name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | TIMU ya Azam FC imesema haiwahofii Pyramids FC ya Misri itakayokutana nayo mzunguko wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Azam FC itakutana na Horseed ya Somalia katika hatua za awali na ikipita itakutana na Pyramids mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo. Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Mtendaji Mku... |
null | MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda amemkabidhi pikipiki Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Milambo iliyopo kijiji cha Mingela Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui wilayani Iramba, Mwalimu Hussein Kionda, kwa lengo la kuondoa changamoto ya usafiri unaomkabili mwalimu huyo. Mwenda ameyasema hayo Nov... |
null | TANZANIA na China zimedhamiria kuendeleza ushirikiano wa kuwanoa wakunga ili wakasaidie kuokoa wanawake wajawazito vijijini kujifungua salama. Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Tanzania China Friendship Promotion Association (TCFPA) Joseph Kahama kwenye uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya wakunga cha ‘Angel o... |
null | MICHEZO ya soka ya Ligi Kuu tano bora barani Ulaya inaendelea kwa patashika kwenye viwanja tofauti. Manchester City inaongoza Ligi Kuu England ikiwa na pointi 23 baada ya mechi tisa wakati Ligi Kuu Hispania vinara ni Barcelona ikiwa na pointi 30 baada ya michezo 11. SOMA: City, Arsenal ukilala umelaliwa Huko Ujerumani ... |
null | WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mshikamano na waandishi wa habari hapa nchini umeweza kunyanyua Sekta ya Elimu na kukuza teknolojia. Mkenda amesema hayo leo Novemba 1, 2024 katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC ) uliofanyika mkoani... |
null | BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo inashuka dimbani katika mechi ya ‘Derby’ ya Dar es salaam dhidi ya Azam ikishikilia rekodi ya kutopoteza mchezo wala kufungwa bao katika raundi nane. Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Yanga inaongoza Ligi Kuu ikiwa na p... |
null | SERIKALI kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) imesaini mikataba 93 ya Sh bilioni 868.56 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya dharura ya barabara na madaraja iliyoathiriwa na mvua za El Nino na Kimbunga Hidaya. Akizungumza leo Novemba 1, mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi... |
null | Africa Kimataifa Tanzania Benki ya Dunia yatoa mabilioni Dar byImeandikwa na Matern Kayera (Dar) na Anastazia Anyimike (Dodoma).October 6, 2022 |
null | DODOMA – WAZIRI wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147 ili kuelekeza asilimia 2 ya mapato ya ushuru wa bidhaa yanayokusanywa kutoka kwenye bidhaa za urembo, vinywaji laini na na vileo (bia na pombe kali) kwenye Bima ya Afya kwa wote. Akisoma bajeti kuu y... |
null | Kanda Tanzania Uwekaji mifugo hereni za kielektroniki watua Tanga byNa Amina Omari, TangaOctober 7, 2022 Biashara Kanda Tanzania Uchumi Ufugaji samaki Rungwe wazalisha ajira 729 byNa Lucy NgowiOctober 7, 2022 Jamii Kanda Tanzania Watakiwa kufanya maandalizi kidato cha kwanza byNa Swaum Katambo, KataviOctober 7, 2022 |
null | KILA majira ya joto, katika saa zinazoambatana na wakati wa chakula, kuna watoto kwenye ukwe au kando ya bwawa, wakingojea kwa subira mchakato mmeng’enyo wa chakula ukamilike. Ni muda gani utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula hukamilika – Wataalamu wanasema huchukua kati ya dakika 30 na saa mbili – lakini inategemea na a... |
null | OKTOBA 29, ilikuwa Siku ya Shampeni na dunia iliadhimisha siku hiyo kwa kuinua glasi ya shampeni katika sherehe zilizofanyika katika nchi nane tofauti. Nchi hizo ni Tanzania ,Ufaransa, Morocco, Afrika Kusini, Uturuki, Nigeria,Ujerumani na Marekani Nchini Tanzania sherehe hii ilifanyika jana Posta, Dar es salaam ambapo ... |
null | JE, unajua kuwa unatakiwa unywe kiasi cha lita 200 za maziwa kwa mwaka? Wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) likipendekeza kila mtu kunywa kiasi cha lita 200 za maziwa kwa mwaka, hapa Tanzania hali ni tofauti. Kwa mujibu wa Msajili wa Bodi ya maziwa nchini, Dk George Mutani, takwimu zinaonesha kuwa kila mtanzania anatu... |
