaharibu kesi zinazoripotiwa, naomba mlalamikaji aje tuwasiliane,” alisema. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Fredrick Lukuna, alisema kumekuwa na kasumba iliyojengeka miongoni mwa wazazi na walezi ya kuripoti matukio ya mimba kwa watoto wao katika vituo vya polisi, lakini mashauri yanapofikishwa mahakamani wamekuwa wakikacha kufika kutoa ushahidi.
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu nchini (TFS), Nurdin Chamuya alisema hayo juzi Dar es Salaam katika uzinduzi wa filamu ya matumizi endelevu ya misitu.Chamuya alisema misitu ni rasilimali muhimu kwa Watanzania hasa kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla ambapo jamii inatakiwa kuisimamia na kuilinda vyema ili iweze kuendelea kuongeza mapato ya taifa.“Serikali haijafumbia macho suala hilo, hivyo kutokana na mapenzi yake kwa watanzania imetoa fursa ya kumiliki na kusimamia misitu iliyo katika eneo lao,” alisema Chamuya na kuongeza kuwa ni vyema rasilimali hizo zikatumiwa kwa njia endelevu.Alisema kwa mujibu wa utafiti wa TFS kwa mwaka 2012 Tanzania ina jumla ya hekta milioni 48.1 za misitu zilizoko mikoa yote nchini na imekadiriwa kuwa asilima 55 ya ardhi ya Tanzania ni misitu ambapo kwa mwaka huingiza asilimia 20 ya pato la taifa.“Pamoja na rasilimali zote hizi, nchi yetu bado inapoteza mapato yatokanayo na misitu…tunapoongelea matumizi endelevu ya rasilimali hizi tunamaanisha utumiaji uwe wenye faida kwa kila mtanzania anayeishi leo na hata atakayezaliwa kesho", alisema Chamuya.Kuhusu filamu hizo ambazo zimeandaliwa na kampeni ya Mamamisitu alisema zimelenga kuelimisha jamii juu ya matumizi endelevu ya rasilimali misitu kupitia ushiriki wa jamii katika kusimamia rasilimali hizo.
5
MFANYABIASHARA Khamis Luwongo maarufu Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Luwongo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka ya mauaji katika kesi namba 4/2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.Akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka ya mauaji kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu Namba 196 sura 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2002. Alidai kuwa mshitakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam, anadaiwa Mei 15, mwaka huu akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua mtu anayeitwa Naomi Marijani.Wankyo alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo aliomba mahakama kupanga tarehe ya kutajwa. Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13, mwaka huu kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la. Kabla mshitakiwa kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Ally alimtaarifu kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hivyo, hapaswi kujibu chochote. Hata hivyo, wakati mshitakiwa huyo anatolewa mahabusu na kupandishwa mahakamani, alifunika sura yake kwa kutumia kofia ya koti lake kwa lengo la kutotaka kuonekana sura yake.
3
Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM MMOJA  wa waasisi wa Uhuru na aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Tanganyika, Sir George Kahama (88), alifariki dunia Dar es Salaam jana. Akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Stephen, alisema Sir Kahama alipatwa na  mauti jana saa 4:40 jioni. Alisema Sir Kahama alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali isiyoridhisha na kupokewa katika chumba cha uchunguzi kwa ajili ya matibabu. MTANZANIA ilipomuuliza ugonjwa uliokuwa ukimsumbua, John alisema kwa suala hilo linaweza kuzungumziwa na familia na si yeye. “Tulimpokea hapa hospitali Ijumaa, hakuwa  katika hali nzuri  ya afya na aliingizwa katika chumba cha uchunguzi na  kupatiwa matibabu lakini leo (jana) saa 10.00 jioni aliaga dunia ,’’alisema John.  Kahama maarufu kama Sir George Kahama  alizaliwa Novemba 30, 1929  na aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (1961-1962) kabla nafasi hiyo haijachukuliwa na  Oscar Kambona  kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 1962 hadi 1963.  Sir Kahama ambaye alizaliwa Novemba 30, 1929 aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (1961-1962) kabla nafasi hiyo haijachukuliwa na  Oscar Kambona  kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 1962 hadi 1963. Alikuwa mtumishi wa umma kwa miaka mingi  na mwanasiasa   mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika za kudai uhuru katika  miaka ya 1950 hadi kujitawala mwaka 1961. Mwanasiasa huyo   alipelekwa   Uingereza na Chama cha Ushirika wa   Kahawa cha jimbo lililokuwa likiitwa Ziwa Magharibi wakati huo, likiwa la Wilaya za Bukoba, Karagwe, Biharamulo na Ngara.  Kwa sasa ni Mkoa wa Kagera. Katika kutimiza dhana yao ya kuzima harakati za Nyerere za kudai uhuru na kwa vile hakuwa peke yake katika harakati hizo, wakoloni walimpatia masurufu yasiyokidhi mahitaji yake akiwa masomoni ili akose uwezo wa kuwasiliana na waasisi wenzake. Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanachuo wenzake kutoka Tanganyika   katika vyuo mbalimbali vya Uingereza walidokezwa uwepo wake nchini humo.   Mwalimu Nyerere alifurahi akawa na matumaini ya kusaidiwa, kwanza kwa sababu alikwisha kuona ushirikiano wa Watanganyika wengine hivyo akajua hata Kahama atamsaidia. Kwa mujibu wa Sir George, katika moja ya mahojiano yake kabla ya kupatwa na mauti, alisema tumaini la Mwalimu Nyerere wakati huo lilizidishwa na ukweli kwambawao ni watani wa jadi.  Sir George aliingizwa kimyakimya katika harakati za kudai uhuru wa iliyokuwa Tanganyika. Alikuwa rafiki wa karibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu  Nyerere,   chanzo cha urafiki wao likiwa ni  jibu la jinsi gani   alivyoingizwa kwa siri katika siasa za Tanganyika.   Nyerere na Kahama waliporejea nchini kila mmoja aliripoti kwa mwajiri wake, huku  Mwalimu Nyerere akilazimika kujiuzulu kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam   kusudi aendeleze kwa ukamilifu siasa za kudai uhuru. Naye  Kahama aliendelea na kazi katika chama cha ushirika wa zao la Kahawa jimboni Ziwa Magharibi (BCU) mjini Bukoba. Wakati inaundwa Serikali baada ya Uhuru, ndipo Mwalimu Nyerere alipomwita Sir George kutoka Bukoba  ajiunge na Baraza la Mawaziri la Serikali hiyo  na akamteua kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko na mwenyewe (Nyerere) akawa Waziri Mkuu. Baadhi ya mawaziri walioteuliwa walikuwa Paul Bomani, Chifu Abdallah Fundikira, Rashid Mfaume Kawawa, Solomon Eliofoo, Nsilo Swai, Said Maswanya, Dereck Noel Bryceson, Sir. Ernest Versey na Amir Jamal. Sir. George alikuwa Waziri wa kwanza wa Mambo ya Ndani ya Nchi na baadaye Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alimteua tena kuwa Waziri wa Ushirika. JPM amlilia Rais Dk. John Magufuli, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mmoja wa Waasisi wa Taifa na Waziri Mstaafu, Sir George Kahama.   Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kwamba   Dk. Magufuli, alisema Taifa limempoteza mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru, maendeleo na ustawi wa jamii ya watanzania akiwa katika nyadhifa mbalimbali za uongozi hususan kuwa miongoni mwa mawaziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri. “Sir George Kahama alikuwa kiongozi shupavu, mzalendo, mwanasiasa mahiri, aliyewapenda Watanzania na aliyejitoa kushirikiana na viongozi wenzake akiwamo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kupigania uhuru, kujenga misingi ya Taifa likiwamo Azimio la Arusha, kujenga misingi ya uchumi wa ujamaa na kujitegemea na mengine mengi.  Kwa hakika hatutamsahau,” alisema.
