name stringclasses 429
values | text stringlengths 0 767k ⌀ |
|---|---|
null | DODOMA : WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema tangu kuanzishwa kwa mradi wa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) serikali imezalisha ajira za watu zaidi ya 30,176 za moja kwa moja na 150,000 zisizo za moja kwa moja. Akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2... |
null | BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limetoa wiki moja kwa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini(TARURA ) kuhakikisha wanatoa majibu juu ya hatua waliyochukuwa kuhusu ujenzi wa barabara ya kwenda Dampo Kata ya Kizumbi kutokana na miundombinu yake kuharibika. Agizo hilo limetolewa na Mstahiki Meya M... |
null | For instance, in October 2019, Google LLC partnered with NASA, and Oak Ridge National Laboratory to provide the best quantum computing service in the world, also other major industries are investing heavily in quantum computing startups, such as D-Wave systems for R&D. For instance, industry giants such as Lockheed Mar... |
null | WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, amesema serikali inatarajia kunufaika na mpango wa msaada wa miaka mitatu utakaogharimu dola za Marekani bilioni 30, ulioahidiwa na Rais wa China, Xi Jinping wa kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na umaskini. Dk Nchemba alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipozungu... |
null | KAMPUNI kubwa ya nishati ya Urusi, Gazprom imetangaza Ijumaa kwamba usafirishaji wa gesi asilia hadi Umoja wa Ulaya kupitia bomba la Nord Stream 1 utasitishwa kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 2 kwa matengenezo. “Mnamo Agosti 31, kitengo pekee cha kujazia gesi cha Trent 60 kinachofanya kazi kitafungwa kwa siku tatu kwa a... |
null | WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka waandishi wa habari nchini kutumia vyema taaluma yao na kujikita katika habari za uchunguzi ili kufichua maovu hali itakayosaidia serikali kufanya maamuzi sahihi. Pia, ameelezea kusikitishwa kwake na namna baadhi ya vyombo ya habari hususani v... |
null | NASA imetangaza kuwa imechagua maeneo 13 yaliyoko katika ncha ya kusini mwa Mwezi ambayo yatatumika kama vituo vya wanaaga wa Artemis III, mradi unaotazamiwa kupeleka tena wana anga Mwezini mnamo 2025. “Kuchagua maeneo haya kunamaanisha kuwa tumekaribia kuwarejesha wanadamu Mwezini kwa mara ya kwanza tangu Apollo,” ali... |
null | MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP), Camillus Wambura kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa Jeshi la Polisi na kuwachukulia hatua askari wachache wanaoharibu taswira ya jeshi hilo. Dk Mpango alitoa maagizo hayo jana ofisini kwake Dar es Salaam alipok... |
null | IDADI ya watumiaji wa internet nchini China imefika bilioni 1.032 mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 83 ikilinganishwa na mwaka 2012, mapinduzi yaliyotokana na maboresho katika sekta ya mawasiliano nchini humo. Maboresho hayo pia yamechangia katika ongezeko la mapato kufikia Sh trilioni 504.4 (Yuan trilioni 1.47... |
null | IDADI ya watumiaji wa simu za 5G nchini China ilifikia milioni 475 mwishoni mwa Julai, mwaka huu kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari (MIIT). Idadi hiyo ilisajili ongezeko la jumla la watumiaji milioni 120 ikilinganishwa na Desemba 2021, Ofisa wa MIIT aliuambia mkutano wa waandishi wa habari. Hadi ku... |
null | SERIKALI imeongeza fedha za utafi ti kutoka Sh bilioni tatu hadi kufi kia bilioni tisa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa ajili ya kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu utakaowezesha kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga alisema hayo hivi karib... |
null | KAMPUNI ya Apple imeonesha dosari ya kiusalama kwa bidhaa zake za iPhone, iPad na Mac ambayo inaweza kuruhusu wavamizi kuchukua udhibiti kamili wa vifaa hivyo. Apple ilitoa ripoti mbili za usalama kuhusu suala hilo Jumatano wiki hii, ingawa hawakupata uangalizi mkubwa nje ya machapisho ya teknolojia. Ufafanuzi wa Apple... |
null | MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amesema mfuko umepata matokeo makubwa na mazuri ya uwekezaji kutokana na kuwekeza kwenye maeneo salama. Mshomba alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko pamoja na vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2022/23. ... |
null | Kiongozi wa Israel, Benjamin Netanyahu ameidhinishwa kuwa Waziri Mkuu wa Israel baada ya baraza lake la mawaziri lenye misimamo mikali ya mlengo wa kulia likiapishwa kwa ahadi za kupanua makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kufuata sera nyingine zinazokosolewa ndani na nje... |
null | MAREKANI : MGOMBEA wa Chama cha Republican nchini Marekani,Donald Trump ametangazwa kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani na kuahidi kuliponya taifa hilo. Matokeo ya uchaguzi yamemuweka mgombea huyo wa Republican kifua mbele dhidi ya mgombea wa Demokratic Kamala Harris . Akiwahutubia wafuasi wake mapema leo hata kabla ... |
null | ULAYA : MAWAZIRI wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi saba tajiri duniani la G7 pamoja na nchi nyingine, wamelaani vikali kitengo cha Korea Kaskazini kupeleka wanajeshi wake Urusi. Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia hao wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutumika kwa wanajeshi hao katika uwanja wa vita nchini... |
null | MAREKANI : WIZARA ya Sheria nchini Marekani kwa kushirikiana na mwendesha mashtaka maalum,Jack Smith wako katika majadiliano kuhusu jinsi ya kumaliza mashtaka dhidi ya Donald Trump. Smith kwa sasa anaongoza kesi nyingi dhidi ya Trump, ambaye atakuwa rais wa kwanza kuchukua madaraka wakati akikabiliwa na kesi kadhaa. Hi... |
null | MAREKANI : VIONGOZI mbalimbali duniani wamempongeza mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump alipotangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais wa Marekani. Miongoni mwa viongozi waliompongeza Donald Trump ni Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ambaye amesema ataendelea kushirikiana na Marekani kwa ukaribu, “ni ... |
null | CONGO : MAWAZIRI wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamethibitisha haja ya pande zinazozozana kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano mashariki mwa Congo. Wawakilishi wa Congo na Rwanda walikutana na waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete Antonio mjini Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini,... |
null | NIGERIA : MKUU wa Jeshi la Nigeria Jenerali Taoreed Lagbaja amefariki dunia baada ya kuugua akiwa na umri wa miaka 56. Akitangaza kuhusu taarifa ya kifo cha Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Jenerali Taoreed Lagbaja,Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Jenerali Taoreed Lagbaja aliaga dunia usiku wa kuamkia leo jijini Lagos. Jen... |
null | CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza serikali kupitia Wizara ya Kilimo kumwondoa haraka Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora kwa madai amekuwa chanzo cha kukwamisha jitihada za kuwainua wakulima wa zao la tumbaku. Aidha, kimeshauri kujengwa kwa kiwanda cha kuchakata tumbaku pamoja na kiwanda cha kutengeneza siga... |
null | NCHI za Ushirikiano wa Mpito wa Bonde la Mto Nile (NBI) zimetakiwa kutengeneza mikakati ya kulinda rasilimali maji ya Bonde la Mto Nile ili kulinda chanzo hicho cha maji kinachotumiwa na watu zaidi ya milioni 278 wanaoishi katika bonde hilo. Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, ... |
null | KILA Novemba 19 huwa ni maadhimisho ya siku ya choo duniani. Katika taarifa ya kuadhimisha siku hii, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Matshidiso Moeti amesisitiza juhudi ziongezwe zaidi kuhakikisha kila mtu anakuwa na choo salama ifi kapo 2030. Amesema kulingana na takwimu za Mpango wa Pamoja wa Ufuatili... |
null | AKIWA ziarani mkoani Njombe mwezi uliopita, Rais Samia Suluhu Hassan aliwataka viongozi wanaopewa dhamana ya kuhudumia wananchi wazingatie utawala bora na kuelekeza juhudi na akili zao katika kuhudumia wananchi badala ya kujifanya watawala. Rais Samia anasema suala la utawala bora, viongozi wa ngazi za mikoa na wilaya ... |
