Datasets:

Modalities:
Text
Formats:
parquet
ArXiv:
Libraries:
Datasets
pandas
License:
Dataset Viewer
Auto-converted to Parquet Duplicate
text
stringlengths
1k
17.3k
label
int64
0
5
MAADHIMISHO ya Siku ya Nyuki duniani, yameanza kuadhimishwa kitaifa katika viwanja vya Nyerere Square jijini hapa huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Tuwalinde Nyuki’.Akizungumza katika mahojiano jana, Mkurugenzi Msaidizi Uendelezaji Ufugaji Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Allen Richard alisema hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya maadhimisho hayo .Alisema lengo ni kuhakikisha jamii inaweza kutambua umuhimu wa nyuki hasa kwenye suala la uchavushaji.“Tunataka wananchi watambue umuhimu wa nyuki katika usalama wa chakula , nyuki ni mdudu anayechavusha vizuri mazao,” alisema.Alisema tafiti zinaonesha asilimia 90 ya mazao yanachavushwa na nyuki na kwa sababu ya shughuli mbalimbali za binadamu, wanatumia viuatilifu kwenye mashamba nyuki, wanaweza kufa na siku za mbele kuna uwezekano wa kukosa makundi ya nyuki .“Kwa kuona hilo tuliona tuwe na siku ya nyuki ili kujenga uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa nyuki kwa ajili ya maisha ya binadamu,” alisema.Alisema wanaelimisha wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti, itakayotumiwa na nyuki kwa ajili ya chakula ili kumuenzi nyuki mwenyewe Richard alisema chimbuko la maadhimisho ya Siku ya Nyuki ni nchi ya Solvenia, ambapo Antonio Janser alikuwa akijishughulisha na ufugaji nyuki na alifanya hivyo baada ya kuona nyuki wanavyofanya kazi zao kwa juhudi na maarifa .Janser alizaliwa mwaka 1734 na alifariki dunia akiwa na miaka 39 baada ya kuugua.Ilipofika mwaka 2012 viongozi wa nchi ya Slovenia waliona ipo haja ya kuwa na Siku ya Nyuki duniani ili kuenzi mchango wa Janser, ndipo wakapeleka mapendekezo kwenye Umoja wa Mataifa na wakapendekeza Mei 20 iwe Siku ya Nyuki duniani.Alisema mwaka jana nchi nyingine zilianza kuadhimisha siku hiyo na Tanzania inafanya maadhimisho hayo kwa mara ya kwanza.Ofisa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Dodoma, Gakune Charles alisema maonesho hayo ni fursa kwa wajasiriamali, kutangaza bidhaa na shughuli wanazofanya.Mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho hayo, Abasi Abdallah alisema maonesho hayo yamempa hamasa ya kuanza ufugaji wa nyuki.
3
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema serikali ina uwezo kutatua changamoto zikiwemo za uchakavu wa majengo zinazokabili kituo cha matunzo ya watu wenye ulemavu wa ukoma na wazee wasiojiweza cha Chazi ,wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile ameyasema hayo baada ya kusomewa risala ya watu hao wanaokaa Kituo cha Chazi wilayani Mvomero.Dk Ndugulile alikuwa pia mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ambayo yalifanyika kitaifa Kitongoji cha Chazi, Kijiji cha Kigugu, wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro.“Nimebahatika kutembelea kituo cha matunzo ya watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza na nimekiona hali yake, nimeshatoa maelekezo ngazi ya Wilaya ya Mvomero juu ya ufuatiliaji wa karibu…pia nitatoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa wizara afike Chazi kuangalia changamoto za Kituo cha matunzo kwa watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza,” alisisitiza Naibu Waziri Dk Ndugulile.Alisema kuwa anaamini changamoto serikali ina uwezo wa kuzitatua ili kuwawezesha watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza waishi katika mazingira mazuri.Pamoja na changamoto hizo, Naibu Waziri huyo alifurahishwa kuona wazee wenye ulemavu wa ukoma wamejikita kwenye kilimo cha uzalishaji wa mazao ya chakula yakiwemo mahindi.Kutokana na juhudi hizo, alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuwapatia pembejeo za kilimo na wizara itasaidia.Katika risala yao iliyosomwa na mwakilishi wa watu wenye ulemavu wa ukoma kutoka kwenye kituo , Fikira Matumbi alisema mbali na kupongeza wadau kuwawezesha kuwa na vikundi vya ujasiriamali, bado wana changamoto ya kuishi kwenye majengo machakavu ambayo yalijengwa tangu mwaka 1957.Kwa mujibu wa risala hiyo, changamoto nyingine ni kukosa umeme, huduma ya maji na kushindwa kujimudu kimazingira na kuiomba serikali kuyakarabati majengo hayo na kutoa huduma nyingine.Waziri aliuagiza uongozi wa Wilaya ya Mvomero kufuatilia kiasi cha chakula kinachoingizwa na kutoka kwenye kituo hicho ili kuthibiti upotevu na udanganyifu wa chakula na fedha zinazotolewa na serikali.
3
IDADI ya vifo vya waendesha bodaboda nchini vitokanavyo na ajali imepungua katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu kinachoanzia Januari hadi Machi, ikilinganishwa na idadi ya vifo vya bodaboda kwa kipindi kama hicho kwa mwaka jana. Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Afande Deusi Sokoni akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu alisema kuwa idadi ya waendeshaji bodaboda waliopoteza maisha kwa mwaka huu ni 73 huku majeruhi wakiwa 121.Alisema, kwa mwaka jana kwa kipindi kama hicho waliopoteza maisha walikuwa ni 108 huku waliojeruhiwa ni 214. Sokoni aliongeza kuwa robo ya kwanza ya mwaka huu kwa upande wa waendesha baiskeli waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani walikuwa 23 idadi ambayo ni sawa na ya majeruhi lakini mwaka jana kuanzia Januari hadi Machi, idadi ya waliokufa ilikuwa ni 34 huku waliojeruhiwa wakiwa 30. Alisema pia waendesha mikokoteni tisa wamekufa na wanne wamejeruhiwa huku mwaka jana aliyekufa alikuwa mmoja na 12 walijeruhiwa. Kundi la watembea kwa miguu ambalo ni moja kati ya waathirika wakubwa wa ajali kwa mwaka huu wamekufa 90 na kujeruhiwa 106. Wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 163 na kujeruhiwa 179. Kwa upande wa abiria waliokufa kwa ajali kwa mwaka huu ni 108 na 393 wamekumbwa na majeraha mbalimbali wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 191 na majeruhi 575.
3
WALIMU 21 wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kuripoti kwenye vituo vya vipya vya kazi huku wengine wakiwa wamechukua posho ya kujikimu.Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Michael Magesa alibainisha hayo wakati alipokuwa akijibu hoja ya madiwani waliotaka kujua sababu ya walimu hao kusimamishwa kazi wakati shule nyingi katika halmashauri hiyo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu.Alisema sababu ya kusimamishwa kwa walimu hao ni kutekeleza hatua za awali za hatua za kinidhamu na kwamba tayari tume imeundwa kuchunguza jambo hilo ambapo uongozi wa halmashauri hiyo umeshahojiwa kuhusu hilo.Magesa alisema kuwa walimu hao walihamishwa na kupelekwa kwenye vituo vipya ambapo wote waliripoti kwenye vituo vipya na watano kati yao wameshalipwa fedha za kujikimu za uhamisho lakini tangu waripoti, hawajawahi kurudi tena kwenye vituo vya kazi kufundisha.Alisema walimu wengine waliripoti vituo vyao lakini malipo ya fedha za kujikimu yakachelewa hivyo wakagoma kufanya kazi na wengine walifanya vurugu wakafikishwa polisi na kuwasimamisha ni hatua za awali za kinidhamu wakati shauri lao likiendelea kusimamiwa na Tume ya Utumishi ya Walimu (TSD).Awali Diwani wa kata ya Bitale, Mathias Bwami alitaka kufahamu sababu ya idadi kubwa ya walimu waliosimamishwa kazi wakati halmashauri ina uhaba mkubwa wa walimu katika shule zake. Bwami alisema baadhi ya shule zilikuwa na walimu wa masomo ya hesabu na sayansi na kuwa sasa masomo hayo hayafundishwi na katika baadhi ya shule ikiwemo Mgawa sekondari ina mwalimu mmoja wa hesabu anayefundisha watoto 700 wa shule hiyo.
3
ALGIERS, ALGERIA MFANYABIASHARA na kiongozi wa upinzani nchini Algeria Rachid Nekkaz amekamatwa jana katika hospitali mjini Geneva, Uswisi baada ya kutaka kumfikia rais Abdelaziz Bouteflika anayepokea matibabu katika hospitali hiyo. Nekkaz anayetaka kuwania urais dhidi ya Bouteflika katika uchaguzi ujao nchini humo amesema alikwenda katika hospitali hiyo kutaka habari zaidi kuhusu Matibabu ya rais huyo mwenye umri wa miaka 82. Aliandaa maandamano madogo nje ya hospitali hiyo kabla ya kutaka kuingia ndani. Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Jean-Philippe Brandt ambaye aliviambia vyombo habari kuwa Rachid Nekkaz amekamatwa na jana hiyo alitarajiwa kukabidhiwa kwa mwendesha mashtaka. Rais Bouteflika, aliyeko madarakani tangu mwaka 1999, hajaonekana hadharani tangu alipougua kiharusi mwaka 2013. Azma yake ya kutaka kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa Algeria unaotarajiwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu imesababisha maandamano makubwa nchini humo yanayoongozwa na vijana wanaomtaka Bouteflika kuondoka madarakani.
2
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa takwimu za ukatili wa kijinsia kwa watoto huku akitaja ubakaji kuongoza kutokana na kuongezeka kila mwaka. Waziri Ummy ametoa majibu hayo kwa njia ya maandishi akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Ruge (Chadema), aliyetaka kujua mkakati wa serikali kudhibiti ubakaji. “Kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ulawiti na ubakaji kwa wanafunzi vinavyofanywa baina ya wanafunzi wenyewe kwa wenyewe au watu wa karibu katika familia, je, serikali ina mkakati gani wa dharura kudhibiti matendo hayo?,” ameohoji. Akijibu swali hilo Ummy amesema tatizo la ukatili wa kijinsia kwa watoto bado ni kubwa ambapo Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo mwaka 2017 matukio yalikuwa 13,457, mwaka 2018 matukio 14,419 na mwaka 2019 matukio 15,680. “Aidha, kwa mwaka 2019 vitendo vya ukatili vilivyoongoza ni Ubakaji (6,506), mimba za wanafunzi (2,830) na Ulawiti (1,405). “Mikakati ya serikali katika kukabiliana na ulawiti pamoja na ubakaji ni kutoa elimu kwa jamii kupitia watu mashuhuri, viongozi wa kisiasa, dini na mila ili kushiriki katika kubadilisha tabia na mienendo ya baadhi ya watu wanaoendeleza tabia za aina hiyo katika jamii kwa kuchukua hatua kali za kisheria kuwafikisha mahakamani wale wote wanaotenda makosa hayo ili haki itendeke kwa mujibu wa Sheria. “Pia kuna huduma za simu bila malipo kwa watoto ambayo inawezesha jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili,” amesema.
0
Ikiwa imebakia takribani miezi minne kueleka kwenye uchaguzi mkuu mwanamuziki Zuena Mohammed (Shilole) amesema kuwa anafikiria kwenda kugombea Ubunge kwenye jimbo la Igunga mkoani Tabora mambo yakikaa sawa. Akizungumza na kituo cha televisheni cha East Africa Shilole amesema anataka kuwapa wananchi kile ambacho yeye anaona kinakosena kwenye jimbo hilo kupitia tiketi ya chama chake cha CCM. “Nimefikiria na natumaini mambo yataenda, nipo vizuri kwenye mapambano, nataka niwe pale kwenye jimbo langu la Igunga, nataka niwape wananchi kile ambacho nataka, mimi ni mwaka huu, chama changu ni @ccm_tanzania” amesema. Shilole anakuwa mwanamuziki wa tatu kutangaza nia ya kugombe ubunge ikiwa ni baada ya Harmonize pamoja na Mwana FA wote kutangaza kuwa wanaweza kufikilia kugombea ubunge.   "Nimefikiria na natumaini mambo yataenda, nipo vizuri kwenye mapambano, nataka niwe pale kwenye jimbo langu la Igunga, nataka niwape wananchi kile ambacho nataka, mimi ni mwaka huu, chama changu ni @ccm_tanzania" @OfficialShilole kuhusu kugombea Ubungehttps://t.co/SZIqcCYlPV pic.twitter.com/sP9TZns95P — eastafricatv (@eastafricatv) June 18, 2020
1
WABUNGE wamesisitiza haja ya serikali kuboresha huduma za matibabu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kulinda maisha ya Watanzania hususani wa vijijini na wasio na uwezo.Kwa nyakati tofauti, wakichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kujenga miundombinu ya sekta ya afya ameonesha kuwa mazo zaidi utolewe kwenye kuboresha matibabu katika sehemu za kutolea huduma za afya. Baadaye jana wabunge walipitisha bajeti hiyo ya Wizara ya Afya.Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) amesema katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa ipasavyo kwa wananchi ni vyema serikali kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya.“Utaratibu kushirikisha serikali na watu binafsi utaratibu muhimu ambao unapaswa kuendelea kwa mapana yake. Pia tunapoboresha hospitali za serikali tusisahau umuhimu wa kuhakikisha kwamba zile ambazo tulikuwa nazo tunalinda uwezo wake kwa sababu tusije ikawa kama ule msemo wa ‘tusiwibie Paulo kumlipa Petro.’“Sina budi kusema kwamba hospitali siyo majengo ila ni huduma na katika hili, waziri pia aangalie hali halisi ya hospitali za Referal (rufaa), napongeza juhudi za serikali ya awamu ya nne iliyokamilisha Hospitali ya Mloganzila lakini hospitali hiyo ni hospitali majengo kwani hakuna hospital town pale kwa ajili ya madaktari kukaa karibu na hospitali,” aliongeza Profesa Tibaijuka.Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) aliwapongeza wauguzi na madaktari kwa kazi nzuri wanazofanya nchi nzima na kuomba wizara kusaidiana na Tamisemi kuwezesha hospitali ya wilaya ili kupunguza mzigo wa wagonjwa.
3
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewapongeza wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma kwa kuhakikisha wanatumia mashine za kielektroniki (EFDs) kila wafanyapo mauzo na kusema kuwa mfano wao unapaswa kuigwa.Meneja msaidizi anayesimamia madeni na makusanyo ya TRA mkoani hapa, Jeremia Maunde alisema hayo mwisoni mwa wiki. Alikuwa katika operesheni maalumu ya maofisa wa TRA kukagua na kuona kama mashine hizo zinatumiwa na wafanyabiashara kwa usahihi.Alisema katika operesheni yao katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamebaini wafanyabiashara waliokaguliwa wenye maduka walikuwa wanatumia mashine hizo na akawapongeza kwani ni hatua inayosaidia kukusanya kodi.Hata hivyo, alisema, TRA haijafikia lengo la kuongeza ukusanyaji mapato kwani bado wapo wafanyabiashara kadhaa hawana machine hizo. Alisema wanawaelimisha matumizi ya mashine hizo na watakaokutwa hawana machine bila sababu za msingi watachukuliwa hatua kali.Kwa upande wao, wafanyabiashara wa mjini Kigoma wameitaka TRA kutofanya kazi kama Polisi badala yake kukaa na wafanyabiashara kuwaelimisha changamoto zinazojitokeza za kuharibika kwa mashine na taarifa zinazotoka.Mmoja wa wafanyabiashara, Pamela Otonde alisema utoaji wa risiti za EFD unasaidia pia kuweka mahesabu ma makadirio ya kodi vizuri. Alitaka hamasa itolewe kwa wafanyabiashara hao badala ya kuwakamata na kuwalipisha faini.Naye Asajile Mwakalambile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kyusa General Traders ya mjini Kigoma alisema kitendo cha watumishi wa TRA kuwafikia wafanyabiashara na kuzungumza nao kinaongeza ushirikiano katika utendaji kazi wao. Alisema pia kinasaidia kuuliza maswali ambayo yanasaidia katika uendeshaji wa shughuli zao.
3
Ofisa Mwandamizi Mkuu Elimu wa TRA, Hamis Lupenja alisema hayo wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyofanyika jijini hapa mwishoni mwa wiki.“Vituo vya mafuta hawatoi risiti za TRA licha ya baadhi yao kuwa mashine za EFD’s, katika kukabiliana na hilo utaratibu wa kufunga kifaa cha kodi ndani ya pampu ili kuondoa ukwepaji kodi unafanyika,” alisema.Alisema mashine za kielektroniki (EFD’s), sio mali ya TRA, bali ni mali ya mfanyabiashara, lakini taarifa za kodi za TRA zipo ndani hivyo wanapoziweka pembeni na kuacha kuzitumia ni njia mojawapo ya kukwepa kodi, ndio maana Serikali inafanya utaratibu mwingine.Alisema ili kutatua tatizo la upatikanaji wa mashine hizo, TRA imeongeza idadi ya watengenezaji wa mashine kutoka wanne hadi kufikia nane na idadi ya wasambazaji, imeongezeka kutoka sita hadi 10.Kwa mujibu wa Lupenja, walifanya utafiti juu ya matumizi ya mashine hizo, ambapo baadhi ya wafanyabiashara walikiri kuwa mfumo wa mashine za EFD’s upo wazi na ni rahisi kujikadiria, kutunza kumbukumbu na kupunguza wizi.Alitaja aina ya mashine hizo kuwa ni pamoja na Rejesta ya Kodi, ambazo hutumika kwa wafanyabiashara wa rejareja wanaotoa risiti kwa maandishi ya mkono ambayo huhamishika.Nyingine ni Printa za Kodi za Kielektroniki, ambazo hutumia umeme na mashine ya alama ya kodi ambayo hutumiwa na kampuni zinazotoa hati za madai.
5
MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji mstaafu Dk Steven Bwana amesema bado kuna watumishi wa umma ambao hawana maadili na amewataka kujirudi, kujisahihisha na kujirekebisha haraka.Aidha amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa wakati wote wanapotekeleza majukumu yao, na viongozi wasisite kuchukua hatua stahiki pale watumishi walio chini yao wanapofanya makosa na kutenda kinyume na maadili ya kazi na ya taaluma zao. Dk Bwana aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana na kusisitiza kuwa viongozi na watumishi wa umma wanapaswa pia kutambua kuwa wana kazi kubwa ya kuboresha utumishi wa umma nchini. “Bado kuna matatizo kwenye halmashauri zetu, wizara na taasisi za umma.Kupitia vikao vya kisheria tunavyokaa Tume tunaona bado kuna baadhi ya watumishi wa umma si waadilifu na hawana maadili hivyo wanapaswa kujirudi, kujisahihisha, kujirekebisha na wafanye kazi zao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu, miongozo iliyopo na maelekezo halali yanayotolewa na viongozi wao,” alisema. Akizungumzia ubora katika utoaji wa huduma kwa wananchi, Dk Bwana ameipongeza serikali kwa hatua mbalimbali inazozichukua kuhakikisha kunakuwepo na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na jitihada zinazofanyika za kuwaletea maendeleo Watanzania.“Wakati haya yanafanyika, tuna kazi kubwa ya kuboresha utumishi wa umma, wapo baadhi watalalamika kuhusu hatua zinazochukuliwa. Watailalamikia serikali na watailalamikia Tume ya Utumishi wa Umma, lakini tunapaswa sote tuungane, watumishi wa umma na Watanzania, nchi hii ni yetu sote. “Tutambue na kuamua tunaijenga, tunaiboresha ama tunaibomoa. Tutambue hakuna njia ya mkato kufikia maendeleo na kila mmoja wetu na kwa nafasi yake anapaswa kuchapa kazi, ni sisi wenyewe tusingoje kupata wawekezaji wa kuja kutuletea maendeleo.Tunapokosea, tukubali tumekosea na tujisahihishe,” alisema. Aliwataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa watumishi wao mara kwa mara kwa lengo la kukumbushana wajibu wao na nini matarajio ya waajiri na serikali kwa ujumla. Vile vile alisema, waajiri ni muhimu wakatoa mafunzo kwa watumishi kabla ya kuanza kazi, kwa waajiriwa wapya ili kuwaelimisha kuhusu maadili ya kazi, miiko na misingi ya majukumu ya kazi mbalimbali yanazokwenda kuzitekekeza, wajue wanatakiwa kufanya kazi zao kwa uadilifu, kutumia weledi na pia kuwa wazalendo.
3
Yanga ilianza ligi kwa kishindo Jumapili baada ya kuishinda Coastal Union ya Tanga kwa mabao 2-0 na hivyo kukalia usukani wa ligi hiyo, wakati Prisons ilipoteza mechi yake ya kwanza dhidi ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo leo inatafuta ushindi wa kwanza kwenye ligi hiyo.Kocha wa Prisons, Salum Mayanga aliliambia gazeti hili jana kuwa ana imani timu yake itapata matokeo mazuri licha ya kukiri kuwa mechi hiyo haitakuwa nyepesi.“Mechi itakuwa ngumu kama unavyojua Yanga ndio mabingwa watetezi hawatakubali kupoteza mchezo kirahisi, lakini nimeiandaa timu yangu baada ya kufanyia kazi makosa yaliyotokea kwenye mechi ya kwanza,” alisema kocha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.Hata hivyo, mara nyingi Prisons imekuwa ikipata tabu kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga katika miaka ya karibuni. Yanga ndio inaongoza msimamo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya kwanza, hivyo leo inawania kuendeleza ushindi ili iendelee kukaa kileleni.Akizungumzia mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm alisema hana wasiwasi na wachezaji wake.“Kwanza nashukuru nimeshinda mechi ya kwanza, lengo langu kuendeleza ushindi katika mechi zote zinazofuata… sikatai ushindani lazima uwepo sababu kila timu imejiandaa kushinda,” alisema kocha huyo Mholanzi.Mbali na mechi hiyo ya Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba inaendelea kuwa ugenini dhidi ya Mgambo Shooting. Simba ilishinda bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi uwanjani hapo dhidi ya African Sports matokeo ambayo kocha wake, Dylan Kerr ametamba kuyaendeleza.Kerr aliiongoza Simba kwa mara ya kwanza kwenye ligi mwishoni mwa wiki iliyopita na kutamba kuwa timu yake inao uwezo wa kushinda katika kila mechi. Kerr amekuwa akisema anataka kushinda mechi zote mbili za ugenini Tanga ili kuwapa wachezaji wake kujiamini.“Ukishinda mechi ya kwanza ya pili na ya tatu timu inazoea kushinda na wachezaji wanajenga kujiamini katika mechi zinazofuata mpaka kutwaa ubingwa kila siku naamini hivyo,” alisema kocha huyo Muingereza. Mgambo ilianza ligi kwa sare dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara.Majimaji baada ya kuifunga JKT Ruvu bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi, leo itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.Mechi hiyo haitarajiwi kuwa nyepesi kwani kama Majimaji inatambia uwanja wake wa nyumbani, wapinzani wao Kagera Sugar walishinda bao 1-0 ugenini Sokoine dhidi ya Mbeya City hivyo si ajabu hata leo ikitamba ugenini.Mbeya City na JKT Ruvu zitacheza Sokoine leo huku kila moja ikiwania ushindi wa kwanza baada ya kupoteza mechi za ufunguzi.Kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga, Stand United itamenyana dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC huku Toto African ikimenyana na Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Ndanda ikiikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limebaini kuwepo kwa vitendo vya wanafamilia wa soka Tanzania kujihusisha na masuala ya siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira yenye nembo za klabu na wadhamini wa Ligi.Ikinukuu Katiba ya TFF Ibara ya I (4), taarifa ya shirikisho hilo jana ilieleza: “TFF inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na sare za michezo zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa Stars au za washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.“Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa. “Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya Katiba za TFF na FIFA.”Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepokea maombi ya Klabu ya Young Africans (Yanga) ya kutaka kufanya uchaguzi wake mkuu.“TFF imeiomba klabu hiyo kufanya mkutano wake wa uchaguzi wa viongozi baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Rais, Wabunge na Madiwani) utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
4
WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (pichani) amewaasa watumishi wa ofi si yake kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma katika utendaji kazi wao.Mhagama alitoa kauli hiyo jijini hapa wakati akifungua kikao cha kwanza cha mwaka cha Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo na kuwataka watendaji wote kuona umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa weledi huku wakizingatia sheria za utumishi wa umma.“Ni lazima mtumishi wa umma afanane na kanuni na sheria za kiutumishi kwa kuwa na maadili mazuri awapo kazini na nje ya kazi ili kujipatia sifa njema kuanzia muonekano hadi tabia kwa ujumla…”Mhagama pia aliwakumbusha watendaji wa ofisi hiyo kuzingatia nafasi zao za kiutendaji wawapo kazini kwa kuzingatia jukumu la ofisi yake ni kuratibu shughuli zote za serikali hivyo lazima iwe ofisi ya mfano.“Ofisi yetu inaratibu shughuli zote za serikali, muone ni kwa namna gani sisi ni viungo kwa serikali hii hivyo mtumie fursa ya baraza hili kukumbushana wajibu wetu kwa kuhakikisha mnatekeleza majukumu kwa nidhamu ya hali ya juu sana.”Mhagama pia aliutaka uongozi kuendelea kuwa na umoja na kufanya kazi kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji ili kujenga tija kwa kupitia vikao ambavyo vitaibua changamoto zinazowakabili pamoja na kuishauri vyema serikali kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu.Alisema kuwa ni muhimu viongozi wote kuanzia ngazi ya Vitengo, Idara na Taasisi zote kuendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu kwa kufuata sheria, miongozo na kanuni za utumishi wa umma huku wakiwa na upendo kati yao.Naye, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Tixon Nzunda aliahidi kutekeleza maagizo na maelekezo yaliyotolewa, ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili mazuri na kuahidi kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo juu ya utoaji wa huduma bora inayozingatia viwango vya hali ya juu.
3
BUENOS AIRES, ARGENTINA TIMU ya Taifa ya Argentina, ipo hatarini kukosa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi baada ya mchezo wao wa juzi wa kuwania kufuzu kutoka suluhu dhidi ya wapinzani wao Peru. Kwa hatua waliyofikia, Argentina wanahitaji kushinda mchezo mmoja uliobaki ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki, lakini wakishindwa kufanya hivyo basi wataingia kwenye historia mpya kwa mara ya kwanza kutoshiriki michuano hiyo tangu mwaka 1970. Bara la Amerika ya Kusini timu tano zinatakiwa kufuzu Kombe la Dunia, tayari kuna baadhi ya timu ambazo zimeanza kuonesha dalili ya kufuzu ikiwa ni pamoja na Brazil ambao wanaongoza wakiwa na pointi 38, wakifuatiwa na Uruguay wenye pointi 28, Chile pointi 26, Colombia pointi 26 na Peru wakiwa na pointi 25. Hata hivyo, Argentina wana pointi 25, jambo ambalo linawapa wakati mgumu wa kufuzu kwa kuwa wanalingana pointi na wapinzani wao Peru, lakini wapinzani mwingine ambao wanakutana na Argentina ni Paraguay wenye pointi 24, hivyo kama watashinda mchezo unaofuata na Argentina wakapoteza pamoja na Peru, basi Paraguay watakuwa wanafuzu huku wapinzani hao wakibaki. Argentina wanaweza kuishangaza dunia endapo watashindwa kufuzu Kombe la Dunia, ikiwa miaka mitatu iliyopita katika fainali zilizofanyika nchini Brazil walifanikiwa kufika fainali dhidi ya Ujerumani. Katika mchezo huo wa juzi, mshambuliaji wa timu hiyo, Lionel Messi, alijaribu kupambana kuhakikisha wanapata ushindi, lakini mambo yalikuwa magumu japokuwa shuti lake lilikwenda kugonga mwamba na kutoka nje. Baada ya mchezo huo kumalizika, wachezaji wa Argentina walionekana kukata tamaa wakitoka nje na vichwa wameinamisha chini, lakini bado mashabiki wao walionekana kuwa na imani na mchezo wa mwisho wiki ijayo dhidi ya Ecuador, mchezo huo Argentina watalazimika washinde ili kujihakikishia kufuzu. Timu nyingine ambazo zimejihakikishia kufuzu ni pamoja na mabingwa watetezi Ujerumani baada ya kuwachapa wapinzani wao, Ireland Kaskazini mabao 3-1 mjini Belfast. Timu nyingine ni England baada ya kuichapa Slovenia bao 1-0, lililowekwa wavuni na nahodha ambaye ni mshambuliaji wao, Harry Kane, katika dakika ya 90.
4
Na TUNU NASSOR–DAR ES SALAM MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, ameonya tabia ya unyanyasaji dhidi ya wajane unaofanywa na baadhi ya wanafamilia pindi mume anapofariki. Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa ibada  ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Ukonga, marehemu Leornad Lukala iliyofanyika katika Mtaa wa Mongolandege. Alisema hivi sasa familia nyingi zimekuwa na dhana potofu ya kuwanyanyasa wajane huku ndugu wa familia wakidiriki kuwadhulumu mali jambo ambalo huwafanya kuishi katika  mazingira magumu na upweke. Mwita alisema jambo hilo halikubaliki wala kuvumilika katika jamii ya kitanzania na hivyo kumtaka kila mmoja kuchukua tahadhari . “Kumekuwa na tabia ya watu kunyanyasa wajane, hawa watu walioondokewa na wenzi wao …familia zimekuwa na sauti badala ya mfiwa, wanadhulumu mali, jambo linalosababisha kuongezeka kwa kesi za mirathi mahakamani.  “Niwaombe sana, wajane wasitengwe, wapewe huduma zao kama ilivyokuwa awali, msifanye watu hawa wakajutia kubaki duniani, msitumie nafasi zenu kuwadhalilisha, wapeni huduma kama wengine,” alisema Mwita. Alisema kuwa dhuruma na kuwatenga wajane ni jambo ambalo limekuwa likiwatesa na kusababisha kushitaki. Katika hatua nyingine Meya Isaya, aliwataka viongozi mbalimbali waliopewa nafasi za kuhudumia wananchi wanapaswa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuacha alama pindi wanapomaliza muda wao. “Naomba sana viongoziambao tumepata nafasi za kuwatumikia wananchi, iwe ni kwenye sekta ya dini, kisiasa, serikalini, na sehemu nyingine, tujitahidi kutekeleza majukumu yetu kikamilifu ili tunapoondoka duniani tuache kumbukumbukwa vizazi vijavyo,” alisema. Mchungaji Lukala alifariki dunia juzi alipokuwa akipelekwa kwenye kituo cha afya cha Mongolandege ambapo atazikwa leo kijijini kwao Mwanalumango Kisarawe mkoani Pwani.
