name
stringclasses
429 values
text
stringlengths
0
767k
null
Matangazo Katika jitihada ya kupata ahadi bora za uchangiaji wa fedha kwa mataifa yaliondelea kwa ajili kukabiliana na athari za kimazingira. Rasimu ya makubaliano ya mwisho ya Jana Ijumaa ilionesha ahadi ya dola bilioni 250 kila mwaka hadi ifikapo 2035, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya lengo la awali la dola bilioni 10...
null
Matangazo Wakati zaidi ya asilimia 99 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa, Georgescu anaongoza kwa kupata asilimia 23 ya kura akifuatiwa na mgombea wa mrengo wa kati kulia Elena Lasconi huku Waziri Mkuu Marcel Ciolacu, aliyekuwa akipigiwa upatu kushinda, akishikilia nafasi ya tatu. Hesabu ya hivi karibuni inaonyesha kuw...
null
China imetangaza hatua mpya zinazolenga kuimarisha biashara ya kigeni, huku Beijing ikipambana kuboresha uchumi wake unaozidi kutishiwa na sera zinazotarajiwa kuwa za uhasama za Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump. Uchumi huo wa pili kwa ukubwa duniani umekuwa ukipambana kufufuka tangu mlipuko wa janga la UVIKO-19, n...
null
Ilipendekeza ufadhili wa dola bilioni 250 kwa mwaka ifikapo 2035 kutoka kwa nchi tajiri kuelekea nchi maskini. Kiasi hicho cha fedha kinaziridhisha nchi zitakazokuwa zikizitoa, lakini sio zile zitakazokuwa zikipokea. Soma pia:Azerbaijan kutoa pendekezo jipya la ufadhili wa tabianchi Ni zaidi ya mara mbili ya lengo la a...
null
Siasa20.11.2024 Matangazo ya MchanaTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video59:59Siasahttps://p.dw.com/p/4nCHtNakili kiunganishiMatangazo
null
Rais wa China Xi Jinping, ameanzisha kampeni madhubuti ya kidiplomasia kuifanya nchi yake kuwa kinara wa utandawazi na ushirikiano wa kimataifa, katika ulinganisho na ajenga ya Donald Trump ya kutanguliza maslahi ya Marekani, baada ya Mrepublican huyo kuchaguliwa tena kwa muhula wa miaka minne. soma: Rais Xi Jinping aa...
null
Matangazo Iran imetangaza kuwa itafanya mazungumzo ya nyuklia na nchi tatu za Ulaya — Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza — wiki ijayo mjini Geneva. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 29 na yatahusu mzozo wa mpango wa nyuklia wa Iran, kufuatia azimio lililopitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti w...
null
Matangazo Katika ziara hiyo iliyolenga kuakisi uhusiano wa karibu, urafiki, ushirikiano, na mshikamano kati ya Morocco na China, Xi, alikutana na Mwanamfalme Moulay ElHassanhe. China imekuwa ikiwekeza zaidi katika miundombinu ya Morocco hasa reli katika miaka ya hivi karibuni. Morocco inavutia wafanyabiashara wa China ...
null
Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano ulimwengu unapoadhimisha Siku ya Mtoto Duniani, inatoa mitazamo tofauti, inayoonesha maendeleo katika afya na elimu ya mtoto, lakini pia inaibua wasiwasi kuhusu changamoto zinazotokana na hali ya hewa. Watoto wanakabiliwa na maelfu ya migogoro Katika taarifa ya kuashiria kutolewa kwa ri...
null
Kabla ya uteuzi wake, Jenerali Maiga alihudumu kama msemaji wa serikali ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ambayo imegubikwa na machafuko ya itikadi kali na ya makundi yanayotaka kujitenga. Mali imeongozwa na jeshi baada ya mapinduzi yaliyofuatana ya mwaka wa 2020 na 2021. Uteuzi wake kuchukua nafasi ya waziri mkuu wa k...
null
Putin amezionya nchi za Magharibi kuwa Moscow inaweza kujibu mashambulizi hayo. Ametangaza kuwa Urusi imetumia aina mpya ya kombora la masafa ya kati, kushambulia kituo cha kijeshi cha Ukraine. Putin amesema, baada ya idhini kutoka kwa serikali ya Joe Biden, Ukraine iliipiga Urusi na makombora sita yaliyotengenezwa na ...
