name
stringclasses
429 values
text
stringlengths
0
767k
null
Wanafunzi wachoma moto pikipiki ya mwalimu na kufyeka shamba lake la mahindi Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, Stella Rutabihirwa amethibitisha kushikiliwa kwa wanafunzi sita wa kidato cha tano na sita Mchepuo wa CBG, kutoka Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo Manispaa ya Singida kwa tuhuma za kuchoma Pikipiki y...
null
Israel na Hamas kwa mara nyingine tena wako vitani baada ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina kuanzisha operesheni kubwa ya anga na ardhini leo asubuhi kutoka ukanda wa Gaza. Zaidi ya makombora 5,000 yamerushwa kutoka Gaza kuelekea Israel, na watu wenye silaha wa Hamas waliingia katika miji na vijiji vingi vya Israel ...
null
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo Novemba 16, mwaka huu. Akizungumza kwa njia ya simu, Rais Samia amesema anatambua kuwa utaratibu wa uokoaji ni saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo, lakini anaamini kuwa Mwenyezi Mungu a...
null
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema kwamba Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa sasa halihitaji ruzuku kutoka serikalini na kuanzia mwaka ujao wa fedha, 2019/20 litaanza kutoa gawio (serikalini). Dk Kalemani aliyesema hayo jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake ambapo alibainisha kuwa T...
null
✕ Habari Siasa Biashara Afya Elimu Maisha Burudani Rubik - © Copyright BKNinja . All Rights Reserved. 24/7 Habari Bila Mipaka Wednesday, December 11 Home › Error 404 404 Page not found Oops! The page you were looking for was not found. Perhaps searching can help. Latest Articles Habari Maisha Dada wa kazi akutwa amejin...
null
Kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wateja nchini Kenya kuhusu bei ghali ya umeme, sasa Wakenya wanafurahia kupunguzwa kwa bei ya tokeni za umeme baada ya Kenya Power kuanzisha punguzo la bei. Uchunguzi uliofanywa na Kenyans.co.ke umeeleza kuwa kwa KSH 1,000 [TZS 17,114] watumiaji wanapokea uniti 37.61 katika mwezi wa...
null
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa ametangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mwaka 2022. Amesema jumla ya wanafunzi 153,219 (wasichana 67,541 na wavulana 85,678), sawa na asilimia 91.8 ya wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga n...
null
Zanzibar: Ashtakiwa kwa kukata viuno hadharani Maulid Hussein Abdallah maarufu kama Mauzinde (29) amefikishwa Mahakama ya Mwanzo katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja Kisiwani Zanzibar, kwa tuhuma ya kukata viuno hadharani. Kijana huyo mkazi wa Rahaleo anatuhumiwa kutenda kosa hilo huko Kibole wilaya ya Ka...
null
Kuongea usingizini ni hali ambayo watu wanaweza kutoa maneno au sauti wakiwa wamelala. Hali hii inaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kwa kila mtu na inaweza kutokea kwa sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na; Kurithi: Kuongea usingizini inaweza kuwa urithi wa kifamilia. Ikiwa wazazi au ndugu wa karibu wana historia ya kuo...
null
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea tabia ya baadhi ya maafisa ununuzi wa umma kukubali zabuni za watoa huduma zenye bei ya juu kuliko bei halisi za soko na kuahidi kuwa ataanza na Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) kulishughulikia suala hilo. Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo wakati akizungumza na wataalamu wa ununuzi na u...
null
✕ Habari Siasa Biashara Afya Elimu Maisha Burudani Rubik - © Copyright BKNinja . All Rights Reserved. 24/7 Habari Bila Mipaka Wednesday, December 11 Home › Error 404 404 Page not found Oops! The page you were looking for was not found. Perhaps searching can help. Latest Articles Habari Maisha Dada wa kazi akutwa amejin...
null
Nafasi ya kampuni za simu katika kukuza teknolojia Tanzania Na Mayala Francis, DIT Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeshuhudia maendeleo makubwa kwenye sekta ya teknolojia hasa linapokuja suala la matumizi ya simu. Hakuna ubishi wowote kwamba intaneti kwa njia ya simu imeleta tija kubwa katika shughuli zetu. Katik...
