doc_id stringlengths 4 9 | title stringlengths 1 70 | text stringlengths 17 5.04k |
|---|---|---|
17#6 | Historia ya Afrika | Baina ya karne ya 1 KK na karne ya 16 BK watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kibantu watokao sehemu za Nigeria na Cameroon ya leo, ndio waliokuwa wameenea kwenye sehemu mbalimbali kusini mwa bara la Afrika, wakiwa wameanzisha vijiji, mashamba na mamlaka katika sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo, za Luba na Mwememutapa, lakini makundi ya wachungaji wa wanyama walianza kuhamia kusini katika karne za 15 na 16 na kukutana na Wabantu. Ndipo walipoanzisha mamlaka zao za Bunyoro, Buganda, Rwanda na Ankole. |
17#10 | Historia ya Afrika | Kati ya miaka 1880 na 1912, Wazungu waligawana bara la Afrika, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa Wazungu isipokuwa Liberia na Ethiopia. |
17#11 | Historia ya Afrika | Wafaransa wakachukuwa Afrika Magharibi na Kaskazini na kwa hivyo nchi za Afrika Magharibi: Dahomey (sasa Benin), Guinea, Mali, Cote d'Ivoire, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (sasa Burkina Faso) zilikuwa chini ya utawala wake. Hali kadhalika, Algeria, Tunisia na Morocco zilitawaliwa na wao. Aidha, Wafaransa walitawala Togoland, Somaliland, Madagascar, Comoro, na Reunion. |
17#12 | Historia ya Afrika | Waingereza nao wakatawala Afrika Mashariki na Kusini, na kuwa sehemu ya Sudan na Somalia, Uganda, Kenya, Tanzania (chini ya jina la Tanganyika), Zanzibar, Nyasaland, Rhodesia, Bechuanaland, Basutoland na Swaziland chini ya utawala wao na baada ya kushinda katika vita huko Afrika ya Kusini walitawala Transvaal, Orange Free State, Cape Colony na Natal, na huko Afrika ya Magharibi walitawala Gambia, Sierra Leone, the Gold Coast na Nigeria. |
17#17 | Historia ya Afrika | Nchi ya kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910. Misri, katika mwaka wa 1922 walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tangier katika mwaka wa 1925. |
17#18 | Historia ya Afrika | Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka wa 1956, na wakarudishiwa Tangier. |
17#19 | Historia ya Afrika | Katika mwaka huu wa 1956, Sudan na Tunisia vile vile walipata uhuru wao, na Ghana katika mwaka wa 1957, Guinea katika mwaka wa 1958, na vile vile Morocco wakarudishiwa Spanish Morocco. |
17#20 | Historia ya Afrika | Katika mwaka wa 1960 Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo (Brazzaville), Cote d'Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (Burkina Faso). |
17#21 | Historia ya Afrika | Vile vile, katika mwaka huohuo wa 1960 Congo (Kinshasa), Nigeria, Somalia, na Togo zikapata uhuru, na katika mwaka wa 1961 Sierra Leone na Tanganyika zikapata uhuru, na Afrika ya Kusini ikawa Jamhuri. |
17#22 | Historia ya Afrika | Katika mwaka wa 1962 Algeria, Burundi, Rwanda, na Uganda zikawa huru, na 1963 zikafuatia Zanzibar, Gambia na Kenya, na katika mwaka wa 1964 Malawi (Nyasaland), na Zambia (Rhodesia ya Kaskazini) zikapata uhuru. |
17#24 | Historia ya Afrika | Aidha, katika mwaka wa 1974 Guinea ya Kireno (Guinea-Bissau) ikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1975 Angola, Cape Verde, Mozambique, Sao Tome na Principe zikapata uhuru. Hispania vilevile ikaitoa Sahara ya Magharibi kwa Morocco na Mauritania katika mwaka wa 1976, lakini wananchi wakakataa kuwa chini ya nchi mbili hizi, kukazuka vita. Mauritania ukaitoa sehemu yake na kuipa Morocco katika mwaka wa 1979, tatizo ambalo mpaka sasa linaendelea baina ya Morocco na Sahara ya Magharibi, na Umoja wa Mataifa unajaribu kutatua tatizo hili. Waingereza wakawapa uhuru Shelisheli katika mwaka wa 1976, na Ufaransa ukatoa uhuru kwa visiwa vya Ngazija (Comoro). |
17#25 | Historia ya Afrika | Katika mwaka wa 1977 Jibuti (Nchi ya Afars na Issas) iliyokuwa ikitawaliwa na Wafaransa ikarudi kwa wenyewe. Rhodesia (Zimbabwe) ikapata uhuru halisi mwaka wa 1980, na South West Africa, iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika ya Kusini ikapata uhuru katika mwaka 1990 na kuitwa Namibia. |