3
Na SAM BAHARI -SHINYANGA MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kishapu na Wilaya ya Kishapu Sulei- man Masoud (Nchambi) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga na kusomewa mashitaka 12 ya uhujumu Uchumi. Akisoma Mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahaka- ma ya Wilaya ya Shinyanga, Ushindi Swalo Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Magreth Ndawala alisema mtuhumiwa anakabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu Uchumi. Mwendesha Mashitaka Ndawala alisema kati ya Mashitaka 12 yanayomkabili mtuhumi- wa Nchambi ni pamoja na kupatikana na silaha 10 na risasi 536 akizimiliki kinyume cha sheria. Mwendesha Mashitaka Ndawala alisema, tuhuma nyingine ni mtuhumiwa kupatikana na nyama mbalimbali za wanyama pori kiny- ume na sheria, na taratibu za nchi. Mwendesha Mashitaka, Magreth Ndawa- la alikuwa akisaidiana na Waendesha Mashi- taka wa Serikali wengine Michael Jairo na Castory Mwenda. Wakili wa upande wa mtuhumiwa, Frank Mwalongo hakupata nafasi ya kujibu hoja yoy- ote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi za uhujumu uchumi. Mbunge huyo Nchambi alikamatwa na Polisi nyumbani kwake Mei 3, mwaka huu na kupatikana na silaha 16 na risasi 536 na nyama za wanyama pori. Kesi ya mbunge huyo iliahirishwa na itata- jwa tena katika Mahakama hiyo Jumatatu Mei 11, mwaka huu.
3
Na FLORENCE SANAWA-MTWARA ZAIDI ya wanafunzi 513 wa Shule ya Msingi Mbae iliyopo Manispaa  ya Mtwara Mikindani, wanatumia matundu mawili ya choo. Akizungumza na MTANZANIA shuleni hapo  wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye majengo ya vyoo vipya 10, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Josephat Mussa, alisema tatizo hilo linaweza kuwasababisha uwepo wa magonjwa ya milipuko kwa wanafunzi hao. Ujenzi wa vyoo hivyo unafadhiliwa na Shirika la Woman for Vision la mjini hapa. “Shule yetu ilianza mwaka 2015 na ina darasa la awali, darasa la kwanza, la pili na la tatu na hadi sasa tuna madarasa matatu. “Pamoja na kwamba wanafunzi wanasomea katika mazingira magumu, walimu nao wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira ya aina hiyo kwa sababu hatuna ofisi na badala yake tunakaa chini ya miti katika kipindi chote tunachokuwa shuleni hapa. “Yaani, hata hapa nilipo chini ya mti ndipo ilipo ofisi ya mwalimu mkuu na wakati huu wa msimu wa korosho, usishangae kuona korosho zinanidondokea. “Kibaya zaidi, wakati mwingine unapokuwa kwenye maandalizi ya kipindi, nyoka anadondoka chini, yaani tuko katika hatari ya hali ya juu. “Pamoja na shida hizo, sasa tumeona madiwani na mkurugenzi wa halmashauri, wamejitahidi kwa kiasi kikubwa tumepata matundu 10 mapya ya choo na pia tumepata ufadhili mwingine wametujengea mengine 10, lakini hatuna ofisi na tuna upungufu wa madarasa manane,” alisema Mussa. Naye Mwenyekiti wa Shirika la Woman for Vision, Adelina Kalumuna, alisema kutokana na uhitaji mkubwa wa matundu ya vyoo katika shule nyingi katika manispaa hiyo, wamelazimika kuanza ujenzi wa matundu 20 ya vyoo katika Shule ya Msingi Mbae na Shule ya Msingi Maendeleo ambazo zilionekana kuwa na uhitaji mkubwa. Akiweka jiwe la msingi  katika vyoo vya shule hizo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, alisema shule hizo ni moja ya shule zenye changamoto nyingi za miundombinu ikiwamo vyoo.
3
Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM                                                      JUMLA ya wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisaha viungo na makovu katika kambi maaalum ya upasuaji iliyofanyika kwa siku tatu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila. Upasuaji huo ambao umefanywa na wataalamu wa Hospitali ya Mloganzila kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka Korea Kusini Prof Jeong Tae Kim ulihusisha  wagonjwa ambo wameathirika na majanga ya moto, ajali za barabarni pamoja na watoto waliozaliwa wakiwa na hitilafu kwenye viungo. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru alimshukuru Prof Kim kwa kujitoa kwake kuja nchini kushirikiana na wataalamu  wa ndani kwa lengo la kutoa huduma na pia kubadilishana ujuzi  ili kuendelea kutoa huduma bora za kibingwa . Prof. Museru alisema lengo la hospitali ni kuendelea kuboresha huduma  za kibingwa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa wa kutibiwa  nje ya nchi. Awali Daktari Mbobezi wa Upasuaji wa kurekebisha viungo katika Hospitali ya Mloganzila  Dk. Laurian Rwanyuma alisema hii ni mara ya kwanza upasuajia huo kufanyika hospitalini hapo  tangu ilipozinduliwa rasmi na serikali.
3
KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema, kilichowafanya wapoteze mchezo wao mbele ya Lipuli FC ni wapinzani wao hao kuwazidi uwezo hivyo mbinu zao zote walizozitumia hazikufanya kazi.Yanga walifungwa mabao 2-0 na Lipuli katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, FA, uliopigwa katika Uwanja wa Samora, Iringa juzi. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo, kocha huyo raia wa DR Congo, alisema kuwa hakutarajia kama atakutana na upinzani mkali kama ule licha ya kuwajua Lipuli ni moja kati ya timu ngumu nchini.Alisema kuwa mbinu alizoingia nazo aliamini kabisa zitawapa ushindi lakini kadiri muda ulivyozidi kusogea akaona wanapata wakati mgumu na kumlazimu kuzibadili. Alifafanua kuwa alifanya mabadiliko ya mfumo kwa kuwatoa Ibrahim Ajib, Haji Mwinyi na Mohammed Issa ‘Banka’ na kuwaingiza Amis Tambwe, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Juma Abdul lakini bado mambo yakawa magumu.“Niliona Lipuli ni wagumu kufungika ndio maana nilimuingiza Tambwe, Juma na Ninja nikamtoa Ajib, Mwinyi na Banka ili kufanya tupandishe mashambulizi na kushambulia kwa kasi, tutumie mipira ya krosi kupata mabao lakini ikashindikana,” alisema Zahera. Kwa upande wa Kocha wa Lipuli, Seleman Matola alisema kuwa kilichowasaidia kupata ushindi katika mchezo huo ni kuzisoma mapema mbinu za Yanga.Alisema kuwa walifanikiwa kuwadhibiti kila upande na kuutawala mchezo na kama wachezaji wake wangeongeza umakini wangeweza kupata mabao zaidi ya mawili lakini akawashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya kuipeleka timu fainali kwa mara ya kwanza. “Hii ni zawadi ya mashabiki wa Lipuli pamoja na watu wa Iringa kwa ujumla, tulitengeneza nafasi nyingi za kupata mabao lakini tukafanikiwa kufunga mawili, kwakuwa tumeenda fainali hayo tuliyoyapata yanatosha.
4
NA KOMBO ALI KOMBO, ZANZIBAR MASHABIKI wa timu ya Simba visiwani hapa wameanza kufurahishwa na viwango vya nyota wao wapya, Paul Kiongera na Hijja Ungando, wakidai wametengeneza kombinesheni nzuri. Ungando na Kiongera, aliyekuwa kwa mkopo KCB ya Kenya, wameanza kufanya vizuri kwenye maandalizi ya Simba kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi hii. Akizungumza mara baada ya mazoezi ya jana, mmoja wa mashabiki hao aliyekataa kutajwa jina gazetini, alisema pacha ya wawili hao itawasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yao msimu huu, wakiungana na kinara wa mabao, Hamis Kiiza, aliyefunga nane. “Kwa sasa yeyote aje, kwani tumetimia, tuko vizuri, imani yangu tutafika mbali, Ungando ni kijana hatari sana na ukiwatizama pamoja na Kiongera ni mapacha wapya watakaotusaidia sana ndani ya timu yetu ya Simba,” alisema. Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, katika mazoezi ya jana alionekana kuwanoa zaidi washambuliaji, hasa Kiongera na Hijja, ambao kwa sasa ni kama pacha iliyokubalika zaidi visiwani hapa. Kiongera tokea ameondoka Simba akipelekwa kwa mkopo KCB, ameonyesha kiwango kikubwa sana, akifunga mabao 11 msimu uliopita wa ligi hiyo, akizidiwa mabao 11 na staa aliyeongoza, Jesse Were wa Tusker. Katika mazoezi hayo, ilishuhudiwa kiungo Awadh Juma, akishindwa kufanya mazoezi kutokana na kusumbuliwa na malaria, vilevile mshambuliaji kinda, Alex Masawe naye aliumia bega baada ya kuanguka, akiwa katika harakati za kufunga bao. Masawe ambaye anawania namba ya kupandishwa kwenye timu kubwa ya Simba, ameumia ikiwa ni siku yake ya kwanza tu kufanya mazoezi na kikosi hicho baada ya kuwasili visiwani Zanzibar tokea juzi.
4
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), leo vinatarajiwa kutoa msimamo  endapo vitashiriki uchaguzi mdogo wa majimbo matatu Januari mwakani. Vyama hivyo vitatu ni Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, Majimbo hayo   ni   Songea Mjini (Ruvuma), Singida Kaskazini (Singida) na Longido mkoani Arusha. Taarifa za awali ambazo MTANZANIA ilizipata zilieleza kuwa vyama hivyo vinatafakari kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo kwa kile vinachodai kuwa demokrasia inaminywa. Kwa mujibu wa taarifa hizo,   vyama hivyo vya upinzani vilisononeshwa na uchaguzi  wa marudio wa madiwani uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita kwa kile vilichodai  ulitawaliwa na ubabe wa polisi. Katika taarifa yake   jana, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema vyama hivyo vitazungumza   na   waandishi wa habari kujadili mustakabali wa masuala muhimu ndani ya nchi hususan mwenendo wa siasa. Hata hivyo, mkutano huo ambao ulipangwa kufanyika jana katika hoteli ya Colosseum   Oysterbay,   Dar es Salaam, uliahirishwa ghafla. Hiyo ni mara ya pili kuahirishwa  mkutano na waandishi wa habari.  Juzi Chadema ilitoa mwaliko kwa vyombo vya habari kwamba kingetoa taarifa kuhusiana na maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichomalizika hivi karibuni. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu aliwaambia waandishi wa habari  waliofika katika hoteli hiyo kwa ajili ya mkutano huo jana  kuwa mkutano hulo uliahirisha kwa kuwa majadiliano yalikuwa hayajakamilika. “Tunaomba mtuwie radhi, kuna maazimio ambayo tuliyafikia lakini kuna wenzetu wamechelewa hatujawa-brief, hivyo muda huu tunarudi kwenye kikao ili tuwa-brief. “Tukisema muondoke halafu mrudi baadaye tutakuwa tunawasumbua, tunaomba tukutane kesho (leo) kwa ajili ya mkutano huo,”alisema Mwalimu.    
3
Akizungumza katika uzinduzi wa kitengo hicho jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, John Lwande alisema benki hiyo imekuwa ikifanya jitihada za kuanzisha huduma mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma zake kwa wateja.“Kuanzishwa kwa kitengo hiki ni moja ya hatua kubwa zilizofikiwa na ACB katika mwendelezo wa kuboresha huduma zake kwa wateja kwa haraka iwezekanavyo na kutafutia ufumbuzi matatizo mbalimbali yanayotokana na ACB Mobile na ATM” alisema.Aidha, alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo, kunatokana na mkakati wa benki hiyo wa kuwajali wateja wake sambamba na kuwavutia kwa kuwa wanaamini kuwa bila wateja hakuna benki.“Hili linajidhihirisha wazi katika utafiti uliofanywa mwaka jana na taasisi ya ukaguzi wa mahesabu ya KPMG ambao ulihusisha taasisi mbalimbali za kifedha kutoka nchi 14 barani Afrika ambapo ACB ilishika nafasi ya kwanza kwa kuwa benki inayotoa huduma kwa gharama nafuu na kwa upande wa huduma kwa wateja ilishika nafasi ya tatu,” alisema.Alisema kupitia huduma hiyo wateja wa ACB, watapata fursa ya kupiga simu moja kwa moja kupitia namba 0655 202011 na 0755 202011 bila malipo.Lwande alisema kitengo hicho kitaendelea kufanyiwa maboresho kwa ajili ya kupanua huduma zake ili kiweze kutoa msaada katika huduma nyingine ikiwemo mikopo na amana.Alisema benki hiyo imekuwa ikifanya mambo mbalimbali yakusaidia jamii ikiwemo kugharimia mafunzo ya wajasiriamali sambamba na kutoa misaada kwenye hospitali na kwa watu wasiojiweza.
5
SERIKALI imeiagiza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatilia kwa kina sakata la kushikiliwa kwa ndege ya serikali iliyoikodisha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Airbus 220-300 ikiwa nchini Afrika Kusini.Ndege hiyo ikiwa na abiria 83 kwa amri ya Mahakama ya Gauteng ya nchini humo, inashikiliwa tangu juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimaitaifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, na ilizuiwa kuruka kurejea Dar es Salaam.Kutokana na tukio hilo, juzi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi), Dk Leonard Chamuriho alitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikimkunuu Waziri wa wizara hiyo, Isack Kamwelwe akiomba radhi abiria waliokuwapo kwenye ndege kwa kushindwa kufanya safari hiyo.Kamwelwe amesema kwa kuwa sakata hilo limehusisha mhimili wa mahakama wa Afrika Kusini, ni dhahiri kuwa linapaswa kufuatiliwa kisheria zaidi hasa ikizingatiwa kuwa yeye kama mwakilishi wa serikali hawezi moja kwa moja kuingilia mhimili huo wa mahakama.Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema abiria hao 83 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wameshaunganishwa na mashirika mengine ya ndege na kurejea nchini salama.Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi amewataka wananchi kutulia wakati suala hilo likifuatiliwa kwa ukaribu zaidi huku akiwataka wananchi kungojea hatma kwa AG.
3
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amezitaka taasisi za umma na sekta binafsi kujitathmini ni kwa namna gani wataifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Alisema maendeleo ya viwanda nchini ambayo yatasaidia kufikia uchumi wa kati yatachochewa na utekelezaji wa mradi wa Kaizen unaosimamiwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kwa lengo la kuboresha viwanda na kutoa mbinu za kukuza ubora wa bidhaa zinazozalishwa ili kuongeza faida.Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri katika kutelekeza mradi huo jana jijini Dar es Salaam alisema kuwa mradi huo umesaidia kubadilisha tabia za wafanyakazi ikiwemo kuthamini muda, kuweka mazingira bora maeneo ya kazi na kupanga bidhaa katika mtiririko unaofaa.Kakunda alisema kuwa imebaki miaka saba ili kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati na wa viwanda na kwamba kama wafanyakazi wataendelea na hali zao, itakuwa ndoto kufikia malengo yaliyopangwa.“’Tunafahamu kwamba mradi huu unakamilika mwakani lakini tunaomba muendelee kuutekeleza hapa nchini ili kuongeza chachu ya mabadiliko katika maeneo ya kazi kwani umelea manufaa mengi ikiwemo wafanyakazi kujali muda na kutambua umuhimu wa kazi,” alisema Kakunda.Alisisitiza kuwa ni lazima taasisi zote za binafsi na umma kutekeleza mradi huo kwa sababu unasaidia katika kudhibiti fedha, muda na vifaa vya kazi pamoja na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka ili kuongeza uzalishaji na kuleta faida.Waziri huyo alisema Kitengo cha Kaizen Tanzania (TKU), kitaongezewa uwezo wa kufikia wafanyabiashara wengi na wenye viwanda, kukuza uzalishaji na kuongeza tija ya bidhaa zao na kwamba kufanya hivyo kutaleta matokeo chanya ya uchumi na maendeleo ya viwanda.‘’Kaizen sio kwa wenye viwanda na wafanyabiashara tu kinachotakiwa ni kuhakikisha taasisi za serikali zinatumia mfumo wa Sasambua, Seti, Safisha, Sanifisha pamoja na Shikilia (5S-KAIZEN) na sio kila taasisi kutekeleza kivyake,’’ alifafanua.Kwa mujibu wa Kakunda, taasisi wanazofanya nazo kazi ni Benki za Biashara, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Serikali za Mitaa, Wakala wa Usalama Mahali pa kazi (OSHA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (Tirdo), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Wakala wa Vipimo (WMA) na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).Waziri huyo alieleza kuwa ili kuboresha mazingira bora ya kufanyia biashara na kupunguza vikwazo wamekubaliana kuwa na chombo kimoja kitakachosimamia masuala yote ili kupunguza gharama za uzalishaji.Hata hivyo amesema bei za uzalishaji za Tanzania ni kubwa kwa sababu ya kuwepo kwa tozo zaidi ya 30 kwa mfanyabiashara moja kwa sababu kila taasisi inataka kutoza kodi hivyo bila kuondoa vikwazo hivyo, gharama za uzalishaji zitaongezeka.Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Shinichi Goto alisema kuwa kutokana na Tanzania kujiandaa kuwa na uchumi imara wa kati waliamua kuja na mradi huo wa Kaizen kwa ajili ya kuongeza uzalishaji
5
Michuano hiyo inayojulikana pia kama Kombe la FA imeingia hatua ya robo fainali, ambapo Jumamosi iliyopita timu ya Mwadui iliifunga Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mabao 3-0 na kufuzu nusu fainali.Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga itacheza Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ikiwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara, wakati Azam FC itakuwa Uwanja wa Azam Chamazi kuivaa Prisons.Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) linatarajiwa kuendelea Alhamisi kwa michezo miwili kuchezwa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Mechi zote zinatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu, huku kila timu ikipania kushinda na kufuzu nusu fainali.Bingwa wa michuano hiyo atawakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) mwaka 2017.Yanga na Azam pia zitatumia michezo hiyo kama maandalizi yao kwa ajili ya mechi za kimataifa mwishoni mwa wiki ijayo, ambapo Azam itacheza na Esperance ya Tunisia na Yanga itacheza na Al Ahly ya Misri.Pia mechi ya leo ni maandalizi ya michezo ya viporo vya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Yanga na Azam zitacheza kuanzia Jumamosi wiki hii. Robo fainali nyingine ya michuano hiyo itakuwa Aprili 9 mwaka huu, wakati Simba itakapokuwa mwenyeji wa Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
4
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imelieleza Bunge kuwa, inaanzisha kambi mpya za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maeneo mbalimbali kwa awamu.Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hussein Mwinyi amesema, Serikali inatambua hitaji kubwa la kuanzisha kambi za JKT kwenye mikoa na wilaya zisizo na kambi hizo."Jeshi la Kujenga Taifa limeelekeza nguvu kwenye vikosi ambavyo vilivyoanzishwa awali na baadaye kusitisha shughuli za kuchukua vijana mwaka 1994" amesema Dk. Mwinyi.Wabunge wameelezwa kwamba, hivi sasa JKT imejikita katika kutoa mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana walkiojiunga na jeshi hilo kwa kujitolea."Lengo ni kuwa endapo vijana hawa watakosa ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama waweze kuajiriwa na taasisi nyingine za Serikali, sekta binafsi au wajiajiri wenyewe" amesema.Waziri Mwinyi ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa.Amesema, vijana wanaopata fursa ya kujiunga na JKT kwa kujitolea ni wachache kulinganisha na mahitaji ameahidi kulifanyia kazi wazo la Mbunge huyo kuanzisha miradi isiyohitaji uwekezaji mkubwa na kuwashirikisha vijana wasio na ajira kwenye maeneo yasiyo na  kambi za JKT.
3
NEW YORK KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na Waziri Mkuu wa Jamaica, Andrew Holness wameitisha mkutano wa pamoja na viongozi wa dunia, Mashirika ya Kimataifa katika mpango jumuishi wa kukabiliana na madhara ya kibinadamu na kiuchumi ya Covid-19. Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha viongozi wa nchi na serikali zaidi ya 50 na ni muhimu wa kusaka suluhu ya fedha kwa maendeleo ya kukabili Covid-19. Vilevile utaangazia maeneo sita muhimu ya kufanyia kazi ili kuhamasisha uchangishaji unaohitajika kukabiliana na kupata unafuu.  Maeneo hayo yanajumuisha kutanua uwezo wa ununuzi katika uchumi wa dunia, kukabiliana na madeni yaliyopindukia, kuzuia mtiririko wa wa fedha haramu, kuongeza uwekezaji ili kujikuza zaidi ndani na kutengeneza ajira na kuunda mfumo wa mataifa kuimarika kwa haraka zaidi, kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, kukabili mabadiliko ya tabia nchi na kurejesha ulinganifu kati ya uchumi na asili.  “Janga hili limeonyesha wazi tulivo katika hali tete, tupo katika janga la kibinadamu lisilo la kawaida kutokana na virusi visivyoonekana kwa macho tunahitajika kukabiliana nalo kwa umoja na ushirikiano na jambo muhimu la mshikamano ni msaada wa kifedha,”alisema Katibu Mkuu wa UN.  Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness, alisema: “Janga hili la Covid-19 linatuhitaji kwamba tuchukue hatua za haraka kukabiliana na madhara yake kwenye uchumi wa mataifa yote, katika kila ukanda wa dunia na kila hatua ya maendeleo,”. Aidha Holness alisema anakubaliana na maeneo yote sita muhimu yaliyoangaziwa kuwa yenye umuhimu wa kutazama, kutanua uwezo wa ununuzi katika uchumi wa dunia hususani kwa mataifa ya kipato cha chini na cha kati.  Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, alisema: “Mataifa yote duniani yameguswa na janga la Covid-19 na hata kutishia kudidimiza hatua ya maendeleo iliyokuwa imefikiwa. “Tunajua njia bora ya kuwasaidia watu wetu na kujenga upya uchumi ni kwa kushirikiana kama jumuiya ya kimataifa, tunahitajika kusaidia hatua jumuishi na za mmoja mmoja kuwezesha unafuu wa ujumla, ustahimilivu wa kudumu ambapo hakuna wa kuachwa nyuma.”  MAENEO 6 MUHIMU YA KUANGAZIWA  Maeneo sita muhimu za kuzingatia ni hitaji la kujenga ukwasi katika uchumi wa dunia na kudumisha uimara wa kifedha na kulinda faida za maendeleo.  Pili ni haja ya kushughulikia uelemewaji wa madeni kwa nchi zote zinazoendelea kuokoa maisha kwa mabilioni ya watu ulimwenguni.  Tatu ni haja ya kuunda mfumo ambao wadau wa sekta binafsi wanaweza kushiriki kikamilifu katika suluhisho bora na kwa wakati unaofaa.  Nne, juhudi za awali za kuongeza uwekezaji na malipo ya ukuaji wa pamoja na kutengeneza nafasi za ajira.  Tano, hatua za kuongeza matumizi sahihi ya fedha na kukuza uhamasishaji wa rasilimali za ndani kwa kuzuia mtiririko wa fedha haramu.  Sita, kuhakikisha ahueni endelevu inapatikana kwa umoja kwa kuambatanisha Sera na Malengo ya Maendeleo Endelevu.  Takwimu za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) zinaonesha kuwa tayari ugonjwa wa Covid-19 umechukua maisha ya watu 34,0000 na zaidi ya visa milioni 5.4 vimeripotiwa duniani. Endapo hatua haitachukuliwwa UN imetabiri kuwa huenda ukapoteza karibu Dola za Kimarekani Trilioni 8.5 kutoka katika uchumi wa dunia katika kipindi cha miaka miwili ijayo, huku ukiwaacha watu milioni 34 katika umasikini wa kupindukia kwa mwaka huu na wengine zaidi ya milioni 130 kwenye huu muongo.  Kuanguka kwa biashara tayari kumeshaanza kusababisha watu kupoteza ajira zao, Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) limesema huenda makadirio ya muda wa kufanya kazi katika robo ya pili ya mwaka 2020 itakuwa asilimia 10.5 chini zaidi ya kabla ya janga ambalo ni sawa sawa na kazi za kudumu milioni 305. Hata kabla ya mlipuko wa janga hili, karibu nusu ya nchi zote zinazoendelea na nyingine zenye uchumi duni zilikaribia au kulemewa kabisa kwa madeni.  Gharama za ulipaji wa deni kwa nchi hizo umeongezeka kwa zaidi ya mara mbili kati ya 2000 na 2019, hadi kufikia asilimia 13 ya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya asilimia 40 katika robo ya nchi zote zinazoendelea za visiwa kidogo (SIDS). 
2
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ameshindwa kufi ka kijiji cha Iwondo kutokana na ubovu wa barabara uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha huku msafara wake ukikwama mara kwa mara.Msafara wa Dk Mahenge ulikwama zaidi ya mara tano na mara kadhaa kusimama ili kunasua magari yaliyokwama na safari kuendelea.Hata hivyo, ulipofika kijiji cha Igoji kilomita 115 kutoka Mpwapwa Mjini huku ikiwa zimebaki kilomita nane kufika kijiji cha Iwondo hali ya barabara ilikuwa mbaya zaidi na ziara hiyo kukwama kuendelea.Wakizungumzia ubovu wa barabara, Kahaga Yusuph alisema hali hiyo ya barabara ni mbaya na inayowapa wakati mgumu hasa wanapokuwa na wagonjwa na wanataka kuwafikisha hospitalini.“Hapa ukiwa na mjamzito unataka kumuwahisha hospitali ni shida sana, barabara ni mbaya, ni mashimo matupu hata kupanda pikipiki ni shida kubwa,” alisema.Alisema kutokana na ubovu wa barabara magari yanayokwenda Mpwapwa yamekuwa yakipita saa sita badala ya asubuhi.Mkazi mwingine, Sospeter Malogo amesema kutokana na ubovu wa barabara safari zimekuwa zikichukua muda mrefu na kutolea mfano kufika eneo la umbali wa kilomita tano unatumia wastani wa saa mbili hadi tatu.“Serikali ifanyie marekebisho hali za barabara ni mbaya kutoka Mima kwenda Chitemo, Igoji na Iwondo. Mkazi wa kijiji cha Berege, aliyejitambulisha kwa jina la Kedmond Luseko alisema ubovu wa barabara kutoka Mpwapwa kwenda Berege, Mima, Igoji, Isalaza umekuwa ukiwapa shida wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kufika shuleni .Alisema kutokana na mvua hizo miundombinu mingi ya shule kama vyoo na madarasa kwa baadhi ya maeneo vimebomoka.“Hii barababara ni mbovu haijafanyiwa ukarabati kwa miaka mitano au sita sasa, tunamuomba Rais John Magufuli atusaidie katika hili.” alisema.Akizungumzia changamoto hiyo ya ubovu wa barabara, Dk Mahenge alisema amejionea hali halisi .“ Kutokana na hali mbaya ya barabara wananchi katika kipindi hiki hawana muungano wa shughuli za kijamii na kiuchumi kwa sababu ya ubovu wa barabara,” alieleza.Alisema baadhi ya maeneo wananchi wameanza kuvuna mahindi na viazi wanahitaji kufikisha sokoni kwa wakati ili mazao hayo yasiharibike. Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema, baadhi ya barabara zitafanyiwa ikarabati hivi karibuni ili kuwaondolea adha wananchi.
3
