text
stringlengths
1k
17.3k
label
int64
0
5
NA JONAS MUSHI MGAHAWA wa Vitabu-Soma umeanza kufanya utafiti wa kuwatambua wasanii wa kike waliosahaulika licha ya kushiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanzania. Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya kuwakumbuka wanawake walioshiriki kupigania uhuru, Mkurugenzi wa Soma, Demere Kitunga, alisema wapo ...
1
MRADI wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania umeshika kasi baada ya Tanzania kuanza utekelezaji katika hatua mbalimbali huku majadiliano ya ndani kwa nchi yakikamilika Januari mwakani.Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amesema hayo baada ya kikao cha mawaziri wa sekta zinazo...
5
UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kughushi inayomkabili mfanyabiashara, Shabani Hussein maarufu ‘Ndama Mtoto wa Ng’ombe’ katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, umedai upelelezi wa shauri hilo unahusisha nchi mbili za Tanzania na Australia.Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Maira...
3
Mkataba huo ulisainiwa Dar es Salaam jana kati ya mamlaka hiyo na Wizara ya Fedha, ambapo, upande wa TRA uliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka hiyo, Bernard Mchomvu na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, kwa upande wa serikali. Kiasi hicho cha fedha ndicho kilichoainishwa katika bajeti ya mwaka...
5
Mwito huo ulitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa wakati wa uzinduzi wa kadi maalumu ya Benki ya Posta (ATM card) kwa ajili ya vikundi vya Vicoba nchini.Kadi hiyo iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam inatazamiwa kuwarahisishia wanachama wa Vi...
5
Mwandishi wetu-Mbeya KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede, amewataka wazalishaji wanaotakiwa kutumia stempu za kodi za kielektroniki (Electronic Tax Stamp – ETS) kuendelea kuzitumia kama ilivyoelekezwa na sheria na taratibu za kodi kwa kuwa ina faida kwa wazalishaji wenyewe. Dk. Mhede aliy...
3
Hadi dakika ya 30 Yanga ilikuwa inaongoza kwa mabao mawili. Maboa hayo yamefungwa na Papii Tshishimbi kwa penati na Obrey Chirwa.Mabingwa hao watetezi ni wa pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na pointi 34 na wanahitaji ushindi ili kuwakaribia vinara Simba, ambao wanaongoza wakiwa na pinti 41.Simba ke...
4
    Na MWANDISHI WETU, KUNA msemo usemao mama ndiyo kila kitu katika maisha. Mtoto anapokosa mama huwa mpweke hivyo kujikuta akiishi maisha asiyoyapenda. Upendo wa mama hauwezi kufananishwa na kitu chochote kile, ndiyo maana wazee wanakwambia radhi ya baba inapoteza mawazo wakati ya mama inaua. Ukimdhar...
0
WATANZANIA wameanza kuchangamkia soko la mihogo la tani milioni mbili nchini China, baada ya viwanda zaidi ya vitano vya kuchakata zao hilo kujengwa nchini.Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema mpaka sasa kuna viwanda vitano vya kuchakata zao hilo kwenye mikoa ya Pwani na Tanga, vilivyojengw...
3
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) yenye jukumu la kukadiria, kukusanya na kuhasibu mapato ya serikali, ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo mstari wa mbele kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa vitendo katika kutekeleza azma ya serikali ya kuleta maendeleo.Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitatu, im...
3
Na Mwandishi Wetu Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah maarufu Super Sami, atazikwa leo Alhamisi Machi 16, nyumbani kwao wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza saa tisa alasiri baada ya uchunguzi wa kitatibu kukamilika. Akizungumza na Mtanzania Digital leo kaka wa marehemu Amini Sambo amesema atazik...
3
Mwijage aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika viwanda vinne ikiwemo kiwanda cha nondo cha Kamal na viwanda vitatu vya vilainishi mitambo.Alisema kutekelezwa kwa sheria hiyo kutasaidia ukuaji wa viwanda vingi ambavyo kwa sasa vipo katika hali mbaya baada ya bidhaa zilizo chini ya viwango kuin...
