name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | SERIKALI imeahidi kuwawezesha wajasiliamali vijana na wanawake kwa kuwapatia maarifa, masoko, fursa za kijamii na kiuchumi ili kupiga hatua katika kujenga uchumi wa familia na jamii. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete ametoa ahadi hiyo leo Novemba 15, 2024 kwenye... |
null | MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imesema Bandari ya Mtwara iko imara na inaendelea kuhudumia mizigo ikiwemo shehena ya korosho kwenda nje ya nchi. Meneja wa bandari hiyo, Ferdinard Nyathi amesema mpaka sasa meli tano zimefika na kupakia shehena ya korosho na kusafirishs kwenda masoko ya nje. ‘Napenda kuwahakikishi... |
null | HALMASHAURI ya Mji wa Babati mkoani Manyara imekabidhi hundi ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa vikundi 19 vya vijana, wanawake na makundi maalum. Fedha hizo zimetokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri ya asilimia 10 zinazolenga kutoa mkopo usio na riba kwa wajasiriamali wadogo ili kujiinua kiuchumi. Akikabidhi... |
null | Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imeokoa zaidi ya Sh milioni 13 ambapo milioni 4.8 zilitokana na thamani ya dawa zilizokuwa zimeibiwa kwenye Zahanati ya Orkirung’rung na kurejeshwa baada ya kufanyika ufuatiliaji wa taasisi hiyo. Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 19, 2024 na Mkuu wa T... |
null | DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi ili serikali ikusanye mapato kwa haki yatakayoiwezesha kutimiza wajibu wake ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii Rais Samia ametoa wito huo kwenye Baraza la Iddi el- Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutan... |
null | Mkutano wa 29 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) umeendelea kuiletea manufaa Tanzania hususan katika hifadhi ya mazingira. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga amesema hayo wakati akizungumza mara baada ya kutembelea banda la... |
null | WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza mkandarasi wa mradi wa maji wa miji 28 kuhakikisha unakamilika kabla ya wakati ili kuwaondolea wananchi adha ya ukosefu wa maji. Maagizo hayo ameyatoa wilayani Pangani wakati alipotembelea ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji katika eneo la Madanga na kimang’a. “Huu mradi fedha zak... |
null | RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameipongeza na kuipatia Timu ya Taifa ya Tanzania shilingi Milioni 700 kwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025 nchini Morocco, baada ya kuifunga Guinea goli 1-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro amese... |
null | DAR ES SALAAM: BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imezindua rasmi mtaala wa wakufunzi wa elimu ya fedha nje ya mfumo rasmi ambapo wananchi watapata elimu ya matumizi sahihi ya fedha ikiwemo akiba ili kuepuka mikopo umiza na kausha damu. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BOT, Emanuel Tutuba... |
null | MBEYA: Mkazi wa Mbeya, Beth Mayunga ameibuka mshindi wa Sh milioni 20 kupitia kampeni ya ‘Ni Balaa’ inayoendeshwa na kampuni ya huduma ya mawasiliano ya Vodacom. Licha ya kupata kiasi hicho, Beth ana jukumu la kuchagua shule moja ambayo kampuni hiyo ya mawasiliano itaifanyia ukarabati, ikiwa miongoni mwa mikakati wa ku... |
null | WAMILIKI wa magari hasa ya abiria wamekumbushwa kujenga tabia ya kuvifanyia marekebisho ya mara kwa mara vyombo hivyo hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ili kuepusha ajali zinazoweka kuepukika. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Karimkee Group, Amit Singh wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha kisasa cha... |
null | MWENYEKITI mpya wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na ushirikiano mkubwa na watumishi na wadau wote wa sekta ya madini. Lekashingo ametoa ahadi hiyo leo Novemba 8, 2024 mara baada ya kuripoti ofisi za Tume ya Madini zilizopo Kikuyu, jijini Dodoma tayari kuanza majukumu yake... |
null | MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango anatarajia kuondoka leo Novemba 08 kuelekea Baku, Azerbaijan, kumwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29), unaotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 11 ha... |
null | NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko leo Novemba 8 amemwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika sherehe za uapisho wa Rais wa sita wa Botswana, Gedion Duma Boko. Uapisho huo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo umeshuhudiwa na mamia ya wananchi wa Botswana pamoja na wageni mbalimbali wa... |
null | HALMASHAURI ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imekabidhi vishikwambi 50 kwa madiwani pamoja na wataalam mbalimbali kwenye manispaa hiyo vilivyogharimu zaidi ya Sh milioni 32. Akitoa taarifa kuhusu vishikwambi hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama Athumani Mfaume am... |
null | JAMII mkoani Mtwara imehimizwa kuzingatia suala la elimu jumuishi na badala yake iondokane na mila na desturi ambazo haziwakubali watoto wenye mahitaji maalumu katika kupata elimu kama haki yao ya msingi. Hayo yamesemwa wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani humo kuhusu kuwajengea uelewa ili waweze kuuelewa mkak... |
null | DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde amesema wizara hiyo imejipanga kutumia njia za kisasa za kupata taarifa za kijiolojia kupitia mpango wa “Vision 2030, Madini ni maisha na Utajiri”, ili kuhakikisha sekta ya madini inalinuafaisha taifa, hivyo kuboresha maisha ya Watanzania. Amesema hatua hiyo inatokana na... |
null | MWENZA Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Jwani Maria Yengi, amenyoshewa kidole na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James, na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Benito Kayugwa, akilalamikiwa kuwa na utendaji usioridhisha na kukosekana kwa ushirikiano na watumishi wenzake. Katika kikao cha Baraza la Madiwani ... |
null | MKUU wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye ameutaka Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) Mkoa Kigoma kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwenye sekta ya maji unajibu mipango ya Rais Samia katika kusogeza huduma karibu na wananchi (kumtua mama ndoo). Akizungumza wakati akikabidhi gari kwa ofisi ya Meneja wa Ruwa... |
null | RIPOTI ya kwanza ya uwajibikaji kwa Jamii mwaka 2023 iliyozinduliwa leo na Kampuni ya China Communications Construction Co Ltd imeonesha kuwa na ushawishi mkubwa wa kuboresha viwango vya sekta ya ujenzi Tanzania. Katika ripoti hiyo, kampuni hiyo imeeleza miongoni mwa ushawishi walionao ni mwongozo wa kiufundi ambapo vi... |
null | MANYARA: Umoja wa Wenza wa viongozi “Ladies of New Millenium Women Group” wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyokabiliana mafuriko yaliyosabisha maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang, mkoani Manyara. Akizungumza na waathirika katika kambi iliyopo shule ya se... |
null | SHINYANGA: JESHI la polisi mkoani Shinyanga limekamata simu 61 zilizokuwa zikimilikiwa na wanawake ambao wanajihusisha na wizi maeneo tofauti ya kwenye minada ya Kahama na Mwanza kwa kipindi cha wiki tatu kuanzia Novemba hadi Desemba mwaka huu. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Janeth Magomi amesema hayo leo alipozungumza... |
null | SIMIYU: WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema mwezi ujao serikali inatarajiwa kutangaza nafasi za kazi 25,000 kwenye sekta ya afya na elimu ili kukabiliana na upungufu wa watumishi uliopo. Pia amewataka watendaji na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kut... |
null | DAR ES SALAAM: SERIKALI imefanikiwa kukusanya Sh bilioni tano kwa ajili ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na maji kutoka mlima Hanang wilayani Hanang mkoani Manyara yaliyotokea alfajiri ya Desemba 3, mwaka huu. Sambamba na hilo, serikali imepokea misaada ya chakula, vitu na vifaa mbalimbali kutoka kwa watu b... |
null | MAHAKAMA ya Juu ya Colorado imeamua kuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump hastahili kugombea urais wa taifa hilo kwasababu ya shambulio analohusishwa nalo la mwaka 2021 katika makao makuu ya Bunge Capitol Hill. Uamuzi huo ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwamba Kifungu cha 3 cha Marekebisho ya 14, a... |
