text
stringlengths
1
1.32k
alisema mtandao wa jinsia utaendelea kuipigania haki ya wanawake mahali popote ili kila mwanamke mtanzania awe na uhuru wa kutetea nafsi yake anapoona UNK
alisema UNK mahakama kuu kwa kufanya kazi yake bila kutetereka hivyo kutoa uamuzi wa ukweli katika kesi hiyo ya UNK dhidi ya serikali
mkurugenzi huyo alisema kupitia baraza hilo wanawake wengi watanufaika kwa kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao ikiwemo ushauri na mambo mengine
alisema ni jambo la kushukuru kwa mahakama kuruhusu baraza hilo kuendelea na kazi zake kwa kuwa wanawake wanahitaji msukumo ili waweze kujikwamua katika matatizo mbalimbali ukiwemo umasikini
bibi liundi alisema mahakama UNK haki na amewaomba wanawake wote wawe na imani wakati wa kufuatilia jambo bila kukata tamaa
watu saba wamefariki dunia na wengine kumi na tano kujeruhiwa vibaya baada ya lori la mizigo walilokuwa wakisafiria kutoka chunya kwenda mbeya mjini kupinduka
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya bwana advocate nyombi alisema tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji cha tete UNK wilayani chunya ambapo gari hilo lenye namba za usajili t mia nane na thebathini na nne UNK lililokuwa limebeba mahindi samaki na UNK UNK na kusababisha vifo hivyo
kamanda nyombi aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na UNK UNK ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari southern highland iliyopo jijini mbeya UNK UNK mkazi wa mbeya na UNK UNK mkazi wa mkwajuni chunya
wengine ni bwana pele UNK mtoto wa miezi saba rose simon bwana simon haule na mwanamke mmoja aliyetajwa kuwa mke wa UNK wote wakazi wa kijiji cha udinde wilayani chunya
waliojeruhiwa ni bwana patson UNK mwanafunzi wa sekondari ya shitete UNK mbeya vijijini
wengine ni patricia UNK patrick venance beatrice UNK celina UNK bibi juliana nestory wote wanafunzi wa shule ya sekondari ya southern highland iliyopo jijini mbeya
wengine ni bwana ombeni UNK mkazi wa wa tunduma bwana UNK UNK bibi rehema UNK mkazi wa udinde chunya bwana petro kimaro mfanyabiashara wa kiwira rungwe elizabeth UNK mkazi wa udinde chunya na bwana eric yohana mkazi wa UNK
majeruhi wengine ni bwana amon patson mkazi wa shitete UNK mbeya vijijini bwana UNK UNK mkazi wa udinde chunya
wote wamelazwa hospitali ya wilaya ya chunya
kamanda nyombi alisema dereva wa gari hilo alitoroka baada ya ajali hiyo polisi wanaendelea UNK
UNK siku ya pili bungeni
pinda UNK kamati ccm kuokoa
wabunge waapa UNK nyuma mustakabali wa bajeti ya wizara ya miundombinu iliyowasilishwa bungeni jumatano wiki hii na waziri wa wizara hiyo daktari shukuru kawambwa umezidi kuwa mashakani baada ya kugonga mwamba kwa siku ya pili na kushindwa kupitishwa
nuksi katika bajeti hiyo iliibuka kutoka na hoja ya sumu UNK na mbunge wa ilemela bwana anthony diallo akitaka kufanywa marekebisho makubwa kabla ya bajeti hiyo UNK
utata wa suala hilo ulizidi UNK jana baada ya naibu spika bibi anne makinda kutangazia bunge kwamba hoja hiyo imeahirishwa tena kuhitimishwa jana kama ilivyotarajiwa hadi leo asubuhi kutokana na serikali kuomba muda wa kuikamilisha kutokana na uzito wake
alisema baada ya serikali UNK na kamati ya miundombinu imeomba muda kulimaliza hivyo isingekuwa rahisi kuhitimishwa jana baada ya kipindi cha maswali na majibu kama ilivyopangwa na UNK bunge kwamba litakutana leo asubuhi kwa ajili ya hoja hiyo
wakati naibu spika akitoa taarifa hiyo habari kutoka ndani ya kikao kati ya serikali na kamati ya miundombinu UNK juzi jioni hadi usiku zilieleza kushindwa kufikia muafaka kutokana na kamati hiyo kukubaliana na hoja ya bwana diallo kuwa ni ya msingi kwa kuwa inazingatia taratibu zilizowekwa ambazo UNK na serikali
chanzo hicho kilieleza kwamba kutokana na hali kuwa tete kati ya serikali na kamati ya miundombinu iliyoonekana kuunga mkono hoja ya bwana diallo baada ya mbunge huyo kuitwa kwenye kamati hiyo kutoa maelezo ya kina yaliyoonekana kuwa na msingi wa taratibu zote zilizopo serikali UNK kutafuta njia ya kujinusuru kuhusu h...
