global_id
stringlengths
1
4
messages
listlengths
1
201
label
stringclasses
20 values
7100
[ { "role": "assistant", "content": "Atbara (kwa Kiarabu: نهر عطبرة, Nahr ʿAṭbara) ni tawimto la Nile linalopatikana kaskazini magharibi mwa Ethiopia na katika Sudan.\n\nChanzo chake ni katika milima ya Simien (Ethiopia) takriban km 50 kaskazini kwa Ziwa Tana au km 30 magharibi kwa mji wa Gondar. \n\nTawimto...
wiki:sw
7101
[ { "role": "assistant", "content": "Mihozo ni ndege wa jenasi Oenanthe, Saxicola na Campicoloides. Zamani wataalamu waliwaweka katika familia ya mikesha (Turdidae), lakini siku hizi mihozo huainiwa baina ya shore (Muscicapidae). Mihozo wana mabaka maalum meusi na meupe au mekundu na meupe kwa kiuno na mkia w...
wiki:sw
7102
[ { "role": "assistant", "content": "Ujerumani (pia: Udachi, kwa Kijerumani: Deutschland) ni nchi ya Ulaya ya Kati.\n\nImepakana na Denmark, Poland, Ucheki, Austria, Uswisi, Ufaransa, Luxemburg, Ubelgiji na Uholanzi.\n\nNdiyo nchi yenye watu wengi zaidi katika Ulaya, isipokuwa Urusi. \n\nUchumi wa Ujerumani u...
wiki:sw
7103
[ { "role": "assistant", "content": "Okapi (jina la kisayansi: Okapia johnstoni) ni mamalia wa familia ya twiga. Umbo lake hufanana na farasi ina michoro miguuni kama punda milia lakini haina uhusiano naye, ni aina ya twiga. \n\nOkapi ni mnyama aliyejulikana na wenyeji wa maeneo yake tu hadi mwaka 1901. Hapo...
wiki:sw
7104
[ { "role": "assistant", "content": "Limpopo ni mto wa kusini mwa Afrika unaoishia katika Bahari Hindi. \n\nChanzo kipo katika milima ya Witwatersrand, kati ya Pretoria na Johannesburg, nchini Afrika Kusini. Sehemu ya kwanza inaitwa \"Krokodil\" (Kiafrikaans kwa mamba). Baada ya kupokea mto wa Marico jina lin...
wiki:sw
7105
[ { "role": "assistant", "content": "Kisiwa cha Msumbiji (kwa lugha ya Kireno: \"Ilha de Moçambique\") ni kisiwa kidogo (na pia mji) kilichopo km 3 mbele ya mwambao wa Msumbiji ya kaskazini. Urefu ni km 3 na upana kati ya m 500 hadi 200. Kisiwa ni sehemu ya mkoa wa Nampula. \n\nKisiwa kilikuwa chanzo cha kolo...
wiki:sw
7106
[ { "role": "assistant", "content": "Kasubi ni jina la kilima ndani ya mji wa Kampala mji mkuu wa Uganda. Kasubi imejulikana hasa kama mahali pa Makaburi ya Kasubi ya wafalme wa Buganda. \n\nMwaka 1882 ikulu ya Kabaka Mutesa I. ilijengwa kwenye kilima cha Kasubi. Alipokufa ikulu ikawa kaburi lake jinsi iliyvo...
wiki:sw
7107
[ { "role": "assistant", "content": "Bustani ya wanyama ni mahali ambapo wanyama, hasa wanyamapori wa aina mbalimbali, wanatunzwa ili watu wapate kuwatazama. Siku hizi bustani Za wanyama zimekuwa pia mahali pa kutunza spishi au aina za wanyama walioko hatarini kutokomea. Vile vile bustani za wanyama zimewekwa...
wiki:sw
7108
[ { "role": "assistant", "content": "Kabaka ni cheo cha mfalme wa Buganda ambayo ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Cheo kingine pamoja na Kabaka ni Ssebataka. \n\nTangu mwisho wa karne ya 19 Makabaka wamekuwa Wakristo Waanglikana wakipokea taji katika kanisa kuu la Kianglikana la Kampala. Makabaka wa mwis...
wiki:sw
7109
[ { "role": "assistant", "content": "UNESCO ni kifupisho cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization yaani Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.\n\nNi kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani.\n\nKisheria ...
wiki:sw
7110
[ { "role": "assistant", "content": "Kofi Atta Annan (8 Aprili 1938 - 18 Agosti 2018) alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Annan na Umoja wa Mataifa walipata Tuzo ya Amani ya Nobeli mwaka 2001. Alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa Kofi Annan Foundation na pia mwenyekiti wa Elders, shirika la ...
wiki:sw
7111
[ { "role": "assistant", "content": "Shaka (pia: Tshaka, Tchaka au Chaka; halafu: Shaka Zulu, Shaka ka Senzangakhona) (* takriban 1781 - 1828 BK) alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo. \n\nSifa z...
wiki:sw
7112
[ { "role": "assistant", "content": "Afrika Kusini ni nchi kubwa ya Afrika ya Kusini yenye wakazi takriban milioni 54. \n\nImepakana na Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji na Uswazi. Nchi nzima ya Lesotho iko ndani ya eneo la Afrika Kusini.\n\nMji mkubwa ni Johannesburg. Majukumu ya mji mkuu yamegawiwa kati...