Na MOHAMED KASSARA TIMU ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, imejikuta ikiangukia pua na kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cape Verde katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa Afrika (Afcon) uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, jijini Praia. Kipigo hicho kimezidi kufifisha ndoto ya Tanzania kufuzu fainali za Afcon zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon. Stars itarudiana na Cape Verde keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars itaingia katika mchezo huo, ikiwa haina cha kupoteza kwani itahitaji kushambulia zaidi ili kupata ushindi wa kuiweka pazuri katika msimamo wa kundi lake. Matokeo hayo yaliifanya Stars kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi L, ikiwa na pointi mbili, huku Cape Verde ikifikisha pointi nne na kupanda hadi nafasi ya pili. Stars tayari imecheza michezo mitatu bila kupata ushindi, ikianza kwa sare ya bao 1-1 na Lesotho, Uwanja wa Azam Complex,  Dar es Salaam, suluhu dhidi ya Uganda, Uwanja wa Nelson Mandela jijini Kampala, kabla ya juzi kuchapwa mabao 3-0 na Cape Verde. Hadi sasa kikosi cha Stars ndicho kilichoruhusu mabao mengi katika kundi hilo, ambapo imepigwa mabao manne huku yenyewe ikifunga bao moja. Kwa maana hiyo, Stars itahitaji kushinda michezo yake mitatu iliyosalia kwenye kundi hilo ili kufufua upya matumaini ya kufuzu kwa fainali hizo ambazo kwa mara ya mwisho ilishiriki mwaka 1980. Ilipoangukia Stars Katika mchezo wa juzi, Stars iliangushwa na mambo mengi lakini kubwa ni plani ya mchezo na kukosekana kwa umakini. Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, aliamua kuingia na mpango wa kujilinda zaidi na kushambulia kwa tahadhari ili kupata angalau pointi moja katika mchezo huo. Mpango huo ulilenga kuhakikisha timu yake inapata ushindi kupitia mashambulizi ya kushtukiza, lakini kama hawatafanikiwa basi wasipoteze mchezo. Amunike aliingia na mpango huo kwa kuwa alikuwa ugenini. Mfumo huo ulimsaidia kuanza kazi yake vizuri kwa kupata pointi moja katika mchezo mgumu dhidi ya Uganda. Kocha huyo raia wa Nigeria, alianzisha kikosi kile kile kilichompa pointi moja kule Uganda. Lakini kutokana na kutowafahamu vizuri wachezaji wa timu pinzani katika mchezo wa juzi, plani yake ilijikuta ikishindwa kumpa matokeo chanya. Mpango huo wa kujilinda ulifanikiwa katika mchezo wa awali kutokana na wachezaji wa Tanzania na Uganda kufahamiana hivyo ilikuwa rahisi kuwadhibiti wapinzani hao. Katika mchezo dhidi ya Cape Verde, kikosi cha Stars kilikuwa na sura mpya moja. Waliosalia walikuwa wale wale walioanza dhidi ya Uganda. Katika mchezo huo alikosekana kiungo, Frank Domayo, ambaye nafasi yake ilizibwa na Himid Mao. Ukiangalia mchezo uliopita, Stars japo ilijilinda lakini ilikuwa inamiliki mpira na kutengeneza mashambulizi kuelekea lango la Uganda, tofauti na ilivyokuwa Cape Verde. Katika mchezo wa Cape Verde ilicheza kwa tahadhari ya juu hali iliyowapa mwaya Cape kutawala maeneo yote na kutengeneza mashambulizi yaliyowapa mabao mawili ya haraka. Hii inaonyesha Amunike na benchi lake hawakupata muda wa kutosha kuitazama Cape Verde, ndiyo maana aliingia na mpango huo kutokana na kuiheshimu zaidi. Kitaalamu unapokuwa unawapa nafasi wapinzani wako kukaa na mpira kwa muda mrefu unatoa nafasi pia kwako kupoteza umakini hivyo kufanya makosa, kwa vile muda mwingi utakuwa unakimbia kuutafuta mpira. Hili lilidhihirika pale Stars ilipofungwa bao la kwanza, ambapo mfungaji aligusa mpira mara kadhaa kabla ya kufunga bila mabeki watatu wa Stars kuondoa mpira huo katika eneo la hatari. Stars ilikuwa na wachezaji wengi kwenye eneo lao la ulinzi, lakini walikuwa wanakosa umakini na kuruhusu wapinzani wao kupenyeza mipira iliyokuwa na madhara. Mfumo wa kujilinda uliwanyima uhuru  Mbwana Samatta na Simon Msuva,  kusukuma mashambulizi langoni mwa Cape Verde kutokana na kukosa mipira kutoka kwa viungo ambao walikuwa bize kukaba. Hali hiyo ilimfanya Samatta kutokuwa na madhara kwenye lango la Cape Verde kwa kuwa alikuwa analazimika kushuka chini kwenda kuchukua mpira na kutumia nguvu nyingi kuisogeza mbele, lakini hata hivyo alikuwa akikosa msaada kutoka kwa Msuva na Thomas Ulimwengu. Akizungumza baada ya mchezo huo, Amunike alikiri wachezaji wake walikosa umakini na kuruhusu bao rahisi dakika 20 za mwanzo. “Tulipoteza mchezo katika kipindi cha kwanza kwa sababu tulishindwa  kutimiza majukumu yetu kama timu, naamini bado tuna nafasi ya kujisahihisha katika mchezo ujao nyumbani, kundi bado liko wazi, kwa kuwa tukishinda Jumanne tutafikisha pointi tano, inaumiza kupoteza, lakini tunapaswa kujifunza kutokana na makosa,” alisema.
4
Yanga itacheza na Al Ahly Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 9 mwaka huu, lakini Yanga ikitakiwa kucheza mechi tatu za viporo vya Ligi Kuu ndani ya siku 11, jambo ambalo Pluijm ameliita ni kuwachosha wachezaji wake.Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema ratiba hiyo mpya imevuruga mipango yake ya kuongeza umakini katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly.“Nilikuwa na programu za mazoezi ambazo nilikuwa nimeziandaa kwa ajili ya mchezo wetu na Al Ahly, lakini kwa ratiba hii ni kama imeharibika kwa sababu mechi za viporo tunazocheza ni ngumu ambazo tulazimika kucheza kwa nguvu ili kupata ushindi, lakini nyingine ni za mikoani hivyo inatubidi kusafiri,” alisema Pluijm.Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema kwa kiasi kikubwa ratiba hiyo haikuzingatia ushiriki wao kwenye michuano ya Afrika na imewapa wakati mgumu kujipanga.Alisema kutokana na ratiba hiyo wanalazimika kufanya mazoezi mara moja kwa siku ili kuwapa muda wa kutosha wachezaji wao waweze kupumzika, ili kupata nguvu za kupambana kikamilifu katika mechi zijazo.Katika marekebisho yaliyotangazwa juzi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara yanaonesha kuwa Yanga itaanza mechi zake za viporo Aprili 3 kwa kuikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na siku tatu baadaye itacheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja huo huo.
4
NEW YORK, MAREKANI  BIFU la mwanamitindo Blac Chyna na familia ya Kardashian, haliwezi kwisha baada ya mrembo huyo kuionya familia hiyo kutotumia jina la mtoto wake Dream katika kipindi chao cha runginga cha Keeping Up With The Kardashians. Blac alipata mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili sasa wakati yupo kwenye uhusiano na Rob Kardashian, lakini baada ya kuachana mrembo huyo amekuwa na mgogoro na familia ya Rob kwa madai kijana wao hatoe huduma kwa mtoto huyo. Hata hivyo Kim, Khloe, Kylie wamekuwa wakimzungumzia mtoto huyo wa kaka yao kwa namna tofauti, lakini Blac alianza kumuona Rob kuwa, aiambie familia yake iachane na mpango wa kumzungumzia mtoto wake. Inasemekana kuwa Blac na yeye anataka kuwa na kipindi chake cha runinga ambacho kitakuwa kinajulikana kwa jina la The Real Blac Chyna, hivyo hayupo tayari kuona mtoto wake akizungumziwa kwenye vipindi vingine. “Vipindi vingine vinafanya vizuri kutokana na kutaja majina ya watu, Keeping Up With The Kardashians sitaki kuona wakimzungumzia mwanangu,” alisema Blac.
1
NA ZAINAB IDDY, LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/17 unaoshirikisha timu 16, tayari umeanza kutimua vumbi tangu mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa sasa hivi mchezaji mmoja mmoja au timu kwa ujumla wapo katika vita ya kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita. Kwenye ligi iliyopita tuliona jinsi kulivyokuwa na upinzani wa mchezaji mmoja mmoja kiasi cha kuzua maswali mengi kwa wadau juu ya nani atatwaa tuzo mwishoni mwa msimu. Miongoni mwa waliong’ara ni wachezaji wazawa ambao licha ya ushindani ulioonekana baina yao na wageni lakini waliweza kuonyesha kiwango bora, swali ni je, msimu huu watatisha tena? Juma Mahadhi Hakuna asiyejua uwezo wa Mahadhi akiwa uwanjani, licha ya muda mfupi alijiunga na Yanga na kuichezea mechi mbili za kimataifa za Kombe la Shirikisho. Mahadhi amejiunga na Yanga akitokea Coastal Union ya mjini Tanga, baada ya kuonesha uwezo mzuri na kuwa mwiba kwa wapinzani licha ya timu hiyo kushuka daraja. Ubora wake uwanjani ulipelekea kuzigonganisha timu za Simba na Yanga katika usajili, lakini mwisho akaangukia mikononi mwa Wanajangwani waliomfunga miaka miwili kwa dau la milioni 35. Tayari amewateka mashabiki wa timu hiyo, kutokana na uwezo alioonyesha kwenye michezo miwili ya Yanga, akianza na ule wa TP Mazembe kabla ya Medeama, kwa sasa anaaminika kwenye kikosi cha Yanga lakini je, ataweza kung’ara kama ilivyokuwa Coastal Union msimu uliopita katika ligi hii? Shiza Kichuya Kiungo mpya mshambuliaji wa Simba, aliyejiunga na timu hiyo katika kipindi hiki cha usajili akitokea Mtibwa Sugar. Msimu uliopita Kichuya aling’ara katika ligi na mashindano ya mapinduzi, jambo ambalo limemwezesha kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi kwenye ligi ya msimu uliopita. Mbali na kupata tuzo hiyo, kiwango chake kiliweza pia kumpa nafasi ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioingia katika kinyang’anyiro cha uchezaji bora wa msimu na ule wa mchezaji bora chipukizi ambazo hakubahatika kupata. Licha ya kutopata tuzo kutoka kwa wadhamini wa ligi, bado Simba wamemsajili ili kupata huduma yake, kikosi ambacho kinaushindani mkubwa na Yanga. Mudhamir Yasini Kiungo mpya wa Wekundu wa Msimbazi, amejiunga katika kikosi hicho hivi karibuni baada ya kuonesha kiwango bora katika ligi iliyopita. Mudhamir amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar, lakini akitarajiwa kukutana na changamoto kubwa ya namba hususani kutoka kwa Jonas Mkude. Hassan Ramadhan Beki huyo wa kulia wa Yanga anaupinzani mkali na Juma Abdul ambaye wanacheza namba moja. Kessy amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba alikoitumikia kwa kipindi cha miezi 17 kati ya 18 aliyopewa. Beki huyo ambaye ni zao la Mtibwa Sugar, alilazimika kuitumikia Simba kutomaliza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo baada ya kusimamishwa kwenye michezo mitano ya mwisho ya ligi kutokana na kumchezea vibaya Edward Christopher wa Toto iliyopelekea apewe kadi nyekundu. Licha ya kuingia mgogoro na Simba ambao umesababisha kutoitumikia Yanga kwa muda, lakini uwezo wake haujifichi na ndicho kilichowashawishi Wanajangwani kumsajili, lakini swali ni kwamba ataweza kumweka benchi Abdul na kuyaendeleza makali yake? Juma Abdul Alistahili kupewa tuzo cha uchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, kutokana na juhudi zake alizozionyesha katika kuhakikisha timu yake ya Yanga inapata mafanikio. Abdul ambaye amewabwaga Kichuya na Tshabalala katika tuzo hizo, ameiwezesha timu yake kutwaa ubingwa wa ligi, kombe la TFF lakini pia kutinga hatua ya makundi kwenye michuano ya kimataifa ya Shirikisho. Katika ligi iliyopita, Abdul aliteuliwa pia kuwa mchezaji bora wa Aprili na kutwaa kitita cha Sh milioni moja baada ya kuwashinda Donald Ngoma kutoka Yanga na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu. Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ Msimu wa 2015/16, ulikuwa wa mafanikio kwa beki huyo wa Simba baada ya kujinyakulia tuzo tatu tofauti zilizotokana na ligi. Katika ligi iliyopita, Tshabalala alionekana kutokuwa na mpinzani wa kudumu ndani ya Simba na hivyo kuweza kuitumikia vilivyo hadi kuiwezesha kumaliza ikiwa kwenye nafasi ya tatu. Kinda huyo aliyetengenezwa na Wekundu wa Msimbazi chini ya kocha Seleman Matola, alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi  Oktoba kwa timu yake, lakini pia amefanikiwa kutwaa ile ya msimu mzima baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa Simba. Kiwango kizuri cha Tshabalala kimemwezesha pia  kuingia kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa msimu pamoja na mchezaji bora chipukizi ambacho amepata tuzo yake. Bado mashabiki wa Simba wanamwamini kijana wao kuwa ana nafasi ya kuisaidia timu hiyo, lakini usajili uliofanywa kipindi hiki cha usajili unaweza kumweka katika wakati mgumu wa kuendelea kuwa kwenye ubora wake wa msimu uliopita. Farid Mussa Licha ya kutopata tuzo yoyote msimu uliopita, Farid ni moja ya wachezaji walioweza kuonyesha kiwango kizuri uwanjani msimu huo. Farid aliingia katika kinyang’anyiro cha mchezaji bora chipukizi na wadau wengi walionekana kutupa karata kwake lakini hali ikawa kinyume baada ya kwenda kwa Tshabalala. Kupewa tuzo hiyo Tshabalala kuliwafanya wanamichezo wengi hususani wa soka kupaza sauti zao wakidai kuwa hakustahiki, hii inaonyesha ni jinsi gani uwezo wa Farid uliweza kuonekana na wengi. Licha ya changamoto hiyo, bado ana nafasi ya kujituma na kutwaa tuzo zaidi ya hiyo, licha ya kuonekana huenda atakata tamaa. Mbali nawachezaji hao wapo pia Deogratius Munishi ‘Dida’  (Yanga), Miraji Adamu (alikuwa Coastal), Hassan Hatibu (Toto African msimu uliopita), Ibrahim Ajib (Simba), Aishi Manula na Shomari Kapombe (Azam FC).
4
BODI ya Ligi Kuu Tanzania imezipa muda klabu zinazowakilisha nchi kimataifa Simba na Mtibwa kujiandaa na michezo yao ya raundi inayofuata ili kufanya vizuri zaidi.Timu hizo zilizofanya vizuri katika michezo iliyopita ya Ligi ya mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika tayari zimerejea Dar es Salaam juzi. Katika michezo ijayo Simba inatarajiwa kusafiri kwenda Kitwe, Zambia kwa ajili ya mchezo dhidi ya Nkana ya huko utakaochezwa kati ya Desemba 14 na 16 kisha kurudiana Dar es Salaam kati ya Desemba 21 na 23 tarehe ambazo Mtibwa pia, itacheza na KCCA ya Uganda.Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugenzi wa Bodi ya ligi Boniface Wambura alisema muda uliobaki kwa timu hizo kucheza michezo hiyo ni mdogo hivyo wameona wasiwachanganye na badala yake kuwapa muda kisha wakirudi katika michezo ya kwanza watacheza michezo ya ligi. “Simba na Mtibwa hazitakuwa na mechi, tumewapa muda wa kujipanga katika michezo yao ya kimataifa kwasababu umebaki muda mdogo na wanatakiwa kusafiri, baada ya michezo hiyo watarudi kucheza viporo,” alisema.Aidha, wekundu hao wa Msimbazi wanatarajiwa kuweka kujiandaa na mchezo huo lengo ni kuhakikisha wanafanya vizuri ugenini na nyumbani. Mwenyekiti wa klabu hiyo Sued Mkwabi alisema Dar es Salaam jana kuwa watafanya maandalizi yao bila kusumbuka kwenda popote ili kocha apate muda wa kuandaa kikosi chake kwa utulivu na kwamba tayari ameanza kuwafuatilia wapinzani.Simba imesonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kuiondoa Mbabane Swallows ya eSwatini kwa jumla ya mabao 8-1. Huku Mtibwa Sugar ikiwaondoa Northern Dynamo ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 5-0. Lakini wakati timu hizo zinaendelea na maandalizi yao ya kimataifa, mechi za Ligi Kuu zitaendelea kama kawaida kwa timu nyingine zilizobaki ambapo leo Mwadui itacheza dhidi ya Alliance na Ndanda dhidi ya Prisons.
3
WAHADHIRI wa vyuo vya elimu ya juu wameunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kwamba baadhi ya shahada zinazotolewa na vyuo vikuu sasa hazina hadhi bali wanafunzi wanamaliza vyuo ili kupata vyeti.Aidha wameshauri kufanyika kwa maboresho ya elimu na kuwe na msukumo wa kuwajali walimu kimaslahi lakini pia kuwaendeleza kitaaluma.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wasomi hao wamesema tatizo la shahada za ‘kudesa’ katika vyuo vikuu nchini ni kubwa na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha nchi inapata wasomi wazuri wanaomaliza vyuo na vyeti vinavyolingana na elimu waliyoipata.Juzi Rais Magufuli akizindua Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha shahada wanazotoa zina viwango vya juu na si shahada za ‘kudesa’ na kuwataka wahadhiri kuwa wakali.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Frank Tillya alisema walimu wanaowafundisha wanafunzi hao nao pia wanachangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa elimu ya vyuo vikuu."Walimu nao wanachangia kwa kiasi kikubwa, wengi hawana maadili kwa sababu kama una maadili huwezi kukubali kuona mwanafunzi anatoka hajui kitu, wanafunzi wengi wanatoka hawana kabisa quality (kiwango) ya shahada kwa sababu hawakufundishwa kufikiri," alisema.Alisema wanafunzi wengi wanafanya tu mitihani ili kufaulu, lakini elimu yao haiakisi hadhi ya shahada hata wanapomaliza vyuo, jambo ambalo linaleta changamoto katika kupata kazi kwani wanakuwa hawana uwezo wa kushindana."Hata ukiangalia 'interview' za kazi utabaini tatizo kubwa kwani vyeti wanavyokuja navyo vinakuwa na ufaulu mkubwa lakini wanapohojiwa unabaini kichwani hawana ujuzi unaofanana na ufaulu wao,” alisema.Dk Frank alisema ingawa Rais Magufuli hakueleza kwa kirefu ukubwa wa tatizo hilo, lakini ni suala linalohitaji mjadala wa kitaifa ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema shahada ya sasa haimfanyi mhitimu kupata uwezo wa kuchanganua mambo wala kufikiri kwa mapana."Hili ni tatizo la kitaifa sijui tumejikita zaidi katika elimu nyingine, kijana amehitimu chuo lakini ukimwambia akuandikie barua au mpe habari ya kurasa tatu mwambie aifupishe hawezi," alisema Dk Bana.Hata hivyo, Dk Bana alisema moja ya sababu ya kushinda kuimarika kwa kiwango cha elimu ni mfumo wa elimu ya juu ambao alisema hauvidhibiti vyuo kuzalisha elimu bora kwa kiwango cha kutosha.Aidha alisema baadhi ya walimu wanatekeleza wajibu tu lakini hawana moyo wa kuwasaidia wanafunzi kupata maarifa na wengine hawana sifa kabisa za ualimu ambapo alishauri kufanyike maboresho ya elimu ya juu.Alisema elimu ya vyuo vikuu inashuka hasa vyuo vinavyoanzishwa sasa na kwamba mwanafunzi anavyojibu mtihani wake na alama anazopewa na mwalimu wake havilingani na kwamba wanafunzi wanataka matokeo mazuri bila kuyasumbukia.Na aliyewahi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwete amesema uongozi wa vyuo uwe tayari kushughulikia tatizo hilo ili kuongeza ubora wa elimu nchini.Alisema tatizo hilo lipo katika vyuo vingi kwani wanafunzi wengi hawana bidii ya kujisomea ili kupata maarifa badala yake wanataka kuhitimu ili wapate vyeti safi vya kwenda kutafutia ajira.
3
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amewaonya baadhi ya askari wa Kituo cha Polisi Kata ya Salawe kutumiwa na viongozi kwenda kuvuruga amani kwa wananchi, kinyume cha maadili ya kazi yao inayowataka kulinda usalama wa raia na mali zao.Inadaiwa diwani wa kata hiyo, Joseph Buyugu anawatumia baadhi ya askari kuonea wananchi hasa wanaofichua maovu kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi wakuu kwa kuwapiga na kisha kuwatia mbaroni.DC Mboneko ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alitoa onyo hilo juzi wakati alipofanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwenye kata hiyo, ambapo hivi karibuni kulitaka kutokea machafuko ya amani kwenye eneo hilo. Alisema amesikitishwa na viongozi wa maeneo hayo kulitumia Jeshi la Polisi vibaya kutaka kuvuruga amani ya nchi na kujichukulia mamlaka ambayo yapo nje ya utawala wao kwa kuwapiga wale ambao wamekuwa wakifichukua maovu yao pamoja na kuwavunjia nyumba wananchi na kuharibu mali zao.“Jeshi la Polisi nawaonya msitumiwe na viongozi kuvuruga amani ya nchi ninyi kazi yenu ni kudumisha amani na kulinda usalama wa raia na mali zao na si vinginevyo, acheni kutumika kuonea wananchi pamoja na kuwaomba rushwa, kama mnaona mishahara yenu haitoshi acheni kazi,” alisema Mboneko. “Na nyie viongozi msiwe chanzo cha machafuko ya kuvuruga amani kwa wananchi, kazi yenu ni kuwatumikia na kutatua kero zao pamoja na kuwa hamasisha kwenye masuala ya maendeleo, na siyo kugeuka miungu watu na kuanza kuwaonea huku mkiwapiga, kuwavunjia nyumba zao, na kisha kuwasweka rumande,” aliongeza.Awali baadhi ya wananchi wa kata hiyo ya Salawe wakiwakilisha kero zao kwa mkuu huyo wa wilaya akiwamo Seke Nyeke na Dumila Hamis, alisema malalamiko yao mengi yalikuwa ni viongozi wa maeneo hayo akiwamo na diwani wamekuwa wakishirikiana na askari Polisi kuwaonea na ili kutoka rumande, lazima watoe kitu kidogo.Kwa upande wake, diwani Buyugu alikana tuhuma hizo za kulitumia Jeshi la Polisi kuvuruga amani huku Kamanda wa Polisi Wilaya ya Shinyanga, Claud Kanyolota akiwaonya askari hao kutorudia tabia hiyo na kubainisha malalamiko hayo atayafanyia kazi ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje alisikitishwa na kitendo cha diwani wa Salawe aliyechaguliwa na wananchi na matokeo yake kuwakandamiza huku tatizo hilo limkionekana analifanya kwa wale ambao ana chuki nao, jambo ambalo halifai na ni hatari alimuomba aache tabia hiyo ili wananchi waishi kwa amani.
3
KAMISHNA Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Anna Makakala amepewa salamu za heshima kutoka kwa mataifa mbalimbali kwa kuindoa Tanzania kuwa uchochoro wa vitendo vya rushwa na kupitisha dawa za kulevya kwenda Ulaya.Nchi zilizotoa pongeza na kumpa heshima kwa kutambua mchango wa Kamishna Makakala ni China, Marekani, India, Ujerumani, Uingereza na Saudi Arabia. Salamu hizo za heshima zilitolewa Dra es Salaam juzi kwenye kongamano la viongozi wa dini lililoandaliwa na Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini nchini na kushirikisha wajumbe 437 kutoka mikoa yote ya bara na visiwani.Aidha wajumbe kutoka mataifa hayo akiwemo Profesa Yi gen kutoka China, Dk Brooks Lasmax wa Ujerumani , Shehe Dk Syudih Muhmed wa Saudia Arabia, Askofu Owen kennedy kutoka Marekani, Mchumi George Frank kutoka Uingereza na Dk Surani Snjaly wa India walisema kwa nyakati tofauti kuwa mabadiliko chanya katika masuala ya uhamiaji sio tu yamesaidia kwa asilimia kubwa kupungua kwa biashara ya dawa za kulevya nchini Marekani na Ulaya lakini imeiletea heshima Tanzania kwa kutokuwa tena barabara ya kupitisha dawa za kulevya.Walidai kuwa siku za zamani wakiwa wageni waliokuwa wakipita mara kwa mara na kuingia Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA), maofisa uhamiaji walikuwa wanapokea mgeni kwa kumuuliza atampa dola ngapi kabla hata hajafanya ukaguzi na walikuwa wakipewa Dola za Marekani 100 mgeni hakaguliwi kabisa lakini sio sasa.Dk Surajy walimwagia sifa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa kuigeuza idara hiyo kuwa chombo cha heshima kwa nchi mbalimbali na kuongeza kuwa hivi sasa raia wa India wanatamani kuja Tanzania kujifunza njia rahisi ya kuondoa rushwa.
3
Marekani Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Shirika la Kijasusi la nchi hiyo (CIA) halijahitimisha uchunguzi wake kwa kumlaumu mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, kuamuru mauaji ya mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi. Kauli hiyo Rais Trump, ameitoa jana Novemba 22, wakati ambapo Bin Salman, ameanza ziara ya kikazi nje ya nchi yake tangu Khashoggi, alipouawa. Kwa sasa yupo katika Falme za Kiarabu (UAE) ambayo ni mshirika mkubwa wa Saudia ndani ya kanda ya Mashariki ya Kati. “CIA wana hisia mbalimbali, ninayo ripoti yao na hawajahitimisha sijui kama kuna mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kusema Mwanamfalme Bin Salman, aliamuru mauaji,” amesema Trump. Taarifa ya maofisa wa CIA kwa vyombo vya habari nchini Marekani, imesema kuwa operesheni ya kumuua Khashoggi, lazima ilihitaji ruhusa ya Bin Salman, ili kutekelezwa. Huku mamlaka za Saudia zikisisitiza kuwa operesheni hiyo ilikuwa haramu na Bin Salman, hakuwa na ufahamu wowote wa kutokea kwake. Vile vile, gazeti moja la Uturuki limeripoti kuwa Mkurugenzi wa CIA Gina Haspel, aliwaambia maafisa wa Uturuki kuwa shirika lake lina mkanda wa sauti ya bin Salman akitoa maagizo kuwa Khashoggi anyamazishwe haraka iwezekanavyo. Wakati huo huo, Ufaransa imetangaza kuwawekea vikwazo raia 18 wa Saudia ambao wanahusishwa na mauaji hayo. Watu hao pia wameshawekewa vikwazo na Marekani, Uingereza na Ujerumani. Hata hivyo, Bin Salman, hayupo kwenye orodha hiyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa amethibitisha. Khashoggi, aliuawa Oktoba 2, mwaka huu ndani ya Ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki. Wakati wa uhai wake alikuwa mkosoaji mkubwa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman. Mwaka 2017, Khashoggi alikimbilia Marekani akihofia usalama wake.                                                 
2
VIONGOZI wa dini katika makanisa mbalimbali nchini, wametoa ujumbe mzito katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi, huku wakitaka uwepo wa utawala wa kidemokrasia nchini. Pia wamekemea vitendo vya ukatili, ikiwamo matukio ya utekaji nyara na mauaji ya kinyama, hali inayotishia kutoweka kwa amani ya nchi iliyoasisiwa na waasisi wa taifa kwa miaka mingi. Viongozi hao wa kiroho, wakiwamo maaskofu na wachungaji, walitoa mahubiri hayo wakati wa ibada zilizofanyika jana asubuhi na kwenye mkesha wa Krismasi. Akihubiri jana katika ibada ya Krismasi ambayo kitaifa ilifanyika Zanzibar, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Shao, alisema siasa safi ndiyo msingi wa Tanzania, hivyo kuna haja ya tofauti za mitazamo ya kisiasa kuheshimika na kila mtu. Askofu Shao alisema mfumo wa vyama vingi umesaidia katika kukosoa, kutofautisha na kutoa uwazi serikalini, hivyo ni vyema kuheshimu mawazo. Alisema ishara mbaya ni katika uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 11, mwaka huu kwa wahusika kushindwa kufahamu namna ya misingi bora ya demokrasia inavyotakiwa kuwa. “Katika chaguzi ndogo zilizopita kulikuwa na mizengwe ya hapa na pale iliyoendelea, haikufaa kwani imekiuka demokrasia. Tunatakiwa kutambua kuwa siasa ni kama mchezo wa mpira, mnamaliza kushinda kisha mnakuwa marafiki,’’ alisema Askofu Shao.  UCHUMI Katika hatua nyingine, askofu huyo alisema licha ya kukua kwa uchumi, lakini umasikini mkubwa umeongezeka miongoni mwa Watanzania. Alisema wakati uchumi umekua, umaskini kwa Watanzania umeongezeka huku baadhi ya viongozi wakiwa matajiri kupitiliza. Askofu Shao aisema hali ya viongozi wa kisiasa kiutajiri inatisha jambo ambalo linashangaza kwani wakiingia madarakani wanatangaza idadi ya mali zao, lakini baada ya kuongoza kwa muda wanakaa kimya. Alisema kukaa huko kimya ni dalili kwamba wamekuwa wakiomba nafasi mbalimbali za uongozi ili kutaka kujifungulia milango ya utajiri na kujilimbikizia mali. “Viongozi wengi wanataja mali zao kabla ya kuingia madarakani na baada ya hapo hutowasikia tena wakitaja, kwanini wanafanya hivyo?” alihoji Askofu Shao. Pia aliwataka viongozi kufanya mambo kwa haki ya kweli kwa kujali wananchi na kujifunza kujinyima ili watu wote wawe na haki sawa, huku akieleza hakuna mabaya au maovu yatakayoshinda mema. “Mungu ameagiza tuwe wahanga kuondoa giza kwa wenzetu ili haki na amani iweze kupatikana kwa kila mtu,’’ alisema. Askofu huyo alisisitiza kila aliyeshiba anatakiwa kumjali mwenye njaa na kwamba kila mtu afanye aliyoagizwa na Mungu kufanya.  AJIRA KWA VIJANA Askofu Shao ameitaka Serikali kuwasaidia vijana waliokosa mikopo na wasio na ajira wapate ajira kwani vijana ni muhimu katika taifa lolote. Alisema vijana wengi waliomaliza vyuo licha ya kusoma kwa bidii na kufanikiwa, wamekuwa wakihangaika mitaani bila mafanikio, hivyo ameitaka Serikali isaidie katika eneo hilo. “Vijana wetu wanahitaji ajira ili nao waweze kufurahia maisha, ni vizuri Serikali iwasaidie katika kusoma na kupata ajira kwani yapo mataifa kwa sasa yanateseka kwa kushindwa kuendeleza vijana wao,’’ alisema. Alisema kama vijana hawatasaidiwa, Tanzania ya viwanda inayotarajiwa itakuwa ni ndoto kufikiwa. Askofu Shao pia aliwataka wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi kwa wakati ili iweze kusaidia nchi katika harakati za maendeleo. Alisema wanafunzi kukosa ada na dawa hospitalini kunasababishwa na wafanyabiashara wakubwa kukwepa majukumu yao ya kulipa kodi na kulinyonya taifa. “Serikali ya awamu ya tano inasisitiza uwajibikaji, ukusanyaji wa kodi ni haki na wajibu kwa kila mfanyabiashara kuzingatia hilo ili maendeleo ya nchi yaweze kupatikana. “Wakwepaji wengi wa kodi ni wafanyabiashara wakubwa na hao hao ndio wamekuwa waharibifu wakubwa wa miundombinu yetu. “Mfano wanaofanya biashara kwa kutumia magari makubwa wanaharibu barabara, lakini ndio hao hao ambao leo wamekuwa wakwepa kodi,’’ alisema Askofu Shao.  WAFUNGWA HURU Pia alimpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaachia huru wafungwa, huku akiamini waliopo magerezani wakiwamo vijana, wataendelea kujirekebisha na kuwa na tabia njema inayompendeza Mungu na jamii nzima. Askofu Shao alisisitiza amani nchini kwa kujitakasa upya hasa katika Sikukuu ya Krismasi, huku akiwataka Watanzania kila mmoja kuheshimu mawazo ya mwenzake hata kama wanatofautiana.  