3
TIMU ya Taifa ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys, imeshika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Rwanda kwa penalti 4-3 katika mchezo wa mashindano ya Cecafa ya kutafuta kufuzu Afcon uliochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Katika mchezo huo, Serengeti Boys ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 39 baada ya beki wa Rwanda, Eni Niyomugisha kujifunga akijaribu kuokoa shuti lililopigwa na mshambuliaji wa Serengeti Boys, Edson Jeremia na kudumu hadi mapumziko.Baada ya mapumziko timu zote zilirejea kwa nguvu mpya kila moja akijaribu kupenya ngome ya mpizani wake lakini Uganda walifanikiwa kusawazisha kwa njia ya penalti na Serengeti wakasawazisha kwa penalti baada ya Kelvin John kufanyiwa faulo wakati akienda kufunga, bao likifungwa na Morice Michael dakika ya 81.Wakati Serengeti Boys wakiendelea kushangilia bao la pili, Rwanda walisawazisha dakika ya 87 kwa mpira wa faulo ya adhabu kubwa iliyopigwa na Innocent Mariza na Clever Kazungu akafunga bao kwa shuti akiwa nje ya eneo la penalti na kufanya mchezo umalizike kwa 2-2.Baada ya dakika 90, zilipigwa penalti na Serengeti Boys walifunga penalti 4-3 huku Benard Paul wa Serengeti Boys akipiga nje na kipa wao Mwinyi Yahya akipangua penalti mbili za Rwanda mbele ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad ambaye alikuwepo uwanjani.Katika mchezo wa fainali, Uganda ilifanikiwa kupata tiketi ya kuungana na Tanzania kuwakilisha ukanda wa Cecafa katika fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani hapa Tanzania baada ya kuifungwa Ethiopia kwa mabao 3-1.Mfungaji bora wa michuano hiyo ni Naanol Tesfaye wa Ethiopia na kipa bora ni Alazar Malko wa timu hiyo pia. Mchezaji bora ni Kelvin John wa Serengeti Boys, na timu yenye nidhamu ni Serengeti Boys ya Tanzania.Mashindano ya Cecafa yalianza Agosti 11 yakichezwa katika Uwanja wa Azam Complex na Taifa, Dar es Salaam yakishirikisha timu tisa ambazo ni wenyeji Tanzania, Uganda, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Burundi, Djibouti, Sudan na Sudan Kusini.
4
Harare, Zimbabwe Mwanamuziki nguli wa muziki wa Jazz kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ‘Tuku’ amefariki dunia katika hospitali ya Avenues mjini Harare nchini Zimbabwe alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mutukudzi amefariki akiwa na umri wa miaka 66 leo Jumatano Januari 23, taarifa za kifo chake zimetangazwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini humo. Mwanamuziki huyo aliyekuwa na ziara za kimuziki katika nchi mbalimbali duniani, ilimlazimu kuzikatiza sababu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. Amefariki ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo cha gwiji mwingine wa muziki wa Jazz, Hugh Masekela kutoka nchini Afrika Kusini, amefariki akielekea kuwa na miaka 67 na akiwa katika maandalizi ya albamu yake ya 67. Muziki wake wa mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani, amekuwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miongo minne, na amefanikiwa kutoa albamu 66. Nyota huyo wa muziki kutoka Zimbabwe alikuwa akipewa heshima ya muziki wa Afrika kama ilivyo kwa wasanii wengine wengi kutoka nchi mbalimbali barani hapa ambao muziki wao umeleta hamasa kwa jamii. Mutukdzi amezaliwa mnamo Septemba 22 mwaka 1952 mjini Harare Zimbabwe na katika uhai wake mbali na uanamuziki alikuwa pia mfanyabiashara, mhisani kwa watu wasiojiweza na Balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto duniani (UNICEF) kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Mara baada ya taarifa za kifo chake Mutukudzi kusambaa, wasanii wenzake na mashabiki wake wametuma salamu zao za rambirambi katika mitandao ya kijamii.
2
SAO PAULO, BRAZIL NYOTA wa zamani wa klabu ya Real Madrid na AC Milan, Ricardo dos Santos ‘Kaka’, ametangaza rasmi kustaafu soka huku akiwa na umri wa miaka 35. Mchezaji huyo ambaye alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, amestaafu soka akiwa anaitumikia klabu ya Sao Paulo ya nchini Brazili, ambapo alikuwa anacheza kwa mkopo akitokea klabu ya Orland City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani. Nyota huyo wa Brazili mara ya mwisho kucheza soka katika klabu yake ilikuwa Oktoba mwaka huu, huku timu yao ikikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Colombus Crew, hivyo aliamua kuweka wazi kuwa muda wake umefika wa kustaafu soka. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Kaka aliamua kuwaaga mashabiki zake huku akisema ni maamuzi sahihi kwa upande wake. “Baba, ninaweza kusema maisha yangu sasa ni zaidi ya vile ambavyo nilikuwa nafikiria, naomba maisha yangu yawe chini ya Yesu. “Nakushukuru sana kwa kunifanya niwe hapa, safari yangu ilikuwa ndefu na sasa nipo tayari kwa safari nyingine ya maisha yangu. Kwa jina la Yesu. Amen,” aliandika Kaka. Mchezaji huyo alianza kuonesha ubora wake kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2002 ambapo walifanikiwa kulitwaa akiwa na kikosi chake cha Brazili, baada ya hapo klabu mbalimbali barani Ulaya zikawa zinagombania saini yake kuanzia mwaka 2003 AC Milan walifanikiwa kumsajili nyota huyo. Mbali na kutwaa Kombe la Dunia, lakini alifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu nchini Italia msimu wa 2003/2004, Italian Super Cup 2004/05, Confederations Cup 2005 na 2009, Ligi ya Mabingwa 2006/07, UEFA Super Cup 2007/08, Spanish Cup 2010/11, Ligi Kuu Hispania, 2011/12. Amewahi kuchukua tuzo mbalimbali ikiwa pamoja na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2006/07, mchezaji bora wa mwaka nchini Italia, 2004 na 2007, mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya wa UEFA 2007 na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA Ballon d’Or 2007. Mchezaji huyo aliongeza kwa kusema lengo la kustaafu soka ni kuwapisha vijana wenye damu changa waweze kutumia nafasi hiyo na kuonesha vipaji vyao kwa ajili ya kupigania Taifa pamoja na klabu zao kwenye michuano mbalimbali duniani.