null | MICHEZO ya 13 ya Mataifa ya Afrika itafanyika Accra, Ghana mwakani na Tanzania ni miongoni mwa nchi 53 zinazotarajia kushiriki michezo hiyo. Wachezaji watakaoshiriki watatumia michezo hiyo kama maandalizi kwa ajili ya kufuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Paris, Ufaransa mwaka 2024. Michezo ya 22 ya Jumui... |
null | KATIKA jamii yetu kumekuwepo na wimbi la matukio ya kuuana kwa wapenzi au wanandoa kutokana na sababu mbalimbali kuanzia wivu wa mapenzi hadi imani za kishirikina. Matukio haya yamekuwa yakiongezeka kila uchwao huku yakiteketeza watu ambao ni tegemeo katika familia zao na taifa kwa ujumla. Hali hiyo imekuwa ikiacha fam... |
null | TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kesho inaendelea na kampeni zake za kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) itakapoikaribisha Uganda au The Cranes kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Hii ni hatua ya pili kwa Taifa Stars katika mbio za kusaka ku... |
null | SIMBA Queens imemaliza hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) bila kufungwa baada ya kuifunga Yei Joints Stars mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo Simba Queens imefikisha pointi tisa ikiwa kinara... |
null | Michezo na Burudani Mauritania yajitoa mashindano ya FAU ikituhumu ‘mamluki’ byNa Mwandishi WetuAugust 21, 2022 |
null | KOCHA wa timu za soka za Taifa za wanawake, Bakari Shime amesema anaamini Twiga Stars itakwenda kutetea ubingwa wa mashindano ya Cosafa (Baraza la vyama vya soka Kusini mwa Afrika) yanayotarajiwa kuanza Agosti 31, Port Elizabeth, Afrika Kusini. Akizungumza na gazeti hili jana, Shime alisema Twiga Stars ambao wamepangwa... |
null | UTATA umeibuka baada ya Timu ya wavulana chini ya miaka 15 U15 ya Mauritania kuamua kujiondoa katika mashindano ya FAU Kanda ambayo yanafanyika nchini Liberia. Sababu ni tofauti ya umri kati ya wachezaji wao na wale wa Sierra Leone, ambao walifunga 6-0 kwenye mechi ya ufunguzi. Picha zinaonyesha tofauti za urefu na sur... |
null | VITA ya kuwania taji la Ligi Kuu Bara kwa watani wa jadi Simba na Yanga imeanza kunoga baada ya jana kushinda mechi zao kwenye viwanja tofauti. Shangwe zilianza kwa mabingwa watetezi wat aji hilo Yanga, walokuwa wageni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kuikabili Coastal ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. ... |
null | KOCHA Mkuu wa Simba, Zoran Maki ame wapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kuvuna pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Huo ni mchezo wa pili Simba kushinda tangu ligi ianze baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold kwenye Uwanja huohuo. Akizungumza baada y... |
null | SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limeahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kutoa vifaa vya kutosha vya matayarisho muhimu ya kudhibiti viashiria vya tishio la ugonjwa wa Ebola. Mtaalam wa Maabara wa Shirika la Afya (WHO) nchini, Mura Ngoi, akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa jana Septemba 3,2022, alis... |
null | WAKALA wa Majengo nchini (TBA), imewahahakikishia Watanzania kuwa itaendelea kubuni, kutathmini, kutekeleza na kusimamia miradi ya ujenzi kwa ufanisi, kwani serikali imeweka mazingira wezeshi kwa TBA kuwajibika. Meneja Uhusiano kwa Umma wa TBA, Fredrick Kalinga, amesema hayo kwa waandishi wa habari katika maonesho ya t... |
null | JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia Nestory Elias (62), mkazi wa Bon’gola, Kata ya Kilakala, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Mwajuma Sadru (75), mkazi wa mtaa wa Bong’ola. Bibi huyo anadaiwa kuuawa na mwili wake kutelekezwa, kisha kufunikwa kwa mawe umbali wa mita 180, kutoka nyumbani kwake eneo... |
null | HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 710 kwa shule 33 za msingi katika manispaa hiyo. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliofanyika leo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala ameishukuru halmashauri kwa kutoa madawati hayo. Amesema madawati hayo yamegharimu zaidi... |