wiki:sw
7113
[ { "role": "assistant", "content": "Eswatini (jina rasmi tangu mwaka 2018 ni Umbuso weSwatini; kifupi cha Kiswati: eSwatini; kwa Kiswahili pia: Uswazi; kwa Kiingereza: Eswatini) ni nchi ndogo ya Kusini mwa Afrika isiyo na pwani katika bahari yoyote. \n\nImepakana na Afrika Kusini na Msumbiji.\n\nMji mkuu ni ...
wiki:sw
7114
[ { "role": "assistant", "content": "Mto Vaal ni tawimto mrefu wa mto Oranje katika Afrika Kusini. \n\nChanzo chake ni katika milima ya Drakensberg mkoani Mpumalanga mashariki kwa mji wa Johannesburg. \n\nInaelekea kusini-magharibi hadi kuungana na mto Oranje karibu na mji wa Kimberley mkoani Northern Cape. \...
wiki:sw
7115
[ { "role": "assistant", "content": "Côte d'Ivoire (tamka: kot divwar; kwa Kifaransa jina lina maana ya Pwani ya pembe za ndovu; kwa Kiingereza: Ivory Coast; kwa Kiswahili pia: Kodivaa) ni nchi ya Afrika ya Magharibi.\n\nImepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana...
wiki:sw
7116
[ { "role": "assistant", "content": "Abidjan ndio mji mkubwa zaidi nchini Cote d'Ivoire pia ni bandari kuu ya nchi kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki. Abidjan haiko baharini moja kwa moja lakini kwenye wangwa ya Ebrie inayotengwa na bahari kwa kanda nyembamba ya mchanga. \n\nIlikuwa pia mji mkuu ra...
wiki:sw
7117
[ { "role": "assistant", "content": "Sierra Leone ni nchi ya Afrika ya Magharibi. \n\nImepakana na Guinea na Liberia, upande wa magharibi iko bahari ya Atlantiki.\n\nJina la nchi lina asili ya Kireno na linamaanisha \"Mlima wa Simba\". \n\nNi koloni la zamani la Uingereza na tangu 27 Aprili 1961 ni jamhuri hu...
wiki:sw
7118
[ { "role": "assistant", "content": "Freetown ni mji mkuu pamoja na badari kubwa na kitovu cha uchumi wa nchi Sierra Leone. Iko kwenye kando la Atlantiki kwenye rasi ya Freetown. Idadi ya wakazi ni 1,070,000. \n\nMji uliundwa 1787 kwa ajili ya watumwa wenye asili ya Afrika waliowekwa huru. Hapo ni asili ya ji...
wiki:sw
7119
[ { "role": "assistant", "content": "Senegal (pia Senegali) ni nchi ya Afrika ya Magharibi iliyopo upande wa kusini wa mto Senegal. \n\nImepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea na Guinea-Bisau kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi. \n\nNchi ya Gambia inazungukwa n...
wiki:sw
7120
[ { "role": "assistant", "content": "Brazzaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo. Una wakazi 2,308,000 (mwaka 2019) ambao ni sawa na 40% ya wananchi wote. \n\nUko kando ya mto Kongo ukitazamana na mji wa Kinshasa ng'ambo ya mto. \n\nBrazzaville una bandari kwenye mto Kongo na mwanzo wa reli kuelekea pwani.\n\...
wiki:sw
7121
[ { "role": "assistant", "content": "Kinshasa (jina la awali kwa Kifaransa: Léopoldville, na kwa Kiholanzi: Leopoldstad) ni mji mkuu na mji mkubwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, iliyojulikana kama Zaire miaka 1971-1997. Mji uko kwenye Mto Kongo .\n\nZamani pahali pa vijiji vya uvuvi, Kinshasa sasa ni j...
wiki:sw
7122
[ { "role": "assistant", "content": "Karl Peters au Carl Peters (27 Septemba 1856 – 10 Septemba 1918) alikuwa mpelelezi na mwanasiasa Mjerumani aliyeanzisha koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.\n\nUtoto na masomo \nPeters alizaliwa mwaka 1856 Neuhaus de Elb, ndani ya ngome ya Hannover, katika Ujeruman...
wiki:sw
7123
[ { "role": "assistant", "content": "Unajimu (wakati mwingine pia: astrolojia kutoka Kiingereza: \"astrology\") ni mafundisho yasiyo ya kisayansi juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha hapa duniani. Wafuasi wa unajimu hufundisha ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio duniani kama amani, vita au...
wiki:sw
7124
[ { "role": "assistant", "content": "Nigeria (kwa Kiswahili pia: Nijeria au Naijeria) ni nchi ya Afrika ya Magharibi kwenye pwani ya Bahari Atlantiki. \n\nImepakana na Benin, Niger, Chad na Kamerun. \n\nMji mkuu ni Abuja ikitanguliwa na Lagos hadi mwaka 1991. \n\nNigeria imepata uhuru wake tarehe 1 Oktoba 196...
wiki:sw
7125
[ { "role": "assistant", "content": "Tiba (au: Uganga) ni elimu kuhusu magonjwa ya binadamu mwilini na rohoni, jinsi ya kuzuia magonjwa na kurudisha uzima. Matibabu ni muhimu kwa afya ya binadamu na yanahitajika sana ili kumpa maisha mazuri.\n\nTiba imeendelea kiasi cha kuwa na matawi yanayoangalia hasa:\n ma...