null
Dada wa kazi akutwa amejinyonga Musoma December 11, 2024Hatua 5 za kukamilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 December 11, 2024Polisi Arusha watoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya December 10, 2024 More News - Nafasi 121 za Ajira Serikalini November 28, 2022 - Serikali yaruhusu wenye visima kusambaza maji Oct...
null
Mafanikio yako katika kazi kwa kiasi kikubwa yanategemea mtazamo wako na jinsi gani unatumia muda wako unapokuwa kazini au katika shughuli yoyote ile yenye manufaa kwenye maisha yako. Fuatilia njia hizi zitakazokusaidia kuongeza ufanisi na kukufanya kuwa bora zaidi kazini; Simamia vipaumbele vyako Ili kuboresha utendaj...
null
Chama cha Marubani chasema marubani hujiongoza wenyewe kutua Bukoba Katibu wa Chama cha Marubani Tanzania (TAPA), Kapteni Khalil Iqbal amesema kuna baadhi ya makampuni ya ndege ambayo yanawashinikiza marubani kufanya safari zao katika mazingira hatarishi hali inayohatarisha usalama wa abiria na wafanyakazi. Akizungumza...
null
Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF) kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa litakalofanyika ikiwa ni siku chache kabla ya siku ya kumbukizi ya kifo cha Mkapa Julai 23. Katika kongamano hilo litakalofanyika kwa siku mbil...
null
Tanzia: Rais Mstaafu Benjamin Mkapa afariki dunia Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia leo Julai 24, 2020. Rais Magufuli amesema Rais Mkapa amefariki dunia hospitalini Jijini Dar es Salaam ambako al...
null
Benjamin William Mkapa alikuwa mwanasiasa wa Tanzania ambaye alikuwa Rais wa Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hadi mwaka 2005. Katika kipind hicho alikuwa pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Mzee Mkapa amefariki dunia Julai 23, 2020 hospitalini jijini Dar es Salaa...
null
Diamond afuta picha zenye bendera ya ubaguzi Mwanamuziki Diamond Platnumz amefuta picha alizoweka kwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya kukosolewa vikali na watumiaji wa matandao huku kutokana na picha hizo hizo kuonesha bendera inayoibua kumbukizi za ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Diamond ameweka picha hizo mapem...
null
Mahakama ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imemhukumu aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri hiyo, Paulo Teveli kifungo cha miaka 20 jela bila faini baada ya kukutwa na hatia ya uhujumu uchumi. Hukumu hiyo imetolewa Machi 19, mwaka huu na Hakimu Hellen Hozza huku shauri hilo la uhujumu Uchumi Na 23/2022 likiendeshwa na Wa...
null
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema wanawashikilia watu 10 kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu akiwemo mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kutumia hirizi akiamini hatakamatwa na polisi huku akitumia funguo bandia kufungua milango. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Bukumbi ameeleza Emmanuel Hassan a...
null
Maneno ya Abdul Nondo baada ya kufutiwa kesi Mahakama ya Rufani Tanzania, Masjala ya Iringa imefuta kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP). Abdul Nondo alikuwa anashtakiwa kwa makosa mawili, moja ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na mbili, kutoa taarifa za uongo kw...
null
Rais Samia Suluhu Hassan ameboresha kituo cha afya katika Kata ya Idodi mkoani Iringa na hivyo kuwezesha wananchi wa kata mbili zinazokadiriwa kuwa na wananchi 14,630 kupata huduma za afya za uhakika. Kituo cha afya Idodi kinatoa huduma zote muhimu ikiwemo huduma za upasuaji, uongezaji wa damu na huduma za uzazi ambao ...
null
Godbless Lema akamatwa Kenya akitafuta hifadhi Ubalozi wa Marekani Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiando nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpanga wa Namanga. Kwa mujibu wa tovuti ya The Standarnd Media ya Kenya Lema alikuwa na mkew...
null
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi watatu wa Shirika la Posta Tanzania kuanzia Aprili 30, 2021. Kwanza, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Prof. Tadeo Andrew Satta. Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia pia ametengua uteuzi wa wajumbe sita...