null | SERIKALI imeahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara, ili kufungua shughuli za kiuchumi, ambapo kwa sasa miudombinu ya barabara za wilaya zimeimarishwa kutoka asilimia 15 mpaka asilimia 25. Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff, leo Oktoba 3,... |
null | MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Dustan Kyobya, amelitaka Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Mtwara, kutumia wiki ya huduma kwa wateja, kuelimisha wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo na namna bora ya kuzipeleka kwa wananchi kwa haraka. Kyobya ametoa agizo hilo leo wakati akizundua utoaji wa huduma hizo ... |
null | MKAZI wa Kitongoji cha Manyata wilayani Chemba, Nada Songo amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi maeneo ya kifuani na mguu wa kulia huku askari na mgambo wakijeruhiwa kwa mishale. Tukio hilo lilitokea Jumapili katika Kitongoji cha Manyata, Kijiji cha Chioli kilichopo Tarafa ya Goima wilayani Chemba mkoani Dodo... |
null | BENKI ya NMB Jumatatu imezindua mashine ya kutolea fedha (ATM) ya kwanza katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro (KIA) yenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni kwenda shilingi za Kitanzania. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema wateja na hata wasio wateja wa N... |
null | MKUU wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila alisema mkoa huo hadi juzi kazi ya kuhesabu watu, sensa ilifikia asilimia 97.4 na walitarajia kuimaliza jana kwa ufanisi. Chalamila alisema makadirio yaliyokuwa yamefanywa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ni kufikia kaya 644,655 za Mkoa wa Kagera na hadi Jumatatu saa 2 asubuhi kaya ... |
null | RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema serikali yake inayakaribisha mashirika ya bima yaende Zanzibar kuwekeza kwenye miradi. Dk Mwinyi alisema hayo jana alipofungua mkutano wa 44 wa Umoja wa Wanabima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI). Alisema wakati serikali inafanya mageuzi ya kiuchumi kuna haja y... |
null | OFISA Afya Mazingira Kata ya Viwandani jijini Dodoma, Gwantwa Mbwile amesema elimu bado inahitajika kwa wajasiriamali ili waweze kujisimamia wenyewe, waepukane na faini wanazotozwa kwa mujibu wa sheria ndogo za jiji. Alisema hayo Jumapili wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye oparesheni ya ukaguzi wa usafi u... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan ameridhia wanafunzi 28,000 waliokidhi vigezo waliopaswa kusajiliwa vyuoni waende vyuoni kuendelea na usajili chini ya uratibu wa Wizara ya Elimu wakati taratibu muhimu zikikamilishwa. Akitoa hoja ya kuahirisha Bunge leo Ijumaa, jijini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaeleza wabunge kuwa ... |
null | SPIKA wa Bunge Dk Tulia Ackson ametangaza kuwa wabunge wamechanga kiasi cha Shilingi 5,023,000 kwa lengo la kumpongeza kijana Majaliwa Jackson aliyeshiriki kuwaokoa abiria wa ndege ya Precision Air. Awali, Mbunge Hamisi Kigwangalla aliomba mwongozo bungeni akitaka wabunge wakatwe kiasi cha Sh 50,000 kutoka kwenye posho... |
null | MVUA iliyo ambatana na upepo mkali imeharibu nyumba 31 katika kijiji cha Tukoma, Kata ya Itenka halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi hali iliyopelekea baadhi ya familia kulala nje huku nyingine zikikosa kabisa makazi. Akitoa taarifa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mpanda, Afisa mtendaji wa Kata ya Iten... |
null | Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania wote hususan wasanii wa kizazi kipya, kuepuka kuiga kila tamaduni bila kuchuja wala kuzingatia maadili ya taifa. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo linalofanyika katika Taasisi ya Sanaa na ... |
null | Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa hoja ya kuahirisha Bunge leo jijini Dodoma huku akizipongeza timu za Simba na Yanga kwa kuingia hatua za makundi katika mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika. Mbali na Simba kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikitinga hatua ya Makundi ya Ko... |
