id
stringlengths
1
6
url
stringlengths
31
202
title
stringlengths
1
120
text
stringlengths
8
182k
1876
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20ya%20maoni
Kura ya maoni
Kura ya maoni zinatumika katika demokrasia ili kuchagua viongozi wa nchi au kuamua kama sheria fulani itumike. Kawaida kura ya maoni hupigwa na wale wote wenye umri halali wa kupiga kura ili kukubali au kukataa pendekezo, sera, sheria, mabadiliko ya katiba, katiba mpya, kukataa au kumuunga mkono kiongozi fulani. Kura y...
1877
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20juu%20ya%20katiba%20mpya%20ya%20Kenya%20%282005%29
Kura juu ya katiba mpya ya Kenya (2005)
Kura ya maoni juu ya katiba mpya ya Kenya ilipigwa tarehe 21 Novemba 2005. Asilimia 58 ya Wakenya waliopiga kura waliikataa. Rais wa Kenya na baadhi ya mawaziri walipiga kampeni kutaka Wakenya waiunge mkono katiba hiyo. Kundi lililokuwa likiiunga mkono katiba mpya lilikuwa likiwakilishwa na alama ya ndizi na kundi li...
1878
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
Demokrasia ya moja kwa moja
Demokrasia ya moja kwa moja ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, kijamii, kisheria, na kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kama vile bunge. Uwezo huu wa wananchi kutoa maamuzi unaweza kuwapa wananchi hata uwezo wa kimahakama ingawa mara nyingi wananch...
1879
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
Bunge
Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka katika dola. Mihimili mingine ni mahakama na serikali. Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana...
1890
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
Mahakama
Mahakama ni mfumo wa wataalamu na kamati maalumu ambao unatafsiri na kutumia sheria katika jina la wananchi, la jamhuri au la mfalme. Mahakama pia inatoa mfumo wa kutatua migogoro. Chini ya mfumo wa mgawanyo wa madaraka mahakama kwa ujumla haitungi wala haiundi sheria (ambayo ni kazi ya bunge) wala kutekeleza sheria ...
1891
https://sw.wikipedia.org/wiki/Katiba
Katiba
Katiba ni sheria au kanuni zinazoaInisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao. Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi. Kuna aina kuu mbili za K...
1899
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
Ukimwi
Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi UKIMWI; kifupisho cha Kiingereza AIDS) ni ugonjwa unaotokana na virusi ambavyo kwa Kiswahili vinaitwa kifupi VVU ("Virusi vya UKIMWI"; kwa Kiingereza: HIV, yaani "Human Immunodeficiency Virus") na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maambukizi nyemelezi yanay...
1901
https://sw.wikipedia.org/wiki/Desemba
Desemba
Desemba ni mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya Gregori na ni kati ya miezi saba katika kalenda hiyo yenye siku 31. Tarehe 21 ya mwezi huo wa Desemba (katika miaka mingine inawezekana kuwa tarehe 20 au 22) ni siku ya solistasi ya Kusini (kutoka Kiingereza solstice), yaani wakati Jua linapokuwa kusini kabisa mwa I...
1904
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
Mmea
Mimea (kwa Kiingereza: "plants", kutoka Kilatini "Plantae") ni moja kati ya makundi ya viumbe hai duniani likijumuisha miti, maua, mitishamba na kadhalika. Kuna zaidi ya aina 300,000 ya mimea. Sayansi inayochunguza mimea huitwa botania ambayo ni kitengo cha biolojia. Kwenye uainishaji wa kisayansi mimea hujumlishwa ka...
1907
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usanifu%20majengo
Usanifu majengo
Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo. Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu majengo". Wanahitaji elimu ya ujenzi, hesabu, sanaa, t...
1908
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mipango%20miji
Mipango miji
Mipango miji ni sayansi na sera kuhusu maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kimazingira katika miji na vitongoji vyake. Mgiriki Hippodamus anasemekana kuwa ndiye baba wa mipango miji kutokana na ubunifu wake wa mji wa Miletus ingawa kumekuwa na miji iliyopangwa kabla yake. Taaluma ya mipango miji imechipuka toka kwenye ta...
1910
https://sw.wikipedia.org/wiki/IRC
IRC
Internet Relay Chat (IRC) ni aina ya mawasiliano ya papo kwa hapo kupitia mtandao wa Intaneti. Teknolojia hii imeundwa hususan kwa ajili ya mawasiliano ya watu wengi kwa wakati mmoja, lakini pia mawasiliano ya mtu mmoja kwa mmoja yanawezekana. Teknolojia hii ilitengenezwa na Jarkko Oikarinen Agosti 1998 ili kuchukua n...