wiki:sw
7126
[ { "role": "assistant", "content": "Khartoum (الخرطوم al-Khartūm) ni mji mkuu wa Sudan na pia mki mkuu wa dola la shirikisho la Khartoum. Mji uko mahali mito ya Nile nyeupe na Nile ya buluu inapokutana. Kisheria \"Khartoum\" ni eneo tu mashariki ya Nile nyeupe na kusini ya Nile ya buluu lakini hali halisi Kh...
wiki:sw
7127
[ { "role": "assistant", "content": "Omdurman (au: Omdourman, Kar: أم درمان Umm Durmān ) ni mji mkubwa kabisa nchini Sudan kando la mto Nile ikitazama mji mkuu Khartoum. Pamoja na Khartoum na Bahri ni mji mmoja kubwa sana unaounganishwa kwa madaraja kadhaa.\n\nIna wakazi wanaokadiriwa kufikia karibu milioni...
wiki:sw
7128
[ { "role": "assistant", "content": "Wadi Halfa (Kar: وادي حلفا) ni mji wa Sudan ya kaskazini kwenye mwambao wa Ziwa Nasser. Ni mwisho wa reli kutoka Khartoum na bandari ya feri kwenda Aswan nchini Misri.\n\nMji huu ulianzishwa katika karne ya 19. Baada ya 1976 wakati wa kumaliza lambo la Aswan palikuwa na mi...
wiki:sw
7129
[ { "role": "assistant", "content": "Kairo (kwa Kiarabu القاهرة al-Qāhira – „mwenye ushindi“) ni mji mkuu wa Misri na mji mkubwa wa nchi zote za Kiarabu, pia moja kati ya majiji makubwa duniani. \n\nKairo yenyewe inakadiriwa kuwa na wakazi 10,230,350 , kanda ya jiji pamoja na mitaa ya nje na mapembizo ni 15,6...
wiki:sw
7130
[ { "role": "assistant", "content": "Songwe ni jina la mito miwili ya Tanzania: mmoja uko katika mkoa wa Mbeya, mwingine katika mkoa wa Songwe. \n\nSongwe ya Kusini ina chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya ikielekea kusini na kuishia Ziwa Nyasa. Baada ya kupita Itumba (Ileje) mto ni mpaka ...
wiki:sw
7131
[ { "role": "assistant", "content": "Hans Adolf Krebs (25 Agosti 1900 – 22 Novemba 1981) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Mwaka wa 1933, kwa vile wazazi wake walikuwa Wayahudi alilazimishwa kuhamia Uingereza. Hasa alichunguza athari za kikemia ndani ya chembe hai. Mwaka wa 1953, pamoja na Fritz Li...
wiki:sw
7132
[ { "role": "assistant", "content": "{{Infobox_Person \n| jina = Edward Albee\n| nchi = Marekani\n| majina_mengine =\n| picha = Edward Albee.jpg\n| ukubwawapicha = 200px\n| maelezo_ya_picha = Edward mnamo 1961\n| jina_la_kuzaliwa = Edward Franklin Albee III\n| tarehe_ya_kuzaliwa ...
wiki:sw
7133
[ { "role": "assistant", "content": "Thornton Niven Wilder (17 Aprili 1897 – 7 Desemba 1975) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Aliandika riwaya na tamthiliya. Mwaka wa 1928 alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa riwaya yake The Bridge of San Luis Rey. Tena alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya m...
wiki:sw
7134
[ { "role": "assistant", "content": "William Carlos Williams (17 Septemba 1883 – 4 Machi 1963) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Marekani. Pamoja na kufanya kazi kama daktari, aliandika mashairi, insha za historia na riwaya fupi. Mwaka wa 1963 wakati alipokuwa ameshafariki aliteuliwa kuwa mshindi wa...
wiki:sw
7135
[ { "role": "assistant", "content": "Tuzo ya Pulitzer ni tuzo iliyoanzishwa na Joseph Pulitzer katika hati ya wasia yake. Tangu mwaka wa 1917 imetolewa kila mwaka na Chuo Kikuu cha Columbia katika mji wa New York kwa ajili ya maandishi hodari yanayoendeleza uandikaji habari na fasihi ya Marekani kwa jumla.\n\...
wiki:sw
7136
[ { "role": "assistant", "content": "Auguste Marie Francois Beernaert (26 Julai 1829 – 6 Oktoba 1912) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Ubelgiji. Kuanzia 1884 hadi 1894 alikuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Baadaye alikuwa mwakilishi wa Ubelgiji kwenye mikutano ya amani iliyofanyika katika mj...
wiki:sw
7137
[ { "role": "assistant", "content": "Mtakatifu Thomas Aquinas (Roccasecca, katika eneo la watawala wa Aquino, leo katika wilaya ya Frosinone, Italia, 1224 au 1225 - Fossanova, wilaya ya Latina, Italia, 7 Machi 1274) alikuwa mtawa wa Shirika la Wahubiri na padri wa Kanisa Katoliki. \n\nMwenye akili kubwa ajabu...
wiki:sw
7138
[ { "role": "assistant", "content": "Sir Ralph Norman Angell Lane (26 Desemba 1872 – 7 Oktoba 1967) alikuwa mtaalamu wa uchumi na mwandishi wa habari kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alijitahidi kutekeleza amani ya kimataifa. Anajulikana sana kwa kitabu chake “Uwongo Mkubwa” (kwa Kiingereza Great Illusion) kili...