null | JESHI la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia mwanamke Mwazanije Dadi, mwenye umri wa miaka 34, akidaiwa kumuua mtoto wake Najma Ahmad mwenye umri wa miaka 4. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, amesema mwanamke huyu alitenda kosa hilo Desemba 12, 2022 Kijiji cha Sinde, Kata ya Msanga Mkuu wila... |
null | Zaidi ya Sh bil 1.1 zimetumika kufanya ukarabati wa kivuko cha Mv Tanga, ambacho kinatoa huduma ya usafiri eneo la Pangani – Bweni wilayani Pangani, mkoani Tanga. Akizungumza katika hafla ya mapokezi ya kivuko hicho, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba amesema kivuko hicho kilianza kukarabatiwa Juni mwaka huu na hadi ku... |
null | JESHI la Polisi mkoani hapa linamshikilia Hoka Mazuri na watu wengine wanne wakiwemo wanawake wawili, kwa tuhuma za kula njama na kisha kumuua mume wake kutokana na ugomvi wa kifamilia. Wengine wanaoshikiliwa kwa mauaji hayo yaliyotekelezwa Desemba Mosi, mwaka huu ni Shija Masalu, Makoye Lusana, Masunga Mange na Paskal... |
null | MTANDAO wa Kupinga Rushwa ya Ngono Tanzania, umemwomba Rais Samia Suluhu Hassan na Bunge la Tanzania, kukataa pendekezo la kifungu cha sheria kinachofananisha rushwa ya ngono na nyingine. Mtandao huo wenye mashirika jumuishi zaidi ya 150, ulitoa ombi hilo Dar es Salaam jana katika tamko la pamoja lilisomwa na Mwenyekit... |
null | WANAMTANDAO wa kupinga rushwa ya ngono Tanzania wenye mashirika jumuishi zaidi ya 150, yanayounda mtandao wa kupambana na rushwa ya ngono wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan asikubali kipendele kinachomhukumu anayedaiwa rushwa. Akitoa tamko hilo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa mtandao huo, Ruth Meena amesema wanamu... |
null | POLISI Mkoa wa Arusha imeendesha operesheni maaalum, ambapo waendesha pikipiki 127 pamoja na pikipiki 125 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo taa ambazo zimepigwa marufuku, namba bandia, pamoja na pikipiki ambazo zimefutwa namba. Akitoa taarifa hiyo hii leo Desemba 14, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kami... |
null | SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchi (TPDC) limeanza mchakato wa kuzalisha gesi asilia katika eneo la Ntorya lilipo katika kata ya Nanguruwe Mkoani Mtwara. Mkurungenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio amesema wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurungezi kuwa uzalishaji wa gesi utaanza baada ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo k... |
null | MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remedius Mwema Emmanuel amesema mamlaka wilayani humo zimefanikiwa kuondoa umati wa wananchi uliokuwa umevamia lori la mafuta lililopinduka ili kujipatia mafuta. Mapema leo, Habarileo ilichapisha habari kuwa lori la mafuta limepata ajali Gairo na kwamba askari walishindwa kuzuia ... |
null | We continue with letter CH Cheka,ku- Cheka means to laugh,also there are other word like chekelea,chekesha,this also means to laugh or to smile,another is chekesha to amuse ,sample translated sentence mtoto anacheka sana Leo,Juma anajua kuchekesha,waridi anatabasamu,acha kucheka(you don’t laugh) Chelewa means to be lat... |
null | DAR ES SALAAM: Watanzania wametakiwa kuzingatia matumizi bora ya umeme ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaondokana na matumizi yasiyokuwa ya lazima, kuwa na miundombinu bora ili kupunguza upotevu wa umeme. Hatua hiyo itapunguza matumizi mabovu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 14 ya umeme unapotea kutokana na sa... |
null | MECHI nne za raundi ya tatu Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara zinapigwa leo viwanja tofauti. Bingwa mtetezi Simba Queens ipo ugenini dhidi ya Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. SOMA: Ligi Kuu wanawake kuanza kutimua vumbi leo Yanga Princess itakuwa uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam kuikari... |
null | WAZIRI wa Maliasili na Utali, Balozi Dk Pindi Chana amemwagiza Kamishina wa Wakala wa Huduma na Misitu (TFS) Professa Do Santos Silayo kuhakikisha idara hiyo inakujikita katika kukusanya mapato kupitia mfumo Tehama ili idara hiyo iongeze mapato. Balozi Dk Chana ametoa agizo leo Novemba 5, alipofungua Mkutano Mkuu wa Ta... |