4
Na ZAINAB IDDY NI mwaka mmoja sasa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli aingie madarakani katika awamu ya tano. Rais Dk. Magufuli aliapishwa rasmi na kuanza majukumu yake ya kuliongoza taifa Novemba 5, 2015 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Watanzania wengi wakishuhudia tukio hilo. Kwa sasa ametimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani huku akizigusa sekta za uchumi, elimu, kilimo na michezo katika utendaji wake wa kazi. Tangu Serikali mpya ichukue madaraka, kuna mambo mbalimbali tumeyashuhudia kwenye sekta mbalimbali, huku baadhi ya watendaji wakitumbuliwa na sekta ya michezo nayo ikiwa ni mojawapo iliyoguswa. Bajeti ya michezo 2016/17 Katika mwaka huu wa fedha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, bajeti imepunguzwa kwa asilimia 21, ukilinganisha na mwaka uliopita wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2015/16, wizara hiyo iliyopo chini ya Waziri Nape Nnauye, iliidhinisha Sh bilioni 21.957 kwa matumizi ya kawaida, lakini mwaka huu wa fedha ulioanza Julai zimetengwa Sh bilioni 17.326, ikiwa ni punguzo la Sh bilioni 4.631 sawa na asilimia 21 ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha uliopita. BMT yatumbuliwa Katika harakati za kuziboresha sekta ya michezo nchini, Februari 19 mwaka huu, Waziri Nape, alitengua uteuzi wa Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya. Uamuzi huo ni baada ya kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo na msaidizi wake, Juliana Yasoda. Waziri Nape alifikia uamuzi huo wa kumtoa Lihaya kutokana na kukaa kwenye wadhifa huo kwa muda mrefu, bila kuonekana maendeleo ya kueleweka huku akiteuliwa, Mohammed Kiganja, kukaimu nafasi hiyo mpaka atakapoteuliwa katibu mpya. Umitashumta na Umisseta Juni 13 mwaka huu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene, alitangaza kusitisha mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Nchini (Umitashumta na Umisseta), ambayo ilipangwa kufanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 13 hadi Julai 5 mwaka huu. Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa kupisha zoezi la kumalizia ukamilishaji wa madawati ili kutimiza agizo la Rais Dk. Magufuli la kuondoa upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini. Mfumo wa ukodishwaji na hisa Klabu za Simba na Yanga nazo zilijikuta katika mgogoro na Serikali baada ya kutaka kuingia kwenye mfumo wa uendeshaji na uwekezaji wa klabu zao. Sakata hilo lilianza baada ya klabu hizo kuamua kutoka kwenye umiliki wa timu wa wanachama kuelekea kwenye umiliki wa hisa na ukodishwaji. Katika suala hilo, Mwenyekiti wa Yanga, alitaka kuikodisha timu hiyo kwa miaka 10, akiimiliki nembo na timu Yanga, wakati kwa upande wa Simba mfanyabiashara, Mohamed Dewji (Mo), akitaka kuchukua hisa asilimia 51 ya kumiliki klabu hiyo. Wakati wanachama wakibariki mabadiliko hayo ya mfumo wa uendeshaji na Yanga ikiwa tayari imeingia mkataba wa miaka 10 wa ukodishwaji na Kampuni ya Yanga Yetu Limited, Septemba mwaka huu, Simba ikiwa katika hatua ya mwisho kumkabidhi klabu hiyo Mo kwa umiliki wa hisa za asilimia 51. Serikali kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Mohamed Kiganja, alitoa uamuzi wa kusimamisha michakato hiyo hadi timu hizo zitakapofanya mabadiliko ya katiba zao. Alisema iwapo kama Yanga na Simba zinahitaji kubadili mifumo ya uendeshaji wa klabu zao, ni lazima zifanye marekebisho ya katiba zao kwa mujibu wa Sheria ya Baraza hilo na Kanuni za Msajili namba 442 Kanuni 11 kifungu kidogo cha (1-9). Kufungwa Uwanja wa Taifa Katika hali inayoonyesha Serikali imekerwa na vitendo vya uharibifu wa mali zake, Oktoba mbili mwaka huu iliamua kuzizuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo ni baada ya kufanyika kwa uharibifu wa miundombinu ya uwanja huo katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya timu hizo Oktoba mosi mwaka huu na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Mkono wa TRA waigusa TFF Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wilaya ya Ilala, ilizuia fedha zote kwenye akaunti za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa madai ya shirikisho hilo kuwa na malimbikizo ya kodi ya Sh bilioni1.6. TRA ilikuwa ikidai asilimia kubwa ya malimbikizo ya kodi hizo yatokanayo na makato ya mshahara (P.A.Y.E) ya makocha wa kigeni wa timu za taifa katika kipindi cha mwaka 2010-2013, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen. Pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mchezo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazil uliofanyika mwaka 2010, ulichangia deni hilo la kodi kwa asilimia kubwa. Simbu aweka rekodi Olimpiki Kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki tangu mwaka 1980, baada ya Suleiman Nyambui na Filbert Bayi kufanya vizuri nchini Moscow, mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Simbu, aliweka rekodi baada ya kushika nafasi ya tano kwenye mbio za marathon za kilomita 42, Agosti 21 mwaka huu mjini Rio de Janeiro, Brazil. Kujengwa uwanja mkubwa Dodoma Miongoni mwa mambo yaliyowafariji wanamichezo wengi nchini ni baada ya Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, kuahidi kujenga uwanja wa kisasa wa michezo mkoani Dodoma. Rais Dk. Magufuli alimwomba mfalme huyo alipotembelea Tanzania hivi karibuni kwa ziara ya siku tano. Ombi hilo la Rais Dk. Magufuli lilikubaliwa na mfalme huyo ambaye aliahidi kuijenga uwanja huo utakaogharimu dola milioni 80 hadi 100, sawa na Sh bilioni 171.216.