null
Rais Filipe Nyusi amemualika Venancio Mondlane ofisini kwake mjini Maputo Novemba 26 baada ya vifo vya watu kadhaa katika ukandamizaji wa polisi dhidi ya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9. Soma pia:Upinzani nchini Msumbiji kuomboleza vifo vya watu 50 kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi Mondlane, mg...
null
Matangazo Mawaziri hao wa G7 watajadili pia juu ya waranti wa kukamatwa iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkuu wa kijeshi wa kundi la Hamas, na athari zinazoweza kujitokeza katika vita vya sasa vya Gaza na Lebanon. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anto...
null
Waandamanaji nchini Pakistan wanaoshinikiza kuachiliwa kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan wamewaua maafisa wanne wa vikosi vya usalama vya taifa hilo, huku umati wa waandamanaji ukikaidi amri ya polisi na kufunga njia ya katikati mwa mji mkuu.Makubaliano ya kusitisha yafikiwa Pakistan baada ya watu 82 kuuliwa Waziri ...
null
Urusi imerusha kombora la masafa marefukutoka mkoa wake wa Astrakhan katika shambulio dhidi ya Ukraine, ikiwa ni matumizi ya kwanza ya silaha yenye nguvu kubwa zaidi katika vita hivi, wakati mvutano ukiongezeka baada ya Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa kutumia makombora kutoka Marekani na Uingereza. Kombora hilo...
null
Uamuzi huo wa kuongeza muda wa vikosi vya mataifa ya kusini mwa Afrika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo umefikiwa katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare, wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC uliofanyika hapo jana Jumatano. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ni miomngoni mwa nc...
null
Wawakilishi na wapatanishi kutoka nchi 175 wanakutana leo mjini Busan nchini Korea Kusini katika jitihada ya mwisho kuandaa mkataba wa kushughulikia mgogoro wa uchafuzi wa plastiki duniani. Hii ni mara ya tano mataifa ya dunia yanakutana kuandaa mkataba wenye mafungamano ya kisheria. Mbali na wajumbe wa mataifa tofauti...
null
Matangazo Ulijiri miezi mitatu baada ya WHO mwezi Agosti kutangaza dharura ya afya kutokana na kusambaa kwa mpox, ikifahamika awali kama homa ya nyani, barani Afrika. Soma pia:Kongo yakabiliwa na uhaba wa chanjo ya Mpox Aina mpya ya kirusi cha ugonjwa huo, inayofahamika kama Clade 1b, ambacho kilisambaa kutoka Jamhuri ...
null
Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Kanali Assimi Goita, amemuondoa waziri mkuu Choguel Maïga pamoja na serikali yake siku ya Jumatano, siku chache baada ya Maïga kuikosoa serikali ya kijeshi. Hatua hiyo ilitangazwa kupitia amri ya rais iliyosomwa na katibu mkuu wake kwenye kituo cha televisheni ya taifa, ORTM. Mali imekuwa i...
null
Matangazo Hii ni baada ya kuifunga Guinea 1-0 katika mechi ya kusisimua iliyochezwa Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Bao la ushindi na la kipekee limefungwa na mshambuliaji Simon Msuva kunako dakika ya 61. Burundi ilishindwa kufuzu baada ya kufungwa mabao 2-0 na Senegal mjini Dakar. Tanzani...
null
Matangazo ICC pia ilitoa waranti za kukamatwa waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant na mkuu wa kijeshi wa Hamas Mohammed Deif. Zilitolewa kuhusiana na tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu na uhalifu wa kivita katika vita vya Israel dhidi ya Hamas huko Gaza, vilivyochochewa na shambulizi la kundi hilo la wa...
null
SiasaMatangazo ya Jioni 22.11.2024 To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nKvCNakili kiunganishiMatangazo
null
Amri iliyotolewa na Kanali Goita na kusomwa kwenye televisheni ya taifa ORTM imesema majukumu ya waziri mkuu na maafisa wa serikali yamesitishwa. Maiga, ambaye aliteuliwa na jeshi mwaka wa 2021, Jumamosi iliyopita alilaani hadharani ukosefu wa uwazi kuhusiana na kukamilika kwa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kira...