wiki:sw
7139
[ { "role": "assistant", "content": "Kigali ni mji mkuu wa Rwanda na pia mji mkubwa kuliko mingine yote nchini.\n\nIko karibu sana na mstari wa ikweta kwenye kimo cha 1400 - 1600 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya wastani hakuna baridi kali wala joto kali.\n\nKigali ina wakazi 600,000.\n\nHistoria \nKigali ilian...
wiki:sw
7140
[ { "role": "assistant", "content": "Ruanda-Urundi ni jina la zamani kwa ajili ya nchi za Rwanda na Burundi. Zote mbili zilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi 1916. Wakatu wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia jeshi la Force Publique la Ubelgiji kutoka Kongo lilivamia maeneo yake; katika ugawaji w...
wiki:sw
7141
[ { "role": "assistant", "content": "El Aaiún (pia Laâyoune, العيون = al-ʿUyūn) ni mji mkubwa wa Sahara ya Magharibi kwenye bonde la Saguia el Hamra karibu na mwambao wa Atlantiki. \n\nHadi mwaka 1976 ilikuwa makao makuu ya utawala wa kikoloni wa Hispania. Baadaye mji ulivamiwa na Moroko pamoja na sehemu kubw...
wiki:sw
7142
[ { "role": "assistant", "content": "Libreville ni mji mkuu na mji mkubwa nchini Gabon. Iko kwenye pwani la Atlantiki kiasi ndani ya mdomo wa mto Komo au mto Gabon. Kuna bandari. \n\nLibreville ina wakazi 578,000 (2005). Jina la “Libreville” lina maana ya “mji huru” au “mji wa watu huru” kutokana na historia ...
wiki:sw
7143
[ { "role": "assistant", "content": "Malabo ni mji mkuu wa Guinea ya Ikweta mwenye wakazi 90,000 - 100,000. Iko mwambaoni wa Atlantiki kwenye pwani la kaskazini ya kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Po).\n\nMji ulianzishwa kwa jina la Port Clarence kuanzia 1827 na Waingereza waliokuwa wamekodi kisiwa cha Fern...
wiki:sw
7144
[ { "role": "assistant", "content": "Harare (zamani: Salisbury) ni mji mkuu wa Zimbabwe pia mji mkubwa nchini ukiwa kitovu cha utawala na uchumi. Uko kwenye kimo cha mita 1,500 juu ya UB. \n\nIdadi ya wakazi imehesabiwa kufika 1,492,000, pamoja na mitaa ya nje hadi 3,120,000. Mtaa wa nje ulio mkubwa ni Chitun...
wiki:sw
7145
[ { "role": "assistant", "content": "Luanda (kirefu: São Paulo de Luanda: pia Loanda) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Angola ikiwa na wakazi 2,487,484 (katika rundu la jiji 7,805,000) wanaongezeka haraka kutoka ndani na nje ya nchi na ya bara la Afrika.\n\nJiografia \nMji wa Luanda uko mkoani Luanda, kaskazini ...
wiki:sw
7146
[ { "role": "assistant", "content": "Kwanza (kwa Kireno: Cuanza, pia Coanza, Quanza au Kuanzani) ni mto katika Angola. Chanzo chake ni katika Nyanda za Juu za Bie ambako mito mingi mikubwa inaanza.\n \nJina la mto limekuwa pia jina la mikoa miwili ya Cuanza Norte (kaskazini kwa mto) na Cuanza Sul (kusini kwa ...
wiki:sw
7147
[ { "role": "assistant", "content": "Bié ni mkoa wa Angola wenye eneo la km² 70,314 na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya lakhi nane na milioni moja.\n\nMakao makuu ya mkoa yako mjini Kuito (Cuito). \n\nHali ya hewa haina joto kali kutokana na milima na mvua ya mara kwa mara. Hayo yote huwezesha kilimo cha mah...
wiki:sw
7148
[ { "role": "assistant", "content": "Nyanda za Juu za Bie ziko kwenye kitovu cha nchi Angola. Zinapanda hadi ya kuwa na kimo cha 2,619 m juu ya UB.\n\nKutokana na kiasi kikubwa cha mvua kinachopatikana hapa eneo ni chanzo cha mito mingi muhimu ya Afrika ya Kusini na Afrika ya Kati.\n\nMito muhimu inayoanza Ny...
wiki:sw
7149
[ { "role": "assistant", "content": "Kunene (au Cunene) ni mto wa Afrika ya kusini-magharibi. \n\nChanzo chake kiko Angola katika Nyanda za Juu za Bie, unaelekea kusini hadi kufikia mpaka wa Namibia kwenye mji wa Ruacana. \n\nKuanzia hapo mto ni mpaka kati ya Angola na Namibia hadi kufikia bahari ya Atlantiki...
wiki:sw
7150
[ { "role": "assistant", "content": "Bloemfontein (tamka: \"Blumfontain\" - Kiholanzi/Kiafrikaans \"chemchemi ya maua\") ni kati ya miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini pamoja na Pretoria na Cape Town. Jina la Kisotho ni Mangaung linalomaanisha \"kwa duma\". \nBloemfountain ni makao ya Mahakama Kuu ya Afrika Ku...
wiki:sw
7151
[ { "role": "assistant", "content": "Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India na Burma. Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. \n\nJina “mwarobaini” li...