null
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema Serikali kuzuia mtoto wa umri wa miaka 14 kuolewa ni kuzuia kumuabudu Mungu na kumruhusu shetani aingie kati. Akizungumza na Swahili Times, Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikhe Hassan Chizenga amepinga kubadilishwa kwa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, hasa kipengele kinach...
null
TRA: Hatukusanyi kodi kwa mabavu tena Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Uledi Mussa amesema kitengo cha ‘task force’ kilichokuwapo huko nyuma kimeondolewa na sasa wanakusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara bila kutumia mabavu. Mussa amesema hayo leo Jumanne Novemba 15, 2022 katika kikao baina ya ...
null
Kushiriki kufanya mapenzi si tu shughuli ya kufurahisha kimwili, bali pia ina athari kubwa kiafya ambazo zinaweza kuwa na faida kubwa kwa mwili na akili. Kutofanya mapenzi kwa muda mrefu kunaweza kuwa na athari mbalimbali, lakini athari hizi zinaweza kutofautiana kwa watu tofauti kulingana na sababu za kisaikolojia, ki...
null
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Fred Milanzi amemsimamisha kazi muuguzi wa Zahanati ya Basanza, Alex Lyimo ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma za kutotekeleza majukumu yake ipasavyo. Hatua hiyo imefuata baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mama mjamzito (jina lim...
null
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ambaye pia ni Muwakilisha wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya (EU), Jestas Nyamanga amekanusha taarifa kuwa EU imeazimia kuinyima Tanzania mikopo na misaada. Katika taarifa yake ya Novemba 19, 2020, Nyamanga amesema uamuzi huo haukutolewa na Bunge la EU bali ni hoja za wabunge watano wa...
null
Polisi wachunguza bilioni 6 zilizoingizwa kwenye akaunti za THRDC Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi hilo linashikilia akaunti za benki za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kuchunguza kiasi cha fedha TZS 6 bilioni zilizoingizwa kwenye akaunti zao. Sirro amesema l...
null
Kwa mujibu wa Business Insider Africa imetoa orodha ya hoteli kongwe zaidi barani Afrika huku baadhi ya hoteli hizo zikipokea wageni kwa takribani miaka 200. Hizi ni Hoteli kongwe zaidi barani Afrika pamoja na bei zake kwa usiku mmoja; 1. Hoteli ya Houw Hoek, Afrika Kusini Hoteli hii imekuwepo tangu mwaka 1779 katikati...
null
Jeshi la Polisi limesema endapo kuna mtu yeyote ametishiwa maisha kutokana na sababu mbalimbali, afike kituo cha polisi ili awasilishe ushahidi alionao kwa ajili ya uchunguzi ikiwemo kuwakamata wahusika. Wito huo umetolewa kufuatia baadhi ya watu kujitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kudai wametishiwa maisha kwa sab...
null
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema wananchi hawapaswi kuaminishwa kwamba katiba mpya ndiyo tiba ya kutatua kila tatizo lilipo nchini. Ameyasema hayo baada ya kuwasilisha maoni yake mbele ya kikosi kazi maalum kilichoundwa kukusanya maoni mbalimbali kuhusu demokrasia, na kusisitiza kuwa j...
null
Maelfu ya wamiliki wa magari pamoja na waendesha boda boda katika mji wa mpakani wa Namanga wanaendelea kuingia nchini Tanzania ili kununua mafuta kwa bei rahisi. Hivi karibuni shirika la kudhibiti bei ya mafuta nchini Kenya (EPRA) liliongeza bei ya mafuta kwa mujibu wa sheria ya fedha ya 2023, ambayo VAT iliongezeka k...
null
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. Katika mazungumzo hayo, Merkel amempongeza Rais Samia kwa kushika hatamu za Urais nchini Tanzania na kumpa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Pia amempongeza Rais S...
null
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo wa ‘Nitasema’ wa msanii Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego ikisema wimbo huo umekiuka kanuni ya baraza hilo. Kwa mujibu wa taarifa ya BASATA iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Nay wa Mitego imesema maneno yaliyotumika kwenye wimbo huo ambayo yanaishtumu Jes...