null
Guterres ameyasema hayo katika mazungumzo yanayoelekea kukwama kwenye mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika mjini Baku, Azerbaijan. Akizungumza katika mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi COP29 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hakuna nafasi ya mazungumzo hayo kushindwa kupata makubaliano. Am...
null
Maafisa wa Pakistan wametangaza siku saba za usitishaji mapigano baada ya mapambano makali ya risasi kati y amakabila katika wilaya ya Kurram, kaskazini magharibi mwa nchi, ambayo yamesababisha watu kiasi 82 kuuwawa na wengine 156 kujeruhiwa. Msemaji wa serikali ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, Muhammad Ali Saif, amesema...
null
Matangazo Rais mhafidhina wa Uruguay Luis Lacalle Pou amempigiaa simu na kumpongeza mgombea wa upinzani Yamandu Orsi kama rais mteule wa nchi hiyo ya Amerika Kusini na kumsaidia kuanza mchakato wa kukabidhi madaraka. Lacalle Pou ameandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kura za maoni baada y...
null
Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Tom Fletcher ameelezea wasiwasi kuhusu kile alichokitaja kama "janga la unyanyasaji wa kingono" dhidi ya wanawake nchini Sudan. Akizungumza katika ziara yake ya kwanza katika mji wa Port Sudan, Fletcher, ambaye anaongoza Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala...
null
Shin, amesema hayo katika kipindi cha televesheni cha kituo cha SBS na kuongeza kuwa Korea Kusini imegundua kuwa Urusi ilipokea si tu makombora bali pia vifaa vingine vya kuimarisha ulinzi wake wa anga katika mji mkuu Korea Kaskazini, Pyongyang. Shin pia amesema Urusi ilitoa msaada wa kiuchumi kwa Korea Kaskazini pamoj...
null
Mamlaka za Marekani zimesema Adani na washtakiwa wengine 7 akiwemo mpwa wake Sagar Adani, walitoa rushwa kwa maafisa wa serikali ya India ili kupata mikataba ambayo ingewaingizia faida ya zaidi ya dola bilioni 2 katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 na kuendeleza mradi mkubwa wa nishati ya umeme wa jua nchini India. Som...
null
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema leo kwamba juhudi zinazoongozwa na Marekani kufanikisha usitishaji mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah wa nchini Lebanon ni nafasi ya mwisho ya kupatikana mkataba wa kudumu wa kukomesha makabiliano. Mwanadiplomasia huyo ameyasema hay...
null
Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewataka wananchi kuandamana kupinga mpango wa Rais Felix Tshisekedi kuandika katiba mpya. Tshisekedi alitangaza mwezi uliyopita kuundwa kwa tume ya kuandaa katiba mpya, hatua ambayo imeibua hofu miongoni mwa wapinzani kuhusu uwezekano wa ku...
null
Siasa25.11.2024 Matangazo ya AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video52:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nO0sNakili kiunganishiMatangazo
null
Vifo hivyo vinafikisha idadi ya vifo nchini Haiti mwaka huu kupindukia 4,500. Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ameonya katika taarifa kuwa ongezeko la karibuni la machafuko katika mji mkuu wa Haiti ni ishara ya hali mbaya zaidi ijayo. Soma pia: Haiti: Polisi kwa kushirikiana na raia waua wanach...
null
Matangazo Wapiga kura wa Romania wapiga kura leo Jumapili kumchagua rais wao mpya. Waziri Mkuu Marcel Ciolacu wa chama cha Social Democratic Party (PSD) anatarajiwa kuongoza kwenye duru ya kwanza, lakini hata hivyo matokeo hayatabiriki. Kura ya maoni kabla ya uchaguzi ilionyesha kuwa huenda waziri mkuu Ciolacu akabilia...
null
Matangazo Kiongozi huyo wa zamani ameliambia shirika la utangazaji la hapa Ujerumani DPA kwamba yeyote anaefikiri anaweza kuwakamata wakimbizi na watu wengine kwa waranti ni kosa. Alisema kuwa wasafirishaji haramu wanafanya kila wawezalo kuepuka ukaguzi rasmi wa polisi. Na kuongezaa kwamba ukweli huo unajidhihirisha ka...