32#0 | Lugha | Lugha (kutoka neno la Kiarabu: لغة) ni utaratibu wa kuwasiliana kati ya binadamu (wengine wanadai hata kati ya viumbe wenye akili). |
65#0 | Madola | Katika mabara, lile lenye nchi nyingi zaidi ni Afrika likiwa na nchi au madola 54, likifuatiwa na bara la Ulaya likiwa na madola 48, kisha Asia likiwa na madola 44, halafu Amerika ya Kaskazini pamoja na Amerika ya Kati likiwa na madola 23, na baada yake ni Australia na Pasifiki (Oshania) likiwa na madola 14, na mwishowe ni Amerika ya Kusini likiwa na madola 12. Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 195 ulimwenguni. |
71#0 | Sayansi | Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa. |
71#1 | Sayansi | Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa. |
72#49 | Sheria | Falsafa ya sheria kwa kawaida inaitwa jurisprudensi. Jurisprudensi unaozidi kuongezka wenyewe ni falsafa ya kisiasa, na unauliza "sheria inafaa kuwa nini?", huku jurisprudensia ya uchambuzi inauliza "sheria ni nini?". Jibu la kiutumikaji la John Austin linajibu kuwa sheria ni "amri, zinazoandamana na matishio ya vkwazo, kutoka kwa mtawala, ambaye watu wote wamezoea kumtii". Mawakili wa sheria ya kimaumbile kwa upande mwingine, kama vile Jean-Jacques Rousseau, wanadokeza kwamba sheria inaangazia sheria isiyobadilika ya tabia ya kimaumbile. Dhana ya "sheria ya kimaumbile" iliibuka katika falsafa ya Kigiriki ya zamani kwa wakati mmoja na kwa pamoja na dhana ya haki, na iliingia mkondo wa utamaduni wa Magharibi kupitia maandiko ya Thomas Aquinas na maoni ya mwanafalsafa wa Kiislamu na mwanasheria Averroes. |
78#0 | Ushairi | Ushairi ni utungo wa kisanaa ulio na madhumuni ya kutumbuiza au kuelimisha. Tena, ushairi ni tawi mojawapo la fasihi andishi. Kinyume chake ni nathari. |
78#9 | Ushairi | Katika kujenga hoja mbalimbali za ushairi ni nini. Wakongwe na magwiji wa ushairi wa awali walieleza maana mbalimbali za ushairi kulingana na utunzi. Wakongwe hao waliamini kuwa mtunzi ana uhuru wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira. Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi. |
693#0 | Kiswahili | Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (30%), lakini sasa ya Kiingereza pia (10%), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki. |
693#2 | Kiswahili | Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu. |
693#3 | Kiswahili | Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani, waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu, walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasiliano yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba karibu theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu. |
693#7 | Kiswahili | Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi iliandikwa mwaka 1848 na Dokta Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa. |
693#14 | Kiswahili | Kati ya nchi nyingine ambapo Kiswahili kinatumika kuna Kenya, Uganda, Kongo-Kinshasa, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia na visiwa vya Bahari Hindi kama Visiwa vya Ngazija (Komoro). |
693#15 | Kiswahili | Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika nchi zifuatazo:
Kiasili Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza tu ya wakazi wa miji ya Waswahili kwenye pwani, katika sehemu za pwani pia kijijini. Baada ya kuenea kimekuwa lugha ya watu wengi mjini hasa Tanzania lakini pia Kenya. |
693#19 | Kiswahili | Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, na hasa Afrika, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali, na kukusanya kwake watu wa makabila na nchi kadha wa kadha wakaweza kufahamiana kwa lugha moja, hasa ilivyokuwa ni lugha mojawapo katika lugha kubwa za Africa ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni na Wakoloni, kama Kiarabu, Kiurdu, Kiebrania, Kireno na kadhalika. |