5
Na ASHA BANI BENKI ya Biashara Afrika (CBA) Tanzania Limited imeungana na Serikali katika kuhakikisha inapambana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona. Katika hilo, CBA imetoa msaada wa matanki ya kuwekea maji yenye thamani ya Sh milioni 10 kwa hospitali kubwa nne za jijini Dar es Salaam kwa lengo...
0
SERIKALI imeagiza mashine zaidi ya 60 za kusafi shia fi go kutoka nchini Saudi Arabia zifungwe katika hospitali za rufaa za mikoa ili kuwarahisishia wahitaji wa huduma ya kusafi shwa fi go kuifi kia kirahisi.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hayo bungeni jana wakati akij...
3
DAVAO, PHILIPPINES KATIKA mlolongo wa kauli zake tata kuhusu mashambulizi ya kingono, Rais Rodrigo Duterte ameripotiwa akisema atawapongeza wabakaji wakitenda jinai itakayowahukumu kifo. Akizungumza na wanadiplomasia wa Ufilipino Ijumaa iliyopita katika mji wa nyumbani wa Davao, ambako alihudumu kama meya kwa zaidi ya...
2
Ujenzi wa Kituo cha Afya Msanzi mkoani Rukwa, haujaanza kwa miezi nane sasa, kutokana mvutano uliopo kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura.Kwa sasa kila mmoja ana na eneo lake, ambalo anataka kituo hicho kijengwe, huku Mbunge wa Jimbo la Kalambo ambaye pia ni Naib...
3
NA LULU RINGO TIMU iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19, African Lyon leo imemtambulisha kocha na mchezaji wote raia wa Ufaransa kwa lengo la kusaidia timu hiyo ifanye vizuri kwenye ligi hiyo. Kocha huyo mpya anayetambulika kwa jina la Soccoia Lionel na mchezaji anayetambulika kwa jina la ...
4
KWA mwaka 2017 na 2018 waajiri tisa wamefi kishwa mahakamani kutokana na kukiuka taratibu na sheria za ajira.Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu, Hadija Nasri (CCM). Katika swali lake, Na...
3
NA OSCAR ASSENGA, TANGA ULIPUAJI wa milio kwenye pikipiki (Exose) maarufu kama jango moshi, umetajwa kuwa miongoni mwa ugaidi mpya unaoitesa jamii ya Watanzania wengi ambao wameshindwa kuishi kwa amani. Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi limetakiwa kuona namna ya kudhibiti hali hiyo. Hayo yamesemwa jan...
3
WIKI hii, Julai 1, Benki ya Dunia iliingiza Tanzania katika kundi la nchi zenye kipato cha kati. Hizi ni habari njema hata pamoja na kwamba wapo wanaoona kuna mapungufu fulani fulani katika utendaji. Hatua ya kutoka katika umaskini na kupanda kwenda katika hatua nyingine ya juu huusisha suala zima la uchumi au maendele...
5
Elizabeth Kilindi,Njombe KUTOKANA na agizo la Rais Dk. John Magufuli la kutaka stendi kuu mpya  ya Njombe  kuanza kutumika ifakapo Mei 10,2019 hatimaye stendi hiyo imeanza kazi rasmi. Akizingumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri, aliwapongeza wananchi kwa kuitikia wito wa...
3
WATAHINIWA 91,442 wa shule na wa kujitegemea wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) unaoanza leo nchini kote. Aidha, jumla ya shule za sekondari 731, vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 229 na vyuo vya ualimu 90, zitatumika kufanyika mitihani hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa...
3
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hi...
5
Umejikita kuhakikisha Tanzania inajenga uchumi wa viwanda na kuongeza kiwango cha ajira na uzalishaji. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Thomas Samkyi aliyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam jana.Alisema, benki hiyo imeamua kusaidia utekelezaji huo ili kuwezesha upatikanaji wa utoshelezi na usal...
5
KINARA wa mabao Ligi Kuu Bara, Salim Aiyee wa Mwadui hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars chini ya kocha Emmanuel Amunike, suala ambalo amekiri limezidi kumuongezea hasira na changamoto ya kufanya vizuri zaidi ili wakati mwingine ajumuishwe katika kikosi hicho.Aiyee, ambaye ana mabao 15 dhidi ya ...