null
MigogoroVita vya Ukraine vinachukua sura mpya, nini kitatokea?To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video03:53Migogorohttps://p.dw.com/p/4nGfJNakili kiunganishiMatangazo
null
Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema ofisi yake haiwezi kuzungumzia ripoti hizo au masuala ya kiutendaji. Uingereza imekuwa ikiipa Ukraine makombora ya masafa marefu ya Storm Shadow tangu mwaka jana lakini ilikuwa imeruhusu yatumike katika maeneo yanayokaliwa ya Ukraine pekee. Soma pia: Urusi yasema...
null
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva aliunga mkono kauli hizo wakati alikutana na Xi na akasisitiza kuhusu ramani ya pamoja ya kupatikana amani nchini Ukraine ambayo wanaipendekeza. Lula alisema katika ulimwengu uliogubikwa na migogoro ya kivita na kisiasa, China na Brazil zinaweka mbele amani, diplomasia na mazung...
null
Ripoti ya waangalizi wa kimataifa iliyotolewa leo Jumanne imesema kwamba mizozo, machafuko na majanga kote barani Afrika yameiongeza mara tatu idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao barani humo katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Kulingana na ripoti ya shirika linalofuatilia mienendo ya watu kulazimika kuya...
null
Matamshi hayo aliyatoa katika mkutano wa IAEA mjini Vienna, Austria, huku mataifa yenye nguvu ya Ulaya na Marekani yakiwasilisha azimio la kuikemea Iran kwa ushirikiano wake mbaya na IAEA. Soma pia:Iran yaonya azimio la nchi tatu za Ulaya ndani ya IAEA litavuruga mambo Akizungumza na waandishi habari, Grossi alikaribis...
null
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuitumia Ukraine kama eneo la majaribio ya silaha, akidai kwamba Moscow ilirushakombora la masafa marefu la kuvuka mabara - ICBM kuelekea Ukraine, ambalo, likithibitishwa, litakuwa mara ya kwanza kutumika katika vita. Zelensky amesema kombo...
null
Siasa19.11.2024 Matangazo ya JioniTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nAdtNakili kiunganishiMatangazo
null
Mawaziri wa Ulinzi kutoka Ujerumani, Ufaransa, Poland, Italia na Uingereza wanakutana mjini Berlin kujadili hatua za kuimarisha ulinzi na usalama barani Ulaya. Soma zaidi: Nchi za NATO zapania kuimarisha utengenezaji silaha Ukraine Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema kipaumbele ni kuunda na kununua dr...
null
Matangazo Afisa mmoja wa usalama wa Mali alithibitisha shambulio hilo na kusema kwamba watu kadhaa walikufa. Wapiganaji wa kundi la Wagner wamekuwepo nchini Mali tangu mwishoni mwa 2021, kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini humo. Wakati huo huo, wapiganaji wa Urusi wa Wagner wametuhumiwa kufanya mashambulizi ya droni a...
null
Human Rights Watch imeongeza kuwa polisi imewakamata "mamia ya watoto bila ya kuzijulisha familia zao, hatua ambayo ni kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu." Hata hivyo, mamlaka haijajibu ripoti hiyo iliyotolewa na Human Rights Watch. Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imekumbwa na ghasia tangu uchaguzi wa Ok...
null
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran Abbas Araghchi ameyaonya leo mataifa matatu ya Ulaya dhidi ya kushinikiza kupitishwa azimio la kuikosoa Iran kwenye mkutano wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki IAEA unaoanza leo Jumatano mjini Vienna. Akizungumza na waziri mwenzake wa Ufaransa, Araghchi, amesema Iran inako...
null
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendelea, CHADEMA, kimelalamika kwamba wagombea wake wengi "wameenguliwa kwa njia zisizo za haki" kuwania katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakafanyika wiki ijayo. Taifa hilo la Afrika Mashariki litafanya uchaguzi wa viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji ...
null
Matangazo Hii ni mara ya kwanza kumwita hivyo, ikiwa ni karibu miezi minne tangu ufanyike uchaguzi wenye utata. Kauli hiyo ya Marekani imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Anthony Blinken na imezusha hasira kali kutoka kwa serikali mjini Caracas, ambayo imeitaja kuwa "ujinga na upuuzi." Soma pia: Bunge la Ulaya lamtambu...