null | SERIKALI imesema itaingia mkataba na sekta binafsi kwa ajili ya uendeshaji wa kivuko cha Kigamboni lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi, Rais Samia Suluhu Hassan amethibitisha leo akiwa Kigamboni, mkoani Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ma... |
null | SERIKALI imewataka wahandisi wa maji kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ili kuondoa tatizo la upatikanaji maji nchini na kuleta hali ya sintofahamu kwa wananchi. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati alipotembelea miradi ya maji iliyopo Jimbo la Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa. “Niwaombe radhi wananchi,... |
null | KAMPUNI ya Japan Tobacco Incorporation (JTI), imeahidi kununua kilo milioni 30 za tumbaku kutoka kwa wakulima wa Tanzania msimu ujao wa kilimo. Ahadi hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 na Rais na Mtendaji Mkuu wa JTI, Masamichi Terabatake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliyetembelea ofisi zao, ili ku... |
null | WANANCHI mbalimbali, leo wamejitokeza kumzika mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Zaituni Saedia, aliyefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Zaituni amezikwa jioni hii katika makaburi ya Bakwata, Kinondoni, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wenzake wa TSN,... |
null | Afya Chakula & Vinywaji Dodoma Jamii Tanzania WHO: Kila mtu anywe maziwa lita 200 kwa mwaka bySifa LubasiSeptember 26, 2022 |
null | MAHAKAMA ya Wilaya ya Iringa, imemuhukumu kifungo cha maisha, Ayubu Kiyanza (22) mkazi wa eneo la Don Bosco Manispaa ya Iringa, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka sita. Alifikishwa katika mahakama hiyo akituhumiwa kutenda kosa hilo Januari 11, 2021, baada ya kumv... |
null | MIFUKO ya hifadhi ya jamii nchini, imetakiwa kutoa elimu ya pensheni kwa watumishi kabla hawajastafu. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya TUGHE mahali pa kazi. Katambi amesema mafu... |
null | TAASISI tatu zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo, zimeridhishwa na uwekezaji unaofanywa na Kampuni ya Global Agency katika kuhakikisha inazalisha mbegu bora za mahindi, ngano na soya. Hatua ya kampuni hiyo itasaidia kuendana na lengo la serikali kuhakikisha nchi inajitoshekeza katika mazao ya mbegu na kupunguza gharama ... |
null | RAIS Samia Suluhu Hassan amepokea ripoti ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi yenye mapendekezo mbalimbali ambayo amesema ataunda vikosi kazi ndani ya serikali kuyafanyia kazi. Alisifu kazi nzuri iliyofanywa na kikosi hicho akisema baadhi ya mapendekezo ni mepesi na yanaweza kufanyiwa... |
null | MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya, ameitaka ofisi ya Mkurungezi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaoiba fedha za walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF). Pia Kyobya amemtaka Mkurungezi huyo kuanisha kaya zenye wazee sana katika manispaa, kusimamia na kuhakikisha ... |
null | Search Mwanzo Matangazo: Maelekezo na Bei Kuhusu HabariLEO Nunua E-Paper Home HABARI KUU: Oktoba 20, 2022 Podcast HABARI KUU: Oktoba 20, 2022 by Sylvester Domasa October 20, 2022 Audio Player https://habarileo.co.tz/wp-content/uploads/2022/10/SAUTI.mp3 00:00 00:00 00:00 Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease vo... |
null | Podcast Sauti ya Balozi Kairuki akieleza mambo yaliyojiri ziara ya Samia nchini China bySylvester DomasaNovember 3, 2022 |
null | KIKOSI Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kimetoa mapendekezo mbalimbali ikiwamo yanayotaka mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini iruhusiwe kufanyika. Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, wakati aki... |
null | WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ametaka kila panapokuwa na mradi mkubwa wa maji kuwepo na watalaam wa kutoka chuo cha maji na mhasibu ili kufanya miradi hiyo idumu na kupunguza changamoto ya ajira. Akizungumza katika kongamano la pili la Kimataifa la Sayansi ya Maji linalofanyika Ubungo Plaza Dar es salaam, Aweso ameshanga... |