1911
https://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu%20za%20mkononi
Blogu za mkononi
Blogu za mkononi ni aina ya blogu zinazotumia zana zinazoshikika mkononi kama vile simu za mkononi. Kwahiyo, habari, maoni, au visa vinatolewa katika mtandao wa kompyuta kwa kutumia zana hizi. Teknolojia hii ilianza huko Japan ambapo simu za mkono zenye kamera zilianza kupatikana kwa urahisi. Inasemekana utumaji wa h...
1912
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paul%20Simon
Paul Simon
Paul Simon ni mwanamuziki wa country, anaimba na kupiga gitaa. Amewahi kushirikiana na wanamuziki wengi; moja ya makundi hayo ni Ladysmith Black Mambazo. Nyimbo alizowahi kuimba ni "Homeless", "Mother and child reunion" na "Diamond in the sole of her shoes". Paul Simon alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1941 katika mji wa New...
1928
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
Shaaban Robert
Shaaban Robert (1 Januari 1909 - 22 Juni 1962) alikuwa mshairi na mwandishi wa riwaya. Mchango wake katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa kwani kazi zake zinaheshimika katika fasihi ya Kiswahili na pia zinatumika shuleni. Maisha Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 katika kijiji cha Vibambani, jirani na Machu...
1930
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya
Mbeya
Mbeya ni jina la: Mji wa Mbeya Mkoa wa Mbeya katika Tanzania Kusini-Magharibi Wilaya za Mbeya mjini na vijijini Jimbo Kuu la Mbeya la Kanisa Katoliki Tanzania Makala zinazotofautisha maana
1950
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
Mkoa wa Mbeya
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, ukipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa, mbali na mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka ule wa Mbeya upande wa magharibi mwaka 2016. Una Postikodi namba 53000. Kabla ya kugawiwa kulikuwa na wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya V...
1951
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ladysmith%20Black%20Mambazo
Ladysmith Black Mambazo
Ladysmith Black Mambazo ni kundi la muziki ambalo linaimba bila kutumia ala za muziki. Kundi hili lipo Afrika ya Kusini. Neno "Mambazo" linamaanisha "shoka" kwa Kizulu. Na "Ladysmith" ni kitongoji katika jimbo la Natal alichotoka Joseph Shabalala kiongozi na mwanzilishi wa kundi hili. Ladysmith Black Mambazo lina alba...
1952
https://sw.wikipedia.org/wiki/Arusha
Arusha
Arusha ni neno la kutaja watu na mahali katika Tanzania kaskazini-mashariki: Kabila la Waarusha Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arusha Mji wa Arusha ni makao makuu ya mkoa na wilaya, pia makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Tanzania Makala zinazotofautisha maana
1953
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
Mkoa wa Arusha
Mkoa wa Arusha ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 23000, na ni wa pili kwa utajiri nchini. Wakazi ni 2,356,255. Eneo Eneo lake ni km za mraba 34,526 zikiwemo km² 707 za maji ya ndani.. Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani, kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, ...
1954
https://sw.wikipedia.org/wiki/Deutsche%20Welle
Deutsche Welle
Redio Deutsche Welle (DW), au Sauti ya Ujerumani ni kituo cha Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa ajili ya matangazo ya nje. Kituo kimeanzishwa mw. 1953 kilitoa matangazo ya Kijerumani kwa ajili ya Wajerumani kote duniani kwa njia ya SW. Leo (2005) kituo hutangaza kwa redio za SM na FM kwa lugha 30 halafu kwa TV k...
1956
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilomita%20ya%20mraba
Kilomita ya mraba
Kilomita ya mraba (km²) ni kipimo cha eneo; eneo lenye upana na urefu wa kilomita moja Msingi wake ni mita ya mraba (m²). Kilomita ya mraba hutumika kwa upimaji wa maeneo makubwa duniani kama mji, mkoa, nchi au dunia yote. Kilometa 1 ya mraba (km²) ni sawa na: eneo la mraba yenye urefu wa kilomita moja kila upande ...
1958
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usawa%20bahari%20wastani
Usawa bahari wastani
Usawa wa wastani wa maji ya bahari hutumika kama kipimo cha kulinganisha kimo cha mahali duniani toka usawa wa bahari. Hali halisi usawa wa bahari hubadilika kati ya mahali na mahali na muda hadi muda. Kwa hiyo kuna kadirio la wastani wa vipimo hivyo inayotumika kuwa usawa bahari wastani. Kawaida hutumika katika sente...
1959
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
Alfu Lela U Lela
Kitabu cha Alfu Lela U Lela au Usiku Elfu na Moja (كتاب ألف ليلة وليلة kwa Kiarabu au هزار و یک شب kwa Kiajemi) ni mkusanyiko wa fasihi katika muundo wa visa kutoka Mashariki ya Kati. Maandishi na historia yake Visa hivi vinatokana na kitabu cha zamani cha Kiajemi kiitwacho Hazâr Afsâna (Visa vya Ngano Elfu Moja). In...