PENGO NA HOFU YA MUNGU Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amewataka Watanzania kutenda matendo mema huku wakiongozwa na hofu ya Mungu. Akizungumza jana wakati wa misa ya pili ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Askofu Pengo alisema maendeleo hayawezi kuja kama Watanzania wenyewe hawana maadili au hofu ya Mungu. Askofu Pengo alisema kila mmoja awe mwananchi au kiongozi, anapaswa kuwa na hofu ya Mungu ambayo itamwongoza katika kufanikisha mipango iliyokusudiwa. Alisema pia Watanzania wanapaswa kukubali kuongozwa na kuwaombea viongozi wao ili kuhakikisha jitihada zinazofanywa zinazaa matunda. “Naunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli na Serikali katika kuleta maendeleo, lakini hatuwezi kufanikiwa kama hakuna maadili. “Hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha kuwa anakuwa na maadili na hofu ya Mungu, jambo ambalo linaweza kutusaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa,” alisema Askofu Pengo. Alisema katika maisha ya kila siku binadamu wanapaswa kumtegemea Mungu kwenye shughuli mbalimbali ili kufanikisha mipango wanayokusudia. “Hatuwezi kupata maendeleo kwa njia ya mkato halafu hatuna maadili wala hofu ya Mungu, kwa sababu naamini mwisho wa siku tutaishia kubaya, hivyo basi kila mmoja anapaswa kuwa na hofu hiyo ambayo itamwongoza katika mipango yake,” alisema. Alitoa mfano wa nchi mbalimbali ambazo zilikuwa zinahangaikia maendeleo kwa kumtegemea Mungu na mwisho walifanikiwa na kupata maendeleo hadi sasa. Alisema Watanzania wanapaswa kujifunza kutoka kwenye nchi hizo ili waweze kufanikiwa malengo yao. Askofu Pengo alisema nchi ambazo zilipiga hatua bila ya kumtegemea Mungu wala kutokuwa na maadili mwisho ziliishia kubaya na kufilisika kabisa. Alisema Watanzania wanapaswa kujirekebisha makosa yao na kuongozwa kwa maadili na kufanya kazi kwa bidii ambayo itawasaidia kufanikisha malengo yao na kupata maendeleo. “Wananchi wakiwa na maadili, nchi inafanikiwa na kupiga hatua za maendeleo, hivyo basi kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha kuwa anasimamia maadili na hofu ya Mungu ili nchi iweze kufanikiwa,” alisema. Alisema anatambua kuwa binadamu anapotafuta maendeleo anatumia njia nyingi ili kuhakikisha anafanikiwa, lakini kikubwa ni kuhakikisha kuwa unapoangaikia suala hilo, lazima uwe na hofu ya Mungu ambayo itakuongoza ili kufikia malengo yako.  HOFU KWA WANANCHI Kwa upande wake, Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, Isack Amani, amekemea vitendo vya ukatili kama vile utekaji nyara na mauaji ya kinyama yanayoendelea nchini kuwa vinatishia kutoweka kwa amani iliyopiganiwa na waasisi wa taifa kwa miaka mingi. Akihubiri katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme Moshi, Askofu Amani, alisema katika kipindi cha muda mfupi nchi imekumbwa na matukio mbalimbali jambo linalohatarisha kutoweka kwa amani. Alisema kutokana na kuendelea kwa matukio hayo, hofu imetawala miongoni mwa wananchi jambo ambalo ni tofauti na miaka ya nyuma “Uvamizi wa vituo vya polisi, ulevi wa kupindukia, ulegevu wa imani za dini, mauaji ya kinyama yakiwamo ya wazee, ni baadhi tu ya mambo yanayotokea nchini na kuzua hofu kwa wananchi. Dalili hizi ni mbaya na zinaashiria kutoweka kwa amani yetu,” alisema. Alisema ni vema mamlaka husika zikachukua hatua mapema ili kudhibiti hali hiyo ambayo imeonekana kuwakosesha amani Watanzania. “Mamlaka husika ni vema wakachukua hatua stahiki haraka ili kudhibiti matukio haya ya kinyama yanayoendelea kwani Tanzania tuliyonayo sasa si ile ya miaka ya nyuma,” alisema. SHOO AONYA VITISHO Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo, amesema kumekuwepo na watu wanaotishwa na kujengewa hofu ili kushindwa kutoa maoni yao kulingana na kile wanachokiamini katika taifa lao. Dk. Shoo alisema watu wanapaswa kusimama katika kweli na kuacha woga wa kuyasema yale wanayoyaona ni sahihi katika kulijenga taifa. Aliyasema hayo wakati akihubiri katika ibada ya Krismasi iliyofanyika jana KKKT Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro. Askofu Shoo ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, alisema katika kusimamia kweli watu wasiyumbishwe na kujikuta wanaogopa kusema na kutoa maoni ya kile wanacho kiamini. “Tusione woga wa kutetea kile tunachokiamini, kuna baadhi ya watu wanajaribu kuwajaza wengine hofu na kuwatisha ili wasiseme ukweli na kutoa mawazo yao kwa kile wanachokiona,” alisema Askofu Shoo. Alisema Watanzania wanapaswa kuwa wakweli katika Kristo licha ya kwamba katika ukweli huo kuna watu watakaowachukia. Mbali na hilo Askofu Dk. Shoo, aliwataka Watanzania kutobaguana kwa itikadi za kisiasa, kiuchumi, kikanda na kikabila. Alisema ni wakati wa kushirikiana na kuhakikisha wanadumisha mshikamano na amani ya nchi ambayo ilipiganiwa kwa muda mrefu na waasisi wa taifa.  MALASUSA AHIMIZA UPATANISHO Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, amewataka Watanzania kutumia Sikukuu ya Krismasi kupatana na kuwa wamoja. Akizungumza katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front, Dar es Salaam, Askofu Malasusa alisema kuna watu wengi wanaishi bila kupatana hata ndani ya kanisa. “Neema inatuagiza kukataa dhambi na inatukumbusha kuwa watu wa kutafuta amani na upatanisho. “Lazima tuwe patanishi, tuukatae ubaya, ugomvi, tupatane. Watu wasiishi kwa kuangalia macho chini kwa sababu wako wengine hata ndani ya kanisa wanaishi bila kupatana,” alisema. Pia aliwatahadharisha waumini wa kanisa hilo kuacha kuhangaika kwenye madhehebu na badala yake watambue kuwa anayeweza kuwabadilisha ni Mungu na wala si binadamu. “Nyakati tunazoishi si za kawaida, wapo wengi wanahangaika na makanisa na siku hizi watumishi tumebadilisha majina mengi tu, lakini tutambue kuwa Yesu ndiye atakayekubadilisha na si mwanadamu,” alisema. Askofu huyo pia alitawataka Watanzania kujiepusha na matendo maovu na kuwa mawakala wa amani. “Tuukatae ubaya wa aina yoyote, wizi wa mali za umma, uvivu, uzembe na mengine mengi. Watu wanatakiwa wayaone matendo yako na si mpaka wasikie jina zuri,” alisema. Pia aliwatia moyo wale wote waliokata tamaa na kusema kuwa suluhisho pekee ni kumfuata Yesu Kristo. “Kuna watu wamekataliwa na wenyewe wanajikataa, hata wale ambao dhambi zao zimedhihirishwa Yesu anawahitaji. “Zimepita Krismasi nyingi, lakini hii iwe ya kipekee, Yesu Kristo azaliwe mioyoni mwetu,” alisema Askofu Malasusa.  RUVUMA Askofu wa KKKT Dayosisi ya Ruvuma, Amon Mwenda, amewataka waumini wa kanisa hilo kujiimarisha katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kiuchumi ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya kidunia. Akitoa salamu za Sikukuu ya Krismasi wakati wa ibada, alisema waumini wanatakiwa kutambua kuwa dunia ya sasa imebadilika, hivyo ni vyema wakajifunza kubadilika katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kiuchumi. Alisema kama waumini watakubali kuingia kwenye mabadiliko hayo, yatawafanya waendane na ulimwengu wa sayansi na teknolojia, ambao unahitaji kutumia elimu ili kufanikiwa zaidi. Alifafanua kuwa changamoto za kiuchumi zimekuwa zikiathiri hadi makanisa na si jamii pekee, hivyo bila uchumi injili itakwenda kwa muda ambao haukustahili.  IRINGA Kwa upande wake, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Blaston Gavile, amewataka Watanzania kuacha kulalamika kuhusu vyuma kukaza na badala yake kumrejea Mungu awapiganie wafanikiwe kimaisha. Akizungumza mara baada ya ibada katika Usharika wa Kanisa Kuu, Askofu Gavile alisema Wakristo hawana sababu ya kuungana na wanaolalamika vyuma kukaza bali wanapaswa kufanya kazi na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo. “Tunalalamika vyuma vimekaza kwa sababu hatufanyi kazi kwa juhudi na maarifa, Rais Dk. Magufuli kila wakati yupo kwa ajili ya kututumikia na kuona Taifa linasonga mbele,” alisema Askofu Gavile. Alisema jukumu kubwa la viongozi wa dini na Watanzania ni kuendelea kuiombea nchi amani na kumwombea Rais Magufuli ili aendelee kuwatumikia Watanzania vema. “Kazi anayoifanya rais wetu ni nzuri na sisi tunazidi kumwombea aendelee kuifanya na zaidi azidi kuzingatia katiba yetu kama anavyofanya,” alisema.  MTOKAMBALI ATAHADHARISHA Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuzingatia wajibu wao katika kutoa huduma za kiroho na kuacha kuingiza siasa katika nyumba za ibada. Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk. Barnabasi Mtokambali, katika imaadhimisho ya miaka 43 ya kanisa hilo yaliyofanyika mkoani Morogoro. “Viongozi wa dini wanaaminiwa na kundi kubwa la watu, lakini baadhi yao wamekuwa wakitumia nyumba za ibada kama majukwaa ya siasa,” alisema Dk. Mtokambali. Alisema kitendo hicho kinabadili mitazamo ya waumini na kuacha kuzingatia mafundisho ya kiroho. Askofu huyo aliwataka viongozi wa dini kuishi kutokana na mafundisho wanayoyatoa kwa jamii ili kuwa kielelezo na mfano wa kuigwa. Naye Mchungaji Kiongozi Kanisa la TAG Sabasaba Morogoro, Anania Aloyce, alisema baadhi ya viongozi wa dini hawaishi kile wanachokifundisha na kuwataka wabadilike kimatendo. Kwa upande wake Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood (CCM), ambaye pia alihudhuria ibada hiyo, alisema Serikali haina dini na kuwaomba viongozi wa dini wanapokuwa na jambo la kuishirikisha Serikali wasisite kufanya hivyo.  DODOMA Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), Dk. Dickson Chilongani, amesema viongozi wa Serikali na dini wanatakiwa kujishusha kwa wananchi wa hali ya chini ili kusikiliza kero zao badala ya kujikweza na kuwasahau. Akizungumza wakati wa ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Mjini hapa, Askofu Dk. Chilongani alisema tabia ya viongozi kujikweza imekuwa ikiwakatisha tamaa watu wa chini ambao kwa sehemu kubwa wanawategemea viongozi wao. “Wabunge na madiwani wanapoomba kura huwa wanyenyekevu, lakini wakishapata hujiweka juu mahali ambako wapigakura wao hawawezi kufika, tabia hii ikiachwa itajenga matabaka,” alisema Askofu Chilongani. Aliwataka viongozi wengine kuiga mfano wa Rais Dk. John Magufuli ambaye amekuwa akijishusha na kuwatetea wanyonge. Alisema analofanya Rais Magufuli lilifanywa na Yesu Kristo mwenyewe aliyeshuka na kuwa mwanadamu ili aweze kuwa na watu wote. Naye Askofu wa Kanisa la International Evangelism Sinai la Ipagala mkoani hapa, Silyvester Tadey, aliwaonya waumini juu ya matumizi ya anasa katika kipindi cha sikukuu. Akihubiri kwenye ibada ya Krismasi, Askofu Tadey aliwataka watunze akiba kwa ajili ya watoto wao watakapokwenda mashuleni. Kwa upande wake, Mchungaji Evance Chande wa Kanisa la Evangelism Assembless of God Tanzania (EAGT) Soloam la mjini hapa, amewataka Watanzania kuisheherekea sikukuu hiyo kwa kuisaidia Serikali katika kuhakikisha ulinzi unakuwepo badala ya kuliachia Jeshi la Polisi pekee.  MBEYA Mchungaji wa KKKT Usharika wa Mbeya Mjini, Amani Mwaijande, amesema ili nchi iweze kukua kiuchumi na kufikia malengo iliyojiwekea, ni lazima wananchi wakubali kuumia kwa kipindi kifupi. Akizungumza na MTANZANIA baada ya ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Usharika wa Mbeya Mjini, mchungaji huyo alisema nchi zote zilizoendelea duniani wananchi wake waliumia wakati wa utekelezaji wa mipango endelevu ya kukuza uchumi, hivyo amewataka wananchi kutokuwa wepesi wa kukata tamaa. Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo walisema viongozi wote waliopita na waliopo wamekuwa na utaratibu wa kuiendesha nchi, hivyo hakuna sababu ya wananchi kulalamika, zaidi ni kujipanga kimkakati. “Ukiangalia kila kiongozi alikuwa na utaratibu wake wa kuendesha nchi, kwahiyo hatuna sababu ya kulia maisha magumu, tujikite katika kufanya kazi,” alisema mkazi wa Mbeya, Adamu Mbaliezi. Nao Elizabeth Joseph, Aminaery Richard na Esther Mwakiboke, walimwomba Rais Magufuli kuwaangalia wajasiriamali wadogo kwani wengi wanashindwa kuendesha biashara zao kutokana na kudaiwa na taasisi za kibenki. Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, Braison Mwampashi, amewataka Wakristo kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa kumwogopa Mungu badala yake wakumbuke matendo ya Yesu yaliyo mema. Akizungumza katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Ushirika wa Ruanda jijini Mbeya, Mchungaji Mwampashi alisema wanadamu wanatakiwa watende matendo mema ya kumpendeza Mungu na si kumuudhi. “Unaposema wewe ni Mkristo, hakikisha kweli unatenda yale yanayompendeza Mungu,” alisema Mchungaji Mwampashi. TANGA Mchungaji wa KKKT Ushirika wa Mikanjuni, Warehema Chamshama, amewataka Wakristo kuacha kutenda maovu ili waweze kuwa wapya kwa Kristo kuzaliwa mioyoni mwao. Sambamba na hilo, aliwaasa kuacha kutoa na kupokea rushwa kwani jambo hilo ni baya na linasababisha haki na wajibu kupindishwa. “Wakati huu mwokozi Yesu anazaliwa lazima tukae kwenye maadili yanayompendeza Mwenyezi Mungu kwani kazi tulizonazo ni mipango yake, tuhakikishe tunaishi kwa upendo na amani na jamii zinazotuzunguka,” alisema Mchungaji Chamshama.  Habari hii imeandaliwa na Nora Damian, Asha Bani, Patricia Kimelemeta (Dar), Eliud Ngondo, Upendo Fundisha (Mbeya), Ashura Kazinja (Morogoro), Upendo Mosha (Kilimanjaro), Amon Mtega (Ruvuma), Francis Godwin (Iringa), Ramadhan Hassan (Dodoma) na Oscar Asenga (Tanga).
3
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imevunja rekodi ya ufanisi wa makusanyo ya asilimia 100.20 kwa mwezi tangu ianzishwe miaka 23 iliyopita, kwa kukusanya Sh trilioni 1.987 Desemba 2019 kutoka lengo la kukusanya Sh trilioni 1.983, ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni tano.Kwa mara ya kwanza, TRA Septemba mwaka jana iliandika rekodi ya kukusanya Sh trilioni 1.767 iliyokuwa sawa na asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 1.817.Aidha katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2019/2020 inayohusisha Oktoba, Novemba na Desemba, TRA imefanikiwa kukusanya mapato ya jumla ya Sh trilioni 4.972 sawa na ufanisi wa asilimia 97.49 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 5.100.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu makusanyo ya kodi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2019, Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede alisema baada ya makusanyo ya Septemba mwaka jana kuvunja rekodi, Desemba imevunja rekodi zaidi tangu mamlaka hiyo ianzishwe mwaka 1996.Dk Mhede alisema pamoja na kwamba makusanyo ya kodi katika miezi hailingani moja kwa moja, lakini miezi ya kikodi ya Septemba na Desemba inawiana, hivyo TRA imevunja rekodi yake yenyewe iliyoiandika Septemba mwaka jana.“Makusanyo haya ya Desemba mwaka 2019 ni sawa na ufanisi wa asilimia 100.20 kutoka katika lengo la kukusanya Sh trilioni 1.983 katika kipindi hicho ambayo ni ukuaji wa wastani wa asilimia 22.05 ikilinganishwa na makusanyo ya Sh trilioni 1.628 kwa Desemba mwaka 2018,” alisema.Kamishna Mkuu huyo alisema katika robo ya pili ya mwaka 2019/2020 kwa ujumla, ufanisi umeongezeka baada ya makusanyo ya Sh trilioni 4.972 kuwa sawa na ukuaji wa asilimia 19.78 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa robo ya pili ya mwaka 2018/2019 ambapo TRA ilikusanya Sh trilioni 4.151 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 87.59 kutoka katika lengo la kukusanya Sh trilioni 4.739.Akieleza makusanyo ya Oktoba na Novemba, Dk Mhede alisema Oktoba mwaka jana mamlaka hiyo ilikusanya Sh trilioni 1.484 na Novemba ilikusanya Sh trilioni 1.501.“Makusanyo haya yalikuwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 93.98 kwa Oktoba kutoka lengo la kukusanya Sh trilioni 1.579 na asilimia 97.59 kwa Novemba kutoka lengo la kukusanya Sh trilioni 1.538,” alisema.Alisema makusanyo hayo, yanaonesha ukuaji wa asilimia 14.40 kwa Oktoba na asilimia 23.31 kwa Novemba kulinganisha na makusanyo ya Oktoba 2018 na Novemba 2018.“Makusanyo haya ni muendelezo wa kiashiria cha wazi kwamba walipakodi na Watanzania walio wengi wameendelea kuelewa, kukubali na kuitikia wito wa Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli wa kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu,” alisema.Dk Mhede alimshukuru Rais Magufuli, kwa kufuatilia na kuweka msingi imara wa uelewa kwa Watanzania umuhimu wa kulipa kodi na kuonesha kwa vitendo namna kodi zao, zinavyotekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya kimaendeleo nchini.Alisema mafanikio hayo, si ya serikali peke yake, bali ni ya walipa kodi wote wa Tanzania na mamlaka hiyo inajivunia wananchi na wafanyabiashara wote, wanaotekeleza wajibu wao bila kushurutishwa kwa mujibu wa sheria.Alisema TRA itaendelea kuweka nguvu katika kukusanya kodi, kwani pamoja na mafanikio hayo, inaamini bado hawajafika mahali pa kuridhika na ukusanyaji huo, hivyo watawatumia wataalamu wa ndani kutengeneza mifumo ya kitekkolojia ya kuongeza mapato nchini.
3
Na NORA DAMIAN-DAR ES SAALM SIKU chache baada ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Wilaya ya Ngara  mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61) kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake, kiongozi huyo wa dini ametoa waraka unaohusu umuhimu wa Katiba mpya. Katika waraka huo alisisitiza kuwa maoni yake kuhusu Katiba mpya  hayawakilishi msimamo wa Kanisa Katoliki bali  ni yake binafsi. Askofu Niwemugizi ambaye juzi aliliambia MTANZANIA kuwa aliitwa mara mbili na Uhamiaji kuhojiwa, alisema ataendelea kuizungumzia Katiba mpya kwa sababu inagusa maisha yake na Kanisa analolitumia   na maisha ya watanzania kwa ujumla. “Bado nitaendelea kuizungumzia Katiba kwa sababu inagusa maisha yangu na Kanisa   ninalotumikia, lakini pia inayagusa maisha ya raia wenzangu wote. “Kwa vyovyote naheshimu tofauti zetu za kuwaza na kuona mambo, kwa sababu  ndivyo ilivyompendeza Mungu kutuumba, hatufanani tangu sura hadi kuwaza. “Nilifurahi nilipopingwa, nikajua kuwa lengo limefanikiwa kuchokoza  tuanze tena kuzungumzia mchakato wa Katiba. “Bado siogopi kukoromewa na sauti nzito, nikijua kuwa hata Yesu alikoromewa na wakuu!  Naamini hatimaye kitu kizuri kitazaliwa baada ya michango ya mawazo kwa lengo la kujenga. “Mimi siamini kuwa Katiba mpya ilikuwa kipaumbele wakati ule tu na sasa siyo. Kwa hiyo kwa kweli si kwamba tunavumbua gurudumu jipya, bali ni kulifanya lile lililokwisha kuanza kuzunguka liendelee,”alisema askofu huyo. Askofu Niwemugizi alisema hata   ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilibeba agenda hiyo kama jambo la kukamilisha katika   miaka mitano ijayo. Alisema anaamini  watanzania wengi wanahitaji Katiba hivi sasa lakini yawezekana wale wenye jukumu la kuhakikisha inapatikana wana majukumu mengi. Aliwashauri wenye majukumu hayo washughulikie haraka yale wanayoona yinafaa haraka zaidi kwanza kabla ya Katiba. SOMA WARAKA WA ASKOFU  NIWEMUGIZI NENO KWA NENO KATIKA GAZETI HILI KESHO.
3
['Arsenal wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, lakini si kwa Manchester United ama Liverpool. (90min.com)', 'Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, ameiomba klabu yake ya Crystal Palace imruhusu ahamie Arsenal. Palace inamthaminisha streka huyo streka huyo kuwa na thamani ya pauni milioni 80. (Mirror)', 'Manchester United wanamini kuwa wataweza kukamilisha usajili wa kuwanasa Sean Longstaff, 21, kutoka Newcastle na Bruno Fernandes, 24, kutoka Sporting Lisbon ya Ureno. (Evening Standard)', 'Real Madrid watalazimika kulipa kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili kiungo Mfaransa Paul Pogba 26, kutoka Manchester United. (Mirror)', 'Gareth Bale yawezekana akasilia na Real Madrid baada ya klabu hiyo kushindwa kumpata mnunuzi anayemtaka winga huyo mwenye miaka 29. (Mirror)', 'Chelsea wanampango wa kumtangaza Frank Lampard kuwa kocha wao mpya kabla ya wachezaji kurudi mpaumzikoni wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. plan to announce Derby. (Sun)', 'Liverpool wamefikia makubaliano na Sporting ada ya usajili ipatayo pauni milioni 7 ili kumnunua mshambuliaji kinda Rafael Camacho, 19. (Evening Standard)', "Kumefanyika mkutano baina ya viongozi wakuu wa Atletico na Real Madrid juu ya usajili wa usajili wa mshambuliaji Antoine Griezmann, 28, kuelekea dimba la Bernabeu. (L'Equipe - in French)", 'Streka wa Colombia Radamel Falcao, 33, anataka kujiunga na timu inayomilikiwa na David Beckham nchini Marekani Miami pale mkataba wake watakapofiki tamati na klabu ya Monaco. (Sun)', 'Aston Villa wapo tayari kutuma maombi ya kutaka kumsajili beki wa Southampton Matt Targett. (Express and Star)', 'Kocha wa West Brom Slaven Bilic anamtaka mchezaji mwenzake wa zamani klabuni hapo Julian Dicks kujiunga naye kama sehemu ya benchi la ufundi.. (Express and Star)', 'Manchester United inafikiria kumnunua beki wa Ufaransa na Barcelona Samuel Umtiti, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 23, anasalia kuwa mchezaji anayelengwa sana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich msimu huu licha ya mpango huo kusita hapo awali. (Sky Sports)', 'Mkufunzi wa klabu ya Sporting Marcel Keizer anaamini kwamba nafasi ya kumzuia kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandez katika klabu hiyo ni ndogo, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zimevutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 (Record, via Manchester Evening News)', 'Babake mshambuliaji wa Juventus Moise Kean, 19, ametangaza kwamba raia huyo wa Italia anataka kuhamia Inter Milan. (Mirror)', 'Atletico Madrid inafikiria kumsajili mchezaji wa Real Madrid na Colombian James Rodriguez, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa hahitajiki tena Real . (Cadena SER, via AS)', 'Naibu mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola ataondoka Chelsea wikendi hii wakati ambapo kandarasi yake itakuwa inakamilika baada ya kukataa ofa ya kuwa balozi wa klabu hiyo. (Guardian)']
4
Na JANETH MUSHI -ARUSHA UCHAGUZI wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Arusha Mjini umeanza kwa vurugu, baada ya baadhi ya wajumbe kupigana ngumi hadharani. Vurugu hizo zilijitokeza kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo, uliowahusisha pia wajumbe wa mkutano wa wilaya wa UVCCM uliofanyika jana, ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose, baada ya wapambe wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti kuzichapa nje ya ukumbi huo wakati walipoanza kutuhumiana. Kutokana na vurugu hizo, uongozi wa hoteli hiyo ulilazimika kuita gari la ulinzi la Kampuni ya Ultimate Security. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, vurugu hizo zinadaiwa kutokea kwa muda wa dakika 15 hadi 20, baada ya wapambe hao kudaiwa kushikana mashati na kutwangana ngumi nje ya ukumbi huo, huku umati ukishuhudia tukio hilo, wakiwamo watembea kwa miguu na watu wenye ofisi katika hoteli hiyo. Wagombea nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi huo ni Jimmy Pamba na Godliving Kisila, wanaochuana kumrithi Martin Munisi, anayemaliza muda wake na inadaiwa kuwa ugomvi huo ulianza baada ya wapambe wao kutofautiana. Mmoja wa wapambe wa Kisila, Hussein Abdallah, anadaiwa kumtuhumu Lameck Dudu, anayedaiwa kuwa kambi ya Pamba, kuwa si mjumbe wa mkutano huo na kudai kuwa ni tapeli wa kisiasa, hivyo hakupaswa kuwapo katika uchaguzi huo. Kutokana na kauli hiyo, Dudu anadaiwa kumrushia ngumi Hussein na kuanguka chini, hali iliyofanya wapambe wengine wa pande zote mbili kutokukubaliana na hali hiyo na kuanza kupigana. Vurugu hizo zilisababisha askari mmoja wa kike wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) aliyekuwa karibu na eneo hilo kujaribu kutuliza vurugu hizo, ila ilishindikana na baadaye kikosi cha askari polisi walifika katika eneo hilo na kutuliza vurugu hiyo na kuwataka wajumbe hao kurudi katika ukumbi wa mkutano. Mmoja wa vijana aliyepigwa na aliyejitambulisha kwa jina la Silvester Meda, alidai kuwa, licha ya kupigwa na kuchaniwa nguo zake, hajui kosa lake ni lipi. “UVCCM Arusha imezungukwa na wahuni, hivyo chama kinapaswa kuwachukulia hatua wote walioiaibisha jumuiya hiyo kwa maslahi yao,” alisema. Naye Katibu Hamasa wa UVCCM Wilaya ya Arusha, Abdi Marijana, alidai kuwa, Dudu ndiye chanzo cha vurugu hizo, pia si mjumbe halali wa mkutano huo. “Polisi walipaswa kumkamata Dudu kwa sababu ni chanzo cha vurugu hizo, ila sijui kwanini polisi hawajamkamata,” alisema. Baada ya vurugu hizo, wajumbe wa mkutano huo walirejea katika ukumbi na kuendelea na uchaguzi.
3
Msimu wa tisa wa Bongo Star Search (BSS) unatarajiwa kuanza mwishoji mwa mwezi huu huku Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) likiwasihi washiriki kujikita zaidi kwenye nyimbo zenye maudhui ya maendeleo ya taifa.Utekelezaji wa ajenda ya uchumi wa viwanda, serikali kuhamia makao makuu ya nchi-Dodoma, kupiga vita maabukizi ya virusi vya Ukimwi pamoja na kuutangaza utalii wa ndani ni baadhi ya maudhui yaliyopendekezwa na Kaimu Katibu mkuu wa Baraza, Onesmo Kayanda."Ni kwa sababu ujumbe kupitia nyimbo huwafikia watanzania wengi kwa wakati mmoja. Wasanii ni kiungo muhimu kwani kazi zao zina michango mbali mbali kwa jamii yetu.Muziki humburudisha msikilizaji na wakati huohuo kumpa ujumbe fulani. Wakati huo huo mtunzi huuza kazi zake na kujipatia kipato chake binafsi wakati akichangia pato la taifa," amesema wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam.Evelyne Byaruhangwa amesema mashindano hayo yatahusisha mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar Es Salaam ambapo mikoa mitatu itatakiwa kutoa washiriki kumi (kila mkoa).Alifafanua kwamba Dar es Salaam itatoa washiriki 20 kutokana na ukweli kwamba mkoa huo una wasanii wengi. "Zoezi la kukusanya washiriki litakamilika mwezi wa kumi na michuano rasmi ya kumpata mshindi wa jumla itaanza mwezi unaofuatia," amesema
3
RABAT, MOROCCO MAHAKAMA ya Morocco imewafunga jela watu 28 baada ya kuwatia hatiani kwa kughushi na kutoa nyaraka bandia kwa ajili ya kutengenezewa vitambulisho vya uraia, Wazayuni. Mahakama ya rufaa ya Morocco siku ya Alhamisi iliendelea kufuatilia kesi za watuhumiwa hao 28 waliokula njama za kuwapa vitambulisho vya uraia Waisrael kinyume cha sheria. Mahakama hiyo imewahukumu kifungo cha miaka sita jela watuhumiwa watatu wakuu akiwemo mkuu wa genge hilo ambaye yeye mwenyewe ni Myahudi pamoja na wanawake wengine wawili. Vyombo vya habari vimetangaza kuwa: “Hatimaye mahakama ya rufaa ya Morocco imelipata genge hilo, na hatia ya kughushi na kutoa vyeti bandia kwa raia wa utawala wa Israel.” Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa al Khalij al Jadid, mahakama hiyo ya Morocco imewatia hatiani pia watu wengine watatu akiwemo Myahudi mmoja na kuwahukumu kifungo cha miaka minne jela kila mmoja. Watuhumiwa wengine waliobakia wamepewa adhabu tofauti na ahakama hiyo. Katika safu ya watuhumiwa hao wamo pia maofisa watatu wa polisi na mkuu wa shirika moja la usafiri la Morocco. Machi mwaka huu, maofisa wa Morocco walitangaa kuwa, wamewatia mbaroni watu 28 kwa tuhuma za kutengeneza vitambulisho na vyeti bandia kwa ajili ya walowezi wa Kiyahudi. Wanane kati ya watu hao ni walowezi wa Kiyahudi. Hata hivyo sehemu kubwa ya watu hao ni raia wa Morocco na uchunguzi unaonesha kuwa walijipenyeza katika taasisi za usalama na zile zinazohusiana na vyeti na nyaraka na kufanya uhalifu huo.
2
Na Mwandishi Maalumu – Pemba RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ametangaza rasmi kuwa kuanzia Julai Mosi, mwakani, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itatekeleza mpango wake wa kutoa elimu bure kwa shule za sekondari za Serikali na michango yote wanayotozwa wazazi haitokuwapo tena. Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana katika kilele cha Sherehe za Tamasha la Elimu Bila ya Malipo zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwamo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, mawaziri, viongozi wengine wa Serikali, wananchi na wanafunzi kutoka Unguja na Pemba. Dk. Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alisema kuanzia bajeti ya mwaka 2018/2019, shule zote za Serikali za sekondari zitatoa elimu bila ya malipo na kwamba ile azma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume ya elimu bure, itakuwa imekamilishwa. Alisema Serikali yake inao uwezo huo na ndani ya bajeti yake bila ya kumkopa ama kumwazima mtu na hiyo ndiyo ahadi yake na ataitangaza siku itakapoanza kutekelezwa rasmi. “Hatuna sababu ya kushindwa kutoa elimu bure, iwe ya maandalizi, msingi ama sekondari na naiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Wizara ya Fedha na Mipango, wawe makini katika kuipanga Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya mwaka 2018/2019,” alisema. Kuhusu elimu ya juu, alisema utaratibu wa kutoa mikopo utaendelea kama ilivyo hadi pale zitakapofanywa taratibu nyingine. Alisema katika kipindi cha miaka 53 ya mapinduzi, mafanikio makubwa yamepatikana katika kuyatekeleza malengo yake na katika kipindi chote hicho, Serikali imeendelea kutoa elimu bila ya malipo, ingawa si kwa kiwango cha miaka 15 ya mwanzo baada ya mapinduzi. Dk. Shein alisema hatua hiyo inatokana na sababu za matatizo ya uchumi na ongezeko la idadi ya watu yaliyoikumba nchi na Serikali ililazimika kuwaomba wananchi wachangie elimu kwa utaratibu maalumu ulioandaliwa kuanzia shule za msingi hadi sekondari. Pia alisema kuanzia Julai, mwaka juzi, suala la uchangiaji wa elimu katika shule za awali na msingi kwa Unguja na Pemba limeondolewa na Serikali inatoa elimu ya msingi bila malipo kama ilivyoamuliwa baada ya mapinduzi. Katika hatua nyingine, alisema Serikali inazitambua changamoto za walimu na itaendelea kuchukua hatua katika kukabiliana nazo na kwa sasa vipaumbele ni kuimarisha ubora wa elimu, miundombinu kwa kujenga shule mpya, kuyakamilisha majengo yaliyojengwa na wananchi, kuzitengeneza shule za zamani, kuzipatia vifaa vya maabara, samani na vitabu. Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma, alisema wataendelea kuimarisha sekta ya elimu na kuhakikisha kuwa juhudi zitaendelea kuchukuliwa katika kuhakisha walimu wanatoa elimu bora.  