693#25 | Kiswahili | Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda. |
889#1 | Uislamu | Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,400 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,200. |
904#0 | Ukristo | Ukristo (kutoka neno la Kigiriki Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta" ) ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa kwa Waisraeli katika historia ya wokovu ya Agano la Kale na hasa Yesu Kristo katika Agano Jipya ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1. |
904#4 | Ukristo | Wakati wa Mababu wa Kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na Mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo. Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwaokoa binadamu. Baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuka, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya Baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasiotubu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao. |
904#14 | Ukristo | Musa, mwanaharakati aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 KK (kabla ya kuzaliwa kwa Yesu), ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi kwa niaba ya Mungu ujio wa Masiya au Kristo (Kumb 18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake na atasema nao yote niliyomwamuru." |
904#15 | Ukristo | Kuja kwake kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika Agano la Kale. Kwani Musa alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na manabii na makuhani. |
904#16 | Ukristo | Yesu alizaliwa miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya Injili vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo mwongozo wa imani hiyo. Maisha na kazi ya Yesu vimeibua mambo mengi katika historia. Ndiyo sababu kalenda iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu ni mchango mmojawapo wa Ukristo katika ustaarabu. |
904#46 | Ukristo | Baada ya Mtume Petro kuhama Yerusalemu, Yakobo Mdogo ndiye aliyeongoza ushirika huo. |
904#50 | Ukristo | Imani ya Ukristo ni juu ya Yesu. Alikuja kwelikweli hapa duniani. Alichagua kuja katika nchi ile ya Israeli miaka 2000 iliyopita. Akawachagua wanafunzi wake ambao tunawaita "mitume". Hakika alikuwa na maana kufanya hivyo. Mitume ndio waliotekeleza maagizo ya Yesu, "Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyoamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dhahari" (Math 28:19-20). Biblia inatupa habari za aina hii: wale Mitume ni mifano ya Ukristo wetu katika nguvu au karama zao, lakini pia katika udhaifu wao. |
904#68 | Ukristo | Ni kwamba kufikia mwisho wa karne ya 4 Ukristo ulikuwa dini rasmi ya Dola la Roma ambalo kabla ya hapo kwa miaka karibu 250 (64-313) lilikuwa limeukataza kikatili. Kabla yake Armenia ilikuwa nchi ya kwanza kupokea Ukristo kama dini ya taifa (301). Ushindi huo ulifanya wengi watamani vyeo ndani ya Kanisa, kwa kuwa viliendana sasa na heshima na mali: hivyo ubora ulipungua. |
904#72 | Ukristo | Katika historia ndefu ya Ukristo, yalitokea mafarakano mengi, waamini wa Yesu wakizidi kutofautiana. Makundi makubwa zaidi ni: Kanisa Katoliki, Makanisa ya Waorthodoksi na ya Waorthodoksi wa Mashariki na madhehebu ya Uprotestanti. Hasa tangu mwaka 1910 madhehebu mengi yanashiriki juhudi za ekumeni kwa ajili ya kurudisha umoja wa awali. |
904#94 | Ukristo | Kwa miaka 100 ya mwisho asilimia za Wakristo kati ya watu wote zimebaki 33, yaani mmoja kwa watatu, lakini uwiano kati ya mabara umebadilika sana, kwa maana katika Afrika, Asia na nchi nyingine zinazoendelea Wakristo wameongezeka, kumbe Ulaya na Amerika Kaskazini wamepunguaPew Research Center inakadiria kwamba mwaka 2050, watazidi bilioni tatu.. Wakati huo Wakatoliki na Waprotestanti huenda wakalingana kwa idadi.