1960
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karne
Karne
Karne ni muda wa miaka mia moja. Karne 10 ni milenia moja. Inawezekana kugawa karne kwa miongo 10. Neno hili limetokana na Kiarabu "ﻗﺮﻥ" linamaanisha kipindi cha miaka mia moja. Kwa kawaida karne si miaka 100 yoyote inayofuatana lakini kipindi kati ya miaka kama vile 1901-2000 au 1801-1900. Karne inakwisha katika mw...
1961
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
Ubuntu
Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko ubinafsi. Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na Kixhosa za Afri...
1962
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malik%20Zulu%20Shabazz
Malik Zulu Shabazz
Malik Zulu Shabazz (amezaliwa mwaka wa 1968 kwa jina la Paris Lewis) ni mwanasheria nchini Marekani na kiongozi wa kundi la New Black Panther Party for Self Defence. Wanasiasa wa Marekani
1963
https://sw.wikipedia.org/wiki/New%20Black%20Panther%20Party%20for%20Self%20Defence
New Black Panther Party for Self Defence
New Black Panther Party for Self-Defense ni kundi la wanaharakati weusi wenye siasa kali na mwamko wa kimapinduzi nchini Marekani. Kundi hili lilianzishwa mwaka 1989 na mtangazaji wa redio, Aaron Michaels, huko Dallas, Texas. Mwanzoni kundi hili lilichukua jina la "Black Panther Party" ambalo lilikuwa ni jina la kund...
1968
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
Bendera ya Tanzania
Bendera ya Tanzania ni ya mstatili unaokatwa pembe kwa pembe na kanda nyeusi yenye milia za njano kandokando. Pembetatu ya juu ina rangi ya majani, pembetatu ya chini ni ya buluu. Matumizi ya bendera inahifadhiwa chini ya sheria ya "The National Flag and Coat of Arms Act, 15-1971". Historia ya bendera Bendera hii im...
1970
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
Jakaya Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015. Asili Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwer...
1985
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
Jens Fink-Jensen
Jens Fink-Jensen (alizaliwa Copenhagen, Denmark, 19 Desemba 1956) ni mwandishi katika lugha ya Kidenishi katika nyanja mbalimbali kama vile semi za kawaida na mashairi. Vile vile yeye ni mpigapicha na mwandishi wa vitabu hasa vya muziki na nyimbo. Alianza maisha yake kama mwandishi wa vitabu vya hadithi 4 Juni 1975 wa...
1989
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
Krismasi
Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki. Jina Kwa Kiswahili kuna majina mawili ya kawaida kwa ajili ya sikukuu hii:...
1991
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto%20Kagera
Mto Kagera
Mto Kagera (kwa Kinyarwanda: Akagera) ni kati ya mito inayounda mto Nile, pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza. Unaanzia Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela km 400 hadi kuingia ziwa Viktoria. Mto Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale una...
1992
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
Mkoa wa Kagera
Mkoa wa Kagera kati ya mikoa 31 ya Tanzania ndio mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa wenye postikodi namba 35000. Jina lake linatokana na mto Kagera. Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mingine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na G...
1993
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kagera
Kagera
Kagera ina maana mbalimbali: Kagera ni mto katika Tanzania Mkoa wa Kagera ni mkoa katika Tanzania. Kagera (Ukerewe) ni kata ya wilaya ya Ukerewe kwenye mkoa wa Mwanza (Tanzania) {maana}} Makala zinazotofautisha maana
1996
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
Yesu
Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK). Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi...
1997
https://sw.wikipedia.org/wiki/Azania
Azania
Azania (kwa Kigiriki: Ἀζανία) ni jina la kihistoria la sehemu mbalimbali za pwani ya Afrika ya Mashariki. Asili yake ni zamani za Waroma na Wagiriki wa kale kwa eneo lililokuwa la watu wa Lugha za Kikushi. Mapokeo ya Waroma na Wagiriki wa Kale Mara ya kwanza jina hili limepatikana katika mwandishi Mroma Plinio Mzee (G...
2000
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jumuiya%20ya%20Madola
Jumuiya ya Madola
Jumuiya ya Madola (jina la Kiingereza ni Commonwealth of Nations) inaunganisha nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake. Umoja huu umeanzishwa mw. 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Dola la Kibritania au Dola la Kiingereza...
2002
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mzunguko%20wa%20Bahari%20Nyekundu
Mzunguko wa Bahari Nyekundu
Mzunguko wa Bahari Nyekundu (kwa Kiingereza: Periplous of the Erythrean Sea) ni kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mabaharia kilichoandikwa mnamo mwaka 70 BK. "Periplous" ni neno la Kigiriki linalomaanisha tendo la kuzunguka bara kupitia bahari kwa merikebu; "Bahari ya Eritrea" ni jina la kale kwa ajili ya Bahari ya Sh...