null
Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia, Poland ilikuwa chini ya uvamizi, maelfu ya Wapoland walipata hifadhi katika maeneo tofauti ulimwenguni na wengine wakafanikiwa kufika Afrika. Walitawanyika katika vijiji zaidi ya ishirini katika nchi sita katika Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika na moja ya maeneo hayo ilikuwa Tan...
null
Serikali yapunguza 50% ya ada za tozo za leseni za maudhui Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema Serikali inakwenda kuondoa 50% ya ada za tozo mbalimbali za leseni kwenye marekebisho ya Kanuni za maudhui ya mtandaoni na maudhui ya utangazaji katika redio na televisheni yaliyofanywa h...
null
Benki ya NMB imesema imeanza kuzingatia kwa karibu masuala ya uhifadhi wa mazingira katika uendeshaji wake na kufadhili miradi mbalimabli kutokana na umuhimu wake katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza jijini Dar es Salaam Alhamisi wiki hii, afisa mwandamizi wa benki hiyo, Bi Hellen Da...
null
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wagombea wote ambao hawajaridhishwa na uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa waweke pingamizi ndani ya siku 2 kuanzia Novemba 08 hadi 09, 2024. Mchengerwa ameeleza kuwa pingamizi hilo ...
null
Timu ya Taifa ya Nigeria imeamua kutocheza mechi ya kufuzu Mashindano ya AFCON 2025 nchini Libya dhidi ya Mediterranean Knights baada ya kukabiliwa na mazingira magumu tangu walipowasili Jumapili nchini humo. Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) imesema wachezaji wameamua kutocheza tena mechi hiyo...
null
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelaani tukio lililovuruga utumbuizaji kwa mwanamuziki Zuhura Othman Soud (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na mashabiki. Aidha, BASATA imetoa rai kwa wadau wa Sanaa na wasanii kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyo na tija. Mbali na hayo, imewataka waandaa...
null
Bunge la Tanzania leo limepitisha muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambayo yanalenga kuongeza umri wa mtegemezi kutoka miaka 18 hadi miaka 21. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi minne tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipotoa maelekezo hayo wakati akizungumza kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi ...
null
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya Watu wa China kuanzia Septemba 02 hadi Septemba 06, mwaka huu ili kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China – Africa Coorperation FOCAC) utakaofanyika jijini Beijing. Katik...
null
More News - Wakamatwa na vifaa vya wizi kutoka Bwawa la Nyerere December 7, 2022 - Fei Toto amshukuru Rais Samia kujiunga rasmi Azam FC June 8, 2023 Yaliyojiri - Polisi Arusha watoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya December 10, 2024 - Nafasi 100 za Ajira Serikalini December 10, 2024 - Benki ya Dunia yapunguza mak...
null
Waziri wa Kilimo nchini Kenya, Mithika Linturi na mwenzake wa Zambia, Mtolo Phiri wametia saini makubaliano ili kupata kati ya hekta 20,000 na 40,000 za ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo kikubwa cha mahindi ili kuilisha nchi ya Kenya. Lengo ni kutenga ardhi hiyo kwa ajili ya wakulima wa Kenya watakaolima mazao hay...
null
TRC yaomba radhi kwa treni kuchelewa kutokana na hitilafu Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeomba radhi kwa abiria waliosafiri kutoka Dodoma saa 2: 15 usiku kuelekea Dar es Salaam Agosti 01, 2024 kwa treni ya mwendo kasi kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hi...
null
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia maisha wanafamilia wawili kutojishughulisha na mpira wa miguu ambao ni Mwenyekiti wa Kitayosce FC, Yusuph Kitumbo na kocha wa mpira wa miguu, Ulimboka Mwakingwe. Wawili hao wametiwa hatiani kwa kujihusisha na upangaji wa matokeo katika mechi y...
null
EQUITY BANK YAZINDUA HUDUMA YA KIDIJITALI ‘LIVE CHAT’ Benki ya Equity imezindua huduma ya Kidigital ya Light Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24. Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 4,...