null
Katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii, Gaetz amesema uteuzi wake umegeuka kuwa usumbufu kwa serikali inayokuja. Mbunge huyo wa zamani wa Florida, ambaye aliteuliwa wiki iliyopita, alikabiliwa na uchunguzi wa Wizara ya Sheria kwa karibu miaka mitatu. Ulihusiana na tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya ngono la...
null
Matangazo Mashuhudia kwenye kijiji hicho wameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanamgambo wa RSF, walio vitani dhidi ya jeshi la taifa tangu Aprili mwaka jana, walikishambulia kijiji cha Wad Oshaib jana jioni. Shuhuda mmoja amesema mashambulizi yalifanywa tena leo asubuhi na wapiganaji wa RSF walikuwa wakipora ma...
null
Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo kwa kauli tata kutoka kwa viongozi wengine wa chama hicho. Mbowe ameyatoa matamshi hayo leo mchana katika mkutano na wanahabari na kueleza kuwa kuna wakati viongozi ndani ya chama wanatofautiana kauli na wanakwenda mbali zaidi, lakini kama chama wanayamaliza ndani kwa...
null
Matangazo Watu 24 wamekufa baada ya boti mbili kupinduka nje ya pwani ya Madagascar katika bahari ya Hindi. Hayo ni kwa mujibu wa serikali ya Somalia. Waziri wa mambo ya nje wa Somalia Ahmed Moalim Fiqi amesema watu 46 wameokolewa. Fiqi amesema wanafanya kila wanaloliweza kuhakikisha walionusurika wanarejeshwa nyumbani...
null
Siasa25.11.2024 Taarifa ya Habari ya AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video08:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nNt4Nakili kiunganishiMatangazo
null
Matangazo Polisi waliendesha oparesheni ya usiku kucha katika kitongoji cha Petionville na kulilenga kundi la Viv Ansanm linaloongozwa na Jimmy Chérizier. Serikali inajaribu kurejesha udhibiti wa mji huo wenye vurugu na machafuko ambao kwa asilimia 80 unadhibitiwa na magenge hayo. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (...
null
Ikulu ya Urusi, Kremlin, leo imeutuhumu utawala unaoondoka madarakani wa rais Joe Biden wa Marekani kwamba unafanya kila unachoweza kurefusha vita vya Ukraine baada ya ripoti kuwa Washington imeidhinisha Ukraine ipatiwe mabomu ya kutegwa ardhini. Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amewaambia waandishi habari mjini Mosc...
null
Kiongozi wa kundi la Hezbollah Naim Qassem, amesema Israel haiwezi kuweka masharti ya kusitisha mapigano nchini Lebanon, huku mjumbe wa Marekani Amos Hochstein akielekea Israel kujaribu kusuluhisha vita hivyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, alisema makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano lazima yahakik...
null
JamiiMaoni: Usalama wa majengo Afrika MasharikiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video42:44Jamiihttps://p.dw.com/p/4nHmnNakili kiunganishiMatangazo
null
Taarifa ya Kremlin imesema viongozi hao wawili walibadilishana mawazo juu mbinu za kukabiliana na kitisho cha ugaidi na kuhakikisha uthabiti kwenye ardhi yote Jamhuri ya Afrika ya Kati. Urusi ina mahusiano ya karibu na Jamhuri ya Afrika ya Kati moja ya mataifa masikini zaidi duniani ambayo imetumbikia kwenye vita vya w...
null
Shirika hilo pia, limeitaka Iran itoe majibu katika uchunguzi wa muda mrefu unaohusu kupatikana kwa chembe chembe za urani katika maeneo mawili ambayo nchi hiyo imeshindwa kuyatangaza kuwa maalumu kwa kuzalisha nyuklia. Soma zaidi: IAEA: Iran yapanua uwezo wa kurutubisha madini ya urani Kwa mujibu wa wajumbe waliozungu...
null
Ushindi huo umeutanua mwanya wa Bayern kileleni na pointi nane kabla ya kuchezwa mechi nyingine za duru ya 11. Kane anaongoza katika ufungaji magoli kwenye ligi baada ya kufikisha 14. Mshambuliaji huyo wa England ndiye mchezaji wa kasi kufikisha mabao 50 katika Bundesliga katika mechi yake ya 43. Hata hivyo, kocha Vinc...