2003
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Eritrea
Bahari ya Eritrea
Bahari ya Eritrea (kwa Kigiriki ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa) ni jina la kale la Bahari ya Shamu na Bahari Hindi. Neno "erythra" katika lugha ya Kigiriki inamaanisha rangi nyekundu ("thalassa" = bahari). Hivyo bahari ile iliitwa "Bahari Nyekundu" (linganisha Kiingereza "Red Sea"). Inasemekana ya kwamba jina hilo li...
2004
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Shamu
Bahari ya Shamu
Bahari ya Shamu (kwa Kiingereza Red Sea; kwa Kiarabu البحر الأحمر Baḥr al-Aḥmar, al-Baḥru l-’Aḥmar; kwa Kiebrania ים סוף Yam Suf; kwa Kitigrinya ቀይሕ ባሕሪ QeyH baHri) ni ghuba kubwa ya Bahari ya Hindi. Jina la kihistoria katika lugha ya Kigiriki lilikuwa Bahari ya Eritrea (ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa). Kaskazini k...
2006
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Watu%20wa%20Zanzibar
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingawa inajitawala katika mambo ya ndani. Hadi mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 nchi hiyo ilijulikana kama Usultani wa Zanzibar. Jina Etimolojia ya Neno Zanzibar Jiografia Eneo lake ni sawa na funguvisiwa la Zanzibar lililopo mbele ya mwamb...
2007
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Tsunami ni wimbi kubwa sana katika bahari linalosababishwa na tetemeko la ardhi, mlipuko wa volkano au matokeo mengine yanayoleta mshtuko wa ghafla chini ya maji. Mshtuko huo unasababisha kutokea kwa wimbi kali linaloanza kupaa juu likifika katika maji kame na kwenye ufuko wa bahari. Neno tsunami linatokana na lugha y...
2008
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Tanganyika African National Union (TANU) kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hiki na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar ulipounda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. TANU ilianzishwa 7 Julai 1954 kutokana na Tanganyika African Association (TAA). TAA ilikuwa na mwelekeo wa kita...
2009
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Benjamini William Mkapa (12 Novemba 1938 - 24 Julai 2020) alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM. Wasifu Mkapa alizaliwa Lupaso karibu na Masasi katika kusini-mashariki ya Tanganyika. Kuanzia 1945 hadi 1951 alsoma shule za msingi pale Lup...
2010
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
''Makala hii yaeleza habari za njia ya reli ya kihistoria kati ya Mombasa na Uganda. Kwa habari za Shirika ya Reli ya Uganda ya kisasa tazama Uganda Railways Corporation. Reli ya Kenya-Uganda ni jina kwa reli kati ya Mombasa na Kampala iliyojengwa na Waingereza kuanzia mwaka 1896. Mwanzoni ilijulikana kwa jina la "Rel...
2011
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Bell
Port Bell
Port Bell ni mji mdogo karibu na Kampala/ Uganda ufukoni wa ziwa la Viktoria Nyanza. Jina la mji limetokana na Sir Hesketh Bell aliyekuwa kamishna (gavana) Mwingereza huko Uganda kuanzia mwaka. 1905-1909. Port Bell ni bandari kwa ajili ya Kampala. Feri zinatoka kwenda Jinja, Kisumu na Mwanza. Kuna viwanda kadhaa kam...
2012
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Chad (pia: Chadi) ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger. Mji mkuu ni Ndjamena. Jiografia Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo...
2016
https://sw.wikipedia.org/wiki/Athi
Athi
Athi ni jina la mto katika kaunti ya Kitui, Kenya, Afrika Mashariki. Sehemu za mto hujulikana pia kwa majina ya Galana na Sabaki, kwa hiyo mto wote huitwa pia Athi-Galana-Sabaki. Ina urefu wa kilomita 390, na beseni lenye eneo la Km² 70,000. Mto wa Athi umeupatia jina lake mji wa Athi River karibu na Nairobi pia kwa ...
2017
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ludwig%20Krapf
Ludwig Krapf
Johann Ludwig Krapf (11 Januari 1810 – 26 Novemba 1881) alikuwa mmisionari wa kwanza wa Uprotestanti nchini Kenya katika karne ya 19 akatunga kamusi ya kwanza ya lugha ya Kiswahili. Masomo Ujerumani na Uswisi Krapf alizaliwa tarehe 11 Januari 1810 katika kijiji cha Derendingen karibu na Tübingen, eneo la Württemberg,...
2018
https://sw.wikipedia.org/wiki/Komori
Komori
Komori (kwa Kiswahili pia: Visiwa vya Ngazija; kwa Kikomori: قمر, Komori, kwa Kifaransa: Comores) ni nchi huru kwenye funguvisiwa katika Bahari Hindi upande wa Mashariki wa Afrika. Iko katika Kanali ya Msumbiji kaskazini kwa Madagaska na mashariki kwa Msumbiji. Jina limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo Juzur al-Qama...
