name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | MCHIMBAJI mdogo wa madini ya Tanzanite Anslemu Kawishe amepata Sh bilioni 2.2 baada ya kuuza vipande viwili vya Tanzanite kwenye hafla iliyo hudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini Dk. Dotto Biteko na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Laurence Luoga. Mwezi Juni 2020, Mchimbaji madini Laizer Kury... |
null | WAFANYABIASHARA wa soko la Mgandini jijini Tanga, wametakiwa kutoa ushirikiano, ikiwemo taarifa kamili kwa makarani wa sensa, wanapopita kwenye maeneo yao, ili kuisadia serikali kupanga bajeti zake kama kuboresha miundombinu ya soko hilo. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Athuman Ramadhani, wakati akizungumza ... |
null | UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Nyamagana, umewataka wakazi wa wilaya hiyo, washiriki kikamilifu kwenye sensa ya watu na makazi pamoja na kutoa taarifa sahihi. Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa UVCC Wilaya ya Nyamagana, Boniphace Zephania, wakati wa Tamasha la kuhamasisha Sensa lililofanyika... |
null | MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA), imezitaka kampuni pamoja na watumiaji wa kemikali ya zebaki kuhakikisha wanajisajili Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, ambaye ndiye msajili wa kemikali za viwandani na nyumbani hapa nchini. Hayo yamesemwa leo na Mkemia mkuu wa Serikali Dk Fidelice Mafumiko, wakati wa... |
null | WALIMU wa Shule Shikizi ya Kijiji cha Nyabange, Kata ya Nyankanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara wanatumia choo kimoja na wanafunzi kwa upungufu wa vyoo. Serikali ya Kijiji hicho inahutuhumiwa kuchelewesha utatuzi wa kero hiyo, licha ya wananchi kuchimba shimo lingine la choo na kuchanga fedha za ujenzi. “Tuna wanafunz... |
null | MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA), Mkoa wa kikodi Kahama, imewataka wafanyabiashara kuacha kuwatumia wahasibu vishoka, ambao wamekuwa wakiwasababishia mtafaruku kwa kupewa madai makubwa ya kodi katika biashara zao. Hayo yamesemwa leo Agosti 22, 2022 na Meneja Msaidizi wa Ukaguzi wa Hesabu kutoka mamalaka hiyo, Honest Mush... |
null | NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amekagua mradi wa kitalu cha miche ya miti wenye thamani ya Sh milioni 43, unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza. Akizungumza leo katika ziara, Masanja amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuitunza miche ya miti ... |
null | LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika Dar es Salaam. Klabu ya Simba itakuwa wenyeji wa KMC kwenye uwanja wa KMC Complex, Mwenge Manispaa ya Kinondoni. Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 baada ya michezo tisa wakati KMC ni ya saba ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 10. SOMA: Viwanja ... |
null | NAIBU Waziri wa Nishati amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Umeme (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio vijiji vinavyolipishwa kuunganisha umeme kwa bei ya mjini ili kulipa bei stahiki ya vijiji ambayo ni Sh 27,000. Kapinga ametoa agizo hilo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk... |
null | MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) ofisi za Geita imeendesha semina kwa wafanyabiashara wa Busolwa wilayani Nyang’hwale iliyolenga kuondoa dhana potofu na utata juu ya masuala mbalimbali ya kodi. Akizungumuzia semina hiyo, Ofisa Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Mkoa wa Geita, Justine Katiti amesema semina hiyo ni mwendelezo... |
null | JANA gazeti hili lilikuwa na makala iliyoeleza wasifu wa Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT-Tanzania), Mary Rusimbi na namna anavyoelezea asili ya harakati za kijinsia, uongozi na alivyoamua kuanzisha kituo cha ‘kutibu’ wanawake kihisia na kisaikolojia. Leo mwandishi Stella Nyemenohi anaangazia harak... |
null | OFISA Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Robert Kwela amesema kundi la vijana wanaotakiwa kupata mkopo umri wao umeongezwa kuanzia miaka 18 hadi 45 tofauti na zamani ulikuwa umri kuanzia 18 hadi 35. Kwela amesema hayo leo kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha robo ya pi... |