1
["Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka 2019 si mwingine bali ni Lionel Messi, ambaye amejichukulia kinyang'anyiro cha kuwa mchezaji bora zaidi kwa mara ya sita.", 'Mchezaji huyo wa Argentina mwenye miaka 32 amenyakua tuzo hiyo baada ya kuikosa toka mwaka 2015 na hii ni kutokana na kuweza kufunga mara 54 katika klabu ya nchini kwake kwa mwaka 2018-19 .', 'Virgil van Dijk alikuwa mshindi wa pili - yeye ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Liverpool katika saba bora, akiwemo Sadio Mane.', 'Mchezaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, aliwahi kutunukiwa tuzo hiyo mara tano na amekuwa watatu katika kura.', 'Toka mwaka 2008 tuzo hiyo maarufu zaidi ya wasakata kandanda duniani imetawaliwa na washambuliaji hatari katika kizazi cha sasa Messi na Ronaldo. ', 'Mpaka kufikia mwaka 2017, kila mmoja wao akishinda mara tano. ', 'Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa la Croatia Luka Modric aliingilia ufalme wa Messi na Ronaldo baada ya kunyakua tuzo hiyo mwaka jana. ', 'Na sasa Messi amerejea kileleni kwa kumpiku Ronaldo na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kunyakua tuzo hiyo mara sita. ', 'Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa mwaka huu kwa Messi, Ronaldo na Van Dijk kuwania tuzo moja kwa pamoja.', 'Mara ya kwanza walikutana katika tuzo za Mchezaji Bora wa Ulaya (Uefa) mwezi Agosti ambapo Van Dijk aliibuka na ushindi. ', 'Mara ya pili wakaminyana katika tuzo za Mchezaji Bora wa Fifa ambapo Messi aliibuka mshindi.', "Tano Bora ya Ballon d'Or", '1. Leonel Messi (Barcelona na Argentina)', '2. Virgil van Dijk (Liverpool na Uholanzi)', '3. Cristiano Ronaldo (Juventus na Ureno)', '4. Sadio Mane (Liverpool na Senegali)', '5. Mohammed Salah (Liverpool na Misri)', "Ballon d'Or ni nini?", "Tuzo ya Ballon d'Or imekuwa ikitolewa nchini Ufaransa kila mwaka toka 1956, na mshindi wake wa kwanza alikuwa mchezaji kutoka Uingereza Stanley Matthews.", 'Awali tuzo hiyo ilikuwa ni kwa wachezaji wa Ulaya tu kabla ya kufanyika mabadiliko mwaka 1995 na kujumuisha wachezaji wa mataifa yote duniani, mradi wanasakata kandanda katika vilabu vya Ulaya. ', 'Orodha ya majina ya wachezaji 30 bora huandaliwa na baadae kupigiwa kura na wanahabari wa michezo kutoka sehemu tofauti duniani, ambapo kila nchi hupiga kura moja. ', 'Kutoka mwaka 2010 mpaka 2015 tuzo hiyo iliunganishwa na ile ya Fifa lakini zilitengana mwaka 2016 ambapo Fifa ilianza kundaa tuzo zao wenyewe. ']
4
IDADI ya watu waliopoteza maisha kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa, imeongezeka na kufi kia watano huku idadi ya watu ambao hawana makazi ikifi kia 2,205.Pia mvua hiyo pia imeharibu nyumba 441, shule mbili na makanisa mawili. Aidha wakazi 165 kutoka Kijiji cha Mshete wilayani Nkasi kujikuta hawana makazi baada ya nyumba zao 33 kubomolewa na mvua za masika juzi huku mwananchi mwenye umri wa miaka 80, akipoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake.Awali wiki mbili zilizopita, watu wengine wanne walipoteza maisha akiwemo Elizabeth Manamba (85) mkazi wa Kijiji cha Kipeta na mwingine ni mtoto mwenye umri wa miaka minane kutoka Kijiji cha Tunko wilayani Sumbawanga aliyepigwa na radi. Wengine ni watoto wawili waliokuwa wakiishi katika Kijiji cha Matala, Laiton Kalindo (10) aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Matala wilayani Nkasi na Mathias Anselimu (8).Mbali ya hayo, watu wapatao 57 wamejeruhiwa huku paa za Shule ya Sekondari Kipeta zimeizuliwa zote. Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo alielezwa kushtushwa kwake na maafa hayo ambayo amekiri kuwa ni changamoto kubwa huku akisisitiza kuwa yanaweza kuwa makubwa zaidi kwa kuwa hizi ni mvua za awali za masika.“Hofu yangu ni kwamba maafa yanaweza kuwa makubwa ya kutisha kadri mvua za masika zinavyoendelea kunyesha hizi ni za awali tu na zimesababisha maafa makubwa kiasi hiki ni changamoto kubwa kimkoa pekee yetu hatuwezi tunahitaji misaada ya mali na hali kutoka ndani na nje ya mkoa,” alisisitiza. Alisema harambee kubwa inatarajiwa kufanyika ili kuwasaidia waathirika ambao wamepoteza kila kitu huku Shule ya Sekondari Kipeta ambayo imeachwa taabani na mvua hiyo ukarabati wake unahitaji zaidi ya Sh milioni 470.“Wanafunzi wapatao 500 wanaosoma katika Shule ya Sekondari Kipeta iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga hawataweza kuanza masomo shule zitakapofunguliwa Januari mwakani kutokana na miundombinu yake ikiwemo vyumba vya madarasa kuharibiwa na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali,” alieleza. Shule hiyo ina wanafunzi wanaosoma Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Sita ikiwa ni shule ya bweni na mchanganyiko.
