name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | WAJASILIAMALI wadogo na kati kutoka barani Afrika wamehimizwa kuwekeza Tanzania hususan sekta ya utalii kwani ndio sekta yenye uhakika wa kipato. Mbali na kuwahimiza kuwekeza wajasiliamali hao wanawake na vijana wametakiwa kujisajili katika mfumo rasmi wa kifedha ili kutambulika na serikali na benki waweze kukopesheka.... |
null | TUME ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewatoa rai kwa wananchi kutojiandikisha zaidi ya mara moja katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakaloanza katika Desemba 11 -17 mwaka huu kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dodoma . Aidha uboreshaji wa daftari hilo kwa mwaka 2924/25 utatumia teknolojia ya BVR Kits zi... |
null | VIONGOZI wa dini na mila wa mkoa wa Rukwa wamepaza sauti wakitaka kujua ni lini serikali itaifanyia mabadiliko Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 waliyosema mapungufu na changamoto zake zinachochea mimba na ndoa za utotoni mkoani mwao na Taifa kwa ujumla. Viongozi hao wamesema wakati Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inamtafsiri... |
null | JITIHADA za Tanzania kukabiliana na wimbi la ajali za barabarani zinazogharimu maelfu ya watu kila kukicha, zinatarajiwa kuchukua uelekeo mpya. Hii ni baada ya jana (Machi 02), Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia waziri wake, Profesa Makame Mbarawa kushuhudia utiaji saini makubaliano ya kuanzishwa rasmi utekelezaji wa... |
null | MAGONJWA yasiyoambukiza (NCDs) ni yasiyoenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Hivi sasa NCDs imekuwa mzigo kwa taifa kutokana na kutumia gharama kubwa ya matibabu kwa muda mrefu na kupoteza nguvu kazi. Wizara ya Afya imesema unene uliokithiri na uzito kupita kiasi ni kisababishi cha magonjwa yasiyoambukiza kwa... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan leo anatimiza umri wa miaka 63. Alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, baba yake alikuwa mwalimu na mama yake alikuwa mama wa nyumbani. Machi 19, 2021 aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Aliapishwa baada y... |
null | TASNIA ya sheria nchini inaadhimisha Wiki ya Sheria iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango Januari 22, 2023, Dodoma na itahitimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Kaulimbiu ya Siku ya Sheria mwaka huu imejikita zaidi katika msisitizo wa Mahakama kutumia usuluhishi kama nj... |
null | TANZANIA kwa sasa inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 40 ambao, zaidi ya asilimia 80 ya wanyama hao ni wa kienyeji na wanafugwa kienyeji pia. Kwa waliotembelea Maonesho ya Wakulima maarufu Nanenane yaliyofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Mbeya walijifunza kwamba endapo wafugaji nchi nzima watatumia ng’ombe walioboreshwa... |
null | CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa katika mchakato wa kuwa na viongozi wa ngazi mbalimbali tangu ngazi za mashina hadi taifa. Katika uchaguzi huo, Watanzania wameshuhudia wanachama wakitumia demokrasia yao kuchagua viongozi ambao kwa imani yao, watakivusha chama katika uchaguzi mwingine unaofuata. Si siri kwamba, mara ... |
null | KUANZISHWA kwa mfumo mpya wa kupima utendaji kazi kubaini mikoa na halmashauri zinazoongoza kukwepa kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi, kutaongeza uwajibikaji. Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama mfumo mpya wa kupima utendaji kazi wa watumi... |
null | H ARAKATI za timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zimegubikwa na maswali mengi baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Uganda kwa bao 1-0. Kabla ya mchezo huo, Taifa Stars ilikuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye Kundi F, kutokana na matokeo ya mchezo w... |
null | CHAMA cha ACT-Wazalendo kimelitaka Bunge la Ulaya kuondoa azimio la kutaka kusitishwa kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga. Msemaji wa Sekta ya Madini katika chama hicho, Isihaka Mchinjita alieleza hayo jana kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.... |