null | WANANCHI 300 kutoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi, matiti na tezi dume huku wataalamu wakitoa ushauri kuwa viashiria vya saratani vikiwahiwa mapema vinatibiwa. Meneja wa Huduma za Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk M... |
null | MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi-COP29. Mkutano huo umepangwa kufanyika Novemba 11 hadi 22 katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku. SOMA: Mikakati yawekwa kukabili mabadiliko ya tabia nchi Kauli mbiu ya mkutano huo... |
null | SERIKALI imefanikiwa kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya wilayani Nyang’hwale mkoani hapa, kutoka asilimia 85 mwaka 2020/21 hadi asilimia 87 mwaka 2021/22. Takwimu hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Jamuhuri William alipokuwa akiwasilisha taarifa ya maende... |
null | Search Mwanzo Matangazo: Maelekezo na Bei Kuhusu HabariLEO Nunua E-Paper Home ATM kupima VVU Afya ATM kupima VVU by Na Vicky Kimaro December 19, 2023 Video Player https://habarileo.co.tz/wp-content/uploads/2023/12/kavishe-lawama.mp4 00:00 00:00 00:48 Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease volume. Total 0 Shares... |
null | WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema watu 163, 131 wamegundulika kuwa na maambukizi mapaya ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa mwaka 2023. Ummy ameyasema hayo leo Januari 10, 2023 jijini Dar es Salaam akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini kwa mwaka 2023. Amesema, jumla ya watu 8,145,576 walipima Virusi vya U... |
null | SHILINGI bil 1.2 za mapato ya ndani Manispaa ya Morogoro zimetumika kujenga kituo cha afya Kata ya Tungi. Kituo hicho kitakachokuwa na zana za kisasa za huduma za matibabu kitahudumia watu takribani 16,793 wanaoishi katika kata hiyo na jirani. Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ally Machela alisema hayo jana wakati akizungum... |
null | WATANZANIA milioni 15.92 tayari wamepata chanjo kamili dhidi ya Covid- 19 huku takwimu zikionesha kuwa bado kuna idadi kubwa ya watu wasiokamilisha dozi. Ofisa Programu wa Uelimishaji Jamii kutoka Wizara ya Afya, Juliana Mshama alisema kuwa mpaka sasa waliopata chanjo kamili ni asilimia 51.92 kati ya watu 30,740,643 wa... |
null | BARAZA la Wafanyakazi la Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) limekutana leo kutathmini huduma zimazotolewa na hospitali hiyo ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma. Baraza ambalo limeketi chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Alphonce Chandika, limefanya tathimini ya huduma ili kuongeza ufanisi. Baraza l... |
null | WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema serikali inathamini mchango unaotolewa na mashirika ya kimataifa kwenye maendeleo ya sekta ya afya nchini. Ummy aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dk Zabron Yoti pamoja na Mwak... |
null | DAR ES SALAAM; TATIZO la ugonjwa wa kuvilia damu na vidonda kwa samaki wa kufugwa aina ya sato, sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya kupatikana kwa chanjo. Hilo limebainika wakati timu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ilipofanya ziara katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kilichopo Morogo... |
null | KESI ya kupinga tozo za miamala ya fedha kwa njia ya simu iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), imesikilizwa jana kwa upande wa walalamikiwa ambao ni serikali kuwasilisha pingamizi la awali mbele ya Jaji John Mgeta. Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata aliwasilisha pingamizi hilo kwa kujikit... |
null | Picha Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC byNa IkuluAugust 18, 2021 Picha Profesa James Mdoe akikata utepe kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa byNa Mpigapicha WetuAugust 19, 2021 Featured Kanda Maisha ya Vijijini Tanzania Kampuni yapewa siku 7 maji yasambae Msomera byNa... |
null | HATMA ya nani atapokea kijiti na kushika nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujulikana Novemba 30 mwaka huu jijini Arusha kwenye mkutano wa kawaida wa marais utakaofanyika jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronika Ndu... |
null | ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameaziagiza taasisi zinazosimamia masoko mapya kuweka viwango vidogo vya malipo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wamudu kulipa na kuendelea na biashara katika mazingira mazuri. Rais Dk,Mwinyi alizungumza wakati alipofungua soko jipya la kisasa la ... |
null | KATIKA hatua muhimu kwa muungano wa kiuchumi wa BRICS, kundi hili limezindua mfumo mpya wa “BRICS Pay” ambao unalenga kufumua mfumo wa kimataifa wa malipo. Kundi hilo lilizidua mfumo huo hivi karibuni kwa kugawa kadi za malipo za BRICS kwa washiriki wa kongamano lililofanyika Kazan, Urusi, kuanzia Oktoba 22 hadi 24. Ka... |
null | INGIDA: WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida leo Oktoba 28,2024 kwa ajili ya kupatia ufumbuzi changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo. Chana amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson ambapo pamoja na mambo m... |
null | JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Derick Derick Junior mkazi wa Salasala Kinondoni kwa tuhuma za kujeruhi na kutishia kwa silaha. Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 28, 2024 na kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Murilo Jumanne Murilo imesema kuwa baada ya uchunguzi wa tukio hilo lililotokea Oktoba 2... |
null | RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema serikali itaendelea kuimarisha uhuru wa kuabudu na kuziagiza taasisi za kidini kuendelea kuiombea nchi amani na umoja. Rais Dk Mwinyi amesema taasisi za kidini zina wajibu mkubwa wa kushirikiana na serikali na kuunga mkono juhudi za ku... |
null | Shule ya Sekondari Huria ya Ukonga Skillful imehimiza wazazi kutowakatisha tamaa watoto wao kuwa hawawezi pale wanapofanya vibaya katika masomo yao bali kuwatia moyo kwa kuwapa maneno ya faraja ili wajitahidi. Akizungumza Dar es Salaam katika mahafali ya 18 ya kidato cha nne ya shule hiyo, Muasisi wa Ukonga Skillful Di... |
null | Search Mwanzo Matangazo: Maelekezo na Bei Kuhusu HabariLEO Nunua E-Paper Home BEI ZA KWENYE GAZETI (USD) BEI ZA KWENYE GAZETI (USD) Pakua Sasa Download 151 File Size 411.30 KB File Count 1 Create Date August 9, 2022 Last Updated March 16, 2023 BEI ZA KWENYE GAZETI (USD) |
null | Search Mwanzo Matangazo: Maelekezo na Bei Kuhusu HabariLEO Nunua E-Paper Home BEI ZA MATANGAZO MTANDAONI (TSH) BEI ZA MATANGAZO MTANDAONI (TSH) Pakua Sasa Download 67 File Size 933.45 KB File Count 1 Create Date August 1, 2024 Last Updated August 1, 2024 |
null | Search Mwanzo Matangazo: Maelekezo na Bei Kuhusu HabariLEO Nunua E-Paper Home BEI ZA KWENYE GAZETI (TSH) BEI ZA KWENYE GAZETI (TSH) Pakua Sasa Download 625 File Size 1.05 MB File Count 1 Create Date August 9, 2022 Last Updated March 16, 2023 BEI ZA KWENYE GAZETI (TSH) |
null | BERLIN : RAIS wa Marekani Joe Biden amewasili mjini Berlin kwa ziara ya kikazi kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wengine wakubwa kutoka Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Katika kikao hicho,watajadili pia mgogoro wa Mashariki ya Kati ambao utakuwa ni ajenda kuu y... |
null | NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, ametoa rai kwa wadau wote wa sekta ya Takwimu Rasmi kushirikiana na Serikali katika kukokotoa viashiria vya maendeleo ili kutathmini hatua zilizopigwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa inayoisha mwaka 2025 na hatua zilizopigwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu yanayoisha m... |
null | SERIKALI imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Japan huku ikitoa wito kwa kampuni za Japan kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali katika sekta zenye maslahi ya nchi zote mbili ikiwa ni pamoja na kukuza uwekezaji binafsi. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo ametoa wito huo jijini Dodoma alipokutana ... |
null | KLABU ya Ken Gold ya Mbeya leo imekataa kuachia pointi zote baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika kipute hicho kilichofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya bao la kusawazisha la Ken Gold limefungwa na Emmanuel Mpuka dakika 87 baada ya Coastal Union kut... |