Kuhusu maeneo ambako Wakristo wanapungua, ni kwamba, kutokana na historia ya Kanisa kuwa na mchanganyiko wa mazuri na mabaya, wengine wanahisi kuwa halina maana tena. Pia kuna makundi kama Wakomunisti na Wamasoni ambayo yanakusudia kabisa kufuta Ukristo kwa kutangaza kasoro za waumini na viongozi wao, pamoja na kuhimiza watu kwenda kinyume cha maadili. |
904#104 | Ukristo | Katika nchi nyingi Kanisa limekuwa nguvu ya kutetea haki za binadamu. Tumesikia habari za Desmond Tutu kule Afrika Kusini au za Janani Luwum katika Uganda, jinsi walivyojaribu kutetea haki za wananchi dhidi ya utawala mbaya. Ikiwa Wakristo wanajisikia wito wa kusimama na kusema mbele ya wakubwa hukumbuka manabii wa Agano la Kale hadi Yohane Mbatizaji. Wanakumbuka pia Wakristo wengi katika historia walioweza kusimama mbele ya wafalme na kutetea haki za watu. Labda tunamkumbuka Askofu Ambrosi wa Milano (aliyemvuta kijana Agostino kuwa Mkristo) alivyomtenga Kaisari na Kanisa kwa sababu ya uuaji wa wananchi wengi wasio na kosa uliofanywa na wanajeshi wa serikali. Msingi wake ni katika mafundisho juu ya kazi ya uumbaji. Mbele ya Mungu tuko sawa: kuna msingi gani kuona wengine ni sawa zaidi? |
904#129 | Ukristo | Wakristo kwa jumla wasijivunie sifa zao kuwa bora kuliko za Waislamu. Anayesoma "Historia ya Kanisa" ataona mifano mingi ya jinsi Wakristo walivyosahau mafundisho ya Yesu na kutendeana kwa unyama. Kwa hiyo mtu asijivune kwamba Ukristo ni dini ya upendo au imani yenye maendeleo kama mwenyewe si mfano wa upendo huo na maendeleo hayo.
Kwa Wakristo wengi ni fumbo kwa nini Mungu alikubali kutokea kwa dini hiyo mpya. Lakini mwanzoni mwa Uislamu Mfalme Mkristo wa Ethiopia alipokea na kuhifadhi wakimbizi Waislamu kutoka Maka. Mapokeo ya Kiislamu yanasema mfalme huyu aliyekuwa na jina "Negasi" aligeukia Uislamu baadaye. Lakini "Negasi" si jina la mtu fulani, ni cheo cha wafalme wote wa Ethiopia hadi mwaka 1974 (kwa kawaida huandikwa "Negus"). Halafu hakuna kumbukumbu ya kwamba mfalme yeyote wa karne zile aliacha Ukristo wake. |
923#0 | Afrika | Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika. |
923#6 | Afrika | Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wa kaskazini mashariki na bara la Asia kwenye rasi ya Sinai . |
923#9 | Afrika | Barani kuna nchi huru 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee na madola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa. |
923#12 | Afrika | Pwani yote ya Afrika ina urefu wa kilomita 26,000. |
923#13 | Afrika | Nchi kubwa ya Afrika ni Algeria na nchi ndogo ni funguvisiwa la Shelisheli katika Bahari Hindi. Nchi ndogo Afrika bara ni Gambia. |
923#16 | Afrika | Nusu ya kaskazini ya bara ni jangwa au angalau yabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo ya savanna na kanda za msitu wa mvua. |
923#17 | Afrika | Afrika ni bara lenye joto kuliko mabara yote na asilimia 60 za uso wake ni maeneo yabisi au jangwa. |
1163#1 | Kuki | Maana yake asili ni "biskuti" au keki ndogo, lakini neno la "kuki" linatumika ili kompyuta yenye kurasa za tovuti iweze kuwasaliana na watazamaji.
Programu za tovuti hizi inahifadhi habari kadhaa za mtazamaji au mtumiaji (k.m. jina la mtumiaji, neno la siri, ruhusa, mapendekezo) kwenye kompyuta ya mtazamaji mwenyewe. Hivi mtazamaji anatambuliwa kila wakati anaingia kwenye tovuti hii. |
1169#17 | Muhammad | Hata alipotimia miaka 12 mwaka 582, alisafiri tena pamoja na baba yake mdogo mwingine, Bwana Abu Talib; safari hii waliazimia kwenda Shamu, lakini walipofika Busra – mji wa kusini kabisa katika nchi ya Shamu – walikutana na padri jina lake Bahyra ambaye alimkataza asisogee na mwanawe zaidi kuliko hapo, akamwambia: “Mtoto huyu namwona ana alama zote za Mtume aliyetabiriwa kuwa atakuja, basi naona ni hatari kubwa akienda Shamu, asije akauawa na Wayahudi huko. Nakusihi sana urejee naye, au umpe mtu mwaminifu arejee naye, nawe uende katika biashara zako”. Abu Talib alimpa mtu arejee naye Makka naye akaendelea na safari yake. |
1169#23 | Muhammad | Wakati mwingine akikaa siku nyingi sana huko porini hata humpasa mkewe Khadija kwenda kumsikiliza na mara nyingine alikuwa akifuatana naye, pamoja na watoto wao. |