4
London, England KOCHA wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte, ana matumaini ya kuthibitishwa kuwa kocha wa muda mrefu wa timu ya Chelsea, kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania Machi 24, mwaka huu. Kocha huyo anaamini anaweza kutua kwenye klabu hiyo na kupata mkataba wa miaka mitatu na kuwazidi makocha wengin...
4
MTOTO wa miaka minne, Ittai James mkazi wa Dar es Salam, aliyekuwa akiugua saratani ya tumbo ameonyesha dalili za kupona baada ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Narayana ya India, kumfanyia upandikizaji wa uroto.Hospitali ya Muhimbili Mloganzil, Dar es Salaam itaanza kupandikiza uroto kwa wagonjwa wa saratani na wen...
3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua channel mpya ya utalii ya shirika la utangazaji TBC, ijulikanayo kama Tanzania Safari Channel. Chaneli hiyo mpya itatoa maudhui mbalimbali yanayohusiana na vivutio vua utalii nchini.Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ofisi za TBC, Mikocheni jijini Dar es Salaam, Wa...
3
LONDON, ENGLAND BAADA ya mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry, ambaye alikuwa kocha wa vijana wa timu hiyo kutangaza kujiuzulu, nafasi hiyo imechukuliwa na aliyekuwa nyota wa klabu hiyo, Tony Adams. Henry ameachana na jukumu la kuwa kocha wa vijana baada ya kupishana kauli na kocha Arsene Wenger, baada...
4
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala amesema Rais Dk. John Magufuli amemaliza kazi 2020, kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM. Akizungumza katika mahojiano maalumu mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na televisheni ya...
3
Mchezaji huyo kwa sasa yupo katika wakati mgumu hasa kutokana na utata uliogubikwa kuhusu mkataba wake na klabu yake hiyo, ambapo kwa upande wake anasema kuwa mkataba wake umemalizika huku klabu hiyo ikisema kuwa bado anao mwaka mmoja wa kuendelea kuwatumikia.Akizungumza na gazeti hili, Messi alisema kuwa kwa jina lin...
4
Kwan hamna wenye ukimwi wanene ?????? Msikalili Ni moja ya comment aliyandika costanciapatrc  moja ya mtumiaji wa mtandao kwenye post ya mwanadada Wema Sepetu  kufuatia alot of comments za watumiaji wa mtandao kudai kuwa mwanadada huyo sio mzima kwa kile wanachoona kama kakonda sana. Katika siku hivi karibuni kwenye p...
1
WIZARA ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo (DP), imeanza mchakato wa kuanzisha Bima ya Mazao (BM) hapa nchini.Akiwalisha bajeti ya Wizara ya Kilimo bungeni jana, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (pichani) alisema kilimo ni moja ya maeneo yenye changamoto kubwa ya kupatikana hasara katika uwekezaji.Hasunga...
3
BAADA ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kufi ka mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kujibu tuhuma za kulidhalilisha Bunge kuwa ni dhaifu, wanasheria na wasomi wamefunguka kuhusu suala hilo.Ndugai alivieleza ...
3
JOSE Mourinho ameibuka na kuzitabiria mabaya timu nne za Ligi Kuu ya England zilizofuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya akidai kuwa zote zitatolewa, huku fainali zikicheza Barcelona na Juventus.Manchester United imepangwa kucheza na Barcelona katika robo fainali na mshindi atacheza ama na Liverp...
4
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki.Makonda ameyasema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa ki...
3
WABUNGE wameonesha kiu ya kuona Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ukiongezewa fedha kutoka asilimia 30 ya sasa hadi kufi kia asilimia 50, ili kuboresha mtandao wa barabara vijijini.Maoni hayo yalitolewa na wabunge kadhaa wakati wa kuchangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikal...
3
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM        |      KUKOSEKANA chombo makini cha kusimamia mchezo wa masumbwi nchini kumesababisha ushindwe kupiga hatua, badala yake umezidi kurudi nyuma na kupoteza mwelekeo. Ukosefu wa chombo makini umesababisha kuwapo kwa migogoro ya mara kwa mara ambayo imeathiri ukuaji wa mchezo huu, ambao...