null
Kimataifa21.11.2024 Taarifa ya Habari AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video08:00Kimataifahttps://p.dw.com/p/4nEBbNakili kiunganishiMatangazo
null
Siasa21.11.2024 Matangazo ya JioniTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nHelNakili kiunganishiMatangazo
null
Siku nne baada ya kukamilishwa kwa vikao kuhusu sheria nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, chama cha kitaifa cha majaji kilikuwa na mkutano mkuu mjini Kinshasa jana jioni ambapo kilitangaza nia yake ya kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi wa ngazi za juu serikalini na pia watafikisha malalamiko yao mahakamani. ...
null
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imetoa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wake wa zamani wa ulinzi Yoav Gallant pamoja na kiongozi wa kundi la Hamas Ibrahim Al-Masri, ikiwashtumu kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kuhusiana na vita katika Ukanda wa Gaza, na ...
null
MigogoroMashariki ya KatiJe, waranti ya kumkamata Netanyahu inamaanisha nini?To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video03:42MigogoroMashariki ya Katihttps://p.dw.com/p/4nG9KNakili kiunganishiMatangazo
null
Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel ameitetea miaka 16 ya utawala wake katika kitabu chake kwa jina Freedom yaani Uhuru, kilichotolewa katika lugha 30 leo Jumanne. Tangu alipoondoka madarakani Merkel amekuwa akituhumiwa kwa kuwa na msimamo mwepesi kuhusu Urusi, akiiwacha Ujerumani ikiwa tegemezi kwa gesi ya be...
null
Urusi inawasajili wanaume kutoka Yemen waende kupigana vita nchini Ukraine kupitia msaada wa waasi wa Houthi nchini Yemen. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Financial Times. Gazeti hilo liliripoti jana Jumapili likiwanukuu watu wanaohusika, kwamba jeshi la Urusi lilikuwa limefanikiwa kuwageuza mamia ya wanaume ...
null
Matangazo Afisa mmoja wa kituo hicho aliyezungumza kwa msaharti ya kutotajwa jina lake aliliambia shrika la habari la AFP kwamba mamlaka ya mawasiliano ya Mali ilizuia leseni ya Joliba TV News kuanzia tarehe 26 Novemba. Hatua hiyo inafuatia malalamiko yaliyowasilishwa dhidi ya kituo hicho Novemba 12 na mamlaka ya mawas...
null
24.11.2024 Matangazo ya JioniTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00https://p.dw.com/p/4nNSpNakili kiunganishiMatangazo
null
Kimataifa23.11.2024 Taarifa ya Habari AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video08:00Kimataifahttps://p.dw.com/p/4nLKXNakili kiunganishiMatangazo
null
24.11.2024 Matangazo ya MchanaTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00https://p.dw.com/p/4nN56Nakili kiunganishiMatangazo
null
Matangazo Waandamanaji hao wamefika hadi pembezoni mwa mji mkuu wa Islamabad huku kukiwa na ripoti za kutokea ghasia katika maeneo mengine. Mamlaka zimeimarisha usalama huku barabara zinazoingia mji mkuu zikifungwa ili kuwazuia waandamanaji ambao Khan amewataka kuandamana hadi bungeni. Maafisa na mashuhuda wamesema usa...
null
Siasa22.11.2024 Matangazo Ya MchanaTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nJihNakili kiunganishiMatangazo
null
Matangazo Pakistan ni nchi yenye Wasunni wengi lakini wilaya ya Kurram, karibu na mpaka na Afghanistan, ina idadi kubwa ya Washia na jumuiya hizo zimepigana kwa miongo kadhaa. Vurugu za hivi sasa zilianza siku ya Alhamisi wakati misafara miwili tofauti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wakisafiri chini ya ulin...
null
Iran imeonya kuwa azimio lililowasilishwa na nchi za magharibi kulaani mpango wake wa nyuklia katika Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), litapunguza na kuvuruga ushirikiano kati ya shirika hilo na Tehran. Mataifa ya Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani yamewasilisha rasimu ya azimio linaloikosoa Iran...