wiki:sw
7152
[ { "role": "assistant", "content": "Pretoria ni moja kati ya miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini na makao makuu ya serikali. Miji mikuu mingine ni Cape Town kama makao ya Bunge na Bloemfontein kama makao ya Mahakama Kuu. \n \nPretoria iko kaskazini mwa jimbo la Gauteng katika bonde la milima ya Magalies kweny...
wiki:sw
7153
[ { "role": "assistant", "content": "Biolojia ni sayansi asilia inayohusu utafiti wa uhai na viumbehai, kama vile mimea, wanyama, kuvu (kama uyoga), bakteria na virusi, na jinsi vinavyohusiana kati yao na katika mazingira yao, pamoja na muundo wao, kazi, ukuaji, asili, mageuko, uenezi, na nadharia ya uainisha...
wiki:sw
7154
[ { "role": "assistant", "content": "Porto Novo (Kireno kwa: \"Bandari mpya\" - inaitwa na wenyeji pia Hogbonou na Adjache) ni mji mkuu rasmi wa Benin. Ni mji wa bandari kwenye kidaka cha Atlantiki. \n\nMwaka 2002 Porto Novo ilikuwa na wakazi 223,552 (sensa 2002) na mji wa pili katika Benin. Hapa ni ikulu ya ...
wiki:sw
7155
[ { "role": "assistant", "content": "Cape Town (yaani \"Mji wa rasi\", kwa Kiafrikaans: Kaapstad; kwa Kixhosa: iKapa) ni mji mkubwa wa tatu wa Afrika Kusini na mmoja kati ya miji mikuu mitatu ya nchi ikiwa ni makao ya Bunge. Pia ni mji mkuu wa jimbo la Rasi Magharibi (Western Cape / Wes-Kaap). Ni sehemu ya Ji...
wiki:sw
7156
[ { "role": "assistant", "content": "Robben Island ni kisiwa kidogo 12 km mbele ya mji wa Cape Town (Afrika Kusini) katika Atlantiki.\nKisiwa kina eneo la hektari 547, urefu ni km 4.5 na upana hadi km 1.5.\n\nKisiwa kimejulikana kutokana na gereza lake na mfungwa mashuhuri Nelson Mandela. Wafungwa pamoja naye...
wiki:sw
7157
[ { "role": "assistant", "content": "Mlima wa Meza (kwa Kiingereza: Table Mountain) ni mlima wenye sehemu ya tambarare juu na mtelemko mkali upande. \n\nMlima wa Meza unaojulikana zaidi ni ule wa Cape Town (Afrika Kusini), ambao urefu wake unafikia mita 1,085 juu ya usawa wa bahari. Lakini umbo hili linapatik...
wiki:sw
7158
[ { "role": "assistant", "content": "Banjul ni mji mkuu wa Gambia. Mji wenyewe una wakazi 34,828 pekee lakini pamoja na mitaa ya nje ni zaidi ya nusu milioni.\n\nBanjul iko kwenye kisiwa cha Mt. Mariamu (au: Kisiwa cha Banjul) mdomoni mwa mto Gambia unapoishia katika bahari ya Atlantiki.\n\nHistoria \nWainger...
wiki:sw
7159
[ { "role": "assistant", "content": "Niamey ni mji mkuu wa Niger. Iko mwambaoni wa mto Niger. Ikiwa na wakazi 1,803,000 hivi (2018) Niamey ni mji mkubwa wa Niger na kitovu cha kiutawala, kiuchumi na kiutamaduni.\n\nKilimo katika mazingira ya mji kina karanga kama mazao ya sokoni; kuna viwanda vya matofali, sa...
wiki:sw
7160
[ { "role": "assistant", "content": "Bamako ni mji mkuu wa Mali pamoja na kuwa mji mkubwa nchini ikiwa na wakazi milioni moja na nusu. Iko mwambaoni wa mto Niger katika kusini ya nchi.\n\nHistoria \nBamako ilianzishwa kama mji katika karne ya 17 BK na machifu wa kabila la Niare Seribadian Niaré na Soumba Coul...
wiki:sw
7161
[ { "role": "assistant", "content": "Matatu ni neno la kawaida nchini Kenya na Uganda la kutaja gari aina ya daladala linalotumika kama usafiri wa umma. \n\nJina \"matatu\" labda lilitokana na nauli ya sarafu tatu iliyokuwa kawaida kwa safari moja matatu yalipoanza.\n\nMatatu huhudumia njia maalumu yenye namb...
wiki:sw
7162
[ { "role": "assistant", "content": "Kiafrikaans (Afrikaans) ni lugha ya Afrika Kusini iliyotokea katika karne nne zilizopita kwenye msingi wa Kiholanzi pamoja na athari za lugha mbalimbali. Hata kama ni lugha iliyozaliwa Afrika na kujadiliwa hapa, kitaalamu ni kati ya lugha za Kigermanik.\n\nImekuwa lugha ra...
wiki:sw
7163
[ { "role": "assistant", "content": "Tunis (kwa Kiarabu: تونس ) ni mji mkuu wa Tunisia na mji mkubwa nchini ikiwa na wakazi 602,560 (mwaka 2022) ambao pamoja na wakazi wa mitaa ya nje wanafikia jumla ya milioni 2.7.\n\nMji uko ufukoni mwa Mediteranea, karibu na Karthago ya Kale. \n\nMji wa kale (Medina ya Tun...