3
Akizungumza jana kabla ya kukabidhi leseni kwa Kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Bahati Nasibu Taifa Abbas Tarimba alisema kutokana na Kampuni hiyo kuwa na vifaa vya kisasa inategemea kuajiri Watanzania 200 kwa ajira za moja kwa moja na 1,000 ambao ni mawakala.Alisema pia, Serikali itanufaika na fedha za uwekezaji katika mwaka wa kwanza ambapo itapata Sh bilioni 56 na itakuwa ikitoa kodi Sh bilioni kwa mwaka wa kwanza Sh bilioni 40.“Kampuni hii kabla ya kuipa leseni tuliichunguza kwa kushirikiana na Mtandao wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) kujua imepata wapi fedha za kuendesha mchezo huo, tukajiridhisha na kuipa nafasi kwa mujibu wa sheria namba 41 ya bahati nasibu, tunategemea Watanzania wengi watanufaika,” alisema.Tarimba alisema kampuni hiyo inatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kwa sasa imepewa muda wa miezi mitano kwa ajili ya kufunga mitambo yake na kuendelea na mchakato wa ajira kuwapata wale wanaowahitaji.Alisema mchezo huo utaendeshwa nchi nzima ambapo tiketi ya kwanza itauzwa rasmi kuanzia Julai 4, ambayo itakuwa ni siku ya uzinduzi na kwamba zawadi ya kwanza itakuwa ni Sh bilioni moja.Alisema michezo ambayo watakuwa wanaendesha ni Loto, kutabiri michezo ya kimataifa na mingine mipya itakayotambulishwa siku ya uzinduzi rasmi.Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Gidani na Murhandziwa Professa Bongani Khumalo alisema ujio wa kampuni hiyo ya pili kwa ukubwa barani Africa unategemewa kuleta manufaa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla waliopo katika sekta rasmi na waliopo katika sekta zisizo rasmi yaani wafanyabiashara binafsi.
5
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM KOCHA Mpya wa Simba, Patrick Phiri, anatarajia kutua leo nchini na kukabidhiwa mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mcroatia Zdravko Logarusic, aliyefungashiwa virago vyake mwishoni mwa wiki iliyopita. Phiri anatarajia kuwasili majira ya saa 8 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Fastjet akitokea nchini kwao Zambia. Akizungumza na MTANZANIA jana, Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, alithibitisha ujio wa kocha huyo leo, huku akidai kuwa walikuwa wanaendelea kumalizia mipango  ili aanze safari. “Kweli kocha anawasili kesho (leo) na hapa tunafanya mpango wa tiketi yake ya ndege, kuhusu suala la mkataba atakapowasili ndiyo tutakaa naye na kuamua kuingia mkataba wa mwaka mmoja au miwili,” alisema. Phiri  ni kocha mwenye historia nzuri na klabu hiyo msimu wa ligi kuu wa 2009/2010, ambapo aliweza kuisababishia timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa ligi hiyo bila kufungwa mchezo hata mmoja. Licha ya kuweka rekodi hiyo, lakini pia amewahi kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu mara mbili akiwa na timu hiyo ambapo pia timu yake hiyo ilikuwa mabingwa 2004/2005, baadaye aliamua kuiacha Simba kwa sababu zake binafsi na kumpa mikoba kocha Milovan. Hata hivyo, Phiri atakabidhiwa timu ikiwa tayari imeshafanya usajili wa baadhi ya wachezaji, huku ikiwa inawaangalia wachezaji watatu, Modo Kiongera wa Kenya, Jerome JJ wa Botswana na Osumani Mane wa Senegal, ambapo atachagua mchezaji mmoja atakayesajiliwa na klabu hiyo ambayo inatarajia kuweka kambi Zanzibar. Licha ya Simba kufanya mabadiliko ya Kocha Mkuu, lakini benchi la ufundi litabaki vile vile ambapo atasaidiana na kocha Selemani Matola.
4
Na MALIMA LUBASHA -SERENGETI FAMILIA ya watu watatu wa Mtaa wa Chamoto, Kata ya Stendi Kuu, Tarafa ya Rogoro wilayani Serengeti mkoani Mara, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watoto wawili wa kike kwa njia ya ukeketaji. Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Pascal Nkenyenge, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Amaria Mushi, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Ikwabe Charali (32), Robi Petro (31) wakazi wa Chamoto na Nyangi Charali (35) mkazi wa Kijiji cha Matare wilayani hapa. Alisema washtakiwa hao ambao ni baba, dada na mke wa mshtakiwa wa kwanza Ikwabe, wanatuhumiwa kuwafanyia ukatili watoto wa kike kwa kuwakeketa Desemba 19, mwaka huu ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi. Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka mawili  yanayowakabili  katika kesi hiyo, walikana kuhusika na tukio hilo kwani walitenda kosa hilo. Hakimu Mushi, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 2, mwakani itakapotajwa tena hivyo kuamuru washtakiwa warudishwe mahabusu. Wakati huo huo, Mkazi  wa Kijiji cha Bonchugu, Kata ya Manchira wilayani Serengeti mkoani Mara, Chacha Matiko (53), amehukumiwa na mahakama hiyo kifungo cha miaka  mitatu  jela na kulipa faini ya  Sh 800,000 baada ya kupatikana  na makosa  ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na kuchunga ng’ombe bila kibali. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile. Alisema mahakama imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
3
Mwandishi Wetu Mwaka 2008, Dunia ilikutana na Paul Karason, mwanamume aliyegeuka kuwa wa rangi ya bluu ku­tokana na kuzidisha dozi ya dawa aliyoinywa na kuipaka katika ngozi yake iliyolenga kutibu madoa madoa usoni. Miaka mitano baadaye, mtu huyo aliyekuwa gumzo mitandaoni baada ya kuchomoza mbele ya dunia na katika ulimwengu wa tiba, ambao ulianza kufanya tafiti kile kilichomsumbua na hatimaye kubadilika rangi ya ngozi yake akafariki dunia. Karason alizaliwa akiwa na ngozi ya kawaida, lakini pia mvulana mwenye madoa doa usoni akiwa na nywele zenye mchanganyiko wa wekundu na kahawia. Lakini baadaye akapata ngozi ya bluu kabla ya mshtuko na nywele zake nazo kugeukia weupe, ikiwa ni ma­tokeo ya maradhi ya nadra yanayoitwa argyria. Argyria au argyrosis ni hali inayo­sababishwa na wingi wa madini ya kemikali za fedha au vumbi la madini hayo. Dalili kubwa zaidi ya argyria ni kwamba ngozi hugeuka kuwa bluu, au zambarau au zambarau-kijivu. Katika kujaribu na kukabili maradhi ya ngozi yake usoni, Karason pia alianza kutumia dozi za ‘colloidal silver, ambazo ni za kimininika cha rangi ya fedha. Karason alikuwa na umri wa miaka 62 wakati alipofariki dunia Septemba 2013 katika Hospitali ya Washington, nchini Marekani, ambako alilazwa baada ya kuugua shambulio la moyo na baadaye kupata maradhi ya pneumonia na kiharusi kikali, hii ni kwa mujibu wa mkewe Anna Karason Rangi ya ngozi yake ilimpatia umaarufu kiasi cha kuitwa ‘Papa Smurf,’ neno ambalo, mjane wake anasema alilifurahia tu wakati lilipo­toka midomoni mwa watoto. Jina hilo la utani lililomaanisha kikaragosi mtu maarufu katika tel­evisheni cha rangi ya bluu, alilikubali kutegemeana na nani aliyelisema. Kwa mfano, iwapo ni mtoto aliyem­kimbilia akisema ‘Papa Smurf,’ utaona tabasamu likipamba katika uso wake, lakini iwapo linatoka mdomoni mwa mtu mzima, huwa hafurahii. Karason alivuma katika mitandao ya jamii kwa miaka kadhaa kwa kuwa na ngozi hiyo bluu chakavu kufuatia matumizi ya dozi kwa zaidi ya mwongo mmoja zilizolenga kutibu maradhi ya ngozi usoni mwake. Aliishi maisha ya kujitenga sana hadi alipojitokeza katika vipindi vya televisheni mwaa 2008 akianzia NBC kujadili hali yake hiyo inayojulikana kwa kitaalamu kama argyria. Karason alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 62 baada ya kutibiwa maradhi ya pneumonia katika hospitali ya Washington baada ya kuugua sham­bulio la moyo. Awali pia alikumbwa na kiharusi kikali,. Aidha, Mtandao wa Habari wa ABCNews ulimfanyia mahojiano Kara­son mwaka huo, wakati akiishi Oregon. Katika mahojiano hayo, alisema rangi yake ya ngozi bluu ilianza mwongo mmoja uliopita kabla ya hilo aliona tangazo katika jarida moja likiipigia chapuo ‘colloidal silver.’ Aakaondokea kuitumia sana kwa siku akiitengeneza mwenyewe nyumbani na hakuwa amebaini wakati mabadiliko ya ngozi yakijitokeza, hadi rafikiye wa zamani alipomtembelea na kumshtua. “Na aliniangalia na kusema, Ume­fanya nini usoni?’ ‘sina chochote usoni mwangu!” Karason alimjibu. Anasema: “Sawa, inaonekana umepaka kitu kama vipodozi au kitu fulani zambarau. Akaendelea kusema kwamba ile ngozi yangu ya awali haipo tena badala yake ana mwonekano mpya na hapo ndipo akashtuka. Wakati katika miezi hiyo ya awali, akiwa hajaona dalili ya mabadiliko ya ngozi yake bali aliyashuhudia katika afya yake. “Nilianza kuhisi baridi yabisi katika mabega yangu, hali ilikuwa mbaya, sikuweza kuvua fulana. Na kitu kilichofuata, baadaye hali ikatoweka mithiri ya homa ya vipindi,” anasema. Na iwapo aliamini colloidal silver ingemponya, Karason alisema, “Si­kuwa na shaka na hilo katika moyo wangu”
2
WABUNGE wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kurudisha zana za wavuvi zilizochukuliwa na kukamatwa wakati wa Operesheni Nzagamba II na wale walioziingiza nchini nyavu zenye saizi hizo ndogo wachukuliwe hatua.Wakichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa na Waziri Luhaga Mpina, wabunge wamesema nyavu zilizoharibiwa haziwezi kurudishwa, lakini injini za boti zinaweza kurudishwa.Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Christina Ishengoma alisema operesheni hiyo ya kutokomeza uvuvi haramu, ilisaidia kuongeza samaki, lakini akaomba waliohusika kuingiza nyavu zenye matundu madogo nchini wachukuliwe hatua.Alisema elimu pamoja na nyavu kuchomwa ni sawa, lakini akaomba walioingiza nchini nyavu hizo wachukuliwe hatua kutokana na kuwatia wavuvi hasara.Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (CCM) alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa ajili ya kulinda rasilimali hizo za nchi, lakini sera na sheria zilizokuwapo ziliathiri maisha ya wananchi kutokana na kuteketeza nyavu hizo.Alisema wananchi walinyang’anywa mashine na injini walizopata kwa jasho, hivyo inatakiwa warudishiwe mashine hizo ili waendelee na uvuvi na kulinda rasilimali za nchi kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.Alisema wizara inatakiwa kwenda mbali zaidi badala ya kuzuia kwa kuangalia saizi ya nyavu, zuio hilo linatakiwa kutolewa kwa vipindi, kuruhusu miezi kadhaa na kukataza mingine kuvua samaki.Alisema zuio limekuwa likifanyika nchini katika Ziwa Victoria, lakini nchi jirani za Kenya na Uganda, zimekuwa zikiendelea kuvua samaki ambao wanasafiri kutoka eneo moja hadi lingine na Tanzania kuendelea kupata hasara.Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) alitaka kujua wale waliochomewa nyavu zao katika operesheni hiyo serikali imeweka mkakati gani wa kuhakikisha wanafidiwa.Lakini pia alisema vifaa ambavyo bado vimeshikiliwa kama injini wanatakiwa kurudishiwa ili kuendelea kufanyia kazi.Mbunge wa Mtwara Mjini, Naftaha Nachuma (CUF) amesema operesheni hiyo ilisababisha nyavu za wavuvi wengi kuchomwa, lakini waliozileta nchini hawajachukuliwa hatua.Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba (CCM) alisema operesheni iliwahusu wananchi wake takribani asilimia 90, hivyo anaunga mkono serikali kupiga vita uvuvi haramu, lakini haungi mkono njia zilizotumika katika kufanya operesheni hiyo ambayo haikuzingatia sheria za nchi.Amesema operesheni hiyo ilihusisha pia vitendo vya rushwa kwani baadhi ya watendaji walitumia mwanya huo kupokea rushwa.Mbunge wa Viti Maalumu, Jacqueline Msongozi (CCM) alisema uvuvi haramu umeleta shida katika maeneo mbalimbali nchini.
3
Uongozi wa Simba umesema jana watampitia Niyonzima kwao Rwanda timu yao itakaporejea Jumamosi kutoka Afrika Kusini ilikopiga kambi kujiandaa na Ligi Kuu ya soka Tanzania bara msimu ujao.Niyonzima aliyemaliza mkataba na timu yake ya zamani ya Yanga amesaini mkataba wa miaka miwili Simba na kilichobaki ilikuwa kutambulishwa rasmi. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema jana Dar es Salaam Niyonzima sasa ni mchezaji wao halali wa Simba na wameshamalizana.“Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba. tumeshamalizana naye, anaweza akaenda Afrika Kusini kuungana na kikosi au akawahi kuja au tukampitia Rwanda kwani kikosi kitakuja na RwandAir,”alisema. Alisema mchezaji huyo anatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Simba Day dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Manara alisema mchezaji huyo alichelewa kujiunga na wenzake Afrika Kusini kwa kuwa alikuwa na mambo binafsi anayamalizia Rwanda na kwamba alikuwa akifanya mazoezi na timu ya APR. Manara pia alizungumzia tetesi za beki wao wa kati, Juuko Murshid kwenda Orlando Pirates ya Afrika Kusini akisema bado ni mchezaji wao na ana mkataba hivyo anayemhitaji akazungumze nao.Alisema wanaendelea na mazungumzo naye kuona namna ya kuboresha mkataba wake. Wakati huo huo, suala la mfadhili wa Simba, Mohamed Dewji kukabidhiwa timu linatarajiwa kupelekwa kwa wanachama kwenye mkutano mkuu Agosti 13, mwaka huu kabla ya mkutano wa kubadilisha Katiba yao Agosti 20, mwaka huu.Wakati Simba ikiwa kwenye mchakato wa kuzungumza na wanachama, wadhamini wa klabu hiyo walijitokeza kupinga timu kuendeshwa na mtu mmoja wakidai hiyo ni timu ya wanachama wote na si mtu mmoja.Akizungumzia madai ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Klabu, Manara alisema wanachama wana haki ya kutoa maoni lakini wanapaswa kutambua haki hiyo ina kiwango chake na utaratibu wake “Simba ina ‘platform’ ambayo wanachama wana haki ya kuzungumza kutoa maoni yao, kero na ushauri nayo ni mkutano mkuu ambao utasimamiwa na Kamati ya Utendaji kwa sababu viongozi wetu wakuu hawapo lakini wapo wanaokaimu,” alisema.Manara alisema anawaheshimu wazee hao na kuwaomba kuwa watulivu hasa kipindi hiki cha usajili ambacho wako kwenye maandalizi ya kuanza msimu mpya na Simba Day na kuwataka watumie busara na kuwaacha viongozi wafanye ya muhimu.Alisema wanahitaji kufanya vizuri msimu ujao kwa kutwaa ubingwa akihoji kuwa watachukuaje kama wanalumbana. Alisema ili kuelekea mabadiliko ya kuingia katika mfumo wa Kampuni na hisa wiki hii wataanza mchakato wa kutoa elimu kwa wanachama wake katika wilaya mbalimbali ili kujua faida zake kabla ya kuitisha mkutano wa Katiba Agosti 20, mwaka huu.Manara alisema kesho atatoa ratiba kamili ya safari hiyo ya mabadiliko ya kampuni. Alisema Simba imezindua rasmi wiki ya Simba kuelekea kilele cha maadhimisho ya sherehe yao, Simba Day Agosti 8.Hii ni mara ya pili Simba kuadhimisha siku hiyo iliyoanzishwa mwaka jana. Mwaka huu wataitumia kusaidia jamii na kutembelea makundi maalumu na kuwapa misaada. Akizungumzia siku hiyo jana, Mkurugenzi wa EAG Group, mshauri wa masoko na biashara Simba, Imani Kajura alisema katika kuadhimisha siku hiyo watafanya matukio ya kijamii wakianza na leo watakapozindua huduma mtaa kwa mtaa.
4
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM KIKOSI cha Yanga, kinatarajia kwenda Mwanza, Septemba 4 mwaka huu, kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wao wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco. Mchezo kati ya timu hizo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilitinga hatua hiyo, baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Township Rollers ya Botswana, kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1. Timu hizo zilipokutana Agosti 10,  Uwanja wa Taifa,  Yanga ililazimisha sare ya bao 1-1, lakini  zilipokutana katika mchezo wa marudiano uliochezwa Agosti 24 jijini Gaborone vijana hao wa  Jangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Salahe, alisema kwa sasa wanaendelea na programu ya mazoezi, huku wakipanga kwenda Mwanza kuweka kambi ya kuiwinda Zesco. “Timu inatarajia kwenda Mwanza, Septemba 4, kuweka kambi, lakini vile vile tutacheza kama mechi mbili za kirafiki ikiwemo pia dhidi ya Pamba  ili kujiweka fiti kabla ya kuvaana na Zesco,” alisema. Alisema wachezaji wao wanaoendelea na mazoezi ni wale ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu za taifa zinazojiandaa na michezo ya kusaka nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia. Hafidhi alisema mikakati wanayoipanga wanaamini itawasaidia kuendelea kupata matokeo mazuri na kusonga mbele. Tanzania  imesaliwa na timu mbili katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika(Caf), ambazo ni  Yanga inayoshiriki Ligi ya Mabingwa na Azam FC,  Kombe la Shirikisho. Awali ilikuwa na timu nne, nyingine ni Simba iliyokuwa inashiriki Ligi ya Mabingwa kabla ya kutupwa nje na UD Songo ya Msumbiji na KMC iliyoondolewa Kombe la Shirikisho na AS Kigali ya Rwanda.
4
    NAIROBI, KENYA NJAA na gharama za juu za maisha zimefanya wananchi kusahau janga la ufisadi linalolikumba taifa. Matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Utafiti la Ipsos, yamebainisha idadi kubwa ya Wakenya wanaamini njaa na bei kubwa ya bidhaa muhimu ndiyo matatizo makuu zaidi yanayoikumba nchi, ikilinganishwa na ufisadi. Utafiti huo uliofanywa kati ya Mei 11 na 23, mwaka huu, unaonyesha asilimia 36 ya Wakenya walitaja gharama kubwa ya maisha kuwa tatizo linaloikumba nchi, huku asilimia 21 wakiamini njaa ndiyo tatizo kuu. Kwa upande mwingine, ufisadi ulitajwa na asilimia 15 pekee ya Wakenya, wakifuatiwa na asilimia 13 waliosema tatizo kuu ni ukosefu wa ajira. Hali hiyo ni tofauti na ilivyokuwa Januari, kwamba asilimia 21 walikuwa wanaamini ufisadi ndio tatizo kuu, na asilimia 14 pekee wakati huo walisema njaa inatatiza zaidi. Hata hivyo, mchambuzi wa utafiti huo, Dk. Tom Wolf, alisema matokeo hayo hayamaanishi Wakenya wamesahau changamoto ya ufisadi unaoikumba nchi. “Ni kwa vile tu suala hilo halijapewa uzito ikilinganishwa na masuala mengine kama vile ukame na ukosefu wa chakula cha kutosha. Sababu ya hali hiyo huenda ni kutokana na vyombo vya habari kutoangazia zaidi ufisadi wakati huu,” alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Utafiti pia ulionyesha Nairobi inaongoza kwa idadi ya wanaokabiliwa na umasikini (asilimia 52), ikifuatwa na Pwani, Nyanza na Rift Valley kwa asilimia 46 kila eneo. Asilimia 45 ya waliohojiwa walisema hali hii inaweza kutatuliwa kwa kuongeza nafasi za ajira.
2
Kaijage aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.Alisema matokeo ya mchezo huo ni mazuri ingawa si mazuri sana, lakini cha msingi alikuwa akiangalia mambo ambayo anataka kuyafanya.Hivyo alisema kimsingi ni kwamba mechi hiyo imewapa changamoto ya kuweza kuona kama kuna makosa gani. “Lengo letu ni kucheza mchezo huu ili tuweze kuona makosa ambayo tukienda kwenye mashindano tujuwe tumerekebisha nini,” alisema Kaijage.Alisema katika mchezo huo ameona tatizo la umaliziaji alilosema ni tatizo la Tanzania, lakini atalifanyia kazi.“Sasa hivi nafikiri kutoka nyuma kuja mbele kumeanza kidogo kujengeka, lakini hapo mbele kwenye umaliziaji kama mlivyoona mpira, lakini hili ni tatizo la Tanzania katika ufungaji wa magoli ila nitalifanyia kazi, kucheza tumecheza kilichoshindikana ni ufungaji wa magoli,” alieleza Kaijage.Twiga Stars imepiga kambi kisiwani Unguja kujiandaa na Michezo ya Afrika inayotarajiwa kufanyika jijini Brazzaville katika Jamhuri ya Congo mwezi ujao.
4
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema litavifutia usajili vyama vyote vya michezo vilivyoshindwa kukidhi vigezo na sifa zilizowekwa kuendesha shughuli zao.Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga amesema jijini Dar es Salaam kuwa, sifa za vyama vya kitaifa ni pamoja na kuwa na ofisi inayotambulika, akaunti ya benki na mipango yao ya maendeleo.Amewaeleza waandishi wa habari kuwa, endapo chama kitakosa vitu hivyo, kitapoteza sifa ya kuwa cha kitaifa kinachotambulika.“Huwezi kuwa na chama cha kitaifa hakina ofisi, akaunti ya benki, hakina mipango wala hakitoi taarifa zozote za matumizi na mahesabu, wanatakiwa wafanye kazi zao kwa mujibu wa katiba,” amesema.Tenga aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) alizungumzia mikakati yao katika maendeleo ya kimichezo kuwa ni kufanya tathmini ya hali halisi ya michezo nchini.Pia, alisema wataendelea kufanya mapitio ya sera na sheria ya michezo iliyoundwa na BMT ili iendane na hali halisi, kufanya mikutano na wadau, kutoa mafunzo ya utawala bora, kuhamasisha ujenzi wa miundombinu na kuhakikisha vyama vya michezo vinaheshimu katiba zao.Aidha, Tenga alizungumzia umuhimu wa vyama vya michezo kushiriki katika shughuli za kijamii kama kusaidia kampeni za kitaifa za chanjo kwa watoto, kupambana na Ukimwi, kutokomeza malaria na kupiga vita dawa za kulevya.Aligusia pia suala la migogoro katika vyama mbalimbali vya michezo na mashirikisho na kuvitaka kuzingatia katiba zao kutafuta haki na kutatua changamoto hiyo.“Migogoro ni sumu ya maendeleo ya michezo kwa hiyo ni wajibu wetu tuondokane nayo ili kuwavutia mashabiki, wadhamini na washirika wengine tunaowahitaji kwa maendeleo ya michezo,” alisema.
4
Na ATHUMANI MOHAMED ELIMU kuhusu mafanikio haina mwisho. Kila siku tunapaswa kujifunza. Tunapaswa kupanua mawazo yetu mara kwa mara ili kujua namna ya kujitanua kimafanikio. Kwa asiye nacho ni nafasi yake ya kujifunza mbinu za kupata lakini hata kwa yule ambaye tayari anacho, anatakiwa kujifunza namna ya kulinda kile alichojaaliwa. Hiyo ndiyo sababu nimesema elimu ya mafanikio haina mwisho. Kama jana umejifunza, leo unatakiwa kujifunza tena na hata kesho pia uendelee kujifunza. Katika mada hii ambayo leo ni sehemu ya mwisho tunajifunza vitu au mambo ya hatari ya kukaa nayo mbali ili kujisogeza kwenye mafanikio. Ndugu zangu, tukubali au tukatae kuna vitu au mambo ambayo ukiwa nayo karibu basi unajiweka kwenye hatari ya kuingia kwenye matatizo ambayo yatakuchelewesha au kukusababishia ushindwe kutimiza malengo yako ya mafanikio. Ni kweli matatizo yapo kila siku na kuna wakati tunaweza kusema matatizo hayana taarifa, lakini kuna mengine ni kama tunajitakia wenyewe. Hapa tunajifunza yale ambayo tunapaswa kukaa nayo mbali ili tusizibe mianya ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio kwenye maisha yetu. Lakini nieleze jambo moja kubwa ambalo wengi wanalipuuza; tusibweteke, tusake maisha kwa nguvu zote. Vijana wengi kwa mfano wenye degree zao hawataki kusikia kazi ambazo siyo zenye hadhi. Wanataka kazi za ofisini tu. Sawa, umesomea labda mambo ya masoko, lakini mbele yako kuna kazi nyingine hata kama siyo ya ofisini lakini inalipa, kwanini usifanye kuliko kusubiri hiyo ya ofisini ambayo huna uhakika nayo leo? Hili somo nitalifafanua vizuri siku zijazo ambapo nitajitolea mfano mimi mwenyewe ambaye nimekubali kuweka degree yangu ndani na kujiajiri kwenye ujasiriamali. Sasa kwa leo tunamalizie somo letu, jiandae kwa somo hilo kwa undani wiki ijayo.   FUATA SHERIA ZA NCHI Ni vizuri sana kufuata sheria za nchi, maana tunaongozwa na utawala wa sheria. Ukivunja sheria maana yake unajiweka kwenye matatizo na kitakachofuata ni kushitakiwa mahakamani. Yapo makatazo ya wazi kisheria, mfano kuna watu wanaohangaika na wanafunzi, wakati sheria inazuia na wanajua wazi kuwa ukitiwa hatiani miaka 30 jela inakuhusu. Ni jambo la hatari. Kwanini uyatafute matatizo? Mtu mzima, una familia yako lakini unahangaika na watoto wa shule, kwanini? Au mwanafunzi yupo shule lakini akili yake iko kwenye mapenzi. Huko ni kujiharibia maisha yako yajayo. Tayari Rais Magufuli ameshasema, mwanafunzi ukipata mimba, hurudi tena shuleni. Kwanini ujitakie matatizo ya namna hiyo? Ishi kwa kuzingatia mambo ya msingi, ujijali mwenyewe na maisha yako yajayo. Mafanikio ni safari, lazima ukae mbali na vizingiti.   KUWA MAKINI NA MADENI Mikopo inaweza kukusaidia kufanikisha baadhi ya mipango yako, lakini inakupasa uwe nayo makini sana. Kukopa sana au kukopa fedha nyingi nje ya uwezo wako ni hatari. Kabla ya kukopa, tafakari kuhusu marejesho. Je, ni kweli utaweza kurudisha mkopo wako bila kuathiri mipango yako mingine? Kudaiwa sana kunaweza kukurudisha nyuma. Lakini lenye umuhimu zaidi ni kwamba kopa fedha kwa ajili ya kuzalisha. Ukizalisha inakuwa rahisi kurejesha, ingawa unaweza kukopa kwa ajili ya kununua aseti ila uwe makini na marejesho yasiwe makubwa juu ya uwezo wako na kukusababishia matatizo yatakayokurudisha nyuma. Maisha hayawezi kusonga bila kutumia akili nyingi, kufanya mambo kwa akili na maarifa ni bora na muhimu zaidi. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine. Ni mimi rafiki yako katika mafanikio, Athumani Mohamed. Wasalaam.
0
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro ameomba Serikali ya Tanzania na Morocco kuongeza ushirikiano kwa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ili kuongeza kasi ya ushirikiano na kuwa jukwaa madhubuti la kusimamia utekelezaji wa mikataba iliyopo ya ushirikiano.Alisema hayo kwenye hafla ya kumbukumbu ya miaka 20 ya uongozi wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco iliyofanyika Ubalozi wa Morocco jijini Dares Salaam, na kuhudhuriwa na mabalozi wanaowakilisha nchi mbali mbali nchini, wakuu wa mashirika ya kidiplomasia, maofisa wa Serikali ya Tanzania na wafanyakazi wa ubalozi huo. Dk Ndumbaro alisema Serikali ya Tanzania inajivunia ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili ambao unazidi kuimarika kila siku.“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli, natoa pongezi kwa Serikali ya Ufalme wa Morocco kwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya uongozi thabiti wa Mfalme Mohamed VI ambao umeleta maendeleo katika nyanja mbali mbali nchini humo na kufanikisha miradi ya ushirikiano nje ya nchi hiyo,” alisema. Alisema ziara ya kihistoria ya mfalme huyo aliyoifanya nchini Oktoba mwaka jana ilifungua ushirikiano baina ya nchi hizi katika sekta za kilimo, uvuvi, nishati, utalii, viwanda, reli, biashara, bima, afya, gesi, sayansi na utamaduni. Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi wa Morocco nchini, Abdellilah Benryane alisema “Kumbukumbu ya miaka 20 ya Mfalme Mohammed VI kwenye kiti cha enzi cha utukufu wake ni siku kubwa katika historia ya nchi yetu ya Morocco ambayo pia tunaitumia kujivunia na kufanya tathmini kubwa ya maendeleo yaliyopatikana chini ya utawala wake ikiwa ni nchi ya kisasa inayotekeleza misingi ya kidemokrasia.” Alisema kila mwaka katika kuadhimisha siku hiyo, wananchi wa Morocco wamekuwa wakitathmini kwa kuangalia Morocco mahali ilipotoka, mahali ilipo na inapoelekea na kutangaza mafanikio yaliyopatikana na mikakati ya kusonga mbele siku za usoni.Kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco, alisema ni mzuri na miradi yote ya ushirikiano iliyosainiwa na viongozi wa nchi hizi mbili, utekelezaji wake unaendelea vizuri. Alisema hivi karibuni ujumbe wa Morocco ulitembelea Tanzania kujadili mradi wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa soka wa Dodoma ambako ulikutana na Rais John Magufuli na watendaji wengine wa Serikali ya Tanzania. Kwa upande wa uchumi wa taifa hilo, alisema miaka 20 ya utawala wa Mfalme Mohammed VI imeshuhudia miradi mbali mbali mikubwa ya maendeleo ikianzishwa kama vile miradi ya barabara, bandari, viwanja vya ndege, mabwawa makubwa, mitambo ya nishati na viwanda vya kutengeneza vipuri vya magari na ndege. Alitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyoazishwa na kupata mafanikio makubwa katika kipindi cha mfalme huyo kuwa ni mradi wa bandari ya Tanger-Med iliyopo kaskazini mwa nchi hiyo, mradi wa kuzalisha nishati ya umeme wa Quarzazate na mradi wa treni ya mwendo kasi ambao umeunganisha maeneo mengi ya nchi hiyo. Mkakati wa Taifa wa nchi hiyo wa kukuza sekta ya utalii wa mwaka 2010 na Dira yake ya mwaka 2020 vimelenga kuvutia watalii milioni 20 kwa mwaka ifikapo mwakani 2020. Mkakati huo pamoja na dira hiyo ambavyo vilizinduliwa na Mfalme huyo kati ya mwaka 2001 na 2010, vimelenga pia kuwapatia wananchi wa Morocco makazi bora kwa gharama nafuu.Mikakati hiyo miwili imekuza uchumi wa nchi na kuboresha makazi kwa kiasi kikubwa, hivyo kuifanya Morocco kuwa moja ya nchi zinazoongoza kuvutia watalii barani Afrika na katika ukanda wa Mediterranean.