null | PAZIA la Ligi Kuu ya mpira wa miguu kwa wanawake Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 linafunguliwa leo kwa michezo mitano viwanja tofauti. Bingwa wa simu uliopita Simba Queens itaanza kampeni kutetea taji hilo dhidi ya Mlandizi Queens kwenye uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni Dar es salaam. Miamba mingine ya so... |
null | Jukwaa linaloongoza kwa huduma za usafiri Tanzania Bolt, limetangaza ongezeko la nauli ya asilimia 10 baada ya kushughulikia maombi yaliyotolewa na wabia wake (madereva) kuhusu mapato yao. Kwa mujibu wa jukwaa hilo, ongezeko jipya la nauli limeanza Novemba 5, mwaka huu na dhamira yake ikiwa ni kuhakikisha madereva wana... |
null | KOCHA Mkuu timu ya taifa “Taifa Stars’ Hemed Suleiman ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiandaa na michezo miwili kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) dhidi ya Ethiopia na Guinea. Kocha Hemed amewataja wachezaji hao kuwa ni Aishi Manula, Zuber Foba, Metacha Mnata, Lusajo Mwaikenda, Shom... |
null | KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya kwamba wanawazidi Tabora United kwa ubora wataingia uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Novemba 7 kwa kuwaheshimu kuhakikisha wanapata pointi tatu. Gamondi amesema hayo leo Dar es Salaam kuelekea mchezo huo kwenye Uwanja wa Azam Complex. “Yanga ndio timu... |
null | BAADA ya rekodi ya kutopoteza mchezo wala kufungwa bao raund nane kuingia doa, klabu ya Yanga leo inashuka dimbani dhidi ya Tabora United katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Yanga ilipoteza mchezo iliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Az... |
null | MKUU wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian amewahimiza wakuu wa wilaya na wasimamizi wa uchaguzi mkoani humo kuhakikisha upigaji kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, mwaka huu unafikia asilimia 100. Dk Batilda ameyasema hayo leo na Dk Batilda alipofanya ziara ya kukagua maandalizi ya uchaguzi huo katika ... |
null | KIKAO cha kamati ya pamoja cha wataalamu wa Tanzania na Uganda kimeanza mkoani Kagera kujadili uiamarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo. Kikao hicho kimeanza Novemba 5, na kutarajiwa kumalizika Novemba 7, na kinafanyika katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa kuhusisha wataalamu kutoka nchi za Tanzania na... |
null | DAR ES SALAAM: JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni Dar es Salaam, limepanda miti 500, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji katika mkoa huo, Elisa Mugisha ameeleza hayo baada ya kukamilisha upandaji miti aina ... |
null | ZAIDI ya kampuni 100 zinatarajiwa kushiriki maonesho ya famasia maarufu kama ‘Pharmatech East Africa’ yanayorajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Agosti 30 hadi Septmba Mosi, mwaka huu. Hayo yameelezwa na Rais wa Chama cha Wafamasia nchini (PST), Fadhili Hezekiah wakati wa semina kwa wanahabari iliyofanyika leo, Ijumaa... |
null | WATU 1,648,219 kati ya 8,599,228 waliochoma chanjo ya Pfizer na Sinopharm katika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti 14 hawajarudi kupata chanjo ya pili, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya. Taarifa ya Wizara ya Afya inafafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Julai watu 1,712,107 walichoma chanjo ya Pfiz... |
null | HUDUMA za kibingwa za Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) zitaanza kutolewa katika hospitali mpya na ya kisasa ya rufaa ya kanda Mtwara ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ahmed Abbas alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesh... |
null | DAR ES SALAAM: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa rai kwa wadau wa maendeleo kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwekeza kwenye sekta ya afya nchini huku wakiiga mfano wa Kampuni ya uzalishaji wa Dawa ya Cure Afya ambayo iko mbioni kuanza uzalishaji wa dawa hapa nchini. Waziri Ummy ameyasema hayo leo Desemba 20,202... |