3
WIKI hii, Julai 1, Benki ya Dunia iliingiza Tanzania katika kundi la nchi zenye kipato cha kati. Hizi ni habari njema hata pamoja na kwamba wapo wanaoona kuna mapungufu fulani fulani katika utendaji. Hatua ya kutoka katika umaskini na kupanda kwenda katika hatua nyingine ya juu huusisha suala zima la uchumi au maendeleo ya kiuchumi. Lakini pamoja na hayo maendeleo ya kiuchumi huguswa na vitu au mambo mengi mfano kutenda haki, amani, usalama, utulivu nakadhalika. Mtu yeyote anapokuwa katika mazingira yenye kutenda haki, amani, utulivu humwezesha kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuwa mzalendo kwa nchi yake ikiwa ni pamoja na kulipa kodi. Sasa mazingira yanapokuwa tofauti na hayo, ndiyo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi . Kwa sababu hiyo sisi tunaweza kusema tumekuwa mabalozi wazuri wa kusisitiza suala la haki kila wakati, kwa sababu tumekuwa tukiamini haki ni msingi wa mambo yote mazuri. Na ndio maana tumekuwa tukikosa na wakati mwingine kukumbusha kutenda haki hasa katika vyombo vile vya kimaamuzi na kiutendaji. Tumekuwa tukisisitiza kwamba vyombo hivyo vinapaswa kutambua wajibu wao kuwa ni kutafuta namna ya kutatua matatizo na si kuyaongeza. Yapo baadhi ya matukio si yote ambayo yamefanywa na vyombo hivyo na hivyo kutoa taswira ya kukomoa au kuumiza baadhi ya watu kwa makusudi. Tumekuwa tukisisitiza  hayo kutokana na kuwapo kwa ripoti ambazo zinaonyesha kuwa barani Afrika kwa muda mrefu sasa watu wameumizwa na vitendo vya kudhulumiwa haki zao msingi. Kwa mujibu wa ripoti hizo hata kutopea katika umaskini wa kimawazo, na hivyo wengi kuhadaika na kauli za wanasiasa, viongozi na watu wenye nafasi katika jamii, msingi wake ni dhuluma ya haki zao za msingi.  Kwa misingi kama hiyo sisi kama  chombo cha habari  tunao wajibu wa kukumbusha kwamba vyombo hivyo kila inachofanya kabla ya kutoa uamuzi wowote basi vitambue vinao wajibu wa kuchunguza, kusikiliza, kubadilisha na kuboresha. Zipo nyakati tumeshuhudia vyombo hivi vikichukua uamuzi wa ghafla hata katika masuala nyeti sana katika mifumo ya sheria, utumishi nk.  Vyombo hivi vinapaswa kutambua kwamba chochote kitakachofanyika bila kufuata misingi hiyo tuliyoitaja hapo juu kitakwenda kuathiri mustakabali mwema wa Taifa letu. Wakati fulani aliyepata kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedikto wa XVI, alitoa changamoto kubwa kwa watawala wa dunia.  Kwa maneno yake mwenyewe alisema; “jamii yenye haki hujengwa na wanajamii wenye haki”.  Maana yake tukitaka kujenga jamii yenye haki hatuna budi sisi wenyewe kuwa wenye haki. Kiongozi huyo alikwenda mbali na kusema; wao kama kanisa hawana mbinu za kiufundi wala nafasi ya kuingilia mambo ya siasa moja kwa moja lakini alibainisha wazi utume ambao alisema kama kanisa haliwezi kuuacha hata kidogo ni ule wa kuutangaza ukweli. Ukweli si jambo ambalo linapaswa kubebwa na taasisi zetu za kidini tu bali hata katika serikali zetu na taasisi zake, mahakama zetu, vyombo vya ulinzi na uslama kama Jeshi la Polisi,  Bunge nk. Kuna msemo mmoja kwamba; ukweli ndio utakaowaweka watu wote huru: iwe katika siasa au katika nyanja yoyote ya kijamii.  Kwa sababu hiyo tunaamini ujenzi wa jamii yenye misingi ya haki ni wajibu wetu sote lakini serikali, mahakama na Bunge linawajibika kujenga dhamira hiyo.  Mahakama itambue kama ni taasisi ya kupigania haki, serikali ni wakala wa haki vivyo hivyo hata Bunge.  viongozi  wakiwamo wale wa kisiasa, na wananchi watambue kuwa wao ni wawajibikaji katika shughuli za kijamii na iwapo wote hawa watauzingatia ukweli ndani ya dhamiri zao zilizojengwa juu ya ukweli na ukweli tupu, basi jamii ina uhakika wa kujenga haki na amani na matokeo ya hayo ni kupaa kimaendeleo.
5
Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Florens Seiya alisema hayo jana wakati akizungumza na HabariLeo na kuongeza kuwa soko litakalofanyiwa marekebisho ni soko dogo huku lile la shimoni likibakia kama lilivyo likiwa kama ni ukumbusho.Alisema soko hilo litafanyiwa maboresho kulingana na mahitaji ya sasa kwani limekuwepo kwa muda mrefu tangu mwaka 1974 likiwa na wafanyabiashara 800,000 na kwa sasa lina wafanyabiashara wanaofikia milioni tano.“Wengi sana wanategemea hili soko kwa bidhaa mbalimbali, huduma zimepanuka kukiwa na vyakula mbalimbali na aina nyingi za pembejeo,” alisema Seiya na kuongeza kuwa lengo la maboresho ni kujenga soko kubwa litakalokidhi matakwa.Alisema pindi ujenzi ukianza, Shirika hilo litatoa mkataba wa makubaliano kwa wafanyabiashara waliomo katika soko hilo ili kupisha ujenzi na pindi ukikamilika wao ndio watakaopewa kipaumbele cha kurejea.Alisema hadi kufikia Machi mwaka huu Shirika hilo litaeleza kuhusu picha halisi ya ujenzi huo kwa maana unaanza lini huku wakiwa wanatoa taarifa kwa watu wao wanaohusika kwani hawawezi kufanya lolote bila kuwajulisha.
5
WASHINGTON, MAREKANI KUMEKUWA na vurugu na mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minneapolis nchini Marekani, baada ya kifo cha mwanaume mmoja mweusi akiwa mikononi mwa polisi. Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na waandamanaji walirusha mawe na kupulizia mapambo ya graffiti kwenye magari ya polisi. Mashuhuda walieleza kuwa vurugu hizo zilianza siku ya Jumanne jioni, wakati mamia ya watu walipofika katika eneo ambalo tukio lilitokea, Jumatatu jioni. Waratibu walijaribu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuzingatia masharti ya kukaa mbalimbali, waandamanaji waliimga “siwezi kupumua na ingeweza kuwa mimi”. Mmoja wa waandamanaji, Anitha Murray aliliambia gazeti la Washinton Post: “Inaogopesha kuwa hapa wakati wa janga la corona, lakini kwa nini nijiweke mbali?” Kundi la mamia ya watu baadae waliandamana mpaka kwenye idara ya polisi, ambapo maofisa waliohusika na kifo hicho walikuwa wakifanya kazi. Mtu mmoja alikiambia chombo cha habari cha CBS: “Hii ni mbaya sana. Polisi lazima watambue kuwa hali hii wameitengeneza wenyewe.” Polisi walisema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi lakini taarifa za kina hazijatolewa kuhusu tukio hilo. Maofisa wanne wa polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani wamefutwa kazi kufuatia kifo hicho ambaye alikuwa amekamatwa na kuonekana akizuiliwa chini kwa kushikwa shingo. Ofisa Mkuu wa Polisi katika jimbo hilo, Medaria Arradondo alisema kwamba maofisa hao wanne sasa “sio wafanyakzi wa kikosi hicho”. Kanda ya video inaonesha, mtu huyo kwa jina George Floyd, akilia na kuwaambia maofisa hao weupe “siwezi kupumua”. Kisa hicho kinafanana na kile cha Eric Garner, mtu mweusi aliyefariki akikamatwa na polisi mjini New York mwaka 2014. Shirika la ujasusi nchini Marekani (FBI) lilisema litachunguza kisa hicho cha Minneapolis kilichofanyika Jumatatu jioni. Maofisa wa polisi wa Minnesota walisema kwamba Floyd mwenye umri wa miaka 46, ambaye alikuwa anafanya kazi kama ofisa wa usalama katika mkahawa mmoja alifariki akifanyiwa matibabu kufuatia malumbano na maofisa wa polisi. Siku ya Jumanne, Meya Jacob Frey alithibitisha kwamba maofisa hao wanne waliohusishwa na kisa hicho wamefutwa kazi.  