null
Mhubiri kutoka nchini Kenya, Eliud Wekesa maarufu kama ‘Yesu wa Tongaren’, ameendelea kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Bungoma kwa siku nne zaidi hadi upelelezi utakapokamilika. Mahakama imetoa uamuzi huo siku ya Ijumaa ikisema kwamba uamuzi huo utaruhusu wapelelezi kutoka Kurugenzi ya Makosa ya Jinai (DCI) kukami...
null
Klabu ya Simba na Yanga zimeahidi kumiliki viwanja vyao wenyewe ndani ya miezi sita ikiwa ni baada ya agizo la Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa kuelekeza vilabu vyote kumiliki viwanja vyake vyenyewe. Mchengerwa ameyasema hayo alipokutana na watendaji wakuu wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu jiji...
null
✕ Habari Siasa Biashara Afya Elimu Maisha Burudani Rubik - © Copyright BKNinja . All Rights Reserved. 24/7 Habari Bila Mipaka Wednesday, December 11 Home › Error 404 404 Page not found Oops! The page you were looking for was not found. Perhaps searching can help. Latest Articles Habari Maisha Dada wa kazi akutwa amejin...
null
Mahakama ya kupambana na rushwa nchini Kenya imeagiza akaunti ya benki ya ya mwanafunzi, Felesta Njoroge (21) ifungwe kwa siku 90 ili kuruhusu Wakala wa Urejeshaji Mali (ARA) kufahamu chanzo cha TZS bilioni 2.3 zilizopo kwenye akaunti hiyo. Wakala huyo inashuku kuwa fedha hizo ni matokeo ya utakatishaji wa fedha na hiv...
null
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa ametangaza msamaha kwa Mchungaji wa Ushirika wa Kijitonyama, Dkt. Eliona Kimaro ambaye alipewa likizo ya siku 60. Msamaha huo umetolewa leo Februari 19, 2023 katika ibada iliyoongozwa na Askofu Malasusa ambapo ...
null
Katika bara la Afrika, kuna mtindo wa watu kuhama kutoka nchi zao kwenda nchi za nje kutafuta maisha bora. Hata hivyo, Watanzania wengi wanapendelea kubaki nyumbani kuliko kuhamia nchi za kigeni. Hii inaweza kuonekana tofauti na mataifa mengine ya Afrika, ambapo idadi kubwa ya watu wanaishi ughaibuni. Hapa kuna sababu ...
null
Katika jimbo la Kusini-Mashariki la Enugu nchini Nigeria, mamlaka zimepiga marufuku matumizi ya magari yenye vioo vilivyokuwa ‘tinted’ ikiwa ni jitihada za kupunguza uhalifu nchini humo. Kwa mujibu wa afisa wa Serikali ya jimbo, wamiliki wa magari yenye vioo vya hivyo, wamepewa muda hadi Septemba 4 mwaka huu ili kupata...
null
Linapokuja suala la kununua miwani, kuamua saizi ya uso wako na umbo ni muhimu kwa sababu itakusaidia kupata miwani ya jua inayofaa zaidi kulingana na aina ya uso wako. Miwani ya jua inayofaa inaweza kukupa mwonekano maridadi. Ili kupata miwani bora zaidi ya uso wako, utahitaji kupima uso wako, kuamua umbo la uso wako,...
null
Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi tatu, ambapo kwanza amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe. Dkt. Shein anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas A. Samatta ambaye anamaliza muda wake. Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa ...
null
Jeshi la Polisi Mkoani Songwe linamshikilia mke na hawara yake kwa tuhuma za mauaji ya mumewe, Victor Mwakapenda (41) mkazi wa Mtaa wa Ilembo wilayani Mbozi huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa marehemu alitowe...
null
Rubik - © Copyright BKNinja. All Rights Reserved. https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/selection/psle_selection.htm
null
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amepokea ushahidi kutoka kwa wabunge wawili aliowaagiza Juni 3 mwaka huu kuleta uthibitisho kwa kile walicholalamika kuhusu wananchi wa majimboni mwao kuuawa. Dkt.Tulia amesema Jumatatu Mbunge Tarime Vijijini, Mwita Waitara alidai kuwa baadhi ya wananchi wake wameuawa kwa kipigwa risa...
