text stringlengths 2 8.91M |
|---|
mgawanyo allocation wa fedha hizi umezingatia vipaumbele vya mambo yanayotakiwa katika ukamilifu wa huduma za afya zinazotolewa na kituo cha huduma za afya |
aidha mgawanyo unazingatia kuwa fedha za uchangiaji ni nyongeza complementary funds kwenye fedha nyingine zinazotolewa na serikali katika kugharamia huduma za afya |
vilevile mgawanyo huu umezingatia vipaumbele vya serikali kwa sasa |
hivyo matumizi ya fedha za uchangiaji ni lazima yazingatie mgawanyo ufuatao i |
matumizi katika ununuzi wa dawa vifaa tiba na vitendanishi yasipungue ya mapato yote yatokanayo na fedha za uchang iaji ii |
matumizi kwa ajili ya malipo ya masaa ya ziada na motisha za watumishi yasizidi ya mapato yatokanayo na fedha za uchangiaji iii |
ukarabati mdogo wa miundombinu katika kituo cha kutolea huduma usitumie zaidi ya fedha za uchangiaji iv |
matumizi kwa jili ya matengenezo na matengenezo kinga ya vifaa ambavyo vinatumika kwa ajili ya matibabu medical equipment yasizidi ya mapato yatokanayo na fedha za uchangiaji v |
matumizi mengineyo yasizi di ya mapato ya tokanayo na fedha za uchangiaji fedha za uc hangiaji wa huduma za afya zinakusudia kuimarisha na kuboresha huduma za afya katika vituo |
taratibu za kufanya malipo malipo katika ngazi mbali mbali za vituo vya kutolea huduma za afya yata takiwa kuzingatia taratibu heria kanuni na miongozo ya malipo ya fedha za umma |
watia saini katika hundi katika kila kundi watia saini watachaguliwa kulingana na sheria taratibu na miongozo iliyotolewa na serikali |
hospitali maalum za kanda hospitali ngazi ya taifa katika kundi hili watia saini watachaguliwa kuli ngana na sheria taratibu na miongozo ya fedha iliyopitishwa na bodi za hospitali husika |
ii |
hospitali ya rufaa ya mkoa halmashauri watia saini watakuwa wawili mmoja kutoka kundi na mmoja kundi b |
kundi a mganga mkuu wa mkoa mganga mkuu wa halmashauri na mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa halmashauri katibu wa hospitali kundi b katibutawala mkoa mkurugenzi wa halmashauri au mhasibu wa mkoa mweka hazina wa halmashauri |
iii |
katika vituo vya afya na zahanati kundi a mganga mkuu wa halmashauri na mganga mfawidhi wa kituo cha afya au zahanati kundi b mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya kituo na mjumbe mmoja wapo atakayechaguliwa miongoni mwa wajumbe wa kamati |
muhimu i |
hairuhusiwi kwa wajumbe wa kundi moja kutia saini hundi wote wawili kwa wakati mmoj ii |
kabla ya malipo ya kituo kufanyika ni lazima yapitishwe na kamati ya usimamizi ya kituo iii |
malipo yote ya hospitali vituo vya afya na zahanati yasiyozidi milioni tatu yaidhinishwe na mganga mkuu wa halmashauri |
iv |
malipo yote ya hospitali vituo vya afya na ahanati lazima yaidhinishwe na mkuugenzi mtendaji wa halmashauri v |
malipo yoyote kwa watu wa nje yafanyike kwa hundi iliyofungwa |
kuchacha kwa hundi hundi ikimaliza miezi sita baada ya kuandikwa bila kuwasilishwa benki haitakubalika tena na benki hundi ya namna hii huwa imechacha |
ni muhimu kituo kuchukua hatua za tahadhari kuepuka athari za hundi kuchacha kwa kuhakikisha kuwa hundi zilizopokelewa zinapelekwa benki mara moja bila kuchelewa |
wateja pia washauriwe kuwasilisha benki hundi za malipo yaliyofany wa bila kuchelewa |
hundi ya malipo yaliyofanywa na kituo ikichacha marekebisho yafanyike katika daftari la fedha |