Katika mkutano na vyombo vya habari mapema, a Frey alikitaja kisa hicho kama cha kushangaza. “Ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango chochote kile. Kuwa mtu mweusi nchini Marekani hakustahili kuwa hukumu ya kifo,” alisema. Ni madai ya hivi karubuni ya unyanyasaji unaotekelezwa na maofisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi. Visa maarufu vya hivi karibuni vinashirikisha afisa mmoja wa eneo la Maryland ambaye alimpiga risasi mtu mmoja akiwa ndani ya gari la kupiga doria. Kisa hicho cha Minneapolis kilianza baada ya ripoti kwamba mteja mmoja alikuwa anajaribu kutumia noti bandia ya dola 20 katika duka moja. Ofisa huyo alimuona mshukiwa akiwa ndani ya gari lake, mtu huyo alikataa kukamatwa kulingana na maofisa wa polisi. Waliambiwa kwamba mtu huyo ambaye hajatambulika alikuwa ameketi juu ya gari la rangi ya buluu na alionekana kana kwamba ametumia kishawishi fulani. Baada ya kuagizwa kuondoka na kusimama kando ya gari hilo, jamaa huyo alikataa kukakamtwa lakini maofisa walifanikiwa kumfunga mikono yake kwa pingu na akaonekana kana kwamba alikuwa anaugua tatizo la tiba, taarifa hiyo iliongezea. Katika kanda hiyo ya dakika 10 iliochukuliwa na shahidi, mtu huyo aliwekwa ardhini na ofisa huyo na katika wakati mmoja alisikika akisema ”musiniue”. Shahidi mmoja alisikika akimwambia ofisa huyo kuondoa goti lake katika shingo ya mshukiwa huyo, akidai kwamba alikuwa hayumbi. Mwengine alisema pua yake inatoka damu, huku mwengine akiomba ”ondoka katika shingo yake”. Mtu huyo anaonekana ametulia kabla ya kuingizwa katika ambulansi na kuondoka naye. BBC
2
MFANYABIASHARA Khamis Luwonga, maarufu kama Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, ameiomba Mahakama ya Hakimu Kisutu, Dar es Salaam apatiwe laini zake mbili za simu zenye zaidi ya Sh milioni 5 kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake, ikiwemo kumlipia ada mwanawe.Luwonga amefika mahakamani hapo akiwa na pingu miguuni, baada ya hivi karibuni kutoa vitisho mahakamani hapo kwa waandishi wa habari, kwamba atawafanyia kitu kibaya.Alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.Baada ya Simon kueleza hayo, mshitakiwa huyo alinyoosha mkono na kudai kwamba ana mambo mawili muhimu, ikiwemo kupatiwa nakala yake ya hati ya mashitaka na laini zake za simu zilizopo Kituo Kikuu cha Polisi.Alidai laini hizo zina zaidi ya Sh milioni 5, hivyo zinaweza kutumika kwa matumizi madogo madogo pamoja na kumlipia ada ya mwanaye.“Sitaki simu ila naomba nipatiwe laini, ambazo nitampatia ndugu yangu atoe fedha kwa ajili ya matumizi, ikiwezekana zitolewe hata Polisi wakiwepo,” amedai Luwonga.Wakili Wankyo alidai kuwa simu hizo ni sehemu ya upelelezi, hivyo kwa sasa itakuwa ngumu kumpatia, kwa sababu hawawezi kuamini moja kwa moja, kama kweli anahitaji kutoa fedha.Pia alidai kuwa kesi hiyo ni ya mauaji na maombi hayo alipaswa kuyawasilisha katika Mahakama husika, yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, ambayo ni Mahakamani Kuu.Pia, alidai kama anahitaji fedha hizo, basi amuandikie barua Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally alimuelekeza mshitakiwa kutumia mbinu ya kuandika barua na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10, mwaka huu itakapotajwa.Katika kesi hiyo, mshitakiwa anakabiliwa na kosa moja la mauaji kinyume cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Namba 196 Sura 16, kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.Katika kesi hiyo ya muaji namba 4 ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, mwaka huu akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni, alimuua Naomi Marijani.
3
KATIKA kutatua migogoro ya ardhi, Jiji la Dodoma limeanzisha programu maalumu ya kutoa viwanja vya makazi bure kwa wananchi waliojenga kwenye maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za umma, ili kuwezesha kuondoka katika maeneo hayo.Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, aliliambia Baraza la Madiwani jana kuwa programu hiyo itasaidia kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo wameirithi kutoka iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA). “Mpaka sasa, tumetenga viwanja vipya 1,170 katika eneo la Kata ya Ipagala kwa wananchi ambavyo vitakuwa na maeneo ya wazi, barabara za mitaani na ardhi kwa ajili ya kujenga taasisi za umma, lengo ni kuwaondoa katika maeneo yaliyokuwa kwa matumizi ya umma,” alisema.Akifafanua zaidi, Kunambi alisema wananchi ambao watakuwa kwenye mpango huo wa kupewa viwanja bure kwa ajili ya makazi, watatakiwa kulipa ada ya kisheria kwa Jiji na kuwa mamlaka zitathibitisha majina ya wananchi hao. Aidha, Kunambi alisema Jiji pia limeanza kupima viwanja vipya vya makazi maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dodoma katika maeneo ya Hombolo, Iyumbu, Kikombo na Nzuguni. “Wananchi wa Dodoma kwa sasa anaweza kumiliki kiwanja cha makazi kwa Sh 900,000 ikiwa ni gharama ya chini,” alisema.Kunambi alisema Jiji limekuwa na mafaniko makubwa katika upimaji na upangaji wa miji wa kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne na kuwa mpaka sasa mamlaka hiyo imepima viwanja kwa matumizi mbalimbali 100,000 katika maeneo mbalimbali ya jiji. Naye, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alilipongeza Jiji la Dodoma kwa mafanikio na mikakati iliyofanya na kusisitiza kuwa kwa sasa migogoro ya ardhi imepungua. Mavunde alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa Jiji kutembelea na kusikiliza kero za wananchi ili waweze kutatua changamoto hizo ikiwamo ile ya migogoro ya ardhi.