null | BODI ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji (RBWB) imezuia vibali 125 vya shughuli katika Bonde la Rufiji kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan. Rais alitoa agizo hilo Desemba mwaka jana wakati akizindua uingizaji maji katika bwawa la kufua umeme kwa kutumia maji la Julias Nyerere (JNHPP). Akizungumza na HabariLEO jana, m... |
null | KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo amekutana na bilionea Laizer katika mkutano wa shina namba 26 Tawi la Naisinyai wilayani Simanjiro mkoani Manyara na kumpongeza kwa kuchangia maendelea katika wilaya hiyo. Bilionea Laizer ni moja ya wanachama wa CCM katika shina na tawi hilo, ambalo Chongolo leo ... |
null | WAKATI dunia ikiadhimisha siku ya wanawake leo Machi 8,2023 Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) kimesema bado Kuna mapengo kadhaa yanayoibua changamoto za usawa wa kijinsia. Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Rose Reuben amesema leo Machi 8,2023 kuwa Tamwa inaamini katika kuibua changamoto zinazowakabili wanawake na watoto... |
null | IMEELEZWA kuwa wasichana 8,000 wenye umri kuanzia miaka 10 hadi 19 wamepata ujauzito kuanzia Januari mpaka Disemba 2022 katika Mkoa wa Mtwara. Tatizo hilo limetajwa kuwa ni kubwa mkoani humo. Akizungumza leo Machi 8, 2023 wilayani Tandahimba katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Mkoa wa Mtw... |
null | WAZIRI wa Maji, Juma Aweso amezindua kongamano la pili la kisayansi la kimataifa la maji chini ya uratibu wa chuo cha maji katika ukumbi wa Ubungo plaza uliopo jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2023. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Machi 8-10 mwaka huu, lengo likiwa kuzikutanisha taa... |
null | MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoka wito kwa waandishi wa habari kuandika habari za kuhamasisha wanawake kushiriki na kijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 2024. Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, Ofisa ... |
null | RAIS Dk Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini leo Oktoba 29 kuelekea Des Moines, lowa, nchini Marekani kuhudhuria Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug ulioandaliwa na Taasisi ya World Food Prize Foundation ya nchi hiyo. Mjadala huo hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na viongozi, wataalamu, watu mashuhuri... |
null | WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) wamekamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyote 785 katika Mkoa wa Mtwara. Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA) Jones Olotu amesema hayo leo Octoba 28 wakati wa hafla ya uzinduzi wa umeme katika kijiji cha mwisho cha Makome Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara. Amesema ukamilishaji huo um... |
null | WADAU wa haki jinai Mkoa Kigoma wamefanya ziara kutembelea shughuli za mamlaka ya bandari katika Bandari ya Kigoma na Kibirizi ili kuwezesha kuwa na uelewa mpana wa shughuli za bandari iweze kuwasaidia yanapotokea mashauri mahakamani kuhusiana na jambo lolote la kesi za jinai na madai zinazotokea bandarini. Mkurugenzi ... |
null | QATAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi wa Qatar anayeshughulikia masuala ya Nishati Saad bin Sherida Al- Kaabi. Mazungumzo hayo yametoa nuru kwa Qatar kuiuzia Tanzania mbolea aina ya Urea kwa gharama nafuu. Kikao hiki pia... |
null | QATAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ametembelea kituo kikubwa cha kujitolea cha Qatar kinachojishughulisha na kutoa misaada kwa wenye mahitaji mbalimbali -Qatar Charity na kujionea shughuli zinazofanywa na kituo hicho. Dk. Mwinyi ameonesha kufurahishwa na mapokezi ma... |
null | MWANZA : MKUU wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri, amefariki Dunia leo jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu. Jenerali Musuguri alizaliwa Januari 4, 1920 huko Butiama Mkoani Mara, na kutumikia nchi katika Jeshi kuanzia Mwaka 1942 hadi 1988 ambapo alihitimisha uongozi wake kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kat... |