2021
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jomo%20Kenyatta
Jomo Kenyatta
Jomo Kenyatta (1893-1978) alikuwa rais wa kwanza wa Kenya. Jina lake halisi lilikuwa Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagĩkũyũ wanauita kenyaata. Maisha Alisoma katika shule ...
2022
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwanza%20%28sarafu%29
Kwanza (sarafu)
Kwanza (kifupi: KZ) ni pesa inayotumika kwa malipo halali katika nchi ya Angola. Wakati wa uhuru Angola ilirithi pesa ya escudo kutoka Ureno. Mwaka 1977 Kwanza yenye Lwei 100 imeingizwa nchini kama pesa ya kwanza ya kitaifa. Kutokana na kushuka kwa thamani ya fedha mara kwa mara pesa ya Kwanza imebadilishwa mara nne ...
2023
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwanzaa
Kwanzaa
Kwanzaa ni sikukuu inayosherehekewa kati ya Wamarekani Weusi nchini Marekani kwa muda wa siku saba toka tarehe 26 mwezi wa disemba hadi tarehe 1 mwezi wa Januari. Sikukuu hii ilianzishwa Kalifornia na Maulana Ron Karenga tarehe 26 Diesemba mwaka 1966. Karenga alitunga neno jipya "Kwanzaa" kutokana na neno la Kiswahil...
2024
https://sw.wikipedia.org/wiki/Visa%20vya%20Esopo
Visa vya Esopo
Visa vya Esopo vinatokana na masimulizi ya Esopo, ambaye inaaminika kuwa alikuwa ni mtumwa wa Kiafrika aliyeishi kati ya mwaka 620 na 560 Kabla ya Kristo katika Ugiriki wa Zamani. Visa vyake hutumiwa kutoa mafunzo na kuburudisha. Visa hivi hutumiwa kwa wingi katika vitabu vya watoto na vikaragosi. Historia ya Esopo...
2026
https://sw.wikipedia.org/wiki/Guinea
Guinea
Guinea (pia: Gine, Gini) ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Guinea-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Guinea-Bissau na Guinea ya Ikweta. Imepakana na Guinea-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Côte d'Ivoire, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari Atlantiki upande wa magharibi. E...
2027
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
Abu Nuwas
Abu Nuwas (kwa Kiarabu أبو نواس) alikuwa mshairi Mwarabu aliyeishi 760-815. Katika utamaduni wa Kiswahili ni jina la mhusika katika hadithi za “Hekaya za Abunuwasi”. Maisha Mshairi Abu Nuwas alizaliwa Ahwaz (Irak). Mama yake alikuwa Mwajemi na baba alikuwa mwanajeshi Mwarabu ambaye hakupata kumjua. Jina lake halisi l...
2032
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
Bi Kidude
Bi Kidude (jina halisi: Fatuma binti Baraka; amefariki Bububu, Zanzibar, 17 Aprili 2013, akikisiwa kuwa na umri wa miaka 102) alikuwa gwiji wa muziki katika bara la Afrika. Bi Kidude alikuwa msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu. Muziki huo, ambao ni mchanga...
2033
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
Binyavanga Wainaina
Binyavanga Wainaina (18 Januari 1971 - 21 Mei 2019) alikuwa mwandishi kutoka nchini Kenya. Maisha Alizaliwa Nakuru, nchini Kenya. Alihudhuria masomo ya msingi na sekondari nchini Kenya kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Transkei, Afrika Kusini. Baada ya kumaliza masomo yake alihamia katika jiji la Cape Town ambapo ...
2035
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkutano%20huria
Mkutano huria
Mkutano huria ni mkutano ambao unaendeshwa na wahudhuriaji au wajumbe badala ya mwandaaji au waandaaji wa mkutano. Katika mkutano wa aina hii hakuna watoa mada na wapokea mada, hakuna watoa hotuba na wasikilizaji. Wahudhuriaji wote ndio watoa mada na wapokea mada. Dhana hii imepewa umaarufu na wataalamu wawili wa progr...
2036
https://sw.wikipedia.org/wiki/Podikasiti
Podikasiti
Podikasiti ni neno lililoanza kutumiwa mwaka 2004 pale matumizi ya programu ya RSS ilipoanza kutumiwa kusambaza matangazo kwa ajili ya kusikiliza kupitia tarakilishi au zana nyingine za mkononi kama vile aipodi. Podikasiti ni mafaili ya video au sauti ambayo yako kwenye mtandao wa tarakilishi kwa ajili ya yeyote yule...
2042
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
Mkoa wa Singida
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania: mkoa huu upo kanda ya kati, ukipakana na mikoa ya Manyara upande wa kaskazini , Dodoma mashariki, Iringa, Mbeya kusini, Tabora upande wa magharibi na Shinyanga. msimbo wa posta ni 43000. Kuna wilaya sita za Iramba, Manyoni, Singida Vijijini na Singida Mjini, Ikungi na M...