3
Mwandishi Wetu -Singida BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 katika wilaya kadhaa nchini. Misaada iliyotolewa na benki hiyo inayoongoza kwa kutengeneza faida kati ya benki zote zinazofanya biashara humu nchini ndani ya miezi mitano mwaka huu, inahusisha vifaa vya ujenzi, madawati na vifaa vingine vinavyowezesha ukamilishaji wa miradi ya afya,elimu na usalama wa raia. Benki  ya NMB imeshatoa  msaada wa  vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa mikoa ya Kanda ya Kati. Akifafanua kuhusu misaada hiyo wakati akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani ingida, Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Nsolo Mlozi, alibainisha kuwa misaada hiyo ya zaidi ya Sh milioni 200 iliyotolewa imelenga sekta ya elimu, afya  na majanga kwa mikoa mitatu ya  Kanda ya kati. Akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, MkoaniSingida, katika shule ya Sekondari ya New Kiomboi, Mlozi alisema fedha hizo zilizotolewa na NMB zimetumika kununua madawati, viti vya shule za sekondari,vitanda na vifaa tiba kwenye sekta ya afya. Aidha, alisema lengo la misaada hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali. Pia alisema misaada hiyo imekabidhiwa kwa baadhi ya shule, zahanati, hospitali katika mikoa ya Singida, Dodoma na Manyara. Pia NMB walikabidhi madawati 250 na vitanda 80 vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 29.5 kwa baadhi ya shule za Wilaya ya Iramba mkoani humo. Katika hatua nyingine, Benki hiyo imevipatia kituo cha Polisi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro pamoja na shule ya msingi Msowelo mabati 160 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa ajili ya kuezekea maboma. NMB iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni mpango wa kuzipunguza baadhi ya changamoto kwa taasisi za serikali hapa nchini, Meneja wa NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus, alisema na kubainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia kuinua miradi ya maendeleo. Baraka alisema kuwa kati ya mabati hayo, kituo cha polisi wilaya kimepa tamabati 80 huku shule ya msingi Msowelo nayo ikipata mabati 80.
5
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuimarisha mshikamano ili mwenendo wa usimamizi wa rasilimali madini usaidie kuimarisha uchumi.Aidha, amevitaka vyombo hivyo kutumia weledi na utashi kuhakikisha vinaweka mazingira bora katika maeneo yao yatakayowezesha kuvutia wawekezaji.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifunga rasmi Semina ya siku mbili iliyoshirikisha Wizara ya Madini, Vyombo vya ulinzi na usalama kutoka mikoa yote nchini pamoja na wadau wa madini iliyolenga katika kuimarisha usimamizi na udhibiti wa rasilimali madini.Majaliwa amewataka maofisa madini kote nchini kuimarisha ushirikiano na wadau pamoja na vyombo vya ulinzi ili kuwezesha shughuli za madini kutelekelezwa kikamilifu.Katika hatua nyingine, amevitaka vyombo hivyo kuacha matumizi ya lugha za jazba na zinazokatisha tamaa pindi inapotokea changamoto na kuvitaka kutoa nafasi za kujieleza ili kuendelea kuwatia moyo wawekezaji.“Hatutaki kuona wawekezaji wanatuibia lakini kuna njia zinazofaa kuchukuliwa wakati wa kushughulikia masuala haya. Tumieni sheria, kanuni na miongozo mahususi iliyowekwa katika kusimamia sekta hii,” alisema  Waziri Mkuu.Hatahivyo, amevitaka vyombo hivyo kujenga mazingira rafiki ya kazi, kuaminiana na kufanyakazi kwa umoja na ushirikiano huku vikizingatia nafasi na taaluma za wengine wanaohudumu kwenye sekta ya madini.Akizungumzia semina hiyo, Waziri wa Madini Dotto Biteko alimweleza Waziri Mkuu kuwa ni hatua ya mwanzo ya kujenga mazingira ya kuvutia mitaji ya uwekezaji katika sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi na kwamba kukutana huko kumesaidia kujenga uelewa wa pamoja katika kuimarisha usimamizi wa sekta ya madini.Semina hiyo ni ya kwanza kufanyika nchini kati ya Wizara ya Madini na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
3
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imejipanga kuendeleza bandari kiushoroba kuongeza ufanisi wa huduma na kuzisogeza karibu zaidi na wateja.Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema, ili kuweza kupata manufaa hayo, bandari hizo hazina budi kwenda sambamba na maendeleo ya ushoroba ndani ya nchi na kieneo.Amesema kwa upande wa ushoroba wa Kati Kaskazini (Mwanza), imelenga uboreshaji wa bandari ya ziwa Victoria na ujenzi wa bandari kavu ya Fela- Mwanza na utasogeza huduma za bandari kwa wateja wa Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Uganda na Sudan Kusini.Aidha alisema kwa upande wa Kati- Kaskazini-Magharibi inayohusisha Isaka- Kibanga/Rusumo, wataboresha bandari kavu ya Isaka kwa kushirikiana na TRC ambapo kwa pamoja kutarahisisha usafirishaji wa shehena ya bandari kwenda na kutoka nchi za Rwanda na Burundi.“Sambamba na juhudi hizi ni mpango wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali…Pia uboreshaji na ujenzi wa bandari za Ziwa Tanganyika na Bandari Kavu ya Katosho-Kigoma utasogeza huduma za bandari kwa wateja wa magharibi mwa Tanzania na nchi jirani za Burundi na DRC,” alisema.Amesema TPA inashirikiana na TAZARA ili kuhakikisha huduma za reli ya TAZARA zinarejea angalau kwa kiwango cha kuridhisha ili kuhudumia wateja wa Kusini Magharibi mwa Tanzania, sambamba na mpango wa kujenga bandari Kavu ya Inyala-Mbeya ili kuhudumia shehena inayokwenda nchi jirani za DRC, Malawi na Zambia.“Kwa upande wa ushoroba wa bandari ya Tanga, tunaendelea na uboreshaji ikiwa ni pamoja na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa namna bora ya kuongeza kina cha bandari ya Tanga,” amesema.Amesema ili kusogeza karibu huduma za shehena kwa wateja wa ushoroba wa Tanga, TPA imebainisha eneo karibu na Arusha ili kwa na bandari kavu itakayotoa huduma za bandari ikiwa ni pamoja na kuhimili ushindani kutoka bandari ya nchi jirani.“Ushoroba wa Tanga utaimarika zaidi kama reli ya Tanga-Arusha-Musoma itajengwa ili kuhudumia wateja wan chi jirani za Uganda na Sudan Kusini,” amesema.Aidha amesema hivi sasa wanaendelea na maboresho ya bandari ya Mtwara ili pamoja na juhudi za wadau wengine, ushoroba huo uwe na uwezo wa kuhudumia wateja wa kusini mwa Tanzania na kuhimili ushindani kutoka bandari za nchi jirani za Afrika Kusini, Msumbiji na Namibia.