null | WAFANYABIASHARA, wachambuzi wa masuala ya uchumi na wanasiasa wamepongeza serikali kwa kuweka mfumo wa tozo ili kutekeleza miradi ya maendeleo. Wamesema hayo jana katika mjadala wa kitaifa kuhusu tozo uliofanyika kwa njia ya Zoom ulioratibiwa na Taasisi ya Watch Tanzania. Mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji aliip... |
null | VIONGOZI wa vyama vya siasa nchini wameipongeza serikali kurekebisha tozo na wameshauri itafute vyanzo vingine kuongeza mapato. Katibu Mkuu wa chama cha ADC, Doyo Hassan Doyo alisema tozo si tatizo kwa sababu malengo yake yalilenga maslahi ya Watanzania, lakini ilitakiwa kwanza kuwepo na ushirikishwaji wa wadau na elim... |
null | “MAONESHO ya kimataifa ya Afrika Mashariki ni muhimu sana kwa ajili ya sekta ya viwanda, lakini zaidi tunafurahi kwamba maonesho hayo yamefana sana mwaka huu, kwa sababu nchi nyingi zimeshiriki, ingawa India ndio wamejitokeza zaidi,” hiyo ni kauli ya Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe. Ametoa ... |
null | SERIKALI imesema mazao kutoka Tanzania, yamekuwa yakiuzwa kwenye soko la kimataifa, ikiwemo Nchi za Jumuiya ya Ulaya pasipo mashaka yoyote kutokana na kuwa na viwango vinavyokubalika vya ubora, baada ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA), kupata ithibati. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kili... |
null | WANANCHI wametakiwa kujengea utamaduni wa kujiwekea akiba ya fedha, ili ziweze kuwasaidia kwa maisha ya baadae. Mwezeshaji kutoka Taasisi ya Dhamana ya Uwekezaji na Usimamizi wa Rasilimali Tanzania (UTT-AMIS), Grace Ngailo, ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo juu ya uelewa na ujuzi kwenye masuala ya kifedha katika sem... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan Jumanne anatarajiwa kuzungumza na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS), Moshi mkoani Kilimanjaro. Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema Rais Samia atafungua kikao kazi cha maofisa wakuu waandamizi wa makao makuu, makamanda wa polisi mikoa n... |
null | MKOA wa Arusha umefikia asilimia 99.5 ya kaya zilizotakiwa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu linalotarajiwa kumalizika leo usiku Mkoa wa Arusha umefanikiwa kuhesabu kaya zaidi ya 562,300 kati ya kaya 565,800, ambapo ni sawa na asilimia 99.5 Akizungumza leo jijini Arusha, Msimamizi wa Sensa Mkoa wa Arusha, Mloka ... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo manne kwa Jeshi la Magereza Tanzania ikiwemo kuzingatia weledi, kuzingatia haki zote kwa wafungwa, kuboresha utawala bora na kuhakikisha wanarekebisha tabia za wafungwa. Rais Samia alisema hayo wakati akiwaapisha majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Kamishna Jenerali wa Magereza... |
null | MCHUNGAJI wa Kanisa la KKKT Makedonia Lubaga, Manispaa ya Shinyanga, Harold Gamalieli Mkaro, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga na kusomewa shitaka la kujaribu kulawiti mtoto wa miaka 8. Mchungaji huyo alifutiwa kesi ya awali namba 107, Agosti 24, 2022 na Jamhuri katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyang... |
null | MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mkoani Mtwara, imefikia asilimia 91. Amewaambia waandishi wa Habari ofisini kwake mapema leo kuwa mpaka kufikia muda wa kufungu shughuli ya sense leo usiku, mkoa huo utakuwa umefikia asilimia 100. “Mpaka jana saa mbili usiku tulikuwa tu... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan amewaagiza majaji wafanye kazi kwa kuzingatia haki, weledi na maadili. Alisema hayo jana katika Ikulu ya Chamwino Dodoma baada ya kuwaapisha majaji na Kamishna Jenerali wa Magereza. Rais Samia alisema uapisho huo wa majaji 21 kati ya 22 umejaza idadi ya majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Ruf... |
null | DAR ES SALAAM; Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat, wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU). Maadhimisho hayo yanafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ju... |