moja ya njia ya kusaidia serikali hususan wizara ya miundombinu ni kuitisha kikao cha wabunge wote wa ccm kuwekana sawa na kupunguza ukali wa mambo fulani lakini hata tukienda kwenye kikao chetu hoja zipo palepale labda watu wabadilike lakini hali ilivyo sasa tunataka tanzania yenye neema na UNK kwa kukataa UNK
kilisema chanzo chetu ndani ya ccm UNK shughuli za bunge mchana bibi makinda alitangaza kuwepo kwa kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa ccm na kufuatiwa na kikao cha wabunge wote wa ccm jana usiku baada ya shughuli za bunge
akizungumza na majira mara baada ya kusitisha shughuli za bunge bibi makinda alisema ni jambo la kawaida kuwepo vikao hivyo na kukanusha kuhusishwa na bajeti ya wizara ya miundombinu
ni jambo la kawaida vyama kuwa na vikao na kabla ya kikao hicho UNK na kile cha kamati ya uongozi alisema bibi makinda akiwa anaelekea katika ukumbi wa pius msekwa tayari kuhudhuria kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa ccm kwa kawaida kikao cha kamati ya uongozi wa ccm ndicho UNK ajenda za kikao cha wabunge wote ...
akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum jana bwana dialo alisema alichofanya ni jambo la kawaida kwa bunge kwa kuwa UNK kufanyika hata mwaka elfu moja na mia tisa na tisini na saba na kuongeza kwamba bunge ni sehemu ya kufuata kanuni na taratibu na si eneo ambalo mtu anaweza kuchezea
alisema aliamua kuwasilisha hoja hiyo kama fundisho kwa mawaziri na baadhi ya watendaji wengine serikali UNK taifa pabaya kwa kujipendelea katika miradi ya maendeleo kwa kuwa jambo hilo linaweza kufikisha nchi pabaya
alipoulizwa kama maoni yake UNK kazi kama UNK alisema mimi UNK hoja kwa nia ya kutaka kushinda UNK ni ujumbe ufike na kutoa elimu kuwa kuna taratibu zinazotakiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa hili si mtu kujiamulia cha kufanya UNK
alipoulizwa uvumi kwamba barabara hizo zinahusishwa na ukanda kutokana na kupitia katika majimbo ya waziri wa fedha na uchumi bwana mustafa mkulo mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi daktari abdallah kigoda na hata daktari shukuru kawambwa alisema hawezi kuzungumzia hilo kwa kuwa na yeye anasikia tu uvumi huo
katika mapendelezo yake bwana dialo UNK shilingi bilioni thebathini saba UNK toka barabara za dumila kilosa handeni mkata hadi mkumba korogwe na kuelekezwa barabara za iringa dodoma kondoa hadi babati ambayo ni ya kimataifa
awali daktari kawambwa alielekeza jumla ya shilingi bilioni sitini na moja nne katika utengenezaji wa barabara za barabara dumila kilosa handeni mkata hadi mkumba korogwe katika kiwango cha lami huku barabara hizo UNK kuibukia mezani kwake kwa kuwa hazikwepo kwenye bajeti ya miaka iliyopita
makamu wa rais daktari ali mohamed shein amesema serikali haifurahii kuona bidhaa za tanzania zinaendelea kuuzwa nje ya nchi zikiwa ghafi hivyo kushindwa kuongezeka thamani
daktari shein alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua maonesho ya thebathini na tatu ya biashara ya kimataifa dar es salaam yanayofanyika katika viwanja vya mwalimu julius nyerere barabara ya kilwa
alisema hatua hiyo inafanya bidhaa za tanzania kuuzwa kwa bei ndogo ikilinganishwa na gharama za uzalishaji
mbali na kukabiliwa na changamoto hiyo daktari shein alisema tanzania bado inategemea mazao ya asilia kama chanzo kikuu cha mapato yake hali ambayo imeendelea kuathiri mapato ya serikali pindi bei ya mazao hayo inapoporomoka katika soko la dunia