3
Na Johns Njozi Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) limetoa fomu maalumu kwa wale wanaohitaji kuwa mawakala wa wachezaji wa mpira wa miguu. Msemaji wa shirikisho hilo Clifford Ndimbo, amesema fomu hizo zinapatikana kwenye ofisi za (TFF) na tovuti ya shirikisho hilo na mtu anayetaka kuwa wakala wa mchezaji anapaswa kujaza fomu hizo ili aweze kupata kibali cha kufanya shughuli hizo. “Kwa wale mawakala wa wachezaji tunaofahamu kwamba taratibu zimebadilika kwa hiyo utaratibu mpya ndio tunaanza kuutumi na tayari fomu zimeanza kutolewa. Lakini moja kati ya vitu vinavyo kamilisha fomu hiyo kukamilika ni pamoja na ripoti ya Interpol ambayo itasaidia kujua masuala mbali mbali ya atakayejaza fomu,” alisema Ndimbo. Ndimbo ameongeza kwamba gharama za kupata kibali ni dola za kimarekani 2000 zaidi ya shilingi milioni nne za kitanzania kwa miaka miwili na baada ya hapo itakuwa inalipiwa dola za marekani 500 kila baada ya mwaka ambazo ni zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania kama ada ya kubadilisha kibali hicho kitakapoisha muda wake. Fomu hizo zinazopatikana kwenye tovuti ya (TFF), zinajazwa mtandaoni na mwisho wa kujaza na kuzirejesha fomu hizo ni Decemba, 30 mwaka huu.
4
  Hamisa Mobetto aliiwasha mitandao kwa picha maridadi siku baada ya kuonekana na gari la Diamond Ni dhahiri kuwa Hamissa ni Mobetto ni kati ya wasichana warembo zaidi si humu nchini Tanzania tu bali pia katika kanda ya Afrika Mashariki kwa jumla Uhusiano kati yake na Diamond huenda hautaisha hivi karibuni licha ya wawili hao kutangaza miaka miwili nyuma kuwa walitengana Licha ya kuachana na Diamond, inaonekakana kuwa urembo wake haumpi amani msani huyo Huku mianya ikizidi kuonekana katika uhusiano kati ya msanii Diamond Platinumz na mpenziwe raia wa Kenya Tanasha Donna, ukarimu na ukaribu unazungumziwa kati ya msanii huyo na mpenziwe wa zamani Hamissa Mobetto. I followed my Heart, And it led me here 🌊 . . Kimono – @2colections_dubai A post shared by HamisaMobetto (@hamisamobetto) on Feb 9, 2020 at 3:42am PST   Inadaiwa kuwa Diamond aliitoroka sherehe ya uzinduzi wa kanda uliondaliwa na Tanasha mjini Nairobi, hii ni baada ya wawili hao kutofautiana kwa jambo ambalo hadi sasa halijabainika. Wanavyosema wasemao, paka akitoka panya hutawala, Hamisa naye hajaona haja ya kusubiri hadi paka atoroke, tayari anautumia ufa uliopo kati ya wawili hao kutawala. Hivi majuzi, alioenekana akiliendesha gari la Diamond Platinumz, msanii huyo akiwa ndani. Mwanadada gani asiye na raha ya kuwa katika uhusiano na msanii wa hadhi ya Mondi? Hamissa anaonekana kurembeka zaidi na zaidi, hii ikikisiwa kuwa chambo kwa Diamond ili kurudi kwenye wavu wa mapenzi.   Picha aliyoichapisha katika ukurasa wake wa Instagram na kuiwasha mitandao ni thibitisho, urembo wake unanata ajabu. Wafuasi wake walioweza kuina picha hiyo waliajabia urembo wake, baadhi wakimshauri Mondi kurudi nyumbani na kuukarabati uhusiano wao. Inadaiwa kuwa Hamisa hana tatizo kuwa katika uhusiano na Mondo licha ya msanii huyo kuwa katika mahusiano mengine, kwake lilokuu ni kuhudumiwa zamu yake.
1
WAKAZI wa Makambako mkoani Njombe na viunga vyake wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole. Kampeni ya Mnada kwa Mnada ambayo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inashirikiana na kampuni za simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na mkoa ikiwa na lengo kwa wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA, Asajile John alisema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mji Mdogo wa Makambako kufika katika Viwanja vya Idara ya Maji kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA.Alisema katika kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ili kila mwananchi awe na namba ya Taifa au kuwa na kitambulisho kutokana ushirikiano na NIDA kuwa katika kampeni hiyo. Alisema kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda uliobakia ni mdogo.
3
BENJAMIN MASESE-MWANZA MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa imebaini utapeli na ukiukaji  mkubwa unaofanywa na mawakala kutoka kampuni mbalimbali za mawasiliano  nchini wakati wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole (biometric) unaoendelea. Kutokana na hali hiyo, TCRA imefanya operesheni ya kushtukiza katika Jiji la Mwanza na kuwakamata mawakala mitaani ambao  wanadaiwa kuhusika na utapeli kwa kusajili laini zinazojuliokana kwa jila la ‘Take away’  na kuwafikisha katika vituo vya polisi kwa hatua za kisheria. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo, alisema hatua hiyo imetokana na kupata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kutapeliwa fedha na mawakala hao sambamba na kusajili laini mbili na kuwauzia watu wengine ambao hufanyia uhalifu ikiwamo utapeli. Alisema kabla ya kufanya operesheni hiyo walijiridhisha kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa kwao na kulazimika kufanya msako nchi nzima kuanzia jana na kwa Mkoa wa Mwanza walifanikiwa kuwakamata mawakala zaidi ya 10. “Tunapozungumza hapa zoezi la kuwakamata linaendelea mitaani, tayari mawakala zaidi ya 10 tumewatia nguvuni kwa kushirikiana na polisi, kama TCRA tumechukua hatua zaidi kwa kuwaandikia barua kampuni zote na kuwapa masharti na vigezo vinavyotakiwa kwa mawakala hao.  “Kwanza ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na uthibitisho wa kuidhinishwa na mtoa huduma za mawasiliano, pili yeyote anayejihusisha na uuzaji, kusambaza au kusajili laini za simu anatakiwa kuwa na ofisi ya kutolea huduma ya usajili na si kutembea barabarani,” alisema Mihayo.
3
SERIKALI kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wamezindua mabaraza ya ujuzi ya kisekta ili kuwajengea uwezo wanavyuo kwenye soko la ajira.Akizindua mabaraza hayo Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema mabaraza hayo yatasaidia kupunguza tatizo la ujuzi katika nyanja mbalimbali za maendeleo.“Mabaraza haya yatasimamiawa na kuratibiwa na TPSF kwa kuwa wao wapo katika nafasi kubwa ya kuzalisha ajira,” alisema Profesa Ndalichako. Alisema mabaraza hayo yana nafasi nzuri ya kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025. “Napenda kutoa ombi kwa sekta binafsi kuendelea kuwapokea vijana au wanachuo wanaokuja kufanya mafunzo kwa vitendo (internship) ili kuwajengea uwezo na utayari wa kuingia kwenye soko la ajira,” alisema.Kwa upande wake, Mwenyeketi wa TPSF, Salum Shamte alisema mabaraza yatakuwa ni fursa pekee ya kuunganisha taasisi binafsi, serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka nje ya nchi katika kuleta ufanisi katika maendeleo. “Tumefikia hatua nzuri mpaka kuyazindua mabaraza haya ambayo yatakuwa chachu katika kuongeza ujuzi zaidi kwa wahitimu wa vyuo mbambali,” alisema Shamte.Shamte alisema, TPSF imekuwa ikitoa ushauri na mapendekezo mbalimbali kwa serikali kupitia Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) katika ngazi ya Wilaya, Mkoa, Wizara na hata Taifa ili yaweze kufanyiwa kazi.“Huu ni mwendelezo wa mambo ambayo serikali imekuwa ikiyafanya kwa kushirikiana na TPSF kwani huko nyuma tumekuwa na majadiliano mengi yenye tija kwa mustakabali wa ustawi wa uchumi wa Tanzania,” alisema.Aidha, katika hatua nyingine, Shamte alisema mabaraza hayo yatajikita katika sekta kuu sita ambazo ni Kilimo, Utalii, Tehama, Uchukuzi, Ujenzi na Nishati, hali ambayo itaongeza ushirikishwaji mpana kwa wadau katika kukuza ujuzi nchini.Kuanzishwa kwa mabaraza hayo kumeungwa mkono na wadau mbalimbali huku wakieleza ni kwa namna gani yatakwenda kusaidia katika mnyororo mzima wa kukuza ujuzi nchini.Fabian Mwakatuma ambaye ni mjumbe katika sekta ya kilimo alisema mpango mkakati wa ubia wa serikali na TPSF utasaidia sana kupunguza changamoto ya wajuzi katika sekta mbalimbali “Watu wanaohitimu Stashahada na Shahada ni wengi kwa sasa hapa nchini, lakini wengi wao hawana ujuzi na kushindwa kuleta ushindaji katika soko la ajira, hivyo uwepo wa mabaraza haya utawaongezea thamani wahitimu wa vyuo mbalimbali,” alisema Mwakatuma.Profesa Preksedis Ndomba kwa upande wake alisema huu ni mpango wa pili wa serikali wa kuhakikisha kunakuwa na viwanda na rasilimali yenye weledi katika sekta mbalimbali.“Ujuzi ni jambo ambalo ni mtambuka kwani linagusa maeneo mengi ya kisekta hivyo mabaraza haya yanakwenda kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kiuchumi na viwanda,” alisema Profesa Ndomba. Serikali na TPSF wamekuwa na majadiliano ya mara kwa mara katika kuhakikisha baadhi ya changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi ili kuimarisha mazingira rafiki kwa upande wa uwekezaji hali ambayo imeleta mafanikio makubwa.
3
Na LEONARD MANG’OHA DAR ES SALAAM LICHA ya taarifa za Benki ya Dunia (WB) kuonyesha kuwa pato la chini zaidi kwa mtu mmoja kwa mwaka linapaswa kuwa dola za Marekani 3,000, kwa hapa nchini pato hilo ni kati ya dola 900 na 1,000, hali inayotajwa kusababisha Watanzania wengi kulalamikia ugumu wa maisha. Kauli hiyo ilitolewa na Meneja Takwimu za Pato la Taifa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Daniel Masolwa, katika maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Masolwa alisema ikiwa Taifa litafanikiwa kuimarisha sekta muhimu kama vile kilimo na viwanda, ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa Watanzania walio wengi, itawezesha kufikia malengo hayo ya WB na kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi. “Tunatakiwa kutoka katika kilimo cha jembe la mkono na kwenda katika kilimo kinachozalisha kwa kiwango kikubwa kinatakachotosheleza mahitaji ya chakula na kuhakikisha mazao yanayozalishwa yasiuzwe yakiwa ghafi, badala yake yaongezwe thamani kwa kuyasindika na kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi. “Suala la viwanda ni la lazima kwa sababu usipokuwa na viwanda unageuka kuwa soko la bidhaa za wengine, hivyo ni lazima kuanzisha viwanda na kutafuta masoko ya ndani na nje kwa ajili ya mazao ya wakulima,” alisema Masolwa. Aliongeza kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa kilimo kimechangia asilimia 29 ya pato la taifa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, hivyo kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha katika robo ya mwisho ya mwaka huu, ni wazi kuwa pato la Taifa litatetereka kutokana na uzalishaji wa mazao ya kilimo kutegemewa kushuka. “Tunapopambana kukuza uchumi tunapaswa pia kuzingatia umuhimu wa kutunza mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira, unaochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi ili kuendelea kuwa na mazingira yanayoruhusu kufanya shughuli za kilimo,” alisema Masolwa. Mmoja wa wakufunzi waandamizi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dk. Camillus Kassala, alisema mfumo wa ugawaji wa pato la taifa ndio unaosababisha kuwapo kwa tofauti kubwa ya pato kati ya mtu mmoja na mwingine. “Ili kupata mgawanyo mzuri, ni lazima kujua unakusanya kiasi gani na idadi ya watu ulionao ambao ndio wahitaji”. Kassala alisema takwimu nyingi zinakusanywa bila kuzingatia kanuni 10 muhimu za kukusanya takwimu. “Ndiyo maana sasa tunataka kila mtu anayekusanya takwimu awe amesoma walau ngazi ya awali ya ukusanyaji takwimu,” alisema Kassala.
3
Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari UNAWEZA kusema hali si shwari tena duniani kutokana na virusi vya corona kuendelea kusambaa na kufika katika nchi takribani 40 huku mataifa mbalimbali yakionekana kuchukua hatua za kujifungia mipaka. Athari pia imeonekana wazi kwenye uchumi baada ya masoko kuendelea kuanguka katika maeneo mbalimbali duniani. Wakati mataifa mbalimbali duniani yakiendelea kuchukua hatua za kujilinda kwa kujifungia mipaka na watu waliokuwa China vilikoanzia virusi hivyo, Nigeria na nchi tano  nazo tayari zimekumbwa na upepo huo mbaya.   Jana Nigeria ilithibitisha kuwepo kwa mtu mmoja mwenye maambukizi ya virusi vya corona na hivyo kuingia katika orodha ya nchi tatu barani Afrika baada ya Misri na Algeria. Mgonjwa huyo, raia wa Italia anayefanya kazi nchini Nigeria inaelezwa alisafiri kwa ndege kwenda mji wa kibiashara wa Lagos akitokea Milan  Februari 25. Mamlaka zinasema anaendelea vizuri na hakuna dalili ya hatari na hivi sasa anapatiwa matibabu hospitalini jijini Lagos. Mamlaka zimesema zimeanza kuwatambua wale wote waliokaribiana naye tangu aliporejea Nigeria. Zaidi ya watu 80,000 wameripotiwa kuathirika katika nchi 40 na  zaidi ya watu 60 wamepoteza maisha nje ya China ingawa idadi ya maambukizi nchini humo imeendelea kushuka. NCHI ZAZIDI KUFUNGA MIPAKA Nchi ya India nayo imetangaza kuchukua hatua inayofanana na ile ilichokuliwa mwanzo kabisa na Marekani na nchi nyingine za Ulaya  ya kupiga marufuku raia waliokuwa China kuingia nchini humo. Katika taarifa yake India imeeleza kuwa raia yeyote wa kigeni aliyekuwa China baada ya Januari 15, 2020 hataruhusiwa kuingia nchini humo kupitia usafiri wa anga, barabara au majini na katika mipaka yake yote na nchi za Nepal, Bangldesh na Myanmar. Hatua hiyo ya India imekuja baada ya ile ya Saudi Arabia ya kuzuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, ikiwemo wanaotembelea miji mitakatifu katika dini ya Kiislamu – Makka na Madina. Bado haijajulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai iwapo itaathirika na zuio hilo kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona duniani. Urusi nayo ilikuwa ni miongoni mwa nchi za mwanzo kutangaza kufunga mipaka yake na China kama njia ya kujilinda na maambukizi ya virusi hivyo. Mapema hivi karibuni Urusi pia ilitangaza kuzuia raia wa Iran kuingia nchini humo. Urusi pia ilisema itazuia raia wa Korea Kusini kuingia nchini humo kuanzia Machi 1. Nchi hizo zote mbili, Iran na Korea Kusini zimeshambuliwa na virusi hivyo. Mamlaka ya nchini Iran inasema virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 24 hadi sasa,  huku idadi ya walioathirika ikiwa ni karibu ya 250. Jana Wizara ya Afya ilitangaza kufuta sala ya Ijumaa katika miji mikubwa yote. Waislamu wanasali mara tano kwa siku, lakini sala ya Ijumaa inaonekana kama ni muhimu sana. Korea Kusini kwa upande wake imetoa rekodi inayoonyesha watu 2,000 wameathirika na virusi hivyo huku 13 wakipoteza maisha. Urusi pia imezuia raia wa China kuingia nchini humo. Afrika Kusini nayo inaonekana kutaka kuelekea njia hiyo hiyo, kutokana na uamuzi wa Rais wake, Cyril Ramaphosa wa kuwaondoa raia wa Afrika Kusini 132 wanaoishi mjini Wuhan nchini China. Uamuzi ulitangazwa siku ya Alhamisi baada ya kikao cha baraza la mawaziri kutokana na maombi ya wana familia wa raia hao wanaoishi Wuhan. Haikuelezwa ni lini wataondoshwa huko lakini serikali imesema raia 132 kati ya 199 wanaishi mjini Wuhan wameomba warejee nyumbani. Hakuna kati yao aliyegundulika kuathirika na virusi au kuwa na dalili za ugonjwa huo, lakini watawekwa  karantini kwa siku 21 watakapowasili nchini Afrika Kusini kama ”hatua ya tahadhari”, ofisi ya rais imetangaza. Sanjali na hilo, Shirika la ndege la Afrika Kusini limesitisha safari za moja kwa moja kwenda China. ATHARI KWENYE MASOKO Wakati kukiwa na orodha ya mashirika kadhaa ya ndege yaliyotangaza kusitisha safari zake nchini China kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo, Shirika la ndege la nchini Uingereza la EasyJet  limesitisha pia baadhi ya safari zake nchini Italia ambako virusi hivyo vimeonekana kutikisa na kusababisha vifo na maambukizi kwa watu kadhaa. Katika taarifa yake iliyotolewa jana EasyJet ilisema imesitisha baadhi ya safari zake za ndani na nje ya Italia na katika mataifa mengine ya Ulaya kutokana na mlipuko wa virusi hivyo. EasyJet pia imesema itapunguza matumizi yake, ikiwa ni pamoja na mishahara, kusitisha kuajiri watu wengine na kutoa mafunzo. Shirika la ndege la British Airways nalo linatarajia kusitisha baadhi ya safari zake katika nchi za Italia, Singapore, na Korea Kusini. Shirika hilo la ndege limesema pia litasitisha safari za kwenda na kurudi 56  kutoka katika viwanja vya ndege vya Heathrow na Gatwick  na nyingine  kadhaa za Italia ikiwamo Milan, Bologna, Venice  na Turin kati ya Machi 14 – 28. Pia itasitisha safari za kurudi sita kutoka Heathrow kwenda Singapore kila baada ya siku nyingine hadi Machi 15  ambapo itakuwepo safasi moja tu kwa siku Wakati huo huo, Soko la hisa la Australia  Ijumaa – lilishuka kwa 3.3% hadi 6,441. ASX200 imeanguka zaidi ya 10% tangu rekodi yake ya hivi karibuni ya 7,162 Alhamisi iliyopita. Hili ndilo  anguko kubwa la kila wiki kwa soko la Australia tangu mwaka 2008, wakati wa  mtikisiko wa uchumi duniani. NCHI TANO ZATHIBITISHA MAAMBUKIZI MAPYA Nchi za New Zealand,  Netherlands, Belarus, Nigeria na  Lithuania zimethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya corona. Hali hiyo inaonyesha kitisho cha kuendelea kuenea kwa virusi hivyo katika nchi nyingine duniani. MASHINDANO YASITISHWA Umoja wa nchi za Kiarabu umesitisha mashindano ya fainali za baiskeli kwa mwaka huu wa 2020 baada ya Waitaliano wawili wanaoshiriki kwenye timu  kuonekena kuambukizwa virusi hivyo. Waitaliano hao sasa wanachunguzwa. Wengine waliokaribiana na Waitaliano hao watawekwa chini ya uangalizi. MICHUANO YA OLYIPIKI HATARINI Waandaaji wa mashindano ya Olimpiki kwa mwaka huu wa 2020,  Japan  wamesema watatangaza wakati wowote wiki ijayo juu ya mipango ya michezo hiyo katika wakati huu ambako virusi vya corona vimeendelea kuwa tatizo la kidunia. Tayari watu nane wamefariki dunia nchini Japan, huku karibu 200 wakiwa wameathirika na virusi hivyo ( maambukizi hayo ni mbali na yale ya kwenye meli ya Diamond Princess).
2
PARIS, UFARANSA MSHAMBULIAJI wa timu ya PSG, Neymar Jr, juzi aliungana na timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu na kufanikiwa kuifungia bao la pekee katika dakika za lala salama kwenye mchezo dhidi ya Strasbourg. Neymar alikuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kutokana na kusumbuliwa na majeruhi pamoja na kushinikiza kutaka kuondoka kwa matajiri hao. Neymar aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa timu hiyo hivyo mashabiki na viongozi walifikia makubaliano ya mchezaji huyo kuondoka, lakini hadi dirisha la usajili ilinafungwa Septemba 2, hakuna timu ambayo ilifikia makubaliano na uongozi wa PSG juu ya uhamisho huo. Mbali na kushindikana kwa uhamisho wake, bado mashabiki wanamtaka mchezaji huyo kuondoka, hivyo kwa mara ya kwanza tangu kufunguliwa kwa msimu mchezaji juzi alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha PSG ikiwa ni mchezo wao wa tano wa ligi. Mchezo huo ambao PSG walikuwa nyumbani, ulionekana kuwa mgumu, lakini Neymar alifanikiwa kuifungia bao la ufundi wa hali ya juu huku zikiwa zimebakia sekunde mchezo huo kumalizika. Muda mwingi mashabiki walikuwa wanamzomea mchezaji huyo kila akigusa mpira, wengine walionekana akiwa wamebeba mabango ya kumtaka aondoke, lakini kelele zao alizinyamazisha kwa bao la tikitaka na kuifanya PSG iondoke na pointi tatu. “Kila mmoja anajua kwamba nilitaka kuondoka, niliweka wazi na sitaki nilizungumzia hilo kwa kuwa kuna watu nitawaumiza, lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa PSG na lengo langu ni kuwa na furaha nikiwa uwanjani. “Niliweka wazi kuwa, sina chochote kwa PSG wala mashabiki, lakini kunizomea kwao ni mambo binafsi, lakini hayo yote yamepita na sasa tunaangalia mbele na hii ni mara ya kwanza na mwisho kuzungumzia suala la uhamisho wangu, ninachokiangalia sasa ni PSG, nitahakikisha ninarudi kwenye ubora wangu kwa ajili ya timu,” alisema Neymar.
4
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema Serikali itatumia muda mwingi kadri itakavyoona inafaa ili kujiridhisha na manufaa ambayo taifa litapata kabla ya kusaini mikataba ya sekta ya nishati, hususani ya mafuta na gesi.Ameyasema hayo wakati akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Maurel & Prom kutoka Ufaransa, wanaotafiti na kuchimba gesi eneo la Mnazi Bay.Waziri Kalemani ametoa msimamo huo wa Serikali baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa kampuni hiyo iliyowasilishwa na Makamu Mkurugenzi Mkuu, Elias Kilembe ambayo pamoja na mambo mengine, waliomba serikali iharakishe mchakato wa utiaji saini mikataba ya uwekezaji zaidi katika sekta husika, ambayo walishiwasilisha.Waziri Kalemani alisema, serikali haikusudii kumchelewesha mwekezaji bali kinachofanyika ni kujiridhisha hatua kwa hatua, namna taifa litakavyonufaika."Tutatumia muda wa kutosha kujiridhisha, hata kama ni miaka 40, lakini lazima mikataba iwe na manufaa. Huo ndiyo msimamo wa serikali," alisema na kuongeza:"Sisi tunapenda wawekezaji, tunataka waendelee kuwekeza ili tupate manufaa ya gesi na mafuta, lakini tusiibiwe".Aidha, katika ziara hiyo, Waziri Kalemani aliutaka uongozi wa kampuni hiyo kuchukua hatua stahiki za makusudi na haraka katika kudhibiti changamoto ya maji ya bahari kusogea karibu zaidi na kisima cha gesi cha Mnazi Bay, hivyo kuwepo hofu ya maji hayo kuingia kwenye kisima husika.Vilevile, Waziri alipongeza ukamilishwaji wa mfumo wa kuunganisha visima vyote vya gesi vya Mnazi Bay, hali ambayo alieleza itasaidia katika kuimarisha ukaguzi na udhibiti."Naagiza, kuanzia sasa kila gesi inayotoka katika visima vilivyopo, ipite kwenye mfumo huu mpya ili ituwezeshe kujua ni kiasi gani imetoka na kiasi gani kilipwe," alieleza.Akikagua Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, ulio chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Waziri alipongeza kazi nzuri inayofanywa na shirika hilo na kuwataka waongeze bidii zaidi katika usimamiaji wa rasilimali hizo za mafuta na gesi kwa manufaa ya watanzania.Katika ziara hiyo, Waziri pia alikagua utekelezaji wa miradi ya umeme iliyo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika Mtaa wa Ufukoni na Mbae Mashariki, Manispaa ya Mtwara; ambapo aliwaagiza viongozi wa shirika hilo katika maeneo hayo, kuhakikisha wananchi wote waliolipia umeme wanaunganishiwa huduma hiyo ifikapo Desemba 20 mwaka huu.Aidha, alitoa maagizo kwa mameneja wote wa Tanesco nchi nzima kuwa tarehe ya mwisho kuwaunganishia wananchi waliolipia umeme ni Desemba 31 mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
5
Mwandishi Wetu, Mbeya RAIS Dk. John Magufuli, amewataka waajiri na wamiliki wa sehemu za kazi wote kuzingatia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 pamoja na sheria nyingine za kazi ili kuboresha mazingira ya kazi hapa nchini. Kauli hiyo aliitoa wiki hii alipowahutubia wafanyakazi na wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Sokoine kusherehekea siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi). “Lakini kuhusu uboreshaji wa mazingira na usalama sehemu za kazi natoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanazingatia sheria za kazi ikiwemo Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi. Aidha, waajiri hawana budi kutekeleza matakwa mengine ya kisheria ikiwamo kutoa mikataba ya ajira na kuruhusu uwepo wa vyama vya wafanyakazi katika sehemu za kazi,” alisema Magufuli. Kauli yake hiyo ilikuwa inajibu hoja mbalimbali zilizotolewa na hotuba ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), katika hotuba yao iliyowasilishwa katika sherehe hizo na Katibu Mkuu wake, Dk. Yahya Msigwa, aliyesema uwapo wa baadhi ya waajiri ambao hawazingatii masharti ya afya na usalama mahali pa kazi kama Sheria ya Osha inavyoelekeza. Pia suala hilo la uzingatiaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi lilielezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, aliyoiwasilisha katika sherehe hizo na alifafanua juu ya tozo mbalimbali za Osha zilizoondolewa ili kuboresha mazingira ya biashara miongoni mwa wawekezaji. “Nafurahi kukwambia sisi katika ofisi ya Waziri Mkuu tuliwaagiza Osha wahakikishe wanaondoa tozo zote ambazo ni kero. Kwa mwaka wa fedha unaoishia mwaka huu, tayari Osha wameshaondoa tozo zifuatazo; tozo ya usajili iliyokuwa inaanzia shilingi 50,000 hadi 1,800,000, ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi, wamefuta pia faini zilizokuwa zinahusiana na vifaa vya kuzimia moto shilingi 500,000, tumeondoa ada ya leseni kwa matakwa ya sheria na tumewaambia Osha watafanya kazi hiyo kwa kuwa Serikali imewaajiri hawana tena nafasi ya kuendelea kukusanya tozo ya leseni, lakini watawajibika kuendelea kutoa leseni kwa waajiri wanaofuata masharti ya kulinda afya na usalama mahali pa kazi,” alisema Mhagama.
3
['Vioja vya shabiki sugu wa timu ya taifa Tanzania katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika - Bongo Zozo amewaacha wengi hoi katika mitandao ya kijamii nchini humo baadhi wakiguswa na ushabiki wake kwa timu hiyo.', ' Ametoa matumaini kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo licha ya kipigo cha 2-0 walichopokea Taifa Stars katika mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri dhidi ya Senegal siku ya Jumapili.', 'Bongo Zozo, kama anavyojiita katika mitandao ya kijamii ikiwemo You Tube, anaonekana katika mojawapo ya kanda ya video iliosambaa mitandaoni akitembea mjini Cairo akiwa amevaa jezi huku akipeperusha bendera ya Tanzania huku akizungumzwa kiswahili na mashabiki wengine wa Tanzania.', 'Nchini kwenye Tanzania kwenyewe, picha zake zimesambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwemo hata makundi ya Whatsapp.', 'Baadhi wakifurahia namna Bongo Zozo anavyozungumza kiswahili na kuimba wimbo wa taifa.', 'Ni swali wanaloniuliza watu wengi "Mzungu mswahili ametuzidi uzalendo" baadhi wakiandika katika mitandao ya kijamii.', 'Bongo Zozo - ambaye jina lake halisi ni Nick Reynolds - alizaliwa Zimbabwe na kuwahi kuishi Tanzania kabla ya kuhamia Uingereza.', 'Ameeleza kwamba anazipenda Tanzania na Zimbabwe mataifa yalio karibu sana moyoni mwake.', '"Mimi ni shabiki wa timu mbili Ya Zimbabwe na timu ya Tanzania\'', 'Anasema anaishabikia Zimbabwe sababu ndiko alikolizaliwa Zimbabwe, na Tanzania kwa upendo alio nao kwa taifa hilo. ', "'Napenda na navutiwa sana na mpira wa Afrika lakini sanasana mpira wa Tanzania, sababu kuna fujo isiyoumiza. Yaani watu tuna kelele sana kuliko (mashabiki wa timu nyingine) watu.'", 'Hatahivyo anaongeza kuwa Kenya pia ni timu anayoishabikia kwasababu zote ni timu za Afrika mashariki kiashiria cha kwamba watu wote ni wamoja.', '"Nimeishi Tanzania kwa muda wa miaka kumi na minane tangu mwaka 98 hivi, nilikutana na mwanamke nikamuoa alafu basi nimekuwa Mtanzania," amesema.', 'Anasema anafurahia sana Tanzania kufuzu katika mashindano ya kombe la mataifa mwaka huu baada ya kusubiri kwa miaka 39."', 'Je kura anaitupa wapi katika mpambano wa Alhamisi wa Taifa stars dhidi ya Harambee stars ya Kenya?', "'Tanzania lazima tuwakung'ute (Kenya)'.", "'Sema nitalia machozi hata ya damu kama ni droo - sababu kama tunashindwa kuwafunga Kenya, naombeni mutufunge sababu ikiwa droo basi hatufuzu sisi (Tanzania) na Kenya haiwezi kufuzu' anaeleza Nick."]