null | DAR ES SALAAM: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM- NEC), CPA Amos Makalla amesema CCM inaendelea kupokea wanachama kutoka katika vyama vya upinzani baada ya kishindo cha ufunguzi wa kampeni. Pia amesisitiza kuwa kishindo walichoanza nacho watamaliza nacho huku akiongez akuwa wanataka ushindi wa... |
null | DAR ES SALAAM :Wamiliki wa kampuni za bima, watu wa wanaohusika na gereji za magari, wametakiwa kufuata mwongozo sahihi wa utoaji wa huduma hizo uliotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Ili kuondokana na malalamiko ya udanganyifu, ucheleweshaji wa malipo na huduma mbovu kwa wateja wao. Hayo yamesemwa... |
null | KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) , Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema Chama hicho hakicheki na mtu katika kushika dola na katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanashinda kwa kishindo. CPA Makalla ameyasema hayo leo Movemba 23,202... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuajiri walimu wa somo la biashara 4,000 kwa ajili ya kufundisha wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Walimu hao watafuata mtaala mpya unaotumika, unaolenga kuleta mapinduzi ya elimu nchini kwa kuimarisha elimu ya biashara kwa wanafunzi. Akifungua Maf... |
null | MKUU wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, amewaagiza viongozi wa mitaa, vijiji na kata kwa ushirikiano na makarani wa sensa kuhakikisha wanawaandaa wachimbaji wadogo, ili kufanikisha sensa kwenye maeneo ya migodini. Shigella ametoa maelekezo hayo alipokuwa akizungumuza na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale... |
null | WIZARA ya Maji imetoa siku saba kwa Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Handeni, Hosea Joseph amsimamie mkandarasi wa kampuni inayotekeleza Mradi wa Maji katika Kijiji cha Msomera ahakikishe maji yanafi ka kwenye tangi na kuyasambaza kwa wananchi. Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi alitoa agizo hilo jana alipokagua mradi ... |
null | KIEV, Ukraine – Maafisa wawili wa Usalama ambao walidaiwa kuwa sehemu ya njama ya kuwaua maafisa wakuu wa serikali na jeshi wamekamatwa, Idara ya Usalama ya Ukraine (SBU) imetangaza. Shirika hilo, lilidai katika chapisho kwenye Telegram kwamba washukiwa hao wawili walikuwa wakipanga kumuua Rais wa Ukraine Vladimir Zele... |
null | SUDAN: MWAKILISHI wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu,Tom Fletcher ameonyesha wasiwasi wake kuhusu vitendo vya udhalilishaji wa kingono vinavyoendelea kufanywa dhidi ya wanawake wa Sudan. Akizungumza katika ziara yake ya kwanza katika mji wa Port Sudan, Fletcher ambaye anaongoza Ofisi ya Um... |
null | DAR ES SALAAM :Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TANTRADE) imeandaa shindano la kutengeneza logo ya Made In Tanzania itakayotumika kama nembo ya bidhaa na huduma zinazotengenezwa nchini Tanzania. Logo hiyo ambayo ni sehemu ya mpango wa nembo ya taifa inalenga kuwa ishara ya taifa inayounganisha na kuwakilisha... |
null | WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Novemba 22 anamwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la tano ya Maendeleo ya Biashara na Uchumi linalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma. Kongamano hilo linatoa fursa kwa wanafunzi, taasisi za elimu, wataalamu wa sera, wajasiriamali, na... |
null | DAR ES SALAAM: Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imetoa jumla ya mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.1 tangu kuanzishwa kwake huku ikizindua huduma ya LIPA POPOTE kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa biashara. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja wadogo na wakati wa TCB, Lilian Mtali wakati wa... |
null | DAR-ES-SALAAM : MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari nchini imesema Chama cha Ushirika cha Kuweka na kukopa cha mamlaka hiyo kimesaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa Mamlaka hiyo na kupata nguvu ya kuhudumia mizigo inayofika katika bandari hiyo na kukuza uchumi wa nchi. Akifungua mkutano mkuu wa 56 wa C... |
null | SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imefanya kongamano la kodi kikanda kwa kuwakutanisha wadau kutoka sekta binafsi wakijumuisha wataalam na washauri wa kodi, wadau wa sekta mbalimbali nchini, wafanyabiashara, wazalishaji wa bidhaa na mazao mbalimbali pamoja na makundi maalum ili kuboresha mifumo ya kodi itakayochochea ma... |
null | BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imezifungia programu tumizi 69 zilizokuwa zikitumika kutoa mikopo kidijiti. Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba ameeleza kuwa wamebaini kuna ma jukwaa na programu tumizi yanayo jihusisha na utoaji wa mikopo kidijiti bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka BoT. Tutuba alieleza kuwa programu hizo 6... |
null | WATUMISHI na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jumuishi ya Ruhinda iliyopo Kata ya Nyaishozi Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wameishukuru serikali kwa kuwafikishia huduma ya umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Licha ya kupata huduma hiyo pia wameomba kuwaboreshewa miundombinu ya nishati ya kupikia. Ombi hilo ... |
null | MASHINDANO ya mpira wa miguu ya ‘Samia Kagera Cup’ yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mkoani Kagera yakiubeba ujumbe wa elimu mahususi ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024. Akizungumza leo Novemba 8, 2024 mwanzilishi wa mashindano hayo, Leonard Kache... |
null | NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema mafanikio yanayoonekana sekta ya nishati ni jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwani ndiye anayetafuta fedha za kutekeleza miradi ya nishati nchini. Kapinga amesema hayo leo Novemba 07, bungeni jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na wab... |
null | Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeahidi kujenga mifumo ya nishati safi ya kupikia pamoja na jiko katika Shule ya Sekondari ya Mchanganyiko ya Ruhinda iliyopo Wilaya ya Karagwe, Kagera. Ahadi hiyo imetolewa Novemba na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy wakati wa muendelezo wa ziara ya viongozi mbalimbali wa... |
null | RIPOTI ya Benki ya Dunia na Takwimu za Taasisi ya Jiolojia ya Marekani kuhusu makisio ya utajiri wa mashapo ya Madini ya Kinywe ifikapo mwaka 2050 imeitaja nchi ya Tanzania kushika nafasi ya Sita (6) Duniani na nafasi ya Tatu (3) Afrika huku Msumbiji ikishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Madagascar kwa upande wa nchi... |
null | SIMIYU: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema hatamvumilia Mkurugenzi yeyote wa halmashauri ambayo ataitia aibu serikali na kuifanya itukanwe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Mchengerwa ametoa kauli hiyo baada ya kufika katika shule ya msingi Mwama... |
null | DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Upimaji wa Afya kwa Jamii wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Dk Pedro Pallangyo amewashauri wananchi kunywa maji lita mbili kwa siku ili kukabiliana na hali ya kukaukiwa na maji mwilini. Akizungumza na Daily News Digital daktari huyo ame... |
null | WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa jitihada za kutangaza vivutio vya utalii nchini huku akisisitiza kuwa hayo ndio maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza falsafa ya 4R. Falsafa hiyo ni Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi ... |
null | HALMASHAURI ya Wilaya ya Ngorongoro imenunua jumla ya dozi 44,000 za chanjo kwa ajili ya kuchanja mbuzi na kondoo ili kudhibiti ugonjwa wa homa ya mapafu (CPPP) kutoka kwa Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania Kanda ya Kaskazini (TVLA). Hayo yamesemwa wilayani Ngorongoro na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya... |
null | Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Lameck Nchemba amesema Serikali itaendelea kukiwezesha kibajeti Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) ili kiweze kuwa na miundombinu na rasilimali watu inayokidhi mahitaji ya utoaji wa elimu kwa viwango bora. Akizungumza kwa niaba ya Dk Nchemba katika Mahafali ya 38 duru ya kwanza ya... |
null | WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ni muhimu kuunganisha taaluma na viwanda katika sekta ya utalii na ukarimu ili kufungamanisha maarifa ya kitaaluma na ujuzi ili kuziba pengo la wahitimu wasio na ujuzi stahiki. Mkenda ametoa kauli hiyo jijini Arusha katika kilele cha Kongamano la Kimatai... |
null | JESHI la Polisi linawashilikia na kuwahoji kwa kina mkazi wa Mikocheni, Diva Gissele Malinzi(36), na Jenifer Jovin Bilikwija(25), mkazi wa Salasala Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kukusanya fedha kwa kutumia kwa ajili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo la ghorofa jijini Dar es Salaam Novemba 16 kwa kutumia ak... |
null | Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Mifumo Ikolojia (EBARR), unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais umewezesha upimaji wa mipaka ya vijiji sita, utayarishaji wa ramani na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji vinne katika Halmashauri ya Simanjiro mkoani Manyara. Hayo yamebainishwa na Kai... |
null | WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara jijini Dodoma ya kukagua utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia kwenye taasisi zenye watu zaidi ya 100 zilizopo jijini Dodoma. Katika ziara hiyo iliyofanyika leo Novemba 7, Majaliwa ametembelea kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Makutupora (834 KJ), Shule... |
null | TANZANIA inatarajia kunufaika kiuchumi utakaotokana na kukuza utalii wa mikutano na matukio (MICE Tourism) na kutangaza utalii kimataifa wakati itakapokuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali wa Afrika (AAAGs) unaotarajia kufanyika Desemba 2 hadi 5, mwaka huu mkoani Arusha. Mhasibu Mkuu wa Se... |
null | SERIKALI imesema shughuli za uchumi nchini zimeendelea kuimarika licha ya changamoto zinazoikabili kutokana na utekelezaji wa Sera za ya Fedha ya kupunguza ukwasi katika nchi zinazoendelea Ikiwemo pia migogoro ya kikanda na kimataifa, kuongezeka kwa bei ya petrol, gharama kubwa za mikopo na mabadiliko ya tabianchi. Waz... |
null | WATAFITI wametakiwa kutoa matokeo ya tafiti zao ili ziwanufaishe wananchi katika kuhakikikisha changamoto za jamii zinatatuliwa sambamba na kukuza uchumi. Hayo yamesemwa jijini Arusha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu, D... |
null | MAREKANI : WAENDESHA mashtaka nchini Marekani wamesema nguli wa miondoko ya muziki wa Rap na mtayarishaji wa muziki Sean Diddy Combs anavunja sheria za gereza kwa kuwasiliana na mashahidi wa kesi yake kinyume cha sheria. P DIddy anashutumiwa kwa kushawishi mashahidi kwa kutumia simu za wafungwa wengine huku akiendelea ... |
null | TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Morogoro imeazisha na uchunguzi wa awali kwenye miradi kadhaa ukiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Tungi kilichopo Manispaa ya Morogoro yenye thamani ya Sh milioni 720. Mkuu wa Takukuru Mkoa, Pilly Mwakasege amesema hayo Novemba 26, 2024 wakati akitoa taarifa kwa umma ya ... |
null | TANZANIA kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa kuwa nchi mwenyeji kwenye wa Makutano wa saba (7) wa Kimataifa wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia Novemba 29 hadi Desemba 10, 2024 jijini Dar es salaam. Katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa U... |
null | MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paulo Mkonda,amesema kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, mwanachi yoyote atakayetupa taka hovyo atatozwa faini ya Sh milioni 1, lengo kuimarisha usafi wa jiji la Arusha. Makonda amesema hayo leo jijini humo Arusha mara baada ya kuzindua kampeni ya usafi katika soko la Kilombero, kata ya Levolosi. Am... |
null | CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimehitimisha kampeni zake kwa kishindo katika mtaa wa Wambi, Mafinga mjini, kikiwataka wanachama wake kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura ili kufanikisha ushindi wa kishindo, hata katika maeneo yasiyo na wagombea wa upinzani. Akihutubia umati wa wanachama wa CCM, Mju... |
null | OKTOBA 13, 2022, HabariLEO ilipita katika Taasisi ya Ocean Road (ORCI) na kushuhudia wagonjwa wakiendelea na matibabu. Baadhi walikuwa waliowahi matibabu ugonjwa ukiwa bado katika hali ya chini na wengine wakiwa wamechelewa na ugonjwa ulikuwa juu. Nje ya ukuta wa jengo hilo watu wawili walikuwa wakitoka hospitalini hap... |