null | MKURUGENZI wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dk. Ntuli Kapologwe amesema mbio za ‘Reunion Fun Run’ zilizoandaliwa kwa msimu wa tatu na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) zimelenga kutengeneza miundombinu ya michezo ya chuo hicho, sambamba kujikinga na magonjwa mbalimbali. Mbio hizo zinakutanisha ... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan amesema njia pekee ya kuwa na vijana watakaosaidia kulijenga taifa lenye maendeleo kwa siku za mbeleni ni kuwekeza kwenye mtaji wa elimu na serikali yake imeshaanza uwekezaji huo na itaendelea kuwekeza. Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 26, 2023 katika mkutano wa wakuu wanchi za Afrika kuhusu... |
null | LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu ikipigwa viwanja tofauti. Katika mchezo wa mapema ‘Wachimba dhahabu’ wa Chunya, Ken Gold itakuwa wenyeji wa ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Coastal ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 12 baada ya miche... |
null | DODOMA: WABUNGE leo Jumatatu Juni 3, 2024 wamepitisha bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2024/25, yenye vipaumbele 8. Ijumaa Mei 31, 2024, Waziri wa Utalii, Angellah Kairuki aliwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake mwaka wa Fedha 2024/2025, , ambapo aliiomba iidhinishiwe Sh 348,125,41... |
null | MWENYEKITI wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amezisisitiza nchi za Jumuiya hiyo kuunga mkono juhudi za kidiplomasia za kumaliza uhasama uliopo baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC na Rwanda chini ya mchakato wa Angola. Rais wa Zan... |
null | MWANARIADHA wa Jeshi la Polisi Konstebo Transfora Mussa ameshinda mbio za kilomita 10 za Fulham zilizofanyika Uingereza huku akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa kukimbia muda mfupi zaidi. Mwanariadha huyo ambaye amepata medali ya dhahabu, amevunja rekodi hiyo kwa kutumia dakika 31:53 tofauti na rekodi ya iliyowe... |
null | WADAU wa maendeleo wameombwa kuendelea kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania, hasa kwa kundi la vijana na wanawake ili kuhakikisha wanaleta mchango katika sekta hiyo. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Amina Khamis Shaaban ametoa ombi hilo wakati akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano kujadili fursa za uweke... |
null | RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo. Katika taarifa ya Ikulu Rais Dk. Samia ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu kutoka Brazil na Waziri Mkuu Majaliwa kuhusiana na zoezi la uokoaji na ... |
null | WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama leo Novemba 20 amewajulia hali majeruhi watatu wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa iliyotokea Kariakoo, Dar es Salaam Novemba 16, ambao wamelazwa katika Taasisi ya Mifupa- MOI wakiendelea na matibabu akiwemo mwanafunzi wa kidato cha nne. Waziri Mhagama amewatembelea majeruhi hao a... |
null | JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia Christina Mponzi (34), mkulima mkazi wa Kihesa mjini Iringa baada ya kumkamata akiwa na kete 33 za dawa za kulevya aina ya Heroine. Mponzi alikutwa na kete hizo katika mkoba wake baada ya wasamalia wema kutoa taarifa hiyo na kufanyiwa upekuzi katika tukio lililotokea hivi ka... |
null | Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kikao cha pamoja na Mawaziri wa Kisekta, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa na wilaya za Morogoro cha kujadili changamoto za usimamizi wa ardhi kitatoa mwelekeo wa kutekelezwa nchi nzima kwa kuthibiti uharibifu wa vyanzo vya mazingira na vyanz... |
null | MAMLAKA ya kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Afrika Kusini imemkamata Ahmadi Mbwana Chonde (50) ambaye ni raia wa Tanzania akiwa na kilo mbili za dawa za kulevya aina ya heroin. Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA,) usiku wa kuamkia leo, imesema kuwa Chonde, mwenye ha... |