null | DAR ES SALAAM: MKURUGENZI Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, ametoa zawadi kwa wafanyakazi wake kwaajili ya Kusherehekea Sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya. Christmas itakuwa Jumatatu ya wiki ijayo ambapo wakristo wote ulimwenguni watasherehekea sikukuu hiyo ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo... |
null | DAR ES SALAAM: MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeboresha huduma za kitita cha mafao na kuleta unafuu kwa mwananchi katika gharama za ushauri, dawa na matibabu yakiwemo ya kuchuja damu na upasuaji. Kwa mfano katika eneo la kuchuja damu, gharama ya kufanyiwa haemodialysis ni Sh 240,000 lakini bei iliyoboreshwa ni ... |
null | MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imefanya oparesheni maalum ya siku nne ya ukaguzi na msako wa bidhaa za afya na kukamata dawa na vifaa tiba bandia na duni, dawa na vifaa tiba vya serikali na bidhaa zilizoisha muda wake. Oparesheni hiyo imefanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mikoa ya Dar es Salaam, ... |
null | DAR ES SALAAM: KUNAWA kwa kuingiza vidole sehemu za uke, kujifukiza na matumizi ya bidhaa mbali mbali ikiwemo asali kuwekwa ukeni, wapenzi wengi, kujamiiana katika umri mdogo, maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kumetajwa kusababisha ongezeko kubwa la saratani ya kizazi. Tafiti zinaonesha kuwa wale wanaojisafisha seh... |
null | DAR ES SALAAM: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka Taasisi ya Saratani Ocean Road hadi kufikia Februari Mosi, 2024 kuanza kutumia mashine ya Pet-CT Scan ili rufaa za kwenda nje ya nchi zipungue. Waziri Ummy ametoa tamko hilo leo baada ya kufanya ziara ya kujionea huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Saratani Ocean R... |
null | DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila awewaagiza watendaji wote wa serikali zoezi la kufanya usafi ni kwa kila wiki sio kila mwezi kama ilivyokuwa awali ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko. Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam, kwenye mkutano na watendaji wa serikali kuhusu tahadhari dhidi ... |
null | MAKAMU wa Rais, Philip Mpango ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu majumbani na kuwakosesha haki ya kupata elimu. Akizungumza wakati akifungua shule ya msingi ya elimu mjumuisho Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Ma... |
null | HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando iliyopo jijini Mwanza kwa mara nyingine imeingia mkataba na Kampuni ya Utengenezaji wa Mifumo ya Kielektroniki Sekta ya Afya (GPITG) kwa lengo la kuendelea kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma za afya hospitalini hapo. Akizungumza leo Januari 11, 2024 jijini Mwanza, Mkurugenzi w... |
null | HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa imepokea msaada wa kadi za Bima ya Afya kwa mama na watoto 200 kutoka kwa kampuni ya tekenolojia ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia kampeni yake ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha.’ Baadhi ya wanawake na watoto wenye sifa za kupata kadi hizo zitakazowawezesha kupata huduma za ... |
null | DODOMA: WIZARA ya Afya imewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa macho mekundu (Red eyes) maambukizi ya kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” iliyoibuka nchini hivi karibuni. Hayo yamesemwa leo Januari 15, 2023 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wiza... |
null | MADAKTARI bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano. Akizungumza leo Januari 16, 2024 Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mwanaada Kilima amesemashanga hiy... |
null | BAGAMOYO, Pwani: KATIKA kuokoa mali za serikali kwa kuokoa ajali za barabarani madereva wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wameanza kupewa mafunzo na Jeshi la Polisi. Mafunzo hayo yanatokana na kuitikia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilolitoa Septemba 23, 2023 wakati akizungumza na madereva na kusisitiza ush... |
null | DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza huduma za dharura zipelekwe kwenye maeneo yaliyopata athari kutokana na kimbunga Hidaya. Hayo yamesemwa leo Mei 06, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye kikao cha dharura cha Kamati ya Maafa Kitaifa alichokiitisha kupokea taarifa ya hatua zilizochukuliwa kwenye maeneo ya... |
