name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | Pete ya uchumba ni alama ya upendo inayowavusha wapenzi kutoka kwenye hatua ya awali ya mapenzi na kwenda kwenye hatua nyingine rasmi na muhimu kuelekea katika safari ya ndoa. Pete ya uchumba kwa kawaida ni gharama kubwa, endapo unahitaji kumshtukiza mpenzi wako juu ya uchumba wenu, hakikisha unafanya chaguo lililo sah... |
null | Nafasi 100 za Ajira Serikalini December 10, 2024Nafasi 38 za Ajira Serikalini December 2, 2024Nafasi 80 za Ajira Serikalini November 26, 2024 More News - Fei Toto apeleka TFF ombi kuvunja mkataba na Yanga March 6, 2023 - Mwekezaji wa Misri aahidi kuleta wawekezaji 50 nchini August 13, 2021 Yaliyojiri - Dada wa kazi aku... |
null | Ashikiliwa kwa kumbaka na kumuua mtoto wa chekechea wakati akienda shuleni Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia Maulid Hassan Maulid (18) mkazi wa Mwera Pongwe katika Wilaya ya Kati mkoani humo kwa kosa la kumwingilia kimwili na kusababisha kifo cha mtoto Khadija Mhoda mwenye umri wa miaka 6 na mwanafunz... |
null | Wadukuzi warusha picha za utupu kwenye mkutano wa Spika wa Bunge la Afrika Kusini Katika kupambana na virusi vya corona, shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko ya watu kama vile mikutano zimezuiwa katika nchi mbalimbali, huku watu wakishauriwa kufanya mikutano hiyo kwa njia ya video. Licha ya kamati ya bunge la ... |
null | Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema anategemea kuwa kama Tanzania ilivyokuwa kinara kwenye ukombozi wa Afrika basi itakuwa kinara pia katika kuchangamkia fursa ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika kukuza biashara ikizingatiwa kuwa kupitia miundombinu yake ya bandari imewez... |
null | Miaka ya 20 ni wakati wa mapambano ya kuyaweka maisha yetu katika hali bora hapo baadaye. Nyakati hizi watu wengi hufanya makosa mengi lakini kubwa zaidi hutupa mafundisho na kutufanya kuwa imara. Katika miaka hii kuna mengi unayopaswa kuzingatia na kujifunza ambayo yatakujenga kwa maisha yako yote, na haya ni baadhi y... |
null | Sababu za Rais Samia kutunukiwa Udaktari wa Heshima na chuo kikuu India Chuo Kikuu maarufu nchini India cha Jawaharlal Nehru, leo Oktoba 10, 2023 kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa shahada hiyo na chu... |
null | Mjadala mkubwa umeibuka tena duniani baada ya mtafiti kutoka nchini China kubaini uwepo wa virusi vya corona katika shahawa za mwanaume, hivyo kuibua mjadala juu ya uwezekano wa ugonjwa huo kuambukizwa kwa njia ya kujamiiana. Uchunguzi uliofanywa na daktari kutoka katika Hospitali ya Manispaa ya Shangqiu nchini China u... |
null | Hukumu ya Sabaya: Mafunzo matatu kwa wanasiasa vijana Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Katika kesi hiyo iliyomhusisha Sabaya na waliokuwa walinzi wake wawili, ... |
null | ✕ Habari Siasa Biashara Afya Elimu Maisha Burudani Rubik - © Copyright BKNinja . All Rights Reserved. 24/7 Habari Bila Mipaka Wednesday, December 11 Home › Uncategorized › Orodha ya mashirika 16 ya umma yanayounganishwa na manne yanayofutwa Uncategorized Orodha ya mashirika 16 ya umma yanayounganishwa na manne yanayofu... |
null | Linah azungumzia kiwango cha mahari yake Mwanamuziki Lina Sanga (31) amefikisha miaka 11 kwenye muziki wa Tanzania, akiwa ni sehemu ya wasanii wachache wanaoendelea kufanya vizuri licha ya ukongwe wao. Mwenyewe amesema kuwa siri ya kuendelea kufanya vizuri kwa muda wote ni pamoja na kutunga nyimbo nzuri hasa zinazoenda... |
null | Mchanganuo wa ajira 32,000 zilizotangazwa leo na serikali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ametangaza ajira mpya zaidi ya 32,000 katika sekta za ualimu, afya, kilimo, mifugo, uvuvi na maji huku watumishi 92,000 wakipandishwa vyeo na 6026 wakibadilishiwa kad... |
null | Aliyekuwa mgombea urais kupitia tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Agosti 15, 2022 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati ambapo William Ruto alitangazwa kuwa mshindi. Akizungumza kwa mara ya kwanza kupitia vyombo vya habari, Odinga ame... |
null | Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limewataarifu Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuwa Maulid ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kitaifa yatasomwa usiku wa Jumamosi Oktoba 08, 2022 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam. Siku ya Jumapili litafuatia Baraza la Maulid litakalofanyika katika u... |
null | Uwekezaji ni mchakato wa kutumia rasilimali au fedha katika miradi au biashara kwa matumaini ya kupata faida au kurudisha uwekezaji huo. Katika ngazi ya kimataifa, uwekezaji huchukua sura ya Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) ambapo wawekezaji kutoka nje ya nchi wanawekeza katika miradi ndani ya nchi nyingine. ... |
null | Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ameitikia ombi la Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu la kukutana nae, ambapo wamekutana Brussels nchini Ubelgiji. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, wawili hao wamezungumza masuala ya ustawi wa Tanzania. Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lis... |
null | Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amethibitisha vifo vya Watanzania watano katika ajali ya moto uliozuka kwenye jengo jijini Johannesburg nchini humo. Balozi Milanzi amesema jengo hilo lilishika moto Agosti 31, mwaka huu, huku walioathiriwa zaidi na moto huo wakiwa ni Watanzania na... |
null | Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimeitaka Serikali kufanya mabadiliko madogo ya Katiba iliyopo ili kuruhusu uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na marekebisho mengine ya kikatiba na kuwezesha uchaguzi huru na haki wa mwaka 2024 na mwaka 2025. Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TCD, Prof. Ibrahi... |
null | Jeshi la Polisi limetangaza kuwa kuanzia hivi sasa, mtoto yeyote atakayepotea, kunyanyasika au kutokuwa na usimamizi katika kipindi hiki cha sikukuu, mzazi wa mtoto huyo atachukuliwa hatua. Akizungumza Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam, amewataka wazazi kuhakiki... |
null | Watu kumi wa familia moja, wakiwemo wanawake saba na wanaume watatu wameuawa na watu wenye silaha siku ya Ijumaa katika mji wa Pietermaritzburg, jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini. Inaaminika kuwa watu wawili wenye silaha waliingia kwenye nyumba hiyo na kufyatua risasi kwa familia hiyo, na kwa mujibu wa polisi... |
null | Polisi katika jimbo la Missouri nchini Marekani wanamshikilia bibi wa miaka 78 kwa tuhuma za wizi katika moja ya benki nchini humo. Bonnie Gooch anadaiwa kuingia katika Benki ya Goppert akiwa amevalia barakoa nyeusi, miwani na glovu za plastiki na kukabidhi barua kwa mtoa pesa iliyosema “ninahitaji noti za thamani ya d... |
null | Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa tuhuma za kukiuka utaratibu wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augustino Senga amethibitisha kumshikilia kiongozi huyo pamoja na watu wengine ambao idadi yao ... |
null | More News - Serikali yafuta baadhi ya tozo za miamala kwa maelekezo ya CCM September 20, 2022 - Aina ya watu wanaochelewa kufanikiwa July 24, 2022 Yaliyojiri - Polisi Arusha watoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya December 10, 2024 - Nafasi 100 za Ajira Serikalini December 10, 2024 - Benki ya Dunia yapunguza makad... |
null | Taarifa ya Benki Kuu Tanzania: Alama muhimu kuweza kutambua fedha bandia Dada wa kazi akutwa amejinyonga Musoma December 11, 2024Hatua 5 za kukamilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 December 11, 2024Polisi Arusha watoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya December 10, 2024 More News - RC Burian: Wanaume tumieni ... |
null | Shirika la Transparency International (CPI) linalopambana na rushwa duniani limetoa ripoti yake ya kila mwaka ya rushwa. Nakala ya ripoti hiyo imeonyesha asilimia 90 ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti zilipata chini ya 50, 44 kati ya nchi hizo zilizo na alama za chini sana ni kutoka barani Afrika ambayo inaashiria hali ... |
null | Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Prof. Mussa Assad amesema tatizo lililopo katika suala la ushirikiano wa Tanzania na Dubai kwenye uendeshaji wa bandari ni kuwasikiliza wanasheria ambao hawana utaalamu wa masuala ya uwekezaji. Amesema hayo wakati wa mahojiano na kituo cha Channel Ten ambapo... |
null | Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema chama hicho kitahakikisha kinaimarisha majimbo yote ya Tanzania na Zanzibar ili kufikia dhamira ya kuiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Ameeleza hayo wakati akihutubia katika mkutano mkuu wa jimbo la Geita Vijijini mk... |
null | Akaunti ya YouTube ya Diamond Platnumz yafungwa Akaunti ya YouTube ya mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania, Diamond Platnumz imefungwa kwa kukiuka utaratibu na masharti ya mtandao huo. Platnumz ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul alikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 6 kwenye akaunti hiyo, ikiwa na video ambazo kwa uj... |
null | Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miezi sita au fani TZS 50,000 Sheikh wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Nassoro maarufu kama ‘Kakukulu’ kwa kosa la kumshambulia Asha Aman kwa kummwagia maji ya moto na kumsababishia majeraha makubwa Februari 28, mwaka jana. Mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani... |
null | Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inamshikilia Shaban Adam (54) mkazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutengeneza dawa feki za kulevya aina ya heroini. Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa alikiri kutengeneza dawa hizo, na kueleza kwamba huzisa... |
null | Mpangilio sahihi wa vyeo vya Jeshi la Polisi Tanzania Jeshi la Polisi nchini Tanzania lina jumla ya ngazi 14 za vyeo, cha juu zaidi kikiwa ni Inspekta Jenerali wa Polisi huku cha chini kikiwa ni Kostebo wa Polisi. Kwa mujibu wa tovuti ya jeshi hilo, hapa chini ni mpangilio sahihi vye vyeo hivyo kutoka kikubwa zaidi kwe... |
null | NMB yabainisha mikakati ya kuwakwamua wakulima wadogo Na Mwandishi Wetu Wakulima wadogo wana mchango mkubwa katika kuhakikisha utoshelevu na uhakika wa chakula nchini jambo ambalo Benki ya NMB imeahidi kuendelea kulifadhili na kuliunga mkono kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Akizungumza jana... |
null | Video: Wateja wa TigoPesa waongezewa kiasi cha kuweka na kutuma pesa More News - Meridianbet Waishika Mkono Hospitali ya Madale kwa Kuwapa Vifaa September 27, 2022 - Papa Benedict XVI afariki Dunia December 31, 2022 - Amuua mkewe baada ya kuambiwa mtoto si wake December 23, 2022 Yaliyojiri - Polisi Arusha watoa mitaji ... |
null | Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema gari linaloonekana katika video inayosambaa katika mitandao ya kijamii si lao. Baraza limeeleza kuwa hujitangaza kwa njia mbalimbali ikiwemo kuandaa na kusambaza kava za matairi (wheel covers) zenye ujumbe wa mazingira kwa wadau wake kama linaloonekan... |
null | Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Dkt. Julius Ningu ameshitakiwa katika Baraza la Maadili kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi, vitisho na kuwaweka mahabusu watumishi wa umma. Kikao hicho kimeketi chini ya mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Mstaafu Rose Teemba huku upande wa mlalamikaji ukiwakilishwa na Wakili wa S... |
null | Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni, amekiagiza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) kufanya tafiti zitakazo ibua vyanzo vipya vya mapato na kodi ili kuisaidia Serikali katika kutekeleza mipango ya maendeleo kwa Watanzania. Mhandisi Masauni amesema kuwa vyuo ... |