null | JESHI la Polisi mkoani Rukwa limekamata meno ya tembo 11 na nyama ya nyati vipande 56, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 298. Kamanda Polisi Mkoa wa Rukwa, Theopista Mallya aliyasema hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari jana. Alisema nyara hizo za serikali zilikamatwa kutokana na operesheni na misako mb... |
null | SPIKA wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson amewataka wananchi kuacha tabia za kuendekeza majungu na badala yake wajikite katika kujenga Taifa. Dk Tulia aliyasema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini kwa kipindi ... |
null | MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun amesema Tanzania imetambulika kuwa ni moja ya nchi chache Afrika zilizopiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa. Alibainisha kuwa hatua hiyo imetokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika kuhusu hali ya rushwa duniani ambapo Tanzania ... |
null | MSANII wa Muziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani Sean Combs, ‘P Diddy’, anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono kutoka kwa watu 120 wapya, wakiwemo wanaume 60 na wanawake 60. Mawakili wanaowakilisha waathiriwa wanasema baadhi yao walikuwa watoto wakati wa matukio hayo huku mmoja akidai kuwa alinyanyaswa akiwa... |
null | CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, wasaidizi wake na wachezaji wa Taifa Stars kwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2025 nchini Morocco. T... |
null | Msimu wa Matangazo ya Tamthiliya na Filamu za Televisheni za Beijing Afrika umefunguliwa rasmi Dar es Salaam, ukiongozwa na Idara ya Televisheni na Redio ya Beijing. Tamasha hilo linaadhimisha miaka 10 ya ushirikiano thabiti kati ya Beijing na nchi za Afrika kupitia maonyesho ya filamu bora, likiimarisha urafiki na maw... |
null | DAR-ES-SALAAM : WANAMUZIKI wakongwe wa Tanzania wanazidi kuaga dunia na kuacha ombwe kwenye muziki wa dansi wa asili, na leo kinachoendelea ni msiba wa gwiji King Kikii King Kikii ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 77, akiacha alama kubwa – sauti yake – ambapo aliendelea kuimba hadi akiwa na uzee wake. Simanzi imetawa... |
null | NAHODHA wa Nàccoz Gym, bondia wa ngumi za kulipwa Mfaume Mfaume ameomba pambano la Oscar Richard na Tony Rashid lirudiwe kutafuta uhalali wa mshindi. Kwa mujibu wa Mfaume, mpaka leo hawaamini bondia wao Oscar alipigwaje na Tony kwa kuwa ni mtu mwenye uwezo kuliko mpinzani wake. SOMA: Ishu ya pambano la Mwakinyo kuyeyuk... |
null | Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kesho kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa pia ni utekelezaji wa haki ya kikatiba. Kauli hiyo ameitoa Novemba 26, 2024 wakati wakihitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali... |
null | KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha mapinduzi(CCM) Taifa, Itikadi , Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza mamilion aya watanzania kwenda kupiga kura huku akusisitiza mfano mzuri kwa kushiriki kupiga kura akiwa Ikuru Chamwino. CPA Makalla amesema hayo leo Novemba 26, 2024 akiz... |
null | MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson, amewataka wananchi kuchagua viongozi wenye uwezo wa kushughulika na changamoto zao kwa urahisi. Dk Tulia amezungumza hayo leo wakati akihitimisha kampeni za Uchaguzi w... |
null | KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania wasimame kidete kukataa kufarakanishwa na maneno ya wanasiasa. Badala yake amewasisitiza kusimamia mambo yaliyo ya msingi yenye manufaa kwao na taifa kwa ujumla, huku akipongeza wana CCM kwa kufanya kampeni kwa kuzingatia ut... |
null | WAGOMBEA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) katika vitongoji na vijiji vya Kata ya Mikese , Wilaya ya Morogoro wameomba wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi wa Serikali Za Mitaa kesho. Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kijiji cha Fulwe , Kata ya... |
null | MOJA ya sherehe kongwe zaidi za Kiajemi, Shab-e Yalda (Usiku wa Yalda), ambayo wakati mwingine hujulikana kama Shab-e Chelleh, huadhimishwa kila mwaka Desemba 21 na Wairani kote ulimwenguni. Yalda ni sherehe ya majira ya baridi ambayo hutokea mwishoni mwa vuli na usiku wa siku ya kwanza ya majira ya baridi, ambayo ni u... |