4
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Kigoma imeendesha kikao chake cha kwanza cha mashauriano na wadau tangu kuanzishwa kwake rasmi na Jaji Mkuu wa Tanzania kwa Tangazo la Serikali Namba 112 la Februari 1, 2019. Akifungua kikao hicho juzi katika Jengo la Hakimu Mkazi Kigoma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Ilvin Mugeta, aliwasilisha maeneo makuu matatu katika kuhakikisha kanda hiyo inakuwa ya mfano kwa kumaliza mashauri kwa wakati ili kuondokana na mrundikano wa kesi na kupunguza idadi ya mahabusu magerezani.“Baadhi ya maeneo yenye changamoto ni baadhi ya wadau wetu kutotimiza wajibu ipasavyo, mawasiliano yasiyoridhisha baina ya mtu na mtu, taasisi kwa taasisi na uwezo mdogo wa wadau wetu katika upelelezi, mambo ambayo yanakwamisha azma yetu ya upatikanaji wa haki kwa wakati,” alisema.Jaji Mugeta alitaka kanda hiyo kuwa na mwelekeo sahihi wa namna bora itakayoleta matokeo chanya na kuweka mfumo wa uwajibikaji wa pamoja na viwango vya kupimika katika utendaji kazi wa kila siku.Aidha, aliwataka wajumbe kufungua milango ya mawasiliano ili waweze kufikiana kwa wakati na kupeana taarifa stahiki pamoja na kutambua wajibu wao na kuongeza kuwa upelelezi unapochukua muda mrefu hupelekea kupotea kwa haki za watu. Akisoma taarifa ya Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Naibu Msajili wa kanda hiyo, Hussein Mushi, alisema tangu kuanzishwa kwake Februari hadi Julai mwaka huu, masjala ya Mahakama hiyo imesajili mashauri 59 ya jinai, kati yake 12 yameamuliwa na 47 yamebaki. Aidha, kamati ya kusukuma mashauri Kanda ya Kigoma kwa pamoja walikubaliana kushirikiana katika kuhakikisha wanaondokana na mlundikano wa mashauri na mahabusu kwa kila mdau kutimiza wajibu wake kikamilifu. Baada ya kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kutembelea jengo la Mahakama Kuu lililopo katika eneo la Bangwe mkabala na Shule ya Sekondari Kigoma, ambalo liko katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni Jaji Mfawidhi wa Kanda, Naibu Msajili, Mtendaji wa Mahakama-Kigoma, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mkuu wa Mashtaka Kigoma, Mkuu wa Magereza mkoa, wawakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa polisi, Mkuu wa Upelelezi, Mkuu wa Gereza la Bangwe na Katibu wa Jukwaa la Mawakili wa Kujitegemea Kigoma.
3
Ramadhan hassan – Dodoma MKUU wa Shule ya Sekondari Dodoma, Amani Mfaume, amesema hakuna mwanafunzi ambaye atapata mimba katika shule hiyo na kuendelea na masomo. Kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa ambayo imekuwa ikisambazwa katika makundi ya WhatsApp kwamba kuna wanafunzi nane katika shule hiyo wamepewa ujauzito. Akizungumza na MTANZANIA juzi jijini hapa, Mfaume alisema suala la wanafunzi kupewa mimba huwa linatokea mara moja moja, lakini wanaotakiwa kutoa taarifa ni Ofisi ya Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma. Alisema taarifa za wanafunzi nane kupewa mimba si za kweli, na kwamba utaratibu wao kama mwanafunzi amepata ujauzito, ni kupelekwa nyumbani moja kwa moja. “Wanapata mimba kwa sababu hatukai nao muda wote, mfano walikuwa likizo, huko nyumbani nani alikuwa akiwaangalia? Akipatia mimba nyumbani utanibana mimi tena au utaibana shule? Nenda hospitali walipopima uliza utaambiwa, mimi siwezi kusema kitu. “Hatuwezi kufundisha wajawazito, sisi ni shule yenye nidhamu kubwa sana, kuna watu wanatuchafua tu, hali ya elimu ilikuwa mbaya, lakini tumejitahidi kupunguza ziro kwa kiasi kikubwa. “Mwaka 2017 kidato cha nne kulikuwa kuna ziro 69, mwaka  2018 kulikuwa kuna ziro 67 ila mwaka jana tuna ziro 19 tu, tumejitahidi na tunaendelea kujitahidi,” alisema Mfaume. Kuhusu shule kuwa katikati ya Jiji na kukosa uzio, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRL), Masanja Kadogosa aliahidi kujenga uzio wakati wa mahafali ya Novemba mwaka jana na Jumamosi ya wiki iliyopita alifika kutimiza ahadi yake. Alisema sababu ya kuahidi ni kutokana na kusoma katika shule hiyo hivyo kuamua kurudisha shukrani. “Ameishakuja na hivi karibuni itaanza kujengwa, lakini pia wazazi na walezi kuna kiasi cha fedha wamechanga, tutajenga uzio kama maagizo ya Jafo (Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo) aliyoyatoa kwetu,” alisema Mfaume. Kuhusu wanafunzi kuzagaa mitaani wakati wa masomo, alisema jambo hilo si la kweli na kwamba wanafunzi huwa wanatoka kwa ruhusa maalumu. “Ni wivu tu, unaona hiki kifaa, hapa mwanafuzi anabonyeza ndio anatoka kwenda mfano kanisani au msikitini, sisi hatufanyi kazi kwa kubahatisha, tunaijua kazi yetu na mimi nashangaa kauli hizi zinatoka wapi,” alisema Mfaume. Pia, alisema wameendelea kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita kutokana na walimu kujitoa pamoja na kusimamia nidhamu. “Kama huna nidhamu huwezi kusoma kwetu, sisi ni wafuasi wa nidhamu, ndiyo maana matokeo yetu ya kidato cha sita yanakuwa mazuri, hao wanaozusha huo uzushi, wanaohusika wawachukulie hatua kali za kisheria,” alisema Mfaume.
3
*Simba yatafuta pa kutokea kwa Stand baada ya kipigo NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM VIGOGO wa soka nchini, Yanga na Azam FC, leo watashuka dimbani katika viwanja tofauti kuendeleza dozi ya vipigo katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, huku majeruhi, Simba wakisaka pointi muhimu zitakazorejesha heshima baada ya kipigo kutoka kwa watani wao wa jadi. Vinara wa ligi hiyo, Yanga, wanafukuzana na Azam kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 12, baada ya kucheza mechi nne, lakini wakitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, watakuwa ugenini kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ligi hiyo, wakitarajiwa kuchuana vikali na wenyeji wao, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 2-0 msimu uliopita kwenye uwanja huo. Akizungumzia pambano hilo, Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Van Der Pluijm, amesema mchezo huo unahitaji wachezaji wake kutumia akili nyingi uwanjani kuhakikisha wanavuna pointi muhimu, ambazo zitawawezesha kubaki kileleni mwa ligi hiyo. “Hatuna shaka kwa upande wa maandalizi yetu kuelekea mchezo huo, kwani tangu kuanza kwa Ligi Kuu kikosi kimekuwa bora na matokeo yamekuwa mazuri ya kuridhisha, hivyo hatuna sababu ya kupunguza kasi tuliyoanza nayo,” alisema. Kwa upande wa Azam, wenye rekodi nzuri ya kuchomoza na ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex, watakuwa wenyeji wa Coastal Union, ambao walianza vibaya ligi hiyo kwa kufungwa mechi mbili na kulazimishwa sare mara mbili. Upinzani uliopo Ligi Kuu msimu huu umeanza kumpa wasiwasi kocha Mwingereza, Stewart Hall wa Azam, ambao umemfanya aanze kuwatupia lawama baadhi ya waamuzi wanaochezesha, akidai wanavuruga viwango vya wachezaji wake uwanjani. Simba wanakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Stand United, ambao wamejiimarisha nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi sita katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wekundu hao wa Msimbazi waliojikusanyia pointi tisa, wameshuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya Jumamosi iliyopita kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu wao, Yanga. Kocha Mwingereza wa Simba, Dylan Kerr, ambaye hesabu zake za ushindi zilivurugika na kuambulia kipigo dhidi ya Yanga, atalazimika kufanya kazi ya ziada kwenye safu ya ulinzi ambayo ilimwangusha katika mechi hiyo ili kuondoa makosa yaliyojitokeza. Msimu uliopita Simba walishindwa kufurukuta mbele ya Stand United, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani na baadaye kuambulia kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa marudiano, uliochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, ambao wanautumia msimu huu, kutokana na kutokamilika kwa ukarabati unaoendelea Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. JKT Ruvu, ambao hawajaonja ladha ya ushindi katika mechi nne walizocheza, kwa mara ya kwanza kikosi hicho kitashuka dimbani chini ya kocha msaidizi, Aziishi Kondo baada ya Felix Minziro kudaiwa kuachia ngazi. ‘Wanalizombe’ Majimaji watawakaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea, wakati mkoani Tanga Uwanja wa Mkwakwani unatarajiwa kuwaka moto pale timu za African Sports na Mgambo Shooting zitakapochuana vikali. Maafande wa Tanzania Prisons ambao wamezinduka msimu huu wakinolewa na kocha Salum Mayanga, watakuwa wenyeji wa Mwadui FC kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, wakisaka ushindi mwingine nyumbani baada ya kushinda mechi mbili walizocheza uwanjani hapo.
4
HASSAN DAUDI NA MITANDAO HAIJALISHI una shida zinazoweza kujaza mfuko mkubwa kiasi gani, linapokuja suala la uhai, acha kabisa. Kama hujui, hiyo si kwa binadamu tu, hakuna kiumbe kisichoujua utamu wa kuendelea kuvuta pumzi. Kuliweka sawa hilo, ni tukio la hivi karibuni mjini Istanbul, Uturuki, ambapo mbwa amejikuta akiingia katika duka la dawa baada ya kuumia akiwa kwenye mihangaiko yake. Wengi wameonekana kuvutiwa na kipande cha video kinachomuonesha mbwa akipata matibabu, lakini iliwashangaza zaidi baada ya kusikia kuwa alikwenda mwenyewe, tofauti na wengine ambao hupelekwa na wamiliki wao. Aliyefichua kuwa aliingia bila usaidizi wa binadamu ni video iliyonaswa na kamera za duka hilo, ambayo inamuonesha mbwa huyo akiwa amesimama mlangoni, kana kwamba alikuwa akiomba msaada. Akisimulia ilivyokuwa siku hiyo, mhudumu wa duka hilo, Banu Cengiz, anasema: “Alikuwa ananitazama. Nilimuuliza, ‘mtoto, kuna tatizo lolote?” Cengiz anasema kwa kuwa yeye ni mpenzi wa wanyama, alimpa bakuli ya maji, akidhani alikuwa akisumbuliwa na kiu, lakini mbwa huyo alimpa mguu wake wa mbele. Hapo ndipo Cengiz alipohisi mbwa huyo ameumia na alipomchunguza alibaini kuwa alikuwa na jeraha lililokuwa likivuja damu. “Nilipompa kitanda, badala ya kwenda kulala, aliendelea kusisimama usawa niliokuwa, hadi pale nilipomaliza kumtibu,” anasema Cengiz. Katika huduma yake, Banu, ambaye duka lake lina chumba maalumu kwa mapumziko ya mbwa wa mitaani, anasema alianza kwa kulisafisha jeraha kwa dawa, kabla ya kumpaka nyingine kwa ajili ya kuzuia wadudu. “Nilipomaliza, alilala chini, ishara fulani hivi kama kushukuru, utadhani alikuwa akiniambia ‘nakuamini’,” anaeleza mwanamama Cengiz. Baada ya matibabu, mbwa jike huyo alipumzika dukani hapo kwa muda, kabla ya kuondoka zake. Akizungumzia umuhimu wa kuwasaidia wanyama, Cengiz anasema: “Huwa nafanya hivyo kwa sababu nao wana hisia. Tunapaswa kuwasaidia wale wenye uhitaji. Watu wanatakiwa kuwafundisha watoto wao juu ya kuwapenda na kuwaheshimu wanyama. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuishi pamoja katika ulimwengu mzuri kabisa.” Aidha, video hiyo imewavutia walio wengi, huku baadhi wakielekeza shukurani na pongezi zao kwa Cengiz, wakisema alikuwa na utu kumsaidia mbwa huyo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, mmoja kati ya walioitazama video hiyo, Shivam Kumar, anaandika: “Utu upo kwa sababu ya wewe mama. Shukurani kwa wema wako kwa ulimwengu huu.” Wakati huo huo, huko mitandaoni wapo walioonekana kuwasifia wanyama aina ya mbwa, wakisema wana akili hata kuliko baadhi ya binadamu. Hao ni wale walioandika ‘Mbwa kiboko yao’, ‘Huwa napenda mbwa, wakati mwingine ndiyo navutiwa na binadamu’.
2
Katika mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya, timu hiyo iliibuka kidedea dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, Yanga. City iliweka kambi Sumbawanga ambapo imedai kambi ya huko inatosha kuwamaliza wapinzani wao.Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha wa Mbeya City Kinna Phiri alisema mchezo wao dhidi ya Yanga utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao hao kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao, lakini hawatakubali kuwa ngazi. “Tumefanya maandalizi mazuri na tumerudi kutoka Sumbawanga, ambako tuliweka kambi ya siku tano na kucheza michezo minne ya kirafiki, ambayo tulishinda yote,” alisema Phiri.Pia alisema wanaendelea na mazoezi makali kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi ya kesho watakayohakikisha wanarudi Mbeya na pointi tatu. “Sisi tunachotaka ni kuwafunga tu, haijalishi kama hatuwi mabingwa au hatushuki. Tunataka kulinda heshima kwa kuwafunga mabingwa watetezi itakuwa heshima nzuri kwani hatutaki kuwa ngazi ya ubingwa ya Yanga,” alisema. Mbeya City inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza michezo 28.
4
Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM CHAMA Cha wafugaji Tanzania (CWT), kimeiomba Serikali kuwaruhusu kuingiza mifugo yao katika hifadhi za taifa kwa dharura ili kuinusuru kutokana na ukame unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Wafugaji hao walisema hali ya ukame imekuwa tishio na tayari wamepoteza mifugo mingi inayokufa kwa njaa baada ya majani kukauka kutokana na kukosa mvua kwa muda mrefu. Sambamba na hilo, pia wamealaani matukio ya kuuawa kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini, likiwamo lililotokea hivi karibuni wilayani Arumeru mkoani Arusha ambako watu wanne wamepoteza maisha na wengine watano kujeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi za moto na askari wa Suma JKT. Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa CWT, Magembe Makoye, alisema Serikali ilichukulie suala la ukame kuwa ni dharura na hivyo iwaruhusu kuingiza mifugo ili kupata chakula katika hifadhi hizo na baada ya ukame kupungua mifugo hiyo irudishwe maeneo yake ya awali. “Tunaiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na ile ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuangalia namna ya kuwasaidia wafugaji ili kunusuru mifugo yao ambayo ndiyo uchumi wao na taifa kwa ujumla. “Katika hili, tunashauri wafugaji waruhusiwe kuingiza mifugo hiyo japo mara mbili kwa wiki, wakati wakisubiri mvua kunyesha,” alisema Makoye. Kuhusu mauaji, Makoye alisema kuwa ni ya ukandamizaji dhidi ya wafugaji. “Upo utaratibu wa kisheria wa kuwaondoa wafugaji katika maeneo yasiyo rasmi, lakini si kwa kuwapiga risasi na kuwaua,” alisema Makoye. Aidha Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Francis Nzuki, alisema kuwaua wafugaji na hata makundi mengine ni uvunjifu wa haki za binadamu jambo ambalo hawatalifumbia macho. Katika hatua nyingine, Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), umeikumbusha Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia wananchi Katiba mpya kama ilivyokubaliwa katika mkutano wa haki za binadamu uliofanyika Geneva, Uswisi. Katika mkutano huo uliohusisha pia asasi za kiraia na THBUB, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengulumwa, alisema Tanzania iliridhia mapendekezo 133, likiwamo la kutengeneza Katiba mpya ya wananchi.
3
Nyemo Malecela-Bukoba WATOTO 301 wenye umri chini ya siku nane na mama 22 wamepoteza maisha katika kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu mkoani Kagera. Takwimu hizo zimetolewa na Mratibu wa Huduma za Afya za Mama na Mtoto mkoani Kagera, Neema Kyamba alipokuwa akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu mjini hapa. Alisema takwimu hizo zinaonekana kuwa kubwa zaidi katika Manispaa ya Bukoba kwani katika kipindi hicho cha Januari hadi Mei mwaka huu watoto 39 wenye umri chini ya siku nane na mama watatu wamepoteza maisha. Amezitaja sababu za kutokea kwa vifo hivyo kuwa ni kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, upungufu mkubwa wa damu kwa mjamzito. Sababu nyingine ni kifafa cha mimba, maambukizi mbalimbali wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kama vile malaria ambayo pia usababisha upungufu wa damu, lishe duni na minyoo. Neema alisema kuwa vifo hivyo havitabiriki kwani ni hali inayotokea ghafla ambapo muhudumu anaweza kushindwa kugundua kama mama atapoteza maisha. Kwa upande wa watoto, idadi hiyo pia inajumuisha waliozaliwa wafu. Akizungumzia sababu ya vifo hivyo vya watoto, Neema  alisema; “chochote kibaya kinachomtokea mama mjamzito kinaathiri uhai wa mtoto.” Neema alisema kwa Januari hadi Mei mwaka huu asilimia 79 ya wajawazito mkoani Kagera wamejifungua katika vituo vya afya wakati asilimia zilizobakia walijifungulia njiani na nyumbani. “Katika asilimia 21 za wanawake waliojifungulia nyumbani na njiani, kulitokea vifo vya mama watatu ambao walijifungulia nyumbani. “Kwa mwaka 2016 vimetokea vifo 61, mwaka 2017 vimetokea vifo 73, mwaka 2018 vimetokea vifo 65 kwa akina mama wakati kwa watoto mwaka 2016 vimetokea vifo 1,043, mwaka 2017 vimetokea vifo 1,007 na mwaka 2018 vimetokea vifo 979,” alisema. Neema amewataka wajawazito kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito. “Katika mahudhurio angalu manne mama huyu atasaidia wahudumu wa afya kubaini vidokezo hatarishi wakati wa kujifungua, lakini pia wataweza kumpa ushauri wa namna ya kuchukua tahadhari katika kipindi cha ujauzito,” alisema Neema. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Marco Mbata, alisema kuwa Manispaa ya Bukoba inaonekana kuwa na idadi kubwa ya vifo vya mama na watoto kutokana na uwepo wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa hasa kwa watoto wachanga. “Ikumbukwe mama wanaoletwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matatizo ya ujauzito, pia watoto wanaokuwa tumboni mwao wanakuwa kwenye hatari ya kuchoka au kushindwa kupumua, hivyo matokeo yanaweza kusababisha kumwokoa mtoto au kushindwa kumwokoa. “Pia watoto wanaoletwa katika hali isiyo nzuri kutokana na kuchelewa kwenye jamii au vituo vingine wakati huo manispaa hakuna kituo cha watoto wachanga, kwani kituo cha afya kinachotakiwa kuwahudumia watoto wachanga lazima kiwe kinatoa huduma ya upasuaji,” alifafanua Mbata. Aliongeza kuwa manispaa inajenga kituo cha afya cha Zamzam ili kupunguza mzigo kwa Hospitali ya Rufaa kwani kitatoa huduma ya upasuaji kwa wajawazito pamoja na watoto wachanga.
0
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene amepongeza utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kulitaka kuendelea kusimamia sheria na taratibu katika kutekeleza majukumu yake ili kufi kia malengo ya taifa.Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo na kuzungumza na menejimenti ya NEMC jijini Dar es Salaam jana, Simbachawene alisema mbali ya kuridhishwa na kazi za baraza anategemea kupata ushirikiano mkubwa.“Nahitaji ushirikiano wenu ili niweze kufanikisha majukumu niliyokabidhiwa na Rais John Magufuli ya kusimamia mazingira hapa nchini,” alisema Simbachawene ambaye aliambatana na naibu wake waziri, Musa Sima.“Matumaini yangu kwa baraza ni makubwa kutokana na hali na utayari wa watendaji wake katika kutekeleza majukumu yao na kuifanya nchi kubaki katika hali ya mazingira endelevu.”Alisema jukumu la kutunza mazingira ni la kila Mtanzania, hivyo akalitaka baraza hilo kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi umuhimu wa mazingira na athari zake endapo tahadhari hazitachukuliwa.“Mimi bado mgeni katika wizara hii hivyo nategemea kujifunza zaidi kutoka kwenu watendaji wa baraza hivyo ushirikiano wenu kwangu ndio utaniwezesha kuelewa kwa haraka mambo yote yanayofanywa ili twende sambamba katika utekelezaji wa majukumu,” alisema.Waziri huyo alisema ana uzoefu wa muda mrefu katika uongozi lakini wizara aliyopewa ni mpya kwake na ina changamoto nyingi kutokana na umuhimu wa utunzaji wa mazingira kutokana na kuongezeka shughuli za kibinadamu hivyo kuna kila sababu ya kujifunza zaidi ili kuweza kusimamia kikamilifu mazingira yawe salama kwa kizazi cha sasa na baadaye.Aidha, Simbachawene alielezwa changamoto za kiutendaji za baraza na kuagiza waziainishe na kuwasilisha wizarani ili zipatiwe ufumbuziliweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.“Kumekuwa na lawama nyingi za kiutendaji katika kutoa vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira kwa wawekezaji, hivyo kwa kuwasilisha changamoto zetu wizarani na kufanyiwa kazi nina uhakika hazitakuwapo tena na kutachochea ongezeko la wawekezaji,” alisema.Simbachawene aliitaka NEMC iende sambamba na azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 na kumtaka kila mtumishi katika eneo lake kuondoa vikwazo, upungufu na changamoto zilizopo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka, mbali ya kumpongeza Simbachawene kwa kuteuliwa kwake, alimuahidi kumpa ushirikiano ili aweze kufikia malengo aliyojiwekea.“Changamoto kubwa inayolikabili baraza ni upungufu wa wafanyakazi hali inayochangia ucheleweshaji wa baadhi ya kazi kutokana na mtu mmoja kukabidhiwa miradi mingi ambayo ndani ya muda mfupi inahitaji yote ikamilishwe, hii ndio sababu ya lawama kutoka kwa wawekezaji,” alisema.Alisema baraza hilo lina mpango wa kuanzisha kampeni ya kukagua miradi na viwanda vyote nchi nzima ili kubaini kama vipo kisheria na vinazingatia na kufuata sheria za mazingira.
3
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba leo watakuwa ugenini jijini Arusha dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema, atawapumzisha baadhi ya wachezaji waliocheza dhidi ya Yanga ili wawe fiti kwa mechi ijayo dhidi ya Azam FC.Simba itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na morali ya hali ya juu baada ya kumfunga mtani wake wa jadi, Yanga bao 1-0 katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki iliyopita.Simba na Lyon zinapokutana hupambana, kila mmoja akionesha ubora wake kumkazia mwenzake. Wekundu hao hawataisahau Lyon aliwahi kuwaharibia rekodi msimu wa mwaka juzi kwa kupigwa 1-0 kwenye uwanja wa Uhuru, baada ya kucheza michezo karibu 13 bila kupoteza.Lakini kwa kipindi kile Simba haikuwa na kikosi bora kama cha sasa, wanaonekana kiufundi wako vizuri zaidi ukilinganisha na Lyon ambao wako kwenye wakati mgumu wa kutaka kushuka daraja.Mechi ya leo ni kiporo cha raundi ya kwanza kwa Simba huku Lyon ikicheza mechi yake ya mzunguko wa pili, mechi ya kwanza mabingwa watetezi Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.Mpaka sasa Simba imecheza michezo 16, imeshinda 12, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja ikiwa na pointi 39. Lyon imecheza michezo 26, imeshinda minne, sare tisa na kupoteza 13 ikishika mkia kwa pointi 21.Bila shaka hautakuwa mchezo rahisi kwa kila mmoja, Simba inahitaji pointi tatu kuendeleza rekodi yake ya ushindi na kuwa katika nafasi nzuri ya kutetea taji na Lyon inahitaji kupambana kupata pointi tatu ili kujinusuru katika ukanda wa kushuka daraja.Lyon itakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia washambuaji hatari wa Simba akiwemo Meddie Kagere mwenye mabao tisa, Emmanuel Okwi na John Bocco kila mmoja akiwa na mabao saba.Si hao tu kuna mchezaji hatari kama Zana Coulibaly ambaye mara nyingi amekuwa akipandisha mashambulizi na kutengeneza krosi za hatari na hata kuingia eneo la kufunga.Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema muhimu katika mchezo huo ni pointi tatu ingawa anaona kuna changamoto ya uwanja kutokuwa imara.“Changamoto ninayoiona ni uwanja lakini tutakabiliana nao kupata kile tunachokitaka,” alisema na kuongeza kuwa anatarajia kuwapa nafasi wachezaji wote na kuwapumzisha wengine kutokana na ugumu wa ratiba.Alisema anatarajia mashabiki wengi watajitokeza kwani anaamini kila mkoa wanaoenda wako wengi na kuwaahidi kuwapa raha. Mchezaji wa African Lyon, Jabir Aziz alisema wamejipanga vizuri kuwakabili Simba lengo lao ni kuhakikisha wanafanya vizuri.“Tunaingia tukiwaheshimu wapinzani wetu ni wazuri na ndio wawakilishi wetu wa nchi kwenye michuano ya kimataifa, tumejipanga kupambana nao lengo letu ni pointi tatu,” alisema.
4
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema wizara hiyo inatarajia kuisuka upya Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) ishirikiane moja kwa moja na wadau kutangaza utalii kimkakati.Alisema pia itaundwa bodi shirikishi ya kusimamia fedha za kuendeleza utalii nchini, Tourism Development Levy ( TDL) ili wadau hao waweze kushauri juu ya mipango na matumizi ya fedha hizo katika kutangaza utalii.Naibu Waziri Kanyasu wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa masuala ya utalii, madini, usafirishaji, viwanda na biashara, uwekezaji  na mazingira kilichofanyika jijini Arusha.Kikao hicho kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kilihudhuriwa na Mawaziri na naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mambo ya Ndani ya Nchi, Biashara na Viwanda, Uwekezaji, Muungano na Mazingira, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu.Kanyasu alisema ushirikishwaji huo wa wadau utachagiza ongezeko la watalii kwa kufanya sekta binafsi wanaofanya kazi na watalii kila siku kuwa mstari wa mbele katika kutangaza utalii ndani na nje ya nchi.Alisema ushirikishwaji huo wa moja kwa moja utawapa nguvu wadau wa utalii kushiriki kwa wingi katika maonesho ya kimataifa tofauti na ilivyo sasa.Kanyasu alisema ushirikishwaji huo unaweza kuibadili TTB ya sasa kuwa na mbinu mpya za kunadi vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa sasa.Kanyasu aliwahakikishia wadau hao malalamiko dhidi ya tozo ya leseni ya utalii ( TALA) yataangaliwa upya kwa upande wa hoteli ili kila mdau aweze kulipa kulingana na hadhi ya hoteli anayoimiliki.Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Utalii, (TATO) Willy Chamburo alisema kuwa utangazaji utalii unaofanywa na TTB kwa sasa hauwezi kuwa na ufanisi bila ya kuwa na ushirikishwaji na wadau.Alisema TTB imekuwa ikiwashirikisha wadau kwa kuwaalika maonesho ya kimataifa sio kama washiriki.Mwenyekiti huyo alilalamikia tozo 36 wanazotozwa katika sekta ya utalii kuwa zimekuwa zikiwaletea usumbufu mkubwa hivyo alishauri serikali kuziunganisha zote ili waweze kuzilipa kwa mara moja.
5
WIZARA ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa kupunguza vifo vya akinamama na watoto kwa kufikisha huduma za afya vijijini karibu na wananchi.Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Harusi Said Suleiman akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Viti maalumu Vijana na Wanawake, Viwe Khamis aliyetaka kujua mikakati ya kupunguza vifo vya akinamama.Alisema vifo vya wajawazito vimepungua kutoka 237 hadi kufikia vifo 219 kati ya vizazi hai 100,000 mwaka 2015/17.Aliyataja mafanikio hayo yanatokana na elimu kubwa inayotolewa kwa wajawazito kuhakikisha wanajifungua katika vituo vya afya na kuhudumiwa na madaktari wenye sifa.Alisema mengine yanatokana na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya vijijini kote katika kila wilaya Unguja na Pemba ambavyo huduma za kujifungua kwa akinamama zinapatikana.Alisema kasi ya usambazaji na matumizi ya vyandarua vya kupambana na ugonjwa wa Malaria kwa akinamama imesaidia sana kupunguza vifo vya akinamama na watoto.''Hiyo ndiyo siri kubwa ya kupunguza vifo vya wajawazito. Kasi ya ujenzi wa vituo vya afya na elimu juu ya kujifungulia hospitalini,'' alisema.Aidha alisema vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 79 hadi 56 kati ya vizazi hai 10,000 vilivyotokea katika mwaka 2015-2017. Suleiman alisema juhudi za kupambana na kupunguza vifo vya akinamama na watoto zitaendelea katika mpango wa ugatuzi wa kufikisha huduma za jamii kwa wananchi.Alisema tangu kutangazwa kwa mpango wa ugatuzi wa kufikisha huduma muhimu za afya Halmashauri za Wilaya, mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kuimarishwa kwa vituo vya afya ambavyo hutumiwa na akinamama.
3
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
5
End of preview. Expand in Data Studio