null | ENDORPHINE FAIRYTALE -Shangwe La Sloti Disemba hii! Cheza na ujishindie ZAWADI KABAMBE ZA FEDHA! Amini mwezi Desemba ni mwezi wa maajabu ya kujishindia mawindo yako kirahisi! Waandaaji wa michezo ya sloti Endorphine wanaopatikana Meridianbet pekee wanakuletea zawadi kibao za mkwanja. Meridianbet wanadhihirisha tena kuw... |
null | Dereva wa Bolt ajivunia mafanikio yake Na Mwandishi Wetu Fabian Shao (32) anasema kuwa baada ya kuacha kazi ya udereva katika shirika moja la kimataifa na kuamua kujiajiri na kuwa dereva wa Bolt amepata mafanikio makubwa katika maisha yake. Shao, ambaye ni mkazi wa Chanika Dar es Salaam ana mke na Watoto watatu, anasem... |
null | Marekani yadai wadukuzi wa China wameiba TZS bilioni 46 za msaada wa UVIKO-19 Wadukuzi wanaohusishwa na Serikali ya China wameiba karibu dola milioni 20 [TZS bilioni 46.6] ambazo ni fedha za msaada za Serikali ya Marekani kwa ajili ya Virusi vya Ugonjwa wa Korona (UVIKO19). Waendesha mashtaka wa Marekani wameishutumu k... |
null | Mambo anayoweza kufanya mtoto aliyemaliza la saba akisubiri matokeo Watoto wa darasa la saba leo wamemaliza mtihani ya kuhitimu elimu ya msingi ulioanza jana Septemba 8, 2021 ambapo zaidi ya watoto milioni 1 wamefanya mtihani nchini kote. Kwa hatua hiyo ina maanisha kuwa wana zaidi ya miezi mitatu kukaa majumbani wakis... |
null | App Inc na serikali ya Singapore zimeingia makubaliano ya kushirikiana kwa miaka miwili katika mradi wa kiafya unaofahamika kama LumiHealth ambapo utakuwa unafuatilia na kutoa zawadi kulingana na tabia za matumiaji kwa kutumia saa za Apple (Watch) pamoja na programu tumishi ya iPhone. Kupitia mpango huo raia wa Singapo... |
null | Chanzo kikuu cha mwingiliano wa dawa na maziwa ni madini yaliyomo katika maziwa yajulikanayo kwa jina la kitaalamu kama ‘Calcium.’ Katika mwili, madini haya yanafanya kazi ya kuimarisha mifupa na meno, ufanyaji kazi ya misuli na mfumo wa fahamu. Unapokunywa maziwa muda mfupi baada ya kumeza dawa, madini haya huchangama... |
null | Chama cha ACT Wazalendo kimesema kinaunga mkono uwekezaji kwenye bandari za Tanzania ili kuziwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na tija zaidi kwenye uchumi. Akizungumzia kuhusu msimamo rasmi wa chama hicho juu ya makubaliano ya IGA kati ya Tanzania na Dubai, Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Dorothy Semu amese... |
null | Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kuhakikisha wauguzi, madaktari na watumishi wote wa Sekta ya Afya wanapata stahiki zao pamoja na kuwasimamia na kufuatilia wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwa na lugha zenye staha kwa wagonjwa. Ameyasema hayo leo wakati akiongea na watumishi... |
null | Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa iliyopo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, aliyetambulika kwa jina moja, Said, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na mwanafunzi wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema siku za nyuma mwalimu huyo alijenga urafik... |
null | Vodacom yatambulisha eSIM, kadi ya simu ya kielektroniki iliyo rafiki kwa mazingira. Kampuni ya teknolojia na mawasiliano inayo ongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC imewataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kuwa sasa wanaweza kuhamia kwenye kadi za kielektroniki yaani eSIM zinazopatikana kwenye mtandao supa wa V... |
null | Janga la Virusi vya Corona si tu limeathiri watu kiuchumi, lakini pia kijamii hasa namna watu wanavyoshiriki katika shughuli zinazohusisha idadi kubwa ya watu. Katika Kijiji cha Kapkiruok nchini Kenya kumefanyika harusi iliyowaacha watu midomo wazi baada ya maharusi watatu kutoka familia tofauti kufunga ndoa pamoja ili... |
null | MAELEZO YA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB.), WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WAKATI AKIWASILISHA BUNGENI HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA 2020/21 - Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti... |
null | Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa wabunge wake waliokuwa wamejitenga kwa siku 14 kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli zote za bunge, leo watarejea bungeni kuendelea na majukumu yao. Taarifa ya chama hicho imeeleza kuwa wabunge hao wanarejea bungeni baada ya kuwa na uhakika kwamba hawana m... |
null | Familia mbili nchini Kenya zimeingia katika mvutano mkubwa wa kisheria kuhusu mahali ambapo atazikwa aliyekuwa mume wa wanawake wawili ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 100. Mzozo huo unaohusu kuzikwa kwa mzee huyo, Silas Igweta umefikishwa mahakamani baada ya mkewe wa kwanza, Grace Rigiri, kuchukuwa hatua ya kis... |
null | Mahakama mkoani Lindi imemhukumu miaka 30 jela mkazi wa Kata ya Ndoro, Manispaa ya Lindi, Naibu Ally (20) baada ya kukutwa na hatia ya kupora simu aina ya Tecno 8 yenye thamani ya shilingi laki sita, mali ya Husna Bilali. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya Mkoa, Conslatta Singano baada ya k... |
null | TAMISEMI yaongeza siku 9 za kupokea maombi ya ajira za ualimu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeongeza muda wa siku tosa wa kupokea maombi ya nafasi za ajira ya walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka Septemba 21hadi Septemba 30 mwaka huu. TAMISEMI imechukua hatua hiyo ili kufidia ... |
null | Kauli ya Rais Dk Magufuli kuhusu uzuiaji wa mifuko ya plastiki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza Watanzania kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuacha kutumia mifuko ya plastiki ambayo ina madhara makubwa katika mazingira na viumbe hai wakiwemo binadamu. Mhe. Rais Magufuli... |
null | Kukua kwa teknolojia ya mawasiliano kunavyochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi Tanzania Na Bindu Hassan,UDBS Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Zainab Chaula wiki hii ameeleza namna sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inavyoweza kuchangia zaidi katika ukuaji wa sekta z... |
null | Tanzania yashinda shindano la TEHAMA China Vijana watatu wa Kitanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika Ndaki ya ICT (CoICT) wameibuka washindi katika mashindano ya TEHAMA duniani upande wa Tuzo Kuu za Mashindano ya Mazoezi na Ubunifu ya Huawei yaliyofanyika Mei 23 hadi 26, mwaka huu Shenzhen, China. Vijana h... |
null | Polisi nchini Malawi wanawashikilia wanaume wawili kwa tuhuma za kuiba zulia jekundu la Rais Dkt. Lazarus Chakwera kutoka kwenye gari la Wizara ya Uchukuzi na Utumishi wa Umma. Taarifa iliyotolewa na polisi imeeleza zulia hilo limepatikana baada ya uchunguzi kufanyika, na watuhumiwa hao waliotajwa kuwa ni Lino Richard ... |
null | Serikali yatangaza mlipuko ugonjwa wa Surua. Hizi ni halmashauri zilizoathirika Serikali kupitia Wizara ya Afya imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa surua katika Halmashauri saba nchini huku watu 38 wakithibitika kuwa na ugonjwa huo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habar... |
null | Rais Samia Suluhu Hassan leo amefanya ziara ya kushtukiza kwa kutembelea soko la Kariakoo mkoani Dar es Salaam. Amewatembelea wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao hasa vyakula ndani ya soko kuu na kujionea msongamano mkubwa wa bidhaa, wafanyabiashara na wananchi wanaokwenda kununua bidhaa. Wafanyabiashara hao wamelalami... |
null | ✕ Habari Siasa Biashara Afya Elimu Maisha Burudani Rubik - © Copyright BKNinja . All Rights Reserved. 24/7 Habari Bila Mipaka Wednesday, December 11 Home › Error 404 404 Page not found Oops! The page you were looking for was not found. Perhaps searching can help. Latest Articles Habari Maisha Dada wa kazi akutwa amejin... |
null | Leo, Benki ya NMB imeingia makubaliano na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushirikiana katika uundaji na uboreshaji wa mifumo ya Tehama yenye lengo la kuimarisha uchumi wa kidijitali wa Nchi yetu. Kupitia makubaliano haya, miongoni mwa mambo ambayo NMB watashirikiana na Wizara ni pamoja na: Uundwa... |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
null | null |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.