1169#25 | Muhammad | Baadaye alisimulia kuwa katika mwezi wa Ramadhani 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 unusu wa umri wake alimuona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumuona wapi katokea, akamwambia: “Soma”. Mtume akamjibu: “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujizunza”. Akaja, akamkamata, akambana, akamwambia tena: “Soma”. Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tatu akamwambia: “Soma – Iqraa Bismi Rabbik - ” akamsomea sura ya 96 mpaka kati yake, kisha Mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qurani, ingawa haijawekwa mwanzo. |
1171#0 | Fizikia | Fizikia (kutoka neno la Kigiriki φυσικός, "physikos", "ya kimaumbile", ambalo tena linatokana na φύσις, "physis", "umbile") ni fani ya sayansi inayohusu maumbile ya ulimwengu, hususan asili ya dunia na viumbe vyote. |
1171#17 | Fizikia | Astronomia inatajwa kama sayansi ya kale zaidi, ambapo jamii zilizokuwa zimestaarabika zamani, kama Wasumeri, Wamisri wa kale na jamii kuzunguka uwanda wa mto Indus, takriban miaka 3000 KK zilikuwa na uelewa juu ya elimu ya utabiri kuhusu mienendo ya jua, mwezi na nyota. Nyota na mwezi mara nyingi zilichukuliwa kama alama za kidini, zikiaminika kuwakilisha miungu yao. |
1173#0 | Bara Arabu | Bara Arabu ni ile sehemu ya dunia iliyoko baina ya Bara la Afrika na Bara la Asia ambayo sehemu kubwa yake imezungukwa na bahari, upande wa magharibi Bahari ya Shamu, upande wa kusini na Bahari ya Hindi na ule wa Mashariki Ghuba ya Uajemi. Sehemu za Kaskazini mwa Bara Arabu zimepakana na nchi za ufalme wa Jordani na jamhuri ya Iraq. |
1173#3 | Bara Arabu | Eneo la Bara Arabu kwa jumla ni kilomita mraba 3,191,022, ikiwa Saudia inakalia sehemu nne katika tano ya jumla ya maeneo yake, na sehemu iliyobakia ambayo ni moja katika tano inakaliwa na nchi zilizobakia, zote zikiwepo pembezoni mwa Saudia kwenye bahari ya Ghuba ya Uajemi na bahari ya Waarabu na bahari ya Shamu. |
1173#4 | Bara Arabu | Nchi zilizoko kwenye bara hili ni Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudia, Muungano wa Falme za Kiarabu, na Yemen. Sita za mwanzo, zikiwemo kwenye Baraza la Ushirikiano wa Nchi za Ghuba, zina mfumo wa kifalme katika utawala wake, na ya mwisho ni Jamhuri ya Yemen. |
1173#6 | Bara Arabu | Kuna miji mingi katika Bara Arabu, lakini miji mikuu ya madola mbalimbali ya Bara Arabu ni Riyadh, mji mkuu wa Saudia, ijapokuwa kuna miji mashuhuri na mitukufu katika Saudia kama Makka na Madina. |
1173#11 | Bara Arabu | Rasi ya Bara Arabu ina jangwa kubwa la Rub al Khali kusini mwake na An-Nafud kaskazini mwake. Ni sehemu ya ulimwengu ambayo haina mvua nyingi na ukame ndio tabia ya nchi zilizokuwemo katika bara hili. Kwa hivyo, hali ya hewa huwa ni joto sana katika majira ya joto kufikia hadi daraja 55 C° katika baadhi ya sehemu zake, na kufikia daraja hadi 0 C° katika baadhi ya sehemu nyIngine katika majira ya baridi. |
1173#16 | Bara Arabu | Bara Arabu ina aina nyingi za madini na nishati. Kuna dhahabu, fedha, chumvi, na kadhalika. Inajulikana hasa kwa akiba zake kubwa za mafuta ya petroli na gesi, jambo lililofanya hizi nchi kutegemea zaidi maliasili hizi kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi zao na maendeleo mengine ya nchi. |
1174#11 | Mwenyezi Mungu | Yeye hana kitu kilichofanana naye, hakuzaa wala hakuzaliwa, hana mwanzo wala mwisho. Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu, Mtoa riziki, Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha. Hukumu yote ni yake siku ya Kiyama. Mtukufu na Mkubwa. Bwana na Mola wa walimwengu wote. Yeye tu ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa na Yeye tu ndiye Mwenye kufaa kuombwa na kutakwa msaada. |
1175#2 | Dunia | Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au kizio astronomia 1. Dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756. |
1175#4 | Dunia | Umri wa dunia hukadiriwa kuwa miaka bilioni 4.5. |
1175#7 | Dunia | Umbo la dunia linafanana na tufe au mpira unaozunguka kwenye mhimili wake. "Mhimili wa dunia" ni mstari kati ya ncha zake. |
1175#8 | Dunia | Lakini si tufe kamili. Ina uvimbe kidogo kwenye sehemu ya ikweta; ilhali umbali kati ya ncha mbili ni kilomita 12,713 lakini umbali kati ya sehemu za kinyume kwenye ikweta ni km 12,756, yaani kipenyo hiki kinazidi takriban kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha. Tofauti hii inasababishwa na mzunguko wa dunia. Kani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi. Kwa hiyo mahali duniani palipo karibu zaidi na anga la nje si Mlima Everest kwenye Himalaya bali mlima Chimborazo nchini Ekuador.