4
Kutokana na leseni hiyo, sasa benki hizo mbili zitakuwa zikijiendesha zenyewe huku wakikabiliwa na changamoto ya mtaji ambapo kwa utafiti wao, wanahitaji Sh bilioni 500 kwa miaka mitano, lakini Serikali imewapatia Sh bilioni 110 hivyo wanashirikiana na wadau mbalimbali kupata fedha hizo.Wakurugenzi watendaji wa benki ...
5
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Raymond Mbilinyi alitoa mwito huo kwa wajumbe wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni mjini hapa.Alisema wakati umefika kwa halmashauri kuainisha maeneo yote muhimu yenye fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.“Mkutano huu na wadau wote wa baraza a...
5
HALMASHARUI ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara imekabidhiwa kinyago cha masikitiko kutokana na kufanya vibaya kwa kuwa wa mwisho kimkoa katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018. Kinyago hicho kimepokelewa na Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, Dua Nkurua kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).Akikabidhi kin...
3
Na Leonard Mang’oha-Dar es Salaam JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Meneja wa Maabara wa Tume ya Madini, Donald Njonjo (30), kwa tuhuma za kuiba dhahabu  kilo 6.244 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 507 iliyokuwa imehifadhiwa ofisi za Wakala wa Madini Masaki, Dar es Salaam. Akizungumza na ...
3
Petro alisema ujumbe wa mbio hizo ambazo mwaka huu zinatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ni kupiga vita ujangili wa wanyama.Alisema mbio hizo zitaanzia katika lango kuu la kuingilia na kutokea hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na kumalizikia mjini Karatu katika Uwanja wa Mazingira Bora.Mbali na mbio za nusu marathon...
4
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa Chama cha Ushirika katika eneo la Lambo Estate Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, kutoondolewa katika eneo hilo na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaisha.Uamuzi huo wa Lukuvi wa ku...
3
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, ameagiza mradi wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika chuo cha Ufundi Stadi (Veta), mkoani Njombe, unaotekelezwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) uchunguzwe.Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, kuchunguza mradi huo, baada ya kubaini...
3
Na Mwandishi Wetu, Dodoma Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa ya hali ya hewa ili kurahisisha huduma bora za utabiri kutolewa kwa wakati. Profesa Mbarawa amesema hayo mjini Dodo...
3
JESHI la Polisi nchini limewahakikishia raia wa kigeni wakiwemo watalii, kuwa nchi ipo salama dhidi ya vitendo vya kigaidi; na linaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya nchi.Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime. Alisema hayo wakati akizungumzia hali ya usalama nchini, kwa...
3
Hayo yalisemwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Ahmed Nassor Mazrui wakati akizungumza na wafanyabiashara wanaojishughulisha na bidhaa mbali mbali za vyakula katika maonesho ya biashara huko Maisara.Maonesho ya biashara yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein yakitoa fursa ya wafanyabiashara wa...
5
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame ameushangaza ulimwengu baada ya kuwaachia huru wafungwa 2,140 walioomba msamaha, ikiwa ni pamoja na wanasiasa maarufu nchini humo.Hatua hiyo imepongezwa na wanasiasa walioachiwa huru na imeleta furaha kubwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki, kwa kuonesha mwelekeo mpya wa kisiasa na kide...
3
Na JOSEPH SHALUWA MFALME wa Pop duniani, hayati Michael Jackson ‘MJ’ alifariki dunia Juni 25, 2009. Ndoto zake zote zilizimikia hapo. Chanzo cha kifo chake kinaelezwa ni kuugua, pamoja na maradhi mengine MJ alikuwa akikabiliwa na msongo wa mawazo na matatizo ya kisaikolojia yaliyopelekea kupatwa pia tatizo l...
1
Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inakusudia kupeleka muswada bungeni utakaowabana madereva wa pikipiki za kubeba abiria, maarufu bodaboda kuwa na bima ya afya kabla ya kupewa leseni ya kutoa huduma kutokana na ongezeko la ajali. Akizugumza Dar es Salaam jana w...