null
Rais Filipe Nyusi amemualika Venancio Mondlane ofisini kwake mjini Maputo Novemba 26 baada ya vifo vya watu kadhaa katika ukandamizaji wa polisi dhidi ya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9. Mondlane, mgombea wa kujitegemea, anayesema uchaguzi ulichakachuliwa kukipa ushindi chama cha Nyusi cha Frelimo...
null
Kimataifa22.11.2024 Matangazo ya AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video52:00Kimataifahttps://p.dw.com/p/4nIWpNakili kiunganishiMatangazo
null
Matangazo Vyanzo vitatu vya usalama vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa oparesheni za uokoaji zinaendelea kutafuta manusura zaidi. Kwa mujibu wa utawala katika eneo hilo, boti hiyo ilikuwa imebeba watu 45, wakiwemo watalii 31 na wafanyikazi 14. Gavana Amr Hanasi amesema baadhi ya manusura waliokolewa kwa heli...
null
Kimataifa23.11.2024 Matangazo ya AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video52:00Kimataifahttps://p.dw.com/p/4nLKYNakili kiunganishiMatangazo
null
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura Jumatano kuhusu rasimu nyingine ya azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza katika majaribio yake ya hivi punde ya kuongeza shinikizo la kumaliza vita. Hata hivyo uteuzi wa maneno katika rasimu hiyo umeighadhabisha Israel na kuzusha hofu kwamba hu...
null
Siasa25.11.2024 Matangazo ya JioniTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video59:59Siasahttps://p.dw.com/p/4nPoaNakili kiunganishiMatangazo
null
Muda mfupi baada ya saa nane, Rais William Ruto alipokelewa na naibu wake mpya Profesa Kithure Kindiki aliyeapishwa wiki tatu zilizopita. Kama ilivyo ada, alikagua gwaride la heshima aliloandaliwa kabla ya kuingia bungeni kulikofanyika kikao cha pamoja cha wabunge na maseneta. Hii ilikuwa hotuba ya pili ya hali ya taif...
null
Waangalizi wa kimataifa wamesema kwamba mizozo, machafuko na majanga kote barani Afrika yameiongeza mara tatu idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao barani humo katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika linalofuatilia mienendo ya watu kulazimika kuyahama makazi yao ndani ya nchi za...
null
Matangazo Jasper Inventor, mkuu wa ujumbe wa shirika la Greenpeace kwenye mazungumzo ya COP29 amesema watu wamechoshwa na wamekata tamaa. Inventor amesema ahadi ya mataifa tajiri kutoa dola bilioni 300 kwa nchi masikini haitoshi kwa mahitaji yao. Na kuongeza kuwa shirika la Greenpeace na wengine wanasubiri mkutano ujao...
null
Kauli za Uganda zimejiri siku mbili baada ya afisa mwandamizi wa Kenya kusema Nairobi imeanzisha uchunguzi kuhusu suala hilo. Msemaji wa serikali ya Uganda Chris Byaromunsi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa maafisa wa Uganda na Kenya walifahamu kuhusu kukamatwa na kuhamishwa kwa Dr. Besigye kwenda Uganda. Soma p...
null
Siasa21.11.2024 Matangazo ya AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video51:59Siasahttps://p.dw.com/p/4nEKqNakili kiunganishiMatangazo
null
Vikosi vya Israel vimewaua Wapalestina 15 leo kwenye Ukanda wa Gaza, akiwemo mfanyakazi mmoja wa idara za uokozi, huku vifaru vya kijeshi vikiendelea kupiga doria kote kwenye eneo hilo na kulipua majengo ya maakazi. Hayo yameelezwa na wakaazi pamoja na maafisa wa afya wa ukanda huo unaodhibitiwa na kundi la wanamgambo ...
null
Matangazo Gazeti la Sudan la Post, limemnukuu afisa mmoja wa usalama akisema mkutano huo umeishughulikia mivutano yote mikubwa na kuwa familia ya mkuu huyo wa zamani wa ujasusi wa Sudan Kusini pamoja na familia yake zimehakikishiwa usalama. Hata hivyo bado hakuna kauli rasmi ya serikali kuhusu mkutano huo. Rais Salva K...