null
Tanzania yakaribisha wawekezaji sekta ya nishati Tanzania imekaribisha wawekezaji kutoka kote duniani kuja kuwekeza kwenye sekta ya nishati kutokana na uwepo fursa nyingi kuanzia kwenye uzalishaji hadi usambazaji wa nishati maeneo mbalimbali nchini. Mwaliko huo umetolewa na Waziri wa Nishati, January Makamba jijini Dar...
null
Kampuni Uber inashtakiwa na wanawake 550 wanaodai kufanyiwa vitendo viovu na madereva walipokuwa wakitumia huduma ya usafiri. Malalamiko hayo yaliyowasilishwa Jumatano katika mahakama ya Marekani, yanajumuisha malalamiko mbalimbali yakiwemo utekaji nyara, unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kingono, ubakaji, pamoja...
null
Wawili wakamatwa kifo cha Mwenyekiti wa Vijana CCM Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Machinjioni, Kata ya Bwawani, Michael Kalinga (36) mkazi wa Makongolosi wilayani Chunya. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi...
null
Ulaji wa bamia umekuwa ukikimbiwa na watu wengi licha ya kutajwa kuwa msaada mkubwa katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Healthline, hizi ni faida tano kubwa za ulaji wa bamia katika mwili wako. Hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo Viwango vya juu vya cholesterol vinahusishwa na hatari kubwa ya ugon...
null
Kiongozi wa kanisa afariki akiwa na mwanamke hotelini Kasisi wa Kanisa Katoliki la Jimbo Kuu la Nairobi nchini Kenya ameripotiwa kufariki baada ya kupoteza fahamu katika hoteli moja kaunti ya Murang’a. Kulingana na ripoti ya polisi, Fr. Joseph Kariuki Wanjiku (43) aliingia katika hoteli hiyo Ijumaa usiku akiandamana na...
null
Rubik - © Copyright BKNinja. All Rights Reserved. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwezi Novemba, 2023. MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2023
null
Askari Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke kilichopo Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza a anatafutwa na Jeshi la Polisi baada ya kudaiwa kumvunja miguu na kiuno, Mohammed Khatibu (29) kwa tuhuma za kuwa na mahusiano na mke wake. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gedion Msuya amethibitisha kutoke...
null
Polisi nchini Kenya wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutawanya kundi la wanaharakati wa haki za binadamu akiwemo Jaji Mkuu Mstaafu, Willy Mutunga baada ya kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Nairobi, akitaka kuachiliwa huru kwa waandamanaji waliokamatwa. Jaji na wanaharakati walienda kituoni hapo wakitaka ...
null
Maboresho mradi wa BRT awamu ya kwanza Dar kugharimu shilingi bilioni 18 Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam imesema inatekeleza mradi wa matengenezo ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya kwanza chini ya mradi wa OPBRC (Output and Performance-Based Road Contract) uliosainiwa r...
null
Maeneo 8 ya uwekezaji yenye kuzalisha faida zaidi Tanzania Tanzania imefungua milango yake wazi kwa wawekezaji wanaotamani kunufaika na uwekezaji wao na pia kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Taarifa iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) inaonyesha maeneo nane yenye fursa kubwa za uwekezaji ikiaamin...
null
Dada wa kazi akutwa amejinyonga Musoma December 11, 2024Hatua 5 za kukamilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 December 11, 2024Polisi Arusha watoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya December 10, 2024 More News - Wateja wa betPawa wajishindia TSh53.8 Bilioni ndani ya siku 10 November 2, 2023 - Binti amshitaki mc...
null
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeutaarifu umma kupuuza taarifa zinazosambazwa na baadhi ya watu kuhusu kusimama kwa treni za EMU, Electric Multiple Unit (mchongoko) pamoja na changamoto za umeme, ikisema kuwa haijawahi kuwa na changamoto za umeme tangu kuanza kwa safari hizo Juni 14, mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na...
null
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza matayarisho kuelekea upandikizaji wa ini, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kutoa huduma za ubingwa bobezi nchini, ili kusogeza huduma hizo karibu na wananchi ambazo hazikuwepo kutokana na utalaam, vifaa vya uchunguzi au miundombinu stahiki ya kutolea huduma...