0
Yanga itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata wiki iliyopita katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanahitaji sare au ushindi wowote kuwawawezesha kusonga mbele hatua ya makundi.Ikiwa watafanikiwa basi watajiwekea his...
4
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Azam, Hans Van Der Pluijm amesema kwa sasa hana haraka anarudi nyumbani Ghana kujadiliana na familia yake kuhusu yaliyotokea.Pluijm amesema hayo siku chache baada ya kufukuzwa kazi katika kikosi cha Azam na aliyekuwa msaidizi wake Juma Mwambusi, baada ya kupata matokeo mabaya takriban mechi tat...
4
SERIKALI kisiwa cha Songosongo imetakiwa kushirikisha wananchi katika kuibua na kubuni miradi ya kimkakati ambayo itakujwa endelevu katika kusaidia, kuanzisha na kupanua wigo wa vyanzo vipya vya mapato katika kisiwa hicho. Kisiwa hicho kipo katika wilaya ya Kilwa na maarufu sana kwa uchimbaji wa gesi na uvuvi wa samak...
3
BODI ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali imetakiwa kuhakikisha miradi inayotekelezwa na mashirika hayo inazingatia mipango na vipaumbele vya serikali na wananchi katika eneo husika.Hayo yameleezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati wa kufunga maf...
3
BEIJING, CHINA SERIKALI ya China imesema itaziwekea ongezeko la asilimia 25 la ushuru bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani zenye thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi. Baraza la Ushuru na Forodha la nchi hiyo limesema hatua hiyo ni jibu kwa tangazo la Marekani la kuziongezea asilimia kama hiyo bidhaa za China ze...
2
Na ARODIA PETER DODOMA SERIKALI iko mbioni kukamilisha muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na kuuwasilisha bungeni Septemba. Pia wizara hiyo ipo katika maandalizi ya muswada wa marekebisho ya Sheria ya VVU na Ukimwi sura Na 431 ili kuruhusu watu kujipima wenyewe na kushusha umri wa mtu kupima bila ridhaa ya mzaz...
3
Na SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM UNAUKUMBUKA ule msemo wa Kiswahili usemao ukitaka kazi ya jeshi lazima ugangamale? Kumbe msemo huo sio jeshini tu, hata kwenye mchezo wa gofu kwasababu bila nidhamu na kujituma mambo yanakuwa magumu. Kwa siku za hivi karibuni, gofu imekua miongoni mwa michezo inayoendelea kujiz...
4
Mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana Jumamosi iliyopita aliweka rekodi mpya kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf). Mshambuliaji huyo ambaye aliichezea Yanga mchezo wake wa kimataifa kwa kwanza kuanzia alipojiunga nayo akitokea Mukura ya Rwanda, amekuwa staa kwen...
4
Na Elizabeth Joachim,Dar es Salam TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro kuiwakilisha nchini katika mashindano ya Kuimataifa ya Shirikisho Afrika  mwakani baada ya kunyakua kombe la Shirikisho kwa ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Singida United. Mechi hiyo ya fainali iliyozikutanisha timu hizo zime...
4
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM WAKATI mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu zimeshika kasi, hakuna dalili yoyote inayoonyesha kama mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam utatoa bingwa wa ligi hiyo. Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa inaongoza ligi...
4
Na Mwandishi wetu -Zanzibar  WAZIRI wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Khamis Juma Mwalim, ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kusimamia majukumu yao kwa ufanisi kama sheria na mwongozo inavyoelekeza. Akizungumza na ujumbe kutoka tume hiyo ofisini kwake Mazizini Unguja juzi, Mwal...
3
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene, ametoa siku 14 kwa watengenezaji na wasambazaji wa mifuko mbadala nchini kuhakikisha inakidhi vigezo vyote stahiki ikiwamo uwekaji wa nembo ya mmiliki au kampuni. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muda mfupi ba...
3
Kuna taarifa zinazodai kuwa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam (UDART) yamegoma na kusababisha usumbufu kwa wananchi.Leo saa mbili asubuhi kuna wananchi waliodai kuwa, walikuwa vituoni tangu saa tatu asubuhi na kwamba, hakukuwa na mabasi ya mwendokasi yaliyokuwa yakitoa huduma."Imekuwa kero sana, kwa hiyo nilik...