daktari shein alisema maonesho kama ya sabasaba yanatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara wazalishaji na wawekezaji kujifunza kutoka kwa wenzao
kwa kujifunza ndipo mnaweza kuongeza thamani ya mazao yetu tunayozalisha na hata kutengeneza bidhaa zenye ubora unaokubalika katika soko la kimataifa na hatimaye kukabiliana na bei ya ushindani alisema daktari shein
alisema ili tanzania iweze kushiriki kikamilifu katika biashara ya kimataifa inahitaji kuimarisha masoko la ndani
alielezea kufurahishwa na maonesho ya mwaka kutokana na kuongeza kwa idadi ya wajasiriamali hasa wanawake
haya ni maendeleo yanayotia moyo hasa ikizingatia kuwa viwanda vidogo vina mchango mkubwa kwa sekta binafsi alisema
daktari shein alisema asilimia sabini ya nguvu kazi inatumika katika sekta binafsi kwa kuzalisha asilimia hamsini na nane ya pato la taifa
aliwataka wafanyabiashara wadogo kujiwekea mtandao wa masoko na kuimarisha ubora wa ufungashaji
daktari shein aliwataka wafanyabiashara kuchangamkia kuchangamkia kuuza bidhaa kwenye nchi zisizotoza ushuru india na japan
chadema tutashinda bila helkopta
mrema kifo cha kabuye kimeniacha UNK
makamba awataka wananchi wasirudie makosa leo wananchi wa jimbo la biharamulo magharibi mkoani kagera wanapiga kura kumchagua mbunge atakayeziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu phares kabuye
kampeni za kuwania kiti hicho UNK jana kwa vyama vya ccm chadema na tlp kufanya mikutano ya kampeni katika maeneo mbalimbali huku kila kimoja UNK kuibuka na ushindi
ushindani mkubwa unaonekana baina ya ccm na chadema huku chadema ikionekana kukubalika zaidi maeneo ya mijini na ccm maeno ya vijijini kama ilivyokuwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la busanda geita mkoani mwanza
maeneo ambayo chadema inaonekana kukubalika zaidi ni mjini biharamulo na kata ya lusahunga huku mwenyekiti wa tlp bwana augustino mrema akihitimisha rasmi kampeni za kumnadi mgombea wa chama chake bwana mpeka buhangaza juzi na kuwataka wananchi kumuezi marehemu kabuye kwa kumchagua mgombea wa chama chake kuwa mbunge w...
kifo cha kabuye kimeniacha mgumba sasa ninyi UNK mzee huyo mtakuwa UNK hebu UNK mgombea wa tlp ili UNK kipindi hiki UNK cha mwaka mmoja na nusu si mlikuwa UNK aongoze kwa miaka mitano
sasa mpeni buhangaza alisema bwana mrema
bwana mrema UNK kile alichodai vyama vya chadema na ccm kuvamia jimbo hilo huku UNK kuwa lilikuwa mikononi mwa tlp UNK hatua hiyo na tamaa ya fisi kwa vile tlp UNK mgombea kwenye majimbo UNK uchaguzi mdogo kwa lengo la UNK nafasi vyama UNK na wabunge wao
alisema tlp inajiandaa kusherehekea ushindi wakati kwa upande ccm ambayo imemsimamisha bwana oscar mukasa kuwania nafasi hiyo imetamba kuibuka na ushindi kama ilivyokuwa katika jimbo la busanda
akihitimisha kampeni za chama hicho katika viwanja vya soko jipya mjini biharamulo katibu mkuu wa ccm bwana yusuf makamba aliwataka wakazi wa jimbo hilo kutorudia kosa kama walilofanya mwaka ishirini sifuri tano ambapo jimbo hilo UNK na mgombea wa tlp marehemu kabuye
aliwaambia wakazi wa jimbo hilo kuwa wakichagua mgombea wa upinzani jimbo hilo litaendelea kusuasua kimaendeleo kwa kuwa mbunge huyo atakosa ushirikiano wa wabunge wengine wakiwemo viongozi wa serikali
mgombea wa ccm bwana mukasa aliwataka wakazi wa biharamulo kumchagua ili waweze kushirikiana kuibua fursa mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo
kwa upande wa chadema imewataka wakazi wa biharamulo kumchagua mgombea wake bwana mbasa gervas ili kuongeza nguvu bungeni za kupambana na vitendo vya ufisadi
katibu mkuu wa chama hicho daktari wilbroad slaa aliwataka wakazi wa biharamulo kutomchagua mgombea wa ccm kwa vile chama chake kimeshindwa kuwaondolea kero zinazowakabili watanzania
chama hicho UNK kampeni zake kwa kufanya mkutano mkubwa katika uwanja wa mpira wa biharamulo ambao ulihudhuriwa na mwenyekiti taifa bwana freeman mbowe na naibu katibu mkuu bwana zitto kabwe
pia alikuwepo aliyekuwa naibu katibu mkuu wa cuf aliyejiunga na chama hicho bwana wilfred lwakatare huku bwana mbowe akikaririwa akisema kuwa chama chake kina uhakika wa kuibuka na ushindi katika jimbo hilo bila kutumia UNK
wakati huo huo mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu lewis makame ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa kuzingatia maelekezo yatakayotolewa na tume
UNK vyama vya siasa kuheshimu sheria kanuni na maelekezo nec UNK vurugu siku ya uchaguzi kwa UNK wafuasi wao kwenda kinyume cha UNK alisema alisema vituo vyote vitakuwa wazi kuanzia saa moja asubuhi na vitafungwa saa kumi jioni ambapo kazi ya kuhesabu kura itaanza mara moja huku watu themanini na saba mia moja na them...
yawaagiza makatibu wa mikoa wasipuuze
maaskofu waunganana na serikali
wasema italeta mgongano wa kimaslahi tamko lililotolewa na baraza kuu la waislamu tanzania kupinga uamuzi wa serikali wa kukataa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi umewashutua viongozi wa chama cha mapinduzi na kulazimika kukesha wakijadili suala hilo
habari za kuaminika ambazo gazeti hili limezipata zimeeleza kuwa tangu juzi baadhi ya viongozi wa ccm walikuwa wakikutana mara kwa mara kujadili tamko hilo
kwa mujibu wa vyanzo vya gazeti hili viongozi hao wa ccm juzi walikuwa na mkutano wa kujadili msimamo wa bakwata uliotangazwa na mufti wa tanzania sheikh issa shabaan simba hadi usiku
viongozi hao walifikia hatua hiyo kwa kile wanachodai kuwa tamko hilo ni sumu kali kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
ili kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na tamko hilo la bakwata ccm imewaagiza makatibu wa mikoa na wilaya kutofanyia mzaha tamko hilo tamko hilo kwani linaweza kukikosesha ushindi chama hicho
viongozi wetu wameshutushwa zaidi na jambo hili hasa kutokana uamuzi huo wa serikali kujadiliwa kwenye misikiti mbalimbali kilisema chanzo hicho na kuongeza tumeona kuwa kama hatutajihami tunaweza kukutana na kipindi kigumu wakati uchaguzi
chanzo hicho kilisema ccm inahofia vyama vingine kutumia mwanya huo wa serikali wa kukataa kuanzisha mahakama ya kadhi kujinadi ili kujipatia kura kutoka kwa waislamu ambao hawakufurahishwa na hatua hiyo ya serikali
kwa muda mrefu mwenyekiti wa tanzania labour party bwana augustino mrema amekuwa akiitaka serikali ianzishe mahakama ya kadhi ambapo amekuwa akiungwa mkono na masheikh wa dini hiyo
bwana mrema aliwahi kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka serikali ianzishwe mahakama ya kadhi lakini hoja yake hiyo ilikwaa kisiki
chanzo chetu kimeeleza kuwa bwana mrema na viongozi wa vyama vingine wanaweza kutumia fursa hiyo kupindisha msimamo wa serikali kwa lengo la kujipatia kura ndiyo maana imeanza kujihami mapema iwezekanavyo
akizungumza na waadishi wa habari sheikh simba aliweka mabaya jinsi ambavyo bakwata haikufurahishwa na uamuzi uliotolewa na serikali wa kukataa kuanzishwa kwa mahakama hiyo nchini