null | Search Mwanzo Matangazo: Maelekezo na Bei Kuhusu HabariLEO Nunua E-Paper Home RC Mwanza apokea ujumbe wa SBL Biashara Picha Uwekezajia RC Mwanza apokea ujumbe wa SBL by Mwandishi wetu May 18, 2024 MWANZA: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akimsikiliza Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Neema Te... |
null | DAR ES SALAAM; Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo.... |
null | DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), leo Mei 8, 2024 jijini Dar es Salaam. |
null | DAR ES SALAAM; Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika, wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hay... |
null | DODOMA; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye akiwasili bungeni jijini Dodoma leo Mei 16, 2024, ambapo atawasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2024/2025. #BajetiWHMTH2024/25 #SmartTanzania #TzDigitalTransformation #KaziIendelee |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Dk James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati. Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 21, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus. Dk Mataragio anachukuwa nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine, kw... |
null | DAR ES SALAAM: Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiomba Benki ya Dunia kupitia upya masharti ya manunuzi katika mikataba ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu ili kutoa fursa kwa Wakandarasi wazawa kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo. Bashungwa ametoa ombi hilo katika kikao na Mkurugenzi Mkazi wa Benki y... |
null | ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao yanayozalishwa nchini na usafirishaji. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua mkutano wa pili wa Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho ... |
null | MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ofisi za Mkoa wa Geita imefanikiwa kuandikisha watu 922,000 kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya taifa kati yao watu 440,000 ni wakazi wa Wilaya ya Geita. Ofisa Usajili wa NIDA Geita, Emmanuel Ernest amesema hayo katika hafla ya ugawaji wa vitambulisho kwa watendaji wa kata na... |
null | WIZARA ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa hatua inazoendelea kuzichukuwa katika uboreshaji wa usimamizi wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) Pongezi hizo zimetolewa na mtaalam na mwezeshaji wa mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kutoka Wizara ya Fedha Dk Sako Ma... |
null | MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood amesikitishwa baada ya kubaini kutokuwepo na vyoo vya wanafunzi zaidi 1,000 na vya walimu wao katika Shule ya Msingi Mgulu wa Ndege, Manispaa ya Morogoro na kulazimika kwenda kujisaidia shule ya jirani Mkundi. Abood alijionea hali hiyo baada ya kufanya ziara ya kikazi ... |
null | MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya ligi inarejea leo ikifanyika michezo tisa katika viwanja tofauti. Moja ya mechi za kukata na shoka ni kipute kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund katika uwanja wa Santiago Bernabeu uliopo mji mkuu wa Hispania, Madrid. SOMA: Utamu warejea Ligi ya Mabingwa Ulaya Mchezo huo ... |
null | MIAMBA ya soka nchini Simba na Yanga leo zinashuka katika viwanja tofauti kusaka pointi 3 muhimu katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanznaia Bara. Bingwa mtetezi Yanga itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. SOMA: Pazia Ligi Kuu bara kufunguliwa leo Yanga imetoka kush... |
null | HALMASHAURI ya Wilaya ya Kasulu imesema kuwa 4R za Rais Samia ni miongoni mambo manne yaliyoifanya halmashauri hiyo kufanya vizuri kwenye zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Imeelezwa kuwa Mkoa wa Kigoma umefikisha asilimia 99.7 ya uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la wapiga kura kwa aji... |
null | NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema kuwa uhusiano wa Tanzania na Singapore ni wa muda mrefu na kuwa nchi hizo zinatakiwa kuangalia sababu za uwepo wa uhusiano huo na kuongeza kiwango cha ufanyaji biashara kati yake. Dk. Biteko amesema hayo akiwa nchini Singapore mara baada ya kukutana na kuf... |
null | MBUNGE wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jumaa Aweso amesema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia hivyo uchaguzi ni namna nzuri ya kupata viongozi huku akiwahimiza wananchi kujiandikikisha kwenye daftari la kupiga kura. Aweso ambaye ni Waziri wa Maji amesema hayo leo Oktoba 17, 2024 mara baada ya kujian... |
null | SERIKALI imesema itahakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unakuwa jumuishi na shirikishi Ili kupata viongozi bora ambao watakaoweza kushirikiana katika kuwaletea maendeleo wananchi. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani wakati wa mkutano wa uhamasisha wa wananchi kushiriki kwenye uandikishaji wa... |
null | WATU 604 wamepata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zilizotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC). Akizungumza kuhusu kambi hiyo ya siku tano iliyomalizika mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)... |
null | MAHAKAMA nchini Peru imemhukumu rais wa zamani wa taifa hilo, Alejandro Toledo kifungo cha miaka 20 na miezi sita jela kwa kosa la rushwa na utakatishaji fedha haramu. Waendesha mashtaka wanasema alichukua $35m kama hongo kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil ambayo ilipewa kandarasi ya kujenga barabara Kusini mwa Per... |
null | ZANZIBAR – KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuf Mwenda amesema yeye ni mtu wa vitendo na anamwamini Mungu atamsaidia kutimiza matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan. Ametoa kauli hiyo ya kwanza tangu kuteuliwa kwake na Rais kushika wadhifa huo. Alikuwa akizungumza mjini Zanzibar jana wakati akiagwa n... |
null | KIKOSI cha timu ya taifa “Taifa Stars” kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN) 2024 dhidi ya Sudan kimetangazwa. Kikosi hicho cha wachezaji 24 kinaundwa na vijana zaidi. Wachezaji walioitwa watakaokuwa chini ya Kocha Bakari Shime ni Aisha Manula, Isa... |
null | DAR ES SALAAM: RAIS, Samia Suluhu Hassan amewataka washiriki wa Kongamano pili la Wanawake katika Biashara ndani ya eneo huru la biashara barani Afrika kujadili namna ya kuwezesha ushiriki imara wa wanawake katika biashara ndani ya Bara la Afrika. Akitoa maagizo hayo ya Rais leo Desemba 6, 2023 jijini Dar es Salaam, Wa... |
null | WAZIRI wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewataka vijana nchini badala ya kuuliza nini nchi iwafanyie, ni vema wajiulize wao wataifanyia nini nchi yao. Nyalandu ameyasema hayo, alipohutubia wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana lililopewa jina la Samia Love jijini Mbeya. Amesema taifa la Tanzania lita... |
null | ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Mabalozi wa Nchi za Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania kuimarisha ushirikiano na fursa za kiuchumi pamoja na kuutangaza utalii wa Zanzibar kimataifa. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na mabalo... |
null | TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imemtia mbaroni Suleiman Mwishehe na kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za kujaribu kumhonga ofisa wa taasisi hiyo aliyekuwa anachunguza tuhuma dhidi ya ubadhilifu wa Sh milioni 90 . Fedha hizo ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu na v... |
null | ARUSHA: Katika kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani 2024, Exim Bank Tanzania imechangia jumla ya mitungi ya gesi 1,000 kwa walimu mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika matumizi ya nishati safi. Mchango huu ni sehemu ya jitihada za benki hiyo kuchangia ongezeko la matumiz... |
null | MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imekutana na uongozi wa Kampuni ya Maurel et Prom Exploration Production Tanzania Ltd inayosimamia kitalu cha Mnazi Bay kwa lengo la kujadili utekelezaji wa uchorongaji wa visima vitatu vya gesi asilia unaotarajiwa kuanza mwakani. Wajumbe kutoka pande hizo akiwemo men... |
null | NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema matarajio ya serikali ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania watumie nishati safi ya kupikia. Dk Bitoko amesema hayo katika Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia ambalo limeandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) na Benki ya Uwekez... |
null | BAADHI ya wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamepokea mitungi ya gesi ya kupikia 1,600 inayouzwa kwa bei ya ruzuku ili kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu na nishati mbadala. Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Advera Mwijage amesema hayo katika siku maalum ya nishati saf... |
null | GAIRO, Morogoro: WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) itashiriki katika Maonesho ya Samia KILIMO Biashara Expo 2024 kwa msimu wa tatu yanayotarajiwa kuanza Oktoba 06 wilayani Gairo mkoani Morogoro. Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu, Mha. Advera Mwijage amesena kupitia maon... |
null | TANZANIA itakuwa kitovu cha muunganisho wa mawasiliano Afrika Mashariki na Kati, kufuatia uwepo wa mkongo wa mawasiliano wa 2 Afrika utakapokamilika Februari mwakani. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi, alipofanya ukaguzi wa mkongo wa kituo cha 2 Afrika l... |
null | VIJANA kutoka vyuo vinne nchini, wamesema suala la ajira halitakuwa changamoto kwao, baada ya kupata mafunzo yatakayowawezesha kuanzisha biashara, kuendeleza au kuunda kitu kipya, ambacho kitatatua matatizo yaliyopo katika jamii. Kwa nyakati tofauti wameelezea hayo, wakati wa kufunga mafunzo ya wiki 10 yaliyoanza Julai... |
null | WANANCHI wa Mji wa Makambako wilayani Njombe mkoani Njombe, wameshauriwa kutumia huduma za mawasiliano kujiimarisha kiuchumi ndani na nje ya nchi. Akizungumza katika gulio la wiki lililofanyika katika Soko Kuu la Makambako, Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Asajile John ... |
null | TANZANIA itakuwa kitovu cha maunganisho ya mawasiliano Afrika Mashariki na Kati kutokana na kuwapo kwa mkongo wa mawasiliano wa pili barani Afrika utakaokamilika Februari mwakani. Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi alisema hayo alipofanya ukaguzi wa mkongo wa kituo cha 2 A... |
null | WALIMU 26 wa sekondari wa somo la fizikia kutoka shule 13 za serikali jijini Dar es Salaam, wametakiwa kutumia ujuzi, maarifa na mbinu mbalimbali walizozipataza kuwawezesha wanafunzi waelewe na kulipenda somo hilo, ili kuongeza ufaulu. Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kalanja ametoa wito huo, wakati wa ... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Afrika wakiwekeza zaidi katika sayansi na teknolojia kwa vijana, wanaweza kuwa sehemu muhimu ya kustawisha uchumi kama ilivyo China. Ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo, wakati akifungua Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa dini nchini wakemee maovu zikiwemo na dhuluma, mauaji na mmomonyoko wa maadili. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana aliposhiriki Baraza la Maulid lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW). Rais Samia aliwashukuru ... |
null | ASKOFU Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Donald Mtetemela, amewataka viongozi wa dini nchini kujiepusha na kauli na viendo vitakavyopandikiza chuki na uchochezi kwa waumini wao dhidi ya serikali na dini nyingine. Askofu Mtetemela alitoa kauli hiyo jana, wakati wa ibada ya kumweka wakfu na kumsimika Kasis... |
null | MKE wa Waziri Mkuu msaafu, Jaji Joseph Warioba, Evelyne Warioba, amewataka wanawake wanataaluma kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Taifa. Amesema ufumbuzi unapatikana kwa Mungu na viongozi wanawake waangalie la kufanya, ikiwemo matatizo makubwa yanayowakumba wanawake na watoto. Ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo, ka... |