3
Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM CHAMA cha Damokrasia na Maendeleo(Chadema), kimewaagiza wabunge wake kote nchini kuhoji iwapo kutakuwa na mswaada wa mabadiliko ya tume huru ya uchaguzi, ili Watanzania waweze kupata viongozi wanaowataka kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Kauli hiyo ilitolew...
3
habari za ndani ya klabu zinadai kuwa kiungo mkabaji wa Simba Mghana, James Kotei hana nafasi ya kuendelea kuichezea timu hiyo, hali ambayo imesababisha jina lake lianze kutajwa ndani ya Klabu ya Yanga kwa nia ya kumsajili. Mghana huyo ni kati ya wachezaji waliomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu uliopita na inaelez...
4
Na Fredy Azzah-DODOMA LICHA ya kila Mbunge kulipwa posho ya Sh 220,000 kila anapohudhuria kikao cha Bunge, jana walikataa kukatwa Sh 30,000 za kumsaidia, Mshindi wa Tanzania super model, Asha Mabula, huku wengine wakitishia kwenda mahakamani endapo watakatwa fedha hizo.  Mshindi huyo anatarajiwa kushiriki sh...
3
UONGOZI wa Kampuni ya Acacia kupitia Mgodi wa North Mara umezungumza na serikali kuelezea hatua zilizochukuliwa hadi sasa kudhibiti maji yenye sumu, ikiwa ni wiki moja tu ipite tangu Waziri wa Madini Doto Biteko, atangaze kufunga shuguli za mgodi huo endapo utashindwa kudhibiti maji ya sumu yanayotiririka kwenye makaz...
3
Serikali imelieleza Bunge kuwa, waombaji 12,211 hawakupata mikopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu mwaka 2017/2018 kwa kuwa hawakukidhi vigezo na sifa zilizoainishwa kwenye sheria na mwongozo.Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya amesema, katika muda huo, wanafunzi 46, 131 waliomba mikopo ...
3
WAKULIMA wa njegere wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wameiomba serikali kuwapiga marufuku madalali wa Dar es Salaam kuingia wilayani humo na kununua zao hilo, wakiwatuhumu kuporomosha bei.Badala yake, wakulima hao wameiomba serikali ifungue milango kwa wafanyabiashara kutoka Kenya waliowasifia kununua zao hilo kwa be...
5
Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM NAIBU Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Nyanda ya Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Jennifer Baarn, amemwomba Rais Dk. John Magufuli kuangalia kwa jicho la huruma ushoroba wa kituo hicho ili kufikia Tanzania ya viwanda. “Namuomba Rais Magufuli kusaidia shughul...
3
Iman Mketema –Dar es Salaam  Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo Arusha, Meshack Daniel leo Desemba 1 amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni 226.8 baada ya kushinda mchezo wa Bahati Nasibu unaoendeshwa na kampuni mbili ya M-Bet na Perfect 12.   Meneja wa masoko wa M-bet, Allen...
4
Katika promosheni hiyo iliyoanza mwishoni mwa Novemba mwaka jana, inayolenga kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa jamii inayoizunguka, wateja 82 wameibuka washindi katika droo za kila siku na kila wiki.Akizungumza baada ya kupata washindi wa wiki ya kwanza ya awamu ya pili ya promosheni , katika droo iliyochezwa ju...
5
Tanzania Prisons inatarajia kupambana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.Mpalile alisema hasira za kufungwa na Yanga wanakwenda kuzimalizia kwa Mbeya City japo wanafahamu ni timu nzuri na inafundishwa na mwalimu mzuri.“Tumefungwa na Azam FC ma...
4
['Arsenal inataka kumsaini winga wa Barcelona Malcom, 22, huku Everton ikiwa tayari imewasilisha ofa ya dau la £31.5m kumsaini raia huyo wa Brazil. (Sun)', 'Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Dean Saunders anaamini kwamba Ole Gunnar Solskjaer hatomaliza msimu huu kama mkufunzi wa Manchester United . (talkSPORT) ', 'S...