nyaraka muhimu katika kuidhinisha na kufanya malipo malipo yote yanatakiwa kuambatana na hati ya malipo payment voucher na mpango wa matum izi unaonesha kibali au idhini ya kamati ya uendeshaji bodi ya ushauri ya hospitali |
hati ya malipo ioneshe jina la mlipwaji kasma au fungu husika tarehe aina ya malipo na maelezo yote muhimu kuhusu malipo hayo |
ii |
hati ya malipo iandikwe kwa makini kwa kujaza kwa uwazi na mwandiko unaosomeka vizuri kila kipengele kinachohitajika kujazwa |
iii |
hati ya malipo itoe maelezo ya kina kuhusu sababu za malipo yanayofanyika |
iv |
hati ya malipo iambatishwe na ushahidi wa maandishi unaoonesha uhalali wa malipo kama hati ya madai |
v |
hati ya malipo ikishalipwa pamoja na viambatisho vyote ipigwe muhuri kuonesha imelipwa |
vi |
hati iandikwe nakala tatu kwa kutumia kaboni na kugawanywa kama ifuatavyo a |
nakala ya kwanza ibakie kwenye kitabu kwa ajili ya ukaguzi b |
nakala ya pili itumike kufanya maingizo kwenye daftari la fedha |
nakala ya tatu apewe anayelipwa vii |
anayeidhinisha malipo ni lazima kuzingatia kuwa maelezo yote muhimu yako kwenye hati na nyaraka zote zinazothibitisha usahihi na uhalali wa malipo hayo zimeambatishwa |
utunzaji wa hesabu na taarifa za fedha kila kituo cha kutolea huduma kinapaswa kutunza hesabu za fedha na kuandaa taarifa kwa mujibu sheria taratibu na miongozo ya utunzaji wa fedha za umma |
utunzaji wa hesabu kila kituo cha kutolea huduma za afya kitatunza daftar la fedha lenye kumbukumbu za fedha za mwaka mzima kama ifuatavyo i |
mhasibu wa kituo au mtu yeyote aliyekabidhiwa majukumu hayo atatunza kitabu cha fedha cash book kwa ajili ya kuandika kila fedha zinazokusanywa na zinazotumika |
ii |
stakabadhi zote na hat za malipo zitakuwa zinatayarishwa na mhasibu wa kituo cha huduma za afya au mtu aliyekabidhiwa majukumu hayo |
iii |
waganga wafawidhi wa vituo vya huduma za afya watahakikisha hesabu za kituo zinatayarishwa kila mwezi na kuzituma kwa maafisa masuhuli katik mamlaka husika |
usuluhishi wa benki bank reconciliation mhasibu mganga mfawidhi wa kituo cha kutolea huduma au mtumishi aliyepangwa na mweka hazina mhasibu mkuu katika vituo hivyo watatayarisha usuluhishi wa benki bank reconciliation kila mwisho mwezi kulingana na daftari la fedha cash book na kulingana na taarifa ya benki bank state... |
usuluhishi reconciliation huo wa kibenki utatakiwa kusainiwa na aliyeuandaa na kuidhinishwa na mganga mfawidhi wa kituo |
taarifa za usuluhishi za kila mw ezi zitahifadhiwa pamoja na nyaraka nyingine za fedha ili ziwepo wakati wa ukaguzi |
kitabu cha kasma vote book vituo vya kutolea huduma za afya vinatakiwa kuwa na kitabu cha kasma vote book ambacho wataingiza malipo yote kufuatana na bajeti iliyoidhin ishwa na bodi ya hospitali au kamati ya usimamizi ya kituo wa mwaka husika |
kitabu hiki kinaonesha mwenendo wa matumizi kwa kulinganisha na fedha iliyotengwa kwa kila kasma |
taarifa za fedha taarifa za fedha zitatengenezwa kutokana na muhtasari wa daftari la fedha |
muhtasari huu utatengenezwa kuanzia mwezi julai na kuendelea ili kupata limbikizo la mwaka wa fedha |
kila mwezi msimamizi wa kituo ataandaa taarifa za fedha ambazo zitathibitishwa na bodi kamati ya uendeshaji ya kituo na kuwasilishwa kwa mamlaka husika kila robo mwaka |
taarifa hizo zitajumuisha i |
taarifa ya usuluhishi wa kibenki ii |