null | DODOMA: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa nchini waakisi utashi wa kisiasa wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia na kutekeleza mapendekezo yote yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai. Ametoa wito huo leo Mei 06, 2024 wakati akifungua warsha ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya kuwajen... |
null | DODOMA: WAKATI wimbi kubwa la vitendo vya ukatili wa kijinsia na ushoga vikiwa vimeshamiri, serikali imetoa msimamo wake kuwa atakayebainika kufanya vitendo hivyo ataadhibiwa miaka 30 jela huku ikiwa imeunda kamati 18,186 za ulinzi na usalama wa wanawake na watoto. Akizungumza leo Mei 07, 2024 Naibu Waziri wa Maendeleo... |
null | ZANZIBAR: SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inahitaji uwekezaji mkubwa wa sekta za Maji na Umeme ili kuongeza ufanisi wa huduma za uhakika kwenye sekta hizo. Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa leo imetanabahisha kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumz... |
null | DODOMA: NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk Festo Dugange amesema takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano bado ni kikubwa ambapo kwa Mkoa wa Kigoma ni asilimia 27.1, Katavi asilimia 32.2, Njombe asil... |
null | WAFANYABIASHARA wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), watanufaika na usafirishaji wa haraka wa bidhaa zao kwa gharama nafuu kwenda nchini India, baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya biashara kati ya jumuiya hiyo na serikali ya India. Mpango huo wa pamoja wa utekelezaji utafungua fursa za biashara kati ya pande... |
null | IKIWA ni takribani miezi sita sasa bado bei ya mafuta ya kupikia imeendelea kuwa mwiba, serikali imewatoa wasiwasi wananchi kwamba tatizo hilo linaelekea ukingoni baada ya wakulima kuvuna alizeti kwa wingi. Kwa takribani miezi sita, bei ya bidhaa hizo imekuwa ikipaa kuliko kawaida katika mikoa mbalimbali nchini. Akizun... |
null | Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe akikata utepe kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa jana, baada ya kufanyiwa ukarabati. Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja kukarabati maktaba katika mikoa saba nchini. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Makta... |
null | Picha Profesa James Mdoe akikata utepe kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa byNa Mpigapicha WetuAugust 19, 2021 Michezo na Burudani Picha Kikosi cha Yanga chawasili Sheikh Amri Abeid byNa Mwandishi WetuAugust 20, 2022 |
null | MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) ,Hamza Johari amesema kukamilika kwa jengo la ofisi ya kanda pamoja na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani Arusha kutawezesha utoaji huduma za kisheria kwa wananchi kwa karibu zaidi. Ameyasema hayo wakati wa kutembelea ofisi ya Mwanasheria wa Serikali mkoani Arusha zilizopo nd... |
null | RUVUMA: RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya Sh bilioni 24 kwa ajaili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Nantumbo Mkoa wa Ruvuma. Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ametoa taarifa hiyo leo Novemba 21, 2024 wakati wa... |
null | KATIBU wa NEC, Siasa na Uhusi ano wa Kimataifa (SUKI) na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Rabia Hamid amewataka wakazi wa Kilimanjaro kuwachagua wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho ... |
null | WAZIRI Mkuu, Kassim Majal iwa ameiagiza Kamati ya Wataalamu ya Uchunguzi wa jengo lili loporomoka katika eneo la Kariakoo ifanye kazi kwa weledi. Majaliwa alisema hayo kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam wakati anaizindua kamati hiyo kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuchung... |
null | LITHUANIA : CHAMA cha upinzani nchini Lithuania “Social Democrats” kimepiga kura ya maoni bungeni na kuongoza dhidi ya Chama tawala “Homeland Union Party” kwa kutokuwa na imani na serikali kufuatia ongezeko kubwa la gharama za maisha na usalama wa nchi hiyo . Chama cha Social Democrats kiliongoza kwa viti 33 baada ya k... |
null | MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imeweka wazi kuwa itajikita zaidi katika mfumo shirikishi na elimu kwa mlipa kodi ili kuwawezesha wafanyabiashara siyo tu kulipa kodi kwa wakati bali pia kuongeza faida kwenye biashara zao. Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Paul Walalaze amesema hayo wakati akizungumza na wafanya... |
null | MALI : JESHI la Mali limesema limewauwa magaidi 40 na kuharibu ngome zao katika operesheni mbili zilizofanyika nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Mali nchini humo imesema katika operesheni iliyofanyika Alhamisi na Ijumaa wiki iliyopita katika mji wa Ounguel iliweza kuharibu ngome moja magaidi na... |
null | ISRAEL : WABUNGE nchini Israel wamepitisha mswada wa sheria wa kupiga marufuku wa shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi wa kipalestina – UNRWA kuendesha shughuli zake ndani ya Israel kuanzia mwaka 2025. Hatua hii ya Israel inaweza ikatishia kazi za shirika hilo huko Gaza hasa ukizingatia inategemea v... |
null | MALAWI : KIONGOZI wa chama cha upinzani –UTM nchini Malawi,Patricia Kaliati amefikishwa mahakamani akituhumiwa kupanga njama za kumuua Rais Lazarus Chakwera. Kaliati ni Katibu Mkuu wa chama cha UTM, ambaye alikamatwa wiki iliyopita kwa tuhuma za kutaka kumuua Rais Chakwera. Hapo jana, Mwanasiasa huyo alifikishwa mahaka... |
null | TIMU nane za waendesha pikipiki (bodaboda) zimeanza kupambana katika ligi maalum kwa ajili ya kuhamasisha masuala ya usalama barabarani na masuala ya afya ya uzazi huku mshindi wa mashindano hayo akitarajia kuibuka na kitita cha Sh milioni Mkurugenzi wa kituo cha Main FM Redio ambao ndiyo waandaji wa mashindano hayo, P... |
null | WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Pindi Chana ameelekeza timu ya askari uhifadhi 18 kuweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ili kukabiliana na tembo wanaovambia makazi ya watu. Hatua hiyo inafuatiwa na tukio la hivi karibuni la tembo kuwepo katika eneo hilo na kusababisha taharuki kwa wa... |
null | WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amewahimiza wawekezaji wa mazao ya misitu kutoka nchini China kuanzisha viwanda kwa lengo la kuuza bidhaa zilizokamilika kwa ajili ya masoko ya nje ya nchi. Dk Chana amezungumza hayo leo Oktoba 27, wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Wawekezaji wa Mazao ya Misitu wa Chin... |
null | LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kufanyika Arusha na Mbeya. ‘Wagosi wa kaya’ Coastal Union itakuwa mwenye wa ‘walima miwa’ Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Coastal ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 8 baada ya michezo tisa wakati Kagera Suga... |
null | MWIMBAJI wa nyimbo za Injili kutokea nchini Rwanda, Israel Mboni anayetamba na wimbo wake wa ‘Nina Siri’ ametua nchini tayari Tanzania kutoa huduma katika tamasha la uimbaji. Matamasha hayo yanayotarajia kufanyika Novemba 2 ukumbi wa Mlimani City na Novemba 3 mwaka huu katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. A... |
null | KENYA : ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua ameondolewa haki ya ulinzi na usalama. Akithibitisha hilo, Gachagua amesema lolote likimpata basi Rais William Ruto atawajibika na kadhia hiyo. Gachagua bado ameendelea kusisitiza mashtaka aliyofunguliwa yalichochewa na masuala ya kisiasa dhidi yake. Naye Msem... |
null | MOLDOVA : KURA ya maoni iliyopigwa nchini Moldova ya mabadiliko ya katiba haijaonyesha ushindi wa kuruhusu nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya . Mpaka sasa kura zilizopigwa zinaonyesha kuna mgawnayiko mkubwa wa kura za ndio au hapana ambazo zinaenda sambamba huku zikisalia kura asilimia 2% tu kuhesabiwa Katika kura hi... |
null | MISRI : MKUU wa Shirika la Afya Duniani – WHO, Tedros Adhanom ametangaza ugonjwa wa malaria Misri utabaki kuwa historia . “Malaria ni ugonjwa wa zamani lakini ugonjwa huu uliwasumbua wengi nchini humo lakini sasa ni historia,” alisema Tedros. Katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini humo, Misri iliamua kuchu... |
null | RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema taifa hilo linasitisha ushiriki katika mkataba wake mkuu wa mwisho wa udhibiti wa silaha za nyuklia dhidi ya Marekani. – Katika hotuba yake iliyoitoa leo Mjini Moscow, Putin amesema hajajitoa moja kwa moja katika mkataba huo. “Nimelazimika kutangaza leo kwamba Urusi inasitisha ushi... |
null | NIGER : UTAWALA wa kijeshi nchini Niger umepiga marufuku mauzo ya nje ya nchi ya nafaka kwa nchi zote isipokuwa nchi zinazoongzowa kijeshi ikiwemo Burkina Faso na Mali. Taarifa iliyotolewa na serikali imesema kuwa kiongozi wa kijeshi wa Niger Abdourahmane Tiani amechukua hatua hiyo ili kulinda usambazaji wa soko la nda... |
null | RWANDA : MAAMBUKIZI ya virusi vya ugonjwa wa Marburg nchini Rwanda yamepungua baada ya watu waliokuwa hatarini kuanza kupatiwa chanjo. Waziri wa afya nchini Rwanda Sabin Nsanzimana amesema tangu serikali kwa kushirikiana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC kutoa chanjo maambukizi ya ugonjwa huo yamepun... |
null | CONGO : MAPIGANO yamezuka tena kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huko Mashariki mwa nchi hiyo. Mapigano haya yamevunja makubaliano ya usitishwaji wa mapigano ambayo yamedumu kwa wiki kadhaa. Jumapili ya wiki hii kikundi cha waasi wa M23 walipambana na wa... |
null | DAR ES SALAAM: Takwimu zinawapa nguvu waandishi wa habari nafasi ya kujiamini, kuibua na kuhoji kwa sababu takwimu zipo wazi na hakuna atakayemsumbua. Hayo yamesemwa leo Machi 13, 2024 na Kamisaa wa Sensa Anna Makinda jijini Dar es Salaam akizungumzia usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya Mwak... |
null | MICHEZO tisa inapigwa leo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya ligi. Liverpool inaongoza kundi la michuano hiyo inayoshirikisha timu 36 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo mine wakati Slovan Bratislava ipo mwisho wa msimamo haina pointi. SOMA: Arsenal vs PSG: Kibabe Ligi ya Mabingwa Ulaya Mitanange inayop... |
null | MIAKA 60 ya ushirikiano baina ya Serikali na Tanzania na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA,) imekuwa ya mafanikio makubwa hasa kwa JICA kuendelea kukua na kujitanua kusaidia kutoa misaada na kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na uchumi nchini kwa kushirikiana na Serikali kwa kufuata vi... |
null | WASIMAMIZI na wasimamizi wasaidizi 250 wa vituo mbalimbali vya kupigia kura wameapishwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024. Akizungumza wakati wa ghafla hiyo fupi ya uapisho kwa wasimamizi hao, msimamizi wa uchaguzi katika mani... |
null | KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, Amos Makalla amesema chama hicho kimejipanga kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024. Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibamba na Kawe Dar es Salaam jana, alisisitiza kuwa CCM haina mas... |
null | DAR ES SALAAM: MENEJA wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga amesema kilometa 497 mkoani humo zimeathiriwa na mvua zilizoambatana na Elinino zilizoanaza Oktoba 5 ,2023 hadi Mei 2024 Mkinga amesema kutokana na uharibifu huo Tarura Mkoa wa Dar es Salaam imelazimika kukarabati barabara hizo, vivuko na ma... |
null | DODOMA. SERIKALI imesema ikipokea hoja kutoka kwa wadau walio wengi kuhusu hitaji la mabadiliko ya kanuni ya uchaguzi wa Naibu Meya na Naibu Wenyeviti wa Halmashauri itafanyia kazi. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange kutokana na swali la Mbunge wa Viti Maalum, Janejelly Ntate, ... |
null | DODOMA: Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Jerry Silaa amefunga Masijala ya Ardhi ya Jiji la Dodoma ikiwa ni hatua ya wizara yake kuondoa changamoto za sekta ya ardhi katika jiji la Dodoma. ‘’Tumeamua kufunga masijala hii ya jiji, nimetoka kuweka makufuli tumeifunga. Tunahamisha shughuli hizi za ardhi kutok... |
null | Mallorca, HISPANIA; JENGO la ghorofa mbili katika kisiwa maarufu cha utalii nchini Hispania cha Mallorca limeporomoka na kuua watu wanne na kujeruhi watu 21. Jengo hilo, ambalo lilikuwa na mgahawa, liliporomoka katika eneo la Playa de Palma, Kusini mwa mji mkuu wa Kisiwa cha Mediterania, Palma de Mallorca. Taarifa ya h... |