wiki:sw
7164
[ { "role": "assistant", "content": "Rabat (Kiarabu الرباط Ar-Ribat) ni mji mkuu wa Moroko na mji mkubwa wa pili nchini baada ya Casablanca ikiwa na wakazi 1,622,860 (2004) pamoja na Sale. Jina lenyewe la \"ribat\" linadokeza kwa asili ya mji kuwa boma la kijeshi.\n\nRabat iko mwambanoni wa Atlantiki kwenye m...
wiki:sw
7165
[ { "role": "assistant", "content": "Jamhuri ya Bou Regreg (pia Jamhuri ya Sale) ilikuwa dola dogo katika eneo la miji Rabat na Sale, mdomoni mwa mto Bou Regreg, lililoanzishwa mwaka 1627.\n\nWatawala walikuwa maharamia waliounda serikali baada ya mwisho wa utawala wa ufalme wa Wasaadi.\n\nHalmashauri ya wawa...
wiki:sw
7166
[ { "role": "assistant", "content": "Gaborone ni mji mkuu wa Botswana ikiwa na wakazi 186,000 (mwaka 2001). Iko kusini-mashariki ya nchi.\n\nMji huu ulianzishwa kwenye makao ya chifu Kgosi Gaborone wa BaTlokwa. Waingereza walijenga kituo kidogo cha kiutawala kando ya kijiji cha chifu. Makao haya madogo yaliku...
wiki:sw
7167
[ { "role": "assistant", "content": "Chitungwiza ni mji wa Zimbabwe, kilometa 9 upande wa kusini wa mji mkuu Harare. Mwaka 2022 ulikuwa na wakazi 371,000. Walio wengi wanafanya kazi Harare kwa sababu kuna nafasi chache tu za ajira.\n\nChitungwiza ilipata cheo cha manispaa mwaka 1981. Asili yake ni mitaa mitat...
wiki:sw
7168
[ { "role": "assistant", "content": "Lomé ni mji mkuu wa Togo katika Afrika ya Magharibi pia mji mkubwa wa nchi hiyo pamoja na kuwa kitovu chake cha kiutawala na kiuchumi ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa 796,000 (mwaka 2006). Iko mwambaoni mwa Ghuba ya Guinea ya Atlantiki kwenye pwani fupi ya Togo yenye upa...
wiki:sw
7169
[ { "role": "assistant", "content": "Ghuba ya Guinea ni kidaka kikubwa cha bahari ya Atlantiki kwenye pwani ya magharibi mwa Afrika. \n\nEneo lake linahesabiwa kuanza nchini Liberia kwenye rasi ya Palmas na kwisha kwenye rasi Lopez nchini Gabon.\n\nJina la \"Guinea\" limetokana na jina la kale la sehemu kubwa...
wiki:sw
7170
[ { "role": "assistant", "content": "--Kwa maana mbalimbali za neno Guinea angalia Guinea (maana)--\n\nGuinea ni jina la kihistoria kwa ajili ya kanda ya kusini ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa Sahara na Atlantiki. Nchi zote kuanzia Senegal hadi kaskazini ya Angola zilihesabiwa kuwa \"Guinea\". Waandishi...
wiki:sw
7171
[ { "role": "assistant", "content": "Graça Simbine Machel alikuwa mke wa marehemu Rais wa Msumbiji Samora Machel na tangu 1998 mke wa Nelson Mandela.\n\nAlizaliwa tarehe 17 Oktoba 1946 nchini Msumbiji. Akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto sita wa mzee Simbine na bibi Nelly. Baba yake alifariki majuma matat...
wiki:sw
7172
[ { "role": "assistant", "content": "Mawese ni mafuta ya kula yanayotolewa katika matunda ya mti wa mchikichi (Elaeis guineensis). Ni mafuta ya kupikia ya Afrika, hasa penye asili ya mchikichi kutokana na kupatikana kwa wingi katika nchi za kanda ya Guinea.\n\nMawese kutokana na nyama ya tunda \nKuna aina mbi...
wiki:sw
7173
[ { "role": "assistant", "content": "Yaoundé ni mji mkuu na mji mkubwa wa pili nchini Kamerun baada ya Douala. Ina wakazi 1,299,369 (2021\n\nJiografia \nMji uko kwenye kimo cha 730 m juu ya UB katika vilima vya Kamerun ya magharibi takriban 160 km kutoka mwambao wa Atlantiki. \nHali ya hewa ni ya kitropiki; h...
wiki:sw
7174
[ { "role": "assistant", "content": "Douala ni mji mkubwa wa Kamerun ukiwa na wakazi 1,338,082 (2021). \n\nUko kilometa 24 kutoka bahari kwenye mdomo mpana wa mto Wouri unaokomea kwenye Ghuba ya Guinea ya Atlantiki. Bandari yake inaifanya kuwa kitovu cha uchumi wa Kamerun.\n\nWakati wa ukoloni wa Kijerumani u...
wiki:sw
7175
[ { "role": "assistant", "content": "Mbabane ni mji mkuu wa Eswatini ikiwa na wakazi 70,000 (2003). Ofisi za serikali ziko huko lakini bunge na jumba la mfalme yako mjini Lobamba.\n\nMji uko kwenye milima ya Mdimba kwenye kimo cha mita 1200 juu ya UB.\n\nHistoria \nMji ulianzishwa na Waingereza mwaka 1902 BK ...