SwahiliNewsClassification

An MTEB dataset
Massive Text Embedding Benchmark

Dataset for Swahili News Classification, categorized with 6 domains (Local News (Kitaifa), International News (Kimataifa), Finance News (Uchumi), Health News (Afya), Sports News (Michezo), and Entertainment News (Burudani)). Building and Optimizing Swahili Language Models: Techniques, Embeddings, and Datasets

Task category t2c
Domains News, Written
Reference https://huggingface.co/datasets/Mollel/SwahiliNewsClassification

How to evaluate on this task

You can evaluate an embedding model on this dataset using the following code:

import mteb

task = mteb.get_task("SwahiliNewsClassification")
evaluator = mteb.MTEB([task])

model = mteb.get_model(YOUR_MODEL)
evaluator.run(model)

To learn more about how to run models on mteb task check out the GitHub repository.

Citation

If you use this dataset, please cite the dataset as well as mteb, as this dataset likely includes additional processing as a part of the MMTEB Contribution.


@inproceedings{davis2020swahili,
  author = {Davis, David},
  doi = {10.5281/zenodo.5514203},
  publisher = {Zenodo},
  title = {Swahili: News Classification Dataset (0.2)},
  url = {https://doi.org/10.5281/zenodo.5514203},
  year = {2020},
}


@article{enevoldsen2025mmtebmassivemultilingualtext,
  title={MMTEB: Massive Multilingual Text Embedding Benchmark},
  author={Kenneth Enevoldsen and Isaac Chung and Imene Kerboua and Márton Kardos and Ashwin Mathur and David Stap and Jay Gala and Wissam Siblini and Dominik Krzemiński and Genta Indra Winata and Saba Sturua and Saiteja Utpala and Mathieu Ciancone and Marion Schaeffer and Gabriel Sequeira and Diganta Misra and Shreeya Dhakal and Jonathan Rystrøm and Roman Solomatin and Ömer Çağatan and Akash Kundu and Martin Bernstorff and Shitao Xiao and Akshita Sukhlecha and Bhavish Pahwa and Rafał Poświata and Kranthi Kiran GV and Shawon Ashraf and Daniel Auras and Björn Plüster and Jan Philipp Harries and Loïc Magne and Isabelle Mohr and Mariya Hendriksen and Dawei Zhu and Hippolyte Gisserot-Boukhlef and Tom Aarsen and Jan Kostkan and Konrad Wojtasik and Taemin Lee and Marek Šuppa and Crystina Zhang and Roberta Rocca and Mohammed Hamdy and Andrianos Michail and John Yang and Manuel Faysse and Aleksei Vatolin and Nandan Thakur and Manan Dey and Dipam Vasani and Pranjal Chitale and Simone Tedeschi and Nguyen Tai and Artem Snegirev and Michael Günther and Mengzhou Xia and Weijia Shi and Xing Han Lù and Jordan Clive and Gayatri Krishnakumar and Anna Maksimova and Silvan Wehrli and Maria Tikhonova and Henil Panchal and Aleksandr Abramov and Malte Ostendorff and Zheng Liu and Simon Clematide and Lester James Miranda and Alena Fenogenova and Guangyu Song and Ruqiya Bin Safi and Wen-Ding Li and Alessia Borghini and Federico Cassano and Hongjin Su and Jimmy Lin and Howard Yen and Lasse Hansen and Sara Hooker and Chenghao Xiao and Vaibhav Adlakha and Orion Weller and Siva Reddy and Niklas Muennighoff},
  publisher = {arXiv},
  journal={arXiv preprint arXiv:2502.13595},
  year={2025},
  url={https://arxiv.org/abs/2502.13595},
  doi = {10.48550/arXiv.2502.13595},
}

@article{muennighoff2022mteb,
  author = {Muennighoff, Niklas and Tazi, Nouamane and Magne, Loïc and Reimers, Nils},
  title = {MTEB: Massive Text Embedding Benchmark},
  publisher = {arXiv},
  journal={arXiv preprint arXiv:2210.07316},
  year = {2022}
  url = {https://arxiv.org/abs/2210.07316},
  doi = {10.48550/ARXIV.2210.07316},
}

Dataset Statistics

Dataset Statistics

The following code contains the descriptive statistics from the task. These can also be obtained using:

import mteb

task = mteb.get_task("SwahiliNewsClassification")

desc_stats = task.metadata.descriptive_stats
{}

This dataset card was automatically generated using MTEB

Downloads last month
5

Papers for mteb/SwahiliNewsClassification