null | BABA Mtakatifu Papa Francis, amemtunuku Padri Richard Mjigwa wa Tanzania, nishani ya Msalaba wa Kanisa na Papa kutokana na huduma ya mawasiliano ya Kanisa kupitia Redio Vatican Idhaa ya Kiswahili. Padri Mjigwa pia anahudumu katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Redio Vatican ni Mtanzania ... |
null | SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi amewataka Waislamu kujenga tabia ya kujitolea fedha na mali zao kwa ajili ya kuendeleza mafanikio ya Uislamu. Mufti ameyasema hayo Jumatano wakati akiwaongoza viongozi wa dini ya Kiislamu wa wilaya na kata wakiwemo mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kwenye dua ya kuombea... |
null | MAOMBI maalum ya kuwaombea viongozi wakuu wa nchi,pamoja na Tanzania kwa ujumla yanatarajia kuanza leo Jumatatu jijini Dar es Salaam. Maombi hayo ya wiki moja yatakayoambatana na semina ya neno la Mungu, yameandaliwa na Kanisa la Calvary Tanzania Assemblies of God (CAG) ‘Chuo cha Manabii’, lililopo eneo la Bandari Kavu... |
null | MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ziara ya siku tatu. Kamala ambaye ni mwanamke wa kwanza katika historia ya Taifa la Marekani kushika wadhifa huo, anatarajiwa kuwasili nchini akitokea Ghana akiwa katika ziara ya mataifa matatu ya Afrika ambayo itamfikisha pia Zambia. Anakuja... |
null | SERIKALI imewataka wadau wa sekta ya ufugaji wa kuku na nyama nyeupe kote nchini kuchangamkia fursa kwa kufanya ufugaji wa kimkakati kwani iko tiyari kushirikiana nao ili kuhakikisha tasnia hiyo inakua na kuchangia katika pato la taifa. Aidha imewashauri wadau wa kuku nchini kuwa na wivu na tasnia yao kwa kutokuruhusu ... |
null | WAJANE 100 wamepatiwa kadi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka Taasisi isiyokuwa ya serikali mkoani Mtwara ya Joel Nanauka Foundation zilizogharimu Sh milioni 30. Akizungumza leo katika ghafla hiyo fupi ya ugawaji wa kadi hizo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joel Nanauka amesema wameguswa kufanya hivyo kutoka ... |
null | MSIMAMIZI wa uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini, Kisena Mabuba amesema hakuna ukiukwaji wowote wa sheria na taratibu katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la mkazi kama ambavyo baadhi ya vyama vya siasa vimelalamika. Mabuba amesema hayo kwenye Mwalo wa Katonga Manispaa ya Kigoma Ujiji akitoa ufafanu... |
null | CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimefanikiwa kupata miradi mipya ya utafiti 11 yenye thamani ya Sh bilioni 4.5 katika kipindi cha mwezi Mei hadi Oktoba mwaka huu. Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda amesema hayo katika mahafali ya 44 yaliyofanyika Kampasi ya Edward Moringe na kuhudhuliwa na wada... |
null | MRADI wa Bomba la Mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP) unaotoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga Tanzania umefikia asilimia 45.5 na tayari Sh bilioni 977 zimetolewa na serikali ya awamu ya sita katika utekelezaji wa mradi huo. Hayo yamesemwa leo na mratibu wa mradi huot aifa kutoka Shirika la Maendele... |
null | WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amesema Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni chachu katika kukuza utalii na kuiweka Tanzania katika ramani ya riadha na utalii Kimataifa. Chana ametoa kauli hiyo usiku wa Oktoba 18,2024 wakati wa hafla ya kuzindua mbio za 23 za Kilimanjaro Prem... |
null | ILE siku, tarehe na mwezi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenda soka nchini umefika. Ni mchezo wa dadi ya Kariakoo Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. SOMA: Gamond, Fadlu watambiana Kariakoo dabi Mtananange huo ni mechi pekee ya ligi hiyo leo. Simba ipo nafas... |
null | Kwa mujibu wa tetesi za usajili Klabu ya Real Madrid ina majuto makubwa kuhusu kumsajili Kylian Mbappé majira haya ya kiangazi na wamebaki wakiwa wamevunjika moyo kutokana na kiwango chake cha mchezo. Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, alikuwa mtu pekee aliyetaka kumsajili mfaransa huyo. (Romain Molina) Barcelona na... |