null
[pdf-embedder url=”https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2022/08/Cap-Prices-Publication-wef-3-August-2022-English.pdf” title=”Cap Prices Publication wef 3 August 2022 English”]Bei [pdf-embedder url=”https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2022/08/Cap-Prices-Publication-wef-3-August-2022-English.pdf” title...
null
Serikali imetoa masharti kwa wanafunzi 640 waliomaliza kidato cha sita wenye ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi na hisabati wanaotarajiwa kupata ufadhili kupitia ‘Samia Scholarship.’ Haya ni masharti 6 yaliyotajwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda. 1. Mwanafunzi anapaswa kusoma, kuelewa ...
null
The server is temporarily unable to service your request due to maintenance downtime or capacity problems. Please try again later. Additionally, a 503 Service Unavailable error was encountered while trying to use an ErrorDocument to handle the request.
null
Baada ya taarifa ya Chama Cha ACT Wazalendo kudai kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo kutekwa leo asubuhi, Jeshi la Polisi limesema kiongozi huyo alikamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na watu waliokuwa na gari aina ya Landcruiser nyeupe yenye usajili namba T249 CMV. Taarifa ya Polisi imesema ma...
null
Jeshi la Polisi latangaza nafasi za Ajira katika fani mbalimbali More News - Maeneo 8 ya uwekezaji yenye kuzalisha faida zaidi Tanzania November 28, 2023 - TRA yaweka rekodi kwa kukusanya trilioni 2 Disemba 2020 January 1, 2021 Yaliyojiri - Polisi Arusha watoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya December 10, 2024 - ...
null
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri ardhini (LATRA), leo Aprili 30, 2022 imetagaza viwango vipya vya bei ya nauli za daladala na mabasi ya mikoani itakayoanza kutumika kuanzia Mei 14, mwaka huu. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gillard Ngewe ametangaza viwango hivyo huku nauli ya ...
null
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema ongezeko hili la joto linatokana na kusogea kwa jua la utosi sambamba na upungufu wa mvua katika maeneo mengi nchini. Kwa mujibu wa TMA hapa nchini vipindi vya jua la utosi hufikia kilele mwishoni mwa mwezi Novemba na hali hiyo hujirudia tena mwezi Februari wakati jua la u...
null
Nafasi 100 za Ajira Serikalini December 10, 2024Benki ya Dunia yapunguza makadirio ukuaji wa uchumi wa Kenya 2024 December 10, 2024Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 1548 December 9, 2024 More News - Kontawa ajisalimisha jeshini, aomba kujiunga JKT September 1, 2023 - Marekani yasamehe mikopo kwa mamilioni ya wanafun...
null
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Lusajo Makiwelu ambaye ni dereva anayedaiwa kuwamwagia tindikali Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake wa miezi sita na kuwasababishia maumivu makali. Akizungumza na Swahili Times Kamanda wa Polisi mkoani humo, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Jun...
null
Serikali imesema katika kipindi cha muhula wa pili wa miaka mitano ya Rais Dkt. Magufuli itajikita zaidi katika diplomasia ya uchumi, kuimarisha sekta binafsi, kukuza biashara pamoja na mahusiano na mataifa mengine duniani. Msimamo wa Tanzania umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof...
null
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Hayati Maalim Seif Sharif Hadama ataenziwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kuacha alama nzuri katika uongozi wake hasa wakati alipokuwa kijana na kiongozi mkubwa ndani ya chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mfumo wa chama kimoja. Amesema hayo leo akihutubia katik...
null
Katika hali isiyo ya kawaidia, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Methodist Tanzania, Askofu Joseph Bundala (55) amekutwa amejinyonga katika ofisi za kanisa hilo lililopo mtaa wa Sulungai Meriwa Kata ya Ipagala jijini Dodoma kwa kutumia waya wa simu akidai chanzo ni madeni. Tukio hilo limetokea Mei 16, mwaka huu kwenye choo ch...
null
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Bukindu Mhoja (22) Mkazi wa Kijiji cha Bukoli, Kata ya Bukoli mkoani Geita amefariki dunia baada ya kunywa sumu akihofia kudaiwa elfu 47,000. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Ally Kitumbu amethibit...