4
UTAFITI uliofanywa na Taasisi ya Twaweza, umebaini zaidi ya nusu ya Watanzania hawajisikii huru kumkosoa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Katika utafiti huo ambao unawakilisha Tanzania Bara peke yake, nusu ya wananchi ambao ni sawa na asilimia 47, hawajisikii huru kuwakosoa mawaziri na asilimia 46, wakuu wa mikoa n...
3
JOSEPH HIZA NA MTNDAO PAMOJA na sifa ya utajiri wa kiuchumi na rasilimali likichukuliwa kama Taifa lililostawi zaidi kimaendeleo barani Afrika, wengi hufikiria mara mbili mbili kuitembelea Afrika Kusini kitalii, kimasomo au kikazi. Kundi hilo halihusishi wale vijana wanaozamia nchini humo kwa njia haramu kutafuta mais...
0
 Na RAMADHAN HASSAN–DODOMA  ZAIDI ya abiria 150 wamenusurika kifo huku 32 wakijeruhiwa baada ya gari aina ya Isuzu kuigonga treni iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jijini Dar es salaam katika eneo la Hazina jijini hapa.  Akizungumza na Waandishi wa Habari, jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema ...
3
RAIS Uhuru Kenyatta ameonesha kuguswa na kero ya maelfu ya wakulima wa mahindi ambao wamecheleweshewa malipo ya mazao yao.Akizungumza kwenye Maonesho ya Kilimo ya Nairobi, Rais Kenyatta alisema serikali iliwatengea wakulima pesa kwenye bajeti ya mwaka uliopita, lakini maofisa wa Bodi ya Nafaka (NC PB) wakaamua kuwalip...
3
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mwaka 2015/16 serikali imefanya utafiti na kubaini katika kila watoto wa kike 100, watoto 27 nchini wanakuwa wamepata watoto kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili uliowakutanisha wadau ...
3
Na ASHA BANI -DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Mtandao  wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, amesema anahitaji kupumzika kwa sababu hayupo vizuri kiakili. Akizungumza  jana baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Iringa baada ya kupata dhamana juzi dhidi ya kesi inayomkabili mahakamani, Nondo alisema a...
3
NYOTA wa mpira wa kikapu duniani, Mmarekani Kobe Bryant na binti yake, Gianna, ni miongoni mwa watu tisa waliokufa katika ajali ya helikopta iliyotokea mjini Calabasas, California, Marekani, imeelezwa.Bryant aliyetamba katika mchezo huo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 41, alikuwa akisafiri na helikopta yake bi...
4
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma katika mwaka wa fedha 2019/20, imepanga kukusanya Sh bilioni 72.97 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani.Akiwasilisha Ripoti ya Mapato ya Jiji kwenye Baraza la Ushauri la Mkoa (RCC), Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji, Godwin Kunambi alisema makusanyo hayo katika mwaka huu wa fedha...
3
MABINGWA watetezi wa Michuano ya Chalenji kwa Wanawake ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Kilimanjaro Queens jana imetinga fainali baada ya kuifunga Uganda kwa bao 1-0 katika nusu fainali kwenye Uwanja wa Chamazi , Dar es Salaam.Ushindi huo sasa unawafanya mabingwa hao mara mbili mfululizi kukutana tena na Kenya ka...
3
BEIJING, CHINA RAIS Xi Jinping amesema muungano kati ya China na Taiwan hauepukiki na harakati za kisiwa hicho chenye mamlaka ya ndani kutaka uhuru wake ni ndoto ya mchana. Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 40 tangu kutolewa kwa tamko muhimu juu ya sera ya China kuhusu Taiwan kwenye ukumbi maarufu wa umm...
2
WAKATI mashindano ya 17 ya dunia ya riadha yaanza leo Doha, Qatar, Tanzania inatupa karata yake ya kwanza kwa mwanariadha wake wa kike, Failuna Abdi kukimbia mbio za marathon. Failuna ambaye muda wake bora binafsi ni saa 2:27:55, mbali na kusaka medali ya kwanza ya Tanzania kwa wanawake katika historia ya mashindano h...