wakati huo huo maaskofu nchini wameunga mkono uamuzi wa serikali wa kukataa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi wakidai suala hilo likikubaliwa linaweza kuleta mgongano wa kimaslahi baina ya wakristo na waislamu ndani ya nchi
wakati maaskofu wakiunga mkono uamuzi huo wa serikali tayari waislamu kupitia kamati kutetea haki za waislam wametangaza kuandamana siku ya ijumaa kupinga uamuzi huo
maskofu hao walisema uamuzi wa serikali wa kukataa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi utakuwa umezingatia maoni ya wananchi waliyotoa kwenye tume iliyoundwa baada ya kubaini mahakama hiyo haitakuwa na maslahi kwa taifa
askofu mkuu msaidizi wa jimbo kuu katoliki dar es salaam methodius kilain alisema msimamo wa serikali wa kukataa kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni mzuri kwa kuwa tanzania haina dini
alisema katiba ya jamhuri ya mungano wa tanzania ya mwaka elfu moja na mia tisa na sabini na saba inatoa uhuru wa kila mtu kuabudu dini apendayo pasipo kubuguziwa
askofu kilaini alisema waislamu kama wanataka wanaweza kuanzisha mahakama ya kadhi bila ya kuihusisha serikali
wana uhuru wa kuendesha mambo yao kwenye taasisi zao yanayoendana na masuala ya kiroho bila kuishirikisha serikali
sisi wakatoliki tunazo mahakama zetu kuanzia ngazi ya parokia jimbo hadi roma tunafanya mambo yetu bila ya kuingiliwa na serikali
alisema askofu kilaini
alisema waislamu hawajakatazwa kuanzisha mahakama ya kadhi bali kinachokataliwa ni mahakama hiyo kuwa na mkono wa serikali
alifafanua kuwa msimamo uliotolewa na waislam kuwa hawatachagua viongozi wa ccm ni sehemu ya uhuru wao wa kutoa mawazo
kwa nchi isiyofungamana na misingi ya dini kila mtu ana haki ya kufanya hivyo alisisitiza
askofu kilaini alisema hakuna sababu ya watu kuendelea kuhoji suala hilo kwa kuwa liliundiwa tume ya kukusanya maoni na uamuzi uliotangazwa ndiyo msimamo wa serikali
akizungumza na mjira jumapili kuhusu suala hilo askofu wa kanisa la africa inland churc charles salala alisema waislam hawana sababu ya kuichukia serikali kwa kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania inatamka wazi kuwa serikali haina dini
katiba ya nchi yetu imeweka bayana kuwa serikali haina dini hili ndilo chimbuko la amani tunayojivunia alisema askofu salala
alisema iwapo serikali ingekubali kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi nchi ingeelekea pabaya
ingekubalika kama nchi hii ingekuwa na dini moja lakini kwa mfumo tulionao wa dini nyingi ni vigumu kuwa na mahakama ya kadhi alisisitiza askofu salala
alisema hatua ya serikali kuikataa mahakama hiyo inalenga kutoonesha upendeleo kwa dini yoyote
alifafanua kuwa kama ingeanzishwa ingeendeshwa kwa fedha za walipa kodi wakiwemo wakristo na wapagani
wakristo na wapangani wasingekubali kuona fedha zao zinaendesha chombo ambacho hawanufaiki nacho alisema
alisema kama waislam wanahitaji kuwepo kwa mahakama ya kadhi wanaweza kuianzisha bila ya kuihusisha serikali kama inavyofanya kwenye masuala ya usuluhishi wa ndoa na mirathi
askofu salala alisema kitendo cha waislam kuahidi kutoipigia kura ccm kwa sababu ya serikali kukataa kuanzishwa kwa mahakama hiyo siyo cha kiungwana
naye askofu mkuu wa kanisa la anglikana tanzania daktari valentino mokiwa aliwataka mashekhe hao kutolinganisha msamaha wa kodi uliotolewa na serikali kwa taasisi za dini na mahakama ya kadhi kwani misamaha hiyo iko kwa pande za dini zote na hailengi kunufaisha upande mmoja