null | WAZIRI wa maji, Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kuipa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Dawasa), Sh milioni 500, ili mamlaka hiyo ikamilishe kazi ya kuunganisha maji kwa wananchi wa Jimbo la Kawe wanaohudumiwa na mradi wa maji wa Mapinga Bagamoyo, Mbweni na Tegeta A. Aweso ... |
null | HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila,iliyopo jijini Dar es Salaam, imeanza kutoa huduma ya kupunguza uzito uliokithiri, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza. Hadi sasa watu watatu wenye uzito zaidi ya kilogramu 100 wamepata huduma hiyo inayogharimu kiasi cha Sh milioni 3.5 hadi Sh milioni 4. A... |
null | MAMLAKA ya Bandari nchini (TPA) imesema inapokea zaidi ya magari 2,000 kila siku kupitia Bandari ya Dar es Salaam ambapo asilimia 60 ya magari hayo huenda nchi jirani. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amewaambia wanahabari mjini Bagamoyo wakati wa kikao kazi kuwa Idadi hiyo inatokana na maboresho k... |
null | SERIKALI za Tanzania na Burundi zimeshasaini makubaliano ya kujenga Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Uvinza hadi Gitega kupitia machimbo ya nickel nchini Burundi ambapo mtu binafsi atajenga reli hiyo kutokana na nchi hizo kutokuwa na fedha kwa sasa. Hayo yalibainishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam jana wa... |
null | MAMLAKA ya Usimamizi Bandari nchini (TPA) imesema itachukua rasmi usimamizi wa eneo lilokuwa likiendeshwa na Kampuni Binafsi ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi hapo serikali itakapo amua vinginevyo. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Juma Kijavara amewaambia wanahaba... |
null | MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amemshukuru Rais Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia madarasa ya uanzishwaji wa shule mbili mpya za msingi na sekondari katika Kata ya Mpunguzi jijini Dodoma. Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 21, 2020 Mpunguzi, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Sh... |
null | WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea magari 51 ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa msaada wa dharura wa uboreshaji wa shughuli za Uhifadhi wa Utalii Tanzania katika Hifadhi za Taifa Serengeti, Nyerere na Pori la Akiba Selous wenye thamani ya Euro milioni 20 sawa na Sh bilioni 56. Mradi huo unahusisha ununuzi w... |
null | POLISI Mkoa wa Tanga imefanikiwa kumkamata mkazi wa Dar es Salaam, Zainabu Kagoso (50), akidaiwa kujitambulisha kuwa ni mshauri wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika mambo ya kijeshi na kutumia njia hiyo kutapeli ofisi za serikali na maeneo mbalimbali wilayani Kilindi. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisin... |
null | MAWAZIRI watatu wamekutana kwa ajili ya kujadili jinsi ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto wawapo shuleni na majumbani kutokana na hali hiyo kukua kwa kasi kubwa nchini. Kikao hicho cha dharura kimewakutanisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, George Sim... |
null | CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Magufuli lililopo maeneo ya Daraja hilo linalounganisha mikoa ya Mwanza na Geita ujenzi wake umefikia asilimia 51 na linatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2024. Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania ... |
null | RAIS wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Paul Koy, ameishauri Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kusaidia wafanyabiashara wa Mkoa Mara, ili warasimishe biashara zao. Kauli hiyo ameitoa alipotembelea banda la BRELA kwenye maonesho ya Mara Business Expo 2022, yanayofanyika Musoma, mkoani Mara.... |
null | AJALI haina kinga na alipangalo Mola hakuna mja anaweza kulipangua ni baadhi ya semi ambazo zimekuwa zikitumika sana baada ya ajali au maafa kutokea. Semi hizi zinaweza kuwa ni moja kati ya sababu ambazo zinazopelekea ajali ziendelee kutokea kwa kuwa watu wanaamini kuwa kama Mungu alipanga ajali itokee basi itatokea tu... |
null | MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA – KISARAWE), inatekeleza kazi ya maboresho ya mfumo wa kusambaza maji kwa wateja wa taasisi kwa kuboresha miundombinu ya maji iliyorithiwa kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi Kisarawe (KUWASA). Akizungumzia matengenezo hayo yanayoendelea katika eneo la ofisi za... |
null | WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma waongeze kasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kwa viwango. Majaliwa alitoa agizo hilo Jumapili alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa barabara hiyo ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma. “Kazi ... |
null | WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanya uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyeiti na wajumbe 18 wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Taarifa ya wizara hiyo kwa umma jana ilieleza kuwa uteuzi huo ulifanywa na Waziri mwenye dhamana hiyo, Hamad Masauni. Masauni aliwateua Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Juma... |
null | NAIBU Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Juma Makungu Juma ametoa wiki moja nyumba iliyopo Fuoni Migombani ivunjwe baada ya kubainika imejengwa kinyume na utaratibu wa sheria za mipango miji na vijiji. Agizo hilo linahusu nyumba ambayo hivi karibuni picha yake ilisambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha nyumba ... |
null | POLISI nchini kwa kushirikiana na wenzao wa nchini Malawi wamekamata watu wanne wakiwamo Watanzania watatu na Mmalawi wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa wizi wa magari katika nchi hizo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei Jumatano alitaja Watanzania waliokamatwa ni Yusuph Ramadhan (26) mkazi wa Forest jijin... |
null | WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Baraza la Mawaziri limeruhusu kutungwa kwa sheria itakayolinda taarifa binafsi katika mtandao. Nape alisema hayo Jumatano Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa kongamano la wadau wa teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) wakiwemo wa miundombinu... |
null | WATU wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa, baada ya gari aina ya Toyota Hiace kuligonga lori kwa nyuma katika eneo la Kwedizinga wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Sofia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo saa 12 asubuhi, wakati Hiace ilikuwa ikijaribu kupita lo... |
null | WABUNGE ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wamesifu ubunifu na utendaji wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu. Walisema hayo Dodoma baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mchechu kuwasilisha kazi zilizofanywa na NHC. Mbunge wa ... |
null | WANAWAKE wanaonyonyesha na wajawazito zaidi ya 1200, wamenufaika na elimu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria pamoja na Uviko-19, iliyotolewa na taasisi inayojihusisha na masuala ya afya kwa jamii ya Doris Mollel Foundation. Mbali na elimu hiyo, kundi hilo kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Kagera imehamasishwa na ku... |
null | Rais Samia Suluhu Hassan, leo amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia Kifo cha Malkia Elizabeth II (96) wa Uingereza, aliyefariki dunia jana nchini Uskochi. Rais Samia amesaini Kitabu hicho katika makazi ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Oysterbay jijini Dar es Salaam. |
null | MADIWANI wa Kata za Kyanyari, Kamugegi na Kukirango zinazopakana na Mgodi wa Dhahabu wa Cata Mine,Wilaya ya Butiama mkoani Mara, wanakusudia kufungua kesi mahakamani dhidi ya mgodi huo kwa kutolipa Fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Hayo yameelezwa na Ofisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira wa halmashauri hiyo, Low... |
null | SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetenga sh bilioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya maji, umeme, mahema, uzio pamoja na njia za kupita ikiwa ni maandalizi ya Siku ya Chakula Duniani, itakayoadhimishwa Oktoba 10 hadi 16 Kisiwani Pemba. Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Shamat... |
null | RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kuunda kikosi kazi cha ukusanyaji wa maoni, kuhusu masuala ya siasa na kusema uwepo wake utasaidia kupunguza joto la kisiasa lililopo nchini. Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasilisha maoni yake, Kikwete amesema kuundwa k... |
null | TAASISI ya Mo Dewji inayoshughulikia masuala ya elimu, maendeleo ya jamii, afya na uwezeshaji wa kijinsia jana ilikabidhi hundi ya Sh milioni 100 kwa taasisi ya Tumaini la Maisha (TML), ambayo inashughulikia huduma kwa watoto wenye saratani Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa taasisi ya Mo Dewji, fedha hizo zilizokabidhiwa... |
null | WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, Rahma Kassim Ali, amewataka wakazi wa nyumba za maendeleo kuhakikisha wanalipa kodi, ipasavyo ili kuiwezesha serikali kufikia malengo iliyojipangia. Akizungumza katika ziara aliyoifanya kwenye nyumba za maendeleo eneo la Kikwajuni, amesema kitendo kinachofanywa na baadh... |
null | KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuona namna ya kuweka mfumo wa gesi asilia kwenye pikipiki na bajaji ili kuwasaidia wananchi wengi wanaotumia usafiri huo. Pia amezitaka kampuni nchini kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya kuja... |
null | WAZIRI wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, akipitia nyaraka kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 46 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika leo Novemba 28, Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha. Mawaziri hao watajadiliana kuhusu utengamano wa kiuchum... |
null | DAR ES SALAAM: Wanafunzi wanaosomea fani ya ukarimu katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) sasa watapata mafunzo ya ziada ya miezi mitatu kutoka kwa watalaamu wa Serengeti Breweries Limited (SBL) huku kampuni hii ikilenga kusaidia kujenga kizazi kipya cha wataalamu wa sekta ya utalii na ukarimu inayokua kwa kasi nchini... |
null | USIKU wa mabingwa unarejea leo, ambapo kutapigwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid ambao watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu wakiwakaribisha Machester City. Itakuwa mechi ya kisasi ya nusu fainali ya mwaka jana wakati Madrid ilipoiondoa City mabao 6-5 na kushinda taji la 14 ... |
null | TIMU ya KMC imejihakikishia kucheza ligi kuu msimu ujao maara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 leo hii dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa mtoano mkondo wa pili uliopigwa kwenye dimba la Uhuru Dar es Salaam. Mabao ya KMC katika mchezo huo yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya tatu na Awesu Awesu dakika ya 28... |
null | RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Novemba 20, 2024 Harare nchini Zimbabwe. Taarifa iliyotolewa leo Novemba 18, na Wizara ya Mamb... |
null | DAR ES SALAAM – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza waombolezaji katika zoezi la kuuaga miili 13 ya watu waliokufa baada ya kuangukiwa na jengo katika eneo la Kariakoo siku ya Jumamosi, Novemba 16. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hafla hiyo itafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja ... |
null | MRADI wa maji wa miji 28 unaotekelezwa katika wilaya nne za mkoa wa Tanga unakwenda kumaliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji. Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema hayo leo Novemba 16 alipotembelea eneo la chanzo cha maji Tabora kilichopo Kijiji cha Mswaa wilaya ya Korogwe mkoani humo. Amesema mradi huo unaotarajiwa ... |
null | TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ‘Taifa Stars’ leo inashuka dimbani ugenini huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) dhidi ya Ethiopia. Mchezo huo wa marudiano wa kundi H utafanyika kwenye uwanja wa Martyrs de la Pentecôte uliopo mji mkuu wa DR Congo, Kins... |
null | Timu ya wavuta kamba ya wanaume ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendeleza ubabe katika Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Mkoani Tanga baada ya leo Novemba 16, 2024 kuivuta timu shindani ya TPDC Kwa mivuto miwili kwa nunge. Mchezo huo ulioanza... |