wiki:sw
7176
[ { "role": "assistant", "content": "Bendera ya Senegal ina milia tatu za wima pamoja na nyota ya pembetatu katikati.\n\nMilia ni za rangi nyekundu, njano na kijani kibichi. Nyota ni ya kijani.\n\nMaana ya rangi ni kama zifuatazo:\n Nyekundu hudokeza mapambano ya uhuru, damu iliyomwagika na matumaini ya ujama...
wiki:sw
7177
[ { "role": "assistant", "content": "Bendera ya Eswatini ina milia ya rangi za buluu, njano na nyekundu. Katikati iko ngao ya kijeshi ya Kiafrika yenye rangi nyeusi na nyeupe pamoja na mikuki ya njano.\n\nUpana wa milia ni katika uhusiano wa 3:1:8:1:3. Rangi zina maana ifuatayo:\n Nyekundu hukumusha damu iliy...
wiki:sw
7178
[ { "role": "assistant", "content": "Bendera ya Ethiopia mara nyingi inatajwa kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika. Rangi zake ni kijani kibichi, njano na nyekundu. Kutokana na sifa za Ethiopia za kuwa nchi ya pekee katika Afrika iliyojitetea dhidi ya uvamizi wa ukoloni. Rangi zake zilikuwa kama alama ya umoja ...
wiki:sw
7179
[ { "role": "assistant", "content": "Yamoussoukro ni mji mkuu rasmi wa Cote d'Ivoire tangu 1983 ilipochukua nafasi hii kutoka Abidjan inayoendelea kuwa mji mkubwa na kitovu cha kiuchumi pia kiutamaduni na makao ya ofisi nyingi za serikali. Iko takriban 230 km kutoka pwani karibu na kitovu cha nchi. Kuna wakaz...
wiki:sw
7180
[ { "role": "assistant", "content": "Conakry (pia: Konakry) ni mji mkuu wa Guinea wenye wakazi 2,000,000 (mwaka 2002). Mji una bandari mwambaoni wa Ghuba ya Guinea ya Atlantiki.\n\nHistoria \nChanzo cha Conakry ni kwenye kisiwa cha Tombo kilicho karibu sana na rasi ya Kaloum. Mji ulianzishwa baada ya kisiwa h...
wiki:sw
7181
[ { "role": "assistant", "content": "Bendera ya Guinea ina milia mitatu ya kusimama yenye rangi za nyekundu, njano na kijani - kibichi. Rangi hizi ziko pia kwenye bendera ya Ethiopia na ya Ghana zinaonyesha athira za Ethiopia (nchi ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi ya ukoloni) na pia Ghana (nchi ya kwanza ...
wiki:sw
7182
[ { "role": "assistant", "content": "Buganda ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Mfalme wa Buganda anatumia cheo cha Kabaka. Jina la nchi Uganda ni umbo la Kiswahili la neno Buganda. \n\nTangu karne ya 18 BK hadi karne ya 20 Buganda ilikuwa dola lenye enzi katika eneo la Ziwa Viktoria. \n\nLeo hii ni sehemu...
wiki:sw
7183
[ { "role": "assistant", "content": "Ziwa Viktoria (pia: Ziwa Nyanza au Ziwa Ukerewe) ni ziwa kubwa la Afrika ya Mashariki lililopo baina ya Tanzania, Kenya na Uganda. Eneo la maji ya ziwa limegawanywa 49% (km2 33,700) nchini Tanzania, 45% (km2 31,000) nchini Uganda, na 6% (km2 4,100) nchini Kenya.\n\nZiwa Vi...
wiki:sw
7184
[ { "role": "assistant", "content": "Majiji yasiyoonekana (kwa Kiitalia \"Le città invisibili\", na kwa Kiingereza \"Invisible Cities\") ni kitabu cha hadithi kilichoandikwa na mwandishi toka Italia, Italo Calvino. \n\nKitabu hiki kinaelezea mazungumzo kati ya msafiri Marco Polo kutoka mji wa Venice, Italia,...
wiki:sw
7185
[ { "role": "assistant", "content": "Kombe la Dunia la FIFA au Kombe la dunia la soka ni mchuano wa kimataifa wa mchezo wa soka kwa wanaume. Iliamuliwa 28 Mei 1928 na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa msukumo wa rais wake Jules Rimet, ilikuwa wazi kwa timu zote za mashirikisho yanayotambuliwa na FIFA, wak...
wiki:sw
7186
[ { "role": "assistant", "content": "Orchestra Baobab ni bendi maarufu ya muziki wa dansi toka nchini Senegal. Bendi hii imekuwepo katika ramani ya muziki wa Afrika toka ilipoanzishwa mwaka 1970. \n\nOrchestra Baobab inapiga muziki ambao ni mchanganyiko wa vionjo vya muziki toka Cuba, Visiwa vya Karibiani na ...
wiki:sw
7187
[ { "role": "assistant", "content": "Nouakchott (Kiarabu: نواكشوط) ni mji mkuu wa Mauritania. Iko mwambaoni wa Atlantiki katika magharibi ya nchi. Idadi ya wakazi imekadiriwa kupita milioni moja.\n\nHistoria \nHadi 1958 Nouakchott ilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi. Imekua tangu uhuru. Wakati wa ukoloni Maureta...