null
Mtanzania Elizabeth Mrema ateuliwa kuongoza shirika la Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Elizabeth Maruma Mrema kutoka Tanzania kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP). Bi. Mrema atamrithi Joyce Msuya kutoka Tanzania aliyeteuli...
null
Jeshi la Polisi limesema linafuatilia taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya kupotea kwa kiongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Vwawa, Hussein Mwashambwa kutokana na utata uliogubika mazingira yake. Aidha, Jeshi la Polisi limesema kinachoendelea kuzungumzwa kwenye mitandao kwamba Mw...
null
Wakazi wa Kilimanjaro kumuomba radhi na kumpa tuzo Rais Magufuli Na Dixo Busagaga ,Moshi Wazee katika mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo viongozi wa mila, machifu na malaigwanani wameanza mchakato wa kumpongeza na kumpa tuzo maalumu Rais Dkt. Magufuli kwa kazi aliyofanya katika kipindi cha miaka mitano. Katika tukio hilo wan...
null
Maafisa watatu wa polisi nchini Kenya wanashikiliwa kwa tuhuma za kumtesa na kukandamiza viungo vya uzazi vya mwanamume aliyekuwa ameshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Homa Bay. Mahakama Kuu ya Migori siku ya Alhamisi imetupilia mbali maombi ya dhamana ya maafisa hao watatu, Peter Langat, Peter Nyakundi na Gilbert A...
null
Wafanyakazi wa ngono nchini Ubelgiji sasa wanapata ulinzi sawa na wafanyakazi wa sekta nyingine kupitia sheria mpya ya kihistoria iliyopitishwa mwezi Mei mwaka huu na kuanza kutekelezwa siku ya Jumapili. Sheria hiyo inatoa haki za ajira rasmi, ikiwemo likizo ya uzazi, bima ya afya, posho za ukosefu wa ajira, na malipo ...
null
Kila mtu anatamani kuishi muda mrefu, wengi wanajua nini cha kufanya au kutokufanya ili kufikia lengo hilo, lakini sio wote wenye utayari wa kufanya mambo hayo kwa sababu huambatana na kujinyima baadhi ya vitu. Kwa mujibu wa watafiti mbalimbali duniani, mambo tunayofanya au vyakula tunavyokula kila mara yanaweza kuteng...
null
Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia vifo vya watu 10 katika ajali boti. Ajali hiyo imetokea Januari 4, 2022 katika eneo la bahari ya Kisiwa Panza, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar. Kwa mujibu wa...
null
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema hakutokuwa na ubadilishaji wa machaguo ya shule kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano. Bashungwa amechapisha ujumbe huo katika mtandao wake wa Instagram na kusema, wanafunzi wote waliochaguliwa waripoti kati...
null
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amefunga Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba yaliofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Juni 28, 2022. Katika hotuba yake, Makamu wa Rais amewaasa wazalishaji hapa nchini kuzingatia kanuni za ushindani katika soko, ikiwemo kuheshimu mikataba na kuzalisha bidhaa bora na ...
null
Kutokana na upungufu wa dola unaozikumba nchi mbalimbali hivi sasa, Serikali imesema imeanza kutekeleza sera ya fedha ya kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania ili kupata dola kwa ajili ya kuongeza dola nchini. Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kukosekana kwa dola nchini kumetokana na sababu mbalim...
null
Bashungwa aagiza mkandarasi aondolewe kwa kukosa vigezo Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kumuondoa mkandarasi wa kampuni ya Kay Bouvet Engineering Ltd ya nchini India na kumtafuta mkandarasi mwingine mwenye uwezo na sifa za kujenga miundombinu ya barabara katika kiwanda cha ...
null
Kamati ya Bunge: Serikali idhibiti wavamizi wa mgodi wa Barrick Gold North Mara Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imeagiza serikali kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti kundi la vijana wanaopanga mbinu ya kuvamia mgodi wa Barrick North Mara na kuchukuwa mawe yanayodhaniwa kuwa na madini ya dhahabu. Hayo yameelezwa...