null | NYOTA wa tenisi Novak Djokovic ameanza jitihada zake za kutwaa taji la 25 la Grand Slam kwa ushindi dhidi ya Radu Albot katika raundi ya kwanza ya ubingwa wa US Open. Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa tenisi wa Arthur Ashe uliopo jiji la New York. SOMA: Djokovic akemea vurugu Serbia Taji moja zaidi litampa Djokovi... |
null | DAILYNEWS DIGITAL inakusogezea LIVE : Fuatilia hapa tukio la kuaga miili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo kariakoo. LIVE: Bonyeza hapa kushuhudia tukio hilo DAILYNEWS DIGITAL inakusogezea LIVE : Fuatilia hapa tukio la kuaga miili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo kariakoo. LIVE: Bonyeza hapa kushuhudia tukio h... |
null | MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Burundi ni ishara ya ujirani mwema na undugu kati ya serikali na wananchi. Andengeye amesema hayo leo wakati akifungua kikao cha pamoja cha Kamati ya Wataalamu (JTC) kati ya Tanzania na Burundi kinachoendelea mkoani K... |
null | Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye eneo la Kapeni view point pamoja na Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakati walipokuwa wakiangalia maeneo hayo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga cha kitropiki cha Freddy, Blantyre nchini Malawi Julai7, 20223. (Picha na Ikulu) Comments are closed. |
null | DAR ES SALAAM – Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official amewasili katika uwanja wa Leaders jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga mwili wa nguli wa muziki wa dansi nchini Marehemu Kikumbi Mpango Mwanza (King Kikii) aliyefariki dunia Novemba 15, 2024. Marehemu King Kikii atazikw... |
null | DAR ES SALAAM – Serikali imesisitiza kuwa michango na misaada yoyote kwa ajili ya kusaidia waathirika wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo jijini Dar es Salaam itafanywa kupitia akaunti maalumu ya maafa 9921159801 ambayo ipo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dk Ji... |
null | MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Annamringi Macha amesema viongozi waliochaguliwa kama watakwenda kinyume na utaratibu serikali haitosita kuwaondoa na kuwataka waondoe changamoto ya kutosoma mapato na matumizi kwenye maeneo yao. Macha amesema hayo leo kwenye mkutano maalumu wa kuapishwa viongozi waliochaguliwa wa serikali ya... |
null | NAIBU Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM), Judith Kapinga ameahidi kutoa kompyuta 139 katika shule za msingi 139 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Vijijini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa elimu katika wilaya hiyo. Kapinga ametoa ahadi hiyo Novemba 28, 2024 wakati wa hafla ya uwe... |
null | DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Vunjo (CCM), Dk. Charles Kimei amesisitiza umuhimu wa kuhamasisha uwekezaji kwa sekta binafsi katika uzalishaji wa nishati ya umeme nchini. Akichangia taarifa ya mpango wa maendeleo wa taifa 2025/2026 bungeni Dodoma,Dk. Kimei amesema Mradi wa Uzalishaji wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unaweza ku... |
null | DAR ES SALAAM :Gari litakalobeba mwili wa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani ((WHO) Kanda ya Afrika na Mbunge wa Kigamboni, hayati Dk Faustine Ndugulile limewasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kwa ajili ya kubeba mwili huo kuupeleka Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam . |
null | ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda, amesema anashukuru hukumu ya mahakama kutokana na kesi ya kudaiwa kulawiti iliyokuwa inamkabili na kusisitiza kuwa haki imetendeka na mambo mengine yaliyotokea anamuachia Mungu. Dk. Nawanda ameshinda Kesi ya Jinai namba 18853/2024.iliyokuwa inamkabili katika Mahakama ... |
null | RAIS Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kufungua mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki (EAMJA) utakaofanyika Arusha kuanzia Desemba 2 hadi 7 ,mwaka huu. Lakini pia uboreshaji wa utoaji haki katika migogoro ya kazi ni mojawapo kati ya maeneo matano yatakayojadiliwa katika mkutano. Akizungum... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.