wiki:sw
7188
[ { "role": "assistant", "content": "Maseru ni mji mkuu wa Lesotho ikiwa na wakazi 174.000 Einwohner (2003).\nChuo Kikuu cha Lesotho na kiwanja cha kimataifa cha ndege ni karibu na mji. \nMaseru iko kwa mto Caledon (Mohokare). Ni mji mkubwa wa pekee nchini.\n\nHistoria \nIlikuwa kituo kidogo cha biashara ilip...
wiki:sw
7189
[ { "role": "assistant", "content": "Ndjamena ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa nchini Chad ikiwa na wakazi 1,093,492 mnamo mwaka 2013. \n\nNdani ya manisipaa kuna hara au mitaa kumi.\n\nJina \nZamani mji ulijulikana kwa jina la \"Fort Lamy\". Tangu mwaka 1973 jina limekuwa Ndjamena, N'Djaména, N'Djamena au N...
wiki:sw
7190
[ { "role": "assistant", "content": "Dakar ni mji mkuu wa Senegal ikiwa na wakazi 2,352,000. Iko kwenye rasi la Verde ambalo ni pembe la magharibi ya Afrika. Bandari yake ina nafasi nzuri kwa biashara na Ulaya na Amerika.\n\nMji ulianzishwa na Wafaransa mwaka 1857 walipoondoka kisiwa cha Goree kuhamia bara. U...
wiki:sw
7191
[ { "role": "assistant", "content": "Gorée (kwa Kifaransa: Île de Gorée) ni kisiwa cha Atlantiki mbele ya pwani ya Senegal na sehemu ya manisipaa ya Dakar. Ilijulikana kama kituo cha biashara ya watumwa. Hadi kukomeshwa kwa biashara hiyo mwaka 1848 watumwa walipelekwa kisiwani kutoka bara, kufungwa katika jel...
wiki:sw
7192
[ { "role": "assistant", "content": "Algiers (kwa Kiarabu مدينة الجزائر, madīnat al-djazā'ir, \"mji wa visiwa\"; kwa Kifaransa Alger) ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa wa nchi ya Algeria ikiwa na wakazi milioni 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni 5. Iko mwambaoni mwa bahari ya Mediteranea....
wiki:sw
7193
[ { "role": "assistant", "content": "Uturuki (Jamhuri ya Uturuki; kwa Kituruki: Türkiye Cumhuriyeti) ni nchi ya kimabara kati ya Asia na Ulaya. \n\nSehemu kubwa iko Asia ya magharibi lakini sehemu ndogo ya eneo lake upande wa magharibi wa Bosporus iko Ulaya.\n\nJiografia \n\nSehemu kubwa ya mipaka yake ni bah...
wiki:sw
7194
[ { "role": "assistant", "content": "Afrika ya Kaskazini ni kanda la kaskazini kwenye bara la Afrika.\nKwa kwaida nchi za Afrika kaskazini ya jangwa Sahara huhesabiwa kuwa Afrika ya Kaskazini. \n\nKanda la Afrika ya Kakazini ya UM lina nchi saba zifuatazo:\n<table><td valign=top>\n Algeria\n Misri\n Libya\n M...
wiki:sw
7195
[ { "role": "assistant", "content": "Eldoret ni mji ulio magharibi mwa Kenya. Upo kwenye barabara kuu kati ya Nairobi - Kampala takriban km 300 kutoka jiji la Nairobi katika nyanda za juu magharibi mwa Bonde la Ufa kwenye kimo cha mita 2100 - 2700 juu ya UB. \n\nUkiwa na wakazi 289,380 (wakati wa sensa ya mwa...
wiki:sw
7196
[ { "role": "assistant", "content": "Nakuru ni mji wa Kenya ambao ni makao makuu ya kaunti ya Nakuru. Ukiwa na wakazi 307,990 (sensa ya 2009) ni mji mkubwa wa nne nchini Kenya baada ya Nairobi, Mombasa na Kisumu. \n\nUko kwenye kimo cha m 1860 juu ya UB katika mashariki ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki kan...
wiki:sw
7197
[ { "role": "assistant", "content": "Afrika ya Magharibi ni ukanda wa magharibi kwenye bara la Afrika. \n\nKwa kawaida huhesabiwa humo nchi zilizo kati ya jangwa la Sahara na Bahari ya Atlantiki. Upande wa mashariki ukanda huu unaishia kwenye mstari kati ya mlima Kamerun na ziwa Chad.\n\nKatika lugha ya Kiara...
wiki:sw
7198
[ { "role": "assistant", "content": "Jamestown ni jina la miji mbalimbali duniani. Jina lilipendwa hasa kwa sababu \"James\" ni umbo la Kiingereza la jina \"Yakobo\" aliyekuwa mdogo wake Yesu.\n\nJamestown, Saint Helena — mji mkuu wa eneo hili\nJamestown, Ross-shire, Uskoti\nJamestown, Dunbartonshire, Uskoti\...
wiki:sw
7199
[ { "role": "assistant", "content": "Uskoti ni nchi ya Ulaya. Iko kaskazini mwa kisiwa cha Britania Kuu ikiwa sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini.\n\nJiografia \nUskoti ni theluthi ya kaskazini ya kisiwa cha Britania. Eneo lake ni km² 78,772. Upande wa kusini Uskoti umepakana na Uing...
wiki:sw