5
Ten alisema Mwenyekiti wa kamati hiyo atakuwa ni Majid Suleiman na Makamu wake Mustapha Urungo na Urio Edward ni Katibu. Ten aliwataja wajumbe wengine kuwa ni Rodgers Gumbo, Omary Chuma, Yanga Makoga, Lameck Nyambaya, Samuel Lukumayi, Hussein Nyika, Edgar Mutani, Leonard Chinganga na Yusuph Mohamed.Ten alieleza kamati hiyo imeundwa na Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na inaanza kazi mara moja kuhakikisha Yanga inafanya vyema katika mechi zake za Ligi Kuu. Sanga amekaririwa akisema ana imani kamati hiyo itafanya vyema kazi yake na kutimiza malengo yao kuwa bingwa tena msimu huu.“Ni kamati ya kawaida ambayo ina lengo la kuhakikisha ubingwa unaendelea kubaki Jangwani kwa msimu wa nne na kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema. Yanga inaendelea na usajili kuimarisha safu yake na jana ilikamilisha usajili wa kiungo wake wa kimataifa Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.Wakati huohuo, Simba wameimarisha safu ya ulinzi baada ya kumsajili kipa Said Mohamed ‘Nduda’ aliyeng’ara michuano ya Cosafa kwa mkataba wa miaka miwili. Usajili wake unaifanya Simba msimu ujao iwe na makipa watatu wote wapya. awali ilimsajili kipa Aishi Manula wa Azam na Emmanuel Mseji wa Mbao FC ya Mwanza.Simba pia imemsajili Erasto ambaye awali alikuwa akichezea Azam FC. Nyoni kama alivyo Manula na Nduda wako Taifa Stars. Waliondoka na Stars jana kwenda Kigali, Rwanda kwa mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (Chan).
4
NAIROBI, KENYA WATU zaidi ya 50 wamefariki dunia nchini hapa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu itokayo jijini hapa kwenda Kisumu. Vyombo vya habari vililiripoti jana kwamba ajali hiyo ilitokea katika eneo la Fort Ternan, Kaunti ya Kericho. Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilitoka barabarani baada ya dereva kushindwa kulimudu kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kuserereka mita 20 katika bonde. Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation, miongoni mwa waliofariki ni watoto wanane wa chini ya umri wa miaka mitano. Awali idadi ya waliofarini ilikuwa 40, lakini polisi walielezea hofu yao juu ya vifo kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya. “Bahati mbaya sana tumepoteza watu 51,” Mkuu wa Jeshi la Polisi, Joseph Boinnet alikiambia Kituo cha Redio Capital FM. Mashuhuda walisema ajali hiyo ilitokea  jana majira ya saa 11 alfajiri. Mmoja wa mashuhuda hao aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC kwamba alisikia honi, ikifuatwa na mlio mkubwa wa breki, kisha akawasikia abiria wakipiga kelele. Baadhi ya majeruhi wanatibiwa katika Zahanati ya Fort Ternan, huku wengine wakikimbizwa hadi hospitali ya kaunti mjini Muhoroni kupatiwa matibabu. Taarifa zaidi zilieleza kuwa miili ya baadhi ya watu waliofariki hadi mapema jana ilikuwa bado imekwama ndani ya mabaki ya
2
Na ASHA BANI – Dar es Salaam WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amezitaka sekta za fedha nchini, hasa mabenki kuwa kichocheo cha uchumi wa viwanda. Dk. Mpango ameyasema hayo jana Dar es Salaam wakati wa  uzinduzi wa jina na nembo mpya ya Benki ya Posta Tanzania (TPB). Alisema kuwa sekta ya mabenki ni muhimu hasa katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo na viwanda vya kati  hali itakayoweza kuchangia uchumi wa viwanda vikubwa nchini. “Mabenki, hasa ikiwamo Benki ya Posta ndiyo kichocheo kikubwa katika kuwainua akina mama wanaofanya biashara ndogo ndogo,” alisema. Katika hatua nyingine, Dk. Mpango aliipongeza bodi ya benki hiyo kwa kufanya kazi kwa ufanisi, ikiwamo kuongeza idadi ya matawi kutoka 28 ya awali na kufikia 60 ya sasa. Dk. Mpango alisema benki hiyo imefanikiwa kuwanufaisha wastaafu mbalimbali mijini na vijijini jambo ambalo ni hatua nzuri na ya kupongezwa. Alisema Serikali itahakikisha inafanya nayo kazi bega kwa bega ili kuwaongezea nguvu iweze kusaidia jamii zaidi. Awali Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, alisema benki imekamilisha mchakato wa muda mrefu wa kuisajili kuwa chini ya sheria ya makampuni. Mchakato wake ulikamilika mwanzoni mwa mwaka jana. “Benki iliamua kubadilisha nembo yake ili kwenda sambamba na jina hilo pamoja na mabadiliko makubwa ya kuiboresha yanayoendelea,’’ alisema Moshingi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Profesa Letticia Rutashobya, alimhakikishia Dk. Mpango kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuweka jitihada zaidi ili kuwafikia Watanzania wengi, hususan walioko pembezoni ili waweze kunufaika na huduma hizo za kifedha.
3
Mechi hiyo ni kama marudio ya fainali za mwaka 2012 iliyofanyika kwenye uwanja huohuo wa taifa, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.Mechi ya leo inatazamwa kwa hisia tofauti ikitarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kutokana na uimara wa timu zinazokutana.Yanga imekuwa ikiisumbua Azam FC mara kadhaa kila inapokutana nayo.Mara ya mwisho Yanga kuifunga Azam ilikuwa ni kwenye mechi ya ngao ya jamii Agosti mwaka jana, ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.Kwenye Ligi Kuu msimu uliopita timu hizo hazikutambiana, ambapo katika mechi ya kwanza zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na mechi ya pili zilitoka sare ya 1-1.Timu hizo zilimaliza nafasi mbili za juu kwenye ligi hiyo, Yanga ikitwaa ubingwa na Azam ikishika nafasi ya pili.Kwa sasa timu hizo zimefanya usajili kujiandaa na michuano mbalimbali na hakuna ubishi kwamba kila timu ina kikosi imara, hali inayofanya mechi ya leo kushindwa kutabirika kirahisi.Akizungumzia mechi hiyo kocha wa Yanga, Hans Van der Pluijm amesema anatarajia kupata upinzani mkubwa kutokana uimara wa wapinzani wake. Hatahivyo, alisema hilo halimtishi kwani hata yeye ana kikosi kizuri ambacho anatarajia kitapata matokeo mazuri leo.“Mechi yetu na Azam nafahamu itakuwa ngumu sana kwasababu wapinzani wetu nao wana timu nzuri, lakini hatuiogopi kwani hata sisi timu yetu nzuri naamini wachezaji watatupa matokeo mazuri leo,” alisema.Naye kocha wa Azam Stewart Hall alisema amewaandaa wachezaji wake kuifunga Yanga na hawaiog opi kama wengi wanavyodhani. “Hatuiogopi Yanga, tunao uwezo wa kuifunga na tunaamini hilo litatokea,” alisema.Chini ya Hall kwenye michuano hiyo, Azam imecheza mechi tatu na kufunga mabao manane huku ukuta wake ukiwa haujaruhusu bao hata moja, matokeo ambayo yanaipa kiburi timu hiyo kuona kwamba hata leo Yanga inaweza isione ‘ndani’.Kabla ya mechi hiyo ya wenyeji itakayochezwa saa 10 jioni, mechi ya awali itakuwa ni kati ya KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy ya Sudan.
4