null | MECHI za Ligi Kuu tano bora barani Ulaya zinaendelea leo baada ya kusimama kupisha michezo ya kimataifa nyingine zikiwa zimerejea Oktoba 18. Liverpool inaongoza Ligi Kuu England, Barcelona wakiwa vinara katika LaLiga ya Hispania huku Bayern Munich wakiwa kwenye baridi Bundesliga, Ujerumani. SOMA: Dortmund mwamba unaota... |
null | WANAFUNZI wa shule za sekondari mkoani Geita wamehimizwa kuwa mabalozi wa kuwahamasisha na kuwaelimisha wazazi wao faida za kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito huo alipotembelea vituo vya uandikishaji katika shule za sekondari Bwela iliyo... |
null | SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya Michezo. Makubaliano hayo yameingiwa leo Oktoba 19, Dar es Salaam kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dk. Damas Ndumbaro na Jamhuri ya Kiislam ya Iran iki... |
null | TETESI za usajili zinaonesha Arsenal ina shauku kumsajili winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams, 22, na kiungo wa Real Sociedad, Mikel Merino, 28, lakini inakabiliwa na ushindani toka Barcelona kwa ajili ya wachezaji hao wa kimataifa wa Hispania. Williams amekuwa mojawapo ya majina yanayozungumziwa mno katika soko la... |
null | KAMATI ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeridhishwa na ujenzi wa kituo cha zimamoto kilichopo Mtumba jijini Dodoma chenye thamani ya Sh bilioni 1.9. Akizungumza leo Novemba 18, mara baada ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vita Kawawa amepongeza ujenzi huo kwa kuzingatia mahitaji ya Jes... |
null | MSIMAMIZI wa Uchaguzi Halmshauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) kimepeleka mawakala zaidi ya watatu katika baadhi ya vituo na haijulikani wanania gani. Lakini pia baadhi ya maeneo wagombea wa chadema wanataka kuwa mawakala katika baadhi ya vituo lakini kanuni hazip... |
null | Featured Tanzania Msimamizi wa uchaguzi aeleza kuhusu mawakala Chadema byNa Veronica Mheta, ArushaNovember 27, 2024 Biashara Featured Uchumi Mawaziri EAC kujadili utengamano uchumi, biashara byMwandishi WetuNovember 28, 2024 Africa Featured NeST yaibuka mfumo bora zaidi wa ununuzi wa umma Afrika byMwandishi WetuNovembe... |
null | NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Wilson Mahera amewataka Maafisa Uthibiti Ubora wa Wilaya kutilia mkazo sheria, kanuni, na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao. Dk. Mahera ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo elekezi kwa Maafisa uthibiti ubora wa Wilaya wateule, yali... |
null | DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Kaimu Rais wa Namibia Dk Nangolo Mbumba, mke wa Rais, Monica Kalondo, na wananchi wake kufuatia kifo cha Rais wa taifa hilo, Hage Geingob. “Kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Jamhuri ya N... |
null | KAMPUNI ya vifaa vya michezo, Adidas inapanga kuuza hisa zilizosalia za viatu vya Yeezy ikielezwa Kanye West hajaonesha ushirikiano kamili dhidi ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo ilikata uhusiano na rapper huyo na mbunifu wa mitindo, ambaye pia anajulikana kama Ye, mnamo 2022 baada ya kutoa maoni kadhaa ya chuki kwenye mit... |
null | MATAIFA yote 27 ya Umoja wa Ulaya yamekubaliana juu ya nyongeza ya msaada wa Euro bilioni 50 ($54bn) kwa Ukraine, licha ya vitisho kutoka kwa Hungary kupinga hatua hiyo. “Tuna mpango,” Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema katika chapisho kwenye X. “Hii inazuia ufadhili thabiti, wa muda mrefu, unaotabirika kwa... |
null | WINDHOEK, Namibia: RAIS wa Namibia, Hage Geingob (82) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Lady Pohamba jijini Windhoek alipokuwa akipatiwa matibabu. Akitoa taarifa kwa wananchi wa Namibia, Kaimu Rais, Dk Nangolo Mbumba amesema wanamibia washikamane na kuendeleza utulivu katika wakati huu wa maombolezo kw... |
null | BAADA ya Burkina Faso, Mali na Niger kutangaza kujiondoa ECOWAS, hatua hiyo imezua hisia mbalimbali. Waziri Mkuu wa Burkinabe alihalalisha uamuzi huo. “Tarehe 28 Januari, Burkina Faso, Mali na Niger zilichukua uamuzi wa kihistoria wa kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ECOWAS, ni uamuzi uliozingatiwa... |