2044
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
Kigermanik
Lugha za Kigermanik ni kikundi cha lugha zenye asili ya Ulaya ya Kaskazini. Lugha za Kigermanik zenye wasemaji wengi ni Kiingereza (milioni 380) na Kijerumani (milioni 120). Lugha nyingine za Kigermanik ni lugha za Skandinavia, halafu Kiholanzi na Kiafrikaans wa Afrika Kusini. Historia Mwanzo wa lugha hizi uko gizan...
2048
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
Uganda
Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini. Uganda inamiliki sehemu ya ziwa la Viktoria Nyanza ikipakana huko na Kenya na Tanzania. Uganda ni nchi mwanachama...
2050
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
Mkoa wa Iringa
Mkoa wa Iringa ni mojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 51000. Upo katikati ya nchi, kidogo upande wa kusini. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Njombe, Mbeya, Singida na Dodoma. Makao makuu yako katika manisipaa ya Iringa. Jiografia Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa ...
2055
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
Mkoa wa Dar es Salaam
Dar es Salaam ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Mkoa wa Pwani pande zote barani na Bahari ya Hindi upande wa mashariki. Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani....
2059
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
Mkoa wa Dodoma
Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 41000. Uko katikati ya nchi na umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida. Eneo lote la mkoa lina km² 41,310. Sehemu kubwa ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB. Katika sensa ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa Mkoa w...
2060
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiyunani
Kiyunani
Kiyunani ni jina la Kiswahili cha zamani kwa "Kigiriki", ambayo ni lugha ya nchi ya Ugiriki ("Uyunani") au kwa tabia za Wagiriki ("Wayunani"). Neno la Kiswahili cha zamani limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo يونان yunan linataja kiasili Wagiriki wa eneo la Ionia au wa kabila la Waioni walioishi kwenye pwani ya masha...
2062
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
Roma (maana)
Roma (pia: Rumi) ni jina linalotumika kwa mji wa Roma (mji mkuu wa Italia), ama kwa dola la Roma lililokuwa kwa karne kadhaa kabla na baada ya Kristo dola kubwa kuliko zote duniani, tena kwa Kanisa la Roma ambalo ni kiini cha Kanisa Katoliki lote. Lilikuwa pia jina la mungu wa kike katika dini ya Roma ya Kale. Roma a...
2064
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilatini
Kilatini
Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule, vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili. Ilikuwa pia lugha ya kimataifa ya elimu na hata leo istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kilatini. Historia Kilatini kilikuwa lugha hai tak...
2066
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zambia
Zambia
Jamhuri ya Zambia ni nchi ya Kusini mwa Afrika isiyo na mwambao baharini. Imepakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania upande wa kaskazini, Malawi upande wa mashariki, Msumbiji, Zimbabwe na Botswana upande wa kusini, Namibia na Angola upande wa magharibi. Mji mkuu ni Lusaka (wenye wakazi 1,747,152 mwaka...
2069
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tabora
Mkoa wa Tabora
Mkoa wa Tabora ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 45000. Makao makuu yako Tabora Mjini. Tabora ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania ya kati. Eneo la mkoa ni km2 76,151; mnamo km2 34,698 (46%) ni hifadhi ya misitu, km2 17,122 (22%) ni hifadhi ya wanyama. Jumla ya wakazi ilikuwa watu 3,391,...
2072
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Morogoro
Mkoa wa Morogoro
Morogoro ni jina la mto, mji, wilaya na mkoa wa Tanzania. Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 67000. Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Dodoma na Arusha. Eneo lake ni km² 72 939, ambapo kuna wakazi 3,197,104 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 (kutola 2,218,492 w...
2073
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morogoro
Morogoro
Morogoro ni jina la> Mto Morogoro Mji wa Morogoro Mkoa wa Morogoro na Wilaya za Morogoro Mjini na Morogoro Vijijini. Tanzania Makala zinazotofautisha maana
2080
https://sw.wikipedia.org/wiki/Michael%20Jackson
Michael Jackson
Michael Joseph Jackson (29 Agosti 1958 – 25 Juni 2009) alikuwa mwimbaji, dansa na mburudishaji kutoka nchini Marekani. Hufahamika zaidi kwa jina la kiheshima-utani kama Mfalme wa Pop. Hutambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote, na moja kati ya waburudishaji wenye mvuto na athira kubwa katika ...
2081
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mnazi
Mnazi
Mnazi ni neno linaloweza kutaja: mti wa mnazi (mti) mwenye matunda ya nazi kinywaji cha mnazi (kinywaji) kinachotengenezwa na utomvu wa nazi changa Makala zinazotofautisha maana
2086
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kinywaji
Kinywaji
Kuna vinywaji vingi: Maji Chai Kahawa Maziwa Soda Togwa Maji ya matunda Pombe Mnazi Mvinyo Mbege Bia Kimpumu Chang'aa
2087
https://sw.wikipedia.org/wiki/Swala
Swala
Kwa swala kama ibada ya Kiislamu, taz. Swalah. Swala ni wanyama walao nyasi katika nusufamilia Antilopinae, Aepycerotinae na Pantholopinae za familia Bovidae. Hupatikana katika maeneo yenye nyasi fupi fupi na vichaka vifupi fupi hasa kwenye maeneo mengi ya hifadhi katika Afrika. Spishi nyingine hukimbia kilometa 80 kw...