Kwenye uso wake dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili. Nusu moja ina eneo kubwa la mabara yaani nchi kavu ambayo ni asilimia 47 ya sehemu hii. Kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji ya bahari na eneo la nchi kavu ni asilimia 11 pekee za maeneo yake. |
1175#10 | Dunia | Kwa pamoja maeneo ya maji hufunika 70.7% za uso wa dunia. Nchi kavu huwa na 29.3% na sehemu kubwa ya eneo la nchi kavu ni bara 7 za Asia, Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antarktika, Ulaya na Australia. (Ulaya inaweza kuangaliwa pia kama sehemu ya Asia ikiwa kama rasi yake ya magharibi. Azimio la kutazama Australia kama bara na Greenland kama kisiwa tu ni azimio la hiari si la lazima). |
1175#11 | Dunia | Maeneo ya bahari kuu ya dunia kwa kawaida hugawiwa kwa bahari kubwa 3 za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Sehemu ya chini baharini iko kwenye Mfereji wa Mariana katika Pasifiki (mita 11,034 chini ya UB). Kwa wastani bahari huwa na kina cha mita 3,800. |
1175#15 | Dunia | Matabaka hayo yanafanywa kwa elementi za kikemia ambazo ni feri (chuma) (32,1 %), oksijeni (30,1 %), silisi (15,1 %), magnesi (13,9 %), sulfuri (2,9 %), nikeli (1,8 %), kalsi (1,5 %) na alumini (1,4 %). Mabaki ya 1,2 % ni viwango vidogo vya elementi nyingine. Elementi hizo zinapatikana kwa hali safi au katika kampaundi za elementi. |
1178#0 | Asia | Asia ni bara kubwa kabisa kuliko mabara yote mengine ya dunia. Bara hili lina eneo la kilomita za mraba 44,579,000 (maili za mraba 17,212,000), ambalo ni sawa na asilimia 30% ya ardhi yote. Wakazi wa bara la Asia ni 3,701,000,000 kwa mujibu wa makisio 2003. |
1178#1 | Asia | Bara la Asia lina nchi 44 na visiwa mbali mbali vya madola mbalimbali. Mlima mrefu kabisa ulimwenguni ambao ni mlima wa Everesti wenye urefu wa mita 8,850 (futi 29,035) ulioko Nepal pia uko kwenye bara hili. Kadhalika, nchi zenye wakazi wengi zaidi ulimwenguni China na India pia ziko kwenye bara hili. |
1178#2 | Asia | Ziwa kubwa kabisa ulimwenguni, bahari ya Kazwini (Caspian Sea) lenye eneo la kilomita za mraba 394,299 (maili za mraba 152,239) vile vile liko Asia kati ya ya nchi hizi: Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan, na Uajemi. |
1178#3 | Asia | Bara la Asia linaweza kugawanywa katika sehemu zifuatazo: |
1182#10 | Isa | Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahili kuabudiwa kwa haki. Ujumbe huu ndio ujumbe uleule uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu ili kuwaongoza, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kuzipa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. |
1183#1 | Bara | Neno "bara" lamaanisha nchi kavu, tofauti na bahari au visiwa vidogo karibu na pwani ya nchi kavu kubwa zaidi. Si lazima kutaja maeneo makubwa tunayomaanisha tukiongea juu ya "mabara saba ya dunia". Neno "kontinenti" latokana na Kilatini "terra continens" yaani "nchi (kavu) mfululizo". |
1183#5 | Bara | Vivyo hivyo “Ulaya bara” ni eneo la Ulaya bila visiwa kama Britania, Eire, Malta na kadhalika. |
1183#6 | Bara | Kwa macho ya jiolojia “bara” ni pana kuliko nchi kavu tu: inaweza kutaja pia maeneo ya tako la bara yaliyo chini ya maji yasiyo na kina kikubwa pamoja na visiwa vya sehemu hizi. Kwa mtazamo huu visiwa vya Britania na Eire ni sehemu ya Ulaya na vivyo hivyo Autralia na Guinea Mpya ni bara moja. |
1183#8 | Bara | Kwenye ramani zinazotumia lugha ya Kiingereza kawaida huhesabiwa mabara saba duniani, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo. Mara nyingi visiwa vya Pasifiki hujumlishwa pamoja na Australia kama