null | WALINDA amani wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo wataondolewa wote kufikia Desemba 2024. Umoja wa Mataifa unasema. “Baada ya miaka 25 ya uwepo wa MUNUSCO rasmi wataondoka na na hakuna baadaye zaidi ya ifikapo mwisho wa 2024, Bintou Keita, kiongozi wa zoezi hilo ameeleza. Amesema kuondoka kwa wanajeshi hao nchini humo ku... |
null | MKUTANO Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi, umemvua uongozi na kumtimua uanachama, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia, wakati Makamu wake Angelina Rutairwa akivuliwa wadhifa wake. Pia mkutano huo ulitaka viongozi wote waliohusika na ubadhirifu wa mali akiwemo Mbatia kuchukuliwa hatua za kisheria. mkuta... |
null | MKOA wa Mtwara unatarajia kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Wiki Viziwi Kitaifa, ambayo yatafanyika Oktoba 26, mwaka huuu. Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu: Kujenga Jamii Jumuishi kwa Wote’ yamelenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki ya ustawi kwa viziwi. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewaomba wananchi kus... |
null | MKUU wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amewataka wakulima wa korosho wilayani humo, kutumia maarifa na ujuzi katika suala la utunzaji, ili waongeze tija. Buswelu ametoa rai hiyo kwenye utolewaji mafunzo kwa wakulima wa korosho, namna ya uzalishaji, utunzaji na unyunyiziaji viuatilifu yaliyofanyika Kijiji cha Kabu... |
null | SERIKALI imesema inasimamia kikamilifu sekta ya nishati, ikiwemo kuendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, ili kukuza uchumi. Kutokana na hali hiyo imewahakikishia wadau mbalimbali kuwa mradi huo unateke... |
null | MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoani Kigoma yametumia Sh bilioni 20.4 katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa Kigoma, Msafiri Nzunuri alisema hayo akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengeny... |
null | MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini, imekabidhi mifuko ya saruji yenye thamani ya Sh milioni 5 kwa uongozi Kijiji cha Majalila, kwa ajili ya ujenzi wa shule shikizi ya Inyagantambo, iliyopo Kata ya Tongwe, Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Meneja Uwanja wa Nd... |
null | MKUTANO wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaendelea Geneva, Uswisi, huku ujumbe kutoka Tanzania unaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka. Mkutano huo ulianza jana Jumatatu na unatarajiwa kumalizika Oktoba 7, mwaka huu. Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, inasema kuwa ... |
null | MAKAMU wa Rais wa Uganda, Jessica Alupo, ametembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kuahidi kurudi tena, ili kujifunza kwa kina kuhusu masuala ya urithi adhimu wa historia ya Tanzania. Alupo amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dk Noel Lwoga na kupatiwa maelezo ya uhifadhi wa urithi wa ut... |
null | UBALOZI wa Tanzania nchini China, umeitaka serikali ya mji wa Xian kutoa maelezo juu ya tukio lililotokea jana Septemba 12, 2022, likimuhusisha raia wa Tanzania akishambuliwa na mwanamke raia China mjini humo. Jana kulisambaa video fupi kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha kijana wa Kitanzania akishambuliwa na mwana... |
null | BALOZI wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi amesema wafanyabiashara wa Tanzania wana fursa ya kuuza mbogamboga na matunda katika soko la Ujerumani. Balozi Dk Possi alisema hayo Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa kwa njia ya video akieleza fursa na kazi zinazofanywa na ofisi ya ubalozi ... |
null | KAMATI za kudumu za Bunge za Nishati na Madini, pamoja na ya Bajeti zimewasili mkoani Mtwara leo kwa ajili ya ziara ya siku moja kutembelea miundombinu ya kuchakata gesi asilia Madimba, visima vya gesi MnaziBay na miundombinu ya kupokea mafuta Bandari ya Mtwara. Kamati ya Nishati na Madini inatembelea miundombinu ya ku... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.