2088
https://sw.wikipedia.org/wiki/John%20F.%20Kennedy
John F. Kennedy
John Fitzgerald Kennedy (29 Mei 1917 – 22 Novemba 1963) alikuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 1961 hadi alipouawa. Maisha Alikuwa mtoto wa pili katika familia ya watoto 9. Baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu wa ukoo wenye asili ya Eire. Vita Kuu ya Pili ilipoanza alijiunga na jeshi la wanamaji. Mwaka 1943 alij...
2097
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwarara
Kwarara
Kwarara ni ndege wa nusufamilia Threskiornithinae katika familia Threskiornithidae ambao wana miguu mirefu. Domo refu lao limepindika na hutumika kwa kutafuta chakula ndani ya matope. Spishi nyingi za kwarara huweka matago yao juu ya miti, kwa kawaida pamoja na yange, koikoi au domomwiko. Jike huyataga mayai 2-4. Spis...
2099
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alexander%20Graham%20Bell
Alexander Graham Bell
Alexander Graham Bell (3 Machi 1847 – 2 Agosti 1922) alikuwa kati ya wagunduzi wa mawasiliano ya simu. Alizaliwa katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti lakini baadaye alihamia nchi za Kanada na Marekani. Baba yake alikuwa mwalimu wa watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea. Alifanikiwa katika jaribio lake la kwanza m...
2100
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karl%20Friedrich%20Benz
Karl Friedrich Benz
Karl Friedrich Benz alizaliwa tar. 25 Novemba 1844 akiitwa Karl Friedrich Michael Vaillant huko Mühlburg / Karlsruhe Ujerumani wa Kusini Magharibi. Baada ya kumzaa mamake Josephine Vaillant akaolewa na babake Johann Georg Benz. Hivyo akaitwa Karl Friedrich Michael Benz lakini baadaye akajiita Carl Friedrich Benz. Alik...
2106
https://sw.wikipedia.org/wiki/Isaac%20Newton
Isaac Newton
Isaac Newton (25 Desemba 1642 – 20 Machi 1727) alikuwa mwanahisabati, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka nchi ya Uingereza. Anakumbukwa duniani kote kutokana na michango yake mbalimbali katika sayansi. Ndiye aliyegundua tawi la kalkulasi (sambamba na Leibniz), sheria za mwendo na ya uvutano (graviti). Mchango m...
2108
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtakatifu%20Marko
Mtakatifu Marko
Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος) aliishi katika karne ya 1 BK. Alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao. Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki wa l...
2109
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtakatifu%20Paulo
Mtakatifu Paulo
Mtume Paulo (7-67 hivi) ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa. Alitangaza kifo na ufufuko wake katika nchi karibu zote zilizopo kaskazini kwa Bahari ya Kati. Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma wakati wa dhuluma iliyoanzishwa na Kaisari Nero. Tangu kale anaheshimiwa ...
2116
https://sw.wikipedia.org/wiki/Baada%20ya%20Kristo
Baada ya Kristo
Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani. Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifup...
2117
https://sw.wikipedia.org/wiki/Milenia
Milenia
Milenia (kutoka neno la Kiingereza millennium, ambalo mizizi yake ni katika Kilatini: mille, elfu, na annus, mwaka) ni kipindi cha miaka elfu moja. Hii ni sawa na kusema milenia ina karne kumi. Kwa sasa tuko katika milenia ya pili BK iliyoanza tarehe 1 Januari 2001. Lakini watu wengi walisheherekea tarehe 1 Januari ...
2118
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaizari
Kaizari
Kaizari ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani "Kaiser", lakini asili yake ni Kilatini "Caesar". Asili ya Kiroma Asili ya cheo ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa...
2119
https://sw.wikipedia.org/wiki/Duma
Duma
Duma ni mnyama mbuai aliyemo katika jamii ya paka (Felinae) ambaye hupatikana Afrika na kidogo sehemu za Asia. Chakula chake ni wanyama jamii ya swala . Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgo...
2120
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hijra
Hijra
Hijra (هجرة) ni neno la Kiarabu linalomaanisha tendo la Mtume Muhammad la kutoka Makka na kuhamia Madina mwaka 622 BK. Mwaka huo umekuwa tarehe ya kuanzisha kalenda ya Kiislamu ambayo miaka yake huhesabu miaka baada ya hijra. Maana asili ya neno lenyewe ni "kuachana" au "kutengana", kutokana na historia ya Muhammad li...