4
Serikali imewaagiza makatibu Tawala wa mikoa nchini na maafisa utamaduni kuhakikisha wanasimamia mchakato wa upatikanaji wa vazi la Taifa ili ukamilike haraka. Aidha, amesema wizara imeweka mkakati maalum kwa kushirikana na maafisa utamaduni ili kupata vazi la Taifa. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,...
1
KOCHA wa Lipuli FC, Suleiman Matola amesema kucheza kwa kujituma na kutanguliza malengo ni mbinu itakayokisaidia kikosi cha Simba kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao kimataifa dhidi ya Nkana FC ya Zambia na kutinga hatua ya makundi.Mchezo huo wa raundi ya pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika, unatarajiwa kupigwa kesho kwe...
4
MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa ndoa yake na mumewe, Gustavus Babile haijawahi kuvunjika, kwani ndoa ya Kikristo huwa haivunjiki, ingawa hakuweka wazi kama wanaishi pamoja na mumewe huyo Mbweni, Dar es Salaam au la.Bulaya ambaye jana alikuwa a...
3
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hi...
5
NA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imesema  gharama inazotoza kulipia huduma ya kuhifadhi maiti haijapanda. Kauli hiyo imetolewa baada ya baadhi ya ndugu wa marehemu ambao hufikisha wagonjwa hao na kukutwa na  mauti hospitalini hapo, kulalamikia kupanda kwa gharama kimyakim...
3
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma iko katika mkakati kupata vyumba 52 vya madarasa kabla ya Februari 2, mwaka huu ili wanafunzi 2,610 waliofaulu na kukosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza wapate nafasi hiyo kusoma haraka.Akisoma ripoti mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge kabla ya kuanza ziara kukagua ...
3
MAJADILIANO ya Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, yanaendelea huku serikali ikisema kasi yake ni kubwa, ambayo ikilinganishwa na nchi nyingine zilizowahi kufanya mchakato kama huo, haijawahi kuwa hivyo.Wakati mradi huo wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), unatarajiwa kutekelezwa Septem...
3
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) limekaribisha mradi wa utafiti wa kisomi, kabla ya uchimbaji wa urana (uranium) utakaohusisha Tanzania, Malawi, Namibia na Zambia.Akifungua jana mkutano wa siku moja wa wasomi na wadau wengine wa mazingira jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC, Dk...
3
USIMAMIZI mbovu wa sekta ya madini nchini ni moja ya sababu, zilizofamfanya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.Katika mabadiliko hayo juzi, Rais Magufuli alimteua Doto Biteko kuwa Waziri wa Madini na kumuondoa aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Angella Kairuki, aliyemteua kuwa Waziri wa N...
3
MHASIBU wa Klabu ya Simba, Amos Gahumeni (39) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna washitakiwa Evans Aveva na wenzake walivyotumia fedha za mauzo ya mshambuliaji wa klabu hiyo, Emmanuel Okwi.Gahumeni ambaye ni shahidi wa sita katika kesi hiyo ya utakatishaji fedha alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu...
4
Azam FC usiku wa kuamkia leo iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili Kocha huyo alisema kuwa jitihada zao zote kwa sasa wamezielekeza kwenye michuano hiyo baada ya nafasi finyu waliyokuwa nayo k...
4
    Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM SIKU chache baada ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee (Kawe) na Esther Bulaya (Bunda) kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa mwaka mmoja, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, amesema watakwenda mahakamani. Mdee n...
3
MAREGESI PAUL Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amesema wananchi wamewageuza wabunge wa Tanzania na kuwa kama mashine za kutolea fedha (ATM) na Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS). Kutokana na hali hiyo, amesema kuna haja Serikali kuboresha mafao yao ili yaendane na ...
3
MAMLAKA ya hali ya hewa nchini imetoa tahadhari kwa kaya 48,000 zinazoishi katika maeneo hatarishi kuwa zipo katika hatari ya kupata madhara makubwa kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha mwezi huu.Kutokana na tishio hilo, inakadiriwa kuwa serikali inahitaji kiasi cha faranga trilioni 1.4 kuhamisha kaya hizo k...
3