null | MOROGORO; POLISI mkoani Morogoro inamshikilia dereva wa basi la Kampuni ya Shabiby lenye namba za usajili T 341 EEU, Said Malugula akituhumiwa kusababisha ajali iliyojeruhi abiria 22, baada ya basi hilo kupinduka eneo la Kihonda kwa Chambo mkoani Morogoro. Kamanda wa Polisi Mkoa Morogor, Alex Mkama amesema leo Mei 25, ... |
null | ARUSHA; JESHI la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha, wamekamata watuhumiwa wanne na punda 46 wakisafirishwa kinyume cha taratibu kwenda nje ya nchi. Kamanda wa Polisi kikosi hicho, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (S... |
null | KUELEKEA uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara, Abdallah Mwaipaya amewataka wanavyuo wote na wanafunzi waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Akizungumza kwenye Mtwara Samia Uni Bonanza, mkuu ... |
null | MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameendelea kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa wale wote waliyojiandikisha na wenye sifa ya kupiga kura wasiache kutumia nafasi hiyo kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024. Akizungumza leo mkoani Mtwara alipotoa taarifa hiyo kwa w... |
null | PEMBA, Zanzibar: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imejenga skuli za kisasa za ghorofa mijini na vijijini pamoja na maeneo ya visiwa vidogovidogo ikiwemo Gamba, Kojani, Tumbatu. Amesema ahadi ya CCM iliandika kujenga mabanda ya skuli, ambapo Serikali ya awamu ya nane inaendelea kujenga zkuli za k... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassana amebainisha mambo matatu waliyozungumza katika Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali zenye Uchumi Mkubwa zaidi Duniani (G20) uliofanyika Brazil, mojawapo ikiwa ni ajenda ya nishati safi ya kupikia na mikakati ya kupunguza njaa. Rais Samia alibainisha hayo wakati wa mahojiano baina yake na wahar... |
null | ZANZIBAR; WATAALAMU kutoka Shirika la Kimataifa la Upasuaji wa Wanawake (ISGE) na Chama cha Wanagyna na Wakunga Tanzania (AGOTA) wanatarajia kukutana Zanzibar Mei 21-24, 2025. Taarifa iliyotolewa na Meneja wa mkutano huo, Ibrahim Mitawi wa Showtime Company leo Novemba 25, 2024 imeeleza huo utakuwa mkutano wa 7 wa ISGE,... |
null | Katika mahafali ya 16 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa yaliyoongozwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Jakaya Kikwete leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Chuo hicho na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof William Anangisye, amewahimiza wahitimu kutumia elimu yao kama nyenzo ya kubuni ajira n... |
null | WATU watano wamekufa na 15 wamejeruhiwa baada ya basi la Tanzanite kuacha njia na kupinduka katika mlima Saranda wilayani Manyoni mkoani Singida kwenye Barabara Kuu ya Manyoni – Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 9:30 alasiri, ikihusisha basi hilo lenye na... |
null | JESHI la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limetangaza kuanza oparesheni kukagua magari na kuwachukulia hatua za kisheria madereva wanaofanya makosa barabarani. Jeshi hilo limetangaza oparesheni hiyo siku chache baada ya mfululizo wa ajali za barabarani katika mikoa ya Mtwara, Tanga, Singida, Shinyang... |
null | SERIKALI imewaagiza wamiliki na waendeshaji wa vituo vya kulea watoto nchini kote kuhakikisha kila mtoto anayepokelewa anaandaliwa mpango wa huduma wa kumuandaa kuondoka makaoni. Pia imepanga kuanzisha mjadala wa wadau ili kuja na sheria ya malezi ambayo itawalazimisha wazazi kutimiza wajibu wao kwa malezi ya watoto. M... |
null | MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amefanya ubunifu wa kuzindua namba ya dharura kwa wananchi wa mkoa huo ili kupiga na kutoa taarifa ya changamoto mbalimbali wakati wa sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu. Akizungumza baada ya kukagua mafunzo ya makarani katika kituo cha Buigiri katika S... |
null | SIMIYU: Serikali imetangaza rasmi bei elekezi ya ununuzi wa zao la pamba katika msimu wa mwaka 2024/2025 kuwa ni Sh 1,150 kwa kilo moja ya pamba daraja la kwanza na daraja la pili ikiwa ni Sh 575 kwa kilo moja. Bei hiyo imeongezeka kwa Sh 90 kutoka bei iliyotangazwa msimu wa mwaka jana 2023, ambapo kilo moja ilitangazw... |