null | KIPANDE cha ujenzi wa reli ya kati Tabora- Kigoma kitagharimu dola za Marekani bilioni 2.7 sawa na shilingi trilioni 6.34. Reli hiyo ambayo mkataba wake umesainiwa leo Desemba 30, 2022 SGR LOT 6 (Tabora – Kigoma) katika Ukumbi wa Kikwete – Ikulu jijini Dar es Salaam, itachukua miezi 48 kukamilika. Akizungumza wakati wa... |
null | MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema hakuna mwanafunzi kuanzia shule ya awali, msingi wala sekondari jijini Dar atakayeshindwa kwenda shule kwa kigezo cha uhaba wa madarasa au madawati. Makala ameyasema hayo leo Desemba 20, 2022 katika hafla ya utiaji saini, ambao umehusisha serikali kupitia Shirika la R... |
null | ZIKIWA zimebaki siku nne kuadhimishwa kwa sikukuu ya Krismasi, wafanyabiashara wa nguo mkoani Dar es Salaam wamesema biashara ya bidhaa hizo kwa msimu wa mwaka huu imedorora ikilinganishwa na miaka ya nyuma. HabariLEO lilifanya mahojiano na wafanyabiashara katika maduka mbalimbali mkoani humo ili kujua uhalisia wa mauz... |
null | HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili(MNH), imetangaza kufunga lango kuu la kuingilia kwa waenda kwa miguu kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Desemba 12 ,2022, hadi Machi 30,2023, ili kupisha ukarabati wa eneo hilo. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu Kitengo cha Uhusiano wa Hospitali hiyo, Neema Mwangomo, imesema kufuatia hatua... |
null | Katibu Mkuu Utumishi Dk Laurean Ndumbaro, amewataka watumishi wa bima nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa lugha rahisi, ili kuwasaidia wananchi kufahamu umuhimu wa bima kujikinga na majanga kwa maendeleo yao. Ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano wa tatu wa baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIR... |
null | Pornografia, cu o gamă largă de genuri și teme, poate servi drept platformă pentru diversificarea și crearea de noi idei sexuale. Ne propunem să ajutam persoanele in explorarea rolului porno pentru descoperirea unor noi concepte in materie de sex. Porno oferă un spectru larg de activități și scenarii sexuale, de la van... |
null | KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Nuhu Mruma amewataka waumini wa dini ya Kiislamu nchini na Watanzania kwa ujumla kujitokeza na kushiriki Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti 23. Aidha, amewahimiza viongozi pamoja na waumini wa dini hiyo, kuitumia ibada ya Ijumaa hi... |
null | MAMIA ya waumini wa Kanisa Katoliki wamehudhuria kusimikwa Padri Christopher Nkoronko kuwa Askofu Jimbo Katoliki Kahama. Askofu huyo aliteuliwa na Baba Mtakatifu, Francisko kushika nafasi hiyo tangu Machi 19, mwaka huu. Askofu Mkuu, Paul Ruzoka wa jimbo kuu la Tabora aliyeendesha ibada ya uwekaji wakfu katika Kanisa Ku... |
null | WAUMINI wa dini ya Kiislam kutoka mataifa mbalimbali, wameanza kuwasili mkoani Katavi katika ibada ya siku 3 ya Ijitimai ya kimataifa yenye lengo la kuendeleza amani na utulivu. Akizungumza na waandishi wa habari, Sheikh wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu, amesema Ijitimai ni ibada inayowakusanya waumini wa dini hiy... |
null | WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum, George Mkuchika amezipongeza taasisi za dini nchini kwa kujitoa kushiriki katika kutoa huduma za kijamii kwa Watanzania bila kujali imani za kidini. Mkuchika ametoa pongezi hizo katika kilele cha Jubilee ya miaka 75 ya Shirika la Masista wa Chama Cha Mariam Mtakatifu (CMM) wa k... |
null | WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema serikali inatambua mchango wa makanisa nchini katika kuimarisha ustawi wa jamii. Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto. “Ser... |
null | SERIKALI imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali kama Utalii, Kilimo, Madini, Viwanda, Uvuvi na Ufugaji, kulinda viwanda vya ndani, kuvutia mitaji na uwekezaji nchini. Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, Robert Manyama amesema hayo wakati wa kupokea na kukus... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.