2121
https://sw.wikipedia.org/wiki/Adolf%20Hitler
Adolf Hitler
Adolf Hitler (Braunau, Austria, 20 Aprili 1889; Berlin, Ujerumani, 30 Aprili 1945) alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake. Alihutubia dharau na chuki ya kimbari dhidi ya watu wote wasio Wagermanik na hasa dhidi ya Wayahudi. Alisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia na mateso ya watu milioni kadh...
2122
https://sw.wikipedia.org/wiki/Miaka%20baada%20ya%20hijra
Miaka baada ya hijra
Miaka baada ya Hijra ni hesabu ya miaka katika kalenda ya Kiislamu. Hesabu hii ilianzishwa miaka 17 baada ya tukio lenyewe (638 BK) kufuatana na azimio la Khalifa Umar ibn al-Khattab. Waarabu waliwahi kuwa na kalenda iliyotumia mwendo wa mwezi lakini hawakuhesabu miaka. Kila mwaka ulitajwa kutokana na tukio fulani....
2127
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda%20ya%20Kiislamu
Kalenda ya Kiislamu
Kalenda ya Kiislamu ni mtindo wa kuratibu wakati unaopatikana katika nchi mbalimbali za Kiislamu. Tofauti na kalenda ya kawaida inayofuata jua hii ni kalenda ya mwezi inayofuata kuandama kwa mwezi. Pia Waislamu wanaoishi katika mazingira yasiyo ya Kiislamu hutumia kalenda hii kwa ajili ya kupanga maisha yao ya kidini,...
2128
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Lindi
Mkoa wa Lindi
Lindi ni jina la mji, wilaya na mkoa ulioko Kusini-Mashariki mwa Tanzania. Mkoa wa Lindi ni kati ya mikoa 31 iliyopo nchini Tanzania yenye postikodi namba 65000. Umepakana na mikoa ya Pwani, Mtwara, Ruvuma na Morogoro. Upande wa mashariki hupakana na Bahari Hindi. Eneo la mkoa Mkoa huu umeanzishwa mwaka 1971 na una ...
2131
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa
Kilwa
Kilwa ni jina la wilaya na mahali patatu katika mkoa wa Lindi, Tanzania. Wilaya ya Kilwa iko kati ya Dar-es-salaam na Lindi ufukoni wa Bahari Hindi. Kilwa Masoko ni makao makuu ya wilaya. Kilwa Kivinje ni mji wa kihistoria tangu karne ya 18. Kilwa Kisiwani ni kisiwa karibu na mwambao kinachotazama Kilwa Masoko. Ha...
2135
https://sw.wikipedia.org/wiki/Keremkerem
Keremkerem
Keremkerem ni ndege wa familia ya Meropidae. Wana mwili mwembamba wa rangi maridadi. Mdomo wao ni mrefu na mwembamba na mkia wa aina nyingi za keremkerem una mileli mirefu katikati. Ndege hao wanaishi uwandani kwa kanda ya tropiki na nusu-tropiki ya Afrika, Ulaya na Asia. Hula wadudu, nyuki, manyigu na mabunzi hasa, a...
2137
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
Pangani (mto)
Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia hapa Pangani Mto Pangani ni kati ya mito mikubwa ya Tanzania. Unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari ya Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani. Jina Mto unapita katika maeneo ya jumuiya zenye lugha tofautitofauti, hivyo kuna majina mbalimba...
2138
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rhapta
Rhapta
Rhapta ni jina la soko na mji wa kale katika pwani la Afrika ya Mashariki. Habari zake zilipatikana tangu karne ya kwanza katika mwongozo wa kigiriki kwa ajili ya mabaharia. Jina la Rhapta lilitajwa tena katika vitabu vingine hadi karne ya 6 BK lakini baadaye lilipotea au kubadilishwa. Wataalamu walio wengi hukubalia...
2140
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
Pangani (mji)
Pangani ni mji wa Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania, uliopo ufukoni mwa Bahari Hindi kati ya Dar es Salaam na Tanga ukielekea pande zote mbili za mdomo wa mto Pangani. Leo hii ni mji mdogo mwenye wakazi karibu 8n000 na makao makuu ya Wilaya ya Pangani. Lakini ina historia ndefu, hasa kwa sababu kuna bandari nzuri ya kia...
2141
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Tyndale
William Tyndale
William Tyndale alikuwa mwanatheolojia Mwingereza, kasisi ya kanisa na mtaalamu aliyetafsiri Biblia mara ya kwanza katika Kiingereza cha kisasa. Alizaliwa huko Gloucestershire mnamo mwaka 1494 - aliuawa Vilvoorde (Brabant - Ubelgiji ya leo) tarehe 6.9.1536. Tafsiri yake ya Biblia ilikuwa toleo la kwanza lililochapishwa...