null | DODOMA:Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameipongeza Timu ya Yanga kwa kuendelea kuwa katika kiwango bora kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki. Akizungumza leo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025, Aweso amesema kama mpinzani wa kweli ni lazima akubali ki... |
null | BAADA ya kutopata ushindi kwenye mechi 5 zilizopita, timu ya Mashujaa ya Kigoma, leo imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC ya Kinondoni katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mabao ya mashujaa FC yamewekwa kambani na Josephat Jeremanus dakika ya 11, Ali Hassan dakika 22 kabla ya Reliant Lusajo kukamilisha la tatu... |
null | DAR ES SALAAM; WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema mkakati wa nishati safi ambao umezinduliwa leo utakuwa chombo muhimu cha kuleta juhudi za pamoja na shirikishi kufanikisha ajenda ya utunzaji mazingira Amesema hayo leo Mei 8, 2024 kwenye uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia wa mwaka 2024-2034, ulio... |
null | TANGA: KLABU ya Coastal Union imethibitisha kupokea ofa kutoka timu tatu za Ligi Kuu Tanzania bara wakiwemo Simba SC, Azam FC na Ihefu FC zote zikihitaji huduma ya beki Lameck Lawi ambaye amekuwa na kiwango kizuri ndani ya kikosi cha Wagosi wa Kaya kwa msimu huu wa 2023/2024. Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyeki... |
null | DAR ES SALAAM; WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), unaadhimisha siku ya miliki bunifu, ambayo pia inaonesha namna nchi inavyoweza kutambua mchango wa wabunifu kuleta maendeleo. Mkurugenzi wa miliki bunifu kutoka Brela, Loy Mhando amesema hayo leo wakati akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika kesho D... |
null | LEBANON : KUNDI la Hezbollah limetangaza ushindi dhidi ya Israel baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema wapiganaji wake wako tayari kukabiliana na vitisho vya Israel siku zijazo. Licha ya vikosi vya Israel kusababisha hasara kubwa kwa kundi hilo ikiwemo kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah Hassa... |
null | LEBANON: SERIKALI ya Israeli iko tayari kupitisha mpango wa Marekani wa kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah. Hivi sasa Baraza la Usalama la Israel linatarajia kukutana baadaye leo Jumanne ili kujadili na kuidhinisha mpango huo katika kikao maalum kitakachoongzowa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Tayari mka... |
null | ULAYA: KUJUMLISHWA kwa Botswana kama mthibitishaji kunaonekana kukusudiwa kuokoa mpango wa utekelezaji wa kusitisha kuagiza almasi Urusi baada ya mataifa ya Afrika kulalamika kuwa uchumi wao utaathirika. Botswana ni miongoni mwa nchi zinazozalisha almasi barani Afrika, itaungana na Antwerp kama mthibitishaji wa chimbuk... |
null | ETHIOPIA : Imeelezwa kuwa mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya Shirikisho vya Ethiopia na wanamgambo kaskazini mwa magharibi nchini humo yanaweza kuleta athari kwa wakimbizi wanaotoka Sudan. Haya yamesemwa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, lenye makao yake huko New York, Ma... |
null | “NILISIKIA kama tetemeko ambalo huwezi kujua limetokea wapi na ile kuangalia juu, nikaona nyufa na ukuta unatikisika. “Nilipotaka kutoka, nikaona kitu kama kinanivuta, nikaanguka palepale kwenye mezani kwa chini.” Mmoja wa majeruhi katika ajali ya kuporomoka kwa jengo katika Kata ya Kariakoo Dar es Salaam, Novemba 16, ... |
null | ARUSHA:Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Fedha iimarishe mifumo ya kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha ili baadhi ya watoa huduma wasio waadilifu wasitumie changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya fedha kwa baadhi ya wananchi na kuwadhulumu. Pia, Majaliwa amesema Wizara ya Fedha iendelee kushirikiana n... |
null | DAR ES SALAAM: Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imeungana na wadau wengine wa sanaa katika kikao kazi cha uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Maendeleo ya Filamu na Sanaa Tanzania linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Tamasha hilo ambalo litafanyika Desemba, mwaka huu linaratibiwa na taasisi ya FAGDI (Founda... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.