null
Siasa21.11.2024 Matangazo ya MchanaTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video01:00:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nEuRNakili kiunganishiMatangazo
null
Matangazo Taarifa fupi ya msemaji huyo, Farah Dakhlallah ilieleza kwamba viongozi hao "Walijadili masuala mbalimbali ya usalama wa kimataifa yanayoukabili muungano.”Rutteanatazamwa kama mmoja wa kati ya viongozi bora wa Ulaya katika kufanikisha uhusiano mzuri wa kufanya kazi na Trump wakati wa muhula wake wa kwanza, 20...
null
Matangazo Serikali na Wizara ya Mambo ya Ndani zilitoa tangazo kwamba huduma za mtandao na simu zitaendelea kwenye maeneo mengine ya nchi, bila kutaja maeneo husika na muda itakaodumu hatua hiyo. Wafuasi wa Imran Khan wanataka kiongozi wao aachiwe huru. Khan amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na ana zaidi ya kes...
null
Katika chapisho kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mondlane ametaka pia kuhesabiwa upya kwa kura baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza Daniel Chapo wa chama cha Frelimo kilichopo madarakani kwa karibu nusu karne kuwa mshindi. Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi anayetakiwa kuondoka madarakani mwezi Januari amel...
null
Matangazo Shambulio hilo lilifuatiwa na mengine katika vitongoji vya kusini mwa mji huo baada ya wito wa jeshi la Israel kuwataka watu kuhama katika eneo hilo. Shughuli za uokoaji zimeripotiwa kuendelea huku waokoaji wakiondoa vifusi vya jengo hilo la ghorofa nane, na gari la zimamoto walinzi wa raia wakiwa katika eneo...
null
Matangazo Ijumaa, wizara ya Mambo ya Nje ya Niger iliushutumu Umoja wa Ulaya kwa kutenga dola milioni 1.3 katika misaada ya kibinadamu kwa mashirika kama vile Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Baraza la Wakimbizi la Danmark bila kushauriana na mamlaka. Viongozi wa Niger walisema hatua hiyo haikuzingatia kanuni...
null
Matangazo Mkuu wa Baraza la wakimbizi la Norway, NRC, amesema mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan ni mbaya zaidi kuliko migogoro ya Ukraine, Gaza na Somalia kwa pamoja. Kwenye mahojiano na shirika la habari la Ujerumani DPA, Jan Egeland amesema maisha ya watu milioni 24 yako hatarini nchini Sudan. Egeland aliyefanya zia...
null
Matangazo Na amehoji hali hiyo itakuwa na tafsri gani kwa Ulaya. Kutokana na mashaka yake hayo ametoa wito kwa vyama vya Ujerumani vinavyounga mkono Umoja wa Ulaya kusimama pamoja katika masuala muhimu. Ameelezea wasiwasi wake baada ya uchaguzi wa majimbo katika eneo lililokuwa Ujerumani Mashariki. Metsola amesema kuon...
null
Matangazo Hatua ya Urusi ya kuishambulia Ukraine kwa makombora mapya ya kuvuka mabara, ambayo inatajwa kuwa na athari kwa bara zima la Ulaya, huenda ikawa ajenda kuu ya majadiliano hayo. Mkutano huo unafanyika pia kabla ya kuapishwa rasmi mnamo Januari 20 Rais mteule wa Marekani Donald Trump ambaye ni mkosoaji mkubwa w...
null
Mataifa yamegawanyika kuhusu makubaliano ya ufadhili wa dola trilioni moja, yanayotarajiwa kuchukua nafasi ya ahadi ya kila mwaka ya dola bilioni 100 iliyotolewa na mataifa tajiri kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Azerbaijan ambayo ndio inashikilia urais wa COP29 imesema katika taarifa...
null
Siasa26.11.2024 Taarifa ya Habari ya AsubuhiTo play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video08:00Siasahttps://p.dw.com/p/4nQNmNakili kiunganishiMatangazo
null
Milio ya risasi ilirindima nyumbani kwa mkuu wa intelijensia wa Sudan Kusini aliyefutwa kazi hivi karibuni. Haya ni kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukiliita tukio hilo kuwa jaribio la kumkamata. Akol Koor alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu alipotimuliwa mwezi Oktoba, kwa mujibu wa ripoti...