taarifa ya mapato na matumizi iii |
tathmini ya bajeti iv |
orodha ya mali za kudumu na mali za muda mfupi v |
orodha ya wadai na wadaiwa taarifa za mapato na matumizi ya kituo baada ya uwa zimewasilishwa na kuidhinishwa na bodi kamati za uendeshaji lazima zibandikwe kwenye mbao za matangazo ili wananchi wajue mwenendo wa mapato na matumizi ya kituo |
udhibiti wa ndani internal controls kituo cha kutolea huduma za afya au kamati ya uend eshaji ya kituo wataweka wazi sera zote zinazohusu udhibiti wa ndani |
watumishi wa kituo cha kutolea huduma za afya watafanya kazi zao kulingana na mgawanyo wa kazi uliowekwa na rasilimali zote zilizopo katika kituo lazima zilindwe |
pia kumbukumbu mbalimba li zikiwemo zile za kihasibu zitunzwe kikamilifu na kwa usahihi |
aidha shughuli zote za kituo zitekelezwe kwa ufanisi na kwa kufuata kanuni na miongozo iliyopo |
kituo kihakikishe kwamba i |
majukumu ya kila mtumishi yamewekwa wazi kwa maandishi |
ii |
majukumu ya kila chombo cha utendaji katika kituo yako kwa maandishi |
iii |
mtu mmoja hapewi majukumu ya udhibiti kutoa idhini na kutunza kumbukumbu za mali au vifaa kwa wakati mmoja |
iv |
unajengwa utamaduni wa kuruhusu kazi ya mtu mmoja kuhakikiwa na mtu mwingine anapotekelez kazi yake |
mfano kazi ya mwandika hati ya malipo isahihishwe na yule anayeidhinisha hati ya malipo na anayesaini hundi |
usimamizi shirikishi na ukaguzi wa fedha mamlaka zinazohusika na usimamizi wa vituo vya kutolea huduma zitafanya usimamizi shirikishi ili kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa mwongozo |
aidha timu itakayohusika na usimamizi shirikishi itafanya ukaguzi wa fedha na kutoa ushauri |
usimamizi shirikishi wa kituo usimamizi shirikishi ufanywe na timu kutoka mamlaka husika ili kusaidi na kushauri kituo |
kazi ya usimamizi shirikishi ufanywe angalau kila robo mwaka na kutoa taarifa kwa bodi kamati ya uendeshaji ya kituo |
usimamizi shirikishi uhakikishe kuwa i |
sera taratibu sheria kanuni na miongozo ya serikali imewekwa wazi kwa wananc hi na zinatekelezwa |
ii |
kumbukumbu na takwimu muhimu zinatunzwa inavyotakiwa |
iii |
vitabu vya hesabu vinaandikwa inavyotakiwa |
iv |
taarifa za fedha zinatayarishwa inavyotakiwa na kusomwa katika vikao |
kumbukumbu za vikao zinatunzwa ipasavyo |
vi |
pale ambapo kuna ukiukwaji wa taratibu na kanuni taarifa itolewe kwa mamlaka husika ili wakaguzi waweze kufanya ukaguzi na kutoa taarifa rasmi |
ukaguzi wa ndani mkaguzi wa ndani atatoka katika mamlaka husika kama ifuatavyo ofisi ya waziri amjw ras mkurugenzi mtendaji wa halmash auri |
kazi ya ukaguzi wa ndani ifanyike na taarifa za ukaguzi wa ndani zitajadiliwa katika kikao cha timu ya uendashaji wa kituo cha huduma bodi ya ushauri ya hospitali kamati ya usimamizi ya kituo bodi ya afya ya halmashauri |
ukaguzi wa nje ukaguzi wan je utafanyika kulingana na sharia taratibu kanuni na miongozo iliyopo ya serikali |
sura ya nne ununuzi wa bidhaa huduma na utunzaji wa kumbukumbu |
utangulizi ununuzi wa bidhaa za kituo lazima ufuate mipango iliyoidhinishwa na mamlaka husika |
ununu zi utahusu huduma au bidhaa zilizotengewa fedha kulingana na mpango wa ununuzi wa mwaka ulioidhinishwa katika bajeti ya kituo ya mwaka husika |
aidha pamoja na kuwepo kwa mipango na bajeti lazima taratibu na kanuni za ununuzi wa umma zizingatiwe |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.