null | DAR-ES-SALAAM : MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekabidhiwa rasmi ya rada zake mbili za hali ya hewa zilizopo Mwanza na Dar es salaam zilizokuwa zinafanyiwa uboreshaji na kampuni ya Enterprises Electronic Corporation (EEC) kutoka Alabama, Marekani (USA). Maboresho hayo yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muu... |
null | RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefungua rasmi ofisi ya wakala wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) iliyopo Minhang katika Jiji la Shanghai, China. Katika hafla hiyo fupi ya ufunguzi rasmi wa ofisi, Rais Dk. Mwinyi, amesema kuwa Zanzibar bado inahitaji wawekezaji... |
null | INDONESIA : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Jakarta na ujumbe wake akiwemo mkewe Mama Mariam Mwinyi. Katika uwanja wa ndege wa Ngurah Rai, Bali Rais Dk.Mwinyi aliagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje Indonesia, Balozi Ac... |
null | SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema ina vipaumbele vitano katika sera ya uchumi wa buluu ili kuimarisha uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Dk Aboud Jumbe alitaja vipaumbele hivyo kuwa ni utalii, uvuvi, usafiri wa baharini, nishati na usimamizi... |
null | RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema watendaji wote wa serikali waliotajwa kwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Zanzibar na kuhusishwa na upotevu fedha watachukuliwa hatua za kisheria. Katika kujenga ufanisi wa Mamlaka ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu wa Uchumi (ZAECA) k... |
null | DAR-ES SALAAM : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini kupitia sekta ya utalii yanayoitangaza Tanzania kimataifa na kuitambulisha duniani kuwa nchi ya kwanza Afrika inayofanya vizuri kwa utalii na ya sita dunia nzima. Amesema mafanik... |
null | Rais Dk Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam leo Oktoba 29. Mkutano huo unahudhuriwa na watu kutoka nchi mbalimbali, ambapo miongoni mwao ni Wenza wa Wakuu wa Nchi 15 za Afr... |
null | RAIS Dk Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary jijini Dar es Salaam leo Oktoba 29. Mkutano huo ni Kongamano la kielimu linalofanyika kila mwaka ili kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Bara la Afrika na Asia.(Picha na Ikul... |
null | TANZANIA ikiwa ni miongoni mwa nchi ambazo ziko hatarini kupata ugonjwa wa polio leo nchi sita za Ukanda wa Afrika wamekutana kujadili mikakati ya kutokomeza ugonjwa huo. Nchi za jirani ambazo bado zinakabiliwa na ugonjwa huo ni DR Congo, Msumbiji, Kenya, Uganda na zingine. Akizungumza katika mkutano wa 34 wa siku nne ... |
null | Diplomasia Featured Rais Samia ashiriki mkutano wa 11 wa Merck byNa Ikulu MawasilianoOctober 29, 2024 Diplomasia Featured Rais Samia ahutubia Mkutano wa 11 wa Merck byNa Ikulu MawasilianoOctober 29, 2024 Featured Michezo na Burudani Maandalizi CHAN 2025, AFCON 2027 yapamba moto byNa Wizara ya Utamdauni, Sana na Michezo... |
null | Bunge Featured Picha Waziri Mkuu ateta na Dk Dugange bungeni byNa Ofisi ya Waziri MkuuOctober 29, 2024 Diplomasia Featured Rais Samia ashiriki mkutano wa 11 wa Merck byNa Ikulu MawasilianoOctober 29, 2024 Diplomasia Featured Rais Samia ahutubia Mkutano wa 11 wa Merck byNa Ikulu MawasilianoOctober 29, 2024 Featured Mich... |
null | MKUU wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka (pichani) ametoa mwito kwa wananchi ambao hawajahesabiwa watumie siku zilizobaki kwa faida yao na nchi yao. Mtaka alitoa kauli hiyo jana baada ya kuona kazi hiyo inavyoendelea kwenye maeneo mbalimbali. “Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kushiriki kikamilifu zoezi hili, ... |
null | Infographics Kanda Maisha ya Vijijini Tanzania Mtaka awapa angalizo ambao hawajahesabiwa byOscar JobAugust 25, 2022 Infographics Kanda Maisha ya Vijijini Tanzania Tanga sensa ni shwari byAmina Omari, TangaAugust 25, 2022 Infographics Kishikwambi kilichoporwa kwa karani wa sensa Katavi chapatikana byNa Swaum Katambo, Ka... |