na kuhesabiwa kama bara. |
1183#11 | Bara | Mabara jinsi yalivyo leo hayakuwepo tangu mwanzo wala hayakai vile. Ilhali kila bara inalingana na bamba 1 au mabamba ya gandunia ina pia mwendo pamoja na bamba lake. Wanajiolojia huamini ya kwamba miaka mamilioni iliyopita mabara yote yaliwahi kukaa pamoja kama bara 1 kubwa sana lililoendelea kupasuliwa baadaye. Vipande huelea juu ya koti ya dunia ambayo ni kiowevo na moto. Mwendo wa mabamba umepimiwa kuwa sentimita kadhaa kila mwake. Uhindi zamani haikuwepo sehemu ya Asia, na sasa hivi Afrika inaelekea kupasuliwa kwenye mstari wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. |
1183#12 | Bara | Eneo la dunia yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu. |
1183#15 | Bara | Mabara na mabamba yao ni kama ifuatayo: Afrika (Bamba la Afrika), Antaktika (Bamba la Antaktika), Australia (Bamba la Australia), Ulaya na sehemu kubwa ya Asia (Bamba la Ulaya-Asia), Amerika Kaskazini pamoja na Siberia (Bamba la Amerika ya Kaskazini) na Amerika Kusini (Bamba la Amerika ya Kusini). Mabamba madogo yamejitenga ingawa nchi juu yao inaonekana kuwa sehemu ya bara lingine. Mfano wake ni Bara Hindi iliyokuwa kama bara ndogo au kisiwa kikubwa zamani lakini tangu miaka milioni 10 imejisukuma chini ya bamba la Asia-Ulaya na kuikunja hadi kutokea kwa milima ya Himalaya. |
1191#2 | Tanzania | Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2. |
1191#3 | Tanzania | Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ilikuwa 44,928,923 (nchi ya 30 duniani) kutoka 34,443,603 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2002. |
1191#6 | Tanzania | Mji mkuu ni Dodoma (wenye wakazi 410,956), lakini rais bado yupo Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi, lenye watu zaidi ya milioni 4,364,541. |
1191#9 | Tanzania | Pia ina mito mingi ambayo inaelekeza maji yake katika Bahari ya Hindi mashariki mwa nchi, lakini mingine inachangia Mto Zambezi kupitia Ziwa Nyasa, michache Bahari ya Kati kupitia Ziwa Victoria na mto Naili, mingine tena Bahari Atlantiki kupitia Ziwa Tanganyika na mingine inaishia katika mabonde kama ya Ziwa Rukwa. |
1191#17 | Tanzania | Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti hadi 1964, zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais. |
1191#27 | Tanzania | Ugatuzi, yaani mgawanyo wa kiutawala, unafuata Katiba ya nchi I 2.2. Tanzania imegawiwa kwa mikoa 31. Kila mkoa huwa na wilaya ndani yake. Jumla ya wilaya ni 169, ambazo kati yake 34 ni miji. |
1191#30 | Tanzania | Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kwa wastani kuna mtu mmoja tu kwa kilomita ya mraba (1/km²), lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba na katika Mkoa wa Dar es Salaam ni 3,133 kwa kilomita ya mraba. |
1191#45 | Tanzania | Kiswahili ndiyo lugha ya taifa na inazidi kuwa lugha mama kwa watoto wengi, hasa mijini. Walau asilimia 90 za wakazi wanakitumia walau kama lugha ya pili. Kiswahili ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu: hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini, kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu. Kiswahili kinatumika kama lugha baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo rasmi; kwa hiyo ni lugha rasmi ya dhati. |
1191#46 | Tanzania | Baada ya uhuru, Kiingereza (iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi na kwa elimu kuanzia sekondari ingawa sera mpya inataka Kiswahili kishike nafasi yake hadi chuo kikuu; kwa hiyo ilichukuliwa kama lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi rasmi wa Kiingereza umepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchukulia Kiswahili kama lugha rasmi ya dhati pekee. |