null | KISHIKWAMBI cha karani wa sensa kilichoibwa usiku wa Agosti 23 huko katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi kimepatika, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amethibitisha. Mrindoko amesema licha ya Karani huyo kupoteza kifaa chake cha kazi zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 halikuteteleka... |
null | MKUU wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba amesema hadi sasa sensa ya watu na makazi inaendelea vizuri mkoani kwake na ameomba wananchi ambao hawajafi kiwa wawe wavumilivu. Mgumba alisema jumatano kuwa hajapokea changamoto yoyote zaidi ya kuwa bado kuna wananchi ambao hawajafikiwa na makarani kwenye maeneo mengi mkoani hapa. A... |
null | MKUU wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk Batilda Burian, amesema licha ya changamoto za mtandao, sehemu kubwa ya utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi, umefikia zaidi ya asilimia 100. Amezungumza hayo katika kikao kazi cha Wadau wa Mitandao wa Kanda ya Kati, kilichoitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kinachoend... |
null | TANZANIA imeihakikishia Qatar kuwa ipo tayari kutoa vijana watakaoweza kufanya kazi nchini humo, hususan katika kipindi hiki ambacho mahitaji ya nguvu kazi ni makubwa kutokana na nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia Novemba mwaka huu. Hayo yameelezwa wakati wa mazungumzo baina ya Naibu Katibu Mkuu wa... |
null | ALICE Kibipi mfugaji nyuki wilayani Butiama, mkoa wa Mara amewashauri wanawake wenzake kujikita katika biashara hiyo na kuachana na dhana kwamba hiyo ni ya wanaume tu. Ametoa wito huo leo Agost 26, alipotembelewa na maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kujua maendeleo ya ufugaji wake, pamoja na kumpatia e... |
null | JESHI la Polisi mkoani Pwani, linamshikilia mtu mmoja mwanaume (32), mkazi wa Sanze Wilaya Kisarawe, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa tuhuma za kukutwa na silaha mbalimbali bandia za kivita. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, ACP Pius Lutumo, alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa... |
null | MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema suala la elimu katika tasnia ya habari, linatafutiwa mwarobaini. Amesema, wanapendekeza waandishi waliopo kwenye tasnia ya habari ambao hawana vigezo, wasiondolewe na badala yake wapate mafunzo wakiwa kazini, huku wanaoingia lazima wakidhi vigezo... |
null | MWENYEKITai wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema kosa la mtu mmoja lisisababishe chombo cha habari kufungiwa na kunyimwa haki ya wananchi kupata habari. Balile ameyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa suala la kufungia chombo cha habari kwa kosa la mtu binafsi si sahih... |
null | MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA), inatarajiwa kuufanya Mkoa wa Tanga kuwa wa kimkakati katika ukusanyaji wa mapato nchini Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mcha Hassan Mcha, wakati wa kikao na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga cha kujadili changamoto zinazowakabili katika ukusanyaji wa mapato. Amesema... |
null | WATOTO wanne wa familia moja wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada kibanda cha mganga wa kienyeji walipo kuwa kuungua moto. Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Richard Abwao amesema watu wengine saba wamekimbizwa hospitali na jeshi la polisi lina mshikilia mganga huyo anayedaiwa kuwasha moto katika kibanda hich... |
null | TAASISI ya Wanawake 100,000 imepanga kuwafikia wanawake nchini na kuwaelimisha kuhusu fursa ambazo hawajazifikia hususani katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye utalii, lengo likiwa ni kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla. Mshauri wa Masuala ya Utalii na Uchumi kutoka taasisi hiyo, Dk Theresa Mugodi... |
null | TAASIS ya wanawake Lakimoja imepanga kuwafikia wanawake nchini na kuwaelimisha kuhusu fursa ambazo hawajazifikia, lengo likiwa ni kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla. Mshauri wa masuala ya utalii na uchumi kutoka taasisi hiyo, Dk There’s Mugodi, amesema hayo leo Dar es Salaam, wakati akizungungumza kuhusu kuwepo kwa k... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.