1191#48 | Tanzania | Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi inawezekana ni zaidi azimio la kisiasa. |
1191#60 | Tanzania | Utamaduni wa Watanzania ni pamoja na utaraab. Muziki ana nyimbo za kitaraab ndizo muhimu sana kwa nchi nzima, hasa visiwani na pwani. Pia kuna miziki ya Kinyarwanda, dansi kama intore n.k. |
1201#1 | Uhindi | Kwa eneo ina nafasi ya saba duniani, lakini kwa idadi ya wakazi (1,276,267,000 mwaka 2015) ni nchi ya pili baada ya China. Kati ya nchi za kidemokrasia ndiyo yenye watu wengi zaidi duniani. Tena inakadiriwa kwamba miaka ya hivi karibuni itapiku China. |
1201#13 | Uhindi | Kati ya miaka 1756 na 1763 Uingereza pamoja na mataifa mengine ya Ulaya ilishiriki katika Vita vya miaka saba viliyokuwa vita vya kwanza vya kimabara. Waingereza walipigana pamoja na Prussia dhidi ya Austria, Ufaransa, Urusi na Uswidi. Jeshi la kampuni liliendesha vita hivyo dhidi ya maeneo ya Ufaransa katika Uhindi. Wafaransa walishindwa wakabaki na vituo vidogo tu katika miji kama Pondicherry na Mahe lakini kampuni iliongeza maeneo yake katika Uhindi. |
1203#5 | Afrika ya Mashariki | Aghalabu nchi za Afrika ya Mashariki zinazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kati yao, kwani katika nchi hizi kuna makabila mengi sana na kila kabila lina lugha yake ambayo kawaida inatumika nyumbani baina ya watu wa kabila moja, lakini wakitaka kuwasiliana na makabila mengine, mara nyingi hutumia lugha ya Kiswahili, na hii ni kwa sababu lugha hii ndiyo iliyoenea zaidi na kufahamika zaidi katika eneo hili la dunia. |
1203#6 | Afrika ya Mashariki | Nchi za Afrika ya Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Tanzania ni nchi ambazo ni karibu tangu zamani. Zimeshirikiana historia, zote zimekaliwa hasa na makabila yanayotumia lugha za Kibantu (Kenya na Uganda wana pia idadi muhimu ya wakazi wasiotumia lugha za Wabantu). Katika nchi zote tatu lugha ya Kiswahili imekuwa lugha muhimu ingawa kwa daraja mbalimbali. Wakati wa ukoloni zilitawaliwa na Uingereza iliyoacha taasisi na taratibu mbalimbali zilizosaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa uhuru. |
1203#7 | Afrika ya Mashariki | Tanzania, Kenya na Uganda zina ukubwa wa eneo la maili za mraba; Tanzania 360,000 ikifuatiwa na Kenya 224,960 na Uganda 93,980 upande wa mashariki nchi hizi zimepakana na bahari ya Hindi na upande wa kaskazini mashariki zimepakana na Somalia, upande wa kaskazini zimepakana na Ethiopia na Sudan Kusini upande wa magharibi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jamuhuri ya Rwanda na Burundi, kusini ni Zambia, Malawi na Msumbiji. |
1665#2 | Tofaa | Nchi zinazovuna matofaa hasa ni China, Marekani, Uturuki, Ufaransa, Italia na Uajemi. |
1676#0 | Kenya | Jamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. |
1676#3 | Kenya | Mji mkuu ni Nairobi. |
1676#4 | Kenya | Idadi ya watu imeongezeka sana katika miaka ya karibuni na kufikia milioni 49. |
1676#9 | Kenya | Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya (na la pili kwa urefu barani Afrika): Mlima Kenya, unaofikia urefu wa mita 5,199 (futi 17,0570) na ni eneo lenye mito ya barafu. Mlima Kilimanjaro () huweza kuonekana upande wa kusini, ng'ambo ya mpaka wa Kenya na Tanzania . |
End of preview. Expand in Data Studio
README.md exists but content is empty.
- Downloads last month
- 5